Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

LA VEDA: IDRIS, FEZZA KESSY NA DIAMOND WAMETOA GUNDU KWA WASANII WA BONGO

$
0
0
La Veda baada ya kuwasili jijini Dar akitokea nchini Afrika Kusini alipokwenda kushiriki fainali za BBA.
La Veda akipokelewa baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
La Veda akipozi na baadhi ya wadau waliofika kumpokea.

MWANADADA, aliyeiwakilisha Tanzania katika shindano la Big Brother Hotshots, Irene Neema Vedastous ‘LA VEDA' amefunguka kuwa Diamond, Fezza na Idris wameondoa gundu kwa ushindi wao.

Akizungumza na GPL leo jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati akiwasili kutoka Afrika ya Kusini alipokwenda kuungana na washiriki wengine wa BBA katika fainali, La Veda alisema,

“Binafsi nimefurahi sana kwa Idris kushinda Dola za Kimarekani 300,000, ni furaha kubwa sana kwangu na kwa Watanzania kwani naamini pia Diamond kuchukua tuzo tatu za Channel O na nyingine aliyopata juzi kutoka Nigeria, Fezza kuingia tena mjengoni wote watakuwa wameondoa gundu kwa wasanii wa Kitanzania’, alisema.

Aidha La veda amewaomba Watanzani kujitokeza kwa wingi kumpokea Idris siku atakapowasili maana ushindi wake unazidi kuiweka Tanzania katika ramani nzuri kimataifa.
Kujua zaidi Mahojiano aliyofanya La Veda baada ya kuwasili, usikose kutembelea www.globaltvtz.com
(PICHA / HABARI: Na Gabriel Ng’osha/GPL)

Waziri Kombani aipongeza Seed Trust kuwapigania haki za walemavu

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Selina Kombani (wa pili kushoto) akifungua Kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Selina Kombani (wa pili kushoto) akifungua Kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavuMwenyekiti wa Tasisi ya Seed Trust, Magreth Mkanga (MB), (wa pili kutoka kushoto) akizungumza katika mkutano wa Kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu. Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Seed Trust, Magreth Mkanga (MB), (wa pili kutoka kushoto) akizungumza katika mkutano wa Kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu.Baadhi ya washiriki wa kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu wakiwa katika mkutano huo leo mjini Morogoro. Baadhi ya washiriki wa kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu wakiwa katika mkutano huo leo mjini Morogoro.Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi.  Mary Massay (wa pili kushoto) akizungumza katika Kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu. Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora –Tanzania, Bi. Mary Massay (wa pili kushoto) akizungumza katika Kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu.Baadhi ya washiriki wa kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu wakiwa katika mkutano huo leo mjini Morogoro. Baadhi ya washiriki wa kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu wakiwa katika mkutano huo leo mjini Morogoro.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mr. Mtei akizungumza katika Kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mr. Mtei akizungumza katika Kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu.Baadhi ya washiriki wa kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu wakiwa katika majadiliano ya vikundi. Baadhi ya washiriki wa kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu wakiwa katika majadiliano ya vikundi.Baadhi ya washiriki wa kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu wakiwa katika majadiliano ya vikundi. Baadhi ya washiriki wa kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu wakiwa katika majadiliano ya vikundi.Baadhi ya washiriki wa kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu wakiwa katika picha ya pamoja. Baadhi ya washiriki wa kongamano la Kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu wakiwa katika picha ya pamojaMratibu wa Miradi wa taasisi ya Seed Trust, Peter Mwita akizungumza. Mratibu wa Miradi wa taasisi ya Seed Trust, Peter Mwita akizungumza.[/caption] WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Selina Kombani ameipongeza taasisi ya Seed Trust kwa jitihada zake za kupiga vita vitendo vya ukatili kwa wanawake na watu wenyeulemavu. 

Bi. Kombani ametoa pongezi hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Seed Trust, Magreth Mkanga (MB), leo jijini Morogoro alipokuwa akifungua kongamano la kujadili namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watuwenye ulemavu. Alisema Bi. Mkanga (MB) kupitia taasisi yake na nje ya hapo amekuwa mstari wa mbele kapaza sauti juu ya haki za watu wenyeulemavu na vitendo vya ukatili kwa ujumla.

 “…Binafsi napenda kumpongeza sana Mama Mkanga kwa kweli yeye amekuwa mstari wa mbele katika utetezi wa haki za walemavu…namuona kule bungeni tuko naye na mara zote anapaza sauti juu ya haki za kundi hili…,” alisema Bi. Kombani. Aidha alimtaka kila mwana jamii kushiriki katika kupaza sauti juu ya kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watu wenye ulemavu kwa ujumla. Alisema vitendo vya ukatili vimekuwa vikiathiri jamii yote bila kujali matabaka hivyo kutaka nguvu ya kila mmoja ishiriki katika kuvipinga kwa hali na mali vitendo hivyo. 

Hata hivyo alivitaka vyombo vya sheria yaani mahakimu nchini kuweka kipaumbele kwenye kesi za vitendo vya kikatili kwa makundi yote ili kuhakikisha wahusika wanaovunja sheria wanapambana na mkono wa sheria kwa wakati kupunguza vitendo hivyo. Kongamano hilo la siku mbili lililoandaliwa na taasisi ya Seed Trust kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) limeshirikisha wadau mbalimbali, taasisi na idara ambazo shughuli zao zinagusa na kuhusika kukabiliana na vitendo vya ukatili. 

 Miongoni mwa wadau walioshirikishwa katika kongamano hilo ni pamoja na Jeshi la Polisi kupitia madawati ya jinsia baadhi ya mikoa, Idara ya Mahakama, Idara ya Ustawi wa Jamii, wanasheria na baadhi ya wawakilishi toka asasi za kiraia nchini. Kwa upande wake, Bi. Mkanga (MB) alimshukuru Waziri Kombani na Serikali kwa ujumla kwa kuonesha ushirikiano kwa taasisi yake na kuongeza kuwa kitendo hicho kinaonesha jitihada za Serikali kukabiliana na vitendo vya kikatili kwa wanawake na walemavu kwa ujumla. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

BUNGE LA TANZANIA NA KENYA NGOMA DROO

$
0
0
SAM_0616
Wachezaji wa Tanzania na Kenya wakiwa katika mashindano ya wabunge wa jumuiya ya Afrika mashariki leo,  katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha, mechi hiyo ilivuta hisia za wakazi wa jiji hilo waliomiminika kuja kushuhudia wabunge hao wakimenyana uwanjani, baada ya dakika ya tano bunge la kenya walijipatia bao la kwanza, bao lililofungwa na Mh.Steven Nyatta na hatimaye Tanzania kusawazisha dakika ya 24 kwa njia ya penalt baada ya Mh.Mbunge Joshua Nassari kudondoshwa eneo la hatari kwa kugongwa na mlinda mlango wa kenya Kega Kanin
SAM_0004
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mh Iddi Azan mlinda malango ambaye pia ni kiongozi wa timu ya bunge la Tanzania akinyaka magoli akionyesha umahiri wake wa kudaka mpira hali iliyosababisha mashabiki wa jiji la Arusha kumshangilia
SAM_0003
Mlinda mlango wa Timu ya kenya Kega Kanin akijaribu kuzuia goli lililopatikana kwa njia ya penalt katika dakika ya 24
SAM_0018
Naibu Waziri   wa  Fedha   Adam  Malima akichechemea uwanjani baada ya kuanguka na kupewa huduma ya kwanza
SAM_0613
Muonekano jukwaa kuu
SAM_0012
Wachezaji wa timu ya Tanzania wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza
SAM_0013
Wachezaji wa timu ya Kenya wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza
SAM_0005
Kushoto ni mchezaji wa timu ya kenya Mh.Peter Kaluma katikati ni Mh Dan Wanyama wa kenya mrefu kuliko wote uwanjani alipewa kadi nyekundu baada ya kuonekana akijibizana na mwamuzi aliyekuwa akichezesha mpambano huo kulia ni Mh Joshua Nassari wa Tanzania
SAM_0007
Kushoto Mh Iddi Azan ambaye ni mlinda malango wa timu ya Tanzania akiwa katika mapumziko, aliyeshikilia mpira ni mwamuzi wa mpambano huo Erick Onoko
SAM_0002
Mh Joshua Nassari wa Tanzania akipewa huduma ya kwanza
SAM_0020
Naibu Waziri   wa  Fedha   Adam  Malima akipatiwa huduma ya kwanza
SAM_0024
Mh.Mbunge wa Tanzania akiwa amelala chali akionekana kuwa na maumivu makali baada ya kuumia katika mechi hiyo wabunge wenzake wakijaribu kumsaidia
SAM_0006
Mashabiki wa Kenya wakiwa wanashangilia huku wakiwa wanaonyesha bwebweeee zao
SAM_0614
Umati wa watu waliokuja kushuhudia mpambano wa Tanzania na Kenya
SAM_0014
Mashabiki wa Tanzania wakiwa wanashangilia kwa kuzunguka uwanja
SAM_0615
Watoa huduma ya kwanza kutoka msalaba mwekundu wakiwa wanafatilia mechi ya wabunge wa Afrika mashariki.(Habari Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog Arusha)

