Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 426 | 427 | (Page 428) | 429 | 430 | .... | 1897 | newer

  0 0


  National Arts Council BASATA
   

  Yah: Salaam za Rambirambi
  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii nguli wa tasnia ya muziki wa Dansi nchini Shem Ibrahim Kalenga

  “ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Shem Ibrahim Kalenga ambaye mchango wake katika muziki wa Dansi ni mkubwa mno na  unahitajika sana, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha tunawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.

  Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

   Imetolewa na
  Godfrey Mngereza
  Kaimu Katibu Mtendaji
  Baraza la Sanaa la taifa.


  0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya  Ney wa Mitego anatarajiwa kulipamba Tamasha la amani linalotarajiwa kufanyika mapema jumamosi hii desemba 20 katika viwanja vya Sheik Amri Abeid lililoko mkoani Arusha.
   
   Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa Tamasha hilo Bertha Ismail kupitia kampuni ya Bimo media alisema kuwa Msanii huyo anaetamba na wimbo wake wa “Nakula Ujana” anatarajiwa kutua mkoani Arusha siku ya Alhamisi ya desemba 18 na timu yake nzima ambapo atafanya matangazo katika sehemu mbalimbali za jiji la Arusha kuhamasisha watu kuhudhuria tamasha hilo.
   
   “Mbali na wasanii wengine wa Arusha, Msanii mkubwa ambae anatarajiwa kulipamba tamasha hilo ni Ney wa Mitego ambae tunaamini kwa Arusha atavuta watu wengi kuhudhuria tamasha katika uwanja wa Sheik amri abeid kuja kusikiliza ujumbe wa Amani ambapo utatolewa na Mgeni Rasmi”alisema Bertha.
   
   Alisema kuwa Tamasha hilo litakalohudhuriwa na viongozi mbali wa serikali, Tasisi pamoja vyama vya siasa, lengo kubwa ni kuwaunganisha vijana na kupata ujumbe wa amani hasa katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwakani, ujumbe utakaotolewa na msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi.
   
   “Tunapoelekea uchaguzi tunajua mara nyingi sisi vijana ndio tunaotumika zaidi, hivyo lengo kuu la Tamasha hili ni kuwaunganisha vijana katika umoja  ili wasigawanywe kwa misingi ya dini na siasa hali itakayojenga chuki na kufanyiana fujo, hivyo wasifanye hivyo bali kila mmoja atumikie chama chake au dini yake kwa amani bila vurugu”.
   
   Bertha alisema kuwa Tamasha hilo lililodhaminiwa na kiwanda cha soda cha pepsi, Kituo cha redio five na Sunrise Arusha, Mbali na Burudani ya Ney wa mitego pia kutakuwa na burudani zingine kama Ngoma za asili, sarakasi, maonyesho ya warembo wa mitindo pia vijana chipukizi wa Arusha wataimba nyimbo mbali mbali sambamba na Watangazaji wa redio za Arusha kukimbia riadha hivyo kutumia fursa hiyo kuwaalika wadhamini kutumia nafasi hiyo kutangaza bidhaa zao kwa kushiriki tamasha hilo.

  0 0

  Balozi wa heshima Mhe. Ahmed Issa (watatu toka kushoto) akibadilishana mawili matatu na mgeni rasmi wa sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara Mhe. Dr. Saidi Mohamed Mtanda (wapili toka kushoto), mbunge wa Afrika Mashariki na mwenyekiti kamati ya kudumu ya huduma za jamii katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Mtanda pia ni Mbunge wa jimbo la Mchinga Mkoani Lindi. Kulia ni Cherry Mke wa Mhe. Ahmed Issa.
  Balozi wa Heshima Mhe. Ahmed Issa akitoa salamu za miaka 53 ya Uhuru na baadae kumkaribisha mgeni rasmi kuhutubia wanaCalifornia katika sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyikia Oakland, California siku ya Jumamosi Desemba 13, 2014.
  Mgeni Rasmi Mhe. Dr. Saidi Mohamed Mtanda akihutubia Watanzania Oakland, California siku ya Jumamosi Desemba 13, 2014 katika sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizosherehekewa na Watanzania na amarafiki zao kwenye jimbo hilo la California.
  Vikundi mbalimbali vya ngoma za asili vikinogesha sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara California. 
  Watanzania na marafiki zao wakifuatilia sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 13, 2014 Oakland, California nchini Marekani.
  Watatnzania wa California wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mhe. Dr. Saidi Mohamed Mtanda.
  Kwa picha zaidi bofya HAPA

  0 0

  DSC_0118
  Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dr. Servacius Likwelile mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya AICC jijini Arusha leo.
  DSC_0120
  Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi , akisalimiana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa hifadhi ya jamii.
  DSC_0127
  Mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la watoto duniani (UNICEF), Jama Gulaid.
  DSC_0132
  Mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi (katikati) akiwa na Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum pamoja na mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano.

  DSC_0312
  Picha juu na chini ni mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi, akifungua mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii ulioanza leo jijini Arusha.
  DSC_0328
  Kwa picha zaidi ingia humu
  DSC_0005
  Wageni mbalimbali wanaoshiriki mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ulioanza leo katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC) wakifanya usajili kabla ya kuanza kwa mkutano huo. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

  Na Mwandishi wetu
  MAKAMU wa pili wa rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, amesema mpango wa serikali ya Tanzania wa hifadhi ya jamii ndio msingi wa sera ya kuondoa umaskini miongoni mwa watu wake ili kulifanya taifa kuwa la kipato cha kati ifikapo 2025.

  Kauli hiyo imetolewa leo wakati akifungua mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii.
  Katika Mkutano huo wa siku tatu unafanyika Katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC) serikali imefanya maandalizi kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa kama UNICEF, ILO, UNAIDS na taasisi ya utafiti wa sera za kiuchumi yenye makao makuu nchini Afrika Kusini (EPRI).

  Imeelezwa kuwa mkutamo huo umelenga kuchota maarifa mema kutoka Afrika Kusini ya namna ya kutengeneza sera za kuhudumia makundi maalumu ya wanawake, watoto, wazee, wasiojiweza na vijana ili kuboresha maisha yao, ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa serikali wa kuinua kiwango cha maisha miongoni mwa wananchi wake.
  DSC_0022
  Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma (kulia) akiwasili kushiriki mkutano huo akiwa ameambatana na Afisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Tanzania, Bw. Magnus Minja (kulia) pamoja na Luis Frota kutoka ILO Afrika Kusini.

  Balozi Seif Ali Iddi, alisema kwa kuzingatia nia ya serikali ya kuwa taifa lenye kipato cha kati mwaka 2025 serikali inaona haja ya kuangalia sera ili iweze kutoa haki kwa makundi yote kuelekea ustawi wa jamii ifikapo mwaka huo.

  “Serikali imechukua hifadhi ya jamii kama mkakati wa kufikia dira ya ukuaji na maendeleo nchini. Kongamano hili limekusudia kuhakikisha kwamba muono unatengeneza hatua stahiki zinazotekelezeka kitaifa kukabiliana na changamoto za umaskini hivyo kuhakikisha ukuaji wa uchumi unakuwa endelevu na wenye maana kwa wananchi” alisema.

  Alisema ili kufikia lengo hilo la uchumi endelevu, serikali inataka kuhakikisha wananchi wake wakiwemo wale maskini na wasiojiweza wanawezeshwa ili kutambua haki zao na kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye nguvu na linalotoa haki sawa kwa wote. Aidha kuwa taifa linaloangalia mahitaji ya watoto wake kama lishe, afya na elimu ili kuwasaidia kukua kwa furaha, kuwa wazalishaji na kukwepa mtego wa umaskini unazinga kizazi kwa kizazi.
  DSC_0026
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kulia) akimwongoza Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma kuelekea kwenye chumba maalum cha wageni mashuhuri kabla ya kuanza kwa mkutano. Katikati ni Afisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Tanzania, Bw. Magnus Minja.

