Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEINI AZINDUA SHEREHE ZA MIAKA 38 YA KUZALIWA CCM

$
0
0
 Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzinzibar pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi na WanaCCM wa Mikoa ya Pemba katika uzinduzi wa kuadhimisha sherehe za kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi na WanaCCM wa Mikoa ya Pemba katika uzinduzi wa kuadhimisha sherehe za kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo. 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi na WanaCCM wa Mikoa ya Pemba katika uzinduzi wa kuadhimisha sherehe za kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Katibu Mkuu CCM Taifa Abdulrahman Omar Kinana na Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Bakari Mshindo (wa tatu kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi (kushoto) wakipiga makofi ulipopigiwa wimbo wa Chama kumpokea Dk.Shein alipofika kuzindua Sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa CCM katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba.
 
 Baadhi ya Wananchi na wafuasi wa chama hicho akifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanja hapo,
 Baadhi ya wanaCCM waliohudhuria katika mkutano wa uzinduzi wa kuadhimisha sherehe za kutimia miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzinzibar pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao leo katika uwanja wa wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo.  

WASANII MKOANI IRINGA WAMEMTUNGIA WIMBO MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI FRANK KIBIKI

$
0
0

MSANII wa muziki wa kizazi, kipya mjini Iringa, ONE LEE akitoa zawadi ya ngoma  kwa mwandishi wa Habari Frank Kibiki kwa niaba ya wasanii wenzake, ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kugombea  ubunge katika jimbo la Iringa mjini.
 
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa,  wasanii hao walisema wameamua kutengeneza wimbo huo kutokana na mchango mkubwa wa mwanahabari huyo, katika fani yao.

Msanii huyo Richard Kayombo  ‘One Lee’ ambaye alikabidhi wimbo kwa niaba ya wasanii wenzake alisema wimbo huo, unamtambulisha Kibiki, kama kiongozi wa kuigwa kutokana na tabia yake ya ucheshi na kujichanganya na watu.akizungumza wakati wa kukabidhi WIMBO huo msanii  ‘One Lee’ alisema kuwa FRANK KIBIKI amekuwa akiwapa elimu vijana juu ya kujitambua na kuwasaidia jinsi gani ya kujiajili wao wenyewe na kuonyesha njia ya kutokea kimaisha na dio imekuwa sababu ya wasanii wa mkoani hapa kutunga wimbo huo. 

“Wimbo unaitwa ‘Kuwa mfano wa kuigwa’, tumempa kaka yetu kama zawadi, ili wengine waige mfano wake. Awali tulitamani uitwe Kibiki, lakini kwa sababu tunataka kuuza tumeamua kuuita jina hilo,”alisema One lee.

Alisema miaka miwili iliyopita, aliwahi kukutwa na jambo ambalo alihitaji msaada wa haraka, alihangaika lakini alipokutana na Kibiki ambaye ni Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa, alisaidiwa jambo ambalo lilimfanya aanze kumuheshimu.

Alisema aliposikia kuwa Kibiki ametangaza nia, aliamua kushirikiana na wenzake ili watengeneze wimbo ambao hivi karibuni utaachiwa hewani.

‘One lee’alisena ngoma yake itamtambulisha Kibiki kama alivyo, na kwamba wameamua kumsaidia bila gharama yoyote kama sehemu ya mchango wao wakiamini ikiwa atafanikiwa kupenya na kupata nafasi hiyo, ataweza kuwaunganisha na kuwainua wasanii.
kwa upande wao wasanii wengine wa mkoani irnga walisema kuwa imefika wakati sasa iringa mjini itawaliwe na kiongozi mwenye uelewa juu ya kukuza uchumi wa mkoani na kuzingatia vipaji vya vijana kwa kuwa vijana ndio taifa la leo.

MBUNIFU WA MAVAZI WA KIMATAIFA, SHERIA NGOWI AMVALISHA RAIS MPYA WA ZAMBIA

$
0
0
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum  (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akikagua gwaride rasmi kabla ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish 
 
  Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akila kiapo cha kuwa Rais Mpya wa Zambia  katika sherehe za zilizofanyika  jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish
 Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akitia saini Hati Maalum Muda mfupi baada ya   kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
 
 Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akipokea salaam Maalum Kutoka kwa Rais wa Mpito wa Zambia Guy Scotts Muda mfupi baada ya   kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
  Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi  akiwa na Mkewe Eshter Lungu  Muda mfupi baada ya   kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
-----
Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia kipaji chake cha ubunifu wa mavazi baada ya kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.

Rais Lungu 58, aling’arisha sherehe hizo baada ya kuvaa suti rasmi (Presidential suit) rangi ya bluu, shati jeupe na tai nyekundu zilizobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi. Lungu aliambatana na mke wake, Eshter Lungu walipokuwa wanaingia viwanjani hapo huku wakisindikizwa na ulinzi mkali.