MFUMUKO WA BEI UMEPUNGUA- OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU

$
0
0
 
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Novemba, 2014 leo jijini Dar es salaam.

 
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
8/12/2014, Dar es salaam.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Novemba, 2014 umepungua hadi kufikia asilimia 5.8 kutoka 5.9 iliyokuwepo mwezi Oktoba ,2014 kutokana na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.

Akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa  waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa  Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kupungu kwa mfumuko wa Bei nchini kumesababishwa na kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula na zile zisizo za vyakula.

Amezitaja bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kuwa ni pamoja na Unga wa mahindi , unga wa ngano, tambi na vyakula vya lishe kwa watoto.


Bidhaa nyingine ni mavazi ya wanaume zikiwemo suti, suruali, sare za shule na viatu vya wanaume huku bidhaa za gesi, mafuta ya taa, mkaa, mazulia, vyandarua pamoja na simu na saa za mkononi zikichangia kwa asilimia 17.2.

Kuhusu Fahirisi za bei kwa maana ya kiwango cha badiliko la kasi ya bei  za makundi ya bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na Kaya binafsi kwa kuzingatia kipimo cha mwezi amesema kuwa zimeongezeka hadi kufikia 150.54 mwezi Novemba kutoka 149.70 za mwezi Oktoba, 2014.

Amefafanua kuwa kuongezeka kwa Fahirisi hizo kumechangiwa na ongezeko la bei ya bidhaa za vyakula hususan mchele, vitafunwa vinavyotokana na unga wa ngano,samaki, matunda,mbogamboka,viazi mviringo, mihogo na viazi vitamu.

Akizungumzia uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Novemba , 2014 amesema kuwa umefikia shilingi 66 na senti 43.

“Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma kwa mlaji umepungua ,hii inamaanisha  mtu anahitaji kuongeza ziada  ya shilingi 33 ili aweze kununua bidhaa na huduma zilezile anazozihitaji”

Kwa upande wa mfumuko wa Bei wa mwezi Novemba 2014 katika nchi za Afrika Mashariki amesema  kuwa una mwelekeo unaofanana , Kenya ukipungua  kwa asilimia 6.04 kutoka asilimia 6.43 za mwezi Oktoba, Uganda  mfumuko wa bei ukiongezeka hadi asilimia 2.1 kutoka asilimia 1.8 za mwezi Oktoba.

TRA KUCHAMBUA RIPOTI YA KITUO CHA UTAFITI CHA KODI CHA KIMATAIFA (ICTD)

$
0
0
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade, kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo, Prof Mick Moore, wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha
 Wataalamu wa kimataifa  wa masuala ya kodi  wakiendesha mjadala katika mkutano wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya kodi,mkutano uliofanyika jana  jijini Arusha ,Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), Milly Nalukwago (kushoto), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade (katikati) na  Mtaalam wa Kodi wa Uingereza, Rhiannon Mc Cluskey.
Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA RISHED BADE kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo Prof MICK MOORE wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha

Mwakilishi  wa Channel Ten Arusha, Jamila Omar (katikati) , Mwakilishi wa kituo cha Star TV Arusha, Ramadhani Mvungi ,Iddy Uwesu wa Azam tv Arusha wakifanya mahojiano maalumu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)  Rished Bade jijini Arusha wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo.
 ***********
Mamlaka ya mapato nchini TRA imeanza kuchambua ripoti ya utafiti uliofanywa na kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya kodi na maendeleo inayobainisha changamoto mbalimbali za ulipaji kodi katika
maendeo mbalimbali nchini.

Zoezi la uchambuzi wa ripoti hizo linatajwa kuwa na shabaha ya kuangalia mapungufu yaliyopo na kuboresha mifumo ya sheria na ulipaji kodi kwa hiari.

Sehemu ya Taarifa ya utafiti uliofanwa katika kipindi cha mwaka uliopita na kituo cha kimataifa cha kodi na  maendeleo katika mikoa mbalimbali nchini, inabainisha mazingira tofauti ya ulipaji wa kodi ambapo baaadhi ya maeneo yameonekana kuwa katika changamoto kubwa za ukwepaji kodi.

Kamishana wa TRA Rished Bade kizungumza Jijini Arusha wakati wa Mkutano wa kimataifa baina yao na kundi la wataalamu, wanaofanya utafiti kuhusu masuala ya kodi duniani amesema pamoja na mapitio ya ripoti za utafiti wa taasisi hiyo,fursa hiyo inatoa mwanya kwa wataalamu wa ndani kujifunza mbinu za kushughulikia changamoto za walipa kodi wanaofanya biashara za kimataifa.

Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo Profesa Mick Moore ameeleza kusudio la tafiti zao katika nchi mbalimbali za Afrika kuwa unalenga kuimarisha mifumo ya kodi hususani katika sekta za maliasili zikiwemo Madini,Gas na Mafuta.

Katika hatua nyingine Mamlaka ya mapato nchini TRA imeibuka kinara kwa kuwa na hesabu bora miongoni mwa taasisi za serikali kwa mwaka 2013-2014 zinazotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA ambapo kamishna wa mamlaka hiyo akizungumza Jijini hapa katika hafla ya kukabidhiwa ushindi huo amesema hatua hiyo inazidi kuwajengea imani walipa kodi juu ya utendaji wa chombo hicho.

Raha tele tabu ya nini?: zinaonyesha ongezeko la idadi ya walipa kodi chini,idadi iliyopo sasa inatajwa kuwa ndogo kulinganisha na mataifa mengine kutokana na mfumo wa kibiashara usio rasmi unaopelekea kupunguza idadi ya walipa kodi wanaofikia milioni moja nukta nane hivi sasa.

