Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 428 | 429 | (Page 430) | 431 | 432 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Mkuu wa operesheni wa Benki ya Exim, Bw. Eugen Massawe (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Dar es Salaam, jana, kuzindua ‘Exim Smart App’, program ya simu iliyotengenezwa maalumu kwa ajili ya simu aina ya ‘smartphones’ itakayowawezesha wateja wa benki hiyo kupata huduma za kibenki kupitia simu zao za mkononi. Kulia ni Afisa Masoko wa benki hiyo, Noel Tuga. 

  Katika jitihada zake za kuboresha utoaji wa huduma za kibenki kupitia simu za mkononi, Benki ya Exim imezindua program mpya ya simu ya aina yake kwa wateja wa benki hiyo wanaotumia simu aina ya ‘smart phone’.

  Programu hiyo kwa sasa inapatikana katika simu zilizo na uwezo wa Android, Windows, Black Berry na mfumo wa IOS.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Operesheni wa Benki ya Exim, Be. Eugen Massawe alisema kuwa programu hiyo mpya  inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kufurahia huduma salama za kibenki kupitia simu zao za mkononi kama vile kuangalia miamala, kupokea taarifa za akaunti katika zao pamoja na huduma nyingine nyingi. 

  “Kwa kupitia Exim Smart App, sasa wateja wa Benki ya Exim wataweza kuangalia taarifa mbalimbali zinazohusu akaunti zao na kufuatilia miamala yote itakayokuwa ikifanyika kwenye akaunti zao kwa urahisi zaidi.

  “Programu yetu ya simu ni rahisi sana kutumia ikiwa imeundwa kwa kumzingizatia mteja ili kumuwezesha kuona machaguo mbalimbali punde tu anapoifungua programu hii na hili limefanyika hili kupunguza mlolongo mrefu katika uchaguzi wa huduma ambayo mteja atakuwa anahitaji,” alisema Bw. Massawe.

  Bw. Massawe alisema kuwa Benki ya Exim imekuwa benki ya kwanza ya kitanzania kutambulisha programu ya aina hiyo, jambo lililotokana na juhudi za makusudi zinazofanywa na benki hiyo ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wateja wake.

  “Mteja atahitajika kuwa amejisajiliwa na ‘Exim Mobile Banking’ ili kuweza kutumia program hii mpya ya Exim Smart App itakayomuwezesha kufurahia ulimwengu mpya wa kibenki. 

  Lengo letu ni kuwawezesha wateja wetu kufanya biashara zao kwa urahisi zaidi, kwa njia yoyote ile wanayopendelea, aidha kupitia kompyuta za mezani au kupitia simu zao za mkononi,” aliongeza.

  Huduma za kibenki kupitia simu za kiganjani zimeendelea kupata umaarufu mkubwa, huku wateja wakionyesha kuvutiwa zaidi na njia hii mpya inayowawezesha kufanya miamala pasipo ulazima wa kutembelea tawi la benki.

  Exim Smart App inapatikana bure na inaweza kupakuliwa kutoka kwenye App Store.

  0 0

  DSC_0175

  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyeteuliwa hivi karibuni, Daud Felix Ntibenda alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani humo.
  DSC_0170
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati Mkuu wa Mkoa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wkibadilishana mawazo kabla ya kuanza mazungumzo yao.
  DSC_0178
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyeteuliwa hivi karibuni, Daud Felix Ntibenda akizungumza na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) aliyeambatana na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu.
  DSC_0185
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo na uongozi wa mkoa wa Arusha ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Daud Felix Ntibenda (kulia) na kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Addo Mapunda.
  DSC_0189
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kushoto) katika picha ya pamoja na uongozi wa mkoa wa Arusha.
  DSC_0198
  Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Addo Mapunda akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Daud Felix Ntibenda.

  0 0


  0 0
 • 12/18/14--02:54: JIZAWADIE SMARTPHONE

 • 0 0

  IMG_7245

  Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.(Picha zote na Eleuteri Mangi- Arusha).

