Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA MRADI MKUBWA WA REA WA SHILINGI BILIONI 25.7 MKOANI SIMIYU

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA Awamu ya Pili.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo leo amezindua mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili, mkoani Simiyu ambapo vijiji 170 vimeunganishwa na mradi huo.
Mwananchi kutoka katika kijiji cha Nyanguge kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu akiwasilisha hoja mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa kwanza kulia) mara Waziri alipotembelea kijiji hicho wakati akielekea kwenye uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili wenye thamani ya shilingi bilioni 25.7.
Mbunge wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda (kushoto) akitafsiri hotuba ya shukrani iliyotolewa kwa lugha ya kisukuma na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Shishiyu mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo.



Dkt. Magufuli aagiza kufungwa mfumo mpya wa kielektroniki katika vivuko vyote nchini

$
0
0
Dkt. John Magufuli akikata utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Dkt. John Magufuli na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakifurahia baada ya kukata  utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.
Mfanyakazi wa  kivuko cha Kigongo -busisi mkoani Mwanza akionesha wananchi namna ya kutumia mashine hiyo.

Na JOHN DOTTO,  Mwanza .
 WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ameagiza kufungwa kwa mfumo mpya wa kielektroniki katika vivuko vyote nchini ili kukabiana na wajanja wachache wanahujumu mapato katika vivuko hivyo. 

 Mbali ya hilo, ameagiza kufanywa kwa utaratibu utakaowezesha huduma katika vivuko zinatolewa kwa saa 24 ili kukidhi mahitaji ya wananchi. 
 Dkt. Magufuli alitoa maagizo hayo jana katika uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania. 

 "Tulianze pale Kigamboni na tukaona mafanikio, tulipokuja hapa (Kigongo) tukaboresha na mafanikio yameonekana kwa kiasi kikubwa. Vivuko vyote sasa vifungwe mfumo mpya wa kielektroniki.vivuko vyote nchini," aliagiza Dkt. Magufuli. 

 Alisema mfumo huo una faida kubwa ikiwemo kudhibiti upotevu wa mapato ambapo katika kivuko cha kigongo - Busisi alisema mapato yameongezeka kwa takribani asilimia 40 baada ya kufungwa kwa mfumo huo. 
 Hata hivyo, Dkt. Magufuli alikataa kutaja ni kwa shilingi ngapi mapato hayo yameongezeka kwa hofu kuwa watu wenye dhmira mbaya wakisikia wanaweza kwenda na kufanya uhalifu. 

 Pia, aliagiza Kivuko kwa Kigamboni nacho kiboreshwe mfumo wake kama ilivyokuwa kwa Kigongo - Busisi. Waziri huyo wa Ujenzi, alisema kutokana na mafanikio yanayopatikana katika kudhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi, wafanyakazi husika kwa maana ya wale wa TEMESA maslahi yao yanapaswa kuangaliwa upya na kuboreshwa. "Kama mapato ni mazuri, wafanyakazi nao walipwe vizuri, wasikae kimasikini kwani wanapaswa kuona mwaka 2015 ni ukombozi katika maisha yao. 

 Alisema serikali chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete imefanikiwa kujenga madaraja yote makubwa nchini ambapo kwa sasa kuna madaraja 4880 nchini na kuwa wakati inapata uhuru kulikuwa na madaraja mawili ambayo yalikuwa ya kuvutwa. 

 Mfumo wa kielektroniki katika vivuko vya Kigamboni na Kigongo Busisi ulifungwa na Kampuni ya Africom Tanzania ambaye Mkurugenzi Mtendaji wake Juma Rajabu alisema watahakikisha wanafunga mifumo ambayo itadhibiti upotevu wa mapato na kurahisisha huduma kwa wananchi ambao ndiyo watumiaji.

Dkt. John Magufuli akikata utepe kuzindua  mfumo mpya wa kielektroniki katika kivuko cha Kigongo -busisi mkoani hapa uliowekwa na Kampuni ya Africom Tanzania.

BONGO MOVIE KUPAMBA UZINDUZI WA KITABU CHA MAREHEMU KANUMBA LANDMARK HOTEL

$
0
0

 

UZINDUZI wa kitabu cha msanii wa filamu hayati Steven Kanumba unatarajia kuandika historia kufuatia maandalizi yaliyopangwa anasema mratibu wa tamasha hilo Mohamed Mwikongi ‘Frank’ amesema kuwa kutakuwa na mambo muhimu sana kwa ajili ya kumuenzi msanii huyo ambaye aliitangaza Tanzania kimataifa.


“Tumepanga kufanya mambo makubwa kwa ajili ya mwenzetu na tunataka ijengeke tabia ya kuenzi wasanii mbalimbali, pesa za uzinduzi wa kitabu hiki utafungua Kanumba Foundation kwa ajili ya kusaidia wanawake wajane na watoto yatima,”anasema Frank.


Frank anawakaribisha wadau wa Kanumba kwa kufika na kujione kazi za marehemu Kanumba na kuoshuhudia wimbo maalumu wa Marehemu Kanumba utakaoimbwa na mwanamuziki nyota Christian Bella kwa ajili ya tukio maalum .
                                         

Kitabu cha historia ya maisha ya mwigizaji nyota Swahilihood Hayati Steven Kanumba kinatarajiwa kuzinduliwa tarehe 10 January 2014 katika ukumbi wa Landmark Ubungo, uzinduzi huo utaambatana na maonyesho ya kazi za marehemu Kanumba alizowahi kushiriki na kuzifanya.


Mama yake mzazi akiongea na waandishi wa habari amewashukru wale wote ambao wamekuwa wakijaribu kufanya kazi ambazo kwa njia moja au nyingine zinamkumbuka mwanaye ambaye aling’ara katika tasnia ya filamu Swahilihood na kufanikiwa kutangaza Tanzania.


“Nawashukru sana watanzania na wale ambao si Watanzania wamekuwa faraja sana kwangu, hasa pale ambapo wamekuwa wakiona umuhimu wa kumuenzi Kanumba kwa njia tofauti tofauti, nawashukru sana, na najua kila mtu ana mchango mkubwa si rahisi kuwataja majina maana mpo wengi,”anasema mama Kanumba.