Hazina yapamba tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne

$
0
0
  Vijana wa Kikundi cha “Hisia Theatre Group” wakionesha ujuzi wao wa sarakasi wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini leo Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

 Mwamuzi wa michezo ya sanaa za maonesho na Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Delphine Njewele (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwanasheria wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) Hamisi Tika kwenye banda la PPAA wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

 Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt.Kedmon Mapana (kushoto) akiwa katika banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akifafanua jambo wakati alipotembelea banda hilo wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Wa kwanza kulia ni Afisa Huduma wa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA Njovu K. Njovu na anayefuatia ni Afisa Huduma wa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA Serapio Luanda.
 Mwamuzi wa michezo ya sanaa za maonesho na Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Stephen Ndibalema (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkaguzi Mwandamizi kutoka Bodi ya Michedzo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Milao wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
 Meneja Mawasiliano Jamii kutoka Mfuko wa Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-T) Margaret Mussai akifafanua jambo kwa mteja wake Mashaka Kindamba mkazi wa Mtoni Mtongani Wilayani Temeke wakati alipotembelea banda hilo wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
 Watumishi wa Wakala ya Huduma ya Manunuzi Serikalini (GPSA) wakifuatilia michezo wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
  Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Serikalini (GCU) Ingiahedi Mduma (katikati) wakati wakitoa burudani wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Waamuzi ambao ni Wahadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt.Kedmon Mapana (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Delphine Njewele (wa kwanza kulia) wakionesha utaalamu wao wa sanaa kwa kusakata mzuki kwa saili ya “Kwaito” wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam. Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

DAR LIVE YAFURIKA KATIKA KILELE CHA EFM BAR KWA BAR MUZIKI MNENE

$
0
0
Inspector Haroun 'Babu' akifanya makamuzi wakati wa kilele cha EFM Bar kwa Bar Muziki Mnene ndani ya Dar Lve jana.
Nyomi iliyohudhuria sherehe za kilele hicho.
Burudani mwanzo mwisho.
DJ mkongwe nchini, Majay Majizzo akifanya yake stejini na kupagawisha mashabiki vilivyo.
Babu aliamua kuvua viatu na kubaki peku baada ya burudani kukolea.

Ma DJ kutoka EFM wakitoa burudani.
Mtangazaji wa Michezo wa EFM Radio, Maulid Kitenge akiwaburudisha mashabiki.
Omary Katanga wa EFM naye akifanya yake stejini.
Wafanyakazi wa EFM Radio wakiwa katika pozi wakati wa kilele cha EFM Bar kwa Bar Muziki Mnene.
Kitenge katika pozi na mdau.
Mtangazaji wa EFM, Ssebo katika picha ya pamoja na Meneja Uhusiano wa EFM, Kanky Mwaigomole.
Watangazaji na Ma DJ wa EFM wakifanya yao ndani ya Dar Live.
UMATI wa wapenzi wa burudani jana ulifurika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala, Zakheem jijini Dar katika kilele cha matamasha yaliyoandaliwa na EFM Radio yajulikanayo kama Bar kwa Bar Muziki Mnene.

Burudani kutoka kwa Inspector Haroun zilikonga vilivyo nyonyo za mashabiki huku DJ Makey, watangazaji wa EFM Maulid Kitenge na mwenzake Omary Katanga wakiwapa raha tosha mashabiki waliofurika katika ukumbi huo. (PICHA NA PATRICK BUZOHELA / GPL)

sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara uwanja wa Uhuru jijini Dar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikitoa salamu ya heshma wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Kitaifa wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabalozi wa Nchi mbali mbali wanaoziwakilisha Nchi zao hapa nchini pamoja na Wananchi wakiwa katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es Salaam na Mikoa jirani wakiwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dare Salaam katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambazo hufanyika kila mwaka. Picha na Ikulu.

TIPER yasaini makubaliano kuchangia vitabu vya masomo ya sayansi Shule ya Sekondari Vijibweni

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayoifadhi mafuta ya Tanzania, Tanzania International Petroleum Reserves Ltd (TIPER), Bw Daniel Belair, akikabidhi vitabu vya sayansi vikiwemo vya Fizikia, Baolojia na Kemia kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Vijibweni, Bw Itumbo Kinyonyi wakati wa sherehe ya kusaini makubaliano yatakayoiwezesha kampuni hiyo kuchangia vitabu 200 vyenye thamani ya Shilingi milioni nne kwa shule hiyo iliyopo eneo la Kigamboni wilaya ya Temeke. Shughuli hiyo ilifanyika jana katika viwanja vya shule hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayoifadhi mafuta ya Tanzania, Tanzania International Petroleum Reserves Ltd (TIPER), Bw Daniel Belair, na Mkuu wa Shule ya Sekondari Vijibweni, Bw Itumbo Kinyonyi wakionyesha vitabu vya sayansi vikiwemo vya Fizikia, Kemia na Baolojia baada ya kampuni hiyo kusaini makubaliano ya kuafiki kuchangia vitabu 200 vyenye thamani ya Shilingi milioni nne kwa shule hiyo iliyopo eneo la Kigamboni wilaya ya Temeke. Shughuli hiyo ilifanyika jana katika viwanja vya shule hiyo.
 
KAMPUNI ya kuhifadhi mafuta ya Tanzania, Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER), imesaini makubaliano ya ununuzi wa vitabu  200 vya masomo ya sayansi katika shule ya Sekondari ya Vijibweni iliyopo eneo la Kigamboni, Wilayani Temeke mkonani Dar es Salaam ikiwa ni moja ya mpango wa kampuni hiyo katika kusaidia jamii.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika shuleni hapo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER hapa  nchini, Daniel Belair alisema hatua hiyo inalenga kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini hususani kwenye masomo ya sayansi.

“Ni ukweli ulio wazi kwamba kwa sasa taifa linahitaji zaidi wahitimu wa masomo ya sayansi.Hakuna njia rahisi kufanikisha hilo zaidi ya kuanza kuwaandaa hao wahitimu kuanzia sasa na ndiyo maana na sisi tukaona ni vema tuwe sehemu ya maandalizi hayo,’’ alisema Belair.

Katika kuthibitisha adhma yake ya kusaidia vitabu  hivyo, Mkurugenzi huyo alitanguliza jumla ya vitabu 28 vya masomo ya Baioloji, Kemia na Fizikia vyenye thamani ya sh. Milioni 4 huku akiahidi kukabidhi idadi ya vitabu iliyobakia hivi karibuni.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa shule hiyo, Itumbo Kinyonyi licha ya kuishukuru kampuni ya TIPER kwa msaada huo, alisema msaada huo unakuja wakati muafaka ambapo kwa sasa shuke hiyo ipo kwenye mkakati wa kuongeza ufaulu zaidi wa wanafunzi wake hasa kwenye masomo ya sayansi.

“Vitabu hivi vitatusaidia sana hasa katika kufanikisha ufaulu wa masomo ya sayansi.Katika kipindi ambacho tunaboresha mahabara zetu kulingana na agizo la Mh. Rais Kikwete tunabahatika pia kupata na vitabu vya sayansi… ni bahati kiasi gani?!,’’ alishukuru Mwalimu Kinyonyi.

Hata hivyo, akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo, Musa Ungando alisema pamoja na msaada huo shule hiyo bado inakabiliwa na uhaba wa vifaa vya mahabara zikiwemo kemikali na hivyo kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo wa TIPER ili kuokoa sekta hiyo muhimu.

“Ni jambo linalotia faraja kuona tatizo la uhaba wa vitabu hasa vya masomo ya sayansi kwa sasa linapata suluhisho…hata hivyo bado tunawaomba wadau wengine waige mfano nao wasaidie kutatua changamoto nyingine zinazoikabili shule ikiwemo vifaa vya mahabara zikiwemo kemikali kwa ajili ya mafunzo ya sayansi,’’ alisema Mwalimu Ungando.

Akishukuru kwa niaba ya wanafunzi wenzake, mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule hiyo Ameir Kassim alisema kupatikana kwa vitabu hivyo kutarejesha ari iliyokuwa imeanza kupotea ya wao kusoma masomo ya sayansi.

“Kuja kwa vitabu hivyo kutatuondelea usumbufu tuliokuwa tunaupata wa kubanana wanafunzi wengi kusoma vitabu vichache na wengine  kulazimika kutembea umbali mrefu kwenda shule nyingine kuazima vitabu hivyo kwa wenzetu,’’ alisema mwanafunzi huyo.

