Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46129 articles
Browse latest View live

JEBBY AMERUDI NA WIMBO MPYA

0
0
Msanii wa siku nyingi wa kundi la TMK UNIT jebby anatatajia kuachia wimbo wake mpya kuanzia tarehe 25 mwenzi huu au tareha 5 mwezi wa kumi na mbili mwaka huu.

akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com amesema kuwa alikuwa amekaa kimya mda mrefu bila kuaachia wimbo wowote kutokana na changomoto za kimziki na maisha nje muziki.

hata hivyo jebby aliuambia mtandao huu kuwa wimbo wake ameufanya katika studio mazuu record na producer wa wimbo huu ni mazuu na kuomba watanzania kumpokea tena kama ambayo walikuwa wakimpokea hapo awari.

 edited by fredy mgunda

KIKUNDI CHA SANAA MIALE KUTOKA NA FILAMU MPYA

0
0
  
NA DENIS MLOWE, IRINGA.

MSANII anayekuja kwa kasi Nyanda za Juu Kusini katika tasnia ya filamu Khamis Nurdin amefanikiwa kumaliza filamu yake ya 990 WAMEKUFA’ ambayo pia imewashilikisha wasanii wakubwa wawili Kulwa Kikumba  ‘Dude’ na Mohamed Fungafunga ‘Jengua’

Akizungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki katika ofisi za gezeti hili, Nurdin alisema kuwa filamu hiyo yenye kisa cha baadhi ya watu wanaomini nguvu za giza katika maisha yao na kuifanya mizimu kuwa sehemu ya inakuja kuwageuka baada ya kukosea masharti.

Alisema kuwa filamu hiyo itakuwa na mwendelezo wa sura ya kwanza na ya pili ambayo imeweza kuwakusanya asilimia kubwa ya wasanii wa mkoa wa Iringa na kuwashirikisha baadhi wenye majina kwa makusudi ya kuwaongezea utamu na ujuzi katika filamu kutokana na soko linavyohitaji.

Nurdin alisema kuwa filamu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa Desemba mwaka huu na kuwashirikisha wasanii mbalimbali na viongozi wa serikali na wafanyabiasha wakubwa walioko mkoani hapa katika kumsindikiza katika uzinduzi huo.

“Soko la Filamu mkoani Iringa linakabiliwa na changamoto kubwa sana kwa sasa ila bila juhudi zetu hakika tutashindwa kufikia ndoto ambazo wasanii wengi tunatarajia kufika kwa upande wangu nina uhakika filamu hii itafanya vizuri na nawaomba sana wadau wa kazi za filamu wasisite kununua kazi yangu mara baada ya kutoka sokoni.” Alisema Nurdin

Nurdin aliwashukuru baadhi ya wadau wa filamu kwa kuweza kumsaidia katika kufanikisha umalizaji wa filamu hiyo akiwemo Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga kwa kuchangia na kudhamini siku ya uzinduzi wa filamu hiyo.

Filamu hiyo inatarajia kuvuta hisia za wakazi wengi wa Nyanda za Juu Kusini na Tanzania kwa ujumla kutokana na ubora wa mpiga picha anayefanya vizuri kwa sasa mkoani hapa na baadhi ya mikoa Fulko Makanza

Article 1

0
0

Taratibu za Tiba za Rais zakamilika

0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taratibu za Tiba za Rais zakamilika.

Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.

Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.

Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.

Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.

Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.

Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Novemba,2014

GAPCO YAZINDUA KADI MAALUM ZA SAFARI ZITAKAZOWEZESHA DEREVA KUPATA UNAFUU WA BEI YA MAFUTA KATIKA VITUO VYOTE, TANZANIA

0
0
 Rais wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar akipongezana na Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa tatu kushoto) baada ya kuzindua kadi maalum za Safari za kampuni hiyo zitakazomwezesha dereva kupata huduma ya mafuta kutoka vituo vyote vya Gapco nchini kwa unafuu. Wengine (kustoka kushoto) ni Rais wa kampuni ya RIL ya Mumbai, Ashok Dhar, Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na Mkurugenzi wa kituo cha Gapco, Barabara ya Nyerere, Muntazir Bharwani.
  Rais wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar akikabidhi kadi maalum za Safari kwa Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara na Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki baada ya kuzindua kadi hizo zitakazomwezesha dereva kupata huduma ya mafuta kwa unafuu katika hafla iliyofanyika Kituo cha Mafuta Gapco cha Kamata, Dar es Salaam jana. Wengine (kutoka kushoto) ni Rais wa kampuni ya RIL ya Mumbai, Ashok Dhar, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
Rais wa Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok akionesha kadi maalum za Safari za Gapco baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika kituo cha mafuta cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana. Kadi hizo zitamwezesha dereva kuweza kupata huduma ya mafuta kwa unafuu kutoka vityo vyote vya Gapco Tanzania. Kutoka kushoto ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Gapco Tanzania, Vijay Nair, Diwani wa Kata ya Gerezani, Salum Bisarara, Diwani wa Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa tatu kushoto), Meneja Miradi wa Gapco, Mohit Shirma, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
 Meneja Uendeshaji wa Kadi za Gapco, Shital More akielezea matumizi ya kadi maalum za Safari kwa Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (katikati) baada ya kuzindua rasmi kadi hizo zitakazomwezesha dereva kupata huduma ya mafuta kwa unafuu katika vituo vyote vya Gapco nchini katika hafla iliyofanyika kituo cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana. Wengine (kutoka kushoto) ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu, Meneja Miradi wa Gapco Tanzania, Mohit Shirma, Rais wa kampuni ya Reliance Industries Limited ya Mumbai, Ashok Dhar na maofisa wengine wa Gapco.
Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki (wa pili kulia) akifurahia jambo baada ya kuelekezwa matumizi ya kadi maalum za Safari Gapco na Meneja Miradi wa Gapco Tanzania, Mohit Shirma baada ya kuzindua kadi hizo, katika kituo cha mafuta cha Gapco Kamata, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu na maofisa wengine wa Gapco.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Gapco, Dk. Macharia Irungu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi maalum za Safari zitakazomuwezesha dereva kupata unafuu wa mafuta kutoka katika vituo vyote vya Gapco, Dar es Salaam jana.
 Diwani wa Kata ya Kariakoo, Abdulkarim Masamaki akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi maalum za Safari zitakazomuwezesha dereva kupata unafuu wa mafuta kutoka katika vituo vyote vya Gapco, Dar es Salaam jana.
---
Kampuni inayoongoza kwa uuzaji wa bidhaa za mafuta nchini, imezindua programu aminifu kuwezesha wamiliki wa magari kujipatia pointi wakinunua mafuta ambazo zitawawezesha kupata ‘Mafuta Bure’ Kama faida.
Mpango huu utawanufaisha wakazi wa Dar es Salaam, kwa kuanzia na nchini kote mwakani.
Jerry Slaa, Maya wa Manispaa ya Ilala akizungumza katika sherehe ya uzinduzi iliyofanyika katika kituo cha GAPCO Kamata jijini Dar es Salaam alisema: "kuanzishwa kwa programu ya GAPCO Safari kutasaidia kutatua changamoto za muda mrefu zinazowakabili wamiliki wa magari nchini. Mfumo huu ni muhimu kuelekea jamii ya kufanya malipo bila fedha taslimu.”
Slaa alipongeza GAPCO kwa kuwa Kampuni ya kwanza katika sekta ya mafuta Kurudisha thamani ya fedha kwa wateja wake nakuomba Kampuni zingine kufuata nyayo za GAPCO.Alibainisha kuwa huduma hii itasaidia kupunguza kwa ujumla, gharama za mafuta, kupunguza bugudha ya makaratasi na kusaidia kuendesha biashara kwa ufanisi zaidi.
Slaa aliongeza kwamba maendeleo kama hayo ni muhimu katika kuboresha uchumi wa nchi kwa kuwa usafiri ni moja ya nguzo muhimu ya uchumi wa Tanzania. Slaa alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi hizo ili kuboresha sekta ya usafiri nchini.Dr Macharia Irungu, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) GAPCO Group alisema GAPCO ina maslahi mapana katika soko la Afrika Mashariki na inajivunia kuwa na vituo vya mafuta 63 nchi nzima, na kuifanya GAPCO kuwa moja ya kampuni ya mafuta inayoongoza.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi kuzindua rasmi mpango, Bw. Ashok Dhar, Rais wa Reliance Industries Limited India, kampuni mama ya GAPCO Tanzania Ltd, alisema kuwa mpango huu unawakilisha sehemu ndogo ya faida ya GAPCO.Bw. Dhar alisema anaimani na Uchumi wa Tanzania, na hivyo kampuni yake itaendelea kuwekeza zaidi nchini kwa miaka ijayo.
Akifafanua zaidi juu ya programu ya GAPCO Safari, Vijay Nair, Afisa Uendeshaji (COO) alisema kuwa kadi za Gapco Safari zitakuwa zinapatikana wakati wowote katika vituo vya mafuta vya GAPCO mkoani Dar Es Salaam kwa kuanzia.mtendaji alieleza kuwa huduma hiyo ilikuwa wazi kwa wamiliki binafsi, kampuni na wafanya biashara ya magari.
"Tunataka kuboresha zaidi huduma zetu za uuzaji mafuta kwa wateja wetu. GAPCO tunaandhisha huduma ya kutoa huduma aminifu ambayo ni suluhisho kwa wamiliki wa magari nchini kote… Hii ni huduma ya kipekee tuliyo ianzisha tukiamini kupitia Kauli mbiu ‘……….’," alisema Bw Nair.

