Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 449 | 450 | (Page 451) | 452 | 453 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahimu Lipumba akizozana na polisi muda mfupi kabla ya kukamatwa pamoja na wafuasi wengine 32 wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana. 
   Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahimu Lipumba akiwa chini ya ulinzi,eneo la Mtoni Mtongani jijini Dar jana,baada ya  Polisi kusitisha maandamano ya chama chake.

   ====== ======  ========
  Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata wananchama wa Chama cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti Taifa wa chama hicho,Profesa Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano ambayo si halali.

  Awali polisi ilizuia  maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho ya  kuadhimisha kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na mateso ya wananchi wa Zanzibar na Bara yalifanywa na vyombo vya usalama.

  Akizungumza leo Naibu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam,Simon Siro alisema wanachama waliokamatwa walikuwa 32 kati ya hao wawili ni wanawake na 30 ni wanaume ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano.

  “Wanachama 32 akiwemo Profesa Lipumba tunawashikilia katika kituo cha Polisi Kati kwa kufanya maandamano ambayo hayana kibali, wote wapo hapa tunaendelea kuwahoji,”alisema Siro.Siro alisema walipewa taarifa ya maandamano hayo na viongozi wa chama hicho hivyo jeshi hilo liliwaandikia barua ya kuzuia maandamano hayo kwa kuhofia fujo kutokea.

  Siro alisema sababu kubwa ya kuzuia maandamano hayo yasifanyike kwa kuwa mwaka 2001 yalifanyika maandamano batili yaliyosababisha baadhi ya polisi na wananchi kufa.“Jeshi la polisi likiruhusu hayo maandamano kuna uwezekano wa kutokea fujo na hayo maandamano ya mwaka 2001 yalikuwa si halali na kwenye maandamano hayo walikufa askari polisi,”alisema Siro.

  Alisem sababu nyingine ya kuzuia maandamano hayo ni kuwa hivi karibuni walikamatwa watu wanaojihusisha na mambo ya ugaidi hivyo kutokana na mazingira hayo jeshi la polisi linazuia mikusanyiko mikubwa kwa kuhofia kutokea mambo mabaya.

  0 0
 • 01/27/15--20:23: UNESCO YATAKA UBIA NA MWEDO
 • DSC_0005

  Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera (kushoto) akimkaribisha Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues kwenye ofisi za asasi hiyo kwa ajili ya mazungumzo jijini Arusha.

  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, limesema kwamba litaingia ubia na asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO) ili kuimarisha mradi wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan. Mradi huo mkubwa unaoendeshwa na Unesco kwa kushirikiana na Samsung umelenga kuinua maisha ya jamii ya wafugaji wa kimasai kwa kuwawezesha kielimu, kitamaduni na kiujasirimali.

  Kauli ya kutaka kuingia ubia imetolewa na Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues wakati alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwedo, Ndinini Kimesera katika ofisi za Mwedo mkoani Arusha. Alisema Unesco inataka kutumia uzoefu wa Mwedo katika ushirikishaji wananchi hasa katika uwezeshaji ujasirimali na elimu kufanikisha moja ya miradi mikubwa ya kisayansi katika kijiji cha Ololosokwan.
  DSC_0031
  Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera (katikati) alipotembelea ofisi hizo jijini Arusha. Kulia ni Mshauri wa kiufundi, usimamizi na tathmini wa MWEDO, Bw. Paul Wilson.

  Alisema Rodrigues katika mazungumzo na Mtendaji wa Mwedo kwamba Unesco imetambua haja ya kushirikisha wabia wengi katika maendeleo ili kufanikisha mradi huo mkubwa unaotaka kutoa huduma za afya, elimu na kuleta mabadiliko chanya katika jamii ya wafugaji wa kimasai ili kuweza kutumia raslimali zao walizonazo kupata maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

  Alisema vifaa kwa ajili ya mradi wa kubadili kijiji cha Ololosokwan kuwa kijiji cha digitali vimeshafika katika bandari ya Dar es salaam na wakati wowote kuanzia wiki zijazo vitasafirishwa kuelekea kijiji hicho tayari kwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa aina yake nchini ambao umelenga moja kwa moja wahusika.

  Alisema mradi huo unataka kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano kuwawezesha wananchi wa kijiji hicho kupata mabdiliko makubwa ya kimaisha.

  DSC_0019
  Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera.

  “Tumefika kwenu kuona ni namna gani tutasaidiana kuimarisha mradi huu hasa utoaji wa elimu na ujasirimali na utafutaji masoko” alisema. Alisema mradi huo umetaka kuhakikisha watoto wa wafugaji waume kwa wake wanapata elimu kwa kupitia teknolojia ya kisasa, huku ujasirimali kama utengenezaji wa shanga ukiwa katika soko na kuboreshwa zaidi.

  Alisema kwa watu wazima wanataka kuwapa uelewa ili kuboresha maisha yao kiujasiriamali, kiafya na kiuchumi. Alisema soko la bidhaa za wanakijiji wa Ololosokwan kama urembo wa shanga na mashuka zinazouzwa kwa watalii, zinaweza kupata soko zaidi kwa kuboreshwa.
  DSC_0051
  Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph (kulia) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera (hayupo pichani). Kulia ni Mshauri wa kiufundi, usimamizi na tathmini wa MWEDO, Bw. Paul Wilson.

  Alisema ameridhika na uhodari uliooneshwa na Mwedo katika ujasiriamali na hivyo wanataka kuimarisha uhusiano huo kwa kuhakikisha inawaleta watu wa kusaidia kuboresha elimu ya utengenezaji wa vifaa hivyo kwa soko la mataifa. Alisema kwamba pamoja na kuwataka Mwedo kutafuta hosteli kwa ajili ya wabunifu hao ili kuziongeza thamani bidhaa kwa soko la kimataifa. Naye Mtendaji wa Mwedo amesema kwamba wapo tayari kushirikiana na Unesco katika miradi ya wananchi wa jamii ya wafugaji.
  DSC_0057
  Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera akielezea shughuli mbalimbali zilizofanywa na asasi yake ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari MWEDO ikiwashirikisha wasichana wa kimasai wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa ni wanafunzi waliokosa nafasi ya kupata elimu kwa kuwachukua wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali kwenye jamii ya kifugaji, masuala ya ujasiriamali kwa wanawake wa kimasai pamoja na mambo mengine mengi yanayoendelea kufanywa na asasi hiyo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues (kushoto). Kulia ni Mshauri wa kiufundi, usimamizi na tathmini wa MWEDO, Bw. Paul Wilson.
  DSC_0044
  Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO aliambatana na Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta (kulia) pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kushoto). Katikati ni Afisa Mradi wa MWEDO, Martha Sengeruan.
  DSC_0079
  Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wakinamama wa kimasai kwenye duka la MWEDO mara baada ya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera (kulia). Katikati ni Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta.
  DSC_0094
  Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini, Zulmira Rodrigues (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Maendeleo ya wanawake wa Kimasai (MWEDO), Ndinini Kimesera mara baada ya mazungumzo.

