Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 433 | 434 | (Page 435) | 436 | 437 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Miss Tanzania namba mbili 2006, Mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegelo, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. 
  Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegelo, akimpa zawadi ya ndala mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti.
  Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegelo, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma.

  MISS Tanzania namba mbili 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za kibongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’,  leo ametoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Kulea Yatima cha Extrem kilichopo  Tandare kwa Bi Mtumwa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  Mrembo huyo ambaye pia ni mkurugenzi  wa kampuni ya  Kidoti inayojihusisha na masuala ya urembo, alitoa msaada huo kama zawadi yake ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya kwa watoto hao kama sehemu ya kuwafariji ili nao kujiona wako sawa na wengineo wanaioshi nawazazi wao.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Jokate alisema kuwa ameguswa na kituo hicho ambacho huwa hakikumbukwi na wahisani kutokana na mazingira ya eneo hilo.

  “Nimefika hapa kutoa msaada kama sehemu ya kuonyesha ninavyoguswa na jamii ya watoto kama hawa, lakini pia nikiwa na lengo la kuwafariji ili nao kujiona ni sehemu ya jamii ya Watanzania,” alisema.

  Kidoti alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wenye uwezo, kampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii kwani nao wana haki ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine.

  Msaada aliokabidhi kwa ushirikiano na kampuni ya Raibow Shell, ni mchele, unga wa sembe, sabuni, jozi za viatu vyenye nembo za Kidoti.

  Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, mlezi wa watoto hao, Mwamvua Jumanne, alitoa pongezi kwa Kidoti na kuwasihi wengine kuiga mfano wa mrembo huyo kusaidia makundi maalum.

  Akielezea changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mwamvua alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma elimu ya msingi na sekondari, gharama za matibabu pamoja na kukosa watu wa kuwatembelea ili kuwafariji.


  0 0

  index
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewatimua wanachama wake 42 wakiwemo wagombea walioshindwa kupita kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa hivi karibuni.

  Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, kutimuliwa kwa wanachama wake hao ni hatua ya chama hicho kujisafisha kutokana na kile kinachodaiwa kwamba baadhi ya wagombea hao wanatuhumiwa kufanya hujuma wakati wa mchakato wa uchaguzi serikali za mitaa, vitongoji na vijiji uliofanyika Desemba 14, mwaka huu.

  Akitangaza uamuzi huo mjini humo, Katibu wa Chadema Jimbo la Korogwe Mjini, Ezekiel Mbwilo alisema wahusika waliotimuliwa uanachama wanatuhumiwa kwa kukubali vitisho na wengine kurubuniwa kwa fedha za wapinzani wao, hatua iliyowalazimu kwenda kuondoa majina yao katika hatua za mwisho kuelekea kwenye kinyang’anyiro hicho.

  “Tuligundua kuwa baadhi ya wahusiska walijihusisha na hujuma mbalimbali dhidi ya chama chetu, ikiwamo kukubali kupewa fedha na wapinzani wao ili wajiondoe. Tangu awali, tulishakubalina kwamba ikibainika watu waliofanya hujuma tutawatimua kundini na hapa ndipo tunahitimisha lile tulilokubaliana,” alisema.

  Mbwilo alitaja maeneo wanayotoka wanachama hao waliotimuliwa na idadi yao kwenye mabano ni Kwamsisiwatu (6), Mahenge (10), Kitifu (25) pamoja na mmoja kutoka Manundukati ambaye alidai kwamba mhusika huyo aliamua kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi ukiwa katika hatua za mwisho baada ya kurubuniwa na wapinzani wa chama hicho.

  Akizungumzia vitisho alivyodai vilitolewa baadhi ya wanachama wa vyama vingine dhidi ya wagombea wa Chadema, Mbwilo alisema tayari amewasilisha taarifa hizo kwenye vyombo vya usalama na katika jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi.

  0 0

  *Spice Modern Taarab kuendeleza makali
   
  NA ANDREW CHALE.
  USIKU wa ‘Old Is Gold’ na Spice Modern Taarab, unatarajiwa kurindima  usiku wa Desemba 28, ndani ya   ukumbi wa Safari Carnival uliopo Mikocheni B, jijini Dar es Salaam.
   
