Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 436 | 437 | (Page 438) | 439 | 440 | .... | 1897 | newer

  0 0

  unnamed6SPicha ya pamoja ya kumbukumbu na wakuu wa Ulinzi na usalama.unnamed7SPicha ya pamoja ya kumbukumbu na wanafamilia wa Bw. George.unnamed9SPicha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wenzake.unnamed10SPicha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi Tume ya Sheria.

  0 0


  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akifungua kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   Vijana wadogo kutoka katika kituo cha Nyerere Shaolin Group wakionyesha umahiri wa kuweza kupambana na uhalifu katika sherehe za Uwekaji wa jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

   -Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar akitoa maelezo kuhusiana na Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   Katibu Mkuu Wizara ya mambo yandani Mbaraka Abdullwakili akitoa hotuba na kumkaribisha mgeni rasmi katika Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   Naibu Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akitoa hotuba katika Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.kushoto yake ni Katibu Mkuu Wizara ya mambo yandani Mbaraka Abdullwakili na kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar.
   Naibu Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akimkabidhi Mwalimu Khamis Omar ambae ni mkufunzi wa Vijana wa Nyerere Shaolin Group jumla ya shi,Laki Mbili ikiwa ni mchango wake kwa vijana hao waweze kutatua matatizo yao.
  Naibu Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Haji Mwadini Makame katikati akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Jeshi la Polisi katika Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Na ABDALLA ALI- MAELEZO ZANZIBAR

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein amesema ni jukumu la serikali kuwapelekea maendeleo wananchi katika kutoa huduma za kijamii, kisiasa na kiuchumi katika kuleta mabadiliko nchini.

  Hayo ameyasema huko Umbuji Wilaya ya Kati Unguja katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya njia nne ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Zanzibar.

  Alisema serikali inawajibu wa kuwatumikia wananchi wake kwa kuwawekea mazingira mazuri ya miundombinu ya barabara, afya na elimu kwa lengo la kuleta maendeleo na mabadiliko nchini.

  “Tuna jukumu la kuwatumikia wananchi katika  kuwawekea mazingira mazuri ya kijamii, kiuchumi na kisiasa na leo hii wanakijiji cha Umbuji mnafurahia ufunguzi wa barabara ya njianne iliyo nzuri na lainii kama mgongo wa ngisi kwa lengo la kuletea maendeleo na mabadiliko nchini”, alieleza Dr. Shein.

  Dr. Shein amesema wanakijiji hao wataepukana na shida ya muda mrefu waliyokuwanayo  na kupata usafiri wa uhakika wa kusafirisha bidhaa na mazao yao kwa lengo la kujikwamua kimaisha.

  Dr. Shein amewataka wananchi wa Umbuji kuitumia vyema barabara hiyo na kutofanya shughuli za kilimo wala kujenga pembezoni mwa barabara kwa lengo la kuepukana na hasara baadae.

  Hata hivyo aliwataka madereva kutoendesha gari kwa mwendo wa kasi pamoja na kutozidisha kiwango cha tani kilichowekwa na wataalamu wa barabara ili kuepukana na ajali za mara kwa mara.

  Rais aliwapongeza wananchi wa kijiji hicho kwa kujali maendeleo zaidi ya kijiji chao kwa kutodai fidia ya mali zao kwa lengo la kupata maendeleo ya kijiji chao na kuwataka wananchi wengine kuiga mfano huo ili kuleta maendeleo nchini.

  Akitoa maelezo mafupi Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dr. Juma Malik Akili amesema barabara hiyo imejengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara Zanzibar.

  Nao wanakijiji wa Umbuji waakisoma risala yao wamesema barabara hiyo itakua kichocheo kwa vijana kupata ajira na kufanikiwa kibiashara ikiwemo kilimo na utalii.

  Barabara hiyo ina urefu wa kilomita 5.1, upana mita 6 na yenye uwezo wa kuchukua tani 15 ambayo imegharimu zaidi ya shilingi milioni 800 za kitanzania.

  0 0

   Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Tamasha la Biashara litakalofunguliwa tarehe 7mwezi huu katika  viwanja vya maisara. (kushoto) Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Bi. Thuwaiba Edington Kisasi na (kulia) Mkurugenzi Idara ya Biashara na Ukuzaji Biashara Mohamed Jaffar Jumanne.(Picha na Makame-Mshenga Maelezo Zanziba).
   Mwandishi wa Habari wa ITV  Farouk Karim akiuliza swali katika mkutano wa waandishi wa Habari ulioitishwa na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko kuhusu Tamasha la Biashara litalofanyika kuanzia tarehe  7 hadi 13 mwezi huu katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
  Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbali wakimsikiliza Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Wizara ya Biashara Malindi Zanzibar. (Picha na Makame-Mshenga Maelezo Zanziba).