  Balozi Iddi alisema kwamba amefurahi kuona kwamba ajenda za mkutano pia zimegusia kuzungumzia uimarishaji wa utendaji wa pamoja kati ya mipango ya hifadhi ya jamii kama TASAF, Mfuko wa afya ya jamii (CHF) na huduma za jamii zinazotolewa na wizara husika kama wizara ya elimu, afya, maji nakadhalika. Hata hivyo aliwataka washiriki kuangalia ukusanyaji wa takwimu kuhusu masuala ya hifadhji ya jamii kwani kwa hali ilivyo sasa ukusanyaji huo si mzuri na unazuia maendeleo na uimarishaji wa huduma za jamii.

  Alisema ipo haja ya kuboresha mazingira ya utawala ili kuwezesha kuimarisha hifadhi kwa wale waliokwishaipata, kubadili sheria ili kuwaingiza na wale ambao hawajapata huduma za hifadhi ya jamii. Aliwataka washiriki kuangalia kwa makini changamoto zinazoikumba Afrika na Tanzania katika masuala ya hifadhi na kutolea majibu.
  DSC_0030
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani (ILO) na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma.

  Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni umaskini uliotapakaa ambao unasababisha watu kushindwa kupeleka michango katika hifadhi, misingi ya ukataji kodi ambayo huleta mushkeri kwa fedha za hifadhi, kuwepo kwa kundi kubwa lisilo katika sekta rasmi ya ajira na hivyo kupunguza idadi ya wachangaji katika prgramu zinazohitaji michango mfululizo na mabadiliko ya tabia nchi yanayotishia kuyumba kwa kilimo na ufugaji ambao ndio msingi wa mapato kwa wananchi wengi.

  Alisema pia mabadiliko ya tabia nchi yanasababisha milipuko ya magonjwa mbalimbali kama Malaria na magonjwa mengine mapya kama Ebola na Dengue. Changamoto nyingine ni kuwepo na gharama kubwa za utawala hasa katika siku za mwanzo za uanzishwaji wa mifuko ya hifadhi.

  Mkutano huo wenye washiriki zaidi ya 150 una watu wa kariba mbalimbali wakiwemo watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania.
  DSC_0033
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi.

  Mkutano huo unatarajiwa kutoa mwelekeo wa namna ambavyo Tanzania inaweza kuanzisha mfumo wa hifadhi kwa ajili ya watu maskini na wale wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kupata huduma za afya, elimu na kipato. Naye Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma, amesema Umoja wa Mataifa umefurahishwa na kuwapo kwa kongamano hilo kwani suala la hifadhi ni msingi wa maendeleo katika uchumi wowote endelevu.

  Alisema kuwapo kwa Hifadhi ya jamii inayoeleweka na yenye msingi imara husaidia wananchi kukabiliana na mabadiliko yoyote yale ya kiuchumi katika taifa lao. Alisema shirika hilo katika miaka yote 95 ya uwapo wake inapigania hifadi ya jamii kama njia salama ambayo inahakikisha ukuaji wa jamii unaozingatia uwapo wa jamii inayozingatia ukuaji wa uchumi wenye haki kwa kila mmoja.
  DSC_0065
  Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (kushoto) akiwasili kwenye viwanja vya AICC jijini Arusha kushiriki mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha huku akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dr. Servacius Likwelile (katikati) pamoja na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Jama Gulaid.

  Pamoja na mafanikio ya dunia katika masuala ya afya na elimu, Mwakilishi huyo ameelezea changamoto kubwa inayokabili Tanzania ambayo ni vijana wengi kuingia katika soko la ajira ambalo ni finyu. Mwakilishi huyo amesema kwamba kuanzia mwaka ujao hadi 2030 nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la sahara wanatakiwa kutengeneza nafasi milioni 5 za kazi kila mwaka ili kuendana na ukuaji wa soko la wasaka ajira.

  Alisema kutokana na ukweli huo hatua ya sasa ya Tanzania kutaka kuwa na msingi imara ya hifadhi ya jamii ni muhimu sana ili kukabiliana na mabadiliko yanayokuja katika afya, elimu na ajira. Wakati huo huo Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi mkazi wa UNDP Alvaro Rodriguez amesema hifadhi ya jamii ni kitu muhimu kinachofanya watengeneza sera kukaa pamoja kuona namna nzuri ya kufanikisha masuala hayo.
  DSC_0086
  Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (katikati) akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) pamoja na Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana wakielekea kumpokea mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi.

  Alisema matukio mbalimbali yanayoharibu ustawi wa jamii kama kuporomoka kwa uchumi duniani, mabadiliko kwenye tabianchi kumefanya kuwepo na haja ya kuhakikisha kwamba kuna misingi imara ya kutoa hifadhi kwa wananchi na kuboresha maisha yao. Akizungumza katika mkutano huo kabla ya Makamu wa rais kuhutubia, Alvaro alisema kuna changamoto kubwa zinazokabili dunia.

  Alipongeza serikali ya Tanzania kwa kuona haja ya kushirikiana na wadau wengine kuona namna bora ya kukabiliana na changamoto za maendeleo katika lengo la kuhakikisha kunauwezeshaji wenye lengo la kuwezesha ustawi wa jamii. Alisema mada zitakazojadiliwa zitawezesha mwishoni mwa mkutano kuwapo na maazimio yenye kuwezesha kutengenezwa kwa mising bora ya hifadhi ya jamii ili kuwezesha maono ya maendeleo kufikiwa.

  Mratibu huyo pia alielezea kuridhishwa kwake na mafanikio yanayopatikana nchini Tanzania kupitia TASAF ya kukabiliana na umaskini uliokithiri na kutoa nafasi ya maskini kuwa na uwezo wa kusonga mbele katika maendeleo ili kufikia maono ya taifa ya maendeleo endelevu yanayojali watu wote 2025 wakati taifa litakapokuwa la kipato cha kati.


  0 0

  Mwongozaji wa mjadala huo, Suzan Charles (mbele aliyesimama) kutoka Kituo cha Usuluhishi (CRC) kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) akizungumza katika mjadala huo na wanafunzi. Mwongozaji wa mjadala huo, Suzan Charles (mbele aliyesimama) kutoka Kituo cha Usuluhishi (CRC) kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) akizungumza katika mjadala huo na wanafunzi.Mwongozaji wa mjadala huo, Suzan Charles (mbele aliyesimama) kutoka Kituo cha Usuluhishi (CRC) kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) akizungumza katika mjadala huo na wanafunzi. Mwongozaji wa mjadala huo, Suzan Charles (mbele aliyesimama) kutoka Kituo cha Usuluhishi (CRC) kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) akizungumza katika mjadala huo na wanafunzi. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nachitulo akizungumza na mwandishi wa habari hizi. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nachitulo akizungumza na mwandishi wa habari hiziBaadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Nachitulo walioshiriki katika mjadala wakiwa katika picha ya pamoja. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Nachitulo walioshiriki katika mjadala wakiwa katika picha ya pamoja.

   BAADHI ya wanafunzi wa kike katika Shule ya Msingi Nachitulo Wilayani Newala wamewataka wazazi kuacha tabia ya kuwabagua watoto wa kike kielimu kwani kufanya hivyo ni kumnyanyasa mtoto wa kike kijinsia. Wanafunzi hao walitoa kilio hicho hivi karibuni katika mjadala uliofanyika kwenye shule hiyo uliokuwa ukijadili vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na uelewa wa vitendo hivyo kwa watoto ili kuweza kukabiliana navyo. 

  Mwanafunzi Sofia Damian wa darasa la tano 'B' Shule ya Msingi Nachitulo akizungumza katika mjadala huo aliwaomba wazazi kuacha tabia ya kufanya ubaguzi wa kumjali zaidi mtoto wa kiume kielimu na kumsahau yule wa kike kwani kitendo hicho ni ukatili wa kijinsia. Alisema baadhi ya wazazi eneo hilo wamekuwa wakibagua watoto kwa kumjali zaidi wa kiume na kuwaacha wa kike ni ubaguzi mbaya. "...Kitendo cha kufanya ubaguzi wa elimu katika familia kwa mtoto wa kike na kiume ni unyanyasaji wa kijinsia…yaani kumpeleka mtoto wa kiume shuleni na kumuacha wa kike nyumbaji hilo ni unyanyasaji," alisema Sofia Damian. 

