Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UKARABATI WA BARABARA YA NYAGUGE-MUSOMA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tupa, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi ukarabati wa  Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Eng. Sabyasachi Kar, wakati alipotembelea kujionea mashine za kusaga mawe, zilizopo Kijiji cha Sabasaba Irimba, wakati akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mara, iliyo sambamba na Uwekaji jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mbunge wa Butiama Vijijini, Nimrod Mkono, baada ya kusikiliza maelezo kutoka kwa Eng. Sabyasachi Kar, kuhusu mashine za kusaga mawe wakati alipotembelea kuona mashine hizo, zilizopo Kijiji cha Sabasaba Irimba, wakati akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mara, iliyo sambamba na Uwekaji jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma,leo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tupa, kwakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tupa, kwakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Dr. John Ndunguru, wakati alipowasili kuweka jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.



  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakifurahia burudani ya ngoma ya asili, wakati walipowasili eneo la kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. Jhn Pombe Magufuli, wakifurahia burudani ya muziki wa dansi kutoka kwa bendi ya Msondo Ngoma, wakati walipowasili eneo la kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa vazi la Jadi na mzee wa Mkoa wa Mara, Thomas Sura, wakati akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mara na kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakifurahia vazi la Jadi baada ya kukabidhiwa na mzee wa Mkoa wa Mara, Thomas Sura, wakati wakiwa katika ziara yao ya siku mbili mkoani Mara na kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.
Wasanii wa Kikundi cha sanaa wakitoa burudani wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo Feb 4, 2013. Jiwe hilo limewekwa na Makamua wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
 Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha Sanaa za asili, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo Feb 4, 2013. Jiwe hilo limewekwa na Makamua wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
 Ilikuwa ni burudani ya kutosha kutoka kwa kikundi hicho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Musoma leo Feb 4, 2013 wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma.

Minister urges more institutions to support needy children

$
0
0

 Minister of Health and Social Welfare Doctor Hussein Mwinyi (leftreceives a dummy cheque worth TShs 10 million from the Managing Director of SayedCorporation Limited, Sayed Masoud, donated together with 30 bicycles as support to Victoria Foundation whose headquarters is in Geita region. The handover ceremony took place in Dar es Salaam at the weekend. Center is Founder and Chairperson Vicky Kamata
Minister of Health and Social Welfare Doctor Hussein Mwinyi (left) congratulates the Founder and Chairperson of Victoria Foundation, Vicky Kamata after receiving a cheque worth TShs 10 million and 30 bicycles from Sayed Corporation Limited as support to the children with special needs, under the care of the foundation. Center is Sayed Corporation Managing Director, Sayed Masoud. The handover ceremony took place in Dar es Salaam at the weekend.

=====  ======= ========
Minister urges more institutions to support needy children

By Correspondent

The Minister of Health and Social Welfare Dr. Hussein Mwinyi has called on private institutions, individuals and faith organizations to support Government’s efforts in taking care of vulnerable children and the elderly, for the government’s resources and facilities are overwhelmed.

Speaking during a short ceremony to witness a hand over of a donation from Sayed Corporation limited to Victoria foundation, Dr Mwinyi said the needs of these vulnerable children are far outstripping the existing infrastructure and financial capacity the government currently has, therefore a helping hand was urgently required.

“Tanzania’s is very huge with a population close to 45 million people.  There is no way that the government could take care of all the needy children on its own. This is where organizations, be it Non Governmental Organizations (NGOs), faith-based organizations, private organizations of individuals should come up and give the government a helping hand.

“On behalf of the Government, I m greatly delighted to see organizations like Victoria Foundation voluntarily taking a bold step of providing for this special group, giving them hope and joy of living as other children,” he said.  

The Managing Director of Sayed Corporation Limited, Sayed Masoud, said the 10m/- cheque and 30 bicycles his company donated to Victoria Foundation is a first step towards future support to the foundation.He said his company urged Victoria Foundation management to observe honesty and diligence when handling the aid extended to the foundation by ensuring that it reaches the targeted groups.

On her part Vicky Kamata, the founder and Chairperson to the Foundation, expressed her gratitude to Sayed Corporation for the support, assuring the donors that the aid would help the foundation attain its objectives.   According to Vicky, the Geita Based Foundation which currently takes care of 32 children, strives to improve the quality of life and advance the rights of the children and the youth.

To promote lifelong learning principles among the youth for sustainable development, as well as create an environment around the children and the youth that promotes self-reliance and long-term sustainable development.
It also strives to promote School-Health Program among the children and the youth.

