Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 407 | 408 | (Page 409) | 410 | 411 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Wanachama wa Jumiya ya Watu wanaoishi na maradhi ya kisukari Zanzibar na wafanyakazi wa kitengo cha maradhi hayo kutoka Hospitali Kuu ya Mnazimmoja wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya kisukari Duniani yaliyoanzia viwanja vya Maisara na kumalia viwanja vya Malindi Novemba 14.
  Wanachama wa Jumuiya hiyo wakionyesha bango lenye ujumbe mahasusi wa kimataifa wa siku ya kisukari Duniani katika maandamano ya kuadhimisha siku hiyo Novemba 14.
  Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (suti nyeusi) akiyapokea maandamano ya wanajumuiya ya watu wanaoishi na maradhi ya kisukari Zanzibar katika viwanja vya Malindi Mjini Zanzibar.Picha na Makame Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Makamu wa Rais na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitoa hutuba kwa viongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam leo.
  Makamu wa Rais na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida wakiingia ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya mkutano.
  Viongozi mbalimbali wa chama hicho kuanzia ngazi ya chini wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu za Wilaya na Mkoa wakimkaribisha mgeni rasmi wa mkutano huo, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Garib Bilal (hayupo pichani).

  Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba “Gadafi” akizungumza katika mkutano huo.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, akihutubia kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dk. Bilal.
  Makamu wa Rais ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mpinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Mohamed Gharib Bilal (katikati), akizungumza na viongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam leo, kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu 2015. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
  Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
  Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonah Kaluwa (katikati), akifurahia jambo na viongozi wenzake katika mkutano huo.
  Viongozi mbalimbali wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
  Wanaccm wakiwa wamefurika ukumbi wa Karimjee 
  katika mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea.
  Wanaccm wakiwa katika mkutano huo.
   
  Dotto Mwaibale
   
  MAKAMU wa Rais ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mpinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Mohamed Gharib Bilal ametoa mwito kwa viongozi na wanachama wa chama hicho kuacha misuguano na mifarakano ili kukiepusha chama hicho na mipasuko isiyo ya lazima.
   
  Dk. Bilal alitoa mwito huo Dar es Salaam leo asubuhi wakati akiwahutubia katika mkutano uliowakutananisha viongozi mbalimbali wa chama hicho kuanzia ngazi ya chini wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu za Wilaya na Mkoa kujadili uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015.
   
  Alisema CCM ni chama pekee hapa nchini ambacho kinafanya shughuli zake kidemokrasia na ndio maana kinaendelea kushika dola na kukubalika na wananchi.
   
  Dk.Bilal alisema  katika kipindi hiki cha mchakato wa kuwapata viongozi kuelekea katika chaguzi mbalimbali kunakuwa na changamoto za hapa na pale hivyo wenye dhamana ya kuwateua wagombea wanapaswa kutenda haki kwa kumteua yule aliyepigiwa kura kwa wingi badala ya kufanya ndivyo sivyo.
   
  “Chama Cha  Mapinduzi ndio chama chenye dira na sera zinazotambulika hivyo viongozi wake wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha hakuna makundi yanayoweza kuwagawa wanachama” alisema Bilal.
   
  Alisema  viongozi wa chama hicho  wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika chaguzi zote kwani uwezo wa kufanya hivyo upo kwa kuwa chama hicho kimejipanga vizuri kuanzia ngazi ya shina na kina maadili.
   
  Bilal aliongeza kuwa kila uchaguzi unapofanyika watu na vyama vingine wanaangalia CCM imemsimamisha nani hivyo ni vizuri wakati wa uteuzi wa viongozi wanapaswa kuwa makini kwa kumchagua aliyebora.
   
  Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema wamejifunza mengi katika chaguzi zilizopita ambapo walipoteza maeneo kadhaa kwa kuchuliwa na vyama v, kwa sasa wako katika hatua za mwisho za kupata mgingine kutokana na makosa hayo.
   
  Alisema hivi sasa mwanachama yeyote atakaye shinda kura za maoni ndiye atakayekuwa mgombea katika eneo husika labda tu awe amepita kwa rushwa na mambo mengine ambayo yatathibishwa.
   
