Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 470 | 471 | (Page 472) | 473 | 474 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Sauti Sol toka nchini Kenya mwishoni mwa wiki (21/02/2015) wamepiga show ya kufufuka mtu ndani ya kiota cha burudani chanye hadhi ya kitalii Jembe Beach ndani ya party lililopewa jina la JEMBEKA, likiandaliwa na Kituo kipya cha redio jijini Mwanza Jembe FM 93.7.
  Mashabiki walitoa ushirikiano wa kila htua zilizokuwa zikiendelea stejini.
  Hapo vijEee....!!
  Kenyan Afro Pop (2014 MTV EMA Best Worlwide Act Nominees) walifanya kazi ya ukweli..
  .
  Stage kama screen vile unawochi kitu cha LIVE....
  Kutoka kushoto ni Willis Austin, Savara Mudigi Delvin na King Bienaime.
  'PAMOJA SANA' CEO wa Jembe ni Jembe DR. Sebastian Ndege (wa pili kutoka kulia) akiwa na 'Team Jembe' Dvj Frank (wa kwanza kulia), wengine ni Dvj Chriss Young (wa kwanza kushoto), Dvj David (wa pili kushoto) na G. Sengo (wa tatu kushoto)
  "Mwanza you fill it.................!!"
  Msanii toka home Mwanza ....Director Shahibu aliwachangamsha kinowmer' 
  'Changamka' ilifumuliwa na watu wakaJEMBEKa...!!
  Kundi lililojizolea umaarufu jijini Mwanza kwa sasa THE Mamba Dancerz aka 'Chacha na wanawe' wakifanya yao.
  You whaaaaaat....
  Mtafutano....
  Marafiki toka mataifa mbalimbali nao walijumuika hadi kwenye mashindano ya kusakata katika jEMBEKa Party iliyofanyika mwishoni mwa wiki Jembe Beach jijini Mwanza.
  Drummer Boy...aka mkaanga chips..akiwa kikaangoni.
  "Huyu mtu hatari" says Dvj David.
  Selfie ya GSengo na Keybordist wa Sauti Sol.
  Hapa msanii wa muziki wa kizazi kipya toka Mwanza Director Shahibu alikuwa akiimba wimbo aliomshirikisha mwimbaji wa JJ Band Alice.
  Wow....!
  The crew.
  Mbunifu wa mavazi ambaye pia ni mtengeneza mavazi Seth aka Bikira wa Kisukuma aka FUNDI (katikati) ni sehemu ya watu muhimu tukioni.
  Take two...
  Watu muhimu sana.
  Sauti Sol na mashabiki wao....
  'PAMOJA SANA'
  Kutoka Kituokipya cha redio jijini Mwanza Jembe FM 93.7 hii ni jEMBe Team kutoka kushoto ni Dvj Chriss Young, Dvj David, Dvj Frank, Producer Oxy, Program Master Eliud aka Dj Kagz.
  Wahabarishaji.
  PichaZzzzz....!!
  Ze area...
  Show ya Jembe Djz ndani ya jEMBEKa pARTy.

  0 0

  66
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua  Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva na Katikati ni Katibu wa Tume hiyo, Ndugu Malaba.
  01
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda   na Naibu Katibu Mkuu  ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHEDEMA  John Mnyika wakitazama kadi mpya ya mpigakura baada ya Waziri Mkuu, Kuzindua uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura  katika mji mdogo wa Makambako  Februari 24, 2015.
  02
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekititi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva (kushpoto) , Naibu Katibu Mkuu  na Katibu Mwenezi wa CHADEMA, John Mnyika (kulia), Yusufu Mbungiro ambaye ni Afisa Uchaguzi na Mafunzo taifa wa Chama cha CUF (wapili kushoto) na Allan Bujo ambaye ni Mkuu wa Ulinzi wa CHADEMA baada ya kuzinua Uborereshaji wa Daftarila Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.
  03
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama kazi ya uandiskishaji wapiga kura baada ya ya kuzinua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.
  04
  Baadhi ya watu waliohudhuria  katika Uzinduzi wa Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako wakimsikiliza Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia katika uzinduzi huo  Februari 24, 2015
  Baadhi ya watalaamu wa kuandikisha wapiga  wakiwa na zana  za kazi kabla ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kuzindua Uborereshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Shujaaz Banner
  DJ Tee (19) ni kijana mwenye ndoto kubwa katika maisha yake. Baada ya kuona mahangaiko ya vijana kuelekea kwenye mafanikio, wengi wakiwa wamemaliza shule na vyuo bila kupata kazi, ameamua kuunda redio stesheni ghetoni kwake aliyoipa jina la Shujaaz, ili aweze kushea ideas na vijana wote nchini Tanzania kuhusu mbinu mbalimbali za kuingiza pesa, kuwapa stori za vijana wanaochakarika katika maisha yao pamoja na kuwaburudisha.
  "Nimeamua kuiita Shujaaz kwa sababu, naamini kuwa kijana ambaye anajituma na kuweka mfano bora kwenye jamii ni shujaa". Alisema DJ Tee. "Ndoto zangu zinakaribia kuwa kweli".