Akizungumza baada ya hafla hiyo, Sheria Ngowi alisema amefurahi kupata nafasi ya kipekee ya kumvalisha Rais Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake na kusema ni hatua kubwa katika kazi yake kama mbunifu wa mavazi wa kimataifa.

“Hii ni hatua kubwa katika kazi yangu ya ubunifu wa mavazi, namshukuru Mungu kwa kipaji alichonipa kinachoweza kunitambulisha na kunifanya niaminike hata kufikia hatua ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Mheshimiwa Edgar Lungu”, alisema Ngowi.

Mbunifu Ngowi alisisitiza kuwa juhudi, nidhamu, bidii na kumweka Mungu mbele ndio chachu ya mafanikio katika kila utendaji wa kazi zake akiwa na malengo ya kuipeleka kazi yake katika nyanja za kimataifa hata kutambulika katika sekta ya ubunifu wa mavazi duniani kote.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na aliyekuwa Rais wa muda wa Zambia, Guy Scott na mke wake Charlotte, Mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini(SADC), Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, baadhi ya viongozi wa juu wa Zambaia na nchi mbalimbali pamoja na wananchi wake.

Mbunifu huyo ameendelea kuonyesha na kudhihirisha kuwa Tanzania ni nchi yenye vipaji vinavyoweza kuiletea nchi ya Tanzania sifa na kuinua uchumi wake katika sekta mbalimbali. Hii si mara ya kwanza kwa mbunifu huyo kukata mawingu kuitangaza nchi yetu, kwani ni miongoni mwa wabunifu mashuhuri kutoka Afrika wanaopata fursa kuonyesha ubunifu wa mavazi yao katika maonyesho ya kimataifa kama vile New York Fashion Week nchini Marekani na Mercedes Benz fashion Week nchini Afrika Kusini.

Hii ni changamoto pia kwa wabunifu wa Tanzania kuziwania fursa zilizopo na pia kuongeza juhudi ili kutangaza na kupeleka kazi zao katika soko la kimataifa kama vile Sheria Ngowi alivyofungua mlango.

Mawaziri wa Afya wa Zanzibar na wa Afya wa Jamuhuri ya Muungano wakutana na waTanzania Ujerumani

$
0
0
Waziri wa afya na ustawi wa jamii wa Jamuhuri ya muungano Mhe.Bw.Seif Rashid na waziri wa afya wa ZanzibarMhe. Rashid Seif Suleiman, Siku ya jumapili 25 januari 2015 walikutana na kuongea na baadhi ya watanzania waishio nchini ujerumani katika hoteli ya Martim Hotel mjini Berlin.
 
Mawaziri hao kwa pamoja waliongozana na  balozi Tanzania nchini Ujerumani mheshimiwa Bw.Philip Malmo,katika mkutano huo mawaziri hao wote walielezea jinsi wizara zao zinavyofanya kazi kuhakikisha kuwa huduma za afya zinawafakia walio wengi na pia kuhakikisha siku za usoni kila Mtanzania atatanufaika na huduma hizo kwa kutumia bima ya afya bila kujali tofouti za uwezo wa vipato vyao. 
 
Watanzania waishio ujerumani wamefarajika sana na mkutano huo,pia mawaziri wamewataka watanzania waishio ughaibuni  kuchangia kuwekezakatika sekta ya huduma ya afya hata ikiwa ni sekta binafsi ,mawaziri hao wamesema milango ya wizara zao hipo wazi kwa watanzania wanaotaka ushauri,ushirikiano au kuwekeza katika sekta hizo.
 Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa(katikati)makam mwenyekiti wa UTU Bw.Peter Kazaura(mwenye kitamba shingoni) mdau Shah wa jiji la Berlin Mwenye kofia nao walikuwapo.
 Mkuu wa bendi ya Ngoma Africa Kamanda Ras Makunja akiwa Mhe.Philip Malmo Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ,katika mkutano katika hoteli ya Maritim mjini Berlin.
Waziri wa Afya na ustawi wa jamii ambaye  pia ni mbunge wa Rufiji Mhe.Seif Rashidi akiwa na Ebrahim Makunja aka Ras Makunja mjini Berlin,Ujerumani.
 Waziri wa Afya wa jamuhuri ya muungano mhe.Seif Rashidi akiongea na watanzania waishio Ujerumani,
 Waziri wa Afya wa Tanzania Mhe.Seif Rashid akiwa na baadhi ya watanzania nchini Ujerumani.

NEW YORK CITY YAWAKARIBISHA WATANZANIA WOTE KWENYE PARTY YA NGUVU YA MIAKA 38 TANGU KUZALIWA KWA CCM -JUMAMOSI FEB 21 !

