Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 455 | 456 | (Page 457) | 458 | 459 | .... | 1897 | newer

  0 0

   YAMOTO BAND  COMFIRMED will performing all their major hits including NITAJUTA, NISEME, WAMBEA, NITAKUPWELEPWETA and many more @ The Royal Regency Banquet Hall, Sat 21 Feb 2015 From 8pm to 3:30am, there are limited VIP Tables available book yours now for ultimate VIP treatment or individual place your booking early to avoid disappointment. Table bookings please call 07405824696/ WhatsApp +447557304940
  info@bongodeejays.com or jestinageorge@gmail.com
  Ukumbi wa Royal Regency ndio sehemu pekee ambayo utawaona YAMOTO BAND kwenye jiji la LONDON usiku wa 21. Feb 2015

  Usiku wa tarehe 21 February 2015 The Royal Regency patakuwa hapatoshi. Kwa kuondosha usumbufu wahi ticket yako mapema
   Kiingilio ni:
  £25 kwa Ticket ya kawaida
  £35 kwa VIP ticket
  Kama Unahitaji VIP table for 10 people piga simu 07405824696 kwa maelezo zaidi au tuma email kwenda: info@bongodeejays.com or jestinageorge@gmail.com
  YAMOTO BAND will be alongside supported artist such as Sultan King, OJ, Hyper hype And many more,why wait grab your ticket Now!!!! 
  HOT LINE FOR TICKET 07853482158/07557304940


  0 0

  jakaya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kuchapa kazi ndani ya ndege yake akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea mjini Dodoma ambapo aliongoza kikao cha baraza la Mawaziri(Picha na Freddy Maro)

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akihutubia katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini Mkoni Rukwa leo tarehe 04/02/2015 katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga. Kaulimbiu ya maaadhimisho hayo ikiwa "Fursa ya kupata haki: Wajibu wa Serikali, Mahakama na Wadau". Katika hotuba yake hiyo alisema ipo haja kubwa kwa Serikali kubadili sheria zake ili lugha ya mahakamani na hukumu ziandikwe kwa kiswahili. Kwa upande wa wananchi aliwaasa kujiepusha na tabia ya kujichukulia sheria mkononi ili kudumisha amani nchini.
  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo akipokea gwaride la heshima kutoka kwa kikosi cha Jeshi la Polisi wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria Mkoani Rukwa leo tarehe 04/02/2015.
  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo katikati akisoma hotuba yake ya maadhimisho ya siku ya sheria Mkoani Rukwa ambapo aliwataka mahakimu wote Mkoani Rukwa kutimiza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu miongozo ya mahakama ili kusaidia uharakishwaji wa utoaji haki kwa wananchi kwa wakati. Aliwaeleza pia wadau wote wa sheria wakiwepo mawakili wa kujitegemea kuwa mashauri yote ya kesi yatakua yakisimamiwa na kutolewa maamuzi na mahakama na sio mawakili kutaka kuingilia utendaji wa mahakama.
  Baadhi ya wadau na viongozi wa Sheria na Serikali katika meza kuu.
  Sehemu ya mahakimu, mawakili, wanasheria na wageni waalikwa katika maadhimisho hayo.(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  tecdenTanzania Early Childhood Development Network (TECDEN) is a network that is formed by various Organizations which are working to improve children livelihood in Tanzania.

  This Network was established in year 2000 and officially registered in 2004. The headquarters of the Network are based in Dar es Salaam. To date 2015, the Network has a total of more than 200 members’ organizations in 14 Administrative regions of Tanzania Mainland and Zanzibar.

  1. Goal: The Network aimed at improving the livelihood of young children in Tanzania through provision of various services to enable them grow to their full potentials.
  2. Objectives.

  2.1 Advocating for rights of young children and other issues that affecting young children in Tanzania 2.2 Mobilizing community members to actively participate in promoting early Childhood development in Tanzania through National campaign which is investing to a young child for National Development2.3 Coordinating information sharing among stakeholders on issues affecting young children in Tanzania2.4 Conducting research and situational analysis for the purpose of generating evidence based facts to feed Advocacy work to issues affecting young children in Tanzania.2.5 Strengthening capacities of member organizations on ECD issues to enable them to provide quality services to young children in their respective workplaces.
  3. Early Childhood Development Concept

  This is a total of all actions, practices and programs that are done to young children from pregnancy to the age of 8 years. The early years, the period up to 8 years of age, is a time of vital growth and development for the whole range of human capacities. This period starts when the child is in the womb and a newborn’s health is fundamentally dependent on its mother’s level of nutrition and care during pregnancy, for example, nutrition in utero has a major effect on adult height. 

  Following birth, adequate care of the newborn is also closely linked to the mother’s health and nutritional status. Up to the age of 8 years the young child grows rapidly particularly his/her brain. By the age of 8, while the average person has attained approximately 50% of their adult body weight, the brain has attained 90%. 


