Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 421 | 422 | (Page 423) | 424 | 425 | .... | 1898 | newer

  0 0

  TAMASHA la Utamaduni la NSSF Handeni Kwetu, sasa litafanyika Desemba 20, badala ya Desemba 13, kama ilivyotangazwa hapo awali, huku sababu kubwa ikiwa ni kuwaachia Watanzania washiriki katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa, utakaofanyika Jumapili ya Desemba 14 nchini kote.
  Mratibu Mkuu wa Tamasha la NSSF Handeni Kwetu 2014, pichani akizungumza jambo katika tamasha la mwaka jana lililofanyika kwa mafanikio makubwa wilayani Handeni, mkoani Tanga.
   
  Akizungumzia hilo leo mjini Handeni, Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kwamba hatua ya kusogeza mbele kwa wiki moja, ni kutokana na mguso wa tukio lenyewe na nia ya kuwashirikisha Watanzania wote ili kuliweka tamasha lao katika kiwango cha juu.
   
  Alisema kuwa Desemba 13 ni siku ya mwisho kwa kampeni za ugombea uenyekiti wa serikali za mitaa, vitongoji na mitaa, hivyo kwa kushauriana na jeshi la Polisi wilayani Handeni, wamekubaliana kulifanya Desemba 20.
   
  “Tumeangalia mambo mengi sana hadi kukubaliana lifanyike Desemba 20, ikiwa ni kukosekana kwa wengi, wakiwamo Wakurugenzi ambao kimsingi wao ndio wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo mengi.
   
  “Tunaamini kwa kufanyika Desemba 20, tamasha litakuwa kwenye mvuto pamoja na kukwepa malalamiko kwa baadhi ya wanasiasa ambao huenda wangelalamika endapo lolote lingetokea huku wao kushindwa uchaguzi wao,” alisema Mbwana.
   
  Mbwana alitumia muda huo kuwaomba radhi wadau wote, wakiwamo wasanii, wadhamini na wale waliokuwa wamepanga kutembelea Handeni Desemba 13, huku akiwataka safari yao ifanyike kwa ajili ya Desemba 20, ukizingatia kuwa wote wanaweza kushiriki chaguzi zao na kupata muda mkubwa wa kutembelea wilayani Handeni na mkoa mzima wa Tanga kumaliza mwaka wao vizuri.
   
   Wadhamini tamasha hilo ni Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Phed Trans, SmartMind & Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd kwa kupitia kitabu cha ‘Ni Wakati wako wa kung’aa, Handeni Kwetu Foundation, Wait & Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt Ltd na Michuzi Media Group.

  0 0

  Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo za kuweka mahesabu vizuri kwa taasisi bora za serikali mwaka 2013-2014 iliyotolewa  NBAA. (Na Mpiga Picha Wetu)
  Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima (kushoto) akimkabidhi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Rished Bade Ngao ya ushindi wa kwanza kwa taasisi za serikali kwa kuweka kumbukumbu za mahesabu vizuri  mwaka 2013/14 inayotambuliwa na Bodi ya Wakaguzi wa Mahesabu nchini (NBAA), juzi mkoani Arusha, wanaoshudia ni wafanyakazi wa TRA.
  Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akifurahia jambo na Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade.
  Picha ya pamoja.


  Taasisi za  serikali, mashirika ya umma  wizara na idara  mbalimbali za serikali zimeshauriwa kushiriki katika mashindano ya uwasilishaji wa taarifa bora za fedha za mwaka  tofauti na ilivyo sasa ambapo makundi haya yamekuwa  yakishiriki kwa uchache  sana  na sehemu kubwa ya washiriki  kuachiwa  taasisi na mashirika binafsi. 

  Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo na vyeti kwa washindi  katika uwasilishaji  wa taarifa bora za fedha mwaka  2014, Naibu Waziri wa Fedha, Adamu Malima  amesema  ni wakati mwafaka  kwa  taasisi na idara mbalimbali za serikali kuingia katika mashindano hayo ili kujipima na kuongeza ufanisi katika utunzaji na uandaaji wa taarifa zao kulingana na viwango vya kimataifa IFRS.

   Katika mshindano hayo ambayo huratibiwa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA kwa mwaka huu  jumla ya washiriki 40 walishiriki  ambapo  mamlaka ya mapato nchini TRA Iliibuka mshindi  wa kwanza kwa uwasilishaji wa taarifa bora za  fedha kwa mwaka 2013 -2014. kwa upande wa taasisi za serikali.

  0 0  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh Bernad Membe akikimbia katika mazoezi ya JOGGING,yaliyofanyika leo jijini Dar,katika mazoezi hayo Mh. Membe alifanikiwa kukimbia kilometa nane na ushehe,zilizokuwa zimepangwa.Aidha Jogging hiyo ilishirikisha club za Jogging 83 kutoka mkoa mzima wa jiji la Dar.Jogging hiyo iliandaliwa na club ya Jogging ya Mikocheni.Pichani kwa Waziri Membe ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh.Yusufu Mwenda
   Pichani juu ni baadhi ya vikundi mbalimbali wakishiriki Jogging hiyo mapema leo jijini Dar.
  0 0


  Mshiriki  wa Tanzania anayewakilisha ndani ya mjengo wa Big Brother ‘hotshots’ , Idris Sultan ndiye ameibuka kinara leo usiku katika shindano hilo huko Afrika Kusini. Idris amekuwa Mtanzania wa pili kushinda shindano hilo, baada ya Richard Dyle Bezuidenhout kuibuka kidedea mwaka 2011 katika Big Brother Afrika II.

