Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

WAFANYAKAZI WA PPF IDARA YA UENDESHAJI WAFANYA SHEREHE YA KUFUNGA MWAKA JIJINI DAR ES SALAAM JANA

0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Assumpta Maina Mallya akifungua sherehe iliyoandaliwa na idara yake kwaajili ya kupongezana kwa kazi za mwaka mzima, sherehe iliyofanyika katika hoteli ya Tiffany jijini Dar Es Salaam Jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka idara ya Uendeshaji wakimsikiliza Kwa Makini Mkurugenzi wa Idara hiyo wakati akifungua Sherehe ya Kupongezana kwa Wafanyakazi wa Idara hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Tiffany, Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Assumpta Maina Mallya akikata keki kwaajili ya Kuwarisha wafanyakazi wa Idara yake katika Sherehe ya kufunga mwaka iliyoandaliwa na Idara ya uendeshaji na kufanyika katika hoteli ya tiffany Jijini Dar Es Salaam.
Mbaruku Magawa Mratibu wa Ofisi za Kanda za PPF akimrisha Keki Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa PPF, Assumpta Maina Mallya wakati wa sherehe ya kumaliza Mwaka 2014 iliyofanyika Disemba 30, 2014 katika hoteli ya Tiffany.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Assumpta Maina Mallya akimlisha Keki mmoja wa Wafanyakazi wa Idara hiyo.
Muda wa Kufungua Shampeni ukawadiaBOFYA HAPA KWA MAPICHA ZAIDI»
Cheers kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Assumpta Maina Mallya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya Kufunga mwaka kwa idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Akimpa Zawadi Mkurugenzi wa Idara hiyo Assumpta Maina Mallya katika sherehe ya kufunga Mwaka iliyofanyika Katika Hoteli ya Tiffany Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa pensheni wa PPF (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya Pamoja na Kamati ya maandilizi ya sherehe ya kufunga mwaka kwa idara ya Uendeshaji iliyofanyika Katika hoteli ya Tiffany jijini Dar Es Salaam
Wafanyakazi wa Idara ya uendeshaji wa Mfuko wa PPF wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe ya kufunga mwaka 2014, sherehe iliyofanyika katika Hoteli ya Tiffany Jijini Dar Es Salaam jana.
 Muda wa Maakuli ukawadia na kila mmoja akajisevia
 
 Muda wa maakuli
Picha Zote na Josephat Lukaza wa http://www.josephatlukaza.com

TU UFUNGE MWAKA KWA KUJIHADHARI NA UHALIFU MTANDAO

0
0

Mwaka 2014 Umekua Wenye changamoto nyingi sana kwenye upade wa mitandao ambapo wahalifu mtandao walifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuitikisa anga ya usalama mitandao duniani kote ambapo walifikia kutamba kuwa wameshinda mapambano na wanausalama mitandao.

Kubwa zaidi ni uelewa mdogo wa watumiaji mtandao juu ya kujiweka salama kimtandao iliyo ambatana na wana usalama mitandao kuwa wachache sana katika ngazi ya kidunia huku baadhi ya mataifa kutotoa kipaumbele katika maswala ya usalama mitandao.

Aidha, Mengi katika jitihada yameweza kufikiwa ikiwa ni pamoja na Kikao cha funga mwaka cha tathmini ya hali ilivyokuwa kwa mwaka 2014 ambapo iliweza kutabiri hali ya uhalifu mwaka 2015 na kuweka mikakati ya dhati ya kukabiliana na hali hiyo kwa mwaka 2015 inayotegemewa kuwa na matokeo chanya. Kwenye hili unaweza kulisoma kwenye  “TAARIFA FUPI INAYOSOMEKA HAPA"

Wamarekani nao kupitia “US department of Justice” wameamua kuazisha kitengo maalum kitakachotoa msaada kwa mataifa yote duniani katika upande wa maswala ya usalama mitandao ikisisitiza itaangazia zaidi katika kuzuia matatizo kabla hayajatokea.

Tanzania nayo haikubaki nyumba kwenye hili, Tumeshuhudia warsha, semina, kongamano na mikutano mingine yenye malengo thabiti ya kukuza na kuongezea uwezo wa uelewa wa matumizi salama ya mitandao paoja kukuza uwezo wa kukabiliana na hali ya uhalifu mtandao nchini.

Sheria za usalama mitandao zimeweza kupaziwa sauti na kutoa matumaini makubwa kwa mwaka ujao, Huku vyombo vya habari kuw na jitihada ya dhati katika kampeni ya kutoa elimu na kuhabarisha jamii kuhusiana na janga la uhalifu mtandao linaloweza kuleta athari zaidi kwa taifa.

Nikumbushe tu, Uhalifu Mtandao umeendelea kuja kwa kasi ya juu na njia ambazo watanzania wengi wameweza kuwa waathirika. Kubwa nililoliona ambalo kueleke mwisho wa mwaka limeweza kukamata kasi ni pamoja na uhalifu aina ya “Phishing kama unavyo onekana kwenye picha nilizo tumiwa na baadhi ya raia wema ambapo wengi wameendelea kuathiriwa na uhalifu huu wa kimtandao.

Umakini zaidi unahitajika na tumalize mwaka kwa kuwa salama kimtandao.