  Story ya kijana huyu inapatikana kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kupitia kijarida cha Shujaaz, kitakachokuwa kinasambazwa kupitia gazeti la Mwanaspoti, kuanzia JUMAMOSI HII ya tarehe 28. Kwenye kijarida hicho, utapata ideas mbali mbali ambazo vijana wanaweza kuzifuata na kujiingizia kipato. Pia, kutakuwa na stori za vijana wengine kama Pendo, Semeni na Pepe ambao ni mashabiki wakubwa wa DJ Tee na redio show yake ya Shujaaz.
  DJ Tee akiwa studio
  DJ Tee akiwa studio.
  Kijana huyu ameamua kujiita DJ Tee ili asijulikane na watu wake wa karibu, kwa kuwa ana-hack airwaves za redio stesheni ili aweze kusikika. Sikiliza redio stesheni uipendayo kuanzia wiki ijayo, huwezi jua, inawezekana DJ Tee akawa hewani!

  Wewe pia USIKOSE kuwa sehemu ya mafanikio na harakati za kijana huyu kwa kujiunga naye. Pata nakala yako ya Shujaaz kuanzia Jumamosi hii (28/02/2015) kupitia gazeti la Mwanaspoti. Pia, jiunge naye kwenye ukurasa wake wa Facebook kwa jina DJTee255 ili upige naye story na wewe uweze kushea idea zako za hustle. Unaweza pia ukampata Instagram na Twitter kwa jina @djtee255
  Studio
  Studio.

  0 0

  Natanguliza shukrani zangu mbele ya Mwenyezi Mungu ambaye ameendelea kunipigania kila kukicha,lakini pia niwashukuru wazazi wangu Abdalah Mbaruku na Eustela Massatu kwa malezi mema ambayo mmekuwa mkinipatia hadi leo kijana wenu nimefikia katika umri huu.
  Furaha niliyo nayo leo ni sawa na ile ambayo wanayo wadogo zangu wapendwa Jane,Judi,Juma Busagaga ,Ashura Mbaruku  na mtoto mpendwa Jesca Dixon pamoja na ndugu zangu kaka,Dada,wajomba ,mashangazi,marafiki na wengine wote tuendelee kufanya maombi ili Mwenyezi Mungu atusimamie katika kila jambo.

  0 0

  KAIMU MENEJA WA SIDO MKOA WA IRINGA, MR NIKO MAHINYA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFINI KWAKE
  KAIMU MENEJA WA SIDO MKOANI IRINGA, NIKO MAHINYA AKIWA NA MHANDISI WA KARAKANA YA SIDO IRINGA, MICHAEL MATONYA WAKATI WAKITEMBELEA UTENDAJI KAZI WA KARAKANA HIYO
  FUNDI WA KARAKANA YA SIDO ELAYSON TARIMO AKIANGALIA MASHINE YA KUNOA VYUMA, AMBAYO ILIKUWA IKINOA MAJEMBE YA KUKATIA CHAI
  MSIMAMIZI WA KARAKANA YA KUTENGENEZEA MASHINE MBALIMBALI YA SIDO MKOANI IRINGA, LEONARD LUMATO AKIENDELEA NA KAZI KATIKA KARAKANA HIYO
  KIJANA AKIENDELEA NA KAZI NDANI YA KARAKANA

  NA FRANK KIBIKI, IRINGA

  SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO), mkoani Iringa limewataka watanzania kujenga utamaduni wa kupenda bidhaa zinazotengenezwa ndani, badala ya zile zinazoingizwa kutoka nje ili kukuza uchumi wan chi.
  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa, Kaimu meneja wa SIDO mkoani Iringa, Niko Mahinya alisema ikiwa watanzania wataenzi bidhaa zinazotengenezwa ndani itakuwa rahisi kuinua uchumi wa nchi, na mtu mmoja mmoja.Alisema shirika hilo limekuwa likitengeneza bidhaa nyingi, zikiwemo mashine na pembejeo za kilimo lakini, kutokana na dhana ya kununua bidhaa za nje wamekuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la soko.
  “Tunazalisha mashine mbalimbali, zikiwemo zana za kilimo kama vile, mashine za kusagia nafaka, kuchujia mafuta ya alizeti, kukamulia asali na nyingine nyingi lakini changamoto kubwa ni soko la bidhaa za ndani,”alisema.
  Aidha alisema itakuwa vyema kama serikali itaweka utaratibu au sera itakayofanya watu wajenge tabia ya kuheshimu, kupenda na  kutumia bidhaa za ndani.Kwa upande wao baadhi ya wajasiriamali na wakulima walisema kuwa mara nyingi wamekuwa wakinunua mashine za kichina kutokana na bei yake kuwa chini ingawa hazina ubora.
  “Bidhaa za nje ni bei ndogo kuliko zile zinazotengenezwa ndani, hii ndiyo sababu inayofanya wengi tutumie bidhaa za kichina ambazo hata hivyo hazidumu kwa muda mrefu,”alisema LeoniKA Sanga, mmilikiwa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, mjini Iringa.
  Aliiomba serikali kutoa ruzuku kwa SIDO ili bidhaa zinazotengenezwa zishushwe bei yake na kuweza kuwahudumia wajasiriamali na wakulima wadogo.

