Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live

TFDA kufungua ofisi kanda ya kusini

$
0
0
 Mkurugenzi mkuu  wa TFDA, Hiiti Sillo (katikati), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Halima Dendegu (wa kwanza kulia), katika ziara yake ya  kikazi mkoani Mtwara ikiwa ni harakati za awali za TFDA kufungua ofisi ya Kanda ya Kusini kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi. Kushoto ni Mfamasia wa mkoa wa Mtwara Bw. Musa Nasoro.

KAMPUNI YA IBRALINE YATANGAZA NAULI MPYA KWA MABASI YAKE,ABIRIA SASA KULIPA NUSU BEI YA SUMATRA.

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Moshi.
SIKU chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kutangaza punguzo la bei ya Mafuta Kampuni ya kutoa huduma ya usafirishaji wa ndani na nje ya nchi ya Ibraline imetangaza kushusha nauli kwa nusu ya bei elekezi ya SUMATRA.

Hatua hiyo inakuja wakati baadhi ya wananchi kulalamika kutokuwepo na ahueni yoyote licha ya kwamba serikali imetangaza kushusha bei ya bidhaa ya Mafuta kwa nchi nzima kufuatia  bidhaa hiyo kushuka bei katika soko la dunia.

Akizungumza ofisini kwake mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ibrahimu Shayo alisema Kampuni imefikia hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa wateja wake ambao wamekuwa wakitumia huduma ya usafiri inayotolewa na Ibraline.

“Tumeamua kufanya hivi lengo ni kuwashukuru wateja wetu wanao tumia huduma ya usafiri unaotolewa na kampuni yetu ya Ibraline…ningewajua mmoja mmoja ningeweza kuwapa mkono lakini kwa kuwa wanaishi maeneo tofauti ndio sababu tumeamua kurudisha kile tunachopata kwa njia ya kuwapunguzia bei.”alisema Shayo.

“Hivyo basi kuanzia sasa magari yetu yatatoa huduma zake kwa nusu ya bei elekezi inayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti, Usafiri wa nchi Kavuna Majini (SUMATRA) ambapo abiria watatozwa kiasi cha Shilingi 17,000 badala ya 33,300 kwa usafiri wa kwenda na kutoka Dar es Salaam wakitokea Arusha.”aliongeza Shayo.

Alisema unafuu wa ofa hiyo abiria wataipata endapo watafika moja kwa moja katika ofisi za kampuni hiyo zilizoko Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam badala ya kutumia mawakala wanaopatikana katika vituo vikuu vya mabasi katika mikoa hiyo.

“Unafuu wa gharama ya nauli utaipata pekee endapo utafika ofisi za kampuni yetu zilizoko mikoani ambapo kwa Arusha ofisi ziko Kibla,Kilimanjaro tunapatikana barabara ya Ghala jirani na kiwanda cha kubangulia Kahawa (Cofee Curing) na Dar es Salaam tuko Ubungo ofisi namba 19.”alisema Shayo.

Aidha Shayo alisema hivi sasa Kampuni yake imeanzisha safari za kuelekea Masasi mkoani Mtwara baada ya kupokea maombi ya wakazi wa maeneo hayo na kampuni kuamua kutoa gari tatu za kisasa kwa ajili usafiri wa kuelekea huko.

Alisema kampuni ya Ibraline inategemea kuanza kutoa huduma ya usafiri kwa mikoa zaidi ya nane na kwamba kinachofanyioka sasa ni kuangalia uwezekano wa namna gani inaweza kuingia mikoa ya Dodoma ,Morogoro na
Mbeya.

Juzi baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro walidai hakuna haueni yoyote wanayopata licha ya kushuka kwa huduma hiyo.

Baadhi ya wakazi hao ,Joachim Kimaro, Andrea Lyimo na Yusta Mafangavo waliliambia globu ya Jamii kuwa wanaofaidika na kushuka kwa bidhaa za Mafuta zaidi ni wamiliki wa vyombo vya usafiri .

“Wamiliki wa magari ya biashara kama mabasi na magari makubwa ya kusafirisha mizigo ndio wamenufaika na kushuka kwa bei ya mafuta ,kwa sababu nauli za kusafiria hata kusafirisha mizigo hazijashuka bado ziko pale pale.”alisema Kimaro.

Alisema wengine wanao nufaika na kushuka kwa bei ya mafuta ni wafanyabiashara wa bidhaa katika maduka ambao licha ya kununua mafuta ya taa kwa bei elekezi ya EWURA bado wameendelea kuuza bidhaa hiyo kwa mtumiaji wa kawaida kwa bei ile ile ya zamani.

TAARIFA KWA UMMA

$
0
0
MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI (EWURA).
Kuna taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, kuelezea kwamba kutakuwa na mgomo wa wafanya biashara wa mafuta nchini, na kwa hiyo kutakuwa na uhaba wa mafuta ya jamii ya petroli. 

Aidha, taarifa hizo zinawachochea watumiaji wa bidhaa hizo kununua kwa wingi ili kuepuka usumbufu. 

EWURA inapenda kuutaarifu umma kwamba taarifa hizo si za kweli, hakuna mgomo wala tatizo lolote linaloweza kuhatarisha upatikanaji wa mafuta nchini, na kwamba nchi ina akiba ya kutosha ya mafuta, na hakuna haja ya wadau kuwa na wasi wasi. 

Umma unakumbushwa pia kuzipuuza taarifa za namna hiyo kwa sababu ni za upotoshaji na zinalenga kuvuruga hali ya utulivu wa soko la mafuta nchini. Ikumbukwe pia kwamba ni EWURA tu yenye mamlaka ya kisheria ya kuutaarifu umma juu ya hali ya soko la mafuta na upatikanaji wa bidhaa zake. 

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano, EWURA.

Sitta awapongeza waandaaji wa Tamasha la Pasaka kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake

$
0
0
 WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta ameelezea kufurahishwa na waandaaji wa Tamasha la Pasaka na kusema kuwa katika miaka 15 ya tamasha hilo wana mengi ya kujivunia.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa kamati yake imepokea salamu kutoka kwa Waziri Sitta akizungumzia maandalizi ya miaka 15 ya tamasha hilo.
 
“Ni tamasha lenye tija kwa Watanzania, mimi mwenyewe nimekuwa shahidi wa namna mnavyosaidia yatima, wajane na makundi mbalimbali ya kijamii.
 
“Nimesikia mwaka huu mna tamasha kubwa la miaka 15 tangu muanze kufanya Tamasha la Pasaka, niwatakie kila la heri katika maandalizi na naamini litakuwa tamasha la aina yake,” alisema Msama katika taarifa yake akimnukuu Sitta.

Alisema wamekuwa wakipokea salamu kutoka kwa wadau mbalimbali wakizungumzia kuhusiana na maandalizi ya Miaka 15 ya Tamasha la Pasaka na wakielezea pia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kwa kipindi hicho.

Baadhi ya walioguswa na maandalizi ya tamasha hilo ni waimbaji mahiri wa muziki wa Injili kutoka Afrika Kusini Solly Mahlangu ‘Obrigado’ na Rebecca Malope.

 Wasanii hao wamewahi kwa nyakati tofauti kuja nchini katika Tamasha la Pasaka, ambapo mwaka huu waandaji wamepanga kufanya sherehe ya Miaka 15 ya Tamasha la Pasaka.
 

JESHI LA POLISI NCHINI LASHIRIKI KUZINDUA MAGARI MAPYA YA KAMPUNI YA ULINZI YA SECURITY GROUP AFRIKA JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa akiwa na mkuu wa jeshi la polisi mstaafu Philimon Mgaya akikata utepe wa kuashiria kuzindua magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Katikati yao ni mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Eric Sambu.
 Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi nchini Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa  akipokea msaada wa pikipiki mbili aina ya Boxer toka kwa mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya Security Group Africa ambae pia ni mkuu wa  jeshi la polisi mstaafu Philimon Mgaya kwaajili ya kusaidia jeshi hilo katika oparasheni mbalimbali za kupambana na uhalifu,Katikati yao ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SGA nchini  Eric Sambu.
 Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SGA nchini  Eric Sambu akizungumza kwenye hafla ya kuzindua magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za kampuni hiyo Mbezi Beach jijini Dar Es Salaam.
 Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi nchini Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa  akikagua gwaride maalum la kuashiria kuanza kwa shuguli ya kuzindua magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Kulia kwake ni mkuu wa kitengo cha mafunzo cha SGA bwana Rogers Lumwaji.
 Mwakilishi wa Mkuu wa jeshi la polisi nchini Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa  akipeperusha bendera kuashiria kuanza kutumika kwa magari magari mapya Zaidi ya ishirini ya kampuni ya ulinzi ya Security Group Africa ambayo yataanza kutumika katika kazi mbalimbali za kampuni hiyo hivi karibuni.Katikati yao ni mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Eric Sambu.

WADAU WA VUNJO WAMTAKIA HEPI BESDEI KAMANDA WAO INNOCENT.

$
0
0
Naibu kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wilaya ya moshi vijijini ambae pia anatajwa kutakiwa kuwania ubunge jimbo la vunjo Innocent Melleck shirima leo 06/02/2015 ni siku yake ya kuzaliwa. Kwa niaba ya vijana na wananchi wa jimbo la vunjo tunamtakia afya njema na Mwenyezi Mungu ambariki kuwa na umri mkubwa mara dufu.Tupo nae katika kutekeleza ndoto za maisha yake mwaka huu 2015.

MEYA MANISPAA YA MOSHI AWASEMEA WATENDAJI WANAO HUJUMU MALI ZA UMMA KWA WANANCHI

$
0
0

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi na Mwenyekiti wa Chadema Manispaa ya Moshi Jafary Michael akiwahutubia wakazi wa mji wa Moshi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Manyema mjini Moshi.
Baadhi ya wananchi wakiwa barabarani kumsikiliza Meya wa Manispaa ya Moshi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Manyema.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Meya wa Manispaa ya Moshi ,Jafary Michael katika viwanja vya Manyema ,Meya Jafary alikuwa akizungumzia vitendo vya Uporaji wa Viwanja vya Umma pamoja na tatizo la wafanya biashara ndogo ndogo  maarufu kama wamachinga.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii Kanda ya Kaskazini.

UKEKETAJI BADO NI TATIZO SUGU TANZANIA,LHRC NA MASHIRIKA MENGINE WATOA NENO NZITO,SOMA HAPA

$
0
0
Mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC ndugu HAROLD SUNGUSIA akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam juu ya siku ya kupinga ukeketaji duniani
 NA EXAUD MTEI
Ikiwa leo ni siku ya kupinga  vitendo vya ukeketaji duniani imeelezwa kuwa  bado mapambano dhidi ya ukatili huo hapa nchini kwetu Tanzania yanahitaji nguvu ya ziada kwani bado baadhi ya mikoa imekuwa sugu katika vitendo hivyo ambapo serikali imetakiwa kuchakua hatua mara moja juu ya watu ambao wanahusika katika vitendo hivyo.

