Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

ALEX MSAMA AMWAGA ZAWADI ZA KRISMAS KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

MSAADA KWENYE TUTA. GAZETI LA JAMBO LEO LATINGA MTANDAONI

0
0
Kwa habari za kila siku Soma gazeti la Jambo Leo kupitia website www.jamboleo.co.tz Utajipatia habari mbalimbali ambazo zimetokea nyumbani Tanzania na matukio mengine duniani,gazeti la Jambo Leo linatolewa na kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, inayochapisha Jarida la Jambo Brand Tanzania, gazeti la michezo la kila wiki, Staa Spoti na gazeti la matangazo la Dar Metro linalotoka kila baada ya wiki mbili.

MKURUGENZI WA KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA IRINGA GNSM ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA YATIMA TOSAMAGANGA

0
0
MKurungenzi  wa kampuni ya ujenzi  wa barabara Iringa ya GNSM Bw  Geofrey Mungai na mkewe  Sarafina Mungia katikati  wakikabidhi  baada ya misaada  yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1 kwa  mlezi  wa  kituo cha yatima Tosamaganga Godfrida Mhongole
Bw Mungai  akishuhudia  jinsi  watoto  wanavyohudumiwa
Bi Sarafina  Mungia na Geofrey Mungai  wakiwatazama wahudumu  wakiwalisha watoto yatima wa Tosamaganga  Iringa.
Bw Geofrey Mungai  akisaidia  kuwapa uji  watoto yatima  wa Tosamaganga Iringa baada ya  kumaliza  kuwapa msaada wa chakula  cha Krismas na mwaka mpya
Watoto   wakifurahia msaada  wa chakula
Mlezi  wa  kituo  cha yatima   Tosamaganga  Godfrida Mhongole  kushoto akiwapongeza Mungai na mkewe kwa  msaada wa chakula
Bi sarafina Mungai  akiwa na watoto yatima
majengo ya  kituo hicho
Mtoto akiishangaa  simu ya Bi sarafina
Mungai na mkewe  wakiwa na  watoto  yatima
Mhudumu  wa kituo hicho akimlisha mtoto yatima

Mungai akisaidia  kumnywesha  uji mtoto
Watoto  wakipewa chakula
Mungai na mkewe  wakiwa na watoto  yatima  huku  gari  lililopeleka msaada wa  chakula  likiendelea kushusha
watoto  wakifurahia  msaada  huo


Na matukiodaimaBlog

 MKURUGENZI wa kampuni ya  ujenzi  wa barabara nchini ya  GNSM Contractors Co. Ltd ya mkoani Iringa ametoa msaada  wa chakula chenye  thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1.5 kwa  kituo cha kulea watoto yatima  cha Tosamaganga katika wilaya ya Iringa kwa ajili ya  sikukuu ya Krismas na mwaka mpya .


Huku  akiwapongeza   wahudumu  wa  kituo  hicho kwa  kuendelea  kuifanya kazi  hiyo ya  kulea   watoto  zaidi ya 70 waliopo kituoni hapo kwa moyo wa  kujitoa   zaidi.

Mkurugenzi   huyo Geofrey  Mungai  ambae  aliongozana na mkewe  Bi Sarafina Mungai  alikabidhi msaada   huo jana  ikiwa ni  sehemu ya mwensdelezo  wa kampuni  hiyo na familia yake kuzungukia vituo  mbali mbali  vya yatima kwa  kuwasaidia watoto hao.

Akizungumza  baada ya  kukabidhi msaada  huo  Bw  Mungai  alisema  kuwa  imekuwa ni kawaida  ya kampuni yake kuwakumbuka  watoto  hao  yatima  wa  kituo hicho  na vituo  ikiwa ni moja ya  kuwakumbuka watoto hao  ambao  wanaishi kwa  kutegemea misaada  ya  wasamaria  wema.


Alisema  kuwa jamii inapaswa  kubadilika kwa  kuelekeza  michango  yao  kwa  watoto  yatima ambao wanaishi  kwa misaada ya wahisani  wa ndani na nje  baada  kupoteza  wazazi  wao .

Kwani  alisema  kuendelea kuwasaidia  watoto  hao ni kuwasogezea  faraja ya  pekee  ambayo watoto  hao wanahitaji    kutoka kwa  jamii inayowazunguka badala ya kuwasusa  ama  kuwaachia watu  wachache kulea  yatima  hao.

Aidha  alisema  kuwa  yeye  kama mmoja kati  ya makandarasi mkoa  wa Iringa anaendelea  kufanya mazungumzo  na wenzake  ili  kuweka  mpango wa  kuendelea  kutembelea  vituo  vya yatima kila mwaka  kwa  ajili  ya kuwasaidia misaada  mbali mbali.

Huku  akiishauri  serikali kuangalia  uwezekano kupitia  ofisi  za maendeleo ya   Jamii, Jinsia na Watoto kuweka  utaratibu  wa  kuwakumbuka watoto  waliopo katika  vituo vya yatima kwa  kuwapa mahitaji yao ya  kila  siku .

Bw Mungai  alipongeza  jitihada  kubwa  zinazoendelea  kufanywa na uongozi wa  kituo hicho  cha Tosamaganga ambacho sehemu kubwa watoto  wanaolelewa hapo ni  wale wanaotupwa ama wazazi wao  kufariki baada ya kuwazaa.
 