$
0
0
Hii itakuwa ni Sherehe ya aina yake kufanyika katika Jiji la Wajanja Big Apple,Watu wote bila kujali Itikadi zao wanaalikwa kwani hii ni Birthday Bashhh na sio mkutano wa kisiasa,Njoo uburudike na watanzania wenzako kutoka states mbali mbali pamoja na Nje ya nchi,kutakuwqa na Burudani kutoka kwa wasanii maarufu kutoka Tanzania,Habari zaidi za Wasanii na Mgeni Rasmi kufuata.
                                                   Tuungane Tuiline Tanzania Yetu

                          
                                                  TICKETS PRICE: ADVANCE $40 | DOOR $50
Inclusive of:
*3-Course Dinner
*Soft Drinks
*Elegant Settings
*Entertainment
*Cash - Bar Beer $3| Liqour $5 | Wine $5 | Patron $7
CALL: 347-663-0781  | 917-698-6943 

Pata Filamu ya KUTAKAPOKUCHA kupitia Mtandao.

$
0
0
Katika maisha tunayoishi duniani sio vizuri kufanyiana mabaya, Kwani hujui kesho itakuaje. Malipo ni hapahapa Duniani . Fuatilia hii kupitia mtandao .......

Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo KUTAKAPOKUCHA au Kununua na iwe yako kupitia mtandao.

Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii


Pia unaweza kuangalia au kununua filamu nyingine kupitia mtandao huo huo

TRA YATOA SEMINA YA HIMAYA MOJA YA FORODHA KWA TUME YA MIPANGO

$
0
0
Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Mkuu wa Kongane ya Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kiuchumi, Bw. Paul Sangawe (Kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory).
Mtaalamu wa Masuala ya Forodha kutoka TRA, Bw. Stambuli Myovela (Kulia) akizungumza wakati wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory) kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

DK.SHEIN AFUNGUA KONGAMANO MAALUM LA CCM PEMBA.

$
0
0

8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa  hutuba  yake ya ufunguzi wa Kongamano maalum la Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Mikoa na wasomi wa Vyuo vikuu vya Pemba leo katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Casrto Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
9
Washiriki wa Kongamano maalum la Wanachama wa CCM wa Mikoa na wasomi wa Vyuo vikuu vya Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein wakati akitoa  hutuba  yake ya ufunguzi lililofanyika leo  katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Casrto Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.
3
Washiriki wa Kongamano maalum la Wanachama wa CCM wa Mikoa na wasomi wa Vyuo vikuu vya Pemba wakimkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipowasili katika ukumbi wa Fidel Casrto Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba kufungua Kongamano hilo leo.
4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai(katikati) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Hamadi Bakari Mshindo (kushoto) Katibu wa Kamati  Maalum wa Idara ya SUKI Eng.Hamadi Yussuf Masauni(kulia) wakiwa katika Kongamano maalum la Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Mikoa na wasomi wa Vyuo vikuu vya Pemba lililofanyika leo katuka ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba

6
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akimkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kufungua Kongamano maalum la Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Mikoa na wasomi wa Vyuo vikuu vya Pemba katika ukumbi wa Fidel Casrto Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba leo.
5
Katibu wa Kamati  Maalum wa Idara ya SUKI Eng.Hamadi Yussuf Masauni akitoa taarifa fupi inayohusu Kongamano  mbele ya mgeni rasmi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.

10
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakiwepo na Viongozi wengine baada ya kufungua Kongamano maalum la Wanachama wa CCM wa Mikoa na wasomi wa Vyuo vikuu vya Pemba leo katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Casrto Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,
11
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiagana Wanachama wa Chama cha Mapinduzi alipokuwa akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba kurejea Unguja leo baada ya kufungua Kongamano maalum la Wanachama wa CCM wa Mikoa na wasomi wa Vyuo vikuu vya Pemba katika Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika Skuli ya  Fidel Castro Januari 26, 2015 kufungua  Kongamano maalum la Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Mikoa na wasomi wa Vyuo vikuu vya Pemba. PICHA  ZOTE NA IKULU
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Hamadi Bakari Mshindo mara alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Fidel Castro leo kufungua  Kongamano maalum la Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Mikoa na wasomi wa Vyuo vikuu vya Pemba.


Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Mikoani

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo ya mradi wa nyumba za kuuza za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli na Msimamizi wa mradi huo Bw. Hassan Bendera.
 Hii ni sehemu ya nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli kama sehemu ya juhudi za Shirika hilo za kuwezesha wananchi wengi kumiliki nyumba. Nyumba hizi zinajengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini.

KUTOKA BARAZA LA WAWALIKILISHI ZANZIBAR.