  0 0

  New Picture (4) 
  Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya NHC kujenga nyumba za gharama nafuukatika Halmashauri ya Wilaya Serengeti-Mugumu. Eneo hili lina ekari 134 na miundombinu ya maji na umeme.
  New Picture (5) 
  Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mugumu Serengeti akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NHC ramani ya mpango Miji inayoonyesha eneo la NHC la kujenga nyumba za gharama nafuu.
  New Picture (6)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na kikundi cha vijana Wilayani Serengeti waliyosaidiwa mashine na NHC kwa ajili ya kujiajiri kupitia utengenezaji wa matofali yanayofungamana
  New Picture (7)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakikagua jingo la biashara lililojengwa na NHC eneo la Mukendo Musoma.

  New Picture (8)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelekezo ya matumizi bora ya dari la jengo la biashara la Mukendo lililojengwa na NHC katika Manispaa ya Musoma ili kuongeza mapato ya Shirika.
  New Picture (9)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Buhare Musoma. Jumla ya nyumba 50 zinatarajiwa kukamilika Julai 2015.
  New Picture (10)Vijana wakishiriki kujenga misingi ya nyumba za gharama nafuu eneo la Buhare Manispaa ya Musoma
  New Picture (11)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akijadili namna ya kuongeza ubora wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Amesisitiza kupunguza gharama ya ujenzi ili nyumba zinazojengwa ziwe nafuu.
  New Picture (12)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake walipotembelea Wilayani Tarime kujionea nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC mwaka 1968 na ambazo hadi hivi sasa zinasaidia familia mbalimbali. Nyumba hizi ni za vyumba viwili na zilipewa Halmashauri hiyo mwaka 1991.
  New Picture (13)Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Isibania nchini Kenya kujionea namna nchi hiyo ilivyopanga eneo lao la mpakani.
  New Picture (14)Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Sirari kuona eneo la kujenga nyumba ili kuboresha taswira ya mpaka wa nchi yetu. Ujumbuliongozwa na Maafisa Ardhi wa Wilaya ya Tarime.
  New Picture (15)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake pamoja naongozi wa Wilaya ya Butiama wakikagua eneo lililotengwa na Wilaya hiyo ili NHC ijenge nyumba za gharama nafuu. Bw. Mchechu amesisitiza kuwa NHC itajenga nyumba katika Wilaya hiyo ili kuenzi mchango wa Mwalimu Nyerere wa kulianzisha Shirika la Nyumba la kwanza nchini Tanzania mwaka mmoja tu baada ya uhuru.
  New Picture (17)Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiangalia mnara wa kumbukumbu ya mahali ambapo ilikuwepo nyumba aliyozaliwa Baba wa Taifa.
  New Picture (18)
  New Picture (19)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu aliwa amekaa sehemu maarufu aliyokuwa akikaa Mwalimu Nyerere wakati wa kucheza bao.
  New Picture (20)Hapa ndipo alipozikwa Hayati Mwalimu Nyerere. Ujumbe wa NHC ulizuru makumbusho ya Mwalimu kama sehemu ya kuenzi mchango wake wa kulianzisha Shirika la Nyumba mwaka mmoja tu baada ya uhuru wa Tanganyika.
  New Picture (22)Picha ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na kikundi cha vijana cha Samaritans Association cha Wilaya ya Bunda kilichofadhiliwa na NHC mashine za kutengeneza matofaliNew Picture (23)Bw. Yoramu Salum ambaye ni Afisa Mipango Miji katika Halmashauri ya Busega akionyesha ujumbe wa NHC eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.
  New Picture (24)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiwa katika picha ya pamoja na mojawapo ya kikundi cha vijana kilichofadhiliwa na NHC mashine za kufyatua tofali ili kukuza ajira Wilayani Magu
  New Picture (25)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipokea risala aliyosomewa na kikundi cha vijana Wilayani Magu. Anayekabidhi vijana hao fedha zilizotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Mwalimu Naomi Nnko.
  New Picture (26)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Magu Bibi Naomi Nnko wakikagua ramani inayoonyesha viwanja vya NHC vya kujenga nyumba za gharama nafuu.

  0 0  Mbunge wa Bumbuli na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Habari na Masoko ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye hivi karibuni pia ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa January Makamba(Pichani juu)  hivi karibuni ameainisha adhma yake ya kuinua kiwango cha michezo nchini.

  Azma hizo zimo katika  katika mazungumzo yake na Padre Privatus Karugendo ambayo yamechapishwa katika kitabu ambacho gazeti hili imekipata nakala yake ambapo ameainisha azma ya kujenga vitua vya michezo vya kanda vyenye hadhi ya kiolimpiki.

  Kwenye kitabu hicho, Makamba amejibu swali kwamba kitu gani kifanyike ili Watanzania waweze kujivunia wanamichezo wao. Makamba alisema, “Inafedhehesha sana kuona kwamba asilimia 79 ya Watanzania walikuwa hawajazaliwa mara ya mwisho tumeshiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

  Mwaka huo huo wa 1980 ndio mara ya kwanza na ya mwisho tuliweza kushinda medali za Olimpiki. Rafiki yangu Mzee Suleiman Nyambui na Mzee wetu Filbert Bayi ndio walitutoa kimasomaso kipindi kile. Ni muhimu kurekebisha hili.” 

  Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania imekuwa kama kichwa cha mwendawazimu katika medani ya kimataifa huku tasnia ya michezo ikiendelea kugubikwa na migogoro isiyokwisha. Kutokana na migogoro hii, Tanzania inaendelea kupoteza matumaini ya kung’aa katika medani za kimataifa.

  Katika mazungumzo hayo na Padre Karugendo, Makamba  alinukuliwa akisema, “Lazima tutambue kwamba maendeleo ya michezo yanatokana na vitu muhimu vitatu. Kwanza, ni lazima kuwepo na vipaji, bahati nzuri nchi yetu ina vipaji vya kutosha katika aina zote za michezo. Pili, ni miundombinu na mfumo wa kubaini na kuviendeleza vipaji hivyo, hii  bado ni changamoto . Tatu, ni utawala, uongozi, na uendeshaji wa tasnia ya michezo, hii pia ni changamoto. Hivi vitu vitatu ni lazima viwepo ili tuweze kupata mafanikio kwenye medani ya michezo.”

  Kama mgombea wa kwanza kutangaza nia yake ya kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Makamba anaungwa mkono na vijana wengi kutokana na kuendesha siasa zake kisasa, kibunifu na kuepuka malumbano ya jukwaani.

  Katika mazungumzo hayo Makamba alielezea fikra zake alizonazo hasa hasa kwenye kuendeleza vipaji vya Watanzania ambapo alisema, “Ni lazima tuanzishe vituo vikubwa vya michezo au ‘sports academies’ kwenye kila kanda ya nchi yetu vyenye hadhi ya Kiolimpiki.” 