  Madabida alisema kwamba katika mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi za serikali za mitaa kulikuwa na changamoto za hapa na pale ambazo watahakikisha zinafanyiwa kazi ili mambo yaende sawa.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Stanbick jana wakati alipotembelea banda lao katika maonesho ya wadau Gesi na Oil yanayoendelea mkoani Mtwara.
  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Wilman Ndile akizungumza na Ofisa wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN, Francis Kihinga wakati walipokutana kwenye mkutano wa wadau wa gesi unaoendelea mkoani Mtwara, TSN ni moja kati ya wadhamini wa mkutano huo.
  Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye maonesho ya bidhaa za wadau mbalimbali wa madini yaliyofanyika sambamba na mkutano huo. Maonesho hayo yalifanyika katika umbi wa Mikutano wa Chuo cha Veta Mtwara wakati Mkutano wa wadau ulifanyika katika hoteli ya Naf.
  Afisa Matekelezi wa NSSF mkoani Mtwara, Jamila Mfanga akimkabidhi wa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile vipeperushi vya bidhaa zake.
  Picha na wadau.
  Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile (kushoto) akiangalia bango la mafunzo ya Chuo Kikuu Huria ambao walifungua chuo chao mkoani humo, nao walikuwa ni baadhi ya waliojitokeza kwenye maonesho hayo pia pembeni yake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Tolly Mbwete.
  Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile (kushoto) akiwaonesha baadhi ya wageni waliohudhuria mkutano wa kujadilia masuala ya gesi na Mafuta unaoendelea mkoani Mtwara, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta binafsi nchini (TPSF) Godfrey Simbeye pembeni Mwenyekito wa Bodi ya Ushauri wa Madini, Richard Kasesela.

  0 0

  MWANAMICHEZO ambaye anacheza kwa kutumia pikipiki Bian Capper kutoka nchini Afrika kusini ametoa wito kwa watanzania kucheza mchezo huo ambao mbali ya kufurahisha pia unatumia akili na kukufanya uwe mkakamavu wakati wote.
  Akizungumza jana kabla kuonesha umahiri huo mchezaji wa pikipiki ambaye ni raia wa Afrika Kusini anayefanya ziara katika nchi za Afrika kwa udhamini wa kinywaji cha Redbull atakuwa nchini kwa ziara za ya maonesho ya kuonesha namna ya kucheza na pikipiki kwa siku tatu.
   Onyesho la kwanza lilianza jana kwenye viwanja vya Coco beach , leo Jumapili atakuwa Mlimani City na kesho Jumatatu atakuwa katika eneo la Ubungo Tanesco ambako litakuwa onyesho lake la mwisho.
  Capper amesema kwamba amefurahia kuweza kufika nchini pia tayari ameshafanya maonyesho yake katika nchi za Kenya na Uganda.
  Wakati huohuo Rais wa Tanzania Motorcross Acrobatic Club Blagina Mwihava alisema kwamba wamemleta mwanamuchezo huyo ambaye wana imani kubwa ataleta msisimko mkubwa kwa vijana wa kitanzania kuweza kupata hamasa ya kucheza mchezo huo wenye mvuto. 
  “Hii itakuwa ni shoo kwa watanzania ili waweze kuvutika kucheza mcheo huu wa aina yake .Ziara ya mchezaji huyo imeratibiwa na Kampuni ya Mohans inayosambaza kinywaji cha Redbull nchini maonesho hayo yote ni ya wazi. PICHA ZOTE NA VIDEO NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.

  0 0

  Ugandan President Yoweri Kaguta Museveni delivering his Keynote speech during the 39th World Congress of Africa Travel Association (ATA) in Kampala, Uganda.Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (right) addressing the participants during the 39th World Congress of Africa Travel Association (ATA) in Kampala, Uganda. With him is the Executive Director of ATA Edward Bergman.
  High table stands during the playing of the Ugandan and EAC anthems.
  Part of the Tanzanian delegation attending the 39th World Congress of Africa Travel Association (ATA) in Kampala, Uganda. They are from left: Asantael Melita (Ngorongoro Conservation Area Authority); Philip Chitaunga (Tanzania Tourist Board); Kelvin Nkulila (Tanzania National Parks); Uzeel Kiangi; Lilian Nyaki and Imani Nkuwi from the Ministry of Natural Resources and Tourism.


