Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 411 | 412 | (Page 413) | 414 | 415 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akiwahutubia wahitimu wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere siku ya tarehe 22 Novemba, 2014 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrak Mwakalila.
   
  Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrak Mwakalila.akiwahutubia wahitimu wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere siku ya tarehe 22 Novemba, 2014 jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wahitimu wa ngazi mbalimbali wakifuatlia hotuba toka kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Angellah Kairuki wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere siku ya tarehe 22 Novemba, 2014 jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM).

   ====================
  SERIKALI YAJIDHATITI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA SEKTA YA ELIMU CHINI.

  Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.

  SERIKALI imekuwa ikifanya jitihada za dhati katika kukabiliana na changamoto ya kushuka kwa kiwango cha wahitimu wa kidato cha Nne na Sita katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

  Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mhe. Angellah Kairuki wakati wa Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika 22 Novemba, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Kairuki aliwaeleza wahitimu hao kuwa, katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Chuo hicho inaonyesha kuwa idadi ya wahitimu imepungua kutoka wahitimu 919 mwaka jana, hadi kufikia 689 mwaka huu, hali iiyochangiwa na kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wahitimu wa vidato hivyo vya Sita na Nne.

  Alieleza kuwa, Serikali imefanya juhudi za kukabiliana na tatizo hilo kwa kuanzisha Mikakati mbalimbali ikiwemo; Mpango wa Elimu ya Shule za Msingi, Mpango wa Elimu ya Sekondari, Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi wa miaka mitano (2013/14-2017/18) pamoja na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa “Big Results Now” (BRN).

  Mhe. Kairuki alibainisha kuwa, jitihada hizo zinaonyesha dhamira ya dhati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutatua ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini.

  “Ni matumaini yangu kwamba, juhudi hii za serikali zinazaa matunda na zimeanza kujionyesha kwa kupanda kwa kiwango cha ufaulu katika shule zetu za sekondari nchini, hivyo ni dhahiri kuwa kasi ya udahili katika vyuo vyetu itaongezeka halikadhalika na idadi ya wahitimu kwa siku zijazo”, alisema Kairuki.

  Aliwaasa wahitimu wa chuo hicho na kuwataka kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kuwaharibia maisha yao zikiwemo tabia za ngono zembe pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya.

  “Ninawasihi mjiepushe na starehe na tamaa zinazoweza kuwaletea matatizo makubwa, tumieni vizuri elimu mliyoipata chuoni hapa kwa kutunza afya zenu, kuzingatia maadili mema na kutawala nafsi zenu, lakini pia jiendelezeni kitaaluma, msiridhike na viwango vya elimu mlivyonavyo”, aliongeza Kairuki.

  Naye Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrak Mwakalila alisema kuwa katika kutekeleza matakwa ya kisheria, hususani Sheria Namba Sita ya mwaka 2005 ya Chuo hicho, chuo kiliweza kukamilisha ujenzi wa Tawi la chuo cha Mwalimu Nyerere upande wa Zanzibar ambapo jengo moja lenye ghorofa Nne katika eneo la Bububu mjini humo lilizinduliwa rasmi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein siku ya tarehe 18 Mei, 2013 na limeweza kutoa fursa ya kuendesha mafunzo ya ngazi ya Cheti katika Kazi za Vijana na hivi sasa chuo kinatarajia kuongeza programu nyingine za mafunzo katika tawi hilo.

  Akizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili chuo hicho alisema kuwa, kuna uhaba mkubwa wa hosteli kwa upande wa chuo cha Kivukoni pamoja na Tawi lake la Zanzibar, pia kumekuwepo na ufinyu wa bajeti ambao unaathiri utekelezaji wa majukumu ya chuo hicho, na matatizo mengine ni mmomonyoko wa ardhi katika fukwe za Bahari ya Hindi unaohatarisha kuangusha baadhi ya majengo ya chuo hicho.

  Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 689 wakiwemo wanawake 400 sawa na asilimia 58.1 na wanawaume 289 sawa na asilimia 41.9 walihitimu elimu yao katika ngazi za Cheti, Stashahada ya Kawaida pamoja na Shahada ya Kwanza.

  0 0

   Kijana Datius akiwa katika Picha ya Pamoja na Baba yake Mzazi (nyuma ya babu yake aliyevaa miwani) Babu zake na dada zake wakati alipotunukiwa nondo yake ya elimu kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE hapo jana
   Datius Akiwa katika picha ya pamoja na Baba yake Mzazi (Kushoto) pamoja na Babu yake mdogo (kulia)
   Akivishwa taji na Dada yake aitwaye Neema
  Akiwa na Dada mara baada ya kulamba nondoz.Picha Zote na Josephat Lukaza wa http://www.josephatlukaza.com

  0 0

  SERIKALI kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtaka Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama kuongeza ufanisi zaidi katika Tamasha la Krismasi mwaka huu kwa sababu  kupitia matamasha yake anafanikisha matakwa ya jamii yenye uhitaji maalum. 

  Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza alisema  kwa mwenendo huo bora unaofanywa na Msama anatoa wito kuendeleza mwenendo huo ili kuisaidia jamii.
   
  Mungereza alisema Msama anafanikisha hayo kwa sababu anaipenda jamii ambako alitoa wito kwa wadau wa muziki wa Injili kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 hapa nchini ili kufikia malengo stahili.
   
  Katibu huyo alisema mbali ya kuchangia jamii pia kupitia tamasha hilo wananchi  wa maeneo husika wanapata fursa nyingi katika maeneo yao kama madereva bodaboda, texi na biashara nyingine.
   