“The Foundation has a dream and expectations of putting a smile in the faces of needy children, giving them hope of a better life and seeing that they live a decent life thereafter. This support from Sayed Corporation will go a long way in supporting the realization of this dream,” she said.
During the occasion, Dr Mwinyi also contributed 1m/- to the foundation.
For more information about the foundation visit www.Victoriafoundationtz.org

Msikilize Kingwendu ngwedulile ndani mkasi wa salama

filamu ya SIRI YA MTUNGI NI ELIMU KWA JAMII- CHEUSI.

$
0
0
MSANII kinara katika tamthilia ya Siri ya Mtungi Godliver Godian ‘Cheusi’ (pichani) amesema kuwa katika tamthilia ya Siri ya Mtungi inayorushwa kupitia vituo vya televisheni mbalimbali hapa nchini, waandaaji wa Tamthilia hiyo wamejipanga na kujua nini wanafanya, jambo ambalo anawashauri watengenezaji wa filamu kuiga ili kwenda mbele katika tasnia ya filamu.

“Kuna mambo mengi kama msanii nimejifunza katika uigizaji,nimekutana na waongozaji wa kimataifa ambao si uzoefu tu bali wamesomea kazi hiyo na wanajua jinsi ya kufanya kazi yao wanaelekeza vizuri na kukufanya msanii kuigiza katika ubora wa kimataifa, kwa kifupi wanajua mambo mengi,”anasema Cheusi.
Msanii huyo amedai kuwa awali baadhi ya wasanii walikuwa wakihofia kushiriki katika usahili wakijua kuwa waongozaji na watayarishaji hawajui kuongea Kiswahili lakini hali haipo hivyo pamoja na kutoka Hollywood na Dubay lakini wanaongea vema Kiswahili. Siri ya Mtungi ni tamthilia inayotamba nchini kwa sasa ikiwa imeandaliwa na mfid na kuwashirikisha wasanii wa Tanzania ikiongelea masuala ya afya na maisha ya jamii kwa ujumla.Habari picha kwa hisani ya Filamu Central.


Jumamosi Hii Nyumbani Lounge

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA KIVUKO CHA MV MUSOMA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Kivuko cha MV Musoma, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo Feb 5, 2013 kijiji cha Kinesi Wilaya ya Rorya Mkoani Mara. Kutoka (kulia) kwake ni mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi uzinduzi wa Kivuko cha Mv Musoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho uliofanyika leo Feb 5, 2013, kijiji cha Kinesi Wilayani Rorya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akibonyesha kitufye kupiga alam, kuashiria uzinduzi rasmi wa Kivuko cha Mv. Musoma, wakati wa uzinduzi wa kivuko hicho uliofanyika leo Feb 5, 2013 katika kijiji cha Kinesi. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akipiga makofi kufurahia uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakiwa ndani ya Kivuko cha Mv. Musoma baada ya kuzinduzliwa rasmi na Makamu wa Rais, leo Feb 5, 2013 wilayani Rorya kijiji cha Kinesi mkoa wa Mara
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na viongozi wa Chama na Serikali, wakati akitoka kukagua Kivuko cha Mv. Musoma, baada ya kukizindua rasmi leo Feb 5, 2013 kijiji cha Kinesi wilayani Rorya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa MKoa wa Mara, John Tupa, pamoja na viongozi wa Chama na Serikali, wakiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu baada ya uzinduzi huo. Picha na OMR

Airtel yaongeza MPUNGA -Amka Milionea

$
0
0

·         Airtel "AMKA MILIONEA" zaongeza zaidi ya Milion 270
·         Kwa siku 60  zaidi ya wateja 580  wa Airtel kuibuka na Mamilioni hayo
·         Tuma shinda kwenda 15595 ili kujiweka kwenye ushindi
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeongeza muda wa promoshei yake kabambe ya AMKA MILIONEA pamoja na sambamba na kuongeza kiasi kikubwa cha MPUNGA ili wateja wake kuendelea kujizolea mamilioni zaidi

Meneja Uhusiano wa Airtel ametuhabarisha kuwa promosheni hiyo iliyodumu kwa siku 90 hapo awali na kufanikiwa kuzawadia  zaidi ya milioni 400 kwa wateja wameamua kuiendeleza ili wateja waendelee kufaidi zaidi

“promosheni inaendelea sasa! Kila mteja wa Airtel anaweza akashiriki kwa kutuma neno MILIONEA au SHINDA kwenda 15595 na ataunganishwa bure

Zawadi zimeongezeka kila siku kutakuwa na washindi 10 watakaojishindia mamilioni kama kawa!!!