  0 0  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone:255-22-2114512, 2116898
  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,
        STATE HOUSE,
                1 BARACK OBAMA ROAD,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mkuu Mpya mmoja wa Mkoa na kuwahamisha vituo vya kazi wengine sita kuanzia jana, Jumamosi, Desemba 6, 2014.

  Taarifa iliyotolewa leo, Jumapili, Desemba 7, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi Felix Ntibenda  kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

  Ndugu Ntibenda ataapishwa kesho, Jumatatu, Desemba 8, 2014, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar Es Salaam.

  Taarifa hiyo inasema kuwa wakuu waliohamishwa vituo vya kazi ni Mheshimiwa Elaston Mbwilo anayehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda Mkoa wa Simiyu ambako anachukua nafasi ya Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa, Mheshimiwa Joel Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa wa Manyara kutoka Mkoa wa Morogoro na Mheshimiwa Dkt. Rajabu M Rutengwe anayehamishwa Mkoa wa Morogoro kutoka Mkoa wa Tanga.

  Wengine ni Mheshimiwa Magalula Saidi Magalula anayehamishiwa Mkoa wa Tanga kutoka Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza anayehamishiwa Mkoa wa Lindi kutoka Mkoa wa Pwani na Mheshimiwa Mhandisi Evarist B. Ndiliko anayehamishiwa Mkoa wa Pwani kutoka Mkoa wa Arusha. 

  Wakuu wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu – Dar es Salaam.
  6  Desemba,2014

  0 0

  DSC_0277

  Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiongea na na Vijana (hawapo pichani) kutoka taasisi mbalimbali na mashirika yasiyokuwa yakiserikali wanaofanyaka kazi za kujitolea kwenye jamii wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Siku ya Kujitolea duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Desemba duniani kote ambapo kwa Tanzania kitaifa maadhimisho haya yamefanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

  SERlKALI imesema inatoa kipaumbele kwenye suala la kujitolea ikiwa ni sehemu ya kushirikisha vijana katika maendeleo yao na taifa lao. Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya vijana, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,James Kajugusi wakati akisoma hotuba kwenye madhimisho ya Siku ya Kimataifa yakujitolea kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Fenela Mkangara.

  “ Kama nchi serikali inadhani kujitolea ni hiari si kitu cha kulazimisha… unafanya kwa hiari bila kusukumwa na mtu au kitu inajenga nidhamu.Serikali inaamini kujitolea ni utu na unaonesha ubinadamu wako kwako wewe mwenyewe kwa watu wengine na kwa nchi yako.”

  Kaimu Mkurugenzi huyo alisema kwamba kutokana na Serikali kuthamini na kutambua mchango wa kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya nchi ,ambapo washiriki wake wengi ni vijana, inapanga mkakati wa kutumia uzoefu wa vijana hao katika masuala hayo ili kuinua ushiriki wa vijana katika maendeleo ya nchi.
  DSC_0378
  Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (mwenye suti nyeusi) aliyewamwakilisha Waziri mwenye dhamana wa wizara hiyo, akiongea na Vijana wanaofanyashughuli za kutolea wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

  DSC_0218
  Pichani juu na chini ni baadhi ya vijana kutoka taasisi mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali waliohudhuria maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Waziri Mukangara iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (hayupo pichani).


  “Nilikozaliwa wananchi ndio walikuwa wanatengeneza barabara, visima vya maji, wananchi ndio wanapeleka wagonjwa hospitali..’” na kusema kwamba sasa hali imekuwa mbaya kwa kuwa inadaiwa kitu kwanza kabla ya kufanyika kwa kazi.

  Akizungumzia kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya kujitolea inayosema; Ushiriki na ushirikishwaji katika kuleta maendeleo katika ngazi zote za kitaifa na za kimataifa, amesema inaangalia ushiriki wa vijana katika maendeleo. Alisema Tanzania imetengeneza mikakati kadha aya kuwezesha ushiriki wa vijana ikiwa ni pamoja na kuridhia mkataba wa vijana wa umoja wa Mataifa na kuanzisha baraza la vijana kwa mujibu wa katiba.

  Naye Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodrigues, amesema umoja wa mataifa unajisikia faraja kuadhimisha siku hiyo ikiwakumbuka watu mbalimbali waliofanya utu kwa kujitolea katika shughuli mbalimbali za ubinadamu.
  DSC_0223
  Akiwasilisha neno la katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki moon alisema siku ya kimataifa ya kujitolea ni muhimu kutokana na mahitaji halisi yaliyopo sasa duniani katika ulinzi wa maisha ya binadamu na utamaduni wake.

  Alisema maelfu ya wananchi waliokumbwa na madhila mbalimbali wameweza kutulizwa na wafanyakazi wa kujitolea ambao waliondoa umimi na ubinafsi na kusaidia walio katika matatizo.

  Alisema Umoja wa mataifa ukiwa unathamini amani , haki sawa na maendeleo ya jamii na kwa kuwa na siku ya kujitolea ya kimataifa kunaonesha umuhimu wa juhudi za umoja huo za kusambaza malengo hayo kufanikisha maendeleo na ushiriki wa vijana katika maendeleo yao , kitaifa na kimataifa.