  Na Mwandishi wetu, Arusha
  SERIKALI ya Tanzania imeridhia azimio la arusha kuhusi hifadhi ya jamii nchini Tanzania na kusema litatumika kama dira katika kunemeesha watanzania. Azimio hilo ambalo limetoka baada ya mkutano wa siku tatu wa wadau mbalimbali wa hifadhi ya jamii kutoka bara la Afrika na mashirika ya kimataifa limeelezwa kuwa msingi mkubwa wa ajenda ya Tanzania kuhakikisha wananchi wake wanahaki sawa katika elimu, afya na mwendelezo wa kiuchumi. Lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba hifadhi ya jamii inasaidia kuwa na maendeleo endelevu kwa kuangalia maendeleo ya binadamu katika ujumla wake.

  Mkutano huo wa siku 3 uliohusisha wataalamu 150 kutoka sekta mbalimbali nchini na barani Afrika wakiwemo watengeneza sera, watafiti na wataalamu wa masuala ya hifadhi. Ukiwa umewezeshwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na UNICEF, ILO, UNAIDS na taasisi ya utafiti wa sera za uchumi EPRI iliyopo Afrika Kusini (EPRI) , mkutano huo umeelezwa na waziri wa fedha Saada Mkuya Salumkwamba umeweka misingi imara ya kuwa na hifadhi ya jamii endelevu inayojibu mipango ya maendeleo ya taifa.
  IMG_7158
  Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akisoma Azimio la Arusha linalohusu hifadhi ya Jamii, alisema kuwa historia imejirudia ambapo yapata miaka 47 (1967-2014) iliyopita Tanzania ilipitisha Azimio la Arusha lililolenga kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini ambao Baba wa Taifa Mwl. Julius Kmbarage Nyerere aliwaita ni maadui wa taifa.

  Kukiwa na wataalamu waliobobea katika mifumo ya hifadhi ya jamii kutoka Afghanistan, Bangladesh, Ethiopia, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe ulifanikiwa kutengeneza hoja zitakazotumika kufanya hifadhi ya jamii Tanzania kuwa endelevu.

  Waziri Mkuya alishukuru kwa ushiriki wa mkutano na jinsi ulivyokuwa wazi na jinsi wataalamu walivyoweza kutengeneza azimio ambalo linaenda kuwa msingi katika utengenezaji wa sera na sheria kuhusu hifadhi za jamii nchini Tanzania na afrika kwa ujumla.

  Mada kadhaa ziliwasilishwa katika mkutano huo ambazo zilizaa majadiliano yenye manufaa kuhusu mwelekeo wa hifadhi za jamii,utengenezaji wa mifumo ya kuweza kuendelea kuwepo kwa hifadhi ya jamii na umuhimu wa uratibu ndani ya serikali kuu, mitaa na mashirika yanayiotoa huduma za hifadhi ya jamii.
  IMG_7135
  Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Jama Gulaid (kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb) wakisikiliza azimio la Arusha linalohusu hifadhi ya jamii wakati wa kufunga kongamano hilo.

  Waziri huyo alisema kwamba wakati taifa linaelekea katika uchumi wa gesi utakaofanya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 masuala ya hifadhi ya jamii yatakahakikisha haki katika kugawa keki ya taifa na kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata huduma za elimu, afya, na za kiuchumi kwa haki, kwa kuwa mifumo hiyo pia itatakiw akuchochea ajira na ujasirimali huku ilkilinda afya za wahusika.

  Kwa upande wake Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani aliisifu Tanzania kwa kuanza mapema kusimamia masuala ya kinga ya jamii ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii na misaada inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia mpango wake wa kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi.

  Aidha, Dkt. Gulaid aliipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika na watu wake licha ya kuwa na vivutio vizuri vya mlima Kilimanjaro, hifadhi ya Serengeti na visiwa vya karafuu.
  IMG_7204
  Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha na aliisifu na kuipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika na watu wake.

