Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 406 | 407 | (Page 408) | 409 | 410 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Dear Friends, African community in Germany, Metta community worldwide,

  My Daddy - Mr Andrew Babot Asuwan - AKA - nyung-boy, daddy cool, Papa de Papa left us on Friday, 11 -11 -2014. The Ambassador of the Rep. of Kamerun -H.E Jean Marc Mpay in Berlin - Germany sends condolence, The Lord Major of Tübingen - Boris Palmer sends his condolence. 
   
  The Cameroonian, African community in Reutlingen / Tübingen joins Enie in organizing a wakekeeping on Saturday 29th in Reutlingen / Tübingen Venue and program to be communicated.
  "A great man remains great, for he shall always be remembered about how is life impacted his community" Africans most hidden Heros are our fathers & mothers, though no one writes about them, nor wave their flags, their footprints will never disappear, NYUNG-BOY ALIVE FOREVER!

  May God rest him in Peace

  Sincerely yours

  Susan Enie Tatah  -  Daughter!

  0 0

  Pichani juu na chini ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Dkt.Seif Rashid akizungumza wakati wa kuzindua kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee  akizungumza katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto akifafanua jambo kwenye kongamano la tisa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na Waandishi wa habari lililofanyika leo katika moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani humo,ambapo kauli mbiu ya Kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.
  Mkuu wa Wilaya ya Iramba,Mh.Yahya Nawanda akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari kuhusiana na mmpango mzima wa wananchi wake kutumia bima ya Afya,na pia alifafanua kuhusiana na mikakati mbalimbali anayotumia kuwahamasisha wananchi wake katika suala zima la kuhakikisha kila mtu anakua Bima ya Afya
  Pichani ni Mganga Mkuu wa hospitali ya Singida,Dkt.Doroth Bwajima (RMO),akizungumza mbele ya wanahabari na wadau wengine walioshiriki kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani Dodoma kuhusiana na mada yake iliyohusu Matumizi ya Fedha za Uchangiaji (NHIF,CHF,PAPO KWA PAPO).kongamano hilo limeandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee na pichani kati ni Mgeni rasmi Waziri wa Afya,Mh.Dkt Seif Rashid wakifuatilia na kusikiliza kwa makini baadhi ya maswali na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiulizwa na washiriki wa Kongamano hilo.
  Baadhi ya Wakuu wa Wilaya kutoka wilaya mbalimbali walioko mezani mbele wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kongamano hilo la tisa la NHIF,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Afya,Mh.Dkt Seif Rashid ndiye aliyezindua kongamano hilo lililohudhuriwa na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.

  0 0

  1
  Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo akiongea na wahusijka wa Kampuni ya Kajala Entertainment wakati alipofanya nao mkutano leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapa Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu ya Mbwa Mwitu.
  2q
  3
  4
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajala Entertainment, Kajala Masanja akiweka sahihi ya kukubali kufanya marekebisho katika filamu yake pamoja na malipo ya faini mbele ya Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania wakati aliitikia wito wa Ofisi ya Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelezwa juu ya Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu yake ya Mbwa Mwitu.
  5
  Meneja ambaye pia ni Mratibu wa Kampuni ya Kajala Entertainment, Bi. Leah Mwendamseke akiweka sahihi katika fomu maalum ya kukubali kufanya marekebisho katika filamu iliyokaguliwa na Bodi hiyo mbele ya Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania wakati aliitikia wito wa Ofisi ya Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelezwa juu ya Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu ya Mbwa Mwitu.
  6
  Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo akiagana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajala Entertainment wakati alipofanya naye mkutano leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapa Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu ya Mbwa Mwitu.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM)
   
  Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
  BODI ya Filamu Tanzania imezitaka Kampuni za filamu nchini kufuata Sheria na Kanuni mbalimbali wakati wa kutengeneza filamu ili kuepusha ukiukwaji wa Sheria na Kununi.
   
  Rai hiyo imetolewa leo na Katibu wa Bodi hiyo, Bi Joyce Fissoo wakati alipofanya mkutano na Kampuni ya Kajala Entertainment ambapo mnamo Septemba 22, mwaka huu ilikagua Filamu fupi ya kampuni hiyo iliyopewa jina la Mbwa Mwitu yenye dakika 12 na kubaini baadhi ya makosa.
   