WAKAZI WA TEMEKE NA VITONGOJI VYAKE WALIPOKEA VYEMA TAMASHA LA TUO8JANUARY, JIJINI DAR

0
0
  Hii ilikuwa ni picha ya pamoja ya wasanii na mashabiki waliojitokeza kuunga mkono tamasha hilo la bure ambalo lina lengo la kuhamasisha vijana kushiriki katika maamuzi yenye mustakabali wa nchi.
WASANII wa muziki wa kizazi kipya, jana walitoa burudani ya aina yake pamoja na elimu kwa vijana juu ya ushiriki wao katika masuala ya nchi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Wakiongowa na  Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ pamoja na Niki wa Pili, wasanii aidi ya 10 waliwapagawisha mamia ya mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja hivyo kupata burudani na elimu hiyo.
Akizungumza kabla ya kuimba nyimbo zake kali,Mwana FA akitumia tamasha hilo lililopewa jina la ‘Tuonane Januari’, aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuchagua viongozi wanaowataka.
“Vijana wenzangu.., tusisubili watu wengine watufanyie maamuzi.., ni sisi wenyewe tunatakiwa kuamua tunachokitaka, tushiriki kwenye masuala nyeti ya nhi.., kuna uchaguzi mkuu unakuja, vijana tuwe mstari wa mbele na tuchague viongozi tunaowataka,” alisema Mwana FA.
Mara baada ya kusema hayo, alianza kuimba nyimbo zake zinabamba kwa sasa ukiwemo, mfalme ambao uliwapagawaisha mashabiki wengi viwanjani hapo.
Mbali nma Mwana FA, pia Niki wa pili alipata mapoekzi makubwa viwanani hapo kwa nyimbo zake kali huku pia akisisitiza vijana kuchakua maamuzi sasa ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Wanamuziki wengine waliokonga nyoyo za mashabiki wao ni pamoja na Shilole, Fid Q, Ditto, Linah, Navy and kenzo, Dogo Janja, Madee, Chegge, Temba, mwasiti na Stamina, ambao nyimbo zao ziliwafanya mashabiki waliojitokeza kuimba nao sambamba.
Tamasha hilo pia lilifanyika katika mikoa ya Njombe na Morogoro ambapo linalengo la kutoa elimu kwa vijana juu ya kuwa karibu na kushiriki matukio muhimu ya nchi hususani uchaguzi mkuu ujao ambao utafanyika Oktoba mwaka huu.
PICHANI jUU:  Mkali wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA akitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga jana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Linah akiimba wimbo wake wa OleThemba,mbele ya mashabiki wake (hawap pichani),waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika kwenye viwanja vya sabasaba jana jioni mjini Morogoro. 
 Mtayarishaji nguli wa muziki wa kizazi kipya, Paul Mathyesse `P Funk' akichana mistari na msanii Fid Q katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar jana.
 Baadhi ya wakazi wa Temeke waliojitokeza kwenye onesho hilo la wazi lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar hapo jana.

Wasanii Chegge na Temba kutoka TMK Wanaume Family wakitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga
 Mkali mwingine wa kughani mitindo huru, Godzilla akitumbuiza jana jioni katika viwanja vya Mwembe Yanga,Temeke jijini Dar,kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika hapo jana.
Pichani kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.
Pichani kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.
 Wasanii Aika, na Nahreel wanaounda kundi la Navy & Kenzo wakitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYang,Temeke jijini Dar.
Baadhi ya wadau wakirekodi tukio muhimu
 Pichani Msanii Mwasiti akiimba wimbo wake wa serebuka mbele ya mashabiki wake huku shangwe za mayowe na vifijo zikiwa zimetawala uwanjani hapo  jana.
Wasanii Madee na Dogo Janja ( hayupo pichani) wakitumbuiza katika tamasha la Tuo8January lililofanyika katika viwanja vya MwembeYanga,Temeke jijini Dar.

MWANZA QUEENS WAICHAPA MARA QUEENS GOLI 6 KWA 1 KATIKA MECHI YA UZINDUZI WA WOMEN TAIFA CUP MCHEZO ULIOCHEZWA JIJINI MWANZA LEO

0
0
Baadhi ya Viongozi wa Mpira wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Viongozi wa TFF na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo Wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Mechi ya uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Women Taifa Cup kuanza katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.
 Kikosi Cha Timu ya Mwanza kikiwa tayari kukabiliana na Timu ya Musoma
 Kikosi cha timu ya Mara. 

Kikosi cha Timu ya Mara (jezi Nyekundu) wakisalimiana na Marefa wa mchezo huo tayari kwa Mtanange wa Women Taifa Cup kuzinduliwa leo jijini Mwanza kwa Kuzikutanisha timu za Mwanza na Mara.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Mh Jamal Malinzi akisalimiana na wachezaji wa timu ya Mara kabla ya Mechi ya Uzinduzi wa mashindano ya Mpira wa Miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Women Taifa Cup kuanza katika dimba la CCM kirumba leo Jijini Mwanza
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
  

RAIS KIKWETE ASHEREHEKEA MWAKA MPYA KIJIJINI MSOGA

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakijumuika na wananchi katika kuukaribisha mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa neno la shukurani kwa Mashekhe wa Bagamoyo na wananchi kwa kumuandalia hafla ya kumuombea dua katika mkesha wa mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiomba dua pamoja na Mashekhe wa Bagamoyo na wananchi wakati wa hafla ya kumuombea dua katika mkesha wa mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi wa jamii ya wamasai wanaoishi mkoa wa Pwani. Kiongozi mkuu wa jamii hiyo, Laiboni Tikwa Moreto (wa pili kushoto), Majaliwa Lihalei na Zuberi Tangono katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani. PICHA NA IKULU

SERIKALI YAIJIA JUU KAMPUNI YA STEPS KUSITISHA USHUSHWAJI WA BEI ZA FILAMU NCHINI

0
0

Shindano la Nyimbo za Amani katika tamasha la Sauti za Busara

0
0

Sauti za Busara ni tamasha lililojipatia umaarufu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, ni tukio la kila mwaka ambalo limefanikiwa kuwekwa katika kalenda ya matamasha Afrika. Sauti za Busara huwaleta watu pamoja kusheherekea muziki wa Afrika bila ya kujali dini, rangi, tamaduni na wala wanapotoka.

Busara Promotions inathamini na kushukuru Tanzania kama moja ya nchi zenye amani kuliko zote Duniani. Huku mwaka 2015 ukiwa ni mwaka wa uchaguzi Tanzania,  taasisi hii isiyo ya kiserikali inaamini ili maendeleo yaendelee bila kizuizi, tunahitaji kuimarisha umoja, heshima katika utofauti na kufanya kazi ili kutunza na kulinda amani hii yenye thamani. Kama mwanamziki mwenye tuzo Baaba Maalkutoka Senegal anavyosema, ‘Njia kuelekea amani ya dunia inapatikana katika muziki na uwezo wake wa kuleta watu pamoja.’

Huku likiwaleta pamoja wasanii tofauti na watazamaji kusherekea muziki wa Kiafrika, Sauti za Busara inahodhi shindano, kukiwa na zawadi ya pesa taslimu ambayo ni pesa ya kurekodi kwa washindi wa Nyimbo za Amani. Mkurugenzi wa Tamasha, Yusuf Mahmoud anasema “Sauti za Busara 2015 litaisaidia kukuza amani kwa kutumia muziki; ambapo vikundi 15 kutoka Tanzania, sambamba na vingine vya Kimataifa vitatoa sauti za ujumbe wa amani, umoja na mshikamano katika maonesho yao. Tunatarajia kwamba (sauti) hizi zitasikika kwa nguvu na uwazi”

Wasanii wa Kitanzania katika shindano hili ni pamoja na Leo Mkanyia, Msafiri Zawose, Mohamed Ilyas, Zee Town Sojaz, Ifa Band, Mgodro Group, Mabantu Africa na wengine wengi. Shindano la Nyimbo za Amani linadhaminiwa na Busara Promotions, kwa msaada wa Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam.