  Makamba aliongeza  kwamba, “Kutakuwa na vituo sita vya aina hii katika nchi yetu ambavyo vitazungukwa na shule za msingi na sekondari za ‘boarding’. Vituo hivi vitakuwa na lengo la kukusanya wanafunzi wote kwenye kanda husika ambao wameonekana kuonyesha vipaji ambavyo vinapaswa kuendelezwa. Ukweli ni kwamba bila kuendeleza vipaji katika mazingira mazuri, basi tusahau kabisa kufanya vizuri kwenye michezo. Hili linaweza kufanywa kwa ushirikiano wa serikali na sekta binafsi”.

  Mheshimiwa January Makamba anakuwa mgombea wa kwanza wa Urais kuweka bayana mipango yake ya Tanzania Mpya katika maandishi. Anaendelea kufunguka kwamba katika tasnia ya michezo ni muhimu sana kuwekeza katika watoto. Zaidi ya hapo, kila timu ya ligi kuu ni lazima iwe na akademi na TFF iendeshe ligi kuu ya timu za watoto.

  “Tufikie wakati ambapo timu za taifa za miaka 10 ijayo ziwe zinaandaliwa kuanzia sasa, na serikali itenge bajeti kila mwaka kwa timu hizo  ili kuziwezesha kukaa kambini, kufanya mechi za majaribio na kuziwezesha kushiriki kikamilifu katika mashindano ya kimataifa. Mimi sio muumini wa hizi kamati za zimamoto kusaidia timu ishinde ghafla ghafla wakati siku zote watu hawafanyi maandalizi ya muda mrefu” alimalizia Makamba.

  Makamba pia aligusia kuhusu suala la ukata na ufinyu wa bajeti unaokabili tasnia za michezo. Siku zote tunaona timu za taifa za olimpiki au jumuiya ya madola kukosa fedha za kukaa kambini ambapo huchangia katika matokeo hafifu.

  “Huko nyuma, taasisi na mashirika ya umma yalikuwa na timu za michezo zilizokuwa zinafanya vizuri na kutoa michango kwenye maendeleo ya michezo. Kwa mfano, Pamba ya Mwanza, Sigara, Reli ya Morogoro, ushiriki huu ulichangamsha sana michezo na ni lazima turudishe utamaduni huu,” alimalizia Makamba. 

  0 0

  MBAZI ni kijana aliyezaliwa kwenye familia ya kimasikini mkoani kilimanjaro, anakwenda mkoani kigoma huko anapendana na NYAMIZI binti mkimbizi wa kinyarwanda. Anaamua Kumtorosha na kurudi nae kijijini kwao, lakini Mambo yanapozidi kuwa magumu anaamua kwenda Dar Es Salaam Kutafuta maisha akiamuacha Nyamizi akiwa na mtoto mdogo. 

  Akiwa Dar es Salaam anajikuta akiishia jela na kupoteza mawasiliano na familia yake kwa miaka mitatu anamaliza kifungo na kurudi kijijini na KITENDAWILI, mama yake na Mtoto wake walishafariki na mkewe anaishi na mwanaume mwingine na tayari nu majamizito.. Fuatilia hii kupitia mtandao .......

  Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania mtandaoni iitwayo KITENDAWILI au Kununua na iwe yako tembelea tovuti ya 


  Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

  0 0

  1
  Kiongozi wa Kundi la Bongo Artists Christian Kauzeni (Katikati) akizungumza na wadau wa Jukwaa la Sanaa (hawapo pichani) wakati Kundi lake lilipotoa elimu kupitia Sanaa kuhusu umuhimu wa wananchi kupiga kura mapema wiki hii. (Kulia ), Afisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristide Kwizela na Afisa Sanaa wa baraza hilo Ernest Biseko.
  2
  Moja ya wasanii wa Bongo Artists akiuliza swali kuhusu kutokupiga kura.
  3
  Msanii wa kundi la Bongo Artist aliyepuuza zoezi la kuwachagua viongozi akilia kwa uchungu baada ya kupata taarifa za ndugu yake kufariki Dunia katika hospitali aliyokuwa akitibiwa. Mama huyu alivuta hisia za watu wengi sana.
  4
  Kikundi cha Ngoma kutoka Bongo Artist kikitoa burudani kwenye Jukwaa la Sanaa.
   
  ====  ======  =======
  Wasanii nchini wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili watambue umuhimu wa kupiga kura na kuwaweka madarakani viongozi wanaowataka.Wito huo umetolewa mapema wiki hii na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza wakati akichangia mada kuhusu Umuhimu wa Jamii kupiga kura kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

  “Kama taifa tunazungukwa na matukio mengi yanayohitaji wananchi kupiga kura katika kuamua. Tuna tukio la kupiga kura ya maoni juu ya katiba inayopendekezwa lakini pia uchaguzi mkuu. Wasanii tuna wajibu wa kuwajengea hamasa wananchi kushiriki matukio haya muhimu” alisisitiza.

  Aliongeza kwamba wasanii hawana budi kutambua kwamba wana nafasi kubwa kuhakikisha wanawaelimisha wananchi kuhusu nafasi waliyonayo katika kuamua hatma yao lakini pia kuwa katikati katika kuibua masuala mbalimbali yaliyoko katika jamii ili kuwapa wananchi uchaguzi sahihi linapokuja suala la kupiga kura.

  “Wasanii hampaswi kuwa na upande mnapotoa elimu bali wajibu wenu ni kuibua na kuielimisha jamii kuhusu upigaji kura. Suala la nani apigiwe kura na wananchi linabaki kuwa mikononi mwa mwananchi mwenyewe ambaye ndiye mpiga kura” aliongeza.

  Awali, wakitoa burudani kwenye Jukwaa hilo la Sanaa, wasanii kutoka kundi la Bongo Artists Foundation linaloongozwa na msanii wa maigizo Christian Kauzeni walitoa elimu mbalimbali kuhusu umuhimu wa wananchi kupiga kura huku wasanii hao wakionesha kwa hisia kali madhara yatokanayo na wananchi kutokupiga kura.

  Kundi hilo lililovuta hisia za wadau takribani themanini waliohudhuria kwenye Jukwaa la Sanaa lilionesha madhara ya kutokupiga kura kuwa ni pamoja kupatikana kwa viongozi wabovu wasiyowajibika,kukosekana kwa huduma muhimu za jamii na changamoto nyingine nyingi ambazo zinakwamisha jitihada za wananchi kujikwamua kutoka kwenye ufukara.

