Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

WAWAKILISHI WA MABARAZA YA WAZEE WA KIMILA WAKIMASAI WAKUTANA NA KINANA

$
0
0
  •  Wazee wa Kimasai wamuhakikishia Kinana uaminifu wao kwa CCM
  • Wataka wafugaji wamilikishwe ardhi
  • Waitaka serikali kuboresha maisha ya wafugaji
  • Wataka wazawa wapewe kipaumbele zaidi
  • Watoa salaam kwa Rais ,wampa pole na wamshukuru kwa kutimiza ahadi yake ya kuwapa mifugo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana( kulia) akisikiliza kwa makini wazee wa kimila wa Kimasai pamoja na Mbunge wa jimbo la Longido Michael Lekule Laizer ambaye alisaidia kutafsiri baadhi ya hoja zilizozungumzwa kwa lugha ya kimasai.
 Philipo Kiloe Laiser Diwani wa kata ya Lubomba Longido akizungumzia Wazee wa Kimasai na kuwaelezea kuwa ni watu wenye hekima busara na wanatambulika kwenye jamii.
Esupat Ngulupa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido akichangia jambo wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mzee wa Kimila wa Kimasai wakifuatilia kwa makini mkutano huo ambao ni hatua zaidi za kutafuta suluhisho la migogoro yao .
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Ole Nangole. akiongea machache kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu kuongea.
 Mbunge wa Longido Michael Lekule Laizer akizungumzia masuala mbali mbali yanayoikabili  wamasai na namna ya kuyatatu ikiwa pamoja na kujengwa kwa viwanda vitakavyodhalisha bidhaa zitokanazo na mifugo.

 Mbunge wa Kiteto Benedicto Ole Nangole akizungumza wakati wa kikao hicho.
 Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka akichangia mada wakati wa mkutano wa Wazee wa Kimila wa Kimasai na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alisema suala zima la ajira liwe kwenye uwiano wa sura ya nchi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wazee wa Kimila wa Kimasai na kuahidi kuyafanyia kazi matatizo yanayowakabili kwa muda mrefu kwa kushirikiana na wabunge wa CCM

 Viongozi wakimila wakimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe la baraza la Wazee wa Kimila mara baada ya kumaliza mkutano.
 Diwani wa Viti Maalum Ngorongoro Tina Timan akizungumza wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alitaka mamlaka husika kubadili sheria kandamizi ili jamii ya Wamasai wafaidike na ardhi yao .
 Mwakilishi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Diwani Viti Maalum Maanda Mgoitiko akichangia mada wakati wa mkutano wa Wawakilishi wa Mabaraza ya Wazee wa Kimila wa Kimasai na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Mzee wa Kimila kutoka Ngorongoro Jerubi Mkati akizungumza wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Lembulung Ole Kosyando kutoka Kiteto akizungumza juu ya migogoro ya ardhi inayowakabili ambapo alisema viongozi wa kiserikali na wa kisiasa wanamiliki ardhi kubwa kinyume na taratibu kiasi cha kuleta migongano mikubwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza kwa makini pamoja na Mbunge wa Longido Ndugu Michael Lekule Laizer (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Ole Nangole.
 Sarah Yohana akizungumzia namna wanawake wa Kiteto wanavyoishi kwa mashaka kutokana na maisha yao kuwa hatarini na kuitaka serikali kufanya juhudi katika kutatua migogoro iliyokithiri Kiteto.
Doroh M. Kipuyo Diwani wa Monduli (Wanawake) akizungumzia jinsi wamasai wanavyoumia kuona Serikali haichukui hatua za haraka kwenye matatizo yanayowakabili.
 Wazee wa Kimila wa Kimasai wakiandika yale muhimu wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika Namanga.
 Leboi Sumuni kutoka Monduli akielezea namna wamasai walivyo na mapenzi na Chama Cha Mapinduzi na kutaka Chama hicho kionyeshe mapenzi kwa wamasai kwa kusaidia kutatua kero zao ambazo zinaonekana kuwa kubwa siku hadi siku.
 Wazee wa Kimila wakifuatilia mkutano.

JUST IN:Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajiuzulu

$
0
0

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Article 12

BENKI YA EXIM KATIKA TUZO ZA MWAJIRI BORA WA MWAKA 2014

$
0
0
 Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya Exim, Bw. Frederick Kanga akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda wakati wa tuzo za mwajiri bora wa Mwaka 2014, tukio lililoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) lililofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya Exim, Bw. Frederick Kanga (wapili kushoto) akionyesha cheti baada ya benki yake kushiriki katika tuzo za mwajiri bora wa Mwaka 2014, zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
 Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakisikiliza kinachojiri katika tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2014, zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

MIKATABA YA KIMATAIFA YAISAIDIA TANZANIA HIFADHI YA JAMII

$
0
0
DSC_0382
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana (kulia) akizungumza katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii unaotarajiwa kumalizika leo jijini Arusha. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi Wetu, Arusha
UTIAJI saini wa mikataba ya kimataifa, inayohusu hifadhi ya jamii kumeiwezesha Tanzania kuwa katika hatua nzuri ya kutekeleza ajenda yake ya kuhakikisha kwamba wananchi wake wanakuwa na haki sawa katika kujipatia maendeleo na ustawi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii mjini hapa.

