Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

sherehe za SHIWATA zaihirishwa.

$
0
0
 SHEREHE za miaka kumi ya kuanzishwa kwa Mtandao wa WAsanii Tanzania (SHIWATA)zilizokuwa zifanyike Desemba 25, jijini Dar es Salaam zimeahirishwa.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana kuwa kuahirishwa kwa sherehe hizo kumetokana na wanachama wengi ambao walitakiwa kukabidhiwa nyumba zao kuwa katika sherehe za Krismas nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema kuahirishwa huko kumesababisha pambano la watani wa jadi la Simba na Yanga Veterani lililokuwa lichezwe Desemba 25 kwenye uwanja wa Azam, Charambe mpaka litakapotangazwa tena.

Mwenyekiti Taalib alisema sababu nyingine ya kuahirishwa kwa sherehe hizo ni kutokana na maombi ya mgeni rasmi ambaye hakumtaja kuwa yuko nje ya nchi kikazi ambaye aliomba ahudhurie tamasha hilo la kihistoria.

Nyumba ambazo zitakabidhiwa ni 38 ambazo zimejengwa na kukamilika ambako wanachama hao walichangia ujenzi kwa kutoa fedha kidogo kidogo kupitia benki na kuchangua aina ya nyumba anayoitaka kutokana na kiasi alizochangia.
Ili kuwapatia makazi ya bei nadfuu wanachama wake SHIWATA inajenga nyumba za sh. 631,000, sh. 1,500,000, sh. 3,800,000 na sh. 6,400,000 ambazo mwanachama anagaiwa kila mwezi Juni na Desemba kila mwaka..

Alisema katika makabidhiano hayo wamiliki wa nyumba hizo pia watakabidhiwa vyeti maalum vya kumaliki nyumba zao katika sherehe kubwa itakayofanyika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga. Mpaka sasa SHIWATA ina wanachama 8,000.

Waziri Mkuu awasili Qatar kwa ziara ya kikazi

$
0
0
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewasili jijini Doha, Qatar jana usiku (Jumamosi, Desemba 20, 2014) kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo inayotarajiwa kuanza leo.

Lengo la ziara ya Waziri Mkuu ni kukuza mahusiano baina ya nchi hizi mbili, kuangalia fursa za kiuchumi na miradi mikubwa inayoweza kuzinufaisha nchi hizo na nje ya mipaka yake kwenye Ghuba ya Arabuni (Arabian Gulf) na bara la Afrika.

Vile vile Waziri Mkuu anatarajiwa kutangaza fursa za uwekezaji nchini Tanzania, fursa za biashara, za utalii na kutafuta mitaji kwa ajili ya sekta za uchimbaji gesi na mafuta, usindikaji mazao, uvuvi na mifugo, ajira na uendelezaji miundombinu.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri Mkuu atakuwa na mazungumzo ya kiserikali na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Sheikh Abdulla Nasser Al Thani. Vilevile atakutana na Mawaziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii; Uchukuzi; Miundombinu na Uwekezaji wa nchi hii. Naibu Mawaziri atakaokutana nao ni wa Uchumi na wa Nishati.

Vilevile Waziri Mkuu amepangiwa kukutana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Qatar (Qatar Business Community), wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Qatar (Chamber of Commerce of the State of Qatar) na pia atakutana na Watanzania waishio Qatar. Atatembelea pia Mamlaka ya Bandari ya Qatar na makao makuu ya kampuni ya uchimbaji gesi ya Qatar.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kimani; Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Maalim; Naibu Waziri wa Nishati, Bw. Charles Kitwanga; Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, wabunge wawili Bi. Amina Makilagi na Bw. Aeshy Hilali na wakuu wa taasisi za TPSF na TPDC.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAPILI, DESEMBA 21, 2014

Watanzania kunufaika na ajira Qatar - Pinda

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Watanzania watanufaika na kipato na maarifa ya teknolojia ya kisasa kutokana na ajira ambazo watapata katika nchi ya Qatar baada ya mkataba kusainiwa hivi karibuni.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Desemba 20, 2014) jijini Doha, Qatar wakati akizumgumza na waandishi wa habari ili kuwapa taarifa fupi juu ya mambo yaliyojiri kwenye mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Abdulla Nasser Al Thani.

Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika ofisini kwa Sheikh Abdulla, Waziri Mkuu Pinda amesema wamekubaliana kutoa ajira kwa Watanzania kwa sababu nchi hii inahitaji wafanyakazi wengi kwenye sekta mbalimbali na raia wake ni wachache.

 “Hivi sasa wapo Watanzania wanaofanya kazi hapa lakini ni wachache mno. Mazungumzo yalishaanza siku za nyuma. Tukisaini mkataba katika muda mfupi ujao, tutajua ni idadi gani wanahitajika na wanaweza kuja kila baada ya muda gani,” alifafanua Waziri Mkuu.

“Hapa Qatar kuna uwekezaji mkubwa umefanyika, kwa hiyo wanahitaji watu wa kufanya kazi... kwenye mahoteli, viwandani, na kikubwa hapa ninachokiona watu wetu watapata kipato lakini pia watapata ujuzi kwa maana ya maarifa yanayoendana teknolojia ya kisasa,” aliongeza.

Akeleza mambo mengine ambayo wamekubalina kushirkiana kama nchi rafiki, Waziri Mkuu alisema kuna mambo makuu manne likiwemo hilo la ajira. “La kwanza ni Kilimo.  Hapa Qatar ni jangwa kila mahali. Wamekubali kuja kuwekeza kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi kwa sababu sisi tuko karibu nao zaidi kuliko Marekani au Brazil.”

“Wanaweza kupata mchele, matunda, nyama kwa maana ya machinjio na viwanda vya kusindika nyama lakini pia katika uvuvi wa samaki. Tunayo bahari ila mitaji yetu ni midogo. Kwa hiyo wamekubali kuangalia eneo hilo pia,” alisema.

Alisema eneo la pili ni la gesi na mafuta. “Wamekubali kutusaidia utaalmu ili tushirikiane nao katika namna kutumia gesi kwenye ngazi ya chini hasa viwanda kwa sababu wenzetu wana uzoefu wa muda mrefu. Hata kwenye mafuta wameonyesha kuwa wako tayari,” alisema.
Eneoa la tatu alilitaja kuwa ni kutoa fursa ya ajira kwa Watanzania na la nne ni TEHAMA. “Hawa wenzetu wamechanganya TEHAMA na sayansi na sasa wana Jiji la Sayansi na Teknolojia. Chini ya makubaliano tutakayofikia, watu wetu watakuja kujifunza masuala ya gesi na mafuta.”

