Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

WAFANYAKAZI WA OFISI YA MKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI WAKIELIMISHWA KUHUSIANA NA MIFUKO YA UWEKEZAJI WA PAMOJA(MUTUAL FUNDS) INAYOENDESHWA NA UTT AMIS

$
0
0
Ndugu, Issa Wahichinenda  Mkurugenzi wa uendeshaji wa UTT AMIS akitoa maada kuhusiana na fursa za uwekezaji katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja kwa wafanyakazi wa ofisi ya Mkaguzi wa hesabu za serikali katika kikao cha baraza la wafanyakazi kilicho fanyika hivi karibuni  Mtwara.

UTT AMIS ndiyo magwiji katika kuanzisha na kuendesha Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Mutual Funds) hapa nchini. Mpaka sasa UTT AMIS inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 235.

Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo  muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns). Mifuko hii inayoendeshwa na UTT AMIS ni kwa ajili ya watanzania wote, vikundi, Saccos, taasisi, kampuni na mifuko ya hifadhi za jamii. Wawekezaji wote wananufaika  kwa kupata faida shindani, uwekezaji mseto ili kupunguza hatari za  uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya vipande vya mifuko hutangazwa kila siku za kazi.
 Baadhi ya washiriki wa kikao cha baraza la wafanyakazi la ofisi ya Mkaguzi  wa Hesabu za  Serikali wakifuatilia uwasilishwaji mada kuhusiana na fursa za uwekezaji katika mifuko ya Pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS.

OLOLOSOKWAN WAPIGWA MSASA KUKITUMIA VYEMA KIJIJI CHA DIJITALI

$
0
0
DSC_0022
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (aliyeipa mgongo kamera) wakati wa ukaguzi wa mwisho wa eneo la mradi wa kijiji cha digitali wa Samsung unaoendeshwa na UNESCO lilitolewa na serikali ya kijiji. Katikati ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan wilaya ya Ngorongoro, Kerry Dukunyi .(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

SHIRIKA la Elimu ,sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, limeanza maandalizi ya kuumilikisha mradi wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa wananchi wa kijiji hicho kwa kuendesha warsha ya siku mbili ya kutambua vipaumbele vya wananchi vitakavyoingizwa katika mradi huo.

Vipaumbele hivyo ni katika elimu, afya na uchumi.
Warsha hiyo ilishikirikisha wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi. Katika majadiliano yao wananchi walitambua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja na mazingira na mfumo wa utamaduni walionao wakazi wa eneo hilo.
DSC_0042
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikagua eneo la mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwani wilayani Ngorongro. Kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi na Mratibu wa miradi wa Taasisi ya Irkiramat, Salanga Mako.

DSC_0231
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini mkataba wa kukabidhiwa ardhi iliyotolewa na serikali ya kijiji kwa ajili ya mradi wa kijiji cha kidigitali huku tukio hilo likishishudiwa na uongozi wa juu wa serikali ya kijiji, wataalam kutoka UNESCO na halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na wanakijiji.

Wakazi hao ambao ni wafugaji wenye kuheshimu mila na utamaduni wa kimasai na mfumo wa maisha wamesema kwamba lugha inayotumika katika kufundishia ni tatizo na ingawa wana shule mbili za msingi na sekondari lugha ya Kiswahili ni tatizo na wakifika sekondari lugha ya kiingereza nayo inakuwa tatizo.


Aidha walisema kutokana na wazazi kutokuwa na elimu hawaoni sababu ya kuwafanya watoto wao wenye maarifa makubwa kwenda shule na badala yake hao wanaoelewa vitu hupelekwa kuchunga au wale wenye umri mdogo wa kike huolewa. Warsha hiyo pia ilibainisha tatizo la afya ya wanawake na watoto, ndoa za utotoni na magonjwa ya zinaa ya kuambukiza.
DSC_0047
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiteta jambo na ujumbe wake aliombatana nao kwenye kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya kuwapiga msasa wananchi wa kijiji hicho ikiwa ni maadalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali hivi karibuni.

Kijiji hicho cha digitali ambacho ni nadharia ya Samsung katika kurejesha faida kwa umma kitakuwa na huduma mbalimbali ambazo zikiunganishwa na haja ya wananchi zitasaidia kubadili maisha ya wamasai na kuondokana na utegemezi wa mifugo pekee na kutambua thamani yao katika rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Warsha hiyo ambayo imesimiwa na wataalamu kutoka UNESCO imelenga kuwafungua macho na kuwashirikisha wananchi kuhusu mradi huo mkubwa wa aina yake nchini na duniani.
Kijiji cha dijitali nchini Tanzania ni cha nne cha kwanza kikiwa nchini Afrika Kusini, kingine Gabon na Ethiopia.
DSC_0060
Baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi wakimsikiliza Mkurugenzi mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues (hayupo pichani).

Kijiji hicho ili kiwe endelevu wananchi wanaohusika wanatakiwa kuelewa mradi huo kuweka vipaumbele vyao na kuangalia jinsi ya kutumia mradi huo katika kukabili changamoto zinazowakabili kwa sasa. Katika majadiliano kwenye ngazi za elimu wananchi walielezea haja ya kushawishi wamasai kuanza kujifunza Kiswahili na Kiingereza ili kuweza kufuatilia kwa karibu masomo na pia kuwepo kwa sheria ndogo ili kuzuia utoro wa wanafunzi kwa ajili ya kwenda kuchunga mifugo na pia kuolewa mapema kwa mabinti.

Mathias Herman, mratibu wa program za Afya , UNESCO, alisema kwamba pamoja na kwamba kijiji hicho kitakuwa na zahanati na huduma za mawasiliano ya tiba (telemedicine) hamasa kubwa inatakiwa kutolewa ili wananchi waweze kutumia huduma hizo kwani kwa sasa wamejikita zaidi huduma za waganga wa jadi.
DSC_0066
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiendesha mjadala kwa wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi ikiwa ni maandalizi ya kuupokea mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Alisema katika warsha kulielezwa kuwa kukosekana kwa madaktari katika zahanati zilizopo kijijini hapo kumefanya watu wengi kuendelea kuamini waganga wa jadi na kujifungulia huko hali ambayo imezaa kuwapo kwa idadi kubwa ya wanawake wanaokufa wakati wa uzazi na pia watoto wasiopata chanjo.