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, mwandaaji na mdhamini wa onyesho hilo,  mashabiki  wa Old Is Gold  watapata burudani ya aina yake katika kiota hicho cha burudani kila jumapili kukumbushana enzi.
   
  “Kwa kiingilio cha sh 5,000 tu, wadau watafurahia shoo kabambe kutoka kwa Spice Modern Taarab ndani ukumbi wa Safari Carnival. Huku wadau wakijumuika pamoja na kubadilishna mawazo” alisema Asia Idarous.
   
  Asia Idarous alilielezea kundi hilo ni la magwiji wa muziki huo wa mwambao ikiwemo kupiga nyimbo za taarab za zamani na zile za sasa.
   
  Onyesho  ni la kila siku kwenye ukumbi huo huku likidhaminiwa na Fabak Fashions (Mikocheni), Safari Carnival,  wadau wengine wakiwa ni pamoja na Clouds tv, Michuzi Media Group  wengine wengi.

  0 0


   Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo (Picha na Bashir Nkoromo theNkoromo Blog)
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
   
  Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.

  Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.

  Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.

  Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang’anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.

  “Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto”, alisema Nyalandu
  Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM”, alisema.

  0 0

  NesiWangu Show ni kipindi kinachokusudia kuongeza mwako katika uwanja wa Afya, upatikanaji wa huduma zake na elimu-afya kwa jamii.

  Katika kipindi hiki, tunazungumza na Mkurugenzi wa Jenga Tanzania Foundation, Nassor Basalama anayezungumzia kuhusu kipimo cha Malaria ambacho Jenga Tanzania Foundation inapanga kukisambaza bure kwa watu wa kipato cha chini nchini Tanzania.
  Karibu uungane nasi

  0 0

  Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza(kushoto) akimkabidhi Jezi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi kwaajili ya Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Taifa Women Cup yanayotarajiwa kutimbua vumbi tarehe 1 January 2015.
  Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
  Mkurugenzi wa makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza amkabidhi jezi Rais wa TFF, Mh Jamal Malinzi kwaajili ya michuano ya Mpira wa Miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Taifa Women Cup ambayo yanatarajiwa kutimua Vumbi tarehe 1 Januari 2015 huku Mechi ya Uzinduzi ikiwakutanisha timu kutoka Mwanza na Musoma mechi ambayo itapigwa katika Dimba la CCM Kirumba, Jijini Mwanza.
  Kampuni ya Proin Ndio wadhamini wakuu wa mashindano haya ambayo yanatarijiwa kutimua Vumbi Mnamo tarehe 1 Januari 2015. Proin Imeamua kudhamini mashindano hayo kwa lengo la Kuinua vipaji vya Mpira wa Miguu kwa Wanawake ambapo baadae wachezaji bora wataweza kuingia katika Timu ya Taifa ya Wanawake.
  Vilevile Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mh Jamal Malinzi amewataka pia makampuni mengine Kujitokeza katika Kudhamini Mashindano haya yanayotarajiwa kuanza tarehe 1 Januari 2015 kwa lengo la Kuweza kuinua vipaji vya Mpira wa Miguu kwa Wanawake huku pia wakipata fursa ya Kujitangaza kibiashara kwasababu mpira wa miguu ni mchezo ambao unapendwa sana na watu wengi hivyo ni dhahiri kabisa Kuwa Makampuni mengi yakidhamini mashindano haya yataweza kufikia malengo yao kwa kujitangaza.

  0 0
 • 12/29/14--04:36: DASLAM YETU YA LEO..!
 •  
   
  0 0

  Wakazi wa kijiji cha Mzuri -Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika mradi wa kitalu cha miti moja ya mradi ulioibuliwa na walengwa wenyewe kupitia PWP unaoendeshwa na TASAF ambapo walengwa hulipwa fedha kwa kazi hiyo.
  Kitalu cha miti kilichotayarishwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia mpango wa ajira za muda wa TASAF wenye lengo la kuwaongezea kipato kwa kuwalipa kulingana na ushiriki wao katika kazi hiyo.
  Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini  unaotekelezwa na TASAF wakishiriki katika kazi za kutayarisha kitalu cha miche ya miti katika kijiji cha Mzuri -Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja.
  Mfuko ya miche ya miti iliyotayarishwa na wakazi wa kijiji cha Mzuri Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya kujaza udongo ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa ajira za muda PWP unaotekelezwa na TASAF.

  Kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini -Makunduchi mkoa wa kusini Unguja ambayo ni moja ya mkakati wa TASAF wa kuwaongezea kipato walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia ajira ya muda PWP.
  Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na TASAF katika kijiji cha Kijini Makunduchi mkoa wa kusini Unguja wakishiriki katika kazi za ujenzi wa barabara kupitia mpango wa ajira za muda PWP.
  Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini katika eneo la Kijini Makunduchi mkoa wa kusini Unguja wakiwa katika harakati za ujenzi wa barabara kupitia mpango wa ajira za muda PWP kupitia TASAF.
  Barabara inayojengwa kupitia mpango wa ajira ya muda PWP ambapo walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini kupitia TASAF wakiwa katika eneo la mradi wa barabara yenye urefu wa kilometa Moja .

  Walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wameanza utekelezaji wa miradi ya ajira za muda na kisha kulipwa ujira katika miradi wanayoibua kwenye maeneo yao .
  Walengwa wa vijiji kadhaa vilivyoko kwenye Mpango huo kikiwemo kile cha Mzuri na Kijini vilivyoko katika eneo la Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wameanza kutengeneza barabara yenye urefu wa zaidi ya kilometa moja na vitalu vya miche ya miti ya asili na matunda katika eneo lao na kisha kulipwa fedha chini ya utaratibu ulioandaliwa na TASAF ambao ni moja ya mkakati  wa kuwaongezea kipato walengwa na kupambana na umaskini.

  Akizungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo Sheha wa eneo hilo Bwana Mwita Masemo Makungu amebainisha kuwa mpango huo umeitikiwa vizuri na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika eneo hilo na kuwa jitihada hizo za TASAF zimeamsha ari ya wananchi kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao na kupunguza kero ya barabara iliyokuwa inawakabili.

  Hata hivyo Bwana Makungu amesema pamoja na ushiriki wa wananchi kwenye kazi hiyo kupitia mpango wa ajira za muda bado wananchi hao wanakabiliwa na tatizo la vifaa na utaalamu hususani katika ujenzi wa barabara ambao unahitaji vifaa vizito ambavyo havipo kwenye maeneo yao na hivyo kuomba serikali kuona namna ya kukamilisha kazi hiyo.

  Zifuatazo ni baadhi ya picha za walengwa wa PSSN katika wilaya ya Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi kupitia ajira za muda PWP.

  0 0

    Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akipigapicha ya pamoja na familia ya Katibu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja leo.
    Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kulia) akisalimiana na Katibu mkuu wa   Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea kwa ajili ya kumjulia hali, nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana. Mh   Lowassa alikuwa Zanzibar kwa mapumziko ya kusherekea skukuu ya Krismasi.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kulia) akifurahia jambo na Katibu mkuu wa   Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana. Mh Lowassa alikuwa Zanzibar kwa mapumziko ya kusherekea skukuu ya Krismasi. Kushoto ni Mke wa Sukwa, Fatma Mussa.

  0 0


  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikabidhi vifaa vya Michezo wa Timu ya kata ya Kauzeni kwajili ya Kuendeleza Michezo ndani ya kata hiyo
  Wachezaji wa Timu ya Mzinga ya Morogoro wakimsikiliza  Kwa makini Mbunge wa Morogoro Mjini alipowatembelea Leo.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akikabidhi vifaa vya Michezo kwa Timu ya Mzinga ya Morogoro akiwa kama Mdau Mkubwa wa Michezo hasa Mpira wa Miguu
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea na wandesha bodaboda kutoka kata ya mzinga namna wanavyokabiliwa na changamoto zinazowakabilikatika biashara yao.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akiwasikiliza Viongozi wa CCM wa Kata ya Konga wakati wa Ofisi ya kata hiyo Mara baada ya Mh Mbunge Kufanya Ukaguzi hiyo Na Kuahidi kutoa Msaada wa Bati 100 Kwajili ya Kumalizia Ujenzi wa Ofisi hiyo.