  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya  umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo wilayani Busega Bw.  Steve Thomson (kushoto)
   Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na  wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega (hawapo pichani)
   Mkazi wa kata ya Ijitu  iliyopo wilayani Busega ambaye  jina lake  halikupatikana mara moja akitoa hoja yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto  waliosimama mbele) mara Waziri alipofanya ziara katika kijiji hicho na kusikiliza kero za wananchi
  Diwani wa Kata  ya  Ijitu iliyopo wilayani Busega Vumi Magoti  akielezea kero za umeme katika kata yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto), viongozi na wananchi  (hawapo pichani).
   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka  Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika  Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara  katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi  ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisaini kitabu  cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega kabla ya kuanza  ziara  katika wilaya hiyo ili kujionea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini  pamoja na kuzungumza na wananchi.
   Mkazi wa kijiji cha  Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu   ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali  mbele ya  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi  (hawapo pichani) mara Waziri alipofanya  mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho ili kusikiliza kero zao.
   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo  kwenye mkutano  na  wananchi wa  kata ya  Ijitu iliyopo wilayani Busega
   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma ( wa mwisho kushoto)  ya kuitaka  Tanesco kuongeza kasi ya  usambazaji wa umeme  vijijini.
   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo   katika mkutano wake na wananchi wa kijiji cha  Bushigwamala  wilayani Busega (hawapo pichani)
   Sehemu ya umati wa wananchi wa kata ya Kalemala wilayani Busega waliojitokeza kwenye mkutano na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakifuatilia kwa makini hotuba yake.


  0 0

   Jengo la Skuli ya Secondary ya  Faraja lililofunguliwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi Kwamtipura Mjini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akikunjuwa Kitambaa ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa Skuli ya Secondary ya Faraja Kwamtipura Mjini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   -Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitembelea maeneo mbali mbali ya Skuli ya Secondary ya Faraja Kwamtipura Mjini Zanzibar baada ya kuifungua rasmi ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi kushoto akisalimiana na Muwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan katika ufunguzi wa Skuli ya Secondary ya Faraja Kwamtipura Mjini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   -Baadhi ya Walimu na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Ufunguzi wa Skuli ya Secondary ya Faraja Kwamtipura Mjini Zanzibar  ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   -Wanafunzi wa Madrasa ya Kamaria wakileta burudani ya Kasida katika ufunguzi wa Skuli ya Secondary ya Faraja Kwamtipura Mjini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna akitoa maelezo kuhusiana na Skuli ya Secondary ya Faraja iliofunguliwa na  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi Kwamtipura Mjini Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0


  KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania (Trafic), Mohamed Mpinga (pichani), ametoa onyo kwa  baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi na kuthibitika kama zina ukweli ndani yake.

  Kamanda Mpinga, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la baadhi ya mitando kusambaza taarifa kuwa kulikuwa na basi la Kampuni ya Dar Express limepata ajali.

  Alisema, onyo hilo linatokana na kitendo cha baadhi ya mitandao hiyo, jana kusambaza taarifa kuwa kulitokea ajali iliyohusisha gari namba T 640 AXL, huku ikishindwa kutoa ufafanuzi ilikotokea jambo ambalo limezua taharuki kwa abiria wanaotumia mabasi ya kampuni hiyo.

  Mitandao iliyohusika katika kusambaza picha za ajali hiyo ya uzushi ni Bongo Mzuka, Whatsapp, Facebook na Jamii Forum. 

  “Baada ya picha ya basi hilo kusambazwa katika mitandao hii nilipigiwa simu na baadhi ya watu wakitaka kujua kama ni kweli kulikuwa na ajali kama hiyo, iliwaweze kujua majaliwa ya ndugu zao walio kuwa safarini wakitumia mabasi ya kampuni hiyo,”alisema Mpinga.

  Mpinga, aliwatoa hofu wananchi kuwa hakuna ajali yeyote iliyotokea ambayo ilihusisha basi la kampuni hiyo katika siku za hivi karibuni na kwamba gari lililooneshwa katika mitandao ni la uongo kwa vile haliko barabarani. 

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Dar Express,Yudika Mremi
  “Niwashauri wamiliki hawa kuwa wajaribu kuwa makini na waitumie mitandao kwa ajili ya manufaa yao na watu wengune lakini si kwa matumizi kama haya ambayo yanaweza kuwaletea wengine madhara katika maisha yao na ieleweke watu wa aina hiyo wakipatikana watafikishwa katika vyombo vya sheria,”alisema.


  Nae Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dar Express, Yudika Mremi 
  alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi wa ajali hiyo, alisema hata yeye alishtushwa na taarifa hizo, kwa vile gari lililooneshwa katika mitandao hiyo lilipata ajali miaka mitano iliyopita pia haliko tena barabarani tangu kipindi hicho.

  Alisema baada ya kuona picha hizo alichofanya alikwenda Kituo cha Polisi Kinondoni, kufungua jalada kwa ajili ya polisi kufanya uchunguzi ambao utasaidia kujua nia ya watu waliotoa taarifa hiyo ya uongo.