Shindano la Nyimbo za Amani litafanyika katika tamasha la Sauti za Busara Mji Mkongwe, Zanzibar kati ya saa 10:00 jioni siku ya Alhamisi tarehe 12 na saa 2:00 usiku siku ya Jumapili tarehe 15 Februari 2015. Shindano liko wazi kwa Wakazi wa Tanzania au Wazawa wa Tanzania. 

Vikundi vyote vya Kitanzania vinavyoshiriki kwenye tamasha vinaalikwa kutunga nyimbo maalum yenye dhima ya amani na umoja na kuifanyia onesho katika mida yao ya kutumbuiza katika tamasha. Fedha taslimu zitazawadiwa kwa ajili ya uzalishaji wa rekodi kitaalamu wa nyimbo zenye ubunifu: 4m/- TSh (Mshindi wa 1), 3m/- TSh (Mshindi wa 2) na 2m/- TSh (Mshindi wa 3) 

Maelezo ya Mwanasheria wa Uhamiaji kuhusu sheria mpya za uhamiaji nchini Marekani

0
0
Mwanasheria wa uhamiaji Fatmata Barrie akizungumza na wanaDMV kwenye mkesha wa mwaka mpya
Katika mkesha wa mwaka mpya (2014-2015), Jumuiya ya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia , kulikuwa na matukio mbalimbali.

Moja wapo lilikuwa ni maelezo ya mwanasheria wa uhamiaji Fatmata Barrie kuhusu maamuzi mapya ya serikali ya Marekani kwenye sheria za uhamiaji.
Karibu umsikilize

HAFLA FUPI YA BIRTHDAY YA MWANDISHI WA MICHEZO WA BINGWA,SHARIFA MMASI, ILIVYOFANA (JANUARY 1 2015)

0
0
Kutoka kushoto Deo Macha (ITV), Winnie Queen (Daily News), Sharifa Mmasi (Bingwa) na Fadhili Athumani (Mtanzania) katika hafla fupi ya kumpongeza Sharifa katika siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika Januari 01, mwaka 2015 mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mwandishi wa gazeti la Bingwa, Sharifa Mmasi (Kushoto)  akimlisha Keki, Rodrick Mushi anayeandikia gazeti la Mtanzania (magazeti yote yanachapishwa na kampuni ya New Habari (2006) Ltd)

TAARIFA YA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO KUHUSU MAANDALIZI YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

0
0
1
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akizunguza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya tume ya uchaguzi jijini Dar es salaam wakati alipozungumzia maandalizi ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura, kura ya maoni ya Katiba mpya na uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu, kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Julius Mh.Julius Mallaba.
2
Baadhi ya waadishi wa habari wakiwa katika kutano huo.
.................................................................................................................
Ndugu Waandishi wa Habari,Mkurugenzi wa Uchaguzi,Watendaji wa Tume, Mabibi na Mabwana.

Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisheni kwa mara nyingine katika Mkutano huu. Nawashukuru kwamba, pamoja na majukumu mengi mliyo nayo, mmeweza kuupa umuhimu wa pekee mkutano wetu huu na kuhudhuria kwa wingi. Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, nasema Ahsanteni na Karibuni sana.
Katika mkutano huu, Tume inalenga kutoa taarifa kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la majaribio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (Pilot Registration) kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) zoezi ambalo lilikamilika wiki iliyopita.

Ndugu Wanahabari,Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imepewa jukumu la kisheria Kuandikisha Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuliboresha Daftari hilo kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani. Kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni, Daftari hili la Kudumu pia litatumika katika Kura ya Maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa.

Ndugu Wanahabari; mtakumbuka kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa katika mchakato wa Maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia Mpya ya ”Biometric Voter Registration” (BVR) na mara kwa mara imekuwa ikiomba kukutana nanyi ili kuwapa taarifa kuhusu hatua mbalimbali ambazo Tume imekuwa ikizipitia.

Kwa kuwa Uboreshaji huu ulihusisha matumizi ya vifaa vya teknolojia ya kisasa, vifaa ambavyo vilikuwa havijawahi kutumika katika Uboreshaji nchini, tuliona si vyema kuagiza vifaa vingi kabla ya kuvifanyia majaribio. Zoezi la majaribio lilifanyika ili kuwa na uhakika kuwa vifaa hivi vya Biometric Registration vina uwezo wa kuandikisha Wapiga Kura katika mazingira ya nchi yetu.

 Zoezi hili liliangalia uwezo wa watendaji kutumia BVR katika uandikishaji na pia uwezo wa vyombo vyenyewe katika Software na Hardware kwenye uandikishaji. Katika zoezi hili tuliangalia changamoto zilizojitokeza ili kuzipatia ufumbuzi kabla ya kuanza Zoezi halisi la Uandikishaji wa nchi nzima.
 
Ndugu Wanahabari,Kama nilivyosema, Tume inakutana nanyi ili kuwapa taarifa kuhusu Tathmini ya Utekelezaji wa zoezi la Majaribio la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililofanyika kwa siku saba (7) katika Kata za Bunju na Mbweni katika Jimbo la Kawe, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam; Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja Sitini katika Jimbo la Kilombero Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro; na Kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni katika Jimbo la Katavi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Tume kwa namna ya pekee, inawashukuru sana Waandishi wa Habari kwa kujitokeza na kufuatilia zoezi hili la majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Waandishi wa Habari wamesaidia sana katika kuhamasisha Wananchi wa Majimbo husika kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Vilevile, Waandishi wa Habari wamesidia katika kutoa taarifa za maendeleo ya zoezi hili kitu ambacho kimesaidia kufanikisha zoezi hili.
Jumla ya BVR Kits 250 zilitumika katika Uboreshaji huo kwa mgawanyo ufuatao:- Halmashauri ya Kilombero BVR Kits 80, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele BVR Kits 80 na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni BVR Kits 90. Vituo katika Kata zote vilikuwa vinafunguliwa saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa 12.00 jioni.
Ndugu Waandishi wa Habari,Tume inapenda kuwafahamisha kuwa zoezi hilo la Majaribio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika majimbo matatu yaliyotajwa limefanyika na kukamilika kwa mafanikio makubwa. Changamoto zilizojitokeza hapa na pale zimetusaidia kupata ufumbuzi ambao utatusaidia wakati wa Uandikishaji wenyewe nchi nzima. Tunasema mafanikio makubwa kwa sababu matokeo ya jumla yanaonyesha kuwa idadi ya wapiga kura waliojitokeza kujiandikisha ilikuwa kubwa na kuvuka malengo ya waliokadiriwa kuandikishwa.

