Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 448 | 449 | (Page 450) | 451 | 452 | .... | 1898 | newer

  0 0

  By Abou Shatry Washington DC
  Zaidi ya watu 60 million wataadhithika kutokana na kimbunga kikubwa cha upepo unaoambatana na unyeshaji wa theleji katika eneo la kaskazini mashariki ya Marekani.
  A plow truck clears snow off South Church Street, in Hazleton, Pennsylvania on Monday. The area received another three-inches of snow overnight
  Lori maalumu la usafishaji likiondoa theluji iliondoka barabara ya South Church Street, katika mji wa Hazleton, Pennsylvania siku ya Jumatatu Jan 26, 2015. Photo via .dailymail.co.uk.
   
  Kwa mujibu wa kitengo cha hali ya hewa nchini Marekani, imetaja maeneo ambayo yataathiriwa na tharuba hiyo, ya kihistoria ambayo itapelekea zaidi ya watu kadhaa kukosa huduma ya umeme, pamoja na huduma za usafiri wa anga na nchi kavu.
  Imetaja baadhi ya majimbo ambayo yatakumbwa na kimbunga hicho kuwa ni New York, New Jersey, Massachusetts, Connecticut na Rhode Island, ambapo viongozi wakuu wamajimbo hayo kutangaza hali ya hatari kwa tukio hilo ambalo litatokea siku ya Jumatatu, Jumanne na Jumatano.
  Imetabiriwa kiasi cha unyeshaji wa theluji hiyo 36inches katika jimbo la New York 16 hadi 26 inches katika jimbo la Boston, na kiwango chengine kama hicho katika baadhi ya majimbo mengine.
  Zaidi ya safari za ndege 3,800 zimesimamishwa mapema leo Jumaatatu katia viwavya vya ndege vya JFK, LaGuardia na Newark airports, pia huduma za shule kufungwa siku ya jumanne na jumatano katika majimbo hayo.

  0 0
  0 0


  0 0

  3
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau  akifafanua jambo kwa wageni waliohudhuria hafla fupi ya kusaini mkataba  kati ya shirika hilo na timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Dk. Dau alisema katika uendeshaji wa kituo hicho, Real Madrid itakua na dhamana ya kushughulikia masuala yote ya ufundi, kuwatambua wachezaji, chakula, wataalamu wa saikolojia na wataalamu wa viungo na kwamba wajibu wa shirika lake utakuwa kwenye kujenga tu.
  2 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (aliyekaa kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (aliyekaa kulia) kwa pamoja wakisaini mkataba wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja.
  1
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (kulia) wakibadilishana mikataba ya kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja.
  5
  Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez akifafanua jambo kwa wageni waliohudhuria hafla fupi ya kusaini mkataba  kati ya timu yake  na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kitahusisha wanafunzi 108 watakaogawanywa kwenye timu za chini ya umri wa miaka 13, 15, 17, 19, kikosi cha pili na timu ya wakubwa.
  …………………………………………………

  SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeingia mkataba na klabu maarufu duniani ya Real Madrid ya Hispania wa kujenga kituo cha michezo kwa ajili ya kuzalisha vipaji. 

  Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo wa miaka 18, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhani Dau alisema ujenzi huo utagharimu Sh bilioni 16 na unatarajiwa kuanza kujengwa Mei mwaka huu na kwamba utakamilika baada ya miezi 18.Dk Dau alisema kituo hicho ambacho kitajengwa kwenye kijiji cha michezo cha shirika hilo (NSSF Sports City), kitakuwa eneo la Mwasoga, Kigamboni, Dar es Salaam. 

  “Tuna eneo la zaidi ya ekari 400 ambapo tutajenga viwanja, shule ya michezo, nyumba za kuishi na maduka. Lengo letu tuzalishe na kuuza wachezaji. Tunakusudia kuwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 13, 18, 20, timu B na timu ya wakubwa,” alisema Dk Dau. 

  Alisema utekelezaji wa kituo hicho utaanza hivi karibuni kwa kutumia majengo ya kukodi wakati wakisubiri ujenzi kukamilika.“Hivi hapa baada ya kusaini mkataba, utekelezaji utaanza kwa kutumia majengo ya kukodi ambayo tunadhani yatakuwa maeneo ya Temeke na tutakuwa tukitumia viwanja vya Karume na Uhuru,” alisema. 

  Mkurugenzi Mkuu huyo wa NSSF alisema katika kuendesha kituo hicho, kila kitu kitafanywa na Real Madrid kuanzia masuala yote ya ufundi, kuwatambua wachezaji, chakula, wataalamu wa saikolojia na wataalamu wa viungo na kwamba wajibu wa shirika lake utakuwa kwenye kujenga tu. 

