Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 39 | 40 | (Page 41) | 42 | 43 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi alikikagua na baadae kukikabidhi Kisima cha maji kwa ajili ya matumizi ya wananchi wa Kijiji cha Boma kiliomo ndani ya Jimbo la Kitope. Picha na Hassan Issa – OMPR - ZNZ
   Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akifurahia moja ya darasa la Jengo la Skuli Mpya ya Matetema ambayo tayari wanafunzi wa Kijiji hicho wameanza kulisomea kwa karibu wiki moja sasa.
  Mjumbe wa Kamat Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi vifaa vya ujenzi Mwenyekiti wa CCM Tawi la Boma Ndugu Bakuda Edwanr kwa ajili ya uendelezaji ujenzi wa Tawi hilo.  Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wameaswa kuwa na tahadhari na cheche zinazoanza kupandwa miongoni mwa Jamii za kuichezea amani unaoonekana kufanywa na baadhi ya watu kwa kuendeleza tabia ya  kuhujumu baadhi ya Viongozi wa Dini hapa Nchini.
  Tahadhari  hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi  wakati akizungumza na wana CCM  katika ziara yake ya kukagua harakati za utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho ndani ya Jimbo la Kitope liliomo katika Wilaya ya Kaskazini “ B ”.
  Balozi Seif akiwa pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mbunge wa Jimbo la Kitope alisema matukio ya hivi karibuni ya hujuma zilizopelekea mauaji na majeruhi dhidi ya Viongozi wa Dini zinapaswa kukemewa na wana CCM hao pamoja na Wananchi wote kwa ujumla.
  “ Licha ya cheche  hizi za matukio ya hujuma yaliyoelekezwa Zanzibar hivi sasa lakini bado Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuhubiri amani na Utulivu kama ilani yake inavyoelekeza”. Alisisitiza Balozi Seif.
  Alifahamisha kwamba wanachama wa chama cha Mapinduzi lazima waendelee kujiepusha na ushawishi huo unaopenyezwa kwa kisingizio cha Dini ambao ni hatari  miongoni mwa Jamii Nchini.
  Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM  aliwapongeza Wanachama na Viongozi wa CCM wa Matawi ya Kitope A, Muembe Majogoo na Boma kwa jitihada zao zilizopelekea kujenga matawi yao mapya kwa kushirikiana na Viongozi wao.
  Alisema inafurahisha kuona zaidi ya asilimia Tisini na Tano ya Matawi yaliyomo ndani ya Jimbo la Kitope yameshajengwa katika kiwango kinachokubaliwa ambacho kinakwenda sambamba na hadhi ya Chama chenyewe.
  Aliwaagiza Viongozi na Wana chama wa Matawi yanayoendelea kujengwa ambayo tayari ameshayapatia Vifaa vya ujenzi kuhakikisha wanakamilisha  kazi hiyo kwa wakati ili ifikapo mwaka 2015 mikutano yote ya wanachama katika kupanga safu ya Uchaguzi inafanyika ndani ya Ofisi zao mpya.
  Katika ziara hiyo Balozi Seif pia alipata fursa ya kuangalia jengo jipya la Skuli ya Matetema ambalo tayari wanafunzi wa Kijiji hicho wameanza kulitumia rasmi kwa karibu wiki ya tatu sasa kuendelea na masomo yao.
  Aliuagiza Uongozi wa Kijiji hicho kuanzisha Kamati ya  Skuli itakayosimamia changamoto zinazowakabili ikiwemo ongezeko kubwa la idadi ya watoto Kijijini hapo.
  “ Utaratibu uliopo sasa katika maeneo yetu Wananchi huanzisha  miradi yao ya maendeleo na baadae kuungwa mkono ya Serikali pamoja na Washirika wa Maendeleo. Sasa anzeni jengo jengine ili kukabiliana na changamoto zilizokuzunguukeni na mimi pamoja na Wizara husika tutajaribu kusaidia kutafuta mbinu za kuunga mkono juhudi zenu mlizoanzisha”. Alisisitiza Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope.
   Balozi Seif halkadhalika alikikagua Kituo cha Afya cha Kitope na kutoridhika na hali ya kimazingira na kuwakumbusha watendaji wake kuzingatia usafi wa mazingira yanayokizunguuka Kituo hicho . Katika ziara hiyo Balozi Seif akakabidhi Kisima cha Maji kwa ajili ya matumizi ya Wananchi wa Kijiji cha Boma.
  Akizungumza na Wananchi hao Balozi Seif alisema pamoja na hitilafu ndogo ndogo zilizojitokeza  za uhaba wa maji katika Kisima hicho aliagiza kupatiwa makisio halisi ili kutafuta uwezeshaji utakaosaidia kuliondosha tatizo hilo.
  Katika kuunga mkono juhudi za Wanachama hao wa CCM Balozi Seif alichangia matofali 1000, Saruji mifuko 10, Mchanga na shilingi 100,000/- za Fundi kwa kuendeleza ujenzi wa Tawi la CCM Boma pamoja na shilingi  Laki 220,000/- kwa ajili ya ununuzi wa madirisha ya Tawi la CCM Muembe Majogoo.

  0 0

  1
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris Bi Scholastica Ponera akikabidhi vifaa vya ngoma za asili kwa Ismail Edward Mkuu wa shule ya Sekondari ya St. Antony Mbagala jijini Dar es salaam hivi karibuni, huo ni msaada aliouahidi kwa shule hiyo baada ya kuonekana kuna uhaba wa vifaa vya muziki wa asili shuleni hapo, wanaoshuhudia tukio la makabidhiano hayo katika picha katikati ni walimu Venance Njiku na Bi. Nickyza Bwenge, vifaa hivyo ndivyo vilivyotumiwa na kikundi cha ngoma za asili cha shule hiyo wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo yakishirikisha wazazi, wageni waalikwa mbalimbali , Bodi ya shule pamoja na uongozi wa wanafunzi wa shule hiyo.
  10
  Mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa akiwa katika picha ya pamja na Uongozi wa shule hiyo.

  2Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris Bi Scholastica Ponera akiwa na Ismail Edward Mkuu wa shule ya Sekondari ya St. Antony Mbagala jijini Dar es salaam wakiwa pamoja na baadhi ya wanafunzi mara baada ya kupokea vifaa hivyo.
  4Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris Bi Scholastica Ponera akizungumza na wanafunzi hao mara baada ya kuwatembelea katika mazoezi yao shuleni hapo na kukabidhi vifaa hivyo.
  5Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris Bi Scholastica Ponera akicheza pamoja na kikundi hicho wakati kikiwa katika mazoezi yake shuleni hapo.
  6
  Meshack Mahembe mwalimu wa kikundi hicho akifanya mazoezi pamoja na wanafunzi hao.
  7Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Pongo Safaris Bi Scholastica Ponera, Mkuu wa shule hiyo Ismail Edward kulia na na Meshack Mahembe mwalimu wa kikundi hicho wakiwa katika picha ya pamoja.
  8
  Kikundi cha Ngoma za asili shule ya Sekondari ya St. Antony Mbagala jijini Dar es salaam wakicheza ngoma wakati wa mahafali ya kidato cha Nne yaliyofanyika shuleni hao hivi karibuni.
  9
  Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo akizungumza na wanafunzi na wageni mbalimbali katika mahafali hayo.