Alisema  kuwa  upo uwezekano mkubwa wa  watoto  hao yatima  kuendelea   kusaidia  iwapo watanzania na wadau  mbali mbali  wakiwemo makandarasi  wenzake  kuwekeza kwa  watoto hao

Kwa  upande  wake  Bi Sarafina Mungai akizungumza na wahudumu hao  alisema  kuwa kazi wanayoifanya ni kazi  kubwa ambayo serikali na wananchi hawanabudi  kuitambua na  kuwaunga mkono zaidi.

DIAMOND PLATNUMZ, MZEE YUSUF WAAHIDI KUANGUSHA SHOO YA KUFA MTU DAR LIVE SIKUKUU YA X-MAS

0
0
Wanamuziki Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' na Mzee Yusuf (kushoto) wakipozi baada ya kufanya mahojiano na wanahabari leo.
Wanamuziki hao wakionyesha mbwebwe zao mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akihojiwa na wanahabari leo katika ofisi za Global Publishers Ltd tayari kwa Tamasha la Wafalme kesho, Dar Live.
Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akihojiwa na mwanahabari wa Channel Ten, Freddy Mwanjala.
Mzee Yusuf naye akihojiwa na Freddy Mwanjala wa Channel Ten.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd na Dar Live, Abdallah Mrisho (kulia) akielezea kwa wanahabari jinsi Dar Live walivyojipanga kwa ajili ya kuwapa burudani safi mashabiki hapo kesho.
Diamond akifurahia jambo na Mzee Yusuf aliyekuwa 'busy' na simu yake baada ya mahojiano.

WASANII mahiri nchini Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' na Mzee Yusuf wamewaahidi mashabiki wa burudani hususani wa Jiji la Dar es Salaam kutokosa kesho katika Ukumbi wa Dar Live kushuhudia shoo ya kibabe inayotambulika kama Tamasha la Wafalme.

Wakiongea na wanahabari katika Ofisi za Kampuni ya Global Publishers Ltd zilizopo Mwenge-Bamaga jijini Dar, wakali hao wamesema wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya shoo hiyo itakayoacha historia katika pande za Mbagala-Zakhem, jijini Dar.

Naye Meneja wa Dar Live, Abdallah Mrisho amewataka mashabiki wa burudani kuhudhuria kwa wingi kesho katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live maana kila kitu kiko safi kuanzia ulinzi na huduma zote muhimu.

Shoo hiyo ya aina yake itaanza asubuhi kwa burudani za watoto ambapo kundi la sarakasi la Masai Worriors litahakikisha linatoa burudani ya nguvu kwa watoto wote kwa kuwapa staili mbalimbali za sarakasi na mazingaombwe. Pia watoto wataburudika na michezo kibao kama vile kuogelea, kubembea, kuteleza huku kila mmoja atakayehudhuria kurudi na zawadi kemkem nyumbani kwao. Kiingilio cha Tamasha la Wafalme kitakuwa shilingi 10,000 kawaida wakati kwa VIP kiingilio kikiwa shilingi 20,000.
WOTE MNAKARIBISHWA!

CHAMA CHA TENNIS TANZANIA (TTA) KUANDAA TENA MASHINDANO YA AFRIKA MASHARIKI

0
0
CHAMA CHA TENNIS TANZANIA (TTA) KUANDAA TENA MASHINDANO YA
AFRIKA MASHARIKI (EAST AFRICAN JUNIOR ZONAL CHAMPIONSHIPS) KWA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 16, JANUARI 11-19 2015.

Chama cha Tennis Tanzania (TTA) kimepewa nafasi nyingine tena ya kuandaa mashindano ya vijana wa ukanda wa Afrika Mashariki  (East Africa zonal championships) na yatafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 19 Januari 2015. Nchi shiriki kwa mwaka 2015 ni Burundi, Comoros, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Seychelles, Sudan na Tanzania. 

Tunategemea jumla ya washiriki wapatao 72 (pamoja na Tanzania). Tanzania itawakilishwa na vijana 22 ikiwa na team A na B.

TTA inajivunia kuanzishwa kwa mfumo wa renki unaotoa fursa kwa wachezaji kujikusanyia pointi kwenye orodha ya wachezaji wa tennis Tanzania. Hili limesaidia urahisi wa uchaguzi wa timu na kuepuka lawama za kupendelewa watu flani. Kila mchezaji wa chini ya umri 18 ana nafasi sawa ya kukusanya pointi kwa kushiriki mashindano yanayoandaliwa na TTA au watu binafsi yaliyoidhinishwa na chama. Timu ya Tanzania mwaka huu itawakilishwa na:
 
Boys




Categories
Jina
TTA Rank
Points
Club
Under 12
Deogratus Felex Ernest
1
115
AICC
Yusuph Laurence Godwin
2
100
AICC
Kanuti Omary Alagwa
4
30
AGC
Under 14
Hassan Hamisi Yambi
1
125
AICC
Emmanuel Frank Temba
3
30
AGC
Ali Hamza
4
30
DGC
Adam Mwambungu
3(12&U)
80
KJ
Under 16
Frank Menard Mshana
1
105
AGC
Emmanuel Mallya
5
10
AGC
Omary Hamisi Sulle
4
10
AGC
Hassan Mkajira

2
KJ









Girls




Categories
First Name


Club
Under 12
Ester Paulo Nankulange
1
140
AGC
Emiliana Katabalo
5
15
KJ
Maria Elisha Milanzi
4
25
AGC
Under 14
Emiliana Stanslaus
2
30
KJ
Shadya Maulid Kitenge
12
5
KJ
Jackline Kayuga
2(12&U)
75
KJ
Under 16
Adela Abraham Mollel
1
32
AGC
Georgina Kemmy Kaindoah
N/A
N/A
N/A
Round Robin




Kutokana na uhaba wa wachezaji wa kike kwenye kundi la umri wa chini ya miaka 16, nafasi moja itapiganiwa na wachezaji waliopo lakini hawajapata nafasi ya kushiriki mashindano ya ndani ili kupata pointi kwa mtindo wa mtoano (round robin).

