Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 420 | 421 | (Page 422) | 423 | 424 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Magolikipa wa Simba, Manyika Peter na Ivo Mapunda  wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya The Express ya Uganda, katika mchezo huo timu hizo hazikufunga. 
  (Picha zote na Francis Dande)
  Katongole Henry akimtoka mshambulia wa Simba, Ramadhani Singano 'Mess'.
  Kipa wa The Express, Mutumba Ivan akiruka juu kuokoa moja ya hatari langoni mwake.
  Beki wa Simba, Nasoro Masoud akimtoka mchezaji wa The Express ya Uganda wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

   Ramadhani Singano 'Mess' akitafuta mbinu za kumtoka beki wa The Express, Katongole Henry.
  Kipa wa The Express ya Uganda, Mutumba Ivan.
  Elius Maguri akipata matibabu baada ya kuumia.

  0 0

  Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia ) Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu Mhe. Peter Serukamba , Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar, Dk. Juma Akir (kushoto) Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafii wa Anga Tanzania(TCCA) ambaye pia ni Msaidizi wa Rais wa Mambo ya Kanda, Dk. Nyamajeje Weggoro, wakishirikiana kukata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la TCAA. Uzinduzi huo ulikua sehemu ya maadhimisho ya Siku yaKimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD)
  Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe, akizindua jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Uzinduzi huo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD). Anayeshuhudia kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu TCAA, Bw. Charles Chacha.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Charles Chacha(Kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD) yaliyofanyika kwenye viwanja vya TCAA. Katiti ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Peter Serukamba.

  0 0

    Mwenyekiti wa Muda wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (kulia), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya Jumuiya ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo. 
  Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers).  Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya muda kutoka Zanzibar, Othman Maulid "Mapara".
   Katibu Msaidizi wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha (kushoto),akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa mapitio ya rasimu hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Kamati,  Henry Mdimu.
   Mwenyekiti wa Muda wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (wa pili kushoto), wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya Jumuiya ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo. Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Jumuiya ya  Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers). Kutoka kushoto ni Mjumbe, Othman Maulid, Katibu Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha,  Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe) na William Malecela (Mjumbe).
  Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao uliofanyika katika Mgahawa wa MOG Lounge, jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

  0 0
 • 12/05/14--21:08: USIKUBALI KUIBIWA
 • Wristbands in Tanzania,High Quality Wristbands


  0 0

  KATIBU Mkuu wa CCm Ndg. Abdulrahaman Kinana , amekipongeza Chama Cha ZANU PF Cha Zimbabwe kwa kusimama imara licha ya Changamoto mbalimbali zinazoikabili Zimbambwe ikiwemo vikwazo vya kiuchumi ambavyo vimewekwa dhidi ya nchi hiyo.

  Amewataka wana ZANU PF kuendelea kuunga mkono chama chao na kuongeza mapambano dhidi ya maadui wote wanaotaka kurudisha nyuma jitihada za kupigania maslahi ya nchi yao.

  Akisoma salamu za mshikamano za Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano Mkuu wa ZANU PF unaofanyika mjini Harare Ndg. Kinana aliwakikishia wana ZANU PF na wana Zimbabwe wote kuwa katika mapambano hayo CCM iko nyuma yao na kwamba haitaacha kupaza sauti dhidi ya vikwazo vya uchumi ilivyowekewa Zimbabwe.

  Alisema vikwazo hivyo having uhalali na kwa ujumla wake vinatoa adhabu isiyo ya haki kwa Wananchi wa Zimbabwe wasio na hatia.

  Ndugu Kinana alimpongeza Rais Mugabe ujasiri na kwa msimamo wake usioyumba wa kupigania maslahi ya wana Zimbabwe licha ya vitimbi vya wapiga maendeleo.

  Alisema ujasiri na msimamo wa Mugabe pamoja na Chama anachokiongoza Cha ZANU PF ndiyo uliowezesha Zimbabwe kusimama ilivyo hivi sasa kama Taifa huru na lisilikubali kuyumbishwa.

  Alisema Mugabe na Chama chake wameonyesha kwa mfano kwamba kumbe watu wakisimama imara chini ya uongozi wa chama imara hakuna anayeweza kukwamisha nyendo zao za kimapinduzi zinazoendana na matakwa ya umma.

  Akizungumzia ushindi wa kishindo wa ZANU PF kwenye uchaguzi Mkuu June mwaka jana Kinana alisema hicho ndicho kiashiria cha kukubalika kwa Chama na sera zake.

  Alisema CCM inaipongeza ZANU PF kwa ushindi huo na kwamba wana CCM wanajisikia fahari sana wanapoona ZANU PF ikiendelea kukua na kuimarika.

  Aisha Ndg. Kinana alimpongeza Rais Mugabe na kueleza kuwa CCM na Watanzania kwa ujumla wanafurahishwa na msimamo wa dhati alionyesha Rais Mugabe katika majukwaa mbalimbali ikiwemo mkutano wa wakuu wa nchi za SADC uliofanyika Victoria Falls wa kueleza umuhimu wa kutambua na kuheshimu mchango wa Mwalimu Nyerere katika ukombozi wa Afrika na hasa kusini mwa Afrika.

