Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 38 | 39 | (Page 40) | 41 | 42 | .... | 1896 | newer

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA
  (PSPF)
  TAARIFA KWA UMMA
  Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unawajulisha kwamba Mkutano Mkuu wa wadau utakaofanyika tarehe 07 na 08 Machi 2013 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika Ukumbi wa JB Belmont uliopo ghorofa ya 6 ya Jengo la Maegesho la PSPF - Golden Jubilee Towers , Dar es Salaam.

  Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na changamoto zinazoukabili Mfuko na Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla.

  Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Makao Makuu, Dar es Salaam au Ofisi za PSPF mikoani kabla ya tarehe 05 Machi 2013.
  “PSPF - Tulizo la Wastaafu”
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu
  Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma,
  Golden Jubilee Towers, Ghorofa ya 6-13, Mtaa wa Ohio/Kibo,
  Central Area, Kiwanja Na. 8, 9, 12 na 15,  S. L. P 4843. Dar-es-Salaam.
  Simu: +255 22 2120912/52 au +255 22 2127375 /6
  Nukushi: +255 22 2120930.

  0 0


  0 0

     0 0

  Mkurugenzi Mkuu Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii ya Jamii (NSSF),Ramadhani Dau akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya Shirika hilo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
   Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka akizungumza wakati wakati wa uzinduzi wa bodi mpya Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii (NSSF) 
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Abubakar Rajabu akitoa neno la shukrani baada ya Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka (kushoto) alipozindua bodi hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ramadhani Dau.
   Baadhi ya wajumbe wa bodi.
   Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii ya Jamii (NSSF), Ramadhani Dau mara baada kuzindua bodi mpya ya Shirika hilo.
   Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa bodi ya NSSF, Abubakar Rajabu na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF,  Crescentius Magori.

  0 0


  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa kiroho nchini, Rose Muhando ameongoza kwa kupata kura nyingi kwa mashabiki wanaotaka atumbuize kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama ilieleza kuwa msanii huyo amepata asilimia kubwa ya mashabiki wanaotaka atumbuize kwa waimbaji wa ndani, hivyo tayari kamati yake imempitisha kushiriki tamasha hilo.

  "Tunaendesha kura ya maoni kwa mashabiki wetu kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi au kupiga simu kuelezea ni waimbaji gani wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania wanaotaka wawepo kwenye tamasha la mwaka huu.

  "Kwa hiyo mwimbaji Rose Muhando amepata asilimia kubwa ya mashabiki wanaotaka awepo, zaidi ya asilimia 90 wanamtaka Muhando. Hivyo huyo tayari anakuwa tumeshampitisha tunaomba mashabiki waendelee kutuma maoni yao kwa kamati yangu ili kupitisha wasanii wengine.

  "Dhamira ya tamasha letu mwaka huu ni liwe la aina yake na tuwashirikishe mashabiki wetu, ndiyo sababu kuanzia mikoa litakapofanyika mpaka suala la waimbaji tumewapa fursa mashabiki wenyewe wateue," alisema Msama na kuongeza kuwa msanii atakeyekuwa amepigiwa kura kwa wingi ndiye watakayemtangaza.

  Tamasha la Pasaka limepangwa kufanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

  Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

  Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

  0 0

  Mkazi mmoja kutoka Temeke,jijini Dar akiwa amebeba mzigo mkubwa kuliko uwezo wa kifaa chake cha  kubebea (baiskleli)  kama alivyonaswa na Camera ya Jiachie,upakiaji wa njia hii/namna hii ni wa hatari ambao unaweza kusabisha ajali barabarani.

  0 0


   Entries are welcome in ten categories and are open to reporters and editors working on all media platforms. All entries are assessed and judged by an independent panel. The awards ceremony will be held on Thursday, 11 July 2013 in central London.

  The closing date for entry is Friday, 15 March, 2013.
  Entries can be submitted online at: www.diageoafricabusinessreportingawards.com  There is no entry fee
  About Diageo plc and Diageo Africa & Serengeti Breweries Limited
  Diageo is the world's leading premium drinks business with an outstanding collection of beverage alcohol brands across spirits, wines, and beer categories. Diageo is a global company, trading in more than 180 countries around the world. The company is listed on both the New York Stock Exchange (DEO) and the London Stock Exchange (DGE).