TTA inafanya juhudi kuwataarifu wazazi wa watoto walioingia kwenye timu kwa ajili ya maandalizi. Timu ya Tanzania itasimamiwa na kocha Nico Jonas ambaye ni msimamizi wa High Performance Tennis (HPC) akishirikiana na Majuto Omari wote wakiwa ni makocha wa
level 2 kwa mujibu wa ITF.

Timu inatazamiwa kuingia kambini tarehe 27-12-2015 ambapo watapewa mafunzo mbali mbali pamoja na kufanya shindano la kujipima kabla ya mashindano yenyewe mwezi wa
kwanza.

TTA itafanya mkutano rasmi na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mashindano
mwezi wa kwanza.

Kwa niaba ya uongozi mzima, tunawatakia sikuu njema ya krismasi.

Katibu Mkuu wa TTA.

MWISHO.


Kwa maelezo ya ziada wasiliana na:
1.    Nico Jonas – Kocha Mkuu - +255 754 250 097.
2.    Majuto Majaliwa – Kocha Mkuu msaidizi – 0718 849 889.
3.    William Kallaghe – Maswala yote ya mashindano - +255 754 210 437.

Kikundi cha Ngara Youth Foundation kimeishukuru Serikali kwa kupatiwa Mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

0
0
unnamedqMkurugenzi Msaidizi wa Ufutiliaji na Tathimini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi.Verdiana Mushi akikagua mradi wa kikundi cha vijana kutoka Ngara alipowatembelea kwa ajili ya kutathmini maendeleo ya mfuko wa maendeleo wa vijana. Kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha Hekima Group Ngara Bw.George Kessy.
unnamedq1 
Katibu wa Ngara Saccoss Bw.Joackim Jordan (wapili kushoto) akiwaonyesha Maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipowatembelea hivi karibuni baadhi ya tofali aina ya vibrated blocks zinazotengenezwa kwa udongo na simenti ambazo vikundi kumi vya vijana vilipata mafunzo ya kutengeneza matofali hayo kama sehemu ya miradi wanayofanya. Kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha vijana cha Hekima Group Ngara Bw.George Kessy.Picha na: Anitha Jonas – Maelezo
……………………………………………………………….
Anitha Jonas – MaelezoKikundi cha vijana cha Ngara Youth Foundation chenye wanachama wapatao kumi na moja waliomaliza elimu ya juu wamenufaika baada ya kupata mkopo wa Milioni tano kupitia mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kuanzisha miradi miwili ikiwemo mradi wa kuuza mbao na mradi wa kuosha magari.

Hayo yalisemwa jana na Katibu wa kikundi hicho Bw. Jason Athanas alipotembelewa na maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kutathimini miradi inayoendeshwa na vikundi baada ya kupatiwa mkopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kutokana na changamoto ya ajira iliyopo nchini.Kikundi hicho kimeishukuru Serikali kwa kuwapatia mkopo uliopelekea kuongeza kipato kwa kila mwanachama hivyo kuboresha hali ya maisha baada ya kukosa ajira na kuwafanya kuwa wabunifu katika jamii.

“Tuliamua kuanzisha kikundi hiki baada ya kumaliza chuo na kutafuta ajira kwa muda mrefu hivyo tuliamuamu kuungana kuanzisha kikundi chetu ambapo tulibuni mradi tulioona unafaa na kuomba mkopo, kwa sasa tuna miradi miwili ambayo ni mradi wa kuuza mbao na wakuosha magari (Car Wash)”,alisema Bw. Athanas.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Habari, Vjana, Utamaduni na Michezo Bibi.Verdiana Mushi, aliwapongeza vijana hao kwa juhudi kubwa wanazozifanya na kutoa wito kwa vijana wengine kuiga mfano wa vijana hao kwa kuanzisha vikundi vyao na kuomba mkopo katika mfuko wa maendeleo ya vijana unaosimamiwa na Wizara.

Aidha Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Eliakim Mtawa aliwashauri vijana wa Ngara Youth Foundation kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu huku wakizingati matumizi mazuri ya mapato yanayotokana na miradi yao pamoja na kuendelea kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha kukua kiuchumi na kukuza miradi ya kikundi.

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI USALAMA BARABARANI

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

 

Hali ya usalama barabarani kiujumla kwa mwaka huu 2014 ni ya kuridhisha ukilinganisha na mwaka jana. Kwa mfano ukiangalia takwimu za ajali kwa miezi 11 ya mwaka 2013  Januari- Novemba kulinganisha na takwimu ya ajali kwa miezi 11 ya mwaka 2014 Januari-Novemba utagundua kuwa kuwa kuna upungufu wa ajali kwa asilimia 38.20 za ajali, asilimia 5.63 za vifo na asilimia 28.27 za majeruhi.