  Kwa upande wake Sharifa Bakari toka darasa la sita 'A' katika shule hiyo alisema ubaguzi wa mtoto wa kike umekua ukianzia ngazi za familia kwa watoto wa kike kuwa na kazi nyingi nyumbani zaidi ya mtoto wa kiume kitendo ambacho kinatakiwa kipigwe vita. 

  Mwanafunzi wa darasa la sita 'A' katika shule hiyo, Mwanahamisi Said aliwataka baadhi ya wazazi na walezi kuacha utaratibu wa kumlazimisha mtoto wa kike kuolewa kwa taamaa ya mali (ndoa za utotoni), kwani kitendo hicho pia ni ukatili wa kijinsia. "..Hata kitendo cha mtu mzima kumlazimisha mwanafunzi kufanya naye mapenzi ni ukatili wa kijinsia," alisema Mwanahamisi. 

  Akizungumza mwongozaji wa mjadala huo, Suzan Charles kutoka Kituo cha Usuluhishi (CRC) kilichopo chini ya Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) aliainisha matukio ya ukatili wa kijinsia yanayowapata watoto na kutoa elimu ya kukabiliana nayo kwao, ikiwa ni pamoja na wao kutoa taarifa mapema sehemu husika endapo watatokewa na hali kama hizo.

   Akizungumza awali kabla ya mjadala huo, Mwalimu wa Malezi wa Shule ya Msingi Nachitulo, Blandina Luwongo alisema shule hiyo imefanikiwa kupiga vita vitendo vyovyote vya ukatili wa kijinsia kwa watoto kwa kutumia mradi wa elimisha rika jambo ambalo limeondoa kabisa matukio ya mimba kwa wanafunzi. 

  "...Katika shule yetu hata matukio ya wanafunzi kutiwa mimba hayapo kwa sasa baada ya elimu ya uelimishaji rika kutolewa kwa jamii, wanafunzi na walimu eneo hili. Hata hivyo anabainisha ili kutokomeza kabisa matukio ya unyanyasaji elimu ya kukabiliana na vitendo hivi kwa jamii haina budi kutolewa kiufasaha na kuacha kujikita kwenye adhabu kwa wakosaji." Anasema Bi. Luwongo. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  Frank Mvungi- maelezo.

  Serikali imesema uchaguzi wa  Serikali za Mitaa uliofanyika jana Kote Nchini umefanikiwa kwa Zaidi ya asilimia 98% katika Mikoa yote .

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu mafanikio ya uchaguzi huo.

  Akifafanua Mh. Ghasia amesema kwa kiwango kikubwa wananchi walijitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi wao katika ngazi ya Mitaa,Vijiji, na Vitongoji. Akizungumzia mafanikio ya Uchaguzi huo  Mh. Ghasia alitaja Mikoa ambayo uchaguzi umefanyika katika Halmashauri na Kata zote kuwa ni    Arusha,Mbeya,Kagera,Njombe,Singida,Lindi,Ruvuma,Katavi na Geita.

  Mikoa Mingine iliyofanya vizuri katika uchaguzi huo ni Iringa,Dodoma,Mtawara ambapo Mh. Ghasia aliwapongeza Viongozi na wataendaji wote wa Mikoa na Halmashauri hizo pamoja na wananchi kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya hadi kufanikisha uchaguzi huo.

  Akitoa ufafanuzi Zaidi kuhusu maboresho yaliyofanywa na Serikali katika uchaguzi huo Mh. Ghasia amesema kuwa mojawapo ni kuwepo kwa utaratibu wa kupiga kura kwa kutumia karatasi maalum zilizochapishwa kitu ambacho katika uchaguzi uliopita hakikuwepo.

  Akizungumzia Mikoa ambayo baadhi ya Halmashauri zimeahirisha uchaguzi ama Halmashauri yote au sehemu ya Kata zake kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuchelewa kufika kwa vifaa vya kupigia kura Mh.Ghasia aliitaja kuwa ni Kilimanjaro katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Hai,Manyara katika Halmashauri za Hanang na mbulu.

  Mikoa Mingine ni Morogoro katika Halmashuri ya Wilaya ya Ulanga na Mvomero,Mkoa wa Shinyanga Halmashauri ya Wilaya ya Msalala,Mkoa wa Simiyu Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Itilima ambapo Mikoa mingine ambayo kasoro ndogondogo zilijitokeza na kupelekea uchaguzi kuahirishwa katika baadhi ya Kata ni    Kigoma,Mwanza,Tabora,Tanga,Mara,Rukwa,Pwani na Dar es salaam.
  Akizungumzia Hatua zitakazochukuliwa na Serikali kufuatia dosari zilizojitokeza.

  0 0

   
  WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa Tamasha la Krismas Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
   
  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa maandalizi kuhusiana na tamasha hilo yanaenda vizuri.
   
   “Tulikubaliana katika kamati tumuombe Waziri Mkuu mstaafu Sumaye aje atupe baraka kwenye tamasha la Krismasi, nafurahi kusema ni mtu wa watu, amekubali kujumuika na wadau wengine siku hiyo. Hili ni jambo la furaha kubwa kwetu.
   
  “Wasanii mbalimbali tunaendelea kuzungumza nao kuhakikisha wanashiriki katika tamasha hilo,”  alisema Msama katika taarifa yake.
   
  Sumaye alikuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005, akiwa ndiye Waziri Mkuu aliyekaa muda mrefu katika wadhifa huo kwa historia ya Tanzania.
   
  Alisema wamepanga kufanya maboresho makubwa katika tamasha hilo na moja ya maboresho hayo ni kuweka kiingilio rahisi zaidi ili kila mmoja aweze kuhudhuria na kupata baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu.
   
  “Waimbaji wote maafuru wa muziki wa Injili watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri mno kuhakiksha kwamba tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali.
   
  “Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi kwani watashiba kiroho kutokana na kuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho,” anasema. Baada ya onesho la Desemba 25 mkoani Mbeya, siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Samora Iringa na Desemba 28 Uwanja wa Majimaji Songea.

  0 0


  Na Emanuel Madafa,mbeya

  Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya kikiendelea kupata ushindi katika matokeo ya awali katika uchaguzi wa serikali za mitaa huku vyama vya upinzani vikifuata kwa mbali


  Kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Mwangi Kundya, yanaonesha kuwa, chama hicho kimefanikiwa kuzoa idadi kubwa ya vijiji hadi sasa.


  Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habariKundya amesema matokeo ya awali katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya lenye mitaa 181, CCM imefanikiwa kupata mitaa 106, Chadema71, NCCR-Mageuzi mmoja.


  Wilaya ya Chunya yenye Vijiji 86,ambapo vijiji vilivyokamilisha hesabu ni 74,  CCM ilipata vijiji 67 , Chadema vijiji 7, wakati kwa upande wa vitongoji, CCM ilipata vitongoji 270, huku Chadema ikiambulia vitongoji 18.Wilaya ya Ileje jumla ya vijiji vyote ni 71 ambapo vijiji 32 vimekamilisha matokeo yake, ambapo CCM imepata vijiji 23, Chadema vijiji 9, ambapo kwa upande wa vitongoji.


  Wilaya ya Kyela vijiji vyote 93 vimekamilisha matokeo yake, ambapo CCM imepata 79,Chadema 13 , huku uchaguzi wa kijiji kimoja kurudiwa ambapo kwa upande wa vitongoji 469, CCM vitongoji 377, Chadema 88, wakati vitongoji vine uchaguzi kurudiwa.


  Wilaya ya Mbarali jumla ya vijiji 102, CCM 81,Chadema 16 ambapo vijiji sita vitafanya uchaguzi wa marudio, ambapo kwa upande wa vitongoji jumla ni 713, ambapo CCM imeshinda vitongoji 570 , Chadema ikiambulia 79 na vitongoji 36 matokeo yake yalikuwa bado.


  Wilaya ya Mbozi, vijiji vilivyopo ni 125 ambapo kati ya hivyo 92 matokeo yake yalikuwa tayari ambapo CCM imepata viti 84 na Chadema imepata vijiji nane, huku vijiji 33 matokeo yalikuwa bado, kwa upande wa vitongoji 664, CCM imepata 557 na Chadema 110, CUF viwili,TLP ikiambulia kiti kimoja.


