Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 408 | 409 | (Page 410) | 411 | 412 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Askofu mkuu wa KAnisa la kiinjili la kirutheri la Tanzania KKKT, Alex Malasusa akiweka shahada la maua katika kaburi la askofu mtaafu Cliopa Lukilo, Picha na James Festo.
  ==========   =======  ========
  Na James Festo, Njombe.

  ASKOFU  wa kanisa la  kiinjili la kirutheli Tanzania KKKT,  Alex Malasusa hapo jana  amewaongoza waumini  wa kanisa hilo na wananchi wengine katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa askofu mstaafu wa awamu ya nne  Marehemu Cleopa Akutulaga Lukilo ambaye alifariki novemba 13  nyumbani kwake na kuzikwa hapo jana katika viwanja vya kanisa hilo mjini Njombe.

  Akihibiri katika mazishi hayo yaliyofanyika katika kanisa la kilutheri Dayosisi ya kusini Njombe Askofu Malasusa aliwataka wananchi kuacha kufuatilia tofauti zao badala yake kuuutumia mda huo kufanya shughuli za maendeleo  na kuwasaidia masikini  na wenye matatizo.

  Aidha Malasusa aliwasihi waumini wa kanisa hilo kuepukana na tabia za kulipiza visasi na kutafuta riziki kwa njia halali  na sio kwa njia ya udanganyifu na kujenga mazoea ya kutubu dhambi kwa sababu mwanadamu hajui saa wala dakika ya kufariki kwake.

  "natamani tungekuwa tunaamani muda wote lakini amani haiwezi kuwepo bila ya watu kutengeneza bila watu kutubu dhambi tujifunze kutubu dhambi kwa sababu hakuna anayejua siku ya kufa anayejua ni mungu pekee inatubidi tujiandae siku  zote kwa kutubu" alisema Malasusa.

  Alisema kuwa marehemu alifariki siku nne baadae baada ya kusema kuwa yeye amejiandaa kufa wakati akifungua mkutano wa umoja wa wanawake wamakanisa mkoani Njombe.

  Alisema kuwa marehemu alitaja mara nne kuwa anejiandaa kuwa akisema"Mimi nimejiandaa kufa, mini nimejiandaa kufa vizuru" alisema wakati wa kufungua mkutano huo na kufa siku nne baadae.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk. Rehema Nchimbi akitoa salamu za rambirambi aliwataka waumini wa kanisa hilo kutoka mkoa wa Njombe kuendelea kumuenzi kwa kufuata mema aliyoyafanya marehemu Askofu katika kulitumikia kanisa hilo ikiwemo kuanzisha chuo cha kikuu cha Tumaini tawi la Amani la Njombe.

  Aliwasihi viongozi wa kanisa hilo kuendelea kutumikia vizuri  nafasi za utumishi walizonazo na kuongeza bidii kuliombea Taifa la Tanzania ili kujengeka kiimani na watulivu.

  "Huu ni wakati mgumu sana sote tunatakiwa kuungana kunzia nyinyi viongozi wa kanisa kwa ngazi zote kuendelea kuliombea taifa ukiwemo Mkoa wetu ili tuwe na amani siku zote na tuwe mfano wa kuigwa na mikoa mingine kwa kuwa na amani" alisema Nchimbi.

  Dr. Nchimbi alisema kuwa viongozi wanatakiwa kuombewa  ili wasiweze kutafuna mali za umma na kuwa watiifu wanapokuwa katika uongozi wa wananchi mpaka wanamaliza mda wao wa kuongoza kwani viongozi hao ni moja ya kondoo wanao wachunga.

  Akisoma historia ya marehemu, Katibu mkuu wa dayosisi ya kusini Timias Mhomisoli alisema kuwa Askofu Lukilo alizaliwa mwaka 1949 katika kijiji cha ukemele wilayani Mufindi Mkoani Iringa  na kufariki novemba 13 mwaka huu, maiti yake kuzikwa hapo jana katika viwanja vya kanisa kuu la dayosisi ya kusini Njombe.

  0 0

  Picha ya pamoja, Baadhi ya wana kikundi cha UWF, mwakilishi kutoka Tanzania Women Bank (TWB), Bi Khadija na Baadhi ya washindi wa mradi huo wa Mwanamakuka tangu mwaka 2012 wakiwa katika picha pamoja.
   Pichani kulia ni Mwenyekiti wa UWF na Meneja Mradi wa Mwanamakuka,Bi.Maryam Shamo, akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) Mikocheni jijini Dar,mwishoni mwa wiki,kuhusiana na hafla fupi ya kumkumbuka Marehemu Aziza Mbogolume,ambaye alikuwa mshindi wa kwanza wa shindano la MWANAMAKUKA 2013.
   
  Shindano hilo huandaliwa na kikundi cha UNITY OF WOMEN FRIENDS (UWF),kupitia mradi wao wa MWANAMAKUKA, hafla hiyo pia iliwakutanisha wadau mbalimbali wa kikundi hicho wakiwemo na washindi wa mradi huo ambao umekuwa ukifanya vyema kila mwaka,Anaefutia pichani ni Bi Jane Magembe, , Mwate Madinda na Martha Kalaghe.  
  Mwenyekiti wa UWF na Meneja Mradi wa Mwanamakuka,Bi.Maryam Shamo,akionesha moja ya, kipaji cha marehemu Aziza, ambacho kilikuwa ni uchoraji. 
   Baadhi ya washindi wa mradi huo wa Mwanamakuka tangu mwaka 2012 wakijadiliana jambo,ambapo walikukutana kwa madhumuni ya kumkumbuka Mwanamakuka mwenzao aliyefariki.  

  0 0

   
  Mmoja kati ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania akitoa fedha kutoka katika akaunti yake kupitia mashine ya ATM iliyopo katika tawi jipya la Benki hiyo la Ushirika lililopo katika Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam jana
  ========  ========  =========
  BENKI ya Exim Tanzania imeendelea kutanua wigo kwa wateja wake nchini kwa kufungua tawi jipya lililopo katika mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, ikiwa ni jitihada za Benki hiyo kutoa huduma bora za kibenki kwa kuwafikia wateja wake wote kiurahisi. Tawi hilo la Ushirika linaongeza idadi ya mtandao wa matawi ya Benki ya Exim ambayo yameendelea kusambaa nchi nzima.  

  Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Operesheni wa Benki ya Exim, Bw. Eugen Masawe alisema kuwa tawi hilo jipya linaipa fursa nyingine benki ya Exim kutoa huduma zake za kipekee za kibenki kwa idadi inayozidi kuendelea kuongezeka ya wateja wake. 

  “Tunayofuraha kutangaza kuwa Tawi la Ushirika sasa limefunguliwa rasmi. Hili ni eneo muhimu kwa wateja wetu, kutokana na urahisi wa upatikanaji wa huduma,” alisema Bw. Masawe. 

  Alisema kuwa tawi hilo jipya ni uthibitisho pekee wa ukuaji thabiti wa biashara ya benki yake, ongezeko la idadi ya wateja na jitihada zake za kutoa huduma za kipekee kwa wateja wake na jamii yote ya biashara nchi nzima kwa ujumla. 

  “Tumekuwa na mkakati wa kumuweka mbele mteja, ambayo umetuwezesha kupeleka huduma zetu pale ambapo pana wingi wa wateja wetu.  “Dar es Salaam kwa kuwa kitovu cha biashara Tanzania, tumeshuhudia ongezeko la wateja wengi ambao uhitaji huduma zetu katika mkoa huu. Tukiwa na matawi zaidi ya kumi jijini, pamoja na huduma mbali mbali za kibunifu, benki ipo mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wateja wake wanakabiliana na ubize wa ratiba zao kwa kupata huduma za haraka na bora za kibenki kutoka Benki ya Exim,” alisema Bw. Masawe. 

  Alibainisha kuwa jitihada hiyo ya benki kutanua wigo wake haitoongeza tu mizania ya benki yake kwa kiasi kikubwa na kuongeza idadi ya wateja wake, lakini pia kuhakikisha kuwa benki inayafikia masoko mengine ambayo bado hayajafikiwa nchini.  “Tunampango wa kuendelea kufungua matawi mengine nchi nzima katika siku za usoni. Utekelezwaji wa mkakati huo utaiwezesha benki ya Exim kupeleka huduma zake karibu zaidi na  wateja wake,” aliongeza.

  0 0

  SONY DSCKiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Mwenye koti jekundu) akihoji masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji kwenye manispaa ya Songea.SONY DSCTimu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikishuka kutoka kwenye tanki la kuhifadhia maji ya Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani utakaohudumia zaidi ya wakazi 3000 wa kitongoji ya Kijiji cha Ruhuiko Kanisani na maeneo ya jirani.SONY DSCKiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza mara baada ya timu yake kukagua Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani. Wanaomsikiliza kutoka kulia ni Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara, anayemfuatia ni Msanifu wa Mradi huo Bw. Elezear Ndunguru na Mratibu wa ukaguzi huo Bw. Senya Tuni (Wapili kulia).

  …………………………………………………………………
  Na Saidi  Mkabakuli
  Serikali imetoa wito kwa taasisi za umma kusimamia kwa umakini miundombinu ya miradi ya maji pindi inapokamilika ili kuweza kuwapatia wananchi huduma ya maji ya uhakika mara miradi hiyo inapokabidhiwa kwa kamati za usimamizi wa maji.
  Wito huo umetolewa na kiongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati timu hiyo ilipokuwa ikifanya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya maji ya utekelezaji wa program ya maji na usafi wa mazingira katika vijiji 10 vya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
  Bibi Mwanri ambaye pia ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu, alisema kuwa kwa miaka mingi kumekuwepo na ubadhirifu wa miundombinu ya miradi mingi ya maji hali inayorudisha nyuma juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wananchi wanafikiwa na maji safi na salama kote nchini.
  “Kumekuwa na tabia mbaya ya ubadhirifu wa miundombinu hii, msikubali waiharibu ama kuiba vifaa vya ujenzi wa miradi yote 10 maana kama munavyoona serikali na wafadhili wamejitolea ili kuhakikisha munafikiwa na huduma hii muhimu,” alisema.
  Akizungumza wakati timu hiyo ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ilipotembelea na kukagua Mradi wa Maji wa Ruhuiko Kanisani utakaohudumia zaidi ya wakazi 3000 wa kitongoji ya Kijiji cha Ruhuiko Kanisani na maeneo ya jirani, Msanifu wa mradi huo, Bw. Elezear Ndunguru alisema kuwa mpaka sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 55.
  “Kasi ya utekelezaji wa mradi huu ni ya kuridhisha kwani mpaka sasa tumeweza kujenga vituo 12 vya kuchotea maji kati ya 15, kinachongojwa kwa sasa ni kukamilika kwa tanki la kuhifadhia maji,” alisema.
  Msanifu huyo ameongeza kuwa hadi kukamilikwa miradi yote 10 jumla ya shilingi bilioni 2.77 zitatumika na kuweza kuwahudumia zaidi ya wakazi 9000 wa vijiji vitakavyopitiwa na miradi hiyo.
  Kwa mujibu wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo, lengo kuu kwa upande wa maji ni kuongezeka kwa upatikanaji wa maji safi na salama ni mojawapo ya maeneo yanayotiliwa mkazo ili kuweza kuongeza kasi ya maendeleo na kupunguza umaskini miongoni mwa Watanzania.

  0 0

   Meneja wa Airtel Simiyu Bw. Ezekiel Nungwi akikabidhi msaada wa vitabu vya sayansi kwa Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima.
   Mkuu wa shule ya sekondari ya Bariadi Bw. Pawa Lutema akipokea msaada wa vitabu vya sayansi kutoka kwa mkuu wa wilaya Bariadi.
   Mkuu wa wilaya ya  Bariad Bw. Erasto Sima akisoma Hotuba katika makabidhiano ya msaada wa vitabu vya masomi ya sayansi kwa shule ya sekondari Bariadi uliotolewa na kampuni ya Airtel Tanzania

  ========  =======  ========
  Airtel Yaendelea Kusaidia Sekta ya Elimu hapa Nchini
  ·       Shule ya Sekondari Bariadi yanufaika na msaada huo

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imepiga jeki jitihada za serikali za kuhamasisha masomo ya sayansi kwa kutoa msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule ya sekondari ya Bariadi iliyopo Mkoani Simiyu.

  Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 1.5 unahusisha vitabu vya fizikia, hisabati, baiolojia na kemia kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo shuleni hapo.

  Akipokea msaada huo mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima amesema shule nyingi wilayani hamo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitabu vya masomo ya sayansi licha ya kwamba kuna uhaba pia wa walimu wa masomo hayo.

  “Ni kweli kwamba uhaba wa vitabu unakwamisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi kujifunza kwa ufasaha masomo ya Sayansi wilayani Bariadi hali inayorudisha nyuma ukuaji wa elimu ya sayansi wilayani hapa”. Alisema Bwana Sima.

  “uhaba wa vitabu ni moja ya changamoto, lakini uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ni kikwazo kikubwa kwa utoaji wa elimu ya sayansi kwa wanafunzi wetu hapa Bariadi” aliongeza Bwana Sima.

   Aidha Bw. Sima ameishukuru kampuni ya simu ya airtel  kwa kuona umuhimu wa kuboresha masomo ya sayansi ambayo  ufaulu wake umekuwa mdogo hali ambayo inayotoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa umakini zaidi.

  “Msaada huu utaongeza hamasa kwa wanafunzi wetu kujifunza masomo ya sayansi hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kuona umuhimu wa kusaidia shule hii na hasa vitabu vya sayansi” alimalizia Bwana Sima.

  Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekonderi Bariadi Bw. Pawa  Lutema akipokea vitabu hivyo, amesema hatua hiyo ni sehemu ya utatuzi wa changamoto ya vitabu vya sayansi na kisha kuahidi kuvitunza ili viwe msaada kwa wanafunzi watakaosoma shuleni hapo.

   Awali  meneja wa Airtel Mkoani Simiyu Bw. Ezekiel Nungwi  akikabidhi  msaada huo wa vitabu  amesema kuwa kampuni yake inaendelea na mpango wake wa kutoa msaada wa vitabu kwenye shule mbalimbali nchini kwa lengo la kusaidia ukuaji wa elimu nchini.

  Msaada huo wa vitabu vya masomo ya hisabati,kemia,fizikia na Bailojia utasaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye shule hiyo.
   

  0 0

      Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza (Kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa batiki yaliyoanza mapema wiki hii kwenye Ofisi za Baraza hilo zilizoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni  Bi. Leah Ruhimbi
       Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla akiongea na Wasanii (hawako pichani) waliohudhuria kwenye mafunzo ya wiki moja ya utengenezaji batiki yanayoandaliwa na kituo chake kwa kushirikiana na BASATA na kufanyika makao makuu ya BASATA. Mwingine katika picha ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi. Leah Ruhimbi
        Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi. Leah Ruhimbi akifungua mafunzo ya utengenezaji batiki kwa wasanii wa Sanaa za Ufundi yanayofanyika kwa wiki moja makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba. Wengine kutoka kulia ni  Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka BASATA Bi. Vivian Shalua na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla
      Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka BASATA Bi. Vivian Shalua akiwaelekeza jambo wasanii wanaoshiriki mafunzo ya utengenezaji batiki
  Sehemu ya Wasanii wa utengenezaji batiki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo. Picha, habari na Aristide Kwizela-Afisa Habari BASATA


  ======  ======  ======== =====
  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Ujeruman maarufu kama Goeth Insitut wameendesha mafunzo ya utengenezaji batiki kwa wasanii wa Sanaa za mikono yanayofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA jijini Dar es Salaam.

  Mafunzo hayo yanayotazamiwa kudumu kwa siku tano yaani kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa yanalenga kuongeza ubunifu na weledi miongoni mwa wasanii wa Sanaa za mikono ili kuongeza ubora na tija katika uzalishaji.  

  Mapema akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Leah Ruhimbi alisema kwamba mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija kwa wasanii hao na kuwawezesha kubuni Sanaa zenye ubora zitakazopenya masoko mbalimbali ya Sanaa.“Ni matarajio ya BASATA na wizara kwamba mafunzo haya yatakuwa yenye tija kwa wasanii na yatawawezesha kusambaza ubunifu na uzoefu kwa wasanii wengine nchini. Lengo ni kuwa na sanaa zenye ubunifu na ubora” alisisitiza.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Goeth Institut Bi. Eleonore Sylla alisema kwamba mafunzo hayo yanahusisha wasanii wenye uwezo wa kutengeneza batiki na lengo kuu ni kuwaweka pamoja ili wachangie uzoefu na baadaye kutengeneza batiki zenye ubora zaidi.“Tunajua mnatoka sehemu mbalimbali nchini na wote mna uzoefu katika utengenezaji wa batiki lakini kuwa kwenu pamoja kwenye mafunzo haya kutawafanya mpate uzoefu zaidi na hatimaye kubuni batiki zenye ubora” aliongeza Sylla.

  Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alisema kwamba BASATA kwa kushirikiana na Goeth Insitut wameona kwamba kuna haja ya mafunzo hayo ya wasanii na kwamba baraza litaendelea kuboresha ubora wa kazi za Wasanii kupitia kuwajengea uwezo.

  0 0

  E88A9486

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akimsikiliza Diwani wa Kata ya Matui Wilayani Kiteto Bw.Athuman Kidawa wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa  vifo.kushoto ni Afisa tarafa wa Matui Bw.Eliakimu Ndelekwa.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)E88A9514
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akizungumza na wananchi  wa Kata ya Matui Wilayani Kiteto wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa  vifo. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)E88A9421
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akizungumza na Mtendaji wa Kijiji cha Chekanao, Kata ya Kiperesa , Wilayani Kiteto Bw.Omar Ndee (kulia) wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa vifo.Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Deusdedit Nsimike pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Japhet Chafu (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
   
  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Kiteto.
   