  “Wananchi wa mikoa itakayofikiwa na tamasha hilo watambue kwamba ni lao, hivyo wajitokeze kwa wingi kwani viingilio vitakavyopatikana vinasaidia wenye uhitaji maalum kama yatima, wajane, walemavu na wengineo,” alisema Mungereza.
   
  Kuhusu waimbaji, Mungereza alisema waichukulie sanaa kwamba ni kazi  watumie vipaji vyao hasa wakifikiria jamii kwani wanahitajika kutoa elimu ya uraia kutoka kwao.
   
  Katika hatua nyingine, Kampuni ya Msama imepokea kibali cha kufanikisha Tamasha la Krismasi mwaka huu ambako kampuni hiyo imejipanga kufanya tamasha hilo katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
   
  Naye mmoja wa Watendaji wa Kampuni ya Msama, Jimmy Rwehumbiza aliyepokea kibali cha Tamasha la Kriamsi aliishukuru Basata kwa kufanikisha kibali sambamba na kupokea ushauri na mapendekezo yanayotolewa mara kwa mara yanayofanikisha matamasha hayo.

  0 0

  Nusu ya fainali ya kwanza ya mashindano ya DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP imepigwa hapo jana kwenye uwanja wa Bandari maeneo ya Tandika Mwembe Yanga kati ya Tabata FC na Black Six,mchezo ulimalizika kwa tabata kushinda bao 1-0 na kukata tiketi ya kucheza fainali hapo tarehe 29/11/2014 kwenye uwanja huo huo wa Bandari.mchezo huo uliweka rekodi ya mashindano ya NDONDO kwa kuhudhuliwa na mashabiki wengi.10553574_836086276455319_1176921432347220072_n Mashabiki wa BLACK SIX ya Buguruni.......... 1960140_836086329788647_6126915949753505475_nMshambuliaji wa YANGA Jerry Tegete alikuwa anaongoza mashambulizi ya timu yake ya nyumbani TABATA FC....... 10350425_836086403121973_4713464705511470346_nMkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Bwana Ruge Mutahaba,Fauzia Abdi pamoja na Ibrahim Masoud 'Maestro' walikuwepo kushuhudia mpambano huo..... 
  10382399_836086466455300_4570599094018049969_o
  Nyomiiiii.....10408076_836086479788632_905767488845041078_nMpambano kati ya Tabata FC na Black Six ukiendelea kwenye uwanja wa BANDARI maeneo ya Tandika Mwembe YANGA ukiendelea...... 


  0 0  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imeamua kuunda timu ya watu 10 kutoka kada tofauti wakiwemo viongozi wa dini ambao watapewa jukumu la kufanya kazi ya usuluhishi kwenye vijiji vyenye migogoro baina ya wafugaji na wakulima wilayani Kiteto mkoani Manyara.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Novemba 23, 2014) wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwenye ibada ya kumweka wakfu Askofu wa sita wa Dayosisi ya Central Tanganyika ya Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Dickson Chilongani iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, mjini Dodoma.

  Waziri Mkuu ambaye kwenye ibada hiyo alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete aliyeko nje ya nchi kwa matibabu alisema: “Hali ya Kiteto ni changamoto kama alivyosema Askofu Mkuu, Dk. Chimeledya lakini inahitaji ufumbuzi kutoka kwa wadau tofauti na siyo Serikali peke yake... inataka Serikali, wananchi, vyombo vya dola lakini pia na Kanisa lazima lihusishwe ili kujenga upya maadili ya jamii.

  “Ukiwa na kundi kubwa la watu ambao hawamwogopi Mungu ni tatizo. Na hii ndiyo iliyoko kule. Watu wanauana kwa sababu ya hasira, ni hasira gani hiyo inayokufanya usiogope kutoa roho ya mwenzako,” alihoji.

  Alisema timu itakayoundwa itapewa jukumu la kufanya usuluhishi na kupata maridhiano (reconciliation) kijiji kwa kijiji huku ikipeleka ujumbe wa amani. “Tunataka kutumia Kiteto kama mradi wa majaribio (pilot project) kwenye suala la kutafuta amani kwenye maeneo kama haya,” alisema Waziri Mkuu.

  Alisema wilaya ya Kiteto inaingiliana na mikoa mitano ambayo ni Tanga (Kilindi), Morogoro (Gairo); Dodoma (Kongwa) Manyara (Simanjiro) na Arusha (Monduli) hali ambayo inachangia kuwepo na muingilianio mkubwa wa kijamii.

  Waziri Mkuu alitaja hatua nyingine zitakazochukuliwa na Serikali kuwa ni kupima ardhi inayogombewa yenye ukubwa wa hekta 133,000 na kuigawa kwa wafugaji ili wafuge kwa mtindo wa ranchi na inayobakia igawiwe kwa wakulima. Vilevile, Waziri Mkuu alisema idadi ya vituo vya polisi itaongezwa kwenye miji midogo badala kutegemea kituo kimoja tu cha polisi kilichopo Kibaya.

  Alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Jacob Chimeledya ambaye alisema Serikali ina wajibu wa kulinda maisha ya kila Mtanzania na kutoa mfano wa wilaya ya Kiteto ambako alisema hakuna amani kwa sababu watu wanauana hovyo.