  0 0

  Mgeni Rasmi Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akisoma hotuba fupi mbele ya wageni mbalimbali waliohudhuria kwenye hafla ya wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions Blog,iliofayika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni mwelekeo wa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimisha Machi 8 Duniani kote.
   Mke wa waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akisalimiana na mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda kwenye hafla ya Women's Celebration 2013 iliofanyika leo jijini Dar.
  Mwandaaji wa hafla ya Women's Celebration 2013 kutoka kampuni ya 8020 Fashions Blog, Shamim Mwasha akipongezwa na Mgeni Rasmi Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda kwa kazi nzuri alioifanya ya kufanikiwa kuwakusanya wanawake wenzake na kujadili mambo mbalimbali yakiwemo ya kifamilia na maendeleo kwa ujumla,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuelekea kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa Machi 8 Duniani kote.
   Mwanamuziki mwimbaji mahiri wa miondoko ya taarab,Khadija Kopa akitumbuiza mbele ya wageni waliohudhuria hafla ya  wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions Blog,iliofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.
   
   Mke wa waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (pichani katikati) akijimwaya mwaya pamoja na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
   Naibu Waziri wa Sheria na katiba,Mh. Angellah Kairuki akiwa sambamba na Mke wa waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
  Mmoja wa washiriki wa hafla hiyo akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa.
   
  Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wakifutailia mambo yaliyokuwwa yakijiri ukumbini humo.

  0 0

   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve
  Kilindo (katikati), akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Ibrahim Msengi  msaada wa magodoro kwa ajili ya Hosptali ya Huruma ya wilayani Rombo pamoja na Kituo cha Afya cha Uru Kiaseni katika hafla iliyofanyika Mjini Moshi. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dk. Mtumwa Mwako. Jumla ya magodoro 210 na vyandarua 200 vimetolewa na TBL kwa ajili ya kituo hicho na hospitali hiyo. 
   Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Ibrahim Msengi akikabidhi msaada wa magodoro kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Mtumwa Mwako baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), mjini Moshi . Katikati ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo. Jumla ya magodoro 210 na vyandarua 200 vimlitolewa na TBL kwa ajili ya kituo Afya cha Uru Kiaseni na Hosptali ya Uhuruma .


   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL, Steve Kilindo,(katikati)wakifurahia jambo na kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Ibrahm Msengi (Kulia )pamoja na mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dk Mtumwa Mwako mara baada yaTBL  kukabidhi msaada wa magodoro 210 na vyandarua 200 kwa kituo cha Afya cha Uru Kiaseni na hosptali ya Uhuruma .


  Mganga wa kituo cha Afya cha Rau Kiaseni  Dk. Delfina
  Materu(katikati)akizungumza na wanahabari (hawako pichani)mara baada
  ya kupokea msaada wa Magodoro kutoka kampuni ya bia Tanzania(TBL)shoto
  kwake ni Meneja mauzo wa TBL mkoa wa Kilimanjaro Leiya Hermenegild.

  WADHAMINI wakuu wa mbio za Kilimanjaro Marathon, kampuni ya Bia ya TBL, imekabidhi  msaada wa magodoro na vyandarua kwa uongozi wa hosptali ya Huruma na kituo cha Afya cha Uru Kiaseni kama  sehemu yamaandalizi ya mbio za Kilimanjaro marathon zinatarajia kufanyika leo machi 3.

  Misaada ya aina hiyo hufanywa kila mwaka na TBL wakati wa  maandalizi ya Mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo hufanyika kila mwaka ikiwa ni utaratibu wa kampuni hiyo kurudisha faida iliyopatikana kwa wananchi kutokana na utumiaji wa bidhaa zake.

  Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo, alisema kuwa TBL imeamua kufanyautaratibu huo ambao wamekuwa wakifanya kila mwaka na mwaka huu wameonelea ni vyema wakatoa msaada katika hospitali hizo.

  Kilindo alisema kuwa msaada wa magodoro hayo 210 na vyandarua 200 ni
  jitihada za kampuni hiyo kuhakikisa jamii  ya Tanzania inafurahi na
  kujivunia kilicho chao na kuongeza kuwa hicho wal;ichokitoa ni sehemu
  ya shukuruni kwa watanzania ambao wamekuwa wakiwaunga mkono kila mara.

  “Kama wadhamini wakuu wa mbio hizi, tumekuwa tukishiriki katika shughuli nyingi za kijamii na moja yao ni kutoa msaada katika mahospitali, leo tunatoa magodoro 210 na vyandarua 200 kwa hospitali za Kiaseni ya Rau na Huruma ya Rombo, tunaamini katika hili tutakuwa
  tuimesaidia kwa kiasi fulani,” alisema Kilindi

   Naye Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Ibrahimu Msengi akipokea
  msaada huo kwa niaba ya uongozi wa hospitali hizo aliipongeza TBL kwa
  kuamua kuijali jamii inayonunua na kutumia bidhaa zao na kuongeza kuwa
  msaada huo anaamini utakuwa wa manufaa makubwa kwa wagonjwa katika
  hospitali hizo.

  “Moyo wa kutoa sio lazima uwe nacho, TBL wameonesha kuwa kazi yao sio kutengeneza bia tu, bali wanaweza kujali jamii na katika hili nawapongeza sana na ningependa mashirika na makampuni mengine nayoyangekuwa yanafanya hivi,” alisema Msengi.

  Msengi alitoa wito kwa wafanyabiashara wote na wamiliki wa makampuni kuiga mfano mzuri ulioonesha na TBl na kusisitiza umuhimu wa kutoa kwani jukumu la kuhudumia jamii ni la kila mtu na sio serikali pekee.

  Kuhusu mbio za mwaka huu za Kilimanjaro marathon Dkt. Msengi alisema,mbio hizo kufanyika katika ardhi ya Kilimanjaro ni fahari na kuongeza kuwa matarajio ya wote ni kuona kila mtu akinufaika na mbio hizo huku
  akiwatakia kila kheri wakimbiaji wote hasa wakimbiaji wa Tanzania.

  “Nitumie Fursa hii kuwatakia kila la Kheri wakimbiaji wote wa Kilimanjaro marathon, kila la kheri watanzania wote watakaotuwakilisha keshokutwa naamini tutashinda,” alisema.

