Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

NYUMBA INAPANGISHWA.

$
0
0
Nyumba inapangishwa ipo mita 200 kutoka kituo cha basi makumbusho(nyuma ya ofisi za tigo),Ina maji na umeme,parking kubwa ya gari, vyumba viwili vya kulala kimoja self contained,sebule,jiko,stoo,
dining room,ukuta na geti.Bei laki tano kwa mwezi,ni nyumba nzuri kwa familia ndogo au mtu anaeanza maisha ipo nyuma kabisa ya ofisi za tigo na mtaa wenyewe ni wa kishua.if you are interested call 0765262321 or email roseangel44@yahoo.com (dalali haitajiki).
 




 
 

TRL YAPOKEA MABEHEWA 50 YA KUBEBA MAKONTENA, NI MKAKATI WA KUTEKELEZA BRN

$
0
0
Katibu Mkuu wizara ya Usafirishaji, Shaaban Mwinjaka, (Kushoto), akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Kipallo Amani Kisamfu, wakati akiwasikli bandarini jijini Dar es Salaam, leo Jumatano Nov 19, 2014, kupokea mabehewa 50 ya kubeba makontena.     


Moja kati ya mabehewa 50 ya kubebe makasha, likishushwa kutoka kwenye meli, bandarini jijini Dar es Salaam leo Jumatano Nov 19, 2014. Mabehewa hayo yataongeza utoaji huduma wa Kampuni ya reli Tanzania, (TRL), kutoka kutoa huduma za usafirishaji mizigo chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN), alisema katibu mkuu wizara ya usafirishaji Shaaban Mwinjaka, wakati akipokea mabehewa hayo kutoka India
Katibu Mkuu wizara ya Usafirishaji, Shaaban Mwinjaka, (Kulia), akikagua behewa moja kati ya 50 ya kampuni ya reli Tanzania, (TRL), yalipowasili jana. . Mabehewa hayo yataongeza utoaji huduma wa Kampuni ya reli Tanzania, (TRL), kutoka kutoa huduma za usafirishaji mizigo chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN), alisema katibu mkuu wizara ya usafirishaji Shaaban Mwinjaka, wakati akipokea mabehewa hayo kutoka India.
Mkuruhenzi Mkuu wa TRL, Kipallo Amani Kisamfu, akitoa hotuba fupi
Katibu Mkuu, wizara ya Usafirishaji, Shaaban Mwinjaka, akitoa hotuba yake.
Alama zinazoonyesha tarehe mabehewa hayo yalipakiwa kutoka India kuja Dar es Salaam

TRA yatoa msaada wa vifaa tiba kwa Hospitali ya Mnazi Mmoja,Zanzibar leo

$
0
0
 Mkurugenzi wa Walipakodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard Kayombo (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Dkt. Jamala Adam Taib (wa tatu kushoto) sehemu ya msaada wa vifaa tiba vya hospitali vilivyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania vyenye thamani ya shilingi Mil. 20 vitakavyotumiwa katika hospitali hiyo leo Novemba 19,2014,Zanzibar. 

Makabidhiani hayo yamefanyika kufuatia muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi Tanzania ya TRA yenye Kauli mbiu isemayo Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti" .Wa pili ni Kaimu Kamishna wa TRA (Zanzibar),Mcha Hassan Mcha akiwa pamoja na maofisa wengine wa TRA.
Mkurugenzi wa Walipakodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard Kayombo akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba vya hospitali kwa Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Dkt. Jamala Adam Taib,leo Novemba 19,2014,Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Dkt. Jamala Adam Taib (wa pili kushoto) akizungumza wakati akitoa shukrani zake kwa Uongozi mzima wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kutoa msaada wa vifaa tiba kwenye Hospitali hiyo ya Mnazi Mmoja,Zanzibar leo Novemba 19,2014.
Sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa hospitali ya Mnazi Mmoja,Zanzibar leo Novemba 19,2014.

Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Forum CC yaandaa kongamano la vijana

$
0
0
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya  Forum CC imeandaa kongamano la siku moja kwa vijana kutoka  Asasi za kiraia lililojadili msimamo wa Tanzania juu ya masuala ya Mazingira, hususan Mabadiliko ya Tabianchi  kuelekea Mkutano Mkubwa wa Mazingira Duniani utakaofanyika katika jiji la Lima nchini Peru, Desemba 2014.
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari  (hawapo pichani) mara baada ya kufungua kongamano hilo.
 Sehemu ya Washiriki walioshiriki katika kongamono hilo la siku moja lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Forum CC wakifuatilia mjadala kwa makini.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akijibu maswali ya washiriki katika kongamano la vijana jijini Dar es Salaam katika Hotel ya JB Belmont. Kongamano hilo la siku moja lililenga kukusanya maoni ya vijana na kuainisha changamoto katika suala zima la Hifadhi ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo. Wengine katika picha, (waliokaa) ni Bi. Grace Munna, Mkurugenzi wa Program kutoka Forum CC.