Alisema mikataba mikubwa ya kimataifa ambayo Bunge la Tanzania limeridhia na iliyoleta mabadiliko makubwa katika sera na sheria nchini ni pamoja na Mkataba wa Kufuta Aina zote za Ubaguzi na Unyanyasaji kwa Wanawake (CEDAW) wa mwaka 1979, Mkataba wa Haki za Watoto (CRC) wa mwaka 1989 na Mkataba wa Afrika wa Haki za Watoto.
DSC_0394
Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster, akiibua hoja kwenye mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii unaomalizika leo jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini, Maria Van Berlekom.

Mikataba mingine ni Mpango wa Maendeleo wa Milenia (MDGs), Azimio la Umoja wa Mataifa Namba 1325 la mwaka 2000 na Azimio Namba 1820 la 2006, ambayo inazungumzia ushiriki na uwezeshaji wa wanawake katika kutanzua migogoro na ujenzi wa taifa.

Alisema kitendo cha kuridhia kwa mikataba na maazimio hayo, kinaonesha ni kwa namna gani serikali ina utashi wa utekelezaji wa maazimio hayo kwa lengo la kuhakikisha watoto na wanawake, wanalindwa dhidi ya vurugu za aina zozote na kuwanyima haki zao za msingi.
Dk.Chana alisema kwa kuzingatia ushiriki kuleta katika maendeleo ya nchi, Tanzania imetayarishwa Dira ya Maendeleo ya 2025 ikiwa na vipengele vyote vya haki vyenye lengo la kuongeza wigo wa ushiriki wa wanawake.

Aidha, ili kuhakikisha makundi maalumu yanalindwa, serikali pia imetengeneza Sera ya Maendeleo ya Watoto ya mwaka 2008, ambayo kwa sasa inapitiwa ili kuingiza mambo mengine yanayohusu haki za mtoto.
DSC_0350
Picha juu na chini baadhi ya washiriki wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii wakiwemo watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania unaoendelea jijini Arusha.

Aidha, ikiwa imejikita kuondoa masuala ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia, serikali imefanya maamuzi mengi yenye manufaa pamoja na kushirikiana na wadau binafsi kuboresha maisha ya watanzania.

Alisema kwamba suala la wanawake na maendeleo, limeingizwa katika mkakati wa taifa wa kupunguza umaskini. Alisema mwaka jana serikali ilitengeneza programu ya taifa inayohusu wadau wengi ya miaka mitatu ya kuondokana na ukatili kwa watoto. Mkutano huo unaozungumzia hifadhi, ulifunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ambaye alisema misingi imara imeshawekwa kusaidia hifadhi ya jamii kuelekea dira ya taifa ya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
DSC_0349

MAONESHO YA KIMATAIFA YA ELIMU KUANZA LEO JIJINI DAR.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel (Wa pili kutoka kulia) akiwaonyesha ramani ya maonyesho ya Kimataifa ya Elimu kwa wadau wa Elimu waliojitokeza kushiriki maonyesho yanayoanza Leo Desemba 17-21, 2014 katika viwanja Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel akielezea maonyesho ya Kimataifa ya Elimu yanayoanza kesho Desemba 17-21, 2014 katika viwanja Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel akiwakaribisha wagei katika ofisi za GEL.

 

Washiriki wa maonyesho ya Kimataifa ya Elimu waombwa kuendelea kujitokeza ili waweze kujitangaza kutokana na maonyesho hayo yanayotarajia kuanza leo Desemba 17-21Akizungumza wakati wa kuwagawia mabanda, Mkurugenzi Wa GEL alisema bado wanazo nafasi ni vyema washiriki wakajitokeza kwa wingi.---Hivi wewe ni mwanafunzi? Je wajua :

·Umuhimu na faida ya mchepuo au kozi unayosoma sasa?
·Fursa ya kozi mbalimbali unazoweka kusoma baada ya kuhitimu elimu yako ya sasa?· Fani zitokanazo na elimu unayosoma au kulenga kwa sasa baada ya kuhitimu.·Fursa mbalimbali zilizopo katika soko la elimu kwa sasa?
Yote hayo pamoja na mengine mengi…  zikiwemo taarifa za kozi mbali mbali kama Udaktari, Biashara, Nishati na Madini hususani Gesi, urubani na zingine nyingi zitapatikana kupitia maonyesho ya elimu ya kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwl. J. K Nyerere SabaSaba Dar  s Salaam.
Fahamu pia watakuwepo wauzaji na wasambazi wa vifaa mbali mbali vya elimu kama madaftari, vitabu, uniforms, laptops na kampuni za huduma ya uchapishaji n.kWasubiri nini? Usikose kufika katika onesho la kipekee linaloonza, leo Jumatano tarehe Desemba 17 mpaka Jumapili Desemba 2, 2014 kuanzia saa 3 asbh – 11 jioni.
Usidanganyike urafiki wa kweli zama hizi ni wa elimu tu, hivyo basi usikose kumpatia rafiki yako juu ya onyesho hili.
Pia kwa taarifa zaidi, tembelea tovuti yet www.tiee.co.tz au piga simu namba 0656 200200

IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA NJOMBE YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA WILAYANI MAKETE

$
0
0
 Baadhi ya msaada uliotolewa
 Mkuu wa wilaya akikabidhiwa msaada huo na afisa uhamiaji mkoa wa Njombe
 akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima
 Mkuu wa wilaya katika picha ya pamoja na watoto yatima
Hivi karibuni Idara ya uhamiaji mkoa wa Njombe iliunga mkono jitihada za mkuu wa wilaya ya makete Josephine Matiro kusaidia vituo vya watoto yatima wilayani humo kwa kutoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 1