  0 0


  0 0

   Mwili wa marehemu Naseli Joshua Doriye ukitolewa nyumbani kwao Africana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ibada ya mazishi.
   Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Naseli.
  Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es salaam, Prof. Joshua Doriye ambaye ni mzazi wa Naseli akiwa na mkewe wakati wa ibada ya mazishi nyumbani kwake Africana.

  0 0

  Mwakilishi wa Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA), Labhu Thakkar akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kuranga wakati walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo wilayani hapo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila na mlezi wa Kikundi cha Kiwalani Women Group ambaye pia ni mke wa mbunge wa Mkuranga, Naima Malima.
   Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akizungumza na Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA) walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, pamoja na kutembelea Zahanati ya kijiji cha Msufini Kidete. Kushoto ni mlezi wa Kikundi cha Kiwalani Women Group ambaye pia ni mke wa mbunge wa Mkuranga, Naima Malima.
   Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA), Labhu Thakkar walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, pamoja na kutembelea Zahanati ya kijiji cha Msufini Kidete. 
   Mkutano ukiendelea kabla ya wageni kutoka Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA) kutembelea Zahanati ya Kijiji cha Msufini Kidete iliyopo Mkuranga Mkoa wa Pwani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu waTanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake walipomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  

  Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya rufani Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi,daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama
  Mhe Hussein Katanga.

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.
   Rais Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kaimu Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimuapisha Dkt. Adelhelm James Meru kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 17,2014 Ikulu Dar es salaam.
  Makamu wa Rais na Kaimu Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Adelhelma James Meru wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuapishwa leo Novemba 17, 2014 Ikulu Dar es salaam.
  Makamu wa Rais na Kaimu Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Adelhelma James Meru wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya kuapishwa leo Novemba 17, 2014 Ikulu Dar es salaam.
  Makamu wa Rais na Kaimu Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Adelhelma James Meru wakiwa katika picha ya pamoja na Familia mara baada ya kuapishwa leo Novemba 17, 2014 Ikulu Dar es salaam. (Picha na OMR)

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua shamba lililofadhiliwa na TASAF
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaidiana kuweka tofali pamoja na Mkuuwa wilaya ya Kilwa Abdalla Ulega wakati wa kushiriki ujenzi wa nyumba ya mganga.


  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendesha katapila wakati wa kushiriki ujenzi wa barabara ya Kwa Mkocho mpaka Kivinje.
  Eneo linalovunwa chumvi Miina Kilwa Masoko.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki uvunaji wa chumvi Miina Kilwa Masoko
  Ndugu Said Timamy (kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kiwanda cha chumvi cha Mishindo Salt Works kilichopo Miina Kilwa Masoko.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mavuji wanaojishughulisha na mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa matone umefadhiliwa na TASAF.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia chanzo cha maji ya mto Vuji yatakayotumika kumwagilia  .

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali baada ya kuwatembelea vijana wa kikundi cha ujasiriamali cha Majalala kilichopo Mnazi Mmoja Kilwa.


  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mnazi mmoja Kilwa kabla ya kushiriki ujenzi wa ofisi ya tawi.
  Katibu Mkuu wa CCM akishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi Mnazi Mmoja Kilwa.
  Hili ndo jiwe la msingi lililowekwa na Baba wa taifa mwaka 1987, jengo hili lilisimama mikaka mingi kutokana na matatizo ya umiliki wa kiwanja lakini sasa CCM imepata uhalali wa kumiliki eneo na ujenzi kuendelea.
  Kikundi cha ngoma ya Ngongoti kikitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa CCM mjini Kilwa Masoko.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Kilwa Masoko.
  Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa Bustani ya Mkapa Kilwa Masoko.
  Mwananchi akishangilia jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa Masoko kwenye uwanja wa Bustani ya Mkapa.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kilwa Masoko ambapo aliwaambia kuwa wapinzani hawasemi ukweli unaoendelea kwenye vyama vyao havisemi kama vimekufa.


