Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 410 | 411 | (Page 412) | 413 | 414 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Sehemu ya Wanyama kazi katika Shamba Kubwa la Uzalishaji wa ngo'mbe wa nyama katika Gereza Ubena lililopo Mkoani Pwani. Shamba hilo lina takribani jumla ya ngo'mbe zaidi ya 1500. Uzalishaji wa ngo'mbe umekuwa ukiongezeka kwa mafanikio makubwa kila Mwaka hivi karibuni kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Uongozi wa Jeshi la Magereza katika kuyahudumia mashamba hayo Nchini.
   Lango Kuu la kuingilia Gereza la Mifugo Ubena lililopo Mkoani Pwani ambalo linashughulika zaidi  na Uzalishaji wa Mifugo. Wafungwa katika Gereza hilo wanapata elimu ya Ufugaji bora unaozingatia Kanuni za Ufugaji wa Kisasa ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa jukumu la Urekebishaji kwa Wafungwa.

   Kundi la ndama wakiwa zizini katika Shamba la Uzalishaji wa Mifugo Gereza la Mifugo Ubena, Mkoani Pwani.
  Kundi la ngo'mbe wa maziwa katika Shamba la Mifugo la Mtego wa Simba lililopo Mkoani Morogoro. Shamba hili la Mifugo ni Maalum kwa Uzalishaji wa Ngo'mbe wa maziwa kama inavyoonekana katika picha na Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1944.
   Maziwa yakiwa tayari yamekamliwa na kuhifadhiwa kwenye majokovu kabla ya kwenda kwa walaji. Shamba hilo la Uzalishaji ngo'mbe wa maziwa la Gereza Mtego wa Simba limekuwa likipigiwa mfano hapa nchini(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
   

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji kama ishara ya kuzindua huduma za maji kwa wakazi wa kijiji cha Mpigamiti, mradi huo utahudumia vijiji vingine viwili vya Namakololo na Mitawa ambapo wakazi zaidi ya 6000 watafaidika na mradi huo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi.Hadija Sheweji  mkazi wa kijiji cha Mpigamiti mara baada ya kukagua mradi wa maji.
   Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mangirikiti wilayani Liwale mkoa wa Lindi. 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna haja ya kubadilisha taratibu za ajira badala ya kuwa za kudumu ziwe za mikataba kwani itasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.


   Wananchi wa Liwale wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia kuwa wapinzani kwenye mikoa hiyo hawajai hata kiganjani hivyo wananchi wasipoteze muda kwa wapinzani.

  0 0

  Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe wakisikiliza  uwasili wa taarifa za kamati mbalimbali ,Picha na Habari na James Festo, Njombe.

  Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe limeitaka Halmashauri hiyo kuacha mara moja kitendo cha kuwakata fedha za malipo ya bima ya afya kwa baadhi ya madiwani  ilihali hawanufaiki nayo na hajapata kadi licha ya kuwasilisha viambata vyote zikiwemo picha.

  Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi madiwani wa Halmashuri kuendelea kukatwa fedha kwa ajili ya malipo ya huduma hiyo inayotolewa na wakala wa Bima ya Nchini NHIF kwa vipindi viwili vya miaka mitano, na hawajawahi kutumia bima pindi  wanapohitaji huduma ya afya.

  Wakizungumza  kwa hisia  kali madiwani hao katika baraza la robo ya kwanza ya mwaka 2014/15  madiwani hao akiwemo diwani wa kata ya Idamba Bw. Chabiko Kyenga  ambaye ndiye katibu wao  alisema kuwa amekwisha kupokea malalamiko mengi hivyo hawako tayari kuendelea kukatwa fedha hizo kwenye posho zao kwa ajili ya bima.

  "Kama madiwani tunafanyiwa hivi kwenye haki zetu itakuwaje kwa wananchi wa kawaida, tunaomba turudishiwe hela zetu kwa namna , madiwani wengine wawili wameumwa mpaka wamefariki dunia kwa uzembe huu huu...unapigiwa simu kwamba diwani anaumwa unaona uchungu unaamua kumchangia na mimi hiki ni kipindi cha pili nipo humu ndani siijui kadi ya bima" alisema Kyenga.

  Aliongeza kuwa " sisi sio viumbe wa ajabu kwamba hatuwezi kuugua sisi ni binadamu kama wao kwa nini hawatupi bima zetu mimi kama katibu nilipeleka picha za madiwani ambao walinipa viambatanisho lakini tangu hapo sijaona kama kunahatua yoyote"

  Aidha walisema kuwa kwa sababu muda wa utawala wao unaelekea kuisha hivyo ni vema  wakarudishiwa fedha zao ili wazitumie katika matumizi mengine.

  Naye Makam Mwenyekiti Bw. Shaibu Masasi alikiri kuwa ni miongoni mwa walipewa vitambulisho hivyo vya bima na lakini alitumia ya kuwakumbusha mara baada ya kupata namba zao za simu na kumsihi mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kulitafutia ufumbuzi.

  " hata ukijaza fomu haitoshi na havipatikani kwa urahisi na ukikaa unategemea vitakuja utasahaulika kwa hiyo  mimi nilikuwa nakumbusha na kuwatishiatishia ndio nikapata...na kama havijapatikana na msimu wa uongozi umeisha lazima fedha za madiwani ambao hawajapata zirudishwe" alisema Masasi. 

  Aidha kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw Paul Malala aliwataka madiwani ambao hawakupatiwa vitambulisho kupeleka majina yao ili kulishughulikia tatizo hilo.

  "Nakiri hili ni tatizo na niwaahidi waheshimiwa tunalitafutia ufumbuzi ndani ya mda mfupi....niwaombe madiwani kwa wale ambao hawakupata vitambulisho mnipe majina yenu kabla hamjaondoka ili inirahisishie kuwakumbusha mamlaka husika"alisema Malala.