  “Wimbo huu wa Tanzania tofauti na nyimbo za nchi nyingine ambazo wao wanazungumzia askari, watumwa, watawala wakiwemo Malkia na Wafalme”alisema Dkt. Gulaid. Dkt. Gulaid aliwahakikishia wajumbe wa mkutano huo kuwa wote wapo salama na wapo kwenye mpango wa hifadhi ya jamii kwa kuwa wametambuliwa na kubarikiwa na wimbo wa taifa wa Tanzania ambapo wajumbe waliimba wimbo huo na kuhitimisha kongamano hilo.
  DSC_1058
  Washiriki wa Kongamano hilo wakiimba wimbo wa Taifa baada ya Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid kutoa ombi kabla ya kumalizika kwa kongamano hilo.

  IMG_7109
  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akisistiza jambo wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.
  DSC_1061
  Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitia saini Azimio la Arusha kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii huku viongozi mbalimbali wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa wakishuhudia tukio hilo.
  IMG_7267
  IMG_7269
  Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na washiriki wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha akionesha nakala ya Azimio la Arusha alilosaini kwa niaba ya Serikali.
  IMG_7271
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimpongeza Wazri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum baada ya kusaini Azimio la Arusha kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii (katikati) kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb).
  IMG_7272
  Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (kushoto) akipeana mkono na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb) mara baada ya kusaini azimio hilo huku Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishuhudia tukio hilo.
  IMG_7102
  Baadhi ya wajumbe wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha akifuatilia mada wakati wa kongamano hilo.
  IMG_7173
  IMG_7003
  IMG_7043
  Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) mara baada ya kumalizika kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.

  0 0

  Mr. Hashim Mukudu, ZANTEL Dir. MFS, speaking with journalist (not in picture) at the press conference in Zanzibar.
  GROUP PHOTO – Senior  Management Team from ZANTEL and TIGO.


  Zanzibar, Dec 17th, 2014: ZANTEL and Tigo have officially launched the mobile money interoperability service in Tanzania that will open up a number of mobile money transactions between the customers’ of the two telecom operators. In addition to transactions within their own network, EzyPesa and TigoPesa customers are now able to send and receive cash direct to and from customer friends and family on their partner networks across the country.

  This places ZANTEL and Tigo among the pioneers of this service in the world, a progressive initiative announced by EzyPesa, TigoPesa and Airtel Money early this year.

  How it works

  Zantel Customers:
  Tigo Customers:
  1.       Dial *150*02#
  1.       Dial *150*01#
  2.       Choose : Option 1 (Send Money)
  2.       Choose : Option 1 (Send Money)
  3.       Choose : Option 2 (Send to TigoPesa)
  3.       Choose : Option 5 (Send to Zantel)
  3.1.    Enter TigoPesa Number
  3.1.    Enter Zantel Number
  3.2.    Enter Amount
  3.2.    Enter Amount
  3.3.    Enter Password
  3.3.    Enter Password
  3.4.    Wait for the confirmation SMS
  3.4.    Wait for the confirmation SMS

  There is no surcharge for sending money across networks and charges are priced the same as sending within their home network.  Customers receiving money from another network can cash out from their own networks agents and no longer have to find agents from the other network.

  Zantel’s Commercial Director, Mohamed Mussa, commented that Zantel continues to fulfil its promise of bringing ease to its customers by enabling them with financial mobility through their partnership with Tigopesa.

  By doing this we have increased the customer base that can interact with Zantel customers through sending and receiving. We are at the forefront on the financial traction corridors between Zanzibar and Mainland, concluded Mr. Mussa

  Mobile Finance Director, Hashim Mukudi also added, that Zantel is at the forefront to ensure the rate of financial inclusion and financial participation in Zanzibar is improves. We have ensured our agents network and the support agency mechanism are in place to serve the customers.

  Tigo’s Head of Mobile Financial Services, Andrew Hodgson, said, “We are delighted to expand our customers transacting capacity through our partnership with Zantel. By expanding our customer’s mobile money ecosystem, particularly in Zanzibar where there is still a lot of potential for mobile financial services growth.

  Similar to other telecommunication services like voice calls and text messages there are often huge opportunities to improve the customers experience by cooperating rather than only competing with industry partners massively expanding the digital financial inclusion in Tanzania.