  Akiongea wakati wa mkutano na wadau wa kampuni hiyo, Bi Fissoo alisema kuwa Bodi iliielekeza Kajala Entertainment kuifanyia marekebisho filamu hiyo katika dakika ya 7 ambapo ilionekana wanawake wakidhalilishwa na kubakwa kinyama na pia katika dakika ya 11 ambapo ilionyesha wizi na uvamizi.Alisema kuwa, wahusika walielekezwa kufanya marekebisho hayo kwa kuondoa vipande husika na baada ya kufanya marekebisho hayo waliwasilisha Bodi ya Filamu nakala ya filamu iliyokuwa imefanyiwa marekebisho yenye dakika 12 na kupewa kibali namba 4261 ya tarehe 24 Septemba, 2014.
   
  Bi Fisso aliongeza kuwa, mnamo tarehe 25 Septemba, 2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, filamu hiyo fupi ilionyeshwa bila ya kuzingatia marekebisho yaliyokuwa yameelekezwa kwa mujibu wa Sheria kwa kuzingatia kifungu cha Sheria cha 19 (2) (a).
  “Baada ya ukiukwaji wa Sheria katika kifungu cha 19 (2) (a) na kile cha 24 (i), (m) na (n) vya Kanuni za Sheria ya Filamu husika, wahusika waliitwa mara mbili kufika Bodi ya Filamu lakini hawakufanya hivyo, lakini baada ya kumbushio na kalipio wahusika baadaye walifika Ofisi za Bodi katika kikao cha tarehe 13 Novemba mwaka huu”, alisema Bi. Fissoo.
   
  Alieleza kwamba, wahusika walikiri kuwa walipata ujumbe wa wito wao wa kuitwa na Bodi hiyo ambapo Mratibu wa masuala yote ya Kampuni ya Kajala Entertainment, Bi. Leah Mwendamseke aliieleza Bodi kuwa anaomba asamehewe kwa kuwa walikuwa na shughuli nyingine mbalimbali.
   
  Naye Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Kajala Massanja aliiomba radhi Bodi ya Filamu Tanzania huku akisema kuwa mara nyingi yeye huwa amekuwa akiwaachia wsaidizi wake kutekeleza majukumu ya kampuni yake ingawa yeye kama mmiliki wa kampuni hiyo anawajibika moja kwa moja.
   
  Aidha, Bodi iliitaka Kajala Entertainment kueleza sababu ya kukiuka maelekezo ya Bodi ambayo yalikuwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake licha ya mtunzi na mwandishi wa musuada na muongozaji wa filamu hiyo, Bi. Leah Mwendamseke alijitetea kuwa alifanya utafiti na kukutanana vijana mbalimbali waliowahi kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
   
  Hata hivyo, Leah Mwendamseke alishindwa kuoanisha uhalisia wa matokeo ya utafiti wake na ujenzi wa visa vya hadithi ya filamu ambayo inaweza kupeleka ujumbe chanya kwa jamii, huku wahusika wakieleza kwamba lengo lao kubwa lilikuwa ni kuelimisha jamii kuhusu maovu yanayotokea na namna ya kuyaepuka ambapo mtunzi huyo aliahidi kurekebisha vipengelee husika katika filamu hiyo ili kuwa na filamu bora.
   
  Kwa upande wake Mwakilishi toka Ofisi ya Makao Makuu ya Polisi Tanzania, Sylivester Mganga aliushauri uongozi wa Kajala Entertainment kufuata maelekezo na kuzijua Sheria mbalimbali zinazohusu mambo ya filamu kwa kuvishirikisha vyombo vya ulinzi na usalama kabla ya kujichukulia maamuzi ya kutengeneza filamu zenye kutishia amani ya nchi.
   
  Bodi ya Filamu Tanzania imetoa onyo kali kwa wahusika kwa kutengeenza filamu zenye kuonyesha ama kukuza uhalifu na udhalilishaji bila kuainisha mkondo wa Sheria licha ya msamaha kutokana na kosa hilo ambapo Bodi hiyo imeitaka kampuni hiyo ilipe faini ya shilingi milioni moja kwa mujibu wa kifungu cha 47 (2) (a) cha Kanuni za Sheria ya Filamu ambayo wahusika waliridhia adhabu hiyo.