  0 0

   Pan African Energy (T) Ltd, CSR Manager, Mr. Andrew Kashangaki (L) hands over cement bags worth 18m/- to the Acting Excutive Director of Kilwa District Council, Mr Peter Malekela for construction of 59 laboratories in 27 secondary schools in the district yesterday. Witnessing are Kilwa District and Pan African Energy Executives. (Photo by Cathbert Angelo Kajuna).
  By Cathbert Kajuna from Kajunason Blog, Dar es Salaam.
  As part of its corporate social responsibility (CSR), Pan African Energy Tanzania has donated 1,500 bags of cement worth 18m/- to Kilwa District Council for construction of secondary schools science laboratory in Lindi Region.
  Speaking at the handover ceremony in Kilwa District, Lindi Region, Pan African Energy (T) Ltd, CSR Manager, Mr. Andrew Kashangaki, said the donation was aimed at supporting the district to have science laboratories for secondary schools before end of the month, as per President Jakaya Kikwete’s directive.
  “The company’s investments are found in the southern regions, thus it falls as part of our responsibility to provide support to the surrounding communities, in particular to enhance the quality of education and health services,” he said.
  He said a part from promoting the quality of education, Pan African Energy Tanzania also built a hospital to serve at Nangurukuru, to serve most of the populations of the surrounding area.

  On his part, the Acting Kilwa District Commissioner (DC), Mr Peter Malekela, said the cement donation will help in creating science experts whose skills are vital for the country’s development. He said the bags of cement have been distributed to 24 secondary schools located at Kilwa District where 59 science labs needed to be erected.
  Some of the schools that received the donation include Kikanda, Kandawale, Miguruwe, Kiranjeranje, Nakiu, Likawale, Namayuni and Kibata.
  Pan African Energy Tanzania is the first natural gas producer, supplying gas for power generation at the Ubungo Power Plant in Dar es Salaam.
  Pan African Energy also supplies natural also supplies natural gas to 38 industrial and commercial customers in Dar es Salaam area, reducing their operating costs and contributing to Tanzania’s industrial growth.

  0 0

  1
  Doris Mollel akikabidhiwa vitabu 200 na mkurugenzi wa MAK Solutions Bi Meetal Kirubakaran. Vitabu hivyo vilikabidhiwa kwa shule ya msingi Mpunguzi iliyopo Dodoma kama mchango wa kuadhimisha siku ya watoto duniani.(Picha zote na Albert Manifester).

  Dodoma, Novemba 2014.
  Katika kuadhimisha siku ya watoto duniani inayofanyika tarehe 20 Novemba kila mwaka, Mrembo wa Redds Miss central Zone 2014 Doris Mollel amechangia Vitabu vyenye thamani ya Shilingi Milioni moja (1,000,000/=) katika shule ya msingi Mpunguzi iliyopo katika kijiji cha Mpunguzi mkoani Dodoma.

  Doris, ambaye pia ni mshindi wa tatu kwenye Redds Miss Tanzania 2014 amejikita katika sekta ya elimu kama sehemu ya huduma zake za jamii ambapo amedhamiria kuendeleza mchango kwenye elimu ya msingi kwa kuchangia vitabu kwenye shule zenye uhitaji zaidi.

  Msaada huo wa Vitabu 200 vya kiada na ziada ameutoa kwa ushirikiano na kampuni ya uuzaji wa Vitabu ya MAK Solutions yenye duka lake Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bi Meetal Kirubakaran alisema MAK solutions wanafurahi kutoa vitabu hivyo kama mchango wao katika kusaidia sekta ya elimu Tanzania.
  2
  Doris akijadiliana jambo na Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda (Katikati) mjini Dodoma kabla ya kuelekea Mpunguzi. Wa kwanza kushoto ni Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo na anayefuata ni Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela.

  Akizungumza kwenye hafla iliyofanyika shuleni hapo, Mollel alisema ‘Ni muhimu kuwajengea watoto wetu utamaduni wa kujisomea tangu wakiwa wadogo ili kuwakuza kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa ambayo inahitaji uelewa mpana. Najivunia kuwa sehemu ya kampeni hii na nitaendelea kuongeza jitihada za kuwafikia watoto wengi zaidi’.

  Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda amempongeza Doris kwa juhudi zake za kusadia jamii hasa sekta ya elimu na ameomba wadau wengi kuiga mfano huu kuendeleza sekta hii. Hafla hiyo ya makabidhiano ilihuduriwa na mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mpunguzi Bi Neema Mando, Makamu mwalimu mkuu wa shule Bw Danctan Chipalo, Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo, Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela pamoja na wanafunzi wote wa shule ya Mpunguzi.

  3
  Alipokuwa njiani kuelekea mpunguzi, Doris alipata nafasi ya kuongea machache na baadhi ya wanafunzi wa vijiji vya jirani.
  4
  Wanafunzi wakimsikiliza kwa makini.
  5
  Doris Mollel (kulia) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili shuleni Mpunguzi. Kushoto ni Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo na katikati ni mwalimu mkuu wa shule ya mpunguzi Bi Neema Mando.
  6
  Doris akiuleza uongozi wa shule nia na madhumi ya safari yake. Kushoto ni mwalimu mkuu msaidizi Bw Danctan Chipalo na mwalimu mkuu Bi Neema mando.
  7
  Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo akimsaidia Doris kuchambua vitabu hivyo kutoka kwenye boksi la MAK Solutions Ltd.
  8
  Doris akiwaeleza wanafunzi umuhimu wa kupenda kujisomea tangu wakiwa wadogo.
  9
  Kutoka kushoto: Bw Danctan Chipalo, Bw Mnyagatwa Mazengo Bi Neema Mando na Doris.
  10
  Doris akiwa na baadhi ya wanafunzi baada ya kugawa vitabu.
  11
  Wanafunzi wakifurahia vitabu vyao.
  12
  Akimuelekeza mmoja wa wafunzi juu ya mambo yaliyomo kwenye kitabu cha ‘WATER’
  13
  Wakiwa na Vitabu.
  14
  Makabidhiano.
  15
  Doris akiongea jambo na mwalimu mkuu mara baada ya makabidhiano hayo.
  16
  Akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye viwanja vya shule hiyo muda mfupi kabla ya kuondoka shuleni hapo.