Alisema wamekubaliana na Sheikh Abdulla al Thani kuunda timu ya pamoja baina ya nchi zao ili ifanye kazi ya kuainisha ni maeneo gani wanataka waanze nayo kwanza kulingana na mahitaji. “Nimemuahidi nikifika nyumbani nitaandika barua ili mchakato wa kuunda timu uanze rasmi,” alisema.

Mchana huu, Waziri Mkuu Pinda atakuwa na mazungumzo ya Kiserikali na Mawaziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii; Uchukuzi; Miundombinu na Uwekezaji wa Qatar. Naibu Mawaziri atakaokutana nao ni wa Uchumi na wa Nishati.

Jioni Waziri Mkuu amepangiwa kukutana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Qatar (Qatar Business Community), wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Qatar (Chamber of Commerce of the State of Qatar) na pia atakutana na Watanzania waishio Qatar. Kesho (jumatatu, Desemba 22, 2014) atatembelea Mamlaka ya Bandari ya Qatar na makao makuu ya kampuni ya uchimbaji gesi ya Qatar.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kimani; Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Maalim; Naibu Waziri wa Nishati, Bw. Charles Kitwanga; Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, wabunge wawili Bi. Amina Makilagi na Bw. Aeshy Hilali, Dk. Gideon Kaunda wa TPSF na Bw. Shigela Malocha kutoka TPDC.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAPILI, DESEMBA 21, 2014

UJENZI WA MABWENI SHULE ZA PEMBEZONI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA WANAFUNZI MIJINI.

$
0
0
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

Jamii imetakiwa kuendelea  kuunga mkono juhudi za Serikali za ujenzi wa mabweni katika shule  za Sekondari  zilizoko pembezoni mwa miji hasa maeneo ya vijijini ili kukabiliana na tatizo la msongamano wa wanafunzi mijini linalosababishwa na baadhi ya wanafunzi kushindwa kujaza nafasi wanazopangiwa   maeneo ya pembezoni mwa miji kutokana na umbali.

Kauli hiyo ilitolewa juzi jijini Dar es salaam na Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando wakati akizungumza na viongozi wa Elimu wa mkoa na walimu wakuu wa Shule za Sekondari za mkoa wa Dar es salaam wakati wa kikao cha Kamati ya Uchaguzi wa wanafunzi wa watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015.

Alisema  mwaka huu  mkoa wa Dar es salaam umekuwa na kiwango cha juu cha ufaulu  kitaifa kwa kuwa na wanafunzi wanaokidhi vigezo vya kuendelea na masomo ya sekondari kwa kiwango cha asilimia 78 ukifuatiwa na mkoa wa Kilimanjaro ambao umepata asilimia 69.

Alifafanua kuwa kati ya wanafunzi 60,709 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka huu , wanafunzi 59,577 ambao ni sawa na asilimia 98.14  waliofanya mtihani huo, wavulana wakiwa 28,419 na wasichana 31,158.

Bi. Mmbando alibainisha kuwa  kati ya hao watahiniwa 1,132  sawa na asilimia 1.86 katika mkoa wa Dar es salaam hawawakuweza kufanya mtihani huo kutokana sababu mbalimbali zikiwemo utoro, vifo, ugonjwa na sababu nyinginezo.

Akizungumzia  kuhusu ufaulu wa wanafunzi hao kimkoa alisema wanafunzi 46,434 sawa na asilimia 78 walifaulu mtihani huo na kuufanya mkoa wa Dar es salaam kuongoza kwa kuwa na ufaulu wa juu kitaifa wavulana 22,389 na wasichana 24,086.

Alibainisha kuwa wanafunzi 36,610 walichaguliwa katika chaguo la kwanza kujiunga na shule mbalimbali za Sekondari za ndani na nje ya mkoa wa Dar es salaam na kufafanua kuwa wanafunzi 9824 waliobaki sawa na asilimia 21 ambao nao wamefaulu watachaguliwa katika chaguo la pili kufuatia baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa katika chaguo la kwanza kujiunga na shule zisizokuwa za serikali na nafasi zao kubaki wazi.

Katika kufanikisha zoezi hilo Bi. Mmbando alieleza kuwa mkoa tayari umeunda timu tatu zitakazofuatilia idadi ya wanafunzi watakaoshindwa kufika katika shule walizopangiwa  kuanzia Januari 14, 2015 katika halimashauri za Temeke, Ilala na Kinondoni ili nafasi zao zijazwe na wanafunzi wengine.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Raymond Mapunda akitoa tathmini ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika nchi nzima mwezi Septemba mwaka huu alisema mkoa wake ulifanya vizuri kutokana na juhudi za walimu pamoja na wanafunzi kuuelewa vizuri mfumo wa ufanyaji mitihani uliotumika wa Optical Mark Reader (OMR).

Alisema kuwa wanafunzi wa shule 506 za jiji la Dar es salaam walifanya mtihani walitumia mfumo huo kwa ufanisi mwanafunzi 1 alifutiwa matokeo yake kwa sababu za udanganyifu, 2 walipata alama 0  huku  wavulana 10 na wasichana 10 kutoka wilaya ya Ilala na Kinondoni waliibuka washindi wa nafasi 10 bora kitaifa.

KITUO CHA RADIO 5 WAFANYA KAMPENI YA USHINDI KWA WATOTO YATIMA

$
0
0
SAM_0388Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 Arusha wakikabidhi misaada mbalimbali katika kampeni ya "USHINDI"inayoendeshwa na kituo hicho,misaada hiyo ilitolewa na wahisani mbalimbali kwaajili ya watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima Mkoani Arusha,katika Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo kushoto ni Sarah Keiya wakiwakabidhi watoto wa kituo cha kiwohede ndoo ya mafuta ya kupikia kwaajili ya sikukuya Krismass na mwaka mpya jijini hapa jana katika hotel ya world Garden
SAM_0393Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha kiwohede na huruma katika hotel ya world Garden iliyopo moshono jijini Arusha katika tam
SAM_0390Mkuu wa vipindi wa kituo hicho Mathew Philip akikabidhi moja ya msaada kwa shcha watoto huruma.