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ameahidi kuongeza idadi ya Askari katika kijiji cha Chekanao, kata ya Kiperesa wilayani Kiteto Mkoani Manyara kufuatia wananchi katika kijiji hicho kujitolea nyumba kwa ajili ya kuishi Askari kwa lengo la kuimarisha usalama katika maeneo yao kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi inayosababisha kutokea kwa mauaji.
   
  IGP Mangu aliyasema hayo jana wakati alipokuwa katika ziara Wilayani Kiteto ya kujionea uharibifu uliojitokeza pamoja na kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo iliyopelekea kutokea kwa vifo vya wakulima na wafugaji hivi karibuni katika wilaya hiyo ambapo watu kadhaa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na vurugu hizo.
   
  Alisema kufuatia kuwepo kwa umbali mrefu wa kituo cha Polisi na kijiji hicho atahakikisha askari wa kudumu wanakuwepo ili kushirikiana na wananchi katika kuwabaini wahalifu wanaofanya vurugu na kuendeleza migogoro hiyo ambapo wananchi nao waliahidi kujenga kituo cha Polisi.
   
  Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Chekanao Bw.Omar Ndee alisema wamekuwa wakipata shida kutokana na umbali mrefu wa kituo cha Polisi jambo ambalo limekuwa likifanya kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu vinavyochangiwa na migogoro ya ardhi katika wilaya ya Kiteto.
   
  Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho Japhet Chafu alilishukuru Jeshi la Polisi kwa kuimarisha usalama kijijini hapo tangu kutokea kwa mauji ya wakulima na wafungaji ambapo alibainisha kuwa bila kuwepo wao hali ingekuwa mbaya zaidi kutokana na kutokuwepo na muafaka baina ya wakulima na wafugaji.
   
  “IGP hawa askari wako wasingekuwepo hapa usingekuta mtu lakini tunawashukuru sana hawa askari kwa kuwa hivi sasa hali ya usalama imerejea na hata shambani tumeanza kwenda” Alisema Bw.Chafu.
   
  IGP Ernest Mangu alitumia ziara hiyo kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Wakaguzi wa Tarafa pamoja na Askari Kata ili kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama.

  0 0

    KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII DKT.ADELHELM  JAMES MERU AKIFANYA MAKABIDHIANO YA OFISI  NA ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALISILI NA UTALII, BI. MAIMUNA  TARISHI YALIYOFANYIKA JANA JIONI TAREHE 17/11/2014  MPINGO HOUSE JIJINI DAR ES SALAAM.          

   Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Maimuna  Tarishi, akimkabidhi vitendea kazi  Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Adelhelm  James Meru, yaliyofanyika jana jioni tarehe 17/11/2014  Mpingo House Jijini Dar es salaam.
   Aliyekuwa Katibu Mkuu  wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Maimuna Tarishi,  akipeana mkono   mara  baada ya kumkabidhi vitendea kazi Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Dkt.Adelhelm 
  Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Adelhelm  James Meru,  Akiwa kwenye picha ya pamoja  na aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Maimuna  Tarishi, mara  baada ya kukabidhi  vitendea kazi  yaliyofanyika jana jioni tarehe 17/11/2014  Mpingo House Jijini Dar es salaam. Mwingine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Selestini Gesimba.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.

  Mulongo ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona maduka hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima moto na kusababisha hasara kwa wananchi.

  "Sitakubali kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao mko karibu na Ofisi za Chama Cha mapinduzi wilaya yalipo maduka haya"amesema Mulongo

  Chanzo cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao.
  Habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog
  Baadhi ya Mabaki ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET usiku wa kuamkia leo. 
  Bango la Soko hilo.
  Sehemu ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo


  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imetoa uamuzi katika kesi inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Hans Aingaya Macha (pichani) kuwa ana kesi ya kujibu.

  Uamuzi huo, umetolewa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Devotha Kisoka katika kesi inayomkabili mfanyabiashara huyo ya kugushi hati ya kiwanja cha Ramadhan Balenga chenye namba 183 kilichopo Kigogo, mkataba wa mauziano na hati ya uhamishaji miliki.

  Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Devotha alisema baada ya kupitia ushahidi wa awali wa upande wa mashitaka, mshitakiwa(Macha) una kesi ya kujibu na mahakama inakutaka uanze utetezi katika  kesi yako inayokukabili na dhamana yako inaendelea kama kawaida.

  Kutokana na hali hiyo, Hakimu Devotha aliiharisha kesi hiyo hadi Desemba Mosi na Mbili kwa upande wa mshitakiwa kuanza kutoa ushahidi wake, mahakamani hapo katika kesi hiyo inayoonekana kuvuta hisia kubwa za wananchi jijini Dar es Salaam.

  Kabla ya mahakama kutoa uamuzi huo, Wiki iliopia Hakimu Devotha alisikiliza ushahidi wa mwisho kutoka kwa upande wa mashitaka, ambaye alikuwa Mkuu wa Maabara ya Uchunguzi wa Hati wa Polisi, Mrakibu wa Polisi, Amaan Renatus Saad.

  Renatus alidai mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Devotha kuwa alipokea nyaraka kutoka kwa Ofisi ya Msajili wa Hati ikiomba ifanyiwe uchunguzi katika nyaraka za uhamishaji miliki kutoka kwa Balenga kwenda kwa Macha.

  "Nina uzoefu wa miaka zaidi 10, ambapo nimeupata sehemu mbalimbali ikiwemo Bostwana. Polisi ilipokea barua kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutaka kufanyiwa uchunguzi,''alidai.

  Renatus alidai baada ya kupokea barua, walifanya uchunguzi na kutoa taarifa kwa Wizara ya Ardhi kuwa saini walizochunguza hazikusaini na mtu mmoja, ambaye ni Balenga, hivyo zimegushiwa.

  Alidai uchunguzi wao, ulizingatia mambo mengi ikiwemo mgandamizo wa peni, spidi ya peni, hivyo aliiomba mahakama ipokee ushahidi wake kama kielelezo sahihi katika kesi hiyo na upande wa mashitaka unaoongozwa na Wakili wa serikali, Nassoro Katuga, alidai mahakamani hapo kuwa, wamefunga ushahidi na kutoa nafasi ya upande wa utetezi nao kutoa ushahidi wake.