  Hotuba ya Ndg. Kinana ilipokelewa kwa shangwe na furaha kubwa sana na wajumbe wa mkutano huo ambao mara kwa mara walishangalia kuashiria kuridhika na kauli za kimapinduzi na kidugu kutoka kwa wana CCM.

  Ndugu Kinana na ujumbe wake wataondoka kesho kureke nyumbani. Ujumbe wa Katibu Mkuu kwenye mkutano ulimhusisha pia Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa CCM Ndg. Phares Magesa na afisa wa makao makuu ya CCM Ndg. Thobias Mwilapwa.
   Ndg. Kinana akihutubia mkutano Mkuu wa ZANU PF
  Ndg. Kinana akisalimiana na Rais Robert Mugabe mara baada ya kuhutubia mkutano huo.

   Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Ndg. Kinana , Balozi wa Tanzania Zimbabwe na Mjumbe wa NEC Ndg. Magesa wakishiriki katika mkutano huo
   Baadhi ya viongozi mashuhuri na wajumbe walihudhuria mkutano huo

   

  0 0

  Mgeni rasmi Ofisa Uendeshaji, Rasirimali watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Collins Constantine, akishishirikiana na wafanyakazi wenzake wa TBL kuwasha mishumaa kuwakumbuka wenzao waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa Ukimwi.
    Mgeni Ofisa Uendeshaji, Rasirimali watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Collins Constantine akikabidhi zawadi ya jiko la gesi kwa Christopher Mchome, baada ya kushinda bahati nasibu ya wafanyakazi waliopima afya zao, wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi, Dar es Salaam juzi.
   Mchome akisaidiwa na wenzake kubeba jiko baada ya kushinda bahati nasibu ya wafanyakazi wa TBL.

   Wasanii wakitoa burudani ya michezo mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo kwa wafanyakazi wa TBL.

   Wafanyakazi wa TBL wakisubiri kwa shauku kubwa zawadi zilizotolewa na kampuni hiyo ili zichezeshwe bahati nasibu kwa wafanyakazi waliopima afya zao kwa hiari.
   Wakiwa na shauku ya kupata zawadi, wafanyakazi wa TBL wakipata kinywaji huku wakisubiri bahati nasibu iliyoandaliwa na kampuni hiyo, wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi.

   Mfanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, Joel Saganya akiwa mwenye furaha baada ya kushinda gogoro.
   Wasanii wakionyesha umahili wao wa kucheza Sarakasi
  Sarakasi ilikuwa moja ya michezo iliyowavutia wafanyakazi wa TBL
  Wakiwa na shauku ya kupata zawadi, wafanyakazi wa TBL wakipata kinywaji huku wakisubiri bahati nasibu iliyoandaliwa na kampuni hiyo, wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulimalik Mollel, akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani)

  Kampuni ya Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Wizara ya Elimu na Ufundi pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) wameandaa maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya elimu (TIEE) yanayotarajiwa kufanyika Disemba 17 hadi  21 mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Global link Education, Abdulmalik Mollel, alisema lengo la maonyesho hayo ni kutambulisha wadau wa elimu kwa pamoja ili kuweza kutoa huduma ya pamoja kwa wananchi na kuwaelimisha juu ya mambo muhimu yaliyopo katika kila sekta.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Tred), Jacqueline Mneney, akizungumza jambo.

  Alisema ushiriki wa asasi mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafsi utakuwa na chachu ya mabadiliko ya elimu kwa kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney, alisema wakati umefika kwa Watanzania kujua umuhimu wa maonyesho ya Elimu maana yamekuja kutatua matatizo mbali mbali waliyokuwa wakiyapata wazazi pindi wanapokuwa wanawatafutia shule na vyuo watoto wao.

  Aidha alisema maonyesho hayo yataleta manufaa makubwa na changamoto chanya hasa katika kuongeza ushindani katika sekta ya elimu ambayo itasaidia mpango wa matokeo makubwa sasa. Maonesho hayo yanatarajiwa kupata washiriki zaidi ya 500 na wananchi mbalimbali zaidi ya 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi.

  Kauli mbiu ya maonesho hayo ni ‘KUWEKA JITIHADA ZA PAMOJA KATIKA KUBORESHA MFUMO WA ELIMU TANZANIA NI NJIA THABITI YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA TAIFA.’

