Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 429 | 430 | (Page 431) | 432 | 433 | .... | 1897 | newer

  0 0

   
  Frola Mbasha pichani kulia akiwa na Mumewe Mbasha wakati huo.
   
  Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania,Flora Mbasha,amekwenda katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar-Es-Salaam,akiomba kuvunjwa kwa ndoa yake na mumewe Emanuel Mbasha.

  Flora amefungua kesi ya madai namba 64 ya mwaka huu kesi ambayo inasikilizwa na hakimu mkazi,Devota Kisoka. Flora anadai kuomba kuvunja ndoa hiyo na apewe talaka ni kutokana na tabia ya mumewe kumpiga,kumnyanyasa na kushindwa kumpatia matibabu.

  Katika hati hiyo ya madaianaendelea kudai kwamba mgogoro wao waliwahi kuufikisha kwa ustawi wa jamii,kwa ajili ya upatanishi lakini ilishindikana wakashauriwa walifikishe suala lao mahakamani.

  Flora anaiomba mahakama itoe talaka,iamuru aendelee kukaa na mtoto,matunzo ya mtoto yatoke kwa mbasha na wagawane mali walizochuma pamoja.

  0 0

  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dkt Titus Mlengeya Kamani (Mb) akitoa hotuba ya ufunguzi wa Semina yaViongozi wa Wavuvi (BMU) iliyofanyika Hotel ya Monach Nansio Ukerewe, chiniya udhamini wa mfuko wa Pensheni wa PPF. 
  "Ndugu Meneja wa Kanda, napenda kuupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF ambao unatekeleza mojawapo ya sera zake ya kuhakikisha sekta isiyo rasmi inafikiwa kama ilivyo kwa sekta nyingine za uchumi hapa nchini. Hii itaongeza pato la Taifa hivyo kuzidi kuboresha maendeleo ya Watanzania kwa ujumla na kupunguza umaskini. Napenda kuwaambia kuwa kwa kuandaa semina hii muhimu katika eneo ambalo mimi mwenyewe nalisimamia imenipa faraja sana kwa kuona jinsi Mfuko huu wa PPF unavyowajali sekta zote za uchumu wa nchi. Hongereni sana."
  Kwa mujibu wa Meneja wa Kanda ya Ziwa Ndugu Meshack Bandawe (pichani aliyesimama) alisifia Mahudhurio ya semina hiyo akisema kuwa yanadhihirisha kuwa kuna mwamko wa jamii ya watanzania kuhusiana na masuala ya hifadhi ya jamii unaendelea kukua na kuimarika. 
  Wanasemina wakichukuwa data muhimu.
  Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Mary Onesmo Tesha akitoa neno la shukurani pamoja na kukazia umuhimu wa mafunzo yanayotolewa kwa wananchi na vikundi kuhusu mifuko ya pensheni.
  Huku wakizidi kuongezewa maarifa na manufaa ya semina husika, tayari wavuvi zaidi ya 2000 wameshajiunga na PPF. 
  Pia wanasemina hao walipata fursa ya kuuliza maswali pamoja na kufanya majadiliano ikiwa ni sehemu ya kupima uelewa. 
  PPF imeweka mikakati ya kuwafikia zaidi ya wavuvi 4000 katika wilaya ya Ukerewe. Aidha, PPF mapema mwakani ipo katika mkakati wa kufanya utafiti kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kukopesha vikundi mbali mbali vya ujasiriamali vilivyopo katika sekta zisizo rasmi.

  IFUATAYO NI SEHEMU YA MWISHO YA HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT TITUS KAMANI (MB):-
  Ndugu Viongozi na Wawakilishi wa Wavuvi, nitoe rai kwenu kuipa nafasi semina hii muhimu ili muweze kuangalia wapi panahitaji kuboreshwa kwani hii itawasaidia kupiga hatua katika uvuvi wenu. Kwani kwa taarifa nilizonazo zoezi hili la kujiunga na PPF limefanikiwa sana ila changamoto kubwa ikiwa ni uwasilishaji wa michango yenu PPF.


  Napenda kuwahamasisha kuwasilisha michango kwa wakati katika Mfuko wa PPF kwani ni Mfuko mkongwe ambao vile vile umezidi kuboresha mifumo ya Tehama kwani sasa kupitia simu ya mkononi unaweza kuwasilisha mchango wako kupitia M-pesa,Tigo Pesa na Airtel money. Kwenu nyie kutokana na asili ya kazi yenu ya uvuvi njia hizi ni muafaka zaidi katika kuwasilisha michango yenu kwa wakati.


  Ndugu Viongozi na Wawakilishi wa Wavuvi, kwa kuwa nimeambiwa kuwa hapa tulipo kuna viongozi wa wavuvi wasiopungua 50, hii inaashiria jinsi mlivyolipa uzito suala hili la kujua manufaa yaliyomo ndani ya Mfuko wa PPF na hatimaye muweze kujiunga. Sasa napenda niseme hivi, nyinyi viongozi mliofika hapa mchukue jukumu la kusimamia zoezi hili katika maeneo yenu ya kazi ili wavuvi wengi waweze kukwamua maisha yao kutoka uvuvi duni kwenda uvuvi wa kisasa. Hivyo basi mnapaswa kuangalia kwa makini mambo yafuatayo:-

  ·                    Kila kiongozi awe na orodha ya wavuvi walioko katika kituo chake ambao tayari wamesajiliwa

  ·                    Kila kiongozi lazima afahamu kilammoja anachangia kiwango gani aidha kwa wiki au kwa mwezi na kuweka kumbu kumbu kwa ajili ya mrejesho

  ·                    Kila kiongozi awe na namba za simu za wavuvi walioko katika kituo chake

  ·                    Kila kiongozi ajiridhishe kila mvuvi aliyejisajili awe na kitambulisho cha uanachama cha PPF

  ·                    Kila kiongozi kuhakikisha anafahamu wavuvi wote wasiojisajili na PPF au Mfuko wowote

  ·                    Viongozi wote wachukue jukumu la kuhamasisha wavuvi wote walioko katika vituo vyao wajiunge na kuchangia katika Mifuko ya hifadhi ya jamii kama Mfuko wa Pensheni wa PPF

  ·                    Vile vile nitoe agizo kwa viongozi wote na wawakilishi wa wavuvi wafanye kazi kwa karibu na ofisi ya PPF kanda ya Ziwa  kwa ajili ya ufanisi na manufaa  ya wavuvi kwa ujumla


  Ndugu Meneja wa Kanda, baada ya kusema hayo, sasa naomba niwakabidhi jukumu hili la kutoa semina kwa viongozi hawa wa wavuvi ili mkawasajili wavuvi waweze kufaidika PPF ili kuboresha maisha yenu na ustawi wa jamii.