  0 0

  waziri Nkamia akimkabidhi zawadi  mchezaji  wa  timu ya MTERA
  waziri Nkamia akiwa  na  mchezaji  bora wa  timu  ya mtera Bw.mzambia
  -
  Waziri Nkamia  akimkabidhi kombe  kepteni wa Home Boys

  Mashabiki  wakifuatulia  zoezi la zawadi
  Na MatukiodaimaBlog

  MTERA Shooting yaibuka mabingwa Lukuvi Cup 2014  kwa kata  ya Migoli jimbo la Isimani baada ya kuifunga timu  pinzani ya Home Boys kwa  jumla ya magoli 4-1 katika mchezo wa fainali  ulioshuhudiwa na mgeni rasmi naibu waziri wa habari ,vijana ,utamaduni na michezo Juma Nkamia.

  Mchezo  huo  uliochezwa  juzi katika uwanja wa Migoli Mtera uliokuwa  na upinzani  wa hali ya  juu kwa  timu  zote  kutokana na  kushindwa kuonyeshana  ubabe  dakika  90 za  mchezo kwa  timu hizo kutoka  sare ya goli 1-1  kabla ya  kumsaka mshindi kwa  mikwaju ya  penati ambayo  iliiwezesha  timu ya Mtera Shooting  kuigagadua (kuifunga) Home Boys kwa  jumla ya magoli  hayo 4-1 ambayo  yaliiwezesha  kutwaa kombe na kiteta cha pesa  taslim kiasi cha Tsh milioni 1 kutoka kwa  mbunge  wa  jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ambae ni  waziri wa nchi  ofisi  ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge.


  Kbala ya  dakika  90 za mchezo  kumalizika timu ya Mtera Shooting iliweza  kuwanyanyua mashabiki wake baada ya kujipatia goli la kwanza  dakika ya 86 kwa  mkwaju wa  penati goli lililowekwa  nyavuni na  Mtei Mlimbwa huku dakika ya  88  Frank Jackson aliweza  kuisawazishia timu yake ya  Home boys  goli  hilo hivyo timu hizo  kutoka uwanjani  dakika 90 kwa  bila mbabe  kujulikana.

  Hali  hiyo iliweza  kupelekea mashabiki  wa kila  timu na  wachezaji  kupigwa na butwaa ya nani  kutwaa kombe  hilo kabla ya mwamuzi  kutumia njia ya matuta kumpata  mshindi ambae  alitokana na ujuzi  wa  kugusa  nyavu  za mwenzake.

  Akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu, Naibu Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo, Juma Nkamia,ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, alisema kuwa vijana wengi Tanzania wanapenda michezo japo bado kuna tatizo kubwa kwa viongozi wa michezo hususani walimu wa timu kwa kutokuwa na mafunzo ya ualimu wa timu.

  Mapema  katibu  wa mbunge  Lukuvi ,Thom Malenga  alisema kuwa lengo la mbunge Lukuvi  kuanzisha mashindano hayo ni kuweza  kuhamasisha michezo katika  jimbo  hilo na kuwafanya  vijana  kuepukana na matumizi ya madawa ya  kulevya pamoja na mambo mengine ambayo yanaweza  kuwasababishia  kupata maambukizi ya VVU.

  Mbali na  hilo alisem akuwa  kupitia michezo  wananchi  wanakuwa pamoja na kuondokana na masuala ya itikadi  vya  vyama wakati  wa  kufanya  shughuli za kimaendeleo.

  Pia  alisema mbali ya mashindano hayo ya ngazi ya kata  pia ameanzisha mashindano ya ngazi ya tarafa  ambapo  bingwa atazawadiwa Power tilla kwa  ajili ya kuanzisha vikundi  vya uzalishaji mali katika tarafa.

  Waziri Nkamia akizungumza kabla ya kukabidhi  zawadi kwa  mshindi wa mashindano hayo  alisema kuwa uamuzi  uliofanywa na mbunge Lukuvi katika kuanzisha  michezo ni uamuzi wa kupongezwa kwani mbali ya kutekeleza ilani ya CCM katika  michezo bado amewawezesha vijana kupata  fursa ya kuonyesha vipaji vyao ili kupata nafasi ya kuchezea timu kubwa  zaidi .

  Hivyo alisema katika  mchezo huo kwa upande  wake amependezwa na kiwango cha mchezo cha mchezaji wa timu ya Mtera pia alisema  kuwa mbunge  Lukuvi ametenga zaidi ya Tsh milioni 30 kwa ajili ya mashindano ya soka katika  jimbo  hilo la Isimani na yeye kama waziri mwenye dhamana  ya michezo amependezwa  zaidi na jitihada  hizo

  " Mimi  katika  kuunga mkono  jitihada hizi za Lukuvi  nawaahidi kuwa  nitawasiliana na Lukuvi  ili  mabingwa wakacheze na timu yangu jimboni Kondoa mkoani Dodoma na mchezo mwingine  waje wacheze hapa Mtera hapo vipi ".

  Katika mashindano hayo NKamia alimkabidhi  mshindi wa kwanza kombe na fedha taslimu shilingi milioni 1 huku  mshindi wa pili akuikabidhiwa  kombe na shilingi 500,000,mshindi wa tatu akipewa Tsh  250,000 na mchezaji bora  kutoka timu ya Mtera akipewa Tsh 100,000
  Wachezaji  wa  timu ya Mtera wakiendelea  kuumiliki mpira katikafainali ya Lukuvi Cup kata  ya Migoli Mtera

  Mabingwa wa Lukuvi Cup timu ya Mtera  wakimiliki mpita
  Mchezaji wa  timu ya Home Boys akiwa chini baada ya mchezaji wa  timu ya Mtera kuupiga kichwa  mpira uliokuwa  ukigombewa
  Mashabiki  wakifuatilia  mchezo huo
  Naibu  waziri Nkamia  akiwa na makombe ya Lukuvi Cup
  Uwanja  ukiwa  umezungukwa na mashabiki kabla ya mchezo kuanza
  Shangwe  ya ushindi

  0 0

  Andrew Chale (kulia) akiteta jambo na 'Mwenyekiti' Mjengwa wa Mjengwa blog
  Andrew Chale (kulia) akiteta jambo na 'Mwenyekiti' Maggid Mjengwa wa Mjengwa Blog. ..