  0 0  Leo ni siku ya kuzaliwa blogger Geofrey Adroph kwa jina maarufu ni PAMOJA BLOG .
  Kwanza kabisa natoa shukrani kwa mwenyezi mungu kwa kunifikisha leo  tarehe 06 mwezi wa 12 maana ndio kumbukumbu yangu ya kuingia duniani.
  Namshukuru mama yangu mzazi aliyanizaa na kunilea mpaka hapa nilipo ni kwa uwezo wake nampenda sana mama yangu.
  Nawashuku sana ndugu zangu wote kwa support wanazonipa ili nifikie malengo niliyojiweke na Pia sina budi kuwashukuru Mablogger wanaonipa support ya nguvu maana bila ninyi mablogger sidhani kama kazi hii ingeendelea mpaka kufikia hapa na pia kuna baadhi yao unielekeza kwa kunikosoa hata kunifundisha ni kipi cha kufanya il niweze kufikia malengo,
  Na pia washukuru wadau wetu wanaotembelea Blog Yetu ya Pamoja Blog  maana bila nyie mimi nisingekuwa nafanya kazi hizi.  
  Asanteni sana na pia nawapenda sana munguawalinde na awasimamie katika ujenzi wa taifa letu

  0 0

   Mkurugenzi wa kampuni ya statoil-tanzania bwana Oystein Michelsen iliyofanyika katika ukumbi wa Zanzibar uliopo Hyatt Regency Dar es Salaam.
   Balozi wa Norway nchini Tanzania Mh Hanne Marie Kaarstad akinena jambo wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashujaa wa kesho  iliyofanyika katika ukumbi wa Zanzibar uliopo Hyatt Regency Dar es Salaam.
  Bwa. Nassibu H. Lilumba ambaye ndiye Mshindi wa kwanza aliyejishindia dola 5000.

  Kampuni ya Statoil Tanzania imewatangaza na kuwazawadia washindi wa shindano la Mashujaa wa Kesho katika hafla iliyofanyika siku ya Alhamisi Desemba 4. Mashujaa wa Kesho ni shindano la biashara lililoandaliwa kwa lengo la kukuza dhana ya ujasiriamali kwa vijana mkoani Mtwara.

  Bwana Nassibu Hamimu Lilumba ameibuka mshindi wa shindano la Mashujaa wa Kesho baada ya kutoa wazo la biashara na kIsha kuandaa mpango wa biashara na kutoa maelezo yake katika jopo la majaji. Mshindi alizawadiwa fedha taslimu za Kitanzania zenye thamani ya dola elfu tano (5,000) za Kimarekani katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

  Mpango wa biashara uliolenga kufungua kampuni ya utoaji wa huduma za boda boda kwa utaalamu mkoani Mtwara, uliibuka mshindi kutokana na vigezo ambavyo ni kama vile fursa katika soko, kiwango cha ushindani wa mwenye wazo, uwezo wa kusimamia biashara, uelewa wa masuala ya fedha pamoja na fursa za uwekezaji.

  Sosthenes Njelekela, Zawadi Yusuph Washaru, Vivian Charles na Ali Hassan waliingia katika hatua ya fainali na kupatiwa zawadi zao. Kila mshiriki aliyeingia katika fainali alijipatia fedha taslimu za Kitanzania zenye thamani ya dola elfu moja (1,000) za Kimarekani.

  Shindano lilipata muitikio mkubwa kutoka kwa vijana wa Mtwara ambapo vijana 500 wenye mawazo mbalimbali ya kibiashara katika kilimo, ufugaji wa wanyama na kuku, teknolojia ya habari na mawasiliano, viwanda vidogo na huduma nyinginezo za kibiashara walishiriki. Baadhi ya mawazo hayo yalitoka kwa washiriki mmoja mmoja na mawazo mengine yalitoka kwenye vikundi, kama vigezo vya ushiriki vilivyoelezea.

  Washiriki 40 waliofanikiwa kuvuka mchujo wa awali walipatiwa mafunzo ya ujasiriamali ambapo waliweza kujifunza kuhusu njia za kuandaa na kuendesha biashara kwa ufanisi na namna ya kuandaa mipango ya biashara kutokana na mawazo yao ya biashara. Mipango hiyo ya biashara ilikusanywa na kupitiwa kabla ya mipango kumi ya biashara kupelekwa kwa majaji ili kupata mipango mitano ya biashara kuelekea kwenye fainali. Washiriki wa mipango hiyo mitano walitakiwa kutetea mipango yao ya biashara mbele ya majaji.

  Jopo la majaji watano liliongozwa na Bi. Victoria Tunu Chale, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa People Dynamics Tanzania LTd na Mhandisi, Bwn. Andrew Mnzava ambaye ni mtaalamu kutoka Tanzania Renewable Energy Association, Bwn. Mosses Nkanda, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Mnazi Bay Consulting Ltd ya Mtwara pamoja na Bwn. Justine Lusasi, Mkufunzi Msaidizi kutoka chuo cha Stella Maris ambaye alishiriki kwa ukaribu katika kutoa miongozo kwa washiriki wa shindano hilo na pia katika kusimamia matumizi ya kompyuta zilizotolewa na Statoil kwa ajili ya matumizi ya washiriki wa shindano la Mashujaa wa Kesho.