TASAF YAIBUKA KIDEDEA KATIKA UZINGATIAJI WA TARATIBU ZA MANUNUZI (2013/14)

0
0
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF umekuwa Mshindi wa kwanza miongoni mwa taasisi za serikali na mashirika ya umma yanayofanya manunuzi makubwa nchini na hivyo kutunukiwa tuzo ya uzingatiaji wa taratibu na kanuni za manunuzi kwa kipindi cha mwaka 2013/2014.

TASAF imekuwa miongoni mwa taasisi zilizoshinda tuzo ya ubora wa manunuzi kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka 2013/2014 na kukabidhiwa tuzo katika hafla iliyofanyika mjini Nairobi nchini Kenya ambako Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga aliipokea tuzo kwa niaba ya taasisi hiyo ambayo kwa sasa iko katika jitihada kubwa za kulisaidia taifa kuondokana na umaskini kupitia mpango wake wa kunusuru kaya maskini PSSN.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga  amesema licha ya taasisi yake kufanya manunuzi makubwa kutokana na uwingi wa shughuli za kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya maskini, kanuni, taratibu na sheria za manunuzi ya umma zimekuwa zikizingatiwa kwa kiwango kikubwa. Bw. Mwamanga amesema kwa takribani miaka mitatu mfululizo TASAF imekuwa ikipata hati safi ya manunuzi na kuwa miongoni mwa taasisi za serikali na mashirika ya umma zinazofanya vizuri katika uzingatiaji wa sheria ya manunuzi nchini.

Zifuatazo ni picha za upokeaji wa tuzo hiyo zilizofanyika Nairobi-Kenya
 Mkurugenzi  Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (mwenye Kaunda suti) akiwa  na ngao ya ushindi wa kwanza ya uzingitiaji wa kanuni za manunuzi nchini kwa mwaka 2013/14

 Mkurugenzi  Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (kushoto) aliyeshika ngao ya ushindi  wa kwanza (kulia kwake) ni  Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA Bw. Marten Lumbanga.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Susan Mlawi (kushoto) alikuwa miongoni  mwa wageni walioalikwa kwenye hafla ya kukabidhi  tuzo ya manunuzi kwa taasisi za Serikali na mashirika ya umma kwa nchi za Afrika Mashariki iliyofanyika mjini Nairobi, Kenya
 Baadhi ya viongozi wa taasisi zilizo shinda tuzo ya manunuzi  kwa mwaka  2013/14 kutoka nchi za Afrika Mashariki.

Serikali yaipongeza TPHA katika sekta ya afya nchini

0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk.
Margaret Mhando akifungua kongamano hilo la kisayansi.
 Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk. Elihuruma Nangawe akitoa lecture katika kongamano hilo.