  “Sisi tunachukulia huu mradi ni uwekezaji na hatufanyi hisani, itazingatia misingi ya biashara na faida kubwa ni kwamba NSSF itaongeza kipato, lakini pia kituo kitatumika kuitangaza Tanzania kwa sababu yatakayofanyika yataoneshwa kwenye televisheni ya Real Madrid,” alifafanua Dk Dau. 

  “Lakini pia wakati umefika sasa kwa Tanzania kushiriki Kombe la Dunia Qatar 2022, kama unaandaa vizuri vijana wa miaka 13 sasa mpaka mwaka 2020 wanaweza kuwakilisha vizuri kwenye mechi za kufuzu na mwaka 2022 wakashiriki Kombe la Dunia, wakikosa la Qatar, basi hata hizo zinazokuja, hiyo pia ni moja ya madhumuni ya kituo hicho.” 

  Akizungumzia namna walivyofikia uamuzi wa kujenga kituo, Dk Dau alisema wazo hilo lilipatikana Agosti mwaka jana na kisha likapelekwa kwenye Mkutano wa Wanachama uliofanyika Arusha ambako waliazimia NSSF iwekeze rasmi kwenye michezo kabla ya kuwasilishwa kwenye bodi na utekelezaji kuanza kufanyika. 

  “Tulitembelea sehemu nyingi kuona wenzetu wanafanyaje. Binafsi nilitembelea nchi kadhaa za Ulaya, nilienda kituo cha Manchester United, Sunderland, Real Madrid kwa hapa Afrika nilikwenda Asec Mimosas (Ivory Coast) na TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC) kuona wanafanyaje, ziara ikazaa matunda kwani tulikubaliana na Madrid na ndio wamekuja kusaini mkataba leo (jana),” alifafanua Dk Dau. 

  Naye Mkuu wa Vituo vya Michezo wa Real Madrid, Rayco Garcia aliishukuru NSSF wa kuwa na mpango huo na kuahidi kufanya kazi ili kuipatia Tanzania mafanikio. “Tukifanikiwa kuwatoa vijana hao, Tanzania itaweza kushiriki kwenye michuano mikubwa kama alivyosema Dk Dau, inabidi tufanye kazi ili vijana wafanikiwe, wafike mbali,” alisema Garcia. 

  Mbali na Garcia ambaye pia ni kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18 ya Madrid, wengine walioambatana kwenye msafara huo ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu hiyo, Ruben de la Red, Kocha Mkuu wa timu za vijana, Francisco Martin Ramos na Juan Jose San Roman Milla. Mwaka jana, wachezaji wa zamani wa Real Madrid walifanya ziara nchini.

  0 0

   
   Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali Mstaafu Ludovick Utoah akitoa nasaha katika hafla ya kuagwa kwake aliyoandaliwa na taasisi ya wakaguzi wa hesabu binafsi nchini.
   Mwenyekiti wa taasisi  ya wakaguzi wa hesabu binafsi nchinin Bwana Chacha akimpongeza Bwana Utouh baada ya hotuba yake.
  Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma Zitto Kabwe  akimpongeza  CAG mstaafu katika hafla ya kuagwa kwake aliyoandaliwa na taasisi ya wakaguzi binafsi wa hesabu nchini.

  0 0

  Mapenzi yanamfanya mtoto wa senetor Michael Nsonko kutoka Nairobi Kenya na kuja katika jiji la mwanza Tanzania. Alivutiwa sana na jiji hilo nakujiona ni mwenye bahati. Je kila kiang'aacho ni Dhahabu?. Fuatilia hii kupitia mtandao .......

  Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania mtandaoni iitwayo I LOVE MWANZA au Kununua na iwe yako tembelea tovuti ya 


  Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

  0 0


  Na Anitha Jonas - MAELEZO.

  SERIKALI imedhamiria kupunguza msongamano wa magari  ndani ya jiji la Dar es Salaam kwakujenga barabara sita zitakazo ambazo ujenzi wake utasimamiwa na TANROADS. Ujenzi huo unatarajiwa kugharimu sh. trilioni moja ambapo lengo barabara hizo ni  kupunguza adha ya msongamano wa magari  katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es saalam.

  Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara hizo. “Barabara hizi zinajenga kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 na lengo kubwa la mradi huu ni kupunguza msongamano ndani ya jiji” alisema Magufuli.