Mkoa wa Dar es salaam, Kata za Bunju Wapiga Kura 15,123 waliandikishwa kati ya 27,148 na Kata ya Mbweni Wapiga Kura 6,200 waliandikishwa kati ya 8,278. Takwimu hizi za waliondikishwa inatokana na makisio ya watu tuliyokuwa tumejiwekea kutokana na matokeo ya sensa mwaka 2012. Mkoa wa Morogoro Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja Sitini Wapiga Kura walioandikishwa ni 19,188 wakati makisio yalikuwa watu 17,790 na Mkoa wa Katavi Halmashauri ya Mlele kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni Wapiga Kura 11,210 waliandikishwa wakati makisio yalikuwa watu 11,394. Matokeo haya yanadhihirisha kuwa vifaa vya uandikishaji vilifanya kazi vizuri na hivyo vinaweza kutumika katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa nchi nzima.

Pamoja na mafanikio hayo, kama ilivyo kawaida katika majaribio yoyote kwani ndiyo lengo la kufanya majaribio, zilikuwepo changamoto kadhaa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo. Changamoto hizo zinaweza kuwekwa katika makundi makubwa matano kama ifuatavyo:-i. Matatizo yaliyotokana na ’Settings’ za BVR Kits;• Baadhi ya ”BVR Kits” zilitumia camera iliyo katika Laptop badala ya camera iliyowekwa kwa ajili ya kupiga picha.• Uchukuaji wa alama za vidole (Automatic Process settings) ilisababisha Mfumo kusimama (Crash).• Tatizo la kuchukua picha iwapo viwango vya ICAO vya ubora wa Picha havijafikiwa kama • 

Unrecognise face,• Unrecognise eye,• Stretch photo,• Un even light.• Uwepo wa Majina yenye ”apostrophe”.ii. Matatizo yaliyosababishwa na Software;• Fingeprint Scanner kusababisha Mfumo wa Uandikishaji kusimama (Crash) kutokana na SDK na za vifaa finger print scanner.• Kuharibika kwa baadhi ya file (File Corruption) kutokana na d11 ya finger print scanner.iii. 

Matatizo ya hardware; • Komputa (Laptop) Kupata Joto kutokana na Bati liliwekwa kuzuia kuibiwa Laptop kwa urahisi ambapo mahitaji kuwezesha mzunguko wa hewa ndani ya ”BVR Kit”.• FlashDrive ya pili (Drive G) kutoonekana hivyo kuhitaji kubadilishwa na kuwa SD card.• Uharaka wa uchukuaji alama za vidole ambapo ilibidi kufanya mabadiliko.iv. Matatizo ya lojistiki na matatizo ya Watendaji wa zoezi la Uandikishaji.• ”BVR Kit” kuchelewa kufikishwa katika Vituo.• Vurugu wakati wa uandikishaji ambao unahitaji Ulinzi kuwepo.• 

Baadhi ya ”BVR Operator” kutokuwa na uwezo au kuwa makini katika utumiaji wa ”BVR Kits” hivyo kuhitaji elimu zaidi kwa ”BVR Kit Operator”.• ”BVR Kit Operator” kubadili Kits kwa tatizo dogo linaloweza kutatulika kwa urahisi.• ”BVR Kit Operators” kutokuwa na uelewa wa matumizi ya ”Solar Panel” kwani baadhi ziliwekwa chini ya mti au kutogeuzwa kadri muda ulivyokuwa unakwenda. 

Mbali ya changamoto hizo zilikuwepo pia changamoto nyingine za kimiundombinu na kibinadamu. Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na Hali ya Hewa hususan katika jiji la Dar es salaam na Morogoro. Mtakubaliana nami kuwa pamoja na kuwa jiji la Dar es salaam kwa kawaida lina hali ya hewa ya joto lakini kwa takribani mwezi mmoja hivi uliopita kumekuwa na ongezeko la joto hali iliyosababisha hata baadhi ya vifaa vya kuandikishia hususan ’BVR Kits’ wakati mwingine kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa na hivyo kusababisha shughuli za uchapishaji wa Kadi za Kupigia Kura kuchelewa.  

Aidha, ushirikiano mdogo kutoka kwa Wananchi nao ulikuwa changamoto iliyosababisha zoezi hilo kwenda taratibu. Baadhi ya wananchi kushindwa kuzingatia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na BVR Kit Operators kutokana na uelewa duni kwani ilibainika pia kuwa bado kuna idadi kubwa ya wasiojua Kusoma na Kuandika. Hali hiyo ilifanya zoezi la Uchukuaji wa alama za Vidole (Fingerprint) na Utiaji wa Saini kuwa mgumu.

Kadhalika kumekuwepo na mwamko mkubwa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha. Hivyo, kulikuwepo na watu wengi sana katika vituo vya Uboreshaji wa Daftari hilo la Kudumu la Wapiga Kura. Changamoto zote zilizojitokeza kuhusiana na settings tuliweza kwa ushirikiano na watengenezaji wa vifaa hivyo, kuzipatia suluhisho wakati zoezi linaendelea. Pia chanagamoto za ’software’ nazo zimekwishapatiwa suluhisho. 

Changamoto kuhusu hardware zitarekebishwa wakati wa utengenezaji wa BVR Kits 7,750 ambazo zilikuwa hazijaanza kutengenezwa kusubiri matokeo ya zoezi hili la majaribio.Marekebisho hayo ya hardware pia yatafanywa katika BVR Kits 250 zilizoletwa kwa ajili ya majaribio. Changamoto kuhusu fedha na lojistiki zinaendelea kushughulikiwa kwa ushirikiano na Serikali. Kuhusu changamoto za Watendaji tunaendelea kuzishughulikia kwa kuhakikisha Watendaji tutakaowatumia wanakuwa na utaalam unaotakiwa kuziendesha BVR Kits hizo.