  Consequently, this is a time of great importance for cognitive, emotional and psychological development. Furthermore, there are critical periods when certain kinds of stimulation lead to particular kinds of brain development: emotional control, ages 0-2; vision, ages 0-2; social attachment, ages 0-2; vocabulary, ages 0-3; second language, ages 0-10; math/logic, ages 1-4; and music, ages 3-10 years. During this key development period, the number of cells in some areas of the brain can almost double within as little as a year. 

  The brains of children aged between two and three are 2.5 times as active as adult brains and remain more active for the first ten years of life.Based on these facts therefore there is a need to invest to young children to their early ages. The investment should be done on various thematic areas which includes; Child stimulation and parenting, Health, Nutrition, Education and Child Protection. If all these investment areas to a child are done effectively and efficiently then it guarantee holist child growth to their full potentials. 

  Children will grow physically, cognitively, communication skills, emotionally socially and spiritually. All these services need to available from family level, health facilities, children day care centres, Nursery schools, Primary schools especially standard one and two and the community at large.Children need to be given enough opportunity to learn, to play, to interact, to know the traditions so as to enable them growing holistically.

  TECDEN has been able to implement these activities under the financial support from Children in Crossfire from Ireland and Better Way Foundation from United States of America.

  For further information about TECDEN you can visit our offices which are located at Posta House opposite Ministry of Home affairs 3rd Floor room no 303. You can as well contact the Acting Executive Director through mobile No. +255 754 690556/714 818969 or through e mail ecdnetwork@gmail.com or ghumpibr@yahoo.com or visit our website www. Tecden.org

  0 0
 • 02/05/15--03:16: Article 12


 • 0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki na kisha kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mheshimiwa Javad Zarif na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo, Jumatano, Februari 4, 2015. PICHA NA
  IKULU  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone:255-22-2114512, 2116898
  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425


  PRESIDENT’S OFFICE,
        STATE HOUSE,
                1 BARACK OBAMA ROAD,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Tanzania imesema kuwa dhamira yake ya kufungua balozi katika baadhi ya nchi duniani iko pale pale na itatekeleza mpango wake huo kwa kadri hali ya fedha na uchumi inavyoruhusu.

  Aidha, Tanzania imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Iran katika kupambana na kukabiliana na ugaidi duniani kwa sababu nchi mbili hizo, kama ilivyo dunia nzima, zinahitaji dunia tulivu na inayosaka maendeleo ya watu bila usumbufu na matishio ya ugaidi.

  Mambo hayo mawili yamejadiliwa leo, Jumatano, Februari 4, 2015 katika mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mheshimiwa Javad Zarif.

  Mheshimiwa Zarif amewasili nchini leo akitokea Burundi katika ziara ambayo pia imemfikisha Kenya, Uganda na Rwanda akifuatana na maofisa wa Serikali na kundi kubwa la wafanyabiashara wa Iran.

  Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Zarif kuwa Tanzania bado inakusudia kufungua ubalozi mjini Teheran, mji mkuu wa Iran,  kama ilivyoahidi na kuwa itafanya hivyo hali ya kifedha na kiuchumi itakaporuhusu. Rais ametoa maelezo hayo kufuatia ombi la Waziri Zarif kukumbushia umuhimu wa kuwepo kwa ubalozi wa Tanzania katika Iran.

  “Tunakusudia kufungua balozi katika nchi marafiki ambako kwa sasa hakuna balozi ikiwamo Jamhuri ya Kiislam ya Iran. Katika Afrika, kwa mfano, tunapanga kufungua balozi katika Namibia, Angola, Algeria na Ghana. Hizi ni nchi rafiki ambazo baadhi yake zimekuwa na balozi katika Tanzania tokea uhuru wetu. Mbali na Iran katika Asia, tunaangalia nchi kama Uturuki, Qatar na Kuwait na nyingine marafiki,” Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Zarif.
  Kuhusu mapambano dhidi ya magaidi, Rais Kikwete amesema kuwa ni muhimu kwa Tanzania na Iran kuwa na msimamo ulio sawa wa jinsi ya kukabiliana na ugaidi. 

  “Wakati wote, sote tunakabiliwa na matishio ya ugaidi na hivyo tunalazimika wakati wote kuwa macho na uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi. Sisi Tanzania bado tunakumbuka shambulio dhidi ya Ubalozi wa Marekani hapa nchini. Ulishambuliwa Ubalozi wa Marekani lakini watu wote waliopoteza maisha yao ni Watanzania.”

  Rais Kikwete na Mheshimiwa Zarif pia wamejadili jinsi gani Tanzania na Iran zinavyoweza kuongeza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji katika maeneo mbali mbali ya uchumi na Rais Kikwete amemweleza Waziri fursa zilizoko katika sekta za nishati na reli.