  Magufuli aliendelea kusema “Rai yangu kwa Watanzania  wote ikiwemo madereva wa magari yenye uzito mkubwa  kuacha kupita barabara zisizo stahimili uzito wa magari hayo na kuwaasa wananchi wa maeneo jirani waache  kugeuza  barabara hizo kuwa maduka au fremu za biashara”.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Said Mecky Sadick aliwaasa wananchi wa Dar es Salaam kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali na wakandarasi pale watakapoombwa wasogee  nje ya barabara ili kufanikisha ujenzi huo kwani barabara ni sehemu ya maendeleo na ni vyema kila mmoja kuwa mzalendo na kuacha itikadi za vyama .

  “Nikiwa kama mdau mkubwa wa maendeleo ya jiji la Dar es Salaam nitahakikisha wakandarasi hawa wanamaliza kazi ya ujenzi huu  kwa wakati na nitakuwa nikiwafuatilia kwa karibu katika kuhakikisha  viwango  vinazingatiwa  ili barabara hizi ziweze kuwa mkombozi wa tatizo la msongamano katika jiji,” alisema Sadick.

  Kwa upande wake Mtendaji  Mkuu Wakala wa Usimamizi wa Barabara (TANROADS) Mhandisi  Patrick Mfugale alizitaja barabara zinazotarajiwa kuanza kujengwa katika mradi wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam ni Ubungo Msewe hadi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 2.6, Ubungo Externo hadi Kilungule kilomita 3, Kigogo hadi Tabata Dampo kilomita 1.6.

  Mfugale alisema kuwa barabara nyingine ni Kinyerezi hadi Kifuru kilomita 4 kwa awamu ya kwanza na badae ni Kifuru hadi Maramba Mawili kilomita 10, pamoja na Mbezi Mwisho hadi Goba Tangi Bovu ambayo ni kilomita 20.
  Katika Ziara hiyo ya kuweka jiwe la msingi Waziri Magufuli aliambatana na watendaji na viongozi wa TANROADS, wabunge wa maeneo hayo, watendaji wa wizara.
                                    

  0 0

  Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mh Egon Kochanke akitoa historia fupi ya wahanga wa maangamizi Makuu ya Moto Dhidi ya Wayahudi katika maadhimisho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Utamaduni wa Russia na kuandaliwa na Umoja wa Mataifa Tanzania.
   Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi Usia Nkhoma akiwakaribisha wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar pamoja na wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Jijini Dar ambavyo Kuna Klabu za Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa utamaduni wa Russia wakati wa Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha na kuwakumbuka wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto Dhidi ya Wayahudi.
   Stella Vuzo, Afisa habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC) akimwelezea Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Mh Egon Kochanke wakati alipotembelea katika ukumbi wa Utamaduni wa Russia ambapo baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu waliweza ushiriki katika Kuadhimisha na Kuwakumbuka Wahanga Wa Maangamizi Makuu ya Moto dhidi ya Wayahudi.
   Balozi wa Ujerumani, Mh Egon Kochanke akisoma moja ya bango lililobandikwa katika Ukumbi wa Utamaduni wa Kirusi wakati wa Maadhimisho ya Wahanga wa Mahangamizi Makuu ya moto yanayofanyika kila tarehe 27 January kwaajili ya kumbukumbu
    Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani, Kibasila, Azania na Kisutu wakisoma moja ya bango lenye historia fupi ya Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto.
   Stella Vuzo, Afisa habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC) akimwelezea Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Mh Egon Kochanke wakati alipotembelea katika ukumbi wa Utamaduni wa Russia ambapo wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo waliweza kupata historia fupi ya Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto
   Wanafunzi wakifuatilia historia fupi ya Wahanga iliyokuwa ikitolewa na Afisa Habari wa UN, Bi Usia Nkhoma
   Stella Vuzo, Afisa habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC) akitoa neno mbele ya Mgeni rasmi ambae ni Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Mh Egon Kochanke wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya maadhimisho na kumbukumbu ya Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto dhidi ya Wayahudi ambapo maadhimisho hayo ufanyika kila tarehe 27 Januari.Picha Zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

  0 0


  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linapenda kuwatangazia Wasanii na wadau wote wa Sanaa nchini kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kifungu namba 5 (1) cha Sheria namba 23 ya mwaka 1984 iliyolianzisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) amemteua ndugu Godfrey Lebejo Mngereza kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

  Barua ya Januari 16, 2015 iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga imeeleza kwamba uteuzi wa Mngereza unaanza Januari 23, 2015. 