Kitabu hiki kinachohusu maisha ya Kanumba The Great Fallen Tree kimeandikwa na E. Emmanuel kutoka nchini Canada na kuhaririwa nchini Marekani na kufanyiwa uchapishaji nchini Kenya.


Uzinduzi wa kitabu utasindikizwa na Christian Bella na Bendi ya Malaika kiingilio ni Ths. 20,000/ na utapata kitabu kimoja bure  ukiingia tu mlangoni na kazi zote za Hayati Kanumba zitapatikana siku hiyo. USIKOSE TUKIO HILI LA AINA YAKE!

Airtel kuzindua Airtel UNI 255 J-mosi maalum kwa vyuo vikuu Dar es salaam

$
0
0
Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando amesema “Airtel Uni 255 ni huduma pekee yakibunifu toka Airtel Maalum kwa wanafunzi wa vyuo yenye kuwapa unafuu wa kuwasiliana wawapo chuoni, sasa wanafunzi wote wa chuo wanapotaka kupata nyongeza ya vile wanavyosoma kwenye mtandao huduma  hiii  ndio jibu sahihi kwao kutokana na unafuu wake kwenye inteneti.

Afisa Masoko wa Airtel Henrick Bruno akionyesha moja kati ya vocha za Airtel UNI255 maalum kwa vyuo vikuu nchini tayari kwa uzinduzi jumamosi hii.


 ·                Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole kupamba uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UDSM
                                                                                                             
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imebainisha kuwa mwishoni mwa wiki hii itazindua rasmi huduma mpya maalum kwa ajili ya kutoa huduma nafuu za mawasiliano kwa wanafunzi walioko vyuoni katika chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM ambapo hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama Airtel UNI 255 kwa vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam itafanyika katika viwanja vya Mabibo hostel

Akiongea kuhusiana na uzinduzi wa huduma hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando amesema “Airtel Uni 255 ni huduma pekee yakibunifu toka Airtel Maalum kwa wanafunzi wa vyuo yenye kuwapa unafuu wa kuwasiliana wawapo chuoni, sasa wanafunzi wote wa chuo wanapotaka kupata nyongeza ya vile wanavyosoma kwenye mtandao huduma  hiii  ndio jibu sahihi kwao kutokana na unafuu wake kwenye inteneti, kupiga simu na hata sms. Huduma hii tayari tumeshaizindua kwa vyuo vikuu vingine vya Dodoma, Mbeya, Iringa, Mwanza na imeonyesha mafanikio makubwa sana kwa watumiaji wakiwemo wanafunzi na wale wote wanaotumia huduma hii maeneo ya vyuo”

“Airtel tumeona ni vyema tuizindua hapa katika vyuo vya Dar es salaam wiki hii siku ya Jumamosi pale mabibo hostel ambapo mbali na uzinduzi kutakuwa na tamasha kubwa litakalopambwa na watoa burudani nguli akiwemo Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole pmaoja na DJ maarufu jiji Dj Zero aliongeza kusema Mmbando

Nae meneja wa huduma hiyo ya UNI 255 Anethy Muga alisema “Airtel tumeoana hii ni huduma maalum kwa wanafunzi na ndio maana tukaona ni vyema kuizindulia katika Hostel zao pale mabibo ambapo tunaamini wanafunzi wengi wa chuo kikuu hapa jijini wanaifahamu na wanaishi mabibo hivyo wanakaribishwa katika uzinduzi huo ambapo kiingilo chake ni BURE”

Burudani zitakuwa zakutosha kupitia Airtel UNI 255  siku hiyo

Kampuni ya simu za mkononi ya airtel ilianzisha huduma ya UNI255 ili kuendana sambamba na mkakati wao wa kusaidia vyuo vikuu nchini kutumia ipasavyo huduma za mtandao ili kuboresha sekta ya elimu kwa lengo la kusaidia wateja wake walioko vyuoni kufikia malengo yao.

NAIBU WAZIRI WA MIUNDO MBINU ISSA GAVU AFUNGUA MTAMBO WA KUSAFISHIA MAJI UZING'AMBWA.

$
0
0
 -Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (Gavu)akifungua kitambaa kama ishara ya Ufunguzi wa mtambo wa kubadilishia maji kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama huko Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (Gavu)akikinga Maji yaliobadilishwa kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama baada ya kufungua huko Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Wananchi mbalimbali wakinywa maji yaliobadilishwa kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama baada ya kufunguliwa huko Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (Gavu)akitoa hotuba wakati alipofungua mtambo wa kubadilishia maji kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.kulia yake nimuakilishi wa Taasisi ya Mork Water Solution ya Ujarumani Mikalen na kushoto yake ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Idriss Muhsin Hijja.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Five new year car resolutions

$
0
0
 Save hundreds of bucks on car maintenance costs with these 2015 car resolutions,Advices Carmudi Tanzania.

January 2015, Dar es Salaam, Tanzania –  As we welcome the year 2015, it is, time for us to reflect on the car resolutions most of us never kept. Car owners set goals but often neglect getting maintenance on their cars to keep them in top shape and bring their cars in only when repairs are needed. Carmudi, the fastest way to buy and sell cars online shares with you some easy-to-keep 2015 car resolutions that’ll save you plenty of bucks down the road in the upcoming year.

Resolution 1. Carry out two check ups per year.
Are you confident that your car fluids, battery, brake system, steering and suspension are up to scratch? Think again! Unless you have scheduled two car check ups per year with an expert engineer, you cannot be sure. Only trusted experts can identify the smallest of problems and thus help you save on your maintenance costs in the longer term. If there is a problem, it will be picked up early on, and thus prevent it from turning into a more costly repair job. And when it comes to selling your vehicle, potential buyers will be very impressed both with the condition of your car and the maintenance documents that you can produce at the time of the sale. So get ready to cash in more from your car.
Result: Higher resale value, plus save up to 320,000 TZS on breakdown costs!