“Wakifika hakuna madaktari hawawezi kuamini huduma hii wakati kuna waganga wa kienyeji na wakunga wa kienyeji” alisema Mathias na kuongeza kuwa katika warsha ilihimizwa kwamba watu watambue tatizo lililopo la kiafya linalosababishwa na mfumo wa mazingira na maisha ya wafugaji na kuhakikisha kwamba huduma zinazoletwa zinatumiwa vyema.

Aidha alisema kuwapo kwa kiwango kikubwa cha maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ndoa za utotoni na mimba katika umri mdogo ni sehemu ya matatizo ambayo yanaaminika kwamba yanaweza kutanzuliwa kwa kutolewa elimu na kushawishi wakubwa wa mila kutambua nafasi zao na elimu ya kisasa katika kushughulikia changamoto za kiafya.
DSC_0095
Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta (kulia) akiwa kwenye majadiliano na baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu na nini kifanyike kuboresha sekta ya elimu kwa ujumla katika kijiji hicho na kuishirikisha halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro katika maandalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali.

“mila na heshima kwa wakubwa wa mila kumefanya wamasai kutegemea tiba za asili na mfumo wa asili wa kuendesha maisha bila kujua athari kwao ziwe hasi au chanya” alisema Mathias kauli iliyoungwa mkono na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues ambaye alisema kunahitajika sana ushirikiano wa jamii, viongozi, wazazi kuhakikisha kwamba kijiji kinafanikiwa na kuwa cha kupigiwa mfano.

Kijiji cha Ololosokwan kilichopo Loliondo, wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kikiwa na watu 9000 kupitia mradi huo kitapewa pia mbinu za kuimarisha soko la utalii, kulitambua na kulitumia kwa manufaa yao na pia elimu ya ubunifu ambayo itawafanya wanawake wanaotengeneza urembo mbalimbali kuweza kumudu soko la utalii na la kawaida.
DSC_0103
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph akiendesha mjadala na baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan kuhusiana mradi wa kijiji cha kidigitali na kuuboresha ili kutatua matatizo ya wananchi pamoja na kuwapata taarifa za maendeleo kupitia redio jamii ya Loliondo FM inayofadhiliwa na UNESCO ikiwa ni katika maandalizi ya kuupokea mradi huo wa kijiji hicho unaotarajiwa kuwasili hivi karibuni kijijini hapo.

Aidha mradi huo utafikisha umeme na elimu kwa njia ya Tehama huku, elimu hiyo ya Tehama ikikusudiwa kutumika kutoa elimu ya darasani kwa wanafunzi ambao wapo machungani.
Mfumo wa wamasai ambao umejengwa katika utamaduni na kuthamini mifugo unatakiwa kubadilishwa kwa wazazi kupewa elimu ya kuwawezesha kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao.
DSC_0163
DSC_0145
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias akiongoza mjadala wa nini kifanyike katika kuboresha sekta ya afya na changamoto zinazowakabili wanakijiji wa Ololosokwan kwa ajili ya maandalizi ya kuupokea mradi wa kijiji cha Kidigitali unaoendeshwa na UNESCO kwa kushirikiana na kampuni ya Ki-elektroniki ya Samsung unaotarajiwa kuwasili mapema mwezi februari kijijini hapo. Wa pili kushoto ni Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia.
DSC_0226
Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta akiwasilisha kazi ya kikundi chake baada ya kujadiliana na wanakijiji wa Ololosokwan katika kuboresha sekta ya elimu ikiwa ni maandali ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali kinachotarajiwa kuwasili hivi karibuni kijijini hapo.
DSC_0124
Mmoja wa washiriki wa kikundi kilichokuwa kikijadili masuala ya utamaduni na utalii akiandika changamato mbalimbali zinazowakabili wakinamama wakimasai wanaofanya biashara za urembo wa kimasai kwa watalii wanaotembelea hifadhi ya Ngorongoro.
DSC_0089
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akishiriki kwenye mjadala na wanakijiji wa kijiji cha Ololosokwan katika maandalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali unaotarajiwa kuwasili mapema mwezi februari kijiji hapo.

UJENZI WA BARABARA YA LAMI KUUNGANISHA MIKOA YA MBEYA NA RUKWA WAKAMILIKA, WAZIRI WA UJENZI AAHIDI SERIKALI KUKAMILISHA KUUNGA PIA MIKOA YA KATAVI, KIGOMA NA TABORA

$
0
0
Barabara ya Tunduma-Ikana-Laela hadi Sumbawanga ikiwa imekamilika kwa asilimia mia moja (100%), barabara hii ambayo ni kiungo muhimu cha Mikoa ya Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora imejegwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Msaada kutoka kwa watu wa Marekani.
Waziri wa Wizara ya Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mjini Sumbawanga tarehe 02/02/2015 katika viwanja vya Nelson Mandela akiwa ziarani Mkoani Rukwa kukagua ujenzi unaoendelea wa barabara za lami za Tunduma-Ikana-Laela-Sumbawanga, Sumbawanga-Matai-Kasanga na Sumbawanga-Kanazi-Kizi-Kibaoni hadi Mpanda. 

Katika hotuba yake hiyo aliwaahidi wananchi wa Mkoa wa Rukwa juu ya dhamira ya dhati ya Serikali iliyopo madarakani kukamilisha ujenzi wa barabara za lami kuunganisha Mikoa ya Mbeya-Katavi-Kigoma na Tabora. Alisema hayo yatafanikiwa iwapo wananchi watatoa ridhaa kwa Serikali iliyopo madarakani kuendelea kuingoza nchi kwa miaka mingine mitano ijayo iweze kufikia malengo iliyojiwekea.

Mradi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga umekamilika kwa asilimia mia moja na Mhe. Waziri ameahidi Wizara yake kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya barabara zilizobakia zikiwemo barabara za Manispaa ya Sumbwanga na zile za Wilaya ya Nkasi. Kwa ujumla fedha alizoahidi kusaidia eneo la Manispa na Wilaya ya Nkasi ni zaidi ya Tsh bilioni nne. 