TAMISEMI YATANGAZA TAREHE YA KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
MKURUGENZI WA SERIKALI ZA MITAA BWANA KHALIST LUANDA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI) JUU YA KUKAMILIKA KWA MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MJINI DODOMA LEO AMBAPO ALITANGAZA RASMI TAREHE YA KUANDIKISHA KUPIGA KURA . (PICHA NA HABARI KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI).

======  ========  =====

Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Bwana Kharist Michael Luanda amesema  wananchi wanapaswa kujiandikisha katika daftari maalum la kupigia kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia tarehe 23/11/2014 hadi tarehe 29/11/2014. 

Mkurugenzi huyo alisema kuwa wananchi wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za vijiji, vitongoji na mitaa wanapaswa kuchukua fomu za kugombea kuanzia tarehe 16/11/2014 hadi tarehe 22/11/2014. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Bwana Luanda aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha ili waweze kupata fursa ya kushiriki katika kupiga kura ili kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa wanaowataka.

Alisema sifa za mtu anayestahili kujiandikisha kushiriki uchaguzi huo ni lazima awe raia wa Tanzania, mwenye umri wa miaka 18 au zaidi, mkazi wa eneo hilo na mwenye akili timamu.
Pia alisisitiza kuwa uandikishaji huo utafanyika katika vituo maalum vilivyoandaliwa ambavyo vipo katika majengo ya umma, isipokuwa sehemu ambazo hazina majengo hayo, uandikishaji utafanyika katika vituo maalum kutokana na makubaliano ya Msaidizi wa Uchaguzi na viongozi wa vyama vya siasa.Bwana Luanda amesisitiza kuwa vituo hivyo vitafunguliwa saa 1:30 asubuhi na kufungwa saa 10:30 jioni.

 Aidha alisema kuwa vyama vya Siasa vitaruhusiwa kuweka mawakala wao wakati wa uandikishaji wa wa wapiga kura lakini gharama  za kuwalipa zitakuwa juu ya chama husika. Kuhusu  sifa za mtu anayetaka kugombea nafasi mbalimbali katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mtaa Mkurugenzi huyo alisema kuwa ni lazima awe  mtanzania mwenye umri wa miaka 21 au zaidi na awe mkazi wa kudumu wa eneo husika.

Vile vile alisema  kuwa wasimamizi wasaidizi wa kila kituo wanapaswa  kubandika orodha ya wapiga kura tarehe 30/11/2014, endapo mkazi yeyote au chama cha siasa kitakuwa na pingamizi au maoni juu ya orodha hiyo basi awasiliane na msimamizi msaidizi wa uchaguzi ili kuweza kufanyia marekebisho na orodha ya mwisho itabandikwa siku tatu kabla ya uchaguzi.

Uchaguzi wa serikali za Mitaa Tanzania Bara umepangwa kufanyika disemba 14, 2014, ambapo wananchi watawachagua wenyeviti wa vijiji, vitongoji, Mitaa, Wajumbe wa Halmashauri za vijiji na Wajumbe wa Kamati za Mitaa.

Viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni pamoja na wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji wasiopungua 15 na wasiozidi 25, wenyeviti wa Mitaa na wajumbe wa kamati za Mitaa wasioziidi 6 na wenyeviti wa vitongoji wa kila kitongoji.

HII SI YA KUKOSA MTU WANGU

$
0
0

Lady Jaydee anatarajia ku release single mpya aliyomshirikisha Dabo inayoitwa "Forever' hapo Jumatatu tarehe 24 Novemba. Hii ni baada ya Kimya cha muda mrefu kidogo na siku ya Ijumaa ndio itakuwa official launch day pale M.O.G bar & Restaurant ambapo video ya wimbo huu ita premier for the first time. Wimbo umetayarishwa na producer mahiri Man Water wa Combination Sounds, na video ya wimbo huo imefanywa na muongozaji mkongwe Adam Juma wa Next Level.