  0 0

   Mratibu wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima, Bi Neema Gerald (wa pili kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutangaza uzinduzi wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima, ambazo zitamulika na kutambua mchango wa uongozi uliotukuka wa bodi za wakurugenzi kwenye sekta za benki na bima nchini. Tuzo hizo zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam January 30, 2015. Ameambatana na Bw. Laurence Mwangoka (wa kwanza kulia), Meneja Mauzo wa Serena Hotel ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo pamoja na wawakilishi kutoka Capital Plus International (CPI), Bw. Matthew Kasonta (wa pili kushoto), na Bw. Kassim Malela (kushoto).
  Bw. Matthew Kasonta (katikati), mwakilishi kutoka Capital Plus International (CPI) ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, kutangaza uzinduzi wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima, ambazo zitamulika na kutambua mchango wa uongozi uliotukuka wa bodi za wakurugenzi kwenye sekta za benki na bima nchini. Tuzo hizo zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam January 30, 2015. Ameambatana na Bw. Laurence Mwangoka (wa kwanza kulia), Meneja Mauzo wa Serena Hotel ambao ni moja kati ya wadhamini wa tuzo, Mratibu wa tuzo hizo, Bi. Neema Gerald (wa pili kulia) na mwakilishi kutoka Capital Plus International (CPI) Bw. Kassim Malela (kushoto).  

  TUZO za Bodi yenye Uongozi Bora ijulikanayo kama Best Board Leadership Award (BBLA), ambazo zimelenga kutambua uongozi bora wa Bodi za Wagurugenzi katika sekta ya kibenki na bima, zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi ujao. BBLA iliyopangwa kufanyika mwezi Januari tarehe 30 na kufanyika kwa mara ya kwanza nchini, inaandaliwa chini ya mwamvuli wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) na Chama cha Makampuni ya Bima Tanzania (ATI).

  Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa BBLA Bi. Neema Gerald alisema tuzo hizo zinatoa fursa ya ufahamu wa jinsi gani bodi bora inaweza kusaidia taasisi kupata mafanikio na kufikia utendaji bora hususani katika eneo walilobobea kiutalaam.

  Wadhamini wa tukio hilo la kipekee ni pamoja na Capital Plus Internaional Limited, Real PR Solutions Limited, Afrimax Strategic Partnerships Limited, Serena Hotel na IPP Media, wakati wadhamini wengine wakiaswa kujitokeza zaidi kuunga mkono tuzo hizo.

  "Tumeona umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na wakurugenzi wa bodi katika taasisi zao.Tunaamini kuwa katika kila mafanikio ya taasisi ya kifedha, nyuma yake kuna bodi ya wakurugenzi imara na makini. Sasa, sifa hizo ambazo wajumbe wa bodi wengi wanakuwazo zinapaswa kutambuliwa na kuthaminiwa, "alisema.

  Bi. Neema alisema kuwa utamaduni unaojulikana ni kuwa ni Maafisa Watendaji Wakuu na Wakurugenzi Wakuu pekee ndiyo wanaothaminiwa na kutambuliwa na waajiriwa au jamii nzima kwa ujumla. "Ni wakati muafaka sasa kwa bodi zenye utendaji bora kutambuliwa na kuzawadiwa kikamilifu kwa jitihada zao," alisema. Alibainisha kuwa zoezi hilo, tathmini na upangaji wa mwisho wa matokeo utafanywa na jopo la majaji waliobobea na wenye rekodi bora za kiutendaji.

  Tathmini hiyo italenga zaidi katika ufanisi wa Bodi ya Wakurugenzi katika suala la utawala wa taasisi, usimamizi wa fedha na uwezo wa kuiongoza dira ya taasisi kwa ujumla wake. Maeneo mengine ni umakini wa bodi katika uwazi, uwajibikaji, utendaji, na ufuataji wa hatua madhubuti na  utendaji wake.

  Alitaja maeneo mengine ambayo bodi itafanyiwa tathmini kuwa ni utoaji wa mitazamo yakinifu ya bodi katika kusisitiza umuhimu wa utendaji wa mtaji watu katika ngazi ya bodi na kuweka mbele vigezo vitakavyowezesha utendaji bora zaidi wa bodi, "alisema.

  Aliongeza kuwa tuzo hizo zimeanzishwa kwa wakati muafaka nchini wakati ambapo sekta za Bima na kibenki zinapitia mabadiliko makubwa na kujitokeza kwa makampuni mengi ya bima na masoko zaidi kuongezeka ili kufikia wateja wengi katika nyanja zote za maisha.

  "Kwa mabadiliko haya wakati huu, hasa katika sekta ya fedha ambapo idadi kubwa ya makampuni ya bima na mabenki zimekuwa zikifungua biashara Tanzania, wateja wanahitaji kuwa na uhakika kuwa malipo yao ya bima yako salama na wanaweza kupatiwa kwa wakati wowote", alisema, na kuongeza:

  "Hili litafanikiwa tu endapo kampuni hiyo ya bima au benki itaendelea kufanya kazi kwa mafanikio. Kwa maana hiyo, bodi ya wakurugenzi itakuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha kampuni hiyo haifi, "alisema.