  Katika hotuba yake ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Askofu Chilongani alisema ameanza kukosa usingizi kutokana suala la umaskini na kukosekana mfumo wa pensheni miongoni mwa wachungaji na makasisi wa kanisa hilo hasa wa vijijini ambao alisema hawana kipto cha uhakika.

  “Makasisi na wachungaji hawa wanahudumia Watanzania wote, wanachopata ni kiasi kidogo mno kuweza kuweka kwenye mifuko kama NSSF, bado pia wana mahitaji yao, wanatakiwa wawasomeshe watoto wao... natamani kuwe na mfumo ambao utawawezesha kupata pensheni ili wanapostaafu wajikute hata wana vibanda vya uhakika vya kuishi na familia zao,” alisema na kushangiliwa na mamia ya wachungaji waliohudhuria ibada hiyo.

  Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Dk. Chilongani aliiomba Serikali isimamie zoezi hilo liwe huru na la haki na kuhakikisha linaisha kwa amani. “Niwasihi pia Watanzania wenzangu, wawachague viongozi waadilifu, wasiwachague viongozi ambao wanakimbilia uongozi au wenye kudhani kuwa ubunge au udiwani ni halali yao na siyo dhamana kutoka kwa wananchi,” alisema.

  (mwisho)

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  JUMAPILI, NOVEMBA 23, 2014.

  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu vya mkoa wa Dodoma watumie fursa waliyonayo kuisaidia nchi ya Tanzania isonge mbele na kufikia uchumi wa juu zaidi.

  Alitoa nasaha hizo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanavyuo hao kwenye ukumbi wa Chimwaga, Dodoma wakati wa mkesha wa kusifu na kuabudu (Dodoma Campus Night) ulioandaliwa maalum kwa ajili ya kuwajenga kimaadili wanafunzi wa vyuo vya mkoa huo.

  Dk. Nchimbi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kabla ya kuhamishiwa Njombe, aliwaasa wanafunzi hao waache kuendekeza matumizi ya simu za mkononi kwa kutumiana meseji ambazo zinawatoa kwenye umakini wa masomo yao. “Inasikitisha kuona mwanafunzi akiingia mwaka wa kwanza anakuwa mwema, lakini baada ya muda anarudi nyuma kimaendeleo… kisa meseji anazotumiwa”.

  “Muwe makini na masomo yenu. Angalieni mavazi yenu, angalieni mienendo yenu, jichungeni msiyumbishwe na tabia za makundi lakini kikubwa zaidi ni kutambua nafasi mlizonazo na kusimama imara ili kuisadia nchi hii isonge mbele na kufikia uchumi wa juu zaidi,” alisema.

  Mapema, akimkaribisha kuzungumza na wanafunzi hao, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG-ICC Dodoma, Dk. Gerald Ole Nguyaine aliwaambia wanavyuo kwamba wanapaswa kuiheshimu nafasi hiyo ya pekee ambayo Mungu amewapa.

  “Hebu jiulize ni wanafunzi wangapi ambao wamebaki huko nje na wanatamani kuingia Chuo Kikuu… ni lazima muwe focused ili kuitendea haki nafasi mliyoipata. Na kama unataka kuwa mtu ambaye Mungu alikusudia uwe, ni lazima ujisalimishe kwake,” alisema.


  Akitoa mafundisho kwa wanavyuo hao, Mchungaji Casey Kalaso wa Kanisa la Utume wa Kristo kutoka Kabwe, Zambia aliwataka wanavyuo hao watambue kuwa mafanikio yanakuja pale mtu anapofanya maandalizi na kutumia vizuri fursa aliyonayo.

  “Changamoto kuwa inayotukabili hivi sasa ni kwa mwanadamu kutojua majira aliyomo… watu wengi hatujui nini tunapaswa kufanya na kwa wakati gani. Usipokuwa mwangalifu utalia baadaye wakati ulichezea fursa uliyoipata sasa,” alisema.

  Akitumia mfano wa Samson na Delila kutoka kitabu cha Waamuzi (sura ya 13), aliwataka waithamini nafasi waliyonayo kwani ikipotea ni nadra kuipata tena na kuitumia vizuri.

  “Usiangalie mambo ya nyuma, angalia nafasi ya sasa unayopewa na Mungu na uifanyie kazi. Jihadhari na watu wanaokuja maisha mwako, wako wanaokuja kukuongezea thamani lakini wengine wanakuja ili kukufanya uwe dhaifu zaidi,” aliwaonya.

  Naye Mchungaji Mathew Sasali wa Kanisa la TAG Mbeya aliwataka wanavyuo hao wajitambue nafsi zao na kubaini ni picha gani ambazo zimechorwa maishani mwao kama kweli wanataka kusonga mbele maishani mwao.

  “Kuna watu waliambiwa hutafaulu kwa sababu katika ukoo wenu hakuna msomi, au fulani hutaolewa kwa sababu katika familia yenu hakuna aliyewahi kuolewa. Hizo zote ni picha zinazochorwa kwenye maisha ya watu na kuwazuia kufikia malengo wanayotamani kuyapata maishani mwao,” alisema.

  “Kama hujagundua kuwa kuna picha imechorwa maishani mwako ni lazima tu itakutesa. Hiyo picha inatabiri ni vita ya aina gani unapigana nayo. Na usipoifuta hiyo picha, huwezi kutoka kwenye maisha uliyonayo… iwe ni ulevi, uzinzi, uvivu, na kadhalika,” alisema.