Instragram: @jidejaydee @dabomtanzania
Twitter: @jidejaydee @dabomtanzania

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE YAENDELEA NDANI YA WILAYA YA NACHINGWEA

$
0
0
 Kikundi cha Wakulima cha Umoja Rika wakiinua majembe juu kama ishara ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyefika kwenye shamba hilo la ushirika la Mkotokuyana wilaya ya Nachingwea.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakulima wa kikundi cha Umoja Rika kilichopo Mkotokuyana ,Nachingwea.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakulima wa kikundi cha Umoja Rika kilichopo Mkotokuyana,Nachingwea mkoani Lindi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendesha treka kulima shamba la ushirika la Mkotokuyana huku akiwa amempakia Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Ngugu Mathias Chikawe.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kung'oa visiki katika shamba la Mkotokuyana  wilayani Nachingwea.

 Sehemu ya shehena ya Korosho.  

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia korosho kwenye ghala ambalo hapo awali ilikuwa kiwanda cha korosho cha Nachingwea .
 Kiwanda cha Mafuta ya Ufuta Ilulu Nachingwea ambacho sasa kinatumika kama ghala ya kuhifadhia vifaa vya umeme.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mandai ambao walieleza shida ya maji,zahanati pamoja na ofisi ya Serikali .

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa jiko la kisasa la shule ya sekondari ya Nachingwea High School .
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia majiko ya kisasa ya shule ya sekondari ya Nachingwea.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Nachingwea.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Naipanga ambapo alikagua na kushiriki ujenzi , Katibu mkuu wa CCM aliwaambia wananchi wawe mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Nachingwea na Waziri wa Mambo ya Ndani Ndugu Mathias Chikawe (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nachingwea Ndugu Albert Mnari kuelekea kwenye shamba la ushirika Mkotokuyana  wilaya ya Lindi Vijijini tayari kwa kushiriki shughuli za kilimo.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya serikali ya kijiji cha Naipanga Nachingwea.
 Wananchi wa Nachingwea wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kujenga na kukiimarisha chama mkoani Lindi.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nachingwea ambapo aliwaambia upinzani umepotea kabisa hivyo wasipoteze muda wao kushabikia
 Wananchi wakifurahia hotuba ya Katibu wa Nec Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Mama akichukua matukio kwa simu yake wakati mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Soweto wilaya ya Nachingwea.
 Wananchi wakifuatilia mkutano nje ya senyenge ya uwanja wa mikutano wa Soweto wilayani Nachingwea.
 Mbunge wa Jimbo la Nachingwea na Waziri wa Mambo ya Ndani akielezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010  katika jimbo lake kwenye mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, Nachingwea.
 Bibi Esha Kanduru mwenye umri wa 89 ambaye alishiriki harakati za uhuru na kujiunga na TANU mwaka 1957 akifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa Soweto, Nachingwea.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nachingwea ambapo aliwaambia kuwa CCM itakuwa wakali pindi serikali inapokosea mambo na kuchelewa kuchukua hatua, kwani maumivu na mateso wanapata wananchi, akizungumzia kusikitishwa kwake kwenye viwanda vya korosho ambavyo vimegeuzwa kuwa maghala na hakuna mtu serikalini amestuka kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Ndugu Mathias Chikawe wakati wa mkutano wa CCM mjini Nachingwea kwenye viwanja vya Soweto.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachma kutoka CUF waliojiunga rasmi na CCM wilayani Nachingwea.

WAHALIFU MTANDAO WATEGEMEWA KUELEKEZA NGUVU ZAO BARANI AFRIKA - WATAALAMU

$
0
0
Itakumbukwa katika mkutano uliofanyika  mapema mwezi huu  jijini "CAIRO" hofu ya ukuwaji wa uhalifu mtandao unaoweza kurudisha nyuma uchumi wa mataifa ya Afrika  ulipata kujadiliwa kwa kina huku nchi ya Misri ikionyesha washiriki wa mkutano huo jitihada inayoendelea nayo katika kukabiliana na uhalifu mtandao. 

Ime ripotiwa na Mtandao wa "MGAFRICA" kuhusiana na kilichojiri katika mkutano uliokamilika jijini Johannesburg, Afrika kusini wa maswala ya usalama mitandao ambapo Bara la Afrika limetabiriwa kuwa na ukuaji wa uhalifu mtandao kutokana na mikakati daifu ya kujiweka salama huku ikiwapatia wahalifu mtandao urahisi mkubwa wa kuleta maafa siku za usoni. 

Kumeendelea kuwa na wimbi kubwa la uhalifu mitandao ingawa jitihada za kukabiliana na uhalifu huo zimeendelea  kugharimu mataifa mengi hivi sasa. Mataifa yamekua yakiwekeza kwenye maswala ya usalama mitandao lakini bado wahalifu mtandao wameonekana kuendelea kutamba.