Akizungumza wakati akikabidhi msaada wao afisa uhamiaji mkoa wa Njombe Rose Mhagama alisema wameguswa na suala hilo na kuamua kuvisaidia vituo vya watoto yatima Makete vitu mbalimbali, na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia watoto hao

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Hiyo Bi Josephine matiro amewataka wanamakete kubadilika na kuacha dhana kuwa watoto hao watasaidiwa na wafadhili kutoka nje na badala yake nao wawasaidie watoto hao kwa kitu chochote walichojaliwa na Mungu

Vituo vilivyonufaika ni Nyumba ya yatima Bulongwa, Fema Matamba na Kituo kipya cha Kisinga.Na Edwin Moshi wa eddy blog
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro (kushoto) na afisa uhamiaji mkoa wa Njombe Rose Mhagama wakiwa kituoni hapo.
 Afisa uhamiaji mkoa wa Njombe Rose Mhagama akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa kituo cha Nyumba ya yatima Bulongwa
 Mkuu wa wilaya akifurahia jambo
 Watoto yatima wakipewa zawadi na Idara ya uhamiaji mkoa wa Njombe
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa kituo cha Nyumba ya yatima Bulongwa
 

 
 Afisa Uhamiaji mkoa wa Njombe akisema mawili matatu

MEMBE AZINDUA SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu ambaye ndiye kiongozi wa Timu ya Mabalozi wa Tanzania walioanza zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza mlima na kuvutia wageni wengi zaidi nchini.
 Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajab pamoja na timu ya mabalozi anayoiongoza kupanda Mlima Kilimanjaro akinyanyua juu bendera ya taifa pamoja na kushangilia ikiwa ni ishara ya kuuthamini Mlima Kilimanjaro ambo ni chachu muhimu ya utalii nchini. 
 Baadhi ya Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi wakisikiliza kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa kabla ya uzinduzi rasmi wa zoezi lao la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza ili uweze kuvutia wageni wengi zaidi nchini.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akizungumza na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi muda mfupi kabla ya kuzindua safari yao ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza ili kuvutia watalii wengi nchini.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru akitoa neno la ukaribisho kwa Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Ibrahim Mussa.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Ibrahim Mussa akitoa maelezo ya Mlima Kilimanjaro kwa Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania.
Mabalozi wakiwa tayari kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro katika lango la Marangu. Kutoka kushoto ni Dk. Batilda Burian; Daniel Njoolay; Aziz Mlima; Joseph Sokoine na Ramadhani Mwinyi.

BERNARD MEMBE AZINDUA ZOEZI LA MABALOZI WA TANZANIA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KUTANGAZA UTALII

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali ulimwenguni kuhakikisha kuwa wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ikiwa ni njia mojawapo ya kutekeleza diplomasia ya uchumi.

Waziri Membe aliyasema hayo wakati akizindua zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro linalofanywa na mabalozi mbalimbali wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi kwa lengo la kuutangaza Mlima Kilimanjaro ili uweze kuvutia watalii wengi zaidi.

“Bado idadi ya watalii wanaofika nchini kupanda mlima hairidhishi na jitihada kubwa zinahitajika kufanywa na mabalozi kuhakikisha kuwa wanautangaza vema mlima kwa kuwa ni hazina ya pekee tuliyonayo inayopaswa kuwa kitega uchumi kizuri kwa uchumi wan chi yetu” alisema Membe.

Jumla ya mabalozi 14 wanashiriki zoezi hili ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka kwa lengo la kuutangaza Mlima Kilimanjaro. Mabalozi hao ni pamoja na Adadi Rajabu (Zimbabwe); Ramadhani Mwinyi (Umoja wa Mataifa); John Kijazi (India); Batilda Burian (Kenya); Shamim Nyanduga (Msumbiji); Grace Mujuma (Zambia); na Patrick Tsere (Malawi).

Wengine ni pamoja na Mbarouk Mbarouk (Saudi Arabia); Joseph Sokoine (Mkurugenzi Bara la Amerika); Ladislaus Komba (Uganda); Azizi Mlima (Malaysia); Radhia Msuya (Afrika Kusini); Daniel Ole Njoolay (Nigeria) na Charles Sanga (Balozi mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii )

SERIKALI YATAFUTA SOKO LA UTALII UAE - PINDA

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imeamua kutafuta soko la utalii kutoka nchi za Ghuba na Mashariki ya Kati ili kuongeza idadi ya watalii nchini na kukuza pato la Taifa kupitia sekta hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Desemba 17, 2014) wakati akizungmuza an waandishi wa habari mara baada ya kufungua Kongamano la siku mbili la Utalii na Uwekezaji lilionza leo kwenye hoteli ya Le Meridien, jijini Dubai, Falme za Kiarabu.

“Tunao mkakati wa kukuza utalii nchini lakini wengi wameskuwa wakitoka Ulaya na Marekani. Eneo ambalo tumeona tuwekeze kwa nguvu kwa maana ya kuongeza idaidi ya watalii ni hili la nchi za ghuba na Mashariki ya Kati,” alisema.

Waziri Mkuu alisema kimahusiano Tanzania iko karibu na nchi hizi za ghuba lakini pia wanao uwezo wa kifedha wa kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali ya utalii. “Amani ya nchi yetu ni kivutio kingine kikubwa cha uwekezaji, sisi tuko tayari kuwasaidia wafike huko tunakotaka,” alisema.