AMKA MILIONEA itahakikisha kila siku kunawashindi 10 kushinda kila siku na watagawana jumla ya shilingi  3,000.000, kila wiki jumla ya shilingi milioni 6,000,000 zitashindaniwa na washindi 10 na kila  mwisho wa mwezi  mshindi wawili watashindania na kugawana kitita cha shilingi milioni 30 wakati milioni  50, 0000Tshs itaenda kwa mshindi mmoja mwisho wa promosheni hii.
======  =======  =====
Taarifa zaidi kwa mshiriki 
Vigezo Muhimu .

Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 ya kwa zawad ya kila siku .
Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 yakwa zawadi ya kila wiki Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 zawadi ya kila mwezi.
Mshiriki mmoja unaweza kushinda mara moja zawadi ya kila siku, mara moja zawadi ya kila wiki  na mara 1 zawadi ya kila mwezi. Lakini pia anaweza akajishindia zawadi kubwa ya mwisho wa promosheni


Kujiunga .

Tuma neno "WIN / Shinda", kwenda namba 15595 ( bure), na kisha utapokea ujumbe wa ukaribisho utakaombatana na maswali utakayojibu.

Kila jibu sahihi mteja atapata pointi/alama 20 na akikosea atapata pointi 10 zitakazomuwezesha kushinda, ukijibu maswali mengi unajiongezea nafasi ya ushindi.

moto wateketeza ghala kubwa la vifaa vya ujenzi jijini dar leo

$
0
0


 Msikilize Afande Kenyela akiongelea tukio zima la moto huo eneo la tukio. 
 Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Ultimate Security wakiendelea kuzima moto uliokuwa ukiendelea kuwaka ndani ya ghala hilo,ambao tayari ulikwisha teketeza mali nyingi.
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka ndani ya ghala hilo kama uonekanavyo pichani.
Moto mkubwa umezuka na kuteketeza mali mbalimbali zilizokuwemo kwenye moja ya ghala kubwa la kuhifadhia vitu mbalimbali ikiwemo vikombe vya udongo,Pampas,vigae na vitu vingine ,sehemu ya maghala ya kuhifadhia vitu Shekilango,jijini  Dar,aidha kufuatia tukio hilo mpaka Globu ya Jamii inaondoka eneo la tukio,hasala naa gharama za mali zilizoteketea haikuweza kufahamika mara moja,aidha kwa mujibu wa Kamanda wa mkoa wa Kipolisi Wilaya ya Kinondoni,Afande Kenyela alieleza kuwa mpaka sasa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika isipokuwa juhudi za kuuzima moto huo zilikuwa zikiendelea kwa juhudi kubwa.
Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Ultimate Security wakiendelea na juhudi za kuendelza kuzima moto.
Moto ukiendelea kushika kasi ndani ya ghala hilo
Palitokea mushkeli wa kutoelewana hivii kama uonavyo pichani,lakini baadae mambo yakaenda sawa

Ukuta ukitobolewa kupambana na moto uliokuwa ukiendelea kuwaka kwa kasi.


dkt. mwakyembe atembelea mataruma yaliyoibiwa.

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba akipata maelezo na mataruma yaliyobiwa kutoka kwa ACP Saada Haji ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi Cha Polisi Reli, wakati walifanya ziara ya kuangalia mataruma ya reli yalyibiwa katika vipindi tofauti tofauti yaliyopo katika eneo la Mivinjeni kurasini. (Picha na kitengo cha mawasiliano Serikalini Uchukuzi)
 Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mkwakyembe(mwenye tai nyekundu), akiangalia mataruma 35 yaliyoibiwa kutoka katika stesheni ya Reli ya Pugu na kusafirishwa kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuja kuuzwa kama chuma chakavu . Kulia kwa Waziri wa Uchukuzi ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(aliyevaa tai ya mistari).

 Shehena ya mataruma ya zaidi ya Tani 15 yaliyokamatwa na askari wa kikosi cha reli yakiwa katika eneo la reli Mivinjeni baada ya kukamatwa tarehe 14/2/2013 na dreva wa Lori hilo kukimbia. Waziri wa Uchukuzi na Naibu Waziri wamefanya Ziara katika eneno hilo leo kujionea mzigo wa Mataruma yaliyobiwa katika vipindi tofauti tofauti.
Waziri wa Uchukuzi.Dkt Harrison Mwakyembe (mwenye tai nyekundu),akipata maelezo kutoka kwa ACP Saada Haji Mkuu wa kikosi cha Polisi (Reli)(aliyevaa hijabu) ya namna wezi wa Mataruma hayo walivyoiba na kukamatwa na askari wake tarehe 14 Februari 2013. Kulia kwa ACP Saada Haji, ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba.