  0 0


  Ndugu,  Waandishi wa Habari,
  Siku ya jumamosi tarehe 22/11/2014 itakuwa ni siku ya Ufunguzi wa Michezo ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, utakaofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Dar es salaam Institute of Teckinology (DIT) kuanzia saa mbili (2:00) asubuhi  mpaka saa kumi na mbili (12:00) jioni.

   itafanyika kila mwaka kwa kushirikisha vyuo mbali mbali  vya elimu ya kati  hapa nchini Tanzania na vilivyopata usajili wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali mbali za Tanzania kupitia vyuo vyao vitashindana katika michezo mbali mbali kwa wavulana na wasichana .

  Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Entertainment C.o Ltd,yenye makao makuu yake Mwenge  jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ndiyo itakayokuwa ikisimamia taratibu zote za michezo hiyo wakati wote wa mashindano. 

  Kwa upande wa mkoa wa dare s salaam vyuo vilivyopo katika orodha ni 105 hivyo kulingana na bajeti kuwa kubwa, kama imeweka utaratibu wa kushiriki wenye michuano hiyo ya NACTE ambapo ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA ndizo zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER COLLEGE DAR ES SALAAM.

  Siku ya jumamosi itakuwa ni sehemu ya kwanza( Season one) ambapo vyuo vilivyotaarifiwa kuhusika katika kuwania nafasi hizo mbili za juu ni pamoja na Wenyeji D.I.T, majirani zao C.B.E na wakongwe wa Michezo Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM). 

  Vyuo vingine ni Dar es salaam City College(DACICO) na majirani zao chuo cha Mlimani Profesional, na Royal, na Timu Mwalikwa katika Season hiyo ni Timu ya 100.5 TIMES FM Radio, kwa kuwa katiba ya michuano hiyo inaruhusu kuhusisha timu mbili waalikwa ambao watatokana na vyombo vya habari ama chombo cha habari, hivyo 100.5 Times Fm, wakiwa pia ni kati ya wadhamini wakuu wa matangazo ya radio,  wamepata fulsa ya kushiriki hatua hii ya kwanza (Season one).

  Michezo itakayohusishwa hiyo siku ya ufunguzi ni pamoja na Mpira wa Miguu, Netball, Basketball, na Voleyball na washindi wa kwanza watazawadiwa Kombe wakati washindi wa pili watapata Mpira Mmoja kutoka kwa Wadhamini Wakuu Kampuni ya Simu za Mkononi VODACOM .

  Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji  kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo,Fedha,  na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.

  Mgeni Rasmi  katika Bonanza hilo ni Katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na mgeni mwalikwa atakayekabidhi zawadi kwa washindi ni mkurugenzi mtendaji wa 100.5 -TIMES RADIO, Bw. Leule Nyaulawa. 

  Aidha nichukue fulsa hii kuwaomba ndugu zetu wandishi kuhamasisha Makampuni na wadau kujitokeza kudhamini michuano hii ambayo maleng yake ni kuendeleza vipaji na kuibua vijana watakaokuwa viongozi, pamoja na kuwajengea mazingira ya kushiriki mara kwa mara katika michezo kwani Micheo uleta udugu, Upendano, mshikamano, amani, Afya na pia kijana anayeshiriki mazoezi upata muda wa kutumia akili kutafakali mambo ya Maendelezo zaidi.

    Imetolewa na -Katibu Mkuu Miss Demokrasia Tanzania- HALIMA BAKARI

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa akifafanua jambo wakati alipokuwa akifungua Semina ya siku moja ya kutafuta namna ya kukabiliana na Rashwa mbalimbali ikiwemo ya Ngono kati ya viongozi na watendaji wa chini iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).
  Mwenyekiti wa Chama cha Majaji wanawake Tanzania Jaji Engera Kileo akizungumza katika semina hiyo.
  Shekh Husen Kuzungu akifafanua jambo wakati akichangia mada kwenye semina ya kutafuta namna ya kutokomeza Rushwa ya Ngono iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania  (TAWJA) iliyofanyika Dodoma.
  Mahakaimu, Wabunge, na wakuu wa vyombo vya Dora wakifuatilia jambo wakati mkuu wa mkoa wa Dodoma Chiku Galawa akifungua Semina kuhusu namna ya kukabiliana na tatizo la Rushwa ya Ngono linaloendelea kushamili kati ya wenye vyeo na wasio na vyeo, iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA)
  Wajumbe waliohudhuria warsha ya kutafuta namna ya kukomesha Rushwa ya ngono maofisini kati ya mabosi watendaji wa chini ikiwemo vyuoni na mashuleni iliyoandaliwa na chama cha majaji wanawake Tanzania (TAWJA) iliyofanyika Dodoma
  Majaji, mahakimu, viongozi wa Dini na viongozi wa vyombo vya Dora waliohudhuria semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu mpya wa mokoa wa Dodoma Chiku Galawa.

  0 0

  Habari wadau, naomba kuwajulisha kuwa mwili wa mwandishi wa zamani wa michezo, Innocent Munyuku aliyefariki dunia juzi, unaagwa leo Ijumaa kuanzia saa tano asubuhi hospitali ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Morogoro kwa mazishi.
  Pia mwili wa mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani, aliyefariki juzi utazikwa kesho Jumamosi makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam badala ya leo makaburi Sinza kama ilivyokuwa imetangazwa jana. Msiba upo nyumbani kwa wazazi wa marehemu maeneo ya Mawasiliano Tower, barabara ya Sam Nujoma, Ubungo Dar es Salaam.
  Nawasilisha,
  Katibu Mkuu TASWA
  21/11/2014

  0 0
  Nyumba ya Maarifa (NIP) mkabala ATCL House, Ghorofa ya Kwanza, Mtaa wa Ohio,
  S.L.P. 79868, Dar es Salaam. Simu: +255 22 2127464, Nukushi: +255 22 2126399
   Barua pepe: info@tapsea.org, Tovuti: http://www.tapsea.org
   
  VIONGOZI WAPYA WA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA WATAMBULISHA OFISI MPYA ZA CHAMA

  MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA – TAPSEA ANAWAJULISHA MAKATIBU MAHSUSI WOTE TANZANIA KUWA OFISI YA TAPSEA IMEHAMIA KATIKA JENGO LA NYUMBA YA MAARIFA (NIP) MTAA WA OHIO.  WANACHAMA WOTE MNAOMBWA KUKAMILISHA UANACHAMA IKIWA NI PAMOJA NA KULIPIA ADA YA MWAKA KUPITIA AKAUNTI NAMBA 0150031411800 CRDB AZIKIWE BRANCH, AU AKAUNTI NAMBA 2236600363 NMB HOUSE.  