Resolution 2.  Avoid aggressive driving, be smart.
Are you an adrenaline-seeking, pedal-to-the-metal kind of driver? If so, then this resolution will surely be difficult to stick with. But it’s not impossible, and the savings will be well worth it. Stop the high speed driving, avoid quick starts and hard braking. Drive smart and increase your fuel efficiency by up to 40 per cent. Yes, 40 per cent! You can even further reduce your fuel costs by driving at the optimal fuel saver speed of between 50 and 60 Miles per hour.
Result: Increase your fuel efficiency by up to 40 per cent.

Resolution 3. Maintain proper tire inflation.
Over inflated tires coupled by poor road conditions - potholes, rocky roads etc, can lead to rapid wear and tear and even punctured tires. If you want to get the best performance out of your tires, then you must keep your tire inflation at optimal levels. How? Check the information provided by your tire manufacturer. Keep in mind that under inflated tires can reduce fuel efficiency by up to 15 per cent, reduce your tire life and can lead to maneuverability problems which can cause accidents.  
Result: Save on tire costs, fuel costs by up to 4 per cent, avoid risk of accidents and repair costs.

Resolution 4.  Keep up with fluid changes.
Place great importance on oil and transmission fluids, making sure to carry out regular fluid changes. Why? It will help to ensure the brakes and clutch system is well maintained. If you Ignore these details, you might eventually have to replace your brakes and clutch system. This can be rather expensive and time consuming. Replacing brakes can costs up to 600,000 TZS, and repairing clutch system can cost up to 2000,000 TZS.
Result: Avoid replacing the brake and clutch system - save more than 160,000 TZS

Resolution 5.  Keep your car clean.
Trash or mess can become a hiding place for problem spots and stains. So, keep your car clean and make use of your car care kit to remove spots or stains before they get out of hand. You will be surprised to know that dirt and grime can be very harsh on your vehicle, especially for the interior of your car. Investing in a good quality car mat and vacuuming it on a regular basis can fetch you good long-term returns.

Result: Save up to 5000,000 TZS to replace the entire interior of your car

AFISA HABARI IRINGA ATANGAZA KUMVAA KAYOMBO MBUNGE WA MBINGA MASHARIKI KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA HUU

$
0
0
Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Humphrey Kisika (32)

Katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba mwaka huu
afisa habari  na mahusiano wilaya ya Iringa Hafley Kisika ametangaza
kugombea ubunge katika jimbo la Mbinga mashariki kupitia tiketi ya
chama cha mapinduzi CCM, ili kuleta maendeleo katika jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari KISIKA amesema kuwa sababu
inayompelekea kugombea ubunge katika jimbo hilo ni pamoja na kuleta
siasa safi pia kuunganisha wananchi na wataalamu mbali mbalimbali ili
kusaidia jimbo hilo kuendelea hasa katika maswala ya miundombinu.

Aidha amesema kuwa chama cha mapinduzi kina sera nzuri na kwamba
ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ikiwamo vijana,wazee na makundi
mengine katika jamii kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua jimbo la
Mbinga mashariki kimaendeleo.

KISIKA amekanusha uvumi unaodai chama cha mapinduzi kimepoteza dira na kuongeza kuwa Ccm ni  chama imara na kuwataka vijana watambue
wanafanya nini   na kuwa mstari wa mbele kuleta mabadiliko ya
kimaendeleo  na sio kuleta machafuko.

Ameendelea kusema kuwa pamoja na kuwa na ushindani mkubwa katika siasa lakini ilani na sera za chama husika pamoja na mgombea ndizo ambazo
zinaweza kumtambulisha mtu kama anauwezo wa kuwa kiongozi.

Hata hivyo KISIKA anatarajia kugombea ubunge katika jimbo la Mbinga
mashariki huku akiwa ni mjumbe wa chama cha mapinduzi katika chuo
kikuu cha Tumaini,Mbunge kwa miaka mitatu pamoja na katibu katika
kamati mbalimbali chuo kikuu cha Tumaini mbali na hayo KISIKA ni afisa
habari katika halmashauri ya wilaya ya Iringa.

KWA vyovyote iwavyo, mapigo ya moyo ya Mbunge wa Jimbo la Mbinga
Mshariki mkoani Ruvuma, Gaudance Kayombo yataongezeka mara dufu baada ya kijana msomi; Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,
Humphrey Kisika (32) kutangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo
katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Kisika, msomi mwenye shahada ya kwanza ya uandishi wa habari ambaye
pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, anayesoma shahada ya pili
ya uandishi wa habari na utawala anataka kuwania nafasi hiyo kupitia
chama chake Chama cha Mapinduzi (CCM).

Na Fredy Mgunda

WAOMBA KITUO MAALUMU CHA WATOTO WALEMAVU BUHANGIJA KUSAIDIWA ZAHANATI.

$
0
0
DSC_0002
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kuelekea kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.

Na mwandishi wetu, Shinyanga
MKUU wa wilaya ya Shinyanga AnneRose Nyamubi ameomba jamii ya watanzania kusaidia kupatikana kwa zahanati katika kituo cha kulelea watoto walemavu cha Buhangija ili kupunguza adha wanazopata watoto hao katika huduma za afya.

Kauli hiyo ameitoa katika mazungumzo na mwandishi wa habari hizi ambaye alifika katika kituo hicho akiambatana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukiongozwa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

Nyamubi amesema kwamba ingawa hospitali ya mkoa ina dirisha kwa ajili ya matibabu ya watoto hao,wakati mwingine inakuwa shida daktari maalumu anayehusika anapokuwa hayupo. Aidha alisema kwa namna watoto hao walivyo wanahitaji huduma ya karibu ya kitiba ambayo inawezekana kama kituo hicho kingekuwa na zahanati yake.
DSC_0026
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi kwake, Bi. Chitralekha Massey ( wa pili kulia kwake) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (wa pili kushoto). Wengine katika picha ni Afisa Elimu Sayansikimu, Beatrice Mbonea (wa kwa kulia), Afisa Elimu Msingi wa manispaa ya Shinyanga, Bi. Pudensiana Magnus (katikati kulia), Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga, Festo Kang'ombe pamoja na Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Shadrack Kengese.

Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2010 kwa ajili ya watoto walemavu wasiosikia na wasiiona kwa sasa kinapokea watoto wenye alibnizim ambao wanaokabiliwa na ujahiri dhidi ya maisha yao. Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya kituo hicho ambacho serikali hutenga bajeti kwa ajili ya wanafunzi 50 wasiosikia na kuona, sasa kina watoto wenye albinism 247 ambao hawako katika bajeti na wanaishi kutokana na misaada ya watu mbalimbali.

Alisema kwamba watoto wenye albinism wanahitaji huduma za tiba za karibu zaidi kutokana na mazingira yanawazunguka na dirisha pekee katika hospitali ya mkoa halitoshi kwani wakati mwingine wanalazimika kukaa kwenye foleni kama wagonjwa wengine na hili halipendezi.
Aidha alisema kituo hicho cha Buhangija kwa sasa ni kidogo kuzingatia na uwingi wa wanaohitaji msaada na hivyo serikali inatafuta eneo jingine kwa ajili ya kujenga kituo.
DSC_0053
Mazungumzo yakiendelea ndani ya ofisi za Mkuu wa mkoa wa Shinyanga zinazokaimiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi.

Kufurika kwa watoto hao wenye ulemavu kunatokana na tishio la maisha yao hasa ukanda wa Ziwa ambapo familia zao zimewakimbiza kituoni hapo kwa ajili ya usalama wao. Aidha Mkuu huyo wa wilaya amesema kwamba kituo hicho hakina bajeti na kutaka wasamaria wema kuendelea kuchangia ili watoto hao waendeshe maisha ya kawaida.

Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja Mataifa yaliyopo nchini, Alvaro Rodrigues amesema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kituo hicho na kuwataka wanaotunzwa hapo kutoacha kuishi kama watoto kwani ndio tunu waliyonayo kwa sasa.

Aidha alisema kwamba anauchukua wimbo waliouimba ambao unazungumzia machungu ya maisha yao na kwenda kuwaeleza watu wengine ili nao washiriki katika kubadilisha hali ya kuogofisha na kuleta usalama.
DSC_0068
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema alijumuika kwenye mazungumzo hayo. Pichani akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.

Alisema wao (UN) wamefika katika kituo hicho kuona watoto wanavyoishi na watafanya nini kuwasaidia. Aliwataka Watanzania kuhakikisha wanakomesha machungu ya albino hao na kuishi nao kama watu wengine wa kawaida. Aidha Mratibu huyo alipata nafasi ya kuzungumza na Binti wa miaka 19 Masabu masuka ambaye amejifungua mwaka jana kituoni hapo bila msaada wa wauguzi baada ya kulazimika kuondoka kwao akiwa mjamzito kukwepa mauaji dhidi ya albino yaliyofanyika Mei mwaka jana wilayani Bariadi. Binti huyo alifika kituoni hapo na kaka zake watatu ambao wote ni maalbino kama yeye.
DSC_0075
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi katika picha ya pamoja na ugeni kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa Tanzania na Shirika la UNDER THE SAME SUN.
DSC_0120
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi akiwasalimia watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga kabla ya kumtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
DSC_0150
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akizungumza na watoto wenye ulemavu wakiwemo wa ngozi (hawapo pichani) wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho. Katikati ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi.
DSC_0167
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa zawadi ya maziwa kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.

DSC_0174
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akishiriki kwenye zoezi la kugawa zawadi kwa watoto hao.
DSC_0186
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya Mratibu huyo, Bi. Chitralekha Massey wakiendelea na zoezi la kugawa zawadi kwa watoto hao.
DSC_0203
Mratibu Mkazi huyo Bw. Alvaro Rodriguez akiwasaidia watoto hao kufungua biskuti alizowapekea kama zawadi alipotembelea kwenye kituo hicho.
DSC_0213
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akieleza jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) alipokuwa akikagua mazingira ya kituo hicho na kuona ni jinsi atawasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili kituo hicho.
DSC_0235
Pichani ni jiko la kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wakiwemo wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
DSC_0248
Wapishi wakiendelea na shughuli zao kuwapikia watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.
DSC_0261
Mwalimu Mkuu wa shule ya watoto wenye maalum ya Buhangija Jumuishi, Peter Ajali akitoa maelezo ndani ya moja ya mabweni kituoni hapo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema.
DSC_0278
Mwalimu Mkuu wa shule ya watoto wenye maalum ya Buhangija Jumuishi, Peter Ajali akimwonyesha baadhi ya sehemu ambazo hazisakafiwa ndani ya mabweni kituoni hapo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
DSC_0308
Baadhi ya matandiko wanayotumia watoto hao wenye mahitaji maalum kulali kwenye sakafu ambayo haijasakafiwa na pia kutokana na uhaba wa mabweni inawalazimu kubanana na kulala bila uhuru.
DSC_0311
Bweni lililojengwa na Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred linalohudumia watoto 48 ambalo linahitaji kumaliziwa ili watoto hao nao waweze kulala mahali pazuri.
DSC_0233
Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodrigues akizungumza na binti wa miaka 19 ambaye ni mlemavu wa ngozi na kutosikia, Masalu Masuka ambaye anaishi katika kituo cha watoto walemavu cha Buhangija baada ya kukimbia kwao Bariadi kukwepa wauaji wa albino. Binti huyo alijifungua mtoto wake akiwa kituoni hapo bila msaada wa muuguzi. Kituo hicho kinahitaji msaada wa kujengewa zahanati. (Picha na Zainul wa Mo Blog)
DSC_0331
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akicheza mpira ambao ni moja ya zawadi alizozitoa kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kukitembelea kituo hicho kinachokabiliwa na changamoto mbalimbali na kuwaahidi kuwasaidia huku akiwashirkisha na wadau wengine wa maendeleo. Kushoto mwenye kofia ni Khassan Khamis na kulia ni Emmanuel Deus.
DSC_0346
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiendelea kucheza mpira na kufurahi na watoto hao wenye ulemavu wa ngozi.
DSC_0386
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa amembeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Ghoke Maliwa anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kukitembelea kituo hicho juzi mkoani humo.
DSC_0351
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma ujumbe unaosema "DREAM BIG" kwenye T-shirt ya mtoto Agnes Kabika mwenye ulemavu wa ngozi anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho.
DSC_0315
Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya Mratibu huyo, Bi. Chitralekha Massey akibadilishana mawazo na binti anayefanya shughuli za kujitolea Claire Grubbs kutoka nchini Marekani aliyepiga kambi kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
DSC_0428
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiagana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwenye kituo hicho.