  Through our partnerships with other industry players we are able to expand our customers digital world by leveraging existing technology to effectively combine our mutual customer base, thereby exponentially expand the transactional ecosystem potential. In this way we are able offer additional convenience in terms transaction versatility, speed, safety and security to both our own, and our partner’s customer base.

  Indeed today’s partnership will bring our two companies closer together but more importantly will bring our customers even closer, by providing access to electronic and digitized financial service that they were never previously able to access,”  Hodgson added.

  0 0


  0 0


  Ofisa wa Kiwanda cha Bia TBL Arusha aliyeko katika idara ya uzalishaji akiwaonyesha baadhi ya wanahabari wa Arusha namna bia inavyohifadhiwa wakati wa ziara ya waandishi iliyokwenda sanjari na zoezi la kuonja bia na kutembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.


  Baadhi ya waandishi wa habari wa Arusha wakiangalia utunzaji wa mazingira unavyofanywa na Kiwanda cha Bia cha Arusha (TBL), ambapo maji yote yanayotumika kwa shughuli za kiwandani hapo huhifadhiwa na kuchunjwa kwa ajili ya matumizi mengine yakiwamo bustani na vyooni, waandishi hao walitembelea kiwandani hapo kwa ajili ya kuongeza ufahamu zaidi wa utunzaji mazingira.


  Meneja Mpishi wa Kiwanda cha Bia TBL Arusha Ben Mwanri akiwasilisha mada kwa wanahabari wa Arusha waliotembelea kiwandani hapo kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali ikiwamo pia zoezi la kuonja Bia lililowashiurikisha waandishi hao wa habari.


  0 0


  0 0
   Moja ya Nyumba ya mkazi wa kijiji cha Nungu kilichopo kata ya Matamba wilayani Makete iliyoezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua hivi karibuni, hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na hali hiyo
   Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro (kulia) akiangalia moja ya nyumba iliyobomoka kutokana na upepo huo mkali, kulia kwake ni baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Makete.
   Nyumba iliyobomolewa na mvua na upepo mkali.
   Mkuu wa wilaya akiangalia nyumba ya mkazi mwingine iliyoharibika
  Mkuu wa wilaya ya Makete akitoa maagizo baada ya kujionea hali halisi eneo la tukio
   Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro (kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Makete wakisiliziza jambo eneo la tukio.
  Afisa mtendaji wa kijiji cha Nungu Bw. Ngogo akitoa taarifa mbele ya kamati ya ulinzi na usalama kuhusu tukio hilo (Picha zote na Edwin Moshi wa Eddy Blog)

  Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro ametoa agizo kwa uongozi wa kata ya Matamba kufanya mikutano ya kuwaelewesha wananchi umuhimu wa kujenga nyumba zao katika hali ya uimara pamoja na kupanda miti ya matunda pembezoni mwa nyumba zao

  Ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati alipotembelea eneo lililopata maafa ya kuezuliwa nyumba na upepo mkali ulioambatana na mvua na kugundua kuwa ujenzi hafifu wa nyumba zao nao umechangia kwa kiasi kikubwa hasara hiyo

  "Wananchi wanajenga nyumba hazina makoa, maeneo ni wazi hayana miti achilia mbali ya matunda lakini hata mingine hakuna, haya maafa hayataisha, mtendaji nakuagiza ufanye mikutano na wananchi na taarifa nipewe" alisema Matiro
   
  katika tukio hilo hakuna vifo wala majeruhi ya watu, zaidi ya nyumba na baadhi ya vitu vilivyokuwa ndani kuharibika