  0 0

  Na Maryam Kidiko/Kijakazi Abdalla Maelezo Zanzibar                  

  Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilali amesema kuwa matumizi bora ya teknolojia ya habari yatawawezesha wanafunzi kupata elimu bora kwa urahisi.

  Hayo ameyasema leo  katika skuli ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja wakati  wa uzinduzi wa darasa la kompyuta  ikiwa ni  miongoni mwa shamrashamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi  ya Zanzibar.

  Alisema kuwa matumizi bora ya kompyuta yatawafanya wanafunzi kuimarika vizuri kielimu wakati dunia  hivi sasa imo katika mfumo  wa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ya habari.

  Alisema kuwa teknolojia ya habari imekuwa kwa kiwango kikubwa jambo ambalo limekuwa likichangia ukuaji wa uchumi katika  Taifa.Amewashauri wanafunzi kutumia maendeleo ya teknolojia hiyo  kwa mambo yanayoweza kuwasaidia katika maendeleo ya masomo yao na maisha ya baadae.
  .
  “Vijana itumieni  teknolojia hii  katika njia zilizosahihi   ili iweze kuwaletea  faida” alisema Dkt. Bilali. Amewataka wanafunzi  waongeze bidii  zaidi ili  waweza kumudu masomo hayo na kuleta maendeleo  katika jamii na nchi kwa ujumla .

  Alisema kuwa matumizi ya komputa yanarahisisha kufundisha wanafunzi kwa njia rahisi na kuweza kujifunza mambo mbalimbali kupitia teknolojia hiyo na kupelekea kutanuka  kiakili.

  Aidha Dkt. Bilali ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa china kupitia kampuni ya ZTE kwa msaada wa kompyuta 50  na kuhakikisha kuwa teknolojia hiyo inaenea kwa kiasi kikubwa.   Dkt. Bilali amesema msaada huo utaweza kuleta changamoto zaidi kwa wanafunzi na  kuwa  na wataalamu wengi waliobora kwa  maendeleo ya taifa

  Amesema  kuwa Serikali inathamini sana michango inayotolewa na marafiki wa maendeleo na Serikali itahakikisha michango hiyo inakuwa na faida kubwa kwa Taifa. Katika risala  yao walimu wa skuli ya Kiembesamaki  wameiomba Serikali kuwawekea Uzio katika Eneo la skuli pamoja na usafiri kwa walimu na Wanafunzi.

  Skuli  ya Kiembesamaki  Sekondari inajumla ya Wanafunzi 1,800 kwa sasa na katika sherehe za uzinduzi huo Dkt. Bilal amechangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya maendeleo ya skuli hiyo.

  IMETOLEWA NA IDARA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

  DSC_0300

  Mratibu wa kituo cha TFGM na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mtakatifu Catherine Laboure ya Kijiji cha Masanga kilichopo wilayani Tarime mkoani Mara, Thomas Maruga akiwatembeza maeneo mbalimbali ya shule hiyo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem (kushoto) wakati wa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji (Waiseke wa Kisasa).(Picha za Zainul Mzige wa MOblog).

  Na Mwandishi wetu, Tarime-Mara
  SERIKALI imeombwa kuhakikisha inakomesha ubabe unaotumika kukeketa mabinti wa koo za Kikuria nchini.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga, Tarime Sista Germaine Baibika akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji. Alisema jumla ya mabinti 634 wamehitimu mafunzo ya miezi miwili yanayogusa haki za binadamu, haki zao, masuala ya afya na kuzitambua na kuezinzi mila nzuri.
  Aidha wamejifunza kazi za sanaa na usanii.

  Alisema adha kubwa wanayokumbana nayo mabinti hao waliotoka katika kituo hicho ni kukamatwa kwa nguvu na kupitishwa kisu cha Ngariba bila wao wenyewe kuafiki kwa dai la kuendeleza mila. “Hii sio mila” anasema sista Germaine na kuongeza kuwa hakuna mila inayotengenezwa kunyanyasa watu wengine au kulazimisha mambo yasiyofaa katika jamii, mila hiyo ikiwepo lazima ipigwe vita.
  DSC_0480
  Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudentia Kabaka (wa pili kushoto) akiwasili kwenye mahafali hayo pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem.

  Alisema serikali isiache kuwatetea mabinti hao kwa dai la kuwa hiyo ni mila kwa kuwa wanaofanyiwa vitendo hivyo hulazimishwa na haifanyiki kwa ridhaa yao. Alisema wapo mabinti walioletwa na wazazi wao kuepushwa na janga hilo, wapo waliotoroka kwa wazazi wao na wapo walioletwa katika kituo hicho na polisi kutoka makwao.