  Kwa upande wake Mganga mnku wa mkoa wa Kilimanjaro (RMO), Dk. Mtumwa
  Mwako, akipokea magodoro na vyandarua hivyo kutoka kwa kaimu mkuu wa
  mkoa kwa niaba ya uongozi wa Hospitali za Kiaseni na Huruma, alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kwa mama na mtoto.

  Nao madaktari kutoka katika hospitali hizo, Dkt. Godwin Kiwelu wa hospitali ya Huruma ya Rombo na Dk. Delfina Materu wa hospitali ya Kiaseni ya Rau, walisema kwa msaada huo mzigo wa changamoto zinazokabili hospitali hizo zimepungua huku wakisisitiza kuwa bad kuna changamoto nyngi ambazo inatakiwa jamii inatakiwa kujitokeza kusaidia kama walivyofanya TBL.


  0 0

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akiwa hutubia Wananchi wa Wilaya ya Kinondoni Wakati Sherehe za Kuadhimisha Siku ya Mazingira Barani Afrika Sherehe hizo  zmefanyika kenye Viwanja vya Tanganyika  Packere huko Kawa Jijini Dar es Salaam
   Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Wakifanya Usafi Kuadhimisha siku ya Mazingira Barani Afrika kwenye Viwanja vya  Tanganyika Packers kawe Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam[Picha na Ali Meja]
   Mawaziri wa Nchi  Katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan na Wamazingira  Dk Terezya Huvisa,Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Chalrs Kitwanga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Sar es Salaam Said Meek Sadiki wakifanya Usafi Kandokando Mwabarabara ya kawe Wakati wa Kuadhimisha Siku ya Mazingira Barani Afrika Sherehe hizo zimefanyika kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meek Sadiki akifanya Ufasi  Wajiji katika Barabara ya Kawe kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Wakati wa Kuadhimisha Siku ya Mazingira Barani Afrika Kulia Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Julias Ningu. 

  0 0  0 0

  KENYA ELECTIONS: At the threshold of elections in Kenya, we hope and pray that elections will be conducted in peace and dignity. The success of this election has far reaching effects on the integration of EAC. As EALA MP, i wish our Partner State all the best!!

  0 0


  President to the Institution of Engineers Tanzania (IET), Eng Dr Malima Bundara speaks duringengineers’ public meeting held at the weekend in Dar es Salaam. From his immediate right are former IET president Eng Ladislaus Salema, followed by IET Treasure Eng Rizwan Qadri and Secretary to the institute Eng Swaleh Kassera. Photo by correspondent.
  ========  =======  =========
  TANZANIA’S economic growth hangs in balance if Government does not take stern measures to build capacity for local engineers, the Institution of Engineers Tanzania (IET) has warned.

  The warning was made by a cross-section of engineers who attended the engineers’ public meeting on re-engineering IET and role of engineers in Tanzania’s current challenges as far asemployment, education, abuse of engineering profession and natural resources are concern. Speaking during the event, the IET President Eng. Dr. Malima Bundara said the challenges facing the country’s engineering sector will only be solved with engagement of local engineers.

  “The engineering sector is facing many challenges but such challenges will only be solved if local engineers are incorporated in the problem solving equation. “We should not deceive ourselves that foreign engineers will find lasting solutions to our problems. They come to make money and take it back with them. The only thing to do is build capacity of our local engineers,” he said.

  Bundara cautioned the Government against neglecting local engineers in trying to look for solutions to the current and looming development setbacks facing the country. And engineers on the other hand should abstain from complaining without taking pro active direction in the improvement of the national economy.
  “The backbone of every country’s economic growth is pegged on availability of a strong and well elaborate infrastructure. Infrastructural development and industrial growth lie in the hands of engineers. 

  If the Government and its institutions make good use of competent local engineers, a quick transformation on the country’s economic landscape will be felt,” said Eng. Bundara. He mentioned that IET is embarking on building capacity for local  engineers phase 2 so as to be enable them give professional solutions to issues associated to their professional fields, which also have direct effect to the country’s economy.

  Eng. Ladislaus Salema, former IET President, wondered why a country like Tanzania endowed with abundant minerals and natural resources in varying intensities, is still struggling to create jobs and is ranked among the developing countries. He wanted the Government to work closely with local engineers in unlocking unemployment challenges in the country.

  Eng. Shabbir Khataw (IET member) on the other hand warned his fellow engineers against laziness, saying that some of graduated University engineers like to sit in offices instead ofpractising to gain skills, a habit that he said would not give them room to improve on their expertise.   Similarly, IET has expressed concern over this year’s massive form four failures and that these results will have a direct impact on the universities output in general within a few years to come.

  The engineers pointed out that the poor results will greatly affect the number of students going for higher education as the poor exams results will create a vacuum that will greatly affected growth in all sectors. It was also remarked that selfishness among Tanzanians was undermining collaborative initiatives.

  0 0

  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa kiroho nchini, Upendo Nkone ni miongoni mwa wasanii wa ndani watakaopamba Tamasha la Pasaka Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

  Upendo anakuwa msanii wa tatu wa ndani kutangazwa atashiriki katika tamasha hilo baada ya Rose Muhando na John Lissu ambao walitangazwa Ijumaa na Jumamosi.

  Akizungumza Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema mwaka huu katika tamasha hilo wanawapa mashabiki kile wanachokitaka. “Tunaendesha maoni kwa mashabiki wetu wapendekeze wasanii gani wawepo, hivyo hao watatu ndiyo mpaka sasa wameshika nafasi za juu kwa kupendekezwa sana na mashabiki. Wengine tutawatangaza kadri mambo yatakavyokuwa mazuri na pia tukiwa tumezungumza nao juu ya ushiriki wao, ” alisema Msama.

  Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31, kisha siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, Aprili 3 itakuwa Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri Dodoma na Aprili 7 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

  Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

  0 0


    Millen Magese akikabidhi hundi ya milioni kumi na tano kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Mhe. Wilman Ndile; kulia ni Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hasnain Murji
    Millen Magese akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa mkuu wa wilaya Mtwara kabla ya kuanza ziara ya kutembelea mashuleni. 
  Millen Magese akiongea kabla ya kukabidhi mchango wake wa milioni kumi na tano kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa na madawati.
   Millen magese akiongea na wanafunzi na walimu wakati wa ziara yake mashuleni.