NA ANDREW CHALE, BAGAMOYO.
 
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepongeza juhudi za makusudi zinazofanywa na Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) katika kushughulikia masuala ya afya kwa jamii huku ikiahidi kushirkiana kwa ukaribu katika maboresho  na kukuza juhudi za mashirika binafsi ya sekta ya afya.

Hayo yamesemwa leo Novemba 24 mjini hapa na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk.
Margaret Mhando, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando  wakati wa ufunguzi wa kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa mwaka wa TPHA, katika ukumbi wa Stella Maris, Bagamoyo.

Dk. Margaret Mmbando alisema kuwa juhudi za dhati zinazofanywa na wadau sekta binafsi wa afya serikali inazitambua na watahakikisha wanaendelea kuungana nao kwa hali na mali ilikuisaidia jamaii kwenye mambo yote ya msingi hususani masuala ya afya.

"Tunaipongeza TPHA kwa juhudi hizi za dhati kabisa katka ukuaji na ustawi wa sekta ya afya. Hivyo pia naamini baada ya kongamano hili kwa muda wa siku tano kila atakayetoka hapa atajifunza mambo makubwa na ya msingi katika mustakaba wa sekta hii" alisema Dk.Margaret Mhando.

Aidha, aliwataka TPHA kutanuka zaidi kuwa na matawi mengi ikiwemo kufika pembezoni mwa nchini ilikuweza kutanua huduma zao hizo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk. Elihuruma Nangawe alisema kongamano hilo la kisayansi la 31, linatarajia kuwa la siku tano na huku likitarajiwa kumalizika Novemba 28 mwaka huu ambapo wataalamu wa afya na wadau watajadilina mambo mbalimbali ya afya hapa nchini.

Naye Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga alisema kongamano hilo ni la  kuwakutanisha wataalamu mbalimbali wa afya na mambo ya jamii kutoka serikalini na mshirika binafsi ambapo watajadili changamoto za ukuaji wa sekta hiyo ya afya na maboresho yake kwa pamoja sambamba na kupata ujuzi watakaofanyia kazi.

"Kongamano hili la kisayansi la 31, ambalo kwa
mwaka huutukiwa tunakutana  ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na kutoa mapendekezo namna ya kuleta mabadiliko katika jamii" alisema Dk.Kisanga.

Taarifa ya msiba wa Kamishna Msaidizi wa Polisi mstaafu Leonard Mashaka

0
0
Kamishna Msaidizi wa Polisi mstaafu,Marehemu Leonard Mashaka enzi za uhai wake. 

Mheshimiwa Jaji Lillian Mashaka anasikitika kutangaza kifo cha Mume wake Kamishna Msaidizi wa Polisi mstaafu Leonard Mashaka kilichotokea siku ya Jumapili tarehe 23/11/2014. Msiba upo nyumbani kwake Mikocheni Dar es Salaam(nyumba za serikali).

Mazishi yatafanyika Jumatano tarehe 26/11/2014.
Ratiba itaanzia nyumbani saa 4 asubuhi na hatimaye misa takatifu katika kanisa la Mt. Martha Mikocheni, Saa 7 mchana.

Mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kinondoni (yazamani)kuanzia saa 9 mchana.Taarifa ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote walipo.

Raha ya milele umpe e Bwana na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa amani.

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAKUTANA NA WADAU WA MADINI YA SHABA

0
0
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba. Wengine kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje, Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Uongezaji Thamani Madini, Latifa Mtoro na Mwakilishi wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA), John Mvumula.
Mfanyabiashara wa madini ya Shaba kutoka Kanda ya Kati Doreen Kisia, akisistiza jambo wakati akichangia hoja katika mkutano huo.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo, akiongea jambo wakati akichangia mada kuhusu madini ya Shaba.
Kamishna Msaidizi Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje, akisalimiana na baadhi ya wadau wa madini ya Shaba waliohudhuria mkutano huo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, (kulia) akiongea jambo wakati wa mkutano huo.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba ambao umewajumuisha wafanyabiashara wa madini ya Shaba, wachimbaji wadogo, viwanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishna Wasaidizi wa Madini kutoka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini Wakaazi.