$
0
0
  Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wakifatilia maelezo mbalimbali yanayotolewa mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
 Mwakilishi wa kuteuliwa Marina Joel Thomas akinukuu baadhi ya vipengele vya maswali na majibu ndani ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin katikati akiwa pamoja na Mwakilishi wa Kuteuliwa nafasi za Wanawake Raya Suleiman Hamad kulia na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salum Aljazeera wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Dkt. Fennela Afungua Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini na Wahariri wa Vyombo vya Habari

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwaeleza washiriki wa Mkutano huo umuhimu wa kuelimisha umma kuelekea upigaji kura ya maoni na kuwataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza suala hili la kitaifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JL Communication inayochapisha magazeti ya Jambo leo na StaaSpoti Bw. Theophil Makunga akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara pia aliwataka Maafisa Mawasiliano kutengeneza mazingira yatayowezesha kufanya kazi na wanahabari.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. GEORGE SIMBACHAWENE ARIPOTI OFISINI LEO

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (kushoto) akizungumza  na waandishi wa habari mara baada ya kupokelewa na  uongozi wa  Wizara  hiyo. Kulia ni  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava. Mhe. Simbachawene amesisitiza umuhimu wa sekta za nishati na madini  kama mhimili  mkuu wa ukuaji wa uchumi wa nchi na kuomba ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta za nishati na madini.
 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (kushoto) akipokea ua   la maua kutoka kwa mmoja wa watumishi wa Wizara  ya Nishati na Madini  Lilian Aroko mara baada ya kuwasili  kwenye ofisi za   Makao Makuu ya Wizara  ya Nishati na Madini.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe.  Charles Mwijage (Kulia) akimpokea  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (kushoto) mara waziri huyo alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Wizara  ya Nishati na Madini.
 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George  Simbachawene (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya  Sheria, Salome Makange  mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Makao Mkuu ya Wizara.


Mh. Stephen Masele akabidhiwa ofisi leo

$
0
0
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mh Ummy Mwalimu akimkabidhi Naibu Waziri mpya Ofisi hiyo Mh. Stephen Masele.
Naibu Waziri mpya Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Stephen Masele akiwa katika Ofisi yake aliyokabidhiwa na Mh. Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam leo.
Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi.Angeline Madete akitoa maelezo mafupi wakati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Stephen Masele akikabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Naibu Ofisi hiyo Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.

WATANZANIA WASHIRIKI MAONESHO YA SANAA-MASCUT OMAN

$
0
0

1
Sehemu ya Juu ya Msikiti wa Pili kwa ukubwa duniani “Masjid Sultan” ambayo Taa yake inayoonekana kwa juu  ina uzito wa Tani nane ikiwa imebeba Balbu 2220. Watanzania Wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa na Utamaduni walienda kutembelea Msikiti huo kujifunza zaidi.
Picha zote-Faki Mjaka-Mascut Oman
2
3
Wafanyakazi wa Msikiti wa Pili kwa ukubwa duniani “Masjid Sultan” wakijibu maswali na kutoa ufafanuzi kutoka kwa Watalii mara baada ya kumaliza kutembelea msikiti huo. Watanzania Wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa na Utamaduni nchini Oman nao walienda kutembelea Msikiti huo kujifunza zaidi.
5
Wageni na Baadhi ya Watanzania Wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa na Utamaduni nchini Oman wakiwa Sehemu ya mbele (Qibla) ya Msikiti wa Pili kwa ukubwa duniani “Masjid Sultan”. Msikiti huo umefanywa kama  Kivutio cha Watalii na kujifunza.Watanzania hao walienda kutembelea Msikiti huo kujifunza zaidi.
7
Sehemu ya nje ya Msikiti wa Pili kwa ukubwa duniani “Masjid Sultan”. Msikiti huo umefanywa kama  Kivutio cha Watalii na kujifunza ambapo Watanzania Wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa na Utamaduni nchini Oman waliutembelea Msikiti huo kujifunza zaidi.

…………………………………………………………………….
Faki Mjaka-Mascut Oman
Taasisi za Kidini nchini Tanzania zimeshauriwa kujenga Nyumba za Ibada zitakazokuwa huru kwa Mtu yeyote kuzitembelea na kujifunza ili kuzidisha upendo na mshikamano miongoni mwa jamii.

Kufanya hivyo kutasaidia kupunguza chuki na misimamo mikali ya kidini inayoweza kutokea miongoni mwa Jamii husika. Ushauri huo umetolewa na Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa na Utamaduni baada ya kutembelea Msikiti Mkubwa wa Sultan Qabus uliopo Mascut nchini Omani.

Msikiti huo wa pili kwa Ukubwa Duniani umefanywa kama kivutio cha Utalii na Uwekezaji ambapo Wenyeji na Wageni kutoka Mataifa mbalimbali hupata nafasi ya kuutembelea na kuuliza chochote kwa Wafanyakazi wake.Watanzania hao wamesema kuna mengi ya kujifunza baada ya kutembelea Msikiti huo ambayo yanaweza yakasaidia sana iwapo yataigwa nchini Tanzania.