  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa akitoa salaam zake kwa wana CCM wa Kilwa Masoko kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa Bustani ya Mkapa.
  Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdala Ulega akimpa mkono wa pongezi Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa baada ya kutoa darasa zuri kwa wananchi wa Kilwa Masoko.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kilwa Masoko ambapo aliwaambia watendaji wa serikali kutoa elimu ya kuwafahamisha wavuvi kabla ya kuchukua maamuzi ya kuchoma vifaa vyao vya kazi,pia aliwaambia wananchi hao kuwa Chama Cha Mapinduzi kitajirekebisha makosa yake na kuhakikisha kinashinda kwa kishindo kwenye chaguzi zijazo kwani jimbo la kusini Kilwa limepotea kutokana na migongano ndani ya CCM, hivyo basi uchaguzi ujao tujipange vizuri na kurudisha jimbo.
  Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na kijana wa Kilwa baada ya kumaliza mkutano wake.
  Wananchi wa Kilwa Masoko wakipiga picha na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Bustani ya Mkapa Kilwa Masoko.


  0 0

  Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi ( wa nne kutoka kushoto waliosimama mbele); Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege ( wa tatu kutoka kushoto waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
  Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege (kulia) akitoa maelekezo kwa baadhi ya wawasilishaji mada katika mafunzo yanayoshirikisha maafisa mazingira katika mikoa ya Iringa na Mbeya yanayofanyika jijini Mbeya leo. Lengo la mafunzo hayo ni kuwashirikisha mpango kazi wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na kupata michango yao. Kushoto ni Meneja wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Nyanda za Juu Kusini David Elias. Katikati ni Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Abdullatif Nassor.
  Afisa Misitu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Theodore Silinge akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
  Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege (kulia) akielezea shughuli za Kitengo chake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi ili aweze kufungua mafunzo hayo.
  Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa madini hotuba iliyokuwa inawasilishwa na mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi (hayupo pichani).
  Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi (katikati) akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo.


  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu Lusius Mwenda kutoka Wizara ya Nishati na Madini akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya jinsi ya kuandaa mapendekezo ya miradi, sera pamoja na utekelezaji wake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Bagamoyo. Mafunzo hayo yalishirikisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi (TDGC)
  Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji wa mafunzo hayo iliyokuwa inatolewa na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu Lusius Mwenda (hayupo pichani).
  Afisa Rasilimaliwatu kutoka Idara ya Utawala Judith Ntyangiri akipokea cheti cha ushiriki mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
  Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu Lusius Mwenda kutoka Wizara ya Nishati na Madini ( wa nne kutoka kulia waliosimama mbele) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki waliohitimu mafuzo hayo.

  Na Greyson Mwase, Bagamoyo

  Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini wametakiwa kuboresha ufanyaji wa tathmini ya mapendekezo ya miradi (project proposal) ya Wizara kwa uwazi kwani ina mchango mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo.

  Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Lusius Mwenda, alipokuwa akifunga awamu ya kwanza ya mafunzo ya jinsi ya kuandaa mapendekezo ya miradi, sera pamoja na utekelezaji wake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Bagamoyo. Mafunzo hayo yalishirikisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi (TDGC)

  Mbali na kufunga awamu ya kwanza ya mafunzo hayo, Mwenda alikabidhi vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo kwa washiriki 20. Awamu ya pili ya mafunzo hayo inayoshirikisha washiriki 20 inaendelea ambapo washiriki wanajifunza juu ya uandaaji wa sera na awamu ya tatu itakayofanyika itashirikisha washiriki 20 ambao pia watajifunza juu ya usimamizi wa miradi.

  Mafunzo hayo yanatolewa na kampuni ya Petrogas yenye makazi yake jijini Dar es salaam ikiwa ni pamoja na nchi nyingine duniani Mwenda alisema kuwa maandalizi ya mapendekezo ya miradi ni muhimu sana katika utekelezaji wa miradi ya Serikali na kusisitiza kuwa iwapo tathmini ya mapendekezo ya miradi haitafanyika kwa ufanisi inaweza kuchangia miradi kufanyika katika kiwango cha chini au kutokamilika kwa wakati.