  0 0


  0 0


  Mshindi wa Tigo smartcard promotion Bw. Julius Raphael Kanza akiwa Madrid Hispania tayari kusubiri pambano la el classico kati ya Real Madrid na Fc Barcelona litakalofanyika kesho kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao  cha baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu, Dar es salaam, leo Machi 1, 2013.PICHA NA IKULU.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana  na Balozi wa Umoja wa Nchi za Kifalme za Kiarabu (UAE) aliyemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Mhe. Mallalla Mubarak Al Ameir alipoagana naye Ikulu, Dar es salaam, leo Machi 1. 2013. PICHA NA IKULU
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Balozi wa Umoja wa Nchi za Kifalme za Kiarabu (UAE) aliyemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Mhe. Mallalla Mubarak Al Ameir alipoagana naye Ikulu, Dar es salaam, leo Machi 1. 2013.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Umoja wa Nchi za Kifalme za Kiarabu (UAE) aliyemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Mhe. Mallalla Mubarak Al Ameir alipoagana naye Ikulu, Dar es salaam, leo Machi 1. 2013

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (mwenye blauzi ya kijani) na Mkurugenzi wa Huduma Ikulu Bw. Julius Mogore(mbele)   wakiongoza shughuli za usafi kuzunguka maeneo ya Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 1, 2013 katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Afrika. Siku hiyo itaadhimishwa kitaifa siku ya Jumapili.
    Picha zingine zinaonesha  Wafanyakazi wa kila kada Ikuluy bila kujali nyadhifa zao  wanafanya kazi bega kwa bega kuhitimisha Siku ya Mazingira Afrika kwa kufanya usafi.PICHA NA IKULU.


  0 0


  Nyumba ya vipaji Tanzania, THT, imetangaza leo kuwa jumapili hii ya tarehe 3/3/2013 watafanya usaili wa kusaka vipaji vipya katika ofisi zao za THT Block 41 zilizo karibu na Nyumbani Lounge (Kinondoni).

  Usaili huo utaanza saa tano kamili asubuhi, ukihitaji vijana wenye vipaji kuanzia miaka kumi na sita hadi ishirini na nne. THT inasifika kwa kukuza na kuzalisha vipaji vingi vya kucheza na kuimba hapa nchini, wakiwemo wasanii kama kina Barnaba, Rachel, Linah, Mwasiti, Ali Nipishe, Amini, Ditto, Makomando na wengine wengi.

  Akizungumzia usaili huo,meneja masoko wa THT, Michael Nkya, alisema anawakaribisha vijana wenye vipaji kujiunga THT. ‘THT ni sehemu ya kila kijana mwenye kipaji, hivyo usisite kuja, kama una kipaji njoo, nasi tutakuchagua kwani hakuna upendeleo wowote’ alisisitiza Nkya.


  0 0


   Suma Lee
  ASANTENI, On behalf of the Sporah Show Team

  0 0

  Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa (wapili kutoka kulia) akikata utepe wa kuashiria uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa madhehebu ya Kikristo Mwanza, kulia ni askofu wa Kanisa la Anglican Diosisi ya Nyanza (DVN) Boniface Kwangu akiwa ameshikilia kiasi cha shilingi millioni 40 zilizochangwa ikiwa ni pamoja na hudhi na ahadi zilizowekwa kutunisha Vikoba, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti pia anaonekana pichani wa pili kushoto .
  Na Albert  Sengo.

  WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Serikali ya Zanzibar Dkt.Mohamed Sheni kwa njisi ambavyo wamekuwa wakikazia suala la kudumisha amani nchini, wakiwemo viongozi wa Taasisi za kidini Kalidinali, Askofu Mkuu Polycarp Pengo (Romani),Askofu Alex Malasusa (KKKT), Mufti Shekhe Mkuu wa Tanzania  Simba Bin Simba na viongozi wengine wakiwemo wachungaji wa madhehebu mbalimbali nchini.


  Lowassa alitoa pongezi hizo leo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela uliofanyika katika Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela  na kueleza kwamba viongozi hao wamekuwa wakikemea udini na kutaka watanzania kuendelea kuilinda amani ya nchini kama mboni ya jicho kwani kuipoteza Amani tuliyonayo nchini itatugharimu maisha kuirejesha hivyo amewasihi watanzania wasichoke na Amani ambayo ni kama hewa ikitoweka haiwezi kurudi tena kamwe.

  Lowassa amewataka watanzania wote kuwasikiliza viongozi hao na kuwaunga mkono katika kukemea watu wanaotaka kuwatumia na kusababisha vurugu ili amani tuliyonayo nchini iweze kupotea kwa masilahi yao. 
  Sikiliza alichosema.... 

  Maandamano yalifanyika kutoka viwanja vya furahisha hadi Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela kwaajili ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela. 
  Hatimaye maandamano yalifika katika Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela.


  Ilikuwa ni majira ya saa 3:45 asubuhi na hii ni sehemu ya kusanyiko lililofika kanisani hapa  kwaajili ya kushuhudia uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
  Kwaya ya Anglican Nyamanoro Mwanza nayo ilihudumu kwenye ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.


