Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

Ofisi ya Taifa ya Takwimu yatoa taarifa za mfumuko wa bei nchini.

$
0
0
 
 Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumuko wa bei nchini.
Baadi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumzia suala la mfumuko wa bei nchini.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO).

Wananchi wameombwa kutoa ushirikiano wa dhati kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupitia ofisi za takwimu za mikoa wakati wa ukusanyaji wa takwimu mbalimbali kwa lengo la kutoa taarifa zilizo sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Kwesigabo amesema kuwa pamoja na mambo mengine Ofisi ya Taifa ya Takwimu ndiyo yenye mamlaka ya kutoa taarifa za mfumuko wa bei nchini ambapo kwa mwaka huu unaonesha umepungua kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kuanzia kipindi cha mwezi Oktoba 2013 hadi Oktoba 2014.

Kwesigabo amesema kuwa mwenendo wa bei za bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua bei kwa mwezi Oktoba 2014 zikilinganishwa na mwezi Oktoba 2013 ni pamoja na bei za mahindi asilimia 7.2, unga wa mahindi asilimia 5.5 na unga wa ngano asilimia 4.4.

Bidhaa nyingine za vyakula zilizoonesha kupungua bei ni ulezi asilimia 3.5, tambi asilimia 2.2, samaki asilimia 4.6, mihogo asilimia 2.1 na sukari imepungua kwa asilimia 4.6.

Aidha, Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba 2014 umepungua hadi asilimia 5.9 kutoka asilimia 6.6 tofauti na hali ilivyokuwa mwezi Septemba 2014.  “Hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Oktoba 2014 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwaka ulioishia mwezi Septemba 2014” alisema Kwesigabo.

Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi Bw. Kwesigabo amesema kuwa umepungua kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na kupungua kwa asilimia 0.4 kama ilivyokuwa kwa mwezi Septemba mwaka huu, huku fahirisi za bei za taifa zimepungua hadi kufikia 149.70 kwa mwezi Oktoba 2014 kutoka 149.93 za mwezi Septemba 2014.  

Kwesigabo amezitaja bidhaa zilizochangia ongezeko la fahirisi za bei nchini kuwa ni pamoja na vitafunwa vinavyotokana na unga wa nagano kwa asilimia 2.4, unga wa mahindi kwa asilimia 0.1, samaki kwa asilimia 1.7,ndizi za kupika kwa asilimia 7.5, mbogamboga kwa asilimia 2.2, viazi mviringo kwa asilimia 1.5 na sukari kwa asilimia 1.6.

Aidha, amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii umefikia shilingi 66 na senti 80 kwa mwezo Oktoba 2014 kutoka mwezi Septemba 2010.

Kuhusu ulinganifu mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana na kueleza kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya umepungua hadi kufikia asilimia 6.43 kwa mwezi Oktoba 2014 ikilinganishwa na asilimia 6.60 za mwezi Septemba mwaka huu, huku Uganda ikiwa na mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 1.8 kwa mwezi Oktoba mwaka huu ikilinganishwa na 1.4 za mwezi Septemba. 


MWANAMUZIKI MKONGWE WA TWANGA PEPETA,AMIGOLAS AFARIKI DUNIA

$
0
0

Mwanamuziki Mkongwe kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta,pichani kulia enzi za uhai wake akiwa kazini,ajulikanae kwa jina la Amigolas amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo,katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar,Taarifa za awali ambazo chumba cha habari cha Globu ya Jamii imezipata kutoka kwa vyanzo vya kuwaminika,zinaeleza kuwa Marehemu Amigolas alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Moyo mpaka kufariki kwake.Tutaendelea kupeana taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu kwa kadiri zitakavyokuwa zikiingia.Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi-Amin

Wadau walamba Nondozz katika Mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro

$
0
0
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislam cha Morogoro (MuM),Hajjat Mwantum Malale akiongoza mahafali ya saba ya Chuo Kikuu hicho cha Waislam yaliyofanyika jana Novemba 8,2014 katika viwanja vya Chuo hicho.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Baraza la Shule Chuo hicho,Prof. Mussa Assad.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislam cha Morogoro (MuM),Prof. Hamza Mustafa Njozi (wa pili kulia) akisoma hotuba yake na baadae kuwakaribisha wakuu wa vitivo kuja kuwaorodhesha wahitimu wao wanaostakihi kutunukiwa Shahada mbali mbali.
 Sehemu ya Wahitibu wa Shahada mbali mbali wakiwa katika Mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro.
Bi. Farida Khalfan akiwa akiwa katika pozz la picha mada baada ya kulamba Nondozz yake ya Sanaa na Ualimu (Bachelor of Arts with Education) katika Mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro.
Furaha ya kulamba Nondozz.
Mdau Jaffar Haniu wa TBC akiwa ni mwenye furaha sana baada ya kulambo Nondozz yake ya Sanaa na Mawasiliano ya Umma (Bachelor of Arts in Mass Communication) katika Mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro.
Mdau Jaffar Haniu wa TBC (katikati) akiwa na wahitimu wenzake.