Rais Kikwete amwapisha Msajili wa Mahakama ya Rufaa

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE KUANZA TAREHE 13 – 23 JANUARI 2015

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


BUNGE LA TANZANIA

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawatangazia Waheshimiwa Wabunge wote, wadau na umma kwa ujumla kuwa Kamati za Kudumu za Bunge zitaanza vikao vyake tarehe 13 hadi 23 Januari 2015. Vikao hivyo vitakavyoutangulia mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge la Kumi vitajadili na kuchambua pamoja na mambo mengine Miswada mbalimbali ya sheria.

Miswada  itakayopitiwa na chambuliwa (pamoja na kamati husuka kwenye mabano) ni hii ifuatayo:
        i.            Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji wa Mwaka 2014 [The Immigration (Amendment) Bill, 2014], [Kamati ya Mambo ya Nje]

     ii.            Muswada wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI wa Mwaka 2014 [The Tanzania Commision for AIDS (Amendment) Bill, 2014, [Kamati ya Masuala ya UKIMWI]

   iii.            Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha wa Mwaka 2014 [The Firearms and Ammunition Control Bill, 2014], [Kamati ya Ulinzi na Usalama]

   iv.            Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa Mwaka 2014 [The Disaster Management Bill, 2014], [Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala]

       v.            Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Ajira za Wageni wa Mwaka 2014 [The Non-Citizen Employment Regulation Bill, 2014], [Kamati ya Maendeleo ya Jamii]

   vi.            Muswada wa Sheria ya Wataalam wa Kemia wa Mwaka 2014 [The Chemist Professionals Bill, 2014], [Kamati ya Huduma za Jamii]

 vii.            Muswada wa Sheria ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2014 [The Government Chemistry Laboratory Bill, 2014], [Kamati ya Huduma za Jamii]

 viii.            Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Stakabadhi Ghalani wa Mwaka 2014 [The Warehouse Receipts (Amendment) Bill, 2014, [Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara]. Angalizo: Wakati wa uchambuzi Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara itashirikiana na  Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.

    ix.            Muswada wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya wa Mwaka 2014 [The Drug Control and Enforcement Bill, 2014], [Kamati ya Masuala ya UKIMWI]

       x.            Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2014 [The Written Laws (Miscelaneous Amendments) Bill, 2014, [Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala]. Angalizo: Aidha inashauriwa wakati wa kuchambua Muswada huu Kamati za kisekta zishirikishwe kwenye  kutoa maoni kwenye marekebisho ya sheria ya sekta husika.

    xi.            Muswada wa Sheria ya Bajeti wa Mwaka 2014 [The Budget Bill, 2014], [Kamati ya Bajeti]

Aidha, kwa taarifa hili Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaombwa kuwasili Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Januari 2015 tayari kwa kuanza kazi tarehe 13 Januari 2015.

Imetolewa na Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habri, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa
07 Januari,  2015.

Nigeria kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta za Filamu na Vijana

$
0
0
unnamed 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, vijana , utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati alipokutana na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Balozi Ole Njoolay kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Nigeria katika sekta ya Filamu na Vijana
unnamed1Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Balozi Ole Njoolay (kushoto) akiwa ameshika zawadi ya kinyago aliyopewa na Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ili kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na Nigeria katika sekta ya Filamu na Vijana
unnamed3Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo wa Mheshimiwa Prof. Elisante Ole Gabriel wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria. Mhe. Balozi Ole Njoolay Viongozi hao waliongea kuhusu kudumisha ushirikiano katika sekta ya Filamu na Vijana .Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana James Kajugusi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Joyce Fisso Picha na Benjamin Sawe, WHVUM

SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR LAZINDUA TAGI MPYA YA KUSAIDIA MELI KUBWA KUINGIA NA KUTOKA GATINI

$
0
0

1 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tagi mpya ya Shirika la Bandari Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.2 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tagi mpya ya Shirika la Bandari Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.3 
Tagi iliyozinduliwa ikirusha maji ikiwa ni majaribio ya kuzima moto iwapo tatizo hilo litajitokeza. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………………
Na Miza Kona Na Abdalla Ali – Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri amewataka wafanyakazi wa Shirika la Bandari Zanzibar kufanya kazi kwa juhudi na ufanisi kwa lengo la kuleta maendeleo na mabadiliko nchini. Hayo ameyaeleza huko katika Shirika la Bandari Zanzibar wakati akizindua Tagi mpya ya Shirika hilo MV Shuwari ikiwa ni miongoni mwa  shamrashamra za kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema bandari ni chachu ya maendeleo katika nchi yoyote Duniani na muhimili mkuu wa kuleta maendeleo na mabadiliko yatakayofanywa kwa ufanisi na juhudi kubwa zitakazoweza kuinua uchumi wa  nchi. Amefahamisha kuwa utendaji wa kazi unategemea rasilimali watu na vifaa vya kisasa vinavyo kwenda sambamba na mazingira ya kazi yatakayoleta maendeleo na mabadiliko ya haraka katika kutoa huduma za utendaji.

“Utendaji wa kazi unategemea rasilimali watu na vifaa vya kutosha na vya kisasa ambavyo vinakwenda sambamba na mazingira ya kazi ambavyo vitaleta maendeleo na mabadiliko ya haraka katika kutoa huduma za utendaji”, Alieleza Waziri Omar.

Aidha Waziri Omar ameeleza kuwa ufinyu wa nafasi ya kuhifadhia mizigo bandarini hapo, pamoja na Wafanyabiashara kutoondosha Makontena yao kwa wakati ndio changamoto kubwa zinazoikabili bandari hiyo.

Waziri Omar pia amewataka wafanyabiashara kuchukua juhudi za kutoa mizigo yao bandarini kwa wakati ili kuondosha msongamano uliopo na kulipa ushuru wa mizigo hiyo ili kuliongezea pato la Taifa. Amesema madhumuni ya Tag hiyo ni kuimarisha ufungaji na ufunguaji wa meli bandarini hapo hivyo mategemeo makubwa ni kuona kuwa inatumika ipasavyo kwa kufuata ushauri na maelekezo ya wataalamu kwa lengo la kuleta maendeleo ya bandari na taifa kwa ujumla.