  0 0

   Ujumbe wa wataalamu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA) unatembelea Bandari ya Singapore (PSA) ili kubadilishana utaalamu wa namna ha kuongeza ufanisi na kuimarisha Ulinzi na usalama wa Bandari kwa kutumia Mitambo ya kisasa na Teknolojia ya Habari na mawasiliano (ICT) , Ujumbe wa TPA unaongozwa na Ndg. Phares Magesa , Mkurugenzi wa ICT wa TPA, pia wamo wahandisi wa majengo, wataalamu wa Ulinzi na wataalamu wa  TEHAMA. Ziara hii ni muendelezo wa ushirikiano wa PSA na TPA ikiwa ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa sahihi kati ya TPA na PSA wakati wa ziara ya Mhe. Rais Kikwete alipotembelea nchini Singapore mwaka jana.
    Ujumbe wa TPA ulipotembelea eneo la Bandari ya Singapore linalotumika kwa ajili ya Meli za abiria, starehe na kuvinjari ( waterfront development ).
   Ujumbe wa TPA ukiwa kwenye chakula Cha pamoja na Ujumbe PSA
   Ujumbe wa TPA ukiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa PSA makao makuu ya PSA
   Mkuu wa msafara Ndg. Magesa akisalimiana na Makamu wa Rais Msaidizi wa PSA anayeshugulikia ICT Ndg. Andrew Gill wakati akiwakaribisha makao makuu wa PSA
  Mkuu wa msafira wa TPA Ndg. Magesa akipokea zawadi toka Makamu wa Rais Msaidizi wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore ( PSA) anayeshugulikia biashara Ndg. Vignes kulia

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

  Kulingana na, Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.Dkt. James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. 

  Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-
  ELIMU:-
  Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)
  PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)
  MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
  BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994

  UZOEFU WA KAZI:-
  Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA
  2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu
  2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)
  1994 – 1999 -, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.

  Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.

  Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.

  Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu.
  Dar es Salaam.
  18 Desemba, 2014

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman akizungumza na wageni waalikwa katika sherehe za Uzinduzi wa kitabu cha sheria za Kazi katika lugha nyepesi katika Hoteli ya Double Tree Shangani Mjini Zanzibar.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman na Mkurugenzi wa (ILO) kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma wakizindua kitabu cha sheria za Kazi katika lugha nyepesi, katika Hoteli ya Double Tree Shangani Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  Baadhi ya walikwa waliohudhuria katika Uzinduzi wa kitabu cha sheria za Kazi katika lugha nyepesi Hoteli ya Double Tree Shangani.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Ndg. Michael Mwanda, akifunga semina ya wadau wa mafuta na gesi iliyofanyika Bagamoyo.
   
     Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi, Nobert Kahyoza, akifungua semina ya TPDC kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Semina hiyo ililenga kutoa taarifa muhimu zinazo hitajika kwa wadau katika sekta ya mafuta na gesi kutoka sehemu mbali mbali zikiwemo wizara, taasisi na waandishi wa habari, semina hiyo iliyofanyika Bagamoyo.
   Wadau wa sekta ya mafuta na gesi walioshiriki semina wakifutilia kwa makini mtoa mada (hayupo pichani) katika semina hiyo Bagamoyo.

  1.     Washiriki wa semina ya mafuta na gesi iliyoandaliwa na TPDC na kufanyika Bagamoyo, wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

   Mwanamuziki nguri wa muziki wa dansi nchini, John Kitime ameibukia katika filamu na karibuni amezindua sinema iitwayo ‘Kutakapokucha’ ambayo ina akisi watendaji wasio waadilifu wanavyozitumia vibaya ofisi za umma na kuchangia migongano katika jamii.

  Katika filamu hiyo ambayo Kitime anacheza kama muigizaji mkuu, akitumia jina la Nongwa, ndiye mwanakijiji pekee ambaye nyumbani kwake kuna umemejua akijivunia televisheni wanayokuja kuiangalia na baadhi ya wakazi wenzake kijiji na huduma za kuchaji simu anazozitoa nyumbani kwake.

  Kwa kutumia ofisi yake, anapora ardhi za watu na mbaya zaidi anawachukia wenye mwamko kidogo wa elimu ambao binafsi anaona hawana lolote zaidi ya kuhitaji kiti chake hali ambayo inazua migongano na migogoro mikubwa ambayo mwisho wake ndio kinachoifanya hiyo filamu kuwa na msisimko wa namna yake.

  Filamu hiyo ambayo imeandikwa na Irene Sanga chini ya utayarishaji wa Sylone Malalo na kuongozwa na Simon Mwakifwamba, msambazaji mkuu ikiwa kampuni ya Proin Promotion, licha ya pia ina muigizaji mahiri nchini, Charles Magari ‘Mzee Magari’.