  Ni vya 'Who Is Andrew Chale', 'Nimnukuu Nani?' na ''Mimi ni Historia',

  Mwandishi wa Habari nchini Tanzania, Andrew Chale anayeandikia magazeti ya Tanzania Daima na Sayari yanayotolewa na kampuni ya Free Media ya jijini Dar es Salaam, ambaye pia mwandishi 'msaada' wa blog za habari mbalimbali za hapa nchini na nje ya Tanzania ameanza mchakato rasmi wa kuandika vitabu vitatu (3) vitakavyokuwa vikielezea juu ya Maisha yake.

  Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Novemba 19, Andrew Chale alibainisha juu ya kusudio hilo la kutoa Vitabu vya kuelezea Maisha yake ni ndoto aliyonayo kwa miaka mingi na kwa sasa imetimia.

  "Wengi watajiuliza sasa nimepata wapi ujasiri wa kufanya jambo hili kubwa la kuelezea Maisha yangu?.Ni rahisi sana, Unapokuwa na Mungu kila jambo linawezekana hivyo vitabu hivi vitakuwa ni muongozo kwa Vijana wote hapa Duniani kuelewa kuwa yale yote wanayopitia si ya kuyakatia tamaa, bali kuangalia wapi wataweza kujikomboa na hata kuendana na hali iliyopo kwa kujithamini, kujielewa, uvumilivu na kufikia malengo stahiki ya maisha" alifafanua Andrew Chale.

  Alivitaja vitabu hivyo kuwa ni: "Who Is Andrew Chale?" Sehemu ya Kwanza), 'Who Is Andrew Chale 2?"- 'Nimnukuu Nani?' (Sehemu ya Pili) na Kitabu cha mwisho kitakachojulikana kama "Mimi ni Historia".


  Akifafanua vitabu hivyo vya 'Who Is Andrew Chale' cha kwanza na kile cha pili cha 'Who Is Andrew Chale 2- 'Nimnukuu Nani?', alibainisha kuwa vitaelezea kwa kina Historia yake tokea kuzaliwa hadi alipofikia sasa huku cha Pili cha 'Who Is Andrew Chale 2-'Nimnukuu Nani' kikielezea yale mambo yote yaliyojificha nyuma ya pazia na ukakasi wa maisha aliyopambana nayo kutoka kwa walimwengu na mwishowe anauliza "Nimnukuu Nani?".
  10379994_679143752122499_6894615982670728862_o
  Aidha,kwa upande wa kitabu cha : "Mimi ni Historia" ameweza kuelezea ujumbe juu ya Vijana kutokata tamaa na baadala yake wasonge mbele kwa magumu yote waliyopitia, ikiwemo yeye.

  "Mimi ni Historia", mimi mwenyewe naogopa sana, kwanza kuanzia jina la Kitabu, Nakumbuka nilimuuliza Mama yangu Mzazi juu ya jambo fulani la kifamilia baina yake na Baba, lakini jibu alilonipa ndilo lililonifanya nishike neno hili 'Mimi ni Historia'. 

  Kikubwa kwenye kitabu hichi nitafafanua mambo mbalimbali ya kihistoria bila shaka hata atakayesoma ambaye alipitia mambo kama yangu naye itakuwa ni Historia" alimalizia Andrew Chale. Vitabu hivyo vyote vitajaa Historia ya kweli, itakayotoa mafunzo kwa kila mmoja atakayebahatika kuvisoma Pia vitakuwa ni kama mafunzo, mfano wa kuigwa, na kukuacha ki mdomo wazi na hata kububujikwa machozi.

  Aidha, Andrew Chale, aliomba ushirikiano kwa wadau kujitokeza kumsapoti ilikufanikisha juhudi za vitabu hivyo ikiwemo gharama za kuandaa Mswada, mapitio na uchapaji. "Kwa sasa nipo katika andalio la Simulizi, na lengo kuu nije nichapishe Mkuki na Nyota.Kwa sasa natafuta watu watakao kuwa msaada wa awali wa kufanikisha dhumuni langu hili Ikiwemo ushahuri, msaada wa kifedha, mchango wa kimawazo na mengineo. Tuwasiliane kupitia 0719076376 au 0767076376 au 0688076376 au chalefamily@yahoo.com" alimalizia Andrew Chale.

  Andrew Chale, ambaye kwa sasa anaishi Bagamoyo, Mkoani Pwani akifanya shughuli zake hizo za Uandishi wa Habari, Pia ni Mwanaharakati wa Haki za Watoto nchini, msanii wa masuala ya Vichekesho, Mtunzi wa filamu, maigizo na mshahuri kwenye matamasha ya sanaa na Muziki, mbali hayo pia ni Mjasiriamali katika Sanaa na Utamaduni ikiwemo kukuza Sanaa na Utamaduni kwa Mkoa wa Pwani.

  0 0

  kibonzo10 and 11 nov 2014

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Chuta ambapo aliwaambia kuwa maendeleo yanakuja kwa kufanya kazi na kujituma, ambapo aliwaambia kila nchi itaendelezwa na watu wake.

   Zahanati ya kijiji cha Litipu kata ya Nyangamara ikiwa katika hatua nzuri za ujenzi ambapo inategemewa kukamilika hivi karibuni.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja  na Mh.Bernard Membe Mbunge wa Jimbo la Mtama na ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri wa Mambo ya nje wakiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu wa Matawi wakati wa zoezi la kukabidhi baiskeli.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kukamua  maziwa katika shamba la mifugo Narunyu katika kijiji cha Kiwalala jimbo la Mtama.