  Kabla ya Uteuzi huo Bwana Mngereza alikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA kwa kipindi cha kutoka Februari 2013 hadi 2015 mwanzoni akitokea Idara ya Utafiti na Stadi za Wasanii ya BASATA aliyokuwa akiiongoza kama Mkurugenzi wake.

  Godfrey Mngereza ni msomi mwenye shahada ya uzamili (MA) katika masuala ya Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amepata kuwa Mwalimu wa Chuo Kikuu hicho katika Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho (FPA) hadi mwaka 2008 alipoajiriwa rasmi na BASATA kama Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari ambayo kwa sasa inafahamika kama Idara ya Utafiti na Stadi za Wasanii.  Aidha, shahada yake ya kwanza ilikuwa katika masuala ya Sanaa aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

  Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
  Imetolewa na Kitengo cha Habari- BASATA


  0 0

  1
  Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wa pili kushoto akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Eng. Harold D. Sawaki katikati walipofika Wilaya ya Rungwe jana kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa Wilaya hiyo. Kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Ason Nzowa, wa pili kulia ni Afisa Michezo na Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George Mbijima na wa kwanza kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga.
  2
  Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga kulia akizungumza na vijana wa Wilaya ya Rungwe wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana karika Wilaya ya Rungwe. Katikati ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa na kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.
  3
  Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana karika Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
  4
  Kijana Daudi Essau Seme kutoka katika kikundi cha Tukuyu Bodaboda Saccoss Limited akichangia wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana karika Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
  5
  Baadhi ya vijana wa Wilaya ya Rungwe katika kikundi wakijadiliana namna ya kuandika andiko la mradi baada ya kuelimishwa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
  7
  Maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa makini kijana Boniel Soka (kushoto) kutoka kikundi cha Muungano Makandana kinachojishughulisha na upandaji miti ya aina mbalimbali wakati wa ziara ya kukagua miradi ya vijana wa Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya. Picha zote na : Genofeva Matemu – Maelezo. Rungwe, Mbeya

  0 0

  Na Samia Mussa.
   
  WAKATI wakazi wa mikoa kadhaa hapa nchini wakiomba Tamasha la Pasaka lipite kwenye mikoa yao, baadhi ya waimbaji wakongwe wa tamasha hilo linalotimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake,  wametoa mapendekezo yao kwa wandaaji Kampuni ya Msama Promotions.
   
  Wakizungumza hivi karibuni waimbaji hao, walianza kwa kuipongeza Kampuni hiyo kufikisha miaka hiyo bila kutetereka huku wakitoa mapendekezo mbalimbali yatakayoboresha zaidi matamasha yajayo.
   
  Moja ya mapendekezo hayo ni pamoja na kutaka kila mwimbaji apate nafasi  angalau ya kuimba nyimbo mbili ukizingatia waimbaji hao wana albamu zaidi ya tatu jambo ambalo kwao linawapa ugumu kwao pamoja na mashabiki.
   
  Hayo alisemwa na mwimbaji nguli Upendo Nkone ambapo alisema licha ya kampuni hiyo kujitahidi kufanya vizuri ikiwa pamoja na kuimba kwa kutumia vyombo hivyo Kamati ya Maandalizi inatakiwa kubadilisha vitu vichache ikiwemo kupewa dakika za kuimba kama wanavyofanya nchi zilizoendelea si moja kama ilivyozoeleka.
   
  “Kile ambacho naona kiwekewe mkazo tunaposema tutaimba’live  basi tufanye live kweli na mazoezi yaanze mapema wiki mbili kabla ili mwimbaji afanyie mazoezi nyimbo atakazoimba halafu tunaomba kila mwimbaji angalau aimbe nyimbo mbili, lakini utakuta unaimba nyimbo moja tu kama mimi nina albamu nne nina nyimbo nyingi ambazo watu wanazipenda unapoimba nyimbo moja, watu wanakuwa hawajatosheka kwa sababu wamelipa kiingilio,” na kuongeza.
   
  “Idadi ya nyimbo ingozeke, wenzetu nchi nyingine wanatoa dakika 20-30 kwa kila muimbaji kwa hiyo unangalia nyimbo zenye dakika kati ya 5-7 unachanganya  kwa hiyo nusu saa unaweza ukaimba nyimbo mbili au tatu,”  alisema Nkone.
   
  Nkone pia alitoa pendekezo kupata wajuzi wa muziki ili nyimbo hizo zipigwe kama zilivyo huku akitolea mfano kuwa yeye nyimbo zake zinatengenezwa na wenye upeo wa muziki hivyo lazima zipigwe vile ninavyotengenezewa kwenye CD yake, kwenye ‘live’ kuna vitu vinapungua hivyo awawekee wajuzi wa hali ya juu.
   