  Alisema kuwa Serikali imekuwa ikiandaa mapendekezo ya miradi kwa kushirikisha wataalamu kutoka nje kwa gharama kubwa na kusisitiza kuwa ili kuondokana na changamoto hiyo, Wizara iliamua kuandaa mafuzo hayo kwa wataalamu wake ili kuhakikisha kuwa kazi hiyo inafanywa wa wataalamu wake wa ndani.

  “Mbali na wataalamu kuandaa mapendekezo ya miradi mbalimbali, pia ninaamini mafunzo haya yatawawezesha wataalamu hao kufanya tathmini ya mapendekezo ya miradi yanayoandaliwa na wataalamu kutoka nje wanaoomba kufanya kazi na Wizara katika utekelezaji wa miradi yake.” Alisema Mwenda

  Mafunzo hayo yameandaliwa na mradi unaohusika na kuwajengea uwezo wataalamu wa nishati na tasnia ya uziduaji (CADESE; Capacity Development  in the Energy Sector & Extractive Industries) lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wataalamu kutoka sekta za nishati na madini katika uandaaji wa mapendekezo ya miradi mbalimbali ( project proposals) na sera na hivyo kuepusha gharama ya kutumia wataalamu kutoka nje na kukuza umiliki.

  Mradi wa CADESE unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Maendeleo (UNDP) ulianzishwa mwaka huu unatekelezwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na wadau wengine kama vile Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Taasisi ya Uongozi na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).


  0 0

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Job Ndugai akikabidhi Ripoti maalumu ya  CAG Kuhusu akaunti ya ESCROW kwa Mwenyekiti wa PAC Mhe. Zitto Kabwe na Kaimu wake Mh. Deo Filikunjombe,Bungeni mjini Dodoma leo.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Job Ndugai akikabidhi Ripoti maalumu ya  CAG Kuhusu akaunti ya ESCROW kwa Mwenyekiti wa PAC,Mhe. Zitto Kabwe 
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Job Ndugai akiwa ameshikilia vitambu vilivyo Beba ripoti ya CAG kuhusu akaunti ya ESCROW Kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa PAC Mhe.Zitto Kabwe leo.Picha na Deusdidus Moshi,Globu ya JAmii Kanda ya Kati.

  0 0

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) imeandaa tamasha kubwa la kuadhimisha miaka kumi (10) kutoka uanzishwe mwaka 2004 kwa michezo mbalimbali ukiwemo mpambano wa maveterani wa watani wa jadi  Simba na Yanga litakalofanyika kilele cha sherehe hizo uwanja wa Karume,Dar es Salaam Desemba 25,(Krismasi) mwaka huu.

  Mwenyekiti wa SHIWATA,  Cassim Taalib alisema katika wiki ya maadhimisho hayo, Desemba 24 sherehe hizo zitatanguliwa na ugawaji wa nyumba 38 zilizojengwa na wanachama wa SHIWATA kwa njia ya kuchangiana na kufikisha idadi ya jumla ya nyumba 104 ambazo mpaka sasa zimekwisha jengwa katika kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga chenye ekari 300 kwa ajili ya makazi.

  Alisema ili kuwavutia wenye nyumba hizo wahamie kijijini, SHIWATA imetoa eneo maalumu kwa ajili ya kulima bustani ya mboga mboga na mazao ambayo si ya kudumu ili wajikimu wao wenyewe na familia zinazowazunguka.

  Alisema SHIWATA unaomiliki shamba la ekari 500 katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga unasimamia usafishaji wa shamba hilo kutumia mtambo wa kisasa (bulldozer) lililokodishwa kutoka Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam kwa gharama ya sh. mil. 22 kwa siku 20 kukamilisha kazi hiyo.

  Alisema Bulldozer hilo limefikisha siku kumi sasa kutoka kazi ya kusafisha shamba hilo na kung’oa visiki  ianze, wanachama 90 waliomilikishwa sehemu ya shamba kwa lengo la kulima mazao yanayostawi eneo hilo, wameanza kuchangia gharama za kusafisha shamba hilo.