  Mafunzo hayo ya mwezi mmoja yamelenga kukabiliana na msimu wa ukeketaji ambao sisita huyo alisema mwaka jana ulianza mapema Novemba na unaendelea hadi mwaka huu wakati kimila mwaka huu si wa ukeketaji. Kwa mujibu wa mila za Kikuria ukeketaji hufanyika katika mwaka unaogawanyika, mwaka 2015 haugawanyiki.
  DSC_0492
  Mhashamu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mkoani Mara, Michael Msongazila akiwasili kwenye sherehe za mahafali ya sita ya kituo cha kupambana na ukeketaji Masanga wilayani Tarime mkoani Mara.

  Mafunzo hayo ambayo yamelenga kuwatoa mabinti wa kisasa wenye mwelekeo wa maisha yenye hali bora mabinti wanaofika hapo huwa hawataki kukeketwa na ndio maana mwaka huu walipata tatizo la binti mmoja kuzimia wakati alipomuona baba yake katika maeneo ya kituo hicho.

  Alisema wapo wazazi wakorofi wanaokuja kudai watoto wao lakini pia ipo jamii korofi inayotumia ubabe baada ya wasichana hao kutoka hapo wanakeketwa kwa lazima. Katika hafla hiyo iliyoendeshwa na masista wa shirika la Daughters of Charity of St. Vincent De Paul, Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka aliwapongeza wasichana hao na kuwataka kuwa mfano katika jamii na kutekeleza wajibu wao. Alisema wamekuwa mabinti wa kisasa kwa kukataa ukeketaji na hivyo wao wanastahili kuwa walimu kwa wenzao.

  DSC_0433
  Maandamano ya wanafunzi wa Shule ya Mtakatifu Catherine Laboure iliyopo kijiji cha Masanga wilayani Tarime, mkoani Mara wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali za kukemea ukeketeji wakisindikiza dada zao wahitimu wa kituo cha FGMT katika sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti (Waiseke wa kisasa) waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji yaliyofanyika mwanzoni mwa wiki.

  Aidha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amewataka mabinti hao kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii na kuwa chanzo cha kubadili kizazi kijacho.
  Alisema wamesimama madhubuti kupinga mila potofu na uonevu na kusema kwa kitendo chao wamewafanya wengine kuwaiga na kubadilika.

  Alisema ukeketaji ni mila potofu na kusema kwa msaada wa shirika la Umoja wa mataifa la Mpango wa familia (UNFPA) na taasisi nyingine zinazopambana na ukeketaji kwa kipindi cha miaka saba wamefanikiwa kuwoakoa wasichana 2001 wasikeketwe.
  Aidha mabinti hao wameokolewa dhidi ya ndoa za utotoni, ujauzito wa mapema na kushindwa kuendelea na masomo.
  DSC_0425
  Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem amesema ni vyema mapambano dhidi ya ukeketaji yakaendelea kwa kuwa wanaoshabikia ni viongozi wa kimila na ngumu kuiondoa ila kwa juhudi za jamii yenyewe.

  Katika sherehe hizo ambapo pia askofu wa Musoma alikuwepo na viongozi wengine wa kiserikali pia Ngariba walioacha kazi hiyo walikuwepo kuelezea ubaya wa mila hiyo.
  Suala la ukeketaji ni kitu cha kawaida katika mikoa ya Manyara 71%, Dodoma 64%, Arusha 57%, Singida 51% na Mara 40%.

  Viongozi waliopata muda wa kuzungumza walisema kwamba ukeketaji unatakiwa kukomeshwa mara moja kwani ni tatizo si tu kwa jamii bali kwa wale ambao wanafanyiwa kisaikolojia na kitabibu.
  DSC_0439
  Wahitimu mabinti 37 waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji wa kituo cha TFGM cha kijiji cha Masanga wakiwasili na maandamano kwenye sherehe za mahafali ya sita ya kituo hicho.

  Moja ya kazi inayoifanywa na kituo cha Masanga ni ushauri wa kisaikolojia kutokana na wasichana wengi kufika hapo wakiwa na matatizo makubwa ya magonjwa na hasa msongo wa mawazo. Katika risala yao mabinti hao wameitaka serikali kufanyakazi yake kukabiliana na ubabe unaofanywa na viongozi wa kimila wa kuwalazimisha kukeketwa hata msimu unapokuwa umepita.