  Alisema kuwa sababu nyingine itakayofanikisha maendeleo zaidi katika Tamasha hilo la 15 itafanya Msama Promotions iwe katika kiwango cha juu kwa sababu inabeba waimbaji vingunge waimbaji wazito ni kuanza mazoezi mapema na kwa taratibu zilizopangwa, kupatiwa ratiba ya kila muimbaji ajitambue cha kufanya kabla ya kupanda jukwaani.
   
  Upendo Kilahiro  anaipongeza Msama kwa kutimiza 15 tangu imeanza kuandaa tamasha hilo kubwa hapa nchini, huku akiiomba kampuni hiyo kubwa kumiliki vyombo vyake ambavyo vitatumika katika matamasha yake.
   
  “Naomba Mungu Msama ingepata vyombo vyake kwa sababu  ni kampuni ya muda mrefu na muda huu wote tunakodisha, ingepata vyombo katika ule ubora wake tunaohitaji tukivimiliki wenyewe tutajua muda gani tutavifunga na injinia wenu atakaa sawa avirekebishe  kwa hiyo hadi tamasha linanza hakuna ucheleweshaji”. 
   
  “Kwa sababu vifaa vitakuwa vimekaa vizuri na kwa kuwa ni vyenu mnakuwa mnavijua na mtakuwa mnajua udhaifu mmepiga hatua kubwa, miaka 15  mmeweza kumiliki vyombo vyenu ambavyo vikafaa uwanja wa wazi na ndani itakuwa ni hatua moja na tutawakilisha vizuri kazi zetu  mara nyingi sauti zimekuwa zikituchelewesha kuanza,” alisema Kilahiro.
  Mwimbaji huyo alisema kuwa endapo vyombo vitapatikana Saundi ikiwa nzuri mwimbaji yeyote atafurahi na kazi yake itaonekana na hata watu watafurahi.

  0 0  index
  Na Maryam Kidiko / Kijakazi Abdallah – Maelezo Zanzibar  .
     
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Kuna umuhimu mkubwa Zanzibar kuwa na Afisa muandamizi wa cheo cha Naibu Kamishna wa Mamlaka wa Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kusimamia ukusanyaji wa Mapato yatokanayo na  ushuru wa Fedha na ushuru wa bidhaa  katika juhudi za  kuimarisha shughuli  za uchumi wa Zanzibar.

  Hayo yalisemwa na  Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee wakati akijibu suali la Mh, Jaku Hashim Ayoub Jimbo la Muyuni alietaka kujua kama kuna  ulazima wowote wa TRA kuwa na Afisa muandamizi wa cheo  hicho Zanzibar.

  Amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania  ni Taasisi ya Muungano iliyoundwa kwa mujibu wa sheria Na.11 ya mwaka 1985 ambapo inapaswa kuwa na  Ofisi yake Zanzibar.
  Amesema kuwa kazi ya TRA Zanzibar nikukusanya Mapato ya Muungano yanayotokana na kodi ya Mapato,  Ushuru wa Fordha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini kama ilivyoainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.'

  Ameongeza kuwa kodi itokanayo na ushuru wa Forodha inasimamiwa na Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya 2004 na kwa mujibu wa sheria hiyo Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni moja kati ya sehemu ya nchi wanachma wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Waziri wa Fedha alieleza kuwa  sheria ya ushuru ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki imeweka utaratibu wa uwekaji thamani Bidhaa zinazotoka Nje na Ndani ya Nchi ya Wanachama wa Jumuiya hiyo.


  Amesema kwa  vile Zanzibar ni kisiwa  kutumia Viwango vya Kodi moja kunaweza kuathiri Uchumi wake hivyo Serikali imeweka utaratibu wa viwango vya kodi tofauti kama ilivyoainiswa katika sheria ya ushuru wa Forodha wa bidhaa zinazoingizwa Zanzibar kwa madhumuni ya soko na matumizi ya ndani.Jumla ya skuli ishirini na moja (21) za sekondari zimejengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzinar kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (Badea).

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Zahra Ali Hamad  ameeleza hayo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilshi Chukwani wakati akijibu suali la Mwakilishi  wa Rahaleo Nassor Salim Ali  aliyetaka kufahamu   mpango  wa Serikali  wa kujenga majengo mapya ya kisasa ya ghorofa katika skuli  ya  Mwembeshauri iliyondani ya Jimbo lake kama bado upo.
  Bi. Zahra amemuhakikishia Mwakilishi huyo kwamba mpango wa kujenga skuli ya ghorofa katika eneo la skuli hiyo upo kutokana na kubainika kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi katika mitaa ya karibu na skuli hiyo.