  Mwenyekiti huyo alisema mazao yanayostawi eneo hilo ni mpunga, mahindi, mbaazi, viazi vitamu, ndizi, kunde, korosho, mtama na matunda kama embe, machungwa, matikiti maji na mafenesi.

  Alisema pia kuwa sherehe za maadhimisho hayo zitawakutanisha wakongwe wa soka wa Simba na Yanga ambao ni wanachama wa SHIWATA wamekubali kushiriki mpambano huo.

  Kwa upande wa Yanga, mchezaji wa zamani wa Klabu hiyo, Mtwa Kiwhelo na Athumani Juma Chama kwa upande wa Simba wanawawakilisha wenzao katika maandalizi ya awali ya mchezo huo.

  SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000 kutoka fani mbalimbali za sanaa za maigizo, mpira wa miguu, mpira wa wavu, netiboli, waigizai wa filamu, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, vijana na waandishi wa Habari kila kundi litapewa nafasi ya kuonesha vipaji vyao siku hiyo.

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi wa Shule za St Mary's, mama Getrude Lwakatare akizungumza na wanafunzi wa Shule za St Mary's International za Dar es Salaam wakati akizundua tamasha la kuonyesha vipaji vya wanafunzi wa Shule za St Mary's International za Dar es Salaam lililofanyika mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.PICHA NA PHILEMON SOLOMON
   Mwalimu wa Shule ya St Mary's International, Eric Sendi akiwaasa wanafunzi waandelee kuonyesha vipaji vyao.
   Mkurugenzi wa Shule za St Mary's, mama Getrude Lwakatare (kushoto), akikabidhiwa baadhi ya Peni na Meneja Masoko wa Kampuni ya SILAFRICA, Salman Pathan kama mchango wake kwaajiliya shule za St Mary's International.
   Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania House of Talent (THT), Mwita Mwaikenda akitoa neno la shukrani kama wadhami wa tamasha hilo.
   Mkurugenzi wa Shule za St Mary's, mama Getrude Lwakatare (wakwanza kulia), akiwa na Walimu wa shule hizo wakifuatilia burudani wakati wa tamasha hilo.
   Wanafunzi kutoka shule za St Mary's International za Dar es Salaam wakiwa kwenye tamasha hilo.
   Wanafunzi kutoka shule za St Mary's International za Dar es Salaam wakitoa burudani wakati wa tamasha la kuonyesha vipaji.

  0 0

   Baadhi ya wajumbe wa kikao cha ushauri cha Mkoa wa Manyara, (RCC) wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika jana mjini Babati na kuongozwa na Mkuu wa mkoa huo Elaston Mbwilo.
   Ofisa elimu wa Mkoa wa Manyara, Ibrahim Mbang'o na baadhi ya wajumbe wakifuatilia jambo kwenye kikao cha ushauri cha mkoa huo (RCC) kilichofanyika jana mjini Babati.
  Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara, Christina Mndeme (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Anatory Choya, wakiwa kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo (RCC) kilichofanyika jana mjini Babati.