Kampuni Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  imeeanda tamasha kwa watoto yatima wanaoishi katika vituo lenye jina "Kampeni ya USHINDI"linalowashirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Arusha

Mkurugenzi wa kituo hicho  Robert Francis anachukua jukumu la kuwasihi jamii kwa ujumla kuwa na tabia ya kuwakumbuka mayatima hasa kipindi hichi cha sikukuu ili nao wasijione kutengwa

Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo alisema kuwa kila mtoto anastahili kuwa na furaha na baadhi yao ni wale wenye uwezo mdogo ni vyema kuwakumbuka na tusiwatenge na tukifanya hivi watajiskia vizuri

Meneja masoko wa Redio 5 Sarah Keiya ametoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana na kituo hicho kwa kuwezesha kampeni hiyo kufanikiwa,wadau wakubwa walioshiriki ni Redio 5,Pepsi,Fifis bakery,Arusha meat,Skytel,Monaban,Vibration duo,Brundful company,World garden.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_0363Watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima wakishindana kucheza muziki
SAM_0376Grace Joseph(12)wa kituo cha kiwohed akionyesha ujuzi wake wa kucheza katika shindano
SAM_0400Mtoto anayeishi katika mazingira magumu akiwa jukwaani akiimba wimbo wa "NISEME"wimbo wa moto band
SAM_0358Mashindano yakiwa yanaendelea
SAM_0361Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa mzigoni
SAM_0385Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba moja katika shindano la kucheza muziki
SAM_0384Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba mbili baada ya kushinda katika shindano la kucheza muziki
SAM_0364
SAM_0346Wafanyakazi wa redio5 wakiwa wanaanda sausage kwaajili ya watoto yatima
SAM_0352Muonekano wa watoto wakiwa katika eneo la kuchezea michezo mbalimbali
SAM_0350Meneja  ubunifu wa Redio 5 Bi.Vicky Mwakoyo akiwa Meneja masoko wa Redio 5Bi.Sarah Keiya
SAM_0366Mtangazaji wa kituo hicho Akiba Kilango ambaye alikuwa MC wa shughuli hiyo akiwa anaongea na watoto jukwaani kabla ya mashindano ya kucheza kuanza
SAM_0405Wafanyakazi wa kituo hicho wakiwa katika maandalizi ya kuwaandalia watoto mapochopocho
SAM_0398Kampeni ya ushindi ikiwa inaendelea huku watoto wakiwa wanancheza michezo mbalimbali
SAM_0386
Wadau wakiwa wanafatilia shindano

SAM_0408Kulia ni mtoto Sharon Nelson akiwa anakabidhi msaada alioleta katika kampeni ya ushindi amewataka watoto wengine kujitolea kusaidia wasionacho
SAM_0371
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anafatilia tamasha hilo
 

HERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA KUTOKA FLAVIANA MATATA FOUNDATION

UNESCO YAFADHILI MAENDELEO YA SAYANSI AFRIKA

$
0
0
IMG_7359
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi Wetu, Arusha
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limesema linafanyakazi na nchi 20 za Afrika kutengeneza mifumo ya kitaifa ya sayansi, teknolojia kusaidia mataifa hayo kufikia malengo yao ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Getachew Engida wakati alipopata nafasi ya kutoa kauli ya shirika lake kwenye mahafali ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia iliyopo Tengeru mjini Arusha. Alisema shirika lake limejikita zaidi kuhakikisha kwamba inatoa elimu itakayowezesha mabadiliko ya sayansi na hivyo kuwezesha wanaume kwa wake kufanyakazi kama wajasirimali.

“Elimu hiyo ni pamoja na mafunzo ya ukusanyaji takwimu, uimarishaji wa viashiria na ubunifu wa vifaa vya ufuatiliaji na kuimarisha utenegenezaji wa sera kwa kuangalia matukio yaliyothibitishwa,” alisema Naibu Mkurugenzi huyo.
IMG_7369
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Taasisi hiyo kushiriki mahafali hayo.
Akizungumza mbele ya wahitimu wa Taasisi hiyo na Rais Jakaya Kikwete alisema kwamba sayansi na teknolojia vina nafasi ya pekee katika jamii na hivyo shirika kama UNESCO inachofanya ni kusaidia kuwapo kwa elimu hiyo.Alisema sayansi na teknolojia ni msingi wa maendeleo kwani kupitia kuboreka kwa vitu hivyo viwili serikali nyingi zitaweza kukabiliana na umaskini uliokithiri na kupeleka watu wake katika maendeleo na ustawi.

Kiongozi huyo wa Unesco pia alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuwezesha kuwepo kwa Taasisi hiyo ambayo ilibuniwa katika mkutano wa aliyekuwa Rais wa Benki ya Dunia, James Wolfensohn, na Rais Nelson Mandela wa Afrika Kusini mwaka 2001.Ubunifu huo ulifanyiwa kazi na viongozi wa nchi za Afrika Januari 2005 katika mkutano wao wa Abuja ambapo walikubaliana kuanzisha vyuo vinne vya sayansi na teknolojia kwa jina la Nelson Mandela.
IMG_7570
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida wakipitia ratiba ya mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru, mjini Arusha.

Alisema sayansi inashikilia majibu ya maswali ya maendeleo ya Bara la Afrika katika kukabili umaskini na kuwa na maendeleo endelevu katika sekta zote na jamii. Naye Rais Kikwete akihutubia mkusanyiko huo aliwapongeza viongozi wa Taasisi hiyo kwa kuendeleza umaalumu wake.

“Taasisi hii ni sehemu ya mtandao wa vyuo vya Nelson Mandela vya Sayansi na Teknolojia katika Bara la Afrika. Chuo hiki cha Arusha ni mahsusi kwa ajili ya kanda ya Afrika Mashariki. Ndiyo maana Hati Idhini (University Charter) niliyokipa Chuo hiki inaeleza bayana kuwa Chuo hiki kinapaswa kuwa chenye hadhi maalum (special status). Hadhi hii yapaswa pia ionekane katika ubora wa elimu inayotolewa hapa. “ alisema Rais Kikwete.
Alisema ubora wake ni matokeo ya ubora wa wahadhiri wake, programu zake na miundombinu yake.
IMG_7509
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida akitoa kauli ya shirika lake kwenye mahafali ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia iliyopo Tengeru mjini Arusha. Kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohamed Gharib Bilal na baadhi ya viongozi wa juu wa chuo hicho.