  Alisema kuwa mbali na utekelezaji wa mpango  huo,  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na mfuko wa OPEC inakusudia kujenga skuli kumi  10 za ghorofa ambapo mradi huo ulichelewa kuanza kutokana na kutokamilika  taratibu za kisheria kuhusu makubaliano ya mkopo. Wakati huo huo Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati  inakusudia kumaliza  tatizo la upatikanaji wa huduma za maji ifikapo mwaka 2017 kwa Wananchi wa Mji mkogwe na Ng’ambu.

  Hayo yameelezwa na Naibu  Waziri wa wizara hiyo   Mh. Haji Mwadini Makame wakati akijibu suali la Muwakilishi Ali Salum Haji (Jimbo la Kwahani) alitaka kujua  juhudi za serikali za kuondoa tatizo hilo linalowakabili wananchi wengi hasa sehemu za mjini.

  Amesema kuwa wanakusudia kumaliza tatizo kwa kuimarisha huduma hiyo kwa kuimarisha miundo mbinu ikiwemo kubadilisha  Mabomba ya zamani  ambayo yamechoka na kushindwa kuhimili ongezeko kubwa la wahamiaji.

  Aidha alisema kuwa hali ya upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Mjini inaendelea kuimarika siku hadi siku ambapo kuna baadhi ya maeneo yanapata Maji kwa muda mrefu na mengine yanapata maji kwa mgao hasa wakati wa kiangazi  na maeneo machache hukosa kabisa. Alisema kupitia Mamlaka ya maji wamekuwa wakifanya juhudi kutafuta  ufumbuzi  wa suala hilo ikiwa ni pamoja na  uchimbaji wa Visima  vipya katika maeneo mbali mbali.                      
                                                       
  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0  4
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiapa Bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2015.
  5
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Masaju (wapili kulia) baada ya mwanasheria huyo kuapishwa Bugeni mjini Dodoma Januari 27, 2015.
  1
  Spika wa Bunge, Anne Makinda akiongozwa na Mpambe kuingia kwenye ukumbi wa Bunge Januari 27, 2015.Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu.
  2
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama,Bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2015.
  6
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua nasari, Bungeni Mjini Dodoma Januri 27, 2015.
  7
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Momose Cheyo, Bungeni mjini Dodoma Januri 27, 2015.
  8
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Juliet Masaju (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum, Felista Bura (katikati) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Januari 27, 2015
  9
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na mbunge wa igalu, Mhandisi Athumani Mfutakamba (kushoto) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Januari.
  10
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma  Januari 27, 2015.

  0 0

  7
  Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima (katikati) akielezea maendeleo ya mradi wa Kinyerezi I. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene. Kushoto kabisa ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava.
  10
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akifafanua jambo katika ziara hiyo.

  13
  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kituo cha kuchakata gesi cha Kinyerezi.
  17 Sehemu ya mtambo wa kuchakata gesi wa Kinyerezi
  18
  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage.
  16
  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na wataalamu wa mradi wa kuchakata gesi wa Kinyerezi.


  1
  Mtaalamu kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro iliyopewa kazi ya kujenga kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I Clas-Eirik Strand (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) Katikati ni Meneja Mradi wa Kinyerezi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima.
  2
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage akisalimiana na baadhi ya wataalamu kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro iliyopewa kazi ya kujenga kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I mara baada ya kuwasili kituoni hapo. Aliyeambatana naye kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava.
  3
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio (kulia) mara baada ya kuwasili katika kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi.
  4
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio kwenye eneo la mradi wa Kinyerezi I.
  5
  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye eneo la kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I.
  6
  Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima ( aliyetangulia mbele) akiongoza msafara wa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene kwenye eneo la mradi.