  NA WALE AMBAO HAMJAJIUNGA NA CHAMA MNAOMBWA MJIUNGE, FORM ZINAPATIKANA KWENYE MTANDAO WA TAPSEA, KATIKA OFISI ZA CHAMA NA KWA WAWAKILISHI WA MIKOA.

  OFISI ZIKO WAZI KUANZIA SAA 1:30 ASUBUHI MPAKA SAA 11:00 JIONI. 
  WOTE MNAKARIBISHWA KUPATA HUDUMA ZA CHAMA.


  IMETOLEWA NA

  ZUHURA S. MAGANGA
  MWENYEKITI – TAPSEA


  0 0


  0 0

  Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
   Matinyi akisoma wasifu wa marehemu.
    Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando akitoa salama za rambirambi.
   Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda akitoa salam za rambirambi.

  0 0


   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea ofisini kwake wakati akikabidhi Vifaa mbalimbali kwa wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini Ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi zake alizotoa Kipindi Akiomba kura ya Kuwa Mbunge wa Jimbo Hilo Pamoja za Ahadi anazotoa kwenye Mfululizo wa Ziara zake anazofanya Mara kwa mara katika Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.
   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood akikabidhi Mboa kwa Viongozi wa Msikiti kwajili ya Kumalizia ujenzi wa Msikiti ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa ziara zake za mara kwa mara. 
    Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akikabidhi Tani 2O za Saruji kwa viongozi wa Kanisa la agae la Mjini Morogoro Kwajili ya kufanikisha Ujenzi wa Kanisa Hilo.
   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akimkabidhi Tank la Maji Diwani wa kata ya Bigwa kwa niaba ya wakati wa kata hiyo Ili kutatua kereo ya Maji katiaka kata hiyo 
    Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akikabidhi Hundi ya Shilingi Laki Tano kwa kikundi cha wa mam wajasiriali Kutoka kata ya Kihonda  Magorofani
   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikabidhi Hundi   
  Katika Shuguli yake ya kukabidhi Vifaa mbalimbali Mh Abood alikabidhi vifaa vyenye Jumla ya Shilingi Milioni 1756OOOO/= Katika vikundi Mbalimbali vya Wajasiriamali,Vya Kidini kutoka kata za Jimbo la Morogoro Mjini.Baadhi ya Vifaa alivyokabidhi Mh Abood ni amoja na Matofali ,Vifyuko ya cement,Mabati Mbao na Hundi.
  Akielezea zaidi Mh Abood alisema Maka sasa ameweza Kuchimba Visima  24 Kati ya 36 Vitakavyogharimu Kiasi cha Shilingi Milioni 365. Karibu  kata  Zote za Manisaa ya Morogoro Kwasasa Zina Kisima Kwajili ya kutatua changamaoto Kubwa ya maji inayowakumba wakazi wa Jimbo la Morogoro  Mjini.

  Akielezea zaidi Mh Abood Alisema Anapambana usiku na Mchana 
  kutatua Kero Zote zinazowakumba wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini..
  Akielezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na Ahadi zake alizotoa kwa wananchi wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Abood Amesema karibu ahadi zake zote alizoahidi Amezitekeleza ,Amewaomba wakati wa manisaa ya Morogoro Kushikiana nae Bega kwa Bega katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mainduzi.  0 0

  Dar es Salaam. Mbunifu wa mitindo na muigizaji wa filamu nchini, mrembo Jokate Mwegelo kwa kushirikiana na mshiriki maarufu wa Big Brother Africa, Mganda Gaetano Kagwa wameteuliwa kuendesha kipindi kipya cha Maisha kijulikanacho kwa jina la “Beat the Challenge” kupitia M-Net East Africa.
   
  Kipindi kitashindanisha familia mbalimbali katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda na mshindi atapewa gari jipya kabisa kutoka kwa waandaaji.  
   
  Katika mashindano hayo, kila  familia inatakiwa kuwa na watu wanne ambao ni Baba, Mama na watoto wawili wenye umri kati ya miaka 12 na 17.Familia hizo zitashinda katika kutatua changamoto mbalimbali zitakazowasilishwa na waandaaji na kila familia itakuwa na jukumu la kutatua hiz changamoto kwaa kutumia nguvu kuliko ufahamu wa akili.
   
  Akizungumza jana, Jokate alisema kuwa amejisikia faraja kubwa kupewa nafasi hiyo ambayo itampa uzoefu zaidi katika fani ya utangazaji na kujipanua kimawazo.Jokate ambaye pia ni Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006 alisema kuwa anajisikia faraja kubwa kwa kuzidi kuongeza wigo wa mawasiliano kwani hii si mara yake ya kwanza kuendesha vipindi katika televisheni baada ya kutamba katika kipindi cha Chaneli O.
   
  “Kama nilivyosema, nataka kuishi kwa kutegemea vipaji vyangu na wala si vinginevyo, nimeanza katika urembo, nikaja katika ubinifu na uanaminitindo, MC, muigizaji wa filamu na sasa mtangazaji, kote huko nimefanikiwa, ni faraja kubwa kwangu,” alisema Jokate.
   