   Kaatibu wa NEC Itiakdi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Chiuta ambapo aliwaambia Chiuta ni nyumbani na aliwataka watu wachukue tahadhari na vyama visivyo na sera wala dira.

   Wananchi wakisikiliza mkutano.

   Kila mtu alitaka kusikiliza na kuona.
   Sehemu ya watu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

  Mbunge wa Jimbo la Mchinga Ndugu Said Mtanda akiwahutubia wakazi wa Chiuta kwenye mkutano mkubwa wa hadhara ambao Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni wa heshima.

   Mbunge wa Jimbo la Mtama na ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri wa Mambo ya Nje Mh. Bernard Membe akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Chiuta.
   Watu walikuwa makini sana kusikiliza mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akimkabidhi baiskeli katibu wa Tawi la Nambau LIndi Vijijini.


   Wanachama wapya wakila kiapo
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma kiapo kwa wanachama wapya waliojiunga na CCM katika kijiji cha Chiuta.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akitoa maelezo ya namna CCM ilivyojipanga kutatua kero za wananchi Chiuta ambapo kero zao kubwa ni kutaka Mawaasiliano ya Simu,  na kituo cha afya.
   Sista Maria Mfariji Milanzi wa Msista wa Benedikti wa Bikira Maria Msaada wa Kristo Ndanda Narunyu Novisiati akisoma taarifa ya mradi wa shamba la mifugo Narunyu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alielezwa kuwa shamba hilo lilianza na Ng'ombe 50 na sasa wana Ng'ombe 450,shamaba hilo linasaidia kupatikana kwa maziwa ,nyama na umeme unaotokana na kinyesi cha wanyama yaani Biogas.
  Shamba hilo lililopo katika kijiji cha Kiwalala ,kata ya Kiwalala ,wilaya ya Lindi Vijijini
   Mbunge wa Jimbo la Mtama na ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM na Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa bernard Membe akizungumza na wakati wa Mkutano Mkuu wa Jimbo ulioanyika Kiwalala
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungmza kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo la Mtama.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubangua korosho kwenye mradi wa kikundi cha Wanawake  cha kubangua Korosho Nyengedi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kitabu cha utekelezaji wa ilani ya CCM Jimbo la Mtama wakati alipopita kuwasalimia wananchi.
   Mbunge wa Jimbo la Mtama na ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri wa Mambo ya nje Ndugu Bernard Membe akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyangamara.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Nyangamara
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba mtaro utakaolazwa bomba la maji katika mradi wa maji wa Nyangamara mjini.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga tenki la maji pamoja na Mbunge wa Jimbo la Mtama na ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM na Waziri wa Mambo ya Nje Mh. Bernard Membe katika kijiji cha Nyangamara.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akicheza ngoma pamoja na Mbunge wa Mchinga Ndugu Said Mtanda wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Chiuta.
   Sehemu ya wakazi wa Chiuta wakiwa wamejazana kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama Ndugu Abdulrahman Kinana
   Mbunge wa Jimbo la Mtama na ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM na Waziri wa Mambo ya Nje Mh. Bernard Membe akiwapa salamu wakazi wa Chiuta ambapo aliwaambia kwamba upinzani hautochukua jimbo lolote mkoani Lindi.
   Mwenyekiti wa CCM Mzee Ally Mtopa  akitoa salaam chache kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia wakazi wa Chiuta.

  0 0

  Photo Credits: Ye Olde Vivyl Shoppe
  Baada ya pilika za wiki nzima, na mchamchaka wa maisha, sasa unakuja wakati wa kuburudika na muziki halisi wa zamani. Katika kipindi hiki, utaweza "kuruka majoka" na "kula mangoma" kwa kusikiliza nyimbo ziliotamba miaka ya zamani, kupata historia ya wasanii na vikundi mbalimbali na pia kusikiliza mazungumzo na maDj na wasanii mbalimbali wa zamani.

  Ungana na MixMaster Dj Luke Joe kwenye "one and two" na Mubelwa Bandio nyuma ya kipaza sauti kwenye kipindi kipya cha MISHUMAA YA KALE kitakachokujia kila Ijumaa kuanzia saa 11 kamili jioni mpaka saa 1 kamili usiku kwa majira ya Marekani ya Mashariki (5:00pm - 7:00pm EST)
  Ungana nasi kupitia www.kwanzaproduction.com
  MixMaster DJ Luke Joe. Photo Credits: IskaJojo Studios
  Mubelwa Bandio  0 0
 • 11/19/14--00:56: FOREVER NUTRI-LEAN PROGRAMME
 • FOREVER NUTRI-LEAN PROGRAMME
  Has two step process, combining a 9-day cleansing plan followed by a long –term weight loss plan.
  1. Clean 9- Detoxify-leaves you clean, healthier, happy and helps you to loose between 3kg to 8kg. @ Tsh 265,000.
  2. Forever Nutri-Lean (Life style 30)- burns fats, loose weight between 10kg to 15kg & maintain your weight, leaves you with good eating habits.  @ Tsh 440,000.
  3. Body Toning Kit- Removes cellulites and fats deposits under the skin. Wrap the arms, thighs, stomach and loose up to 2 inches per Wrap. @ Tsh 145,000.
  Loose weight with FOREVER NUTRI-LEAN PROGRAMME and improve quality of your life (Sexual desire and performance, reduce possibilities of diabetes, Cancer and Sleep apnea).
  FOREVER NUTRI-LEAN PROGRAMME has No Drugs (Caffeine, Topiramate, sibutramine, xenical, phentermine, methamphetamine)

  How do you know one is overweight?
    By finding the Body mass Index (B.M.I.) i.e. a ratio of the weight over the height squared
         BMI  =      Weight  (kg)   
                Height (m) X Height (m)
  Less Than 18.9       =    Underweight
                   19 - 24.9 = Normal weight
                    25 - 30    =   Overweight
                Above 30   =   Obese
  Recommended Weight (kg) = Height (m)*Height (m)*24.9
  WEIGHT TO LOSE= YOUR WEIGHT- CALCULATED (Recommended) WEIGHT
  FOR MORE INFORMATION CALL   0769888605/0786139316
  We have just experienced an overall average Growth of 20% during the first quarter of the year…and we are in need of agents (part time or full time) to comply on the growing demand of health and wellness products in the region if you are interested contact usWe have just experienced an overall average Growth of 20% during the first quarter of the year…and we are in need of agents (part time or full time) to comply on the growing demand of health and wellness products in the region if you are interested contact us through