  Wilaya Rungwe jumla ya vijiji 155 , CCM imepata 132,Chadema 22, CUF kimoja na vijiji vitano kufanya marudio, wakati upande wa vitongoji vilivyopo ni 694,CCM 578,Chadema 111,CUF 2 na TLP viwili.


  Wilaya ya Momba ambayo matokeo yake yamegawanywa katika sehemu mbili kutokana na wilaya kuwa na Halmashauri ya mji wa Tunduma. Ambapo kwa upande wa vijiji jumla ni 72, CCM imepata vijiji 43,Chadema24 na vijiji vitano kufanyiwa marudio, wakati kwa upande wa vitongoji, jumla ni vitongoji 302, CCM 189, Chadema 53 na vitongoji 60 matokeo yake bado.


  Kwa upande wa mitaa katika Halmashauri ya mji wa Tunduma jumla ya mitaa ni 71, CCM imechukua mitaa 25, wakati Chadema imeongoza kwa kupata mitaa 46, hivyo kulazimika kuunda Halmashauri ya mji.Wakati matokeo ya Wilaya hizo yakipatikana katika mkoa wa Mbeya kwa upande wa Wilaya ya Mbeya Vijijini matokeo ya awali yameshindwa kutolewa kutokana na utata wa hesabu, lakini pia Jografia ya wilaya hiyo kuwa na changamoto ya mpangilio wake.


  Hata hivyo, habari za uhakika zinadai kuwa katika uchaguzi wa mamlaka ya mji Mbalizi, CCM imepata vitongoji viwili, huku chadema ikipata vitongoji 10 kati ya 12 hivyo kuwa na uhakika wa kuunda baraza la mamlaka ya mji.


  0 0


  Maelezo ya nyumba husika:
  • Ina vyumba vitatu vya kulala (kimoja master bedroom na viwili vya kawaida), dinning room, laundry na stoo.
  • Ina simtanks 2 (lita 2000 na lita 1000).
  • Iko ndani ya uzio na geti. 
  Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0763514988.


  0 0


  Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia, Christopher Yaluma (katikati), na Waziri wa Nishati na Petroli wa Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakisaini Makubaliano ya Awali (MoU) ya mradi wa pamoja wa kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme kati ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya.…
  Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia, Christopher Yaluma (katikati), na Waziri wa Nishati na Petroli wa Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakisaini Makubaliano ya Awali (MoU) ya mradi wa pamoja wa kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme kati ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya.
  Waziri wa Nishati na Petroli wa Kenya, Davis Chirchir (aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla iliyofanyika nchini Zambia ya kutiliana saini Makubaliano ya Awali (MoU) ya mradi wa pamoja wa kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme kati ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya. Wengine katika picha ni Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kushoto), Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia, Christopher Yaluma (wa nne kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini nchini, Eng.Ngosi Mwihava, (wa kwanza kushoto), pamoja na watendaji wengine kutoka nchini Kenya, Zambia na Umoja wa Ulaya.
  Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), (mstari wa mbele) waliohudhuria hafla iliyofanyika nchini Zambia ya kutiliana saini Makubaliano ya Awali (MoU) ya mradi wa pamoja wa kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 400 kati ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya wakimsikiliza mmoja wa wazungumzaji katika hafla hiyo (haonekani pichani). Kutoka kulia ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Eng. Hosea Mbise, Decklan Mhaiki, Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Uwekezaji (Tanesco), Kasindi Malale, Injinia Mkuu (Tanesco), Leonard Masanja, Injinia Mkuu (Wizara) na Mwanasheria, Abbas Kisuju (Wizara).

  Nchi za Tanzania, Zambia na Kenya zimetiliana saini Makubaliano ya Awali (MoU) ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa miundombinu ya kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 400. Makubaliano hayo ya awali yamesainiwa tarehe 15 desemba 2014, nchini Zambia na Mawaziri wanaosimamia sekta ya Nishati katika nchi husika ambao ni Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo,Waziri wa Wizara ya Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia,Christopher Yaluma, na Waziri wa Nishati na Petroli wa Kenya, Davis Chirchir.

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa kukamilika mwa mradi huo kutaziwezesha nchi hizo kuuziana umeme wa bei nafuu ambao utakuwa chini ya senti 10 za Kimarekani kwa uniti moja .“ Mradi huu utakamilika kwa awamu kati ya mwaka 2016 na 2018.
  Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia juhudi za serikali za kuachana na mitambo ya dharura ambayo inauza umeme huo kwa gharama ya kati ya senti 30 na 55 za Kimarekani kwa uniti moja”, alisema Profesa Muhongo.

  Profesa Muhongo aliongeza kuwa Tanzania inahitaji umeme mwingi, wa bei nafuu na wa uhakika ili kuongeza uzalishaji, uwekezaji, ushindani,kutengeneza ajira mpya na kukuza uchumi imara.
  Mradi huo utakuwa na manufaa mbalimbali kwa nchi husika ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa umeme kwa nchi hizo, kutumia rasilimali umeme kwa ufanisi zaidi, kutoa fursa kwa nchi wanachama kuweza kufanya biashara ya kuuziana umeme na kupanua upatikanaji wa umeme kwa wananchi husika.

  0 0


  Na James Festo, Njombe.
  KATIBU wa chama cha Mapinduzi Mkoani Njombe Hosea Mpagike ameviomba    vyama vya siasa Nchini kuacha kutumia nguvu kubwa katika chaguzi   mbalimbali na badala yake kuelimisha  jamii juu ya wanachotarajia   kufanya baada ya kupata nafasi.

  Mpagike amesema kuwa " tunatakiwa kufanya kampeni za kistaarabu kwa
  kujenga hoja atafanya nini baada ya kuchaguliwa lakini sio hoja za
  kuchafua mgombea niwaombe sana suala la siasa ni la kidemokrasia kila
  mmoja anahaki lakini sio ya kuchafua mwingine"

  Ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya hali ya uchaguzi kwa upande wa
  chama chake kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ulionekana
  kukumbwa na changamoto nyingi zikiwamo  za kutoonekana kwa majina na
  kusababisha  wapiga kura kuchukua mda mrefu wakati wa kupiga kura na
  kuelezea hofu yake juu ya watu kupiga kura mara mbili.

  Aliiomba Ofisi ya Waziri mkuu endapo itaendelea kusimamia uchaguzi huo
   wahakikishe wanaweka utaratibu wa kuchapishwa kwa majina sambamba  na    kutatua changamoto zote zilizojitokeza katika vituo vingi nchini.
  "  Katika uchaguzi huu tumekuta mararamiko mengi ambapo walikuwa
  majina yao hawayaoni nje na katika karatasi ya msimamizi ndani walikuw
  awanayakuta" alisema Mpagike.

  Akizungumzia matokeo ya uchaguzi kwa mkoa wa Njombe alisema kuwa
  Wilaya ya  Njombe alisema kuwa kuna vijiji 108 na vijiji saba
  havikufanya uchaguzi na kati ya vijiji vlivyofanikiwa kufanya uchaguzi
  CCM ilipata vijiji 94 sawa na asilimia 93 na chama cha
  demokrasia na maendeleo Chadema kimechukua vijiji 8 sawa na asilinia 7.44.

  Alisema kuwa  katika uchaguzi uliofanyika kwenye mitaa  iliyopo
  Halmashauri ya Mji wa Njombe na Makambako zenye jumla ya mitaa 82
  ambapo CCM ilichukua juma la mitaa 54 sawa na asilimia 66 ambapo
  CHADEMA imechukua mitaa 28 ambapo ni sawa na aslimia 34 na chama cha
  NCCR Mageuzi imechukua kijiji kimoja.

  Aliongeza kuwa katika halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe kulikuwa na vijiji kulikuwana vijiji 108 ambapo vijiji 4 havikufanya uchaguzi na
  katika CCM ilichukua vijiji 102 sawa na asilimia 98.1 na chadema
  ilichukua vijiji 2 sawa na asilimia 1.9.

  Katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa Chama cha CCM kilifanikiwa kuchukua   jumla ya vijiji 77 ambapo vijiji 4 havikufanya uchaguzi na kuwa CCM    ilichukua vijiji 64 sawa na asilinia 97 na Chadema imechuku vijiji 9
  sawa na asilimia 3.

  Aidha Mpagike alisema kuwa halmashauri ya wilaya ya makete CCM
  ilifanikiwa kuchukua viti 46 huku CHADEMA ikichukua  vijiji nane sawa
  na asilimia 68.

  Mpagike alitoa wito kwa watu ambao wamekuwa wakizani kuwa uchaguzi sio     sehemu za kunyeshana nguvu na kuvitaka vyama vya siasa kuacha tabia ya    kuwapakazia wagombea wetu kwa kuaandaa hoja za kuwatumu.


  0 0

  SAM_0190Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiongea na vyombo vya habaria katika ziara yake ya kikazi jijini hapa kwa lengo la kutembelea miradi ya maji iliyokuwa na changamoto kubwa ya upotevu wa maji inayosababishwa na uchakavu wa miundombinu na wizi wa maji
  SAM_0188
   Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala kulia akiwa anasikiliza maelezo kutoka kwa Eng wa maji Bw.Mohamed Ismail katika eneo la chanzo cha maji mto nduruma katikati niKaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian Maganga
  SAM_0178

  Muonekano wa maporomoko ya maji mto nduruma ni chanzo kikubwa kinachotegemewa Mkoani Arusha katika huduma ya maji
  SAM_0191
  Askari anayelinda eneo hilo

  SAM_0183Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala wa nne kulia akiwa anateta jambo katika moja ya maporomoko ya maji ijulikanayo kama mto nduruma wengine ni watumishi wa mamlaka hiyo.
  SAM_0173Kulia aliyesimama ni Makamu mwenyekiti wa bodi ya maji Mkoa wa Arusha Bw.Joshua Kileo akiwa anazungumza wakati Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala alipokuwa anazungumza na watumishi wa mamlaka ya maji Arusha leo
  SAM_0208Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiwa anaangalia moja ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji katika eneo la kisongo ambacho kitasaidia wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya maji
  SAM_0201Hii ni mitambo ya kuwekea maji dawa
  SAM_0200Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiangalia moja ya kisima cha maji katika kijiji cha Olturuto wilaya Arumeru
  SAM_0205Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akionge akatika moja ya chanzo cha maji kinachotengenezwa eno la kisongo Mkoa Arusha

  Na Pamela Mollel wa jamiiblog
  Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kuwafichua wale wote wanaoshiriki katika wizi wa maji ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.Alitoa wito huo jana wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi jijini hapa kwa lengo la kutembelea miradi ya maji iliyokuwa na changamoto kubwa ya upotevu wa maji inayosababishwa na uchakavu wa miundombinu na wizi wa maji

  Waziri Makala alisema kuwa serikali inafanya jitihada ya kuboresha huduma ya maji ikiwa nipamoja na kuboresha miundombinu,kukomesha wizi wa maji kwa kutoa elimu kwa wananchi.“Wizi wa kujiunganishia maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini upo lakini kwa sasa tunaoparesheni ya kuwasaka wale wote wanaotumia maji bila kulipa watambue kuwa kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria”alisema Makala

  Aidha katika moja ya chanzo kikubwa cha maji mto nduruma alisema kuwa chanzo hicho kinategemewa kwa mkoa wa Arusha hivyo alitoa pongezi kwa mamlaka ya maji kwa kuwa wabunifu.
  Naye Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian Maganga alisema kuwa kwa hivi karibuni walikuwa na zoezi la ukaguzi wa nyumba hadi nyumba na kufanikiwa kuwakamata watu wanaohujumu mamlaka hiyo takribani 750 hivyo zoezi hilo bado ni endelevu

  0 0

  Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe ya simu kwa msimu huu wa sikukuu ya Krismasi, ambapo itawawezesha wateja wa Airtel kununua simu za kisasa kwa bei nafuu na kupata vifurushi vya bure vya muda wa maongezi, ujumbe mfupi na huduma ya intaneti. Kushoto ni Meneja Masoko wa Bidhaa za Kisasa wa Airtel, Prisca Tembo.
  Meneja Masoko wa Bidhaa za Kisasa wa Airtel, Prisca Tembo (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde wakionyesha kwa waandishi wa habari, baadhi ya simu za mkononi zilizo kwenye ofa kabambe ya simu kwa msimu huu wa sikukuu ya Krismasi, baada ya kuzindua ofa hiyo, jijini Dar es Salaam jana, ambapo itawawezesha wateja wa Airtel kununua simu za kisasa kwa bei nafuu na kupata vifurushi vya bure vya muda wa maongezi, ujumbe mfupi na huduma ya intaneti.

  Airtel Tanzania  imetangaza ofa kabambe inayoenda sambamba na kuwazawadia wateja wake wakati wa msimu huu wa sikukuu, ofa hii iliyozinduliwa rasmi leo itawawezesha wateja kununua simu za kisasa kwa bei nafuu na kupata vifurushi vya bure vya muda wa maongezi , ujumbe mfupi na internet

  Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa bidhaa za kisasa Bi Prisca Tembo alisema” tunayofuraha kuzindua ofa hii ya msimu wa sikukuu na kuwawezesha wateja wetu kununua simu kwaajili yao na kwaajili ya wale wanaowapenda kwa bei nafuu zaidi sokoni.

  Tembo aliongeza kwa kusema “Ofa hii inaenda sambamba na dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma bora huku tukiwawezesha wateja wetu kufaidika na huduma na bidhaa zetu.  Simu hizi  za kisasa (yaani smart phone) zinapatikana katika maduka yetu ya Airtel nchi nzima kwa gharama  kuanzia  shilingi 125,000/=  hadi 979,000/=. Mteja atakaponunua simu hizi atapata na vifurushi vya muda wa maongezi, sms na internet vya mwenzi mzima, ofa hii itadumu kwa muda wa mienzi mitatu

  Ofa hii si ya kukosa, hivyo Tupenda kutoa wito kwa watanzania kuchangamkia ofa hii kwa kuwa wakwanza kununua simu ya aina wanayoipenda na kufurahia huduma zetu na kuunganishwa kwenye huduma ya internet ya 3.75G .” aliongeza Tembo

  Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” simu tulizonazo kwenye ofa ni pamoja na iphone 6, simu za Huawei na Techno. Simu hizi za kisasa ni rahisi kutumia na zitawapatia wateja wetu uzoefu tofauti si kwa bei rahisi tu bali zimewezeshwa na techonologia ya 3G na kuwawezesha kufurahi internet ya kasi.”

  Natoa wito kwa wateja kutembelea ofisi zetu na kunua simu na kuunganishwa na huduma zetu nyingi ikiwemo Airtel yatosha, Airtel Money, huduma ya internet na vifurushi vya OMG, Switch On pamoja na huduma yetu mpya ya WiFi ya nyumbani tuliyoizindua hivi karibuni aliongeza Matinde.

  0 0

  BAADA ya mechi ya Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga kwa mchezo wa soka, Wafalme wa muziki wa dansi nchini bendi pizani za Msondo Ngoma na  Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae) nao watakuwa na Mtani jembe yao   siku ya Krismasi katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe.

  Mpambano huo wa Mtani Jembe umeandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment. Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu ya Krismasi na kufunga mwaka 2014.

  Pmambano na bendi hizo, utasindikizwa na wakongwe wenzao wa muziki wa dansi nchini Vijana Jazz Band, wakiwa na binti wa aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo Hemed Maneti, Komweta Maneti ambaye ataimba nyimbo zote zilizokuwa zikiimbwa na baba yake.

  Kapinga alisema kuwa pia pambano hilo litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wawili wa muziki wa dansi nchini kwa mwaka huu wa 2014. Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kuondoa malalamiko ya kuhujumiwa. “Tutakuwa na michezo aina mbalimbali ya watoto,” alisema Kapinga.

  Alisema mchuano huo utaanza saa nane mchana hadi liamba.
  Wadhamini ni kinywaji cha Konyagi, Fredito Entertainmernt na Saluti5.