IMG_7496
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues wakifurahi jambo wakati Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (hayupo pichani) alipokuwa akisoma hotuba yake kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia mwishoni mwa wiki Tengeru jijini Arusha.
IMG_7542
Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Madela, Sayansi na Teknolojia wakitoa burudani kwenye mahafali ya pili ya taasisi hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru jijini Arusha.
IMG_7527
IMG_7483
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues wakishuhudia burudani iliyokuwa ikitolewa na wafanyakazi wa taasisi hiyo.
IMG_7487
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) akiteta jambo na Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru, jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.
IMG_7492
Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika tete-a-tete na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (kaitkati). Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.
IMG_7619
Pichani juu na chini ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Gharib Bilal akiwatunuku wahitimu mbalimbali wa shahada za juu za uzamili na uzamivu katika sayansi, teknolojia na tafiti za kisayansi wakati wa mahafali ya pili ya taasisi hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa juma, Tengeru jijini Arusha.
IMG_7626
IMG_7353
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria mahafali hayo.
DSC_0641
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya maprofesa wa taasisi hiyo.
DSC_0653
Pichani juu na chini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu.
DSC_0668
DSC_0703
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya mahafali hayo.

WATANZANIA WASHAURIWA KUITUMIA NEEMA YA GESI KUPELEKA HIFADHI YA JAMII KWA KILA MTU

$
0
0
DSC_0013
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,na Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Mh. Aggrey Mwanri, akiendesha shughuli za mkutano huo uliomalizika hivi karibuni katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC).(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu, Arusha
MTAALAMU mmoja wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, ameishauri serikali kutumia neema ya gesi kutoa hifadhi ya kutosha kwa wananchi wake.

Dhliwayo alisema hayo wakati akijibu hoja ya Naibu waziri Afya na Ustawi wa jamii, Dk Kebwe S. Kebwe namna ya kufikia lengo la hifadhi ya jamii kwa wote kwa kasi kuliko ilivyo sasa ambapo inafikiriwa ifikapo mwaka 2025 ndio tutakuwa tumefikia asilimia 75 ya hifadhi ya jamii.

Dk. Kebwe alisema hayo wakati wa kujadili mada ya uchokozi iliyotolewa na Dhliwayo mtaalamu wa uchumi ambaye alishawahi kufanyakazi nchini Zimbabwe na Msumbiji.
Alisema kwamba mataifa mengi yametumia raslimali zao kufanya mambo makubwa kwa wananchi wao na Tanzania inaweza kufanya hivyo.
DSC_0005
Ofisa anayeshughulikia sera za hifadhi, UNICEF Tanzania, Bi. Usha Mishra akitoa mrejesho walichojifunza washiriki siku ya kwanza na kutoa mwongozo wa mambo mapya wanayotakiwa kujifunza katika mkutano uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.

Alisema ipo nchi ambayo ilitumia utajiri wake wa almasi kutengeneza miundombinu ya barabara na si vibaya kwa Tanzania kutumia utajiri wake wa gesi kuhakikisha kila mtanzania anapata hifadhi ya jamii. Alisema kama taifa linaweza kuamua asilimia Fulani kutoka katika sekta ya gesi kuingia katika kuwezesha hifadhi ya jamii ambayo itahakikisha uwapo wa huduma sawa kwa wote.

Alisema uchumi wa Tanzania kutoka mwaka 2000 hadi sasa umekuwa ukikua kwa kasi ingawa kasi hiyo haionekani kwa wananchi ambapo wengi wamejikuta wakiwa katika umaskini wa kukithiri. Alisema kutokana na tatizo hilo la umaskini wa kukithiri kutoondoka kwa hali hiyo kunasababisha na sekta husika kutotoa ajira za kutosha ambazo zingewezesha watu kuneemeka na uchumi unaokua kwa kasi.
DSC_0079
Mtaalamu wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo akitoa mada chokonozi wakati wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ambao umemalizika hivi karibuni jijini Arusha.


Alisema aidha kaya nyingi zimekuwa na idadi kubwa ya watu ikiakisi umaskini unaoambatana na kaya zenye watu wengi na uzazi wa mapema unaowakuta wasichana.
Alisema pamoja na mpango mzuri wa serikali kupitia TASAF kupunguza umaskini wa kukithiri ukishirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ipo haja kwa serikali kuhakikisha kwamba kunakuwa na uratibu unawezesha mipango ya kupunguza umaskini inafanikiwa.

Alisema iwapo TASAF inashughulikia elimu na afya ni dhahiri itahitaji kuwapo kwa shule na walimu na katika afya hospitali na wauguzi na madaktari na dawa.” Ni lazima kuwepo na uratibu ili kufanikisha yote yaliyolengwa” alisema Dhliwayo. Alisema Tanzania inaweza kujifunza kutoka mataifa ya Rwanda na Eritrea ambayo yamefanikiwa hifadhi ya jamii eneo la afya kufikia zaidi ya asilimia 90 huku wakitumia mifumo thabiti ya afya ya jamii kwa kaya.
DSC_0093
Kuki Tarimo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akitoa mada chonokonozi wakati wa mkutano huo.

Aidha amesema kwamba mataifa hayo yamefanikiwa katika malengo ya millennia na kupunguza idadi ya vifo vya wanawake katika uzazi. Katika mkutano huo ambao uliitishwa na serikali ili kupata misingi ya utengenezaji wa sera na sheria ili kuwezesha watanzania wote kuwa na haki katika kei ya taifa kw akuwezeshwa kuondokana na umaskini wa kukithiri ulihudhuriwa na watalaamu 150 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Pia ulifunguliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi ambaye alisema Tanzania kwa sasa inapojianda kuwa na uchumi wa kipato cha kati ipo haja ya kuimarisha sekta za hifadhi ya jamii.
DSC_0101
Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster akichangia hoja wakati wa mkutano huo uliomalizika hivi karibuni.
DSC_0109
Meneja Mwendeshaji wa Shirika la Under The Same Sun, Gamariel Mboya akiuliza swali kuhusiana na serikali imejipangaje katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wa ngozi wanapataje mafuta ya kuzuia mionzi ya jua inayopelekea ugonjwa kansa ya ngozi.
DSC_0135
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe, akijibu swali kuhusiana na serikali imefanya nini kwa walemavu wa ngozi katika kuhakikisha mafuta kuzuia mionzi ya jua kwa watu hao yanapatikana kiurahisi ili kupunguza athari za kansa kwa walemavu hao. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.
DSC_0159
Mwakilishi wa wazee waliostaafu akiuliza swali kwa Wizara ya afya na ustawi wa jamii kuhusiana na uboreshwaji wa huduma za afya kwa wazee ambapo imekuwa changamoto kubwa kwao.
DSC_0025
Ujumbe wa Makatibu wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ukishiriki wa mkutano huo.
DSC_0115
Mtaalamu wa mawasiliano wa Shirika la UNICEF Tanzania, Jacqueline Namfua akifurahi jambo wakati wa mkutano huo.
DSC_0029
Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.
DSC_0107DSC_0128DSC_0067
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akifuatilia kwa umakini maoni mbalimbali yaliyokuwa yakiwasishwa kwenye mkutano.

