Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 435 | 436 | (Page 437) | 438 | 439 | .... | 1896 | newer

  0 0

   
  Khadija Kopa akijipinda kimadaha wakati akifanya ‘mavituz’ stejini.
  Kundi la Ogopa Kopa kazini.
  Mtoto wa Khadija Kopa aitwae Mohammed Kopa akikamua huku nyuma yake akisapotiwa na wenzake.

  Mkali wa miondoko ya Kigodoro, Msaga Sumu, akivamia jukwaa na kuwainua mashabiki waliokaa vitini.
  Mashabiki wakijimwaya na burudani ya Kigodoro kutoka kwa Msaga Sumu ambaye alikuwa akisapotiwa na Ogopa Kopa.
  Msaga Sumu akimpelekesha Khanifa Khalid anayeserebuka kwa staili ya gwaride.
  Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa (kulia) na Khanifa Khalid wakikamua.
  Aziza Kimodo akikamua.
  Shadya Chotara naye akionesha makali yake.
  Mashabiki wakifurahia burudani.

  WAENDESHA  bodaboda na wamiliki wake walijimwaya na bonge la burudani kutoka kwa Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa na kundi lake la Ogopa Kopa Modern Taarab sambamba na mkali wa muziki wa Kigodoro, Msaga Sumu, kwenye tamasha lao lililofanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhiem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
  (PICHA : RICHARD BUKOS/GPL)

  0 0

  Kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 mpaka Desemba, bei ya mafuta ghafi imekuwa ikishuka kutoka $110 kwa pipa mpaka $56 kwa pipa. Mporomoko huu wa bei wa zaidi ya 40% haujaleta unafuu kwa mtumiaji wa kawaida wa mafuta ikiwemo wenye daladala na kupelekea nauli za usafiri wa umma kupungua. Leo bado bei ya mafuta kwenye vituo vya mafuta ni tshs 2029 kwa Petroli na 1909 kwa dizeli, bei ambayo ni karibia ile ile kwa miezi michache iliyopita.

  EWURA,inasemekana, wamesema kuwa bei za hapa nchini hushuka baada ya miezi 2 kwa sababu waagizaji huagiza kwa ujumla mafuta mengi zaidi na hivyo kutofaidika na punguzo la bei. Hata hivyo bei zimeanza kushuka toka mwezi Julai na hatujashuhudia unafuu wowote kwa wananchi. Ingekuwa bei ya mafuta imepanda tungeona bei zimepanda mara moja na sababu za kununua ' bulky' huwa hazitolewi.

  Ni kweli kwamba Tanzania hununua mafuta yaliyosafishwa na hivyo bei inayoshuka sio hiyo. Lakini hao wasafishaji hununua mafuta ghafi yenye bei ndogo hivi sasa kwa hiyo ni dhahiri lazima bei za pampu zipungue. Vile vile ni kweli kwamba thamani ya shilingi ya Tanzania imeporomoka hivyo wananchi hawawezi kuona unafuu wa bei ya mafuta kwa sababu hununuliwa kwa fedha za kigeni na kuuzwa kwa Sarafu yetu. Hata hivyo kasi ya kushuka kwa bei ya mafuta ni 40% wakati shilingi imeshuka kwa chini ya 10%. Katika hali ya kawaida na kwa kutumia mfumo wa kukokotoa bei wa EWURA, angalau bei ya mafuta ingeshuka kwa kati ya 15% and 25%.

  Ni dhahiri mamlaka za nchi na hasa EWURA wanapaswa kueleza kwa umma ni Kwanini bei za mafuta hazishuki kulingana na bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia. Wananchi wana haki ya kujua na kama hakuna Maelezo basi bei hizo zishuke na wananchi wafaidike na punguzo hilo.

  Zitto Kabwe, Mb

  0 0


   Jengo la Ghorofa 8 likiwa linateketea katika ghorofa ya 4,Jengo hilo linamilikiwa na mfanyabiashara anayejulikana kwa jina la Haji Kube ,vitu mbalimbali zikiwemo Frem za Picha ,maua, vimeteketea kwa moto,ambapo mmiliki wa ofisi hiyo yuko nje kwa safari
   Wananchi wa kiliangalia jenjo la Ghorofa 8 lililokuwa likiteketea kwa Moto katika ghorofa ya 4  kwenye  Barabara ya Agrey maeneo ya Msikiti wa Kibla ten Dar es Salaa leo.
   Hapo wananchi wakikimbizana baada ya nguzo ya umeme kutowa mlipuko  katika Barabara ya Huru na Kongo Dar es Salaam  kama ilivyonaswa na mwandishi wa Jambo Leo alipokuwa akienda katika Jengo la Ghorofa 8 lililopo jirani na Msikiti wa Kiblateni .
  Hapo wananchi wakikimbizana na kuondowa bidhaa zao baada ya nguzo ya umeme kutoa mlipuko  katika Barabara ya Uhuru na Kongo Dar es Salaam  kama ilivyonaswa  na Mmiliki wa Blog ya ujijirahaa, alipokuwa katika pilika zake za kazi

  0 0

   Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum akitoa mawaidha wakati wa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W) iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
   Viongozi mbali mbali wa Kiislam wakijumuika pamoja na Waislam wengine kwenye Maulidi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W) iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana ambaye ndie aliekuwa mgeni rasmi akizungumza machache kwenye Maulidi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwaasa watanzania kupendana na kuheshimiana.
   Sehemu ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa wamejumuika kwenye Maulidi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W) iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Iran nchini Tanzania,Mh. Mehdi Agha Ja'fari (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana zawadi ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W),wakati Maulidi liyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Iran nchini Tanzania,Mh. Mehdi Agha Ja'fari (kulia) akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum zawadi ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W),wakati Maulidi liyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana wakati wa Maulidi liyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano ulioandaliwa rasmi kuwaambia wananchi wa Mponde, Halmashauri ya Wilaya ya Bumburi, Lushoto mkoani Tanga, kuwa Rais Jakaya Kikwete amekubali kukirudisha Kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi baada ya mgogoro dhidi mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mula uliodumu kwa takribani miaka 10 na kusababisha kiwanda hicho kufungwa maiaka miwili iliyopita na kuwaacha wananchi kwenye lindi kubwa la umasikini.

  Hayo ni Mafanikio ya Katibu Mkuu wa CCM,  Abdulrahman. Kinana ambaye katika mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba mwaka jana katika Kijiji cha Mponde, aliahidi kupata suluhu ya mgogoro wa kiwanda hicho ulioshindikana kutatuliwa kwa muda mrefu kwa kuupeleka kujadiliwa katika Kamati Kuu ya CCM na kupata ufumbuzi ndani ya mwezi mmoja, ahadi ambayo aliitimiza.