INAFRIKA BAND AKA WAZEE WA INDEGE WAMESHATUA UJERUMANI

$
0
0
Bendi ya Muziki ya Inafrika Band aka "Wazee wa Indege" yenye makao yake Chan'gombe jijini Dar-es-salaam imeshatua leo 9-12-2014 nchini Ujerumani kwa ziara ndefu ya nchi za ulaya,bendi inafanya kazi chini ya mradi wa sarakasi ya MOTHER AFRICA imekuwa kivutio sana katika maaonyesho hayo,kwa ajili ya mtindo wake wa muziki wenye vionjo vya mitindo ya kiasili ya makabila ya Tanzania. Inafrika band ukipenda waite"Wazee wa Indege" unaweza kusikiliza nyimbo zao katika mtandao wao bofya www.infrikaband.co.tz  au http://www.inafrikaband.co.tz
  

TIMU YA EALA WAICHAPA BURUNDI 4-2

$
0
0
SAM_0035
Wachezaji wa Timu ya EALA waliovalia jezi rangi ya blue wakipambana na wenzao timu ya Burundi.
 
Timu ya wabunge wa EALA wameicharaza mabao manne kwa mbili timu ya Burundi jana katika Uwanja Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya wabunge Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Mchezaji mahiri wa timu ya Eala John King aliipatia mabao 3 timu yake dakika ya 9 na 21 kipindi cha kwanza hali iliyosabaisha mashabiki waliomiminika katika uwanja huo kumshangila
Kipindi cha pili hali ilibadilika  baada ya timu ya Burundi kujipatia mabao mawili  dakika ya nne na dakika ya 18, mpigaji wa magoli hayo ni Simon Gahinja

Baada ya mchuano mkali wa timu zote mbili ,Eala waliongeza bao la 4 lililofungwa na mchezaji Wilyclif Keto dakika ya 25 baada ya kupata penalt dakika 33  ambapo mpigaji penalt alikosa baada ya mlinda mlango wa Burundi Ibrahim Uwizey kudaka
SAM_0039Mbunge wa EALA kutoka nchini Tanzania Mh.Twaha Taslama jezi namba 12 akiwa uwanjani
SAM_0038Mh Mbunge wa Eala Bernad Mrunya akiwa anajiandaa kukabilia na timu ya Burundi katika Uwanja Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)

KAMBI YA WATOTO WANAOHUDUMIWA KATIKA VITUO VINAVYOSAIDIWA NA AGPAHI YAFUNGULIWA MJINI

$
0
0
Mganga mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Mtumwa Mwako akizungumza wakati wa ufunguzi wa kambi ya watoto (Ariel camp) wanaopata huduma katika vituo mbalimbali vya afya vinavyosaidiwa na shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI linalofanya kazi katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
Mkurugenzi wa Miradi wa AGPAHI, Dk Amos Nsheha akizungumza wakati wa ufunguzi wa kambi ya watoto inayofanyika wiki hii katika Hotel ya Uhuru mjini Moshi.
Baadhi ya watoto wanaoshiriki kambi hiyo wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na mgeni rasmi pamoja  na viongozi wengine mbalimbali .
Afisa Mawasiliano na huduma za Mikoba kwa jamii wa shirika la AGPAHI, Jane Shuma akizungumza katika ufunguzi wa kambi hiyo ya watoto mjini Moshi.
Mshauri wa wanafunzi wa Chuo kikuu cha tiba cha KCMC, Mchungaji Deogratius Msanya akitoa mada ya kisaikolojia katika kambi ya watoto hao wanaotoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
Baadhi ya watoto walio kwenye kambi wakifurahi na kuonesha umahiri wao wa kucheza muziki
Mgeni rasmi Dk Mtumwa Mwako akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mganga Mkuu, Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Kilimanjaro, wafanyakazi wa AGPAHI na walezi wa watoto hao mara tu baada ya ufunguzi wa kambi.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na watoto, walezi na wafanayakazi wa AGPAHI.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WAFINYANZI WAOMBA MSAADA WA VIFAA VYA KISASA

$
0
0
DSC_0908
Mratibu wa Mradi wa Ukimwi ILO, Getrude Sima (kushoto) akitoa maelezo ya kikundi cha kina mama ambao ni walengwa wa mradi wa Ukimwi unaofadhiliwa na SIDA chini ya shirika la kazi duniani (ILO), kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe. Kulia ni Practice Specialist HIV/AIDS, Dr Bwijo Bwijo.
DSC_0926
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye picha ya pamoja na kikundi cha kinamama wa Nyololo wanaotengeneza vikapu.
DSC_0967
Baadhi ya vyungu vinavyotengenezwa na kikundi hicho.
DSC_0974
 
Na Mwandishi wetu, Iringa
KIKUNDI cha wafinyanzi wanawake cha Lungemba,kilichopo Wilaya ya Iringa, wameomba kusaidiwa vifaa vya kisasa vya ufinyanzi, ili waweze kutengeneza vitu bora vitakavyokubalika katika soko. Maombi hayo wameyatoa katika risala yao kwa Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Alvaro Rodriguez.

Mratibu huyo alikuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe. Makundi yaliyotembelea ni yale ya ujasiriamali, yanayosimamiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) chini ya mpango wa Kupunguza Maambukizi ya UKIMWI kwa Njia ya Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Wafanyakazi walio katika Sekta Isiyo Rasmi kando kando mwa Barabara Kuu iendayo Tanzania-Zambia maarufu kama “Corridor Economic Empowerment Project (CEEP) “Aidha makundi mengine yaliyotembelewa ni ya wakulima wanaosaidiwa pembejeo na wanaotengeneza vikapu na kufanya shughuli binafsi ikiwamo mabucha.

DSC_0920
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa amembeba mtoto wa mwanachama wa Mtwango SACCOS ya wilaya ya Njombe.

Mmoja wa wanachama hao Anna Nyongole alisema wanafanya kazi hiyo katika mazingira magumu, kwani bado wanatumia mikono pekee, badala ya kutumia vifaa vya kisasa, na hivyo kusababisha bidhaa zao kukosa ushindani katika soko jambo linalowadumaza kiuchumi.
“Tunatengeneza vyungu, sufuria, majiko, mitungi ya maji na ya maua, na vitu mbalimbali, lakini changamoto yetu kubwa ni namna tunavyotengeneza, kwani hatuna mashine za kutengenezea vitu hivyo wala mitambo ya kuchomea, tunaiomba serikali na wadau wa maendeleo nchini watusaidie, kwani tukipata vifaa vya kisasa tutaweza kutengeneza vitu vingi kwa muda mchache kuliko ilivyo sasa,” alisema Nyongole.

Naye Zena Omary amesema kukosekana kwa usafiri wa gari kwenda kusomba udongo wa kufanyia ufinyanzi kunawafanya kutembea umbali wa kilomita 40 kwenda na kurudi, kutoka katika eneo la Ikekeke katika kijiji cha Kitelewasi.
DSC_0904
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Wanchama wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kinachofadhiliwa na SIDA chini ya Shirika la kazi Duniani (ILO).

“Tunakokwenda kuchimba udongo ni Ikekeke katika kijiji cha Kitelewasi, tunatembea kilomita 20 kwenda na kurudi kilomita 20, kwa hiyo unajikuta siku moja umeshindia kuchimba udongo na kusomba tu, na kwa kuwa tunajitwisha kichwani, huwezi kuchukua udongo mwingi,” alisema Zena.

Licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali, akinamama hao wamesema kupitia mafunzo ya UKIMWI na Ujasiriamali waliyopata kutoka ILO wameweza kuboresha biashara hiyo ya ufinyanzi kwa kujenga banda la kuhifadhia bidhaa hizo, kuweka akiba na kukopeshana katika kikundi hatimaye wamefanikiwa kuyabadili maisha yao kwa kujenga nyumba bora na hata kuwasomesha watoto wao kwa kumudu gharama za ada.

“Hapa kila mmoja wetu anayo nyumba ya kisasa ya tofali za kuchomwa na iliyoezekwa kwa bati, na pia tumefanikiwa kusogeza huduma ya maji ya bomba katika nyumba zetu, ili kupunguza usumbufu wa kuchota maji visimani... kwa kweli biashara hii ya ufinyanzi imetusaidia lakini tukiboreshewa zaidi mazingira tutakua zaidi kiuchumi,” Walisema.
DSC_0932
Msafara wa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez ukiongozwa na Mratibu wa Mradi wa Ukimwi ILO, Getrude Sima (kushoto) kuelekea kukagua baadhi ya miradi inayofadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa wilayani Njombe.

Hata hivyo Umoja wa Mataifa UN kupitia Shirika la Kazi Duniani “ILO” Kwa mkoa wa Iringa pekee- limefanikiwa kuwafikia akinamama na vijana wapatao 1,000 wa vikundi mbalimbali vya kiuchumi na vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS), huku wanachama wa vikundi hivyo wakipatiwa mikopo, Elimu ya Maambukizi Virusi vya UKIMWI, pamoja na mafunzo ya Ujasiriamali.

Mratibu huyo alitembelea vikundi hivyo kuona namna msaada wa Umoja wa Mataifa ulivyobadili maisha ya wahusika ambao walikuwa katika mazingira magumu hapo awali.
Makundi mengine yaliyotembelewa yapo Nyololo na pia hospitali ya Mafinga ambako kuna mafunzo yanayoendeshwa kwa ajili ya ushauri nasaha kwa wanawake wenye kuishi na VVU.
Miradi hiyo ambayo mashirika ya UNICEF na IFAD yanashiriki, imelenga kusaidia makundi hata yale yenye wanachama wanaoishi na virusi vya ukimwi kujitambua na kuishi kwa kujitegemea.
DSC_0935
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akicheza na baadhi ya watoto yatima wa kituo cha Nyololo Centre ambao wengine wakiwa ni ndugu wa wakinamama wanaosaidiwa na ILO.
DSC_0946
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikagua shamba la Mradi wa miche na matunda ambalo linasimamiwa na wanawake wa kikundi cha Nyololo wanaofadhiliwa SIDA chini ya shirika la kazi duniani (ILO).
DSC_0952
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishiriki kupanda mti kwenye shamba hilo kama kumbukumbu wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe.
DSC_0954
DSC_0965
Katibu wa Kikundi cha wafinyanzi wanawake cha Lungemba, Bi. Leokadius Mfukwe akisoma risala ya kikundi chao na changamoto zinazowakabili mbele ya Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye miwani) alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi inayosaidiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Iringa na Njombe.

Article 3

Wadau wa Sekta ya Afya kutoka Tanzania Washiriki Maonyesho ya Sekta ya Afya jijini Istanbul -Uturuki. Dec 2014.

$
0
0
Washiriki Kumi na Wanne (14) kutoka Tanzania wajumuika na wenzao 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika katika Maonyesho ya Pili Sekta ya Afya chini Uturuki. Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka na kwa lengo la kuendeleza mahusiano na ushirikiano katika kuboresha Sekta ya Afya kwa nchi husika. Maonyesho ya Mwaka huu yalikuwa na washiriki kutoka nchi 60 duniani kote.  Kwa upande wa Afrika mkutano huu ulioratibiwa na kusimamiwa na kampuni ya kuendeleza mahusiano ya maendeleo na biashara kati ya Afrika na Uturuki iitwayo TurkaAfrica Ltd (www.turkafrica.co.tz).
  Waandaaji wa TurkAfrica wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao TUSMSIAD,na Washiriki kutoka Tanzania.
 Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif Suleiman akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Afya wa Uturuki Hon. Mehmet Müezzinoğlu. Kushoto ni Dr. Lulu Fundikira (kutoka Hopitali ya Taifa Muhimbili) akifuatiwa na Mshauri wa mambo ya Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Uturuki ambaye pia ni Raisi wa Taasisi ya Uchumi na Biashara ya Uturuki (TUMSIAD) – Dr. Hassan Sert. Kulia ni Jumanne Simba.
 Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif Suleiman akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa sekta ya Afya wa Serikali ya Uturuki mara baada ya mazungumzo ya njia mbalimbali za kuboresha sekta ya Afya na mahusiano kati ya Serikali ya Uturuki na Tanzania.
 Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif Suleiman akifanya mazungumzo na Waziri wa Afya wa Uturuki Hon. Mehmet Müezzinoğlu. Kushoto ni Dr. Athuman Ngenya na washiriki wengine kutoka Tanzania.
 Washiriki kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
 Washiriki kutoka Tanzania wakijumuika na washiriki kutoka nchi zingine za Afrika kwa mualiko wa TurkAfrica Ltd.  Kulia ni Dr. Magda Eshaq kutoka Tanzania.
Wapambanaji wa TurkAfrica Ltd, waandaaji na wasimamizi wa washiriki kutoka nchi 6 za Afrika (Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Egypt). Kutoka kulia kwenda kushoto ni Hamim Athumani, Jumanne Simba na Hamisi Miraji.
 Richard Kasesela - Board Member wa  Muhimbili National Hospital na Mlezi wa Tanzania Medical Students - TAMSA (wa tatu kulia) akibadilishana mawazo na viongozi wa sekta ya afya wa Serikali ya Uturuki wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa maalumu kwa ajili ya washiriki kutoka Tanzania. Kulia kwa Kasesera ni Jumanne Simba na kushoto ni Hamisi Miraji wa TurkAfrica Ltd (wasimamizi wa viongozi wa serikali na washiriki wote kutoka nchi Sita za Africa – Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Egypt).
 Washiriki Kutoka Tanzania wakifuatilia kwa umakini hotuba ya kuboresha maendeleo ya Sekta ya Afya kutoka kwa Waziri wa Afya wa Uturuki Hon. Mehmet Müezzinoğlu (hayupo pichani).  Kulia ni Dr. Lulu Fundikira (Idara ya Radiology kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili) na kushoto  – Dr. Rahma Hingora (kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili).

FID-Q AZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAIFA LETU.

$
0
0


 Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Farid Kubanda Fid Q akizungumza na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa City Sports Lounge wakati akitangaza kuanza kwa kampeni maalum ya kuhamasisha vijana kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha  inayoitwa(#Tuo8January).  ambayo itaanza jumamosi mkoani Njombe  kutoka kulia ni Promota  Tale Msanii Dito na kutoka kushoto ni mtayarishaji wa muziki  Lamar Fishcrabmusic na Promota Said Fella wakiwa katika mkutano huo.

=============  ======= ============
Msanii nguli wa miondoko ya Hip-hop Fareed Kubanda – Fid Q amekutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge katikakati ya jiji la Dar es Salaam, kujadili maswala ya msingi yenye mustakabali chanya kwa maendelo ya taifa hili. Ameitisha mkutano huu akiwa kama kijana na mwenye nafasi na ushawishi kwa vijana wenzie katika ushiriki wa kuleta mabadiliko chanya na maendeleo ya nchi yetu.

Fid Q amesukumwa kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kutanabai kwamba vijana japo ni asilimia 80 ya taifa lakini hawana mwamko na msukumo wa kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi wa viongozi waowataka na wanaowaamini wanauwezo wa kuleta mabadiliko ya ki nidhamu kwenye masuala ya msingi ya taifa letu.