Nae Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Cpt. Abdalla Juma Abdalla amesema Tagi Mv Shuwari tayari imeshaanza kazi ya kusaidia kufunga na kufungua meli gatini ambayo inauwezo wa kukabiliana na  majanga ya moto pamoja kusaidia kuokoa maisha ya watu inapotokea ajali ya meli au boti baharini.

Amesema Tagi hiyo imejengwa kwa udhamini wa kampuni ya Damen Shipyards ya Uholanzi kwa kushirikiana na Shirika la Bandari la Zanzibar na imegharimu Tsh.zaidi Bilioni 10 ambapo Bilioni 6.9 ni mkopo kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na ghrama zilizobaki zimelipwa na Shirika la Bandari.

Tag hiyo ina urefu wa mita 22.64, upana mita 7.84, kina cha kueleya mita 3.50, nguvu zake 2720 HP, mwendo 11.70 knots, nguvu za kuvuta tani 38, na uzito wa tani 140 inatarajia kuleta maendeleo makubwa bandarini hapo.

HUYU NA YULE Jumatatu ijayo....... Dr Talib Ali

$
0
0
Katika HUYU NA YULE Jumatatu ijayo tunakuletea mahojiano yetu na Dr Talib Ali

RIDHIWANI KIKWETE AAHIDI KUTATUA TATIZO LA UMEME, MAJI KIWANGWA,CHALINZE

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa ujenzi kutoka Kambi ya Mzinga ya JWTZ, Aloyce Mayunga (kushoto) alipokwenda kukagua ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Kiwangwa wakati wa ziara ya kikazi ya katika Kata ya Kiwangwa, wilayani Chalinze, Pwani leo.Aliwataka wajenzi hao kujenga maabara hayo kwa kuzingatia viwango. Katikati ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bagamoyo, Saleh Mpimbwi.
 Ridhiwani Kikwete akizungumza na wakandarasi kutoka Kambi ya Mzinga ya JWTZ wanaojenga maabara ya Shule ya Sekondari ya Kiwangwa wakati wa ziara ya kuagua miradi ya maendeleo na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge miezi sita iliyopita. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Ridhiwani akinyoosha juu kadi ya Chadema aliyokabidhiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa  Chadema Kijiji cha Masugulu ambaye amehamia CCM katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mwitemo Kata ya Kiwangwa leo
 Ridhiwani akihutubia wananchi  katika Kijiji cha Mwitemo
 Sehemu ya akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Ridhiwani Kikwete akihutubia katika Kitongoji cha Magogoni, Kijiji cha Msinune, Kata ya Kiwangwa.
 Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika Kijiji cha Msinune, Kata ya Kiwangwa.

 Msanii kiongozi wa Kikundi cha sanaa cha Chanzala akifanya maajabu yake wakati mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Ridhiwani Kikwete katika Kata ya Kiwangwa

 Mwenyekiti mpya wa Serikali ya Kijiji cha Kiwangwa, Kata ya Kiwangwa, akifungua rasmi mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete katika Kata ya Kiwangwa ambapo pamoja na kusikiliza kero zao aliwashukuru wananchi kwa kumchagua mwaka jana.

 Mkazi wa Kiwangwa Shabani Dume akiuliza swali kwa kumtaka Mbunge Ridhiwani asaidie kuwepo dampo katika Kijiji cha Kiwangwa
 Kassim Makelele wa Kata ya Kiwangwa akimuomba Mbunge Ridhiwani kununua Ambulance kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Kiwangwa
 Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Msata, Rehema Mno akielezea kwa wananchi jinsi alivyoshiriki kutatua kero za wananchi katika Kata ya Kiwangwa.,
 Ridhiwani akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Kiwangwa, Yahaya Ramadhani  wakati wa mkutano huo
 Sehemu ya umati uliohudhuria katika mkutano huo
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo ambapo aliwaambia viongozi wa Tanesco kuhakikisha wana peleka haraka umeme wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika Kijiji cha Kiwangwa
 Meneja wa Tanesco Wilaya ya Chalinze, Julius Doyi akiwaambia wananchi wa Kiwangwa kuwa umeme utaingia hapo mwezi huu.
 Meneja wa Mamlaka ya Usafi wa Maji Safi na Taka wa Chalinze,Injinia Christer Mchomba akielezea kwa wananchi mikakati mbalimbali ya kuharakisha upatikanaji wa maji katika Kata ya Kiwangwa.
 Ridhiwani akaimkabidhi Bondia Idd Pialali gloves 20 kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa ngumi katika Kata ya Kiwangwa
Ridhiwani akimkabidhi mpira mmoja wa wa manahodha wa timu mbalimbali katika Kata ya Kiwangwa  kwa ajili ya kuendeleza soka katika kata hiyo.

MAELEZO BADILISHENI MFUMO WA UTOAJI PRESS CARD

$
0
0
WASOMAJI na wadau wangu nawasalimu na naimani kuwa Mwenyezi Mungu ametujalia tumeuona mwaka mpya wa 2015 salama salmini. Nawatakia heri na fanaka katika mwaka huu pia na karibuni tena katika porojo zangu za ukweli.

IDARA ya Habari –MAELEZO ndiyo idara ya serikali inayoshughulika na kufanya kazi zake kama chombo cha usimamizi wa vyombo vya habari na waandishi wake.

Idara hiyo pia ndio msemaji wa masuala mbalimbali ya serikali lakini pia ndiyo idara yenye jukumu la kusajili au hata kuyafutia usajili magazeti hapa nchini na vyombo mbali mbali vya hjabari.

Waandishi wa habari waajiriwa na wale wa kujitegemea wameanza mchakato wa kujaza fomu kwaajili ya kupatiwa vitambulisho vipya vya kazi (PRESS CARD) kwa mwaka 2015.

Jambo hili ni zuri kwa waandishi wa habari maana kitambulisho hicho cha serikali hutolewa kwa waandishi walio na sifa za uandishi tu na sio wale waparamia fani za watu maarufu kama kanjanja.