  0 0
 • 12/19/14--01:21: Article 7
 • Kwa nguo zaidi za kisasa tembelea www.vazitz.blogspot.com au Instagram @Vazitz

  0 0

  KIKOSI cha timu ya Friends Rangers, kesho kinajitupa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni Mwembechai, kuvaana na timu ya Ndanda FC ya Mtwara, katika mchezo  wa kirafiki wa kijaindaa na mzunguko wa pili wa ligi daraja   la kwanza.

  Ofisa habari wa timu hiyo Asha Kigundula, alisema kikosi   hicho kinashuka dimbani kikiwa ni sehemu ya maandalizi ya  mzunguko wa pili wa ligi hiyo inayoanza kutimua vumbi  Ijumaa ya Desemba 26.

  Alisema kwa kutambua umuhimu wa michuano hiyo ambapo  wao wataanzia ugenini dhidi ya Lipuli ya Iringa, imejipanga kupata mechi kadhaa za kirafiki, ambapo kesho Jumapili  itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Ruvu Shooting.

  Kigundula alisema kuwa kikosi chao kipo katika maandalizi  makali ya kuhakikisha  kinaendeleza rekodi yake ya  kutofungwa kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo.

  Alisema timu yao chini ya kocha wake Ally Yusuph 'Tigana'  kimewasajili Haruna Moshi 'Boban' Amir Maftah, na Robert, wengine ambao wamekuja kwa mkopoWine Abbas kutoka  Ruvu Shooting na Mahamod Osman kutoka Coastal Union.

  "Tunaendelea kukinoa kikosi chetu kwa kupata mechi nyingi  za kirafiki lengo letu ni kuendelea na safari yetu ya kupanda  daraja, ambapo msimu ujao tunataka kucheza ligi kuu"alisema  Kigundula.

  Friends Rangers inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi  daraja la kwanza, huku Majimaji ikishika usukani wa ligi hiyo.

  0 0

  Meneja wa Bidhaa za Intaneti wa TTCL, Abdul Mombokaleo (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) , anayefuata ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa TTCL, Laibu Leonard.
  Meneja wa Bidhaa za Intaneti wa TTCL, Abdul Mombokaleo (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani), kulia ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa TTCL, Laibu Leonard na Kushoto ni Ofisa habari wa TTCL.
    
  KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imezinduwa huduma mpya kabambe ambayo inampa mteja wa kampuni hiyo fursa ya kufurahia modem ya bure na vifurushi vya intaneti kwa bei nafuu, huduma ambayo imetolewa kama ofa kwa wateja hasa katika kuelekea siku kuu za Chrismas na Mwaka mpya.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam juu ya huduma hiyo, Meneja Huduma za Intaneti wa TTCL, Abdul Mombokaleo amesema kampuni ya Simu Tanzania imeamua kuzindua promosheni mpya ya “DILI LA UKWELI” inayotoa fursa ya mteja wa TTCL kufurahia huduma ya intaneti kwa bei nafuu zaidi na kujipatia modem.

  "...TTCL siku ya leo imezindua promosheni mpya ya “DILI LA UKWELI” inayotoa fursa ya mteja wa TTCL kufurahia huduma ya intaneti kwa bei nafuu zaidi na kujipatia modem ya bure.

  Akifafanua zaidi Mambokaleo alisema promosheni hiyo mpya ya “Dili la Ukweli” inatoa fursa kwa wateja kufurahi modem ya bure pamoja na vifurushi ambavyo vimepunguzwa bei kwa kiwango ambacho Mtanzania wa kawaida anaweza kuimudu.

  Aidha akifafanua juu ya utaratibu wa promosheni alisema ili mteja apate modem ya bure Mteja atapaswa kununua intaneti bila kikomo kwa shilingi 20,000/- tu ambayo itatumika ndani ya mwezi mzima na huduma hiyo ni kwa wateja wapya tu. 

  "...Kwa mteja wenye modem tumewapa fursa ya kuchagua vifurushi ambavyo vimepunguzwa bei. DILI LA UKWELI inatoa fursa kwa wateja kufurahia punguzo la bei ya vifurushi vya intaneti vya siku, wiki na mwezi kwa bei nafuu sana. Intaneti ya TTCL inaubora, ina kasi na uwakika, kwani teknolojia inayotumika ni ya kuaminika zaidi. Katika kuhakikisha wateja wa huduma ya intaneti wanafurahia zaidi, TTCL imeshusha bei ya intaneti ili kuendelea kukidhi mahitaji ya wateja wake.


  0 0

  A PERSONAL JOURNEY: FROM PARASITE IMMUNOLOGY TO DISEASE CONTROL.


  MWELECELE MALECELA


  My career at NIMR is a true story of serendipity rather than design. I joined NIMR in 1987 after graduating form the University of Dar-es-Salaam with a B.Sc. in Zoology in 1986. After an extremely rigorous interview process I was assigned to work at the Amani Center and to specifically focus on a disease they called Bancroftian Filariasis. 

  Now I had heard of this disease in my classes at UDSM and the great tutelage of Dr Parkin but I had know idea what I was going to do. In my mind I wanted to work on malaria which at the time I thought was  more interesting area of research. So I must say I was quite depressed as at the time Malaria research had the most resources in terms of funding and equipment. I was told explicitly that I was to work to revive the Bancroftian filariasis work at Amani.


  As one who always thrives on a challenge I set off for my long trip up the Eastern Usambara Mountains to this place they called Amani. The trip was up a series of undulating hills until we got to a point where I did not see houses or people. My fear was supressed by the breathtaking beauty of the drive, the beautiful forest, and the air getting clearer as we drove up the hill. On arrival at Amani my fears attacked me again, could I do it how was I expected to live here almost in the middle of nowhere. I consoled myself by reminding myself that there were several scientists here and that if they could live here so could I. My dad had a favourite saying that “its up to you to manage your circumstances” and that is exactly what I decided to do.

  After several weeks of orientation I was finally designated to work in the helminthology laboratory where I learnt all about this parasite Wuchereria Bancrofti, the parasite that spreads bancroftian filariasis. I learnt to identify microfilariae of Wuchereria Bancrofti and Onchocerca volvulus. 