  Mabinti hao ambao wengi wametoka shule ya msingi na sekondari wameweza kuwekwa hapo kwa msaada wa UNFPA ambao wametoa hela kupitia Children’s Dignity Fund (CDF), .Wafadhili wengine ni Daughters of Charity of St. Vincent Du Paul, na Askofu wa kanisa katoliki dayosisi ya Musoma, Michael Msongazila
  DSC_0495
  Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akisalimiana na Mhashamu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mkoani Mara, Michael Msongazila mara baada ya kuwasili kwenye mahafali hayo.
  DSC_0504
  Kwaya ya vijana ya mara ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa sherehe za mahafali ya sita ya kituo cha kupambana na ukeketaji Masanga wilayani Tarime mkoani Mara.
  DSC_0547
  Mgeni rasmi Mh. Kabaka, Bw. Alvaro Rodriguez na SSP. Simon Mrashani wakishiriki kucheza wimbo maalum unaohamasisha kukataza vitendo vya uovu vya Ukeketaji kwa watoto wa kike wakati wa mahafali hayo.
  DSC_0499
  Meza kuu ikitoa heshima kwa wimbo wa taifa.
  DSC_0555
  Mkurugenzi wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga (TFGM), Tarime, mkoani Mara, Sista Germaine Baibika akimkaribisha mgeni rasmi pamoja wageni waalikwa kwenye sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
  DSC_0541
  Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akifurahi jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye sherehe za mahafali hayo.
  DSC_0617
  Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akizungumza kwenye sherehe za mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
  DSC_0585
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika sherehe za mahafali sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
  DSC_0630
  Mkuu wa Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, Bw. John Henjewele akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara katika mahafali ya sita ya kituo cha kupambana na ukeketaji cha kijiji cha Masanga (TFGM) cha wilayani Tarime, mkoani Mara.
  DSC_0557
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem, akizungumza kwenye sherehe hizo.
  DSC_0702
  Kaimu kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Tarime na Rorya SSP. Simon Mrashani akieleza jinsi jeshi la polisi linavyoshiriki katika kupambana na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia likiwemo suala la kesi za ukeketaji ambapo pia alitoa takwimu za kesi zilizoripotiwa kituoni mpaka sasa ni 141, huku 80 zikiwa Mahakamani na 20 zimetolewa hukumu.
  DSC_0552
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akifurahi jambo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa sherehe za mahafali hayo.
  DSC_0599
  Wahitimu 37 wakila kiapo cha kutokubali kutoshiriki kukeketwa na kuwa mabalozi wazuri kwenye jamii zao katika kuelemisha madhara ya ukeketaji kwa wanaoendeleza mila na tamaduni hizo pindi warudipo majumbani. Kwa picha zaidi ingia humu

  0 0

  VIJANA wa mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kusimama imara na kudai fursa mbalimbali zikiwamo za kupewa kipaumbele katika ajira zinazotokana na mlima Kilimanjaro.

  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini na Naibu Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Moshi Vijijini, Innocent Melleck alipokuwa akizungumza na waandishi wahabari juu ya mkakati wa kupambana na wimbi la vijana walio mitaani kwa kukosa ajira katika mkoa wa Kilimanjaro .
    Melleck alisema anatarajia kuitisha mkutano maalum kwa ajili ya kuwakutanisha vijana kujadili namna watakavyoweza kufaidika na fursa zitokanazo na mlima Kilimanjaro hususani katika sekta ya utalii.

  Tunatarajia mwishoni mwa mwezi huu kukutanisha vinjana wote wanajishugulisha na shuguli za kupandisha watalii mlimani wakiwepo wabeba mizigo,wapishi na wasimamizi wao ambao ni wazawa ili kuweza kujadili njia sahihi ya kufuata kuweza kushinikiza uongozi wa KINAPA kutoa nafasi kwa vijana wazawa.


  Alisema pindi mlima huo ukiwaka moto vyombo vya usalama kutumika kuwakamata wazawa kwenda kuzima moto huo tena kwa kutumia nguvu wakati katika swala la ajira rasmi na zisizo rasmi wazawa wameonekana sii lolote kitu na nafasi kuwewa wageni.

  Aliongeza ajira katika mlima Kilimanjaro imeendelea kunuka rushwa na ubaguzi mkubwa jambo ambalo linahita mshikamano wa pamoja kwaaji ya ukombozi wa kizazi cha wazawa wa mkowa wa Kilimanjaro,Aliongeza mkoani Arusha katika mlima meru hakuna mtu ambae sii mmeru anayeweza kupandisha watalii katika mlima huo Zaidi ya wameru jambo ambalo ni kinyume mkoani kilimanjaro

  "Lazima vijana wetu wafaidike na fursa hizi za kupata ajira badala ya watu kutoka mikoa mingine kuchukua nafasi hizo na wao kubaki kama watazamaji," Kada huyo wa CCM ambaye ametangaza kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo mwaka huu, alisema unapotokea moto katika mlima huo, vijana ndiyo wanaojitokeza kuuzima hivyo lazima wafaidike nao moja kwa moja.

  Alisisitiza kuwa ajira kwa vijana itakuwa ajenga yake namba moja na atahakikisha analipigania hilo kwa nguvu zake zote. "Mlima Kilimanjaro peke yake ukitumiwa vizuri unatosha kutoa ajira za uhakika kwa vijana wetu wa mkoa wa Kilimanjaro hususani jimbo la Vunjo wilaya ya Moshi vijijini ambao kwa sasa hawana ajira," alisisitiza Melleck

  Kuhusu uchaguzi mkuu ujao, Melleck alisema amejipanga kulikomboa jimbo la Vunjo ambalo kwa sasa linashikiliwa na Augustino Mrema kupitia Chama cha Tanzania Labour Party (TLP).