  Alisema njia pekee ni kuibadilisha na kupambana na picha iliyowekwa mbele ya maisha yao. “Picha iliyo mbele yako siyo ile ambayo Mungu ameileta mbele yako. Taifa la Israel lisingeweza kwenda mbele kama picha nyingine isingechorwa mbele yao ambayo ilibadilishwa na Yoshua na Kaleb,” alisisitiza.

  Ninawasihi tuchane picha zilizoletwa mbele yetu, iwe na ndugu, marafiki, wanaukoo au wachawi. Tuchukue hatua na kuikataa picha iliyo mbele yetu ambayo iko nje ya mpango wa Mungu. Fahamu zetu zikifunguka na kuiona picha  ya Mungu, ndipo tutaanza kuchanua na kufanikiwa,” alisema.

  Katika Campus Night hiyo ambayo ilihudhuriwa na wanavyuo zaidi ya 5,000, yalifanyika pia maombi kwa ajili ya vijana wote wa Tanzania, uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Uchaguzi Mkuu wa 2015 pamoja na mchakato wa Katiba Inayopendekezwa.

  Wanavyuo hao wa dini mbalimbali wanatoka vyuo vikuu vya Dodoma (UDOM), St. John’s, Vyuo vya Mipango, Madini, Mirembe, Hombolo, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na vyuo vya ualimu vya Mitumba na Capital.

  0 0

  Pichani kiijana Suleiman Othuman akiwa amelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12. 

   Assalam Aleikum ndugu zangu mnaotusoma kwenye blog hii kila siku, msaada unahitajika kwa kijana Suleiman Othman Ally mwenye umri wa miaka 19, mkaazi wa Zanzibar, amepatwa na tatizo la uvimbe mkubwa kwenye mgongo wake baada ya kupatwa na ajali  kugongwa na Vespa kwa muda wa siku nyingi tu.

  walimpeleka Hospitali ya Mnazi mmoja ambapo ilishindikana kupata matibabu kutokana na damu nyingi aliotoka wakati wa upasuaji, hivyo kuwalazimu kumshona bila ya kumfanyia operation iliyokuwa wamemkusudia.Kijana Suleiman Othuman hali yake inazidi kudhoofika na maumivu makali alionayo kwa sasa hawezi kukaa kusimama vizuri na hata kulala inavyostahiki kwa sababu ya ule uvimbe aliokuwa nao kwenye kiuno chake kam picha inavyojionyesha.
  Hivi sasa familia yake haina budi kuomba ushirikiano wa msaada wenu kwa ajili ya kuweza kumpeleka nchini India kwaajili ya matibabu na kumgharamikia mtu wa kufuatana nae katika familia, kutokana na gharama ni kubwa na uwezo ni mdogo.Hivi sasa yuko hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12.
  Ndugu zangu tujitahidini kuokoa maisha ya ndugu yetu Suleiman Othuman kwa hali na mali.Kwa mtu yoyote atakayeguswa na habari hii, na mwenye kutaka kuchangia msaada wake anaweza kuwasiliana na Mama yake mkubwa. Bi Salma.
  Numba yaze za simu ni-:
   255777489015
  Tigo: 255655489015
  Pia unaweza kuwasiliana na Mdau wa Blog ya  Abou Shatry Number 301-278, 3977, Email swahilivilla@gmail.com

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akinyanyua mikono juu kuashiria mshikamano na baadhi ya viongozi wa makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan Kusini ambao wako kwenye mgogoro wa kugombea madaraka kwa takribani mwaka sasa. Kinana amekutana na viongozi hao wakati wa mkutano wa hadhara mjini Masasi, Mtwara baada ya kumfuata kutaka ushauri wa upatanishi kutoka kwao Sudani Kuzini. Baada ya ya viongozi hao kupata wasaa wa kusalimia wananchi katika mkutano huo alifanya nao mazungumzo Ikulu Ndogo ya Masasi. 
   Kinana akiwa katika mkutano wa kuwapatanisha viongozi hao, usiku huu Ikulu Ndogo ya Masasi, Mtwara

  0 0

   Kwaya ya pamoja inayojumuisha Vyuo vikuu vyote vya Dodoma (Mass Choir) ikiimba wimbo maalum kwenye mkesha wa kusifu na kuabudu uliosema ‘Dodoma izidi kung’ara’ ikiwa ni sehemu ya maombi yao kwa mkoa huo
      Kwaya ya New Life Band ya Arusha ikitoa burudani ya kuimba kwa bass bila ala za muziki kwenye mkesha wa kusifu na kuabudu (Campus Night) uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Chimwaga, mjini Dodoma. 
  Kwaya ya Abednego & The Worshippers ya Arusha ikitoa burudani kwenye mkesha wa kusifu na kuabudu (Campus Night) uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Chimwaga, mjini Dodoma. Picha zote na habari na Irene Bwire
   MKUU wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu vya mkoa wa Dodoma watumie fursa waliyonayo kuisaidia nchi ya Tanzania isonge mbele na kufikia uchumi wa juu zaidi. 

   Alitoa nasaha hizo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wanavyuo hao kwenye ukumbi wa Chimwaga, Dodoma wakati wa mkesha wa kusifu na kuabudu (Dodoma Campus Night) ulioandaliwa maalum kwa ajili ya kuwajenga kimaadili wanafunzi wa vyuo vya mkoa huo.

   Dk. Nchimbi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kabla ya kuhamishiwa Njombe, aliwaasa wanafunzi hao waache kuendekeza matumizi ya simu za mkononi kwa kutumiana meseji ambazo zinawatoa kwenye umakini wa masomo yao.