  0 0


  unnamed1 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya kinyago Mwakilishi Mkazi wa UNIDO  nchini aliyemaliza muda wake, Bw. Emmanuel Kalenzi ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu kuaga Novemba 13, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0


  Wafanyakazi wa bustani wakihudumia moja kati ya bustani zinazotunzwa na Benki ya Exim jijini Dar es Salaam jana. Benki hiyo imekua ikihudumia bustani mbalimbali zilizopo jijini Dar es Salaam, mpango unaoendana na kampeni ya benki hiyo ya ‘Go Green Initiative’ inayohimiza utunzaji wa bustani mijini na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

  Katika juhudi zake za kuendelea kupendezesha jiji la Dar es Salaam, Benki ya Exim Tanzania inalenga kupanua zaidi msaada wake utakaopelekea benki hiyo kuhudumia bustani mbalimbali zilizopo katika jiji la Dar es Salaam. Benki hiyo, kwa kupititia kampeni yake ya kupendezesha jiji la Dar es Salaam iliyozinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwaka 2012, inatoa mchango mkubwa katika kuhudumia bustani zilizopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.

  “Benki inahudumia jumla ya bustani tatu zilizopo katika maeneo tofauti jijini, ambazo ni pamoja na Bustani ya Ohio, Clock Tower, na Kariakoo. Hadi hivi sasa, bustani nyingi zinazohudumiwa na benki yetu zimekuwa zikiwavutia watu wengi na  hili limetupa ari zaidi ya kuzifikia bustani nyingine katika jiji hili,” alisema Afisa Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Dinesh Arora.

  “Dar es Salaam ni kitovu cha biashara cha Tanzania; hii inapelekea uwepo wa wageni wengi wanaotembelea jiji hili. Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2013, Tanzania ilipokea zaidi ya watalii milioni moja, ambapo wengi wao walipitia jiji la Dar es Salaam.

  “Kwaio mchakato wa kupendezesha jiji unaofanywa na Benki ya Exim umelenga kusaidia harakati za serikali kuinua na kuboresha muonekano wa jiji kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi,” alibainisha.

  0 0

  DSC_0062
  Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Bw. Mike Seo wakibadilishana nyaraka za makubaliano hayo yaliyofanyika ofisi za UNESCO.

  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetiliana saini mkataba na kampuni ya elektroniki ya Samsung ya ujenzi wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan, Loliondo. Makubaliano hayo yalitiwa saini hivi karibuni kati ya Mwakilishi mkazi Unesco nchini Bi. Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Bw. Mike Seo katika hafla iliyofanyika ofisi za UNESCO.

  Kijiji hicho kitakuwa na shule yenye Tehama ikiwa na maunganisho ya intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha teknolojia ya mawasiliano yenye kuwezesha utabibu (telemedicine) na jenereta linalotumia nguvu za jua kwa ajili ya kijiji hicho.

  Utiaji saini huo ulioshuhudiwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, bi. Leah Kihimbi kutoka wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo na Dkt. N. Iriya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dar es Salaam na wafanyakazi wa UNESCO. Katika hafla hiyo Bi. Rodrigues amesema kwamba mradi huo utawezesha UNESCO kuwapatia vijana wa Kimasai elimu kutokana na ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji wamekuwa wakipata shida ya kupata elimu.
  DSC_0002
  Baadhi ya wafanyakazi wa UNESCO na Samsung wakifuatilia kwa umakini hafla hiyo fupi ya kutiliana saini makubaliano baina ya Samsung Tanzania na UNESCO.

  “Kupitia kijiji hiki vijana wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo yao”, alisema Bi. Rodrigues. Naye Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania miongoni mwa manufaa makubwa yatakayopatikana katika mradi huo wa kijiji cha digitali huko Loliondo ni kuweza kupata nishati rahisi na iliyo rafiki kwa mazingira.

  Alisema kwamba Afrika imekuwa mstari wa mbele katika uanzishaji wa vijiji vya digitali. Aidha kwa kitendo hicho Afrika inaonesha dunia ni kwa namna teknolojia inaweza kutumika kuleta mabadikliko chanya yanayotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi waliopo vijijini.
  Bi Leah Kihimbi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya habari,vijana, utamaduni na michezo, alisema kupitia vijiji vya digitali itawezekana kutekeleza program ya elimu kwa watu wanaoishi Loliondo huku tamaduni zao zikihifadhiwa.

  Kijiji hicho cha Loliondo kitakuwa cha nne katika vijiji vya kidigitali barani Afrika. Inatarajiwa kwamba kijiji kingine kitajengwa mjini Zanzibar kwa ushirikiano wa UNESCO na Samsung Electronics mwaka 2015.
  Untitled 1
  Pichani ni muonekano wa mchoro wa kijiji hicho utakavyokua.