Mmoja ya Watanzania hao Fred Halla amesema nchini Tanzania Nyumba za Ibada hugeuzwa kuwa sehemu ya kwenda kufanya Maombi na kuondoka kwa Waumini wa dini husika jambo ambalo haliwaunganishi vyema Watanzania.Amesema umefika wakati kwa Taasisi za Dini kuzifanya Nyumba za Ibada kama kimbilio la watu wa dini Tofauti kwenda kujifunza utamaduni na dini kwa usahihi wake jambo ambalo linaweza kuzidisha upendo zaidi.

“Kule kwetu ni Ajabu Muislamu kwenda Kanisani au Mkristo kwenda Msikitini lakini Katika Msikiti huu unaingia unapotaka na kuuliza chochote na unapata majibu..kwa hili unakuta unapata ukweli wa dini husika kinyume na unavyosikia Mtaani” Alisema Fred.

Amesema alikuwa anaamini kuwa Waislam ndio ambao wanaruhusiwa kuingia Msikitini tu lakini amebaini kuwa Msikitini anaweza kuingia Mtu yeyote na kuuliza chochote ilimradi kafuata sheria. Kwa upande wake Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania nchini Oman Abdallah Kilima amesema mfano wa Miskiti kama huo wa Sultan Qabus unaweza ukatumika pia kama njia ya kupunguza Misimamo Mikali na uelewa mbaya wa dini.

Amesema ni vyema pia Tanzania kuwe na utamaduni unaoruhusu Nyumba za Ibada kuwa sehemu ambayo Muumini wa Dini yeyote anaweza kwenda na kuuliza kwa uhuru kama ilivyokuwa kwa Masjid Sultan.“Kuna mambo mengi watu wanaaminishwa kuwa Misikitini Kuna hili na lile au Kanisani kuna hivi na vile lakini mtu anapopata fursa ya kwenda na kujionea na kuuliza maswali anaondoka akiwa amepata majibu sahihi na kuridhika kama Sisi tulivyopata nafasi hiyo” Alisema Kilima. 

Msikiti huo wa pili kwa ukubwa duniani ulijengwa kwa muda wa Miaka sita kutoka mwaka 1995 hadi 2001 ambapo miongoni mwa maajabu yake ni kuwa na Taa kubwa yenye uzito wa Tani 8 na balbu 1220.

Aidha Msikiti huo wenye huduma Tofauti ikiwemo kumbi za kufanyia mikutano,Kituo cha Taarifa, pia unauwezo wa kuchukua Waumini 10,000 kwa wakati mmoja na Maegesho ya Magari 4,000 kwa pamoja.

UKATAJI MITI YA MIKOKO HUSABABISHA UHARIBIFU MKUBWA WA MAZINGIRA

$
0
0
        Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo ya kwanza wa Rais  Fatma Abdulhabib Fereji  amesema  ukataji wa miti aina ya mikoko husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira  na  kufanya maji ya bahari kuingia katika maeneo ya kilimo na makaazi ya watu.

Hayo ameyaeleza katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani wakati alipokuwa akijibu suala la Mwakilishi  Bikame Yussuf Khamis alietaka kujua mpango  wa dharura wa  Serikali katika kuyanusuru mazingira ya bahari ili kuviokoa visiwa vidogo.

Waziri Fereji amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa  kushirikiyana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kutekeleza mradi wa kujenga uwezo wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabia ya nchi katika maeneo ya ukanda wa pwani ya Tanzania utakaohusisha maeneo ya Bagamoyo , Pangani , Rufiji na Zanzibar.

Amesema eneo la Kisiwapanza ni miongoni mwa maeneo ya Zanzibar yanayotegemewa kuwemo kwenye mradi huu na tayari wataalamu wa mradi  huo wamefika Zanzibar kwa ajili ya kuangalia maeneo ya mradi ambayo ni Kisiwapanza , Tumbe na Ukele kwa  Pemba na  maeneo ya Kilimani na Bwawani kwa Unguja.

Hivi sasa wataalamu hao wako katika hatua ya  mataarisho na kufahamu upeo wa mradi kwenye maeneo husika  ambapo Zanzibar imekadiriwa kupata kiasi cha dola za marekeni 361,300 kwa ajili ya  mradi huo.
 
Akijibu suala la nyongeza aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Chonga Abdullah Juma,  Waziri Fereji amesema Ofisi  pekee haiwezi kudhibiti kina cha maji ya bahari kwani ni suala la maumbile, hivyo wananchi wanapaswa  waelimishwe athari za  uharibifu wa mazingira ili waweze kuachana na vitendo hivyo.
 