  0 0

   Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi  Ngosi Mwihava (kulia) akimkaribisha  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (kushoto) ili aweze kuzungumza na timu  ya majaji na sekretarieti iliyofanya kazi ya  kumtafuta mshindi wa  Tuzo ya  Rais ya Utoaji wa Huduma za Jamii na Uwezeshaji  kwa  makampuni ya  uziduaji  yaani  madini na gesi. Timu  hiyo iliendesha zoezi hilo mapema Septemba, mwaka jana.
  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene akielezea umuhimu wa kuhamasisha makampuni mengi zaidi kujitokeza katika  kuwania   tuzo ya  Rais  katika utoaji  wa huduma kwa jamii na  uwezeshaji  kwa makampuni ya  gesi, mafuta na madini  ili  wananchi wafaidike zaidi na mchango katika sekta za nishati, madini na gesi.

  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (aliyekaa mbele) akizungumza na timu  ya majaji na sekretarieti iliyofanya kazi ya  kumtafuta mshindi wa  Tuzo ya  Rais ya Utoaji wa Huduma za Jamii  na Uwezeshaji kwa  makampuni ya  uziduaji  yaani  madini na gesi.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA NISHATI NA MADINI

  TANGAZO.

  MIGODI YA DHAHABU YA GEITA, BULYANHULU, BUZWAGI NA NORTH MARA KUANZA KULIPA USHURU WA HUDUMA KWA KIWANGO CHA 0.3% YA MAPATO GHAFI KWA
  HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI.

  Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutangazia umma kuwa mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika. Halmashauri zitakazonufaika na malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa Kahama; Wilaya ya Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza tarehe 1 Julai, 2014. 

  Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement - MDA) baina ya Serikali na Migodi ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali.


  Mha. Ngosi C.X. Mwihava
  KAIMU KATIBU MKUU
  25 Februari, 2015

  0 0

    Mfanyabiashara  wa Soko la Jipya  la Kawe,  Grace Pascal Kalengela (wa pili kulia), ambaye aliibuka mshindi wa Droo ya tatu ya promosheni  ya Airtel Yatosha Zaidi akishangiliwa na wafanyabiashara wenzake sokoni hapo, kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota
  IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana.
   Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akikabidhi mfano wa ufunguo wa  gari kwa mshindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi, Grace Pascal Kalengela  wakati wa  kumkabidhi  gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783 DCZ katika hafla iliyofanyika katika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni mume wa mshindi huyo, Daudi Mayunga na (kulia) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
   Mfanyabiashara  wa Soko la Jipya  la Kawe,  Grace Pascal Kalengela (wa pili kulia), ambaye aliibuka mshindi wa Droo ya tatu ya promosheni  ya Airtel Yatosha Zaidi akiwa mwenye furaha, kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783
  DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange.
    Mfanyabiashara  wa Soko la Jipya  la Kawe,  Grace Pascal Kalengela (wa pili kulia), ambaye aliibuka mshindi wa Droo ya tatu ya promosheni  ya Airtel Yatosha Zaidi akiwa mwenye furaha, kabla ya kukabidhiwa zawadi ya gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 783
  DCZ katika hafla iliyofanyika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange


  Wateja watatu Dar wakabidhiwa magari na Airtel baada ya kuibuka washindi
  Dar es Salaam, Februari 24, 2015

  MWANAMKE mchuuzi wa mboga mboga katika Soko jipya  la Kawe jijini Dar
  es Salaam, Grace Pascal Kalengera, jana alikuwa miongoni mwa wakazi
  watatu wa Dar es Salaam waliokabidhiwa zawadi zao baada ya kushinda
  promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi.

  Ijumaa iliyopita, Grace alipigiwa simu na Balozi wa Airtel Yatosha
  Zaidi, mwigizaji maarufu nchini, Lulu, baada ya namba yake kuwa
  miongoni mwa washindi kwenye droo iliyochezeshwa makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kuigiza nchini.

  Siku nne tu baadaye, leo Jumanne, Meneja Masoko wa Airtel, Frederick
  Mwakitwange, alimkabidhi gari lake mama huyo aliyeonekana wazi akiwa
  na furaha isiyo kifani.

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwakitwange alisema: “Sisi Airtel,
  tunafarijika sana tunapowaona washindi wakimiminika ofisini kwetu kila
  wiki kujichukulia zawadi zao. Na kwa ukweli zawadi ya gari si zawadi
  ndogo kwa wengi miongoni mwetu.

  “Tuliamua kwa makusudi kabisa kutoa magari kama zawadi kwa washindi
  kwa lengo la kuonyesha nia yetu ya kuboresha na kuyabadili maisha ya
  Watanzania.” 
  Mbali na Grace, washindi wengine waliokabidhiwa magari yao ni pamoja  na John Freddy Kiwale  mkazi wa Kinondoni ambaye pia ni wakala wa Airtel Money na Donald Fred Baruti mfanyabiashara wa Mwembechai
  Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando, alitoa wito kwa wateja wa
  kampuni hiyo kuendelea kutumia huduma za Airtel Yatosha Zaidi waweze
  kupata nafasi ya kujishindia magari.