  Katika hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi, Vuzo alisema kwamba shughuli za kujitolea za Umoja wa Mataifa zilianza nchini mwaka 1974 katika misingi ile ile ya kufunza jamii kujitolea kwa manufaa yao na maendeleo ya taifa.
  DSC_0227
  Vuzo alisema programu ya kujitolea ya Umoja wa mataifa ambayo hapa nchini inaitwa UNV inasaidia kufanikisha mikakati mbalimbali inayoendeshwa na serikali ili kuboresha hali ya kujitolea nchini kwa manufaa ya taifa.
  Programu hiyo ikiwa imezingwa na mikakati ya kitaifa ya kukabiliana na umaskini kama MKUKUTA na MKUZA na misaada kwa mipango ya maendeleo ya Umoja wa mataifa UN kuanzia mwaka 2011 – 2016, UNV kwa sasa inajishughulisha na masuala ya wakimbizi, utawala bora, Ukimwi vijana na maendeleo sekta binafsi.
  Alisema UNV ikiwa imetimiza miaka 35 imekuwa ikiwasaidia Watanzania katika sekta hizo ambapo wamekuwa wakifanya kazi kwa moyo mmoja kuhakikisha maisha ya watanzania yanabadilika.
  Aidha ametoa wito kwa vijana kujiunga na shughuli za kujitolea kutokana na umuhimu wake kwao na kwa taifa.
  DSC_0507
  Mkufunzi wa ujasiriamali kutoka shirika lisilola kiserikali la Restless Development, Lawrence Ambokile, akitoa ushuhuda wake kwa vijana wenzake ambapo alisema anajisikia faraja na moyo wake una furaha kwa kufanya kazi za kujitolea kwenye jamii ambapo imemsaidia kukuza uelewa wake na pia ni baraka kwa Mungu.
  DSC_0246
  Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kisui akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma yaliyokutanisha vijana kutoka taasisi na mashirika mbalimbali yasiyoyakiserikali wanaofanyashughuli za kujitolea kwenye jamii.
  DSC_0417
  Vijana wanaofanya shughuli za kujitolea kutoka ndanu na nje ya nchi wakiwa wamekusanyika pamoja kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kujitolea yaliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
  DSC_0077
  Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi (kulia) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kisui, Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakielekea kutembelea mabanda kwenye maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
  DSC_0084
  Mfanyakazi wa Shirika la KOICA, Catherine Tarimo akieleza shughuli mbalimbali wanazofanya ikiwemo kujitolea kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (mwenye suti nyeusi) aliyewamwakilisha Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo. Kushoto kwake ni Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo na kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kisui.
  DSC_0119
  Mwakilishi wa kampuni ya 4Life, Nelson Benges (mwenye tai ya damu ya mzee) akielezea virutubisho mbalimbali vinavyotumika kuimarisha kinga ya mwili wa mwanadamu kwa asilimia 437 na kuufanya mwili imara na uweze kupamba na magonjwa kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi Kulia kwa Bw. Kajugusi ni Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo na kushoto kwake ni Programme Officer wa Shirika la UNV, Bi. Stella Karegyesa.
  DSC_0127
  Mtaalam wa Masoko wa UN Volunteer Kitaifa, Catherine Sinje (wa pili kulia) akieleza shughuli mbalimbali za kujitolea zinazofanywa na shirika lake likiwahusisha vijana zaidi katika kufanya kazi za kujitolea kwenye jamii kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi wakati wa kutembelea mabanda kwenye maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
  DSC_0135
  Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi, akizungumza jambo na wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV) alipokuwa akitembelea mabanda kwenye maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

  Alisema ingawa kujitolea kunawezesha kupata uzoezi ili vijana waweze kuajiriwa na kuendeleza taaluma,maana ya kujitolea haipo katika kuajiriwa bali katika hali ya kuona maana yake katika kusaidia jamii kujitambua na kujituma na kuwajibika .

  “Usaidizi katika jamii ndio muhimu kuliko ajira. Haina maana yoyote kuwa na ajira bila kujua maana yake katika kusaidiajamii,” huku akisisitiza kwamba haina maana yoyote kama umeajiriwa na ukaendekeza umimi huku ukiwa hujali maslahi ya umma hata yanapoharibika.

  Alisema Serikali ikiwa inaamini kwamba chachu ya kujitolea ni vijana ametaka watumie njia mbalimbali katika shughuli za kujitolea kwa kuona wenzetu wanafanya nini na kutumia uzoefu wao katika kujenga taifa imara la Tanzania.

  Aidha alisema wakati umefika wa vijana kusaidia kurejesha moyo wa kujitolea uliokuwepo kabla ya miaka ya 1970 ambapo shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ulifanywa na wananchi wenyewe kwa namna ya kujitolea kuanzia miaka ya 1970 moyo wa kujitolea umepungua sana.