  Waziri Zarif pia amemkumbusha Rais Kikwete mwaliko wa kumwomba Rais Kikwete kutembelea Iran kwa ziara ya Kiserikali.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  4 Februari, 2015
   


  0 0

  Baadhi ya Wanasheria ,Mahakimu na watumishi wa Mahakama wakiwa katika maandamano hayo yaliyopita katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi.
  Askari wa Kikosi cha kutuliza wakiwa tayari kwa ajili ya gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya siku ya Sheria nchini iliyadhmishwa Mahakama kuu kanda ya Moshi.
  Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Alishaeli Sumari akiongoza wageni wengine kuelekea katika viunga vya mahakama kuu kanda ya Moshi kwa ajili ya kukagua gwaride la heshima. 
  Askari wakiwa timamu kwa ajili ya gwaride la heshima mbele ya jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Alishaeli Sumari.(hayuko pichani)
  Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Alishaeli Sumari akipokea salamu za heshima toka kwa askari Polisi wakati wa gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya siku ya sheria.


  Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Alishaeli Sumari akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Sheria ambayo kwa mkoa wa Kilimanjaro yameadhimishwa katika mahakama kuu kanda ya Moshi.
  Baadhi ya Mawakili wa serikali na wale wa kujitegemea wakifuatilia tukio hilo.
  Baadhi ya Mahakimu wakiwa katika viunga vya mahakama kuu kanda ya Moshi.
  Jaji Mfawidhi Sumari akiwaongoza wageni wengine kuelekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya wageni .
  Baadhi ya wageni mbalimbali waalikwa wakiwemo watumishi wa mahakama wakifuatilia tukio hilo.
  Msajili wa Mahakama mkuu kanda ya Moshi,Hussein Mushi akisherehesha sherehe ya maadhimisho ya siku ya sheria iliyofanyika kimkoa katika mahakama kuu kanda ya Moshi.
  Baadhi ya wageni waalikwa katika maadhimisho hayo.
  Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi ,Munga Sabuni na mwenzake Julieth Mawole wakiwa katika viunga vya mahakama Kuu kanda ya Moshi.
  Baadhi ya Mahakimu na watumishi wa mahakama wakiwa katika sherehe hizo.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiteta jambo na jaji mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya moshi,Alishaeli Sumari wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo.
  Baadhi ya waviongozi waliokuwa meza kuu .
  Mawakili wakifuatilia kwa karibu tukio hilo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanzania Bara tawi la Moshi ,David Shilatu akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika kwa mkoa wa Kilimanjaro , mahakama kuu kanda ya Moshi.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akiteta jambo na Jaji Benedict Mwngwa wakati wa sherehe hizo.
  Mwanasheria Mfawidhi wa serikali ,Neema Mwanda akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria nchini ambayo kimkoa yamefanyika katika viunga vya Mahakama Kuu Kanda ya Moshi.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akitoa salamu zake katika maadhimisho hayo.
  Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Alishaeli Sumari akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo viongozi wa dini.
  Kikundi cha burudani ya ngoma cha Msanja hakikuwa nyuma katika utoaji wa burudani.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
  Brass Band ya Chuo cha Polisi Moshi ikiongoza maandamano siku ya Sheria nchini kwa mkoa wa Kilimanjaro.

  0 0

  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa viongozi wa dini wa mashauriano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha  Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)p5 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha  mashauriano cha viongozi wa dini kilichofanyika kwenye Kituo cha  Mikutano cha Kimataifafa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 3, 2015. Kulia ni ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam ,Alhad Salum Musa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)p4 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha viongozi wa dini cha mashauriano kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)p5 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha  mashauriano cha viongozi wa dini kilichofanyika kwenye Kituo cha  Mikutano cha Kimataifafa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 3, 2015. Kulia ni ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam ,Alhad Salum Musa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)p1p6 
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa viongozi wa dini wa mashauriano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha  Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
  p7 
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa viongozi wa dini wa mashauriano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha  Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu) p10 
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa viongozi wa dini wa mashauriano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha  Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu) p11 
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa viongozi wa dini wa mashauriano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha  Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu) p12p13 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Dr. Asha Rose Migiro katika mkutano wa mashauriano wa viongozi wa dini  uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere mjini Dar es salaam Februari 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) p14 
  Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na baadhi ya viongozi wa  dini baada ya kuzungumza katika mkutano wao wa  mashauriano uliofanyika kwenye  kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  jijini Dar es sala

  0 0

  unnamedMAWARais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha baraza la mawaziri mjini Dodoma leo(picha na Freddy Maro).

  0 0

  Mr. Bertin Mushi, Marketing Manager Promasidor Tanzania Ltd and Ms. Fatma Fernandes from Abel & Fernandes Company Ltd exchanging ideas with primary school children at the Launch of Hatua Jithamini TV show.
   Children from different primary schools at the launch of Hatua Jithamini Show which will be aired on Star TV every Saturday at 7.30 pm and TV1 at 11.30am.


  Education is more than just reading, writing, and arithmetic. It is one of the most important investments a country can make in its people and its future and is critical to reducing poverty and inequality.