Magunia yaliyotumika kufunikia mataruma ya Reli ambayo yaliibiwa na kusafirishwa kutokea Tabora tarehe 14/2/2012 na kubebwa kwenye Lori la Mizigo la Kampuni ya Unga ya Azania (linaloonekana mbele) kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuuza kama chuma chakavu. Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba wamefanya ziara ya kuangalia mataruma hayo leo mchana jijini Dar es Salaam. Mataruma hayo yamehifadhiwa katika yadi ya Reli iliyoko Mivinjeni Kurasini, Dar es Salaam.

nomination deadline for tanzania women of achievement extended

We are seeking for the partners to sponsor the tournament

hitilafu ya umeme matokeo yake ndio haya....!

mukubwa mambo safi sasa tamasha la pasaka

$
0
0

MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Solomon Mukubwa ameibuka kidedea kwa wasanii wa nje watakaoshiriki Tamasha la Pasaka mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa mashabiki wengi wamempigia kura Mukubwa kuomba ashiriki kwenye tamasha la mwaka huu kama ilivyokuwa matamasha yaliyopita.

“Kwa hiyo leo naomba kumtangaza Mukubwa, ambaye ni raia wa DRC lakini anayeishi Kenya kwamba ni mwanamuziki wa kwanza nje ya Tanzania ambaye tayari kamati imeafiki ashiriki tamasha letu,” alisema Msama. Alisema maandalizi yanaenda vizuri na idadi ya wasanii kutoka nje ya Tanzania waliopendekezwa ni kubwa, lakini wanachokiangalia si kupendekezwa tu lakini pia nafasi ya msanii husika kuja kwenye tamasha hilo.

“Msanii akishapendekezwa vya kutosha kwa njia ya kura za maoni ambazo ni kupiga simu au kutuma ujumbe wa simu ya mkononi kwa kamati,  kinachofuata ni mazungumzo kati ya sisi waandaaji na msanii na tukifikia makubaliano ndiyo tunamtangaza,” alisema Msama.
Mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu mwenye ulemavu wa mkono mmoja, anatamba na albamu mbalimbali ikiwemo Usikate Tamaa, Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.

Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na  litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Wasanii ambao mpaka sasa wameshatangazwa kushiriki ni Rose Muhando, John Lissu na Upendo Nkone ambao wote ni Watanzania.

Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

MARA FOUNDATION YAJIDHATITI KUIBUA VIJANA WAJASIRIAMALI WATAKAOSAIDIA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA

$
0
0



Mgeni rasmi katika ufunguzi wa taasisi ya kibiashara ya Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh. Dkt. Mary Nagu akizungumza wakati kuzindua taasisi ya Mara Foundation ambapo amewataka vijana wajasiriamali kutumia fursa ya taasisi hiyo kujijenga kibiashara.

Taasisi ya Mara Foundation yenye makao yake makuu jijini Dubai sasa imejikita katika nchi za Afrika ambazo ni Uganda, Tanzania, Kenya na Nigenia kwa lengo kuwasaidia wajasiriamali wadogo kuwezeshwa kimuongozo na kuwa wafanyabiashara wakubwa ambao wataweza kutoa ajira kwa watu wengine.