  Kwa picha zaidi ingia hapa

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ushushaji Mizigo Bandarini - Tanzania International Container Terminal (Ticts), Paul Wallace (kulia) akimkabidhi zawadi kwa timu kapteni wa timu ya Operations ambao waliibuka kidedea dhidi ya Workshop kwa kunyakua makombe yote katika michezo mbali mbali iliyochezwa katika Bonanza la Siku ya Familia iliyofanyika mwishoni mwa wiki ndani ya Kiota cha Kunduchi Wet and Wild jijini Dar es Salaam. Lengo la Siku hiyo ilikuwa ni kuwakutanisha wafanyakazi na familia zao zifurahi kwa pamoja.
  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ushushaji Mizigo Bandarini - Tanzania International Container Terminal (Ticts), Paul Wallace akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari.
  Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa akielezea madhumuni ya siku ya familia iliyoandaliwa na TICTS.
  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ushushaji Mizigo Bandarini - Tanzania International Container Terminal (Ticts), Paul Wallace (kulia) akiteta jambo na Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa.

  Salamu zikiendelea...
  Picha ya pamoja na vikombe vyao vya ushindi.

  Michezo kwa watoto ikiendelea.
  Michezo ikiendelea.
  Ilikuwa ni vuta nikuvute mpaka pale Operations walipowatoa mchuzi Workshop.
  Mchezo ulinogeshwa na lile shindano la kukamata kuku.
  Familia zikipata chakula pamoja.
  Maongezi ya hapa na pale yalikuwepo.
  Mashindano ya kuogelea nayo yalishika hatamu.
  Mpira wa mikono nao ulinoga.

  0 0

  DSC_0001

  Balozi wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania kwenye hafla maalum ya kuwakaribisha na kuwapongeza wanajeshi wa kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta chini ya kamanda Peter Christian Semrau (kulia) iliyofanyika ndani ya meli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

  KAMANDA wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta, Peter Christian Semrau, amesema jumuiya ya kimataifa imepata mafanikio makubwa kwa kuwezesha njia inayotumika sana na meli kuwa salama.

  Akizungumza katika mahojiano ndani ya meli hiyo ambayo imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, Kamanda Semrau alisema kwamba kwa mwaka huu hapakuwepo na tukio kubwa ambalo limetikisa eneo hilo la Pwani ya Pembe ya Afrika inayopakana na Somalia na Yemen.

  Alisema kuanzia shughuli za kimataifa kukabili uharamia na ujambazi baharini kuanza mwaka 2009 kumekuwepo na ushindi wa kimataifa kutokana na kuendelea kupungua kwa matukio katika eneo hilo ambapo awali ilikuwa ni tishio kubwa.
  Alisema pamoja na kupungua kwa matukio ya kijambazi na utekaji nyara kazi ambayo inatarajiwa kufanywa mwakani ni kuhakikisha kwamba mataifa yanayopakana na bahari ya Hindi yanawezeshwa kujilinda yenyewe dhidi ya matukio ya baharini.
  DSC_0004
  Pichani juu na chini baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania na mabalozi mbalimbali waliojumuika kwenye hafla hiyo wakisiliza risala ya Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke (hayupo pichani).

  Meli hiyo ambayo inafanya doria kuanzia kaskazini mwa Afrika hadi Kusini imetia nanga Dar es salaam ikitokea Madagascar ambako nako ilipata mapokezi makubwa. Operesheni Atalanta inaendeshwa na vikosi vya Umoja wa Ulaya vikilinda eneo la bahari ambalo lina shughuli nzito kwa meli za biashara.