  Education is a human right and it is also the gateway for children to realize their full potential in societies, and break the cycle of poverty. Nonetheless, many factors contribute to limiting the quality of the education that children receive, and hence their learning, that is, lack of textbooks, poor school infrastructure (overcrowded classes, absent children and teachers, poor use of classroom time), parents unable to monitor homework, developmental delays due to lack of early childhood interventions, inappropriate or insufficient learner assessment and limited teacher skills.

  An estimated 250 million children who attend primary school in developing countries are struggling to read even basic words. According to UNICEF’s 2014 report, in Tanzania the net primary school enrolment was 89.7% in 2013 however net primary school completion was just 55.3% in the same year. In addition, over the last two decades, national education policies and international aid for education have mainly focused on improving access to primary school and completion rates. Progress has been steady on these two indicators, but the focus has to shift to ensuring that children who attend school actually learn.

  According to the Managing Director of Abel & Fernandes Communications Fatma Fernandes, the producer of “Hatua Jithamini” campaign; “The challenge is not finding the problem – that’s easy. The hard part is identifying the solution. We believe that the impact of investing in education is profound; education results in raising income, improving health, promoting gender equality and reducing poverty. From the outset, we recognize that effective measurement of learning is most certainly not the same as improving learning, and that it is only one part of the solution to the many problems facing education especially here in Tanzania.

  Our production team visited 12 regions, that is, Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Tabora, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Iringa, Songea, Mtwara and Lindi to research on the barriers that hinder access to effective education. Among the challenges that have been addressed are poverty, gender disparity, disability, language, malnutrition, HIV and AIDS as well as cultural barriers.  Our hope is to not to find a one-fit all solution but to tackle each case sensitive issue and see a dramatic increase in the number of children learning.

  “Hatua Jithamini” program’s approach is focused on a multi-stakeholder inclusion thus educating students, teachers and parents through developmentally appropriate and culturally relevant, fun and participatory activities that involve social learning via the TV show.

   We acknowledge the efforts of the Ministry of Education for their initiatives to improve education in Tanzania and their support to this project. Moreover we also appreciate Promasidor Tanzania Ltd as the company is supporting the initiative through one of its brand, Cowbell milk which have all the necessary vitamins including vitamin A, C, D, E & K and minerals that are vital for child growth.

  Promasidor’s Marketing Manager, Mr. Bertin Mushi said, “Milk is widely acknowledged and recommended by physicians for strengthening the health of the brain as well as improving body defense systems as a good source of nutrition. We are genuinely proud to get an opportunity to help children and serve the future of the country. Milk is one of the most nutritious foods there is and we want to do what we can to make sure Tanzanian kids grow up drinking it every day.”

  Once children are in school, the next challenge is to ensure that they are actually learning to read, write and count as well as acquiring the life skills they will need to become productive members of society. In short, education has the power to make Africa and Tanzania a better place. We therefore urge parents and the community at large get on our bandwagon and be accountable and support the teachers in ensuring that children get quality education. If all students in low-income countries left school with basic reading skills 171 million people could be lifted out of poverty.

  About Abel & Fernandes: We are a PR, Communication and Strategic Consulting firm primarily based in Tanzania.  In communication, we use different innovative approaches to help organizations to reach audiences through interactive means such as documentary, behavior change campaigns and TV shows, which help learning in the organizations and development context at large to call for social changes.

  About Promasidor Tanzania Ltd: Promasidor Tanzania is a multi-local firm that has its roots firmly established in Africa. It produces, distribute and market quality range of products in 31 countries across the continent. Their products are Cowbell Milk, Cowbell Sweet Milk, Onga Mchuzi Mix and Drink-o-Pop juice powder (Orange, Cola, Blackcurrant and Pineapple).


  0 0

   Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika mazungumzo na viongozi wa jiji la Seattle nchini Marekani katika mazungumzo ya namna ya kuongeza watalii nchini kutoka katika jiji hilo.
   Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru (kulia) akimpa zawadi ya kinyago Naibu Meya wa jiji la Seattle nchini Marekani Bi. Kim mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
   Ujumbe wa Tanzania ulioshiriki katika ziara ya kutangaza vivutio vya utalii nchini katika soko la Marekani Magharibi.
   Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru (kulia) akipokea kitabu maalum chenye kueleze historia ya jjji la Seattle kutoka kwa Naibu Meya wa jiji la Seattle nchini Marekani Bi. Kim.
   Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru (kulia) akiongea na Naibu Meya wa jiji la Seattle nchini Marekani Bi. Kim alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo ya namna ya kuongeza watalii nchini kutoka katika jiji hilo.
  Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa akiongea katika ziara ya kutangaza vivutio vya utalii nchini katika jiji la Seattle nchini Marekani. 