“Kuna kitu kimoja ambacho watu wengi hasa hasa vijana wenzangu hawakifahamu, Nchi yetu ni changa sana. Vijana nchi hii chini ya umri wa miaka 35 ni zaidi ya asilimia 80 ya idadi ya watu, wakati watu wazima zaidi ya miaka 60 ni asilimia chini ya 5 ya watanzania wote. 

Hizi ni takwimu za sensa iliyopita. Nimetanguliza takwimu mapema kwa sababu, twakimu huwa hazisemi uwongo. Changamoto zinalolikumba taifa hili kwa kiasi kikubwa zinatuathiri sisi vijana wa nchi hii ambao ndio wengi wetu. Madhara yanayotokana na uongozi mbovu, vile vile yanatuathiri sana sisi vijana kwa wingi wetu. Tutake tusitake, ustawi na kunawiri kwa vijana ndio kutaamua mustakabali wa Tanzania, vijana tukilala basi na Tanzania pia italala.” Alisema Fid Q.


Bado kuna changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana. Vijana wengi wamezagaa mitaani bila shughuli za kufanya. Hata wale wenye degree hawana kazi. Vijana wanakata tama na kuona kwamba wao sio sehemu ya taifa hili. Kuna changamoto ya viongozi waadilifu watakaosimamia kuhakikisha kwamba keki ya taifa inagawanywa kwa Watanzania wote na hailiwi na wachache.

Baada ya utangulizi huo, ni dhahiri kwamba kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa unaoendelea, na uchaguzi mkuu wa 2015 lazima vijana tuamke na tushiriki kikamilifu. Kwanza, vijana wenye uwezo na sifa za kugombea nafasi za uongozi ni lazima wafanye hivyo, pili vijana wenye vigezo vya kupiga kura pia ni lazima wafanye hivyo maana ni wajibu wetu, tatu, vijana ni lazima tushiriki kikamilifu katika mchakato wa kampeni ili kuhakikisha ishu zetu za msingi zinajadiliwa na wagombea na zinapewa kipaumbele.

Kama vijana wanakuwa na hofu basi niwakumbushe kwamba, Mwalimu Nyerere alikabidhiwa nchi hii akiwa na miaka 39 tu na kuanza harakati za kupigania Uhuru ambao tumeuenzi jana. Alikuwa ni kijana mdogo tu. Mzee wetu Dr. Salim Ahmed Salim alianza kuwa mwanadiplomasia mahiri akiwa na rika dogo tu, akiwa na umri wa miaka 22 alikuwa Balozi wa Tanzania, nchini Misri. Mifano ipo mingi, hivyo vijana tusipate woga – Tumechangia kupatikana kwa Uhuru na kujenga nchi hii, na sasa ni wakati mwingine tena wa kuibadilisha nchi yetu.

“Hivyo mimi Fareed Kubanda, nimeamua kufanya matamasha ili kusimamia haya niliyoyasema hapo juu. Kwa kutumia nafasi zenu ndugu wana habari naomba mnisaidie kutangaza azma yangu hii pamoja na nitawapigia baadhi ya wasanii wenzangu kuwaomba waniunge mkono ili tufanikishe hili na tushiriki katika kuleta uongozi utako leta mabadiliko tunayoyataka na kwa kasi yetu sisi vijana.”

Fid Q aliendelea “Ninatumaini kwamba wasanii wenzangu wataniunga mkono, ili kuanza kuwaamsha vijana wenzetu, tuweze kutimiza wajibu wetu wa kihistoria wa kufanya mabadiliko katika nchi yetu, hasa pale tunapokuwa tunahitajika sana na jamii. Tayari nimefanya mazungumzo na Mkubwa Fela, Babu Tale, Mwana FA, Nick wa Pili, Lamar, P-Funk, Mwasiti, Barnaba, Ditto ambao wamekubali kuwa sehemu ya harakati hizi. Bado nahitaji wasanii wengine wengi washiriki ki mawazao, hali na mali kufikia lengo kuu la Tanzania mpya na bora zaidi”.

Huu ni mwanzo wa harakati hizi, mwakani tutafanya amsha amsha kubwa ya vijana. Mwaka huu tunasema Tuonane January (#Tuo8January). Tutengeneze nchi yetu!! Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania!

TASAF yamuaga Bi. Manjolo

$
0
0
 Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo akifurahia tuzo aliyopewa na TASAF kama ishara ya mafanikio makubwa kufuatia ushirikiano alioutoa kwa TASAF katika kutekeleza mipango ya maendeleo.
 Menejimenti ya TASAF ikiwa katika picha ya pamoja na Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (wa tatu toka kulia walioketi). 
Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (wa tatu toka kulia walioketi) wakati wa hafla ya kumuaga Bi. Manjolo. 
 Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (wa tatu toka kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dokta Servacius Likwelile,   Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha Bw. Said Magonya (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (wa kwanza kushoto). Wengine ni walioketi toka kulia ni Afisa mpya wa Benki ya Dunia anayesimamia shughuli za TASAF Bw. Mohamed Muuderis na Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Ikulu Bi. Suzan Mlawi pamoja na baadhi ya wanafamilia ya Bi Manjolo (waliyosimama).

 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw.Ladislaus Mwamanga akitoa neno katika hafla ya kumuaga Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (hayupo pichani) kwenye hoteli ya Southern Sun.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dakta Servacius Likwelile (aliyesimama) akitoa hotuba fupi ya kumuaga Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (aliyeketi kulia).
 Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF, Bi. Ida Manjolo (kushoto) akiwa na  Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Ikulu Bi. Suzan Mlawi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dakta Servacius Likwelile (hayupo pichani) katika hafla iliyoandaliwa na TASAF kumuaga Bi. Manjolo. 

Madereva wa Magari ya TASAF waliohudhuria hafla ya kumuaga Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo wakifuatalia moja ya tukio (halipo pichani) katika hafla hiyo .


Mfuko wa Maendeleo ya jamii-TASAF kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha umempongeza na kumuaga rasmi Afisa aliyestaafu kutoka Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania ambaye alikuwa akisimamia  shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo.
Bi. Manjolo ambaye amefanya kazi hapa nchini kwa miaka kumi amepongezwa kwa kushiriki kikamilifu katika kuchochea kasi ya utekelezaji wa shughuli za TASAF za kupambana na umaskini nchini .
Akizungumza katika hafla ya kumuaga na kumpongeza Afisa aliyestaafu kutoka Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania ambaye alikuwa akisimamia  shughuli za TASAF (Task team Leader-TTL) Bi. Manjolo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga alibainisha kuwa Afisa huyo alikuwa akitumia falsafa yenye maneno ya "hakuna kulala hadi kieleweke" katika kuwapa moyo watendaji na wadau wa mfuko huo katika kuwahudumia walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini unaosimamiwa na TASAF.
"Wote tunafahamu kuwa katika kipindi ambacho tumekuwa naye, TASAF sasa imepanda chati sana na siyo ndani ya nchi tu, lakini pia hata nje ya nchi huko kwingineko Duniani, na maendeleo ya mpango wa kunusuru Kaya Maskini umekuwa ukiongelewa kwamba ni mpango unaofanya vizuri, lakini haya yote ni kwa sababu ya ushiriki wake mzuri ambao ulikuwepo na amehusika kwa kiasi kikubwa kuuandaa na kuufikisha mahala hapa pazuri tulipo" alifafanua Bw. Mwamanga.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha Dakta Servacius Likwelile amemtaja Bi Manjolo kama kiongozi hodari ambaye wakati wote amekuwa akitekeleza majukumu yake kwa ukamilifu na kuhakikisha kuwa mafanikio yanapatikana.
"Tumekuwa katika safari ndefu lakini yenye mafanikio makubwa kutokana na umakini wa mmoja wa madereva wetu ambaye ni Bi. Manjolo , tulianza naye akiwa ni msaidizi wa TTL hadi akawa TTL na katika kipindi chake chote cha miaka kumi ameiwezesha TASAF kufikia mahala hapa kwa sababu ya uwazi , wepesi na ukarimu wake wa kutaka kuona kwamba tunafanikiwa". Alibainisha Dr. Likwelile.
 Dr. Likwelile ambaye pia amepata kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha hakusita kutoa shukrani zake za dhati kwa mafanikio yaliyopatikana kutokana na ushiriki wa Bi. Manjolo.
"Tunamshukuru Aida kwa uadilifu, uaminifu, ukaribu, udugu na kupenda kutimiza wajibu na akaongeza kuwa siyo rahisi kutekeleza mpango kama huu na ukaleta maana kwa jamii kama hakuna uongozi mzuri na mshauri mzuri". alisisitiza Dr. Likwelile.