Na Asteria Muhozya, Dare s Salaam

Wizara ya Nishati na Madini imekutana na wadau wa madini ya Shaba katika mkutano wa siku mbili ulioanza tarehe 24- 25 Novemba, 2014 na kuwashirikisha wafanyabiashara wa madini hayo, wachimbaji wadogo, viwanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishana Wasaidizi wa Madini kutoka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini Wakaazi.

Akifungua mkutano huo, unaolenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ndogo ya madini ya Shaba na namna ya kuyaongezea thamani madini hayo, Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja amewataka wachimbaji wadogo nchini kutumia fursa zinazotolewa na Wizara ya Nishati na Madini ikiwemo kupata ruzuku ili waweze kuendeleza shughuli za uchimbaji wa madini jambo ambalo litasaidia kuyaongezea thamani madini hayo.

Aidha, Kamishna Masanja ametumia fursa hiyo, kuwataka wachimbaji na wafanyabiashara kuacha kufanya biashara kinyume na sheria na taratibu kwa kuwa jambo hilo linaikosesha Serikali mapato ikiwemo kuchangia madini hayo kutokupata thamani halisi.

Vilevile Kamishna Masanja ameeleza kuwa, Serikali itaendelea kuzuia usafirishaji madini ghafi ya Shaba na kueleza kuwa, “Haturuhusu madini ghafi ya shaba kutoka nje, tunataka yatoke yakiwa tayari ni madini, kwasababu kuna zaidi ya shaba hivyo tunapoteza, tunataka kuyaongeza thamani madini yetu hapa hapa nchini”, alisisitiza Masanja.

Rais Kikwete apokea salamu za kheri toka kwa Rais Barack Obama wa Marekani

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete salamu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa furaha na ujumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Washington DC uliomtembelea kumjulia hali na kwasilisha salamu maalumu za pole  za Rais Barack Obama jijini Baltimore, Maryland.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na maafisa waandamizi  wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington D.C. wakati walipomtembelea mjini Baltimore Maryland ambapo balozi Liberata Mulamula aliwasilisha kwa Rais Kikwete Salamu maalum za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. Picha na Freddy Maro

House For Sale

0
0
Suitable for both office and residential purposes

· Five (5) Total Bedroom(s)

· 2 Dining

· Kitchen, Dining Room, Store room,

· Tittle Deed Available.

· Location (Magomeni Makuti, Somanga Street)

· Contact Person 0767 882 800




WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUTOKA UBELGIJI WATEMBELEA MAENEO YA UWEKEZAJI BAGAMOYO

0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akiukaribisha ujumbe wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji ambao wametembelea mkoa wa Pwani kujionea fursa za uwekezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akiongozana na ujumbe wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji ambao wametembelea mkoa wa Pwani kujionea fursa za uwekezaji.
 Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji wakiwa mjini Bagamoyo wakiangalia maeneo ya uwekezaji.

 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza (katikati) akiwaongoza wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ubelgiji waliotembelea eneo la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.
Eneo la ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani akito ufafanuzi kwa wawekezaji waliotembelea eneo litakalojengwa Bandari ya Bagamoyo. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dk. Diodorus Buberwa Kamala.
 Eneo itakayojengwa Bandari Mpya ya Bagamoyo katika eneo la Mbegani.

Ujumbe wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji wakitembelea eneo la
Mamlaka ya Ukanda Maalum ya Uwekezaji (EPZA) eneo la ekari 300 la Kamal Industrial Estate mjini Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kuangalia maeneo ya uwekezaji.