Mgeni rasmi katika ufunguzi wa taasisi ya kibiashara ya Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh. Dkt. Mary Nagu akikata utepe kuzindua rasmi taasisi hiyo yenye matawi 28 barani Afrika. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Mara Foundation Nina Werner
Washiriki na wageni waalikwa wakifurahi jambo wakati mgeni rasmi Dkt. Mary Nagu akitoa risala kwenye uzinduzi wa Taasisi ya Mara uliofanyika hivi karibuni kwenye jengo la Mayfair Plaza.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi akisikiliza mawazo ya mmoja wa vijana wajasiriamali mwenye nia ya kukataka kukuza biashara yake na kuifanya kuwa endelevu wakati wa uzinduzi wa Mara Foundation ambao uliotoa fursa ya washiriki kuzungumza na wafanyabiashara waliopiga hatua na wenye uzoefu katika kuendesha biashara zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim Limited Emelda Mwamanga akimsikiliza mmoja wa washiriki ambaye ni mjasiriamali anayechipukia aliyetaka kupata uzoefu na mawazo zaidi jinsi ya kuendesha biashara yake.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees ambaye ni Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali akimsikiliza mjasiriamali mdogo mwenye ndoto za kuwa mbunifu wa kimataifa.
Ma-Mentors waliokuja kuzungumza na wafanyabiashara wadogo kwa ajili ya kuwapa mbinu mbalimbali za kibiashara na kuwaongoza kufikia malengo yao.
Taasisi ya Mara Foundation ilianzishwa na Ashish Thakkar ambaye ndie mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Mara Group.
Ashish alitumia muda wake mwingi katika kutimiza malengo ya Taasisi hiyo kwa kuwa alikuwa na imani na wajasiriamali na kuendeleza biashara ndogo.
Tangu mwaka 2009 Taasisi hiyo ililenga mtazamo wake na imefanya vizuri sana nchini Uganda, Tanzania, Kenya na Nigeria katika muelekeo huo.
Kuanzia mwaka 2013 mikakati ya taasisi ya Mara Foundation inaendelea kukua katika nchi za Kusini mwa Jangwa la sahara huku ikiendelea kuongeza wigo wake katika nchi nyingine duniani.
Mara Foundation inafanya kazi ya kubuni na kukuza uchumi endelevu na kufungua fursa endelevu kwa vijana wamiliki wa biashara za kati kwa kupitia vituo vya uwezeshaji vya Mara Launchpad na Mara Launch Fund.
Pichani juu na chini ni Washiriki na wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kabla ya mgeni rasmi Dkt. Mary Nagu kuzindua Taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Mara Foundation Tanzania Nina Werner (kulia) akizungumza machache kuhusiana na malengo ya Taasisi yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mh. Dkt. Mary Nagu kuizindua rasmi.
MC wa uzinduzi huo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Problem Solved Eric Mutta akimkabidhisha Mjasiriamali mdogo Peter Christopher kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (katikati) atakayekuwa mshauri wake wa kibiashara kwa muda wa miezi sita ijayo.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees ambaye ni Mbunifu Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali (katikati) akimpokea mmoja wa wajasiriamali waliohudhuria uzinduzi wa Mara Foundation kwa lengo la kuhakikisha anatimiza malengo yake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim Limited Emelda Mwamanga (kushoto) akipata picha ya ukumbusho na kijana aliyemchagua kumsaidia kimawazo na kumwongoza kwa muda wa miezi sita ijayo mpaka kufikia lengo lake.
Baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi wa Mara Foundation uliofanyika hivi karibuni Mayfair Plaza.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (kushoto) na Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mara Foundation.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi (kushoto) Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha (kulia) na Mkurugenzi wa man Magazine Dismas Massawe (katikati) katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Mara Foundation.

Waziri Mkuu wa Denmark Awasili Tanzania, alakiwa kwa shangwe

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt muda mfupi baaday kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jioni hii
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt wakipokea heshima za nyimbo za Taifa pamoja na saluti ya mizinga 21  katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt na mwenyeji wake wakifurahia burudani mbalimbali
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akipkea shada l maua
Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akisalimiana na kinamama waliofurika uwanjani kumlaki. Picha na Freddy Maro

Waziri Mkuu wa Denmark Awasili Tanzania, alakiwa kwa shangwe

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt muda mfupi baaday kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jioni hii
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt wakipokea heshima za nyimbo za Taifa pamoja na saluti ya mizinga 21  katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt na mwenyeji wake wakifurahia burudani mbalimbali
 Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akipkea shada l maua
Waziri mkuu wa Denmark Mhe.Helle Thorning-Schmidt akisalimiana na kinamama waliofurika uwanjani kumlaki. Picha na Freddy Maro

Venezuelan President Hugo Chavez dies

$
0
0
Venezuelan President Hugo Chavez, the charismatic leftist who dominated his country with sweeping political change and flamboyant speeches, died Tuesday at age 58, after a long battle with cancer that was shrouded in mystery and prevented him from being inaugurated for a fourth term.

Adored or reviled for his self-styled populist revolution, Chavez held sway over Venezuela through a cult of personality, government reforms that championed the downtrodden, and an endless stream of rhetoric denouncing capitalism, imperialism and the United States.

The "Chavistas" praised El Comandante for reducing extreme poverty and expanding access to health care and education. Critics blamed him for high inflation, food shortages, escalating crime and mismanagement of the country’s oil industry.