Tathimini ya ripoti mradi wa GEWE yazinduliwa Dar

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam..
TAMWA Yazinduwa Tathmini ya Ripoti Mradi wa GEWE Mratibu wa Mradi wa GEWE kutoka TGNP Mtandao, Matha Samwel akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_53895" align="aligncenter" width="480"]Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam. kurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_53900" align="aligncenter" width="640"]Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa waliokuwa katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa waliokuwa katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_53893" align="aligncenter" width="640"]Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_53894" align="aligncenter" width="640"]Baadhi ya wanahabari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za TAMWA Sinza Mori Dar es Salaam. Baadhi ya wanahabari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za TAMWA Sinza Mori Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_53896" align="aligncenter" width="640"]Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.[/caption] CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na taasisi anuai za kijamii kimezinduwa tathmini ya ripoti juu ya utekelezaji wa mradi wa Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE). Akizinduwa ripoti hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kwa jamii katika kujitambua na kuibua vitendo vya Ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari kuibua vitendo hivyo zaidi ya hapo awali. Alisema idadi kubwa ya habari, makala na vipindi vya redio na televisheni juu ya masuala ya ukatili vimefanywa maeneo mbalimbali nchini, jambo ambalo limeonesha mafanikio ikiwa ni pamoja na jamii kuelewa zaidi masuala ya ukatili na unyanyasaji na wengine kuanza kuyapiga vita kwa ushirikiano. Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA alisema mradi huo ulitekelezwa kwa pamoja kwa ushirikiano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Kituo cha Usuluhishi cha TAMWA (CRC), kinatekeleza mpango wa kutokomeza ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE II) katika wilaya 10 za Tanzania bara na Zanzibar. Kwa upande wake Matha Samwel Mratibu wa Mradi wa GEWE kutoka TGNP Mtandao, akizungumza alisema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kiasi cha kuibua changamoto ambazo zinaitaji utatuzi kwa ushirikiano na wadau wengine mbalimbali. "...Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi wa GEWE kumekuwa na mafanikio makubwa, moja wapo kubwa ni kuanzishwa kwa vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya zote 10 za mradi, ambapo vituo hivyo vimekuwa vikitumika kama sehemu ya kutolea taarifa kwa jamii...sehemu ambayo wanajamii wanawake na wanaume wanakutana na kubadilishana taarifa na kuangalia namna ya kutatua matatizo yao yanayotoka katika jamii kama kubakwa, vipigo au kulawitiwa na mengineyo," alisema Bi. Samwel. Hata hivyo aliongeza kuwa vituo vya taarifa na maarifa vimekuwa na msaada mkubwa katika maeneo hayo kwani jamii zimeweza kuvitumia pia kwa kujadili namna ya kukuza uchumi kwenye familia zao kwa kuanzisha vikundi vya kijasiriamali vinavyochangia pia kupunguza umasikini kwenye jamii suala ambalo linachangia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii. Anasema vituo vya taarifa na maarifa vimekuwa vikiunganisha nguvu na serikali na vyombo vingine vya dola kuhakikisha wanapambana na vitendo vya ukatili kwa kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake kwa watu wanaohusika ama kutuhumiwa na vitendo vya ukatili. Alitolea mfano katika eneo la Mwananyamala Kituo cha Taarifa na Maarifa kilishirikiana na Serikali kwa kuibua taarifa ya kuteswa kwa binti wa kazi za ndani na mwajiri wake jambo ambalo liliwezesha bosi huyo kufikishwa mahakamani. "...Hivyo waweza kuona matokeo makubwa katika mradi wa GEWE ni kuanzishwa vituo vya taarifa na maarifa sehemu ambayo imekuwa ni kimbilio la wengi, na pili ni nguvu ya pamoja ya jamii katika uwajibikaji. Lakini changamoto iliyopo sasa ni namna ya kuwasaidia kwa kuwaifadhi waathiriwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii," alisema Mratibu huyo. Aidha aliitaka Serikali na wadau wengine kujitokeza na kushirikiana katika kujenga kituo kikubwa cha kuwasaidi wananchi ambao wamekumbana na ukatili wa kijinsia wakati wakipatiwa huduma kabla ya kurejea katika jamii yao. "...Mfano kumekuwa kuna mabinti hata hapa Dar es Salaam wamekuwa wakikimbia kukeketwa na familia zao lakini hakuna sehemu ya kuwaifadhi, hivyo tunaiomba Serikali na wadau wengine wajitokeze ili kuunganisha nguvu tujenge kituo hiki," alisema. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

VETA WATAKIWA KUHAKIKISHA WANASIKILIZA MAONI YA WADAU WAO ILIKUJUA MAHITAJI YAO SANJARI NA KUBADILISHA MITAALA YA ELIMU

$
0
0

WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka  wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwa ajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao.
 Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi akiwa anaongea katika kongamano hilo


wadau kutoka sekta ya gesi na petrol wakiwa wanafatilia


katibu mkuu wa  VET Pro.Sifuni Mchome akiwa anawakilisha mada



waziri wa ajira na kazi  Gaudensia Kabaka akiwa katika picha ya pamoja wadau waliouthuria katika  konga mano hilo
Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Bg Tanzania Ms Kate Sullam anaemfatia ni Mr Jean Van Wetter ni mkurugenzi wa VSO Tanzania
 waziri  kabaka  wa kwanza kulia akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa Idrissa Mshoro wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi ayupo pichani kuhusiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta)
 WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka  wakati alipokuwa akizindua kongamano
baadhi ya waandishi  wakiendelea kufatilia kwa makini kongamano hilo
 washiriki wakifuatilia

picha wakwanza kulia ni mwenyekiti wa bodi ya veta Idrissa Mshoro wa pili kulia ni  Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi wakiwa wanamsikiliza waziri hayupo pichani




picha ya pamoja ya washiriki wa kongamono hilo wakiwa pamoja na waziri wa ajira na kazi nje ya ukumbi wa hotel ya Naura Springs iliopo ndani ya jiji la Arusha 
 


washiriki wakiendelea kufuatilia kwa makini

Na Woinde Shizza,Arusha
 Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta)wametakiwa kuhakikisha wanasikiliza maoni ya wadau ili kujua mahitaji yao sambamba na kubadili mitaala ya elimu ya mafunzo yanayotolewa kwenye vyuo  hivyo ili kuendana na soko la ajira lililopo hivi sasa.

Hayo yanesemwa leo  jijini hapa na WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka  wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao na nini chakuongeza kwa vijana wanaopitia Veta na kupata ajira katika sekta mbalimbali sanjari na kuzindua kitabu kinachoanisha mahitaji ya soko la ajira kwa vijana
Aidha  aliwataka vijana  kutumia fursa za kujiunga na Veta ili waweze kujiariri badala ya kufanya biashara za kuuza vitu mikononi  bali  watumie taaluma walizozipata kuzalisha vitu vyenye ubora.