  Katibu Kawala Mkoa wa Pwani, Mgeni Baruani akizungumza akizungumza wakati wa mkutano uliowakutanisha Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka nchini Ubelgiji na Uongozi wa Mkaoa wa Pwani.
 Ujumbe wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji ukiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa Mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kati ya Tanzania na Ubelgiji, Otieno Igogo.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akizungumza wakati wa Mkutano uliowakutanisha viongozi wa mkoa huo na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ubelgiji.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akizungumza wakati wa Mkutano uliowakutanisha viongozi wa mkoa huo na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ubelgiji.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akizungumza wakati wa Mkutano uliowakutanisha viongozi wa mkoa huo na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ubelgiji.
 Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dk. Diodorus Buberwa Kamala akizungumza katika mkutano huo.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dk. Diodorus Buberwa Kamala akizungumza katika mkutano huo.
 Ujumbwa wa Tanzania ukiwa katika mkutano huo.
  Kamishina wa Biashara kutoka Ubalozi wa Ubelgiji nchini, Ivan Korsak akizungumza katika mkutano huo.
 Kamishina wa Biashara kutoka Ubalozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Ivan Korsak akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ubelgiji na uongozi wa Mkoa wa Pwani waliofika kuangalia fursa za uwekezaji mkoani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza (kushoto) akifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo.
 Shangwe Tamala akitoa mada kuhusu vivutio vya kitalii na maeneo ya uwekezaji katika mkoa wa Pwani.
 Ujembe wa Tanzania na Ubelgiji ukiwa katika mkutano huo.
Mmoja wa wawekezaji kutoka Ubelgiji, Jean-Christophe Van Acker akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akimkabidhi zawadi, mmoja wa wawekezaji kutoka Ubelgiji, Yvan De Coninck.
Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dk. Diodorus Buberwa Kamala.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza (wa tatu kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji kutoka Ubelgiji.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Clara Ibinya akizungumza katika mkutano huo.
 Mmoja wa wawekezaji kutoka Ubelgiji, Jean-Christophe Van Acker akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja kati ya viongozi wa Mkoa wa Pwani na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji waliotembelea maeneo ya uwekezaji Bagamoyo mkoani Pwani.  
 Kamishina wa Biashara kutoka Ubalozi wa Ubelgiji nchini, Ivan Korsak akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
 Jean-Christophe Van Acker akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza.
 Nikki Martine Fedorowicz akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mko wa Pwani.
Jacques Delaunoit akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza.
 Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dk. Diodorus Buberwa Kamala akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kati ya Tanzania na Ubelgiji, Otieno Igogo akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza.

TANGAZO LA MSIBA KUTOKA FAMILIA YA NDG SEBASTIAN MGIMBA WA DAR ES SALAAM - TANZANIA

0
0
Marehemu Mathew Sebastian Mgimba Enzi za Uhai Wake.

2Timotheo 4:7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza Imani nimeilinda.

Familia ya Ndugu Sebastian Mgimba inasikitika kutangaza kifo cha Mpendwa wao Mathew Sebastian Mgimba kilichotokea Nchini Malaysia tarehe 20/11/2014.
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili leo tarehe 25/11/2014 na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwao Sinza Kumekucha.
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi - Amina

UZINDUZI WA TUZO ZA FILAMU TANZANIA WAFANYIKA JIJINI DAR

0
0
_N0A0439
Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Habari, vijana, utamaduni na michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, akiongea neno wakati wa uzinduzi._N0A0239
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba akielezea jambo katika hafla za uzinduzi wa Tuzo za Filamu Tnzania zilizofanyia mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam._N0A0270 Vijana kutoka Kigamboni Community Center wakitoa burudani wakati wa hafla za  uzinduzi wa Tuzo za Filamu Tnzania zilizofanyia mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