Wakati huo huo Naibu Waziri wa  Afya  Mahmoud  Thabit Kombo  amesema  sera ya Serikali ya matibabu bure Zanzibar bado ipo na inaendelea kufanya kazi, licha ya kwamba wananchi wamekuwa wakichangia kwango kidogo  cha huduma za afya.

Akijibu suala la Mh Ali Salum Haji (Jimbo la kwahani ) aliyetaka kujua  mpango wa Serikali wa kuanzisha sera ya msamaha  kwa baadhi ya makundi ya watu  wakiwemo wazee wenye umri mkubwa na watoto chini ya miaka mitano kupata matibabu bila malipo kama zilivyo nchi nyengine jirani.

Naibu Waziri amesema Wizara ya Afya inaandaa miongozo ya uchangiaji wa huduma za afya ambapo makundi maalumu yameainishwa   kupatiwa msamaha wa kuchangia huduma hizo.

Ameyataja makundi hayo ni watoto wenye umri chini ya miaka 5 wazee wasiojiweza , walemavu wasiojiweza, watu wenye maradhi sugu kama vile  ukimwi,  kifua kikuu na saratani, na kwa wale wasiokuwa na uwezo bado wanaendelea kupata huduma za afya kulingana na taratibu zilizowekwa .

 Mwashungi Tahir na Rahma  Khamis  wa Maelezo. 
 IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.


RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA MFALME WA SAUDI ARABIA, AWASILI BERLIN, UJERUMANI, KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
333
Rais  Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa watawala na familia mjini Riyadh, Saudi Arabia Jumapili, Januari 25, 2015, alipofika kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ameendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
 444
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Fawzia Rasheed, Mkuu wa Sera wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) alipotua mjini Berlin, Ujerumani, leo Jumatatu 26, 2015 kuungana na viongozi mbali mbali duniani kujadili  jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.

PICHA NA IKULU

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo azindua chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO)

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa chama hicho kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kushoto kwa Katibu Mkuu ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Innocent Mungy na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bi. Sylvia Lupembe
   Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) Bw. Innocent Mungy akisoma Taarifa fupi ya Chama hicho kabla ya uzinduzi leo Mjini Mtwara
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Maafisa habari Kabla ya Kuzindua Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) ambapo aliwataka kuwa na umoja na Mshikamano ili kujijenga na kukiendeleza chama hicho kitakachosaidia kukuza taaluma na weledi katika utendaji wa kazi leo Mjini Mtwara.
Picha na Hassan Silayo.

WANANCHI WALALAMIKIA UGUMU WA MAISHA LICHA YA KUWA NA RASILIMALI ZA KUTOSHA

$
0
0

 WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini akiwa ametoka kumpokea makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI
 makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI akiwahutubia wananchi katika jimbo la mufindi kaskazini
WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kasikazi akiwahutubia wananchi wa jimbo la mufindi kusini ambako anatarajia kugombea ubunge kupitia chadema.

Wananchi wa wilaya ya mufindi  mkoani Iringa wamelalamikia ugumu wa maisha wanaokumbana nao kila kukicha licha ya wilaya hiyo kuwa na utajiri mkubwa wa rasilimali ya misitu pamoja na mazao ya biashara

Akizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na mjumbe wa mkutano mkuu wa chadema Taifa wilayani mufind Williamu Mungai mmoja wa wananchi hao Clement Mwachanga alisema kuwa wilaya hiyo ni moja kati ya wilaya inayofanya vema kwa kuingiza pato kubwa la taifa lakini wananchi wake wako katika wimbi kubwa la umaskini

Mwachanga amesema anashangaa wilaya kama ya mufindi inayoongoza kwa utoaji wa mbao nyingi lakini cha kushangaza shule nyingi  za msingi hazina madawati jambo linalopelekea wanafunzi wengi kukaa chinii

‘’Hii ni aibu kubwa sana kwa wilaya yetu haiwezekani wilaya inarasilimali za kutosha lakini wananchi wake wengine wanashidwa hata kupata mlo mmoja kwa siku huku watoto wao wakishidwa kupelekwa shule kutokana na kushidwa kulipa ada ya kumuandikishia mtoto ”

Kwa upande wake Williamu Mungai ambaye hivi karibuni ametangaza nia ya kulichukua jimbo hilo la mufindi kaskazi ambalo kwa sasa linaongozwa na naibu waziri wa maliasili na utalii Mahamudu Mgimwa amewataka wenyeviti wa mitaa kuhakikisha watoto wote wanaandikishwa shule za msinga hata kama hawana ada ya kuandikishiwa kwa kuwa elimu ni haki ya kila Mtanzania

Mungai  alisema ni kila mtoto ana haki ya kupata elimu ya msingi kwa kuwa ndivyo katiba inavyosema   na kuwataka walimu kuacha mara moja tabia ya kuwarudisha majumba watoto kwa kisingizio cha kukosa hela ya kuwaandikishia

