Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 453 | 454 | (Page 455) | 456 | 457 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki amewaomba wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh.Joachim Gauck  anayetarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tano.

  Akizungumzia ujio wa rais huyo ofisini kwake  leo jijini Dar es salaam Mh. Meck Sadiki amesema kuwa rais Joachim Gauck na msafara wake atawasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere majira ya saa 2.30 usiku na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.

  Ameeleza kuwa mapokezi rasmi ya rais huyo yatafanyika kesho katika viwanja vya Ikulu majira ya saa 3 asubuhi ambapo rais huyo akiwa na mwenyeji wake atapata fursa ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kupigiwa mizinga 21.

  Amesema kuwa akiwa nchini Tanzania Rais Joachim Gauck atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam na baadaye kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Vyama vya hiari, uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa Dar es salaam.

  Amefafanua kuwa Februari 4, 2015, Rais huyo ataelekea Zanzibar ambapo atakutana na kuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali.

  Aidha kabla ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania  Februari 6, 2015 rais huyo wa Shirikisho la Ujerumani atatembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti ,Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  na Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu jijini Arusha.

  0 0
 • 02/02/15--12:40: TAARIFA YA MSIBA
 •  Familia ya Marehemu Lawrence Maxi Kweka wanasikitika kutangaza kifo cha mama yao  Bibi Caroline Kweka kilichotokea tarehe 1 Feb 2015 Dar es Salaam. Mazishi yatafanyika Alhamisi, tarehe 5 Feb 2015 Maili Sita Moshi. 

  Misa ya kumuaga marehemu itafanyika Jumatano, tarehe  4 Feb 2015, kuanzia saa tano asubuhi nyumbani kwa watoto wa marehemu Bw Theophilus na Bibi Rita Mlaki (MB) wa Mikocheni, Dar es Salaam.

   Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe milele.

  0 0


  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wakazi wa mji wa Tunduma mkoani Mbeya kuwa Serikali itajenga barabara ya njia nne katika mji huo ili kupunguza msongamano wa magari na kuuwezesha mji huo kuwa wa kisasa na kibiashara.

  Amesema hayo katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya barabara inayoendelea katika mikoa ya Mbeya na Rukwa ambapo akiwa mjini Tunduma amekutana na wananchi wanaofanyabiashara katika mji huo.

  “Dumisheni umoja,amani na mshikamano ili mfanye biashara zenu na kukuza uchumi nasi tutahakikisha tunajenga barabara ya njia nne ili kupunguza msongamano wa magari na kuuwezesha mji wa Tunduma kuwa wa kisasa na kibiashara na hivyo kuwa mahali pazuri pa watu kuishi”,amefafanua waziri Magufuli.

  Katika ziara hiyo waziri Magufuli amekagua mizani ya Nkangamo na barabara ya Tunduma –Sumbawanga KM 225, iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kuwataka wananchi wa mkoa wa Rukwa kutumia barabara hiyo kukuza uchumi wao na wa mkoa wao kwa kufanyakazi kwa bidii.

  Akihutunbia wananchi wa Sumbawanga Waziri Dkt. Magufuli amewataka wananchi kutambua kuwa barabara za lami zinajengwa kwa gharama kubwa hivyo wazitumie kwa manufaa na wale walioko kwenye hifadhi ya barabara wabomoe nyumba zao mapema ili kuwezesha ujenzi kufanyika kwa wakati.

  Waziri Magufuli amesema Serikali iko katika hatua za awali kujenga barabara ya Matai-Kasesha KM 50 kwa kiwango cha lami ili kuunganisha mkoa wa Rukwa nan chi ya Zambia na hivyo kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza mjini Sumbawanga na hivyo kutoa fursa za ajira na uchumi kwa wananchi.

  Waziri Magufuli yuko katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya barabara katika mikoa ya Mbeya,Rukwa,Katavi na Tabora ambako kuna miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara za lami inayoendelea.

  Imetayarishwa na kitSengo cha habari na mawasiliano serikalini wizara ya ujenzi.

  0 0

   Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu jijini Dar es salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiwa mwenye furaha mara baada ya kumpokea Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  na Mkewe Bibi Schadt (walioshika maua), uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
   Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  akiwa na mkewe Bibi Schadt  na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakitazama vikundi mbalimbali vya burudani wakati wa mapokezi ya Rais huyo wa Ujerumani uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakifurahia jambo walipokuwa wakitazama vikundi mbalimbali vya burudani vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Rais huyo uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu jijini Dar es salaam.
   Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kumpokea Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck wakiwa na nyuso za furaha.  Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.


  Na. Aron Msigwa -MAELEZO.

  Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na msafara wake amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu majira ya saa 2.40.

  Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt  amelakiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilali pia mapokezi ya burudani za ngoma za asili kutoka vikundi mbalimbali na wananchi waliojitokeza kumpokea.