  “Tuna furaha kumpata mshindi wa shindano hili. Vijana wengi wa Mtwara walijitokeza kushiriki katika shindano, jambo lililotupa ari kubwa katika kutekeleza shindano hili. Statoil ni kampuni inayopenda kuunga mkono vijana wenye vipaji katika nchi ambazo kampuni hii inafanya shughuli zake. Hii ni njia yetu ya kukuza maendeleo katika jamii zinazotuzunguka,” alisema meneja wa Statoil nchini, Øystein Michelsen.

  0 0
  Juma Iddi (mwenye suti nyeusi) ni Mkurugenzi wa jiji la Arusha


  Na Woinde Shizza,Arusha
  Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Juma Iddi amepania kuipandisha ligi timu ya Arusha FC inayoshiriki ligi daraja la pili msimu huu, huku akiwataka viongozi wa sasa wa timu hiyo kuwa kama kamati na jiji hilo kuhakikisha swala hilo linafanikiwa.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mapema ofisini kwake alisema kuwa kwa kuwa tayari usajili umekwisha fanyika kwa sasa wanatafuta kocha mwenye ujuzi na uwezo wa kimataifa wa kuwanoa vijana hao ili kuweza kumudu mikiki ya ligi daraja la pili bila kuwa na woga.

  “Kiukweli mimi napenda michezo na niko hapa halmashauri ambapo kazi kubwa ni pamoja na kuitangaza michezo na kuonyesha mfano hivyo kwa kuanzia tumeipa nguvu ya kushiriki michuano hiyo kwa vifaa vyote walivyohitaji vya michezo lengo wasianze kulalama na vifaa”

  “Na baada ya vifaa sasa tutahakikisha inakuwa mikononi mwetu mapema mwezi ujao baraza la madiwani litakapokaa na kuridhia na baadhi ya watendaji wa halmashauri hii watakuwa miongozi mwa viongozi watakaochaguliwa kuiongoza lengo ni kuileta karibu na kujua mahitaji yao” alisema Juma Iddi.

  Alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa Arusha kuhakikisha wanakuwa karibu zaidi na timu hiyo na ilete chachu ya soka mkoani hapa kwa kuishangilia na mawazo pia maoni yao.

  “sisi kama halmashauri kuimiliki timu hii siyo kuwaweka mbali wananchi bali ni kuweza kuwajulisha kuwa pia kuwa timu hiyo ni yao kwani itakuwa inatangaza jiji pia kodi zao ndio zitatumika na wajue kuwa pia hatutachukua moja kwa moja bali kwa mda ili tu kuipandisha”

  Alitumia fursa hiyo kuwataka mashabiki wa soka wa mkoani hapa pamoja na benchi la ufundi na wachezaji kuwa kitu kimoja na wasiruhusu migogoro kati yao kwani kufanya hivyo kutakatisha matumaini ya kupanda ligi bali wawe kitu kimoja kuhakikisha lengo linafanikiwa.

  0 0

  SAM_0369
  Radio 5 FM 105.7 imeandaa "kampeni ya RADIO 5 viwanjani" katika mkoa wa Arusha ambapo itawakutanisha watangazaji  na madjs na wasikilizaji wao katika kumbi za starehe kwa takribani wiki tano ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki wa Redio hiyo kwa kuwa pamoja kwa mwaka mzima huku mashabiki wakijipatia zawadi mbalimbali katika kampeni hiyo(katika picha ni Mtangazaji wa kituo cha Redio 5 Julius Kamafa aliyejizolea umaarufu mkubwa jijini Arusha kupitia kipindi chake cha funiko base kinachosikilizwa zaidi na vijana akishow love na msikilizaji wake katika kampeni  ya "Redio 5 viwanjani"ndani ya ACTIVE CLUB - Mbauda jijini Arusha
  SAM_0349
  Timu kazi ya Redio 5 wakifatilia show 
  SAM_0350
  Mtangazaji maarufu aliyejizolea umaarufu mkubwa  kupitia kipindi chake cha love cuts Semio Sonyo akiwa anauliza maswali kwa vijana wa Arusha waliofika katika kampeni ya Redio 5 viwanjani ndani ya ACTIVE CLUB - Mbauda jijini Arusha.
  SAM_0358
  Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akifurahia jambo katika kampeni ya Redio 5 viwanjani iliyofanyika jijini Arusha
  SAM_0353
  Mtangazaji maarufu aliyejizolea umaarufu mkubwa  kupitia kipindi chake cha love cuts Semio Sonyo akimuuliza maswali shabiki wa redio 5 katika kampeni ya Redio 5 viwanjani yenye nia ya kuwashukuru wasikilizaji wa kituo hicho kwa kuwa pamoja kwa mwaka mzima.
  SAM_0383
  Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo kushoto akieleza nia ya kampeni hiyo itakayofanyika katika bar mbalimbali jijini hapa ambapo pia wasikilizaji wa kituo hicho watajizolea zawadi mbalimbali zikiwemo T-shart,vikombe,vinywaji kutoka TBL