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amesema adhma ya Serikali ya kuufanya mji wa Mpanda kuwa kitovu cha biashara katika ukanda wa magharibi itakamilika katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

  Amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa barabara za lami unaoendelea mkoani Katavi na kusisitiza barabara zote zinazounganisha mji wa Mpanda na mikoa mingine zitakamilika katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

  “Mkoa wa Katavi una mtandao wa barabara zinazohudumiwa na Wakala wa Barabara Nchini  TANROADS zaidi ya elfu moja na mia moja na kati ya hizo kilomita  474.3 ni barabara kuu na kilomita 627.16 ni barabara za mikoa”, amebainisha Waziri Magufuli.

  Katika ziara hiyo Dkt . Magufuli amekagua barabara ya Kateto-Kibaoni yenye urefu wa KM 20.27 na Sitalike-Mpanda yenye urefu wa KM 36.90  zinajengwa kwa kiwango cha lami.

  Amesisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuunganisha mkoa wa Katavi na mkoa wa Tabora,Kigoma na Rukwa kwa lami na hivyo kufungua ukanda wa magharibi ya Tanzania kiuchumi.

  “ Ni vema viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkatenga maeneo ya huduma za usafiri na makazi zinazoendana na kukua kwa mji huu ambao utaunganishwa na barabara za lami na kuwa njia ya wafanyabishara kutoka Uganda, Zambia, Congo, Rwanda na Burundi ili kunufaika kibiashara”, Amesisitiza waziri Magufuli.

  Amehimiza halmashauri ya wilaya ya Mpanda kutumia fedha za mfuko wa barabara  kujenga barabara za lami za mijini ili kuunga mkono juhudi za kuboresha mitaa katika mji wa mpanda ambao ndio makao makuu ya mkoa wa Katavi. Waziri Magufuli amekagua barabara ya Mpanda-Sitalike KM 36.9 ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 74 na kusisitiza mkandarasi kumaliza kazi hiyo kwa mujibu wa mkataba.

  Amewataka vijana kutumia fursa za ajira zinazojitokeza wakati wa miradi ya ujenzi vizuri ili wanufaike kiuchumi na kusisitiza umuhimu wa kuishi kwa umoja,uaminifu ,upendo na mshikamano ili kuleta maendeleo.

  Mapema akiwa wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa  mkuu wa mkoa wa Rukwa Eng. Stela Manyanya ameipongeza wizara ya ujenzi kwa kukamilisha ujenzi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga KM 225 kwa kiwango cha lami na kuomba ujenzi wa kiwango cha lami katika barabara Matai- Kasesha .

  Naye Kaimu mkuu wa mkoa wa Katavi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima amemweleza waziri Magufuli umuhimu wa kukamilisha barabara za lami mkoani humo kwa wakati kwani mkoa huo unajiandaa kuwa na uchumi wa nishati na gesi kutokana na utafiti unaoendelea katika ziwa Tanganyika hivyo uwepo wa barabara za lami itaufungua mkoa huo na kanda ya nchi za maziwa makuu.

  Imetayarishwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi.

  0 0

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wanaoishi na Saratani Zanzibar Dkt. Msafiri Marjani akitoa elimu juu ya ugonjwa wa Saratani katika mkutano wa maadhimisho ya siku ya Saratani Duniani uliofanyika ofisini kwao Mpendae Zanzibar.

  Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wanaoishi na Saratani Zanzibar Bi. Mwanahamisi Moh’d Abdalla ambae pia ni muhanga wa ugonjwa wa Saratani akitoa ufafanuzi jinsi alivyopambana na ugonjwa huo na hatimaye kupona kabisa  katika siku ya maadhimisho ya siku ya Saratani Duniani kwa upande wa Zanzibar.

  Naibu Waziri wa Afya Mhe. Mahamoud Thabit Kombo akizunguza na wajumbe na waandishi wa habari jinsi ya kuwaelimisha wananchi juu ya kupambana na ugonjwa huo.

  Mwandishi wa habari wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar Leo Nd. Abdi Shamna akiuliza swali kuhusiana na Tenzi Dume wakati wa maadhimisho hayo.