  Rais huyo  ambaye anaitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza kufuatia  mwaliko kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete atapata mapokezi rasmi kesho katika viwanja vya Ikulu majira ya saa 3 asubuhi ambapo rais huyo akiwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete atapata fursa ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kupigiwa mizinga 21.

  Akiwa nchini Tanzania Rais Joachim Gauck atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam na baadaye kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Vyama vya hiari, uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa Dar es salaam.

  Pia Februari 4, 2015, Rais huyo ataelekea Zanzibar ambapo atakutana na kuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Kabla ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania  Februari 6, 2015 rais huyo wa Shirikisho la Ujerumani atatembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti ,Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  na Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu jijini Arusha.

  0 0

  Makamu wa Rais wa kampuni ya Huawei katika idara inayohusika na mahusiano ya serikali Ulimwenguni, Bw. David Harmon (wapili kushoto) akipeana mkono na Makamu Mweyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Bw. Erastus Mwencha (wapili kulia), mara baada ya kusaini makubaliano yatakayosaidia kuongeza  ushirikiano baina yao katika kuimarisha maendeleo katika miundombinu ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano (teknohama). Hafla ya kusaini makubaliano hayo ilifanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande zote mbili.

  Na Mwandishi wetu, Addis Ababa

  Kampuni ya Huawei Technologies inayoongoza katika sekta ya habari na mawasiliano duniani, imesaini makubaliano (MoU) na Umoja wa Afrika (AU), makubaliano yatakayosaidia kuongeza  ushirikiano baina yao katika kuimarisha maendeleo katika miundombinu ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano (teknohama).

  Makubaliano hayo yalisainiwa hivi karibuni mjini Addis Ababa, Ethiopia kwenye Mkutano wa AU wa mwaka 2015 ambao pamoja na mambo mengine ulijadili pia namna ya kuimarisha uelewa wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano (teknohama) kwa nchi wanachama sambamba na kujenga uwezo wa juu katika maendeleo ya miundombinu ya teknolijia hiyo.

  Akizungumza kwenye mkutano huo, Makamu mweyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bw. Erastus Mwencha alisema maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (teknohama) yana msaada mkubwa kwa ukuaji wa uchumi ulimwenguni na pia ni nguzo muhimu katika kuleta madadiliko chanya kwenye setka mbalimbali.

  “Maendeleo ya teknolojia hii yataleta mabadiliko makubwa sana katika sekta mbalimbali na ndio maana tunatafuta washirika wanaoweza kufanya kazi na sisi ili kufanikisha hilo. Huawei kama kampuni imara kwenye teknolojia hiyo tunaamini pia itakuwa ni msaada mkubwa itakapo shirikiana na sisi...tunafurahi kuwa nao kwenye huu mradi,’’ alisema Mwencha.

  Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa kampuni ya Huawei katika idara inayohusika na mahusiano ya serikali Ulimwenguni, Bw. David Harmon alisema kampuni yake ina nia yakukuza kimataifa  maendeleo sekta ya teknohama na ndiyo maana kwa muda mrefu imekuwa ikisaidiana na serikali mbalimbali katika kuimarisha miundombinu inayohusiana na sekta hiyo.

  “Huawei ina jukumu la kuhakikisha tunashikirikaina na washirika wetu kwenye nyanja zote za teknohama  ili kujenga Afrika bora yenye kushikamana, kwa sababu tunaamini kwamba teknolojia ICT, hasa mawasiliano ya simu ni nguzo muhimu si tu kwa Afrika bali ulimwenguni wote.

  "Kwa miaka yetu 17 ya uzoefu katika sekta ya teknohama sambamba na mtandao wa kimataifa ulimwenguni kote ina maana kwamba Huawei ipo katika nafasi  nzuri ya kushiriki kwenye namna bora ya kutafuta ufumbuzi kwa masuala ya teknohama. Tupo tayari kubadilishana uzoefu wetu na Umoja wa Afrika, " Harmon aliongeza.


  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema amevutiwa sana na kazi iliyofanywa katika muda mfupi kwenye shamba la kahawa la Aviv lililoko kwenye kijiji cha Lipokela, wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma.

  Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi saba, eneo kubwa la shamba limepandwa miche ya kahawa na mingine imezaa na imeshavunwa ikilinganishwa na wakati alipofika shambani hapo Julai 2013 na kutembelea tu kitalu cha miche ya zao hilo.

  Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Februari 2, 2015) wakati akizungumza na wafanyakazi na menejimenti ya shamba la Aviv baada ya kulitembelea na kukagua miundombuinu ya umwagiliaji wa matone ya maji kwenye shamba hilo.

  “Mkuu wa shamba hili, Bw. Medu amenieleza kwamba mpaka sasa, wameshavuna kahawa mara moja na wanatarajia kuvuna tena hivi karibuni; lakini ili waweze kuanza kupata faida ni lazima wavune mara nne.”