Alitoa wito kwa makampuni yanayotaka kuwekeza nchini yaangalie fursa zilizopo kwenye ujenzi wa hoteli za kawaida, hoteli za mahema (tented camps) na hoteli zenye kutoa huduma za vyakula (special cuisine restaurant).

Hata hivyo, aliwataka wawekezaji watakaokuja wafanye juhudi ya kushirikiana na Watanzania wazawa ili nao wajione ni sehemu ya uwekezaji huo.

Mapema, akifungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema katika kipindi cha miaka mitano, Tanzania imeweza kuongeza idaidi ya watalii kutoka 714,367 mwaka 2009 hadi kufikia watalii 1,095,884 kwa mwaka 2013.

“Kiwango cha mapato ya watalii hao kiliongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 1.2 hadi kufikia dola za Marekani bilioni 1.8 katika kipindi hicho hicho cha miaka mitano,” alisema na kuongeza kuwa sekta hiyo inaajiri watu zaidi ya 400,000 kuchangia asilimia 17 kwenye pato la Taifa.

Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Lazaro Nyalandu akizungumza na washiriki wa kongamano hilo kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu alisema Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa kuhifadhi rasilmali zake na kuzitumia kwa utalii. “Nchi inayoongoza duniani ni Brazil,” alisema.

Akiainisha fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB), Bi. Devothe Mdachi alisema Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji kupitia sekta ya utalii zikiwemo uendelezaji wa fukwe, michezo ya majini na utalii wa mikutano (conference tourism).

“Kwenye kumbi za mikutano, Tanzania inahitaji kumbi kubwa zenye uwezo wa kuchukua watu kati ya 5,000 na 10,000 na hasa kwenye miji mikubwa kama Arusha, Dar es Salaam na Mwanza,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bibi Julieth Kairuki aliwaeleza washiriki wa kongamano hilo kwamba utalii una fursa kubwa ya uwekezaji kama ilivyo kwenye sekta nyingine za madini na uchumbaji gesi.

“Uwekezaji hivi sasa umepanuka, na soko la utalii nchini Tanzania ni fursa kubwa sana ya kuwekeza. Tunawasihi watu wenye mitaji mikubwa waangalie fursa hiyo na kuichangamkia kama njia mojawapo ya kuwekeza nchini Tanzania,” alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, 17 DESEMBA, 2014.

Mbunge Nassari adaiwa kudakwa na Polisi

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha.

MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kutuhumiwa na tukio la kumteka mtendaji wa kata ya makiba .

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas alisema kuwa mtuhumiwa huyu alikamatwa majira ya saa moja usiku  December 16 katika eneo la Doli lililopo  katika kijiji cha Usa -river  kwenye gari  aina ya land Gruzer  lenye namba za usajili T 753 AQR.

Alisema kuwa    mbunge huyo anatuhumiwa kumteka mtendaji kata aliyefahamika kwa jina la Nemani Ndundu  wa kata ya makiba tarafa ya Mbuguni wilayani Arumeru mkoani Arusha  December 15  majira ya saa mbili asubui katika eneo la maji ya chai  .

Alibainisha kuwa mtendaji huyo alikumbwa na tukio hilo wakati alipokuwakatika pikipiki yake akielekea kwenye kata yake ndipo mbunge huyo alimkamata na kumpiga na kumjeruhi katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimtaka amuonyeshe majina ya wanachama waliopiga kura katika kituo cha  huduma na maendeleo kilichopo katika kata yake   .

Aidha kamanda sabas alisema kuwa  mpaka sasa Joshua Nassari anashikiliwa na polisi na anatarajiwa kufikisha mahakamani  ya wilaya ya Arumeru leo December 17 kujibu tuhuma zinazomkabili.

VIJANA WAFURIKA BANDA LA TBL MAONESHO YA AJIRA KWA VIJANA DAR

$
0
0
 Vijana kutoka vyuo mbalimbali wakiwa katika semina ya jinsi ya kutafuta ajira kwenye taasisi mbalimbali wakati wa Maonesho ya Ajira kwa Vijana, kwenye Ukumbi wa Don Bosco, Upanga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wakijaza kwenye fomu za kutafuta ajira katika Banda la Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakati wa Maonesho ya vijana wa vyuo ya kupata fursa ya ajira katika taasisi mbalimbali  (Careers Fair 2014) katika Ukumbi wa Don Bosco, Upanga, Dar es Salaam. Kushoto ni Lilian Erasmus Ofisa wa Idara ya TBL ya Mauzo na Usambazaji.


 Baadhi ya vijana hao wa vyuo wakijaza fomu za kuomba  ajira katika banda la TBL.
 Meneja wa Uhusiano Mmambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo (kulia0 akizungumza na mmoja wa vijana alifika katika banda la TBL
 Maofisa wasaidisi wa Uhusiano wa TBL, Neema Msechu na Suzan Uiso wakitoa maelezo kwa mmoja wa watu waliotembelea banda la TBL KUHUSU JINSI YA KUSAIDIA AJIRA KWA VIJANA.
 Ofisa Msaidizi wa Uhusiano wa TBL, Neema Msechu (kulia0 akitoa maelezo kwa mmoja wa vijana waliofika katika Banda la TBL
 Wasanii wa muziiki wa kizazi kipya wa kikundi cha Paradise Arts (PAG), wakitumbuiza wakati wa Maonesho ya vijana wa vyuo ya kupata fursa ya ajira katika taasisi mbalimbali katika Ukumbi wa Don Bosco, Upanga, Dar es Salaam
 Waalikwa wakipata vinywaji vilivyokuwa vikitolewa bure katika Banda la TBL
 Vijana wakiwa katika banda la TBL
Sasa ni wakati wa kupata vinywaji bure aina ya Grand Malt na maji aina ya Safari.

AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA

$
0
0
ALIYEKUWA mnenguaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi nchini Aisha Mohammed Mbegu maarufu kama Aisha Madinda amefariki dunia leo nyumbani kwao Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta Luizer Mbutu amethibitisha kuwa Aisha amefariki dunia na alifia nyumbani kwao sababu ambazo bado hazijafahamika. 

Akizunumza kwa masikitiko Mbutu alisema kwamba mwili wa merehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. “Hapa nilipo natetemeka kwa msiba huu sababu marehemu alikuwa mzima na leo  ndiyo ilikuwa aanze mazoezi na bendi ya Twanga Pepeta kwa ajili ya maandalizi ya onyesho la maadhimisho ya miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta” alisema Luizer. 

 Aliongeza kwa kusema: "Hapa natetemeka siamini lakini mwili nimeuona ni kweli Aisha amefariki na amefikishwa hapa hospitalini akiwa tayari amefariki. 

 Naye Mkurugenzi Mtendaji wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka pia amethibitisha habari hizo na hivi sasa yuko njiani kurejea Dar es salaam kwa ndege akitokea Kigoma ambako alikwenda kwa shughuli za uchaguzi wa serikali za mitaa.  Msiba uPo Kigamboni maeneo ya Mikadi Beach .
Aliyekuwa mnengua hodari wa African Stars band "Twanga Pepeta" na Extra Bongo Aisha madinda enzi za uhai wake. 


MSIMU WA SIKUKUU DAR LIVE, WASANII WAELEZEA WALIVYOJIPANGA KUPOROMOSHA BURUDANI KALI

$
0
0
Mfalme wa Muziki wa Taarab nchini, Mzee Yusuf (wa pili kushoto) akielezea kwa wanahabari (hawapo pichani) alivyojipanga kuanguasha shoo ya nguvu katika Tamasha la Wafalme Sikukuu ya Xmas Dar Live. 
Meneja wa Mashauzi Classic, Ismail Rashid 'Suma Ragar' akiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi walivyojipanga kutoa burudani katika msimu wa Xmas Dar Live wakati wa mkutano na wanahabari hao uliofanyika leo kwenye Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza-Afrikasana jijini Dar . Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Benjamin Mwanambuu, Mkurugenzi Bendi ya Extra Bongo, Ali Choki (wa pili kushoto), Mzee Yusuf (wa pili kulia) na Damian Raphael 'MC Dalada Kikombe' kutoka Kundi la Masai Worriors (wa kw nza kulia).
Damian Raphael 'MC Dalada Kikombe' kutoka Kundi la Masai Worriors (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu makamuzi watakayoyafanya Dar Live katika msimu huu wa sikukuu.
KAMPUNI ya Dar Live kwa mara nyingine imetoa ratiba kamili ya burudani katika msimu huu wa kufungia mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015.

Usiku wa Wafalme
Kwa mara nyingine shoo bab’kubwa ambayo ni habari ya mjini kwa sasa ijulikanayo kama Usiku wa Wafalme itagongwa ndani ya ukumbi huo pekee kwa burudani, Desemba 25 ‘Sikukuu ya Krismasi’ ambapo mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ atagonga nyimbo zake zote kali siku hiyo.

Diamond ambaye ni mshindi wa tuzo tatu kutoka Channel O zijulikanazo kama Channel O Africa Music Video Awards (CHOAMVA), siku hiyo atatinga na tuzo zake zote hizo ikiwa ni kuwapa shukrani mashabiki wake wote kwa sapoti waliyoitoa huku akipiga nao picha kwenye ‘red carpet’ na kuongea nao mawili-matatu.

Mashabiki pia watapata nafasi ya kumshuhudia Diamond kwa mara ya kwanza akipiga nyimbo zaidi ya 20 jukwaani pasipo kusimama huku akiwatambulisha madensa wapya sambamba na kupiga pia na nyimbo zake zote ambazo zilishawahi kuachiwa na hazijawahi kuisha mpaka mwisho.
Kwa upande wa muziki wa Pwani, usiku huo utafunikwa pia na Mfalme Mzee Yusuf ambaye siku hiyo ataungana na kundi lake la Jahazi Modern Taarab katika kuwaonjesha mashabiki ngoma zao zote zilizopo katika albamu yao mpya ya Chozi la Mama huku wakifunga mwaka na ngoma ambayo ni habari nyingine kwa sasa ya Mahaba Niue.

Mashabiki watakaofika usiku huo pia watapata bahati ya kushuhudia mshindi wa shindano la kumtafuta mwanaume mwenye mvuto kutoka Gazeti la Ijumaa lijulikanalo kama Ijumaa Sexiest Bachelor ambapo mpaka sasa wamebaki washiriki watatu, Yusuph Mlela, Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba.

Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo watoto wote watakaofika watapata bahati ya kucheza michezo kibao kama vile kubembea, kuteleza, kuogelea na mingine mingi huku kundi la sarakasi la Masai Worriors likiwapagawisha kwa kutoa michezo kibao ya sarakasi , mazingaombwe sambamba na kumwaga zawadi kwa kila mtoto.