  ===  =====  ======  =====
  MWANAMITINDO mahiri wa kimataifa ambae pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2001, Millen Happiness Magese amewagusa wakazi wa Mtwara kufuatia ziara yake ya kimafanikio aliyoifanya mkoani humo na kukabidhi misaada mbalimbali.
  Millen ambae kwa sasa anaishi nchini Marekani akijishughulisha na fani ya mitindo akiwa Mtwara alipokelewa na viongozi mbalimbali wakiwamo Mkuu wa Wilaya ya Mtwara; Mhe. Willman Ndile, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara; Mhe. Simbakali na Mbunge wa Mtwara mjini; Mhe. Hasnain Murji.
  Millen alitoa fedha taslim kiasi cha shilingi milioni 15 ambapo milioni 10 ilikuwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi ya Mjimwema baada ya kutembelea shule hiyo na kuguswa na hali ya mazingira magumu aliyoyakuta katika shule hiyo iliyopo kata ya Magengeni.
  Millen awali alikuwa ametaka kupeleka msaada wake huo katika shule ya msingi ya LiLilungu iliyopo Mtwara mjini lakini alijikuta akimwaga milioni kumi kwa shule ya Mjimwema na kuongeza milioni tano kwa ajili ya madawati ya shule ya Lililungu kwani awali alikuwa ameahidi kutoa milioni kumi.
  Shule hiyo yenye madarasa mawili yaliyojengwa kwa udongo ambapo wanafunzi wakiwa ni wengi huku wengi wao wakiwa hawana viatu na sare zao za shule zikiwa zimechakaa.
  Akizungumza shuleni hapo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Ndile, Millen alisema kuwa akiwa kama mwanamitindo ameguswa na hali mbaya ya mazingira ya shuleni hapo hasa ikizingatiwa kuwa wanafunzi wanasomea katika shule ya udongo huku wakiwa na mazingira duni ya kufundishia.
   Aliongeza na kusema, "Mwaka 2001/2002 nilitembelea mkoa wa mtwara ambao ulinigusa sana kwenye swala zima la elimu haswa mazingira ambayo yanamfanya mtoto akae chini. Na nikaahidi siku moja mungu akijalia nitarudi Mtwara na nimesikitika ni miaka 12 sasa bado watoto wanakaa chini nikaone nirudi kutimiza ahadi na kutoa hamasa kwenye swala hili la elimu Mkoani mtwara”; mbali na milioni kumi na tano pia aliahidi kuwatafutia sare za shule wanafunzi hao jozi mbili kila mmoja na pia alikubali kuwa mlezi wa shule hiyo.
  Pia alipata fursa ya kukaa na wajasiriamali walioandaliwa semina na mkuu wa wilaya pamoja na mbunge wa Mtwara mjini kujadili mbinu za kuwaongezea kipato na kwa kuanzania milioni sita iliyopatikana iligawanywa kwa wajasiriamali kulingana na vikundi ili wao watengeneze madawati kwa ajili ya watoto wao, ambapo milioni tano ilitolewa na Millen Foundation na milioni moja ilitolewa na Mhe. Murji
  Naye mkurugenzi wa manispaa alisema Millen ameweka historia kwani kitu hiki hakijawahi kufanyika Mtwara na mtu binafsi wanaangalia ni jinsi gani Millen Magese atakumbukwa kama muanzilishi wa ujenzi wa shule ya mji mwema.

  Baada ya kuzungumzia ahadi yake hiyo Millen aliwahamasisha wadau wengine aliiongozana nao kuchangia mchango wa shule hiyo akiwamo Mbunge wa Mtwara mjini Murji ambae aliahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kufanikisha ujenzi zaidi wa shule hiyo na shilingi milioni moja kwa ajili ya madawati.
  Naye Mkuu wa Wilaya ya Mtwara; Mhe Ndile pamoja na Mhe. Murji waliwataka wananchi kuhamasika zaidi kwa kuunga mkono harakati za Millen katika kuimarisha elimu mkoani humo kwa kuwa ameonesha mfano mzuri akiwa kama mwanamitindo.

  0 0  0 0

  The Alliance Life Assurance Ltd Assistant General Manager George Nyakundi (right) hands over a dummy cheque to the outgoing Precision Air Services Group Managing Director and Chief Executive Officer Alfonce Kioko (left) meant for payment of an insurance claim for an employee of Precision Air Services who died while in employment. Alliance Life Assurance Ltd has insured employees of Precision Air Services and a claim is paid in case of death of an employee

  0 0


  Usiku wa Epiq Night ndani ya Maisha Club utakuwa ni usiku wa kukumbukwa kwa wapenda burudani wengi hasa baada ya wasanii walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search kutoa burudani ya aina yake.
  Katika usiku huo ambao ukumbi wa Maisha ulikuwa umejaza wapenda burudani na wadau mbalimbali wa muziki, ulishuhudia vijana hao wakiimba kwa mara ya kwanza mbele ya wakazi wa Dar es Salaam tokea walipoimba mara ya mwisho wakati wa fainali za EBSS pale Diamond Jubilee. Wasanii hao wakiwa bado wana moto kutokea burudani waliyoitoa Dodoma wiki mbili zilizopita, walifanya mashabiki waliojazana Maisha kushidwa kukaa na kushangilia wakati wote. Burudani hiyo ilifunguliwa na mkali wa Bongo fleva Rich Mavoko, akifuatiwa na kijana kutoka BSS, Vincent aliyeimba wimbo wake wa INYE NA IWE.

  Ufunguzi huo, ambao ulifanya ukumbi mzima kupiga mayowe, ulizidi kupamba moto baada ya kijana toka Dodoma, Godfrey Levis alipopanda na kibao chake cha MAYA. Shangwe zilizidi pale malkia kutoka THT, Linah alipopanda jukwaani kuimba nyimbo zake kali kama Oliva Twist na Nshafahamu kabla ya kumkaribisha jukwaani, dada mwenye sauti kali, Nsami kuimba wimbo wake wa MUONGO.

  Ilibidi nguvu ya ziada itumike kuwadhibiti mashabiki pale alipopanda dada wa Taarab, Husna, ambapo uchezaji wake na kumiliki jukwaa kuliwafanya mashabiki kutaka kupanda jukwaani kumtuza wakati akiimba wimbo wake unaofanya vizuri, NAWAMIMINA. Huku mashabiki wakizidi kushangilia kwa nguvu, dada mwingine aliyejizolea umaarufu kwa kuimba nyimbo za kiutamaduni, Nshoma, akapanda kuimba wimbo wake wa ‘MAMA AFRIKA’ ambapo uliwakonga mashabiki kwa midundo yake.

  Kama hiyo haitoshi, mashabiki walizidi kushangilia pale mwimbaji bora wa kiume, Barnaba alipopanda kuimba nyimbo zake za Sorry na Magube gube. Ilikuwa burudani baada ya burudani baada ya Barnaba kumkaribisha jukwaani mwanadada mwingine anayefanya vizuri na wimbo wake wa DREAM TONIGHT, Menina ambaye aliufanya ukumbi kumshangilia kwa uwezo wake mkubwa wa kutawala jukwaa.