  “Kilimo kinataka uvumilivu na kinataka uwekezaji mkubwa... ni lazima kiwepo; hata kwa wakulima wadogo ni lazima kiwepo licha ya ugumu wake. Sasa ukisema kilimo ni kigumu na ukaacha kulima wakati una mke na watoto, je hao watakula wapi?”, alihoji.

  Aliwasifu wamiliki wa shamba hilo kwa kuchagua kulima zao la kahawa kwani lina walaji kila mahali ulimwenguni kote. “Wameamua kulima kahawa aina ya Arabica ambayo inakubalika duniani. Uhitaji wa kahawa hii upo kila mahali kwa sababu wanywaji wapo,” alisema.

  Waziri Mkuu alisema pamoja na mafanikio hayo, shamba la Aviv linakabiliwa na changamoto ya nishati kwani linahitaji megawati 2.5 ili liweze kuendesha mitambo yake ambayo kwa sasa inatumia mafuta yanayoligharimu fedha nyingi.

  Aliwataka wamiliki wa shamba hilo waendelee kuwa wavumilivu wakati Serikali ikiendelea kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

  Mapema, akisoma risala ya kampuni ya Aviv, Mkuu wa shamba hilo ambaye pia anasimamia uzalishaji wa zao la kahawa Afrika Mashariki, Bw. Medu Medappa alisema hadi sasa wamekwishalima hekta 1,060 na zote zimekwishawekewa miundombinu ya umwagiliaji wa matone na kati ya hizo, hekta 810 zimekwishapandwa miche ya kahawa.

  “Shamba letu lina ukubwa wa hekta 2,000 na hadi sasa tumeshalima hekta 1,060 na zilizobakia ni kwa ajili ya kutunza mazingira na uoto wa asili kwenye vilima vinavyotuzunguka,” alisema.

  Alisema hadi sasa wamekwishaajiri wafanyakazi 1,500 kwenye shamba hilo na kutoa mafunzo kwa wakulima wanaoishi vijiji vya jirani. “Pia tumewapatia miche ya bure kaya 673 na kutokana na mafunzo tunayowapa, wanavijiji wameweza kulima kahawa inayoendana na viwango vya kimataifa vya uzalishaji kahawa ambavyo ni miezi 22,” alisema.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu akijibu moja ya hoja kwenye risala ya Bw. Medappa iliyohusu eneo la hekta tisa kuchukuliwa na Wakala wa Ujenzi wa Barabara (TANROADS), alisema eneo hilo ni muhimu kwa ujenzi wa barabara za mkoa huo kama ambavyo shamba hilo ni muhimu kwa mkoa huo.

  “Lile eneo limetengwa na TANROADS kwa ajili ya kutengeneza kokoto za ujenzi wa barabara. Barabara za lami tunazitaka. Tunahitaji kazi hii iendelee la sivyo barabara zetu zitakufa,” alisema.

  Alisema watu wa TANROADS wakimaliza kazi yao, lile eneo litabaki tupu na mwekezaji huyo anaweza kulitumia kadri atakavyoona inafaa kwa sababu liko ndani ya eneo lake.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, FEBRUARI 3, 2015.

  0 0

  3 February 2015, Dar es Salaam, United Republic of Tanzania - Visiting German First Lady Daniela Schadt had a compelling interaction with survivors of violence at the Chang’ombe Police Gender and Children’s Desk.

  Schadt and her partner, German President Joachim Gauck, are on a three-day visit to Tanzania and today visited Temeke district’s Police Gender and Children’s Desk.  A patron of UNICEF Germany, Schadt heard the stories of survivors of violence.

  "I am very impressed by the life-changing work you are doing for the women and children of Temeke," Schadt was quoted telling the police officers at the Gender and Children’s Desk.

  With support from the United Nations (UNICEF, UNFPA and UN Women), the Tanzania Police Force is committed to improving its response to survivors of Gender Based Violence (GBV) and victims of child abuse. At the heart of the Police’s response to GBV and child abuse are the Gender and Children’s Desks – specialist units in each police station staffed by trained officers able to handle such cases. In August 2011, the Inspector General for Police committed to establishing Desks in all police stations in Tanzania. 

  The vision of the Tanzania Police Force is to ensure that every child, woman or man that reports to a Desk is treated with dignity and sensitivity and that every case is handled effectively and efficiently. The Police Partner Coordination Group on GBV and child abuse, convened by the Police and comprised of development partners, NGO partners and relevant Ministries, Departments and Agencies, is committed to support the Police to realise  this vision.

  Since the establishment of Gender and Children’s Desks, the number of reported cases has increased significantly in Chang’ombe. The Desk officers conduct awareness raising sessions in schools, in community meetings and in bars. But, most notably, word of mouth from people who have been assisted by the Desk encourages victims and their families to come and ask for help. The Chang’ombe Desk, which was renovated and equipped with UNICEF assistance, provided support to 269 victims of gender based violence and child abuse in 2014 compared to just 71 cases in 2009.