  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akitoa maagizo kwa Mtendaji wa Kata ya Konga Kutafuta Eneo la Ujenzi wa Shule Hiyo haraka Iwezekanavyo.Mh Abood amemuagiza Mtendaji huyo ndani ya mwezi
  Mmmoja wa amepata Eneo la Ujenzi wa Shule na Ujenzi Uanze Mara Moja Ambapo Mh Mbunge Amechangia Shilingi Milion 5 za Kuanza Ujenzi Huo .
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akiongea na Wato wa Kata ya Kauzeni  mara baad ya Kuwasili katika Kata hiyo kwajili ya Kusikiliza Kero Zinazowakabili wakazi wa Kata Hiyo.
  Baadhi ya wakazi wa Kata ya kauzeni walioudhuria Mkutano ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini.


  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akisisitiza Jambo wakati akielezea Namna ya Kutatua Kero kubwa ya Maji Inayowakabili wakazi wa Kata ya Kauzeni Iliyopo Manispaa ya Morogoro Ambapo Mh Aziz Abood Ametoa Million 5 Kwajili ya Kutekeleza Mradi wa Maji wa Kata Hiyo Ili Kutatua Kero Hiyo.
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akitoa Onyo wa Watendaji wa Kata za Jimbo la Morogoro Mjini Kutumia Fedha Zinazoletwa katika Kata Hiyo kwa Maendeleao ya wananchi lasivyo Watakiona kwa wale watakaofuja  Fedha za Wananchi.
  Bi Asha Ally akieleza Kwa Uchungu Kero Kubwa ya maji Inayowakabili wakazi wa Kata ya Kuuzeni.


  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiandika Kero za wananchi wa kata ya Kauzeni Mara baada ya Kuwapa nafasi wa kata Hiyo kueleza Kero zao.


  0 0

   Amani, Heshima na Upendo kwa wana-blog wote.

  Kwanza namshukuru MUNGU kwa baraka ya uhai ambayo mimi nawe tunayo mpaka sasa.

  Pili nikupe pole kwa harakati za maisha ambazo sote twazipitia kufanikisha yale mema tupendayo. Ni harakati kubwa sana hasa katika kusonga na maisha yetu ya kila siku na pia kuendeleza gurudumu hili la blogs
  Nimekuwa nikituma makala, vipindi na kazi zangu kwenu nanyi mmekuwa wakarimu sana kuzipokea. Ushirikiano ambao umenifanya nizidi kujivunia kuwa mmoja wa bloga,Lakini pia, najivunia sana kuwasiliana na kila mmoja wetu hivi sasa ili kuanzisha mjadala wa changamoto zilizo mbele yetu kama JAMII YA WANA-BLOG wenye lengo la kuigusa jamii.

  Ningependa tuanze kwa kujiuliza, Je! Tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu.
  Nashukuru kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya kuigusa jamii. Kaka Luta Kamala aliwahi kuandika akijuliza KWANINI TUNA-BLOG? (Bofya hapa) na hata Kaka Chambi Chachage aliuliza kamauwepo wa blogu zetu unakuza ama kufifisha tasnia nzima ya uandishi (Ipitie hapa)

  Jibu halisi tunalo mioyoni mwetu kulingana na dhamira tulizonazo.
  Lakini kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa safari sote tunajikuta na zao moja ama "mlaji" mmoja ambaye ni JAMII.
  Bloga awekaye picha anataka kuionesha jamii alichokiona.

  Bloga ahabarishaye anataka kuihabarisha jamii. Yule aandikaye Utambuzi anataka jamii ijitambue. Anayeweka kumbukumbu ni sababu anataka jamii ije isome baadaye. Atangazaye biashara anataka jamii ijue palipo na huduma ama biashara husika. Afunzaye mapishi, mitandao, mavazi, mitindo nk, woote wanalenga katika kuielimisha jamii.
  Kwa maana nyingine sote twaiandikia JAMII.

  Na hili ni lengo jema.
  Lakini swali linarejea kuwa......
  Mwaka huu ambao unaomalizika wiki hii unaonekana kuwa hatua gani kwetu?

  Logo hapo juu inaonyesha hatua iliyopihgwa katika siku za mwisho za mwaka. Kuanzishwa kwa mtandao wa bloga ambao (ukitumiwa vema) utakuwa chachu ya mabadiliko ya nchi hasa kwa mwaka huu wa uchaguzi.
  Ninalowaza ni hili.....