  PICHA NA ABDALLA OMAR       MAELEZO-ZANZIBAR

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akikabidhi
  funguo za trekta kwa Mwalimu wa Shule ya msingi Kwadelo Bw. Hamza Haji, matrekta saba yalikabidhiwa leo kwa wakulima chini ya usimamizi wa
  Diwani wa Kwadelo Alhaji Omari Kariati.(Picha na Adam Mzee)
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akikabidhi funguo za trekta kwa Dk. Edmund Mndolwa ambaye ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa ikiwa sehemu ya matrekta saba yaliotolewa na Alhaji Omari Kariati Diwani wa Kwadelo.
   Moja ya matrekta waliokabidhiwa wakulima ,Alhaji Omari Kariati ameshatoa matrekta 100 mpaka leo tarehe 5 februari 2015.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi matrekta saba kwa wakulima yaliyotolewa na Diwani wa Kwadelo Alhaji Omari Kariati ambapo aliwataka viongozi kushiriki shughuli za wananchi (Picha na Adam Mzee).
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu
  kuendesha trekta mojawapo kati ya matrekta saba aliyokabidhi funguo kwa
  wakulima kutoka sehemu mbali mbali nchini, waliopanda trekta hilo
  kushoto ni Mjumbe wa NEC kutoka Wilaya ya Korogwe Vijijini Dk. Edmund Mndolwa na kulia ni Diwani wa Kwadelo Alhaji Omari Kariati.(Picha na Adam Mzee)
   Mafundi wakiendelea kuunganisha matrekta ya Kariati ambayo yametolewa na Alhaji Omari Kariati.
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Kariati inayoshughulika na matrekta ya kilimo Kinondoni Vijana Jijini Dar es salaam.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na MNEC wa Korogwe Vijijini Dk. Edmund Mndolwa (kushoto) kulia ni Diwani wa Kwadelo Alhaji Omari Kariati kwenye ofisi ya Kariati inayoshughulika na matrekta ya kilimo Kinondoni Vijana Jijini Dar es salaam.(Picha na Adam Mzee)

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa PDB Bw. Omari Issa akielezeaumuhimu wa sekta ya Afya kuingia BRN kuungana na sekta nyingine zilizotangulia zinazoendelea kuzaa matunda
  kip2
  Dr Linda Ezekiel ambae ni Mkurugenzi wa sekta za jamii (Afya, Elimu na Maji) PDB akiwasilisha mada kuhusu malengo ya kipaumbele sekta ya afya kwa miaka
  kip3
  Bw. Omari Issa akimkabidhi mwakilishi wa wahisani wa maendeleo mkakati wa sekta ya Afya chini ya BRN
  kip4
  Mmoja wa wahisani akisisitiza umuhimu wa wizara ya afya kuwajibika ki BRN katika maeneo mengine yasiyo ya kipaumbele katika BRN
  kip5
  Dr Oberline Kisanga wa kitengo cha mageuzi katika wizara ya afya akifafanua ushiriki wa TAMISEMI katika mkakati huu wa afya chini ya BRN
  kip6
  Mwakilishi wa jumuiya ya wahisani akipongeza uamuzi wa serikari kuiweka sekta ya afya katika BRN
  …………………………………………………………………………………………
  Annastazia Rugaba, PDB habari, 05 Februari 2015.

  Mtendaji mkuu wa Ofisi ya Rais, usimamizi wa utekelezaji wa miradi (PDB) Bwana Omari Issa, leo amekabidhi rasmi taarifa ya mkakati wa kuboresha sekta ya afya chini ya BRN kwa jumuia ya wahisani wa maendeleo. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za PDB ambapo jumuiya ya wahisani ilipata fursa ya kusikiliza kwa kina namna BRN inavyofanya kazi ya kuleta matumaini mapya kwa watanzania kupitia sekta za kipaumbele.

  Sekta ya afya imekuwa ikijaribu kuboresha utendaji wake lakini kuingia katika BRN kutaleta tija Zaidi. BRN inaamini katika misingi mikuu ambayo ni kuweka vipaumbele, kuwa na adabu ya utekelezaji, uwajibikaji na uaminifu, ufuatiliaji wa kina na wa mara kwa mara na Mawasiliano thabiti kati ya watoa huduma na wapokea huduma. Hizi ni nguzo muhimu zitakazotufikisha katika dira ya maendeleo ya taifa ya Mwaka 2025.

  Awamu ya kwanza ya BRN iliziangazia sekta sita ambazo ni Kilimo, Elimu, Maji, Uchukuzi, Nishati na ukusanyaji wa mapato ambapo sekta za Afya na Uboreshaji wa mazingira ya Biashara zimeanza rasmi Mwaka huu. Sekta sita za mwanzo zimedhihirisha mafanikio anuwai ambayo yaliwavutia jopo la wataalamu wa maendeleo wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Botswana Bw Mogae. Ripoti kamili ya utekelezaji wa BRN kwa Mwaka wa kwanza itazinduliwa rasmi mapema mwezi Machi Mwaka huu.

  Sekta ya afya inakusudia kutekeleza vipaumbele vine ambavyo ni mosi; ugawanyaji sawia wa wahudumu wa afya wenye ujuzi takikana kuanzia ngazi ya chini ya afya ya msingi, pili; utoaji huduma wenye ubora wa nyota tatu katika ngazi zote, tatu; upatikanaji wa dawa na bidhaa muhimu za afya katika ngazi zote, nne; kuimarisha afya ya uzazi na usalama wa mama na mtoto ili kupunguza vifo vya kundi hili muhimu kwa angalau asilimia 60 ifikapo Mwaka 2018.
  Jumuiya ya wahisani wamepongeza uamuzi wa kuiingiza sekta ya afya katika BRN na wakithibisha utayari wao wa kufanikisha mkakati huu, wametoa wito kwa wizara ya afya, PDB, Sekta binafsi na jamii ya kitanzania kwa ujumla kuhakikisha kuwa mkakati huu utafanikiwa.