Kwa mujibu wa Mhe.  Magufuli miradi yote mikubwa ya ujenzi wa barabara Mkoani Rukwa inagharimu fedha za kitanzania zaidi ya shilingi bilioni mia nane (800), ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Serikali iliyopo madarakani (CCM)
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta akitoa salam za pongezi kwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Msaada wa watu wa Marekani katika kusaidia ujenzi wa barabara za lami Mkoani Rukwa.  
Baadhi ya viongozi katika meza kuu wakifuatilia jambo katika mkutano huo wa hadhara.
Sehemu ya mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara.

Waziri wa Wizara ya Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiagwa kwa shangwe na wananchi wa Mjini Sumbawanga mara baada ya hotuba yake nzito kuhusu ujenzi wa barabara iliyowafurahisha wengi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Nelson Mandela tarehe 02/02/2015. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katikati akizungumza leo tarehe 03/02/2015 kwenye ziara ya Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mhe. Dkt John Pombe Magufuli wa pili kushoto ambapo aliishukuru Wizara ya Ujenzi kwa juhudi ilizofanya katika ujenzi unaoendelea wa barabara za lami Mkoani Rukwa. Pamoja na hayo ameiomba Serikali kupitia Wizara hiyo kusaidia pia katika ujenzi wa barabara muhim za Wampembe iliyopo Wilaya ya Nkasi, barabara ya bondeni kwa ajili ya kuunganisha ukanda wa bonde la Ziwa Rukwa unaoongoza kwa uzalishaji wa mpunga na Mikoa ya Katavi na Mbeya, barabara ya Kasesha kwa ajili ya kuunganisha Mkoa wa Rukwa na Zambia na barabara ya kuelekea Kalambo Falls yalipo maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akiteta jambo na Waziri wa Wizara ya Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli muda mfupi kabla ya kumaliza ziara yake Mkoani Rukwa na kuendelea na ziara yake Mkoani Katavi leo tarehe 03/02/2015.(Na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@rukwareview.blogspot.com)

RAIS WA UJERUMANI AWASILI ZANZIBAR LEO

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck mara alipowasili   katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar  leo akitokea Dar es Salaam akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo. 
 Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck  akisalimiana na  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (katikati) mara alipowasili   katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar  leo akitokea Dar es Salam akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo (kulia) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein 
   Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck akiwasili shada la mauwa na mtoto Salma  Issa mara alipowasili   katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar  leo akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mgeni wake Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck (kushoto) mara baada ya mapokezi alipowasili   katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar  leo akitokea Dar es Salaam akiwa katika ziara ya siku moja Nchini (kulia) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi
 Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck akikagua  Gwaride la heshma la Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ ikiwa ni mapokezi ya Rais huyo wa Ujerumani mara alipowasili   katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar  leo akitokea Dar es Salaam akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  na Rais wa Ujerumani Mhe,Joachim Gauck wakipokea salamu ya heshma ya Gwaride la Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ ikiwa ni mapokezi ya Rais huyo wa Ujerumani mara alipowasili   katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar  leo akitokea Dar es Salaam akiwa katika ziara ya siku moja Nchini akifuatana ma Mkewe Daniela Schadt pamoja na viongozi mbali mbali wa Nchi hiyo.[Picha na Ikulu.]

Mazungumzo na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi (Pt 1)

$
0
0
Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hili cha HUYU NA YULE
Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi ambaye ametueleza mengi juu ya safari yake kimaisha
Katika sehemu hii ya kwanza, Mhe. Balozi Nyang'anyi anaelezea
1: Historia yake.
 2: Aliposoma na alivyosoma.
 3: Namna alivyofika / kupata kazi Shirika la Utangazaji Tanganyika (TBC)
 4: Alivyoingia kwenye masuala ya diplomasia na kisha.....alivyoiona nafasi ya ubunge kwa mara ya kwanza 1970. Hii ni safari ndeefu ambayo kwa hakika utapenda kuisikia.
 KARIBU

MAFUNZO YA SIKU TATU YA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII (SOCIAL MEDIA) YAFUNGWA NA KAMISHNA WA KAZI NA UTUMISHI WA UMMA ZANZIBAR.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Elimu Zanzibar (ZEDO) Ussi Said Suleiman (kulia) akimkaribisha Kamishna wa Kazi na Utumishi wa Umma Mr. Kubingwa Mashaka Simba katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media) yaliyofanyika Shule ya VIP mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
 Kamishna wa Kazi na Utumishi wa Umma Zanzibar Mr. Kubingwa Mashaka Simba akitoa nasaha na kufunga Mafunzo ya siku tu ya matumizi sahihi ya Mitandao ya kijamii (Social Media) yaliyofanyika Shule ya VIP mwanakwerekwe Mjini Zanzibar (kulia) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Elimu Zanzibar (ZEDO) Ussi Said Suleiman na (kushoto) Mjumbe wa kamati ya wazazi Ndugu. Makame Ameri Yusuf.
 Kamishna wa Kazi na Utumishi wa Umma Zanzibar Mr. Kubingwa Mashaka Simba akimkabidhi Cheti mmoja wa wanafunzi wa (Social Media) Suhaila Humoud Hilal.
 Mgeni Rasmin Kamishna wa Kazi na Utumishi wa Umma Zanzibar Mr. Kubingwa Mashaka Simba (wakatikati) waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa Mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media).
Baadhi ya wahitimu wa Mafunzo ya siku tatu ya matumizi ya Mitandao ya kijamii (Social Media) wakionyesha veti vyao. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar) .

First lady wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt atembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi Temeke leo.

$
0
0
Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akisalimiana na maofisa wa Jeshi la Polisi wakati alipotembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi Cha Temeke leo.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, DCP Adolphina Chialo akitoa ripoti ya dawati la jinsia na watoto tokea kuanzishwa kwake wakati mke wa rais wa Ujerumani Bi Daniella Schadt alipotembelea dawati la jinsia na watoto katika Kituo cha Polisi cha Chang'ombe kilichopo Temeke.
Baadhi ya wafanyakazi wa UNICEF, Viongozi wa Jeshi la Polisi pamoja na wadau wakisikiliza kwa makini ripoti fupi iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Jeshi la Polisi Nchini, DCP Adolphina Chialo (hayupo pichani).
Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akipelekwa katika ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto iliyopo katika kituo cha Polisi Chang'ombe Temeke wakati alipotembelea kituo hiko kuona jinsi Dawati hilo linavyofanya kazi.
Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akibadilishana mawazo na ripota vijana wa UN kabla ya kufanya nao mahojiano mara baada ya kumaliza kuongea na viongozi wa dawati la jinsia na watoto katika Kituo cha Polisi Temeke.
 