TWIGA CEMENT YAZINDUA CHAMA CHA MAKIPA TANZANIA. TASWA FC WAFUNGUA NJIA.

$
0
0
ippKampuni ya Twiga Cement ya jijini Dar es Salaam, jana imefanikiwa kuzindua rasmi Chama cha Wachezaji wa Nafasi ya Golikipa wanaoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania, ambapo katika uzinduzi huo timu hiyo ya Makipa ilicheza mchezo wa Kirafiki dhidi ya Timu ya Kombaini ya Waandishi wa Habari TASWA F.C.uliofanyika kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam jana.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na Ushindani wa Kipekee kutokana na Timu zote kuwa na Wachezaji Nyota na Tegemeo katika Vipaji vyao, Mashabiki waliofika kushuhudia mchezo huo walifurahishwa na jinsi kila mchezaji alivyoonyesha Ujuzi binafsi na kiwango cha hali ya juu.Timu ya makipa ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufanya shambulizi kwenye lango la timu ya TASWA ambapo dakika ya 26 mchezaji Shaaban Kado alikosa Penalt kutokana na beki wa Taswa Martin Peter kunawa akiwa eneo la kumi na nane na penalt hiyo ilidakwa na kipa nyota wa TASWA Ahmed Famau.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika kikosi cha timu ya Makipa kilikuwa mbele kwa bao 1-0,lililofungwa na Juma Kaseja baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa TASWA, ambapo kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko ambapo Taswa iliwatoa, Majuto Omary, Ibrahim Masoud, Ally Mkongwe, Zahoro Mlanzi, Shafii Dauda, na nafasi zao kuchukuliwa na Salum Jaba, Juma Ramadhani, Hatibu Naheka,na Paul Limoy,mabadiliko ambayo hata hivyo yalishindwa kupunguza kasi ya wachezaji hao Makipa wa Ligi kuu waliokuwa muda wote wakilisakama lango la TASWA FC.

Pamoja na kuwa na wachezaji wa akiba timu ya Makipa lakini walishindwa kufanya mabadiliko, kutokana na wachezaji wengi kuwa na pumzi ya kuwamudu TASWA ambapo Makipa hao walisaidiwa na mlinda mlango kutoka timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars, Fatuma Omary ambaye hata hivyo alionyesha kiwango kikubwa baada ya kudaka michomo ya wazi kutoka kwa washambuliaji wa Taswa,Ibrahim Masoud, Shafii Dauda,Majuto Omary pamoja na Ally Mkongwe waliokuwa wakilisakama Lango la timu ya makipa kila wakati.

goli la pili lilipatikana kunako dakika ya 67 kupitia kwa Ivo Mapunda aliyefunga kwa shuti kali lililomshinda mlinda wa TASWA Ahmed Famau,kabla ya shaaban Kado kuhitimisha Kapu la Magoli kwa timu hiyo ya Makipa. 
 