  Kiwanda hicho kilifungwa baada ya wananchi kususia kuendelea kulima mashamba ya chai kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutatua haraka mgogoro dhidi ya Mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mulla, ambaye walidai kuwa alikuwa anawanyanyasa wakulima wa zao hilo pamoja na wafanyakazi kuwalipa ujira mdogo.

  Kinana amesema Serikali itanunua hisa za mwekezaji ili aondoke na kuwaachia wananchi kiwanda hicho.Pia Serikali itatuma jopo la wataalamu watakao tathmini hasara iliyopo, na kutafuta mtaji wa kukifufua kiwanda  ili kianze kufanya kazi
  Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamba akiishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kukirudisha kiwanda hicho kwa wananchi ambapo pia alimshukuru Rais Jakaya Kiwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman kwa kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata haki yao hiyo walioisotea kwa takribani miaka 10.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba wakati alipowasili jimboni humo katika wilaya ya Lushoto, akiwa katika ziara ya siku mbili ambapo amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Mponde na kuwataarifu wananchi na wakulima wa Chai kuhusu maagizo ya Rais Jakaya Kikwete juu ya kukirejesha kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi .
    Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa hadhara wakisikiliza kwa makini. 
   Wananchi wa Bumbuli wakifuatilia mkutano wa hahara.
   Mkutano ukiendelea katika uwanja wa Mponde,katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga jioni ya leo.
   Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Mh.Majid Hemed akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika kijiji cha Mponde,mkoani Tanga.
   Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa hadhara wakisikiliza kwa makini
   Mmoja wa Wananchi akishangilia kwa namna yake mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kutamka kuwa kiwanda cha Chai cha Mponde Rais Kikwete ameamuru kilejeshwe mikononi mwa Wananchi na Wakulima wa Chai. 
   Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalulla Said Magalulla akiwasalimia na kujitambulisha kwa wakazi wa Bumbuli na Vitongoji vyake,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Mponde,Mkoani Tanga.
   Mbunge wa Jimbo la Lushoto na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga,Henry Shekifu akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa Mponde,Mkoani Tanga.

  0 0

  Karibu katika kipindi cha HUYU NA YULE ambapo wiki hii tumeongea na Dr Crispin Semakla.
  Daktari wa mahgonjwa ya kisukari, shinikizo la damu na pia Mwalimu wa Afya katika Chuo Kikuu nchini Marekani
  Pia ni mwanzilishi wa Access Medical and Dialysis Center iliyopo Dar Es Salaam
  Ameeleza mengi kuhusu maradhi anayoshughulika nayo na pia kituo chake.

  Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production
  Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano ulioandaliwa rasmi kuwaambia wananchi wa Mponde, Halmashauri ya Wilaya ya Bumburi, Lushoto mkoani Tanga, kuwa Rais Jakaya Kikwete amekubali kukirudisha Kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi baada ya mgogoro dhidi mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mula uliodumu kwa takribani miaka 10 na kusababisha kiwanda hicho kufungwa maiaka miwili iliyopita na kuwaacha wananchi kwenye lindi kubwa la umasikini.

  0 0

  DSC_0058
  Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC), Chande Omar (kulia) akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani iliyopo Kusini Pemba. Katikati ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph na kushoto ni Mke wa Mratibu Mkazi wa UN Tanzania, Bi. Fainula Kurji-Rodriguez.
  DSC_0213
  Meneja wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Mkoani Kusini Pemba, Bw. Ali Abbas akisoma risala ya kituo chake mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto visiwani Zanzibar, Mh. Zainabu Omari Mohammed (hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa kituo hicho cha redio.
  DSC_0239
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo visiwani Zanzibar, Juma Yakufi akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri mwenye dhamani ya wizara hiyo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni mkoani Kusini Pemba uliofanyika mwishoni mwa wiki visiwani humo.
  DSC_0252
  Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba, Hemedi Selemani akitoa neno la shukrani wakazi wa mkoani jimbo la Mkanyageni pamoja na wageni waalikwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba uliofanyika mwishoni mwa wiki.
  DSC_0276
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza kwenye uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba uliofanyika mwishoni mwa wiki.

  DSC_0277
  DSC_0315
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimkabidhi cheti Meneja wa Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba, Bw. Ali Abbas wakati wa sherehe za uzinduzi wa Redio jamii hiyo.
  DSC_0186
  Meza kuu.
  DSC_0323
  Mkuu wa Mkoa wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba, Bi. Mwanajuma Abdallah akizungumza machache na wakazi wa mkoani na kuwaasa kukitumia chombo hicho vyema katika kujiletea maendeleo na kupashana habari kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua rasmi kituo hicho cha Redio Jamii.
  DSC_0358
  Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akisoma hotuba yake kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo cha redio ya jamii jimbo la Mkanyageni, Mkoani Kusini Pemba.
  DSC_0183
  Mabinti wa visiwani Pemba wakisoma utenzi wa kulishukuru shirika la UNESCO na ZBC kwa kuanzisha kituo hicho cha Redio jamii jimbo la Mkanyageni mkoani Kusini Pemba.

  DSC_0078
  Pichani juu na chini ni baadhi ya wakazi wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi kwenye sherehe za ufunguzi wa kituo hicho cha Redio Jamii.
  DSC_0167
  DSC_0296
  DSC_0378
  Pichani juu na chini ni Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akikabidhi vyeti kwa baadhi ya wafanyakazi wa Redio Jamii Mkoani ya jimbo la Mkanyageni mkoani Kusini Pemba. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo visiwani Zanzibar, Juma Yakufi.
  DSC_0388
  DSC_0401
  Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha Redio Jamii Mkoani iliyopo Kusini Pemba. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba, Bi. Mwanajuma Abdallah (mwenye mtandio wa bluu), Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba, Hemedi Selemani pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
  DSC_0403
  Sasa kimezinduliwa rasmi....!
  DSC_0465
  Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akitia saini kitabu cha wageni cha kituo cha Redio Jamii Mkoani Kusini Pemba kabla ya kukagua vifaa na studio ya kituo hicho.
  DSC_0438
  Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed akizungumza Live na wananchi wa jimbo la Mkanyageni mkoani Kusini Pemba mara baada ya kuzindua kituo cha Redio Jamii Mkoani ikiwa ni shamra shamra ya sherehe za Mapinduzi mwishoni mwa wiki kisiwani Pemba. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washika dau kutoka UNESCO.
  DSC_0427
  Mtangazaji wa kituo cha Redio Jamii Mkoani ya Kusini Pemba, Bw. Seif Mohammed akiwa kwenye mahojiano na Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed yaliyorushwa Live na kituo hicho mara baada ya kuzinduliwa.
  DSC_0497
  Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Redio Jamii Mkoani, Wajumbe wa Bodi ya Redio Jamii Mkoani, wafadhili pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.
  DSC_0501
  Mgeni rasmi Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Mh. Zainab Omar Mohammed katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba.
  DSC_0515
  Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akiwa kwenye picha na wanafunzi wake wa vituo vya redio jamii ya Mkoani na Micheweni mara baada ya sherehe za uzinduzi.
  DSC_0158
  Kikundi cha Ngoma ya Msembwe cha kisiwani Pemba kikitoa burudani kwenye uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani uliofanyika mwishoni mwa juma Kusini Pemba.
  DSC_0011
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye koti la suti) akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili kuhuduria sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni, Kusini Pemba na kupokelewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph (kulia) aliyeambatana na Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu (aliyeongoza mbele).