Ripota vijana wa UN wakifanya mahojiano na Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt mara baada ya kumaliza kutembelea ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi Temeke.
Akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Jeshi la Polisi, ripota vijana wa UN.Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

Nunua au Angalia Vipindi Vya TMT Season 1.


Makala ya Shule ya Twayyibat Sec

$
0
0

Mkuu wa wilaya Temeke, Sofia Mjema, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Kiislamu, Twayyibat, iliyopo Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita.

Kuwapo kwa shule hizo kutazidi kuongeza idadi kubwa ya watoto wanaopata elimu ya msingi, sekondari na vyuo Vikuu kwa ajili ya kujikomboa katika maisha yao.

Ukiacha mikoani ambako hakuna shule nyingi hususan maeneo ya vijijini, jijini Dar es Salaam kumefanikiwa kuwa na shule nyingi mno, zikiwamo za serikali na mashirika.

Zipo shule za kidini ambazo wakati wote zimekuwa zikifundisha watoto elimu ya Dunia na ile ya kufahamu Mungu ni nani, nazumgumzia pale watoto wanapofundishwa kisawa sawa na kukolea kiimani kama njia ya kumjua Mungu na kutenda matendo ya kiungwana.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, alitembelea katika shule ya Twayyibat Islamic Seminary, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam.

DC Sofia alitumia muda huo kuikagua shule hiyo pamoja na kuzungumza na wadau wa elimu, walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa ajili ya kuona inakuwa kati ya shule bora wilayani Temeke na Dar es Salaam kwa ujumla.

Miongoni mwa mambo yaliyomkosha DC Sofia ni pale alipoambiwa kuwa ada ya shule hiyo kwa mwaka mmoja ni Sh 200,000 tu, jambo ambalo ni agharabu kuliona wala kulikisia katika shule mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Akizungumza shuleni hapo, Mkuu huyo wa wilaya ya Temeke, Sofia, anasema kwamba ameshangazwa na kuwapo kwa ada nafuu katika shule ya Twayyibat.

“Hili bado linanifanya nijiulize urahisi wa ada hizi wakati najua fika siku hizi elimu ni ghari na kuna mambo mengi yanayohitajika ili shule ziweze kujiendesha, ikiwamo mishahara ya walimu.

“Katika hili linanifanya nione serikali hususan Halmashauri ya wilaya ya Temeke inakaa na viongozi wa shule hii kutatua changamoto zinazowezekana kwakuwa kwa ada hizi shule haiwezi kujiendeshaa vizuri na kusonga mbele,” alisema.

DC huyo anasema urahisi wa ada hizo katika shule ya Twayyibat sit u utawafanya wazazi na walezi wamudu kusomesha watoto wao, bali pia kukuza kiwango cha elimu cha Temeke na Tanzania kwa ujumla.

Anasema amefurahishwa na mazingira ya shule hiyo, ingawa hajaona maabara, jambo alilojibiwa na uongozi wa shule kuwa tayari wameshatenga eneo la kujenga maabara kwa ajili ya shule hiyo ya sekondari ya Kiislamu.

“Maabara ni muhimu mno, fanyeni kila liwezekanalo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa inakuwapo, maana kama tungewasiliana kwa karibu na Halmashauri yetu ni wazi tungeangalia namna ya kusaidia katika hilo ukizingatia kuwa shule inatoa huduma na ada zake ni nafuu.

“Tukitoka hapa tutafute namna bora ya kuhakikisha kuwa shule hii inakuwa bora, kwakuwa nimeshaona misingi na dhamira ya kweli kutoka kwa walimu, wadau, viongozi na wanafunzi kwa ujumla ili kuwapa mwanga zaidi, alisema.

DC Sofia aliwasili shuleni hapo saa 7 mchana, huku akipokewa kwa shangwe na wanafunzi wa shule hiyo, wadau wa elimu na wahisani wa shule hiyo, bila kusahau walimu waliokuwa na shauku ya kumpokea mgeni huyo tangu asubuhi.

Baada ya kuingia na kusaini kitabu cha wageni, alianza kutembezwa katika eneo lote la shule hiyo na kujionea hali ya kielimu inavyoendelea na namna wanavyofanya kazi zao.

Akizungumzia hali yaa utendaji kazi na uwajibikaji kwa walimu hao, DC Sofia aliwataka walimu kuongeza bidii ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wao wanafanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya kidato cha nne.

Anasema shule ina matokeo ya kuridhisha kutokana na wanafunzi wao kujisomea vizuri, wakiamini kuwa ni elimu pekee ndiyo inayoweza kuwakomboa katika maisha yao.“Nashauri wanafunzi waelimishwe zaidi umuhimu wa kujisomea ili waachane na mambo ya Kidunia wakiwa bado wadogo kwakuwa wataharibu maisha yao.

“Mambo ya anasa na starehe zisizokuwa na tija zimepitwa na wakati kwakuwa wanaweza kuharibu kabisa mfumo wao wa maisha na kujiweka katika kundi la majuto,” alisema.Aidha DC huyo alitumia muda huo kuwapongeza wahisani na wadau mbalimbali wanaoiwezesha hiyo yenye maskani yake wilayani Temeke, karibu na Msikiti wa Tungi.

Pia aliwakabidhi wahisani hao vyeti vya kutambua mchango wao kutokana na mara kwa mara kujitolea misaada mbalimbali inayochangia maendeleo ya kielimu kwa shule hiyo.

Baadhi ya wahisani waliokabidhiwa vyeti hivyo ni pamoja na Adam Malima, Skywards Construction, Shaimar Kweigir, Zainabu Vullu, Yakubu Chamber&Associate, Alosco, Home Shooping Centre, ambapo baadhi yao waliwakilishwa kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kiserikali.