"Niwatake wenyeviti wangu wa mitaa muhakikishe watoto wote wanaandikiswa  na kama kuna mwalimu atagona kumuandikisha kwa kisingizio eti hana shilingi eflu hamsini jikusanyeni pamoja niiteni na mimi twende wote tuone kama hata muandikisha kwa maana walishasema elimu bure sasa bure waliyosema ikuwapi" alisema Mungai

Hata hivyo mungai alisema imefika wakati wakuikomboa mufindi iliyoko katika wimbi la umaskini kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuataka wanamufindi kuhakikisha  wanachagua viongozi wenye maono ya mbali katika kuwalete maendeleo na sio porojo za kila siku.

Mungai alisema kuwa  atahakikisha anazunguka vijiji vyote 72 vya wilaya ya mufindi katika harakati zake za kujenga chama na kuweza kutambua kero za wananchi na kuangalia ni jinsi gani ya kuzitatua .

WAZIRI DKT. MAGUFULI AZINDUA UJENZI WA BARABARA ZA PETE JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

Waziri wa Ujenzi Mheshimkiwa Dkt.John Pombe Magufuli leo amezindua na kuweka  mawe ya msingi katika Ujenzi wa barabara za pete zitakazopunguza msongamano jijini Dar es salaam.

Barabara hizo zilizowekewa mawe ya msingi ni pamoja na ile ya  Kinyerezi –Kifuru hadi Mbezi Mwisho yenye urefu wa kilometa 14.0, Kigogo-Tabata Dampo yenye urefu wa kilometa 1.6, na Kimara Baruti-Msewe hadi Chuo Kikuu  cha Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 2.6. Barabara nyingine ni ile ya External –Kilungure hadi Kimara Korogwe kilometa 8.0, Wazo Hill-Goba hadi Mbezi mwisho kilometa 20 na Goba-Tangi bovu kilometa 9.0.

Akizungumza wakati akizindua ujenzi wa barabara hizo Waziri Magufuli amewataka wananchi kufuata sheria za barabarani kwa kutoingilia hifadhi za barabara na wale wenye nyumba pembeni mwa barabara kuzibomoa wenyewe ili kupisha ujenzi huo kwenda kwa wakati.

“Nawahakikishieni kwamba mkifuata sheria za kutojenga karibu na barabara barabara hizi zitajengwa kwa kiwango cha lami na kwa wakati ili kupunguza msongamano wa magari katika barabara kuu na ninyi mtanufaika na fursa za kibiashara kwa kuwa karibu na barabara za lami na hivyo kujikwamua kiuchumi”,amesisitiza Waziri Dkt. Magufuli.

Waziri Magufuli amesema barabara ya Wazo HilL –Goba yenye urefu wa kilometa 20 ikikamilika kwa kiwango cha lami itaziunganisha barabara za Bagamoyo na Morogoro ambazo zimekuwa zikikabiliwa na msongamano kwa muda mrefu.

Aidha, amesema barabara ya Kinyerezi- Kifuru hadi Mbezi mwisho yenye urefu wa kilometa 14 itapunguza pia msongamano kwa kiasi kikubwa kwa kuwa itakuwa inaunganisha barabara ya Morogoro na Nyerere hivyo kuwataka wananchi kuanza kuzitumia barabara hizo ambazo zitakamilika kwa wakati.


Amewataka vijana wanaopata fursa za ajira katika ujenzi wa barabara hizo kuwa waadilifu,waaminifu na wachapa kazi na kujiepusha na vitendo vya wizi vitakavyosababisha kuongeza gharama za ujenzi wa barabara hizo.

“Kumbukeni mkiiba vifaa vya ujenzi hamuibi vifaa vya kampuni zinazojenga bali mnajiibia wenyewe kwa sababu hizi ni fedha za kodi ya wananchi bali kufanya kazi kwa bidii na uadilifu kutawezesha ujenzi wa barabara kukamilika kwa wakati na ninyi kujihakikishia uhakika wa ajira”,alisema Waziri Magufuli.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mheshimiwa Said Meck Sadik amezungumzia umuhimu wa wakazi wa jiji la Dar es salaam kutunza barabara kwa kutofanya biashara kwenye hifadhi za barabara na kuahidi hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaokiuka taratibu za kisheria na kutupa takataka katika mitaro ya barabara.