  Na Mwandishi wetu, Pemba
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba itaendelea kuruhusu kuanzishwa kwa Redio za jamii kutokana na umuhimu wake katika kuhimiza maendeleo na kutumika kama daraja kati ya wananchi na serikali yao.
  Hayo yalisemwa na Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa jamii, Vijana, wanawake na watoto, Zainab Omar Mohammed wakati akizundua kituo cha redio ya jamii jimbo la Mkanyageni, Mkoani Pemba.

  Shughuli hiyo ambayo ilifanyika kama sehemu ya shamra shamra za sherehe za mapinduzi kutimiza miaka 51 zilihudhuriwa pia na wafadhili wa mradi huo ambao ni Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

  Waziri huyo alisema kwamba uzinduzi wa kituo cha redio ya jamii katika jimbo la Mkanyageni Mkoani Pemba ni moja ya azma ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwapa haki wananchi wake ya kupata habari ikiwa ni sehemu muhimu sana ya maisha ya wanadamu.
  DSC_0038
  Munekano wa sehemu ya jengo la Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni Kusini Pemba kabla ya kuzinduliwa rasmi.

  Alisema habari ni kitu muhimu sana katika maisha ya sasa na wakati taifa likiadhimisha miaka 51 ya mapinduzi yaliyolenga kubadili maisha ya wazanzibari uwapo wa redio za jamii ni kitu ambacho kitasukuma mbele zaidi madhumuni ya mapinduzi , kumkomboa mzanzibari kiuchumi na kifikira.

  “Redio hizi Jamii, zimewekwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa madhumuni ya kuwapa fursa wananchi kupata habari,kupata burudani, kupata elimu, lakini pia kutoa fursa ya kutoa mawazo yao kupitia redio hizi ili serikali ipate kujua zaidi nini hasa changamoto za wananchi na iweze kuzifanyia kazi kwa urahisi zaidi” alisema Waziri Zainab.

  Pamoja na kuushukuru Umoja wa mataifa kwa kusaidia redio za jamii aliutaka Umoja huo uendelee kuimarisha uwezo wa redio hizo ili wananchi wazitumie kupata maendeleo.

  Naye Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amesema Umoja wa mataifa unajisikia fahari kuwezesha asilimia 60 ya wazanzibari kusikiliza redio za jamii na kuzitumia katika maendeleo yao.
  DSC_0022
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na mkewe akisalimiana na Ofisa mdhani kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed mara baada ya kuwasili eneo la tukio.

  Alisema umoja huo utaendelea na ushirikiano wake na serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kuweka mazingira ya upatikanaji wa habari kuwa bora zaidi, ushirikiano ambao waliuanza mwaka 2008 wakati wa kutengeneza sera ya utangazaji. Alisema ni sera hiyo iliyowezesha kuwepo kwa redio za jamii na utangazaji wa umma.

  Alisema Redio za jamii ni msaada mkubwa katika kutoa elimu kwa jamii inayozunguka kituo hicho na kusema kwamba ni imani yake kituo cha Mkoani kitafanya kazi iliyokusudiwa kwa kuhamasisha mawazo chanya ya maendeleo na kuleta ushirikiano na amani inayotakiwa katika jamii.
  DSC_0036
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph wakipitia ratiba kabla ya kuanza rasmi sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani uliofanyika Kusini Pemba.

  Amesema Umoja wa Mataifa umewezesha kituo hicho vifaa vya utangazaji na kutengeneza uwezo wa wafanyakazi wa chombo hicho. Amesema kupitia mradi wa uwezeshaji demokrasia (EDP) unaoendeshwa kwa pamoja na UNESCO na UNDP chini ya makubaliano ya msaada kwa serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa (UNDAP) , Umoja wa Mataifa umetoa mtambo wa kurushia matangazo wenye nguvu za Watts 600 unaoweza kusambaza matangazo yake eneo lote la Kusini pemba.

  Pamoja na mtambo huo na vifaa vingine vya studio vilitolewa na kumefanyika ufundishaji wa watangazaji namna bora ya mawasiliano na menejimenti ya habari na utawala. Mratibu huyo aliitaka serikali na taasisi zake kukitumia vyema kituo hicho katika kuhakikisha kwamba maendeleo yaliyokusudiwa kwa jamii yanapatikana kupitia vipindi mbalimbali vya kuelimishana.
  DSC_0086
  Mke wa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bi. Fainula Kurji-Rodriguez (kushoto) na Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu wakifurahia burudani ya Ngoma ya Msembwe ya Kusini Pemba ilipokuwa ikisherehesha kabla ya kuwasili wa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
  Pia aliwataka waendeshaji wa kituo hicho kuwa makini na kuwajibika kwa umma, kauli ambayo awali pia ilielezwa na Naibu Katibu Mkuu , Wizara ya habari Utamaduni , Utalii na Michezo Juma Yakufi aliyetaka sheria na taratibu za mawasiliano kuzingatiwa.
  Alitaka vipindi vitakavyotengenezwa kuzingatia utu, silka na utamaduni wa Mzanzibari na redio hiyo kuendeshwa kwa mujibu wa masharti ya redio jamii kwa kuhakikisha hawaingiliwi na taasisi yoyote na kuendeshwa kwa manufaa ya jamii na sio manufaa ya mtu mmoja mmoja.
  Naye Mwa redio hiyo Ali Abbas pamoja na kushukuru kusaidia kuanzishwa kwa redio hiyo aliitaka jamii kuitumia vyema nafasi waliyopewa kuendeleza mbele maendeleo yao na kutumia upashanaji habari kutanzua changamoto za maendeleo.
  DSC_0096
  Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akijumuika kutoa burudani na kikundi cha Ngoma ya Msembwe kutoka Kusini Pemba.