Naye Mkuu wa Shule hiyo, Juma Omari, anasema shule yao imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kutoa ufaulu wa kufurahisha, huku akiihakikishia serikali kuwa watajitahidi kuwapa mwanga wa kielimu watoto wanaosoma Twayyibat.

“Tangu shule hii ilipoanzishwa mwaka 1996 imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na matokeo yake ya Taifa, hili linatufanya tuongeze bidii katika kufundisha wanafunzi wetu tukiamini ndio mpango sahihi.

“Sisi kama walimu tumekuwa tukiongeza bidii katika ufundishaji kwa ajili ya kuhakikisha kuwa shule yetu inakuwa bora kati ya nyingine, huku tukiamini kuwa kwa pamoja tutakuwa tunazifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazotukabili,” alisema.

Mkuu huyo wa shule aliwataka wazazi na walezi kuacha sababu, maanaa shule yao inafikika kiurahisi na imeamua kutoza ada nafuu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba watoto wote wanapata haki ya kupata elimu.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

SUPER STAR "OMMY DIMPOZ " LIVE IN NEW YORK CITY SATURDAY FEB 21 (RED CARPET AFFAIR )

$
0
0
PERFORMING HITS LIKE -NAI NAI / BAADAE /ME &YOU /TUPOGO /NDAGUSHIMA/ 
KIGOMA/ RADIO/ MISS KOI KOI/ CHUKUA TIME /NUMBER ONE AND MORE
                                         * KIINGILIO  $ 40 ADVANCE   |  MLANGONI $ 50 *
                                                                      ( INCLUSIVE OF )
                               *RED CARPET ENTRANCE  PHOTO SHOOT (FROM 5PM-6PM*
                                                                 *3 -COURSE DINNER *
                                                                       *SOFT DRINKS *
                                                   *ELEGANT SETTINGS AND SERVICES*
                                                * POZ KWA POZ LIVE ENTERTAINMENT*
                                       *CASH BAR - BEER $3   | LIQUOR $5   | WINE  $5  *
                          *TICKETS & MORE INFO CALL- 347-663-0781  |  917-698-6943 *

      ***********************************************************************
 ==================================================================

Magazeti yanayomilikiwa na makampuni binafsi yaongoza nchini.

$
0
0
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Ikilu jana jijini Dar es salaam akiwa na mgeni wake Rais wa Ujerumani Rais wa Ujerumani Joachim Gauck (kushoto). Rais Gauck yupo nchini kwa ziara ya kikazi kwa siku tano. (Picha na Benedict Liwenga-MAELEZO)


Na Eleuteri Mangi- MAELEZO

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazosimamia uhuru habari na inaongoza kwa kuwa wa vyombo vingi habari yakiwemo magazeti.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es salaam na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Jakaya Kikwete alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua sababu za kusimamisha uingizaji nchini gazeti la “The East African”, wakati wa mkutano wa waandishi wa habari yeye na Rais wa Ujerumani Joachim Gauck.

Rais Kikwete alisema kuwa gazeti hilo halikufuata utaratibu wa kusambazwa nchini kulingana na sheria na taratibu za nchi, hata hivyo Serikali imeshawasiliana na wahusika na wameelekezwa utaratibu wa kufuata kulingana na sheria za nchi.

“Tanzania injali na kusimamia uhuru wa habari, kuna magazeti mengi yakiwemo ya kila siku, wiki ambayo yanayomilikiwa na makampuni binafsi ikilinganishwa na magazeti yanayomilikiwa na Serikali” alisema Rais Kikwete.
 
Rais kikwete aliyataja magazeti yanayomilikiwa na Serikali kuwa ni pamoja na Daily News na Habari Leo ikilinganishwa na magazeti yanayomilikiwa na makampuni binafsi ambapo aliyataja magazeti hayo kuwa ni The Guardian, The Citizen, Majira, Mwananchi, Nipashe na mengine mengi.

Rais wa Ujerumani na msafara wake wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano ambayo ni mwaliko walioupata kutoka kwa Dkt. Kikwete alipotembelea Ujerumani hivi karibuni na kutunukiwa tuzo ya kufanya vizuri katika suala la chanjo kwa watoto.

Ugeni huo wa Rais Gauck watapata fursa ya kujionea maeneo mengi yenye vivutio vya watalii nchini yakiwemo Visiwa vya Zanzibar na Arusha ambayo yanajulikana kwa utajiri wa vivutio hivyo barani Afrika na duniani.

Ujio wa Rais Gauck nchini na msafara wake unafuatia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizo mbili wa muda mrefu kwa manufaa ya maendeleo ya wananchi wao kiuchumi, kisiasa na kijamii.

WADAU WATAKIWA KUCHANGIA MKUTANO WA CILT WA BARA LA AFRICA UTAKAOFANYIKA ARUSHA

$
0
0

Mkuu wa chuo cha Admin and logistic JWTZ pangani marofu BRIGEDIER HARISON MASEBO ambaye ndiyr makamu mwenyekiti wa kamati ya maandlizi ya mkutano huo utakao fanyika jijini arusha akizngumza na wanahabari leo kuhusu mkutano huo na maandalizi yake yalipofikia
NA EXAUD MTEI
 Wadau mbalimbali wa maswala ya usafirishaji,uchukuzi  na watanzania kwa ujumla wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kusaidia kuchangia katika mkutano ulioandaliwa na CILT (the charted institute of logistics and transport) mkutano ambao unatarajiwa kufanyika kuanzia terehe 4 mwezi wa tatu hadi tarehe 6 katika hoteli ya mount meru mkoani Arusha.

Akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya maandalizi ya mkutano huo wa kimataifa makamu mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo Bregedier HARISON JOSEPH MASEBO amesema kuwa mkutano huo utawakutanisha magwiji wa maswala ya usafirishaji na uchukuzi kutoka katika nchi mbalimbali barani Africa kwa lengo la kujadili maswala mbalimbali ambayo yanaikumba secta hiyo barani africa na Tanzania kwa ujumla.

Amesema kuwa mkutano huo ambao ni wa 12 kufanyika  kimataifa umelenga kutafuta fursa mbalimbali za kutangaa biashara au bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na makampuni mbalimbali nchini,kutoa elimu kwa wadau kuhusu maswala mbalimbali ya usafirishaji pamoja pamoja na kutatua chanagamoto mbalimbali zinazokwamisha secta hiyo hapa nchini na barani Africa.