  SAM_0364
  Shabiki wa Redio 5 aka chali ya Arachuga akionyesha kiduku cha Arushaaaa
  SAM_0365
  Mtangazaji wa kituo hicho Julius Kamafa aliyeshikilia T-Shart akionyesha manjonjo yake
  SAM_0369
  Mtangazaji wa kituo cha Redio 5 Julius Kamafa aliyejizolea umaarufu mkubwa jijini Arusha kupitia kipindi chake cha funiko base kinachosikilizwa zaidi na vijana akishow love na msikilizaji wake katika kampeni  ya "Redio 5 viwanjani"
  SAM_0371
  Mtangazaji wa Redio 5 Mwangaza Jumanne wa kipindi cha kurekebisha tabia"mishemishe"akifanya yake katika kampeni ya Redio 5 ndani ya ACTIVE CLUB - Mbauda,
  SAM_0376
  Mtangazaji wa Redio 5 Mwangaza Jumanne akimkabidhi msanii Reggaa kikombe mara baada ya kushinda kwa kujibu maswali vizuri...msanii huyu anatamba na kibao chake kipya kiitwacho MCHUMBA akishirikiana na msanii mwenzake G BLESS wote wanatoka U.S.O(united streets olmatejoo)
  SAM_0378Mwanaisha Suleiman mtangazaji wa kituo hicho anayewika katika kipindi cha "mishemishe pamoja na rusha roho"akiwa anamkabidhi msikilizaji wa redio 5 kikombe cha chai chenye nembo ya kituo hicho
  SAM_0386
  Hapa Mwanaisha Suleiman akiwa anakabidhi zawadi ya t-shart kwa shabiki wa Redio 5
  SAM_0387
  Shabiki wa Redio 5 akiwa anafurahia t-shart yake
  SAM_0392
  Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa katika pozi wakati kampeni ya Redio 5 viwanjani ikiwa inaendelea
  SAM_0401
  Mdau wa redio 5 Ray kulia,Pamela Mollel mmiliki wa mtandao wa kijamii http://jamiiblog.co.tz/ na Tonnie Kaisoi mtangazaji wa Redio5 wakishow love
  SAM_0403
  Burudani ilichukua nafasi yake ,hapa machali ya Archuga wakifanya yao ndani ya ACTIVE CLUB - Mbauda
  SAM_0416
  Mtangazaji wa Redio 5 Wilfred Mdingi ambaye alikuwa MC katika shughuli hiyo akifanya yake jukwaani
  SAM_0419
  Msanii kutoka Arusha Juma Ujanja akimiliki jukwaa vilivyo kwa kutoa burudani kwa mashabiki wake
  SAM_0410
  Msanii SS boys kutoka Arusha akitoa burudani kwa mashabiki wake
  SAM_0405
  Umati wa mashabiki wa Redio 5 waliojitokeza katika "kampeni ya Redio 5 viwanjani"
  SAM_0414
  (Habari picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog)

  0 0
 • 12/06/14--08:58: Article 2


 • 0 0

   Bi. Stella Massekwe kutoka Uganda akitoa mchango wake kuhusu masuala mbalimbali yaliyozungumzwa wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania, Kushoto ni kijana Baraka Chelego kutoka Tanzania.
   Mbunge kutoka Kenya Mhe. David Ocheng akitoa hotuba wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania.
   Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Jesca Eriyo (kushoto) akitoa mada wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania. Kulia ni mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa.
   
   Mmoja wa vijana kutoka Uganda Bi. Helena Okiring akichangia wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania.

  Baadhi ya Vijana kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo ni Tanzania bara na visiwani, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wakifuatilia matukio yaliyokua yanaendelea wakati wa mkutano wa kwanza wa Vijana wa EAC kuhusu Sera ya Vijana wa EAC unaoendelea makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha Tanzania.
  Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo.

  0 0

   kutoka kushoto ni Dj Romy Jones, Moses Iyobo na Rama Tonsa wakisubili usafiri na huku wakijaribu kupata mawasiliano mara tu baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia tayari kwa kuwasha moto leo kwenye sherehe ya Uhuru itakayofanyika Sheraton ya Downtown Silver Spring.
   Moses Iyobo, Dj Romy Jones wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa mara tu baada ya kuwasili siku ya Ijumaa Desemba 5, 2014 kwa ajili ya sherehe ya Uhuru itakayofanyika leo Jumamosi Sheraton ya Downtown Silver Spring, Maryland.
   Moses Iyobo na Rama Tonsa wakiwasili hotelini mara tu baada ya kutoka uwanja wa ndege.
   Dj Romy Jones (Dj wa Diamond) akiendelea na mawasiliano akiwa hotelini.
   kushoto ni Inno na watatu toka kushoto ni Phanuel ambao ni waratibu na waliomleta Diamond wakishirikiana na DMK (hayupo pichani wakiwa katika picha ya pamoja na Dj Romy Jones, Moses Iyobo
   Wadau kutoka Michigan wakiwasili tayari kwa show ya Diamond. Picha na Vijimambo.