KUMEKUCHA TAMSHA LA PASAKA

Wateja wa zantel na Tigo sasa kufurahia huduma za kutuma na kupokea fedha kwa urahisi zaidi

$
0
0

unnamed
Mkurugenzi wa Huduma za Kutuma na Kupokea Fedha wa Tigo Andrew Hodgson (wa pili kulia) akipongezana na Mkurugenzi wa Huduma za Kutuma na Kupokea Fedha wa ZANTEL Hashim Mukudi mara baada ya kutangaza ushirikiano kati ya huduma zao za TigoPesa na EzyPesa mapema leo Zanzibar. Kutoka kushoto ni Meneja wa Biashara wa ZANTEL Zanzibar Mohamed Mussa, Meneja Miradi wa ZANTEL Shinuna Kassim na Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga (kulia).


Kampuni za simu za mkononi za Tigo na ZANTEL zamezindua rasmi huduma za kutumiana pesa miongoni mwa wateja wake Tanzania. Mbali na huduma hiyo ya kutumiana pesa miongoni mwa wateja wa mitandao hiyo, wateja wa EzyPesa na TigoPesa sasa wataweza kutuma na kupokea pesa kwa marafiki na ndugu walio katika mitandao hiyo popote pale nchini.
Kutekelezwa kwa mpango huo kunazifanya Tigo na ZANTEL kuwa viongozi wa huduma kama hiyo Duniani. Haya ni matokeo ya makubaliano yaliyotangazwa mwanzoni mwa mwaka huu na EzyPesa, TigoPesa na Airtel Money.
Jinsi Huduma hiyo inavyofanya kazi:
Wateja wa Zantel: Wateja wa Tigo:
1. Piga *150*02# 1. Piga *150*01#
2. Chagua: Chaguo la 1 (Tuma Pesa) 2. Chagua: Chaguo la 1 (Tuma Pesa)
3. Chagua: Chaguo la 2 (Tuma TigoPesa) 3. Chagua: Chaguo la 5 (Tuma EzyPesa)
3.1. Ingiza Namba ya TigoPesa 3.1. Ingiza Namba ya TigoPesa
3.2. Ingiza Kiwango 3.2. Ingiza Kiwango
3.3. Ingiza Neno la Siri 3.3. Ingiza Neno la Siri
3.4. Subiri Uthibitisho wa Ujumbe Mfupi wa Maneno 3.4. Subiri Uthibitisho wa Ujumbe Mfupi wa Maneno
Hakuna gharama za ziada mteja anapotuma pesa kwa mtandao mwingine isipokuwa gharama zinakuwa sawa na zile anapotuma kwenye mtandao wake. Wateja wanaopokea pesa kutoka mtandao mwingine wanaweza kutoa pesa kwa wakala wa mtandao wao na hapatakuwa tena na ulazima wa mteja kutafuta wakala wa mtandao wa mtu aliyemtumia pesa.
Akizungumza kutoka Zanzibar, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Andrew Hodgson alisema: “Tunafuraha kupanua wigo kwa wateja wetu kwa ubia na Zantel. Hatua hii ni muhimu hasa kwa Zanzibar ambapo fursa ya kukua kwa huduma za fedha kwa mitandao ya simu bado ni kubwa.”
Anasema kama ilivyo kwa huduma nyingine za simu kama milio ya sauti na ujumbe mfupi wa maneno, kuna fursa kubwa ya kuimarisha huduma kwa wateja kwa kushirikiana badala ya kushindana baina ya wadau katika sekta ya mawasiliano kwa kupanua huduma za kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao Tanzania.
Anafafanua zaidi kuwa kwa kufanya kazi na wadau wengine, kunawawezesha kupanua wigo wa wateja na hivyo kwa pamoja kutoa huduma ambazo ni bora zaidi, salama, na za haraka kwa wateja wa pande zote.
“Ubia ambao tumeingia leo sio tu utaleta karibu kampuni zetu, bali muhimu zaidi ni ukaribu wa wateja wetu kwa kuwapatia huduma za fedha za kielektroniki bora zaidi ambazo hawakuweza kuzipata hapo awali,” alisema Hodgson.
Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, Mohamed Mussa, anasema Zantel inaendelea kutimiza ahadi ya kuwarahisishia huduma za fedha wateja wake kwa kufanya kazi pamoja na Tigopesa.
“Kwa kufanya hivi tunapanua wigo kwa wateja wetu, huduma hii inawawezesha zaidi wateja kutuma na kupokea fedha kwa urahisi zaidi,” anasema.
Anafafanua zaidi kuwa kwa huduma hii itasaidia kuimarisha huduma za fedha kati ya visiwa vya Zanzibar na Tanzania Bara.
“Zantel iko katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa ushiriki wa wananchi wa Zanzibar katika sekta muhimu ya fedha unaimarika na kukua. Tumehakikisha kuwa mtandao wa mawakala wetu na watoa huduma wengine wako tayari kuwahudumia wateja wetu,” anasema Bw. Mussa.


KIWANDA CHA KONYAGI CHAZINDUA KINYWAJI CHA ZANZI CHENYE LADHA ZA CHOCOLATE NA KAHAWA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi Tanzania (TDL), David Mgwassa (katikati), akiwa Meneja Masoko wa kiwanda hicho, Joseph Chibehe (kushoto) na Meneja Bidhaa wa TDL, Warda Kimaro wakionesha vinywaji vipya aina ya Zanzi Chocolate  (ladha ya Chokoleti) na Zanzi Cappuccino (ladha ya kahawa) wakati wa uzinduzi wa  wa vinywaji hivyo uliofanyika katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam.
 Mgwassa akielezea ubora wa vinywaji hivyo.
 Meneja Masoko wa TDL, Joseph Chibehe akitaja bei ya kuuzia vinywaji hivyo, ambapo chupa ndogo yenye ujazo wa ml 200 itauzwa kwa sh. 6,000 na chupa kubwa yenye ujazo wa ml 750 itauzwa kwa sh. 20, 000
Meneja wa Bidhaa wa TDL, Warda Kimaro akielezea jinsi vinywaji hivyo vinavyosambazwa kwenye maduka makubwa  ya Super Market nchini.