Ndio! Uandishi wa habari ni taaluma kama taaluma nyingine, kwa hiyo kila mwanahabari anatakiwa kuwa na Press Card ambacho ndicho kitambulisho cha serikali, kama huna basi wewe sio muandishi au laa hujakomaa kuwa muandishi. SOMA ZAIDI FATHER KIDEVU BLOG

MBUNGE WA JIMBO LA MOROGOGO MJINI MH ABOOD AMWAGA MISAADA KATA YA BIGWA MOROGORO

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akijibu Hoja Mbalimbali Kuhusu kero Zinazowakabili wakazi wa Kata ya Bigwa Katika Ziara yake ya Kutembelea Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.Mh Abood Aliata nafasi ya Kuongea na wakazi wa Mitaa wa Mitaa Mbalimbali inayounda Kata ya Bigwa.Mh Abood alijibu na Kutatua Kero Mbalimbali zinazowakabili wakazi wa Kata Hiyo.Mbunge Huyo alitoa Majibu Kuhusu Kero ya Umeme, Maji ,Barabara na Nyinginezo.Pia Mh Abood alitoa Misaada Mbalimbali iliyogarimu zaidi ya Milioni 20 Katika Kata ya Bigwa.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood akiwa kwenye banda la Mama Lishe maarufu Kama Mama Ntilie Ili Kujionea na kujua  Changamoto Zinazowakabili wamama hao katika kazi yao Hiyo wakati wa Ziara yake ya Kutembelea Kata ya Bigwa Jimbo la Morogoro Mjini
Baadhi ya Misaada aliyotoa Mbunge huyo kwa Wakazi wa Kata ya Bigwa.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akikabidhi vifaa Mbalimbali kwa Vikundi vya wakina Mama wanaojihusisha na Shuguli za Mama Lishe Katika Mitaa ya Vituli, Bomela, Korogozo,Mungi, na Mgolole Iliyopo Kata ya Bigwa.
 

 Wakazi wa Kata ya Bigwa wakiwa wamemzunguka Mbunge wao

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akisikiliza Kwa Makini Kero iliyokuwa Ikiwasilishwa na Mmoja wa wakazi wa Mtaa wa Mgolole kata ya Bigwa alipotembelea Mtaa huo kusikiliza na Kutatua Kero za Wakazi wa Mtaa Huo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea kwa Msisitizo kuhusu watendaji kushugulikia Kero la wananchi wa Kata ya Bigwa kwa haraka.
Badhi ya Wakina Mama wanaojishugulisha na kazi ya Mama Lishe wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiwa Amezungukwa na Vijana wa Kata ya Bigwa wakimweleza Kuhusu kero ya Ajira Na Michezo Ambapo Mbunge Huyo alijibu Hoka Hizo kwa Kuwakabidhi Mpira wa Miguu .Kuhusu Ajira Mh Abood aliwaagiza Vijana Hao Kujiunga kwenye Vikundi vya Kufanya Shuguli za Maendeleo na yeye atawawezesha kwa Kuwapa Mitaji.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Nyumbani kwa Balozi wa CCM Mtaa wa Misongeni B Kata ya Bigwa Ndugu Omary Iddy aliyemgonjwa alipofika Kumjulia hali.


Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akiwa Nyumbani kwa Balozi wa CCM Mtaa wa Misongeni B Iliyopo Kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro Ndugu Omary Iddy aliyemgonjwa kwa Muda Mrefu Alipofika Kumpa Pole.
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Aliofika Kuhani Msiba wa Bi Nuru Binti Ally Ngozi wa Kata ya Bigwa. 


SALE YA UFUNGUZI DUKA JIPYA #AKCLASSIC MLIMANI CITY

$
0
0
TUNAPENDA KUWATAARIFU WATEJA WETU WA #AKCLASSIC SINZA-KUMEKUCHA KUWA TUMEHAMIA OPPOSITE NA TOTAL PETROL STATION  MLIMANI CITY,BARABARA YA KUELEKEA ARDHI UNIVERSITY.
SALE YA KUFA MTU INAENDELEA KWENYE DUKA LETU JIPYA!!
KARIBUNI SANA...
KUONA BIDHAA ZAIDI ZILIZO KWA SALE
INGIA
www.akclassic.blogspot.com
TUPIGIE #0753482909
KUPATA BIDHAA MPK MLANGONI!!!







WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO APATA MAPOKEZI MAKUBWA WILAYANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA. AITWA “MZEE WA NGUZO”

$
0
0

unnamed1ZKaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anna Rose Nyamubi (mbele) akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) pamoja na watendaji wake waliomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza ziara rasmi katika mkoa wa Shinyanga. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mkoa huo kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili pamoja na kuzungumza na wananchi.
unnamed2ZWaziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisalimiana na baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kishapu mara baada ya kuwasili wilayani humo. Kushoto ni Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi
unnamed3Z 
Wakazi wa Kata ya Bubiki wilayani Kishapu wakimpokea kwa shangwe Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mara alipowasili wilayani hapo huku wakiwa na mabango yaliyosomeka “ Profesa wa Kweli, Nchi sasa inang’aa vijijini, Wewe ni Jembe”.
unnamed4Z 
Mmoja wa wakinamama kutoka kata ya Igubi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga akimfunga vitambaa mkononi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kama heshima kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kusambaza umeme katika kata hiyo. Kata hiyo ni moja ya kata zinazonufaika na mradi wa umeme vijijini unaotekelezwa na REA Awamu ya Pili
unnamed5Z 
Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi (katikati) akijumuika na wakazi wa Kata ya Igumbi iliyopo wilayani Kishapu kucheza ngoma ya kumpongeza Waziri wa Nishati na Madini kwa juhudi zake za kusambaza umeme katika kata hiyo pamoja na jimbo lake.

unnamed6Z 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi (kulia) wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na REA Awamu ya Pili iliyokuwa inatolewa na Meneja Utaalamu Elekezi kutoka REA Gissima Nyamohanga (hayupo pichani)
unnamed7Z 
Mtaalamu kutoka kampuni ya kusambaza umeme vijijini ya LTL (PVT) LTD Michael Marenye (kushoto) akitoa taarifa ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika wilaya ya KIshapu. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
unnamed8Z 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu.
unnamed10Z 
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Masoud Nchambi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Wakazi wa Bubiki wilayani Kishapu wakimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi kwa kazi nzuri ya kusambaza umeme katika kata hiyo. unnamed12Z 
Sehemu ya umati wa watu kutoka Kata ya Bubiki wakishangilia hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).