  0 0

  Permanent Secretary, Ministry of Natural Resources and Tourism Dr. Adelhelm Meru (right) presenting a Tanzanian wood carving to Vice Mayor of Beverly Hills Julian Gold of as an expression of appreciation on behalf of H.E. Jakaya Kikwete, President of the United Republic of Tanzania during the private VIP reception held at the Peninsula Hotel in Beverly Hills, California, where the tourism promotion campaign was launched.
  Permanent Secretary, Ministry of Natural Resources and Tourism Dr. Adelhelm Meru delivering his speech during the launching of the tourism promotion campaign in the US West Coast at the Peninsula Hotel in Beverly Hills, California.
   Acting Managing Director of Tanzania Tourist Board Ms. Devota Mdachi giving her remarks during the launching of the tourism promotion campaign in the US West Coast at the Peninsula Hotel in Beverly Hills, California.

  0 0

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

   Rais Jakaya Kikwete anatarijiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya sheria nchini (Law Day) itakayofanyikaFebruari 4, 2015, katika viwanja vya mahakama vilivyopo mtaa wa Chimala jijini Dar es salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Othman Chande amesema kuwa maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaongozwa na maudhui yasemayo  “ Fursa ya kupata haki: wajibu wa Serikali, Mahakama na wadau”.

   Amesema kwa mara ya kwanza maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya Wiki ya   Shera yatakayofanyika  katika viwanja vya Mnazi Mmoja   kuanzia  tarehe  30 Januari  2015  hadi  tarehe  2 Februari  2015 .

  Mh.Chande ameeleza kuwa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini na maonesho ya Wiki ya Sheria yanaashiria mwanzo wa shughuli za mahakama kwa mwaka 2015  na kufafanua kuwa kipaumbele kitatolewa katika kupunguza mrundikano wa mashauri ya muda mrefu yaliyoko mahakamani na kushughulikia mashauri yenye mvuto mkubwa kijamii,miradi mikubwa, uhujumu uchumi, madawa ya kulevya, Biashara ndani na nje ya nchi na Rushwa.

  Kuhusu maonesho hayo amesema yanalenga  kutoa elimu kwa wadau wa sheria na huduma za kisheria kwa wananchi kuhusu Ufunguaji na uendeshaji wa mashauri mbalimbali hasa mirathi, Utatuzi wa migogoro kwa njia ya suluhu, kueleza mfumo mpya wa ulipaji wa tozo za kimahakama kwa njia ya benki, Kutoa msaada wa kisheria, kutolewa vyeti vya mawakili, kupokea maoni na malalamiko kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi.

  Ameeleza kuwa wadau wakuu  watakaoshiriki katika maonesho hayo ni Mahakama, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Chuo cha Uongozi wa Mahakama- Lushoto, Taasisi ya Mafunzo ya Uansheria kwa vitendo Tanzania na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

  Wadau wengine ni Taasisi zinazotoa msaada wa kisheria, TAKUKURU, Jeshi la Polisi, Magereza, Chama cha Mawakili Tanganyika na Tume ya kurekebisha sheria.

  Amesema pamoja na maonesho hayo kutakuwa na matembezi maalum ya kuadhimisha Wiki ya Sheria tarehe 1 Februari 2015 yatakayoongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hassan Mwinyi kuanzia Mahakama Kisutu kupitia barabara za Serena-Ohio, Gymkana –Obama Road, Mahakama ya Biashara, Barabara ya Kivukoni, Sokoine , Railway, Nkurumah, Lumumba na Mkunguni hadi Mnazi Mmoja.

  0 0

  Aliyekuwa waziri wa uchukuzi ambaye sasa ni aziri wa ushirikiano wa africa mashariki mh HARSON MWAKYEMBE akizungumza na wadau mbalimbali walojitikeza katika afla hiyo ya kutafuta fedha za kuendesha mkutano huo utakao fanyika mapema mwezi wa tatu.
   Taasisi ya kimataifa ya uhudumiaji wa bidhaa na uchukuzi wa bidhaa CILT yani THE CHARTERD INSTITUTE OF LOGISTIC AND TRANSPORT Tawi la Tanzania imeandaa mkutano mkubwa nchini ambao utafanyika katika mkoa wa arusha tarehe 3 na 4 mwezi wa tatu mkutano wenye lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maswala ya usafirishaji na uchukuzi kujadili changamoto mbalimbli katika secta hiyo.
  Mwenyekiti wa CILT nchini Tanzania GEORGE MAKUKE akizungumza kuhusu mkutano huo na taasisi hiyo inavyofanya kazi.  Mkutano huo ambao utafanyika katika hoteli ya mount meru jijini arusha una mipango pia ya kuwakutanisha wanataaluma wa maswala ya uchukuzi na usafirishaji wa bidhaa ili kubadilishana uzoefu katika taluma hiyo.

  Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupata chai yenye lengo la kuchangisha fedha ambazo zitasaidia katika kuendesha mutano huo aliyekuwa waziri wa uchukuzi ambaye sasa ni waziri wa ushirikian wa Africa mashariki MH HARSON MWAKYEMBE amesema kuwa Tanzania kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa kama huu ni fursa ya kipekee ambayo nchi inatakiwa kujivunia na kuitumia kujitangaza kimataifa.
   Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ndugu ZAKARIA HANSPOP akizngumza. Amesema kuwa mkutano huo utawasaidia hasa vijana ambao wanasoma maswala haya kukutana na wazoefu katika fani hiyo na kubadilishana uzoefu jambo ambalo litawajengea uzoefu katika kazi zao pindi watakapoingia katika fani.
  Aidha mwenyekiti wa CILT nchini Tanzania GEORGE MAKUKE anesema kuwa kwa sasa katika secta ya usafirishaj wa bidha nchini kumekuwa na watu ambao amewaita makanjanja ambao wamekuwa hawana weledi katika kazi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi jambo ambalo amesema kuwa linafaa kupigwa vita mara moja.
  Katika hatua nyingine mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo ndugu ZAKARIA HANSPOP akizngumza katika hafla hiyo amewataka watanzania hususani wadau wa secta hiyo kujitoa katika kuufadhili mkutano huo kwani una manufaa makubwa katika ukuaji wa secta ya usafirishaji na uchukuzi nchini Tanzania
  Picha tatu za juu zikionyesha washiriki mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo


  0 0

  Na Abdulla Ali Maelezo-Zanzibar .
                                              
  Wananchi wametakiwa kujiepusha na vitendo vya kihalifu ili kuepusha uvunjifu wa amani nchini. 

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe Mhe. Salim Abdalla Hamad.

  Amesema endapo mtu atatuhumiwa kutenda vitendo hivyo vya kihalifu sheria zitatumika bila ya kumuonea au kumkandamiza mtu yeyote ili kuhakikisha amani na utulivu inabakia na kudumishwa nchini.

  Amefafanua kuwa ni utaratibu wa kisheria katika nchi za Jumuiya ya Madola kwamba nchi ina mamlaka ya kumfikisha muhalifu mahakamani na kumshitaki iwapo tukio husika la kihalifu limetokea katika nchi hiyo, hivyo endapo tukio la uhalifu limetokea Tanzania Bara na endapo limetokea Zanzibar, mahakama za Zanzibar pia zinaweza kuwashitaki watuhumiwa hao.
  Ametanabahisha kuwa Katiba ya Zanzibar ya 1984, kifungu cha 101 kinaweka masharti ya kikatiba ya utaratibu wa utekelezaji wa hati za mahakama ndani ya Zanzibar na Tanzania Bara kwa ujumla na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 124 imeweka masharti kama yaliyomo kwenye kifungu cha 101 cha Katiba ya Zanzibar.