Amewataka wabunge wa Mkoa wa Dar es salaam na wabunge wengine wanaoishi mkoani  Dar es salaam kutenga fedha za kutosha za ujenzi wa barabara jijini Dar es salaam ili kuhakikisha Wizara ya Ujenzi inamudu kuzijenga barabara za pembezoni zitakazopunguza msongama na kuliwezesha jiji la Dar es salaam kupitika wakati wote.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini  (TANROADS), Eng.Patrick Mfugale ameiomba Serikali kuongeza bajeti ya barabara ili kuwezesha Miradi ya barabara kukamilika kwa wakati na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ili barabara zijengwe kwa kiwango kilichokubalika katika mikataba.

Ziara hiyo ya Uzinduzi wa barabara za pete imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa jiji la Dar es salaam akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Bw.Ramadhani Madabida,Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa John Mnyika,Segerea-Dkt Makongoro Mahanga,na Kawe mheshimiwa Halima Mdee ambapo kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana ili Wizara ya Ujenzi ipate fedha za kukamilisha miradi hiyo itakayopunguza kwa kiasi kikubwa kero ya msongamano jijini Dar es salaam.

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE LEO WILAYA YA WETE MKOA WA KASKAZINI PEMBA.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba,Ndugu Kassim Mabrouk,mapema leo alipokuwa akiwasili mjini Wilayani Wete mkoa wa Kaskazini Pemba tayari kwa kuanza ziara ya siku tano mkoani humo.Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako Kisiwani Pemba kwa ziara ya Kuhimiza na Kukagua utekeleza wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinaa akisalimiana na baadhi ya Wanachama wa CCM Wilaya ya Wete,alipowasili katika ukumbi wa Jamhuri,ambapo Ndugu Kinana alipokea taarifa ya kazi ya chama na Utekelezaji wa Ilani na pia kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya.
 Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wakiwa katika ukumbi wa Jamhuri wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mambo mbalimbali ikiwemo Utekelezaji wa Ilani.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM katika ukumbi wa Jamhuri mjini Wete mkoa wa Kaskazini Pemba mapema leo,Kinana alizungumza nao mambo mbalimbali ikiwemo Utekelezaji wa Ilani.
Pichani kati ni Meneja Utawala wa shirika la Ununuzi wa Karafu (ZSTC),Bwa.Issa Hassani akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kulia alipokwenda kutembelea Ghala la Karafuu na kuona zoezi la ununuzi wa Karafuu katika Bandari ya Wete,Kaskazini Pemba.
 Katibu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kutembelea na kukagua bei ya karafuu katika ghala la Karufuu katika bandari ya Wete-Pemba.
 Ghala la Karafuu kama lionekanavyo pichani
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na wanachama wengine wa chama hicho,wakitoka kutembelea Kikundi cha Ushirika cha ufugaji wa samaki na uhifadhi wa Mazingira katika Jimbo la Gando,wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mshauri wa kikundi,Bwa.Mwinyjuma Hamad juu ya Kikundi cha Ushirika cha ufugaji wa samaki na uhifadhi wa Mazingira chenye idadi ya washirika wapatao 22,katika Jimbo la Gando,wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Mshauri wa kikundi (Organization for Gando Fishing, Farm & Enviromental Conservation) Bwa.Mwinyjuma Hamad akitoa maelezo mafupi kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana nama mabaki ya miti yanavyoweza kutengenezwa na kutumika kama mkaa ikiwa kama ni sehemu ya kusaidia kutunza mazingira.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki utengenezaji wa Maseredani (Majiko ya Mkaa) yanayotengenezwa  kwa kutumia udongo,Majiko jayo yanatengenezwa na Vijana wajasiliamali wapatao 21 katika kijiji cha Chanjaani,shehia ya Ukunjwi Jimbo la Gando,wilaya ya Wete mkoa wa kaskazini Pemba,ambapo mmoja wao alieleza kuwa wamekuwa wakifaidika na mradi huo kwa kiasi kikubwa,ikiwemo na kujiongezea kipato kwa kuuza kwa wingi majiko hayo,alisema kuwa asilimia 70 ya majiko yanatengenezwa Pemba,hivyo imepunguza uingizwaji wa majiko kutoka nje.
 Pichani shoto ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Zanzibar,Bwan Fakhi Othman Sharif akiwaongoza Katibu Mkuu wa CCM ndugu Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenda kupokea taarifa ya usambazaji wa Umeme na kushiriki kazi za Usambazaji umeme (kusimamisha nguzo za umeme),katika kijiji cha Chanjaani,jimbo la Tambwe,Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.Mradi huo una thamani ya shilingi milioni 84.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana katikati,Balozi Ali Karume kushoto na Dkt.Maua Daftari pichani kulia wakishiriki kufukia mabomba ya maji katika mradi wa usambazaji Maji katika Jimbo la Mtambwe,Wete mkoa Kaskazini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza na wanachama wa Tawi la Kigangani,jimbo la Ole,Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mjini Wete,mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia baadhi ya Wananchi waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mjini Wete,mkoa wa Kaskazini Pemba.

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images