  0 0

   Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando akiwa kwenye kipindi cha maswali na majibu toka kwa Vivek Muthu pembeni yake na maswali mengine toka kwa wadau waliohudhuria kwenye mkutano wa Afya wa Afrika unaoendelea jijini Dar es Salaam.
   Mmoja ya wadau akiuliza swali kwa Katibu mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando.
   Wadau toka nchi mbalimbali duniani wakifuatilia kwa karibu yanayoendelea mkutanoni.
  Mkutano ukiendelea

  0 0

   Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa Amani alipohudhuria katika mkutano wa Mabalozi wa Mkoa wa Magharibi Unguja akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Mikoa ya Unguja,
    Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa Amani alipohudhuria katika mkutano wa Mabalozi wa Mkoa wa Magharibi Unguja akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Mikoa ya Unguja
   Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono Mabalozi waliofika kumpokea  alipowasili viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa Amani alipohudhuria katika mkutano wa Mabalozi wa Mkoa wa Magharibi Unguja akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Mikoa ya Unguja,
   Baadhi ya Mabalozi   wa CCM wa jimbo la Kwamtipura wakimsikiliza Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akihutubia Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Mkoa wa Magharibi Unguja katika ukumbi wa CCM MKoa Amani leo,
   Baadhi ya Mabalozi   wa CCM wa majimbo mbali mbali ya Mkoa wa Mgharibi wakiwa katika mkutano wa  Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Mkoa wa Magharibi Unguja katika ukumbi wa CCM MKoa Amani leo uliohutubiwa na Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,
   Baadhi ya Mabalozi   wa CCM wa majimbo mbali mbali ya Mkoa wa Mgharibi wakiwa katika mkutano wa  Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Mkoa wa Magharibi Unguja katika ukumbi wa CCM MKoa Amani leo uliohutubiwa na Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,
  Baadhi ya Mabalozi   wa CCM wa jimbo la Mpendae wakimsikiliza Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akihutubia Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Mkoa wa Magharibi Unguja katika ukumbi wa CCM MKoa Amani leo,

  0 0
 • 11/19/14--03:25: REMEMBRANCE
 • The Late Donat Samike Mashiku 1947-2013

  Baba, God saw you struggling and no cure in this world was there to make you stay, he then decided to call you that day of 20th November 2013. They were days, weeks, months and now a year without you. It is true that you are gone.

  Our hearts were hurt but we had no choice, we had to let you go. We miss your smile, your words, and many more that we cannot express .We continue praying for you papa, and on 20th Nov 2014,we will gather at your home Mapinga for remembrance of your great life teachings. 

  A holy mass will be held starting at 1500hrs onward followed by late lunch. Our friends and family please join us when commemorating the life of a beloved HUSBAND,DAD,BABU,UNCLE and a BROTHER.
  May your gorgeous soul continue to Rest In eternal Peace. Amen.

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa tatu kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yanayofanyika jijini humo. Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja(wa pili kutoka kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa MadiniTanzania, Richard Kasesera  (wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania  (TAMIDA) Sammy Mollel (wa pili kutoka kulia). 
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (kushoto) akihutubia wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake,  washiriki (exhibitors) na wanunuzi wa madini ya vito ambao wamehudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yanayofanyika jijini humo kuanzia tarehe 18 hadi 20 Novemba, 2014.
   Makamu wa Rais wa Shirikisho  la Wafanyabiashara wa Madini ya Vito na Usonara, nchini Thailand, Tony Brooks akionesha machapisho mbalimbali kuhusu madini ya Vito kwa mgeni rasmi wa maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa pili kutoka kushoto), wengine ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja(wa kwanza kutoka kushoto). Nchi ya Thailand ina uzoefu mkubwa katika uandaaji wa maonesho ya Vito ambapo wameshafanya maonesho zaidi ya 50 na wafanyabiashara wa madini ya Vito kutoka Tanzania wamekuwa wakishiriki Maonesho hayo.
   Wachimbaji wadogo wa madini ya vito kutoka ukanda wa Umba mkoani Tanga waliohudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha wakiwa kwenye banda wanalouzia madini hayo katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. Pamoja nao ni Afisa Madini Mkazi mkoa wa Tanga, Mjiolojia Elias Kayandabila (wa nne kutoka kushoto).
   Makamishna Wasaidizi wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini,wakifuatilia majadiliano uendelezaji endelevu wa madini ya Tanzanite nchini. Kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini-Leseni, John Nayopa, Kamishna Msadizi wa Madini-Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane, na Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim.
   Watendaji kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bruno Mteta, (wa pili kutoka kulia), Meneja Mipango na Utafiti, Julius Moshi (wa kwanza kulia), na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari, Eng. Yisambi Shiwa (wa tatu kutoka kushoto) waliohudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito Arusha, wakisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Eng. Edwin Ngonyani (wa kwanza kushoto) aliyetembelea banda la Wakala huo katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
   Washiriki kutoka nchini Rwanda wakiwa na mgeni rasmi wa maonesho hayo ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa pili kutoka kulia), wengine ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja(wa tatu kutoka kulia mstari wa mbele),Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini Tanzania, Richard Kasesera  (wa nne kutoka kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania  (TAMIDA) Sammy Mollel, (wa nne kutoka kulia_mstari wa mbele).
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava, (wa kwanza kulia) akizungumza na mfanyabiashara wa madini nchini, Peter Pereirra mara alipotembelea banda la mfanyabiashara huyo katika Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha. Kulia kwa Naibu Katibu Mkuu ni Kamishna wa Madini nchini, Eng. Paul Masanja.

older | 1 | .... | 408 | 409 | (Page 410) | 411 | 412 | .... | 1898 | newer