  Mtayarishaji wa filamu hiyo, Malalo anasema movie hiyo inatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu nchini na anawataka wale ambao wanapenda vitu tofauti kuangalia pia inashirikisha wasanii wa Sanaa za mapigano ‘martial arts’.

  Magari ambaye anaigiza kama mtu ambaye anataka mabadiliko kijijini hapo na kuondokana na urasimu na ukiritimba wa Mzee Nongwa, ina waigizaji mahiri ambao pia ni walimu wa Sanaa katika Taasisi ya Sanaa (Tasuba) ambao ni na Thabit Hudu na Mwanaidi Zambo.

  Filamu hiyo ni kazi ya kwanza pia ya mzalishaji Malalo ambaye amebobea katika utengenezaji wa picha za video, documentary na filamu mbalimbali za kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwa ni katika jamii na baadhi ya filamu hizo ni pamoja na ‘Zawadi’ na zingine.
  0 0


  0 0


  03Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje, akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kuandaa miongozo ya Ukaguzi wa Migodi kinachoendelea Jijini Mwanza.
  01Wakaguzi wa Migodi kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiwa katika kazi za vikundi kuandaa miongozo (checklist) itakazotumiwa na Wakaguzi wa migodi nchini katika kikao kinachoendelea Jijini Mwanza.
  02 Mmoja wa washiriki wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi akiwasilisha kazi ya vikundi wakati wa kikao cha kuandaa miongozo ya Ukaguzi wa Migodi
  04
  Sehemu ya Wakaguzi wa Migodi waliohudhuria kikao kazi cha kundaa miongozo ya Ukaguzi wa Migodi nchini wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika kikao hicho.

  ……………………………………………………..
  Na Asteria Muhozya, Mwanza
  Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi Mhandisi, Ally Samaje, amesifu zoezi la kuandaa miongozo (checklist) ya Ukaguzi wa Migodi na kueleza kuwa, litaleta matokeo bora kutokana na kwamba shughuli hiyo imekuwa shirikishi.
  Kamishna Samaje ameyasema hayo katika kikao kazi kinachoendelea Jijini Mwanza na kuwashirikisha Wakaguzi wa migodi kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuandaa miongozo itakayokuwa nyenzo muhimu kwa shughuli za ukaguzi wa migodi nchini.
  “ Kimekua ni kikao kizuri, kila mmoja ameshariki kikamilifu jambo ambalo linaashiria kuwa, tutatoka hapa tukiwa na kitu ambacho kitawezesha shughuli za ukaguzi migodini kufanyika kwa utaalamu ,” amesema Samaje.
  Ameongeza kuwa, miongozo hiyo inatarajiwa kuleta mabadiliko katika shughuli za ukaguzi wa migodi, vilevile shughuli nzima itafanyika katika muonekano unaofafana kutokana na kwamba, miongozo hiyo inaandaliwa kwa ajili ya ukaguzi wa migodi yote nchini , ikiwemo na migodi mikubwa na midogo.
  “Tutatoka hapa na miongozo mizuri, nina imani kwamba tutakuwa tofauti na miaka mingine. Tutaongea lugha moja katika shughuli za ukaguzi, lakini zaidi tutajenga kikosi bora kwa ajili ya shughuli za ukaguzi”, amesisitiza Samaje.
  Aidha, ameongeza kuwa, uwepo kwa miongozo hiyo, utawezesha shughuli za ukaguzi migodi kufanyika kitaalamu zaidi na kuongeza kuwa, “suala jingine la kuzingatia ni kwamba uandaaji wa miongozo hii unakwenda unazingatia hali halisi ya mazingira yetu. Huku masuala ya afya,usalama na uhifadhi wa mazingira yakizingatiwa”, ameongeza Mhandisi Samaje.
  Kwa upande wake, mwezeshaji katika kikao hicho, Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi, Laurian Rwebembera , akifafanua masuala kadhaa katika kikao hicho, ameeleza kuwa, miongozo hiyo inatarajiwa kuwa, shirikishi kutokana na kwamba washiriki wote wameshiriki kikamilifu katika zoezi zima la uandaaji miongozo hiyo.
  “Kimekua ni kikao kazi kizuri, kila mmoja ameshiriki kuonesha uzoefu na namna bora ya kufanya ili kufikia lengo. Miongozo hii itakua nyenzo bora za kufanyia kazi, amesema Mhandisi Rwebembera.