  I learnt to dissect mosquitoes for infective larvae and the lab diagnosis of several parasites including schistosomes, hookworms, Trichuris etc. At the time mine was a predominantly wormy world and the people who truly initiated me into the wonderful world of worms were some great lab technicians and lab assistants who gave me the best hands on training I ever had.

   I treasure this training because it has played a great role in making me who I am today. One lab assistant liked to remind me that he started working on the month I was born. It didn’t affect me that they treated me like a kid I just soaked up all the information that was being given to me and enjoyed every moment. My family sometimes worried about how i was doing I would phone them from our old handle phones connected through the tiny exchange to tell them that I was doing fine and that I actually liked it there.
  My early work included examining the relationship between eosinophilia and helminth parasites, I also looked at the impact of the trials for vector control for malaria on the transmission of Bancroftian Filariasis. I also worked with the late Prof Chris Curtis to control culicines in Muheza town using polystyrene beads.


  I then went on to do my Msc and PhD at the London School of Hygiene and Tropical Medicine of the University of London, where I worked on filarial infection in cats. The cats was an experimental animal model that provided a lot of current knowledge in the understanding of the pathogenesis of filarial infection. The work I did focused on understanding how parasites evaded the hosts immune system and my findings indicated that there were surface immunoglobulins of the host that actually protected the parasite. This added to the body of knowledge on asymptomatic microfilaraemics people who have microfilariae but have no overt symptoms of the disease.


  On my return I was involved in developing a study to understand immunoepidemiology of Lymphatic Filariasis Transmission, a study that took place in sites in Kenya(Kingwende) and Tanzania (Masaika). Several papers came out of this study which allowed us to getter a better understanding of the spatial dynamics of LF transmission which would be very useful in developing effective control programmes.  At the same time I was involved with developing a strategic plan for the Elimination of the Lymphatic Filariasis Program of Tanzania. This followed the WHA resolution in May 1997 that called for the Elimination of Filariasis as a public health problem. The development of the comprehensive plan was followed by appointment to be the Director of the LF programme in 2000.

   In the year 2000 the LF program was launched on the island of Mafia and my legacy from the lab to the field to control came full circle. There is a swahili saying that says “safari moja huanzisha nyingine” literally translated means the end of one journey is the beginning of another! In my case however there has been no end to this journey just different points where I have paused but moved on in the same direction.


  The LF programme has moved from strength to strength and is now functional in 53 districts and has reached 13 million people. With the focus now on neglected tropical diseases the approach has been integrated to include treatment for schistosomiasis, Soil Transmitted Helminths and Trachoma. 

  In many ways my interview at the NIMR Headquarters prepared me for a career in Lymphatic Filariasis Research and Control but like all things in life I did not know it then. It gave me great pride when President Kikwete announced that he was going to start an LF Fund to support the people with the debilitating manifestations of the disease. H.E the President announced this at the Global Alliance Meeting in Arusha and this has raised the profile of the patients both in Tanzania and other countries in Africa. 

  Results from our sentinel site in Tandahima show that the programme may have succeeded in interrupting transmission in the district charting it our to be the first district to have attained interruption of transmission of LF on  Tanzania mainland.
  [IMG_7940.jpg]
  So is this a success story? Its a story about a young girl who dreamed about being a researcher, about a young woman who climbed the hills of Amani in search of that dream, and the woman who is living that dream doing research and contributing to the control of a disease she has worked on all her life! I would say that’s success wouldn’t you!


  I am indebted to so many people who made this journey possible but most of all my parents Dr John Malecela and the late Mrs. Ezerina Malecela who told me in no uncertain terms that “yes I could”.  Relevant publications

  Malecela M.N. Baldwin C.I and Denham D.A (1994) Hosts antigen on the surface of microfilariae of Wuchereria bancrofti and Brugia pahangi.

  Transactions

  Awarded prize for best presentation


  Baldwin C.I., Medieros F, Malecela M.N. and Denham D.A (1994) Humoral responses in cats repeatedly infected with Brugia pahangi. Parasite 1,1S


  Malecela (1995): Microfilariae and the immune response in cats repeatedly infected with Brugia pahangi. Ph.D. thesis, University of London.


  P.E.Simonsen, D.W Meyrowitsch, W.G.Jaoko,M.N.Malecela, D.Mukoko, E.M.Pedersen, J.H. Ouma, R.T.Rwegoshora, N.Masese, P.Magnussen, B.B.A Estambale and E.Michael (2001) Bancroftian Filariasis infection,Diseaese and Specific Antibody Response Patterns in a high and a low endemicity community in East Africa. Parasite Immunology 23: 373-388


  Michael E., Simonsen P.E., Malecela M., Mukoko D., Pedersen E.M., Rwegoshora R.T., Meyrowitsch D.W, Jaoko W.G., (2001)Transmission intensity and immunoepidemiology of bancroftian filariasis in East Africa. Parasite Immunology No 23. Pp 373-388


  Paul Simonsen,Peter Bernhard, Walter Jaoko, Dan Meyerowitsch, Mwele N.Malecela-Lazaro, Pascal Magnussen and Edwin Michael (2002) Filaria Dance sign and subclinical hydrocele in two East African communities with Bancroftian filariasis. Transactions of the Royal Society of Tropical Medicine and Hygiene


  Simonsen,P.E, Meyerowitsch, D.W, Jaoko W.G., Malecela, M.N., Mukoko, D., Pedersen, E.M., Ouma,J.H., Rwegoshora, R.T., Masese.N Magnussen, P., Estambale, B.B.A & Michael E. (2002) Bancroftian filariasis infection disease and specific antibody responses patterns in a high and low endemicity community in East Africa. American Journal of Tropical Medicine and Hygiene Vol 66(5) pp550-559


  Simonsen P.E Meyrowitsch D.W., Mukoko D, Pedersen E.M., Malecela-Lazaro M.N., Rwegoshora R.T., Ouma J.H., Masese, N. , Jaoko W.G., Michael E., (2004) The effect of repeated half-yearly mass treatment on Wuchereria bancrofti infection and transmission in two East African communities with different levels of endemicity. American Journal of Tropical Medicine and Hygiene No 70 pp. 63-71


  Paul E. Simonsen, Stephen M. Magesa, Samuel K. Dunyo, Mwele N. Malecela-Lazaro, Edwin Michael (2004) The effect of single dose ivermectin alone or in combination with albendazole on Wuchereria bancrofti infection in primary school children in Tanzania. Transactions of the Royal Society of Tropical Medicine and Hygiene 98,462-472


  Simonsen,P.E., Meyerowistch D.W., Mukoko,D., Rwegoshora,R.T., Pedersen,E.M., Malecela Lazaro M.N., Jaoko W.G., and Michael E.(2005) The effect of eight half-yearly single-doses treatments with DEC on Wuchereria bancrofti circulating antigenaemia. Transactions 99,541-547.