  0 0

  Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki. Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki.Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi. Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi.Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki. Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia kekiMarion Elias Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, ambaye pia Mratibu wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika maonesho hayo. Marion Elias Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, ambaye pia Mratibu wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika maonesho hayo.Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi. Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi.Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi. Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' watipita kukagua, kupata maelezo ya watengenezaji wa keki hizo kabla ya kuwapata washindi.Keki mbalimbali zilizoshiriki katika Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam. Keki mbalimbali zilizoshiriki katika Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam.Keki mbalimbali zilizoshiriki katika Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam. Keki mbalimbali zilizoshiriki katika Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' katika picha ya pamoja Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' katika picha ya pamoja.Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' katika picha ya pamoja. Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' katika picha ya pamoja.Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' katika picha ya pamoja. Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' katika picha ya pamoja.Keki mbalimbali zilizoshiriki katika Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam. Keki mbalimbali zilizoshiriki katika Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam.Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakijumuisha alama kabla ya kuwapata washindi. Majaji wa Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakijumuisha alama kabla ya kuwapata washindi.Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki. Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' wakipita kuangalia keki.Keki mbalimbali zilizoshiriki katika Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam. Keki mbalimbali zilizoshiriki katika Maonesho ya 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam.

  JOPO la Majaji watatu na mabingwa wa fani za mapishi leo wamewatangaza mabingwa wa utengenezaji keki waliojitokeza katika Maonesho ya bidhaa za keki 'Azam World of Cakes Exhibition' yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam. Jumla ya makampuni na watengenezaji keki wapatao 39 wameshiriki katika maonesho hayo ya keki yalioandaliwa na kampuni ya Insights Productions Limited kwa udhamini wa Kampuni ya Azam Tanzania. 

  Akitangaza washindi katika maonesho hayo ya keki, mmoja wa majaji ambaye pia ni Mpishi Mkuu, toka Ramada Encore ya jijini Dar es Salaam, Edward Mukabana alisema timu ya majaji hao imewapata washindi wa kwanza watatu katika makundi matatu; yaani mshindi wa Keki yenye Radha Bora, Mbunifu Bora wa Keki na Mshindi wa Keki yenye Mvuto Kimuonekano. 

  Jaji huyo wa 'Azam World of Cakes Exhibition' aliwataja Amina Salim kuwa ndiye aliyeibuka mshindi wa keki yenye radha bora zaidi, huku kampuni ya Beta Bakery ikitwaa taji la mbunifu Bora wa Maonesho hayo ya keki. Pia alimtangaza Janeth Muawiriro kuwa ndiye mshindi wa keki yenye Mvuto kimuonekano katika washiriki wote. Jopo hilo la majaji wa 'Azam World of Cakes Exhibition' pia lilimtangaza Leila Dhiyebi kuwa ni mshindi wa kwanza aliyepigiwa kura na wananchi waliotembelea maonesho hayo makubwa ya keki Tanzania. 

  Kundi lingine la washindi ambao keki zao ziliwavutia majaji ni pamoja na Haika Shao na Caroline Gul pamoja na wanae wawili ambao walishiriki kubuni umbo la keki kwa mchoro iliyotengenezwa na mamayao. Akizungumza awali kabla ya kuwatangaza washindi, Jaji Mkuu wa Mashindano hayo ya 'Azam World of Cakes Exhibition', Tom Owino (Excetive Chef) alisema walisema wamezipitia keki zote za washiriki kuangalia vigezo mbalimbali vya upishi, muonekano na kuonja radha ya kila keki kabla ya kukaa chini na kuanza kufanya maamuzi ya pamoja ya majaji kwa kuzingatia vigenzo vya msingi katika utengenezaji keki.

   Aidha kwa upande wake, Marion Elias Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, ambaye pia ni Mratibu wa maonesho hayo alisema maonesho hayo yamekuwa na mvuto baada ya kushirikisha makampuni na watu binafsi huku yakilenga kutangaza bidhaa nzima ya keki na ubunifu katika utengenezaji. 

  Alisema washiriki wote wamepata fursa ya kubadilishana uzoefu na kujifunza ubunifu zaidi wa shughuli hizo toka kwa wataalam wengine jambo ambalo litawabadili kwa namna fulani, ikiwa ni pamoja na kupata zawadi toka kampuni ya Azam na vyeti maalum vya kutambua mchango wao kiushiriki. Kwa upande wake Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma toka Kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan alisema Azam ikiwa ni kampuni inayotengeneza unga bora wa kutengenezea keki imeamua kudhamini ikiwa ni ishara ya kutambua taaluma hiyo ya utengenezaji wa keki nje na ndani ya Tanzania. Wananchi walipata fursa ya kuangalia keki mbalimbali pamoja na kuonja radha zake jambo ambalo lilileta mvuto zaidi kwa washiriki. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  TIMU ya soka Coastal Union ya Tanga inatarajia kusheherekea miaka hamsini na nne ya Uhuru wa Tanzania kwa kucheza mechi ya kirafiki na timu ya AFC ya Arusha itakayochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Desemba 9 mwaka huu.