  0 0

  Na Eleuteri Mangi- Arusha.
   
  Serikali ya Tanzania inaendelea vema na mpango wake wa kutoa elimu ya msingi kwa watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule nchini.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa wakati akiwasilisha mada yake inayohusu “Namna Tanzania inavyoboresha Usawa wa Kinga ya Jamii katika sekta ya elimu” katika kongamano la kimataifa linaloendelea katika siku ya pili jijini Arusha kuhusu Kinga ya Jamii.

  Dkt. Kawambwa alisema kuwa mpango huo unaanzia elimu ya awali, shule ya msingi na sekondari ambapo kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule apate elimu ambayo ndiyo msingi wa kinga ya jamii nchini tofauti na awali ambapo elimu ya msingi ilikuwa kwa watoto wenye umri kuanzia miaka 7 hadi 14.

  Dkt. Kawambwa alisisitiza kuwa mpango huo wa kinga ya jamii nchini unaenda sanjari na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ambao Tanzania imeanza kuutekeleza mwezi Aprili, 2013 ambapo unatarajiwa kuhitimishwa 2017.

  Ili kufikia malengo ya kuboresha mpango wa kinga ya jamii nchini, Dkt. Kawambwa aliwaambia wajumbe wa kongamano hilo kuwa mbinu zinazotumiwa na Tanzania katika kutekeleza mpango wa BRN na kuboresha kinga ya jamii ni pamoja na kuboresha vifaa vya kujifunza na kufundishia shuleni, kusimamamia mpango wa wanafunzi kujua kusoma, kuandika na kuhesabu na kuboresha ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya ndani na ya taifa.

  Mbinu nyingine ni kuwapa motisha walimu, kutoa motisha kwa shule zilizofanya  vizuri katika mitihani ya taifa kwa shule zote iwe ya msingi au sekondari na kuwawezesha walimu na wanafunzi kujua wajibu wao kwenye sekta ya elimu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa ufanisi ili kuongeza nguvu kazi ya wataalam ambao ndio msingi wa kuboresha kinga ya jamii na hivyo kupunguza tatizo la umaskini nchini.

  Aidha, Dkt. Kawambwa alisema kuwa viashiri ambavyo vinaonesha Tanzania inaendelea kupata mafanikio katika kuimarisha sekta ya elimu na kuimarisha kinga ya jamiina ni pamoja na kuongezeka ufaulu katika mitihani ya taifa ambapo mwa 2013 ufaulu kwa shule za msingi na sekondari ulikuwa zaidi ya asilimia 60, mwaka 2014 kwa asilimia zaidi ya 70 na inatarajiwa 2015 ufaulu huo utaongezeka kufikia asilimia 80.

  Akijibu swali la Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Huduma Ali N. Ismail kutoka Kenya aliyetaka kujua kwanini Tanzania bado inatumia mpango wa kupanga shule katika madaraja ambao unaweza kupunguza morali kwa baadhi za shule ambazo inaweza kuwa chanzo cha kupunguza  uwezekano wa kutoboresha mpango wa Kinga ya jamii.

  Dkt. Kwambwa alisema kuwa Serikali inasimamia mpango huo kwa kuwahusisha wanafunzi wote na shule zote bila kubagua na kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, walimu wamepata mafunzo ambayo yanawawezesha walimu hao kusimamia wanafunzi wenye mahitaji maalum kulingana na hali zao na amesema Tanzania ipo tayari kujifunza kutoka Kenya namna wanavyofanikiwa kuacha na mpango wa kupanga shule katika madaraja.

  Kwa upande wa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi, Waziri Kwawambwa alisema kuwa kwenye suala la mitihani wanafunzi hao wamepewa kipaumbele kwenye suala la muda ambapo wao huongezewa baada ya muda wa kawaida wa mtihani kuisha na mitihani yao imeandikwa kwa maandishi makubwa zaidi ili kuwasaidia kusoma vizuri zaidi.

  Kongamano la kimataifa linalohusu Kinga ya Jamii linaloendelea jijini Arusha limeandaliwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Idara ya Kuondo Umaskini kwa kushirikiana na UNICEF, ILO, UNAIDS na EPRI ambapo washiriki wa konngamano hilo wanatoka katika nchi za Kenya, Uganda, Bangladesh, Afghanistan, Msumbiji, Lesotho, Malawi, Afika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudani kusini na mwenyeji Tanzania.  

  0 0

  001

  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani akifungua semina ya siku mbili ya kimataifa inayozungumzia makabila ya asili, haki zao na namna ya kuboresha maisha na mifumo ya chakula . Semina hiyo inayofanyika Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam inajiandaa kwa kongamano la dunia nzima kuhusiana na jamii za asili ambalo litafanyika Roma Italia, Februari 2015.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).
  002
  Mwakilishi Shirika la Kimataifa la maendeleo ya Kilimo, IFAD, Bw.Francisco Pichon akisisitiza jambo wakati wa kongamano hilo.
  003
  Washiriki wa semina hiyo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa kuhusu haki za makabila ya asili na namna ya kuboresha maisha yao na mifumo ya chakula .
  004
  005
  006
  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa kongamano hilo.

  0 0

  Bofya video kumsikiliza Nape Nnauye akizungumza kuhusiana na waliovuruga uchaguzi wa Serikalo za Mitaa.
    Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari,leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kutoa tathmini ya matokeo ya awali uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika juzi nchini kote.
  Baadhi ya Wanahabari Wakimsikiliza  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akizungumza nao,leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kutoa tathmini ya matokeo ya awali uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika juzi nchini kote.PICHA NA GLOBU YA JAMII.
  =======  =====  =======

  NA BASHIR NKOROMO.


  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka watendaji wote waliosababisha kuharibika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika baadhi ya maeneo nchini wachukuliwe hatua kali.

  Kimesema, watendaji hao wanastahili kuchukuliwa hatua kali kwa sababu kilichotokea ni uzembe wa hali ya juu uliofanyika huku ikifahamika wazi kwamba tukio la uchaguzi huo ni kubwa na muhimu sana kwa Taifa.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (pichani) amesema, kulingana na kosa lililojitokeza kuwa la wazi hakuna haja ya kupoteza fedha na muda kufanya uchunguzi kabla ya kuwachukulia hatua waliohusika.

  "Kwa mfano, Mkurugenzi wa Halmashauri ana kila kitu na alijua mapema kuwa uchaguzi utafanyika lini kwa kuwa halikuwa jambo la dharura, inakuwaje anaruhusu karatasi ziende kwenye vituo zikiwa zimechapishwa hovyo au mahali pengine vifaa viwe vichache?" alihoji Nape na kuongeza "Sasa hapa unahitajika uchunguzi gani tena kubaini aliyevurunda?".

  "Mahali pengine zimefika karatasi za kupigia kura jina la mgombea wa CCM nembo ya CUF, au mgombea wa CUF nembo ya CCM! huu ni uzembe wa hali ya juu sana na adhabu yake haistahili kusubiri uchunguzi", alisema Nape.

  Akizungumzia matokeo ya awali ya Uchaguzi huo, Nape alisema licha ya vyama vya upinzani kuwa na umri wa miaka 22 sasa, huku vikifanya harakati za kujaribu kuungana katika umoja wanaouita Ukawa, bado CCM imewagaragaraza vibaya.

  Nape amesema, katika uchaguzi huo, CCM imepata zaidi ya asilimia 80 ya ushindi kwa nchi nzima, huku Dar es Salaam, ikiwa na asilimia zaidi ya 70 licha ya kwamba Chadema wanao wabunge wawili katika mkoa huo.

  "Katika mazingira ya sasa ambayo vyama vya upinzani vina miaka 22, na vinafanya hata harakati za kujaribu kuungana, asilimia 80 si ndogo kwa CCM, na tunaamini huu ni mwanzo mzuri, na hatuoni namna ambavyo asilimia hii itabadilika katika uchaguzi mkuu mwakani, maana uchaguzi huu ni kama kura za maoni", alisema Nape.