Mkutano huo wa maswala ya  usalama mitandao uliangazia kwa karibu  sababu za ukuaji wa uhalifu mtandao na nini kifanyike kwa mataifa ili kuweza kupiga hatua ya kubaki salama kimtandao. Wataalam wa maswala Mtandao kutoka katika mataifa mbali mbali walikutana  kuyajadili mambo hayo kama ifuatavyo: BOFYAHAP

TTCL YAKABIDHI MSAADA WA MABENCHI KATIKA KITUO CHA AFYA BUGURUNI

$
0
0
Mganga mfawidhi katika kituo cha afya Buguruni,Dk. Mwajuma Mbaga (kushoto) akipokea msaada wa mabechi ya kukalia wagonjwa wakati wakisubiri huduma kutoka kwa Kaimu Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL),Bw. Edwin Mashasi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano,iliyofanyika jana  Novemba 19,2014.
Sehemu ya mabenchi yaliyotolewa na kampuni ya simu Tanzania (TTCL). Msaada huo umegharimu shilingi milioni moja na laki saba.
Mganga mfawidhi katika kituo cha afya Buguruni,Dkt. Mwajuma Mbaga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa kituo hicho.Kulia waliokaa ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TTCL Bw. Edwin Mashasi.
Wafanyakazi wa kituo cha afya Buguruni katika picha ya pamoja.

WAKULIMA WA SHAYIRI MONDULI WAELEZEA MAFANIKIO YAO KWA TBL

$
0
0
 Mkulima wa Shayiri akionesha moja ya Ghala lake (Stoo) kwa ajili ya kuhifadhia zana mbalimbali za kilimo ikiwamo utunzaji wa pembejeo, ambapo jengo hilo amelijenga kutokana na fedha za Shayiri.
Baadhi ya Wanawake wanaojishughulisha na kilimo cha Shayiri wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa wa  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha anayesimamia wakulima katika eneo hilo la Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha.
Mkulima wa Shayiri wilayani Monduli Meporoo Losulu akionesha Trekta zake mbili ambazo amezinunua kutokana na kilimo cha Shayiri.

Pichani ni baadhi ya nyumba za Mkulima wa Shayiri, Barrick Kivuyo zikionekana baada ya kuwa amezifanyia ukarabati ikiwa ni pamoja na kuweka umeme wa jua (Solar).

Mkwaja FC mabingwa wapya Mwidau CUP 2014

$
0
0
 Mabigwa wa Mwidau CUP 2014, Timu ya Mkwaja FC wakishangilia ushindi baada ya kukabidhiwa kombe.
   Mbunge Amina Mwidau akikabidhi kombe ya ushindi kwa kapteni wa timua Mkwaja FC, Salim Rashid akiwa pamoja na wabunge wenzake.
 Mbunge Amina Mwidau akikabidhi kombe ya ushindi kwa kapteni wa timua Mkwaja FC, Salim Rashid akiwa pamoja na wabunge wenzake.
Mabigwa wa Mwidau CUF 2014, Timu ya Mkwaja FC wakishangilia ushindi baada ya kukabidhiwa kombe.



Na Mwandishi Wetu,Pangani 
 Timu ya soka ya Mkwaja FC imetwaa ubingwa wa kombe la Mwidau CUP mwaka 2014 baada ya kuifunga timu ya soka ya Kiman’ga kwa mabao 4-2 katika mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Mwera wilayani Pangani. 

 Mchezo huo ambao ulikuwa ni wakuvutanikuvute katika kipindi cha kwanza lakini timu ya Kiman’ga ilionyesha kuzidiwa uwezo kwa kuweza kuruhusu mvua ya magoli katika dakika za awali toka mpira kuanza. Mchezaji wa Mkwaja FC Masoud Ticha ndio alionekana kinara katika mchezo baada ya kuifungia timu yake mabao matatu katika dakika za 8 na 38 kabla ya kwenda mapumziko . 

 Hata hivyo kipindi cha pili Kiman’ga ilionyesha makucha baada ya kuandika bao la kwanza katika dakika ya 49 baada ya mchezaji wake frank kufanikiwa kufunga golo hilo baada ya kumhada mlinda mlango wa Mkwaja. 

 Goli la pili la timu hiyo lilipatikana katika dakika 70 hali iliyoleta matumaini kwa mashabiki wa timu hiyo kuamini kwamba wataweza kurudisha magoli yote lakini shauku yao ilikwisha baada ya dk 80 Mkwaja FC kufunga bao la nne. Akikabishi zawadi kwa washindi hao Mbunge wa viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF), kwa timu ya Mkwaja FC walijinyakulia kitita cha fedha taslimu Sh 500,000, kikombe kikubwa, medali za dhahabu, seti mbili za jezi pamoja na mpira. 