Alisema vijana wanaopitia vyuo vya mafunzo Veta si wengi sana huku wimbi la vijana likiwa bado mitaani na kuuza bidhaa zao mabarabarani hivyo ni vyema sasa vijana hao wakaondoka barabarani na kujiunga na vyuo vya ufundi ili waweze kupata mbinu za kutengeneza vitu sambamba na kupata masoko ya uhakika.
waandishi  wa habari wa Mkoa wa Arusha wakimuoji mwenyekiti wa bodi
Alisema ni vyema sasa Vyuo vya Veta vikaweka mkazo katika sekta ya madini na gesi ili waweze kuangalia mahitaji ya wataalam ni yapi na kutoa elimu hiyo ambayo itawezesha vijana wengi kupata ajira na kukuza uchumi wan chi.
"Mahitaji ya vijana ni mengi katika sekta rasmi na zisizo rasmi na kia sekta inamtegemea mtu fulani hivyo ni vyema Veta mkasikiliza mahitaji ya wadau sambamba na kutafuta mbinu za kufundisha zaidi ili kuendana na mahitaji ya soko na nyinyi vijana tokeni barabarani mkajiunge na vyuo vya ufundi ili kuweza kuuza biashara zenu kwa ubora badala ya kukimbilia kuuza barabarani ".
Naye Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi alisema kongamano hilo hufanyika kila mwaka na kushirikisha wadau katika sekta mbalimbali ili kujadili masuala mbalimbali na mahitaji ya wadau hao katika sekta ya ajira sambamba na kuboresha mitaala itakayokwenda na wakati na kuwezesha vijana wanaopitia Veta kuwa bora zaidi kipindi cha kumaliza chuo na kupata ajira.
Alisema pia Veta inakabiliwa na uhaba wa rasilimali fedha  kwenye ujenzi wa vyuo vipya   kwenye Wilaya mpya ambazo ni Katavi, Geita, Njombe na Simiu lakini pia kuonaongezeko kubwa la vijana na watu mbalimbali ambao wanajiunga na vyuo hivyo nchini kwaajili ya kupata mafunzo mbalimbali yanayowawezesha kupata ajira.

 Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Veta, Profesa Idrissa Mshoro alisisitiza kuwa  Veta inatambua na kuthamini maeneo mbalimbali yanayohitaji soko la ajira ndio maana vijana wanaopata ujuzi kupitia veta wanafanya kazi kwa makini na kujipatia vipato zaidi.

Aliongeza kuwa hivi sasa Veta inashirikiana na tasisi na mashirika mbalimbali hususan ya sekta ya madini na gesi na kutoa mafunzo kwaajili ya kuwasaidia vijana kukabiliana na soko la ajira .

FILIKUNJOMBE AWATIMIZIA AHADI YA MAJI WANANCHI WA KITEWELE ZAIDI YA TSH MILIONI 26 ZATUMIKA

$
0
0
Mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe kushoto akikabidhi  masaada wa vitaa vya  maji  safi  vyenye  thamani ya Tsh milioni 26  kwa wananchi  wa  kijiji  cha Kitewele  kata ya Mawengi Ludewa  leo
Wananchi  wa kijiji  cha  Kitewele  kata ya Mawengi  Ludewa  wakiwa wamebeba bomba za maji  zilizotolewa na mbunge  wao Deo Filikunjombe  kwenda  kijijini kwao umbali  wa  zaidi ya Km 6 kutoka eneo la barabara  ziliposhushwa  bomba  hizo
Wananchi  wa  kijiji  cha Kitelewe wakishiriki kubeba  bomba  za maji zilizotolewa  msaada   na mbunge  wao Filikunjombe.
Wannchi  wa Kitewele  wakimpokea mbunge Filikunjombe kushoto
Baadhi ya  wananchi  wa kitewele  wakiwakatika mkutano huo
Wananchi  wakimsikiliza mbunge  wao kwa makini


 Mbunge Filikunjombe kulia akijibu swali la mkazi wa kijiji cha Kitelewe  kushoto  huku  wakifurahi wote baada ya majibu mazuri ya kutaka wazee na vijana kuungana kushiriki katika maendeleo 
........................................................................................................
 Na matukiodaimaBlog.
WANANCHI wa Kijiji cha KITEWELE kata ya MAWENGI wilaya ya LUDEWA mkoani Njombe , wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama ya bomba baada ya kukamilika kwa ununuzi wa vifaa ikiwemo mabomba ya kutandika ardhini ambayo yamegharimu kiasi shilingi zaidi ya Milioni 26  msaada  uliotolewa na  mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe .

Akizungumza leo na  wananchi hao mara baada ya  kukabidhi vifaa hivyo  mbunge Filikunjombe alisema  kuwa  kukabidhi kwa  vifaa hivyo na mradi huo wa maji ni utekelezaji wa ahadi yake ya maji kwa  wananchi hao aliyoitoa mwaka 2012 kufiatia ombi  la  wananchi hao zaidi ya 800 waliokuwa  wakikabiliwa na adha ya maji .
Mbunge  Filikunjombe alisema  kuwa  toka  nchi itape uhuru mwaka 1961  wananchi  hao  hawajapata kuwa na maji  safi na  salama na  kuwa  miaka  yote  wamekuwa  wakitumia maji ya mito ambayo  si safi na salama kabla ya  kufika na  kuombwa  kuwasaidia kupata huduma   hiyo ya maji  safi .

“Ndugu zangu nikiwa  kama  mbunge  wenu  nimekuwa  nikiumia  zaidi  kuona  wananchi   wangu  mnapata  shida ya maji na  ndio   sababu ya  kuahidi  kuungana nanyi katika  kuwafikishia  huduma ya maji….ombi langu  kwenu tuzidi  kushirikiana  ili  kutatua  kero  zetu  bila  kusubiri wahisani “

Miaka miwili iliyopita, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, DEO FILIKUNJOMBE alishuhudia kadhia hiyo akiwa katika Zahanati ya kijiji hicho na akawaahidi wananchi kuwafikishia maji, ahadi ambayo ameitekeleza mwaka huu na kukabidhi mabomba kwa wananchi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 tayari kwa kuanza kazi ya kuchimba mitaro na kutandika mabomba hayo.

Hata   hivyo  alisema  kuwa  maendeleo ya  wananchi  wa KItelewe  na  jimbo  la  Ludewa  yataletwa na  wananchi  wenyewe  kwa  kuunganisha  nguvu  zao pasipo  kusubiri  wahisani na kuwa baadhi ya  maeneo ya wilaya  hiyo   wananchi   siku  zote  wamekuwa  wakijitolea  kushiriki katika maendeleo  mbali  mbali.

Akielezea  kuhusu adha ya maji katika  jimbo lake na jinsi  alivyoshiriki  kutatua  alisema  kuwa yapo maeneo ambayo wananchi  wamekuwa na adha kubwa ya maji  na tayari  ameanza  kumaliza kero  hiyo.

Kwa  upande  wake  diwani  wa  viti maalum tarafa ya Mawengi Bilgeter Haule aliema  kuwa moja ya  vitu  ambavyo  wana Ludewa  wanajivunia  ni  kumpata  mbunge ambaye  anawajibika kwa  wananchi kama  ilivyo kwa  mbunge   huyo.

“ Tanzania mtu  ambae hatakuj  kusaulik ni pamoja na baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere ambae  alitanagazwa  kuwa mwana heri ila kwetu  Ludewa kutokana na kero  tulizozipata  toka  uhuru  hadi  leo  ambapo  zinapatiwa ufumbuzi kwa pamoja  tutamkumbuka mheshimiwa  mbunge wetu  Deo Filikunjombe kama mwanaheri baada ya  kutatua  kero  zetu na kuondoka katika kundi  la  watanzania wasiofurahia uhuru  wao”
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images