  0 0


  0 0

   
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea kwenye Sherehe za Mazimisho ya Miaka 4o Tangu kuanzishwa Kwa Shule ya Msingi Misufini Iliyopo Manispaa ya Morogoro.Katika Maadhimisho Hayo Mbunge wa Jimbo Hilo alifanya Aliongoza Harambee Nas Jumla ya Shilingi Millioni 5.8 Zilichangwa Ambapo Yeye Alichangia Jumla ya Shilingi Milioni 4.5
     Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akikagua Mazingira Mbalimbali ya Shule ya Msingi Misufini. kwenye Sherehe za Mazimisho ya Miaka 4o Tangu kuanzishwa Kwa Shule ya Msingi Misufini Iliyopo Manispaa ya Morogoro.Katika Maadhimisho Hayo Mbunge wa Jimbo Hilo alifanya Ukaguzi na Kuikuta Shule Hiyo Ikiwa Katika Hali Mbaya Vyumba vya Madarasa ni Chakavu,Havina Milango Wala Madirisha Licha Ya shulie Hiyo Kuafulisha wanafunzi kwa Kiwango Kikukbwa Ndani ya Wilaya ya Morogoro Mjini.
  Uchakavu wa Madarasa ya Shule ya Msingi Misufini iliyotimiza Miaka 4O Tangu Kuanzishwa kwake  Ikiwa Katika Hali mbaya sana ya Uchakavu ya Miuondo Mbinu ya Shule Hiyo.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Misufini Wakiwa katika Gwaride Maalum la Kumpokea Mh Mbunge ambaye alikuwa Mgeni Rasmi Kwenye Maadhimisho ya Miaka 4o ya Shule hiyo.. 

  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Misufini Mwl Jane Mlawa Akitoa Taarifa Fupi kwa Mh Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjni Aziz Abood Kuhusu Shule Hiyo Kabla ya Kuanza Kwa Shuguli
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Meza Kuu na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Misufini Mwl Jane Mlawa Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 4O Tangu Kuanzishwa kwa shule hiyo.
  Baadhi ya Wazazi wa wanafunzi wanaosoma Shule Hiyo
  Walimu wanaofundisha Shule ya Msingi Misufini wakijumuika Kuimba Wimbo wa Taifa kabla ya Kuanza kwa Maadhimisho hayo
  Ngonjera Ikiwasilishwa kwa Ufasaha na Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Misufini Iliyopo Mkoani Morogoro. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Misufini Mwl Jane MlawaAkijumuika na wanafunzi  Wake kuimba wimbo maalumu kwajili ya Mgeni Rasmi.


  0 0

   Jokate na Guoxun wakionyesha mikataba baada ya kusaini
   Jokate na Guoxun wakibadilishana mikataba baada ya kusaini.
   Jokate Mwegelo akizungumza katika hafla hiyo
   Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited  (CEO), Deng Guoxun akuzungumza katika hafla hiyo

   Jokate akiteta jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa kwenye hafla hiyo
   Wageni mbalimbali waalikwa wakishughudia hafla hiyo
  Meya wa Manispaa ya Ilala akiteta jambo na Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mariam Kisangi katika hafla hiyo.

   
  Dar es Salaam. Mbunifu mavazi, Miss Tanzania wa namba mbili 2006,  mwanamuziki na muigizaji wa filamu, Jokate Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na kampuni ya Kichina,  Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.Makubaliano hayo yalisainiwa leo kwenye hotel ya  Serena baina ya Jokate na Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited  (CEO), Deng Guoxun.
   
  Akizungumza katika hafla hiyo,  Jokate alisema kuwa makubaliano hayo ni ya kudumu na kampuni hizo mbili zitazalisha na kuuza bidhaa za kidoti Tanzania nzima na nje ya mipaka yake.
   
  Alifafanua kuwa kampuni ya China itawekeza Tanzania na kuwafaidisha watanzania kwa kutoa nafasi ya ajira. Alisema kuwa pia wanatarajia kujenga kiwanda ili kuinua uchumi wa nchi na maisha ya watanzania.
   
   “Hii ni hatua kubwa ya maendeleo kwangu, kama unavyojua, wakati naanza kujishugulisha na masuala ya urembo, ubunifu na uanamitindo, sikutegemea kufikia hatua hii ya kuingiza bidhaa zangu kimataifa, lakini sasa, ndoto zangu zimetimia na najivunia mafanikio haya,” alisema Jokate.
   
  Alisema kuwa mbali ya kutoa mitindo tofauti ya kisasa ya nguo, kampuni yake pia itazalisha aina mbali mbali za viatu, nywele ikiwa pamoja na  mawigi,  weaving, Rasta na viatu vya wazi (sandals) ambazo kwa sasa zipo tayari kwenye soko la Tanzania. 

  “Mpango wangu ni kupanua soko la bidhaa zangu kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika Kusini na nchi nyingine za Afrika,” alisema.
  Afisa Mtendaji wa Guoxun alisema kuwa wamefurahi kukamilisha ubia na kampuni ya Kidoti na haya ni matunda ya ushirikiano wa kudumu baina ya serikali yao na Tanzania.
   