  DSC_0160

  0 0


  KAMPUNI ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikiwa chini ya uongozi wa kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP) imetangaza kufikia kwa punguzo la bei ya umeme la asilimia 20 baada ya kufanya marekebisho makubwa ya injini za mtambo huo ya masaa 36,000 ikifanya kazi, zoezi iliyokamilika ndani ya mwanka 2014. IPTL pia imetangaza kuwa bei yao ya umeme ikitarajiwa kushuka zaidi kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta mazito. 

  Marekebisho hayo yaliyotumia zaidi ya Dola za kimarekani milioni 25 yameiwezesha mitambo ya IPTL kuwa katika nafasi nzuri ya kuzalisha umeme wa uhakika kwa kufikia megawati 100 na kuingiza katika gridi ya Taifa mara to baada ya kukamilika kwa zoezi hilo mnamo Desemba mwaka 2014.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Harbinder Singh Sethi, IPTL sasa imepunguza bei ya umeme wake inaoutoza kwa Shirika la ugavi wa umeme Tanzania (Tanesco) ambao sasa utakuwa chini ya bei ya awali iliyokokotolewa ya senti 23 dola za kimarekani kwa Kilowati; huku ikihakikisha kupatikana kwa umeme wa uhakika.

  "Tukiwa tunaukaribisha mwaka 2015, IPTL inajivunia kutangaza kuwa imefanikiwa kufanya marekebisho makubwa ya mashine zake ya masaa 36,000 ya kufanya kazi, zoezi iliyokamilika ndani ya mwaka wa 2014. Nimeiomba timu ya IPTL kupanga mapema jinsi gani wanaweza kuongeza juhudi zaidi kufikia marekebisho ya masaa 48,000, katika awamu inayofuata katika mwaka 2015. Tunatarajia uwepo wa IPTL kuwa bora zaidi kwa kuwa sasa tunajipanga kuongeza rasilimali zaidi.

  "Hii ni sehemu ya ahadi ya PAP kuhakikisha kuwa IPTL inaendeshwa vizuri na kwa ufanisi. Wakati sasa umefika kwa TANESCO kuwa na uhakika wa kupata umeme wa uhakika wa megawati 100 katika gridi ya taifa wakati wowote utakapohitajika.

  "IPTL chini ya PAP haiangalii tu uzalishaji wa umeme wa kutosha, lakini pia ipo makini kuhakikisha kuwa umeme huo wa kutosha unakuwa nafuu. Kwa maana hiyo, tumeamua kushusha bei zetu za umeme kufikia chini ya bei iliyokokotolewa ya hapo awali ya senti 23 dola za kimarekani kwa uniti, ambayo sasa inaleta jumla ya punguzo la bei la asilimia 20 kwa ile iliyokuwa ikitozwa na IPTL  kabla ya PAP kuchukua uongozi," alisema.

  Bw. Sethi aliongeza kuwa TANESCO itarajie punguzo zaidi la bei ya umeme kufikia kiwango cha chini ya Senti 8 Dola za kimarekani kwa kila uniti ya umeme mara baada ya mitambo ya IPTL kupanuliwa na kufikia uzalishaji wa megawati 500 mitambo yake ikitumia gesi asilia.  

  Alisema kuwa mpango wa upanuzi wa mitambo hiyo unaendelea vizuri, akiongeza kuwa iko katika hatua za awali za uchanganuzi na upimaji wa udongo.

  "Tunatarajia hatua za upanuzi kwenda haraka ili kuhakikisha kuwa IPTL inatoa huduma bora, ya uhakika na nafuu katika taifa hili. Ningependa kutoka shukrani zangu kwa uongozi wa TANESCO na Gridi ya Taifa kwa kukubali umeme unaozalishwa na IPTL,"alisema.

  Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali kutoka TANESCO, bei za umeme zinazotozwa na IPTL kwa sasa zimeshuka na kufikia chini ya Senti 19 Dola za kimarekani kwa uniti za umeme kutokana na kushuka kwa bei ya Mafuta mazito wakati wa kipindi cha ukokotoaji wa bei hizo.

  Upatikanaji wa umeme wa uhakika kutoka IPTL tayari umeshathibitika wakati wa kipindi cha sikukuu kilichopita ambapo nchi haikukumbana na mgawo wowote ikilinganishwa na miaka iliyopita ambapo ilikuwa ni kawaida kwa umeme kukatika katika wakati wa msimu wa sikukuu ambapo kunakuwa na mahitaji makubwa.

  0 0
 • 01/04/15--22:05: Article 0


 • 0 0  0 0
 • 01/05/15--03:58: Article 14


 • 0 0

   Redds Miss Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akiongea Maneno machache wakati akikabidi mashine mbili za kupumulia kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wa kawaida zenye thamani ya Tsh millioni 1.2 kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa wa Singida, msaada alioutoa kwa ushirikiano na Manifester brand. Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo alikua ni mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Queen Mlozi.
  Redds Miss Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akiwaona watoto njiti baada ya hafla ya kukabidhi mashine mbili za kupumulia kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wa kawaida zenye thamani ya Tsh millioni 1.2 kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa wa Singida, msaada alioutoa kwa ushirikiano na Manifester brand. Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo alikua ni mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Queen Mlozi.(Picha na Albert Manifester).

  Na mwandishi wetu, Singida.

  Katika kuianza safari yake ya huduma za jamii kwa mwaka 2015, Redds Miss Kanda ya kati 2014-2015 Doris Mollel ametoa msaada wa mashine 2 za kupumulia kwenye hospitali ya mkoa wa Singida zenye thamani ya Tsh 1,200,000/=. Mashine hizo huwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya muda wa kawaida (Pre-mature babies) katika mfumo wao wa upumuaji ambao huhitaji msaada wa juu zaidi mara tu wanapozaliwa.

  Doris ambaye pia ni mshindi wa tatu wa Redds Miss Tanzania 2014 ni mwanaharakati wa dhana ya Urembo wenye Malengo endelevu kwa jamii ‘Beauty with a Purpose’. Amefanya kazi kubwa kwenye sekta ya elimu akijikita zaidi kwenye kuchangia Vitabu kwa shule za msingi na sasa, akiwa ni mmoja ya watu ambao walizaliwa kabla ya muda wa kawaida ameamua kupanua wigo wake wa huduma za jamii kuleta mwamko na kusaidia kuokoa maisha ya watoto hawa.