Yanga yaipiga virungu 2-0 Mgambo Shooting

$
0
0
 Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akichuana na beki wa Mgambo Shooting, Bushiru Mohamed katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Golikipa wa Ruvu Shooting, Said Lubawa akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.

Andrey Coutinho akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Mgambo.
Mrisho Ngasa (kulia) akimtoka Bushiru Mohamed.
Simon Msuva akimiliki mpira mbele ya beki wa Mgambo shooting.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli lililofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Simon Msuva wakati timu hiyo ilipopambana na Mgambo Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akimtoka, mchezaji wa Mgambo Shooting, Ally Idd katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

AZIMIO LA ARUSHA LA KUKABILI UJANGILI LAPITA

$
0
0
IMG_5047
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza kwenye mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu ulioshirikisha mataifa ya Afrika, wajumbe wa Bunge la Marekani (Congress) Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mataifa washirika wa maendeleo, wanazuoni na wawakilishi wa taasisi zisizo za serikali uliomalizika jana jijini Arusha na kufungwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.

 Kushoto Mwenyekiti wa mkutano wa kikanda wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush Arha na kulia ni Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli.
========  ========  ======
JUMUIYA ya kimataifa imepitisha Azimio la Arusha lenye lengo la kukabiliana na ujangili na kuendeleza wanyama.

Azimio hilo limepitishwa baada ya mkutano wa siku mbili ambapo pia imekubalika kwamba hali ya baadae ya wanyama barani Afrika ni suala linalohitaji uwajibikaji wa pamoja.
Aidha nchi za Afrika zimetakiwa kuukomesha ujangili na kufanya juhudi ya kuhakikisha wanyama walio katika hatari ya kutoweka wanalindwa na kuhakikisha kundi hilo linakua.

Wanyamama ambao kwa sasa wapo hatarini kutoweka ni tembo, faru na simba. Mkutano huo uliojumuisha mataifa mbalimbali ya Afrika na jumuiya za kimataifa na kufunguliwa na Waziri wa Mali asili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwa niaba ya rais Jakaya Kikwete, umetoa wito kwa mataifa yote kufanyakazi kwa pamoja kukabili ujangili kwa kushirikisha wananchi wanaoishi na kutegemea wanyamapori hao na mapori yenyewe.
IMG_5051
Washiriki mbalimbali wa mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu wakijadilina namna ya kuweka nguvu ya pamoja katika kukabiliana na suala la ujangili.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu, baada ya mkutano ambao uliangalia sheria zilizopo za kulinda mapori na wanyamapori,uhalisia wa mifumo ya ujangili na uhifadhi, washirika wa maendeleo nao walielezea nia zao za kuendelea kusaidia uhifadhi wa wanyamapori na mapori katika ukanda wa Afrika ikiwamo Tanzania.

Mkutano huo ambao ulishirikisha mataifa ya Afrika, wajumbe wa Bunge la Marekani (Congress) Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mataifa washirika wa maendeleo, wanazuoni na wawakilishi wa taasisi zisizo za serikali umeelezwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya London, Uingereza ya kustawisha wanyamapori na mapori yanayowahifadhi.