Ndugu Waandishi wa Habari,Napenda pia niongelee baadhi ya masuala yanayohusu zoezi la Uboreshaji wa Majaribio kwa ujumla. Kwanza ni vyema ieleweke wazi kuwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kwa ajili ya Kura ya Maoni ya Katiba Mpya, Mpiga Kura atatumia Kitambulisho cha Mpiga Kura alichopatiwa na Tume baada ya kuandikishwa katika mfumo huu tu na si vinginevyo. Vitambulisho vilivyotolewa katika uboreshaji huu wa majaribio ni vitambulisho halisi hivyo kila aliyejiandikisha katika zoezi hili la majaribio ni muhimu atunze kadi yake kwa ajili ya matumizi yaliyotajwa kwa kuwa taarifa zake tayari zimeingia katika Kanzi data ya Tume hivyo hataweza tena kujiandikisha kwa mara nyingine hata kama atabadilisha kituo cha kujiandikishia.

Ndugu Wanahabari,Pili, ni muhimu wananchi wakapata taarifa hizi kwa usahihi kwa vile wapo baadhi ya Watu wanaodhani kuwa kwa kuwa hilo lilikuwa ni zoezi la majaribio basi watakuwa na fursa nyingine ya kujiandikisha wakati wa zoezi la nchi nzima. Napenda nisisitize hapa kuwa kwa yeyote aliyejiandikisha katika zoezi hili, hatatakiwa tena kujiandikisha labda tu kwa yule ambaye atahitaji kubadilisha taarifa zake kutokana na sababu kama zilivyofafanuliwa na Tume.

Ndugu Wanahabari.Napenda nisisitize pia kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inayo dhamira ya dhati ya kukuza demokrasia kwa kuandaa na kuendesha chaguzi zake katika mazingira rafiki na wazi yatakayotoa fursa kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 kutumia haki yake ya kikatiba ya kuchagua viongozi wake. Tume itakuwa tayari kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali wa Uchaguzi kuhusu namna bora ya kufanikisha majukumu yake. Aidha, Tume itaendelea kubuni mbinu na mikakati itakayoboresha utendaji kazi wake.

Ndugu Waandishi wa Habari,
Kwa kumalizia, ninapenda tena kuwashukuru wote kwa kuhudhuria Mkutano huu. Tume mara zote imekuwa ikitambua mchango wa Vyombo vya Habari katika kufikisha ujumbe kwa jamii inayokusudiwa. Hali kadhalika, katika zoezi hili la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia BVR vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele katika kuufahamisha umma wa watanzania na kuhamasisha wale wote wenye sifa kujitokeza na kujiandikisha. Tume inatambua na kuthamini mchango wenu huo.

Kwa mantiki hiyo, na kwa mara nyingine natoa rai kwenu na Wadau wengine wa Uchaguzi kutoa taarifa zilizo sahihi na kuhamasisha Wananchi kushiriki katika zoezi hilo kubwa linalotarajia kuanza wakati wowote kuanzia sasa. Ni mategemeo ya Tume kuwa kwa kupitia kalamu na vipaza sauti vyenu taarifa hizi zitawafikia Wapiga Kura wetu na hatimaye wataweza kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha pindi muda huo utakapowadia.

Ndugu Wanahabari,
Nimalizie pale nilikoanzia, kwamba uandikishaji wa majaribio katika baadhi ya Kata za Majimbo matatu ya Kawe, Kilombero na Katavi umefanikiwa kwa kiwango kikubwa licha ya changamoto zilizojitokeza. Kutokana na changamoto hizo, vifaa vya BVR vitakavyo tumika katika zoezi la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini kote vitafanyiwa marekebisho stahili kwa vile 7,750 ambavyo bado havijafika nchini, pamoja na vile 250 vilivyotumika katika zoezi la majaribio.

Hivyo, hapana shaka kwamba, kama mambo yote yataendelea kama ilivyopangwa hadi sasa, mpango wa kuendesha Kura ya Maoni mwishoni mwa Aprili 2015, na Uchaguzi Mkuu October, 2015 kwa kutumia Dafti lililoboreshwa na vifaa vya BVR uko pale pale. Kama kawaida, ili kufanikisha ratiba hiyo, ushirikiano wa kila Mdau -Vyama vya Siasa, Vyama visivyo vya Kiserikali NGO’s, CSO’s, Serikali, Wananchi wote, Wapiga Kura na Wafadhili wote, Tume inaomba uendelee kwa kiwango cha juu. Hili likifanyika, Tume inaamini kuwa zoezi la Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu Octoba, 2015 utafanikiwa kwa amani na utulivu. Hayati Mwalimu J. K. Nyerere alisema, Inawezekana, Timiza Wajibu Wako.

Mwisho kabisa lakini muhimu sana, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi naomba kwa msisitizo kwamba zoezi likianza, wanachi nchini kote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha. Hii itawawezesha kwanza kupiga Kura ya Maoni na baadaye katika Uchaguzi Mkuu, Octoba, 2015. Kukosa kufanya hivyo ni kujinyima HAKI YAKO YA KIKATIBA YA KUCHAGUA VIONGOZI MNAOWATAKA.

MBUNGE WA MOROGORO MJINI MH ABOOD ATOA MILION 11 KUTATUA KERO YA MAJI MKUNDI MOROGORO

0
0
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akizindua Tawi la CCM la Wajasiriamali Bodaboda na Mama lishe lililopo Mgulu wa Ndege Kata Ya Mkundi Manispaa ya Morogoro.Mara Baada ya Kuzindua Tawi Hilo Mh Abood Aliongea na Wanachama wa Tawi Hilo Kisha Kuwaelekeza Kujiunga Kwenye Vikundi vya Wajasiriamali Yeye Atakuwa Tayari kuwawezesha Mitaji ya Kufanya Shuguli za Kujiletea Maendeleo.

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Meza Kuu Sambamba na Katibu wa CCM Kata Ya Mkundi tayari Kusikiliza Kero zinazowakabili wakati wa Kata hiyo,ambapo walimwambia Wanakabiliwa na Kero Kubwa ya Umeme,Maji na Barabara.

Aidha Mh Abood ametoa majibu Kuhusu Kero hizo na kusema kuwa Serikali imeiweka Kata hiyo Kwenye Bajeti ya Serikali ya Mwaka huu .Kuhusu Maji Mh Abood alitoa Shilingi Milioni 11 Kwa jili ya Kununua Vifaa vya Kuwezesha Kufikisha Maji katika eneo la Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi.Pia Alitoa Shilingi Milion 2 kwa ajili ya kuhakikisha barabara zote za Kata hiyo zinachongwa.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi Jimbo la Morogoro Mjini Akisoma Risala yake Kwa Mbunge wa Jimbo Hilo Mh Aziz Abood.
  