NEY WA MITEGO ALIVYOWAKUNA WASOMI WA UDOM KWENYE TAMASHA LA AIRTEL UNI 255 MJINI DODOMA

0
0

AIRTEL YAIBUKA NA UNI 255 KUTOA FULSA KWA WANAFUNZI VYUO VIKUU KUFAIDI INTANET KWA GHARAMA NAFUU KULIKO ZOTE

0
0
 Mkurugenzi wa Airtel Huduma kwa Wateja,Bi.Adriana Lyamba akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Simba ya UDOM kwa kuibuka washindi wa mashindano ya Airtel Uni 255,yaliyofanyika katika viwanja vya michezo ndani ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),Mashindano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
 Timu ya Simba ikishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe lao mara baada ya kuibuka kinara katika mashindano ya Soka ya Airtel 255.
 Aidha Aneth Mugha ambaye ni Meneja Masoko wa Airtel alikifafanua mbele ya Wanafunzi wa UDOM (hawapo pichani),namna vocha mpya ya Airtel Uni 255 inavyoweza kuwanufaisha katika suala zima la kuperuzi kwa gharama nafuu kuliko zote wakiwa chuoni hapo.Bi, Aneth alisema kuwa Airtel Uni 255 ni huduma maalum kwa vyuo vikuu inayomuwezesha mwanafunzi kupata huduma nafuu ya mawasiliano ikiwemo kupiga simu, sms, na intanet ili kwasaidia wanafunzi kutumia huduma hiyo kujiendeleza kimasomo.
 Baadhi ya Wanafunzi wakishuhudia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye jukwaa la Airtel Uni 255,baada ya mashindano ya Soka kumalizika na kumpata mshindi,Wasanii waliotoa burudani kwenye jukwaa hilo ni Roma,Ney wa Mitego pamoja na Vanessa Mdee a.k.a V-Money na burudani nyingine,ambapo wasanii chipukizi walishindana kughani na kuibuka na zawadi mbalimbali zikiwemo simu za mikononi,fulana na nyinginezo.
 Baadhi ya Wanafunzi wa chuo cha Dodoma (UDOM) wakiwa jukwaa wakijiunga na huduma maalum ya UN 255,ambayo imetolewa kwa ajili yao.Airtel Uni 255 ni huduma maalum kwa vyuo vikuu inayomuwezesha mwanafunzi kupata huduma nafuu ya mawasiliano ikiwemo kupiga simu, sms, na intanet ili kwasaidia wanafunzi kutumia huduma hiyo kujiendeleza kimasomo.

Aidha Aneth Mugha ambaye ni Meneja Masoko aliwatangazia Wanafunzi wa UDOM,namna vocha mpya ya Airtel Uni 255 inavyoweza kuwafaidisha kuperuzi kwa gharama nafuu kuliko zote wakiwa chuoni hapo.
 Baadhi ya Wanafunzi wa UDOM wakishangilia burudani iliyokuwa ikitolewa kweye jukwaa la burudani la Airtel Uni 255,ambapo wasanii mbalimbali walitumbuiza akiwemo Ney wa Mitego,Roma Mkatoliki pamoja na Vanessa Mdee a.k.a V-Money.
Sehemu ya umati wa wanafunzi wa UDOM wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri jukwaani kwa usiku huo wa tamasha la Airtel Uni255
Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Ney wa Mitego akitumbuiza kwenye tamasha la Airtel Uni 255, lililofanyika katika viwanja vya michezo ndani ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),Mashindano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Roma Mkatoliki  akitumbuiza kwenye tamasha la Airtel Uni 255, lililofanyika katika viwanja vya michezo ndani ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),Mashindano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
Meneja Mahusiano waAirtel Tanzania,Jakson Mmbando akitoa maelekezo mafupi mbele ya Wanachuo (hawapo pichani) kuhusiana na shughuli nzima ya tamasha la Airtel Uni 255, lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya michezo ndani ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),mkoani Dodoma.
Kikosi cha timu Yanga  ya UDOM wakiwa katika picha ya pamoja,ambao waliibuka washindi wa pili wa mashindano ya Airtel Uni 255,yaliyofanyika katika viwanja vya michezo ndani ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),Mashindano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
 Mmoja wa Wanafunzi mzuka ukiwa umempanda veyama kabisa wakati msanii wa muziki wa kizazi kipya Ney wa Mitego alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha la Airtel Uni 255.
Mmoja wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Vanessa Mdee a.k.a V-Money akiwaimbisha wanafunzi wa chuo cha UDOM,kwenye tamasha la  Airtel Uni 255 lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
 Sehemu ya umati wa wanafunzi wa UDOM wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri jukwaani kwa usiku huo wa tamasha la Airtel Uni255