 Huku mshindi wa pili ambae ni Kimang’a alipata Sh 200,000,kikombe kidogo, medali ya shaba, seti moja ya jezi pamoja na mpira huku timu 40 zilizoshiriki zikipatiwa mpira na 16 zikipatiwa jezi seti moja moja. 

 Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa mchezo huo Mwidau, alisema kuwa atahakikisha anakuza vipaji vya soka katika wilaya hiyo kwa kuwashirikisha kwenye mashindano mbalimbali hapa nchini. Katika mchezo huo wa fainali ulidhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji pamoja na Mbunge wa Chambani, Yussuf Salim wote kutoka CUF.

BUSINESS OPPORTUNITY

$
0
0
Angellifestyle of South Africa invites you to the Business Opportunity Meeting that will be held on 22nd of November, 2014 at JB Belmont - Golden Jubelee Tower by the founder and Managing Director of Angellifestyle... You are all welcome to get and gain financial freedom through Angel Business Opportunity for FREE.. For more details please call 0713089800

TIMU YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YAKAGUA MADARAJA LUHEKEI MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Ruvuma, Mhandisi Abraham Kissimbo akizungumza na timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika ofisini kwake.
 Kiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jekundu) pamoja na timu yake wakijionea Daraja la Luhekei C lenye urefu wa mita 60.
 Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na  mwenyeji wao Mhandisi Lusage Mulenzi katika kibao cha ufunguzi rasmi wa Darala la Luhekei C. Daraja hili lina urefu wa mita 60, lilifunguliwa rasmi tarehe 18 Julai, 2014 na Mheshimiwa Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI

AIRTEL YAMWAGA VITABU VYA MILIONI 15 WILAYANI MAKETE -NJOMBE

$
0
0
Meneja wa Kanda za juu kusini wa Airtel bw, Straton Mushi akikabidhi msaada wa vitabu kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dokta BINILITHI MAHENGE utakaofaidisha jumla ya shule 5 zilizopo wilaya ya Makete mkoani Njombe. Shule zinazofaidika ni Iwawa, Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe wilaya ya Makete. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana katika shule ya Iwawa iliyopo wilayani Makete. Anaeshudia kushoto ni mkuu wa shule msaidizi bw, Fadhili Dononda.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dokta BINILITHI MAHENGE na Meneja wa Kanda za juu kusini wa Airtel bw, Straton Mushi na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari iwawa wakifurahia baadda ya hafla ya makabidhiano ya msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 15 utakaofaidisha jumla ya shule 5 zilizopo wilaya ya Makete mkoani Njombe. Shule zinazofaidika ni Iwawa, Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe wilaya ya Makete. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana katika shule ya Iwawa iliyopo wilayani Makete.

Mradi wa SHULE YETU unaotekelezwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya AIRTEL umeendelea kunufaisha shule kadhaa nchini kwa sasa umeingia wilayani Makete, Mkoani Njombe na kutoa msaada wa Vitabu vya kiada na ziada vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi zaidi ya Milioni 15 kwa shule tano wilayani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dokta BINILITHI MAHENGE ndiye aliyepokea shehena ya Vitabu hivyo ambapo pamoja na mambo mengine amesifu Msaada huo kuwa unaunga mkono Juhudi za Rais JAKAYA KIKWETE katika kufanya mabadiliko makubwa katika sayansi na teknolojia nchini kwa kuwekeza kwenye elimu.

Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo wilayani Makete Mkoani Njombe kwa niaba ya shule zingine zinazofaidika na mradi huo zikiwemo Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe wilaya ya Makete.

MENEJA BIASHARA AIRTEL KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI STRATON MUSHI alisema "Kampuni ya AIRTEL tunakabidhi vitabu vya masomo ya KEMIA, FIZIKIA na HESABU ikiwa ni mwendelezo wa kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha wanafunzi kupenda zaidi masomo ya mchepuo wa sayansi ambapo vyote hivi vinathamani ya shilingi milioni kumi na tano".

Akipokea msaada huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira Dr BINILITHI MAHENGE ameipongeza AIRTELL kwa kuungana na Rais JAKAYA KIKWETE aliyethubutu kufanya mabadiliko kwenye masomo ya sayansi.

DR BINILITHI MAHENGE-WAZIRI WA MAZINGIRA alisema "nchi yetu itaendelea endapo tu tutawekeza kwa uhakika katika elimu, mataifa yalioyoendelea leo hii kila kitu kinafanikiwa kuwa kiwango cha elimu cha wananchi wake ni cha hali ya juu".