Awali akifungua mkutano kwa niaba ya Rais Kikwete, Waziri Nyalandu alisema kwamba mataifa yasidharau nguvu ya pamoja katika kukabiliana na ujangili.
Alisema pia kwamba hali ya baadae ya wanyamapori katika bara la Afrika ni wajibu wa kila mtu na kila taifa na mamlaka nyingine ambazo ni wadau.
IMG_5205
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa ambapo amesema UN itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na mamlaka mbalimbali zinazoendelea kukabiliana na ujangili na kupotea kwa misitu duniani ili kuhifadhi urithi wa dunia.
Alisema Tanzania katika mchango wake imeanzisha mkakati wa kukabiliana na ujangili na kuunda mamlaka ya wanyamapori ili kuwa na uhakika wa kuendeleza masuala yanayohusu hifadhi na changamoto zake kwa kasi na karibu zaidi.
Washiriki wa mkutano huo wa siku mbili walielezea umuhimu wa kulinda mali asili hizo kwa kuwa ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi zote.
Akizungumzia umuhimu wa mali asili Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, alisema ujangili na uhalifu mwingine kwa wanyamapori na hifadhi zao ni changamoto kubwa kwa uchumi unaotegemea utalii, mazingira na maendeleo endelevu.
Alisisitiza kwamba suala la uhalifu kwa wanyamapori na mapori yao ni lazima kufanyiwa kazi kitaifa na kimataifa ikiwamo kikanda.
Mratibu huyo alisema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia juhudi hizo za kuhifadhi wanyama na mapori kwa kusaidia kutoa elimu na kutatua changamoto za kiuchumi zinazokabili watu wanaoishi jirani na misitu hiyo.
IMG_5219
Pichani juu na chini ni washiriki mbalimbali wa mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu uliomalizika jana jijini Arusha.
Alisema Umoja huo utaendelea kusaidia kupeleka elimu ya menejimenti ya wanyamapori na misitu ili wakazi wa maeneo hayo wafaidi raslimali hizo na kuzitunza.
Hata hivyo alizitaka jumuiya za kimataifa na mataifa kushirikiana katika kufanikisha adhma hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya ICCF ambao ni wenyeji wenza wa mkutano huo, Makamu Mwenyekiti Dk Kaush Arha, alisema mkutano huo ulikuwa na manufaa makubwa hasa wito wa kuweka mikakati ya kurejesha makundi ya wanyama walio katika hatari ya kutoweka kama tembo, faru na simba.
Aidha mkutano umekubaliana juu ya masuala kadhaa ambayo yatasaidia Tanzania kuingia makubaliano na majirani zake kuhifadhi wanyamapori.
IMG_5052
Naye Mkuu wa balozi za nchi za Jumuiya ya Ulaya nchini Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi ameipongeza Tanzania kwa hatua iliyochukua kukabiliana na ujangili.
Amesema Jumuiya ya Ulaya ambayo imekuwa mshirika katika kukabilina na ujangili na hifadhi ya wanyama imefurahishwa na mkutano huo kwa kuamini kwamba kunatakiwa kuchukuliwa hatua za kikanda kuweza kunusuru wanyamapori kwa kuchukua hatua za pamoja.
Ameipongeza Tanzania na majirani zake kwa kuchukua hatua madhubuti za kikanda kukabiliana na ujangili na uharibifu wa mazingira na kusema Jumuiya ya Ulaya ipo tayari kusaidia katika juhudi hizo.
IMG_5063
IMG_5094
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishuhudia utiliwaji saini wa Azimio hilo.
IMG_5234
Wawakilishi kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kenya, Malawi, Uganda, Mozambique, Tanzania, na Zambia wakisaini Azimio la Arusha lenye lengo la kukabiliana na ujangili na kuendeleza wanyama kabla ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (wa tatu kushoto) kufunga rasmi mkutano huo uliomalizika jana jijini Arusha.

Mwasisi wa Swahili Blues Leo Mkanyia Azidi Kutikisa Kimataifa

$
0
0
Embedded image permalink
Gazeti la The Citizen la Tanzania linamwita 'lulu iliyofichika' hidden gem, kwa kimombo). Huyu ni Leo Mkamia, msanii wa Kitanzania na mwanzilishi wa aina ya muziki ujulikanao kama 'Swahili Blues.'

Siku chache zilizopita, Leo alirekodi wimbo wake mpya uitwao 'Pamoja.' Miongoni mwa yatakayoonekana katika video ya wimbo huo ni performance ya kihistoria ya msanii huyo katika moja ya vyuo vikuu vikubwa hapa Uingereza, Nottingham University, ambapo Leo alifanikiwa kuwaimbisha Kiswahili baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho kikuu. Katika shughuli hiyo, Leo aliimba na kwaya ya Nottingham Academy.

Kinachomfanya Leo kuwa msanii wa kipekee kutoka Tanzania kuwa na fursa kubwa ya kutawala anga za muziki kimataifa ni ukweli kwamba amefanikiwa kuanzisha kitu kipya- muziki aina ya Swahili Blues- na ambao tayari umeanza kukubalika kimataifa.

Mtaji mkubwa wa Leo ni ukweli kwamba anatoka familia ya muziki.Unamkumbuka mkongwe wa gitaa Henry Mkanyika? Basi huyo ni baba mzazi wa Leo, ambaye alianza kucharaza gitaa akiwa na umri wa miaka minane tu.