  Akiongea kwenye hafla ya kukabidhi mashine hizo iliyofanyika hospitalini hapo, Mollel alisema. “Kiwango cha vifo kwa watoto wanaozaliwa kabla ya kukomaa ni karibu 30% vikichangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa vifaa vya kutosha kusaidia mifumo yao ya upumuaji mara tu wanapozaliwa. Nikiwa moja ya watoto hao ambaye nilibahatika kupata msaada na huduma ya kutosha nilipozaliwa, Ninaelewa ni jinsi gani matunzo haya ya awali yalivyo muhimu kwenye kuokoa maisha ya watoto hawa na ninajikita kuwasaidia”.

  Bw. Albert Mbepera, Mkurungezi Manifester brand ‘huduma kwa jamii ni eneo muhimu sana kwetu. Tunafurahi kujitolea kufanya kazi na Doris katika maswala ya kusaidia jamii na tunaamini kuwa ushirikiano huu utasaidia kukusanya na kuonyesha matatizo ya wahitaji ili kuongeza uelewa na msukumo wa misaada kutoka kwa sekta binafsi na wanajamii kwa ujumla’

  Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Singida Bi Queen Mlozi na ilihudhuriwa na Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Bw. Daniel Tarimo, Daktari bingwa wa watoto wa Hospitali ya Singida, Muandaaji wa Redds Miss Singida 2014 Bora Lemmy na washindi wengine wa Redds Miss central Zone Linda Bureta, blath Chambia, Suzy Wahere.

  Doris Mollel na Manifester brand wanapenda kuwashukuru ANUDHA PHARMACEUTICALS LTS kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha shughuli hii.

  0 0

  Kutua Februari, apania kuzalisha akina Mayweather kibao nchini
  NDONDI ni miongoni mwa michezo maarufu mno hapa Tanzania na duniani kwa ujumla.
   
  Wapo wanamichezo waliojipatia heshima kubwa duniani kutokana na kufanikiwa kupitia mchezo wa ndondi.
   
  Miongoni mwa wanamichezo hao ni nguli Mohammed Ali, Mike ‘Iron’ Tyson, Evender Holyfield, Floyd Mayweather, Manny Pacquiao na wengineo wengi.
  Kwa hapa nchini, wapo mabondia waliojitengenezea majina wakiwamo Emmanuel Mlundwa, Habibu Kinyogoli ‘Masta’ Michael Yombayomba, Stanley Mabesi ‘Ninja’ Rashid Matumla, Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’  na wengineo wengi. 
   
  Lakini ikumbukwe kuwa ndondi ndio mchezo uliotoa mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani kwa sasa ambaye si mwingine bali ni Mayweather, akifuatiwa na mwanasoka raia wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo.
   
  Anayeshika nafasi ya tatu ni mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James, wakati mwanasoka anayechezea Barcelona ya Hispania, Muargentina Lionel Messi akishika nafasi ya nne, huku wa tano akiwa ni mkali wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant.
   
  Pamoja na mafanikio hayo katika ndondi, Tanzania imeonekana kuzidi kulala usingizi wa pono katika suala zima la kuvumbua na kuendeleza vipaji vya mchezo huo kama sehemu ya kutatua tatizo sugu la ajira linaloitesa nchi yetu kwa sasa.
   
  Unapopita huko mitaani, unaweza kukutana na vijana wadogo wakiwa wanafanya mazoezi ya ngumi kwa kutumia vifaa visivyo rasmi ambavyo mwisho wa siku, huishia kuwadumaza badala ya kuwajenga kama walivyotarajiwa.
   
  Hali hiyo imetokana na kukosekana kwa vifaa vya kujifunzia mchezo huo, zikiwamo kumbi na hata wataalam wa kuwapa ujuzi wa kuwawezesha kufikia mafanikioi ya akina Mayweather.
   
  Ni kwa kufahamu hilo, wapo wadau wa ndondi ambao wamekuwa wakijitoa kusaidia vipaji vya ndondi hapa nchini, miongoni mwao akiwa ni Kocha wa Kimataifa wa Ndondi nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’.
   
  Bondia huyu wa zamani, ameshawahi kufanya jitihada kadha wa kadha kuendeleza ndondi hapa nchini, ikiwamo kutoa mafunzo kwa vijana chini ya klabu yake ya Ashanti Boxing Club na kupitia DVD zake zenye mapambano makali yaliyowahi kufanyika hapa nchini na duniani kwa ujumla, yakiwahusisha mabondia nyota.
   
  Katika kuonyesha jinsi anavyoguswa na ndondi, Februari mwaka huu Super D atakuwa na ugeni mkubwa wa bondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchini Deer Park, Victoria, Australia, Omari Kimweri ambaye anatua nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanamasumbwi wa Tanzania.
   
  Akizungumza Dar es salaam jana, Super D anasema kuwa ujio wa Kimweri ni fursa nyingine adimu kwa mabondia wa Tanzania katika kuona ni vipi wanaweza kutimiza ndoto zao za kutoka kimaisha kupitia mchezo huo.
  Anasema kuwa Kimweri atatua akiwa na vifaa mbalimbali vya masumbwi ambapo pia atatoa mafunzo na mbinu mpya zinazotumiwa na mabondia wa nje kwa mabondia pamoja na kushuhudia mapambano kadhaa yatakayofanyika kwa kipindi atakachokuwapo hapa nchini.
   
  “Kimweri anakuja akiwa na msafara wa watu kadhaa, akiwamo mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania. Akiwa hapa nchini, Melanie atapata fursa ya kukutana na wanasoka wa kike wa hapa , kwani amechezea timu nyingi za Ulaya,  Hispania,” anasema Super D.
   
  Anasema kuwa ujio wa Kimweri umewezeshwa kwa kiasi kikubwa na promota wake, Brian Amatruda ambaye ni miongoni mwa mapromota maarufu nchini kwao Australia, akiwa amekubali kutoa baadhi ya vifaa vya kisasa kutoka Hispania na Marekani kwa ajili ya ziara hiyo.
  Super D anasema kuwa Kimweri ambaye ni bingwa wa WBO, atatua nchini akiwa na mikanda yake yote aliyowahi kutwaa, ukiwamo wa ubingwa wa Australia, lengo likiwa ni kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujikita zaidi katika ndondi.
   
  “Nimezungumza na Kimweri na ameonyesha kuwa na uchungu wa kuwainua mabondia wa hapa nchini ili waweze kutimiza ndoto zao na anafanya hivyo chini ya mradi wake wa ‘Kimweri Project’ na atakuwa hapa nchini kwa wiki moja,” anasema.
   
  Anasema kuwa ujio wa bondia huyo uliochagizwa na Super D Boxing Coach and Promotion, umelenga kuwahamasiaha mabondia kucheza mara kwa mara ili kupandisha viwango vyao kwani hiyo ndio siri ya mafanikio ya wanamasumbwi wengi duniani.
   