MKALI WA WIMBO WA 'ZUNGUKA' NA MKALI WA WIMBO WA 'RAHA JIPE MWENYEWE' KUZINDUA KAMPUNI YA KUTENGENEZA MUZIKI NA VIPINDI PASAKA HII CCM KIRUMBA MWANZA

$
0
0
Meneja wa kampuni mpya ya kurekodi muziki, vipindi na video ya COSU Entertainment Albert G. Sengo (kushoto) akitoa taarifa juu ya uzinduzi utakao kwenda kufanyika Siku ya Pasaka tarehe 31/03/2013 ambapo waimbaji Enock Jonas anayetamba na wimbo wake wa Zunguka pamoja na Neema Mwaipopo maarufu kwa wimbo wa Raha Jipe Mwenyewe na wengine wengi watashuka jijini Mwanza kuupamba uzinduzi huo kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Fabian Fanuel. Sikiliza hapo juu.
Mkurugenzi wa kampuni mpya ya kurekodi muziki, vipindi na video ya COSU Entertainment Fabian Fanuel akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari hii leo kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizoko nyegezi jijini Mwanza.


Mkurugenzi wa kampuni mpya ya kurekodi muziki, vipindi na video ya COSU Entertainment Fabian Fanuel akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari  kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizoko nyegezi jijini Mwanza, nyuma ni timu ya baadhi ya wafanyakazi wa idara mbalimbali za utayarishaji muziki na makamera mana wa kampuni hiyo walio tambulishwa leo.


Msikilize hapa..


Meneja wa kampuni mpya ya kurekodi muziki, vipindi na video ya COSU Entertainment Albert G. Sengo (kushoto) akitoa taarifa juu ya uzinduzi utakao kwenda kufanyika Siku ya Pasaka tarehe 31/03/2013 ambapo waimbaji Enock Jonas anayetamba na wimbo wake wa Zunguka pamoja na Neema Mwaipopo maarufu kwa wimbo wa Raha Jipe Mwenyewe na wengine wengi watashuka jijini Mwanza kuupamba uzinduzi huo.  

Meneja wa kampuni ya COSU Entertainment Albert G. Sengo akitoa wazo la jinsi ya kuboresha moja ya kazi za video za muziki kwa  mtayarishaji makini David Kimario ambaye yuko mtamboni, kulia kwake ni Mkurugenzi Fabian Fanuel,  shughuli nyingine zinazofanywa na kampuni hiyo ni pamoja na kumiliki jukwaa la vipaji mbalimbali kama wanamitindo, sarakasi, waigizaji filamu na utoaji huduma za matangazo ya barabarani.
Shughuli ya usanifu ikiendelea chumba cha madaktari wa video.

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakipata maelezo toka kwenye chumba cha mtayarishaji wa Muziki wa kampuni ya COSU Entertainment jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa COSU Entertainment hapa alipata fursa ya kuimba pamoja na wanahabari toka kulia ni Mashaka Bartazar wa Jambo leo na Majira na kushoto ni Sheilah Sezy wa Gazeti lililokuja na mabadiliko makubwa sokoni hivi sasa la Mwananchi.


Hapa kazi iliyokuwa ikisubiriwa ni Sheilah Sezy wa Gazeti lililokuja na mabadiliko makubwa sokoni hivi sasa la Mwananchi kukaanga chips aka kupiga drums.
Ndipo chips zikakaangika...

Hili ndilo gari la PA (matangazo ya barabarani) la Great Zone iliyo ndani ya COSU Entertainment.
Mjengo wa COSU Entertainment ulioko Nyegezi jijii Mwanza.

UZINDUZI WA KAMPUNI ILIYONUIA KULETA MAPINDUZI KWENYE SOKO LA DIGITALI MWANZA COSU ENTERTAINMENT UTAKAOFANYIKA TAREHE 31/03/2013 SIKU YA PASAKA UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA 

Ujio wa COSU Intertainment unakuja wakati Tanzania ikishuhudia Media zake zikiingia katika mfumo wa digitali ambao unahitaji kulishwa ipaswavyo ili kuvutia wadau na wafanyabishara kuweza kushawishika kununua muda wa vipindi husika (kuwa wadhamini) jambo ambalo huchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya utoaji huduma kwa media mbalimbali hapa nchini.


Ikumbukwe kuwa awali Taifa letu lilikuwa kwenye mfumo wa Analojia ambao ilikuwa ukiwa na Luninga yako na nishati na antenna yako ya waya basi mawasiliano utayapata utatizama Tv yoyote hata vipindi visivyokuwa na ubora  au usivyokuwa na mpango navyo alimuradi tu umetizama TV, sasa hizo zama zinatoweka taratibu mikoa baada ya mikoa.