Jan-Nov 2013
Jan-Nov 2014
Tofauti
Asilimia (%)
Ajali
21,791
13,466
-8325
38.20
Vifo
3,642
3,437
-205
5.63
Majeruhi
18,813
13,495
-5318
28.27
 
Hata hivyo, pamoja na juhudi hizi bado matukio ya ajali yanaendelea na tunashuhudia yakichukua maisha ya ndugu na jamaa zetu huku yakiacha majeruhi, vilema na uharibifu wa mali.
 
Ndugu wanahabari,
Wito wangu wa leo napenda kuwakumbusha Madereva  na watumiaji wote wa barabara kuziheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani husasani katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kinachoambatana na sikukuu za Krismas na mwaka mpya.

Mtaungana na mimi kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la ajali za barabarani miaka iliyopita katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambapo sababu kubwa za ongezeko hilo ni za kibinadamu zikiwemo mwendo kasi, ulevi, matumizi ya simu za mkononi wakati wa kuendesha, uendeshaji wa hatari (overtaking), kutofuata alama,michoro na ishara za barabarani ,matumizi ya taa zenye mwanga mkali barabarani na uegeshaji mbaya wa magari barabarani.

Ndugu wanahabari,
Bado kuna ukiukwaji wa sheria inayowataka wapanda pikipiki (madereva na abiria) kuvaa kofia ngumu (helmet) muda wote wanapotumia vyombo hivyo. Tunawakumbusha watumiaji wa vyombo hivyo kuzingatia matumizi ya kofia ngumu muda wote wanapotumia vyombo hivyo hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.


Ndugu wanahabari,
Napenda pia kuchukua nafasi kuwakumbusha askari wote kusimamia sheria na kanuni za usalama barabarani kama wanavyoelekezwa, Kinyume na hapo hatua kali za kisheria na kinidhamu zitachuliwa dhidi ya yeyote atakayekiuka. Niwaombe tu wananchi mtoe ushirikiano kwa kutupatia taarifa za askari wanaokiuka taratibu zao za kazi katika maeneo mbalimbali.

Ndugu wanahabari,
Jeshi la polisi Kikosi cha usalama barabarani limejipanga kikamilifu hususani kimikakati  kupambana na ajali za  barabarani na kadhia zote za sikukuu za mwisho wa mwaka kama nauli na ubabaishaji katika usafiri wa abiria. Tumekuwa na kampeni  zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini zinazolenga kutoa elimu ya usalama barabarani. Dhumuni kubwa ni kupambana na makosa hatarishi yanayochangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la ajali (mwendo kasi, ulevi, matumizi ya simu wakati wa kuendesha, kupita magari mengine na uendeshaji wa hatari)

Katika suala la nauli, tarehe 21/12/2014 kwa kutumia askari kanzu wa Jeshi la Polisi tuliwakamata watu 7 waliokuwa wakiuza tiketi kwa bei kubwa katika kituo kikuu cha Ubungo. Watuhumiwa hao tarehe 22/12/2014 walipelekwa mahakamani ambapo kesi zao zitatajwa tena tarehe 5/1/2015 na 6/1/2015 na wako gereza la Segerea wakisubiri tarehe hizo

1.   Victor Kombe      –Wakala wa KVC

2.   Mussa Msangi     - Karani wa tiketi HAPPY NATION

3.   Walter Nkya        - Karani wa tiketi IBRA LINE

4.   Fredrick Lema    - Karani wa tiketi MBAZI TRAVEL COACH

5.   Ramadhani Mbaga –Usafiri wa TOYOTA NOAH

6.   Stephen Amos       – Usafiri wa TOYOTA NOAH

7.   Jane Gabriel         - Usafiri wa TOYOTA NOAH

Aidha jana tarehe 23/12/2014 asubuhi watu wengine 3 walikamatwa wakiuza tiketi kwa bei ya juu ambao leo taratibu zikikamilika watapelekwa mahakamani,
1.Kassim Azaria           - Usafiri wa NOAH
2.Kelvin Charles           - Wakala wa Islam
3. Mbaraka Tariba Kombo  - Wakala wa Islam

Nipende tu kuwajulisha watumiaji wote wa barabara kuwa  askari wataendelea kuwa wakali sana katika kipindi hiki  ambapo hatua kali za kisheria zitachuliwa kwa yeyote atakayekamatwa  akivunja sheria za usalama barabarani. Niwaombe tu watumiaji wote  wa barabara watii sheria bila shuruti .


Ndugu wanahabari,
Mwisho lakini sio kwa umuhimu napenda kuwaasa  wananchi na wadau wa usalama barabarani kwa ujumla, watupe ushirikiano zaidi kwa kutoa taarifa za uhalifu wa usalama barabarani, kufuata sheria, kanuni na maelekezo kwa ajili ya usalama wao watumiapo barabara. Kila mmoja atambue haki na wajibu wake akiwa barabarani ikiwa ni kuwa na subira na kujali watumiaji wengine wa barabara kwani wana haki sawa ya kutumia barabara. Watoto wasiachwe kutembea barabarani bila ya uangalizi wa watu wazima.
                     Ninawatakia heri ya Xmas na Mwaka Mpya.