  Meli hiyo ambayo itakuwa katika operesheni hadi februari mwakani itapokewa kazi hiyo na meli nyingine ya FGS Bayern. Naye Balozi wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke akizungumza na waandishi wa habari akiwakaribisha katika melivita hiyo alisema kwamba amefurahishwa na mchango wa taifa lake katika kuhakikisha pwani ya Bahari ya Hindi upande wa Afrika inakua salama na watu wanapata huduma zinazotakiwa.
  DSC_0005
  Alisema moja ya kazi kubwa ya meli hiyo ni kusindikiza meli zenye vyakula au huduma mbalimbali za kijamii kwa mataifa ambayo yanashida ili kupunguza maumivu.
  Alisema pamoja na meli hiyo kutia nanga Dar es Salaam kuonesha ushirikiano wa kutosha kati ya taifa lake na Tanzania, anatarajia mwakani mahusiano ya Tanzania na Ujerumani yatazidi kuimarika hasa katika nyanza za hifadhi na maendeleo ya jamii.
  Aidha balozi huyo alisema kwamba taifa lake linaongeza fedha zaidi kwa ajili ya uanzishaji wa mamlaka ya wanyamapori nchini Tanzania kwa lengo la kuifanya iwe na nguvu na uwezo wa kulinda wanyama hao.
  Pia alisema inafikiria namna ya kufanya na meli ya MV Liemba ambayo alisema ni moja ya vielelezo hai vilivyopo vyenye maana kubwa katika uhusiano wa Tanzania na Ujerumani.
  DSC_0006
  Alisema meli hiyo inafaa kufanyiwa ukarabati ili kuweza kutoa huduma kandoni mwa ziwa Tanganyika.
  Aidha alisifu ukuaji wa demokrasia nchini Tanzania hasa kwa kuzingatia uhuru uliopo wa vyombo vya habari na majadiliano yenye afya bungeni yenye lengo la kujenga taifa lenye nguvu.
  Aidha alisema Ujerumani itaendelea kukuza uhusiano na Tanzania ambayo ni nanga ya usalama kwa mataifa ya Afrika Mashariki na ukanda wa Bahari ya Hindi kwa upande wa Afrika.
  DSC_0015
  Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke akifanya cheers na mmoja wa makamanda wa jeshi la wanamaji kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika ndani ya meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck inayofanya doria ya kubaini maharamia kwenye pwani ya ukanda wa Bahari ya Hindi.
  DSC_0017
  Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha maji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck kwenye hafla maalum ya kuwapongeza na kuwakaribisha nchini Tanzania iliyoandaliwa na ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania.
  DSC_0022
  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa maafisa wa bandari ya Dar es Salaam.
  DSC_0029
  Sehemu ya muonekano wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck wakati hafla ya kuupongeza msafara wa kikosi cha wanamaji wa jeshi la Ujerumani kilichoongozwa na Kamanda Peter Christian Semrau.
  DSC_0030
  Baadhi ya makanda wa kikosi cha wanamaji wa jeshi hilo wakilinda lango kuu la kuingia ndani ya meli hiyo.
  DSC_0036
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wanakikosi cha maji wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck iliyotia nanga kwenye bandari ya Dar es Salaam.
  DSC_0038
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akihoji jambo kwa mmoja wa wanakikosi cha maji wa meli ya kivita ya ya Ujerumani FGS Lübeck ambaye jina lake halikuweza kufahamika kiurahisi.
  DSC_0032
  Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.
  DSC_0071
  DSC_0065
  Kamanda Peter Christian Semrau anayeongoza kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa.
  DSC_0057
  Wageni waalikwa wakiendelea kupata picha ya kumbukumbu na Kamanda Peter Christian Semrau anayeongoza kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta kubabili maharamia.
  DSC_0059
  Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke katika picha ya pamoja na Afisa wa kitengo cha habari Ubalozi huo, John Meirikion.
  DSC_0069
  Pichani ni baadhi ya wageni waalikwa wakipata picha ya pamoja ndani ya meli hiyo ya kivita.
  DSC_0070
  Afisa wa kitengo cha habari Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania, John Meirikion akipata picha ya pamoja na mmoja wa wageni waalikwa ndani ya meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck iliyotia nanga bandari ya Dar es Salaam.

  0 0


   Meneja Msaidizi wa Uwekezaji na Biashara Kubwa wa Benki ya Exim, Thobius Samwel (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo juu ya huduma za kibenki zitolewazo na benki yake  kwa washiriki wa shindano la Gofu liloandaliwa kwa watendaji wakuu wa makampuni mbali mbali jijini Dar es Salaam lililofanyika katika viwanja vya Gofu vya Lugalo, mwishoni mwa wiki jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Afisa Mauzo, wa benki hiyo Bw. Ishaq Samailla. Benki ya Exim ilikuwa miongoni mwa wadhamini.
   Meneja Msaidizi wa Uwekezaji na Biashara Kubwa wa Benki ya Exim, Joseph Lema (katikati) akichukua moja ya vipeperushi vyenye maelezo juu ya huduma za kibenki zitolewazo na benki yake, kumpatia mshiriki wa shindano la Gofu liloandaliwa kwa watendaji wakuu wa makampuni mbali mbali jijini Dar es Salaam lililofanyika katika viwanja vya Gofu vya Lugalo, mwishoni mwa wiki jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Afisa Mauzo, wa benki hiyo Bw. Ishaq Samailla.Benki ya Exim ilikuwa miongoni mwa wadhamini.
   Meneja Msaidizi wa Uwekezaji na Biashara Kubwa wa Benki ya Exim, Joseph Lema (katikati) akitoa maelezo juu ya huduma za kibenki zitolewazo na benki yake, kwa mmoja wa washiriki wa shindano la Gofu liloandaliwa kwa watendaji wakuu wa makampuni mbali mbali jijini Dar es Salaam lililofanyika katika viwanja vya Gofu vya Lugalo, mwishoni mwa wiki jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Afisa Mauzo, wa benki hiyo Bw. Ishaq Samailla.Benki ya Exim ilikuwa miongoni mwa wadhamini.
  Meneja Msaidizi wa Uwekezaji na Biashara Kubwa wa Benki ya Exim, Thobius Samwel (kulia) akitoa maelezo juu ya huduma za kibenki zitolewazo na benki yake  kwa washiriki wa shindano la Gofu liloandaliwa kwa watendaji wakuu wa makampuni mbali mbali jijini Dar es Salaam lililofanyika katika viwanja vya Gofu vya Lugalo, mwishoni mwa wiki jijini Dar Es Salaam.