  “Kama mnavyoona, hata mawakala wa Airtel Money wanaweza kushinda. Hii ni kwa sababu tu kwamba nao pia ni wateja wetu. Inafahamika kuwa kuna vigezo na masharti katika kushiriki na sisi tunazingatia sana hilo,”
  alisema Mmbando.

  Washindi wengine wa wiki iliyopita watakaopewa magari ya oleo ni Simon
  Grayson (Yombo, Kisiwani), Bilal Juma Mlendela (Tabata) na  Maxbeth
  Isack Manene (Tabata Segerea), kisha mkazi na mkulima kutoka Bukoba,
  Kajala Kokutima Said, naye atapewa gari wiki hii.

  Tayari magari 17 kati ya 60 yamekwishapata wamiliki wake wapya.


  0 0

  Miss Singida kanda ya kati 2014/15,Doris Mollel akisikiliza jambo kutoka kwa Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali wakati akipokea vitabu kutoka Children’s Book Project for Tanzania.

  Shule tatu za msingi katika mkoa wa Singida,zitapokea vitabu 200 wiki hii kusaidia katika mchakato wa kuboresha elimu ya shule ya msingi. Vitabu hivi vimetolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Children’s Book Project for Tanzania na italenga maelfu ya watoto nchini kote katika kuwakomboa kielimu.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi vitabu hivyo,Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali alisema kuwa Watoto wanaotakiwa kupata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya kunufaika zaidi kielimu.

  "Watoto wanaopata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya kunufaika zaidi kielimu. vitabu hivi vinatolewa kwa watoto ili waweze kutumia katika masoma yao ya kila siku shuleni.” alisema Ramadhani

  Msaada huu wa vitabu umejikita katika kukomboa hali ya elimu Tanzania, huku serikali ikijitahidi kuwekaza katika elimu nchini kwa kipindi kirefu. Inakadiriwa kuwa asilimia kubwa ya watoto wa shule ya msingi Tanzania hawajui kusoma na kuandika,Ukosefu wa vitabu unachangia wanafunzi wa shule ya msingi kushindwa kusoma na kuandika.

  Tafiti mbalimbali kutoka za serikali na sekta binafsi zinaonyesha wazi kuwa kujifunza kusoma mapema ni uwekezaji katika siku zijazo kwa mtoto,kwani elimu katika ngazi ya chini kwa mwanafunzi inachangia kuboresha maisha yake ya baadae.

  Kwa upande wake Doris Mollel ambaye ni Balozi wa Elimu mkoani Singida anatambua umuhimu wa elimu katika ngazi ya chini na anatumia muda wake mwingi katika harakati za kukomboa elimu ya shule ya msingi. Ziara zake nyingi hujikita katika mikoa ya ukanda wa kati hususani Singida na Tanzania kwa ujumla,Vile vile ni mshauri wa wanafunzi wa shule za msingi.

  "Msingi wa kujifunza kusoma hufungua uwezo wa kufikiri kwa mwanafunzi akiwa na umri mdogo bila kiini hiki cha msingi maendeleo na mafanikio ya mwanafunzi ni magumu.” alisema Doris

  Doris Mollel ni Miss Singida kanda ya kati 2014/15 na analenga katika kuboresha maisha ya jamii kwa kupitia elimu na masuala mengine ya kitamaduni.

  0 0

  whatsapp and facebook post
  Na Andrew Chale wamodewji blog
  Bonanza kubwa la Nyama ya kuku ‘’Chicken Wings’ litakalokutanisha watu mbalimbali wakiwemo marafiki na familia mbalimbali linatarajia kufanyika Februari 28, ndani ya Azura Beach Club, Kawe, Jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jaunt Africa Ltd, Acquiline Mlulla waandaji wa Bonanza hilo la ‘Chicken Wings Bonanza & Family Out’ linalotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza, Alisema tayari maandalizi yamekamilika na watu mbalimbali wameombwa kujitokeza kwa wingi ikiwemo na familia zao kufurahia siku hiyo muhimu na familia zao na kufurahia Nyama ya kuku.

  “Bonanza la ‘Chicken Wings, ni la kipekee kwani si la kukosa kabisa hiyo Februari 28, kwa kiingilio cha sh 10,000 kwa watu wazima na sh 4,000 kwa watoto. Ambapo milango itakuwa wazi kuanzia saa nne asubuhi tiketi zitakatishiwa hapo hapo huku saa sita mchana likianza rasmi na kuendelea hadi usiku.

  Familia na watu wote wataburudika, watafurahia nyama ya kuku zitakazoandaliwa kwa utaalamu wa hali juu pamoja na shamra shamra mbalimbali na muziki na matukio ya ‘surprise’ kwa kila atakayefika” alieleza Acquiline Mlulla.

  Acquline Mlulla alibainisha kuwa, Bonanza hilo litakuwa la kipekee kwa hapa nchini, kwani pia litakuwa na michezo ya ufukweni ikiwemo Beach Soccer, swimming pool, pamoja na madansa maalum watakaokuwa wakitoa burudani kutoka kwa Ma-dj wakubwa wa Bongo.
  Bonanaza hilo limedhaminiwa na Jaunt Africa Ltd, Dodoma Wine, Hot Spot Magazine, Coca- Cola, Michuzi Media Group na wengine wengi.