˝Maamuzi yako barabarani ni hatima yetu-Fikiria kwanza”.

Imetolewa na:  
MOHAMMED R.MPINGA – DCP
KAMANDA WA POLISI,
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T)

UNIC YAELIMISHA SIKU YA CHOO KWA VIJANA WALIO NJE YA SHULE

0
0
Siku ya choo duniani ambayo huadhimishwa tarehe 19 Novemba. UNIC waliadhimisha siku hii kwa kuwakutanisha vijana walioko nje ya shule tarehe 23 Desemba 2014 kwa lengo la kuwaelimisha na kuwahamasisha utumiaji wa vyoo ili na wao waweze kuelimisha jamii zinazowazunguka juu ya umuhimu wa kuwa na vyoo.
Tukio hili liliwakutanisha vijana toka vikundi 5: Azimio Youth Group, Makangarawe Youth Development Fund, Mashine Ya Maji Youth Development Centre,Temneke Youth Development Foundation na Tanzania Youth Development Society. Yafuatayo ni baadhi ya matukio katika picha.
TOILET DAY 2014 3 blog 1
Vijana wakiwa katika makundi kujadili na kuweka mikakati watakavyosaidia jamii kuhusu utumiaji wa vyoo na usafi wa mazingira.
TOILOET DAY 2014 4 blog 1
Afisa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma-Ledama akitoa mada kuhusu siku ya Choo duniani pamoja na umuhimu wa utumiaji vyoo, na kampeni maalumu ya uhamasishaji wa kuwa na vyoo.
TOILET DAY 2014 8 blog 2
TOILET DAY 2014 14 blog 2
Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za Vijana Temeke (Temeke Youth Development Network -TEYODEN), Ismail Mnikite akitambulisha vijana waliohudhuria kutoka makundi mbalimbali.
TOILET DAY 2014 13 blog 2
Baada ya majadiliano, vijana wakiwasilisha maazimio na mikakati waliyoyakusudia kufanya ndani ya vikundi vyao katika jamii zinazowaunguka.
TOILET DAY 2014 25 blog 2
TOILET DAY 2014 19 blog 1

Vijiji 45 mkoani Mara kupatiwa umeme

0
0

indexaWaziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa vijiji vipatavyo 45 vilivyopo katika mkoa wa Mara vinatarajiwa kuunganishiwa na huduma ya umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
 Profesa Muhongo aliyasema hayo katika ziara yake ya siku sita katika mkoa wa Mara lengo likiwa ni kukagua na kuzindua miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco).
 Profesa Muhongo alisema ziara yake iliyohusisha wilaya za Musoma Vijijini, Tarime, Rorya, Bunda na Serengeti ililenga pia kubaini na kukagua mahitaji ya umeme katika wilaya hizo ili vijiji vilivyokosa umeme kwenye awamu ya pili viingizwe katika awamu nyingine ya umeme vijijini.
 Alieleza kuwa Wizara imekuwa ikisambaza umeme katika kila Mkoa na Wilaya za Tanzania kwa awamu kulingana na mahitaji na idadi ya watu katika maeneo hayo.
 Alisema kwa sasa umeme unaosambazwa upo katika awamu ya pili ambapo awamu ya tatu itakuja baada awamu ya pili kumalizika.  Alisema vipaumbele vinavyotolewa katika uunganishaji wa umeme vijijini Profesa Muhongo alitaja kuwa ni maeneo yenye huduma muhimu za kijamii kama vile mashule, vituo vya afya, makanisa, misikiti, ofisi za vijiji na kata, na sehemu zenye miradi ya maji.


“Lengo letu kuu kwanza ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za jamii kwa urahisi na baada ya kuboreshwa kwa huduma hizo tunakwenda kuwaunganishia umeme wananchi mmoja mmoja, ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha maisha ya wananchi yanaboreshwa kupitia nishati ya umeme”, alisema Profesa Muhongo .
  Profesa Muhongo aliongeza kuwa ili nchi yoyote duniani iweze kupiga hatua katika ukuaji wa uchumi wake, inahitaji nishati ya umeme na kuongeza kuwa kwa kutambua hilo serikali imeanza kwa upande wa vijijini ili wananchi hao waweze kujiingizia kipato kupitia ajira za kujiajiri.
 Alifafanua kuwa wananchi wa vijijini kupitia nishati ya umeme wanaweza kuwekeza kupitia mashine za kusaga nafaka, kukamua mafuta, kuhifadhi vyakula vya kuuza kwenye majokofu na kujipatia fedha na kuongeza kuwa itapunguza wimbi la watu kukimbilia mjini kutafuta ajira.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa kijiji cha Bukabwa Thomas Makwera alisema kuwa wananchi wa kijiji chake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kutokuunganishiwa umeme kwa muda mrefu hali inayopelekea maendeleo ya kijiji hicho kudorora.Hata hivyo aliongeza kuwa wakandarasi wamekuwa wakionekana wakisimika nguzo za umeme hali inayotia hamasa kwa wananchi ya kutaka kujua ni lini wataunganishiwa na huduma ya umeme.

Akijibu swali la Mwenyekiti huyo Profesa Muhongo alimtaka mkandarasi anayesimamia mradi huo kutoka kampuni ya Derm Electrical Huseni Ayubu kutoa ufafanuzi ambapo mkandarasi huyo alieleza kuwa kazi ya kusimika nguzo pamoja na kuunganisha umeme inatarajiwa kukamilika mapema Februari mwakani.