  0 0

  1
  Kituo cha Kisasa cha Uchunguzi na Matibabu ya magonjwa ya binadamu kinachojengwa katika Chuo Kikuuu cha Dodoma (UDOM)  kikiwa katika hatua za mwisho mwisho za kukamilika.

  Kituo hiki kitahudumia wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya jirani ya na mkoa wa Dodoma na kinajengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kwa gharama ya shilingi Bilioni 36 ambazo zimetolewa na mfuko huo kwa  silimia 100.

   Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali wanaohudhuria kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya linalofanyika kwenye hoteli ya Dodoma mjini humo walipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

  Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Mlacha Shaaban amesema “Kituo hiki kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya uchunguzi na utafiti  pia kitatoa wataalamu kutoka katika kitivo cha afya cha Chuo kikuu cha UDOM na wataalamu watakaofanya kazi katika kituo hicho watakuwa wakifundisha wanafunzi na kuhudumia wagonjwa. Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo Januari 2015"
  2
  Jengo la kituo cha Utafiti na tiba cha UDOM kinachojengwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF.
  3
  Kaimu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha UDOM Profesa Mlacha Shaaban akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali walipotembelea ujenzi wa kituo cha Tiba na Utafiti kinachojengwa katika chuo kikuu cha UDOM.
  4
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamotoakizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo hicho
  5
  Waandishi wa habari wakisubiri kupata  maelezo ya kituo hicho.

  0 0

  Bondia Thomasi Mashali kushoto akitia saini ya kupigana na Abbdallah Pazi kulia baada ya makubaliano na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa friends corner manzese Dar es salaam .
  Bondia Abbdallah Pazi kulia akitia saini ya kupigana na Thomasi Mashali kushoto baada ya makubaliano na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam.
  Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi  ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam.
  Promota Kassim Texas katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Abdallah Pazi kuashilia makubaliano ya mpambano wao utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese .
  Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi  ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa Picha na SUPER D BLOG.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari kuhusiana na mpango mzima wa wananchi wake kutumia bima ya Afya,na pia alifafanua kuhusiana na mikakati mbalimbali anayotumia kuwahamasisha wananchi wake katika suala zima la kuhakikisha kila mtu anakua Bima ya Afya,lakini pia alieleza kuwa Wilaya yake ya Igunga ina vijiji 98,vijiji 78 vimejengwa zahati,lakini mpaka sasa zahanati 31 hazijasajiliwa,hivyo ameiomba Serikali kupitia wizara ya Afya kuhalakisha suala la usajili wa zahanati hizo katika kuwasaidia wananchi.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee  akifafanua jambo katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo Dodoma hotel,ikiwa ni siku ya pili ya hitimisho la Kongamano hilo,Kauli mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kongamano hilo lilizinduliwa jana na Waziri wa Afya Dkt Seif Rashid,ambapo pia Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.
  Mmoja wa Maofisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),Bi.Gaudensia Semwanza akifafanua jambo  katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.   
    Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athman Rehani akizungumza mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili,kuhusiana na mchango wa Wanahabari katika kuboresha sekta ya Afya na umuhimu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa watoa Huduma
   Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu,Mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahya Nawanda pamoja na  Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athman Rehani kwa pamoja wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili,kuhusiana na mchango wa Wanahabari katika kuboresha sekta ya Afya na umuhimu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa watoa Huduma
   Pichani shoto ni Mmoja wa Maofisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),Bi.Gaudensia Semwanza na Mdau wakifuatilia mada mbalimbali ndani ya kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.   
   Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu pamoja na Mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahya Nawanda  wakijadiliana jambo.
  Washiriki katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo Dodoma hotel ikiwa ni siku ya pili ya kilele chake huku likiwa limebeba kauli mbiu ''Tanzania na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kongamano hilo lilizinduliwa jana na Waziri wa Afya Dkt Seif Rashid,ambapo pia Kabla ya uzinduzi wa kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36 zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema mwakani.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo- Maelezo-DSM.

  Serikali ya Marekani na Tanzania zimetiliana saini kwa ajili ya kuandaa miradi katika sekta ya nishati itakayofadhiliwa katika awamu ya pili ya Mkataba wa Millennium Challenge Corporation (MCC).