Akizungumza na wanahabari leo mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC akiwakilisha mashirika zaidi ya 15 yanayohusika na ukeketaji nchini Tanzania wakili HAROLD SUNGUSIA amesema kuwa mwaka 2014 umeshughudia watoto wengi wakikeketa, pamoja na jitihada za kutokomeza vitendo hivyo ambapo ametolea mfano wilaya ya tarime pekee takribani watoto 1400 walikeketwa na watoto hao ni kutoka katika koo za bukira watoto 212,bukenye watoto 230,iregi watoto 800,pamoja na nyabasi watoto 160,ambapo ni idadi kubwa sana na ikizingatiwa kuwa ni wilaya moja tu.
IMELDA URIO ambaye ni mkurugenzi wa uwajibikaji na uwezeshaji kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC akizungumza na wnahabari 
 Amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa sheria zinazolikemea tatizo hilo bado cha kusikitisha ni kuwa mila hii imekuwa ikitekelezwa kwa kasi sana katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania katika baadhi ya jamii zetu.

“tunaitaka serikali kwa kupitia jeshi la polisi kusimamia sheria na kuwachuklia hatua za kisheria watu wote watakaobainika kufanya vitendo hivi”amesema SUNGUSIA
Ameongea kuwa ukeketaji ni kosa la jinai, na kosa la jinai huwa haliishii yani halina ukomo wa muda hivyo wanatarajia kuwa kama serikali inamaanisha kweli kupinga ukeketaji huo basi iweze kufwatilia huko vijijini na kuwabaini wale wote wanaoshiriki kukeketa watoto na kuwachukulia hatua stahiki
Mwakilishi kutoka chama cha wanahabari wnawake tanania TAMWA bi GOGFUDA JOLA akizngumzia kuhusu shirika lao linavyoshgulikia tatizo la ukeketaji katika maeneo mbalimbali nchini.
Wasaka habari wakiwa wanasikiliza kwa makini 
Aidha mashirika hayo yanayotetea na kupinga vitendo vya ukeketaji wamewaomba wadau wengine na watanzania kwa ujumla kujiuga kwa pamoja kupinga vitendo hivyo kwani ni vitendo vya kikatiki kwa mtoto wa kike na ni kumnyima haki zake za msingi kama mwanadamu,ikiwa ni pamoja na kutoa elimu zaidi juu ya madhara ya ukatili huo.

Baadhi ya mashirika ambayo leo wameungana kwa pamoja kupinga vitendo hivyo ni TAWLA,TAMWA,DIAC,CCT,WORD VISSION,NAFGEM,AFNET,WOWAP,CDF,WLAC,TGNP MTANDAO,WILDAF,BAKWATA,TGNP pamoja na HOUSE OF PEACE.
TAMKO NZIMA LIKO CHINI





MAHAKAMA: MACHA MNUNUZI HALALI NYUMBA YA BALENGA

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imethibitisha kwamba mfanyabiashara Hans Macha alinunua nyumba kwa kufuata utaratibu na kihalali kutoka kwa Ramadhani Balenga.

Hayo yalithibitishwa leo kupitia hukumu iliyosomwa na Hakimu Mkazi Frank Moshi kwa niaba ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, ambaye alisikiliza kesi ya kughushi inayomkabili Macha.

Katika kesi hiyo, Macha alikuwa akikabiliwa na mashitaka matatu ya kughushi hati ya umiliki wa kiwanja kilichopo eneo ya Kigogo, Dar es Salaam, kinachodaiwa kuwa mmiliki wake ni Ramadhani Balenga.

Pia alikuwa anadaiwa  kughushi mkataba wa mauziano wa eneo hilo kuonyesha kwamba Balenga alihamisha umiliki wa kiwanja hicho kwenda kwake na kuwasilisha nyaraka ya kughushi.

"Mahakama imepata muda wa kutosha wa kupitia ushahidi na vielelezo vyote. Makosa yote matatu hayajathibitishwa ipasavyo. Mlalamikaji  (Balenga), alimuuzia mshitakiwa eneo hilo kwa kufuata utaratibu na kihalali," alisema Hakimu huyo.

Alisema mahakama inamuachia mshitakiwa kwa mashitaka yote matatu na mlalamikaji ana nafasi ya kukata rufani.

Baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Nassoro Katunga, aliuliza iwapo nakala ya hukumu ipo tayari, ambapo Hakimu Moshi alimwambia haipo tayari na kama wanaitaka wafuate taratibu kwa kuwasilisha maombi mahakamani hapo.

Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, upande wa Jamhuri uliita mashahidi na upande wa utetezi ulileta mashahidi takriban 10 akiwemo mshitakiwa mwenyewe na aliyekuwa mke wa mlalamikaji Balenga, Nury Ahmadi.

Baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wao, Novemba, mwaka jana, mahakama hiyo ilimuona Macha ana kesi ya kujibu nahivyo kutakiwa kuwasilisha utetezi wake.

Wakati akijitetea mfanyabiashara Macha alidai tuhuma zinazomkabili ni za uongo na kuiomba mahakama kumuachia huru.

Katika utetezi wake, mfanyabiashara Macha aliiomba mahakama huyo kutupilia mbali mashitaka hayo kwa kuwa tuhuma hizo ni za uongo na Balenga anajua wazi kwamba alimuuzia hiyo nyumba namba 183 kitalu A iliyoko Kigogo.

Akiongozwa na Wakili Deo Ringia, Macha alidai alikuwa akimkopesha Balenga fedha huku akiweka dhamana hati za nyumba, hadi deni lilipofikia sh. milioni 879  ambalo hakuwahi kulilipa.

"Baada ya kushindwa kulilipa nilipomuuliza aliniambia makontena yake yalikamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hivyo hakuwa na fedha ya kunilipa tena.

"Alinijulisha ana hati nyingine ya nyumba ya ghorofa tano iliyoko Kigogo, hivyo aniuzie na nyumb nyingine ya Manzese ambayo hati yake nilikuwa nayo na nimuongeze na sh. milioni 20," alidai

Macha alidai Balenga alimuambia  nyumba ya Kigogo,  amekopea mkopo benki ya Azania, hivvyo hati ipo huko na kumwahidi ataenda kuitoa ili wabadilishane kwa kumuuzia hiyo nyumba na kumuongezea sh. milioni 20  na baada ya hapo amrudishie hati nyingine nne alizokuwa amezishikilia.

"Makubaliano hayo tuliweka maandishi ya mauziano baada ya kuletya hati yake ya Kigogo. Hiyo ilikuwa mwaka 2011, nyaraka ya mauziano nakumbuka ilikuwa mkataba wa mauziano na pande zote mbili mimi na Balenga tulitia saini ofisini kwangu katika hoteli ya Rick Hill, iliyoko mtaa wa Kipata, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam," alidai

Alidai wakati wanatiliana saini kulikuwa na mashahidi ambao ni Mashaka (mjomba wa Balenga), David (rafiki wa Balenga) na John Mboya na mkataba huo ulishuhudiwa na wakili Henry Mkumbi  ambaye aligonga mhuri baada ya kumueleza makubaliano yao  na alimkabidhi Balenga sh. milioni 20 mbele ya wakili huyo.

Macha alidai baada ya mauziano walitia saini hati ya kubadilisha umiliki na Balenga alimkabidhi nyaraka nyingine zinazohusiano na jengo hilo zikiwemo kibali halisi cha ujenzi, ofa ya jengo, michoro halisi ya jengo inayotoka Manispaa, mkataba alioingia na mjenzi na risiti mbalimbali.

Alipoulizwa na wakili anaielezeaje mahakama kuhusu madai ya Balenga kwamba hajamuuzia nyumba hiyo, Macha alidai ni ya uongo kwa kuwa alimuuzia na Balenga anajua kwamba alimuuzua hiyo nyumba.

Shahidi mwingine alikuwa aliyekuwa mke wa Balenga, Nury Ahmadi ambaye aliieleza mahakama kuwa mlalamikaji alimtamkia kwamba amemuuzia nyumba Macha.

Mashahidi wengine wa upande wa utetezi walikuwa mawakili wa kujitegemea Henry Mkumbi na Castro Rweikiza, ambao walidai walishuhudia utiliaji saini wa mkataba wa mauziano  baina ya Balenga akiwa muuzaji na Macha mununuzi na hati ya kuhamisha umiliki. Walidai katika nyaraka hizo, wao walitia saini na kugonga mihuri ya ofisi zao.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMFARIJI JAJI MSTAAFU AGOSTINO RAMADHANI KWA KUFIWA NA MAMA YAKE MSAZI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya M uungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu cha kumbukukmbu kufuatia kifo cha mama mzazi wa Jaji Mkuu mstaafu Agostino Ramadhani nyumbani kwake Kimara leo Februar 06, 2015 alipofika kwa ajili ya kumfariji.
 Maka wa Rais wa Jamhuri ya M uungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwafariji wana familia ya Jaji Mkuu mstaafu Agostino Ramadhani alipomtembelea nyumbani kwake Kimara leo Februar 06, 2015,  kutokana na kufiwa na mama yake mzazi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Jaji Mkuu mstaafu Agostino  leo alipomtembelea nyumbani kwake kimara leo Februar 06, 2015 kwa ajili ya kumfariji kutokana na kufiwa na mama yake mzazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Jaji Mkuu mstaafu Agostino Ramadhani Baada ya kumfariji kutokana na kufiwa na mama yake mzazi alipomtembelea nyumbani kwake Kimara leo Februar 06, 2015. (Picha na OMR)
 

Airtel yaitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi kwa wakazi wa Arusha

$
0
0
Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (katika)  akiongea na wandishi wa habari wakati wa kuitambulisha promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Mkoani Arusha wakishuhudia Meneja Mauzo kanda ya kaskazini Bwana Brighton Majwala na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma .

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetambulisha promosheni yake ya Airtel yatosha kwa wakazi wa Arusha  na kusisitiza kuwa kila mtanzania ana nafasi ya kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku.

Akiongea na waandishi wa habari Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde Amesema “tumeona ni vyema kutambulisha  promosheni hii kwa wakazi wa Arusha kwani wao pamoja na watanzania katika mikoa mbalimbali  wananafasi ya kujishindia. Promosheni hii tuliyoizundua rasmi mwanzoni mwa wiki hii inampa nafasi mteja wa Airtel kushiriki na kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia Toyota IST pindi atakaponunua kifurushi chake chochote cha Airtel yatosha”

Matinde aliongeza kwa kusema ”Mteja atakaponunua kifurushi chake cha siku anaingia kwenye promosheni kwa simu hiyo lakini akinununa cha wiki namba yake itaingia kwenye promosheni kwa muda wa siku saba na akinunua cha mwezi namba yake itaingia kwenye droo kila siku kwa siku thelathini.  Lakini mteja atakaponunua kifurushi chake cha Airtel yatosha cha siku zaidi ya mara moja namba yake itaingia kwenye droo ya siku hiyo kwa idadi ya vifurushi vya siku alivyonunua.