BENKI YA WANAWAKE TANZANIA (TWB) YATOA HATI ZA VIWANJA KWA WATEJA WAKE

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya Wanawake  Tanzania (TWB), Magareth Chacha  (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichai) wakati wa hafla ya kukabidhi hati za viwanja kwa wateja walionunua na waliomaliza kulipa mikopo yao, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Benki hiyo, Aaron Nyanda na Mwanasheria wa Ardhi Plan Ltd, Musa Maghimbi. (Picha na Francis Dande) 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya Wanawake  Tanzania (TWB), Magareth Chacha  (wa pili kushoto) akimkabidhi hati ya kiwanja, Mhindi Mayenga wakati wa hafla ya kukabidhi hati za viwanja kwa wateja walionunua na waliomaliza kulipa mikopo yao, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Benki hiyo, Aaron Nyanda na kulia ni Mwanasheria wa Ardhi Plan Ltd, Musa Maghimbi. 
Wateja wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) wakiwa wameshika hati zao za viwanja baada ya kukabidhiwa na uongozi wa benki hiyo. Kutoka kushoto ni Belinda Rweyemamu, Mhindi Mayenga na Gabriel Kameka.

WATANZANIA TUMPE SUPPORT MISS TANZANIA HAPPINESS WATIMANYWA KWENYE SHINDANO LA MISS WORLD 2014‏‎

0
0
    Happiness Watimanywa (20) aliyekuwa Redds Miss Tanzania 2013 sasa yuko jijini London Uingereza kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World 2014. 

Happiness ambaye kwa sasa anashikilia taji la Miss World Tanzania 2014 amesema ana kila sababu ya kurudisha taji nyumbani ikiwa watanzania watamuunga mkono kwa kusambaza video zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

"Hebu angalia uzuri wa taifa letu, amani, upendo na vivutio mbalimbali vya utalii. Hebu niangalie na mimi mwenyewe... tuna kila sababu ya kurudisha taji nyumbani." alisema Happiness Watimanywa

Shime shime watanzania, tumuunge mkono wa nyumbani kwa ku-retweet, ku-like na ku-share post zake mbalimbali kwa kutumia Hashtag #Happiness4MissWorld
HAPPYNESS WATIMANYWA (MISS TANZANIA 2013/2014) ANAHITAJI KURA YAKO KATIKA KINYANG’ANYIRO CHA MISS WORLD MPIGIE KURA MISS TANZANIA HAPPYNESS WATIMANYWA. BAADA YA KUDOWNLOAD APP YA MISS WORLD NENDA VOTE FOR YOUR TOP3 KISHA UMPIGIE MREMBO MWENYE SURA HIYO HAPO KWENYE PICHA KATIKA WATATU UTAKAO WAONA
DOWNLOAD APP YA  KUPIGA KURA  KATIKA LINK HII  HAPA CHINI

TBL YAWA KINARA ULIPAJI KODI TANZANIA

0
0
Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, akikabidhi Kombe la mshindi wa Meneja wa Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Alois Qande, wakati wa maadhimisho ya nane ya mlipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, Dar es Salaam hivi karibuni.

UPDATES YA MSIBA WA NDG SEBASTINA MGIMBA : MWILI WA MAREHEMU SEBASTIAN MGIMBA WAWASILI NCHINI LEO, MAZIKO KUFANYIKA KESHO KATIKA MAKABURI YA KINONDONI.

0
0
 Ndugu pamoja na jamaa wa marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki dunia nchini Malaysia wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam eneo la Mizigo ukitokea nchini Malaysia.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki nchini Malaysia likiingizwa katika gari maalumu la kubebea jeneza katika uwanja wa Ndege wa Dar Es Salaam katika eneo la kutolea na kusafirishia mizigo mara baada ya mwili huo kuwasilini Nchini Leo ukitokea Nchini Malaysia.
Mchungaji akiendelea na ibada fupi iliyofanyika katika eneo la Kutolea mizigo katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam mara baada ya Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba kuwasili nchini leo.Picha zote na Josephat Lukaza - Wa http://www.josephatlukaza.com.
Msiba wa Marehemu Sebastian Mgimba upo Sinza Kumekucha ambapo baada ya mwili kupokelewa leo uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam umepelekwa Kwake Sinza na Hatimaye Kesho Kutakuwa na Misa ya kumuombea marehemu na hatimaye Mwili wa Marehemu kupumzishwa Katika Nyumba yake ya Milele Katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amina
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe
Viewing all 46129 articles
Browse latest View live




Latest Images