  Alikuwa ni Norman, aka we mbaya, aliyefanya mashabiki kujazana stejini alipopanda kuimba wimbo wake wa ‘SI WEWE’. Norman ambaye kutolewa kwake kwenye EBSS kuliwasikitisha wengi, alifanya show ambayo wengi walizidi kuamini kwamba alistahili kufika mbali. Hadi wakati mshindi wa tatu wa shindano la EBSS, Wababa Mtuka anapanda jukwaani kuimba kibao chake cha ‘My Wife’ na Kitorondo mashabiki walikuwa bado wakishangilia namna alivoonyesha uwezo katika kuimba na kucheza.

  Wa mwisho kabla ya mshindi wa milioni hamsini kupanda alikuwa ni mkali wa RNB Tanzania, na mshindi wa tuzo za kili, Ben Paul, ambaye aliwakonga nyoyo mashabiki wake kwa nyimbo zake kali kama Pete na Samboira kabla ya kumkaribisha jukwaani Walter. Mashabiki hao waliokuwa wakimsubiri kwa hamu, walianza kupiga kelele Walter Walter, kabla ya kuwatuliza kwa kuimba wimbo wake mpya wa ‘Siachi’ akifuatiwa wimbo wake mwingine wa ‘Mamy Love’ pamoja na ‘RINGA’.

  Walter alipata wakati mgumu jukwaani ambapo mashabiki walimuomba azirudie nyimbo zake zaidi ya mara tatu hali iliyoonyesha kukubalika kwa hali ya juu. Mashabiki wengi wakizungumza baada ya burudani hiyo walionyesha kuwakubali vilivyo wasanii wa EBSS, huku wakiwatabiria makubwa. 

  ‘Hakika vijana wana vipaji na wanajua hasa kutoa burudani, wakipewa sapoti watafika mbali sana’ alisema Jumanne Sally mmoja wa mashabiki aliyehudhuria burudani hiyo. Ziara hiyo ya washindi wa Epiq BSS inaelekea Mtwara baada ya wiki mbili. 

  0 0


   The Exim Bank Assistant Marketing Manager Anita Goshashy addresses guests during the the 2013 Women celebrations sponsored by Exim Bank at the weekend
   The Exim Bank Assistant Marketing Manager Anita Goshashy (right) handover Exim Bank - Tumaini account details to the wife of the Prime Minister Mama Tunu Pinda (left) during the 2013 Women celebrations sponsored by Exim Bank at the weekend. 
   The Exim Bank Assistant Marketing Manager Anita Goshashy (right) poses for a photo with the wife of the Prime Minister Mama Tunu Pinda during the 2013 Women celebrations organized by 8020 Fashions and sponsored by Exim Bank at the weekend
   The Exim Bank Sales Executive Vivian Humphrey (right) explains a point to a prospective customer during the 2013 Women celebrations sponsored by Exim Bank at the weekend. 
  A cross-section of Exim Bank representatives during the 2013 Women celebrations sponsored by Exim Bank at the weekend
  ========  ============  =============
  Exim Bank pledges more support to women empowerment
  By Staff Reporter

  EXIM Bank Tanzania has pledged its continued support for women empowerment in a various parts of the country in a bid to support long-term economic growth. Speaking during the Women Celebrations 2013 in Dar es Salaam sponsored by Exim Bank at the weekend, the Exim Bank Assistant Marketing Manager Anita Goshashy said her bank has got tailor-made banking products specifically designed to cater for women.

  Goshashy said economic empowerment of women helps to enhance their contribution to the growth of the country’s economy urging that increased opportunities for women leads to better outcomes for families, societies and the country at large. “Economic empowerment of women is crucial if the country is to achieve sustainable economic development. Exim Bank has got tailor-made banking products specifically designed to cater for women empowerment,” Goshasy said.

  Goshashy said the bank had until December last year spent over 21 bn/- to support women through its Women Entrepreneurs Financing Programme (WEF).  “We chose to empower women because we believe women have a role to play in the country’s economic development. “If a woman is economically empowered, the nation is assured of healthy households which would contribute to the socio-economic development processes.” she added. She said the bank has also empowered women engaging in small and medium enterprises with basic skills on creating sustainable and profit making businesses.

  Earlier, the Prime Minister’s Wife Mama Tunu Pinda who officiated as Guest of Honor for the event challenged women to invest in agriculture since the sector has ready market. “Women should invest in agriculture because market for agricultural products is always there. Time to invest is now. Don’t wait until you retire. Invest now,” she said.

  0 0

  Mshindi wa Tigo Smartcard promotion Bw.Julius Raphael Kanza akiwa uwanja wa Santiago bernabeu akishuhudia mechi kati ya Real Madrid na Fc Barcelona juzi ambapo Madrid walishinda 2-1.

  0 0


   Prof Muhongo akiongea na Watanzania, kulia Balozi P Kallaghe © 2013 Urban Pulse Creative
    Balozi Kallaghe akimkaribisha Waziri kuongea na Watz UK
    Andy Mkwavi akiuliza swal
   Evans Mela akiuliza swali
   Ellly Njau-Benichou aliyeuliza swali kuh gesi na elimu

  Kadamnasi ikimsikiliza Waziri

  ========= =====   ========  ========
  WAZIRI ALIPOZUNGUMZA  NA WATANZANIA KWA  SAA NNE LONDON...
  -Imeandikwa na Freddy Macha
  -Picha za Urban Pulse 

  Wapo waliokuja  kuuliza maswali.  Au waliotaka tu kufahamishwa.  Wapo waliojaribu kumbana  Waziri wakijibishana naye masuala ya kisiasa. Wote walipewa nafasi katika hizo saa nne.  Muhimu ilikua kuithamini nchi yako.

  Balozi wetu London, Mheshimiwa Peter Kallaghe alipomkaribisha mgeni alisema hawa ni Watanzania wanaoipenda nchi yao.  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mwenye miaka 58 ni mwanataaluma aliyebobea  kielimu.  Mbali na tuzo saba za kitaifa na kimataifa alizoshapewa ni mhariri wa jarida la kisayansi Afrika (Africa Earth Science Journal). Anaheshimika kiulimwengu na si ajabu anao wadhifa wa Makamu Rais wa Tume ya Ramani ya Madini duniani iliyoundwa 1881  Ufaransa. Lengo lake ni kuendeleza masuala ya mazingira, madini na hali ya hewa. Mtanzania huyu ni pia mwanachama wa Jumuiya mbalimbali za jiolojia, Tanzania, Marekani, China na Uingereza.