  Malengo haya yote yanahitaji juhudi kubwa na ya pamoja kutoka kwa jamii, wizara na taasisi zake zote hadi ngazi ya kijiji, wahisani wa maendeleo na sekta binafsi. “tusingoje nani aanze, sote tuwajibike, kila mmoja ajitazame kama anawajibika ipasavyo. Dira ya maendeleo ya Taifa tunayotaka itupeleke kuwa nchi yenye uchumi wa kati haiwezi kufikiwa tusipofanya kazi kwa pamoja bila kunyoosheana vidole. BRN ni treni iliyoanza safari tayari, kila mmoja anawajibika kuingia kwa wakati na kwa nia Chanya, ukichelewa ukakuta imeondoka bado una fursa ya kuikimbilia kituo kinachofuata ili twende pamoja” Bw Omari Issa ametoa wito huo kwa wahisani wa maendeleo na jamii kwa ujumla.

  0 0

   Mbunge wa Bunge kla Afrika Mashariki ambaye pia ni mkazi wa Mbweni, Shy Rose Bhanji akiwa na Mwenyuekiti wa Serikali ya Mtaa Mbweni-Malindi, jijini Dar es Salaam, Bariki wakisimamia ukarabati wa barabara yao leo.
   Mbunge wa Bunge kla Afrika Mashariki ambaye pia ni mkazi wa Mbweni, Shy Rose Bhanji akielekeza jambo kwa mkandarasi.
  Barabara ya Mbweni-Malindi inavyonekana baada ya kuanza kufanyiwa ukarabati.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran Mohammed Javad  Zarif alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.]
  shei2 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akizungumza na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran Mohammed Javad  Zarif (wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.]shei3 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  akizungumza na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya  Kiislamu ya Iran Mohammed Javad  Zarif (kulia kwa Rais ) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.]

  0 0


  Na Bashir Yakub

  Yapo mambo  ambayo huwaumiza  watu vIchwa  yumkini  yakiwa   ni mambo madogo na ya kawaida.  Tatizo mara nyingi  huwa ni taarifa. Taarifa  zikimfikia  mtu ndipo huhisi jambo  ambalo alikuwa halijui  kuwa ni jepesi. 

  Lakini kabla  ya taarifa mtu  huendelea kufikiria jambo hilo kwa ugumu. Katika kipindi kama hiki kuwa na kitu kama pasipoti si jambo la  anasa  au ufahari tena isipokuwa ni jambo  ambalo limeishaingia katika matumizi ya kawaida   ya kila siku ya walio wengi. 
  Hii ni kutokana na kukua kwa  biashara za kimataifa, mawasiliano, utalii,usafirishaji  na kila kitu ambacho husababisha  watu kutoka nchi moja hadi nyingine.  Kwasasa kuwa na pasipoti  hata kama huna safari ya hivi karibuni ni jambo muhimu sana. 
  Yumkini  usisubiri ikutokee safari ya ghafla halafu ndio uanze kukimbizana  na  pasipoti. Pasipoti inayo manufaa mengi  lakini moja ni kuwa pasipoti  ni mali kama mali nyingine. Pasipoti inaweza kumdhamini mtu kama  mali nyingine inavyoweza kumdhamini  mtu.Pasipoti  ni amana tena amana ya kuaminika. Ni  kutokana na umhimu huu nikaona leo nieleze  pasipoti na namna ya kupata pasipoti. 

  Kusoma Zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  exim1 
  Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim, Bi. Elizabeth Mayengoh, akikabidhi vitabu kwa mmoja wa watoto waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenye wodi maalum ya watoto wanaougua ugonjwa wa saratani katika kuadhimisha siku ya saratani duniani. Wanaoshudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim na wazazi wa watoto hao. Benki hiyo ilikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya kuchezea, sabuni, vifaa vya shule nk, lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusiana na ugonjwa wa saratani mpango unaoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Saratani Duniani inayosema kuwa tatizo la saratani “lipo ndani ya uwezo wetu”.
  exim2 
  Meneja masoko msaidizi wa Benki ya Exim, Bi. Anita Goshashy akishikana mikono na Dr. Livin Mumbari  Daktari wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi vifaa mbalimbali kwa watoto waliolazwa hospitalini hapo kwenye wodi maalum ya watoto wanaougua ugonjwa wa saratani katika kuadhimisha siku ya saratani duniani. 

  Wanaoshudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim na wazazi wa watoto hao. Benki hiyo ilikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya kuchezea, sabuni, vifaa vya shule nk, lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusiana na ugonjwa wa saratani mpango unaoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Saratani Duniani inayosema kuwa tatizo la saratani “lipo ndani ya uwezo wetu”.