Naye Profesa Muhongo aliwataka wanakijiji wa Bukabwa kuchangamkia fursa ya kuunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000. wakati mradi wa umeme ukiwa bado upo katika kijiji chao.

Alisema kuwa lengo la utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote ambavyo umeme umepita lakini havijaunganishiwa vinaunganishiwa ili kuhakikisha vijiji vyote vilivyopitiwa umeme vinapata umeme kwa kufuata utaratibu huo.

HELP THEM TO MAKE THIS CHRISTMAS SPECIAL FOR THE LESS FORTUNATE. YOU CHOOSE, THEY DONATE!

0
0
Untitled
In light of the holiday season Hellofood and Rotary Club of Bahari (Dar es Salaam) is running a Corporate Social Responsibility campaign called Light Up A Soul. This campaign allows the public to go to the following page http://lightupasoul.hellofood.co.tz/csr/ and choose what they would like to donate and Hellofood will donate it for them.

MGENI RASMI WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRICK SUMAYE AWASILI JIJINI MBEYA, TAYARI KWA KUONGOZA TAMASHA LA KRISMAS

0
0
1Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akiwasili  na ndege ya shirika la ndege la Fastjet kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe mjini Mbeya huku akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT), Askofu David Mwasota kushoto na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama Tayari kwa kuhudhuria Tamasha la Krismas ambalo linafanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Mh, Sumaye atakuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litashirikisha waimbaji wengi kutoka hapa nchini na nchi jirani.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE -MBEYA) 2Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akiwasili  na ndege ya shirika la ndege la Fastjet kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe mjini Mbeya huku akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT), Askofu David Mwasota na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama wa pili kutoka kushoto, mwisho kushoto ni MC Mwakipesile wa jijini Mbeya 3Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama  wakimsikiliza MC Mwakipesile mara baada ya kuwasili  na ndege ya shirika la ndege la Fastjet kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe mjini Mbeya. 4Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama  wakifurahia jambo kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT), Askofu David Mwasota na MC Mwakipesile. 5MC. Mwakipesile kulia na John Melele mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo wakifurahia jambo kwenye uwanja wa Ndege wa Songwe mkoani Mbeya.

Lowassa ahudhuria ibada ya Krismas Zanzibar

0
0
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akizungumza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania la Mwanakwerekwe, mjini Unguja, Zanzibar alipohudhuria ibada ya Skukuu ya Krismasi jana. Kulia ni Mchungaji wa Kanisa hilo, Philip Mvungi.
 Ibada ikiendelea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania la Mwanakwerekwe, mjini Unguja, Zanzibar,ambapo Mh.Lowassa na familia yake walihudhuria ibada ya Sikukuu ya Krismasi leo. 
 Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na mkewe Regina wakiwa na mjukuu wao, Angelica Freddy wakisoma Biblia katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania la Mwanakwerekwe, mjini Unguja, Zanzibar walipohudhuria ibada ya Skukuu ya Krismasi leo.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na mkewe Regina wakiwa na mjukuu wao, Angelica Freddy katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania la Mwanakwerekwe, mjini Unguja, Zanzibar walipohudhuria ibada ya Sikukuu ya Krismasi leo.
 Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Regina (kulia) akiwasalimia waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania la Mwanakwerekwe, mjini Unguja, Zanzibar walipohudhuria ibada ya Sikukuu ya Krismasi leo.
 

SERIKALI YALIFUNGIA SHINDANO LA MISS TANZANIA KWA MIAKA MIWILI

0
0

Serikali imelifungia shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili kutokana na sababu mbalimbali na ukiukwaji wa taratibu walizojiwekea, ikiwemo udanganyifu mkubwa unaojitokeza kila mwaka kwenye shidano hilo.

Maamuzi hayo yamechukuliwa na BASATA, ambapo Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kukaa kikao cha tathmini ambapo Kamati ya Miss Tanzania ilishindwa kujibu hoja za msingi za wadau na kukiri kuwepo udhaifu katika uendeshaji wa shindano hilo.

Baada ya kupitia maelezo yote na taarifa ya tathmini ya shindano hilo ni vyema tulisimamishe kwa muda ili mwandaaji ajipange upya, atakaporejea arejee kwa nguvu na kuandaa shindano lenye hadhi kubwa kuliko ilivyo hivi sasa'' alisema Mngereza.

Shindano hilo limekumbwa na kashfa mbalimbali tangu mwaka 2006 ikiwemo ya kuvisha mataji warembo wasiokidhi vigezo.

Chanzo cha Habari: Gazeti la Mtanzania, December 25.