  Waziri Aboud amesema kwa mujibu wa masharti ya vifungu vya katiba vilivyotajwa ni utaratibu halali wa kisheria wa mtuhumiwa kukamatwa upande mmoja wa Muungano na kupelekwa upande mwengine wa Muungano endapo uhalifu umetokea na kutendwa katika eneo husika.

  Aidha Waziri Aboud amefafanua kuwa misingi ya katiba zote mbili kuna utaratibu pia wa kisheria ambapo Mzanzibari au Mtanzania yeyote ambae atatuhumiwa kutenda kosa lolote la uhalifu nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kukamatwa na kupelekwa nchi ambayo atatuhumiwa kutenda kosa na kushitakiwa.

  Amesema Sheria hizo ni Sheria ya kubadilishana wahalifu Sura ya 368 (Extradition Act Cap. 368) na Sheria ya kusaidiana katika mambo ya jinai Sura ya 254 (The Mutual Assistance in Criminal Matters Act Cap. 254) sheria hizo zote zinaweka masharti na utaratibu wa kubadilishana wahalifu.


  0 0

  Na Abdulla Ali Maelezo-Zanzibar  .                                         
  Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili Zanzibar Mhe. Mtumwa Kheir Mbarak amewataka wananchi kutokata misitu ya asili na kuchimba mchanga ovyo kwani ndizo sababu zinazopelekea mabadiliko ya Tabianchi.

  Hayo ameyaeleza katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Wawi Mhe. Saleh Nassor Juma.

  Mhe. Mtumwa amesema ukataji wa misitu ya asili pamoja na uchimbaji mchanga ovyo husababisha kukosekana kwa mvua za misimu na kuathiri maisha ya wakulima na wananchi kwa ujumla.

  Amesema ikiwa wananchi wataendelea kukata misitu ya asili hususan mikoko ambayo huzuia upepo wa Bahari na kupandisha kina cha maji, kutapelekea Visiwa vya Zanzibar kukatika vipandevipande na maji kujaa hadi katika makaazi ya watu kama ilivyo hivi sasa kwa baadhi ya vijiji hapa zanzibar.  

  “Na athari za ziada zitafuata baadae ikiwa wataendelea kukata hasa mikoko ambayo inazuia upepo wa Bahari na kupandisha kina cha maji, matokeo yake visiwa vitakatika vipande vipande na maji yatapanda mpaka viamboni (katika makaazi ya watu) na mfano hai hayo sasa yanatokea katika vijiji vya Jozani, Mziwanda, Koowe na kwengine kwingi”, alieleza Naibu Waziri Mtumwa. 

  Aidha ametanabahisha kuwa Serikali imechukua juhudi mbalimbali katika kuhakikisha kwamba athari za mabadiliko hayo zinapungua, miongoni mwa juhudi hizo ni kuanzishwa vikundi mbalimbali vya jamii husika kwa matakwa yao wenyewe kutunza misitu ya asili iliopo katika maeneo yao wanayoishi Unguja na Pemba, Udhibiti wa msumeno wa moto kutotumika mpaka kwa ruhusa na kibali maalumu.


  Sambamba na hayo Mhe. Mtumwa amesema kuwa Serikali imeanzisha miradi mbalimbali ili kuondokana na tatizo hilo ikiwemo mradi wa TASAF unaojishughulisha na mpango wa kujenga miundombinu ya umwagiliaji maji ambao umesaidia umwagiliaji kwa kilimo cha Mpunga, Mboga na Matunda, pia wakulima kusomeshwa njia bora za ukulima na kuwapa fedha za kuanzishia mashamba kupitia mradi wa PADEP, ASSP na ASDPL.

  Akiongezea Mhe. Mtumwa amesema serikali imeanzisha sheria maalumu za kuzuia ukataji wa miti ovyo ikiwemo sheria ya COFMA ambayo imetungwa ili kudhibiti wanaoharibu misitu kiholela.

  Mhe. Mtumwa amewataka viongozi na wananchi kwa ujumla kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupiga vita ukataji wa misitu ya asili na uchimbaji mchanga ovyo ili kuondokana na janga la Tabianchi na ukosefu wa mvua za misimu na kutilia mkazo kilimo cha kisasa pamoja na upandaji wa miti.

  0 0

   
  Na Abdulla Ali Maelezo-Zanzibar .
                                           
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Abdilahi Jihadi Hassan amesema Serikali ina mipango madhubuti ya kuongeza upatikanaji wa samaki ili kukidhi mahitaji ya hoteli za utalii na walaji kwa ujumla.

  Hayo ameyaeleza katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe. Ali Salum Haji.

  Amesema mikakati hiyo ni kuwawezesha wavuvi kuvua katika kina kirefu cha maji ambapo hivi sasa Wizara yake imeshawapatia mafunzo ya uvuvi wa bahari kuu Vijana 25 katika chuo cha uvuvi Mbegani na hatua ya kupeleka wengine zinaendelea kulingana na hali ya fedha itakavyoruhusu.

  Vilevile amesema mkakati mwengine ni kuwezesha uzalishaji wa samaki kwa njia ya Ufugaji na mazao mengine ya Baharini ambapo mikakati hiyo itaongeza upatikanaji wa samaki kwa wingi na hivyo kupunguza uwezekano wa kuingizwa samaki wasio na uhakika  na usalama kwa walaji nchini.
  Waziri Abdilahi amefafanua kwamba itakapotokea uingizaji wa samaki nchini, watachunguzwa na kuhakikishwa ubora wao na mamlaka zinazohusika ikiwemo Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi kabla ya kuruhusiwa kuingizwa nchini.

  Wakati huohuo Waziri Abdilahi ametanabahisha wakati akijibu swali la muakilishi wa jimbo la Wawi Mhe. Saleh Nassor Juma kuwa uzalishaji wa samaki bado ni mdogo na unakidhi soko la ndani pekee kwa sasa.
  Hivyo Wizara yake imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuwashawishi Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika Sekta ya Uvuvi ili kuongeza uzalishaji wa samaki ikiwa ni pamoja na kujenga Viwanda vya kusindikia samaki.

  Amesema hayo yatatekelezwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uwekezaji na Taasisi nyengine na hivi sasa kuna wawekezaji kadhaa ambao wameonyesha nia ya kuwekeza katika sekta ya Uvuvi pamoja na kujenga viwanda hivyo.