   “Tumefurahi sana kukamilisha makubaliano haya, tunatarajia kuongoza katika soko la hapa nchini na wenzetu (wachina) watafaidika pia, ” alisema Guoxun.


  0 0

  Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (katikati) akizindua rasmi Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 leo jijini Dar es salaam. unnamed1 
  Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servicius Likwelile chapisho la lenye Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam. unnamed2Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa(Kushoto) akitoa ufafanuzi wa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa iliyofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu iliyotumia tafiti za taifa zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka 2001 hadi 2007.Kulia ni Waziri wa Fedha Mh. Saada Salum Mkuya.unnamed3 
  Baadhi ya viongozi na wageni waliohudhuria uzinduzi wa usambazaji wa Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 wakimsikiliza Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Bw. Daniel Masolwa wakati akiwasilisha mada kuhusu Pato la Taifa leo jijini Dar es salaam.

  ....................................................................................................
  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  . Dar es salaam.
  Serikali imesema kuwa Pato la Taifa kwa mwaka 2007 limeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 26.8 ikilinganishwa na trilioni 20.9 za mwaka 2001, ambapo wastani wa pato la mwananchi mmoja mmoja limeongezeka kutoka shilingi milioni1,186,200/= mwaka 2001 hadi shilingi milioni 1, 561,050/= mwaka 2013. 
  Akizindua usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum ameeleza kuwa matokeo hayo ni sawa na ongezeko la ukubwa wa Pato la Taifa kwa asilimia 27.8.  Amesema ongezeko hilo ni matokeo ya juhudi za Serikali kuweka mazingira mazuri na kutengeneza fursa za kuwawezesha wananchi kufanya kazi za kujiajiri na hatimaye kupata kipato halali kwa kazi wanazofanya. 
  Mh. Mkuya amesema kuwa kukua kwa uchumi wa Tanzania kumechangiwa na kujumuishwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo Sayansi na Teknolojia ambako kumetoa fursa kwa wananchi kujiongezea kipato hususan matumizi ya simu za kiganjani ambazo zimerahisisha mawasiliano na utafutaji wa masoko ya bidhaa ndani na nje ya nchi.
  Amezitaja shughuli nyingine kuwa ni ukamilishaji wa miamala mbalimbali ya kibenki na mikopo ambazo zimekuzwa na sekta ya mawasiliano , kuongeza ajira na kupunguza muda wa kusubiri huduma za malipo katika maeneo mbalimbali nchini.   Aidha, amefafanua kuwa kuongezeka kwa thamani ya Pato la Taifa kunaiongezea Serikali uwezo kimapato kupitia kodi na kuiwezesha kugharamia ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
  “Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya Binafsi ya mwaka 2012 unaonyesha asilimia 60 ya kaya zote nchini zinapata maji safi na salama hasa hususan maeneo ya mijini,zaidi ya asilimia 20 ya kaya zote nchini zinatumia nishati umeme haya ni mafanikio makubwa ya matokeo ya ukuaji wa uchumi nchini” Amesisitiza Mh. Mkuya. 
  Akizungumzia mchango wa Sekta Binafsi katika kukua kwa pato la taifa nchini amesema kuwa ajira zipatazo laki nne kati ya laki sita katika sekta iliyo rasmi zimepatikana.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema kuwa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa imetumia Tafiti za Taifa zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka 2001 hadi 2007.
  Amezitaja tafiti hizo kuwa ni pamoja na utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya wa mwaka 2007, Sensa ya Kilimo iliyofanyika mwaka 2008 na Takwimu nyingine za utawala kutoka katika Wizara na Idara za Serikali.
  Aidha, amefafanua kuwa ukokotoaji wa takwimu hizo umefuata mfumo wa Umoja wa Mataifa wa kutayarisha takwimu za Pato la Taifa wa mwaka 1993 na 2008 kwa lengo la kuhakikisha kuwa takwimu hizo zinalinganishwa na takwimu nyingine duniani.

  0 0
  0 0

  Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Dk. Ave Maria Semakafu akizungumza katika mkutano huo na wahariri wa vyombo vya habari. Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Dk. Ave Maria Semakafu akizungumza katika mkutano huo na wahariri wa vyombo vya habari.Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mtandao wa Wanawake na Katiba pamoja na TAMWA wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa. Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mtandao wa Wanawake na Katiba pamoja na TAMWA wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa.Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Valerie Msoka akiwasilisha mada katika mkutano huo wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na TAMWA. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Valerie Msoka akiwasilisha mada katika mkutano huo wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na TAMWA.Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akiuliza swali katika kipindi cha majadiliano mara baada ya uwasilishaji mada. Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akiuliza swali katika kipindi cha majadiliano mara baada ya uwasilishaji madaMmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akiuliza swali katika kipindi cha majadiliano mara baada ya uwasilishaji mada. Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akiuliza swali katika kipindi cha majadiliano mara baada ya uwasilishaji mada.

   MTANDAO Wanawake na Katiba nchini pamoja na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) wamesema wanaunga mkono Katiba iliyopendekezwa na kujivunia hatua waliopiga katika kudai haki mbalimbali za mwanamke kwenye Katiba hiyo ukilinganisha na ile ya Mwaka 1977. Mtandao huo umetoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuzungumzia hatua ambayo mtandao huo unaoshirikisha zaidi ya hasasi 50 zinazopigania haki anuai katika jamii.

   Akizungumza katika mkutano huo na wahariri wa habari, Mjumbe wa Mtandao huo, Dk. Ave Maria Semakafu alisema harakati za kutetea haki za binadamu na hususani za wanawake na watoto zilipata mwanya katika mchakato wa Katiba uliyomalizika jambo ambalo alisema ni hatua kubwa ya safari ya kumkomboa mwanamke. 