  0 0
 • 12/18/14--07:00: SING'OKI NG'O.!
 • Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari kwenye hotel ya Hyatt Regency Dar Es Salaam, The Kilimanjaro  
  .
  Dar es Salaam,
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka,amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia sakata la Akaunti ya Escrow,huku akisema haoni sababu ya yeye kujiuzulu kutokana na kudaiwa kuhusika katika sakata hilo.

   Alisema hawezi kufikia uamuzi wa kujiuzulu kwa kuwa hana kosa kwani hajatajwa mahala popote katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG ),ingawa hakupewa nafasi ya kujitetea na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).


  Alisisitiza fedha alizopewa na Rugemalila ni mchango wa Shule ambapo alisema lengo lake kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu bora.
   Alipoulizwa kuhusu kujiuzulu  alisema hawezi jiuzulu kwani haoni sababu ya yeye kujiuzulu.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtunuku shahada ya heshima ya Uzamivu PhD Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika Jamii, kitaifa na kimataifa pamoja na kufanikisha kuanzishwa kwa Taasisi hiyo kwenye Mahafali ya pili  iliyofanyika leo  jijini Arusha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtunuku shahada ya PhD ya Sayansi Uhandisi na Hesabu Bw. James Philip kwenye Mahafali ya pili ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo jijini Arusha.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Mahafali ya 2 ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyofanyika leo jijini Arusha.
   Sehemu ya wahitimu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela 
   Wahadhiri katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanmzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika maandamano na viongozi wa Taasisi hiyo pamoja na wahitimu, wakati wa Mahafali ya 2 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo  jijini Arusha.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa Shahada ya Uzamili na Uzamifu kwenye Mahafali ya 2 ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyofanyika leo jijini Arusha. 
  Picha na OMR


  0 0

  Waandishi wa Gazeti za Mwananchi Mac Namara Ng'ambi na Bi Ester Mwimbura kufunga pingu za maisha katika kanisa la Anglikana lililopo pande za kihonda  Mkoani Morogoro.
    Paparazi wa Mtandao wa Global Publisher Dustan Shekidele akiwa kazini kwenye haursi hiyo.
              Wakikata kike yao ya harusi

   Bi,Harusi akipeleka zawadi kwa wakwe zake kwa staili ya kupiga magoti


   Kipengele kilichokuwa kikisubiriwa na wengi'Menyu'
             


   Waandishi wa habari wakiongozwa na Ramadhani Libenanga'Kutty Fella'mwenye shati la Mistari  kulisakata Twisti.
   Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Lilian Lucas'Kasenene'akiwasilisha zawadi yake ya waksi
   Mstahiki Meya wa Mji wa Morogoro Mhe Amir Juma Nondo akiwapa mkono wa pongeza maharusi hao.
   Wakiga baada ya kukamilika kwa harusi hiyo
   Mwandishi wa habari Gazeti la Nipashe Ashtoni Balaingwa na mkewe ndio waliobeba jukumu la kuwasimamia maharusi hao kwenye ndoa yao.


  Baada ya kufunga ndoa hiyo mpango mzima ulihamia ndani ya Ukumbi wa Mambo klabu ambapo kulifanyika sherehe ya kufa mtu kwa Mstahiki Meya wa Mji wa Morogoro Amir Juma Nondo kuwaongoza wageni waarikwa wengi wao wakiwa waandishi wa habari na familia zao pamoja na wadau wa tasnia ya habari mkoa wa Morogoro kura,kunywa na kucheza muziki katika sherehe hiyo iliyofanya.

older | 1 | .... | 428 | 429 | (Page 430) | 431 | 432 | .... | 1896 | newer