Ili kujiunga na vifurushi vya Airtel yatosha Mteja anatakiwa kupiga *149*99# au kununua vocha ya yatosha au kununua kupitia huduma ya Airtel Money

Huduma ya Airtel yatosha inampa fulsa mtumiaji wa huduma yetu ya Airtel yatosha kupata vifurushi bora na vya bei nafuu sokoni lakini pia inamuwezesha kushinda Toyota IST aliongeza Matinde

Kwa upande wake Meneja Mauzo kanda ya Kaskazini Bwana Brighton Majwala alisema, “promosheni hii ni ya pekee na haina gharama yoyote kujiunga, mteja anapata nafasi ya kushinda kutokana na matumizi yake ya kila siku. 

Wakazi wa Arusha kesho wanapata nafasi ya kuyashuhudia magari haya yakitembea katika mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha na tutawapatia wateja wetu nafasi ya kununua line, kujisajili na kupata huduma zetu nyingi na kuwawezesha kujiunga na vifurushi vya yatosha ili waweze kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia

Hii ni nafasi ya pekee kwako mkazi wa Arusha kuchangamkia zawadi hii nono kwa kujiunga kwenye vifurushi vya yatosha sasa aliongeza Majwala

Airtel yatosha Zaidi ni promosheni yenye lengo la kuwazawadia wateja wake  nchini nzima ambapo kila siku Airtel itatoa Toyota IST moja kwa mshindi wa siku.

SPLM YAANZA UTEKELEZAJI WA MAKUBALIANO YA ARUSHA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya na Ujumbe wa Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini 



Ujumbe wa Viongozi wa Makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan ya Kusini yalifanya mazungumzo  na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mjini Dar es Salaam jana.
Mazungumzo haya yalilenga kuandaa utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa mjini Arusha  mwezi wa januari tarehe 21 ambayo yanalenga kuyaunganisha makundi matatu katika chama cha SPLM kurudisha Amani na kuunda Serikali itakayowajumuisha viongozi kutoka makundi yote.
Katika mazungumzo ya jana makundi haya yamekubaliana kuendelea na mkakati  wa utekelezaji wa makubaliano ya Arusha kwa lengo la kuandaa utaratibu wa viongozi  wa makundi yote kurudi Sudan ya Kusini mapema iwezekanavyo.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AKABIDHI MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFALI ZILIZOTOLEWA NA (NHC) KWA VIKUNDI VYA VIJANA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akizungumza wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Mkuu wa wilaya ya Temeke akizungumza wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Baadhi ya vijana wakiwapo wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akikata utepe kuashiria kukabidhi mashine wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akikata utepe kuashiria kukabidhi mashine wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akikabidhi mashine kwa viongozi wa vkundi vya vijana wa Dar es Salaam wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akikagua shughuli ya ufyatuaji tofali wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akikagua shughuli ya ufyatuaji tofali wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwashiriki wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akikagua shughuli ya ufyatuaji tofali wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick akikagua shughuli ya ufyatuaji tofali wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana
Vijana wakiendelea na ufyatuaji tofali wakati wa hafla hiyo. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Vijana wakijenga jengo la mfano wakati wa hafla hiyo. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Vijana wakijenga jengo la mfano kumuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dae es Salaam namna matofali hayo yanavyojenga nyumba wakati wa hafla hiyo. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Vijana wakijenga jengo la mfano kumuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dae es Salaam namna matofali hayo yanavyojenga nyumba wakati wa hafla hiyo. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Vijana wakijenga jengo la mfano kumuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dae es Salaam namna matofali hayo yanavyojenga nyumba wakati wa hafla hiyo. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Viongozi wa vijana hao wakizungumza wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana.
Baadhi ya vijana wakiwapo wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Mashine za kufyatulia tofali za kufungamana zikiwa zimewekwa kwaajili ya kukabidhiwa kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam.
Meya wa Temeke Maadadi Hoja na voongozi wenzake wakifuatilia shughuli hiyo ya makabidhiano
Baadhi ya vijana wakiwapo wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Baadhi ya vijana wakiwapo wakati wa ufungwaji wa mafunzo ya ufyatuaji tofali na makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa wilaya zote tatu za mkoa wa Dar es Salaam kwa vikundi vya vijana. Shirika la Nyumba la Taifa limeongeza mashine zingine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Bendi ya Mlimani Park ikiendelea kutoa burudani katika shughuli hiyo

ZIARA YA VYOMBO VYA HABARI YAMKUTANISHA NAPE NA MBOWE

$
0
0
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnuye akikutana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alipofika katika Ofisi za Free Media, wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima, leo akiwa katika ziara katika vyombo vya habari ambayo aliianza jana, jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana kwa furaha na Mhariri Mtendaji wa Free Media, Nevile Meena alipowasili kwenye kampuni hiyo leo akiwa katika ziara kwenye vyombo vya habari mjini Dar es Salaam
Nape akizungumza na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima leo jijini Dar es Salaam
 Nape akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za gazeti la Jambo Leo, leo mjini Dar es Salaam, akiwa katika ziara hiyo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concept inayochapisha gazeti hilo, Teophil Makunga.
 Nape akiwa katika mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Jambo Concept
 Nape akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo na uongozi wa Jambo Concept

Nape akimuonyesha Makunga Kalenda ya CCM ya mwaka huu (2015) kabla ya kumkabidhi kama zawadi.
 Nape akimkabidhi zawadi ya kalenda ya CCM, Makunga
 Baadhi ya waandishi wa habari katika chumba cha habari cha magazeti ya Jambo Leo
 Nape akiwa kwenye chumba cha Breaking news cha magazeti ya Jambo Leo
 Nape akiagana na mpigapicha mkuu wa Jambo Leo Richard Mwaikenda mwishoni mwa ziara katika chumba cha habari cha magazeti hayo. Picha na Bashir Nkoromo na Adam Mzee

SEND OFF YA ZOURHA MALISA WA TIMES FM RADIO YAFANA DAR

$
0
0
 Mtayarishaji wa Vipindi wa Radio FM, Zourha akimkabidhi zawadi ya Laptop mume wake mtarajiwa  ambaye pia ni Mtalaamu wa IT wa kituo hicho, George Zuri wakati wa sherehe ya kuagwa jana kwenye Ukumbi wa Quality Centre, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Bibi Harusi mtarajiwa, Zourha akilia baada ya kuagwa na babake, Malisa kushoto
 Zourha akiwapatia keki wazazi wake wakati wa sherehe hiyo
 Wafanyakazi wenzie na baba wa Zourha, Mzee Malisa kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwa na furaha wakati wa sherehe hiyo
 Zourha na mpambe wake Mary Thomas wakicheza muziki
 Zourha na mpambe wake Mary Thomas

 Shampain ikifunguliwa
 Zourha akigongeana glasi za champain na wageni waalikwa kwenye sherehe hiyo
 Zourha akicheza ngoma ya asili ya kabila la wanyaturu  na ndugu jamaa na marafiki pamoja na wageni waalikwa
 Zourha akicheza muziki namarafiki zake
 Zourha akizawadiwa na wazazi wake ramani ya nyumba na sh, mili 5 za kusaidia ujenzi wa nyumba


 Mzee Malisa akikata keki aliyoandaa kwa ajili ya sherehe hiyo
 Bwana harusi mtarajiwa George Zuri akiwa katika picha ya pamoja na mkewe mtarajiwa Zourha pamoja na shemeji yake
 Zourha na George wanapendeza
 Mzee Malisa akipiga picha na mkewe (kushoto) Zourha (kulia0 na mwanawe mwingine
 Zourha akizwadiwa
 Zourha akicheza muziki na waandishi wa habari wa gazeti la Majira aliuwahi fanya nao kazi kabla ya kuhamia Times Fm Radio
Zourha akiagwa na waandishi wa habari wa Majira

TAMKO LA PAMOJA KWA SIKU YA KIMATAIFA YA KUKOMESHA UKEKETAJI DHIDI YA WA WATOTO WA KIKE

$
0
0
10945033_856755441041229_6165141623154796543_o
UNFPA, UNICEF, Shirikisho la Kimataifa la Wakunga na Shirikisho la Kimataifa la Magonjwa ya Wanawake na Uzazi.

Wito kwa wafanyakazi wa afya duniani kote ili kuhamasisha kukomesha ukeketaji Kwa mwaka 2015, ujumbe wa kimataifa wa siku ya kupinga ukeketaji umewalenga wahudumu wa afya; “Uhamasishaji na ushirikishwaji wa wafanyakazi wa Afya ili kuharakisha kutokomeza ukeketaji”. Na hii ni kwa sababu asilimia 34 ya ukeketaji duniani hufanywa na wahudumu wa afya.

Pamoja na ujumbe huu mahsusi kwa wahudumu wa afya, wadau wengine wote unawahusu.

Ujumbe unasema hivi: Ukeketaji wa wasichana na wanawake unakiuka haki za binadamu na unadhoofisha afya na ustawi wa wasichana takriban milioni 3 kila mwaka. Zaidi ya wasichana na wanawake milioni 130 katika nchi 29 barani Afrika na Mashariki ya Kati ambapo hadi leo hii vitendo hivi vimekithiri wamekwisha fanyiwa aina fulani ya ukeketaji - na athari kwa maisha yao ni kubwa sana.

Duniani kote, tunashuhudia kuongezeka kwa utayari wa jamii na serikali ili kuondokana na vitendo vya ukeketaji - lakini hii haitoshi kwani jitihada zaidi zinahitajika. Leo, tunapoadhimisha Siku ya Kimataifa ya kukomesha ukeketaji dhidi ya watoto wa kike, tunatoa wito kwa wafanyakazi wote wa afya – kuanzia wakunga, wauguzi madaktari wa magonjwa ya wanawake na watu wote katika sekta ya Afya kutoa hamasa dhidi ya kukomesha vitendo vya ukeketaji wa watoto wa kike. 

Mchango wa wafanyakazi wa sekta afya katika jitihada za kimataifa za kukomesha ukeketaji dhidi ya watoto wa kike ni muhimu sana kwani wana uelewa mpana wa mienendo na desturi ya kijamii katika jumuiya wanazozihudumia. Hivyo wafanyakazi wa afya wanaweza kuharakisha kupungua kwa kasi kwa vitendo vya ukeketaji kwani watu wanaowahudumia wana imani kubwa dhidi yao.