  For updates or to find out more about CHICKEN WINGS BONANZA or to request a sponsorship details, please contact us at: +255 755 048 362 or +255 658 289 737 Email: info@jaunt-africa.com or SKPE: acquiline.mlulla

  0 0

  1
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakifanywa na wanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekndari ya Igomelo wilayani Mbarari akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Mbeya Februari 24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  PATO LA MWANANCHI MBEYA LAVUKA LENGO LA KITAIFA

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameupongeza uongozi wa mkoa wa Mbeya kwa kuvuka lengo la wastani wa pato la mwananchi kitaifa na kuwataka waendeleze kasi ya kupambana na umaskini kwa wakazi wa mkoa huo.

  Ametoa pongezi hizo jana usiku (Jumanne, Februari 24, 2015) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa huo na wilaya zote wakiwemo wadau mbalimbali na viongozi wa dini mara baada ya kupokea taarifa ya Mkoa wa Mbeya.

  Alisema katika mipango yake, Serikali ililenga kwamba pato la mtu kwa mwaka liwe sh. 1,186, 200, lakini kwa sababu ya jitihada mbalimbali mkoa huo umelivuka. “Katika taarifa aliyonisomea, Kaimu Mkuu wa Mkoa amesema wastani wa pato la mwananchi umeongezeka kutoka sh. 711,201/- mwaka 2008 hadi kufikia sh 1,420,427/- mwaka 2013 na kwamba mkoa unachangia asilimia 7.43 ya Pato la Taifa,” alisema.

  Alisema kipato cha mtu mmoja kwa siku ni sh. 3,891/- ambazo ni zaidi ya Dola mbili za Marekani (sh. 3,400/-). “Wakubwa hawa wanatupima kwa kuangalia kipato cha mtu kwa siku. Wanasema nchi ni maskini iwapo watu wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku (sawa na sh. 1,700/-).”

  “Mbeya imeendelea kushika nafasi ya tatu kwa kuchangia vizuri Pato la Taifa ikiwa imetanguliwa na Dar es Salaam na Iringa. Ninawapongeza kwa sababu mmevuka malengo ya Taifa katika eneo la pato la mtu mmoja mmoja,” alisema Waziri Mkuu.

  Mapema, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Deodatus Kinawilo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chunya, alisema pato la mkoa limeongezeka kutoka sh. trilioni 1.779 mwaka 2008 na kufikia sh. trilioni 3.951 mwaka 2013. 

  “Uchumi wa mkoa huu unategemea kilimo, ufugaji, uchimbaji madini, uvunaji mazao ya maliasili, biashara, uzalishaji viwandani na ajira katika taasisi za serikali na sekta binafsi,” alisema.

  Wakati huohuo, uongozi wa mkoa wa Mbeya umetakiwa kuongeza bidii ili uweze kuinua kiwango cha ufaulu wa elimu ya kwa sababu umekuwa ukiendelea kushuka na kuwa chini ya kiwango cha asilimia 60 kilichowekwa na Serikali.

  Waziri Mkuu aliutaka uongozi huo ubuni mbinu za kisomi zitakazowawezesha wanafunzi wa shule za msingi kuelewa wanachofundishwa, hivyo, kufaulu mitihani yao vizuri. ”Ufaulu wenu kwa shule za msingi ni asilimia 46.6, uko chini ya kiwango cha kitaifa cha ufaulu kwa asilimia 13.4. Ni matokeo yasiyoridhisha, fanyeni utaratibu maalum ili yapande,” alisema.

  (mwisho)

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, FEBRUARI 25, 2015.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wawasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka Zambia na kupokewa na mwenyeji wao Rais Edgar Lungu wa Zambia leo asubuhi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.(PICHA NA FREDDY MARO WA IKULU)ZAM2 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wawasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka Zambia na kupokewa na mwenyeji wao Rais Edgar Lungu wa Zambia leo asubuhi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili( ZAM3ZAM4 
  Rais Kikwete na Rais Lungu wa Zambia wakipokea heshima ya mizinga 21 mara baada ya kuwasili.

  0 0

   Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakiteremsha baadhi ya maboksi ya dawa mbalimbali, vipodozi, mchele, na tende zilizoharibika kwaajili ya kuviangamizwa. 
   Maboksi ya dawa yaliomaliza muda wake yakiangamizwa kwa kuchomwa moto katika eneo la kibele Wilaya Kati Unguja.
   Mchele ulioingia nchini ambao haufai kwa matumizi ya binaadam na tende vikiangamizwa kwa kuchomwa moto kijiji cha kibele Wilaya Kati Unguja.

  Mafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakisimamia zoezi la uteketezaji wa dawa, vipodozi, mchele, na tende ambavyo vitu vyote hivyo havifai kwa matumizi ya binadam.


   (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).


  0 0

  Na   Bashir   Yakub.