  Vipi tunaweza kuweka nguvu na jitihada zetu pamoja kuweza kuitumikia vema na kwa ufasaha jamii yetu???
  Mafanikio ya bloga mmoja mmoja yanaweza kudhihirisha kuwa TUNAWEZA, lakini tunalostahili kufanya sasa, ni kushirikiana na kuwa makini katika kila jema tutendalo.

  Tunapoumaliza mwaka 2014, tuangalie nyuma na kujiuliza, mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama nyuma??


  Na jibu la swali hili, liwe CHANGAMOTO YETU sote

  Baraka kwenu nyote

  Heri ya Mwaka Mpya 2015

  0 0

  Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura kulia, akizungumza jambo katika makabidhiano ya hundi kwa bwana  Kennedy Kaupenda kushoto kwake, Makao Makuu ya Bayport, mapema wiki hii. Picha zote na Mpigapicha Wetu.

  TAASISI ya kifedha ya inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Tanzania, imempatia Sh Milioni tatu mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE), Kennedy Kaupenda, kufuatia huduma mpya ya Bima ya Elimu inayoendeshwa na taasisi hiyo nchini.

  Huduma hiyo mpya ya Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania ilianza mapema mwaka huu kwa ajili ya kuwapatia fursa wanafunzi kuendelea na masomo baada ya mzazi aliyejiunga na huduma hiyo kufariki Dunia.

  Mwanafunzi wa MUCE, Kennedy Kaupenda kushoto, akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi yake ya Sh Milioni 3 kutoka kwenye Bima ya Elimu inayoendeshwa na Bayport. Kulia kwake ni Mratibu wa Bima hiyo, Ruth Bura.   

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Bima ya Elimu inayotolewa na Bayport Tanzania, Ruth Bura, alisema Kaupenda alitajwa kama mnufaika kwa mzazi wake aliyefariki Dunia, hivyo waliamua kumtafuta kwa ajili ya kumpatia mafao yake kwa ajili ya kuendelea kupata elimu bila vipingamizi vyovyote.

  Alisema huduma hiyo ina vipengele vine ambavyo ni Bronze, Gold, Silver na Exucutive, huku akisema kuwa makato ya kila mwezi ya Bronze ni Sh 2,500, ambapo fao lake ni Sh Milioni 3, wakati makato ya Gold ni Sh 6,250, huku fao lake likiwa ni Sh 7,500,000.
  Ruth Bura, Mratibu wa Bima ya Elimu Bayport Tanzania kulia akimkabidhi hundi bwana Kennedy Kaupenda kwa ajili ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu baada ya kufariki mzazi wake.

  Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura, kulia akizungumza jambo baada ya kumkabidhi Kaupenda hundi ya Sh Milioni 3 kutoka kwenye huduma hiyo mpya iliyoanzishwa kwa ajili ya kukamilisha ndoto za elimu kwa uwapendao.

  “Pia tunacho kipengele cha Silver ambapo makato yake kwa mwezi ni Sh 3,800, huku mteja akilipwa fao la Sh Milioni 4,500,000 na kipengele cha Executive kikihusisha makato ya Sh 9,000 na kumpatia mteja fao la Sh 10,800,000, huku tukiamini kuwa huduma hii ni sehemu ya kuhakikisha kuwa Watanzania wanawawekea ulinzi wa elimu watoto wao na yoyote wanayemchagua wao,” alisema Ruth.

  Akizungumzia fao hilo, Kaupenda alisema hakuwa na imani kuwa angesoma vizuri baada ya baba yake kufariki, ila baada ya kutafutwa na Bayport na kutaarifiwa juu ya mafao hayo, amepata nguvu mpya.

  Kennedy Kaupenda akitafakari baada ya kuiona hundi iliyoandaliwa kwa ajili yake kutoka Bayport Tanzania juu ya fao la Bima ya Elimu.
   
  “Nasikitika sana baba kwa kunificha juu ya kujiunga na huduma hii sambamba na kuwa mkopaji wa Bayport, hata hivyo namshukuru kwasababu fedha hizi zimekuja kunipa mwanga mpya wa kuhakikisha kuwa nasoma kwa bidii, nikiamini kiasi cha Sh Milioni tatu kitaniweka katika wakati mzuri mno,” alisema Kaupenda, huku akiwasisitiza wazazi kujiunga kwenye huduma hiyo kwa manufaa ya familia zao.