  Mbali ya mafunzo kutoka kwa Kimweri, pia katika ziara zake zote sehemu mbalimbali nchini, kutakuwa na uuzwaji wa DVD za Super D zenye lengo la kutoa mafunzo kupitia mapambano ya mabondia maarufu duniani, akiwamo Floyd Mayweather,Manny Paquaio, Mohamerd Alli, na wa hapa nchini kama Mbwana Matumla, FrancisMiyeyusho,Ibrahimu Class’ King Class Mawe’ ambaye ni bingwa wa WPBF Africa na wengineo

  0 0

   Naibu Wazir wa Maji Waziri Makala akifuatana na wajumbe wa Bodi na Menejimenti, watendaji wa DAWASCO, waandishi wa habari na wananchi wa Boko wakati wa Ziara yake ya kushtukiza katika eneo la Boko jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya maeneo yenye matatizo ya maji ambayo yanasababisha wananchi wengi kukosa huduma hiyo muhimu katika masiha yao.
  Naibu Waziri wa Maji Waziri Makala pamoja na wananchi wakishuhudia moja ya eneo ambalo linahusishwa na kuhujumu maji katika eneo la Boko mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO.

  Na Eleuteri Mangi- MAELEZO.
  Naibu Waziri wa Maji Amos Makala ameiagiza Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka ya jiji la Dar es salaam (DAWASCO) kuviwezesha vitengo vya Habari na Biashara ili vifanye kazi karibu na wananchi.

  Naibu Waziri Makala alisema hayo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara ya kushtukiza ya kukagua na kujionea namna miundo mbinu ya maji ya DAWASCO inavyohujumiwa na baadhi ya watu wachache na kuwakosesha wananchi waliowengi huduma muhimu ya maji katika maeneo yao wanakoendesha maisha yao ya kila siku.

  “Kumekuwa na mawasiliano mabovu kati ya baadhi ya viongozi wa DAWASCO na wananchi, ni lazima mbadilike na kila mmoja atoe taarifa kwa wananchi ili wawe wanajua tatizo la wao kutokupata maji ni nini na litatatuliwa linatatuliwaje” alisema Makala.

  Akizungumza na wakazi wa Boko jijini Dar es salaam, Makala alisema kuwa viongozi wanamaelezo mazuri ila hawana mawasiliano mazuri na wananchi pia wawe na lugha nzuri kwa wateja wao wanapofika ofisini kuhitaji huduma ya kuunganishiwa maji, kutoa kero zinazowasibu au tatizo la miundo mbinu ya maji kwenye maeneo yao inayosababisha upotevu wa maji mengi bila sababu. 

  Aidha, wakati wa ziara hiyo Naibu Waziri Makala aliwasimamisha kazi Meneja wa DAWASCO eneo la Boko Robert Mugabe na Meneja wa Kimara Peter Chacha na kuagiza Bodi na Menejimenti ya DAWASCO kuwapangia kazi nyingine na nafasi zao zijazwe mara moja.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DAWASCO alisema kuwa operesheni ya wahujumu maji Dar es salaam itakuwa ni endelevu, wale wote waliokamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na sheria itachukua mkondo wake.

  Ziara ya Naibu Waziri Makala akifuatana na wajumbe wa Bodi na Menejimenti, watendaji wa DAWASCO na waandishi wa habari ilianzia kukagua maeneo yenye matatizo maji ambayo yanapelekea wananchi kukosa maji ya maeneo mbalimnbali jijini Dar es salaam yakiwemo Mgomeni, Manzese, Boko na kuhitimisha ziara hiyo maeneo ya Kimara.

  0 0

  Mrembo wa miss Universe Tanzania 2014 ameondoka rasmi nchini kuelekea nchini Marekani kwenye fainali za  dunia za Miss Universe zitakazofanyika jijini Miami tarehe 25 mwezi huu wa januari.

  0 0
 • 01/05/15--04:26: Article 9


 • 0 0

  Are you an exceptional change leader with outstanding potential and significant achievement in shaping your community?

  Joining the Dar Es Salaam Hub of the Global Shapers Community offers you a unique opportunity to work with other change leaders in the city. This is your chance to join the most exceptional young thought leaders in a multitude of fields working to improve the state of the world and particularly the city of Dar Es Salaam!!! Membership to the hub presents you an opportunity to join the Global Shapers Community and exchange wonderful opportunities for driving the global development agenda.

  The Global Shapers Community is a network of Hubs developed and led by young people who are exceptional in their potential, their achievement and their drive to make a contribution to their communities. Through the Global Shapers Community, Shapers are provided with opportunities to connect with the worldwide network of Global Shapers, to network with other World Economic Forum communities, and to represent the voice of youth at World Economic Forum events. Shapers are united by a common desire to channel the members’ tremendous energy and enthusiasm into building a more peaceful and inclusive world.

  What does it take to become a global shaper?

  · A proven experience and track record of change making and service to community through business enterprise, civil society, public service, media or the arts.

  · A demonstrable record of leading a cause, campaign, institution or initiative in Tanzania or beyond

  · Strong and proven commitment to improving the state of the world

  · Must be a resident of Dar Es Salaam

  · Must be aged between 20-29 as December 2014

  Applications should be received by 1700hrs 5th Feb 2015. Please submit your application to Darshapers@gmail.com. For your application to be complete please send in your Application/ Introduction letter along with your most updated resume.

  For further information about the Dar Hub of the Global Shapers Community, please visit: http://www.globalshapers.org/Dar Hub

  To learn more about the Global Shapers Community of the World Economic Forum please visit: http://www.globalshapers.org/ 

  xoxo
  Missie Popular

  0 0

  Sune Mushendwa-Mkito.com  
  Sune Mushendwa[/caption] Kwa miaka nenda rudi, wasanii wa kitanzania walikuwa na kilio kinachofanana. Ungekaa pembeni bila kuwaona, ungedhani kutokana na mwangwi wa kilio chao, anayelia ni mmoja. Hapana. Wote walikuwa [na pengine bado wanaendelea kulia] kutokana na kunyonywa “jasho lao”. Kimsingi “jasho” wanalolilia limekuwa ni soko na usambazaji. Kipaji unacho na watu wanakubali kazi zako. Tatizo utaifikishaje kazi yako kwa mashabiki zako?

   Ni wazi kwamba unahitaji msaada wa kimasoko na usambazaji. Kusema utaweza kufanya kila kitu peke yako ni kujidanganya.Nani? Yupo wapi na utampa kazi zako kwa thamani gani? Kilio chao kilianzia hapo. Wengine wakaamua kuachana na muziki [wengine muziki umewaacha wao] kutokana na ukosefu wa soko la uhakika na kuona kadhaa ya kupanga foleni ukisubiri “hela yako”. 