  Hapa kwetu Tanzania  habari ya kubambakiziana kesi ni kama mtindo. Mara nyingi matendo haya yamekuwa yakifanywa na watu wenye uwezo  kifedha dhidi ya wasio na fedha  pia kati ya  maofisa wa polisi na raia. Mtu kwasababu ana pesa au cheo anaweza kuamua  kumfungulia yeyote mashtaka.  Watu wengi wako magerezani kwa kubambikizwa kesi, hili wala sio siri tena. Siseme walio mahabusu, hao nao hawana idadi. Inasikitisha mno. Ni wazi kuwa wengi wao wamefikia huko aidha kwa kusingiziwa kosa na askari au mtu mwenye cheo au  fedha. Lakini zaidi wametoka mikononi mwa askari kwakuwa hata huyo mwenye cheo au fedha hawezi kumbambikizia  mtu kesi  bila kupitia kwa askari. Kwahiyo askari  ndio  tatizo  kubwa  katika  hili.

   1.NINI  MAANA  YA   KUBAMBIKIZWA   KESI.

  Kubambikizwa kesi au kumshtaki mtu kwa  hila  maana yake ni kumfungulia mtu kesi ya jinai  bila  mafanikio , na bila sababu za msingi za kufanya hivyo  na mtu huyo  akapata  athari zozote kutokana na kumfungulia kesi hiyo. Athari ni pamoja  na kupotezewa muda, gharama, usumbufu, kudhalilishwa, kupata hasara kibiashara au kikazi kutokana na kushikiliwa na kila kitu ambacho kimekuwa kama  matokeo ya kusingiziwa kesi  ni athari kwa maana hii.

  2. SABABU   ZA   KUWABAMBIKIZA  WATU   KESI.

  Sababu  za kumuuzia mtu kesi  huwa ni nyingi. Ni  nyingi  kutokana  na kuwa kila aliyebambikizwa  kesi huwa kuna mgogoro nyuma uliosababisha  jambo hilo  na migogoro  kawaida inatofautiana. Pamoja  na hayo sababu  kuu  za kubambikizia  mtu kesi huwa ni kwa ajili ya kumkomoa  au kulipiza kisasi kutokana na chuki zilizotokana na mgogoro  kama  nilivyosema.

  3. WELEDI  WA ASKARI WETU  NA KUWABAMBIKIZIA  RAIA KESI. 

  Wakati  mwingine  askari  wetu  huwabambikizia  watu kesi  katika  mazingira  ya  kushangaza kabisa. Askari  anaweza  kumbambikizia  raia  kesi  kwasababu  tu  raia  amehoji  jambo  fulani. Kwa mfano mtu anaweza kumuuliza askari nioneshe  kitambulisho  chako kabla  hujanikamata. Utasikia  askari akimwambia  mtu unajifanya  mjuaji tutaona, mara unanifundisha  kazi utanitambua n.k. Eti mazimgira kama hayo kwa askari wetu utakuwa tayari  ni mgogoro  na  mtu atapofikishwa  kituoni  basi ni rahisi  kupewa  kesi ambayo si  yake  ilimradi tu askari  aoneshe  kuwa aliposema  utanitambua, utaona  alikuwa  na uwezo  wa kufanya  hivyo  kweli.


  0 0

  Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) akipokea hati ya mradi wa mkongo wa mawasiliano nchini (Fiber Optic) toka kwa Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge (kulia). Mradi huo umeunganisha matawi ya benki ya TPB kimawasiliano ya kisasa. Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) akipokea hati ya mradi wa mkongo wa mawasiliano nchini (Fiber Optic) toka kwa Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge (kulia). Mradi huo umeunganisha matawi ya benki ya TPB kimawasiliano ya kisasa.Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (wa pili kulia) akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini. Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (wa pili kulia) akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini.Mtatuzi wa Masuala ya Kiufundi, Fredrick Bernard akifafanua jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika jana Makao Makuu ya TPB Dar es Salaam. Mtatuzi wa Masuala ya Kiufundi, Fredrick Bernard akifafanua jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika jana Makao Makuu ya TPB Dar es Salaam.Baadhi ya Maofisa wa TTCL wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini. Baadhi ya Maofisa wa TTCL wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini.Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) pamoja na Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge wakipongezana kwenye hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini. Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) pamoja na Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge wakipongezana kwenye hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini.Picha ya pamoja ya maofisa wa TPB na TTCL walioshiriki katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini. Picha ya pamoja ya maofisa wa TPB na TTCL walioshiriki katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini.

   BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imedhamiria kuunganisha matawi yake yote katika mfumo wa kisasa wa mawasiliano kupitia mkongo wa mawasiliano nchini (Fiber Optic) ili kuberesha huduma na mawasiliano katika huduma zake. Taarifa hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa alipokuwa akizungumza katika makabidhiano ya mradi mpya wa benki hiyo uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo mbalimmbali nchini.

   Tawa alisema mpaka sasa matawi ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Samora, Metropolitan, YWCA, Mkwepu, Ubungo na Kijitonyama tayari yameunganishwa kwenye mfumo huo mpya na wa kisasa kimawasiliano. "..Mpaka hivi sasa matawi yetu Kumi na Moja (11), yakiwemo Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Samora, Metropolitan, YWCA, Mkwepu, Ubungo, Kijitonyama, tayari zimeunganishwa kwenye mfumo huo. 