Kwa upande wao baadhi ya wananfunzi wa shule mwenyeji waliopokea vitabu hivyo kwa niaba ya shule nyingine wameeleza kufurahia kwao kupokea msaada wa vitabu hivyo vitakavyokuwa ni suluhisho la uhaba wa vitabu unavyowakabili wanafunzi wa shule 16 za sekondarii zilizomo wilayani Makete.

"Tunaishukuru sana Airtel sisi wanafunzi wa shule ya sekondari ya Iwawa tutavitumia kwa uangalifu kwa manufaa ya wengi na pia tunawaahidi Airtel na Mheshimiwa Waziri kuwa tutahakikisha tunapata matokeo ya ufaulu mzuri kwa kuvitumia ipaswavyo" alisema Kiranja mkuu wa Shule hiyo.

Airtel imeanzisha mpango wa Airtel Shule yetu ili kuendeleza Elimu Inchini Tanzania kwa kusaidia shule mbalimbalikali ambapo hadi sasa zaidi ya shule 15000 zimeshapewa vitabu vya kiada kupitia mradi huo.

Mkutano Mkuu wa Bandari za Africa na Ulaya Wafanyika Mombasa

$
0
0
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakisikiliza hotuba , Kushoto ni mjumbe  toka Afrika kusini katikati ni Mkurugenzi wa ICT TPA Ndg. Phares Magesa, na kulia ni Mkurugenzi Mkuu TPA Eng.Madeni Kipande
  Ndg. Magesa akifuatilia mkutano huo
 Gavana wa County ya Kwale akitoa hotuba kwenye ufunguzi na kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua mkutano huo
 Waziri wa Biashara na Viwanda wa Kenya Mhe. Adan Mohamed akitoa hotuba rasmi ya ufunguzi wa mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA , Mwenyekiti wa bodi TPA, Katibu Mkuu wa PMEASA , na Mkurugenzi Mkuu TPA wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

Article 4

$
0
0
TURKISH ENVOY TO TANZANIA , H.E. ALİ DAVUTOĞLU SPEAKS ON TURKISH AFRICAN PARTNERSHIP IN REFERENCE TO AN ONGOING SUMMIT THE  SECOND TURKEY - AFRICA PARTNERSHIP SUMMIT ONGOING IN MALABO, EQUATORIAL GUINEA, ON 19-21 NOVEMBER 2014.
Africa is now in an impressive surge of growth, urbanization and modernization. The natural and human resources are abundant and diverse. One can easily see Africa re-emerging with many promising developments. Africa has an average annual growth rate of 5 percent over the last decade and is expected to continue this trend in the coming years. 6 out of 10 fastest growing economies in the world are in now Africa.

In terms of Turkish Foreign policy Relations with Africa constitutes one of the prime orientations of Turkish foreign policy, which is not based temporary political and economic considerations. On the contrary, it is the process of strong historical and cultural ties that we have with Africa.Following a multi-faceted policy in Africa, establishing close political relations and intensifying bilateral high level visits. Also economic field is another area that we help African nations overcome their challenges through more trade, investment, technical and humanitarian assistance.

Turkey is doing its level best to contribute through diplomacy to the peaceful settlement of conflicts and disputes in Africa. Therefore, we do not consider ourselves as outsiders to the continent, rather a strategic partner. Turkey-Africa relations have gained a substantial momentum since the declaration of Turkey as a strategic partner of the Continent by the African Union in January 2008. Turkey-Africa relations have gained a substantial momentum since then. For example, in the year of 2009 there were only 12 Turkish Embassies in Africa. There is now 39. It is not one sided. We see, today, a growing number of African Embassies in Ankara. It reached 30 while it was merely around 10 five years ago.

For Turkey it is not just about diplomatic representation and developing political relations. People-to-people contacts have intensified tremendously as a result of direct flights between Turkey and African countries as well as ever growing numbers of students, business people and tourists travelling both ways. Turkish Airlines has become major international airline connecting the continent to the world with a total number of flights to over 40 destinations in 28 African countries. 

Direct flights of Turkish Airlines had an immense effect on bilateral trade volume reaching 23,4 billion USD in 2013 with all Africa. It is 7,5 billion USD with Sub-Saharan Africa. When we compare the figures in 2000 which was about 750 million USD and those of 2013, we see an increase of almost tenfold. When people get to know more about each other, they stand ready to deepen their relations. More than 200 thousand people travel mutually between Turkey and the African countries for business, tourism and cultural purposes. Turkey provides around 500 scholarships annually for students from Africa.