CCM YALAANI VIKALI VURUGU ZILIZOFANYWA NA WAFUASI WA CHADEMA NA CUF KWA VIONGOZI WAO WA SERIKALI ZA MITAA.

$
0
0
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itakutana Zanzibar Januari 13, kwa kikao cha kawaida cha siku moja chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete. 

Kikao hicho cha Kamati Kuu kitatanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu kitakachofanyika Januari 10, jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo CCM inalaani vikali vurugu zilizofanywa na wafuasi wa Chadema na CUF kwa viongozi wetu wa serikali za mitaa katika maeneo kadhaa nchini ikiwemo mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam na Mbeya.

Vurugu hizo zilizosababisha baadhi ya viongozi wetu kujeruhiwa zimetokea katika mkoa wa Mwanza ambapo Ndugu Christopher Mgeta kutoka Mtaa wa Ibungilo na Ndugu Pascal Charles wa Mtaa wa Kitangiri A katika wilaya ya Ilemela walivamiwa na kupigwa wakati wa kuwaapisha.

Katika mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Sultan Jeta wa mtaa wa Ukwamani katika jimbo la Kawe alifanyiwa fujo na wafuasi hao na Katika Mtaa wa Msisiri A kata ya Mwananyamala katika jimbo la Kinondoni Ndugu Juma Mbena alipigwa na kuvunjwa mkono.

Katika Manispaa ya Ilala, wafuasi hao wa vyama vya upinzani walifanya vurugu wakati wa kuwaapisha viongozi hao wa serikali za mitaa wilayani humo na kusababisha zoezi hilo kuahirishwa.

Mkoani Mbeya vurugu za aina hiyo zimetokea katika wilaya za Kyela na Rungwe ambapo wilayani Kyela zoezi la kuapisha viongozi wa serikali za mitaa lilishindika na kuahirishwa kutokana na vurugu za kurushiwa mawe zilizofanywa na wafuasi wa Chadema walioletwa kutoka katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Katika kijiji cha Ilundo wilayani Rungwe wafuasi hao wa Chadema waliwapiga mawe viongozi na wanachama wa CCM na baadae kufyeka mashamba yao ya migomba na kusababisha vijana sita kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Rungwe kwa sababu ya hasira za kushindwa uchaguzi.

Vurugu hizi ni mwendelezo wa tabia na mazoea ya vyama vya upinzani nchini kutoheshimu na kufuata sheria na taratibu za nchi.  Tabia hizi si za kiungwana na ni uthibitisho wa kuharibikiwa na kufa kwa vyama vya upinzani nchini.  Mara zote wamekuwa wakikataliwa na wananchi kwa kura, wao hukataa uamuzi huo wa wananchi kwa kufanya fujo na vitimbi.  Asiye kubali kushindwa si mshindani.  Vurugu hizi sasa inatosha.

 Imetolewa na:-
  
Nape Moses Nnauye,    
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
09/01/2015

ARUSHA KUPATA MIJI MIWILI YA KISASA-NHC

$
0
0
Wawasilishaji, James Kisarika, Yusufalli Murad, Meneja Mradi Wa USA River Satellite City na Ms. Meena Pandit, Mkurugenzi , PHILS International  ambao ni Washiriki wa NHC katika katika uendelezaji wa Mradi huo.
 Pichani.
James Kisarika akisalimiana na  Katibu Tawala Mkoa, Ndugu Ado Mapunda, muda mfupi Kabla kuanza mawasilisho ya Mradi Wa Safari City.
 Yusufalli Murad, Meneja Mradi Wa USA River Satellite City akitoa mada kuhusu mradi huo .
 Baadhi ya Washiriki wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) wakifutilia mawasilisho ya miradi ya Miji Midogo ya Safari Satellite City na USA River Satellite City.
Baadhi ya Washiriki wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) wakifutilia mawasilisho ya miradi ya Miji Midogo ya Safari Satellite City na USA River Satellite City.
 Mkuu Wa Mkoa mpya wa Arusha akifungua kikao cha RCC kabla ya Mawasilisho.

Arusha to get 2 new towns: NHC

The National Housing Corporation (NHC) plans to construct two satellite towns on the outskirts of Arusha, the Regional Consultative Committee (RCC) meeting was told here on Wednesday. The NHC regional manager for Arusha, Mr James Kisarika, named the sites as Usa River Satellite City to be put up on the southern fringes of the city and Safari Satellite City to be built at Mateves.
Mr Kisarika said the ambitious projects were in line with the vision of the oldest state-owned real estate corporation to address market needs for world class settlements.
“Arusha does not benefit much from tourism, as much of the receipts accrued from the hospitality industry go to hotels in Karatu township and national parks,” he observed.
Mr Kisarika said while the Usa River Satellite City targeted the tourism industry, the Safari one was meant for de-congesting the Arusha Central Business District (CBD).
Phils International, a firm manned by Tanzanians living in Dubai, which built Dubai Sports City, will construct the Usa River Satellite City at a 1.17-million-square-metre block situated a stone’s throw from Dolly Estate near Kilimanjaro International Airport. “One can reside at the Usa River Satellite City and work in Moshi Municipality or Arusha City,” Phils International director of Projects Murad Yusufali told the RCC.
He said the design of the city would enable each of the 19,000 dwellers in four petals of the residential segment to view both mounts Meru and Kilimanjaro from their living rooms.
“The city will tap underground water and use solar for street lights,” said Mr Yusfali, adding that a US firm would construct a sewerage system which would recycle sewage for irrigation usage.
He said the Lands, Housing, and Human Settlement Development ministry had approved a master plan for the project ready for the construction work to begin. CHANZO THE CITIZEN TANZANIA
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images