 

Kwa sasa Leo ni miongoni mwa wasanii wachache mno, sio tu wa Tanzania, bali Afrika nzima kwa ujumla, ambao sura na sauti zao sasa 'zimezoeleka kwenye vituo vya radio na televisheni vya kimataifa kama BBC. Na katika kuthibitisha hjilo, Leo alihojiwa na BBC mara baadha ya performance hiyo ya kihistoria huko Nottingham.



Pamoja na kufanya vizuri kimataifa, Leo bado anathamini asili yake. Kama video ya pili inavyoonyesha, Leo alifanya mahojiano na mtandao mkubwa na maarufu wa burudani Tanzania na Afrika kwa ujumla wa Bongo5. Kadhalika, msanii huyo anapata sapoti kubwa kutoka kwa mmoja wa waasisi wa muziki wa Hip-Hop nchini Tanzania, lejendari @XamiaSiku4Saa4 wa kundi maarufu kabisa la Kwanza Unit. Ieleweke kwamba katika shughuli za muziki, kupata 'endorsement' ya mkongwe wa muziki ni uthibitisho kuwa msanii husika anafanya kazi nzuri mno.

Kama Watanzania, tuna wajibu na kila sababu ya kumuunga mkono Leo, kwani sio tu anaitangza Tanzania yetu bali pia anautambulisha utamaduni wetu-kwa maana ya lugha ya Kiswahili- kupitia muziki wake wa Swahili Blues.

Unaweza kufuatilia maendeleo yake ya kimuziki kwa akaunti zake mbalimbali za mitandao ya kijamii: Twitter na Facebook  na katika tovuti yake sambamba na ukurasa wake wa YouTube

Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema “Hatutetereki”