  Mhe. Abdilahi amesema mazingira ya uwezekezaji yameshawekwa na serikali, hivyo amewataka wawekezaji kujitokeza ili kutimiza lengo hilo na kusaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia shughuli za uvuvi.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa Biashara ya kilimo kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa FMD yenye makamo yake Nchini Kenya Bw. Fergus Robley wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara ya kilimo kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa SUGECO CHAIR Dkt. Anna Temu alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara ya kilimo kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa afisa muendeshaji Mkuu wa kampuni ya FARMEQUIP Rattan Singh alipotembelea maonesho ya Biashara ya kilimo kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa afisa muendeshaji Mkuu wa kampuni ya FARMEQUIP Rattan Singh alipotembelea maonesho ya Biashara ya kilimo kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa makampuni ya Biashara ya nyenzo za kilimo, wakati wa  mkutano wa Biashara ya kilimo kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2015.                 (Picha na OMR)

  0 0

  1
  Spika wa Bunge Anne Makinda akizungumza Bungeni Mjini Dodoma Januari 28, 2015.
  2
  Spika wa Bunge, Anne Makinda akitoka Bungeni baada ya kulazimika kuahirisha kikao kabla ya muda wake.
  3
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah (kulia) na Mary Mwanjelwa kwenye jengo la utawala la Bunge mjini Dodoma.
  4
  Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge  (kulia) na Mbunge wa Mji  Mkongwe Ibrahim Sanya kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
  5
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Rose Kamili kwenye viwanja vya Bunge mjini  Dodoma Januari 28, 2015.(Picha zote na Ofisiya Waziri Mkuu)

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na MNEC wa CCM Taifa,Bwa.Daudi Ismaili pamoja na baadhi ya wanachama wa CCM,mara baada ya kuwasili katika mkutano wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Wilayani Chake  Chake,Mkoa wa Kusini Pembaa mapema leo.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Wilayani Chake Chake,Mkoa wa Kusini Pemba mapema leo,ambapo pia Ndugu Kinana alipokea taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
   Pichani Kulia ni Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba,Mh.Mwanajuma Maggid Abdallah akizungumza jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana (pichani shoto),wakati Ndugu Kinana alipokwenda kushiriki ujenzi wa Taifa wa tawi la CCM Mchangani katika jimbo la Wawi,wilaya ya Chake Chake-Mkoa wa Kusini Pemba.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani shoto akishiriki ujenzi wa tawi la CCM Mchangani katika jimbo la Wawi,wilaya ya Chake Chake-Mkoa wa Kusini Pemba akiwa sambamba na Wananchi na wanachama wa CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mbele ya Wananchi wa Uwandani katika jimbo la Wawi,kabla ya kukagua utekelezaji  wa Ilani chama cha Mapinduzi na kushiriki Ujenzi wa Madarasa ya Skuli ya Uwandani
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana sambamba na Wananchi wakishiriki ujenzi wa Madarasa ya Skuli ya Uwandani,katika jimbo la Wawi,wilaya ya Chake Chake,Mkoa Kusini Pemba.Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa mbele ya katibu Mkuu Ndugu Kinana,imeeleza kuwa mradi wa ujenzi wa jengo hilo litakalokuwa na jumla ya vyumba sita,litagharimu kiasi cha shilingi milioni 18 zitakazomilisha mradi huo.
   Katibu Mkuu wa CCM na ujumbe wake pamoja na wananchi wakikatiza kwenye shamba la miti linalosimamiwa na Kikundi cha Utunzaji Mazingira kiitwacho Hatugombani Cooperative,kilichopo Kilindi,Wilaya ya Chake Chake,mkoa wa Kusini Pemba.Kikundi hicho kina jumla ya Wanachama wapatao 49,ambapo shughuli kubwa ya kikudi hicho ni utunzaji wa mazingira kwa upandaji miti ya Mivinje,Mikaratusi,Mikungu na Mitondoo.Mradi huo wa kuhifadhi Mazingira una eneo la eka 20,ambapo mpaka sasa mradi huo una thamani ya shilingi Milioni 40 na zaidi
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akishiriki kupanda mti katika shamba la miti linalosimamiwa na Kikundi cha Utunzaji Mazingira kiitwacho Hatugombani Cooperative,kilichopo Kilindi,Wilaya ya Chake Chake,mkoa wa Kusini Pemba.Kikundi hicho kina jumla ya Wanachama wapatao 49,ambapo shughuli kubwa ya kikudi hicho ni utunzaji wa mazingira kwa upandaji miti ya Mivinje,Mikaratusi,Mikungu na Mitondoo.Mradi huo wa kuhifadhi Mazingira una eneo la eka 20,ambapo mpaka sasa mradi huo una thamani ya shilingi Milioni 40 na zaidi
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akielekea katika kijiji cha Chanjamjawiri,jimbo la Chake Chake akiwa ameongoza na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya na Mkoa CCM Kusini Pemba kushiriki upandaji wa miche ya Mikarafu,katika ushirika wa uitwao Hatukosani wenye jumla ya Watu 25.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kuotesha miche ya Mikarafuu katika bustani ya kikunndi cha Hatukosani,wakati alipotembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na kikundi hicho chenye wanachama wapatao 25 kilichopo Chanjamjawiri-Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipewa taarifa ya kikundi cha Ushirika cha Jitihada Mbele cha Ufugaji  wa Samaki chenye jumla ya wanachama 10.Kikundi hicho kilianzishwa kwa lengo la Ufugaji wa samaki ili waweze kujikwamua kiuchumi na pia kusimamia sera ya chama cha CCM,ikiwemo kujikusanya kwa pamoja ili kuanzisha vikundi vya ushirika kwa ajili ya kujiajiri wenyewe.Kwa Mujibu wa Msomaji wa taarifa alieleza kuwa mradi huo wa samaki una jumla ya thamani ya shilingi milioni 10.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishirik kuchimba moja ya mabwawa ya wanakikundi hao wa Jitihada Mbele akiwa sambamba na baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM. 
   Mbunge wa Viti Maalum Pemba,Mh.Faida Bakari akifafanua mambo mbalimbali yaliyomo ndani ya Katiba mpya inayopendekezwa,inayotarajiwa kupigiwa kura mnamo Aprili 30,Mbunge huyo ameawata Wananchi wa Pemba kuipigia kura ya ndio katiba hiyo ili ipite,kwani ina mambo mengi mazuri kwa Zanzibar
   Baadhi ya Wanachi wakifuatilia kwa makini mkutano wa hadhara uliofanyika mapema jioni ya leo Pujini Kunvini Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.
  Mbunge wa Viti Maalum,Mh.Asha Abdul Haji akihutubia katika mkutano wa hadhara  uliofanyika mapema jioni ya leo Pujini Kunvini Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba,ambapo pia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana aliwahutubia wananchi wa eneo hilo.
  Baadhi ya Wanachama wa CCM wakishangilia jambo katika mkutanno wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Pujin Kumvini-Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba. 
   Mfuasi wa Chama cha CUF Ghalib Bedui Khamisakikabidhi kadi yake kwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na kukabidhiwa kadi mpya ya uanachama wa CCM.
   Mfuasi wa Chama cha CUF Said Abdallah Ibrahim akionesha kadi yake ya zamani kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kabla ya kukabidhi na kupewa kadi mpya ya uanachama wa CCM,mbele ya Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Pujini Kunvini Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa Pujini Chake Chake,mkoa wa Kusini Unguja.