 “tunawaomba wadau mbalimbali wajitokeze kwa wingi katika kuudhamini mkutano huu kwani ni nafasi pekee ya makampuni ya kitanzania kutangaza bidhaa zao kupitia mkutano huu kwa kuwa kutakuwa na watu kutoka maeneo mbalimbali Africa hivyo ni fursa pekee”alisema masebo

Baadhi ya mada ambazo zinatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano huo ni pamoja na ajali za barabarani na jinsi ya kukabiliaa nazo,usalama katika vyombo vya usafiri,kuibuka kwa dhana mpya katika logistic,msongamano katika bandari,msongamano wa magari barabarani,pamoja na mada nyingi ambazo zimetajwa kuwa ni manufaa kwa washiriki watakaoshiriki katika mkutano huo.
CILT ni taasisi ya kimataifa ambayo Tanzania ni mwanachama hai katika taasisi hiyo ambayo imekuwa ni kimbilio la watanzania katika kupata elimu ya logistic na uchukuzi ambapo lengo kuu la CILT ni kutoa taaluma kwa kiwango cha cheti na stashahada ya juu,kuandaa mikutano na warsha na semina pamoja na kutoa ushauri kwa serikali,mashirika,na makampuni ya watu binafsi ikiwa ni pamoja na kuwakutanisha wadau mbalimbali katika usafirishaji kujadili changamoto mbalimbali.

FREE CLINICAL BREAST EXAMINATIONS AND BREAST HEALTH AT AGA KHAN HOSPITAL

NAFASI ZA KAZI. ( WAPISHI/COOKERS ).

$
0
0
Kampuni  inayo  jihusisha  na  upishi wa  vyakula, inahitaji    vijana wa  kike kwa  ajili ya  kufanya  kazi  ya  upishi  kwenye  vituo  mbalimbali  vya  upishi  vinavyo milikiwa  na  kampuni, vilivyopo  katika katika  mkoa  wa  Dar  es salaam.

SIFA  ZA  MWOMBAJI :
1.Awe  wa  jinsia  ya  kike
2.Awe   anajua  kupika  vyakula  vya  aina  mbalimbali.
3.Awe  msafi  na  maridadi.
4.Awe  mwaminifu  na  mwenye  kujituma.
5.Awe  anaishi  jijini  Dar  Es  salaam.


MAJUKUMU  YA  KAZI :
Kupika   vyakula  mbalimbali  kwenye   kituo atakacho  pangiwa.
MAHALI  VILIPO  VITUO  VYA  KAZI:
Vituo  vya  kazi   hii  vipo  katika  maeneo  yafuatayo:
1.Ubungo
2.Buguruni
3.Kariakoo
4.Kimara
5.Mbezi  Juu
6.Mbezi  beach
7.Tegeta
8.Kawe
9.Makongo Juu
10.                  Mawasiliano  Tower.
11.                  Makumbusho
12.                  Magomeni
13.                  Sinza
14.                  Msasani
15.                  Ilala
16.                  Tabata
17.                  Tandika
18.                  Temeke .

IDADI   YA  NAFASI :
NAFASI  MBILI  KILA  KITUO.

JINSI  YA  KUTUMA  MAOMBI:
Tuma  maombi  yako  kwenda : neemarecruitmentagency@gmail.com

AU  YALETE MOJA  KWA  MOJA  OFISINI  KWETU.
TUAPATIKANA  JIJINI  DAR  ES  SALAAM, KATIKA  ENEO LA CHANGANYIKENI  KARIBU  NA  CHUO  CHA  TAKWIMU  MBELE  YA  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.

KUFIKA  OFISINI  KWETU, PANDA  GARI ZA  MAWASILIANO  -CHANGANYIKENI, SHUKA  KITUO  CHA  TAKWIMU, KISHA  TEMBEA  HATUA  ISHIRINI  MBELE  HALAFU  TAZAMA UPANDE  WAKO  WA  KULIA, UTAONA  BANGO LETU.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana  nasi  kwa Simu  :  0688049687.
MWISHO  WA  KUPOKEA  MAOMBI  NI  TAREHE  21 FEBRUARI  2015  SAA  NANE  KAMILI  MCHANA.

MBUNGE JOSHUA NASSAR AWAONGOZA WANANCHI KATIKA MAKABIDHIANO YA HEKARI 92 ZA SHAMBA LA MADIIRA ARUMERU.

$
0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Dastan Malya akiwa na watendaji wengine wa serikali katika ofisi ya mtendaji wa kata ya Siela Sing’isi wakati mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar alipofika kwa ajili ya kwenda kutembelea Shamba la Madiira.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akitia saini katika kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Siela Sing'isi alipotembelea katika kijiji hicho cha Sing'isi.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akiongozana na Diwani wa kata ya Mbunguni Paul Laizer maarufu kama Askofu (shoto) wakati alipowaongoza wakazi wa vijiji vya Sing'isi na Malala kwenda kuangalia shamba la Madiira ambalo hekari 92 zimetolewa kwa vijiji hivyo.
Wananchi wa vijiji vya Sing'isi na Malala wakitizama sehemu ya eneo la Shamba la Madiira lililotolewa kwa wananchi wa vijiji hivyo.
Mpima wa Halmashauri ya wilaya ya Meru ,Seveline Luambano akiwaonesha wananchi wa vijiji vya Sing'isi na Malala,mipaka pamoja na michoro ya ramani ya eneo la hekari 92 zilizotolewa kwa vijiji hivyo .zoezi hilo limeshuhudiwa na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar.
Wananchi wakiwa katika Shamba la Madiira kutizama mipaka ya eneo ambalo limetolewa kwao.
Sehemu ya Shamba la Madiira.
Mbunge Nassari akiwaongoza wananchi wa vijiji vya Sing'isi na Madiira wakitembelea shamaba la Madiira kutizama mipaka ya eneo la Hekari 92 lililotolewa kwao.
Mbunge Nassari akimsikiliza Mwenyekiti wa kijiji cha Sing'isi  Elishiria Kimoto akitoa maelezo ya kusitishwa kwa zoezi la kuoneshwa eneo hilo hadi pale Maofisa Ardhi wa Halamashauri hiyo watakapo weka mionundo mbuni ya barabara katika eneo hilo.
Mbunge Nasari akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo mara baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya eneo la Shamba la Madiira ambao aliwataka kusitisha kilimo ili kuruhusu maofisa Ardhi kupitishwa greda kwa ajili ya kuchonga barabara pamoja na mitaa katika eneo hilo.
Wananchi wakiwa katika kikao cha pamoja.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

RAIS JAKAYA KIKWETE AMUANDALIA RAIS WA UJERUMANI DHIFA YA KITAIFA YA CHAKULA CHA USIKU, IKULU.