   “Inasikitisha kuona mwanafunzi akiingia mwaka wa kwanza anakuwa mwema, lakini baada ya muda anarudi nyuma kimaendeleo… kisa meseji anazotumiwa”. “Muwe makini na masomo yenu. Angalieni mavazi yenu, angalieni mienendo yenu, jichungeni msiyumbishwe na tabia za makundi lakini kikubwa zaidi ni kutambua nafasi mlizonazo na kusimama imara ili kuisadia nchi hii isonge mbele na kufikia uchumi wa juu zaidi,” alisema.

   Mapema, akimkaribisha kuzungumza na wanafunzi hao, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG-ICC Dodoma, Dk. Gerald Ole Nguyaine aliwaambia wanavyuo kwamba wanapaswa kuiheshimu nafasi hiyo ya pekee ambayo Mungu amewapa. 


   “Hebu jiulize ni wanafunzi wangapi ambao wamebaki huko nje na wanatamani kuingia Chuo Kikuu… ni lazima muwe focused ili kuitendea haki nafasi mliyoipata. Na kama unataka kuwa mtu ambaye Mungu alikusudia uwe, ni lazima ujisalimishe kwake,” alisema.
  Akitoa mafundisho kwa wanavyuo hao, Mchungaji Casey Kalaso wa Kanisa la Utume wa Kristo kutoka Kabwe, Zambia aliwataka wanavyuo hao watambue kuwa mafanikio yanakuja pale mtu anapofanya maandalizi na kutumia vizuri fursa aliyonayo. 
   “Changamoto kuwa inayotukabili hivi sasa ni kwa mwanadamu kutojua majira aliyomo… watu wengi hatujui nini tunapaswa kufanya na kwa wakati gani. Usipokuwa mwangalifu utalia baadaye wakati ulichezea fursa uliyoipata sasa,” alisema. 
   Akitumia mfano wa Samson na Delila kutoka kitabu cha Waamuzi (sura ya 13), aliwataka waithamini nafasi waliyonayo kwani ikipotea ni nadra kuipata tena na kuitumia vizuri. 
   “Usiangalie mambo ya nyuma, angalia nafasi ya sasa unayopewa na Mungu na uifanyie kazi. Jihadhari na watu wanaokuja maisha mwako, wako wanaokuja kukuongezea thamani lakini wengine wanakuja ili kukufanya uwe dhaifu zaidi,” aliwaonya. 
   Naye Mchungaji Mathew Sasali wa Kanisa la TAG Mbeya aliwataka wanavyuo hao wajitambue nafsi zao na kubaini ni picha gani ambazo zimechorwa maishani mwao kama kweli wanataka kusonga mbele maishani mwao. 
   “Kuna watu waliambiwa hutafaulu kwa sababu katika ukoo wenu hakuna msomi, au fulani hutaolewa kwa sababu katika familia yenu hakuna aliyewahi kuolewa. Hizo zote ni picha zinazochorwa kwenye maisha ya watu na kuwazuia kufikia malengo wanayotamani kuyapata maishani mwao,” alisema. 

   “Kama hujagundua kuwa kuna picha imechorwa maishani mwako ni lazima tu itakutesa. Hiyo picha inatabiri ni vita ya aina gani unapigana nayo. Na usipoifuta hiyo picha, huwezi kutoka kwenye maisha uliyonayo… iwe ni ulevi, uzinzi, uvivu, na kadhalika,” alisema. 

   Alisema njia pekee ni kuibadilisha na kupambana na picha iliyowekwa mbele ya maisha yao. “Picha iliyo mbele yako siyo ile ambayo Mungu ameileta mbele yako. Taifa la Israel lisingeweza kwenda mbele kama picha nyingine isingechorwa mbele yao ambayo ilibadilishwa na Yoshua na Kaleb,” alisisitiza.

  " Ninawasihi tuchane picha zilizoletwa mbele yetu, iwe na ndugu, marafiki, wanaukoo au wachawi. Tuchukue hatua na kuikataa picha iliyo mbele yetu ambayo iko nje ya mpango wa Mungu. Fahamu zetu zikifunguka na kuiona picha ya Mungu, ndipo tutaanza kuchanua na kufanikiwa,” alisema. 
   Katika Campus Night hiyo ambayo ilihudhuriwa na wanavyuo zaidi ya 5,000, yalifanyika pia maombi kwa ajili ya vijana wote wa Tanzania, uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Uchaguzi Mkuu wa 2015 pamoja na mchakato wa Katiba Inayopendekezwa. 

   Wanavyuo hao wa dini mbalimbali wanatoka vyuo vikuu vya Dodoma (UDOM), St. John’s, Vyuo vya Mipango, Madini, Mirembe, Hombolo, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na vyuo vya ualimu vya Mitumba na Capital.

  0 0

  Kundi linalojulikana kwa jina la Kataa Unene Family (KUF) linaloongozwa na mwanadada Angel Msangi limeadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake na kujiwekea malengo ya kusaidia idadi kubwa zaidi ya wenye uhitaji wa afya bora kwa kula kwa afya na mazoezi.