TATIZO LA WAMACHINGA NA OMBA OMBA MAENEO YASIYORUHUSIWA DAR KUTAFUTIWA DAWA .

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akifuangua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando.
==============   ========  =========
Aron Msigwa –MAELEZO.
 
Jiji la Dar es salaam linaangalia upya utaratibu wa kuwaondoa ombaomba na wafanyabiashara ndogondogo(wamachinga)  katika maeneo yasiyoruhusiwa katika jiji la Dar es salaam kufuatia sheria na hatuazinazochukuliwa ikiwemo kuwarudisha ombaomba hao katika mikoa wanayotoka kutokuzaa matunda na kuwa endelevu kufuatia wengi wao kurudi katika maeneo ya awali kila wanapoondolewa.
 
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki wakati akifungua kikao cha wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) kilichofanyika leo jijini Dar es salaam kujadili masuala mbalimbali ya mendeleo katika jiji la Dar es salaam.
 
Amesema kuwa kuendelea  kuwepo kwa wafanyabiashara hao katika maeneo yasiyo rasmi ni moja ya changamoto inayolikabili jiji la Dar es salaam kutokana na biashara wanazozifanya kuchangia kuzuia maeneo ya barabara ya waenda kwa miguu, kusababisha uchafuzi wa mazingira,kusabisha msongamano wa magari kwa baadhi yao kuweka bidhaa  barabarani.
 
Amesema kutokana na hali hiyo baadhi ya wafanyabiashara walio na biashara rasmi  ambao hulipa kodi za Serikali wamekuwa wakilamikia hali  ya ukwepaji wa kodi inayofanywa na wafanyabiashara hao.
 
Bw. Sadiki amesema mpango wa mkoa wa sasa ni kuendelea kuwatumia wafanyabiashara hao kama  fursa ya mtaji wa rasilimali watu ambayo itatumika kama chanzo cha mapato katika kuleta maendeleo ya mkoa.
 
Amesema watendaji na viongozi wa halmashauri za mkoa wa Dar es salaam wanalojukumu la kuweka mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao na kuwatumia katika shughuli za uzalishaji kwa utaratibu mzuri utakaowekwa ili waendelee kunufaika na shughuli wanazofanya.
 
Akizungumzia kuhusu uboreshaji wa huduma za jamii zikiwemo za Maji, Elimu na Afya katika jiji la Dar es salaam  amesema kuwa Serikali inaendelea kuzijengea uwezo shule kwa kuongeza majengo ya madarasa, maabara na kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaofaulu elimu ya msingi wanapata fursa ya kuendelea na masomo ya Sekondari.
 
Kuhusu huduma za afya amesema kuwa mkoa unaendelea na maandalizi ya ujenzi wa jengo la ghorofa nane, eneo la Magomeni katika manispaa ya Ilala litakalotumika kutolea huduma ya Afya ya Mama na Mtoto na kuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 500.
 
  Sasa tuko kwenye maandalizi ya ujenzi wa jengo maalum la kutolea huduma ya Afya ya Mama na Mtoto katika jiji la Dar es salaam litakalogharimu zaidi ya shilingi bilioni ishirini na moja, tayari benki ya Tanzania Investment Bank imeshakubali kutoa mkopo kwa ajili ya jengo hilo” Amesisitiza.
 
Aidha, katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ametoa ufafanuzi kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchi nzima  Desemba 14 mwaka huu na kueleza kuwa baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam ambayo uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo vurugu, uchaguzi huo utarudiwa ndani ya siku saba.
 
Ameeleza kuwa katika mkoa wa Dar es salaam uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika kwenye mitaa 561 lakini kutokana na changamoto mbalimbali ulifanyika kwenye mitaa 491 na kuahirishwa kwenye kata 70.
 
Amelitaka jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa linaimarisha ulinzi na usalama wakati wa marudio ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika ndani ya siku 7 katika mitaa yote ambayo uchaguzi uliahirishwa .

NASSARI AACHIWA HURU KWA DHAMANA NA MAHAKAMA YA MWANZO YA MAJI YA CHAI

$
0
0
Na Woinde shizza,Arusha

Hakimu David Mwita wa Mahakama ya mwanzo ya maji ya chai ameahirisha hadi december 24, shauri la kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariki Joshua Nassari (CHADEMA), kwa tuhuma za kuharibu mali ya uma kwa kuichoma yenye dhamani ya shilingi laki mbili (bendera ya CCM),pamoja na kumteka mtu na kumtishia kwa bunduki tukio ambalo anatuhumiwa kufanya december 15 mwaka huu

mahakama hiyo imemuachia mbunge huyo mara baada ya kutimiza mashariti ya dhamana, ambapo shariti la kwanza ni kuwa na wadhamini wa tatu ambao wanamali zisizo hamishika zenye dhamani ya shilingi milioni moja na nusu kila mmoja.