  Tunavyokuja kumsikiliza tunataka ukweli, maana wanayansi hawaropoki ovyo.
  Lakini...Mtanzania hahitaji  usomi na taaluma pekee; anatalilia kutatuliwa matatizo ya mgao wa umeme, nyumba, chakula, kusomesha watoto wetu nk... Na hayo sasa ndiyo ya kutafakari kuhusu makutano na Waziri  Muhongo Jumanne iliyopita tarehe 26 ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania,  Uingereza.  
  Waziri aligawa maongezi  mafungu matatu.
  1.     Umeme
  2.     Madini
  3.      Maswali na majibu.
  Kiwajihi na  kisaikolojia  hakuna hata nukta moja Mbunge huyu wa kuteuliwa alipopepesa pembeni kutazama kijikaratasi au kumwomba Katibu wake aliyeongozana naye (Bw Sosthenes Massola) amkumbushe kitu. Ni kiongozi anayefaham anachokisema. Kwa saa nne nzima takwimu, mahesabu na maelezo vilimbubujika kinywani bila kusita.

  1.     SUALA LA UMEME
  Alisisitiza nchi yetu haiwezi kondokana na umaskini bila kuendeleza umeme. Wastani wa kipato chetu kitaifa (“Gross National Income”) ni dola 23 hadi 24 bilioni.  Hizo zikigawanywa kwa kila Mtanzania ni dola 500 (takiban shilingi laki nane na nusu) na yathibitisha sisi taifa maskini. Lengo  ni kufikisha   dola 1,250 hadi 1,300 mwaka 2025.  Asilimia 18.4 ya Watanzania tu ndiyo wanaotumia umeme. Kati yao asilimia 6.6 wako vijijini.

  BILA KUTUMIA UMEME HATUWEZI KUONDOKANA NA UMASKINI.  
  Sababu kibao. Mabwawa ya maji ya kizamani. Muundo wa  shirika la Umeme (TANESCO)  wenye mfumo wa kizamani, nk. Lengo la Wizara yake ni kufikisha umeme kufikia asilimia 30 mwaka 2015.  Moja ya masuluhisho yaliyoshaanza ni  bei ya kuunganisha umeme kushushwa toka laki 4 au 5 hadi laki 1.7.

  WATANZANIA TULIO NJE TULIKUMBUSHWA KUJENGA NYUMBANI.
  Kuunganisha umeme  shule ya msingi ya kijijini kwako  ni shilingi milioni nne; “ukitaka kujenga zahanati ni milioni kumi”. CHANGIA MAENDELEO KWENU. LAKINI TATIZO HILI SI LA BONGO TU.  Nchi zilizoendelea ki uchumi Afrika zina umeme kila sehemu. Asilimia 99 ya wananchi wa Mauritius  wanao, ilhali Afrika Kusini ni 75%.

  WAZIRI ALIKUMBUSHA TWAHITAJI KUWA NA NJIA NYINGI  KUPATA UMEME.
   Gesi inapatikana kwa wingi. Kwa sasa tunatumia kidogo sana (toka Songo Songo); akatoa takwimu akasema nyingine zimegunduliwa Mtwara na maeneo hayo yote. Hivyo matumizi ya gesi  ndiyo yatakayotuondoa choo cha umaskini. Kila siku magunia 40,000 ya mkaa yanatumika Dar es Salaam. Tunaweza pia kutumia mimea (“bio-energy”); nchi nyingi duniani hutumia  mimea; mathalan  miwa na sukari kupata petroli, Brazil. WATANZANIA TUNATAKIWA TUWE WATU WA KARNE YA 21 SIO  WA KUNI NA MIKAA.

  2. SUALA LA MADINI.

  Hapa Profesa Muhongo alisisitiza  azma yake si kupoteza muda kwa kelele za  malumbano. Alisema iko migodi sita ya dhahabu, Tanzania. Akagusia juu ya sheria ya Madini ya mwaka 2010 ambayo imepandisha mrabaha kutoka asilimia 2 kwenda asilimia 3 na kodi ya mamlaka kufikia asilimia 30. Alikumbusha juu ya faida za migodi kama kutoa ajira na kuwafariji wananchi wanaoizunguka.

  Hapa tukirukia baadaye wakati wa maswali  kuna aliyetaka kujua iweje kuna watu binafsi wanafaidi. Waziri akafafanua madini ni mali ya taifa. HUWEZI UKAUZA DHAHABU YAKO POPOTE. KUNA SOKO LA KIMATAIFA NA SHERIA ZAKE. Dhahabu ni pato kubwa la kitaifa. Akatoa mfano wa serikali ya Marekani inayomiliki tani 10,000 za dhahabu. Ndiyo maana Marekani taifa tajiri.

  Akagusa mengi lakini moja muhimu la kukumbuka ni kuwa dunia ya leo pia ina madini mpya ambazo zamani hazikuangaliwa. Madini zinazotumika kujenga tarakilishi, ndege na simu za mkononi mathalan.


  CHINA INAONGOZA DUNIA KWA MADINI HIZI MPYA KWA ASILIMIA 95. Ndiyo maana kila nchi (ikiwemo Tanzania) zinatafuta migodi. Tunayo madini. Lindi kuna mawe. Singida yapo matale (“granite”). Matale tunavyojua hutumika kujenga madaraja, majumba, maeneo ya juu ya fenisha nk. 3.MASWALI NA MAJIBU- TUBADILI MTAZAMO Kila muulizaji alipoanza swali na “serikali inafanya au itafanya nini” alikumbushwa huo ni “mtazamo wa kizamani.”

  SERIKALI SI SAYARI NYINGINE. TUSIWE TUNASEMA SERIKALI, SERIKALI. SISI WENYEWE NDIYO SERIKALI.
  Aliposema hivyo alinikumbusha Rais wa zamani Marekani hayati John Kennedy aliyemtaka kila mwananchi kujiuliza utalifanyia “nini taifa lako badala ya taifa litakufanyia nini.”
  Waziri alitoa mfano wa Wakenya walipokuwa wakichangiana kumtuma mtoto wa mwenzao kusoma India au Marekani. Sisi tukitoa michango ni kufanya arusi. Mantiki yake Waziri hapa ni moja.
   WATANZANIA TUJITUME NA TUPENDANE.

  Yupo dada aliyejuza vipi serikali itaelemisha watu kuhusu matumizi ya gesi. Waziri  alisisimama hapo kwamba sisi wenyewe tuelemishana na kusaidiana, badala ya kutegemea sana serikali. Watanzania hatuna  tabia ya kusoma. YALIKUWEPO MADUKA MENGI YA VITABU MIAKA YA SITINI NA SABINI MIJINI. LEO YAMEGEUZWA MADUKA YA NGUO. Watanzania wavivu kusoma kiasi ambacho unaweza kutoa vijikaratasi vya kuelezea matumizi ya gesi, mtu akayatumia kufungia vitumbua Asilimia 60 ya magazeti ni  ya udaku, starehe kuliko kuelemisha.