Mmoja wa Wakazi   wa Kata ya Mkundi waliojitokeza Kwa Wingi Kwenye Ziara ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Akieleza Kwa msisitizo Kero Kubwa Inayowakabili wakazi wa Kata Hiyo                   









  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiandika Baadhi ya Keo ambazo wananchi wa Kata ya Mkundi walimweleza wakati wa Ziara yake ya kutembelea Kata za Jimbo la Morogoro Mjini.

 Wakazi wa Kata ya Mkundi wakimsikiliza kwa Makini Mbunge wao

Wakazi wa Kata ya Mkundi wakimshangilia Mh Abood mara Baada ya Kutatua kero Kubw ya kata hiyo tatizo la Maji. 
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akijibu Baadhi ya Kero zinazowakabili wakazi wa Kata ya Mkundi.

KIKUNDI CHA VIJANA WAJIITAO PANYA ROAD WAFUNGA MITAA NA KUZUA TAFRANI KUBWA JIJINI DAR.

0
0
Sikiliza hapo chini taharuki ya panya Road ilivyozua tafrani na hofu kubwa kwa maeneo mbalimbali ya wakazi wa jiji la Dar. Baadhi ya Wadau walikumbana Live na rabsha hiyo ya Panya Road
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar,Kamanda Kova akitoa ufafanuzi wa habari za taharuki katika vyombo vya habari hususani televisheni,kuhusiana na sakata la kundi la Vijana wajiitao Panya Road,amesema suala hilo lilikuwa dogo,lakini baadhi ya watu wamelikuza na kupelekea hofu kubwa kwa Wananchi ''Jiji mpaka sasa liko salama na wananchi watulie wasiwe na hofu kwa sababu jeshi la Polisi liko imara kuhakikisha amani inakuwepo ya kutosha,na hao vijana hawawezi kulishinda Jeshi la Polisi'',alisema.Alisema Wananchi waondoe hofu waendelee na shughuli zao kama kawaida.
 katika hali isiyo ya Kawaida na ya kuogopesha,kumeibuka taharuki kubwa usiku huu kwa Wakazi wa maeneo mbalimabali ya jiji la Dar,ikiwemo,Sinza,Kinondoni,Mwananyamala,Mabibo,Magomeni,Manzese,Kagera na Mburahati kwa kile kinachoelezwa kuwa vijana waitwao Panya Road wamevamia maeneo hayo na kuwajeruhi watu kwa vitu vyenye ncha kali,visu na mapanga na kuwapora vitu (mali zao) walivyokuwa navyo,kama vile haitoshi baadhi yao wamevunjiwa vioo vya magari yao.
Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa vijana hao waitwao Panya Road wameibuka na kufanya uhalifu huo mara baada ya tukio la Mwenzao mmoja kudaiwa kuuwawa na Polisi.

Aidha Chanzo hicho kimebainisha kuwa baada ya taarifa kusambaa kwa haraka,kimeeleza kuwa Jeshi la Polisi limeingia kazini kuwasaka watuhumiwa hao walioibua tafrani kubwa usiku huu. 

Wadau tutazidi kuwaletea taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo kadiri ya zitakavyokuwa zikipatikana.

RIDHIWANI KIKWETE AANZA ZIARA YA KIKAZI KATIKA VIJIJI 40 CHALINZE

0
0
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni. Ridhiwani yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea vijiji 40 jimboni humo.Pia Ridhiwani alishauri shule hiyo yenye majengo yaliyojengwa tangu 1952 ifungwe ili kuepusha maafa zaidi hadi itakapojengwa upya.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu, ambapo aliwapongeza wananchi kuchagua viongozi wa Serikali ya Vijijini kutoka CCM.
 Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa uzinduzi wa Kisima cha Maji kilichojengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo kwa gharama ya sh. mil. 13.
 Ridhiwani akinunua ndizi na kuzigawa kwa watoto katika Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa ziara yake jimboni Chalinze jana.
Watoto wakigawiwa ndizi na Ridhiwani.
 Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja ambapo aliwaahidi kutatua tatizo la mawasiliano ya simu kwa kuwapelekea mnara
 Sehemu ya umati wa wananchi uliohudhuria mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja
 Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Mduma, Kata ya Kibindu, ambapo aliwahidi  kuboresha barabara na mawasiliano ya simu
Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika Kijiji cha Kwa Mduma wakati wa ziara yake katika jimbo lake la Chalinze, Kata ya Kibindu

2003 LAND ROVER FREE LANDER INAUZWA

0
0


2003 LAND ROVER FREE LANDER: T373 bas


Make: Land Rover
Model: Freelander

Year: 2003

Price: TZS 7,000,000/-
Negotiable: Yes
Kilometers: 78,540
Fuel: Petrol

Colour: Blue

Transmission: Automatic
Four Wheel Drive: No
Vehicle Current Location: Dar es Salaam
Contacts: 0784587088 & 0712155221

Vehicle is in Good Condition, its Blue in Color...has a RAV 4 3S Engine with Gear Box



Gari lipo katika hali nzuri na linatembea, pia limefungwa injini ya RAV 4 3s Engine.

MIMI SI MENEJA TENA WA ROSE MUHANDO-MSAMA

0
0


HATIMAYE Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, ameibuka na kutamka yeye si Meneja wa malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando akisema amekuwa akishirikiana naye katika mazingira ya kawaida kama ilivyo kw
a waimbaji wengine.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msama kwa vyombo vya habari jana, yeye akiwa mlezi wa waimbaji wote wa muziki wa Injili, amekuwa akishirikana nao kwa karibu kutokanana nafasi yake katika huduma hiyo ya uimbaji kwa kipindi cha miaka 15.

Msama, mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini kutokana na kuandaa matukio ya muziki huo kama Tamasha la Pasaka, uzinduzi wa albamu na Tamasha la Krismas, alisema ameamua kutoa tamko hilo kutokana na malalamiko ya muda mrefu ambayo amekuwa akipata juu ya Rose. 

“Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi ikiwemo kutoka kwa viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji, kwamba pengine nimekuwa nikimzua Rose (Muhando) katika mtamasha wanayomualika na kushindwa kutokea.