  Watu wa mataifa mbalimbali nao wamekuja katika kusanyiko hili Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela kwaajili ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.


  Sambamba na tukio la uzinduzi wa vikoba lililofanyika kanisani hapa vilevile ikumbukwe kuwa siku hii ni sehemu ya Maadhimisho ya Maombezi ya kinamama duniani hivyo akinamama walifanya maombezi hayo kisha baadaye ukafuata uzinduzi uliosimamiwa vyema na mh. Lowassa.


  Ibada ya maombezi ikiendelea kanisani.


  Umoja wa akinamama wa Madhehebu ya Kikristo Mwanza ukimkabidhi zawadi Mh. Lowassa kwaajili ya mkewe ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maombezi ya Kinamama Duniani katika Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela. 


  Umoja wa akinamama wa Madhehebu ya Kikristo Mwanza pia ulimkabidhi zawadi ya Biblia Mh. Lowassa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maombezi ya Kinamama Duniani katika Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela. 


  Umoja wa akinamama wa Madhehebu ya Kikristo Mwanza pia ulimkabidhi zawadi ya Biblia Mh. Lowassa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maombezi ya Kinamama Duniani katika Kanisa la D.V.N Angilikana lililopo Nyamanoro Wilayani Ilemela.


  Aidha Mbunge huyo wa Jimbo la Monduli na Mjumbe wa NEC CCM Taifa wa Wilaya ya Monduli amewataka wanasiasa wote nchini kumuunga mkono kuiomba serikali kurudisha fedha za Mabilioni ya JK na kuhakikisha yanapelekwa moja kwa moja kwa wanawake wa vijijini walioanzisha VICOBA ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi hali ambayo itawawezesha wanawake wengi kuondokana na umasikini. 

  Sikiliza alichosema..

  Utaifa zaidi ndani ya kwaya ya kanisa la DVN.

  Aidha amewataka watanzania wote kuwasikiliza viongozi hao na kuwaunga mkono katika kukemea watu wanaotaka kuwatuawa  na kusababisha vurugu ili amani tuliyonayo nchini iweze kupotea kwa masilahi yao kamwe wasikubali hivyo ni vyema wakaungana kuwakataa kwa nguvu zote kwani hadi sasa wagombea Urais wan chi ya Kenya wanawataka wakenya kuwa kama watanzania hivyo hivyo na Waganda wamekuwa wakihubiliwa kutuiga kutokana na umoja na amani tuliyonayo hapa nchini.  Furaha ya mchungaji na mwanae.


  Katika kuuzindua mfuko wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza, Mfanyabiasha ambaye ni mkurugenzi wa Gold Crest Hotel, Bw. Mathias Manga alitoa cheki yenye thamani ya shilingi millioni 5.


  Waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa akimpa mkono wa pongezi MNEC wa Busega Bw. Raphael Chegeni mara baada ya kuwasilisha mchango wake wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Vikoba vya umoja wa wanawake wa Madhehebu ya Kikristo Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela uliofanyika katika Kanisa la D.V.N 


  Furaha. 


  Saa 6:30 mchana shughuli ya uzinduzi inamalizika na Mh. Lowassa anaondoka eneo la tukio huku akipeana mkono na waumini. 


  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mwendesha Mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa(ICC) Bibi Fatou Bensouda wakati alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa (ICC) Bibi Fatou Bensouda(Wapili kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine katika picha kushoto ni Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Bibi Angellah Kairuki(Wanne kushoto) na kulia Mwendesha Mashtaka mkuu wa Serikali Bwana Feleshi(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Na Ripota Wetu

  MWIMBAJI anayekuja juu kwenye muziki wa kiroho nchini, John Lissu ni miongoni mwa wasanii wapya watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka huu.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema jana kuwa mwimbaji huyo anakuwa msanii wa pili wa hapa nchini kutangazwa baada ya kung’ara katika upigwaji wa kura za maoni kwa mashabiki zilizoendeshwa na kamati hiyo, ambapo wa kwanza alikuwa Rose Muhando.

  “Tulimtangaza Rose Muhando na sasa tuna John Lissu, kadri mambo yatakavyokuwa tutazidi kuwatambulisha. Hawa tayari tumekubaliana nao kuwatangaza washiriki kwenye tamasha letu,” alisema.

  Kwa upande wake, msanii huyo alisema atatumia tamasha hilo kutambulisha nyimbo zake mbalimbali zilizopo kwenye albamu zake mbili ambazo ni Yehova Yu Hai na Upo Hapa alizozieleza kuwa ni moto wa kuotea mbali.