  ‘Ending violence is everyone’s business. All violence against children can be prevented’, said Birgithe Lund-Henriksen, UNICEF Tanzania’s Chief of Child Protection. ‘Promoting and providing services for children and their families that identify, offer help, support and care, as well as mechanisms to report incidences of violence, is one of the key strategies UNICEF is implementing to prevent and respond to violence. 

  Services help children cope with their situation, and also break the cycle of abuse and reduce further harm. We commend the Police for its dedication to ending violence in communities by ensuring that there are fully equipped Desks in every police station across the country. UNICEF is proud to be partnering with the Police in realizing this vision’.

  The United Nations has supported the Tanzania Police Force to develop a 3 year action plan (2013 – 2016) which focuses on improving the infrastructure ofthe Police Gender and Children’s Desks, enhancing the skills and knowledge of staff working at the desks to effectively handle cases of GBV and Child Abuse, and raising awareness of the public on how and where to report cases. 

   The action plan sets out clear objectives, activities, and targets for enhancing Gender and Children’s Desks for the next three years. The Tanzania Police Force selected six priority regions to start with in implementing the action plan (Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Mara, Mbeya, and Dar es Salaam).

  The Violence Against Children Survey, launched by the Ministry of Community Development, Gender and Children and UNICEF in 2011, highlights the specific vulnerability of children to physical and sexual violence in Tanzania: nearly 1 in 3 girls and 1 in 7 boys experience sexual violence and over 70 per cent of both girls and boys experience physical violence before the age of 18 years. However, most survivors never tell anyone about their experience and relatively few cases are reported to the Police.  

  0 0


  0 0

  WASANII WANAOTAKA KUSHIRIKI TAMASHA LA MUUNGANO DAY LA WASANII WA TANZANIA ,UJERUMANI WAJIANDIKISHE 

  Tamasha litafanyika mjini Koloni,Ujerumani  April 2015

  Wasanii wanaotaka kushiriki katika katamasha la kongamano la wasanii wa Tanzania na afrika mashariki linalotarajiwa kufanyika mjini Kolon,Ujermani mwezi April  2015 mnaombwa mjiandikishe kwa kuwasiliana katika namba ya simu  +49(0)15778645623 .
   
  Tamasha hili linania ya kutangaza sanaa za maonyesho za Tanzania nchini ujerumani,wasanii wa ngoma za asili,Sarakasi,Maigizo, Muziki n.k mnakaribishwa kujiandikisha kushiriki Tamasha hili ,Wasanii mnaombwa mtumie nafasi hii kuonyesha vipaji vyenu katika uwanja wa kimataifa ili kujitangaza zaidi.
   
  Ushiriki wenu katika tamasha hili ndio dira ya ukombozi kwa wasanii wote!
  Maelezo zaidi piga  simu  +49(0)15778645623

  0 0

   Grace Charles akiendelea na ukataji wa madini huku akitumia
  kifaa maalumu.
   picha  Kulia ni Gladness John pamoja na Loveness Marteen wakiwa wanaendelea na shughuli ya ukataji
  Magret Joseph akiwa anaangalia kwa makini namna alivyokuwa
  akikata jiwe kwa kutumia mashine maalum(picha zote na woinde shizza
  ,Arusha

  Na Woinde Shizza,Arusha.

  Sekta ya madini nchini bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali
  ikiwemo uhaba wa walimu na wataalamu wa kufundisha ukataji wa vito vya
  madini hali inayosababisha kuuzwa kwa madini ghafi nje ya nchi na
  kupelekea kuuzwa kwa bei ya chini na pesa nyingi kwenda nje ya nchi .

  Hayo yameelezwa jana na mratibu wa kituo cha jimolojia Tanzania Musa
  Shanyangi wakati akiongea na waandishi wa habari katika kituo hicho
  kina kinachotoa mafunzo ya ukataji madini ya vito wakati wa mahojiano
  maalum na waandishi wahabari chuoni hapo ambapo wameanza kutoa mafunzo   ngazi ya cheti kwa wahitimu 15 wakike ambapo chuo kipo katika
  halmashauri ya manispaa ya jiji la arusha. Alieleza kuwa hivi sasa madini ghafi yanauzwa sana nje ya nchi kwa bei   ya chini lakini kama wangeweza kuuza madini hayo yakiwa yameongezwa  thaman na kuuzwa kwa bei ghali na kuwezesha fedha za kigen kubaki  nchini na kuongeza pato la taifa .

  Shanyangi aliongeza kuwa hivi sasa wameanza kuwafundisha kozi ya miezi
  6 kwa wanafunzi 15 wakike ambapo wanafadhiliwa na Arusha women
  foundation fund iliyoko mjini ikiwa na lengo la kuwasaidia mabinti ili
  kuweza kusaidia sekta ya madini na kuweza kukabiliana na uhaba wa
  wataalamu wa ukataji madini nchini.