Besides, Turkey has become a leading country in humanitarian activities all over the continent. Turkish International Cooperation and Coordination Agency (TİKA) has a central role in organizing and funding humanitarian projects that many people can benefit. TİKA currently operates 11 Program Coordination Offices in Africa and the number is expected to increase.

After the first Summit in Istanbul in 2008, Second Turkey-Africa Partnership Summit will be held on 19-21 November 2014 in Malabo, Equatorial Guinea. We preferred to name it as Partnership Summit not just because we want to further develop our relations with Africa, but also we want to surpass what we achieved after the First Summit. That’s why the theme of the Summit is called “a new model of partnership to enhance a sustainable development and integration of Africa”.

Halmashauri ya Mji Handeni lawamani

$
0
0
MKUTANO wa kwanza wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation uliyofanyika juzi Novemba 19, katika kijiji cha Misima, wilayani Handeni, mkoani Tanga na kuwakutanisha wananchi wote umeibua kero nyingi za wananchi, ikiwamo ya kijiji chao kuingizwa kwenye Halmashauri ya Mji bila ridhaa yao. 
Mmoja wa wakazi na wananchi wa kijiji cha Misima, akilalamikia eneo lao kuingia kwenye Halmashauri ya Mji kinyume cha sheria ya utawala bora, ikiwa ni pamoja na kutoshirikishwa kwa lolote na viongozi wa juu.
 
Taasisi hiyo ilianzishwa mapema mwaka huu na kuzinduliwa Mei 8 jijini Dar es Salaam, ilifanya mkutano mkubwa wa hadhara Misima, ambapo umati wa wanchi ulihudhuria, huku kero nyingi zikiwasilishwa na kudhihirisha changamoto za utawala bora zinazoathiri maendeleo ya Tanzania.
 
Wakizungumza kwa uchungu mkubwa, mwananchi wa Misima aliyejitambulisha kwa jina la Mhina Ally, alisema viongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na madiwani waliamua kuingiza kijiji chao katika Halmashauri ya Mji bila ya kuwashirikisha, ikiwamo kubandika tangazo la pingamizi kwa siku 90 katika maeneo yao kama sheria inavyotaka.
 
Alisema kutoka Handeni Mjini hadi katika eneo lao ni kilomita 16 zilizozunguukwa na mapori yanayowafanya wananchi wajihusishe na kilimo kwa asilimia 99, hivyo kuingizwa kwenye sheria za mji ni kusababisha ugumu wa maisha.
 
“Inashangaza mno kusikia Tanzania kuna utawala bora wakati viongozi wachache wanaweza kufanya watakavyo; hali inayoweza kuleta mapigano makubwa, endapo wananchi tutasimama kidete kudai haki zetu zinazokandamizwa na viongozi kila siku,” alisema.
 
Ally alifika mbali zaidi kwa kusema walisikia tangazo redioni la kuingizwa kwenye Halmashauri ya Mji, huku tangazo la pingamizi likishindwa kuwekwa kijijini kwao kwa hofu ya kupingwa na wananchi wao.
 
“Viongozi wa serikali ya kijiji waliamua kutoliweka tangazo la pingamizi kijijini kwetu kwasababu wanajua fika tusingekubali, hivyo inashangaza malalamiko yetu kufumbiwa macho na serikali inayoitwa sikivu, licha ya kuzunguuka sehemu nyinyi, kama kwa Mkuu wa wilaya na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa Tanga, alipokaimu DC Halima Dendego, ambaye sasa amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,” aliongeza.
 
Naye Naye Idd Kisege alisema kuwa ili kuona viongozi wanaogopa kufika Misima, hata namba kwenye nyumba zao hakuna ingawa wanatangaza uchaguzi kwa sheria za mji katika kijiji chao, jambo lisiloweza kuvumiliwa na kila mpenda maendeleo ya Misima.
 
“Watu wa Misima tunaambiwa sisi ni watata, wakorofi tunapodai haki zetu, ili waendelee kutuburuza, ndio maana kwenye ziara ya Mheshimiwa Rais, Profesa Jakaya Mrisho Kikwete waliniburuza Polisi kwasababu ya kuonyesha bango kwa mheshimiwa ili kuona kero zetu,” alisema Kisege.
 
Naye Mkomwa Athuman alisema kuwa Misima haipo tayari kutumikia sheria za Mji kwakuwa ni mapema mno kwao, hivyo wanaomba serikali, ikiwamo ofisi ya Waziri kulifuatilia suala hilo kwa kina.
 