  Hii ni katika hatua ya mwanzo tu ya mradi huu, kwani benki ya Posta imekusudia kuyaunganisa mtawi yake yote kwenye mfumo huu," alisema Tawa. Alisema baada ya kukamilisha matawi ya TPB katika mfumo wa Mkongo (Fiber Optic), imepata mafanikio makubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo matawi haya yalikuwa yameunganishwa na mtandao wa teknolojia ya Copper (Copper network). 

  Aidha akizitaja faida ambazo benki hiyo imezipata baada ya kujiunga na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unaosimamiwa na kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ni pamoja kupungua kwa msongamano wa wateja kusubiria huduma kwenye matawi, kuongezeka kwa ufanisi na kupungua kwa dharura ya kusitisha huduma kwa muda.

   "...Pia tumeboresha uwezekano wa kutambua tatizo lolote linalotokana na kukatika kwa mawasiliano kwani huu ni mfumo wa kidijitali...kupungua kwa gharama za uendeshaji katika benki yetu." alisema Tawa. Kwa upande wao TTCL ikikabidhi mradi huo kwa TPB, Mtatuzi wa Masuala ya Kiufundi, Fredrick Bernard alisema mfumo huo wa mkongo unafaida kubwa kwani, mbali na kuwa salama zaidi pia unauwezo wa kugundua tatizo la mawasiliano kabla ya kutokea hivyo kufanyiwa kazi mapema. 

   Alisema hata hivyo alisema njia za kupitisha mawasiliano hufanya kazi kwa kutegemeana na zipo zaidi ya moja hali ambayo huwezesha hata njia moja kuisaidia nyingine inapopata tatizo huku tatizo lililojitokeza likishughulikiwa kwa wakati huo. Faida hizo pamoja na nyingine nyingi zinaifanya benki ya Posta iamini kuwa huduma hii ya Mkongo itolewayo na TTCL ni bora nchini na itatusaidia sana sisi benki ya Posta kuboresha huduma zetu na kuongeza ufanisi katika shughuli zetu za kibenki.

  0 0

  kutokana na Maombi ya mashabiki wengi vijana wa Yamoto Band wameamua kufanya show moja na ya mwisho nchini Uingereza basi kama ulikosa ile ya London hii itakuwa si ya kukosa vijana kama kawaida yao wameahidi kufanya vitu fulani amazingg siku hiyo


  DATE: 
  Saturday 28th February 2015

  VENUE:
  Kitty Oshea's (Nest to pure gym)
  St. peter's Way
  Northampton NN1 !PS

  YAMOTO CLASSICS

  Nitakupwelepweta

  0 0

  Mkutano uliowakutanisha Mawaziri wa nchi tano za Afrika Mashariki wakiwemo Mabalozi wa nchini zao nchini Marekani ulifanyika leo siku ya Jumatano Februari 25, 2015 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, mkutano huo  uliohusiana na maandalizi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya nchi ya Marekani na nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania.

  Mkutano huo uliongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Harrison Mwakyembe Waziri wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  Balozi   Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.

  Washiriki wengine kwenye mkutano huo kutoka Tanzania walikua ni Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Usafirishaji Mhe. Samwel Sitta, Maria Bilia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Amantius Msole, Naibu Katibu Mkuu  MEAC Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

  Washiriki kwenye mkutano huo kutoka Burudi walikuwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Burundi Mhe.Mzigiyimana Marie Rose, Balozi wa Burundi nchini Marekani Mhe. Ndabashinze Ernest, Ntibarutaye Glorioje ambaye ni mshauri ofisi ya Wizara ya Biashara ya Burundi, 

  Wawakilishi kutoka Kenya walikuwa ni James  Kiiru amabaye ni Mkurugenzi masaidizi MFA & IT Kenya, Balozi  Nelson Ndirangu ambaye ni mkurugenzi  MFA & IT Kenya, Bi.  Phylus Kandie Cabinet Secretary MEACT Kenya, Ronnie Gitonga Naibu Katibu Ubalozi wa Kenya nchini Marekani na Esther Chemirmir  PA to CS MEACT Kenya.

  Wawakilishi kutoka Uganda walikua ni Balozi wa Uganda nchini Marekani Mhe. Alfred  Nwam na Stilson  Muhwezi. Rwanda waliwakilishwa na Waziri wa Bisahara na Viwanda Mhe. Robert Opirah na Innocent Kabandana.

  Mkutano huo ni mwendelezo wa ule mkutano wa mwishoni mwa mwaka jana nchi ya Marekani ilipowaalika Marais wa Afrika katika mkutano kama huo ulioongozwa na Rais Barack Obama.
  Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Harrison Mwakyembe ambaye alikua mwenyekiti wa mkutano wa kujiandaa kutiliana saini makubaliano ya biashara na uwekezaji wa nchi za Afrika Mashariki na Marekani. Utiliano saini huo utafanyika siku ya Alhamisi Februari 26, 2015 katika Ofisi za Wizara ya Biashara Marekani, kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.
  Ujumbe wa Tanzania
  Ujumbe wa Burundi
  Ujumbe wa Kenya
  Ujumbe wa Uganda na Rwanda
  Mkutano ukiendelea.
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.