  Mbali na huduma hiyo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao, pia Bayport inajihusisha na mikopo kwa watumishi wa umma na kampuni zilizoidhinishwa, ambapo mwishoni mwa mwaka 2014 walizindua huduma ya Mikopo ya Bidhaa, ambapo bidhaa za bodaboda aina ya Lifan, Toyo na Boxer zinakopeshwa kwa wateja wa Bayport Tanzania.

  0 0


  Na Andrew Chale

  SAFARI Carnival kwa kushirikiana na Asia Idarous Khamsin (Fabak fashions) usiku wa 31/12/2014, Wameandaa shoo maalum ya Mkesha wa mwaka mpya 'Old Is Gold taarab', Ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, Kawe jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin alieleza shoo hiyo maalum wadau

  mbalimbali watakutana kuupokea mwaka kwa pamoja huku wakipata burudani ya muziki wa taarab wa zamani 'Old is Gold' pamoja na 'Surprise' kibao."Kwa kiingilio cha sh 5,000, tu, Fabaki fashions na Safari Carnival, tumeandaa usiku huu maalum wa Mkesha wa mwaka mpya.

  Utakaoambatana na burudani ya taarab za zamani na za sasa pamoja na Surprise mbalimbali" alisema Asia Idarous.Aidha,  Asia Idarous alisema usiku huo, pia umedhaminiwa na Michuzi Media Group, Clouds fm,Gone Media, Maji Poa na wengineo.

  0 0


  Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba (wa pili ktoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana katika  ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kuanza kwa msimu wa tatu wa kipindi chake ‘The Mboni Show’ kinachotarajia kuanza Jan 2, 2015. Kushoto ni kiti Simpompa na kuanzia kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba.
  Kutoka Kulia Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema akizungumza wakati wa uzinduzi kipindi cha Mboni Show uliofanyika katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba pamoja na Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba.


  Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba ameamua kuhamishia kipindi cha Mboni show katika kituo cha utangazaji cha Taifa (TBC) kutoka EATV ili kuvutia watazamaji wengi na wapya kwa wazee pamoja na vijana.

  Kipindi cha Mboni Show kitaanza kurushwa TBC kuanzia January 2 mwaka 2015 siku yaIjumaa saa 3 Usiku-4 Usiku na marudio Jumanne saa 9:00 mchana-10:00mchana.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mboni Masimba ametoa shukrani kwa EATV kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote alichokuwa nao,na kusema kuwa amehamishia kipindi cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia watazamaji wengi hakuna atakaye tumia jina la Mboni Show na hakuna kitakachomkwamisha kwa vile ana hati miliki.

  “Nimeamia TBC kwa kuwa nahitaji watazamaji wengi ,wote wazee na vijana na hakuna atakaye tumia jina langu la Mboni Show kwa kuwa nina hati miliki ya jina hili”alisema Mboni.

  Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw.Fadhili Chilumba amesema wamefurahi kuwepo kwa Mboni Show katika kituo cha Taifa(TBC) na kutoa wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama wakina Mboni na wanamkaribisha sana.

  Nao wadhamini wa Mboni Show,Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema wamesema wanamwezesha Mboni kuwepo hewani ili kuhamasisha,kuelimisha pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania.

  0 0
  0 0

  Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akimkabidhi zawadi ya mwaka mpya Msimamizi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life kilichopo Boko, Mwanaisha Magambo kwa ajili ya watoto 102 waliopo kituoni hapo, tukio hilo lilifanyika juzi.
  Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akiwa na Miss Kinondoni Maria Shila wakiwa wamembeba mtoto aliekuwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life cha Boko, mtoto huyo alifikishwa hapo akiwa na siku nne tu tangia kuzaliwa kwake.
  Sehemu ya Watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life kilichopo Boko,wakimsikiliza Miss Tanzania Lilian Kamazima.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Mhe. Djelloul Tabel, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Zoka, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga akienda kuanza kazi rasmi nchini Canada.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Alexander Rannkikh, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.