  Kundi hilo lenye wanachama 30 limeadhimisha mwaka kwa kufanya mazoezi ya pamoja ikiwa ni pamoja na Aerobics, Kuogelea na Kucheza dansi katika Gym ya Rio iliyopo jijini Dar es Salaam na baadae kupata chakula cha pamoja cha usiku.
  KUF ina wanachama kutoka mikoa mbalimbali nchini Ujerumani, Marekani na Uingereza.
  Akizungumza katika sherehe hiyo ya maadhimisho ya mwaka mmoja, kiongozi wa kundi hilo Angel Msangi amesema anafarijika kuona watu wanapungua na kuwa na miili na ngozi nzuri kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu na kuwa na nia kutoka moyoni
  Kula kwa afya na kufanya mazoezi.
   Wanakikundi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kufanya mazoezi. 
   KUF wakifanya mazoezi.

   Badhi ya Wanakikundi cha KUF walipokutana pamoja.
   Kila mmoja akitafakari.
   Marafiki wakifurahi.
   Mpiga picha wetu Ester Ulaya nae akipata ukodak.
  Ukodak.
   Zoezi la kuogelea likiendelea baada ya Aerobics.
   Chakula
  Kiongozi wa KUF Angela Msangi akikabidhiwa zawadi na Agnes Byera kwa kazi nzuri anayofanya ya kulingoza kundi.


  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Uwekezaji Nchini (UTT-AMIS), Joseph Kuzilwa akizungumza wakati wa Mkutano Maalum wa Tatu wa Wawekezaji uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa UTT-AMIS, HamisKibola, akizungumza wakati wa Mkutano Maalum wa Tatu wa Wawekezaji.
  Simon Higangala, akifafanua jambo wakati wa Mkutano Maalum wa Tatu wa Wawekezaji.
  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (UTT-AMIS), Joan Msofe akifafanua jambo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano Maalum wa Tatu wa Wawekezaji nchini.

  Baadhi ya wanachama wa UTT, wakichangia mada wakati wa Mkutano Maalum wa Tatu wa Wawekezaji nchini.
  Baadhi ya wanachama wa UTT, wakichangia mada wakati wa Mkutano Maalum wa Tatu wa Wawekezaji nchini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Uwekezaji (UTT-AMIS), HamisKibola (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Uwekezaji Nchini (UTT-AMIS), Joseph Kuzilwa.
  Wanachama wa Mfuko wa Uwekezaji (UTT-AMIS).

  0 0  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori  akitoa akifafanua jambo wakati wa semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na NSSF na kufanyika mjini Bagamoyo, mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu, Meneja wa Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma  na Meneja wa NSSF Mkoa wa Kibaha, Ummy Lweno. 
   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kufanyika mjini Bagamoyo.
   Meneja wa Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma akizungumza katika semina hiyo.
    Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori  akitoa mada wakati wa semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na NSSF na kufanyika mjini Bagamoyo.
   Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
   Washiriki wa semina wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwakilishwa.
   Wadau wa NSSF wakiwa katika mkutano huo.
   Maofisa wa NSSF wakiwa katika mkutano huo.
   Maofisa wa NSSF wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
  Meneja wa Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Chiku Matesa.
   Mgeni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo.
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu akiagana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori mara baada ya kufungua semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kufanyika mjini Bagamoyo jana. Katikati ni Meneja Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma.
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu (katikati), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kulia) na Meneja Idara za Serikali na Balozi NSSF, Rehema Chuma wakiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wakati wa semina ya wadau wa Kada ya Utumishi wa Idara na Asasi za Serikali iliyoandaliwa na NSSF mjini Bagamoyo.
    
  Na Mwandishi Wetu

  NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hab Mkwizu, amewataka waajiri na wanachama wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kujadili changamoto zinazokabili shirika hilo na kuzitatua.

  Mkwizu aliyasema hayo mjini Bagamoyo katika semina iliyoandaliwa na NSSF ikiwa ni utaratibu wa shirika hilo kukutana na wadau wake.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji sekta ya kilimo hasa kwa wakulima wadogo wadogo, mkutano huo ulifanyika leo Novemba 23-2014 katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha.
  Washiriki wa mkutano wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji wa Sekta ya kilimo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akifungua mkutano huo leo Novemba 23-2014 katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji sekta ya kilimo leo Novemba 23-2014 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa 17 wa kitaifa wa Taasisi za Fedha kuhusu changamoto na fursa katika suala zima la uboreshaji sekta ya kilimo leo Novemba 23-2014 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa AICC Arusha. (Picha na OMR)

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu (kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (wa pili kushoto), wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mpango Maalum wa Airtel kwa wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia) na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Lyamba wakipiga ngoma baada ya Waziri, kuzindua Mpango Maalum wa Airtel kwa wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akionyesha kadi maalum ‘Premier Card’ aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), baada ya kuzindua Mpango Maalum wa Airtel kwa wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa Mpango Maalum wa Airtel kwa wateja wake wakubwa ‘Airtel Premier’ utakaowawezesha kunufaika na huduma za hadhi ya juu katika viwanja vya ndege Duniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 watakaponunua bidhaa na kupata huduma mbalimbali nchini, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua mpango maalumu utakaowawezesha wateja wake wakubwa kufurahia huduma za ziada wawapo kwenye kazi zao.  Mpango huu wenye lengo la  kuwazawadia wateja wa Airtel utakuwa na  kadi maalumu ya kusafirisha yaani (Priority Pass)  itayowawezesha wateja wakubwa wa Airtel kupata huduma ya hadhi ya juu kwenye viwanja vya ndege duaniani na  pia  kupata punguzo la hadi asilimia 30 pindi watakapo nunua bidhaa na kupata huduma nchini

  Kufatia uzinduzi huo wateja wa Airtel sasa wataweza kuunganishwa na huduma za hadhi ya juu kwenye viwanja vya ndege zaidi ya 700 duniani na  hivyo kupata  viburudisho, urahisi wa huduma yaani (VIP services) pindi wasafiripo na kuwawezesha kufurahia safari zao

  Sambamba na hilo wateja hao pia watapata punguzo la hadi asilimia 30 pale watakapopata huduma au kununua bidhaa katika maeneo mbalimbali ikiwemo hotel, migahawa, maduka makubwa and sehemu nyingine nyingi.