  0 0


  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe na Garry Hutchinson Mkurugenzi wa Biashara wa timu ya ligi kuu ya Uongereza ya Sunderland wakionyesha jezi ya iliyoandikwa Tanzania yenye rangi za timu hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa matangazo ya Utalii wa Tanzania yanayotangazwa katika uwanja wa timu hiyo huko Sunderland04Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe katikati akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Bodi ya Utalii kutoka kulia Meneja wa Masoko wa (TTB) Bw. Geofrey Meena, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi na kutoka kushoto ni Mdau wa Utalii Bw. Nesto Mapunda na Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Teddy Mapunda4Wachezaji wa timu ya Sunderland wakipasha mwili huku wakiwa wamevalia fulana nyeusi zenye maandishi yanayotangaza na kukaribisha watalii na kutangaza utalii nchini Tanzania.5Matangazo yakiendelea kuonyeshwa kwenye mbao za matangazo wakati mchezo kati ya Chealsea na Sunderland ukiendelea.6Fulana zinazotangazo utalii wa Tanzania ikiwa zimewekwa kwenye vyumba vya kubadilishia jezi wachezaji wa timu ya Sunderland.7Majarida yanayotangaza utalii wa Tanzania yakiwa yamesambazwa kwenye meza katika mgahawa wa timu ya Sunderland kwenye uwanja wao wa Sunderland8Mabango na yanayotangaza utalii wa Tanzania yakiwa yamewekwa kwenye makumbusho ya timu hiyo.9Haya ni baadhi ya mabango yanayoonyeshwa katika uwanja huo wakati wa michezo ya Ligi kuu.10Bendera yenye maandishi ya kukaribisha watalii kutembelea Tanzania ikiwa imepandishwa katika miliongoti katika lango kuu la uwanja huo.

  0 0

   
   Sehemu ya meza kuu,kutoka kulia ni Imam Abbasi Maunda  (mdau), Bi Halima Mamuya (mdau), Balozi Amina Salum Ali (mgeni rasmi), Fatma Khalfan (Mwenyekiti wa bodi), Juma Omari (mkuu wa shule) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mahafali hayo ya kidato cha nne,yaliyofanyika mwishoni mwa wiki,Temeke jijini Dar.
  Mkuu wa Shule ya sekondari Twayyibat,Juma Omari akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa mbalimbali,waliofika kwenye hafla hiyo ya mahafari iliyofanyika mwishoni mwa wiki Temeke,jijini Dar.
  Mwenyekiti wa Bodi,Bi Fatma akizungumza machache kwenye hafla ya mahafari ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya Twayyibat,Temeke jijini Dar,iliyofanyika mwishoni mwa wiki. bi
   Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nee wa shule hiyo wakitoa burudan ya igizo
   Mmoja wa wanafunzi aliyehitimu,akipokea cheti chake wakati wa mahafali shuleni hapo
  Pichani ni mmoja wa Wanafunzi,Sada Abubakar akipokea cheti cha Mwanafunzi bora

  0 0

  KAMPUNI ya Msama Promotions imeanza rasmi kusambaza Dvd ya Uniongoze ya nyota wa nyimbo za injili nchini Zambia, Ephraim Sekeleti tangu mwezi Novemba mwaka huu. Akizungumza na Dira ya Mtanzania, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama DVD hiyo ina nyimbo nane  ambazo ameziimba katika lugha ya Kiswahili.

  Msama alisema hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki wa injili kutoka kwa muimbaji huyo anayetamba na kibao cha ‘Uniongoze’ imeingia sokoni kwa kishindo kutokana na ubora wa albamu hiyo.

  Alisema msanii huyo kutoka Zambia alijizolea umaarufu hapa nchini baada ya kushiriki kwenye matamasha ya Pasaka na Krismasi kutokana na uwezo wake wa kumiliki jukwaa pamoja na sauti yake. Msama albamu hiyo ya Uniongoze imetayarishwa na Msama Video Productions na kusambazwa na Msama Promotions ambayo ina ubora wa hali ya juu, hivyo mashabiki na waumini mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujionea kazi zilizofanywa na kampuni hizo.

  Aidha Msama alijipambanua kwa kueleza kwamba inapatikaba kwenye maduka ya Msama yaliyopo Kariakoo mtaa wa Masasi na Msimbazi na Posta mtaa wa Mkwepu. Nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni Uniongoze, Baraka za Mungu, Kidonge cha Yesu, Wewe uko, Ndani ya jina, Kuna wakati Nachoka, Mungu mwenyewe na Ephraim Sekeleti interview.

  0 0
  0 0


  Mipawa to GhanaMeneja wa kituo cha Kahama FM Redio, Marco Mipawa (kushoto) akielekea kukwea pipa kuelekea nchini Ghana kwenye ziara ya mafunzo ya wiki mbili.

  Na Marco Mipawa, Accra- Ghana.
  Tanzania inaweza kuwa nchi ya kwanza katika maendeleo ya uchumi iwapo itaweka sera madhubuti za uzalishaji wa Gesi na kuwa na viongozi wenye dhamira dhabiti ya kuiendeleza nchi na kuboresha maisha ya watu.

  Haya yamebainishwa na Meneja wa Redio Kahama FM Marco Mipawa leo wakati akiendelea na ziara ya mafunzo nchini Ghana ya kujionea jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi na jamii katika suala zima la maendeleo.Mipawa ameyasema hayo baada ya kuona kuwa nchi ya Ghana inalo tatizo kubwa la upatikanaji wa nishati ya umeme hata kuliko Tanzania inavyoathirika na tatizo hilo lakini maisha ya watu ni mazuri na uchumi uko juu.

  Amesema, katika jiji la Accra umeme hukatika takriban robo tatu ya siku na matumizi ya jenerata ni makubwa lakini thamani ya pesa yao iko kubwa ikilinganishwa na ya Tanzania ambapo kukatikakatika kwa umeme ni mara chache. Mipawa amesema, dola moja ya marekani inathamanishwa na Sedisi tatu za Ghana ikiwa ni sawa na Shilingi 1770 za Tanzania hali inayoonyesha uchumi wa Tanzania uko chini ukilinganishwa na wa Ghana.