  Kuna uvivu wa kusoma kiasi ambacho kuna mtu yuko radhi kununua shahada za udokta ilhali kamaliza darasa la saba. IKIWA BAADHI YA VIONGOZI WANANUNUA SHAHADA ZA BANDIA JE, WATOTO WATAMWIGA NANI? Ndani ya mada hii liliamka tena nyigu la tafrani za Mtwara, ambazo Waziri alitoa maelezo marefu. Sababu si tu za kicuhumi alisisitiza Waziri. KUNA MENGINE.  Akasema alipolihutubia Bunge mwaka jana  alitawanya maelezo  DHAHIRI ya mabomba na uchimbaji gesi. Akasema anakumbuka suala la mabomba lilikua ukurasa wa 79. Wabunge walisoma kisha wakapitisha hoja yake. Baadaye “wakamgeuka.”
  Akaendelea kusema  Wizara iligharimu kuwapeleka madiwani na viongozi waliochaguliwa toka Lindi, Mtwara na Kilwa kujisomea ughaibuni : Trinidad, Tobago na Norway. Lakini waliporudi hawakutekeleza walichokisoma.


  0 0   March 2013- Tanzania Women of Achievement Awards nomination deadline has been extended from the 28th of February 2013 to the 16th of  march 2013 due to a significant amount of requests from the public to push the nomination deadline forward so that more nomineesfrom upcountry can participate. The awards ceremony that was due to take place on the 8th of March 2013 will now take pace on the 28thof March 2013 at the Serena Hotel in Dar es Salaam.


  “In 2009 during the first year of TWAA we received around 200 nominations, in the second year we received over 380 nominations, this year the response has grown overwhelmingly and we hope to receive more than 500 nominations. We have decided to push the awards dates forward so as to accommodate the many requests made by upcountry supporters who are mobilizing for nominations to ensure that we have better participation from the regions. There are so many women in the regions who are doing amazing things and we would like to make sure that they get the opportunity to be recognized.”  Said Irene Kiwia, President of TWAA.


  These bi-annual awards were first launched in 2009 to honor women in different sectors across the country who through their work have contributed significantly to the development of their communities in one way or the other.


  Ms. SadakaGandi, TWAA committee chair added that “TWAA was launched to recognize women who have not only achieved success in their own respective fields but who through their work and initiatives have made a significant difference in their communities and society as a whole. These women are everywhere in Tanzania. 

  Upcountry Tanzanian societies are faced by far more challenges, and its not just the government that is doing things to help but its also the people within the communities, and most of these people are women. And these are the women that we want to recognize.” Ms. Gandi continued urging that “we therefore hope that by extending the nomination deadline we will get more nominees from the regions.”


  The Categories for this year’s awards are Arts and Culture, Business Entrepreneur, Information and Communication, Sports, Professional, Education, Health, Social Welfare, Science and Technology, Public Sector, Young Achiever, Agriculture, Lifetime Achievement and the overall Woman of the Year.


  The TWAA committee comprises of Mrs. Mary Rusimbi – Activist and Founder of Tanzania Gender Networking Program, Judge Joaquine De Mello - Commissioner for the Commission of Human Rights and Good Governance, Dr. MarcelinaChijoriga –Former Dean University of Dar es Salaam Business School,  MrsLudovickaTarimo – Gender Specialist at USAID,Innocent Mungy- Communication Director Tanzania Communication Regulatory Authority, SadakaGandi – Counselor Psychologist and Social worker, Irene Kiwia – Founder and Managing Director Frontline Porter Novelli.  For more information visit www.twa.or.tz .

  ABOUT TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA)

  TWA is a non-governmental, voluntary and independent women empowerment umbrella established in 2009. The main goal of TWA is to consolidate women's roles and capabilities in the Tanzanian community through enhancing their social, political, economic and cultural participation. TWA conducts awareness campaigns, trainings, seminars, conferences and workshops that foster an exchange of information and mentorship to Tanzanian women and young girls to ensure that human rights, gender equity, economic engagement and socio-political participation are promoted.


  Our mission is to improve lives, expand opportunities, and help women across Tanzania flourish across who will in turn help societies and the country flourish. We work with innovative leaders, individuals, communities, NGO’s, the government, private sector and outside donors to build effective institutions and advance path breaking transformations. We are committed to Tanzania’s continued development till every woman becomes the change.  0 0

  Baadhi ya Vijana mbalimbali waliokuwa wamekusanyika kwenye kiunga cha moja ya ofisi za taasisi hiyo ya THT,Kinondoni Block 41,jijin Dar kwa ajili ya kushiriki mjadala uliohusu changamoto mbalimbali zinazowakumba wasanii wa Kike wakiwa katika picha ya pamoja na mwanamuziki kutoka nchini Marekani aitwaye Maya Azurenca.


  Pichani juu ni Mwanamuziki kutoka nchini Marekani aitwaye Maya Azurenca akimba mbele ya vijana mbalimbali (hawapo pichani),wakati wa kushiriki mjadala uliohusu changamoto mbalimbali zinazowakumba wasanii wa Kike , mjadala uliohusisha wasanii wa kike kutoka THT,wasichana kutoka nyumba ya kulelea watoto yatima wa KIWOHEDE  .
  Baadhi ya Wasanii wa Kike waliopo kwenye kituo cha THT na waliowahi kupita kituoni hapo,kwa pamoja wakiimba jukwaani kabla ya kuanza mjadala uliohusisha wasanii wa kike kutoka THT,wasichana kutoka nyumba ya kulelea watoto yatima wa KIWOHEDE
  Msanii Kutoka THT aitwaye Norman akiimba jukwaani.
  Muziki ni hisia wajameni.
  Wakifuatilia.
  Ilikuwa burudani kabisa mbele ya vijana.
  Burudani ikitolewa kutoka kwa vijana wa THT.
  Baadhi ya Vijana na wadau mbalimbali waliokuwa wamekusanyika kwenye kiunga cha moja ya ofisi za taasisi hiyo ya THT,Kinondoni Block 41,jijin Dar kwa ajili ya kushiriki mjadala uliohusu changamoto mbalimbali zinazowakumba wasanii wa Kike,ambapo mwanamuziki kutoka nchini Marekani aitwaye Maya Azurenca alishiriki.Mjadala huo umeanzishwa ikiwa ni Katika kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya kimataifa ya wanawake duniani itakayofanyika mnamo machi 8.  ==== ======   ======= ======= ==== 

  THT yaandaa mjadala kuhusu changamoto zinazowakumba wasanii wa kike, pamoja na mwanamziki wa kimarekani,Maya Azurenca.


  Katika kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya kimataifa ya wanawake duniani, leo Nyumba ya vipaji Tanzania, THT, imeandaa majadiliano kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo wasanii wa kike hapa nchini, mjadala uliohusisha wasanii wa kike kutoka THT,wasichana kutoka nyumba ya kulelea watoto yatima wa KIWOHEDE na mwanamuziki kutoka Marekani, Maya Azurenca ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku kadhaa.