  Mabadiliko ya masoko ya kazi za wasanii duniani kutoka kwenye mifumo ya ki-analojia kwenda kwenye dijitali na pia kutoka katika mifumo ya vitu kama CD mpaka kwenda kwenye matumizi ya simu na vikabrasha vingine vya mikononi, kulimaanisha kwamba soko la wasanii wa kitanzania [na Afrika kwa upana wake] lilikuwa linazidi kufifia.

   Hakuna tena shabiki anayetaka kubeba furushi la CD. Inakuwaje? Hapo ndipo baadhi ya vijana wakaona fursa kuthibitisha kwamba penye tatizo ndipo pa kukimbilia.Fursa ni kama dhahabu au almasi.Huwezi kuiokota kando ya bahari ikiwa imetupwa ufukweni na mawimbi ya bahari. Wazo la fursa likazaa Mkito.Com mahali ambapo wasanii sasa wanapumua na huku changamoto pekee ni kuwashawishi mashabiki kupakua kazi zao kutoka Mkito.Com. 

  Kila mara shabiki anapofanya hivyo, msanii ananufaika na kupata nguvu zaidi ya kuingia tena studio kunogesha mambo. It’s a win win situation.   Sune Mushendwa [pichani juu] ni mwanzilishi-mwenza wa Mkito.Com. Kujua mengi zaidi nilimtafuta na kupiga naye story kidogo. Ameelezea mengi. Nakukaribisha usome mahojiano yangu naye ili ujue yote ambayo umekuwa ukitaka kuyajua kuhusu Mkito.Com .Twende pamoja;   

   BC: Sune karibu sana ndani ya BongoCelebrity. Hii ni mara yako ya kwanza hapa na bila shaka wasomaji wangependa kupata japo kwa kifupi tu historia yako. Ulizaliwa wapi,ukakulia wapi na kusomea wapi na mambo kama hayo?SM: Asante sana kwa kunikaribisha. Mimi nimekulia Arusha na ndipo niliposoma pia. Baada ya sekondari nilienda kusoma chuo kikuu nchini Finland ambako mama yangu ndipo anapotokea. 

   BC: Wajasiriamali wengi ambao nimewahi kufanya nao mahojiano huniambia kwamba waliamua kufanya wanachokifanya baada ya kukosa au kubughudhiwa na kitu fulani.Huwa kuna kisa au mkasa nyuma ya pazia. Kwa upande wa Mkito kuna kisa au mkasa wowote? Ilikuwaje mpaka ukasema Aha…Mkito ikaanza? Na hili jina lilikuja namna gani?   

  SM: Baada ya kutoka masomoni nilianzisha studio ya muziki Arusha.Lakini tatizo kubwa lililoonekana moja kwa moja ni kwamba wasanii pamoja na studio zinapata tabu sana katika kusambaza na kuuza kazi zao. Niliona tunahitajika njia ya kuweza kusambaza muziki kirahisi na pia kuingiza kipato kwa msanii. Baada ya research na maandalizi ya zaidi ya miaka 4 ndipo Mkito.com ilipozaliwa tarehe 30 April 2014. BC: Mpaka sasa Mkito imefanikiwa kuwa na wasanii wangapi? Nini masharti ya msanii kujiunga au kuweka kazi zake katika Mkito? 

   SM: Kuna wasanii takriban 600 waliojiunga mpaka sasa na wanaongezeka kila siku. Masharti ya kujiunga ni marahisi, uwe umerekodi wimbo anghalau mmoja wenye ubora. Baada ya hapo msanii anaweza kujitengenezea akaunti yake kupitia tovuti www.mkito.com na kupakia[upload] nyimbo zake mwenyewe. Msanii baada ya hapo anaweza kufuatilia mauzo yake mwenyewe kupitia akaunti yake aliyoitengeneza.    

  BC: Bado nikiwa katika swali au maswali ya wasanii. Msanii akishaingia katika mkataba au makubaliano na ninyi, bado anakuwa na haki na uhuru wa kuendelea kusambaza kazi zake katika platforms zingine kama vile iTunes,Spotify,Google Play nk?
    SM: Tunaamini kuwa kazi ya msanii ni mali yake pekee kwahivyo hatumzuii msanii aliyejiunga nasi kusambaza kazi zake kwa njia yoyote nyingine aipendayo. Kama huduma yetu ni bora basi tunaimani msanii mweyewe atachagua kutumia huduma zetu siyo mpaka tumfunge kupitia mikataba.   

   BC: Nilisoma mahali kwamba mlipoanzisha Mkito lengo lilikuwa kuwa na watumiaji waliojiandikisha [registered users] milioni 1 katika mwaka wa kwanza. Mpaka sasa mmefikia wapi katika lengo hilo?  SM: Nilishasoma hilo mimi pia lakini siyo ukweli kuwa lengo ni kufikisha watumiaji milioni 1. Lengo ni kufikisha watumiaji waliyojiandikisha laki 5 ndani ya mwaka moja. Tumekaribia nusu ya hiyo idadi mpaka sasa na dalili zote ni kuwa tutafika na kuvuka hiyo idadi.    

  BC: Kuna baadhi ya wasanii ambao nimeongea nao kuhusu huduma kama hii ya Mkito na nyinginezo wanasema kwamba huduma hizi kimsingi zinawapunja au kuwadhulumu kwa sababu hamuendi nao bega kwa bega katika matayarisho ya muziki [kwa maana ya gharama na karaha zote za maandalizi] bali nyie mnasubiri wapike kisha muwasaidie tu kupakua huku nanyi mkijitengenezea faida. Unawaambiaje wasanii kama hao na kuna tofauti gani kubwa kati ya wasambazaji wale wa zamani na nyie hapo?  