  Hata hivyo kituo hicho kinatarajia kuongeza wanafunzi mpaka kufikia 60
  ili kuweza kuongeza ufanisi na kuweza kuboresha sekta hiyo ya madini
  ili kuweza kuongeza wataalamu ,pia wanamkakati wa kuweza kusomesha
  walimu wazawa ili kuweza kukidhi nakuwa na walimu na kupunguza gharama za kuchukua mwalimu kutoka nje yanchi ambapo hivi sasa wamemuajiri raia kutoka Sri lanka hali ambayo wanatumia gharama kubwa kumlipa mtaalamu huyo toka nje ya nchi.

  Shanyangi aliwataka wadaumbalimbali nchini pamoja na wawekezaji
  wawekeze katikak kufundisha wataalamu wazawa ili kuweza kukidhi
  mahitaji ya wakataji na wataalamu nchini.

  Kituo hicho kimegharimu zaidi ya shilingi billion 1.2na mashine
  mbalimbali za kituoni hapo zimegharimu zaidi ya milioni 450 za ukataji
  na kusafisha madini hayo Kwa upande wake mwanafunzi katika chuo hicho
  Bi.Joice Patrick alisema kuwa kupitia mafunzo hayo ya ukataji wa
  madini na ung'arishaji itawasaidia katika swala zima la ajira huku
  akiwataka wanawake kuchangamkia fursa hiyo "Ni fursa sasa kwa wanawake kujitokeza katika kazi hii na waione kama kazi zingine na si kuwaachia wanaume tu "alisema Joice

  0 0  Ulikuwa ni usiku wa manane majira ya saa nane na nusu, ambapo Mzee Jengo alikuwa amepumzika kitandani akiwa na mtoto wake wa kiume ambaye alikuwa anaitwa Rony.
  Alikuwa ni kijana mdogo mwenye umri  kati ya miaka nane au tisa, Usiku huo hali ya Mzee Jengo ilikuwa si nzuri kwani alianza kujisikia vibaya ghafla kiasi kwamba hata alipojaribu kunyanyuka alishindwa. Kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyasikia aliamua kumuamsha mtoto wake, taratibu alinyoosha mkono na kuanza kumvuta Ronyhuku akizungumza kwa sauti ya unyonge sana.


   “Rony, Rony …..aaaaa…amka ukamwambie ….dada mimi naumwa, Rony mwanangu nenda kamwite dada yako najisikia vibaya sana” Alikuwa akizungumza kwa shida sana, lakini Rony alimsikia, na kwa haraka aliamka huku akiwa anafikicha macho yake kutokana na kushtuka kutoka usingizini, alimtizama baba yake, na moja kwa moja alishuka kutoka kitandani huku akiwa anamuuliza Baba yake, “Baba unaumwa nini,  nani atakupeleka hospitali Baba,”. 


  0 0

  nchimbi 3

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Mkoani Ruvuma.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

  Mwenyekiti wa maandalizi ya sherehe za maika 38 ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi amesema kuwa chama chake kina kila sababu ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuwa kina mfumo na muundo imara.

  Akizungumza muda mfupi baada ya maadhimisho hayo mjini Songea, Dkt Nchimbi ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho alisema kuwa chama chake hakina tatizo la kimfumo wa muundo na kuongeza kuwa ushindi ni lazima. “Chama hakina tatizo la muundo wala mfumo na tutakachofanya ni kubadilisha mikakati tu ili kujihakikishia ushindi katika uchaguzi ujao,” alisema
  nchimbi 4
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Mkoani Ruvuma katikati ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho.

  Aliongeza, “Kwa kwa kaida hakuna mkakati unadumu. Mar a zote mikakati hubadilika kulingana na mazingira na hiki ndicho tutakachokifanya,” Akizungumzia kuhusu kauli ya mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete kuwataka viongozi wa chama kuwatembelea wanachama na kushawishi wanachama wapya, alisema CCM ni chama kikubwa na ndani yake wapo viongozi waliolala ambao mwenyekiti wa taifa aliwakumbusha kuamka na kufanya kazi.

  “Chama hakiwezi kuwa na maisha marefu kama viongozi katika ngazi zote ha hawajitumi. Katika jeshi kubwa kama hili la CCM wapo watu ambao lazima wasukumwe na ndiyo ahwa mwenyekiti wetu wataifa aliwasukuma kupitia hotuba yake. Hawa wanatakiwa kuamka na kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kukiwezesha chama kushinda kwa kishindo kama ambavyo kimekuwa kikishinda tangu kuanza kwa siasa za vyama vingi,” alieleza
  nchimbi 2
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

  Dkt Nchimbi aliishukuru halmashauri kuu ya chama kwa kuweza kuuchagua mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya maazimisho ya miaka 38 ya chama hicho na kueleza kuwa kwa miaka mingi Ruvuma imekuwa ngome imara ya CCM.

  Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho alisema kuwa alisema kuwa chama chake kimeshaanza kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu . “Nimeshawaagiza viongozi wa chama katika ngazi ya mkoa na wilaya kuanza vikao kwa ajili ya na kuweka mikakati thabiti ya ushindi katika uchaguzi mkuu ujao,”

  Alieeleza kuwa, chama katika mkoa wake tayari kilishaanza mikakati ya kujitegemeza ikiwa ni kufuata agizo la mwenyekiti wa taifa ambapo tayari kimejipanga vyema kuendeleza vyanzo vyake vya mapato pamoja na kuanzisha vyanzo vipya kwa ajili ya kukifanya kujitegemea.
  nchimbi 1
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.

  0 0
  1
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkaribisha Ikulu Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt wakati alipowasili kwenye viwanja vya Ikulu Dar es Salaam tarehe 3.2.2015.
  2
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Suleiman Kova kwenye viwanja vya Ikulu
  3
  Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Bwana Joachim Gauck na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokea salamu ya heshima mara baada ya mgeni huyo kuwasili Ikulu akiwa kwenye ziara ya kiserikali hapa nchini.
  45
  Rais Jakaya Kikwete na Mke wake Mama Salma wakiandamana na wageni wao Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Bwana Joachim Gauck na Mke wake Schadt wakingia Ikulu huku mamia ya wananchi wakishangilia kwa furaha huku wakipeperusha bendera za hizo nchi mbili.
  7
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Schadt   Ikulu.
  8
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt akifurahia jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, wakati mgeni huyo alipowasili kwenye ofisi hizo akiambatana na mwenyeji wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
  9
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mke wa Rais wa Ujerumani Mama Daniella Schadt wakipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya WAMA, Mama Hulda Kibacha (kushoto ni Blandina Nyoni (kulia) wakati mgeni huyo alipotembelea ofisi hiyo
  10
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt akiweka saini yake kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za WAMA akiambatana na mwenyeji wake Mama Salma Kikwete.
  11
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikabidhi Jarida la WAMA kwa Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Schadt wakati alipotembelea ofisi za WAMA.
  13
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi mgeni wake Mke wa Rais wa Ujerumani Mama Schadt zawadi ya kanga.
  14
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Schadt kwenye ofisi za WAMA.
  15
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Schadt akiagana na wajumbe wa bodi ya WAMA pamoja na wafanyakazi mara baada ya kutembelea ofisi hizo
  16
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiambatana na mgeni wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani Mama Daniella Scahdt wakimwangalia mgonjwa Kundi Girogui aliyetoka wilaya ya Serengeti ambaye aliyefanyiwa upasuaji wa mdomo kwenye hospitali ya CCBRT huko Msasani.
  18
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na mgeni wake Mama Daniella Schadt, Mke wa Rais wa Jamhuri ya Ujerumani mara baada ya viongozi hao kutembelea hospitali ya CCBRT huko Msasani

  0 0
  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya NBS na wadadisi wa Sensa ya Viwanda. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wadadisi 200 wa Sensa ya Viwanda itayofanyika nchi nzima  mwezi huu. Mafunzo hayo yanafanyika chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam.
   Kaimu Mkurugenzi wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Bw.Hussein Kamote akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi 200  watakaokusanya takwimu wakati wa  Sensa ya viwanda itakayofanyika nchini mwezi huu.
   Mkuu wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam Prof.Ngalinda Innocent akizungumza na wadadisi watakaokusanya takwimu za Sensa ya Viwanda mwezi huu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku 14.
   Baadhi ya wadadisi wa Sensa ya Viwanda wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukusanya takwimu sahihi wakati wa Sensa ya Viwanda leo jijini Dar es salaam.

    Mkuu wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Ngalinda Innocent akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Maria Bilia (katikati) na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makzi Bi. Hajjat Amina Mrsiho Said leo jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa  akizungumza na wadadisi 200 watakaokusanya takwimu za viwanda wakati wa Sensa ya Viwanda itakayofanyika nchini nzima mwezi huu leo eneo la Chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika jijini Dar es salaam.


  WAMILIKI WA VIWANDA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WA SENSA YA VIWANDA.

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  3/2/2015,Dar es salaam.

  SERIKALI imewataka wamiliki wa viwanda kuwapa ushirikiano wadadisi wa Sensa ya Viwanda watakaopita katika maeneo yao kwa lengo la kukusanya takwimu sahihi za viwanda  vilivyopo nchini na mchango vinaotoa katika maendeleo ya taifa.

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku 14 ya wadadisi wa Sensa ya Viwanda yanayoendelea katika chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam.

  Amesema kuwa mafanikio ya Sensa hiyo yatatokana na wamiliki wa viwanda kuthamini na kutambua umuhimu za Sensa hiyo kwa kutoa ushirikiano kwa wadadisi watakaopita katika maeneo yao kupata taarifa zinazohusu masuala mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa bidhaa na masuala ya ajira;

  Amesema upatikanaji wa takwimu sahihi kuhusu Sekta ya Viwanda nchini Tanzania utaiwezesha Serikali kuweka Sera na mipango endelevu ya maendeleo itakayoisaidia sekta hiyo kupiga hatua kimaendeleo.