  Alisema kuwa anashukuru kuona kuwa filamu yake ya Mikono Salama kwa sasa inatamba sana na inamuongezea sifa kubwa katika fani hiyo. “Hata kidoti Fashion nayo inatamba, hivyo kwa nashukuru Mungu kwa kuniwezesha,” alisema.
   
  Kwa upande wa Tanzania, utafutaji wa washiriki utafanyika Jumamosi Novemba 22), New Africa Hotel, wakati Uganda watafanyia kwenye hotel ya Silver Springs, Kampala na Kenya kwenye studio za Supersport zilizopo katika Barabara ya Jamhuri.Kipindi cha kwanza kitarushwa Desemba 13 kupitia chaneli ya Maisha Magic 161 kuanzia saa 2.30 usiku kwa mujibu wa Jokate.
   

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Mkutano wa pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na Virutubisho (ICN2) uliofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome, Italia juzi Novemba 19, 2014.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakati wa mkutano huo wa ICN2 (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, James Nsekela na Msaidizi wa Rais katika Masuala ya Lishe Dkt. Wilbald Lorri.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango Maalum wa Chakula Duniani (WFP) Ethria Cousin (kushoto) na Balozi Wilfred Ngirwa wakati wa mkutano huo wa ICN2, uliofanyika juzi Novemba 19, 2014, Jijini Rome Italy.
   Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi walioshiriki katika Mkutano huo wa ICN2. Kulia ni Mfalme Letsie III wa Lesotho.
  Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa FAO Jose Graziano da Silva, wakati alipomtembea ofisini kwake na kufanya naye mazungmzo, juzi Novemba 19, 2014. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid. Picha na OMR.


  =======  =======  =======
  MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA PILI WA KIMATAIFA KUHUSU LISHE NA VIRUTUBISHO JIJINI ROME, ITALIA NOVEMBA 21, 2014

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal Novemba 19, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na Virutubisho uliofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la 
  Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome Italia. 

  Mkutano huu umefanyika ikiwa ni miaka 22 baada ya mkutano wa kwanza maarufu kwa jina la ICN1 kufanyika katika jiji la Rome na kuazimia kuwa, upo umuhimu wa kuhakikisha binadamu wanapata Lishe bora yenye virutubisho ili kusadia kujenga afya ya binadamu duniani. Mkutano huu wa pili pia umeandaliwa kwa pamoja na Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).

  Mkutano huo ulifunguliwa na Balozi wa Kudumu wa Italia katika Umoja wa Mataifa Gianni Ghisi aliyesoma hotuba kwa niaba ya Rais wa Italia Giorgio Napolitano ambapo alifafanua kuwa Rome inawakaribisha wawakilishi wan chi mbalimbali na kwamba inatamani kuona mkutano huu unatoka na majibu ya tatizo la lishe duni kwa watu wa mataifa mbalimbali. 

  Katika siku ya ufunguzi pia hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon iliwasilishwa pamoja na uzoefu wa masuala ya Lishe kutoka Italia ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Italia Paolo Gentiloni aliwasilisha hotuba yake huku akiwakaribisha washiriki wa mkutano huu wa ICN2 katika jiji la Rome na kufafanua kuhusu matarajio ya Italia katika mkutano wa sasa ukilinganisha na ule uliofanyika miaka 22 iliyopita.

  Akiwasilisha taarifa ya Tanzania, Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau wa Maendeleo ambao wamekuwa wakichangia katika sekta za Afya na Kilimo na akafafanua kuwa Tanzania imepiga hatua tangu ICN1 na sasa inahitaji kuona mkutano huu unatoka na maamuzi yanayotekelezeka ili kuwasaidia wananchi wa mataifa mbalimbali hasa watoto na akina mama wajawazito kuwa na uhakika wa lishe bora yenye virutubisho.

  Mheshimiwa Makamu wa Rais alifafanua kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambavyo vingi vilitokana na lishe duni na kwamba serikali ya Tanzania inaendelea kulipatia msukumo suala la lishe na virutubisho kwa wananchi wenye uhitaji ili kujenga taifa lenye afya na lenye watu wenye uwezo wa kusaidia nguvu zao katika kuleta maendeleo.

  Akizungumza siku ya pili ya Mkutano huo Baba Mtakatifu Fransis alisema haki ya chakula bora si tu kuwa imetolewa na Mwenyezi Mungu kwa binadamu bali pia ni haki inayoashiria utu na ambayo haipaswi kutolewa kama zawadi kwa wanadamu. 

  Papa Fransis aliendelea kusema kuwa, katika dunia ya sasa masuala ya chakula, lishe na mazingira yametokea kuwaunganisha binadamu wa mataifa yote sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma na akazitaka serikali za dunia kuhakikisha zinapunguza utupaji wa vyakula sambamba na kuongeza mikakati ya kuhakikisha kila mwanadamu anapata lishe bora.

  ICN2 inatazama pia kuhakikisha kuwa nchi zinakuwa na mikakati ya kupunguza utapiamlo na kwamba chakula kinachopatikana kiwe kile kilichoboreshwa ama kuongezewa virutubisho ili kusaidia jamii zinazokabiliwa na matatizo kama utapiamlo kuepukana nayo 
  na hivyo kuwa na kizazi chenye afya bora na chenye uwezo wa kutumika katika uzalishaji ama katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

  Dkt. Margareth Chan, Mkurugenzi wa WHO aliueleza mkutano huo kuwa suala la lishe ni mhimili katika kufanya jamii inayoweza kukabiliana na magonjwa huku pia Mkurugenzi wa FAO Jose Graziano da Silva akifafanua kuwa, shirika lake linautumia mkutano huu unaoshirikisha nchi 172 kutoa mwongozo kwa dunia kuhusu jambo hili muhimu katika maisha na hasa sasa ambapo tunaelekea kukamilika kwa Malengo ya Milenia na kuanza malengo mapya.

  Katika mkutano huo, licha ya Mheshimiwa Makamu wa Rais, Tanzania pia iliwakilishwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid pamoja na Waziri wa Mifugo Dkt. Titus Kamani sambamba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim. 