  0 0
 • 01/06/15--21:22: Taarifa ya HITMA
 • Familia ya Sakapala inapenda kuwataarifu kwamba kutakuwa na HITMA ya Marehemu Jamila Simba itakayofanyika January 17 2015 (Jumamosi) Kuanzia saa 8 mchana (Tafadhali zingatia muda) Ukipata taarifa hii naomba umtaarifu na mwingine.
  Anwani ya itakapofanyika ni..;
  Wheaton Claridge Local Park
  11901 Claridge Road, Silver Spring
  Maryland - 20902
  Kwa maelekezo zaidi wasiliana na... Zawadi Sakapala (301 379 2342)
  Simba Abdoul (202 758 7805)

  0 0
 • 01/07/15--03:26: DALA DALA LAIVU.
 • Zaidi zinapatikana humu kila siku; https://www.facebook.com/pages/Daladala-Laivu/1539495843003489    Vunja mbavu, tupa stresi kule!


  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi mjini Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, Pwani jana, ambapo pamoja na kuwashukuru kwa kumchagua, pia alisema atatumia unasheria wake kuwasaidia baadhi ya wakazi wa jimbo hilo wanaonyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuporwa ardhi.
   Mkazi wa Chalinze, Bibi akitoa malalamiko yake mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete ya kudhulumiwa shamba lake na watu wasiojulikana.
   Mkazi wa Chalinze Methodius Kaijage, akiuliza swali kuhusu alama za x zilizowekwa kwenye nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa barabara ambazo alidai ni takribani miaka kumi imepita bila kupewa fidia hivyo kusababisha kukosa maendeleo.
   Sehemu ya wakazi wa Kata ya Bwilingu, wakiwa katika mkutano na mbunge wao mjini Chalinze.
   Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kitongoji cha Chalinze Mzee wakati wa ziara ya kuwashukuru wananchi na kusikiliza kero zao
   Ridhiwani akimsalimia mmoja wa wazee wa Kitongozi cha Chalinze Mzee
   Mmoja wa vijana wa Chalinze Mzee akiuliza swali
   Mzee Ibrahim Koga akielezea mbele ya Mbunge asivyotendewa haki na Baraza la Kata ya Bwilingu la kuporwa ardhi yake
  Mama mwenye Jamii ya Kimasai Rehema Lazaro akilalamika mbele ya mbunge kitendo cha baadhi ya wananchi kutoa lawama kwa wafugaji wote badala ya wafugaji wanaofanya vurugu kwa kupeleka mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kuchafua visima vya maji.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

  0 0

  Wananchi na viongozi wa manispaa ya Iringa wametakiwa kujitolea katika
  maswala mbalimbali yahusuyo jamii kwa kuwajibika ipasavyo hasa katika
  swala la kufanya usafi katika mazingira yanayotuzunguka.

  Akizungumza na nuru fm  mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa FRANK
  KIBIKI amesema kuwa ameamua kufanya usafi katika maeno mbalimbali ya
  manispaa ya iringa kwa kuwa kikundi chao kimejitolea kufanya kazi hiyo
  pamoja na kujitambulisha kwa uongozi wa halmashauri ya manispaa.

  KIBIKI ameongeza kuwa kiongozi lazima uwe mfano kwa jamii husika
  katika kuleta maendeleo mbalimbali hasa kuwajengea vijana uwezo wa
  kujitambua na kupenda kujifunza na kuijijali wao wenyewe hasa swala la
  usafi.

  KIBIKI ameongeza kwa kusema kuwa kila mtu anayeishi duniani anaweza
  kuzibzdili changamoto kuwa fursa ambazo zitakuwa na faida kubwa kwa
  jamii husika lakini akasema kuwa sio kiasi gani cha fedha
  alizizoziacha dunia buli ni familia gani ya familia aliyoiacha
  duniani.

  aidha KIBIKI amewata wananchi wa manispaa  kuwafundisha vijina jinsi
  gani ya kufanya usafi hivyo watakuwa wamechangia kuioka jamii katika
  swala afya kwa kuwa wananchi wote watakuwa wanajua umuhimu wa wa
  kutunza mazingira.

  KIBIKI amemalizia kwa kuwataka wananchi kuwa wasafi na kuwaridhisha
  vijana kujua na kujifunza juu ya kufanya usafi hivyo usafi ukianzia
  nyumbani  basi hata mitaa yetu itakuwa misafi na tutakuwa
  tumewatengezeza viongozi wazuri.