  Baadhi ya wananchi wa Accra wamemwambia Mipawa kuwa, kinachoisaidia nchi ya Ghana ni Uzalishaji mali katika kilimo, madini na ufugaji; huku sera na sheria za nchi zikisimamiwa kwa umakini mkubwa kwa maslahi ya nchi. Wamesema suala la kudhibiti rushwa na kusimamia utii wa sheria vikiambatana na uwazi na ukweli wa serikali na viongozi wa Ghana, ndiyo silaha mahususi zilizoifanya Ghana kuwa na uchumi imara na maisha mazuri ya watu.

  Ziara ya mafunzo ya wiki mbili ya kujionea utendaji wa vyombo vya habari nchini Ghana, imehusisha watu tisa kutoka Tanzania wakiwemo waandishi wa habari na viongozi wa vyombo vya habari mbalimbali kwa udhamini wa Tanzania Media Fund (TMF).

  0 0  0 0

  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi  huduma mpya ya HOME WI-FI itakayowawezesha wateja wake watumiaji INTANETI kufurahia kutumia kifurushi kimoja familia nzima kwa kuwaunganisha na Wi-fi watu 32 ndani ya familia na kuunganisha wanafamilia wengine wanne waliopo mahali popote nchini Tanzania  kufurahia internet ya 3.75G.  kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Home WiFi,Gaurav Dhingra.
  Meneja Masoko wa Airtel Home WiFi,Gaurav Dhingra (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi  huduma mpya ya HOME WI-FI itakayowawezesha wateja wake watumiaji INTANETI kufurahia kutumia kifurushi kimoja familia nzima kwa kuwaunganisha na Wi-fi watu 32 ndani ya familia na kuunganisha wanafamilia wengine wanne waliopo mahali popote nchini Tanzania  kufurahia internet ya 3.75G.  Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Jackson Mmbando na kushoto ni Ofisa Masoko wa Airtel Tanzania,Ndevonaeli Eliakimu.
  Airtel Tanzania leo imezundia huduma ya kwanza ya kibunifu nchini ijulikanayo kama “Home WiFi with bundle share” (WiFi ya nyumbani na kufurushi cha pamoja) itakayowawezesha watanzania na wateja wa Airtel kupata huduma ya Wi-Fi na kuunganisha zaidi ya vifaa vingine 32 vitakavyotumia WiFi .

  Huduma hii vilevile itaunganisha hadi simu 4 za mkononi zilizoko kokote nchini kwenye akaunti moja na kuwapatia internet ya kasi ya 3.75G.  hii inamaanisha kifurushi cha internet kilichopo kwenye kifaa cha WiFI ya nyumbani  sasa kitakuwa na matumizi mawili yaani Wifi ya nyumbani na internet kwenye simu za mkononi pindi mteja akiwa  nje ya nyumbani

  kwa sasa wanafamilia na watumiaji wa intenet Tanzania hawana haja ya kununua vifurushi vya intenet kwa kila simu , kompyuta, Television au vifaa vyovyote vinavyoweza kuunganishwa na internet na badala yake watakachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi kwenye WiFi ya nyumbani na kuwawezesha kila aliyeunganishwa na kifaa hicho kupata kifurushi chake kulingana na gawiwo alilowekea na hivyo kutumia kifurushi kimoja

  ili kujipatia kifaa hichi cha HOME WiFi unaweza ukalipia : shilingi 195,000/-  na kupatiwa kifurushi cha kuanzia cha 40 GB  kwa mwenzi au unaweza kulipia shilingi 250,000/- na kupatiwa kifurushi cha kuanzia cha 120 GB  kwa mienzi mitatu, Aina zote mbili za ofa zinatoa huduma ya kutumia kifurushi kimoja na kuunganisha wanafamilia wanne wenye simu za mkononi ya malipo ya awali (prepaid line)

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja masoko na bidhaa hii wa Airtel Bw, Guarav Dhingra alisema” Dunia inabadilika na kukua kwa kasi ndivyo ilivyo kwa matumizi ya internet, kwa sasa internet si kwa ajili ya baba na mama, bali ni muhimu kwa familia nzima ikiwa ni pamoja na watoto kwaajii ya burudani, masomo,  na nyingine nyingi.  Ongezeko kubwa la simu za kisasa, komputa ndogo, Television za Kisasa, saa za kisasa, tablet katika nyumba zetu ni ushahidi tosha wa hili.

  Wakati ongezeko na upatikanaji wa vifaa hivi ukiwa rahisi,  njia za kuunganiswa na huduma za internet zinazidi kuwa ngumu kwa wateja,  kwani inamgharimu mteja kuwa na simcard kwa kila kifaa, na kila simcard inabidi kusajiliwa na kuwekewa muda wa maongezi wakutosha , kisha kuingiza namba maalumu na kuchangua kirufushi na ndipo kuanza matumizi.