  Sambamba na kuhudhuria mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata fursa ya kukutana na Jumuiya ya Watanzania wanaishi Italia na kufanya nao mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa sambamba na kukutana na Mkurugenzi wa FAO ambaye alionesha furaha yake kuhusu hatua mbalimbali ambazo Tanzania imepitia na kuahidi ushirikiano zaidi katika masuala ya Kilimo. 

  Mheshimiwa Makamu wa Rais na ujumbe wake umeondoka kurejea nyumbani Tanzania tayari kuendelea na shughuli nyingine za Kitaifa leo Ijumaa Novemba 21, 2014.
   
  Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
                         Rome, Italia
                   Novemba 21, 2014.


  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mbaraka Abdualwakili, akizindua chapisho la tathmini ya Polisi Jamii nchini, hafla hiyo ilifanyika jana Makao Makuu ya Polisi  Jijini Dar es Salaam. Picha Alexander Mpeka – Jeshi la Polisi
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Bw.  Mbaraka Abdualwakil, Mwakilirishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia  ambaye ni Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu, Bi Selina Lyimo wakiwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Abdulrahaman Kaniki pamoja  timu iliyoshiriki katika utafiti wa tathmini ya Polisi jamii. Picha na Alexander Mpeka – Jeshi la Polisi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Bw.  Mbaraka Abdualwakil, Mwakilirishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia  ambaye ni Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu, Bi Selina Lyimo wakiwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Abdulrahaman Kaniki pamoja  makamishina wa Jeshi la Polisi wakati wa hafla ya makabidhiano ya chapisho la utafiti wa tathmini ya Polisi jamii . Picha na Alexander Mpeka – Jeshi la Polisi.

  =======  =======  =======

  Na. Tamimu Adam - Jeshi la Polisi.

  Jeshi la Polisi nchini  limetakiwa kutumia matokeo ya utafiti  wa tathmini ya Polisi Jamii  uliofadhiliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya taifa ya Sayansi na teknolojia( COSTECH) katika kuboresha mkakati wa Polisi jamii ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwani matokeo hayo yana manufaa makubwa katika kubaini, kuzuia, na kutanzua uhalifu na kero mbalimbali katika jamii.

  Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bi. Selina Lymo  kwa niaba ya  Katibu  Mkuu wa  Wizara ya Mawasiliano, Sayansi  na teknolojia wakati wa hafla ya kukabidhi chapisho la  utafiti  wa matokeo ya tathmini ya Polisi jamii  nchini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Bw. Mbaraka Abdulwakili . 

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Bw. Mbaraka  Abdulwakili alisema atahakikisha utafiti huo unafanyiwa kazi ipasavyo na amewataka watendaji wa Jeshi la Polisi kutumia utafiti huo katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kuwa askari waliopo hawatoshi na Polisi jamii imeonyesha  mafanikio makubwa katika kuzuia vitendo vya uhalifu na wahalifu.

  Naye, Mtaalum Mwelekezi wa Utafiti wa Tathmini ya Polisi Jamii ambaye pia ndiye Mtafiti Mkuu   Dkt  Haji Semboja alisema kuwa utafiti huo ulifanyika katika kanda saba ambapo matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa uhusiano wa kiutendaji baina ya wananchi na Jeshi la Polisi umeboreshwa kwa kiwango kikubwa kupitia dhana ya Polisi jamii.

  Alisema kuwa jambo hilo linasaidia katika kutengeneza mazingira ya amani na hivyo shughuli nyingine za kiuchumi  na kijamii zinaweza kuendelea kufanyika bila hofu na kwa uhakika wa ulinzi na usalama.

  Aliongeza kuwa, utafiti huo umeonyesha kwamba, watu wengi wanaamini kuwa, matokeo ya kuanzishwa kwa Polisi jamii katika maeneo yao  kuna mafanikio makubwa katika kuhimiza na kutia moyo uvumbuzi wa njia mpya za kukabiliana na vitendo vya uhalifu ambapo wananchi wamekuwa wakihimizwa utoaji wa taarifa za uhalifu kupitia njia mbalimbali ikiwemo njia ya ujumbe mfupi. 

   Naye, Naibu Inspekta Jenerali  wa Polisi, Abdulrahman Kaniki aliipongeza timu nzima iliyofanya utafiti huo na kusema kuwa Jeshi la Polisi kama watekelezaji wakuu wa Programu ya maboresho  yaliyojikita katika mihimili mikuu mitatu ambayo ni Weledi, Usasa na Polisi jamii,  wanatambua na kuthamini kazi nzuri iliyofanywa na watafiti hao na amewaomba kuangalia namna wanavyoweza kufanya utafiti katika mihimili  mingine miwili iliyobaki ambayo ni Usasa na Weledi ili Jeshi  Polisi  liweze kuwa na tathimini halisi ya Maboresho yake.

  Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dr. Flora Tibazarwa alisema kuwa madhumuni ya mpango wa utafiti huo yalikuwa ni kuimarisha uhusiano baina ya  Jeshi la Polisi na wananchi katika kuzuia na kutatua matatizo ya jamii, msisitizo ukiwa kuzuia uhalifu kabla haujatokea.

  Aliongeza kuwa matokeo ya utafiti huo yatawasaidia watunga sera na watoa maamuzi kutoa maamuzi na kutunga sera mbalimbali za usalama wa raia na mali zao kwa faida ya taifa letu. 

  0 0

   Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt. Fatma Mrisho akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani isemayo, Tanzania Bila Maambukizi Mapya ya VVU, Vifo vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi na Unyanyapaa inawezekana inayolenga kupunguza maambukizi Mapya ya Ukimwi, kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na kukomesha vitendo vya unyanyapaa kwa asilimia Sifuri.
   Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani yatakayofanyika kitaifa mkoani Njombe kuanzia Novemba 24, 2014 na kufikia kilele chake Desemba 1, 2014.
   Mkurugenzi wa ufuatiliaji wa Tathmini wa Ofisi ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi  Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu utoaji wa huduma na upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa watu wanaoishi na VVU katika maeneo mbalimbali nchini.