KOCHA SUPER D AMPIGA TAFU YA VIFAA BONDIA MUSSA CHITEPETE WA SONGEA VIFAA

0
0
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akimkabidhi vifaa bondia Mussa Chitepete wa Songea vilivyotolewa na Super D kwa kushilikiana na marafiki zake wa kwenye mtandao wengine kulia ni Kiliani Shayo na Rajabu Mkamba ambaye ni mdau mkubwa wa kuhamasisha kusaidia mchezo wa masumbwi Picha na SUPER D BOXING  

KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kwa kushilikiana na marafiki zake wa kwenye mtandao wa kijamii wa watsupp wamemkabidhi vifaa bondia Mussa Chitepete wa Songea kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumwi nchini

Super D alimkabidhi vifaa hivyo bondia huyo hivi karibuni alivyotembelea jijini Dar es salaam kuja kushiliki mchezo wa masumbwi ambapo alipatiwa glove,gum shit,clip bandeji pamoja na kamba kwa ajili ya kurukia

vifaa hivyo vilivyotolewa na super D kwa kushilikiana na mdau mkubwa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mkumba ambaye ndie mwamasishaji mkubwa katika mtandao huo kwa ajili ya kusaidia mabondia

baada ya kukabidhiwa msaada huo bondia Mussa Chitepete wa Songea alishukulu wadau   mbalimbali kwa kumpatia vifaa na kumpongeza kocha Super D kwa kuanzisha mtandao ambaoumekuwa muhimu sana kwangu kwa mimi kupata vifaa najua sitotumia peke yangu wapo na wenzangu tutakao tumia nao pamoja vifaa hivi ambavyo itakuwa chachu ya kuinua mchezo wa masumbwi Songea

nae mdau mkubwa wa masumbwi nchini Rajabu Mkamba amesema kwa kushilikiana na Super D wamefanya mambo mengi kwa ajili ya kuinua mchezo wa masumbwi nchini hivyo atutoishia hapa tutaendelea kutoa sapoti kwa mabondia na wadau mbalimbali ili mchezo usonge mbele na wadhamini wajitokeze kusaidia ili vijana wawe na moyo wa kucheza mchezo wa masumbwi.

FREDRICK SUMAYE: KUWENI NA HOFU YA MUNGU, NAYE ATASIKIA MAOMBI YENU KWA TAIFA

0
0
1

SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIKA SIKU YA KWANZA

0
0
Desemba 16 mwaka huu Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi ,Mh Benard Membe alikabidhi bendera kwa Balozi Adadi Rajabu kwa niaba ya Mabalozi ,ikiwa ni ishara ya kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro na safari hiyo ilianza kwa muda wa siku sita.
Baada ya kupumzika katika eneo la Kisambioni na kupata chakula ,safari iliendelea ya kwenda kituo cha Mandara.
Kila mmoja alikuwa na Morali ya juu wakati wote wa kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baada ya kuongoza msafara wa Mabalozi kama ishara ya kuanzisha upandaji wa mlima Kilimanjaro kwa Mabalozi,hatimaye Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard Membe alifika eneo la Nusu njia.

TAMASHA LA WAFALME: DIAMOND, MZEE YUSUF WAWEKA HISTORIA DAR LIVE

0
0
Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Diamond na Idris wakifanya yao stejini.
Idris Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.
Diamond akichana mistari ya wimbo wa Muziki Gani na mshikaji aliyepanda stejini kumwakilisha Nay wa Mitego.
Baada ya mshikaji huyo kufanya makamuzi ya hatari, Diamond aliamua kumpatia shilingi 50,000.

Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live.
Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Diamond akifanya makamuzi na dansa wake.
Dansa wa Diamond akionyesha umahiri wake stejini.
...Sebene time.
Diamond akilitawala jukwaa kwa sarakasi.
NIMEMALIZA: Diamond baada ya kuwakonga nyoyo mashabiki wake waliofurika Dar Live na wao kuridhika aliamua kupozi nao kwa picha hii.
Ijumaa Sexiest Bachelor anayemaliza muda wake, Yusuf Mlela akiwasalimia mashabiki.
Diamond akisalimia na msanii wa filamu, Yusuf Mlela baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor. Taji hilo alikuwa nalo Mlela.
Diamond akipokea tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor kutoka kwa Mkurugenzi wa Kijumosi Traders Ltd, Mohammed Mustapha.
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa waandaaji wa shindano hilo, Amran Kaima akimkabidhi Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz cheti.
Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz akipozi na tuzo yake pamoja na cheti.
Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.
Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.
Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.
Mashabiki baada ya kupagawa na shoo ya Mzee Yusuf.
Diamond akiwachombeza mashabiki.
Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live.
Diamond akiwa kwenye jukwaa la kupanda na kushuka.
Mfalme Mzee Yusuf on da stage.
Mfalme akiwapa 5 mashabiki wake waliofurika Dar Live.
Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.
Nyomi ikiwa imedata na shoo kali kutoka kwa Mzee Yusuf.
Mzee Yusuf akicharaza gitaa.
Diamond akicheza sebene ndani ya Dar Live.
Platnumz akizidi kufanya yake stejini.
Diamond akimtambulisha kwa mashabiki mshindi wa zaidi ya milioni 500 za Big Brother Hotshots, Idris Sultan.


MFALME wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa Krismasi amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye Tamasha la Wafalmelililodhaminiwa na VODACOM pamoja na COCACOLA.

Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani.

Mbali na Diamond, Mfalme wa Taarab nchini, Mzee Yusuf naye alifanya shoo kali na kuwapagawisha mashabiki waliofika kwa wingi kuliko siku zote katika ukumbi huo wa kisasa wa Dar Live.
(PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA / GPL)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA INDIA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mtoto, Nabil Hahya (4) kutoka Jijini Dar es Salaam, mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Amina Yahya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.