  Dk. Maria Semakafu alisema kwa kuona mwanya nahatua waliopiga wanaharakati katika masuala hayo, kwa kupitia Mtandao wa Wanawake na Katiba pamoja na TAMWA wanaiunga mkono Katiba Pendekezwa kwa kile kuwa na utofauti mkubwa kimaboresho ukilinganisha na ile ya mwaka 2014. Alibainisha kuwa licha ya mapungufu kidogo yaliopo lakini umoja huo umefanikiwa. "..Mtandao unatambua kuwa kuna mapungufu yaliopo lakini kubwa zaidi ni kwamba ukilinganisha naKatiba ya Mwaka 1977, Katiba Pendekezwa imemtambua Mwanamke na imempa nafasi stahiki kushiriki katika kujenga, kulinda, kuilinda na kuitetea demokrasia inayozingatia haki za usawa," 

  alisema Dk. Maria Semakafu. Akitolea mfano alisema madai ya msingi 12 ambayo mtandao ulipaza sauti kutaka kuingizwa ni pamoja na haki za Wanawake kuainishwa kwenye Katiba Mpya, sheria Kandamizi kubatilishwa, kulindwa kwa utu wa mwanamke, utekelezwaji wa mikataba ya kimataifa kuhusu haki za wanawake na haki sawa katika nafasi za uongozi. 

  Aliongeza kuwa mambo mengine ni haki za watoto wa kike, haki za kufikia, kutumia, kunufaika na kumiliki rasilimali, haki za uzazi salama, haki za wanawake wenye ulemavu, haki za kufikia na kufaidi huduma za msingi, kuwepo kwa tume ya usawa wa kijinsia na kuwa na mahakama ya familia katika katiba mpya.

   "...Kwa kiasi kikubwa katiba iliyopendekezwa imezingatia masuala mengi yaliodaiwa na mtandao. Tunatambua juhudi kubwa zilizofanywa na wanawake na wanaume wote wa Bunge Maalum la Katiba, na kuwapongeza kwa yale yote waliyoyatetea kwa nguvu zote na hatimaye kuzingatiwa katika Katiba," alisema Dk. Maria Semakafu. 

   Akizungumza awali kabla ya kumkaribisha Dk. Maria Semakafu, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Valerie Msoka alivipongeza vyombo vya habari kwa kukubali kupaza sauti juu ya madai anuai ambayo yalitolewa na wanawake ili kuingizwa kwenye mchakato. "...Tunatambua pia mchango wa vyombo vya habari katika kujenga ufahamu kuhusu mchakato wa katiba na hasa kuhusu kwanini katiba mpya izingatie usawa wa kijinsia." alisema Msoka. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0


   
  huyu ndiye mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa  Frank Kibiki aliyetangaza nia. 

   Na fredy mgunda,iringa.
   
  MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa,  Frank Kibiki,  ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Iringa mjini, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
   
  Akizungumza na waandishi wa Habari leo  ofisini kwake, Kibiki amesema ni wakati wa vijana kushika hatamu kwa kuwania nafasi mbali mbali, ndani ya CCM na hatimaye kwenye umma wa watanzania.
   
  Kibiki ambaye ni Katibu mwandamizi wa Umoja wa Vijana, katika wilaya mbali mbali nchini amesema ameamua kuomba kupitishwa nafasi hiyo na CCM ili aweze kusaidiana na wananchi wa manipaa ya Iringa katika kuwaletea maendeleo.
   
  Mjumbe huyo wa Mkutano mkuu wa ccm Taifa, amedai kuwa zipo changamoto nyingi zinazowakabili vijana na wananchi kwa ujumla na kwamba, njia pekee ya kuzitatua ni kuwa na uwakilishi toka miongoni mwao kwenye vyombo vya maamuzi.
   
  Kitaaluma, Kibiki ni mwandishi wa habari mwandamizi kupitia magazeti ya Uhuru na Mzalendo, mkoani Iringa.

  0 0

   ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Fredrick Mwakalebela Desemba 26 anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Krismasi mkoani Iringa.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Mwakalebela anatarajia pia kuwaongoza waumini mbalimbali mkoani humo kwa lengo la kumtukuza Mungu kupitia waimbaji mbalimbali hapa nchini.

  Msama alisema Mwakalebela atafanikisha lengo la kusaidia wenye uhitaji maalum kama Yatima, Wajane na walemavu ambao wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali.

  Msama alisema Mwakalebela ni mdau ambaye anatakiwa aendane na kauli mbiu ya Tanzania ni yetu, Tuilinde na Kuipenda ambayo inachochea wadau ambao wanatakiwa kusaidia wadau hao.

  Tamasha hilo linatarajia kuanza Desemba 25, kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kabla ya kuhamia Iringa  na kumalizia Desemba 28 Wilayani Songea kwenye uwanja wa Majimaji.

  0 0

  Mwimbaji wa muziki wa injili Tumaini Njole akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kampuni ya Msama Promotion ambayo inaandaa Tamasha la Pasaka litakalofanyika sikukuu ya Krismas tarehe 25/12/2014 mkoani Mbeya wakati alipozungumzia maadalizi ya tamasha hilo na jinsi alivyojipanga kukonga mioyo ya mashabiki wa nyimbo za injili mkoani Mbeya , Tamasha hilo linatarajiwa kuanza muda wa Saa nane mchana viingilio vikiwa ni shilingi 5000 kwa watu wazima na watoto shilingi 2000, Katika tamasha hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye na waimbaji wengine watakaotumbuiza ni Faraja Ntaboba, Upendo Nkone, Upendo Kirahilo, Rose Muhando, Bony Mwaiteje Edson Mwasabwite, Ambwene Mwasongwe na wengine wengi, Pia matamasha mengine yanatarajiwa kufanyika mkoani Iringa tarehe 26/12/2014 na Songea tarehe 28/12/2014, Katika Picha kushoto ni Mwimbaji Joshua Mlelwa. 2Mwimbaji wa muziki wa Injili Edson Mwasabwite akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam , Kushoto ni mwimbaji Joshua Mlelwa na katikati ni Mwimbaji Tumaini Njole3Mwimbaji Joshua Mlelwa akielezea maandalizi yake wakati wa Tamasha la Pasaka litakalofanyika mkoani Mbeya wakati wa Sikukuu ya Krismas kulia ni Mwimbaji Tumaini Njole.