“Mzozo huu umeshakuwa mkubwa na kuondoa ushirikiano kabisa kwa viongozi na wananchi wa hapa Misima, hivyo tayari malalamiko yetu yamefikishwa Ofisi ya Waziri Mkuu kulishtakia suala hilo kwasababu sheria ya kuingia kwenye Mamlaka ya Mji Handeni haijafuatwa na imeanzishwa na watu wachache ili kuzima uozo wa ardhi waliyoufanya kwenye kijiji chetu,” alisema.
 
Katika kila mwananchi aliyezungumza kwenye mkutano huo alionyesha kuguswa na kero hiyo ya mji, huku wakisema kutoka Handeni Mjini hadi Misima ni mbali pamoja na viongozi kushindwa kufuata sheria za utawala bora.
 
Awali, mkutano huo ulioanza saa tisa alasiri ulifunguliwa na mtoa mada wa kwanza, Kambi Mbwana, ambaye ndiye Msemaji Mkuu wa taasisi hiyo, aliyejikita sababu na dhamira kuu ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo.
 
Mbwana alisema kuwa sababu kubwa ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha utawala bora, ikiwa ni njia moja wapo ya kuwafanya Watanzania wote wajiletee maendeleo kwa kushirikiana baina yao na viongozi wote.
 
Akizungumzia utawala bora, Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Adam Malinda, alisema kwamba matatizo mengi katika jamii yamekuwa yakichangiwa na viongozi wasiojua nini maana ya utawala bora.
 
“Utawala bora ni somo muhimu na lazima lipigiwe kelele na watu wote, maana malalamiko mengi ya watu wa Misima yamesababishwa na tatizo hilo, ndio maana unaona kero zimepamba moto,” alisema.
 
Malinda aliwataka viongozi wa juu, wakiwamo wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kuzungumza na wananchi wa Misima ili kutatua mtafaruku huo kwa ajili ya kuwafanya wananchi waendelee na shughuli za kujiletea maendeleo, sambamba na serikali kuwafanyia kazi watendaji wabovu.
 
Kuhusiana na mzozo huo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, alikaririwa akisema kuwa utaratibu ulifuatwa, ikiwamo kutoka kwa siku 60 za pingamizi, ingawa wananchi hao walishindwa kupita njia hiyto kwa ajili ya kufanikisha malengo yao.

Warsha ya Sanaa na Harakati kwenye Jamii yaanza kufanyika jijini Dar es Salaam

$
0
0
Nafasi Art Space kwa kushirikiana na Tunawea leo wameendesha Warsha ya siku mbili ya Sanaa na Harakati iliyowakutanisha baadhi ya Wasanii, Waandishi wa Wanaharakati nchini Tanzania ambapo Mpiga picha na Mwanaharakati Boniface Mwangi kutoka Kenya ndio mwezeshaji katika warsha hiyo
 Mpiga picha na Mwanaharakati Boniface Mwangi kutoka Kenya, akizungumza na washiriki wa warsha hiyo
 Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada mbalimbali
 Mpiga picha na Mwanaharakati Boniface Mwangi kutoka Kenya, akizungumza na washiriki wa warsha hiyo
 Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo
Mwazilishi wa Change Tanzania, Maria Sarungi Tsehai akichangia mada wakati wa warsha ya Sanaa na Harakati iliyofanyika jijini Dar es Salaam

SIKU YA UHURU WA OMAN WASHINGTON, DC

$
0
0
 Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Bwn. Suleiman Saleh(kulia) akimwakilisha Balozi Liberata Mulamula kwenye tafrija ya siku ya Uhuru wa nchi ya Oman iliyofanyika Washington, DC siku ya Jumanne Novemba 18, 2014. Mwingine katika picha ni Seif Ameir ambaye ni mfanyakazi kwenye Ubalozi huo.
 Toka kushoto ni Bi. Farida Saleh na Bi. Nargis Ameir wakiwa katika picha ya pamoja walipohudhuria sharehe ya uhuru wa nchi ya Oman iliyofanyika siku ya Jumanne Novemba 18, 2014 jijini Washington, DC.
Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Bwn. Suleiman Saleh(kulia) akimwakilisha Balozi Liberata Mulamula kwenye tafrija ya siku ya Uhuru wa nchi ya Oman iliyofanyika Washington, DC siku ya Jumanne Novemba 18, 2014. Wengine katika picha toka kushoto ni Bwn. Seif Ameir akifuatiwa na mama mwenye nyumba wake Bi. Nargis Ameir na  Bi. Farida Saleh ambaye ndiye barafu ya moyo wa  Afisa Suleiman Saleh.
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images