   SM: Mkito.com ni kampuni ya usambazaji wa muziki na siyo studio ya kurekodi au kampuni ya management. Kwa maana hiyo sisi faida tunaingiza katika uuzaji wa muziki kupitia tovuti yetu tu. Kama tungehusika na kurekodi na management ya wasanii basi tungedai makato kwenye mauzo yote kama ring tones, CD, shows n.k. lakini kama nilivyosema faida yetu ni katika uuzaji wa muziki tu. Kuhusiana na tofauti ya Mkito.com na makampuni mengine; tangia mwanzo tumehakikisha kuwa mauzo yote yanawekwa wazi ili msanii ajue muda wote kuwa mauzo yake yakoje. Hili bado sijaona likifanyika na wengine ingawa ni la muhimu sana. Inabidi kujiuliza madhumuni ya haya makampuni kutokuweka mauzo wazi. Mkito   
  BC: Kwa mtu ambaye hajui Mkito ni nini na angependa kufahamu zaidi na hata kujiunga na huduma ya Mkito[nazungumzia mtu mtumiaji wa kawaida] ungempa maelezo gani kwamba Mkito ni nini na nini ategemee pindi atakapoingia Mkito.com?  SM: Mkito.com ni huduma ya kwanza nchini ya kusambaza muziki kidigitali ambapo mtu anaweza kupakua nyimbo kwa sh 250 tu kupita simu yake au computer. Pia nyimbo zote zinapatikana bure lakini zinaambatanishwa na matangazo mafupi ya kibiashara. Haya matangazo katika nyimbo za bure ndiyo yanawalipa wasanii. Ni muhimu kujua kwa Watanzania wote kuwa ni jukumu letu kulinda muziki wetu na unavyopakua nyimbo kupitia Mkito.com unakuwa unauhakikia kuwa msanii analipwa kwa kazi yake na wewe pia unasaidia kuuendeleza muziki wa Kitanzania. 

    BC: Bila shaka kwenye biashara kama ya Mkito ambayo kwa ukaribu sana inahusiana na tekinolojia za mitandaoni,matatizo hujitokeza.Kuna mtu kushindwa kupakua[download] wimbo au nyimbo na kuna kero zingine nyingi.Mkito mnashughulikiaje matatizo kama hayo? Na kimsingi ni changamoto gani ambazo mnakabiliana nazo kila siku au mara kwa mara?  SM: Kuna maelfu ya aina tofauti za simu na computer ambazo kila siku zinatumika kupakua nyimbo Mkito.com. Sasa ni vigumu kuhakikisha kuwa tovuti itafanya kazi na kila aina ya simu lakini kwa kiasi kikubwa sana tumefanikiwa kutatua matatizo yanapojitokeza. Pia tunayo huduma kwa wateja ili mtu akipata shida anaweza kutuandika barua pepe au kupiga simu na tunamsaidia kutatua tatizo lake haraka.  

   BC: Kwa upande wa muziki, wasanii,wasimamizi [managers] wao nk nikikupa nafasi hii kuongea nao moja kwa moja ungewaambia nini au ungewapa ushauri gani kuhusiana na suala zima la muziki nk?  SM: Muziki ni biashara, wote tunafahamu hilo. Kwahiyo ninawakaribisha wasanii wote kuja kujiunga Mkito.com tuwasaidie kutangaza, kusambaza na kuuza muziki wao. Nafahamu kuwa wengi wanakuwa na wasiwasi kuwa wataibiwa – hili siyo kweli kwa upande wa Mkito.com, labda waliotutangulia. Kama nilivyokwisha sema kila kitu kinawekwa wazi na kama wewe ni msanii mwenye kazi nzuri basi kuwa na imani kuwa unaweza kujipatia kipato kizuri kutokana na mauzo ya muziki wako kupitia Mkito.com  

   BC: Shukrani sana kwa muda wako Sune. Nakutakia kila la kheri katika kazi zako   Asante sana. Lakini na mimi nikuulize wewe swali moja. Je, umeshapakua nyimbo ngapi mpaka sasa kupitia Mkito.com ili kuwapa support wasanii wa Tanzania? J BC: Mpaka leo,nimeshapakua nyingi.Sikumbuki idadi kamili. Lakini mchango wangu zaidi ni kuwajulisha watumiaji wengine [wasomaji wangu kwa mfano] juu ya kazi mpya za wasanii na wapi pa kuzipata. Asante kwa swali zuri Sune.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa mkoa wa Tanga kwenye uwanja wa Tangamano ambapo alitoa salaam za mwaka huu ambapo alisema CCM mwaka huu itaweka mkazo kwenye maadili ya Viongozi.
    Wananchi wakiwa wamefurika uwanjani Tangamano kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati wa kuwashukuru wananchi hao kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwezi Desemba 2014.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa mkoa wa Tanga kwenye uwanja wa Tangamano ambapo alitoa salaam za mwaka huuambapo alisema CCM mwaka huu itaweka mkazo kwenye maadili ya Viongozi. 
    Wananchi wakiwa wamefurika uwanjani Tangamano kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati wa kuwashukuru wananchi hao kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwezi Desemba 2014.  
    Baadhi ya Viongozi waliohudhuria mkutano Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa kushukuru wananchi kwa kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa January Makamba,Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Abdalah Kigoda na Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mheshimiwa Mboni Mgaza.
   Wananchi wa Tanga mjini wakimpa mkono wa kumuga Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kuwashukuru Watanzania kwa kuichagua CCM na kuwashukuru kwa imani yao kwa kutambua chama kinaweza kuongoza.
   Wananchi wakishangilia jambo 
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimkabidhi kadi ya CCM aliyekuwa mwenyekiti wa chama CUF-Pongwe,Bwa.Mbaraka Saad Mbaraka kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Tangamano mjini Tanga.
   Wakazi wa mji wa Tanga wakiwa wamejitokeza kwa wingi jioni ya leo katika uwanja wa Tangamano,kwenye mkutano wa hadhara,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alizungumza nao kuwashukuru kwa kufanya vyema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni nchini Kote
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwaaga  Wakazi wa mji wa Tanga waliojitokeza kwa wingi jioni ya leo katika uwanja wa Tangamano,mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alizungumza nao kuwashukuru kwa kufanya vyema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni nchini Kote.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Tanga,katika uwanja wa Tangamano jioni ya leo,baada ya aliyewahi Kugombea Ubunge Tanga Mjini kwa tiketi ya chama cha CHADEMA mnamo mwaka 2010,Kassim Omar Mbarak almaarufu Makubel,alipotangaza rasmi kuhamia chama cha CCM,baada ya kuvutiwa na hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza na wakazi wa Mji wa Tanga kuwashukuru kwa kufanya vyema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni nchini Kote.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Tagamano,mkoani Tanga,wa kuwashukuru wananchi walioichagua CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 2014 nchi nzima ambapo mkoa wa Tanga umekuwa wa pili kwa kushinda kwa asilimia 97. 
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira,Mh.Ummy Mwalimu akitafuta taswira 
   Mzee Yusuf akiwasalimu wakazi wa Tanga mjini ambapo anatazamiwa kutumbiza jioni ya leo kwenye uwanja wa Mkwakwani ikiwa kama ahadi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyoitoa wakati wa ziara yake ya mkoa wa Tanga mwishoni mwa mwaka 2014. 

older | 1 | .... | 435 | 436 | (Page 437) | 438 | 439 | .... | 1896 | newer