  Akiongea wakati wa uzinduzi huo,Waziri wa Nchini katika ofisi ya Waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr. Mary Nagu alisema” nawapongeza sana Airtel kwa kuzindua mpango huu maalumu na kuwazawadi wateja na watanzania nchini.  Nafurahi kuona pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya mawasiliano lakini bado tunashuhudia Airtel inajipanga na kujikita katika kuboresha huduma kwa wateja wake.

  Natumaini kadi hizi maalumu tunazozindua leo zitawaweza watanzania kupata mwanya wa kutengeneza mahusiano na kutanua wigo wa marafiki wa kibiashara na mwisho kuweza kuvumbua fulsa mbalimbali za kibiashara duniani.”

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema “ kupitia huduma hii tunadhirisha lengo letu la kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma zetu. Tunauhakika kadi hii maalumu  ya kupata huduma zenye hadhi katika viwanja vya ndege mbalimbali duniani hazitarahisha  safari zao tu bali zitawawezesha kufanya mahusiano ya muda mrefu ya kibiashara kwa wale watakaokutana nao wakati wa safari.

  Ni matumaini yangu kuwa mpango huu utaleta tija na kuwapatia wateja wetu unafuu wa kutanua biashara  zao,

  Katika halfa hiyo Airtel pia ilizindua pia huduma yake ya internet ijulikanayo kama Home Wi-Fi solution,

  kwa kupitia huduma hii ya Airtel Wi-Fi mteja anaweza kuunganisha simu zaidi ya 32 katika kifaa kimoja cha Wi-Fi , kuunganisha hadi simu za mkononi 4 na kuwaunganisha na Wi- Fi ya nyumbani hata kama wakiwa mbali na nyumbani wakati wote mahali popote nchini. Hii ina maana kwamba sasa wateja wa Airtel wanaunganishwa na kifaa kimoja cha familia , kwa kupitia kifurushi kimoja, kupitia huduma hii mpya ya Airtel Wi-Fi


  0 0

  MSANII wa muziki wa mashairi, Said Machenje, amesema ameanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kuhakikisha kuwa anakuwa mmoja wa wasanii watakaotoa burudani kali katika tamasha la NSSF Handeni Kwetu, linalotarajiwa kufanyika katika Desemba 13 mwaka huu, katika Uwanja wa Azimio, mjini Handeni, mkoani Tanga.

  Machenje anayeshindana vilivyo na mkali wa muziki huo, Mrisho Mpoto alisema kuwa maandalizi yake yanakwenda sambamba na shauku ya kutembelea kwa mara ya pili wilayani Handeni.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Machenje alisema kwamba mwaka jana alipanda jukwaani kuimba kwa kushirikiana na kikundi cha Naukala Ndima, ila msimu huu amefanikiwa kupata mwaliko wake binafsi.

  Mwimbaji huyo wa 'Kajenge kwa Mumeo' na 'Mila', alisema kwa kualikwa binafsi, kunamfanya apate hamu ya kujiandaa kwa ajili ya kufanya mambo makubwa zaidi ili kuonyesha umahiri wake katika tasnia ya muziki wa mashairi.

  “Nashukuru Mungu kwa kupangwa kuwa mmoja wa wasanii watakaotoa burudani katika tamasha la NSSF Handeni Kwetu 2014, wilayani Handeni mkoani Tanga kwakuwa ni mwelekeo mzuri katika maisha yangu ya sanaa.

  “Nafanya mazoezi makali kwa ajili ya kujiweka sawa ili nifanye shoo nzuri Desemba 13, katika Uwanja wa Azimio, ukizingatia kuwa nina uzoefu sasa na jukwaa la tamasha hili la aina yake,” alisema.

  Wadhamini tamasha hilo ni Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Phed Trans, SmartMind & Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd kwa kupitia kitabu cha ‘Ni Wakati wako wa kung’aa, Handeni Kwetu Foundation, Wait & Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt Ltd na Michuzi Media Group.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu mwishoni mwa wiki amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mkinga na Pangani kuhimiza wanawake kujiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuunga mkono juhudi za Serikali katika ujenzi wa Maabara.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Mh. Ummy Mwalimu akikabidhi kadi ya (UWT) kwa Bi. Halima Kassim mmoja wa wanachama wapya katika Kata ya Maramba, Wilaya ya Mkinga.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Mh. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wapya wa UWT mara baada ya kuwakabidhi kadi zao. Waliosimama kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mkinga, Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Bi. Mboni Mgaza na Mbunge wa Viti Maalumu Al-Shymaa Kwegyir.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Mh. Ummy Mwalimu (Wa nne kutoka kulia) akipata maelezo ya ujenzi wa maabara kutoka kwa Mwalimu Cyprian Taabani kutoka Shule ya Sekondari Daluni, wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Daluni Mwanakombo Gobeto.
  Mh. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga akikabidhi bati (50) kwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Hafsa Mtasiwa ikiwa ni jitihada za kuunga mkono ujenzi wa maabara.