  "Wanaosema, asilimia ya CCM imeshuka, wajue kwamba tuliposema tunataka mfumo wa vyama vingi maana yake tulitaka ushindani katika demokrasia, katika demokrasia ya ushindani ni vema kuruhusu vyama vya upinzani vikakua ili ushindani huo uonekane", alisema Nape nakuongeza.

  "Hata hivyo inasikitisha kwamba licha ya vyama vya upinzani kuwa na umri wa miakaa 22 sasa, bado havijaweza kujenga imani ya kutosha kwa Watanzania kuwa vinaweza kuongoza, lazima wapinzania wazidi kujijenga ili Watanzania wawaamini, asilimia hii 14 waliyopata karika uchaguzi huu wa serikali za mitaa bado ni ndogo sana kwa uhai wa miaka hiyo".

  Amesema, asilimia iliyopata CCM wakati matokeo mengine yakisubiriwa ambako uchaguzi uliahirishwa, ni dalili za wazi kwamba, Ukawa bado ni muungano wa mashaka kwa sababu kama wangeungana na kuachiana maeneo ni kweli wangeweza kufika mbali.

  "Hebu jiulizeni na ninyi, kama kweli UKawa ulitumika vema, ni kwa nini kwenye karatasi za matokeo ya uchaguzi huu, kila chama kina mtu wake na idadi ya kura alizopata? Kwa nini zisiwe za mgombea mmoja wapo wa Ukawa?... Hii inamaanisha ndoa hii ya ukawa bado sana", alisema Nape.

  Nape aliwashukuru wananchi nchini kote kwa kuendelea kuiamini CCM, na kuchagua wagombea wake, huku akivipongeza vyama vya upinzani kwa maeneo waliyochaguliwa, akiwataka kuchapa kazi vinginevyo siku za baadaye wananchi watawahukumu kwa kuwatosa.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa akiwa anaongea wakati wa uzinduzi  wa baraza la ushauri wa chuo cha mafunzo ya hoteli na utalii cha mamlaka ya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi (VHTTI) Kilichopo Njiro mkoani Arusha.
  baadhi ya watumishi wa VETA  akiwemo Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi wakiwa wanabadilishana mawazo nje ya viwanja vya chuo  cha mafunzo ya hoteli na utalii


  mkuu wa wilaya ya Arumeru akiwa anamkabidhi nyaraka ya kutendea kazi mmoja wa wajumbe wa baraza la chuo cha VHTTI ambaye ni mwakilishi wa chama cha wamiliki wa makampuni ya utalii(TATO) bw, Peter Lindstrone  wadau mbalimbali wakiwemo wajumbe wa chuo hicho wakiwa wanafatilia uzinduzi huo wa baraza la chuo kwa makini
  mkurugenzi wa VETA wa kwanza  kulia Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi akifuatiwa na mwenyekiti wa bodi  pamoja na mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa na wakwanza kushoto ni mkuu wa chuo cha VHTTI Flora Hakika wakibadilishana mawazo


  waandishi wa habari mbalimbali wakiongea na mkuu wa wilaya mara baada ya uzinduzi huo wa baraza la ushauri wa  chuo cha  mafunzo  ya hoteli na utalii cha VHTTI

  wageni waalikwa wakiwa wanafatilia uzinduzi huo kwa makini sana


  Na woinde shizza ,Arusha

  Baraza la ushauri la chuo cha  mafunzo ya hoteli na utalii (VHTTI) limetakiwa kuhakikisha linaandaa wanafunzi vyema na wenye viwango vya kimataifa   ili kukabiliana  na ushindani mkubwa ulioko katika sekta ya hoteli na utalii duniani.

  Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyerembe Munasa wakati akizindua baraza hilo  jana ndani ya chuo cha hoteli na utalii cha VHTTI kilichopo  nje kidogo ya jiji la Arusha .

  Alisema kuwa kutokana na changamoto kubwa ya  hoteli zetu kuajiri watu kutoka nje ya nchi ikiwemo kenya na hata nchi za bara ya ulaya  kwa kile kinachodaiwa vijana wazawa kutokuwa na elimu ya kutosha  kuhusiana na sekta ya hoteli na utalii hivyo ni wajibu wao kuakikisha wanafundisha wanafunzi ili waweze kuwa na elimu ya kiwango cha kimataifa .

  Alibainisha kuwa  wanatakiwa wahakikishe wanachuo ambao wanawafundisha wanakuwa na sifa zinazotakiwa huku akiongeza kuwa mafunzo wanayofundishwa yawe bora yanayokidhi maitaji ya ajira .

  Aidha alisema kuwa iwapo watawafundisha wanafunzi hao vyema na kuwapa elimu inayoitajika kuoendana na soko hii itawasaida kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira kwani wanafunzi hawa pindi watakapo maliza elimu yao itakuwa raisi kupata kazi kulingana na elimu walikuwa nayo.

  ''pia napenda kuwashauri  kuanzisha lunga zote za kimataifa katika chuo chenu ili mwanafunzi anaetoka katika chuo hichi aweze kuwasiliana na mgeni yeyote ambaye atakuja kutoka katika nchi yoyote huko kazini kwake anapoenda kwakweli inachekesha sana kuona mgeni anakuja alafu mwanafunzi anaanza kuongea lunga mfano ya kingereza kwa kukosea kosea au anaongea frechi kwa kukose  kosea''alisema  munasa

  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi  alisema kuwa    wao kama Veta wameamua kuanzisha chuo hichi cha  hoteli na utalii ili kuweza kupunguza tatizo la ajira ambalo linaendelea kwa vijana wengi.

  Aliesema kuwa  chuo hichi  kitatoa mafunzo ya hoteli na utalii katika ngazi ya cheti na shahada  kwa wasimamizi na waangalizi wa hoteli zetu.

  Naye mkuu wa chuo hicho   Flora Hakika alisema kuwa wataji taidi kuwafundisha wanafunzi  vyema na wataanza kwa kuaandaa mitaala mipya huku wakiwa wanaangalia zaidi  jinsi wenzetu wa nchi za nje wanavyo fanya pia watajitaidi  kulenga kupata maitaji ya soko linavyoitaji ili kuweza kuinua zaidi utendaji kazi  wa vijana wa kitanzania


  0 0
 • 12/16/14--08:19: Mamia wamzika Shem Karenga
 •  Baadhi ya wadau wa muziki wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Tabora Jazz, marehemu Shem Karenga wakati wa maziko yake yaliofanyika leo kwenye makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
   Ras Inocent Nganyagwa akitafakari jambo wakati wa maziko ya mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi marehemu Shem Karenga.
   Hassan Rehan Bichuka (kulia) akiwa na wanamuziki wenzake wa zamani wakibadilishana mawazo na Ankal walipokuwana katika maziko ya mwanamuziki nguli wa bendi ya Tabora Jazz, marehemu Shem Karenga.
   Ankal akiteta jambo na mwanamuziki mkongwe wa Band ya Sininde Ngoma ya Ukae.
   Mwili wa marehemu Shema Karenga ukiwasili katika makaburini ya Kisutu.
   Mamia ya waombolezaji wakielekea makaburini.
   Mwanamuziki mkongwe Kassim Mapili (katikati) akiwa na wadau wa muziki kulia ni mwanamuziki Tshimanga Asosa na kushoto ni mdau wa muziki Ankal Michuzi.
  Mdau wa muziki John Jambele (kushoto) akiwa na Tshimanga Asosa