Katika kesi hiyo inayomkabili mbunge huyo ambayo mlalamikaji wa kesi hiyo akiwa ni mtu binafsi hakimu wa kesi hiyo mara baada ya kusikiliza mashitaka hayo alichukuwa nafasi ya kuhairisha kesi hiyo adi december 24 ambapo kesi hiyo itatajwa tena kwa mara nyingine.

Akiongea mara baada ya kuairisha kesi hiyo wakili wa mbunge huyo wa Arumeru mashariki James Ole milya alisema kuwa amesikitishwa sana na tukio la mahakama hiyo kumpa mashariti makubwa mteja wake kwani kesi yake ilikuwa haitaji mashariti makubwa hivyo .

Aidha alisema kuwa mbali na kupewa mashariti hayo angependa kesi hiyo ipelekwe katika mahakama ya wilaya ili yeye kama wakili wa mbunge huyo aweze kumtetea kwani katika mahakama ya mwanzo hairuhuu kuweka wakili.

“unajua kwakweli mbali na hivyo pamoja kuwa sio jamuhuri imemshitaki mh Nasari bali ni mtu binafsi lakini nasikitika sana kwa mashariti ambayo wameweka ,kwani ata bila ao wathamini watatu wakiwa na kitu kisichoamishikika chenye dhamani ya shilingi milioni moja na nusu,huyu ni mbunge ambapo angeweza kujidhamini ata yeye mwenyewe kwani mtu huyu ni kioo cha jamii na awezi kukimbia sehemu yoyote kwanini wasinge mpa mdhamana mapema mpaka apate wadhamini hawa na mashariti haya”alisema Milya

Aidha alisema kuwa anashangazwa sana na maamuzi haya kwani kuna mtu ambaye amemzalilisha mwanamke ambaye alikuwepo mahakamani hapo na akamvua mwanamke huyo nguo lakini yeye alishangazwa sana kwa mtuhumiwa wa kosa ilo la uzalilishaji yeye kupewa mashariti mapesi ya kuwa na mdhamini mmoja na kutoa laki tano laikini mbunge yeye amepewa mashariti ya kuwa na wadhamini watatu ambao wanamalizi zenye dhamani ya shilingi milioni moja na nusu uku akitilia shaka kuwa katika kesi hii wanahisi kuna chama cha siasa kinachangia kuongeza nguvu.

WASANII WAKONGWE WAPANIA KUFANYA KUFURU KATIKA UZINDUZI WA KAONE SANAA GROUP NDANI YA DAR LIVE

$
0
0
Mastaa waliokuwa wakiunda kundi la zamani la Kaole wakiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi walivyopania kufanya kweli kwenye uzinduzi wa kundi lao jipya la Kaone, Boxing Day ndani ya Dar Live.
Muhogo Mchungu akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni msanii Thea. 
Wasanii hao wakongwe wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo na wanahabari. Mkutano huo umefanyika leo katika Hoteli ya The Atriums iliyopo Afrikasana, Dar.
Msanii Thea (kulia) akielezea jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).
Msanii Kingwendu akitoa burudani wakati akiongea na mwanahabari wa TBC.

ZIKIWA zimesalia siku chache kuelekea ule Usiku wa Wasanii Wakongwe Desemba 26 ‘Boxing Day’ ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar, mastaa kibao waliokuwa wakiunda kundi la zamani la Kaole watazindua rasmi kundi jipya linalojulikana kama Kaone.

Usiku huo utakaokuwa wa aina yake, utawakutanisha wale wakali wote kutoka Kaole kama vile Swebe, Davina, Koletha, Zawadi, Nyamayao, Kingwendu, Muhogo Mchungu, Kibakuli na wengine kibao ambao kwa mara ya kwanza watajulikana kama Kaone na kuzindua tamthiliya yao mpya ya Kipusa itakayoanza kuruka hewani Januari 4, 2015 ndani ya Runinga ya TV1. Usiku huo pia utapambwa na wasanii wa Bongo Fleva, Baby Madaha pamoja na Isabela Mpanda ‘Bela’ ambapo watatoa burudani mwanzo mwisho.

Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo Kundi la Masai Worriors litawapagawisha watoto kwa kuwapa chemsha bongo, mazingaombwe sambamba na kutoa zawadi kibao huku watoto wengine wakipata nafasi ya kubembea, kuteleza na kuogelea.

NAIBU MKURUGENZI MKUU WA UNESCO AWASILI JIJINI ARUSHA KUSHIRIKI MAHAFALI TAASISI YA MANDELA

$
0
0
DSC_0499
Ofisa mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack (kushoto) akijadiliana jambo ndani chumba cha mapumziko cha wageni mashuhuri na Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues pamoja na Afisa mipango kitaifa, kitengo cha Sayansi UNESCO,Tanzania, Gabriela Lucas kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida.
DSC_0516
Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues akimlaki Naibu Mkurugenzi Mkuu waShirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi naUtamaduni (UNESCO), Getachew Engida wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili kuhudhuria mahafali ya pili ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha yanayofanyika kesho. Kulia ni Ofisa mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack na wa pili Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
DSC_0517
Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akimlaki kwa furaha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida (kushoto) aliyewasili jioni hii jijini Arusha na shirika la ndege la Ethiopia. Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
DSC_0518
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida akisalimiana na Ofisa mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
DSC_0524
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida akiwa na mwenyeji wake Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues mara baada ya kuwasili wakielekea kwenye chumba cha mapumziko cha wageni mashuhuri.
DSC_0526
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images