PAMOJA NA MVUA KUBWA, TAMASHA LA KRISMAS LAACHA HISTORIA MJINI IRINGA

0
0
1Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akimtunza Mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchini DRC Congo wakati akiima kwenye tamasha la Krismasi lililofamyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili wakiwemo Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Bony Mwaiteje, Faraja Ntaboba kutoka DRC Congo, Solomon Mukubwa, Edson Mwasabwite Joshua Mlelwa, Ambwene Mwasongwe, Tumaini Njole, Emmanuel Mgogo na wengine wengi, hata hivyo mvua kubwa iliyonyesha mkoani Iringa imewafanya mashabiki wengi kutojitokeza katika tamasha hilo, Kundi zima la wanamuziki hao limekonga nyoyo za mashabiki mjini Iringa na linatarajiwa kuondoka kesho kuelekea Songea mkoani Ruvuma ambapo tamasha kama hilo litafanyika Desemba 29 kwenye uwanja wa majimaji.2Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akicheza wakati mwimbaji Faraja Ntaboba akiimba kushoto ni mwimbaji Upendo Kilahiro akishiriki kucheza.4Mwimbaji Edson Mwasabwite akiimba mbele ya mashabiki wake katika tamasha la Krismas kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.5Mwimbaji Edson Mwasabwite akiimba mbele ya mashabiki wake katika tamasha la Krismas kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.6Tumaini Njole na kundi lake wakitumbuiza kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.7Tumaini Njole akitumbuiza kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
8Baadhi ya mashabiki wakicheza muziki wakati wa tamasha hilo.9Mwibaji Upendo Kilahiro akiimba jukwaani.10Mwibaji Upendo Kilahiro akiimba jukwaani.11Emmanuel Mgogo akifanya vitu vyake.12Martha Mwaipaja akiimba kulia ni mwibaji Bony Mwapiteje.13Mwibaji Joshua Mlelwa akionyesha uwezo wake jukwaani.14Alex Msama kushoto akiwa na John Melele 15Waimbaji Ambwene Mwasongwe na Solomon Mkukubwa wakiongoza waimbaji wenzao jukwaani wakati alipokuwa wakiimba kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.16Upendo Nkone akiimba mbele ya mashabiki wake
Upendo Nkone kulia na Tumaini Njole wakicheza jukwaani.
19Mwimbaji Bony Mwaiteje akifanya vitu vyake jukwaani.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-IRINGA)

Mwigulu Nchemba mgeni rasmi Tamasha la Upendo wa Mama Dar

0
0
 
 NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuongoza Tamasha Maalumu la 'Upendo wa Mama' linalotarajiwa kufanyika katika Kanisa la Rutheran Mabibo Extenal jijini Dar es Salaam na kushirikisha waimbaji wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania. 

Akizungumzia tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam, Rais wa taasisi ya Upendo kwa Mama Foundation yenye makao makuu yake mkoani Arusha, Injinia Carlos Mkundi alisema Naibu Waziri Nchemba ndiye mgeni rasmi wa Tamasha hilo maalumu ambalo pamoja na mambo mengine linafanyika kutambua mchango mkubwa wa mama kuanzia katika ngazi ya familia na jamii nzima. Injinia Mkundi alisema tamasha hilo litakalofanyika Januari Mosi, 2015 chini ya uratibu wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, litashirikisha waimbaji wa injili akiwemo Faraja Ntaboba kutoka Congo, Stella Joel, Ado Novemba, Jane Misso, Edson Mwasabwite wote kutoka jijini Dar es Salaam. 

Na Rose Molel, Helen Kigazi wote kutoka mkoani Arusha. Injinia Carlos Mkundi na mwimbaji wa muziki wa injili ambaye naye atatumbuiza katika tamasha hilo, aliwataja waimbaji wengine ambao watashiriki katika tamasha ni pamoja na Mbunge, Matha Mlatta, Kwaya ya Mamajusi kutoka Moshi, mwimbaji Tumaini Njole, Messi Chengula na waimbaji wengine wengi. 

"...Washiriki kila mmoja anaweza kuja na mamayake anayempenda pamoja na zawadi yake maalum, ambayo atamkabidhi wakati itakapotangazwa...kutakuwa na waimbaji wa muziki wa injili kutoka nje na ndani ya nchi ili kuleta mvuto zaidi tunawaomba wananchi wajitokeze zaidi kuja kutambua mchango wa mama na kuonesha upendo kwa mama zao," alisema Injinia Mkundi. 

Akifafanua zaidi alisema Tamasha la Upendo kwa Mama litakuwa la bure na litaanza majira ya saa saba mchana siku hiyo na kuendelea hadi jioni litakapofungwa. Alisema siku hiyo washiriki wanaombwa kuja na zawadi maalumu ambayo kila mmoja atamkabidhi mamayake anayempenda katika familia zao. Rais wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, Injinia Caros aliongeza kuwa lengo lingine ni pamoja na kuwatia moyo akinamama na kuwaonesha upendo juu ya kazi kubwa wanayoifanya katika familia zao na jamii kwa ujumla.

 Alisema baada ya uzinduzi wa tamasha hilo kanisani hapo yataandaliwa matamasha mengine makubwa na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa pamoja na mengine katika mikoa mbalimbali. Aidha aliongeza tamasha kama hilo pia lilifanyika mkoani Arusha Novemba 16, 2014 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeib na kuwashirikisha akinamama zaidi ya 40,000.
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images