  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu wa Mstaafu Mhe  Edward Lowassa walipohudhuria sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha leo
   
  Picha ya pamoja
   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe.  Edward Lowassa akiongea na  maofisa waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwemo na Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange (kushoto) kwenye sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha leo
   Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa alipowasili kwenye sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli
   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa (kulia) akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi walipohudhuria sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli
   Maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu wakila kiapo cha utii mbele ya Rais Jakaya Kikwete baada ya kutunukiwa kamisheni katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha
    Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa kwenye sherehe hizo.
   Burudani katika sherehe hizo
   Maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu wakitembea kwa ukakamavu walipokuwa wakitoa heshima kwa Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa hao, Monduli, mkoani Arusha
    Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiongea na Waziri  Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda
  Wimbo wa Taifa ulipopigwa

  0 0

  3Kiwanja kipya cha maraha Uefa Goo Night Club kinatarajiwa kuzinduliwa mkesha wa sikukuu ya Krismas jijini Dar es salaam Kiwanja hiki ni cha Kisasa kiko maeneo ya Ukonga Mombasa Barabara ya kuelekea Moshi Baa Karibu na njia panda ya Mahitamita 200 kutoka barabara kuu iendayo Pugu, siku ya mkesha wa Krismas burudani kibao zimeandaliwa na na kiko katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha kila kitu ili kuwapa burudani wateja wake ikiwa ni pamoja na Ligi mbalimbali za ulaya, muziki wa kisasa kama vile Bongofleva na muziki wa zamani na vyakula mbalimbali vitapatikana. 

  12 
  Hizi ni baadhi ya picha zinazoonyesha jengo kwa nje na maendeleo ya kukamilisha ujenzi kwa ndani kwenye klabu hiyo ambao umefikia asilimia 99 kabla ya kufunguliwa mkesha wa Krismas.7654

  0 0

    HOJA ZA MSINGI ZA PROFESA ANNA KAJUMULO TIBAIJUKA KWA NINI HAONI MANTIKI YA KUJIUZULU WALA KUWAJIBISHWA- UJUMBE MFUPI
  1. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), inayoongozwa na Zitto Kabwe hakuniita ili kupata nafasi ya kujitetea, kutokana na shutuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwangu, kwamba nilipewa fedha kupitia akaunti ya Escrow.

  2. Kujiuzulu sio fasheni, kwa kuwa fedha nilizopata ni kwa ajili ya mchango wa shule ya Barbro Johansson ya jijini Dar es Salaam na kujiuzulu ni kitu ambacho kina sababu zinazohitaji uwajibikaji. Nijiuzulu kwa kuwa nimepata mchango wa shule?

  3. “Nijiuzulu kwa sababu gani?… kwa kupata mchango wa shule!… kujiuzulu ni kitu chenye sababu zake, kujiuzulu sio fasheni, lazima kuwe na sababu, hata Rais aliyenipa kazi atashangaa. Naona ufahari kufanikisha mchango wa shule yangu.

  4. Aidha, serikali haijatamka kama James Rugemalira ana fedha haramu na kama fedha hizo, zikitajwa kuwa za haramu, shule yangu itazirudisha, kwa kuwa shule yangu haiwezi kupokea fedha iliyo haramu.

  5. “Nilipostaafu kazi UN, Sweden waliniambia kuwa sasa naweza kuendelea kuomba mchango katika nchi yangu na ni kweli kwamba kadri taifa linavyokua wapo watu wenye uwezo na wanaoweza kuchangia katika masuala mbalimbali,” alisema na kuongeza kuwa ndio maana alianza kuomba michango kwa watu mbalimbali wakiwamo wa ndani ya nchi. 

  Na kutokana na kuomba mchango, hata Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi aliwahi kutuchangia Sh milioni 278 kwa kuona umuhimu wa kuendeleza elimu ya mtoto wa kike na mwaka 2012, ndipo nilipomuomba mchango James Rugemalira kupitia kampuni yake ya Mabibo akiwa kama ndugu yake.

  6. Nilipomwandikia Rugemalira, alinjibu nitachangiwa, lakini kwa masharti ya kwamba fedha hizo zipitie Benki ya Mkombozi. Na mimi sikuwa na akaunti katika benki hiyo na Februari 23 mwaka huu ndipo nilifungua na haukupita muda mwingi alinipigia na kuniambia kuwa tayari ameshachangia.

   Baada ya kupata mchango huo, niliwapigia viongozi wa Bodi ya shule kuwaeleza kwamba wamepata mchango `babu kubwa’ na alihamisha fedha hizo na kuzipeleka Benki M kwa ajili ya kulipa mikopo ya shule.

  7. Profesa Tibaijuka anasema: “Nimejitolea maisha yangu kutafuta wafadhili kwani ada za shule hizo ni kubwa kwani ya Dar es Salaam ni Sh milioni nne na nusu na ile ya Bukoba ni Sh milioni mbili huku pakiwepo pia wanafunzi ambao hawalipi ada wakipatiwa ufadhili.”

  0 0

  Afisa Uhusiano mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (Kushoto), akipena mikono na Ummy Shaaban,  mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Buyuni II,  iliyoko Chanika, wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam,wakati akikabidhi msada wa madawati kwa ajili ya shule hiyo mwishoni mwa wiki. (Katikati ni mwalimu mkuu wa shule hiyo,  Rogather Palla. 
   Afisa Uhusiano mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akiwaelimisha wanafunzi hawa wa shule hiyo, kuhusu huduma mbalimbali  zitolwewazo na Mfuko huo  Wanafunzi wakishangili msada huo wa madawati
   Baadhi ya Wanafunzi wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa madawati hayo

  Afisa Uhusiano mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Njaidi, (Kushoto), akitoa elimu kupitia vipeperushi kwa baadhi ya walimu wa shule hiyo.
   Wanafunzi wakibeba dawati kupeleka darasani.
   Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameketi kwenye madawati hayo.


older | 1 | .... | 429 | 430 | (Page 431) | 432 | 433 | .... | 1897 | newer