  “Sensa hii ya viwanda ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu, na mafanikio yake yatatokana na wenye viwanda kutupa ushirikiano maana bila  wao kutoa takwimu sahihi mipango ya maendeleo kuhusu viwanda haitatekelezeka kwa sababu ya kukosa takwimu sahihi” Amesema Bilia.

  Kuhusu sampuli ya viwanda  vitakayoguswa na Sensa hiyo amesema  ni pamoja na maeneo ya viwanda yaliyoajiri watu wengi  na yanayohusisha uzalishaji mkubwa wa bidhaa za viwandani ,maeneo ya uzalishaji wa bidhaa za kokoto, bidhaa za vyakula na maeneo yaliyoajiri mtu zaidi ya mmoja.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema kuwa Sensa hiyo ya viwanda itakayohusisha viwanda vyote nchini inafanywa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Wizara ya Viwanda na Biashara.

  Amesema kukamilika kwa Sensa hiyo kutaliwezesha taifa kuwa na takwimu sahihi za viwanda na kutambua mchango wa Sekta ya viwanda katika uchumi wa taifa na mchango wa ajira kwa wananchi.

  Kuhusu mafunzo hayo ya siku 14 kwa wadadisi 200 watakaoendesha zoezi hilo amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupitia Chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika inaendesha mafunzo hayo kwa vitendo na nadharia ili kuwawezesha na kuwajengea uwezo wadadisi hao kukusanya takwimu bora.

  “Lengo la kuendesha Sensa hii  ni kuhakikisha kuwa nchi yetu inapiga hatua na kuwa nchi yenye maendeleo ya kati kwa kuwa na matumizi sahihi ya takwimu ztu”

  Kaimu Mkurugenzi wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Bw.Hussein Kamote akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya wamiliki wa Viwanda nchini amesema kuwa Sensa ya viwanda itakayofanyika nchini mwezi huu italiwezesha taifa  kuwa na takwimu sahihi zinazohusu sekta ya viwanda.

  “Sensa hii ya viwanda ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa nawaomba wenye viwanda watoe ushirikiano wa kutosha maana bila wao zoezi hili litakuwa gumu”

  Ameongeza kuwa Sensa ya viwanda ni muhimu kutokana na mchango wake katika nchi nyingi za Asia ambazo zimefanikiwa na kupiga hatua kimaendeleo kwa sababu ya kuwa Sensa endelevu na takwimu sahihi za sekta ya viwanda na mchango wake katika pato la taifa.


  0 0

  1
  Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha mgeni wake Ikulu Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck ambaye ameongozana na mke wake Bibi schadt leo tarehe.03.02.2015.
  2
  Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akimtambusha Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa waliojitokeza kumpekea leo tarehe.03.02.2015 katika viwanja vya Ikulu.
  3
  Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mgeni wake Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck wakipata mapokezi kwa kuimbwa kwa nyimbo za taifa za mataifa hayo mawili.
  4
  Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na kikosi cha jeshi la wananchi wa Tanzania kwa ajili yake leo katika viwanja vya Ikulu
  5
  Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na ujembe kutoka ujerumani uliondamana na Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck wakati Rais huyo alipowasili Ikulu.
  6810
  Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck akipokelewa na wanafanyakazi wa Ikulu,wananchi mbalimbali pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za mkoawa wa Dar es salaam waliojitokeza viwanja vya Ikulu leo tarehe.03.02.2015 kumpokea.
  11
  Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck Ikulu na kufanyanaye mazungumzo.
  12
  Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck pamoja na ujumbe wake . (PICHA ZOTE NA FREDDY MARO)

  0 0

   Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhandishi Athumani Mfutakamba akisoma taarifa ya kamati hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo bungeni mjini Dodoma.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yaMasuala ya Ukimwi Lediana Mng'ong'o akiwasilisha taarifa ya kamati yake.
   Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma.
   Baadhi ya wageni waliofika kwenye Bunge la Jamhuri wakifuatilia Bunge.
   Baadhi ya wabunge wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma akiwemo Mbunge wa Morogoro Kusini Dkt. Lucy Nkya (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Jasson Rweikiza.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mhe. Kapt (Mstaafu) George Mkuchika (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge kwenye mlango wa Bunge mjini Dodoma.Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO,Dodoma

  0 0

   Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akijibu swali Bungeni mjini Dodoma.

  Na Lorietha Laurence-Maelezo Dodoma.

  Naibu Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia amewataka wamiliki wa vyombo vya habari  kuwakatia wafanyakazi wao bima ili ziweze kuwasaidia wakati wanapopatwa na madhara wakiza kazini.

  Akijibu swali la mbunge wa viti maalum Anna Mallac,  kuhusu mpango wa Serikali kuwapatia ulinzi waandishi pale wanapokuwa wakifanya kazi katika matukio hatari, Naibu Waziri  Nkamia alisema kuwa serikali  inafahamu mazingira ya kazi ya wanahabari na inawajibika kikatiba katika kutoa ulinzi kwa raia wake wote wakiwemo wanahabari.