Wafanyakazi wa afya pia wana uelewa wa kina juu ya madhara yanayotokana na vitendo vya ukeketaji kwani wanashuhudia madhara katika njia ya mkojo, njia ya hedhi, maambukizi katika via vya uzazi ikiwa ni pamoja na kutoka damu nyingi na hatimae vifo, pia hushuhudia athari za kisaikolojia dhidi ya wale waliofanyiwa vitendo vya ukeketaji hali ambayo ni ya kudumu katika maisha yao.

Wafanyakazi wa afya pia wapo katika nafasi nzuri ya kuongoza jitihada za kupinga mienendo mibaya inayoibuka katika nchi nyingi. Katika baadhi nchi ukeketaji unafanywa na wahudumu wa afya, mathalan takriban msichana mmoja kati ya watano wamekeketwa na watoa huduma waliopatiwa mafunzo, na katika nchi zingine idadi hii inaongezeka inafikia kati ya wasichana watatu hadi wanne.

Ukeketaji ni kinyume cha sheria katika nchi nyingi, Tanzania ikiwemo chini ya sheria ya masuala ya kujamiiana 1998, na watoa huduma za afya ambao wanafanya vitendo hivyo katika maeneo haya wana vunja sheria. Ifahamike kuwa katika nchi zote, aidha sheria zao ziwe zinaruhusu au haziruhusu vitendo vya ukeketaji ni kukiuka haki za msingi za wanawake na wasichana. 

Wataalamu wa afya hususan wale walio katika zahanati na vituo vya afya mara nyingi wanaweza kuwa na shinikizo kubwa la kufanya ukeketaji. Lakini endapo watahamasishwa kupinga shinikizo hilo, wanaweza kuwa sehemu ya ufumbuzi. 

Hivyo, kwanza kabisa, tunatoa wito kwa wafanyakazi wote wa afya kama wapo wanaoshiriki vitendo vya ukeketaji kuachana na vitendo hivyo na kutumia ushawishi walionao katika jamii wanazofanyia kazi na kuhamasisha wenzao katika jamii zingine kukomesha vitendo vya ukeketaji katika maeneo yote. Pia tunatoa wito kwa wafanyakazi wote wa afya kulinda afya ya uzazi na ujinsia ya wasichana wote ambao tayari wamekeketwa.

Tunajua kwamba wafanyakazi wa afya hawawezi kufanya hivyo peke yao. 
 Mashirika kama UNFPA, na UNICEF, kupitia mpango wetu wa Pamoja wa kukomesha ukeketaji, pamoja na Shirikisho la kimataifa la Wakunga, na Shirikisho la Kimataifa la magonjwa ya wanawake na uzazi, tuko tayari na tunayo nia ya kusaidia jitihada za kuwapatia wafanyakazi wa afya ujuzi na taarifa yoyote itakayohitajika ili kuongeza kasi katika kukomesha ukeketaji na pia kutoa tiba dhidi ya madhara yaliyotokana na ukeketaji.

Kanuni za kijamii, hususan katika jamii ambazo zina mshikamano na umoja huwa zina nguvu kubwa juu ya maisha na mienendo ya jamii husika. Lakini kanuni hizi zinaweza kubadilika endapo watu wataamua kufanya hivyo. Pia endapo wafanyakazi wa afya, viongozi, wataalam, na, zaidi ya yote, wasichana na familia kwa ujumla, watakemea na kuchukua hatua dhidi ya mienendo mibaya.

Katika Siku ya Kimataifa ya kukomesha ukeketaji, Tushikamane kupinga ukeketaji kwani Afya, Haki na Ustawi wa mamilioni ya wasichana unategemea umoja wetu.

WIKI YA ULINZI NA USALAMA WA MTOTO

MAKALA YA SHERIA: NJIA YA KISHERIA YA KUKUEPUSHA KUNUNUA ARDHI YENYE MGOGORO.

$
0
0
Na Bashir Yakub
Makala zilizopita  nilieleza   mambo au taarifa muhimu  zinazopaswa kuwa kwenye  mkataba wako  unapokuwa unanunua  nyumba/kiwanja. 
Nikasema  katika niliyosema  kuwa mkataba  lazima uoneshe  ukitokea mgogoro  utatatuliwa vipi,  ueleze kuwa  utapotokea mgogoro  muuzaji  lazima  awajibike kuhakikisha anakupa ushirikiano  mnunuzi  ili kumaliza  mgogoro huo na kuwa muuzaji  kama ana  mke  basi  mke wake ni lazima  aandaiiwe  nyaraka iitwayo  ridhaa ya mwanandoa ambayo  ni  tofauti  na mkataba  na  aisaini  pamoja na kuweka picha yake.  
Nilieleza  mengi  lakini hayo ni baadhi tu. Kwa wale ambao  hawakubahatika kuyasoma hayo basi  waandike neno "MAKALA  SHERIA"  kwenye google watapata makala  hizo. 
Leo  tena naeleza hatua  muhimu sana au ya lazima  na lazima haswaa  kwa mnunuzi wa kiwanja/nyumba  ambayo anatakiwa  apitie  kabla ya kufanya manunuzi.
Hatua hii kwa  jina la  kitaalam huitwa OFFICIAL  SEARCH  kwa lugha rahisi tu waweza kuiita  utafiti,upekuzi,  upembuzi au upelelezi rasmi  ambayo hufanywa na wanasheria. Mi napenda niite upelelezi. 

HOTUBA YA WAZIRI MKUU PINDA YA KUAHIRISHA MKUTANO WA 18 WA BUNGE

$
0
0
HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P.  PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO
WA 18 WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAREHE 7 FEBRUARI, 2015

I:          UTANGULIZI 

(a)      Masuala ya jumla

Mheshimiwa Spika,
1.            Tumekuwepo hapa kwa takriban siku 12 katika shughuli za Mkutano wa 18 wa Bunge lako Tukufu. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.

2.            Lakini tumekutana hapa tukiwa tumeshuhudia mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na Wenyeviti wa baadhi ya Kamati za Kudumu za Bunge. Niruhusu nitumie nafasi hii ya awali kuwapongeza Mawaziri na Naibu Mawaziri wote ambao wameteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali katika mabadiliko hayo. Aidha, napenda niwapongeze Wenyeviti watatu pamoja na Makamu mmoja kwa kuchaguliwa kuongoza Kamati za Kudumu za Bunge ikiwemo Kamati ya Bajeti, Kamati ya Nishati na Madini na Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala. Tunawatakia afya njema Mawaziri, Naibu Mawaziri na Wenyeviti wote katika kutekeleza majukumu yao mapya.

Mheshimiwa Spika,
3.            Tangu tulipomaliza Mkutano wa 16 na 17 wa Bunge lako Tukufu, kumetokea majanga katika sehemu mbalimbali Nchini ikiwemo mafuriko na mapigano ya Wakulima na Wafugaji kule Morogoro, pamoja na ajali za barabarani. Naomba nitumie nafasi hii kuwapa pole wote walioathirika na majanga, maafa na ajali za barabarani.  Kwa wale waliopoteza maisha tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amina.

b)      Maswali

Mheshimiwa Spika,
4.            Katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge wamepata fursa ya kuuliza maswali ya kawaida na yale ya papo papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Jumla ya maswali 122 ya msingi na 313 ya nyongeza yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali.  Aidha, Maswali 15 ya msingi na 13 ya nyongeza yaliulizwa na kujibiwa kwa utaratibu wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

(c)     Miswada na Taarifa Mbalimbali

Mheshimiwa Spika,
5.             Tunahitimisha Mkutano huu tukiwa tumekamilisha kazi kubwa ya kusoma na kujadili taarifa mbalimbli za Kamati za Bunge za Kisekta na zisizo za Kisekta. Kamati za Kisekta ambazo Taarifa zake zimewasilishwa na kujadiliwa na Waheshimiwa Wabunge ni zifuatazo:
i)             Kamati ya Miundombinu;
ii)            Kamati ya Nishati na Madini;
iii)           Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira;
iv)           Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji;
v)            Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala;
vi)           Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa;
vii)         Kamati ya Masuala ya UKIMWI;
viii)        Kamati ya Ulinzi na Usalama;
ix)           Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa;
x)            Kamati ya Huduma na Jamii; na
xi)           Kamati ya Maendeleo ya Jamii.

6.            Aidha, Bunge Lako Tukufu lilipokea na kujadili Taarifa za Kamati zisizo za Kisekta zinazosimamia Fedha za Umma zifuatazo:
i)             Kamati ya Hesabu za Serikali;
ii)            Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa; na
iii)           Kamati za Bajeti.

Mheshimiwa Spika,
7.            Vilevile, tumepokea na kujadili taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza sababu za migogoro baina ya Wakulima, Wafugaji Wawekezaji na Watumiaji wengine na Ardhi Nchini.


Mheshimiwa Spika,
8.            Katika Mkutano huu, tulipanga na tulitarajia kujadili Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa mwaka 2014 (The Tax Administration Bill. 2014); Muswada wa Sheria ya Takwimu wa mwaka 2013 (The Statistics Bill, 2013); na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na. 2) wa mwaka 2014, (The Written Laws Miscellaneous Amendments (No. 2) Bill, 2014) ambao ndio pia ulihusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kiislamu Sura 375.  (The Islamic Law (Restatement) Act) unaotambua Mahakama ya Kadhi. 

Mheshimiwa Spika,
9.            Hata hivyo, hatukuweza kuijadili Miswada hiyo katika Mkutano huu, ili Kamati husika zipate nafasi na muda wa kupitia na kutoa ushauri kwa Bunge lako Tukufu. Ni matumaini yangu kwamba Miswada hii itapata nafasi ya kuwasilishwa na kujadiliwa katika Mkutano ujao wa 19 wa Bunge lako Tukufu.

d) Hoja za Wabunge na Kauli za Mawaziri

Mheshimiwa Spika,
10.         Pamoja na shughuli zilizopangwa katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge walipata pia fursa ya kupokea na kujadili Hoja ya Mheshimiwa James Mbatia kuhusu kukamatwa na Polisi kwa Mwenyekiti wa Chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba kutokana na maandamano ya Wafuasi wa Chama hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam kiyume cha Sheria.  Aidha, Serikali kupitia Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika ilipata nafasi ya kutoa kauli ya Serikali kuhusu kutatua changamoto za soko la Sukari Nchini. 

Mheshimiwa Spika,
11.         Nitumie nafasi hii kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa kushiriki kupokea na kujadili taarifa mbalimbali zilizowasilishwa. Napenda kuliahidi Bunge lako Tukufu kwamba michango ya Waheshimiwa Wabunge, maoni na mapendekezo ya Kamati zote kwa ujumla yatazingatiwa na Serikali kwa utekelezaji.