  Na Mwandishi Wetu  MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, leo alasiri walijitokeza kumzika nguli wa muziki wa dansi nchini, Shem Ibrahim Karenga aliyefariki juzi asubuhi na kuzikwa jana alasiri katika Makaburi ya Kisutu.  Karenga (64), aliyewahi kutamba na bendi mbalimbali maarufu nchini akianzia Tabora Jazz, alifariki katika akiwa katika hospitali ya Amana, ambako alilazwa baada ya kukimbizwa Jumapili usiku kutokana na kuzidiwa ghafla.  Miongoni mwa wanamuziki na wasanii walioshiriki mazishi ya nguli huyo ni ni mkongwe wa kupiga gitaa Said Mabela, aliyemwelezea Karenga kama taa ya muzimki wa dansi iliyozimika ghafla.  Mabela alisema, kifo cha Karenga kimemgusa sana kwani sio tu kama mwanamuziki mwenzake, ni mtu aliyefahamiana naye kwa mufa mrefu wakati huo akiwa mkoani Kigoma na Bendi ya Ujiji Jazz.  "Karenga ametuachia pengo kubwa katika tasnia ya muziki wa dansi. Ni mtu aliyeufanyia mengi muziki wa dansi. Alikuwa ni mtu mwenye juhudi binafsi na upendo kwa wengine, lakini kazi ya Mungu haina makosa,” alisema Mabela wa Msondo Ngoma.  Naye mmiliki wa Bendi ya Tabora Jazz, Ibrahim Didi alisema Karenga ni miongoni mwa wanamuziki ambao wamejaaliwa kipaji cha aina yake akiweza kuimba na kupiga gitaa kwa wakati mmoja.  "Nimepoteza jembe, isitoshe ni mtu niliyetoka naye Tabora, pia hadi anafariki alikuwa yupo katika bendi hii ya Tabora Jazz, imenima sana. Karenga alikuwa mtu wa watu," alisema Didi, kiongozi wa zamani wa Yanga.  Mwingine aliyemzungumzia Karenga, ni Ally Choki ambaye alikiri kuwa kwake alikuwa ni mwalimu wake wa kupiga vyombo hasa gitaa akifanya naye kazi mwaka 1992.
  "Alinifundisha mengi na alikuwa mwalimu wangu katika tasnia hii..ya muziki, kwa kweli ametuachia pengo kwasababu ni ambaye aliniongoza kaatika masuala mengi, nilikuwa namfuataga kwake Kariakoo ili anifundishe na kweli alinifundisha,"alisema Choki.
  Naye Sajenti mstaafu wa Bendi ya Polisi Jazz ya jijini Dar es Salaam, Kassim Said Mapili, alisema Karenga Shem alikuwa ni mpiganaji mkongwe katika tasnia ya muziki.  "Nilijuana naye  wakati tulipokutana Tabora wakati yupo Lake Tanganyika Jazz, alikuwa na uwezo mkubwa tofauti na vijana wa sasa hivi wanashindwa kuimba bila ya kutumia 'playback' CD," alisema.

  Shem Ibrahim Karenga, aliyezaliwa mwaka 1950, kitongoji cha Bangwe, Kigoma, alipata elimu ya msingi shule ya Kimishionari ya Kihezya kuanzia mwaka 1957 hadi 1964.
  Baada ya hapo, mwaka 1964 alijiunga na bendi ya Lake Tanganyika Jazz ambayo maskani yake yalikuwa mjini Kigoma.

  Tangu aingie Lake Tanganyika akiwa mwimbaji na mcharazaji wa gitaa la besi, alikuwa na ujuzi wa kutengeneza gitaa kwa kutumia vifaa vya kuokoteza.
  Aidha katika miaka yake minne katika bendi ya Lake Tanganyika Jazz, alijifunza vyombo vingine vya muziki kama Drums, Kinanda, gitaa la Rithym na la Solo’. Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
                    

  0 0

  1Bima ya Afyaaa
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee wa pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya mfuko huo wakati walipoonyesha tuzo ambazo mfuko huo ulitunukiwa nchini Morocco na Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) nchini Morocco hivi karibuni. kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto wakiwa katika mkutano huo uliozungumzia tuzo hizo.
  Bima ya Afya
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee wa pili pamoja na wakurugenzi wa shirika hilo kulia Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto wakionyesha tuzo zilizokabidhiwa kwa mfuko huo kutoka Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) nchini Morocco hivi karibuni

  ....................................................................................................................
  Kwa miaka mingi sasa, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekuwa mwanachama wa mashirikisho mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA), Shirikisho la Hifadhi ya Jamii la Nchi za Afrika Mashariki na Kati (ECASSA), na Shirikisho la kimataifa la Uchumi wa Afya (IHEA). Mashirikisho haya husaidia katika kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali, ushauri wa kitaalamu, viwango vya huduma, miongozo ya kiutendaji pamoja na kutumika kama jukwaa kwa wanachama kujenga na kuhamasisha mifumo endelevu katika hifadhi ya jamii. Taasisi hizi za kimataifa vilevile huhusika katika kutoa tuzo kwa Taasisi ambazo zinafanya vizuri katika ubunifu katika maeneo mbalimbali.

  Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) limekuwa na utaratibu wa kushindanisha mifuko ya hifadhi ya jamii duniani kwenye maswala ya ubunifu katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji yakiwemo; kuboresha huduma, utawala bora, matumizi ya teknolojia, ukusanyaji wa michango na matekelezo, uwekezaji, kufikisha huduma kwa wananchi waliyo sehemu ngumu kufikika, uhamasishaji wa Afya na uepushaji wa hatari makazini, pamoja na utekelezaji wa tathmini za uhai wa mifuko. Mashindano haya yalianza tangu mwaka 2008 na hufanyika kila baada ya miaka mitatu.

  Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizi, Mfuko umekuwa ukishinda tuzo katika maeneo mbalimbali. Mwaka 2008 Mfuko ulishinda tuzo moja ya ubunifu katika kuboresha huduma na mawasiliano kwa wanachama kupitia siku ya wadau (Clients Days). Mwaka 2011 Mfuko ulishinda tuzo nne katika masuala yafuatayo; Uboreshaji wa kitita cha mafao yanayotolewa na Mfuko;Usimamizi wa Mfuko wa Afya ya Jamii: 

  katika kupanua wigo na jitihada za kufikia lengo la afya kwa Watanzania wote; Utoaji wa mikopo ya vifaa tiba na Uboreshaji wa majengo inayotolewa na Mfuko; Ugatuzi wa shughuli za Mfuko kwa kufungua ofisi za mikoa kuwasogezea huduma wananchi: Usimamizi bunifu kuongeza ufanisi katika utendaji.Kwa mara nyingine Mfuko umeshinda tuzo tatu za ubunifu katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika katika sherehe za kukabidhi tuzo hizo zilizofanyika tarehe 3 Disemba 2014 katika hoteli ya Sheraton mjini Casablanca, Morocco. 

  Tuzo ambazo NHIF ilikabidhiwa ni katika eneo la utoaji wa huduma za matibabu za kibingwa maeneo magumu kufikika, kazi ambayo Mfuko umekuwa ukifanya kwa kushirikiana na wataalamu wa hospitali za rufaa nchini tangu mwaka 2012. 

  Tuzo nyingine ni katika eneo la TEHAMA katika utayarishaji pamoja na uwasilishaji wa madai ulioanzishwa kwa dhumuni la kupunguza malalamiko ya baadhi ya vituo vya Afya kuchelewa kulipwa madai yao. Kupitia mfumo huu, muda wa ulipaji wa madai hasa katika hospitali kubwa nchini umepungua kwa kiasi kikubwa sana. Mfumo huu ulianza tangu Januari 2012.

   Tuzo ya tatu ni juu ya huduma za matibabu kwa wanachama wastaafu ambayo imeanza tangu mwaka 2011. Fao la wastaafu linalenga kuwapa wananchi ambao walikuwa wanachama wa Mfuko na wenza wao uwezo wa kutibiwa kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya baada ya kustaafu ajira mpaka mwisho wa maisha.

  Mfuko utaendelea kufuata miongozo inayotolewa na mashirika ya kimataifa ili kutekeleza shughuli zake kiufanisi na kuhakikisha unatoa huduma bora kwa wanachama wake.Mfuko vilevile unadhamiria kuendelea kuboresha shughuli zake ili uweze kukidhi viwango vya kimataifa vinavyotolewa na Shirika la viwango la kimataifa (ISO) na hatimaye kuthibitishwa kwa kutimiza viwango hivyo katika kipindi kifupi kijacho.  

  NHIF Mfuko pia unatarajia kwa kipindi kijacho kuweza kukidhi viwango vilivyowekwa na Shirikisho la kimataifa la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (ISSA) na kupata ithibati ya kukidhi viwango vya kimataifa.

older | 1 | .... | 426 | 427 | (Page 428) | 429 | 430 | .... | 1897 | newer