Walianza Dar es salaam, Dodoma, Tanga sasa Mwanza nayo imeingia kwenye mfumo wa digitali mwisho wa siku wilayani, vijijini na Taifa kwa ujumla litakuwa digitali.


Kwa hali ya sasa ndani ya mfumo wa digitali ili upate mawasiliano ya televisheni lazima uwe na king’amuzi ambacho unalipia, sasa wamiliki wa ving’amuzi tulivyonavyo (vi 3 sasa) ili kuvutia wateja kwa malengo ya kupata soko kubwa wanalazimika kuweka channel zenye mvuto na zenye ubora ili kukidhi soko la ushindani.

Kupitia ushindani itafika kipindi ndani ya king’amuzi kimoja kutakuwa na chanel  200 hivi za ndani na nje hapa tutashuhudia tukishindanishwa na televisheni za kimataifa, kwa mfumo huu vituo vingi vitakuwa vikishindana kwa kuwa na maudhui nzuri na kuwa na vipindi vya kipekee  ili vipate matangazo na wadhamini wa kutosha.


Ni suala lililo wazi kuwa wenye matangazo yao hukimbilia vituo vinavyotizamwa.


Media kwa sasa ziko kwenye mahitaji ya kiushindani, hivyo zina mahitaji na mahitaji, kwa mtindo huu basi COSU Entertainment tumeona kuwa kuna mwanya hapo, nasi ni vijana wakongwe katika tasnia ya media tuko kwaajili ya kuuziba mwanya huo, na hizi ndizo juhudi sasa za kuitikia wito wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kuzifanyia kazi zile ajira ambazo tumeelekezwa zipo nasi kushuhudia kweli zipo.


COSU Entertainmen tuliojikita zaidi katika uandaaji na utayarishaji kuanzia vipindi, Audio music, Video za muziki pamoja na kujenga jukwaa la vipaji mbalimbali nchini Tanzania tumeliona soko hilo la ajira na sasa tunataka kuudhihirishia umma wa Watanzania kuwa mapinduzi yatafanyika kupitia sisi.


Hatujaishaia hapo pia tumeliona soko jingine la ajira lililopo vijijini na wilayani hapa tunazungumzia Muziki wa Asili, huu ni muziki ambao kwa sasa vionjo vyake vinakuja kwa kasi na kuboresha muziki wa kisasa na muziki huo wa asili ukionyesha kuwa na dira ya maisha marefu sokoni.


Tizama marafiki zetu Afrika Magharibi, Afrika ya kati, Afrika ya kusini wote hao vionjo vya muziki asili vimechangia kuubeba sana muziki wao kutamba katika soko la kimataifa na sasa ndiyo wameiteka dunia. Mifano iko mingi – akina Werason, Koffi  Olomide, Fally Ipupa, J. Martins na wengine wengi wote hawa style zote mpya wanazokuja nazo nyingi zinatoka vijijini, ambako hufanya mashindano ya vipaji mbalimbali iwe waimbaji, wapigaji muziki hadi wachezaji na kuubebea muziki huo kwenye soko hatimaye makubwa mapinduzi tunayashuhudia.

Sasa kwa hili tukirejea nchini na kuanzia hapa Kanda ya ziwa, Kanda inayosifika sana kwa vipaji vya nyimbo asili tena za kuchezeka, anzia Kagera kwa akina Saida Karoli, Maua, Papaa Kishaju wote muziki wao unadumu, Ingia Shinyanga kuna ngoma asili pale kama Bolaboka, Wigashe, Bogobogobo, rudi Mwanza na wilaya zake nenda Ukerewe na Kadogoli, Dungu, ngoma nyingi za kuchezeka tena za kusisimua na hata tumeshuhudia mara nyingine zikitumika kwenye  maharusi na dhifa mbalimbali na kadhalika.


Hivyo basi nina uhakika tukitumia vyema muziki huu mengi yatafanyika. Katika project tutakazozifanya kuna watu wakajkuja kwetu kurekodi kwa fedha na kuna watu tutawasaka nao warekodi kwa gharama zetu hawa ote tutashirikiana nao kutengeneza matirio zenye maudhui ya kuuzika, zenye Ushawishi.

Ndugu zangu waandishi wa habari huduma zetu ingawa zimeanza kufanya kazi kwa kurekodi baadhi ya vipindi kwaajili ya vituo vya televisheni mbalimbali, pamoja na kurekodi video za kwaya na bendi mbalimbali kwa sasa, uzinduzi rasmi tutaufanya mnamo tarehe 31/03/2013 katika sherehe ya sikukuu ya Pasaka uwanja wa CCM Kirumba ambapo tutafanya tamasha la Muziki wa Injili tulilolipa jina la PASAKA GOSPEL FESTIVAL ambapo wakazi wa Mwanza watashuhudia tamasha lililoandaliwa kwa ubunifu wa hali ya juu likishirikisha waimbaji wakubwa kama Enock Jonas (ZUNGUKA), na Neema Mwaipopo (RAHA JIPE MWENYEWE).