  0 0

   -Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,Mohd Gharib Bilal akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kompyuta cha Skuli ya Secondary ya Kiembe Samaki mjini Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,Mohd Gharib Bilal akitoa hotuba katika ufunguzi wa Kituo cha Kompyuta cha Skuli ya Secondary ya Kiembe Samaki mjini Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.kulia yake ni Balozi mdogo wa china alieko Zanzibar Mr.Xie Yunliang na kushoto yake ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna.PICHA NA YUSSUF SIMAI.MAELEZO ZANZIBAR.

   Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,Mohd Gharib Bilal akipata maelezo kuhusiana na Compyuta kwa Balozi mdogo wa china alieko Zanzibar Mr.Xie Yunliang katika ufunguzi wa Kituo cha Kompyuta cha Skuli ya Secondary ya Kiembe Samaki mjini Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,Mohd Gharib Bilali kushoto akisalimiana na Balozi mdogo wa China alieko Zanzibar Mr.Xie Yunliang katika ufunguzi wa Kituo cha Kompyuta cha Skuli ya Secondary ya Kiembe Samaki mjini Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   Baadhi ya Walimu na Wanafunzi waliohudhuria katika sherehe ya ufunguzi wa Kituo cha Kompyuta cha Skuli ya Secondary ya Kiembe Samaki mjini Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  0 0

   Naibu Waziri wa Fedha,Mwigulu Mchemba leo ameadhimisha miaka 40 tangu kuzaliwa kwake. Katika maadhimisho hayo Naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi ameitumia siku hiyo ya leo kwa kutembelea wagonjwa katika wodi ya Wazazi ya Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam, kuchangia damu pamoja na kuwatembelea na kuwapa zawadi yatima katika kituo cha CHAKUWAMA.
   Mwigulu akiwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala.
   Mwigulu Mchemba akiangalia mmoja wa watoto waliozaliwa siku ya leo.
   Mwigulu Mchemba akitoa misaada ya vitu mbalimbali katika kituo cha yatima CHAKUWAMA.
  Naibu Waziri Mwigulu Mchemba akichangia damu katika benki ya damu Salama.
  Akipiga picha ya pamoja na watumishi wa Benki ya Damu Salama.  wananchi wa jimbo la Iramba Magharibu, Familia yake na watanzania wote kwa ujumlawanamtakia heri na fanaka katika maisha yake na Mungu amjalie Hekima na Busara.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita aliyelazwa akipata matibabu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaaam jana.Brigedia Jenerali Hashim Mbita ni mwanasiasa mkongwe ambaye aliwahi kuwa  mmoja wa viongozi waandamizi katika harakati za ukombozi Barani Afrika(picha na Freddy Maro) unnamed1N 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita aliyelazwa akipata matibabu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaaam jana.Brigedia Jenerali Hashim Mbita ni mwanasiasa mkongwe ambaye aliwahi kuwa  mmoja wa viongozi waandamizi katika harakati za ukombozi Barani Afrika(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF.  Prof, Ibrahim Lipumba   alipokuwa akiwashukuru wananchi wa Buguruni Dar es Salaam jana kwa  kupiga kura na kukipa ushindi  mkubwa na imani walio ionyesha kwa wagombea wa chama hicho kuwezesha kunyakuwa mita 5 na Chama cha Mapinduzi CCM kunyakuwa mta 1, nakuwaomba wananchi wazidi kuwa na imani na cha hicho.(PICHA NA KHAMISI MUSSA) JAMBO LEO
   Mjumbe wa Chama cha Wananchi CUF.  na Kiongozi wa Sanaa Mshikamano cha Temeke Shamte Mpendaraha  alipokuwa akisoma risala kabla ya mgeni Rasmi kuongea
   Wanachana wa chama cha wananchi CUF  pamoja na wanachi wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Chama hicho Prof Ibrahim Lipumba

   Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Prof  Ibrahim Lipumba akiwahutubia maelfu ya wananchi  waliojitokeza  kumsikiliza alipokuwa akiwashukuru wananchi wa Buguruni kwa kukiwzesha chama hicho ushindi katika chaguzi za Serekali za Mita zilizofanyika hivi karibuni nakuzidi kuwaomba wananchi wajitokeze kujiandikisha katika Daftari la wapigakura. 
   Wanachama wa chama hicho wakiwa katika utulivu mkuwa wakimsikiliza Mwenyekiti wao Pro. Ibrahim Lipumba  alipokuwa akiwashukuru wananchi hao eneo la Buguruni Shell Dar es salaa jana.
   Mwanacha wa Chama hicho cha CUF, akiwa amevalia kofia ya chama hicho.
    Wanachama wa chama hicho wakiwa katika utulivu mkuwa wakimsikiliza Mwenyekiti wao Pro. Ibrahim Lipumba  alipokuwa akiwashukuru wananchi hao eneo la Buguruni Shell Dar es salaa jana
   Wanachama wakicheza ngoma baada ya kwisha kwa Mkutano
   Baadhi ya Wenyeviti wa Chama cha Wananchi CUF ,walio fanikiwa kuchaguliwa katika chaguzi za Serelali za Mita kupitia chama hicho .
    Wanachama wa chama hicho wakiwa katika utulivu mkubwa wakimsikiliza Mwenyekiti wao Pro. Ibrahim Lipumba  alipokuwa akiwashukuru wananchi hao eneo la Buguruni Shell Dar es salaa jana
  ( Watoto CUF),  ni watoto 200 wanao lelewa na Chama cha Wananchi  cuf  kwa kufundishwa maadili ua Uongozi na Miiko ya Uongozi na mambo ya Rushwa, ambao wanaoandaliwa hapo baadaye wawe Viongozi bora watakao kitumikia chama hicho na wazazi wanaombwa kupeleka watoto wakapate maadili.