  0 0

   Hayawi hayawi yamekuwa , Dk. Neema Nalitolela (kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na mpambe wake Winne Temu (kulia) wakifurahia jambo wakati wa sherehe ya kumuaga (Send off) iliyofanyika  hivi karibuni katika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam.
   DK. Neema Nalitolela akikata keki wakati wa sherehe ya kumuaga (send off ) huku akishuhudiwa na wazazi wake  Mr &mrs Nalitolela( kushoto)   na upande wa wazizi wa mmewake mtarajiwa Mr&mrs  Kabyemero( kulia)  sherehe hiyo ilifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam, Neema ni  Daktari wa magonjwa ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
    Dk. Neema Nalitolela akipongezana na mpambe wake Winne Temu wakati wa sherehe ya send off yake iliyofanyika  hivi karibuni katika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam. Neema ni  Daktari wa magonjwa ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
   Nakupemda sana naomba ukanitunze vyema ,Dk Neema  Nalitolela akimkabidhi zawadi mmewake mtarajiwa Thomas Kabyemero zawadi  wakatiwa sherehe ya kumuaga iliyofanyika hivi hivi karibuni katika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam.
   TUDUMISHE MILA ZETU KWANZA HAPO TUTAUONA UZEE. DK. Neema Nalitolela akiwana furaha  wakati  alipomkarisha mme wake mtarajiwa Thomas Kabyemero kumuonyesha mira na desturi za kwao   za Wayao wakati wa sherehe ya kumuaga send off iliyofanyika  hivi karibuni katika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam.

   TUDUMISHE MILA ZETU KWANZA HAPO TUTAUONA UZEE. DK. Neema Nalitolela akiwana furaha  pamoja na  mme wake mtarajiwa Thomas Kabyemero wakati aalipokuw akichezewa ngoma ya Kimira ya  Wayao wakati wa sherehe ya kumuaga send off iliyofanyika  hivi karibuni katika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam.
   Baba mzazi wa bibi harusi mtarajiwa DK. Neema Nalitolela akiwa na familia yake akitoa nasaha kwa njia ya kuimba shairi wakati wa sherehe ya kumuaga mwanae (send off ) iliyofanyika  hivi karibuni katika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam. Neema ni  Daktari wa magonjwa ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
   Familia na wanakamati wakicheza muziki wakati wa wa sherehe ya send off yake iliyofanyika  hivi karibuni katika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam.
    Biharusi mtarajiwa Dk.Neema Nalitolela akiwa na mpambe wake Winne Temu wakimiminiwa shampeni na mmoja wa maraki zao wakat wa sherehe ya kumpongeza Send off iliyofanyika hivi karibunikatika ukumbi wa Marantha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam
   TUNAMSHUKURU MUNGU TUMEFANIKISHA TUNAMTAKIA NDOA NJEMA.Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya kumuaga Dk,Neema Nalitolela akiwa katika picha ya pamoja na wanakamati wote .
  HII SIKU NILIINGONJEA SANA ACHA NICHEZE LEO Bibi harusi mtarajiwa Dk. Neema Nalitolela akiwa na mpambe wake Winne Temu wakiingia ndfani ya ukumbi kwa stari ya kucheza muziki .

  0 0

  Afisa Mtendaji Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Kamugisha Kazaura (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa MS Huawei Technologies,Bruce Zhang wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya kupanua na kuboresha mtandao wa TTCL wa simu za mezani, mkononi pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao unagharimu zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani milioni 182.
  Afisa Mtendaji Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Kamugisha Kazaura (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa MS Huawei Technologies,Bruce Zhang wakisaini mikataba ya makubaliano ya kupanua na kuboresha mtandao wa TTCL wa simu za mezani, mkononi pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambao unagharimu zaidi ya kiasi cha dola za kimarekani milioni 182.
  Picha ya Pamoja.


  0 0  0 0

  Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukikatiza mapema jioni ya leo katikati ya msitu akielekea katika kijiji cha Mnarani -Makangale kuzungumza na wanachama wa chama hicho,micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na baadhi ya Vijana wapatao 105 waliokuwa chama cha CUF na kuhamia CCM,katika kijiji cha Mnarani Makangale,ambapo alikwenda kushiriki ujenzi wa tawi lao liitwalo Maskani tuheshimiane.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Vijana wapatao 105 waliokuwa chama cha CUF na kuhamia CCM.Wakisoma taarifa yao kwa Ndugu Kinana walieleza manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CUF,walieleza kuwa tangu wamehama chama hicho wamekuwa wakibugudhiwa na kufanyiwa fujo kiasi ambacho wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao za kimaendeleo ikiwemo na shughuli zao za uvuvi kusimama,hivyo wamemuomba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kulishughulikia jambo hilo ili waweze kuendelea na shughuli zao bila kubugudhiwa kwani wanataka kuishi kwa amani na utulivu.

  Akizungumza Ndugu Kinana alisema kuwa chama cha CUF hakitendi haki katika suala zima la demokrasia, ''kwani kila mtu ana uhuru wa kuhamia chama anachotaka na haitaji kubugudhiwa,hivyo Viongozi wa CUF,wanapaswa kulitambua hilo na kuwaacha wananchi waamue watakavyo ili mradi hawavunji sheria za nchi wala kumbugudhi mtu'' alisema Kinana.