Pamoja na Kufungwa kwa Taabu 3-0 timu ya TASWA FC, iliweza kuwachezesha mputa mputa wachezaji hao nyota wa Ligi kuu pamoja na kwamba wachezaji hao muda mwingi wanakuwa kwenye Mazoezi Makali na Timu zao za ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara,kitendo ambacho kiliwafanya kuonekana wakiwa na Uhai wa kukimbiza huku na kule katika kipindi cha dakika zote za mchezo.
Taswa ambayo kwa asilimia kubwa iliwachezesha wachezaji wake wengi ambao ni wafanyakazi wa vyombo mbali mbali vya habari, ilisifiwa na mashabiki waliohudhulia mchezo huo kwa kuwa Muda mwingi wanakuwa katika shuguli za kiofisi ambapo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Timu hiyo wachezaji ukutana mara moja kwa wiki kwa ajili ya mazoezi ya Pamoja.
“timu yetu ni nzuri sana hii TASWA, mwenyewe umeona wachezaji walivyowapeleka mpuata hawa Makipa pamoja na kwamba hii timu ya Makipa ni Wachezaji wa ligi kuu, nasema ligi kuu kwa kuwa wanashiriki hiyo ligi isipokuwa tofauti wao ni makipa, na tunapozungumzia suala la Wachezaji, mwenyewe unajua timu ili iwe bora ni lazima kwanza iwe na Makipa wazuri ndipo iwe bora, na kipa bora ni yule anayeweza kuwapanga wachezaji wake, hivyo kama hawa wachezaji ndiyo wapangaji wa timu zao wakati wa Mashindano, mimi nasema tumecheza na Timu ya Taifa na si kama unavyofikili wewe, na ndiyo maana nathubutu kusema kuwa kufungwa kwetu mabao 3-0 ni sawa na kupata ushindi sisi, maana hata hivyo wametuleta kwenye Uwanja wao, nadhani wakati wa mchezo wa Marudiano bila shaka itakuwa zamu yetu kuibuka na ushindi maana leo wameshinda wao na mpira ni mchezo wa mmoja kushinda, asiyekubali kushindwa siyo mshindani” alisema majuto
na kuongeza kwamba mchezo huo kwa pande zote mbili umewapa changamoto ya kuifanya sasa timu hiyo ya Kombaini ya Makipa kutambuliwa kote Nchini.“mkakati uliopo sasa ni kuhakikisha kwamba timu hii inazunguka kwenye Majiji Makuu kwa ajili ya kufanya michezo yake ya kirafiki na timu za Mikoa, lakini lengo kubwa ikiwa ni kuwapa Fursa wakazi wa Maeneo hayo kuwatambua zaidi hawa Makipa wetu, lakini pia wakati wachezaji hawa wakiwa kwenye hayo maeneo ya Majiji watakuwa na jukumu la kuwaandaa wachezaji wengine zaidi vijana katika nafasi za kipa ili kuweza kuwa na Makipa wengi zaidi kwa ajili ya Faida ya Taifa letu la Tanzania” alisema Majuto
Naye kocha wa Taswa FC Ally Mkongwe wakati akizungumza na wachezaji wa timu zote alisema kuwa ni jambo la kufurahisha ambalo limeweza kufanikiwa kwa asilimia 100 kwa kuwa lengo ilikuwa ni kufanya uzinduzi na timu zote zimeweza kucheza kwa hali kubwa bila vurugu wala kuonyeshana mchezo mbaya.
“tumefurahi sana, niwapongeze wachezaji wote yaani Makipa na Taswa, jambo hili si la mzaha kama tulivyofikili hapo mwanzo, lakini kumbe mwitikio wa watazamaji ulikuwa ni mkubwa sana na wengi wamekuja kuwatazama wachezaji na Waandishi wa habari, Watangazaji, na wakati umefika tukae tuangalie namna ya kuboresha mahusiano haya yawe ya kudumu baina ya TASWA na timu hii ya Kombaini ya Makipa wa Ligi kuu, isipokuwa tusameheane kwa yale Mapungufu madogo yaliyotokea maana sisi ni binadamu lakini wakati mwingine nadhani hayatatokea kwa pande zote mbili endapo yametokea kwa mchezo wa leo” alisema Mkongwe.
Hata hivyo wachezaji hao Makipa wametakiwa kufanya jitihada za kuhakikisha wanakuwa chachu ya kuleta Makipa wengine nyuma yao kutokana na kwamba nafasi ya Makipa kwa Tanzania inazidi kupungua kutokana na nafasi hiyo kuwa ngumu ukilinganisha na nafasi za wachezaji wengine wa ndani ambao wanakuwa ni wengi.
Naye mmoja wa Makocha wasaidizi wa timu ya TASWA Ibrahim Masoud aliwaasa wachezaji hao kuwa kioo kwa wenzao na kuwa kishawishi cha kuwapata vijana wengine watakaokuwa makipa wa Tanzania miaka ijayo”Sina Mengi ya Kusema kwa kuwa Kocha na Mwenyekiti wameeleza kwa kirefu lakini mimi niko tofauti kidogo na wenzangu, kikubwa hapa mimi ni kuhusu nyie Makipa wetu, kumbukeni kwamba nyinyi kina Kaseja, Ivo Mapunda, Shaaban Kado, Dida, mstafa na nyinyi wote, nyie sasa mnaelekea Ukingoni, ni kama kina Mwameja wakati wao, kina Manyika, Mfaume,nk, walikuwapo lakini walipopotea hao makipa Tanzania iliyumba sana kuwapata nyinyi, na hiyo inatokana na kwamba Wachezaji wengi Makipa hawapati Fursa ya kuandaliwa, na niwatake sasa kutumia mwanya huu kwa kuwa tayari mmekuwa ni makipa Hodari kuhakikisha kwamba wakati wa Mapumziko ya Ligi, muweze kuingia Darasani kwa ajili ya kupata ujuzi wa kuwa Walimu wa Makipa, Kila mmoja kwa wakati wake lengo mtakapomaliza muda wenu wa kuitumia Tanzania katika Soka, muweze kuwa walimu wazuri na wazalishaji wazuri wa Makipa wengine” alisema Ibrahim Masoud(Maestro)
Kwa Upande wao Makipa hao wao hawakuwa na la kusema isipokuwa kwa niaba ya wachezaji wote wa Makipa Ivo Mapunda alisema kuwa wanashukuru kwa Sapoti kubwa kutoka Chama cha TASWA, ambao mara zote wamekuwa mstari wa mbele kuwapa maelekezo, kitendo kilichowaweka karibu zaidi hata wakati wa Uzinduzi wa Chama hicho cha Magolikipa,” Sisi binafsi tumefurahi kukutana na timu hii ya TASWA, maana kiujumla wachezaji wengi wa Taswa wanafahamu mpira, ila tumewafunga kutokana na kukosa Pumzi tofauti na sisi wengi tunafanya mazoezi kila siku na timu zetu tena timu kubwa za ligi kuu, mimi Kesho( Leo) naelekea Zazibar Kambini, kujiunga na Timu yangu, kwa hiyo unaona jinsi mchezo huu ulivyokuwa ni muhimu sana kwetu hata nimeshindwa kuongozana na wachezaji wazangu pamoja na Mwalimu wangu kutaka nisicheze hii leo lakini nimemkatalia kwamba ni lazima nijumuike na Makipa wenzangu kwenye jambo hili la Umoja, maana sasa sisi Makipa pia tumekuwa ndugu wa karibu na Marafiki wa Kweli, zama za kale kwamba huyu na huyu aziivi eti kwa kuwa wote ni Makipa imepitwa na wakati, utatukuta mimi, Kaseja, Kado, Dida, Mstafa, na wengine tukizungumza na kufurahi pamoja, sisi siyo maaduni ni marafiki tena niwapongeze Wadhamini wa Mpambano huu(Uzinduzi) Kampuni ya TWIGA CEMENT kwa kufanya jambo hili, limezidi kutuweka karibu zaidi, na naamini kwamba watazidi kutuunganisha na kuandaa michezo Mingi zaidi kwa ajili ya kuwapa Raha wakazi na mashabiki wetu Mikoani” alisema Ivo Mapunda Akizungumzia mchezo huo Afisa Masoko wa TWIGA CEMENT,Alex Gideon, alisema kuwa maandalizi yamekwenda kama walivyopanga isipokuwa mkanganyiko umetokea kwenye eneo dogo la Uwanja, ambapo awali mchezo huo ilikuwa ufanyike kwenye uwanja wa KARUME kwa mujibu wa Matangazo yaliyofanywa na vyombo vya habari,” sitaki kulizungumzia sana suala la mkanganyiko wa Uwanja, lakini nadhani TFF katika hatua za mwisho imeshindwa kuruhusu mchezo wetu kufanyika kwenye viwanja vyao ambako vyombo mbali mbali vilitangaza, hivyo mashabiki wengi walifika Karume, na nichukue fulsa hii kuwataka radhi sana wote waliotufuata kwenye viwanja vya Karume, mchezo wetu ulibadilishwa uwanja kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu na kwa kuwa ni TFF wenyewe waliopanga hatua za Mwisho Mchezo wa Ligi daraja la kwanza kufanyika humo hatukuwa na kipingamizi, ni jambo la kimchezo na ukizingatia ni ligi yetu pia sisi watanzania hivyo hilo niombe radhi kwa mashabiki wetu wote, lakini kuhusu wadhamini wetu kama ulivyoona mwenyewe wamejitaidi na huu ni mwanzo na maandalizi yamefanyika kwa siku chache zana, wakati ujao tutaboresha na kulifanya jambo hili kuwa la kudumu na lenye kuleta tija ya Maendeleo kwa hawa Makipa wetu, kingine niwapongeze TASWA kwa ushirikiano wao maana wametufariji na kutupa sapoti kubwa” alisema Alex Gideon aidha mchezo huo ulikuwa kwa ajili ya kujenga mahusiano mema baina ya timu zote, wachezaji pamoja na kufanya Uzinduzi wa Chama cha Makipa Tanzania, waandishi na Makipa wanaocheza ligi kuu Ya Vodacom Tanzania.