II:         KILIMO

a)      Hali ya Uzalishaji na Upatikanaji wa Chakula
Mheshimiwa Spika,
12.         Hali ya uzalishaji na upatikanaji wa chakula nchini kwa ujumla imeendelea kuwa ya kuridhisha katika maeneo mengi kufuatia mavuno mazuri katika msimu wa kilimo wa 2013/2014. Tathmini ya awali ya uzalishaji wa mazao ya chakula Nchini hadi mwezi Septemba, 2014 inaonesha kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula katika msimu wa kilimo wa 2013/2014 ulifikia jumla ya Tani Milioni 16.0 zikiwemo Tani Milioni 9.8 za mazao ya nafaka na Tani Milioni 6.2 za mazao yasiyo ya nafaka.

13.         Katika kipindi hicho, makadirio ya mahitaji ya chakula Nchini kwa mwaka 2014/2015 zilionesha kuwa tunahitaji Tani Milioni 12.8. Hivyo, kutokana na uzalishaji huu, Nchi ina ziada ya Tani Milioni 3.2 za chakula, na tumewezesha kujitosheleza kwa chakula kwa Asilimia 125. Napenda kutumia fursa hii kuwapongeza Wananchi na hasa Wakulima wote Nchini kwa kuitikia  wito  wa  Serikali wa Mpango wa “KILIMO KWANZA”, na kuongeza tija katika uzalishaji, ambao umetuwezesha kupata mavuno mengi na kupata ziada hii ya chakula. Serikali itaendelea kuweka juhudi zaidi katika uzalishaji wa mazao ya Chakula ili kulihakikishia Taifa letu kuondokana na njaa na aibu ya kuomba chakula kutoka nje ya Nchi.

Mheshimiwa Spika,
14.         Tathmini hii pia imeonesha kuwa, uzalishaji wa nafaka kwa ujumla umeongezeka kutoka Tani Milioni 7.6 msimu wa 2012/2013 hadi Tani Milioni 9.8 msimu wa 2013/2014. Kati ya Tani hizo Milioni 9.8, Tani Milioni 6.7 ni za mahindi, Tani Milioni 1.7 ni za mchele na Tani Milioni 1.4 mtama. Kutokana na mahitaji ya nafaka kwa msimu wa 2014/2015 kuwa Tani Milioni 8.1; Taifa lina ziada ya Tani Milioni 1.4 za nafaka. Uzalishaji wa mahindi ambayo ni chakula kikuu umeongezeka kutoka Tani Milioni 5.2 katika msimu wa 2012/2013 hadi kufikia Tani Milioni 6.7 katika msimu wa 2013/2014. Kutokana na mahitaji ya mahindi kwa mwaka 2014/2015 kukadiriwa kuwa Tani Milioni 5.2, Taifa lina ziada ya Tani Milioni 1.5 za Mahindi sawa na Asilimia 29.7. Vilevile, uzalishaji wa mchele umeongezeka kutoka Tani Milioni 1.3 msimu wa 2012/2013 hadi Tani Milioni 1.7 katika msimu wa 2013/2014. Kwa vile makadirio ya mahitaji ya mchele kwa mwaka 2014/2015 ni Tani 900,000, Taifa lina ziada ya Tani 800,000 za mchele, sawa na Asilimia 89.

b)    Hali ya Akiba ya Chakula

Mheshimiwa Spika,
15.         Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) walianza ununuzi wa nafaka katika msimu wa 2014/2015 wakiwa na akiba ya chakula ya Tani 189,493.7. Hadi kufikia tarehe 29 Januari, 2015 NFRA ilikuwa imeshanunua jumla ya Tani 298,122.3 za nafaka sawa na Asilimia 107.1 ya lengo la ununuzi. Aidha, kiasi cha chakula kilichochukuliwa katika maghala hadi tarehe 29 Januari, 2015 kilikuwa Tani 29,290.5.  Jumla ya Tani 1,117.5 ziko njiani kutoka vituo vya Vijijini kwenda katika maghala ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa katika Kanda mbalimbali. Hivyo hadi tarehe 29 Januari, 2015, akiba ya chakula katika maghala ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa ilikuwa Tani 460,175.5 zikiwepo Tani 451,589.1 za mahindi; Tani 3,939.6 za mpunga; na Tani 4,646.8 za mtama.

c)    Changamoto ya Hifadhi ya Nafaka

Mheshimiwa Spika,
16.         Pamoja na mvua nzuri zilizonyesha katika msimu wa 2013/2014, ongezeko hili la uzalishaji wa chakula limechangiwa na juhudi za Serikali za kuhimiza Wananchi kuongeza matumizi ya zana kubwa za kilimo (Matrekta) pamoja na kutoa pembejeo za ruzuku kwa wakulima. Aidha, bei nzuri ya kununulia mahindi ya Shilingi 500 kwa kilo iliyotumiwa na Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa iliwavutia wakulima wengi kupeleka mahindi yao katika vituo vya ununuzi vya Wakala jambo lililowafanya Wakala kushindwa kununua nafaka za ziada kutoka kwa wakulima na hivyo kusababisha kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wakulima. Hadi kufikia tarehe 11 Novemba 2014, uwezo wa Wakala wa kuhifadhi nafaka katika maghala   yake ulikuwa ni Tani 246,000 tu, hivyo kutokana na akiba kubwa iliyopo sasa ya Tani 460,175.5, imewalazimu Wakala kuhifadhi sehemu ya akiba hiyo katika maghala mengine Vijijini, katika Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi; na nje ya maghala ya Wakala kwa kufunikwa na maturubai.

d)    Mpango wa kuongeza maghala ya Hifadhi ya Taifa

Mheshimiwa Spika,
17.         Makadirio ya mahitaji ya hifadhi Kitaifa kwa kipindi cha muda  mfupi  ni  tani  400,000; kwa kipindi cha muda  wa kati  ni  tani  700,000;  na  tani  1,000,000  kwa  kipindi cha muda  mrefu.  Katika  jitihada  za  kukabiliana na changamoto ya upatikanaji  wa  maghala  ya  kutosha ya kuhifadhi nafaka katika maghala ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa, Serikali imeandaa mpango maalum unaotarajiwa kugharimu takriban Shilingi Bilioni 212 wa kuongeza uwezo wa NFRA wa kuhifadhi nafaka hadi kufikia Tani 400,000 ifikapo mwaka 2015/2016. Chini ya mpango huo, Serikali itajenga maghala au vihenge vya kisasa (Silos) katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa nafaka.

e)    Ujenzi wa Vihenge vya Kisasa (Silos)

Mheshimiwa Spika,
18.         Kutokana na kuwepo kwa changamoto ya ujenzi wa Silos, nilipokuwa Nchini Poland mwezi Oktoba 2014 nilipata fursa ya kukutana na Viongozi wa Serikali ya Poland pamoja na kutembelea Kampuni ya Mtynpol inayohusika na ujenzi wa Silos, kuhifadhi na kusindika nafaka kwa kutumia teknolojia za kisasa. Nilitumia fursa hiyo, kumwomba Makamu wa Rais wa Chama cha Wafanyabiashara cha Poland, Bwana Witold Karczewski ambaye pia ndiye Mwekezaji wa maghala (Silos) na Viwanda vya usindikaji Nchini Poland kutembelea Tanzania ili kuona uwezekano wa kujenga Silos zitakazotumia teknolojia inayoendana na mazingira ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika,
19.         Tarehe 4 hadi 5 Oktoba, 2014; Bwana Witold alifika hapa nchini na kwa pamoja tulitembelea maghala ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa yaliyopo Kizota – Dodoma. Baada ya ziara hiyo, mwezi Novemba, 2014 Serikali ya Tanzania  imewasilisha  maombi  ya kupata Mkopo wa masharti  nafuu  kutoka Serikali ya Poland. Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa tayari Serikali ya Poland imepokea na kuyapitia maombi yetu; na mwishoni mwa mwezi huu wa Februari, 2015; Wizara ya Fedha inatarajia kukamilisha mazungumzo ya kupata mkopo huo wa masharti nafuu. Ni matumaini yangu kuwa utekelezaji wa mradi huo utaanza mapema mwaka huu baada ya Serikali ya Poland kuridhia maombi hayo.

f)     Hali ya Usambazaji wa Pembejeo ya Ruzuku Nchini

Mheshimiwa Spika,
20.         Kuanzia mwaka 2003/2004 hadi mwaka 2007/2008, Serikali imekuwa ikitoa ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa wakulima kama fidia za gharama za usafiri ili pembejeo hizo ziuzwe kwa bei moja Nchi nzima. Kutokana na changamoto mbalimbali za kiutendaji, Mfumo huo ulibadilishwa na kuanzisha utaratibu wa kutumia Vocha kati ya mwaka 2008/2009 hadi msimu wa 2013/2014.

Mheshimiwa Spika,
21.         Mpango huo katika kipindi hiki cha miaka kumi umewezesha uzalishaji wa mazao ya chakula kuongezeka kutoka Tani Milioni 7.7 mwaka 2003/2004 hadi kufikia Tani Milioni 16 mwaka 2013/2014. Ongezeko hili limechangia ongezeko la viwango vya utoshelevu wa chakula Nchini kutoka Asilimia 88 mwaka 2003/2004 hadi kufikia Asilimia 125 mwaka 2013/2014. Aidha, uzalishaji wa zao la mahindi umeongezeka kutoka Tani Milioni 3.2 mwaka 2003/2004 hadi Tani Milioni 6.7 mwaka 2013/2014. Uzalishaji wa mchele umeongezeka kutoka Tani 600,000 mwaka 2003/2004 hadi Tani Milioni 1.7 mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Spika,
22.         Ongezeko la uzalishaji wa mazao hayo pamoja na sababu nyingine limechangiwa na ongezeko la matumizi ya pembejeo zilizotokana na mpango wa ruzuku. Pamoja na mafanikio ya mpango wa ruzuku ya pembejeo za kilimo kupitia utaratibu wa Vocha, pamekuwepo na changamoto katika ngazi mbalimbali za utekelezaji, ikiwemo ubadhirifu, upotevu wa Vocha na ucheleweshaji wa Vocha, hali iliyosababisha wakulima wengi kushindwa kupata pembejeo kama ilivyokusudiwa.

g)    Mfumo mpya wa usambazaji wa pembejeo Mwaka 2014/2015

Mheshimiwa Spika,
23.         Katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika Mpango wa Ruzuku ya Pembejeo kwa kutumia vocha; na katika jitihada za kutekeleza azma ya kuwapelekea wakulima pembejeo kwa ufanisi zaidi, Serikali katika msimu wa 2014/2015 imebuni utaratibu mpya wa majaribio ambao lengo lake ni kuviwezesha vikundi na Vyama vya Ushirika kuchukua mikopo ya pembejeo za kilimo kutoka Taasisi za za fedha; na vikundi vya wakulima, VICOBA na Vyama vya Ushirika moja kwa moja kutoka katika Makampuni ya Pembejeo.

h)   Hatua za Utekelezaji wa Mfumo mpya wa Ruzuku za Pembejeo

Mheshimiwa Spika,
24.         Jumla ya Kaya 946,000 zinatarajiwa kunufaika na Mpango wa Ruzuku ya Pembejeo za Kilimo kutoka Taasisi za Fedha na Makampuni ya pembejeo. Hadi sasa AMCOS 247 katika Mikoa ya Tabora, Kigoma, Mbeya (Chunya) Katavi, Singida, Iringa na Shinyanga zimepata mikopo ya pembejeo ya jumla ya Shilingi 74,737,708 kupitia Benki za CRDB. Benki ya NMB imetoa mikopo kwa vikundi sita (6) vinavyojishughulisha na kilimo cha mpunga yenye thamani ya Shilingi Milioni 600. Kupitia Benki za Wananchi, vikundi vya wakulima 147 katika Wilaya za Mbinga, Njombe, Mufindi, Kagera na Tandahimba vyenye wanachama 3,242 vilipata mikopo ya pembejeo yenye thamani ya Shilingi Milioni 844.4.