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (wa pili kutoka kulia) na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck (wa tatu kutoka kulia) wakifurahia wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyomwandalia  kiongozi  huyo jana usiku, Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mke wa Rais wa Tanzania, mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt.unnamedc2 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete(wa pili kutoka kulia) akiwa na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck (wa tatu kutoka kulia) wakiwa wamesimama wakati wimbo taifa wa Tanzania na ujerumani ulipopigwa wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyomwandalia  kiongozi  huyo jana usiku, Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mke wa Rais wa Tanzania, mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt. unnamedc3 
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Serikali waliohudhuria dhifa hiyo jana usiku, Ikulu jijini Dar es salaam. unnamedc4 
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Gehazi Malasusa (wa pili kutoka kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakiwa kwenye dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyoandaliwa Rais wa Ujerumani Joachim Schadt na Rais Jakaya Kikwete jana usiku jijini Dar es salaam.
unnamedc5 
Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck wakielekea sehemu ya nyuma ya ukumbi kutazama Brass bendi ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikitoa burudani wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyomuandalia mgeni wake jana usiku Ikulu jijini Dar es salaam. unnamedc7 
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck akitoa ujumbe wake kwa wageni mbalimbali waliohudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu. unnamedc9 
Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania wakitazama vikundi mbalimbali vya ngoma za asili vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa dhifa ya kitaifa  Ikulu jijini Dar es salaam. unnamedc10 
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck (wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi jana usiku wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt na mama Sitti Mwinyi Mwinyi.
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck (wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi jana usiku wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt na mama Sitti Mwinyi Mwinyi. unnamedg6 
Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema (kushoto) akiongea na baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Diana Melrose (aliyesimama) wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Rais  Jakaya Kikwete kwa Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck , Ikulu jana usiku. unnamedg8 
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania wakitazama Brass Bendi ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa dhifa hiyo Ikulu jijini Dar es salaam.

MULTICHOICE YAZINDUA KING’AMUZI KIPYA CHA DStv HD

$
0
0
DSC_0100 
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (Katikati) akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari (hawapo pichani), wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa king'amuziki kipya cha DStv HD leo jijini Dar. Kulia ni kwake ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Andrew Chale
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa ving’amuzi vya DStv, leo imezindua king’amuzi kipya cha DStv HD ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza hapa Nchini. Akizungumza na wandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, akielezea umuhimu wa huduma hizo alisema king’amuzi hicho kina ubora wa hali ya juu ikiwemo kuonyesha picha zenye ubora mzuri zaidi.

Pia alieleza kuwa, DStv HD mteja atapata kuona picha zenye mvuto zaidi pamoja na kiwango cha juu cha sauti Dolby Digital 5.1. “Wateja wa DStv watafurahia ving’amuzi hivi kwa ubora wa hali ya juu hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa kwani ndio mara ya kwanza kuingia kwa Tanzania” alisema Ronald Shelukindo.
DSC_0239
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akielezea ubora wa king'amuzi hicho cha DStv HD wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo jijini Dar.

Ronald Shelukindo akielezea kwa kina, alisema DStv HD, mteja anaweza kufurahia vipindi mbalimbali ikiwemo mifumo na mipangilio ya kila vipindi kwa kupendekeza atazame kipi gani, muda gani na wakati gani?.

King’amuzi cha “DStv HD, mteja anaweza kujipangia atazame kipindi gani ama kwa wakati autakao yeye, ambapo anachoweza ni kuseti hicho kipindi akipendacho na kisha anaweza kukiangalia kwa wakati wake, hata kama muda umepita kwa wakati huo kinarushwa kwenye chaneli husika” alifafanua Ronald Shelukindo.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu aliwahimiza watanzania kuchangamkia vinga’muzi hivyo vya DStv HD, ambavyo kwa sasa vipo karibu maduka yote ya Mawakala wa DStv, kwa bei rahisi kabisa vikiwa vinapatikana kwa sh 99,000/ kwa mteja mpya huku kwa wateja walio na ving’amuzi vya zamani vya DStv watakaotaka kubadilishiwa, watalipia sh 39,000/ tu.
DSC_0140
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha king'amuzi kipya cha DStv HD kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

“Ofa hii ni kwa ajili ya kipindi hiki cha fainali za AFCON, hadi hapo michuano hii itakapofikia tamati ambapo bei itabadilika kutoka hizi za sasa, hivyo ni wakati wa kuchangamkia ofa hii ya kipekee na kwa mara ya kwanza, kupata kitu cha ubora wa hali ya juu na kwa bei rahisi.” Alisema Furaha Samalu.

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi alieleza kuwa, siku zote MultiChoice itaendelea kuwa mstari wa mbele kwa kutoa huduma zilizo bora na za kisasa katika ulimwengu huu wa digitali ambapo bidhaa hizo za DStv zimeendelea kuwa bora kila siku. “Huduma za DStv siku zote zimekuwa bora ikiwemo kutoa huduma zisizoleta usumbufu. Ving’amuzi vyetu daima vinaonyesha ubora wa hali ya juu na hutoweza kusumbuliwa na ukatikaji wa picha ama mikwaruzo... Hivyo ni wakati sasa wa kuchangamkia ofa hizi.” Alibainisha Barbara Kambogi.
DSC_0194
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua bei za king'amuzi hicho kipya ambapo kwa wateja wapya watajipatia kwa ofa ya Tsh. 99,000/ kuanzia leo hadi siku Jumapili kilele cha fainali za michuano ya AFCON huku ambao ni wateja tayari wanabadilishiwa kwa gharama ya Tshs. 39,000/ ambayo pia ni ofa. Ving'amuzi hivyo vipya vya DStv HD vinapatikana kupitia mawakala wote wa DStv Tanzania nzima.