   “Uandishi wa habari ni taaluma kama zilivyo taaluma  nyingine muhimu katika jamii kama ilivyo taaluma ya sheria ualimu na udakatari na ni muhimu kufahamu  na kuzingatia miiko ya taaluma pale wanapokuwa katika eneo la kazi”alisema Nkamia.

  Aidha alibainisha kuwa  jukumu la kwanza kwa waandishi wa habari ni kujilinda na kujihami wao wenyewe kwa kuwa wanayafahamu mazingira yao ya kazi na pia kuzingatia  miiko ya taaluma yao kwa kuangalia wanayotakiwa kufanya na kutofanya katika eneo husika. Aliongeza kuwa wanahabari wanatakiwa wazingatie sheria bila shuruti kwa kuwa nao ni wananchi kama walivyo wananchi wengine na hakuna aliye juu ya sheria .

  Hata hivyo Serikali  imekuwa ikiwapatia waandishi wa habari vifaa maalum katika matukio mbalimbali ya kitaifa  ikiwemo vitambulisho na mavazi maaalum ya kuwatambulisha wakiwa katika eneo la kazi ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuwalinda na madhara yeyote.

  Naibu Waziri Nkamia alieleza kuwa kwa sasa wizara yake imekuwa ikiandaa muswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao utawasilishwa mbugeni wakati wowote kuanza sasa.                                                         
    

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (wa pili kushoto) akizungumza katika mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.Ujumbe huo unaongozwa na Waziri wa Masuala ya Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig (wa pili kulia). Picha zote na Othman Michuzi.
  Mratibu wa Uwekezaji wa Kimataifa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Zacharia Kingu akifafanua jambo wakati akiwasilisha taarifa ya uwekezaji katika maeneo mbali mbali nchini wakati wa mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.
  Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani pamoja uongozi wa TIC ukifatikia kwa makini taarifa ya uwekezaji iliyokuwa ikitolewa na Mratibu wa Uwekezaji wa Kimataifa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Zacharia Kingu (kushoto).

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (katikati) akitoa ufafanuzi wa maswala mbali mbali ya uwekezaji kwa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani waliotembelea kituo hicho jana jioni,jijini Dar es salaam.
  Kiongozi wa Msafara wa Wafanyabiara hao ambaye ni Waziri wa Masuala ya Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki. 
  Meneja wa Kitengo cha Uratibu Miradi ya Ubia (Sekta ya Umma na Binafsi) wa TIC,Said Amir akitoa ufafanuzi juu ya maswala ya ubia katika miradi,wakati wa mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.
  Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirika wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Revocatus Arbogust akichangia jambo katika mkutano huo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (katikati) akifafanua jambo katika mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.
  Kiongozi wa Msafara wa Wafanyabiara hao ambaye ni Waziri wa Masuala ya Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig akizungumza na mmoja wa wafanyabiashara aliofatana nao.
  Sehemu ya Wafanyabiashara hao wakifatilia kwa makini taarifa ya uwekezaji.
  Sehemu ya Ujumbe wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ukifatilia kwa makini mkutano huo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (wa pili kushoto) akiongea na ujumbe huo wakati akiwaonyesha moja ya Jengo lilalotumiwa Kituo hicho lililojengwa na Wajerumani.

  0 0

  IMG-20150203-WA0039
  Waziri wa maji profesa jumanne maghembe akielezea utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa BRN chini.
  ....................................................

  Waziri wa maji kupitia mpango wa BRN,kuanzia mwaka 2013 hadi sasa,imefanikiwa kuwafikishia maji wananchi milioni 4.3 wanaoishi maeneo ya mijini Aidha zaidi ya watu milioni 2 wanaoishi maeneo ya vijijini wamepatiwa huduma ya maji kupitia BRN.

  Waziri wa maji profesa jumanne maghembe ameyasema hayo Februari 3, 2015 mjini Dodoma alipokuwa akizungumzia utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa BRN chini ya wizara ya maji katika ukumbi wa Fr.Vicent uliyopo ndani ya hotel ya St.Gasper

  Profesa Maghembe amesema kuwa,mpango huo wa BRN umeonyesha kwa muda mfupi tofauti na ule mpango wa Taifa wa maji uliyonza mwaka 2017 hadi mwaka 2014,Amesema serikali kupitia mpango wa BRN itahakikisha inawafikishia wananchi maji katika maeneo mbali mbali ili kuwapunguzia kero ya maji.

  Kadhalika Maghembe amewataka wafanyakazi wa mamlaka za maji hapa nchini kufanya kazi kwa kasi kubwa na sio mazowea,Katika mkutano huo viongozi wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira za miji mikuu ya mikoa zimetia saini makubaliano ya miradi ya maji na mazingira kwa kutumia utaratibu wa BRN

older | 1 | .... | 453 | 454 | (Page 455) | 456 | 457 | .... | 1897 | newer