  Utiaji saini wa mkataba huo ulifanyika katika Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam ambapo Makamu wa Rais wa MCC Bw. Kamran Khan  anayeshughulikia Mikataba na Uendeshaji wake pamoja na Waziri wa Fedha  wa Tanzania , Mhe. Saada Mkuya ukishuhudiwa na Balozi wa Marekani nchini Mark Childress.

  Akiongea wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba huo, Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya alisema kuwa MCC imeipatia Serikali ya Tanzania shilingi bilioni 17 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa MCC II ambapo mraadi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa hapo mwakani ukiwa na lengo la kusaidia miundombinu ya umeme nchini.

  Makubaliano hayo ni muendelezo wa ubia imara kati ya Marekani na Tanzania kati ya mwaka 2008 na 2013 ambapo MCC ilitekeleza mkataba wa miradi mikubwa ya uwekezaji katika sekta za maji, barabara, na nishati ya umeme nchini.

  Miradi hiyo iligharimu jumla ya Dola za kimarekani milioni 698, chini ya mkataba huo mtandao wa nyaya za umeme wenye zaidi ya kilometa 3,000 ulijengwa.

  Kwa kuzingatia mafanikio hayo katika utekelezaji wa wa programu zilizokuwa chini ya mkataba wa kwanza kuwahi kutolewa na MCC, taasisi hiyo iliichagua tena Tanzania kuingia katika mkataba wa pili utakaolenga sekta ya Nishati katika miundombinu pamoja na mageuzi ya kisera na mifumo ya udhibiti na kitaasisi.

  Aidha, upembuzi yakinifu utaiwezesha Tanzania kuandaa miradi itakayoleta mageuzi katika sekta ya Nishati ikiwa ni pamoja na kuboresha utendaji wa shirika la ugavi wa umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) katika maeneo ya kiufundi, usimamizi wa fedha na uendeshaji na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya umeme katika maeneo ya vijijini.

  Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) ni Taasisi ya Serikali ya Marekani inayotoa misaada kwa nchi zinazoendelea, shughuli zake zinajengwa katika misingi kwamba msaada utaleta ufanisi na matokeo makubwa pale unapoimarisha utawala bora, uhuru wa kiuchumi na uwekezaji katika watu ambao unakuza uchumi na kuondoa umaskini.

  0 0  Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya ENGEN Tanzania leo Novemba 14,2014 wameungana na wafanyakazi wenzao Barani Afrika kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo.Engeni ni Kampuni iliyojikita katika uuzaji wa Mafuta bora ndani na nje ya Tanzania,huku ikiendelea kujivunia kwa Ubora wake.Pichani ni Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni hiyo ya Engen hapa nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya jengo lao Kurasini jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya ENGEN Tanzania,Mubita Akapelwa (wa pili kulia) akikata keki wakati wa Kusherehekea Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo,iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Shaaban Kayungilo.

  Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Shaaban Kayungilo akichua kipande cha Keki iliyokatwa vyema na Dada Jullieth Lwato (alieshika sahani) wakati wa Kusherehekea Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo,iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Katika
  mazungumzo maalum na Kituo cha Mlimani TV cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amewasisitiza waandaaji wa matamasha na mashindano ya Sanaa na urembo kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo katika kuendesha matukio yao.

  Pia,amewataka waandaaji wa mashindano na matamasha katika vitongoji kuwa makini katika kusimamia taratibu kwani ndiyo wanaoandaa washiriki ambao baadaye wanakuja kushiriki kwenye ngazi ya taifa. 

  Katika hili amewataka kutumia upembuzi yakinifu kabla ya kuruhusu washiriki ama wasanii kushiriki katika matukio yao ili kukwepa aibu kwa taifa.

  "Kama kuna vielelezo au nyaraka zinahitajika, waandaaji lazima waziombe kwa washiriki na wazihakiki kikamlifu. Kama kuna utata wahakikishe wanahusisha mamlaka zinazohusika mapema ili kuupata ukweli" aliongeza Mngereza.

  Aidha, amesisitiza kwamba BASATA litaendelea kuwabana waendeshaji/waandaaji wa matukio ya Sanaa kwani ndiyo wenye jukumu la kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na ndiyo wanaopewa idhini ya uendeshaji na Serikali.