   Mkurugenzi wa ufuatiliaji wa Tathmini wa Ofisi ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi  Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu utoaji wa huduma na upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa watu wanaoishi na VVU katika maeneo mbalimbali nchini.
  Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa TACAIDS akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mbinu na elimu inayotolewa na TACAIDS katika maeneo mbalimbali ikiwemo matumizi ya mipira ya kike kwa wanawake ili kuzuia maambukizi mapya ya VVU.


  0 0


   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa Ruangwa Likangara tayari kuhutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
   Wananchi wa Ruangwa wakionyesha furaha yao wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye uwanja wa mkutano Ruangwa Likangara.
   Wananchi wa Ruangwa wakiwa na mabango yaliyobeba ujumbe wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kujenga na kukiimarisha chama,Katibu Mkuu wa CCM ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Ruangwa ambapo aliwaambia CCM inaimarika kutokana na kuwa na sera zenye kuleta maendeleo kwa Watanzania pamoja na kuthamini amani iliyopo nchini.(Picha na Adam Mzee)

  Umati wa wakazi wa wilaya ya Ruangwa wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wao wa CCM Taifa.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa wilaya ya Ruangwa waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza,Kinana amekuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kuzunguka nchi nzima ,kushiriki kwenye miradi mbali mbali ya maendeleo,kukagua ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 pamoja na kutoa elimu kwa wananchi hasa ya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii.
   Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wakazi wa Ruangwa ambapo alielezea katika kipindi chake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge ameshiriki shughuli mbali mbali za maendeleo jimboni kwake.
   Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa Ruangwa ambapo alichukua muda wa kutosha kufafanua kwa wananchi namna alivyotekeleza wakatoi wa kipindi chake kama Mbunge wa Jimbo wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anafanya ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Ruangwa ambapo alisema uongozi mbovu kwenye vyama vya ushirika ni chanzo cha kusababisha matatizo kwenye zao la korosho,aliwaambia wananchi hao hakuna sababu ya msingi ya kuwa na utitiri wa vyama vya ushirika.
   Wananchi wa kijiji cha Mibure wakiwa na furaha wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  kwenye kijiji chao kilichopo wilaya ya Ruangwa.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Mibure ambapo aliwapongeza uamuzi wao wa kujenga Zahanati ya kijiji kwa kushirikiana na Mbunge wao pamoja na Halmashauri.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Mibure ambapo aliwashauri vijana kujiunga vikundi na kufanya shughuli za ujenzi kwani kuna miradi mingi ambayo vijana wanaweza kupatiwa fursa ya kuifanya kwa gharama nafuu.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua jengo la zahanati ya kijiji cha Mibure ambacho kinajengwa na mafundi wa kawaida wa kijijini hapo.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wananchi wa kata ya Chienjele wilayani Ruangwa.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya Chienjele wilaya ya Ruangwa ambapo aliwaambia vijana kuwa bado kuna fursa nzuri nchini katika kuleta maendeleo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCMkata ya Nandagala wilayani Ruangwa.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia chanzo cha maji kwenye mto Ole kijiji cha Ng'au kata ya Mnachu wilaya ya Ruangwa.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda miti kwa ajili ya kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Ng'au Ole wilaya ya Ruangwa ambapo aliwahimiza kutunza mazingira kwa kutokata miti badala yake wapande miti kutunza vyanzo vya maji.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Nandagala ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama mkoa wa Lindi.

  0 0

   Mbunge wa Kigoma Kusini Mhe David Kafulila akiwa na mai waifu wake Jessica Kishoa wakijiandaa kukata utepe wa kuingia katika mnuso kwenye ukumbi wa Annex uliopo Uvinza, Kigoma,  jana Jumamosi Novemba 22, 2014
   Mhe David Kafulila akiwa kanisani  na mai waifu wake wa Jessica Kishoa wakati wa  kufunga ndoa katika kanisa la Roman Catholic katika Parokia ya uvinza, Kigoma, jana Jumamosi Novemba 22, 2014
   Mhe David Kafulila na mai waifu wake Jessica Kishoa pamoja na wapambe wao Mhe. Deo Filikujombe na mke wake Sarah Filikunjombe wakipeleka keki kwa wazazi wa bwana harusi 
  Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliopamba  harusi ya Mhe. David Kafulila katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Mhe Deo Filikunjombe. Mhe.David Kafulila ambaye ndiye Bw. Harusi, Mhe  Zitto Kabwe na Mhe David  Silinde. Picha zote na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma

  0 0

   Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimtukuku Shahada ya Uzamili katika Uchumi wa Maendeleo Amina Salum Mwanja wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
   Mkuu wa kwanza wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Askofu Dkt. Saimon Chiwanga akitoa neno baada ya Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene kumaliza shudhuli ya kutunuku vyeti kwa wahitimu wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.

   Baadhi ya wahitimu wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
   Mwanafunzi wa mwaka wa pili anayesomea Shahada ya kwanza ya Mipango ya Usimamizi wa Mazingira katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Azizi Mshau  akimweleza Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene namna bora ya kundaa mipango miji inayokuwa rafiki kwa mazingira.
   Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akiagana na Mkuu wa kwanza wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Askofu Dkt. Saimon Chiwanga mara baada ya sherehe ya mahafali ya 28 ya Chuo hicho.
  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene () akiwa katika picha ya pamoja na wahadhiri wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) mara baada ya mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma. (Picha zote na Eleuteri Mangi- Dodoma).

  Na Eleuteri Mangi- Dodoma
  Serikali imesema  inaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuweka mazingira rafiki kwa kuboresha mifumo ya ajira katika sekta ya umma na ile ya binafsi ili kujenga uchumi wa kisasa unaozalisha ajira pamoja na kuwawezesha vijana wasomi nchini kujiajiri.

  Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene kwa niaba ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) yaliyofanyika jana mjini Dodoma.