  0 0

  unnamed3
  Makamu wa Pili w Rais wa Zanzibar Balozi Seifa Ali Iddi akifungua mkutano wa tisa wa tathmini ya sekta ya Afya Zanzibar uliofanyika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanizibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  unnamed4
  Washiriki wa maendeleo katika sekta ya Afya na baadhi ya waalikwa wa mkutano wa tisa wa tathmini ya sekta hiyo wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo katika Hoteli ya Ocean Views Kilimani.
  unnamed5
  Meza kuu katika mkutano ikiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakimsikiliza Dkt Mkasha alipokuwa akiwasilisha mada ya MKUZA namba mbili katika mkutano wa tathmini ya sekta ya Afya Zanzibar.

  unnamed
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Muhammed Saleh Jidawi akizungumza katika mkutano wa tisa wa tathmini ya sekta ya Afya kwa mwaka uliopita huko Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  unnamed2
  Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufungua mkutano wa tisa wa tathmini ya Afya Zanzibar.

  unnamed6
  Picha ya pamoja ya mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa  mkutano wa tathmini ya sekta ya Afya Zanzibar pamoja na baadhi ya washiriki wa maendeleo na wageni waalikwa. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  ………………………………………………………………………….
  NA RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR   
             
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa  ya maendeleo katika sekta ya Afya na ipo karibu sana kufikia malengo ya Mellenia.
  Amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana ushirikiano wa pamoja wa wafanyakazi wa sekta hiyo na kuimarisha miundo mbinu ya afya ikiwemo ujenzi wa barabara, mawasiliano, umeme na usambazaji wa maji safi.

  Balozi Seif ameeleza hayo alipokuwa  akifungua  mkutano wa tisa wa mwaka wa tathmini ya sekta ya Afya Zanzibar kwa mwaka uliomalizika katika Hoteli ya Ocean View Kilimani. Amesema Zanzibar hivi sasa imepiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga ambavyo hapo zamani ilikuwa ni tishio kubwa kwa taifa.

  Balozi Seif amesema Serikali imejitahidi katika kuimarisha  Hospitali zake na  kuwasogezea wananchi huduma za afya karibu na makaazi yao kwa kujenga vituo vya afya katika vijiji mbali mbali Unguja na Pemba na kuimarisha upatikana wa dawa muhimu.

  Ameelezea  mafanikio mengine ni kupunguza kwa kiwango kikubwa maradhi ya malaria na kufikia chini ya asilimia moja na janga la  HIV/AIDS limebaki katika makundi maalum ya watu wakiwemo wafanya biashara ya ukahaba, wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na wanaotumia madawa ya kulevya na kiwango chake kipo chini ya asilimia moja.

  Balozi Seif amewashauri wanasiasa na wananchi wanaopenda kuunga mkono juhudi za kuimarisha miundo mbinu ya Afya nchini kujitokeza kujenga nyumba za wafanyakazi karibu na vituo hivyo na kuchangia vifaa na madawa.

  Ameeleza kuwa tatizo la wafanyakazi wa sekta ya afya limepungua kwa kiasi kikubwa hivi sasa na wengi wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya kitaalamu ndani na nje ya nchi. Amekumbusha kuwa miaka minne iliyopita Zanzibar ilikuwa madaktari mabingwa wazawa 11 tu na hivi sasa wapo madaktari 69 ambao 16 kati yao wamesomea fani maalumu.

  Makamu wa pili wa Rais amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajivunia vijana wake 38 waliohitimu mafunzo ya udaktari hivi karibuni kwa ushirikiano wa mkubwa wa Wizara ya Afya na Chuo Kikuu cha Matanzascha cha Cuba. Amezishukuru nchi na washirika wa wakubwa wa maendeleo katika sekta ya Afya ikiwemo Marekani na Mashirika ya WHO na DANIDA kwa michango yao ya hali na mali iliyowezesha sekta ya afya kupiga hatua kubwa.

  Akizungumza katika mkutano huo Mwakilishi wa WHO Zanzibar kwa niaba ya Mwakilishi Mkaazi wa Shirika hilo Tanziania Dkt. Andymichael Ghirmany ameipongeza Zanzibar kwa mafanikio makubwa iliyopata katika sekta ya Afya.

  Amesema ni nchi chache Dunianiani zilizoweza kupiga hatua kubwa katika sekta hiyo na inatoa matumaini  kwa washirika wa maendeleo kuendelea  kusaidia sekta hiyo.

  0 0

  unnamed 
  Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Bibi Nuru Mwendapole kushoto akizungumza na Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa jana wakati wa ziara ya kutembelea Wilaya hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa vijana wa Wilaya ya Busokelo Mkoa wa Mbeya.
  unnamed2Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa akiwasisitizia vijana wa Wilaya ya Busokelo umuhimu wa kuijua Sera ya Maendeleo ya Vijana jana wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Mkoa wa Mbeya.
  unnamed4 
  Maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa makini kijana kutoka kikundi cha Vijana Maendeleo wanaofuga samaki wakati wa ziara ya kutembelea vikundi vya vijana wa Wilaya ya Busokelo Mkoa wa Mbeya.

  unnamed5 
  Samaki wakionekana kwa mbali katika bwawa la samaki linalomilikiwa na kikundi cha Vijana cha Maendeleo kilichopo Wilaya ya Busokelo Mkoa wa Mbeya.
  unnamed6 
  Kutoka kulia ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa, Afisa Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George Mbijima, Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga na Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele wakiangalia nguruwe wa kikundi cha Search Group Wilaya ya Busokelo walipowatembelea kuangalia shughuli zinazofanywa na kikundi hicho.