  “Kama katika ngazi ya vitongoji,wilaya na kanda waandaaji wangeweka msisitizo, changamoto zisingekuwepo. Kuna ulegelege wa kudhibitiwa” Aliongeza. 

  Amewataka waandaaji wote kusimamia kanuni  na taratibu zao  kwa haraka pasipo kusubili mashinikizo na malalamiko kutoka kwa jamii.

  0 0

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO

  Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam kimetoa tuzo kwa wanafunzi bora 12 waliohitimu na kufanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka wa masomo 2014/2015 ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa chuo hicho kuenzi na kuthamini mchango walioutoa katika maendeleo ya taaluma chuoni hapo.

  Akikabidhi tuzo hizo katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mwenyekiti wa sasa wa wanafunzi  waliomaliza chuo cha CBE, Bw. Harry Kitilya amesema kuwa wahitimu hao wanayo nafasi kubwa ya kutumia elimu waliyoipata na kuwa mfano katika kuleta mabadiliko nchini.

  Amesema chuo hicho tangu kuanzishwa kwake  mwaka 1965 kimekua mfano wa kuigwa kwa kuwajengea uwezo wanafunzi wanaohitimu  ili waweze kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Biashara nchini kwa kuongeza  nafasi za ajira kwa kujiajiri wenyewe  kupitia shughuli za ujasiriamali,uanzishaji wa makapuni na miradi mbalimbali.

  Bw.Kitilya amewataka wahitimu hao kujiendeleza zaidi kielimu ili waweze kukabiliana na ushindani wa ajira uliopo hususan katika soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii na kuepuka vitendo vya rushwa na uzembe pindi wanapoingia katika ajira.

  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema akizungumza na wahitimu wa mwaka 2014 wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo ulioshuhudiwa na wanafunzi waliosoma miaka ya nyuma ni utaratibu wa chuo hicho kuenzi na kuthamini juhudi walizozionyesha katika taaluma.

   Amesema utoaji wa tuzo hizo umehusisha  fani za Uhasibu,Udhibiti wa Biashara, Usimamizi wa Masoko,Manunuzi na Ugavi na kuongeza kuwa utafanyika katika kampasi nyingine za chuo hicho zilizoko Zanzibar, Mbeya, Dodoma na Mwanza.

  “Siku ya leo mbali na zoezi hili la utoaji wa tuzo, wahitimu wote wa sasa na wa zamani wanakutana kujadili namna ya uendelezaji wa chuo chetu, siku hii ni muhimu sana kwa kuwa inaongeza ushiriki wao katika kujadili masuala mbalimbali ya kukiendeleza chuo” Amesema Prof. Mjema.

  Ameongeza kuwa lengo la kuwakutanisha wahitimua wa miaka iliyopita ni kujenga umoja imara na kupata mrejesho kutokana na huduma wanazozitoa kwa jamii, mahitaji ya soko la ajira na mabadiliko ya kiuchumi yaliyopo.
  Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa mwaka 2014 na wale miaka iliyopita wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa hafla hiyo, wameiomba Serikali kendelea kupanua wigo wa Elimu ya Biashara kwa kuongeza matawi mengi zaidi kwa lengo la kuwafikia wananchi wengi katika maeneo yao.

  Wameiomba Serikali kupitia wizara ya Viwanda na Biashara kuwaendeleza na kuwawezesha wahitimu wanaoonyesha nia ya kujiajiri wenyewe na kuanzisha makampuni yao hapa nchini.

  Aidha ,wametoa wito kwa walimu kutoa mafunzo yanayoendana na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea duniani ili kuwawezesha kukidhi soko la ajira  huku wakitoa wito  kwa wahitimu wa vyuo kujenga utamaduni wa kujitolea ili waweze kupata uzoefu.

  0 0

  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana kesho November 15, 2014 anatarajia kuanza Ziara katika Mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara). Ziara hiyo ya Katibu Mkuu inategemea kuanza kesho katika wilaya ya Kilwa iliyopo Lindi na Kisha kuendelea katika wilaya zingine kwa takribani siku kumi na sita za kutembelea majimbo, kata, matawi na mashina ya Chama Cha Mapinduzi.

  Ziara hii ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahaman Kinana ni muendelezo wa Ziara za Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ambazo zimekuwa zikiendelea kote nchini tangu Sekretarieti hiyo ilipoteuliwa mwanzoni 2012.