Katika hatua nyingine, DStv wamezindua huduma mpya kwa wateja wao waliounganishwa na ving’amuzi hivyo vya DStv kuweza kuendelea kufurahia huduma hiyo kupitia simu zao za viganjani zenye uwezo wa ‘Android’, Kompyuta mpakato (Laptop), Tablet, na vifaa vingine vyenye uwezo wa kupokea usajili wa ‘App’.

Akielezea, juu ya huduma hiyo, Ronald Shelukindo, alibainisha kuwa, kinachotakiwa ni kwa mteja wa DStv, kwenda kwenye simu yake au Laptop, ama Tablet na kisha kujisajili kupitia ‘App’ kwa kujisajili kwa kuandika ‘DStv Now’.

Aidha, Ronald Shelukindo alisisitiza kuwa, huduma hiyo ya DStv Now ni kwa wateja waliouganishwa na ving’amuzi hivyo tu ambapo wataifurahia huduma hiyo kwa kuendelea kuangalia chaneli zaidi ya 12 za DStv, ikiwemo ya Super Sport 3, za filamu, na nyinginezo mbalimbali.
Pia kwa maelezo zaidi wateja wanaweza kutembelea tovuti ya DStv.com
DSC_0209
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha huduma mpya ya DStv Now ambayo mteja ataweza kuangalia vipindi vya DStv kupitia simu yake ya kiganjani, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na Tablet. Huduma hii ni kwa wateja ambao wameunganishwa na ving'amuzi vya DStv kupitia akaunti zao.
DSC_0225
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (katikati), Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia) na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kushoto) wakiangalia promo ya namna ya kujiunga na huduma ya DStv Now "application" inayopatikana katika simu zote za Android pamoja na kompyuta mpakato (Laptop) unajiunga kwa kutembelea www.dstv.com
DSC_0228
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar leo.
DSC_0247
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) na Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kulia) na Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kushoto) wakipozi na king'amuzi kipya cha DStv HD.

ujumbe wa Taasisi ya Kijerumani ya Hanns Seidel Foundation waitembelea Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiwakaribisha ofisini kwake  Mkuu wa Taasisi ya Ujerumani iitwayo Hanns Seidel Foundation  kwa Afrika na ukanda wa Sahara Bw. Claus Liepert (wa pili kushoto) pamja na mwakilishi mkazi wa taasisi hiyo hapa Tanzania Bi. Julia Gabler (wa kwanza kushoto).
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation Bi.  Julia Gabler (wa kwanza kulia) na Bw. Claus Liepert (wa pili kulia).


 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na ujumbe wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation ulioongozwa na Mkuu wa Afrika na Kanda ya Sahara  Bw. Claus Liepert.
 Mkuu wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation  kwa Afrika na kanda ya Sahara Bw. Claus Liepert akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
 Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation  Tanzania Bi.  Julia Gabler (wa pili kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiagana na ujumbe kutoka Taasisi ya Hanns Seidel Foundation ulioongozwa na Bw. Claus Liepert (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake.

RAIS KIKWETE MGENI RASMI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA

$
0
0
Rais Prof. Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akitoa salamu zake kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria kilichofanyika leo kwenye viwanja vya Mahakama vilivyopo kwenye mtaa wa Chimala,Jijini Dar es salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania,Mh. Mohamed Chande Othman akitoa hotuba yake katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria kilichofanyika leo kwenye viwanja vya Mahakama vilivyopo kwenye mtaa wa Chimala,Jijini Dar es salaam.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA MWAKA WA MAFUTA NA GESI ULIOANDALIWA NA GENERAL ELECTRIC (GE) (GE OIL & GAS ANNUAL MEETING 2015)

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene (aliesimama katikati) akibadilishana mawazo na CEO wa Exxonmobil (Moja ya Kampuni kubwa ya Mafuta na Gesi duniani). Aliesimama sambamba na Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dr. James Mataragio na aliekaa ni Rais na CEO wa GE Oil & Gas, Lorenzo Simonelli.
unnamedl2 
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene (MB) akisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dr. Mataragio (Hayupo pichani) akiongea kuitangaza Tanzania kwa wadau na wawekezaji wakubwa wa Mafuta na Gesi duniani, aliekaa kushoto kwa Waziri ni Rais na CEO wa GE Oil & Gas, Lorenzo Simonelli.
unnamedl3 
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. George Simbachawene (MB) akihutubia wadau mbalimbali wa mafuta na gesi duniana katika mkutano wa mwaka ulioandaliwa na GE Oil & Gas uliofanyika Florence, Italy.
…………………………………………………………………………………………
Pamoja na kuwepo kwa changamoto za kushuka kwa bei ya mafuta duniani, Tanzania bado imeendelea kuvutia wawekezaji kutoka pande zote za Dunia kuja kuwekeza katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi nchini. Akiongea katika mkutano wa mwaka wa GE Oil & Gas, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (MB) aliwaalika wawekezaji wakubwa kutoka pande zote za dunia kutembelea Tanzania na kuona nafasi za uwekezaji zilizopo.

Mkutano huo uliofanyika Florence, Italy uliwakutanisha wadau wakubwa wa Mafuta na Gesi duniani kujadili changamoto katika sekta hiyo na namna ya kuzikabili. Kauli mbiu ya mwaka huu ililienga zaidi kuangalia namna ambavyo sekta hii itachochea maendeleo ya dunia nzima kwa kuhakikisha kuwapo kwa nishati endelevu na yenye kujali mazingira. 

Tanzania iliwakilishwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dr. James Matargio ambaye alipata fursa ya kuitangaza Tanzania kwa kuonyesha fursa zilizopo katika sekta ya Mafuta na Gesi nchini. Dr. Mataragio alisema “ pamoja na kuwa bei za mafuta zinaendelea kushuka, bado kuna fursa ya kutumia gesi kusaidia upatikanaji wa nishati endelevu na yenye kulinda mazingira kwa vizazi vya sasa na baadae”
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>