  Mechi hiyo ni maandalizi kwa timu hiyo kujiandaa na mechi zake za Ligi kuu soka Tanzania bara baada ya mapumziko ya siku kumi kutokana na Ligi kuu kusimama kwa muda ambapo itaendelea Desemba 26 mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa mechi hiyo itakuwa ni muhimu kwa timu hiyo kujitayarisha kwa ajili ya raundi inayofuata kwenye michuano hiyo.

  Amesema kuwa baada ya kumalizika mechi hiyo wataangalia uwezekano wa kutafuta mechi nyengine ya majaribio kabla ya kuanza ligi hiyo ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani mkubwa

  Aidha amesema kuwa timu hiyo ya AFC yenye makazi yake Mkoani Arusha inatajiwa kuwasili mkoani Tanga Desemba 8 mwaka huu kwa ajili ya mtanange huo lengo likuwa kuziandaa timu zote mbili kwa mashindano yanayowakabili.

  Amesema kuwa mechi hiyo ina umuhimu kwa timu zote mbili sisi ni kujiandaa na Michuano ya Ligi kuu Tanzania bara raundi inayofuata na wapinzania wetu  wanajiandaa na Ligi daraja la kwanza hapa nchini.

  Hata hivyo amesema kuwa mazoezi ya timu hiyo yameendelea kushika kasi kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga baada ya wachezaji wote waliokwenda mapumziko kurejea kwa asilimia kubwa.

  0 0

  Prezida wa Wasafi Diamond Platnumz akiwa pamoja na wacheza showa wake Roma Tonsa na Moses Iyobo wakitoa burudani katika kunogesha sherehe ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika Sheraton Hotel ya Silver Spring, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na mashabiki wake kutoka kila pembe ya Marekani huku mashabiki wengine wakitokea Tanzania, Picha na Vijimabo Blog
  Mzuka unazidi kupanda Diamond Platnumz asaula koti lake.
  Balozi akimshukuru Diamond kwa kuwezesha kunogesha usiku wa Uhuru wa Tanzania na pia aliwashukuru wadhamini wa sherehe hiyo ya moaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
  Diamond akizidi kuwapa burudani mashabiki wake
  Shabiki akicheza wimbo wa mdogo mdogo
  Shabiki akijumuika na Diamond kwenye jukwaa.


  0 0

   Wahitimu wa digrii ya  elimu jamii katika taaluma za maendeleo jamii wakishangilia baada ya Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya kuwatunuku katika mahafali ya 8 ya chuo hicho, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana.
   Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Rigobert Buberwa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, Dar es Salaam. Buberwa ametunukiwa  digrii hiyo baada ya kufanikiwa kufanya utafiti unaohusu "Kuelekea modeli ya mfumo wa kompyuta wa kutunza taarifa za ardhi na mabadiliko ya umiliki wake: Nyenzo mpya ya Usimamizi wa Ardhi nchini Tanzania." PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu (Doctor of Phylosophy Degree), Deusdedit Kibassa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo.Mada ya utafiti aliyoifanya inahusu: "Umuhimu wa kutumia maeneo ya kijani kupunguza athari zitokanazo na kuongezeka kwa hali ya joto katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam."
   Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Dawah Mushi, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Mada  ya utafiti aliyoifanya Mushi  inahusu: "Uhamishwaji wa makazi ya watu wengi waliobomolewa makazi yao katika mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam."


   Daniel Mbisso akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
  Joel Msami akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
   Eliwaha Msangi akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
   Margareth Ntiyakunze akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
   Sara Phoya akitunukiwa digriii ya uzamifu
   Baadhi ya wahitimu wakipiga picha wakati wa mahafali hayo
   Bendi ya JKT ikiongoza maandamano ya viongozi na wahadhili wa chuo hicho kuingia ukumbini
   Wahadhiri na viongozi wakiingia kwa maandamano kwenye ukumbi
   baadhi ya wahitimu wakisubiri kutunukiwa digrii
   Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Ardhi, Tabitha Siwale akihutubia katika mahafali hayo
   Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idrissa Mshoro akihutubia wakati wa mahafali hayo
   Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), wakiweka kofia kichwani ikiwa ni ishara ya kutunukiwa digrii ya uzamili ya sayansi ya usimamizi na uchumi ujenzi, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam

   Ni furaha iliyoje baada ya kutunukiwa
   Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wa wahitimu wakiwa katika mahafali hayo
   Waziri Mkuu wa zamani, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha ARU, Cleopa Msuya akitoka baada ya mahafali hayo kumalizika leo
   Msuya akiongoza maandamano kutoka nje baada ya mahafali hayo kumalizika
  Hali ilivyokuwa nje ya ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya mahafali kumalizika