  Prof. akiongea na wananchi pamoja na wanachama wa Chama hicho Buguruni Shell jijini Dar es Salaam jana

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Fukayosi, Kata ya Fukayosi, wakati wa ziara ya kikazi pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge miezi  sita iliyopita.Ridhiwani kutoruhusu hata kipande cha heka moja kuporwa na matapeli katika jimbo lake la Chalinze.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Kijana Salumu Khamis akiuliza swali mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete kuhusu tatizo la maji katika Kijiji cha Fukayosi
   Mkuu wa Miradi wa Mkoa wa Pwani wa Tanesco, Leo Mwakatobe, akielezea jinsi umeme utakavyosambazwa katika Kijiji cha Fukayosi na vijiji vingine Jimbo la Chalinze.
   Mwenyekiti mpya wa Serikali ya Kijiji cha Fukayosi, Salum Mkwecha akimshukuru mbunge kwa ahadi mbalimbali alizozitoa katika miradi mbalimbali katika kijiji hicho.
   Ridhiwani akibadilishana mawazo na mmoja wa watawa baada ya kumalizika kwa mkutano katika Kijiji cha Fukayosi Jimbo la Chalinze.
   Mwenyekiti mstaafu wa Kata ya Fukayosi,Adam Masoud  akimuomba Mbunge Ridhiwani kuhikisha anaweka miundombinu ya barabara na maji na masuala ya afya katika Kijiji cha Mkenge,wakati wa ziara yake katika Kata ya Fukayosi ya kuwashukuru kwa kumchagua pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuangalia jinsi ya kuzitafutia ufumbuzi.

   Mkazi wa Kijiji cha Mkenge, Khamis Mwanga akielezea kero ya barabara ya Mwavi hadi Mkenge ambayo alidai inarudisha nyuma maendeleo ya kijiji hicho hivyo kumtaka Ridhiwani awasaidia kuijenge barabara hiyo ili iweze kupitika bila matatizo katika vipindi vyote. Ridhiwani aliwajibu kuwa tayari barabara hiyo imepata mkandarasi anayetarajia kuanza kazi katika siku chache zijazo.
   Katibu wa CCM Tawi la Mkenge, Omar Seleman akimuomba Mbge Ridhiwani asaidie kumalizia ujenzi wa msikiti wa Mkenge, Ombi ambalo alilikubali na kuahidi kupaua kwa gharama zake.
   Ridhiwani akijibu maswali mbalimbali ya wananchi wakati wa mkutano katika Kijiji cha Mkenge
   Ridhiwani akikagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti wa Mkenge ambao ameahidi kuchangia mabati na mbao za kupaua jengo hilo la ibada.
   Mwenyekiti wa CCM Kata ya Fukayosi, Olnjurie Marigwa akihtubia katika mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mwavi, Kata ya Fukayosi
   Masoud Fundikira akimuomba Mbunge wao Ridhiwan, anzishe mashindano ya mpira wa miguu kuwania kikombe cha Ridhiwani Cup ili kuendeleza michezo katika jimbo hilo. Ridhiwani alilikubali ombi hilo kwa kuanzia kutoa misaada ya mipira na jezi katika kila timu ya kata za jimbo hilo.
   Ridhiwani akihutubia katika Kijiji cha Mwavi ambapo aliahidi kufuatilia kwa karibu kuhusu suala la alilogawiwa Mkorea ili kijiji cha mwwavi kipate haki.
   Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Kombo Kamote, akiwafunda viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwavi waliochaguliwa hivi karibuni ili wawatendee haki wananchi.
   Ridhiwani akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Kidomole, ambapo aliwajia juu anaowaita matapeli wanaouza ardhi katika Jimbo la Chalinze bila kufuata sheria na utaratibu. Alisema kuwa hayuko tayari kuona hata heka moja ya jimbo hilo ikikuzwa bila utaratibu.
  Ridhiwani akiagana na Meya wa  Morogoro, Amir Nondo ambaye ni mzaliwa wa Kata ya Kiwangwa katika jimbo hilo la Chalinze.

older | 1 | .... | 436 | 437 | (Page 438) | 439 | 440 | .... | 1897 | newer