  0 0

   .Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya SILAFRICA Tanzania, Alpesh Patel (kulia), akikabidhi funguo za gari kwa mshindi wa shindano la Uza na Ushinde bidhaa za SIMTANK bwana Hiren Chandarani ambaye ni Mkurugenzi wa RAVI STEEL, anayeshuhudia (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa RAVI STEEL, Ravi Chandarana.makabidhiano hayo yalifanyika makao makuuu ya SILAFRICA Tanzania Novemba 22, 2014 jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya SILAFRICA Tanzania, Alpesh Patel akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumkabidhi mshindi gari.
  Wakiwa kwenye picha ya pamoja. HABARI /PICHA NA PHILEMON SOLOMON
  Kampuni ya Silafrica Tanzania Ltd, inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya plastiki imekabidhi gari aina ya RAV 4 kwa wakala wake wa bidhaa za SIMTANK ambaye aliibuka  mshindi wa kwanza wa shindano la Uza na Ushinde lililokuwa likiendeshwa na kampuni hiyo kwa lengo la kuhamasisha mauzo ya SIMTANK pamoja na kuthamini mchango wa mawakala katika kampuni hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano hayo, Ofsa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa SILAFRICA, bwana Alpesh Patel alimtangaza bwana Hiren Chandarana kutoka  RAVI STEEL kuwa ndiye mshindi wa kwanza wa promosheni yao.

  Leo tunamkabidhi zawadi yake mshnindi wa kwanza, ambayo kimsingi inahitimisha promosheni yetu kwa mwaka huu, hivyo niwapongeze mawakala wote walioshiriki promosheni yetu, na wajiandae kujitokeza kwa wingi mwakani’ alisema Alpesh.

  Akiielezea zaidi promosheni ya Uza na Ushinde, Bwana Alpesh alisema zaidi ya mawakala 27 wamejishindia zawadi kutoka SIMTANK.

  Bwana Alpesh pia alimshukuru bwana Hiren kwa juhudi zake katika mauzo na kuwaomba mawakala wengine kuongeza bidii ili kujiweka katika nafsi kushinda zawadi kutoka SIMTANK siku zijazo.

  Akipokea zawadi hiyo Bwana Hiren aliipongeza kampuni ya SIMTANK kwa kuzalisha bidhaa bora ambazo pamoja na kumuingizia kipato lakini zinasaidia watanzania kupata huduma bora.

  Naishukuru sana SIMTANK kwa zawadi hii,lakini pia niwape shukrani mawakala wenzangu kwa kushiriki katika kuhakikisha tunaboresha maisha ya mamilioni ya watanzania wanaotumia huduma za maji safi na salama yaliyohifadhiwa katika tanki imara na salama” alisema Hiren.


  0 0
 • 11/24/14--10:22: Article 5


 • 0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi na kuwaambia kila mtu kwenye utumishi wa serikali inabidi awajibike katika kufanikisha lengo na asiyeweza inabidi aachie ngazi alisema lazima tutangulize utumishi kwa umma.
   Kadi zilizorudishwa kutoka kwa wananchama wa vyama pinzani ambao kwa hiyari yao leo wamerudi na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi ya aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama cha NLD Taifa Ndugu Frank Rashid Maulano aliyejiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa jimbo la Lulindi wilayani Masasi.
  Wanachama wapya waliojiunga na CCM pamoja na jumuiya zake wakinyoosha kadi zao juu wakati wa kula kiapo cha uanachama mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Machombe ambapo alipita kukagua ujenzi wa Bwawa la maji litakalo saidia kaya 150 kata ya Marika jimbo la Lulindi wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
   Wananchi wa Kijiji cha Machombe wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana anayetembea nchi nzima kukagua miradi mbali mbali ambayo zilikuwa ahadi za CCM.

   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Bwawa la maji akiongozana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mh. Farida Mgomi pamoaja na wanakijiji cha Machombe kata ya Marika.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizorudishwa na wapinzani wakati wa kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Marika wilayani Masasi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Marika ikiwa sehemu ya kujenga na kukiimarisha chama cha Mapinduzi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Chiungutwa jimbo la Lulindi wilayani Masasi ambapo alikagua maendeleo ya mradi wa maji wa Chiungutwa mradi ambao utasaidia vijiji 27,tarafa 3 ambapo watu zaidi ya elfu 60 watanufaika na mradi huo.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa wilaya ya Masasi ambapo aliwapongeza kwa kutambua utapeli wa vyama vya upinzani katika kijiji chao na kuamua kujitenga nao kabisa.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa ambapo aliwapongeza kwa kuwa na Mbunge mchapa kazi anayejali wananchii wake,Kinana aliwaambia wananchi hao wahakikishe wanajiandikisha tayari kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa.
   Mbunge wa Jimbo la Lulindi ( CCM ) Jerome Bwanausi akihutubia wakazi wa kijiji cha Chiungutwa na kuwaeleza maendeleo ya utekelezaji wa ahadi za CCM kwenye jimbo lake wakati wa mkutano wa hadhara ambao mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
   Mbunge wa zamani wa mkoa wa Mtwara John Aidi aliyekuwa mbunge wa Mtwara miaka ya 75 mpaka 85 na aliwahi kuwa mbunge wa Masasi miaka ya 65 mpaka 70 akifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye kijiji cha Chiungutwa wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.

older | 1 | .... | 411 | 412 | (Page 413) | 414 | 415 | .... | 1898 | newer