  0 0

  Msanii wa muziki wa Injili, Bonny Mwaitege(kulia) akisalimiana Mtangazaji wa Radio Kasibante Mwl. Joyce Ruboz punde leo hii wakati wa kipindi cha Gospal flava cha Kasibante fm 88.5, Rose Muhando, Bonny Mwaitege na Gaston Sapula wanatarajia kupamba fainali za Mashindano ya Biblia leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba mjini kuanzia saa 8 Mchana. Shindano hili lililokuwa likiendelea hapa Bukoba na kuzikutanisha Wilaya mbalimbali zikiwemo Wilaya ya Muleba, Karagwe, Misenyi na sasa kufikia tamati leo hii Jumapili Dec. 5. Fainali ambazo zitafanyika leo na Mgeni Rasmi ni Mbunge wa Bukoba Mjini(CCM) Mh. Khamis Sued Kagasheki.
  Mtumishi wa Mungu na muimbaji wa nyimbo za injili Rose Muhando akiwa kwenye Ofisi za radio Kasibante Fm 88.5 akionekana mwingi wa Furaha huku akiteta jambo na Mtangazaji katika live ya kipindi cha Gospal Flava leo ambapo wamepata fursa ya kuongea na Wananchi na kuwataka kusogea baadae katika Fainali za Biblia zitakazofanyika leo kwenye Uwanja wa kaitaba Bukoba Mjini.
  Mtangazaji wa kipindi cha Gospal Flava Mwl. Joyce Ruboz akifurahia jambo baada ya kuwaona Waimbaji wa Injili wakiporomosha sauti zao tamu wakati wa kipindi chake leo Asubuhi.
  Mwalimu Joyce Ruboz pia ni Mmoja wa Waratibu wa Fainali hizi za Biblia hapa Bukoba katika swala zima la Kutanua na kuendeleza jamii kupitia Vipindi vya Dini. Wasanii hao Kutoka Jijini Dar es salaam Rose Muhando, Bonny Mwaitege na Gaston Sapula walitinga ndani ya Radio Kasibante fm na tayari kupamba fainali za mashindano ya Biblia leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba kuanzia saa 8 MchanaBoniface Mwaitege akiwa na Msanii mwenzake wa Nyimbo za Njili Gaston Sapula kwenye Studio za radio kasibante Fm Bukoba.
  Rose Muhando akiwa na Gastona SapulaRose Muhando akiwa Katika Ukumbi wa Radio Kasibante FmMtangazaji wa radio kasibante Fm 88.5 Abera nae alikuwepo na hapa akionekana wa furaha baada ya kukutana tena na Rose Muhando katika Ofisi zao za radio kasibante Fm.
  Picha ya pamoja Mwalimu Joyce Ruboz na Wasanii wa Injili wanaotarajia kupamba fainali za Biblia leo katika Uwanja wa Kaitaba.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera (RPC) Henry Mwaibambe nae alipata picha ya pamoja na wasanii hao.

  0 0

  Mfalme wa masauti, Christian Bella ‘Obama’ akifanya yake usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
  Nyomi ya mashabiki walijitokeza katika uzinduzi wa albamu yake mpya ya Nani Kama Mama ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
  Madansa wa Malaika Music bendi wakifanya yao.
  Mashabiki wakicheza na Christian Bella ‘Obama’.
  Mashabiki wakiwa wamepagawa na shoo ya mfalme wa masauti, Christian Bella ‘Obama’ (hayupo pichani).
  Christian Bella ‘Obama’ akizidi kuwapagawaisha mashabiki wake.
  Madansa wa  Christian Bella wakifanya yao.
  Mashabiki wakicheza na kuimba wimbo wa Nakuhitaji wa Bella.
  Bella na wacheza shoo wake wakifanya yao.
  Christian Bella akiimba wimbo wa Nani Kama Mama akiwa na shabiki wake.
  BENDI ya muziki wa Dansi ya Malaika chini ya Christian Bella ‘Obama’ usiku wa kuamkia leo iliutikisa Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar baada ya kuwapagawisha mashabiki kwa shoo ya nguvu.

  Onyesho hilo lililoanza saa tatu usiku ambapo Malaika bendi walikuwa wakiwapa ladha mashabiki kwa kupiga kopi mbalimbali ya nyimbo za Kikongo zinazobamba.

  Ilipofika saa nne na nusu ukumbi ulilipuka kwa shangwe baada ya kiongozi wa bendi hiyo Christian Bella kupanda jukwaani kwa wimbo wake wa Yako Wapi Mapenzi ambao ulisababisha mashabiki kuinuka katika viti vyao na wale ambao walikuwa wakinyemelewa na usingizi kuamka.

  Bella alizidi kuwapagawisha mashabiki kwa kupiga nyimbo kali mfululizo ambazo zinatamba katika redio na vyombo mbalimbali vya habari ukiwemo Nani Kama Mama, Yako wapi Mapenzi, Msaliti, Usilie na nyingine kibao.
  (PICHA/HABARI: ISSA MNALLY/ GPL)

older | 1 | .... | 420 | 421 | (Page 422) | 423 | 424 | .... | 1898 | newer