  Malengo ya ziara hii ni kukagua uimara wa Chama katika mikoa hiyo pamoja na kujenga na kuhimiza Uhai wa Chama katika kanda ya kusini ambayo kwa muda wote imeendelea kuwa ngome muhimu kwa Ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

  Lakini pia ziara hii inalenga Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2010 - 2015 ambayo imeendelea kutekelezwa kwa mafanikio na Serikali katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Tunawaomba wananchi wa Mikoa ya Kusini kuwa tayari kujitokeza kwa wingi katika Mikutano ya hadhara iliyoandaliwa na kusema kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili ili ziweze kufanyiwa kazi na kutekelezwa mara moja.

  Katika ziara hiyo Katibu Mkuu ataongozana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, ndugu Nape Nnauye.

  UMOJA NI USHINDI.

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

  0 0


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Daktari Bingwa Edward Schaeffer kutoka Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Mgeni rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi ambaye ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akitoa nasaha zake kwa washiriki wa Bonanza hilo lililofanyika leo Novemba 15,2014 kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Picha zote na Othman Michuzi.
  Kaimu Mkurugeni wa Elimu na Huduma wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Allan Kiulla (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi lililofanyika leo kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Bonanza hilo lililogeshwa kufanyika michezo mbali mbali,ikiwepo mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na mingine mingi.Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki ambaye ndie alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Bonanza hilo.
  Sehemu ya Wafanyakazi wa  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyakazi wa NSSF ambao ni Waalikwa walioshiriki kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi wakifatilia kwa makini nasaha za Mgeni Rasmi,ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti".
  Mtanange wa kukata na shoka kati ya Timu ya TRA na timu ya NSSF ulipigwa katika Uwanja wa TCC Chang'ombe,Mtanange uliowatoa kifua Mbele vijana wa NSSF kwa Mabao 4-2 dhidi ya wenzao wa TRA.
  Mbio za kuku kwa kina Baba zilikuwa ni sehemu ya michezo iliyofanyika leo Uwanjani hapo.
  Vijana wa Kundi la Wanne Star wakionyesha makeke yao mbele ya wadau wa TRA waliofurika kwa wingi kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo.


  0 0
 • 11/15/14--07:30: WANA CCM BEIJING WAKUTANA
 • Wanachama wapya wa Tawi la CCM China waliopo Beijing wakikabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa Tawi Ndugu Boniphace Shija Nobeji.


  Kada na Mtumishi wa CCM Makao Makuu Ndugu Suleiman Serera akitoa semina iliyohusu itikadi na imani ya CCM kwa wanachama wa CCM Beijing.


  Sehemu ya wanachama waliohudhuria wakiuatilia kwa makini semina iliyokuwa ikitolewa.

  Wanachama wa mashina ya CCM Beijing wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza Mkutano wao uliofanyika katika Chuo cha Beijing Normal.

  0 0

  DSC_0317-1024x682
  CEO of MeTL GROUP, Mohammed Dewji.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari (hawapo pichani) wakati alipokutana nao nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana kwa mazungumzo
  Mhariri wa gazeti la Jamhuri, Jackton Manyerere, akichangia mada wakati wa mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, yaliyofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana Novemba 14, 2014
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile na Mhariri wake, Jackton Manyerere (kulia) mara baada ya kumalizika mazungumzo na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari yaliyofanyika kwenye Makazi ya Mhe Makamu wa Rais Oysterbay, jijini Dar es Salaam, jana usiku Novemba 14, 2014.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Wahariri wa Gazeti la Mwananchi mara baada ya kumalizika mazungumzo na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari yaliyofanyika kwenye Makazi ya Mhe Makamu wa Rais Oysterbay, jijini Dar es Salaam, jana usiku Novemba 14, 2014. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wahariri hao baada ya mazungumzo. Picha na OMR.

  0 0

  1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivalishwa Skafu na vijana na wa Chipukizi wakati alipowasili eneo la Somanga wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi akianza ziara yake ya siku 16 katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza sughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi, Katibu Mkuu huyo anaongozana naNape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na Mjumbe wa NEC mkoa wa Lindi na Mbunge jimbo la Mtama Mh. Bernald Membe.3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kilwa na Mkoa wa Lindi waliofika katika eneo la Somanga kwa ajili ya mapokezi Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliofika kumpokea katika eneo la Somanga wilayani Kilwa kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. 


older | 1 | .... | 406 | 407 | (Page 408) | 409 | 410 | .... | 1897 | newer