  Mjadala huo pia ulitoa fursa kwa kinadada walio kwenye muziki, kama Mwasiti, Trio, Linah, Vumi na Rachel kuelezea changamoto na uzoefu wao katika tasnia ya muziki. Mjadala huo uliwapa nafasi kina dada wanamuziki wa Tanzania kujifunza kutoka kwa Maya, ambaye ni mwanamuziki wa muda mrefu kutoka Marekani.

  Maya ambaye pia ni balozi wa utamaduni, ameimba nyimbo mbalimbali zinazohusu haki za binadamu na pia amefanya matamasha nchi nyingi duniani kwa lengo la kuhamasisha kuhusu haki za binadamu. Katika mjadala huo, wasichana waliozungumza walisema kinadada katika tasnia ya muziki wanakumbwa na changamoto nyingi na pia ni vigumu kwa waimbaji wa kike kupata fursa ya kufanikiwa kulinganisha na wenzao wakiume.

  Wakizungumza katika mjadala huo, mwanamuziki wa kundi la kike la TRIO, Angela Karashani, alielezea changamoto kubwa ambayo anakumbana nayo ni watu kudhani wao ni wahuni hasa kwa kuwa wanajihusisha na muziki. ‘Ukiwa mwanamuziki wa kike kwanza huwa ni shida sana kupata sapoti, lakini pia watu wengi wanachanganya muziki na uhuni, ukiwa mwanamuziki wengi wanakufata wakidhani wewe ni mhuni pia’ alisema Angela.

  Mwanadada Maya aliwapa chanagamoto kinadada hao wanamuziki kwa kuwaambia kuwa waweke juhudi katika muziki na hakika watafika mbali. ‘Kitu kikubwa ambacho nimejifunza kwenye maisha yangu ya muziki na ningependa kuwaambia hapa ni kuwa kuwa mwanamuziki wa kike sio jambo rahisi, lakini kikubwa ni kuamini kile unachofanya na kuweka juhudi katika hilo na kujiamini’ alisema Maya. Mwanamuziki huyo pia ametoa fursa ya kufanya nyimbo kadhaa na wanamuziki wa kitanzania wakati wa ziara yake hii hapa nchini ili kuwapa fursa ya muziki wao kusikika kimataifa zaidi.

  0 0


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akiwaonyesha ng’ombe wafugaji wa Kabila la Wamasai waliomtembelea katika shamba lake la mifugo kijijini Kwake Msoga,Kata ya Chalinze,wilayani Bagamoyo jana(Jumapili).(picha na Freddy Maro).

  Na Freddy Maro Msoga,Bagamoyo.

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa wafugaji nchini kupima na kupanga ardhi kwaajili ya ufugaji bora wenye tija na kuepusha migogoro kati ya wakulima na wafugaji inayotokana na ufugaji wa kuhamahama kutafuta malisho.

  Rais Kikwete alitoa rai hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wafugaji wa kabila la wamasai kutoka mkoa wa Pwani na Morogoro waliomtembelea nyumbani kwake kijijini Msoga kata ya Chalinze, wilayani Bagamoyo jana(Jumapili).

  “Ni lazima mtambue kwamba ufugaji wa kuhamahama hauna tija kwakuwa watu wengi sasa wametambua thamani ya ardhi wanaipima na kuimiliki na hivyo maeneo ya kuchunga mifugo yanapungua.Huu ni wakati muafaka wa kupima ardhi na kuimiliki kwaajili ya ufugaji wa kisasa,” alisema Rais Kikwete.

  Sambamba na kutenga maeneo maalumu kwaajili ya ufugaji Rais Kikwete amewahimiza wafugaji hao kuotesha  majani kwaajili ya malisho ya mifugo ili kuepuka upungufu wa lishe ya wanyama wakati wa kiangazi na kuhakikisha mifugo hiyo inabakia na afya njema kwa faida ya wafugaji.

  Wakizungumza awali,wafugaji hao waliiongozwa na kiongozi wao Mkuu Laiboni Tikwa Moreto walimshukuru Rais Kikwete kwa kuwajengea Shule ya Sekondari kwaajili ya Watoto wa wafugaji ambayo sasa hivi ina jumla ya wanafunzi 146.

  “ Tunakushukuru sana kwa kutujengea shule ya Sekondari Moreto na watoto wetu sasa wamepata fursa ya kusoma na tuna kuomba utusaidie ili tuweze kuongeza madarasa,mabweni na maji ya kutosha ili wanafunzi waliopo waweze kusoma kwa ufanisi,”walisema katika risala yao kwa Rais Kikwete.

  Akijibu Rais Kikwete aliwapongeza kwa kuitunza shule hiyo na kusema kuwa maisha ya kuhamahama  kwa wafugaji yanawakosesha watoto wao fursa ya kupata elimu na kuahidi kuendelea kuisadia shule hiyo ili watoto wengi zaidi waweze kunufaika na elimu ya sekondari.

  Baadaye wafugaji hao walipata fursa ya kutembelea shamba la mifugo la Rais Kikwete kijijini Msoga na kujionea ufugaji wa kisasa unaozingatia kanuni bora za kitaalamu ambapo ngo’mbe mmoja anaweza kufikia uzito wa kilo miasaba.

  0 0

   President Jakaya Mrisho Kikwete in a group photos with (from left)  Mr Steve Kaufman, the Millenium Challenge Corporation's Chief of Staff (right) MCC's Vice President for East and Southern Africa, Mr Andrew Mayock (second row right),the US Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt (front row left) Mr Matt KAvanagh, MCC Resident Country Director (second row left) and the Minister for Finance Dr Willim Mgimwa and Mr Bernard Mchomvu, the CEO of the Millenium Challenge Account (MCA) -Tanzania,  at the State House in Dar es salaam today March 4, 2013. Centre is the US Chief of Staff, Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt.
  President Jakaya Mrisho Kikwete greets Mr Steve Kaufman, the Millenium Challenge Corporation's Chief of Staff, who paid him a visit at the State House in Dar es salaam today March 4, 2013. Centre is the US Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt.
  President Jakaya Mrisho Kikwete holds talks with (from left)  Mr Steve Kaufman, the Millenium Challenge Corporation's Chief of Staff, MCC's Vice President for East and Southern Africa, Mr Andrew Mayock,the US Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt. and Mr Matt KAvanagh, MCC Resident Country Director ,  who paid him a visit at the State House in Dar es salaam today March 4, 2013. Centre is the US Chief of Staff, Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt.STATE HOUSE PHOTO

older | 1 | .... | 39 | 40 | (Page 41) | 42 | 43 | .... | 1897 | newer