  0 0

  FullSizeRender

  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento (kushoto) wakitiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa kutoa elimu kwa jamii kupitia ujumbe mfupi maneno katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mratibu mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa jijini Dar. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dkt. Jama Gulaid.(Picha na Umoja wa Mataifa).

  KAMPUNI ya simu ya Push Mobile imetiliana saini na serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa (UN) ya kuwafikia watu milioni 10 ikiwahabarisha kuhusu ugonjwa hatari wa ebola.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mjini hapa kampuni hiyo ya simu imesema kupitia ushirikiano huo kampuni hiyo ya simu itaunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa wa kutoa elimu dhidi ya ugonjwa huo ujumbe mfupi utakaoelezea ugonjwa wa ebola.

  Kama sehemu ya makubaliano, Push Mobile , UN, serikali na wadau wake watatoa taarifa kuhusu ugonjwa huo wanapohitajika. Watanzania wanaweza kupata habari za ugonjwa huo kwa kuandika neno EBOLA kwenye namba 15774 na kupata taarifa za ugonjwa huo bure bila kutozwa gharama.
  IMG_8005
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento wakionyesha hati za makubaliano ya ushirikiano huo.

  Wakitia saini Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento amesema kwamba kama Ujumbe mfupi unaweza kuokoa maisha kampuni yake iko tayari kushiriki katika kampeni hiyo.


  “..Teknolojia inatoa fursa ya pekee ya kuandaa jamii dhidi ya ugonjwa wa ebola na nini cha kufanya ukitokea. Kupitia ushirikiano huo kati yetu na Umoja wa Mataifa na Wizara ya afya na ustawi wa jamii tunaamini tutasaidia wananchi kuelekewa na kutambua dalili za ebola, kuzuia na kudhibiti maambukzi ya virusi vya ebola”, alisema Manento.

  Katika miezi iliyopita vifo kutokana na ugonjwa wa ebola vimefikia 9000 huku vifo vingi vikitokea katika nchi za Liberia, Sierra Leone, na Guinea. Hadi sasa watu 23,000 wameelezwa kukumbwa na ugonjwa.
  photo(36)
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento kwa pamoja wakionyesha ujumbe mfupi wa maneno unaotoa elimu ya ugonjwa wa ebola kwa baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria hafla hiyo.

  Tanzania ikiwa na watumiaji wa simu milioni 30 na kufanya uwezekano wa kufikia watu hao kuwa ni asilimia 68. Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez amesema teknolojia ya simu itasaidia sana kuleta uelewaq wa ugonjwa huo miongoni mwa Watanzania.
  “Mlipuko wa ugonjwa wa ebola umepungua sana Afrika magharibi na Tanzania haijawahi kukumbwa na ugonjwa huo.

  Lakini kunahitajika mtu mmoja tu kuwa na ugonjwa huo na kuleta mashaka makubwa katika maisha ya watu nchini. Tukiungana na sekta binafsi, Umoja wa mataifa unaunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii kuongeza upeo wa utayari katika kukabiliana na Ebola .”
  FullSizeRender (4)
  Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dkt. Jama Gulaid akimshukuru Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento (kushoto) mara baada ya hafla fupi ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano huo. Kulia ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishuhudia tukio hilo.

  0 0

  5
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la zahanati ya Kimondo , Mbeya Vijijini akiwa katika ziara ya mkoa  wa Mbeya, Februari 25, 2015. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Dr. Norman Sigalla.
  4
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Kimondo, Mbeya Vijijini  kabla ya kuweka jiwe la Msingi la zahanati yao akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Februari 25, 2015. Kushoto kwake ni Mbunge wa Mbeya Vijijini, Luckson Mwanjale na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman Sigalla.
  3
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua soko Kuu la Mjini Mbeya la Mwanjelwa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wake akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya, Februari 25, 2015.
  2
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwasikiliza wanafunzi wa shule ya sekondari ya Iwambe mjini Mbeya wakati alipofungua na kukagua maabara tatu za shule hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeaya Februari 25, 2015. Kushoto ni mkewe  Tunu. 
  6
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wananchi baada ya kufungua vyumba vitatu vya Maabara katika shule ya sekondari ya Songwe mkoani Mbeya Febrari 25, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  9
  Max Oswald (kushoto) na  Ivan Kina wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara  uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kijiji cha Igoma , Mbeya Vijijini Februari 25, 2015.
  Wasanii Max Oswald ( Wapili Kulia) na  Ivan Kina  (wapili kushoto) wakisaidiwa kuvua nyasi walizokuwa wamejifunika kwa ajili ya kutoa burudani katika mkutano wa hadhara uliohutuibiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katia kijiji cha Igoma, Mbeya vijijini Februari 25, 2015.  Wanaowasaidia ni Oscar Ben (kulia) na Obadia Dandu.


  0 0

  unnamed
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Zambia Michael Sata aliyefariki mwaka jana katika eneo la maziko ya viongozi wa kitaifa jijini Lusaka Zambia leo.Rais Kikwete alitumia  wasaa huo pia kuweka shada la maua katika marais wa Zambia waliofariki Marehemu Frederick Chiluba na Levy Mwanawasa. (picha na Freddy Maro)

older | 1 | .... | 470 | 471 | (Page 472) | 473 | 474 | .... | 1897 | newer