  0 0

   MOJA ya makampuni makubwa yanayoshughulika na ushauri wa jinsi ya kuongeza ufanisi katika maeneo ya kazi, NFT Consult wameendesha kongamano kubwa la kutambua haja ya mahitaji ya wadau mbalimbali wa maendeleo hapa nchini. Kampuni hiyo ya kimataifa ambayo imeingia nchini mwaka 2010 ikiwa na matawi Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini imesema kongamano hilo limelenga kuonesha uwezo wao katika kubadili mifumo ya utendaji kazi.

  Ofisa Mtendaji wa kampuni hiyo, Badru Ntege amesema kwamba wamekuwa wakiendesha mafunzo mbalimbali yenye kueleza thamani ya mfanyakazi na mdau wowote ambapo uthamini wa wadau ndio unaotoa mwanya wa mabadiliko chanya yanayotakiwa “Mafanikio ya eneo lolote lile linatokana na wadau kusikiliza wenzao na kisha kufanyia kazi kauli za upande wa pili.” Alisema Ntege.
  DSC_0361
  Timu ya NFT Consult ikijitambulisha kwa washiriki kabla ya kuanza warsha hiyo. Kutoka kushoto ni Inside Business Partner wa NFT Consult, Aisu Mori, Client Partner wa NFT Consult, Immaculate Mwaluko, Ofisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya NFT Consult, Badru Ntege, Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong na Client Partner wa NFT Consult, Sophia Shuma.

  Alisema katika mafunzo ya kuthamini ,kanuni kubwa inayotumika ni kujipanga katika nafasi husika na kutumia changamoto kama fursa za kubadili mazingira ya kazi na kazi yenyewe ili kupata matokeo yanayotakiwa.

  Alisema kwamba changamoto zinazotolewa na wadau katika kubadilisha mazingira yao ndio zinatumiwa na kampuni hiyo katika kuhakikisha makampuni na taasisi zinazotoa huduma zinazokidhi haja kwa muda unaotakiwa katika mazingira yanayobadilika kwa kasi.

  Naye Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong akizungumzia shughuli wanazofanya alisema kwamba lengo kubwa ya warsha ya jana ni kuwaeleza wadau nini wanachoweza kuwapa ili wabadili mazingira yao ya kazi.
  _DSC0594
  Pichani juu na chini ni Ofisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya NFT Consult, Badru Ntege akitoa mada kuhusu mifumo saba ya kitabia katika utendaji wa kazi kwa maofisa rasilimali watu na watoa mafunzo kutoka makampuni mbalimbali nchini kwenye warsha ya siku moja iliyoratibiwa na kampuni ya JB's PR and Events.

  Alisema watu wengi wamechoshwa na mazingira yale yale na kukata tama lakini kupitia mafunzo yao wamekuwa wakihakikisha kwamba wadau wanapata msukumo mpya wa kufanyakazi na kupata matokeo chanya kwa kasi.

  Alisema kwamba tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo imefanikiwa kubadili wadau wao na kuanza kutambua kuthamini watu, kuwasikiliza na kujadiliana nao ili kupata matokeo yanayotakiwa. Alisema kwa sasa NFT Consult imepata uzoefu na kufanyakazi katika nchi 6 za kusini mwa jangwa la sahara.

  Nchi hizo ni Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
  Amesema mabadiliko makubwa katika namna ya kusimamia shughuli kunawezesha mabadiliko ya utendaji na kuleta ufanisi.
  _DSC0585
  Alisema kazi ya taasisi hiyo pamoja na kusaidia uwapo wa menejimenti na rasilimali watu zenye uhakika pia husaidia kupatikana kwa kada inayotakiwa kwa taasisi mbalimbali wakiombwa kufanya hivyo.
  Nao washiriki kutoka TGNP waliohojiwa wakati wa mafunzo hayo walisema ipo haja kampuni hiyo ikaongea na watendaji wa serikali ili wakapatiwa mafunzo yatayogeuza changamoto kuwa fursa za kuleta tija katika uendeshaji wa serikali.
  _DSC0672
  Washiriki wakijaza chemsha bongo wakati warsha hiyo ya siku moja kwa maofisa rasilimali watu na watoa mafunzo kutoka makampuni mbalimbali nchini. “Mafunzo haya yanawezesha kutambua ubora wa kuthamini na kuhakikisha unasikiliza kila mtu kwa ajili ya maendeleo, na changamoto za serikali mafunzo haya yanafaa sana kwao” alisema Shakila Maimana.
  Alisema anaamini mafunzo hayo yanaweza kugeuza changamoto kuwa fursa za maendeleo.Naye Diana Sembende alisema kwamba mafunzo hayo yamembadilisha na anaamini kwamba serikalini watumishi wanayahitaji sana.
  _DSC0676
  Kwa matukio zaidi ingia humu
  DSC_0252
  Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyoendeshwa na kampuni ya NFT Consult kwa maofisa rasilimali watu na watoa mafunzo kutoka makampuni mbalimbali nchini wakifanya usajili kabla ya kuanza kwa warsha hiyo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).


older | 1 | .... | 455 | 456 | (Page 457) | 458 | 459 | .... | 1897 | newer