“Lakini, naomba watumishi wa Mungu wanielewe katika hili, sipokei mialiko wala simzuii Rose. Mimi ninapokuwa na matamasha, nimekuwa nikimualika kama wafanyavyo wengine.

“Nimekuwa nikimlipa kiasi cha fedha anachotaka na hakuna zaidi, hivyo mimi sio Meneja wake,” alisema Msama katika taarifa hiyo na kuongeza:


“Agosti mwaka huu, kampuni yangu ilidhamini uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu, haikuwa na maana kwamba ni Meneja wake. 

“Nilimualika uzinduzi wa albamu ya Uko Hapa ya msanii John Lissu Oktoba mwaka huu, nilimlipa fedha, lakini hakutokea kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wengine ambao wamekuwa wakilalamikia tabia hiyo,” alisema Msama.

“Pia wiki iliyopita nilikuwa na Tamasha la Krismasi tulikubaliana aje katika maonesho hayo, lakini hakutokea na tulishamlipa,” alisema Msama kwa masikitiko na kuongeza kuwa amemsamehe na anamuombea kwa Mungu aweze kubadilika.

Alieleza kuwa hana tatizo na mwimbaji huyo, wala hana ugomvi naye, lakini amekuwa akipata taabu kutoka kwa baadhi ya wachungaji pale Rose anapoalikwa halafu hatokei na inaonekana yeye ndiye amemzuia.

“Sijawahi kupokea mialiko kwa niaba ya Rose, kila kitu anafanya mwenyewe, hivyo ni vyema wadau wakafahamu hilo,” alisema Msama na kusema angekuwa mwepesi wa kulalamika, angeshafanya hivyo muda mrefu dhidi ya Rose.

Aidha, Msama amekana kuhusiana na madai ya Rose kutumia dawa za kulevya na kusisitiza kuwa hajawahi kumuona akijidunga kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti na kuongeza kama ikiwa ni kweli, hilo pia ni suala binafsi.

“Baadhi ya vyombo vya habari vinaandika ni mjamzito, nafikiri pia hayo ni mambo yake binafsi na hakuna mtu mwenye haki au uhalali wa kuhoji hilo.Yule ni mtu mzima na mwenye kujielewa,” alisema Msama.

Rose ni mwimbaji mahiri wa muziki wa injili nchini aliyejipatia sifa ndani na nje ya ukanda wa Afrika Mashariki ambaye mwishoni mwa mwaka 2013, alisaini mkatabawa kufanya kazi na kampuni ya muziki ya Sony ya Afrika Kusini. 

Miongoni mwa albamu zilizompa umaarufu Rose kiasi cha kuwa alama ya mafanikio ya muziki wa injili nchini, ni ‘Uwe Macho,’ Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa, Kitimutimu, ‘Mungu Anacheka’ na Wololo na Kamata Pindo la Yesu aliyoachia hivyo karibuni.

Diamond Platnumz visits the Kigali Memorial Centre at Gisozi

0
0

The Tanzanian singer Diamond Platnumz has who is in Rwanda for two forthcoming concerts, visited the Kigali Genocide Memorail centre to have a glimpse of what happened in  1994 when the genocide against the Tutsi was committed.
Diamond and Zari  seeing one of the historical archaives displayed in the Kigali Genocide Memorial centre 
He visited different rooms where historical archives are displayed for visitors and he deposed flowers to the tombs where thousands bodies of innocent Tutsis are resting in peace.The singer  Diamond has expressed his swallow feelings about what he saw and his lover Zari Hassan has cried so much due to what she saw at the Kigali Genocide Memorial centre. During a press conference that took place after the visit, Diamond urged Rwandan artists to work hard and reach beyond Rwandan borders as to become more popular and earn more money.
During  the Press conference  
During the Press conference
He urged local artists to be more professional and reach high 
He urged local artists to be more professional and reach high
As they arrived at Kigali Genocide memorial centre  
As they arrived at Kigali Genocide memorial centre
Listening to the explanations of the tour guide Listening to the explanations of the tour guide
Heading to another room 
Heading to another room
As they saw images displaying the horror  committed during the 1994 genocide the couple become horrified  
As they saw images displaying  how the 1994 genocide was committed,  the couple become horrified
The wife fell into tears  
The wife fell into tears
He wrote into the books for visitors  
He wrote into the books for visitors
After visiting the centre, the couple went back in the Hotel where they are accommodated  
After visiting the centre, the couple went back in the Hotel where they are accommodated.

Rais Kikwete ateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya

0
0
Bwana George Mcheche Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya.


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Rais ateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

3 Januari, 2015
 

RIDHIWANI KIKWETE KUHARAKISHA MAENDELEO CHALINZE

0
0
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika Kijiji cha Changarikwa wakati wa ziara ya kikazi pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kuchagua viongozi wa Seikali ya Kijiji wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.CCM imepata ushindi wa Vijiji vyote katika 74 katika jimbo hilo.
 Ridhiwani akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika kijiji hicho ambapo aliwataka kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa ama sivyo vijiji vitageuka jangwa.
 Mkazi wa Kijiji cha Kwaluhongo, Dustan Sangi akiuliza swali kwa Mbunge wake Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano  uliofanyika kijijini hapo
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwaluhonbo ambapo alijibu maswali mbalimbali ya wananchi kuhusiana na kero mbaalimbali walizonazo pamoja na suluhisho

 Ridhiwani akizungumza jambo na Khamis Ibrahim baada ya mkutano kumalizika katika  Kijiji cha Kwaluhongo, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya Mbwewe, Chalinzi, wilayani Bagamoyo jana.