  (Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo. Busokelo, Mbeya)

  0 0

  unnamed 
  Mtaalamu wa Mambo ya Mawasiliano toka Uingereza Bw. Simon McDowall akiwasilisha mada kuhusu uandishi wa hotuba na namna bora ya uwasilisha wa mada wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano leo Mkoani Mtwara.Picha na Hassan Silayo
  unnamed1 
  Baadhi ya Maafisa Mawasiliano wakishiriki katika mafunzo kwa kujibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Bw. Simon McDowall wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano leo Mkoani Mtwara.

  unnamed2 
  Baadhi ya Maafisa Mawasiliano wakishiriki katika mafunzo kwa kujibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Bw. Simon McDowall wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano leo Mkoani Mtwara
  Mtaalamu wa Mambo ya Mawasiliano toka Uingereza Bw. Simon McDowall akimueleza jambo Afisa Mawasiliano toka Tume ya vyuo vikuu Bi.Thea Mtau wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano leo Mkoani Mtwara unnamed4 
  Maafisa Mawasiliano wakisikiliza Hotuba iliyowahi kutolewa na Martin Luther King ikiwa ni sehemu ya Mafunzo kutoka kwa Mtaalamu wa Mambo ya Mawasiliano toka Uingereza Bw. Simon McDowall wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano leo Mkoani Mtwara
  unnamed5 
  Maafisa Mawasiliano wakisikiliza Hotuba iliyowahi kutolewa na Martin Luther King ikiwa ni sehemu ya Mafunzo kutoka kwa Mtaalamu wa Mambo ya Mawasiliano toka Uingereza Bw. Simon McDowall wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano leo Mkoani Mtwara

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika hatua mbalimbali za mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika hatua mbalimbali za mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani,  Rais wa Mali Mhe Ibrahim Boubacar Keïta, Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Erna Solbergna Mwenkekiti Mwenza wa Bill&Melinda Gates Foundation, Bw. Bill Gates, wakiwa jijini Berlin, Ujerumani, wakati wa chakula cha mchana cha mazungumzo baada ya kumalizika kwa mkubwa wa kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.


  0 0

  Wadau wa Elimu, Abdulaziz Jaar kulia, akizungumza jambo katika matembezi ya Shule ya Kiislamu ya Twayyibat Islamic Seminary ya Temeke jijini Dar es Salaam. Katikati ni mdau kutoka Yukubu Chamber&Associate.
   
  MKUU wa wilaya Temeke, DC Sophia Mjema, ameipongeza shule ya Sekondari ya Kiislamu inayojulikana kama Twayyaibat Islamic Seminary Secondary School kwa kufanya ada nafuu inayoweza kuwafanya wazazi na walezi wamudu gharama za kusomesha watoto kwenye shule binafsi.
  mwanafunzi kutoka Twayyibat Islamic Seminari akisoma Quraan katika shule hiyo walipotembelewa na Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, hayupo pichani.

  DC Mjema aliyasema hayo alipofanya ziara katika shule hiyo na kukuta uongozi wa Twayyaibat, ukitoa ada ya Sh 200,000 tu kwa mwaka, jambo ambalo ni agharabu mno hususan kwa shule za kulipia na zinazomilikiwa na taasisi za kidini.

  Akizungumza kwa mshangao mkubwa mbele ya wadau wa elimu, DC Mjema alisema ameshangazwa na shule hiyo kufanya ada nafuu, hivyo ni jukumu la wazazi na walezi kujitokeza kuwasomesha watoto wao kwa nguvu zote.
  Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia akimkabidhi cheti Mr Yakubu kwa kutambua mchango wake kwa maendeleo ya shule ya Twayyibat Islamic Seminary, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam jana.
  Meneja wa Skywadrs Construction, Saeed Pirbaksh Mulla, akipokea cheti cha kutambua mchango wa kampuni yao kwenye shule hiyo. Cheti hicho anakabidhiwa na Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia.

  Alisema pamoja na ada hiyo kuwa nafuu, ni jukumu la serikali hususan Halmashauri ya Wilaya Temeke kupanga mbinu bora zinazoweza kuisaidia shule hiyo kwa hali na mali ili waweze kufanya kazi ya kutoa elimu kwa kiwango cha juu.

  “Hii naweza kuiita shule ya sekondari ya mshangao hasa baada ya kuona unafuu wa ada yake, nikiamini kuwa Dunia ya leo kukuta unafuu wa namna hii unaonyesha namna gani kuna wadau wana mtazamo wenye maendeleo.

  “Naomba wadau, walezi, wazazi na serikali kupanga namna wanavyoweza kuisaidia Twayyaibat ili waweze kuhakikisha kuwa vijana wetu wanasoma kwa bidii kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kwasababu Dunia ya leo elimu ni lazima,” alisema DC Mjema.

  Naye Mkuu wa Shule hiyo, Juma Omari, alisema shule yao imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kutoa ufaulu wa kufurahisha, huku akiihakikishia serikali kuwa watajitahidi kuwapa mwanga wa kielimu watoto wanaosoma kwenye shule hiyo.

  “Tangu shule hii ilipoanzishwa mwaka 1996 imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na matokeo yake ya Taifa, hili linatufanya tuongeze bidii katika kufundisha wanafunzi wetu tukiamini ndio mpango sahihi,” alisema.

  Katika hatua nyingine, DC Mjema alitumia muda huo kukabidhi vyeti vya kuthamini mchango wa wadau wanaoisaidia shule hiyo, huku waliopewa vyeti hivyo ni Skywards Construction, Yakubu Chamber&Associate, Mheshimiwa Adam Malima, Sheimar Kweigir, Zainabu Vulu, Alosco.
  Kazumari Nambeya, akiiwakilisha Home Shooping Centre katika kupokea cheti cha kutambua mchango wa shule hiyo, mbele ya Mkuu wa wilaya Temeke, Sofia Mjema, jana, jijini Dar es Salaam.

  Alisema pamoja na ada hiyo kuwa nafuu, ni jukumu la serikali hususan Halmashauri ya Wilaya Temeke kupanga mbinu bora zinazoweza kuisaidia shule hiyo kwa hali na mali ili waweze kufanya kazi ya kutoa elimu kwa kiwango cha juu.

  “Hii naweza kuiita shule ya sekondari ya mshangao hasa baada ya kuona unafuu wa ada yake, nikiamini kuwa Dunia ya leo kukuta unafuu wa namna hii unaonyesha namna gani kuna wadau wana mtazamo wenye maendeleo.

  “Naomba wadau, walezi, wazazi na serikali kupanga namna wanavyoweza kuisaidia Twayyaibat ili waweze kuhakikisha kuwa vijana wetu wanasoma kwa bidii kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kwasababu Dunia ya leo elimu ni lazima,” alisema DC Mjema.

  Naye Mkuu wa Shule hiyo, Juma Omari, alisema shule yao imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kutoa ufaulu wa kufurahisha, huku akiihakikishia serikali kuwa watajitahidi kuwapa mwanga wa kielimu watoto wanaosoma kwenye shule hiyo.

  “Tangu shule hii ilipoanzishwa mwaka 1996 imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na matokeo yake ya Taifa, hili linatufanya tuongeze bidii katika kufundisha wanafunzi wetu tukiamini ndio mpango sahihi,” alisema.

  Katika hatua nyingine, DC Mjema alitumia muda huo kukabidhi vyeti vya kuthamini mchango wa wadau wanaoisaidia shule hiyo, huku waliopewa vyeti hivyo ni Skywards Construction, Yakubu Chamber&Associate, Mheshimiwa Adam Malima, Sheimar Kweigir, Zainabu Vulu, Alosco.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, akizungumza na wanafunzi na wadau wa shule ya Twayyibat, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa elimu na wasaidizi wa shule ya Twayyibat Islamic, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 449 | 450 | (Page 451) | 452 | 453 | .... | 1897 | newer