  Kinana yupo katika ziara ya siku tano ya Kikazi kisiwani Pemba,akihimiza na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kukagua uhai wa chama kisiwani humo.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiri ujenzi wa  Maskani ya tawi la CCM-Tuheshimiane katika kijiji cha Mnarani Makangale,Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.
   Baadhi akina mama Wakulima wa Mpunga wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyekwenda Bonde la Mpunga Koowe kuangalia na kushiriki ujenzi wa tuta la Kuzuia maji chumvi katika bonde hilo.
   Pichani kati ni Afisa Mkuu wa Idara ya Umwagiliaji maji-Pemba Mbarouk Ali Mgau akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokwenda bonde la Mpunga Koowe-wingwi, kuangalia na kushiriki ujenzi wa tuta la Kuzuia maji chumvi katika bonde hilo.Afisa Mbarouk alieleza kuwa mradi huo umegharibu kiasi cha shilingi Milioni 170 zilizotolewa na TASAF.
   Ndugu Kinana akiwa na baadhi akina Mama ambao ni wakulima wa zao la Mpunga katika Bonde la Koowe,wakishiriki ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi katika bonde hilo
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimia na Mganga Mkuu wa Wilaya ya  Micheweni,Dkt.Rashid Daud mara baada ya kuwasili katika hospitali ya Wilaya ya  Micheweni,Kaskaini pemba mapema leo.
    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizingumza na baadhi ya Madaktari wa hospitali ya Wilaya ya Micheweni,mara baada ya kuwasili katika hospitali hiyo,Kaskazini Pemba mapema leo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la upasuaji katika hospitali ya wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba, wanaoshuhudia ni madaktari viongozi mbalimbali wa wilaya ya Micheweni na hospitali hiyo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa  Dkt.Rashid Daud Mkasha Mganga Mkuu wa Wilaya ya Micheweni wakati alipokuwa akikagua ukarabati wa wodi katika hospitali hiyo.
   Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Majenzi mjini Micheweni.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kweny uwanja wa Majenzi mjini Micheweni. 
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na baadhi ya viongozi wa chama cha CCM,alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Shaame Mata,Wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba mapema  leo.Pichani kulia ni Mbunge wa Viti maalum Pemba,Mh Maida Hamad Abdalllah na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Ndugu Vuai Ali Vuai.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid Karume (kulia) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi wengine na waislamu mbali mbali wakijumuika kwa pamoja kumswalia  aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Utalii Marehemu Issa Ahmed Othman katika Masjid Mahfoudh Mazizini, Marehemu alifariki juzi Nchini India na kuzikwa leo Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.unnamed2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati)Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid Karume, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi mbali mbali na Waislamu mbali mbali wakijumuika kwa pamoja kumuombea dua baada ya kumswalia  aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Utalii Marehemu Issa Ahmed Othman katika Msikiti Masjid Mahfoudh Mazizini,Marehemu amezikwa leo Kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja,[Picha na Ikulu.]unnamed4 
  Baadhi ya Vijana na wananchi waliobeba Jeneza la Marehemu Issa Ahmed Othman aliyekuwa Mashauri wa Rais Utalii Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiupeleka kuzikwa kijijini Kianga Wilaya ya magharibi Unguja leo jioni,marehemu alifariki juzi Nchini India ambako alikwenda kwa matibabu,[Picha na Ikulu.]unnamed5 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi (katikati) pamoja na Viongozi wengine na waislamu mbali mbali wakijumuika kwa pamoja katika mazishi ya aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Utalii Marehemu Issa Ahmed Othman katika Kijiji cha  Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja leo jioni,[Picha na Ikulu.]

  0 0


   Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Dorice Malulu (kulia), akikabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 45, kwa Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mji Mwema, Kigamboni, Bw. Richard Mwita, zilizotolewa na TBL kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Omari Kombe (kushoto), Bi. Upendo Mwabulambo (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Mganga wa Manispaa ya Temeke, Bw. Shaidi Simba (wa pili kulia).
  Mwakilishi Mkuu wa Mganga wa Manispaa ya Temeke, Bw. Shaidi Simba (kulia), akimkabidhi Mhandisi Amiri Msangi mfano wa hundi ya milioni 45 zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji kwenye Zahanati ya Mji Mwema. Katikati ni Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo, Dkt. Richard Mwita, Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Omari Kombe (kushoto) na Muuguzi, Bi. Upendo Mwabulambo.

older | 1 | .... | 448 | 449 | (Page 450) | 451 | 452 | .... | 1898 | newer