  0 0

  Picha Na 3 (1)
  Na Greyson Mwase, Mbeya
  Maafisa Mazingira katika   wilaya zilizopo katika mikoa ya Iringa na Mbeya wametakiwa kuacha kuwabembeleza wawekezaji wasiozingatia sheria za uhifadhi wa mazingira.
  Kauli hiyo imetolewa na  Kaimu Katibu  Tawala Mkoa wa Mbeya , Constantine Mushi wakati akifungua mafunzo  ya siku  tano yaliyoshirikisha maafisa mazingira kutoka katika wilaya  14 za mikoa ya Iringa na Mbeya ikiwa ni pamoja na  Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)  na Ofisi ya  Mkemia Mkuu wa Serikali.
  Mushi alisema kuwa   wapo baadhi ya wawekezaji katika sekta za madini na nishati wasiozingatia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 inayotaka shughuli yoyote ya maendeleo  kuendana na uhifadhi wa mazingira na hivyo kuchangia uharibifu mkubwa wa mazingira.
  Alisema kuwa maafisa mazingira wanatakiwa kusimamia  sheria za mazingira kwa kuhakikisha kuwa zinafuatwa ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali wawekezaji wasiozingatia sheria hizo.
  Alisema kuwa katika sekta ya nishati kuna shughuli za utafutaji  wa mafuta na gesi unaoendelea sehemu mbalimbali nchini  katika  nchi kavu, kwenye  ukanda wa bahari, katika maji ya kina kirefu baharini (deep sea) na kwenye maziwa na kusisitiza kuwa hii ni  changamoto kwa maafisa mazingira katika kutoa ushauri na kuhakikisha kuwa binadamu  na viumbe wengine hai hawaathiriwi na uwekezaji huu.
  Alieleza kuwa uwekezaji katika sekta ya nishati ni mkubwa sana kwani nishati ya umeme ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo suala la mazingira linatakiwa lizingatiwe ili kuhakikisha kuwa wananchi na  viumbe wengine hawaathiriwi na uwekezaji huu.
  Aliongeza kuwa uwekezaji katika sekta ya madini  katika miaka ya karibuni  umekua kwa kasi kubwa sana lengo lake likiwa ni kuleta maendeleo na kusisitiza kuwa shughuli za uchimbaji madini zisipofuata kanuni na  sheria za mazingira zinaweza kuacha nchi ikiwa jangwa na kuathiri mabadiliko ya tabia nchi.
  “Ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa shughuli zote za maendeleo zinafanyika bila kuleta athari kubwa katika mazingira yetu kwa kusimamia sheria na kanuni za mazingira pasipokuwa na upendeleo,” alisisitiza Mushi.
  Alisema kuwa kuzingatia hitaji  la sheria ya mazingira, Wizara ya Nishati na Madini  imeandaa mpango kazi wa mazingira wa sekta za nishati na madini (sector environmental action plan) ambao utekelezaji wake utaenda hadi katika ngazi ya wilaya.
  Wakati huo huo Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara  ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege alisema lengo la mafunzo hayo  ni kuwashirikisha  maafisa mazingira mpango kazi wa mazingira  wa sekta za nishati na madini  wa Wizara,  kuwapa elimu ya mazingira  na kupata michango yao ili kuwa na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha kuwa sheria na kanuni za mazingira zinafuatwa.
  Mhandisi Kasege alisema kuwa awamu ya kwanza ya mafunzo hayo yalishirikisha mikoa ya Kanda ya Pwani kama vile Dar es Salaam, Tanga, Mtwara,  Morogoro na Kilimanjaro, awamu ya pili katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Simiyu,  Geita, Mara, Kigoma na  Tabora na kuongeza kuwa awamu ya tatu inahusisha mikoa ya Iringa na Mbeya.
  Alisema kuwa mafunzo haya ni endelevu na kusisitiza kuwa mikoa iliyobaki kama Katavi,  Rukwa, Njombe, Ruvuma, Dodoma, Arusha ambayo bado haijafikiwa itashirikishwa katika awamu ya nne.
  Alieleza kuwa mpango huo wa miaka mitano ulioanza mwaka 2011 unatarajiwa kukamilika mwaka 2016.
  Naye Kamishna Msaidizi wa Madini  Kanda ya Kusini Magharibi  Wilfred Machumu alisema kuwa mafunzo hayo yatatumika kama fursa ya maafisa mazingira kubadilishana uzoefu na changamoto katika usimamizi wa mazingira na hatimaye kupata mkakati wa pamoja wa kuboresha usimamizi wa mazingira.

  0 0

   
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi saruji kwa ajili ya kusakafia soko.
   Katibu Mkuu wa CCM akifungulia maji kama ishara ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Namkongo.
   Mbunge wa Jimbo la Mchinga akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa Namkongo
   Katibu mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha maji Bi.Rehema Anafi mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika  kijiji cha Namkongo wilaya ya Lindi Vijijini.

   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ,Mbunge wa Jimbo la Mtama na mlezi wa wilaya Kilwa na Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Bernard Membe akiwasalimia wakazi wa Milola waliojitokeza kwa wingi kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman.