25.         Kwa vile Halmashauri za Wilaya zitahusika moja kwa moja katika suala la usimamizi wa mpango huu, na kwa vile Kamati za pembejeo za Wilaya zitakuwa chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya, ninawaagiza Viongozi wa Mikoa na Wilaya kusimamia kwa karibu zoezi la kuhamasisha vikundi kuchukua mikopo katika Taasisi za fedha na vyombo vingine na kuhakikisha kuwa usambazaji wa pembejeo hizi unafanyika ipasavyo ili tuongeze idadi ya wanufaika wa mfumo huu na kuufanya kuleta mafanikio yaliyotarajiwa kwa manufaa ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.

i)     Mwenendo wa Malipo ya Madeni ya Ununuzi wa Mahindi kwa Msimu wa 2014/2015

Mheshimiwa Spika,
26.         Kama nilivyoeleza hapo awali, Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa ilikuwa na kazi kubwa ya kununua nafaka kutoka kwa wakulima; vikundi vya wakulima na wafanyabishara. Kutokana na wakulima kupewa bei nzuri; na kutokana na wakulima kwa hiyari yao kuomba mazao yao yanunuliwe na Wakala kwa mkopo kuepuka kuharibika, wakulima walifika kwa wingi katika vituo vya mauzo tofauti na kiasi cha fedha ambacho Wakala walikuwa wametenga kwa ununuzi hivyo kuliwasababishia wakulima adha kubwa.

Mheshimiwa Spika,
27.         Hadi kufikia Mwezi Desemba 2014 Serikali ilikuwa inadaiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 89 za Wakulima waliouzia Wakala mahindi.  Aidha, hadi kufikia tarehe 29 Januari, 2015, Serikali ilikuwa imelipa wakulima hao kiasi cha Shilingi Bilioni 15 na kubakiza deni la Shilingi Bilioni 74.  Katika juhudi za Serikali za kutatua changamogo ya deni hili, Mwezi Februari 2015 Serikali inatengemea kulipa kiasi cha Shilingi Bilioni 40 na kubakia na deni la Shilingi Bilioni 34 ambazo tunategemea zitalipwa kutokana na mkopo wa CRDB wa Shilingi Bilioni 15 na Bajeti ya Serikali.  Aidha, Serikali pia imepanga kuuza kiasi cha Tani 175,000 kutoka katika akiba yake ya chakula kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wafanyabishara. Nichukue fursa hii kuwapa pole wakulima wanaoidai Serikali kwa usumbufu wanaopata. Hata hivyo, ninapenda  kuwahakikishia  kuwa  wote  watalipwa stahili zao katika  kipindi  kifupi  kijacho.

III.        ELIMU

(a)          Jitihada za Utengenezaji wa Madawati
Mheshimiwa Spika,
28.         Moja ya changamoto tulizonazo katika kipindi hiki kwenye Sekta ya Elimu ni pamoja na suala la madawati katika Shule za Msingi na Sekondari Nchini. Taarifa nilizo nazo ni kuwa, hadi sasa mahitaji yetu kama Nchi ni madawati Milioni 3.3 kwa Shule za Msingi, na tayari tunayo Madawati Milioni 2.1 sawa na Asilimia 63 ya mahitaji. Kwa maana hiyo, tuna upungufu wa madawati Milioni 1.2 sawa na Asilimia 37. Kwa upande wa Shule za Sekondari tunayo madawati Milioni 1.4 kati ya madawati 1.5 yanayohitajika au Asilimia 92 ya mahitaji. Kuna upungufu wa madawati takriban 120,000 sawa na Asilimia Nane ya mahitaji. Upungufu huo ni kwa idadi ya wanafunzi walioko Shule za Msingi na Sekondari kwa sasa.

29.         Wakati tunazungumzia upungufu huo wa madawati idadi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari inaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kadiri idadi ya watu inavyoongezeka. Hivyo, kasi yetu ya kuondoa upungufu wa madawati inatakiwa kuwa kubwa kuliko kasi ya ongezeko la wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari kwa mwaka. Ni jukumu letu wote Serikali, Sekta Binafsi pamoja na Wananchi kwa ujumla kuondoa upungufu huo hususan katika Shule za Msingi.

Mheshimiwa Spika,
30.         Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuondoa tatizo hili la madawati. Hatua hizo ni pamoja na kupeleka fedha za ununuzi wa madawati kutoka Serikali Kuu kwenda kwenye Serikali za Mitaa. Aidha, kiasi cha Shilingi Bilioni 12.3 zilizotokana na fedha za fidia ya Rada zilielekezwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya kununulia madawati. Hadi sasa madawati ya plastiki 30,996 yameshasambazwa Nchini. Usambazaji wa madawati 61,468 ya mbao utaanza hivi karibuni. Vilevile, Serikali imekamilisha mikataba ya kusambaza madawati mengine ya plastiki 75,699. Tunatarajia kuwa fedha hizo za Rada zitapunguza uhaba wa madawati kwa asilimia 5.1. Katika mwaka 2014/2015, kiasi cha Shilingi Bilioni 1.1 kimetengwa na Halmashauri kwa ajili ya kununua madawati 152,000.

Mheshimiwa Spika,
31.         Serikali imekuwa ikishirikiana na Taasisi za Umma, Wahisani, Sekta Binafsi na Mwananchi mmoja mmoja katika kupunguza uhaba madawati Nchini, Nitumie nafasi hii kuwashukuru, wote ambao wamekuwa wakichangia Sekta ya Elimu hasa katika tatizo hili la upungufu wa madawati.

a)    Ujenzi wa Maabara katika Shule za Sekondari.
Mheshimiwa Spika,
32.         Mtakumbuka kuwa Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa kwenye ziara Mkoani Singida mwaka 2012 alielekeza kila Shule ya Sekondari Nchini iwe ina vyumba vitatu vya maabara ifikapo tarehe 30 Novemba 2014. Tangu wakati huo hadi sasa Viongozi wa Serikali Mitaa na Tawala za Mikoa wamekuwa wakitekeleza maelekezo hayo. Hali ya ujenzi wa vyumba vya maabara Nchini inaonesha kuwa hadi mwezi Desemba 2014 vyumba 3,607 sawa na Asilimia 34 ya mahitaji ya vyumba 10,653 vya maabara Nchini vilikuwa vimejengwa. Aidha, Vyumba 6,249 sawa na Asilimia 59 ya mahitaji vilikuwa vinaendelea kujengwa na Asilimia 7 bado vilikuwa havijaanza kujengwa.

Mheshimiwa Spika,
33.         Mkoa uliofanya vizuri katika kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais hadi kufikia Desemba 2014 ni Mkoa wa Njombe ambao ulifanikiwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya maabara kwa Asilimia 96 ya shule za sekondari zilizopo Mkoani humo. Mkoa wa Ruvuma nao ulikamilisha ujenzi kwa Asilimia 81, ukiwa ni Mkoa wa pili Kitaifa. Napenda kutumia fursa hii kuipongeza Mikoa hii miwili kwa kutekeleza vizuri maelekezo ya Mheshimiwa Rais. Imeonesha mfano mzuri katika kutekeleza maelekezo ya Kiongozi wetu wa Nchi.

Mheshimiwa Spika,
34.         Katika zoezi hili Mkoa wa Morogoro ulikuwa Mkoa wa tatu ambao ulijitahidi kujenga vyumba vya madarasa kwa kufikia kwa asilimia 53 ya mahitaji.  Mikoa 22 iliyobaki haikuweza kufikia asilimia 50 ya lengo kwa kipindi chote cha mwaka 2012 – 2014. Kati ya Mikoa hiyo ambayo haikuweza kufika hata robo ya lengo (Asilimia 25) katika kipindi tajwa cha takribani miaka mitatu ni Mikoa sita; nayo ni Mtwara (Asilimia 21), Lindi (Asilimia 20), Tabora (Asilimia 17), Dodoma (Asilimia 12), Rukwa (Asilimia 11) na Kigoma (Asilimia 10). Tunaweza kusema hii ndiyo Mikoa ya mwisho katika kutekeleza agizo la Rais.  Mikoa 16 ambayo sikuitaja hapa iko katika kundi la Asilimia kati ya 26 hadi 49.

Mheshimiwa Spika,
35.         Mheshimiwa Rais katika hotuba yake kwa Wananchi  ya tarehe 31 Desemba 2014 aliongeza miezi sita zaidi hadi Juni 2015 kwa wale ambao hawajakamilisha ujenzi wa maabara hizo ili waweze kukamilisha. Ni matarajio ya Mheshimiwa Rais kuwa muda huo unatosha kwa kila Sekondari iliyopo Nchini kuwa na vyumba vitatu vya maabara  na  aliweka  bayana  kuwa  hakusudii kuongeza tena muda baada ya muda huo kupita yaani Juni 2014. Hivyo, ninawataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Miji Nchini kuhakikisha maagizo haya yanatekelezwa.  Aidha, ninatoa rai kwa Waheshimiwa Wabunge na Madiwani kutoa msukumo stahiki katika utekelezaji wa maagizo haya kwa maslahi ya Taifa letu.

36.         Kwa upande wa Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI haina budi kuhakikisha agizo hili la Mheshimiwa Rais linatekelezwa ndani ya muda uliotolewa. Aidha, katika kufanya hivyo wahakikishe kuwa vyumba vya maabara vinavyojengwa vina ubora stahiki na vinalingana na thamani ya fedha zilizotumika. Ubadhirifu wa aina yoyote usipewe nafasi na watakaobainika kuhusika wachukuliwe hatua za kisheria mapema. Nitapenda OWM - TAMISEMI waendelee kufuatilia suala hili na kunipa taarifa mara kwa mara.