 Mama mkazi wa Kijiji cha Changarikwa akiuliza swali kwa mbunge kuhusu tatizo la kijiji hicho kutokuwa na Zahanati
 Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo,Kombo Kamote akiwafunda viongozi wapya wa Serikali ya Kijiji cha Changarikwa ambapo aliwataka kujali sana maendeleo ya wananchi badala ya maslahi yao binafsi.
 Wazee wakisikiliza kwa makini wakati Ridhiwani akihutubia katika Kijiji cha Changarikwa, Kata ya Mbwewe.
 Ridhiwani akiifariji familia ya marehemu Jangili Shaban alipokwenda kuhani msiba baada ya kumalizika kwa mkutano katika Kijiji cha Changarikwa
 Mzee Athuman Mnemwa akielezea mbele ya Mbunge wake Ridhiwani Kikwete jinsi Kijiji cha Kwang'andu kinavyoteseka na kero ya maji.
 Mwanahawa Habib akielezea mbele ya Ridhiwani jinsi wakazi wa kijiji hicho wanavyonyapaliwa na Daktari na wauguzi wa Zahanati ya kijiji hicho
 Mzee Athuman Kisuli akisisitiza umuhimu wa kupelekewa maji katika Kijiji cha Kwang'andu
 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu akiwasalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwang'andu ambapo aliahidi kusaidiana na Ridhiwani kutatua tatizo la maji linalowakabili wananachi wa kijiji hicho
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo na kuahidi kutatua kero mbalimbali ikiwemo ya maji katika kijiji hicho cha Kwang'andu, Kata ya Mbwewe
 Mwananmke aliyejitangaza kuwa anaishi na virusi vya Ukimwi Pili Mbwana akiomba mbunge Ridhiwani kusaidia kuwasaidia kupata mikopo  watu wanaoishi na VVU katika Kijiji cha Kunduchi Kata ya Mbwewe ili iwasaidie kuondokana na umasikini walio nao
 Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kijiji kipya cha Kunduchi wakati wa ziara yake atika Kata ya Mbwewe jana
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao

 Ridhiwani akizungumza na Pili Mbwana anayeishi na virusi vya Ukimwi ambapo aliahidi kumsaidia jinsi ya kupata mkopo
Ridhiwani akiteta jambo na Mzee Suleiman Kadagala baada ya kumalizika kwa mkutano huo

MISS SINGIDA 2014 DORICE MOLLEL ATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA WODI YA WATOTO NJITI

0
0
DSC03176
Miss Singida 2014 Dorice Mollel akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa mjini Singida. Miss Singida huyo ambaye mwaka jana alikuwa pia mshindi wa kwanza Miss kanda ya kati na kushika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema ametoa msaada huo kwa sababu na yeye alizaliwa mapacha njiti.

Na Nathaniel Limu, Singida
JUMLA ya watoto 284 hadi 300, huzaliwa kila mwaka katika hospitali ya mkoa iliyopo mjini Singida wakiwa hawajatimiza umri wa kawaida wa kuzaliwa (njiti).

Kati ya watoto hao,inakadiriwa 60 hadi 83 hufariki kutokana na sababu mbalimbali kila mwaka ikiwemo ya tatizo la kupumua.
Hayo yamesemwa na kaimu mganga mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida,Dk.Daniel Tarimo,wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba vitakavyotumika kwenye wodi ya watoto njiti katika hospitali ya mkoa mjini hapa.

Kuhusu watoto hao njiti wanaofariki dunia,Dk.Tarimo alisema vifo vingi vinachangiwa na baadhi ya akina mama wajawazito kujifungulia nyumbani mahali hakuna wataalamu wa huduma ya afya.

“Watoto wa aina hii kwa kawaida wanakuwa na matatizo ya kupumua.Sasa mama akijifungulia nyumbani,wakiwa njiani kukimbiza watoto/mtoto wa aina hiyo hospitalini,mtoto/watoto husika hupata tatizo la kupumua linalopelekea vifo vyao”,alifafanua zaidi Dk.Tarimo.
DSC03187
Miss Singida 2014 Dorice Mollel akimkabidhi Kaimu Mganga Mfawidhi Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Singida, Dk.Daniel Tarimo, msaada wa vifaa mbali mbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwa wodi ya watoto njiti.

Kaimu mganga huyo,alitumia fursa hiyo kuwakumbusha akina mama wajawazito kujenga utamaduni wa kuanza mapema kuhudhuria kliniki ili endapo watagundulika wana tatizo,waweze kuhudumiwa mapema kabla tatizo husika halijaleta madhara makubwa.

Aidha, Kaimu Mganga Huyo Mfawidhi,amemshukuru Miss Singida 2014 Dorice Mollel kwa kutoa msaada huo wa vifaa tiba kwa ajili ya wodi ya watoto njiti.Amewataka wadau wengine kuiga kitendo hicho.

Kwa upande wake Miss Singida 2014, Dorice Mollel alisema amechukua hatua hiyo ya kusaidia watoto njiti kwa madai kuwa na yeye alizaliwa akiwa njiti pacha na kwa vyo vyote kuna watu walijitolea kuwasaidia katika kipindi hicho.
DSC03191
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida, Dk.Daniel Tarimo, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba vilivyotolewa msaada na Miss Singida 2014 Dorice Mollel kwenye wodi ya watoto njiti hospitali ya mkoa wa Singida.

Aidha,alisema hatua hiyo ni kuiunga mkono serikali katika kupunguza vifo vya watoto wachanga nchini.Ametaka wadau wengine kusaidia kundi hilo la watoto ili kuwapunguzia matatizo mbalimbali yanayowakabili wakati wa ukuwaji waoa.

Kwa mujibu wa Miss Singida 2014, Mollel baadhi ya vifaa hivyo ni suction mashine-manual na electronic na mizani vyote vina thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni.Mollel pia ni Miss kanda ya kati na alikuwa mshindi wa tatu katika shindano la kusaka Miss Tanzania la mwaka jana.
DSC03207
Miss Singida 2014 Doris Moleli,akimwangalia mtoto mchanga aliyelazwa kwenye wodi ya uzazi kawaida iliyopo kwenye hospitali ya mkoa mjini Singida.
DSC03195
Miss Singida 2014, Dorice Mollel akiangalia watoto njiti pacha waliolazwa katika hospitali ya mkoa mjini hapa.(Picha na Nathaniel Limu).

YAMOTO BAND LIVE KWA MARA YA KWANZA KWENYE JIJI LA LONDON.

0
0
 
 Confirmed...21Feb2015..Yamoto! Yamoto! Yamoto Band Live in the UK For the first Time Ever...When we Say Live, we mean 

Live with Full Band & Dancers...
This is one show that's not to be Missed... Sponsored by @officialjestinageorgeblog @bongodeejays@zuriihouseofbeauty
 Zurii House of Beauty CEO akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa yamoto band Maromboso na Aslay  baada ya makubaliano ya kuwadhamini band hiyo kuja  kufanya show yao jijini London @maromboso @aslayisihaka
 Zurii House of Beauty CEO akiwa kwenye picha ya pamoja na mameneja wa yamoto band
 It's gonna be bigger and better! UK & Europe people Save the Date. Their Live Performance is a must see..If you love live music.
Make sure you get your tickets mapemaaaa...Hili ni Bonge la show kuwahi kutokea na watoto wameahidi kuweka historia


Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images