   Umati wa watu ukimsikiliza mbunge wao Said Mtanda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Milola ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
   Mbunge wa Jimbo la Mchinga Ndugu Said Mtanda akihutubia wakazi wa Milola ambapo aliwaambia asilimia kubwa za ahadi zake zimetimia.


   Msanii wa sanaa ya mashairi  Farida rajabu akiimba utenzi maalum wa mkoa wa Lindi.
   Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinunua kashata kwenye soko la kijiji cha Namkongo, wengine pichani ni Mkuu wa wilaya ya Lindi vijijini Dkt. Hemid Nassoro (kulia),Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mbunge wa jimbo la Mchinga Ndugu Said Mtanda (kushoto).
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kukagua tenk la maji kijijini Namkongo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini mbunge wa Jimbo la Mchinga Ndugu Said Mtanda wakati wa mkutano na wananchi wa Kilangala.
   Katibu mkuu akipitia taarifa mbali mbali za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Kilangala ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM ina viongozi bora na shupavu hivyo wasiwe na wasiwasi wajitokeze kwa wingi kupiga kura wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kilangala na kuwataka wazidi kushikamana na CCM kwa maendeleo ya baadae.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli kwa viongozi wa matawi kata ya Kilangala.
   Jiwe la msingi la ofisi ya CCM Tawi la Kilanga
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Mchinga II wakati wa kukagua na kushiriki ujenzi wa zahanati ya Mchinga II
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Michee ambapo aliwataka wananchi kuweka mkazo kwenye elimu za watoto kwani elimu ndio urithi pekee kutoka kwa mzazi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wakati akiingia kwenye uwanja wa mikutano Milola.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Milola, wilaya ya Lindi Vijijini ambapo aliwaambia
   Wananchi wakiwa mkutanoni Milola.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Milola jimbo la Mchinga ambapo aliwaambia wapinzani wamekosa sera mbadala matokeo yake wamekuwa wakitumia muda mwingi kuishambulia CCM
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuwakabidhi vyeti vya kuhitimu mafunzo ya kuendesha boda boda.
  Wananchi wa Milola wakiomba kupatiwa kadi za uananchama wa CCM kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mchinga Ndugu Said Mtanda wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika Kitomanga  Mkwajuni jimboni hapo wilaya ya Lindi vijijini.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa jimbo la Mchinga waliojitokeza kumpokea.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza wimbo maalum wa mapokezi kutoka kikundi cha uhamasishaji cha CCM Mchinga mara baada ya kuwasili Kitomanga Mkwajuni jimbo la Mchinga.
   Katibu Mkuu wa CCM akishiriki ujenzi wa ghala la kijiji ambalo litatumika kuhifadhia chakula kwa wakazi wa Kitomanga Mkwajuni

   Wananchi wa kijiji cha Namkongo wakimpokea Katibu mkuu wa CCM kwa namna yake mara baada ya kuwasili kijijini hapo ambapo alizindua mradi wa maji na kukabidhi saruji kwa ajili ya ujenzi wa soko.

   Mbunge wa Mchinga  Ndugu Said Mtanda akisoma taarifa ya mradi wa maji kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
   Kila mtu wa kijiji cha Namkongo alikuwa na shauku ya kumuona Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
   Mbunge wa Mchinga Said Mtanda akishiriki kuimba kwaya ya Kikundi cha Changamoto wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana  katika jimbo la Namkongo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mbunge wa Jimbo la Mchinga  Ndugu Said Mtanda  namna wananchi wa kijiji cha Namkongo walivyopata tabu ya kutafuta maji
   Wananchi wa Namkongo walipata shida ya kutafuta maji hii picha inaonyesha aina ya visima ambavyo wananchi walitegemea kupata maji.

   Wananchi wakisoma vitabu vinavyoelezea utekelezaji wa ilani pamoja na ahadi za CCM  katika kijiji cha Mchinga II vilivyoandaliwa na Mbunge wao Said Mtandaolder | 1 | .... | 407 | 408 | (Page 409) | 410 | 411 | .... | 1897 | newer