  “Ninafarijika sana kusikia vijana wa chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini wameweza kuonesha njia kwa kuweka kwa vitendo waliyojifunza kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi katika sekta ya kilimo kama njia ya kujiajiri” alisema Mbene.

  Naibu Waziri huyo aliwahakikishia vijana hao kuwa Serikali ipo tayari kusaidia juhudi hizo kupitia fursa mbalimbali za kuwasaidia vijana na wajasiriamali kupitia fursa zinazoendelea kutolewa na Serikali.

  Naibu Waziri Mbene alisema kuwa ili kutekeleza lengo hilo, Serikali inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika kilimo, uchimbaji wa madini na uwezo wa kuongeza thamani mazao yetu yanayozalishwa.

  Mbene aliongeza kuwa maeneo yote hayo yanatoa fursa nyingi kwa wahitimu vijana nchini kuajiriwa katika ngazi mbalimbali za Serikali, sekta binafsi na kujiajiri.

  Akimkaribisha Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo Dkt. Razack Lokina alitoa kilio cha chuo hicho cha kuomba kada ya mipango kupewa nafasi stahili katika mfumo wa ajira Serikalini.

  Akifafanua suala hilo Dkt. Razack alisema kuwa kukosekana kwa kada ya Mipango kumesababisha kazi za kada hiyo kutotekelezwa ipasavyo kwa kiwango cha ufanisi unaotakiwa.

  Aidha, Dkt. Razack alisema kuwa taaluma ya Mipango inamtayarisha Afisa Mipango ambaye jukumu lake ni kubuni, kupanga, kufuatilia, kutathmini, kuratibu shughuli na rasilimali katika maeneo ya Mipango ili kufikia malengo ya maendeleo ya jamii kusudiwa tofauti na taaluma ya Uchumi ambayo inamuandaa Afisa kuwa na jukumu mahususi la kuchambua ili kutoa hali halisi ya mazingira ya kiuchumi kisekta.

  Kwa upande wake Chuo hicho Constantine Lifuliro alisema kuwa wahitimu wa chuo chake wameandaliwa vya kutosha wapo tayari kutoa huduma katika nyanja mbalimbali kwenye maeneo waliyojifunza hasa katika kuandaa, kusimamia, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini mipango ya maendeleo katika maeneo mbalimbali  watakayofanyia kazi.

  Naye mhitimu Baltazar Ngeze, kwa niaba ya wahitimu wa mwaka huu wa chuo hicho aliushukuru uongozi wa chuo kwa kuwaandaa vema kwenda kutekeleza majukumu yao ya taaluma ya Mipango katika jamii watakayokuwepo.

  Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 1,909 waliotunukiwa tuzo zao katika kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.

  Kati ya wahitimu hao, wapo wanaume ambao idadi yao ni 1,003 sawa na asilimia 52 ya wahitimu wote na wanawake idadi yao ikiwa ni 906 sawa na asilimia 48 ya wahitimu wote.

  Idadi hiyo ya wahitimu wa mwaka huu inaonesha wameongezeka wahitimu 63 sawa na silimia 3.4 zaidi ya wale waliohitimu masomo yao mwaka jana 2012/2013 ambao walikuwa 1,846 kati yao wakiwa wanaume 1,037 sawa na asilimia 56 na wanawake walikuwa 809 sawa na asilimia 44.
  Mwisho.


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye uwanja wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia CCM inasimamia uwajibikaji na kama mtu amekosea awajibike na akishindwa atawajibishwa mapema.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi hao CCM ni chama pekee chenye mfumo ulioanzia chini hivyo watu waache unyonge Serikali hii ni ya CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa pongezi vijana Lindi waliojiunga na UVCCM mkoa wa Lindi kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini mkoa Lindi.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu wilaya ya Lindi mjini ambapo aliwaambia wananchi wa Lindi ni muda wa kuwaondoa wapinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Desemba mwaka huu kwa kuipigia kura CCM.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma Katiba iliyopendekezwa kwa wananchi wa Lindi mjini kuwapa elimu wananchi juu ya mambo ya msingi hasa maadili katika Katiba iliyopendekezwa .

   Mkuu wa wilaya ya Lindi Nassoro Ally Hamidi akihutubia wananchi wa Lindi kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu mkoani Lindi.
  Wafanyabiashara ndogo ndogo wakiuza bidhaa zao za vyakula wakati wa mkutano wa CCM kwenye uwanja wa Ilulu.

    Balozi Abdul Mohamed akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye shina lake namba 2 Rahaleo wilaya ya Lindi mkoani Lindi
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa shina namba mbili kwa Balozi Abdul Mohamed wa Raha leo ,wilaya ya Lindi mkoani Lindi.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) akiwa ameketi chini na wanachama wa shina namba 2 Raha leo kwa Balozi Abdul Mohamed  wilaya ya Lindi mjini.
   Katibu Mkuu wa CCM akipandisha bendera ya CCM kwenye Shina la wakereketwa la Wanya Kahawa  Lindi.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wanachama wa shina la CCM la Wanywa Kahawa Lindi.
   Hii ndio ilivyokuwa mitaa ya Lindi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki uvuvi kwenye mradi wa ufugaji samaki wa ASM Trading 2005 mradi ambao umetoa ajira kwa vijana 10 wa manispaa ya Lindi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi wa dini wa mkoa wa Lindi alipotembelea mradi wa ufugaji samaki wa ASM Trading 2005 mradi ambao umetoa ajira kwa vijana 10 wa Manispaa ya Lindi,
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na viongozi wa CCM wilaya ya Lindi mjini pamoja na wananchi kubeba zege kwa ajili ya kuweka zege ya nyumba ya Mwalimu wa shule ya msingi Nanyanje.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki palizikatika shamba la kikundi cha kuzalisha mbegu bora ya mihogo Chikonji wilaya ya Lindi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba mtaro wa maji kijiji cha Mnazi Mmoja mkoani Lindi.

older | 1 | .... | 410 | 411 | (Page 412) | 413 | 414 | .... | 1898 | newer