Hazina SACCOS yakadhi hati za viwanja ambavyo ni rasmi zaidi kwa 150 kwa wanachama.

$
0
0
 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kulia) akiwasili viwanja vya Mkumbusho ya Taifa mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa  Mkutano Mkuu wa Mwaka wa siku mbili (Disemba 20-21) wa wanachama wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina, mkutano huo  unaongozwa na kauli mbiu isemayo “Viwanja Rasmi Suluhisho la Makazi Bora”. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Eligius Mwankenja. 
 Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya kufungua  Mkutano Mkuu wa mwaka wa siku mbili mwishoni mwa wiki (Disemba 20-21) wa wanachama wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina, mkutano huo  unaongozwa na kauli mbiu isemayo “Viwanja Rasmi Suluhisho la Makazi Bora”.

 Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina Eligius Mwankenja akitoa neno wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofaviwanja vya Mkumbusho ya Taifa  mwishoni mwa wiki (Disemba 20-21) jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum wakati wa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofaviwanja vya Mkumbusho ya Taifa mwishoni mwa wiki (Disemba 20-21) jijini Dar es salaam.
 Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofaviwanja vya Mkumbusho ya Taifa mwishoni mwa wiki (Disemba 20-21)  jijini Dar es salaam.
. Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina waliokabidhiwa hati zao za viwanja mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofaviwanja vya Mkumbusho ya Taifa mwishoni mwa wiki (Disemba 20-21) jijini Dar es salaam. Mkutano huo unaongozwa na kauli mbiu isemayo “Viwanja Rasmi Suluhisho la Makazi Bora”. (Picha zote na Eleuteri Mangi)

EXCLUSIVE INTERVIEW: DIAMOND AFUNGUKA KUHUSU WEMA, ZARI, MENINA NA PENNY. UNAJUA KATI YA WEMA NA PENY NANI ALIMFUNDISHA KIINGEREZA? WHY HANA MTOTO?

Waandaaji wa Tuzo za Filamu nchini washauriwa kuzimtangatia viwango na ubora wa kazi za wasanii

$
0
0
 Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akiwa katika kikao cha majadiliano na kamati ya Maandalizi ya Nyumbani Kiswahili Film Awards yaliyofanyika hivi karibuni ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi  Nyumbani Kiswahili Film Awards Bw. Fadhil Francis Mfate akichangia hoja wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu maandalizi ya Tuzo hizo yaliyofanyika katika ofisi za Bodi ya Filamu hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Utawala wa Kampuni ya Bao Limited Bw. Joseph Noel na Mjumbe wa Kamati ya maandali ya tuzo hizo Bi. Lucia Joseph.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tabasamu Film Production Bw. Hamza Shaban akifafanu jambo akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu maandalizi ya uandaaji wa tuzo za Nyumbani Kiswahili Film baina ya Bodi ya Filamu na Kamati ya Maandalizi ya tuzo hizo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM.

PROIN PROMOTIONS LTD WISH YOU MERRY XMASS AND HAPPY NEWS YEAR

Timu ya Makipa yaichapa 3-0 Taswa FC

$
0
0
 Mshambuliaji wa timu ya chama cha makipa Tanzania (TAGA), Ivo Mapunda akimiliki mpira na kiungo wa Taswa FC, Martin Peter katika mchezo maalumu wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Bora kijitonyama. TAGA FC ilishinda kwa mabao 3-0.
Kiungo-mshambuliaji wa timu ya makipa Tanzania (TAGA), Deogratius “Dida” Munishi akiwania mpira na mshambuliaji wa Taswa FC, Ibrahim “Maestro” Masoud katika mchezo maalumu wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Bora kijitonyama. TAGA FC ilishinda kwa mabao 3-0.
 
 
Timu ya soka ya Chama Cha Magolikipa Tanzania (TAGA) imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Timu ya soka ya waandishi wa habari za Michezo nchini (Taswa FC) katika mchezo maalum wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini. 

Mchezo huo maalum awali ulitakiwa kufanyika kwenye uwanja wa Karume,  ulihamishiwa uwanja wa bora kutokana na ‘Mizengwe’ ya dakika za mwisho  ya wamiliki wa uwanja huo.
 
Timu zote zilianza mchezo huo kwa kasi na kukosa nafasi kadhaa za wazi. TAGA ndio ilikuwa ya kwanza kulifikia lango la Taswa FC ambayo ilizindua jezi zake kwa mara ya kwanza zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), hata hivyo mshambuliaji wake, Ivo Mapunda akipiga nje.Makipa walikuwa katika nafasi nzuri ya kufunga tena katika dakika ya sita ya mchezo, hata hivyo penati ya Shaaban Kado ikipanguliwa na kipa wa Taswa, Ahmed Famau.
 
Taswa FC iliibuka katika dakika ya nane ya mchezo na Zahoro Mlanzi alikosa bao la wazi akiwa na kipa wa TAGA FC, Fatuma Omari ambaye pia alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira miwili ya kona iliyokuwa ikiingia wavuni kutoka kwa Majuto Omary. 
 