Wengine ni Nesta Sanga (JIANDAENI), Danni Safari, John Shahban, Jeska Julius, Isaya Msangi (SHETANI IMEKULA KWAKO), Danny Sanga kutoka Iringa, Tumaini Mbembela  kutoka Mbeya na mkoa wa Arusha utawakilishwa na Neema Munisi.


Kwaya za mkoa wa Mwanza ni nyingi za kutosha Anglican Vijana kwaya, EAGT City Centre kiufupi kwa zote zitaweka kambi kwenye shughuli yetu ya Pasaka.


Jumatatu ya pasaka tutakuwa Geita uwanja wa CCM Katoro

Kiingilio kwa maeneo yote kitakuwa ni shilingi. 2000/= tu

Hivyo tunawakaribisha wote kwenye uzinduzi huo.


Nanyi ndugu zangu wanahabari twawaomba mtusambazie habari hizi kwani hili linatoka kwa watu wenu na msishangae waandishi nanyi kupitia vipaji vyenu mkapata fursa katika soko la ajira la COSU Entertainment, tukawa tukiwakodisha mara kadhaa kutokana na either kuzidiwa na mahitaji hivyo tunawasihi msisite kufungua milango ya ushirikiano ili tujenge Tanzania yetu.


Zidumu fikra za Maendeleo!

Aksanteni kwa kutusikiliza.


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE BUTIAMA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Mama Maria Nyerere, wakati alipomtembelea nyumbani kwake Butiama Machi 4, 2013.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Mama Maria Nyerere, wakati alipomtembelea nyumbani kwake Butiama Machi 4, 2013. Kushoto ni Mke wa Makamu, Mama Asha Bilal.

MKUU WA MKOA WA RUKWA AKAGUA MIRADI YA USIMAMIZI WA ZIWA TANGANYIKA (PRODAP) KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwa na msafara wake wakikagua ujenzi unaoendelea wa daharia (bweni) katika shule ya sekondari Kasanga. Mradi huo ni sehemu ya miradi inayofadhiliwa na mradi wa usimazi wa ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na miradi mingine ya ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Muzi na ujenzi wa wadi ya kujifungulia kinamama kijiji cha Samazi. Miradi yote hiyo itawanufaisha wakazi wa mwambao wa ziwa Tanganyika na inagharimu zaidi ya shilingi milioni 150. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Samazi mwambao na ziwa Tanganika alipofika kukagua ujenzi wa wadi ya kujifungulia kinamama katika kijiji hicho. Mkuu huyo wa Mkoa alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kuwafuatilia kwa karibu wahandisi wanaojenga miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati. Aliwaasa pia wananchi kuzingatia uzazi wa mpango katika kuboresha maisha yao pamoja na kuwaendelezea watoto wao kielimu tofauti na hali ilivyo hivi sasa ambapo muamko wa elimu Mkoani Rukwa upo chini. Aliwataka pia kuboresha hali ya ulinzi katika maeneo yao ya mipakani kwa kutokuwakaribisha wageni bila kuwa na taarifa zao za kutosha. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na msafara wake wakikagua ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya Msingi Muzi yaliyowekwa jiwe la msingi na Naibu Waziri wa TAMISEMI Aggrey Mwanri ambayo mpaka kukamilika kwake yatagharimu zaidi ya shilingi Milioni 50.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Muzi iliyopo pembezoni mwa Ziwa Tanganyika Mkoani Rukwa baada ya kukagua ujenzi unaoendelea wa madara yanayofadhiliwa na mradi wa usimamizi wa ziwa Tanganyika mradi ambao upo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira. Aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwaahidi kuwapa ushirikiano wale watakaofaulu vizuri na kukosa uwezo wa kujiendeleza. 
Sehemu ya fukwe ya Ziwa Tanganyika katika kijiji cha Samazi Mkoani Rukwa ambapo mradi wa usimamizi wa ziwa Tanganyika unatekeleza mradi wa ujenzi wa wadi ya kinamama kwa ajili ya kujifungulia katika Zahanati ya kijiji hicho.
(NA HAMZA TEMBA - OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA - rukwareview.blogspot.com)
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images