  Airtel kwa kuona hii changamoto imekuja na huduma ya WiFi ambapo sasa unaweza kuunganisha vifaa hivi vyote kupitia kifaa cha WiFi cha nyumbani  na kupata intenet ya kasi bila kuhitaji simcard yoyote ya ziada.  Na tumewawezesha wanafamilia kuweza kuongeza kifurushi cha intenet kwa kupiga *148*20# na kuunganishwa na kifurushi kimoja

  Tunaamini familia nyingi zaidi nchini Tanzania watafurahia na kutumia huduma hii ya pekee toka Airtel na hivyo kutuamasisha kuongeza huduma nyingi za kibunifu za  internet” aliongeza Guarav Dhingra

  Huduma hii inapatikana kwa kupiga 0784104800 ambapo utaweka oda yako kwajili ya kupata kifaa hiki cha  WiFi ya nyumbani, na  kisha Airtel itakuletea mahali ulipo na kukunganisha na huduma hii.


  0 0


  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi  Ngoma Africa Band almaarufu FFU-Ughaibuni yenye makao nchini Ujerumani,inawatakia kila la heri katika kusherehekea miaka 53 ya Uhuru . Salam hizi za heri ya 9 Disemba ziwafikie watanzania wote walio nyumbani na nje ya nchi.Ngoma Africa band chini ya uongozi wake Kamanda ras Makunja unaweza kuwasikiliza pia katika kambi yao ya FFU-ughaibuni bofya http://www.ngoma-africa.com  pia at https://itunes.apple.com/album/id947329929 au 

  0 0

   Naibu waziri wa fedha Adam Malima akimkabidhi meneja wa fedha wa benki ya CRDB Sosteness Biseko  tuzo  ya NBAA ya ushindi  katika  uandaaji wa taarifa bora za fedha mwaka 2013-2014,jumla ya benki tisa zilishiriki ambapo Benki ya CRDB iliibuka mshindi wa kwanza katika kundi la mabenki, hafla hiyo ilifanyika juzi katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha
  *********

  Mashirika binafsi ,taasisi na idara mbalimbali za serikali zimehimizwa   kushiriki katika mashindano ya tuzo zinazotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA katika uandaaji bora wa taarifa za fedha za mwaka ili kuboresha hesabu za mashiriki hayo na kuongeza uwazi katika shughuli za biashara za ndani ya nchi na kimataifa 

  Mwenyekiti wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA Profesa Issaya Jairo ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati wa kufunga  mkutano mkuu wa mwaka wa bodi hiyo ulio enda sambamba na utoaji wa tuzo na vyeti kwa washindi  katika uaandaaji  bora wa taarifa za fedha za mwaka ambapo kwa mwaka 2014 jumla ya washiriki 40 walishiriki ambao waligawanywa katika makundi 11 kulingana na huduma wanayo itoa


  Katika kundi la mabenki, benki ya crdb ilibuka mshindi  wa kwanza kwa mwaka2013-2014 na kupata tuzo maalumu ya uandaaji  wa taarifa bora  za fedha za mwaka iliyokabidhiwa na naibu waziri wa fehda Adam Malima  kwa meneja wa fedha wa benki hiyo Sosthenes Biseko ambaye akizungumzia ushindi huo amesema ni njia mojawapo ya kuudhihirishia umma wa watanzania kuendelea kuwa na Imani na benki.
  Wafanyakazi mbalimbali wa benki ya CRDB wakiwa katika picha wakati wa makabidhiano hayo.

  0 0


   Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Profesa Abdulkarim Mruma (kushoto waliokaa) na Naibu Mkurugenzi Mkuu  wa  Kurugenzi ya Utafiti wa Madini ya  Uturuki Dkt. Abdulkerim Yorukoglu ( kulia waliokaa) wakisaini makubaliano ya  awali (MoU) kwa ajili ya ushirikiano wa taasisi hizo katika masuala ya  utafutaji wa madini na ubadilishanaji  wa ujuzi, uzoefu na teknolojia.  Waliosimama kushoto ni Kamishna Msaidizi  wa Madini, Ukaguzi wa Migodi  Mhandisi Ali Samaje na kulia ni  Balozi wa Uturuki Nchini, Ally Davutoglu.
   Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akisisitiza jambo  kwenye ufunguzi  wa kikao kwa ajili ya kusaini  makubaliano ya awali (MoU) kati ya  Kurugenzi ya Utafiti wa Madini ya  Uturuki na Wakala wa Jiolojia  Tanzania  (GST)

   Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Profesa Abdulkarim Mruma akielezea  majukumu ya wakala huo katika kikao hicho.
  Kamishna Msaidizi  wa Madini, Ukaguzi wa Migodi  Mhandisi Ali Samaje akielezea aina  za madini  yanayopatikana nchini Tanzania katika kikao hicho.


   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akielezea mchango wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) katika nishati ya umeme nchini  pamoja na mikakati ya  Serikali katika kuhakikisha kuwa nishati hiyo inakuwa ni ya uhakika. Kulia ni Balozi wa Uturuki Nchini Ally Davutoglu.
   Mmoja wa washiriki wa kikao hicho  kutoka ujumbe wa Uturuki  akichangia mada katika kikao hicho.
   Baadhi ya washiriki kutoka ujumbe wa Uturuki  wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inatolewa na Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Profesa Abdulkarim Mruma (hayupo pichani)

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Uturuki Nchini Ally Davutoglu.

older | 1 | .... | 421 | 422 | (Page 423) | 424 | 425 | .... | 1898 | newer