  “Hivi sasa nina albamu yangu inaitwa Uko Hapa ambayo ni moto wa kuotea mbali, nataka mashabiki wote wafurahie na waitambue siku hiyo. Hii ni mara yangu ya kwanza kupata nafasi ya kushiriki kwenye tamasha hilo, hivyo lazima niwape furaha kubwa mashabiki,” alisema msanii huyo.

  Alizitaja baadhi ya nyimbo zake zilizopo katika albamu ya Uko Hapa kuwa ni Wa Kusifiwa, Yu Hai Yehova, Fungua Macho, Uko Hapa, Hakikisha, Uko Juu, Nitakushukuru na Nijaze.

  Kabla ya albamu hiyo aliwahi kutamba na albamu ya Yehova Yu Hai iliyokuwa na nyimbo kama vile Nisimamishe, Wastahili, Tunakuabudu Bwana na Tunakushukuru.

  Tamasha la Pasaka litafanyika Machi 31 mwaka huu jijini Dar es Salaam, kasha Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

  Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

  Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

  0 0  Mshindi wa DStv Rewards, Ahmed Salim Saleh, akisaidiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake kushangilia kwa kuibuka mshindi wa Tshs, 5,000,000 alizoshinda.


  Ahmed Salim Saleh, mshindi wa Tshs, 5,000,000 za DStv Rewards akiwa na uso wa furaha huku ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa.

  Katika muendelezo wa kampeni ya DStv Rewards kampuni ya MultiChoice Tanzania inayo furaha kumtangaza rasmi mshindi wake wa tatu. Mshindi huyo ni Ahmed Salim Saleh, mfanyakazi wa Access Bank ya jijini Dar-es-Salaam.   Kupitia droo ya DStv Rewards, MultiChoice Tanzania inaibua baadhi ya wateja wao kuwa “mamilionea” ambapo katika kila wiki mteja mmoja huibuka mshindi wa kitita cha Shilingi Milioni 5. (Tshs 5,000,000)
  Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu, akiwa na mshindi wa DStv Rewards kwa wiki ya tatu, Ahmed Salim Saleh, baada ya kumkabidhi mfano wa hundi ya kitita cha Tshs. 5,000,000 alichojishindia.

  DStv Rewards ni sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania kuwashukuru wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwao.   Kampeni hiyo maalumu ilianza tarehe 5 February, 2013 na inaendelea mpaka tarehe 10 April, 2013. Wateja ambao wanakuwa na nafasi ya kuibuka “mamilionea” ni wale ambao hulipia akaunti zao za DStv kabla hazitajakatwa kwa kulipia kifurushi chochote kati ya DStv Access, DStv Family, DStv Compact, DStv Compact Plus na DStv Premium.

  0 0

   Mwakilishi wa Mji Mkongwe ambae pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF Ismail Jusa Ladu akihutubia wananchi wa Jimbo la Kwamtipura katika Mkutano wa hazara uliofanyika ktk kiwanja cha mpira kwamtipira. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 
   Mwakilishi wa Mji Mkongwe ambae pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF Ismail Jusa Ladu wakushoto akiwa na Mkurugenzi wa Habari,Uwenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF Salum Abdallah Bimani wakisikiliza kwa makini risala ya vijana wa jimbo la Kwamtipura katika mkutano wa hazara uliofanyika katika kiwanja cha mpira kwamtipura. 

  Wananchi wa Jimbo la Kwamtipura wakisikiliza kwa makini hutuba ya Mwakilishi wa Mji Mkongwe ambae pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF Ismail Jusa Ladu hayupo pichani katika Mkutano wa hazara uliofanyika huko ktk kiwanja cha mpira kwamtipira.
   

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Ulinzi na Usalama, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wazee wa Chama cha Mapinduzi, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakifurahia burudani ya ngoma ya asili, wakati walipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
  ***********************************
  MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MARA
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo jumapili Februari 3, 2013 ameanza rasmi ziara ya siku mbili ya kikazi katika mkoa wa Mara.

  Akiwa Mkoani Mara Mhe. Makamu wa Rais, anatarajia kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kufungua Barabara inayounganisha Mkoa mpya wa Simiyu na Mkoa wa Mara.

  Aidha Makamu wa Rais, atazindua rasmi Kivuko cha Mv. Musoma, kinachofanya kazi ya kusafirisha wananchi ambao ni wakazi wa Rorya na Musoma, ambapo pia atazindua mradi wa nyumba za Watumishi wa Umma, mkoani Mara na kuzungumza na wananchi kabla ya kuondoka kurejea jijini Dar es Salaam.


older | 1 | .... | 38 | 39 | (Page 40) | 41 | 42 | .... | 1896 | newer