  0 0

   Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika shehia ya Mpapa mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya uchimbaji wa mtaro wa maji kupitia Mpango wa ajira za muda ambao huwawezesha walengwa kulipwa fedha .
   Mtaro wa maji uliochimbwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja inayotekelezwa chini ya mpango wa ajira za muda kupitia TASAF.
  Mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini wa TASAF katika shehia ya Mpapa wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akishiriki kazi ya kuchimba mtaro wa maji.

  WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF WACHIMBA MTARO WA MAJI  KUPITIA UTARATIBU WA AJIRA YA MUDA KATIKA SHEHIA YA MPAPA,MKOA WA KUSINI UNGUJA.

  Maelfu ya wakazi wa shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji unaotekelezwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiwa  na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa utaratibu wa ajira ya muda PWP.

  Wakizungumza katika eneo la mradi baadhi ya walengwa hao wameonyesha utayari wao katika kuchimba mtaro huo huku wakiipongeza  serikali kupitia TASAF kwa kubuni utaratibu huo ambao wamesema licha ya kuwaongezea fedha lakini pia utapunguza kero ya upatikanaji wa maji katika eneo lao .

  Chini ya utaratibu wa ajira za muda ,walengwa kutoka kaya maskini huibua miradi katika eneo lao na kuitekeleza na kisha kulipwa ujira ikiwa ni mkakati wa TASAF wa kuziongezea kaya maskini kipato kwa kukidhi mahitaji muhimu hususani katika Nyanja za elimu,afya,lishe na uchumi, ambapo kwa mujibu wa utaratibu asilimia  75 ya fedha ni malipo kwa walengwa wakati asilimia 25 ni kwa ajili ununuzi wa vifaa .

  Mpango wa ajira za muda utatekelezwa nchini kote wakati wa kipindi cha hari au kipindi kigumu kama wakati wa ukame au mafuriko kupitia Mpango wa Kunusuru  kaya maskini,PSSN ambao umebuniwa na  serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na unatarajiwa kuhudumia kaya maskini zipatazo laki tisa na ishirini elfu nchini kote kazi ianayotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Marchi 2015.

  ifuatazo ni picha za baadhi ya wananchi wa shehia ya Mpapa mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya kuchimba mtaro wa maji kupitia utaratibu wa ajira za muda.


  0 0

  Sheikh Shariff Matongo  akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake  jijini Dar es Salaam (hawapo pichani)kuhusu  ndoto yake ambayo ameoteshwa kuelekea mwaka 2015.

  NA CHALILA KIBUDA,GLOBU YA JAMII,DAR.

  Sheikh Sharif Matongo amesema ameoteshwa ndoto ya mwaka 2015 na kupata ushauri kwa mashekh mbalimbali Duniani ambavyo vitatokea nchini na viongozi wasipuuze ndoto hiyo. Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba likiwemo la kupata Rais ajaye ambaye kiongozi ambaye muda mwingi ameishi nje ya nchi kwa kufanya kazi.

  Alisema katika ndoto nyingine kifo cha kiongozi mkubwa  ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali na  mwenye kambi katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Sheikh  alisema ndoto nyingine  kutokea kwa mvua nyingi ambapo watu wanaoishi mabondeni ,kutokea kwa vifo vya watoto vingi ,wafanyabiashara kupata mafanikio  makubwa kwa mwaka utaoanza kesho.

  Vijana wengi watashinda katika uchaguzi ujao na wazee wataangushwa sana hivyo wanatakiwa kujitokeza,katiba inayopendekezwa  itapita lakini kutakuwa na vurugu ambazo zitaibuliwa na vijana.

  ‘’Ndoto yangu  niliooteshwa sikukaa nayo peke yangu, niliweza kupata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Mufti wa  Abhu Dhabi,Mufti wa Nigeria  na wengine wote wakaniambia suala hilo nisikae nalo,niwashirikishe na Watanzania wenzangu’’alisema Sheikh Shariff Matongo.

  Sheikh Shariff alisema katika usafiri wa bahari utakuwa mbaya kutokana na bahari kuchafuka na chombo kimoja kitazama kutokana na kuchafuka huko.


  Alisema ndoto hizo ni lazima kuzingatia kutokana na kupata ushauri wa watu wengi wenye kuaminika katika jamii katika mataifa mbalimbali ulimwenguni.

older | 1 | .... | 433 | 434 | (Page 435) | 436 | 437 | .... | 1898 | newer