IV:       SEKTA YA NISHATI

a)            Hatua iliyofikiwa ya Upatikanaji wa Nishati Vijijini
(Miradi ya REA)

Mheshimiwa Spika,
37.         Serikali imedhamiria kuimarisha na kuongeza kiwango cha huduma za upatikanaji wa Nishati ya Umeme  Vijijini ili kujenga msingi wa uchumi imara na wa kisasa wa Taifa linalojitegemea. Moja ya hatua zinazochukuliwa ni utekelezaji wa Mpango Kabambe wa usambazaji Umeme Vijijini.

Mheshimiwa Spika,
38.         Ili kufikia azma hiyo, Wakala wa Nishati Vijijini umeanza kutekeleza Mradi Kabambe wa Awamu ya Pili unaohusisha usambazaji wa umeme Vijijini katika Mikoa yote ya Tanzania Bara. Mradi huu unahusisha ujenzi wa Vituo 6 vya kupoozea umeme na njia ya kusambaza umeme kwenye maeneo yenye msongo wa 33kV yenye urefu wa Kilomita 15,000. Vilevile, utahusisha ujenzi wa njia za kusambaza umeme yenye msongo wa kilo-Volti 400 zenye urefu wa Kilomita 8,000 na ufungaji wa Vipooza Umeme 3,300. Mradi huu utakapokamilika utakuwa umeunganisha Wateja wa awali takriban 250,000 katika Vijiji 1,142. Mradi huu unafuatia baada ya kukamilika kwa zaidi ya Asilimia 80 ya Mradi Kabambe wa Awamu ya Kwanza ambapo Wateja 17,688 wameunganishwa kwenye miundombinu ya usambazaji wa umeme Nchini.

Mheshimiwa Spika,
39.         Mradi Kabambe wa Awamu ya Pili unakadiriwa kugharimu Shilingi Bilioni 881. Hadi sasa takriban Shilingi Bilioni 278 zimelipwa kwa Wakandarasi ikiwa ni malipo ya awali ya Asilimia 10 na gharama za kununua vifaa na hati za dhamana zenye jumla ya Shilingi Bilioni 439 kwa Miradi yote 35 zimefunguliwa.

Mheshimiwa Spika,
40.         Kutokana na juhudi za Serikali za kuongeza kasi ya kuunganisha umeme Vijijini ambazo zimechochewa na kupunguza gharama za kuunganisha umeme kwa wananchi hasa waishio Vijijini idadi ya Watanzania waliounganishiwa umeme imeongezeka kutoka Asilimia 2.5 kwa Mwaka 2007 hadi Asilimia 18.4 kwa Mwaka 2010 na kufikia Asilimia 24 kwa Mwaka 2014.

b)    Utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Bomba la Gesi

Mheshimiwa Spika,
41.         Kuanzia mwaka 2013 Serikali ilianza kutekeleza Mradi wa ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara na mitambo ya kuchakata na kusafisha gesi unaendelea vizuri. Mpaka kufikia mwezi Oktoba, 2014 ujenzi wa bomba ulikuwa umefikia Asilimia 97 na ule wa mitambo ulikuwa umefikia Asilimia 84. Kwa wastani mradi mzima sasa umekamilika kwa Asilimia 92. Matarajio ni kumalizika kwa ufungaji wa mitambo yote na kuanza majaribio ya awali. Mara majaribio yote ya miundombinu yatakapokamilika, miundombinu hii itakabidhiwa kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kwa uendeshaji. Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika mwezi Juni, 2015.

Mheshimiwa Spika
42.         Ili kujiandaa kunufaika na upatikanaji wa Gesi Asilia, TPDC imeanzisha Kampuni yake Tanzu (GASCO) ambayo imepewa majukumu yote ya kumiliki miundombinu yote ya usafishaji, usafirishaji na usambazaji wa gesi asilia hapa nchini pamoja na kukusanya gesi kutoka vyanzo mbalimbali. Ili kufanikisha azma hii ya Serikali, tayari GASCO kupitia TPDC imeajiri Wafanyakazi wapya wapatao 120 kwa ajili ya mitambo ya kusafisha gesi na wengine 50 kwa ajili ya kuendesha bomba la gesi.

Mheshimiwa Spika,
43.         Manufaa mengine yatakayopatikana kutokana na upatikanaji  wa  Gesi  Asilia  ni kupata  umeme  wa  uhakika   na matumizi  viwandani, magari na majumbani. Aidha, Nchi itaokoa Dola za Marekani Bilioni Moja (sawa na Shilingi za Tanzania Trilioni 1.6) kwa mwaka kutokana na mitambo iliyopo nchini kutumia gesi asilia badala ya mafuta. Faida nyingine za mradi mpya ni pamoja na ajira katika mitambo itakayojengwa Madimba na Songo Songo kwani kila mtambo utahitaji wastani wa Wafanyakazi 60. Pia, mradi utatoa ajira katika Sekta zote na hususan za Afya, Elimu, Maji, Usafiri pamoja na huduma nyingine za Kijamii zitakazohitajika katika maeneo husika.  Natoa wito kwa Wananchi wote kulinda miundombinu ya Gesi Asilia ambayo inajengwa kwa gharama kubwa. Aidha, nawahimiza Wakandarasi wa Mradi wa Bomba la Gesi kukamilisha ujenzi kwa muda uliopangwa.

V:        UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

a)    Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
 Mheshimiwa Spika,
44.         Uchaguzi wa Mamlaka za Serikali  za Mitaa uliofanyika Nchini tarehe14 Desemba 2014 ulihusisha uchaguzi wa Wenyeviti wa Vijiji 12,261, Wenyeviti wa Vitongoji 63,319, Wenyeviti wa Mitaa Mijini 3,884, Wajumbe wa Serikali za Vijiji/Mitaa na Wajumbe wa Viti Maalum. Jumla ya watu 8,137,974 sawa na asilimia 69 ya watu waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza kupiga kura. Vyama vya Siasa 17 sawa na asilimia 81 ya Vyama vyote vyenye usajili wa kudumu vilishiriki kwenye uchaguzi huu.

45.         Taarifa ya matokeo inaonesha kwamba katika nafasi ya Wenyeviti wa Vijiji, CCM kilishinda kwa asilimia 79.4, CHADEMA asilimia 15.1 na CUF asilimia 4.6. Vyama vingine kwa ujumla vilipata asilimia 0.9.  Matokeo ya Wenyeviti wa Vitongoji yanaonesha kuwa CCM imeshinda kwa asilimia 79.3, CHADEMA asilimia 15.6, CUF asilimia 4.3 na vyama vingine vilipata asilimia 0.8.  Nafasi za Wenyeviti wa Mitaa CCM kilishinda kwa asilimia 66.5, CHADEMA asilimia 25.4, CUF asilimia 6.8 na vyama vingine vilipata kwa asilimia 1.3.  Matokeo ya Wajumbe wa Serikali za Vijiji/Mitaa ni kuwa CCM ilipata asilimia 79.3, CHADEMA asilimia 15.7, CUF asilimia 4.3 na Vyama vingine vilipata asilimia 0.7.  Kuhusu matokeo ya Wajumbe wa Viti Maalum ni kuwa CCM walipata asilimia 82.1, CHADEMA asilimia 13.7, CUF asilimia 3.5 na Vyama vilivyobaki navyo vilipata asilimia 0.7.

b)    Changamoto Zilizojitokeza
Mheshimiwa Spika,
46.         Pamoja na mafanikio yaliyopatikana wakati wa uchaguzi huo, zipo changamoto zilizojitokeza katika mchakato mzima wa upigaji kura.  Hii ni pamoja na kuwepo kwa vurugu siku za uchaguzi, wagombea kufariki au kujitoa, ukosefu wa umakini katika usimamizi na ucheleweshaji wa vifaa vya kupigia kura. Kutokana na kasoro hizo asilimia 1.2 ya maeneo yaliyostahili kupiga kura bado hawajapiga kura. Hata hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI wamejipanga vizuri kuhakikisha kwamba uchaguzi wa maeneo yaliyobaki na tathmini yake unakamilika mapema iwezekanavyo.

47.         Aidha, kutokana na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri kuonesha udhaifu katika kusimamia uchaguzi huo, Serikali ilichukua hatua ya kutengua uteuzi wa Wakurugenzi sita (6) ambao ni Mkurugenzi wa Mkuranga, Kaliua, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda. Vilevile, wapo Wakurugenzi waliosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa makosa yao wakiwemo Wakurugenzi wa Hanang’, Mbulu, Ulanga, Kwimba na  Manispaa ya Sumbawanga.

Wapo pia, Wakurugenzi waliopewa “ONYO KALI” ambao ni Wakurugenzi wa Rombo, Busega na Muheza. Wakurugenzi waliopewa “ONYO” pekee ni wa Manispaa ya Ilala, Hai, na Mvomero. Watumishi wa ngazi za chini pia walichukuliwa hatua na Halmashauri ambazo ni mamlaka zao za nidhamu. Utekelezaji wa hatua hizi utasaidia kupeleka ujumbe kwa wale wote ambao watashindwa kutoa usimamizi thabiti kwenye chaguzi zijazo.

c)    Pongezi na Shukurani kwa Wananchi     
Mheshimiwa Spika,
48.         Kwa kuzingatia mchakato mzima wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014, naomba uniruhusu nitumie fursa hii kushukuru na kuwapongeza Wananchi wote walioshiriki na hivyo kufanikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014.  Nipongeze pia Vyama vyote vya Siasa vilivyojitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.  Kipekee kabisa niwapongeze Viongozi na Wanachama wote wa Chama cha Mapinduzi kwa ushindi mkubwa na wa kishindo katika maeneo yote kuanzia nafasi za Vijiji, Vitongoji, Mitaa, Wajumbe wa Serikali za Mitaa/Vijiji na Viti Maalum.

VI:       HALI YA MAENDELEO YA ZANZIBAR
Mheshimiwa Spika
49.         Tarehe 10 Januari, 2015 nilibahatika kuhudhuria katika sherehe ya uwekaji jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari ya Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja.  Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Shule ya Sekondari ya Kibuteni (Unguja) ambayo nilikwenda kuiwekea jiwe la msingi pamoja na shule nyingine ya Mkanyageni – Pemba zinajengwa kwa ushirikiano na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) ambapo BADEA imetoa mkopo wa Dola za Kimarekani Milioni Sita na Serikali ya Zanzibar imatoa Dola 600,000 ambazo ni Asilimia 10 ya gharama zote. Gharama za ujenzi kwa fedha za kitanzania inatarajiwa kufikia Shilingi Bilioni 3.0.