Pamoja na kuwa na umri mkubwa na kutofanya mazoezi kila siku kulinganisha na timu ya makipa, wachezaji wa Taswa, Ali Mkongwe, Martin, Majuto, Ibrahim Masoud,  Zahoro Mlanzi, Shafii Dauda, Wilbert Molandi, Sweetbert Lukonge, Muhidini Sufiani, Salum Jaba, Juma Ramadhani na Julius Kihampa walionyesha uwezo mkubwa katika mchezo huo .
 
 Makipa walitumia mazoezi yao ya kila siku vizuri na kupata bao katika dakika ya 14 lilolofungwa na Mapunda kufuatia krosi safi ya Saleh Malande alicheza vizuri na Juma Kaseja na Ali “Barthez” Mustapha ambaye pia alifunga bao la tatu. Bao la pili la makipa lilifungwa na Shaaban Kado baada ya kazi nzuri ya Deogratius “Dida” Munishi.
 
Rais wa makipa hao, Alex Ndembeka alisema kuwa wamefarijika sana mchezo huo ambao umetumika rasmi kuzindua chama chao ambacho lengo lake kubwa ni kuendeleza fani hiyo kwa kuvumbua vipaji na kuondoa fikra za kuwa ‘magolikipa’ hawapendani.
 
“Tunawapongeza waandishi kwa kukubali wito wetu na kufanikisha kuzindua chama hiki, nadhani umeona jinsi ilivyo kwa makipa wetu kucheza pamoja, kufurahi na kuondoa mtazamo hasi wa kuwa makipa hawapendani,” alisema Ndembeka.
 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASMI MAJENGO YA TAASISI YA MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO TANZANIA.

$
0
0

03
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo Desemba 22, 2014.
04 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi katika Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo hayo uliofanyika leo Desemba 22, 2014.
06
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la viwanja vya Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, baada ya kuzindua rasmi majengo hayo yaliyopo eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam leo Desemba 22, 2014.
02
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania kwa ajili ya kuzindua Taasisi hiyo iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam, leo Desemba 22, 2014.
Picha zote na OMR
01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akizindua rasmi Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo Desemba 22, 2014.
09
010


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASMI MAJENGO YA TAASISI YA MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO TANZANIA.

NEWZ ALERT:JOHNSON LUKAZA WA KESI YA EPA ASHINDA KESI

$
0
0
Johnson Lukaza
Mwesigwa Lukaza 


Na Happiness Katabazi (UB)
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachilia huru Mwenyekiti  wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza na mdogo wake Mwesiga Lukaza waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Sh.Bilioni Sita Katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu(EPA), baada ya kumuona Hana hatia Katika Kesi iliyokuwa ikimkabili.

Hukumu hiyo Imetolewa Jaji wa Mahakama Kuu Edson Mkasimongwa aliyekuwa alisaidia na Hakimu Mkazi Pamela Mazengo.
Lukaza ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) alikuwa akitetewa na Wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Mkasimogwa alisema Kesi hiyo ya Mwaka 2008 , Mahakama imesikiliza ushahidi wa pande zote mbili Na kupitia vielelezo mbalimbali, Mahakama yake Imefikia uamuzi wa kuwaachiria huru washitakiwa wote Wawili kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi thabiti ambao ungeishawishi Mahakama hiyo iwakute na hatia washitakiwa Hao.

Airtel yawapatia kundi la walemavu mtaji na mafunzo ya biashara

$
0
0
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akikata utepe kama ishara ya kukabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu wenye ulemavu, wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), kwa ajili kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamari, katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Buguruni Viziwi jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya na (kulia) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Abubakar Rakesh na mnufaika wa kibanda hicho, Hebron Mwansele (kwenye baiskeli).
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akihutubia wakati wa hafla hiyo.
Sehemu wa wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), wakiwa katika hafla hiyo.

ALIKIBA AZINDUA VIDEO “MWANA”

$
0
0


NYOTA WA MUZIKI AFRIKA MASHARIKI, ALIKIBA AZINDUA VIDEO “MWANA” ILIYOKUWA IKISUBIRIWA KWA HAMU KWA KISHINDO, KATIKA VITUO VIKUU VITANO AFRICA PAMOJA NA DUNIA NZIMA
 
Akiwa ana nyimbo za “Mwana” na “Kimasomaso” zikiongoza  katika vituo mbali mbali Africa, Alikiba aachia video ya “Mwana” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu jana ,Ijumaa tarehe 19 Decemba 2014 kwa mamilioni ya mashabiki Africa na duniani. “Mwana” ni nyimbo ya kwanza  baada ya kufunga mkataba wake na kampuni ya Rockstar4000 Management na Rockstar Publishing.

Rekodi ya “Mwana” ni nyimbo ya kwanza kutoka kwenye albamu ya tatu ya Alikiba baada ya kutokuwa katika muziki kwa muda wa miaka mitatu. Alikiba alifafanua kwa kusema “ Hii ni album itayoonyesha kukua kwangu kimuziki na kuonyesha utofauti mbali mbali katika kipaji changu nilichojaliwa.”  

Alikiba alitoa kibali ili video ya “Mwana” iruke hewani jana “exclusively” kwa masaa 24 kwenye vituo vya televisheni vitano Africa katika vipindi maarufu kwenye vituo hivyo na kuwafikia mashabiki zaidi ya milioni 500 kwa pamoja. Vituo vya televisheni hivyo ni Clouds TV kuonyesha exclusive Tanzania, Nation TV kuonyesha exclusive UgandaOne Music Networks kuonyesha exclusive Cameroon, Angola, Ethiopia, USA na UK, Sound City kuonyesha exclusive Nigeria na Ghana na Citizen TV exclusive kwa upande wa Kenya, DRC Congo na Rwanda

MHE . UMMY MWALIMU AENDESHA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WASICHANA WA WILAYA YA MUHEZA – TANGA

$
0
0
04
Mhe Ummy Mwalimu Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kujitambua na kujithamini Wilayani Muheza mwishoni mwa wiki.
03
Mhe Ummy Mwalimu Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais akifungua mafunzo kwa wasichana wa Wilaya ya Muheza juu ya kujitambua na kujithamini katika masuala ya Afya ya uzazi. Mafunzo hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Muheza
01
Wasichana wa Wilaya ya Muheza wakifanya majadiliano na mawasilisho katika vikundi juu ya changamoto wanazokumbana nazo katika kipindi cha ujana.
02 
Wasichana wa Wilaya ya Muheza wakifanya majadiliano na mawasilisho katika vikundi juu ya changamoto wanazokumbana nazo katika kipindi cha ujana.

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images