50.         Ujenzi wa Shule hiyo ya kisasa ni mwendelezo wa juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya kusukuma maendeleo ya Elimu katika sehemu zote za Zanzibar. Aidha, Shule hii ni miongoni mwa Shule za Sekondari 27 zilizojengwa katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Saba inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein ambapo Shule 19 zimekamilika na 18 kati ya hizo zimekwisha funguliwa.

Mheshimiwa Spika,
51.         Chini ya mkopo wa Benki Kuu ya Dunia Skuli tatu za Sekondari zimefanyiwa ukarabati mkubwa, kampasi mpya ya Chuo cha Ualimu cha Benjamini William Mkapa huko Pemba imejengwa, madawati na vitabu vya ziada na kiada, vifaa vya maabara na kompyuta vimenunuliwa. Pia, mafunzo ya Ualimu kazini yameendeshwa kwa muda wa miaka mitano. Mradi huo umegharimu Dola Milioni 48 ambapo Dola Milioni 42 zimetolewa na Benki ya Dunia na Dola Milioni sita ni mchango wa Serikali.

Mheshimiwa Spika,
52.         Wakati tunaadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein alieleza mafanikio yaliyopatikana Zanzibar baada ya utekelezaji wa Dira 2020, MKUZA II, Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2010 – 2015 na Malengo ya Milenia.  Miongoni mwa mafanikio muhimu yaliyopatikana ni kukua kwa uchumi ambapo kuanzia mwaka 2010 hadi 2014 Pato la Taifa limeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 942.3 mwaka 2010 hadi Shilingi  Bilioni  1,442.8  mwaka 2013 sawa na Asilimia 53.0.  Aidha, katika kipindi hicho uchumi wa Zanzibar ulikua kutoka Asilimia 6.4 mwaka 2010 hadi kufikia Asilimia 7.4 mwaka 2013.  Pato la Mtu Binafsi nalo limeongezeka kwa wastani wa Asilimia 38 kutoka Shilingi 778,000 mwaka 2010 na kufikia Shilingi milioni 1.1. mwaka 2013. Kwa mwaka 2014 kasi ya kupanda kwa bei za bidhaa na huduma (Mfumuko wa Bei) ilibaki katika wastani wa tarakimu moja ya Asilimia 5.6, ikilinganishwa na 6.1 kwa mwaka 2010.

Mheshimiwa Spika,
53.         Mafanikio yanaonekana pia katika ukusanyaji wa mapato ambapo, katika miaka minne 2006/2007 hadi 2009/2010, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilikusanya mapato ya Shilingi Bilioni 484, ikilinganishwa na Shilingi Bilioni 997 zilizokusanywa katika kipindi cha 2010/2011 mpaka 2013/2014. Takwmu hizi zinaonesha ongezeko la Asilimia 106.

Mheshimiwa Spika,
54.         Katika kuimarisha mazingira ya biashara kwa kushirikiana na Sekta Binafsi, Zanzibar imeweza kusafirisha bidhaa zenye thamani ya Shilingi Milioni 94,235.8 kwa mwaka 2014 kutoka bidhaa zenye thamani ya Shilingi 87,799.6 kwa mwaka 2013, sawa na ongezeko la Asilimia 7.3. 

55.         Kwa upande wa Sekta ya Utalii, idadi ya Watalii imeongezeka kutoka Watalii 132,836 mwaka 2010 na kufikia Watalii 274,619 mwaka 2014.  Hili ni ongezeko la Asilimia 107.  Katika elimu idadi ya Shule za maandalizi imeongezeka kutoka Shule 238 mwaka 2010 hadi 279 mwaka 2014, ongezeko hili ni sawa na Asilimia 17.  Shule za Msingi zimeongezeka kutoka 299 mwaka 2010 hadi 359 mwaka 2014 ongezeko la Asilimia 20.  Shule za Sekondari zimeongezeka kutoka 194 mwaka 2010 hadi Shule 210 mwaka 2014.  Ongezeko hili ni sawa na Asilimia Nane (8%). Idadi ya Wanafunzi katika Vyuo Vikuu imeongezeka kutoka 3,624 mwaka 2010 hadi 6,038 mwaka 2014.  Ongezeko hili ni sawa na Asilimia 67.

Mheshimiwa Spika,
56.         Katika Seka ya Afya, idadi ya Wataalam wa Afya imeongezeka kutoka 3,634 mwaka 2010 hadi kufikia 4,618 mwaka 2014.  Katika kutoa huduma za maji safi na salama, baadhi ya maeneo yamefikisha Asilimia 87.7 ya mahitaji halisi katika Mkoa wa Mjini Magharibi Kaskazini Unguja Asilimia 71.7, Kusini Unguja 76.4 Kaskazini Pemba, Asilimia 56.4 na Kusini Pemba Asilimia 74.1.

57.         Mafanikio yapo pia na yanajionesha katika Sekta zingine zote kama vile Barabara, usafirishaji na uimarishaji wa Miundombinu ya Bandari, Viwanja vya Ndege, Kilimo, Ardhi, Upatikanaji wa Umeme, Sekta ya Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Spika,
58.         Nimeamua kuyasema mafanikio haya kuonesha hatua iliyofikiwa kutokana na juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kujenga uchumi imara wa watu wake. Napenda nichukue nafasi hii kumpongeza kwa dhati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na Wananchi wote wa Zanzibar kwa jinsi wanavyoshirikiana katika kuhakikisha wanapiga hatua ya maendeleo ya kukuza uchumi wa Zanzibar. Pamoja na pongezi hizi ni matumaini yangu kwamba Wananchi wa Zanzibar wataendeleza ushirikiano uliopo chini ya uongozi wa Dkt, Ali Mohamed Shein katika kukuza uchumi wa Nchi yao.

VII:      HITIMISHO

Mheshimiwa Spika,
59.         Kama ilivyo ada, naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru wote waliosaidia kufanikisha mkutano huu. Nikushukuru wewe Mheshimiwa Spika, kwa kutuongoza vizuri  na  kwa  busara kubwa.  Niwashukuru Wenyeviti wa Bunge kwa kazi nzuri ya kuongoza vikao vya Bunge lako Tukufu. Kipekee niwatambue Mheshimiwa Lediana Mng’ong’o na Mheshimiwa Kidawa Salehe ambao wamekalia kiti kwa mara ya kwanza lakini kwa weledi mkubwa Hongereni sana!!.

60.         Niwashukuru tena Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge za Kisekta na zisizo za Kisekta kwa kuwasilisha taarifa za Kamati zao vizuri.  Aidha, niwashukuru tena Waheshimiwa Wabunge kwa kazi nzuri ya kujadili taarifa hizo na kwa michango mbalimbali wakati wa Mkutano huu. Mapendekezo ya Kamati zote tuliyokubaliana tumeyaweka pamoja ili kupata urahisi wa kuyatekeleza.  Tunaomba Waheshimiwa Wabunge wote wawe na nakala ya mapendekezo hayo kwa ajili ya ufuatiliaji.

Mheshimiwa Spika,
61.         Nitumie nafasi hii pia kumshukuru Katibu wa Bunge na Wasaidizi wake wote kwa kazi nzuri ya kuhakikisha mkutano huu unakamilisha shughuli zake kama ilivyopangwa. Niwashukuru Wataalam wote wa Serikali na Taasisi zake ikijumuisha Taasisi za Sekta Binafsi, kwa misaada ya Kitaalam na huduma mbalimbali za kufanikisha Mkutano huu.

62.         Niwashukuru pia Waandishi wa Habari kwa kazi nzuri walizofanya kuhakikisha kuwa taarifa za majadiliano na maamuzi mbalimbali ya hapa Bungeni zinawafikia Wananchi. Niwashukuru Madereva kwa kazi nzuri waliyofanya ya kuwasafirisha kwa usalama Waheshimiwa Wabunge, Viongozi mbalimbali, Wataalam na Wasaidizi wote walioshiriki katika Mkutano huu.

Mheshimiwa Spika,
63.         Nimalizie kwa kuwatakia wote safari njema mnaporejea kwenye maeneo yenu ya kazi na katika majimbo yenu. Ninaamini kwamba, Mwenyezi Mungu atatulinda na kutuweka salama sote kama tulivyo hadi kukutana tena katika Mkutano ujao.

64.           Baada ya kusema hayo, naomba sasa kutoa Hoja kwamba, Bunge lako Tukufu liahirishwe hadi tarehe 17  Machi,  2015 saa 3:00 Asubuhi litakapokutana katika Mkutano wa 19 kwenye Ukumbi huu hapa Dodoma.

Mheshimiwa Spika,
65.         Naomba kutoa Hoja.

NAPE: CCM HAIWEZI KUPOTEZA HISTORIA YA TANU

$
0
0

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa akizungumza kwenye ofisi ya gazeti la Jambo leo ikiwa sehemu ya ziara yake kwenye vyombo vya habari.
………………………………………………………………………………………
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye amesema CCM
haiwezi na wala haina mpango wa  kupoteza historia ya mahali ilipozaliwa
TANU.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na
wahariri wa gazeti la JamboLeo siku ya Ijumaa tarehe 6 februari 2015 alipotembelea ofisini kwao katika ziara ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari nchini. 
 
Alisema kumekuwa na maneno mengi kama vile ukarabati unaofanywa kwenye ofisi ndogo ya CCM Lumumba ni kupoteza historia ya TANU.
 
Alisema kinachofanyika ni maboresho ya ofisi ndogo ya CCM Lumumba ifanane na hadhi, mahitaji na wakati wa Chama hicho, lakini historia itabaki kama kielelezo cha Mahala ilipozaliwa TANU.
 
Alifafanua kuwa awali ofisi ya mwanzo ilikuwa nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa makuti, kisha ikaondolewa makuti na kuezekwa mabati ya madebe,baadae ikabadilishwa na kuwekwa bati za kisasa.
 
“Historia ya TANU iliyopo kwenye jengo la Lumumba, tutaendelea kuitunza na hatutoibomoa kwani ni kielelezo cha tulikotoka na tunajivunia historia
hiyo, tutaitunza”
 
Alisema kama tusingefanya maboresho maana yake tungekuwa na jengo la udongo ambalo limeezekwa makuti mpaka leo. Akadai wanaolalamika hawajui historia ya eneo hilo, ila akawashukuru kwa mapenzi yao mema kwa Chama hicho.
 
Aliongeza  kuwa hakuna namna CCM itaruhusu historia ifutike na huku ikiendelea kuhifadhi historia za vyama vingine, hasa bile vya ukombozi kusini mwa bara la Afrika. 
 
Nape pia alikanusha uvumi kuwa CCM inawekeza kitega uchumi eneo hilo, akasema wanakarabati ofisi na itakuwa ofisi sio kitega uchumi.
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live




Latest Images