$
0
0
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Kamati ninayoongoza ya PAC kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu kuhusu ukaguzi maalumu wa akaunti ya Tegeta Escrow, kumekuwa na kampeni za chini chini zinazoendeshwa kwenye korido za Bunge na kwenye mitandao dhidi yangu binafsi na baadhi ya wabunge waliosimama kidete dhidi ya wizi wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania akaunti ya Escrow.
Baadhi ya tuhuma nimezipeleka kwenye vyombo vya dola ili zichunguzwe kwani zina vielelezo vya mahala pa kuanzia (kama leseni ya udereva ya mwanamke anajulikana kama Vivian Emmanuel Sirikwa na muhuri wa kampuni ya uwakili inayomilikiwa na Bwana Joseph Mkandege).
Description: Baadhi ya Tuhuma
Baadhi ya Tuhuma
Baadhi ya tuhuma nitazijibu moja baada ya moja.
Waziri mmoja ambaye ni mtuhumiwa wa wizi wa fedha za Tegeta Escrow anazunguka kwa wabunge akisema tuhuma hizi kupikwa kama njia yake ya kuhamisha mjadala kutoka uporaji wa Tshs 200 bilioni kwenda kwenye masuala binafsi.
Tuhuma hizi zenye kichwa cha habari "Zitto na Filikunjombe wanatumiwa na Kenya na Uingereza kuvuruga na kudhoofisha Uwekezaji nchini mwetu" zinajibiwa hapa chini. Utaona ndugu Filikunjombe ametajwa kwa kichwa cha habari ili kumtaja tu bila sababu yeyote ile.
Tuhuma #1:
Zitto anaye rafiki yake Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao kwa pamoja wameanzisha Gombe Advisors Co. Ltd (registered on 24 November 2011, Certificate No 87387) kwa ajili ya kufanya biashara na Makampuni ya Gesi na Mafuta yanayofanya kazi nchini hapa.
Majibu:
Gombe Advisors ni kampuni binafsi isiyofanya faida yaani ‘Company Limited by Guarantee’. Haina kazi na kampuni yoyote ya Gesi na Mafuta na wala yenyewe haijuhusishi na biashara hiyo. Gombe advisors haijafanya kazi yoyote ile na kampuni nyingine zaidi ya kusaidia wasanii wa kundi la Kigoma All stars. Upotoshaji hapa unalenga kupindisha mjadala.
Tuhuma #2:
Zitto amemsaidia Ongangi kupata uraia wa Tanzania na kwa sasa ni raia wa pasipoti. Zitto na Ongangi walimtafutia CEO wa Shell aitwae Axel Knospe nyumba na gari ya kukodi.
Majibu:
Raphael ni mtu binafsi ambaye anafanya shughuli zake hapa nchini, amesoma hapa nchini na ameoa na ana mtoto. Tuhuma hizi hazina msingi wowote ule maana ni uwongo. Wanaotoa tuhuma hizi waonyeshe hiyo pasipoti ya Bwana Ongangi kuthibitisha madai yao.
Tuhuma #3:
Mikataba ya STATOIL iliyokuwa inar
ushwa kwenye mitandao ya jamii na kuchapishwa kwenye magazeti ya Kenya ya hapa nchini (The Citizen na Mwananchi) mwandishi mkuu alikuwa huyo CEO wa Shell.
Majibu:
Mkataba uliovujishwa wa StatOil ulivujishwa na waandishi wa habari wa Norway. Uchambuzi wa mkataba huo nimeufanya mwenyewe kwa kutumia utaalamu wangu niliosomea wa kuchambua mifumo ya kodi kwenye sekta ya mafuta na gesi. Kwa namna yoyote ile, huyo anayetajwa kuwa CEO wa kampuni ya Shell hahusiki. Tuhuma hii wanaoitoa watoe ushahidi usio na chembe ya mashaka.
Ikumbukwe kuwa mkataba wa StatOil utaipotezea Tanzania mapato ya dola za Marekani bilioni 12 (takribani Tshs 20,400,000,000,000/=) katika kipindi cha miaka 15 baada ya gesi kuanza kuchimbwa.
Uamuzi wa Kamati ya PAC kutaka mikataba yote ya Gesi kuwa wazi una lengo la kuchambua kuona kama mikataba yote nchini haipotezi mapato kwa nchi. Uamuzi huo umewakasirisha sana baadhi ya waliohusika kuingia mikataba Serikalini maana wanajua kuna madudu kwenye mikataba na wanataka umma wa watanzania usijue!
Tuhuma #4:
Kampuni ya SHELL imechukizwa sana kucheleweshwa kwa kupata kibali cha kutafuta gesi na mafuta kule Pemba. Vilevile SHELL haina uwekezaji mkubwa Tanzania Bara kwani ilishindwa kwenye tenda zenye vitalu vyenye gesi nyingi upande wa Bara.
Majibu:
Ukweli ni kuwa Kampuni ya Shell ina vitalu 4 huko Zanzibar na tayari ina makubaliano na Serikali ya Zanzibar kuhusu utafutaji mafuta huko katika vitalu namba 9,10,11 na 12. Shell inafanya kazi na kampuni ya Petrobras ya Brazil kwenye kitalu namba 6 na namba 8. Taarifa hizi zipo wazi kwenye tovuti ya TPDC. Tuhuma nyepesi namna hii dhidi ya kampuni kubwa kama Shell zinaonyesha dharau na kiburi kinachotokana na uelewa mdogo wa mambo wa watu wanaotuhumu.
Tuhuma 5:
Ongangi anapokea maelekezo kutoka Serikali ya Kenya kuhujumu uwekezaji nchini mwetu.
Majibu:
Nazifahamu mbinu nyingi zinazotumika kufanya propaganda, lakini mbinu hii imeshindwa ikiwa mapema sana. Ni vema wanaotoa tuhuma hizi wazithibitishe vinginevyo ni mwendelezo wa propaganda zisozingatia diplomasia ndani yake dhidi ya jirani zetu wa Kenya. Hizi ni propaganda hatari ambazo hata hao wanaotuhumiwa wakisikia watatudharau sana.
Tuhuma #6 (juu ya Uingereza):
Uingereza imekuwa inamfadhili Zitto kwa miaka mingi kwa mambo yake ya kisiasa kwa hiyo sasa hivi Ubalozi wa Uingereza unamlipa Zitto na Kafulila kuhakikisha kwamba Standard Chartered ya Uingereza inalipwa deni lake lisilotambulika kisheria nchini mwetu.
Majibu:
Nimetangulia kusema hapo awali kuwa kuna propaganda ambazo haziangalii hata diplomasia; nyingine ni hii. Pamoja na kukanusha uzushi huu, ni vizuri wanaotoa tuhuma za namna hii kuthibitisha. Mimi binafsi sijawahi kufadhiliwa kisiasa na Taifa lolote lile. Inaelekea kuna wanasiasa wanaofadhiliwa na mataifa mengine ambao kwakuwa kwao ndiyo maisha wanaamini na wengine tupo kama walivyo.
Kwangu itikadi yangu ni ‘Uzalendo kwa nchi yangu’, ni jambo ambalo halina mbadala wake. Siku zote nasema “Right or wrong, my country first".
Kurudia kurusha tuhuma kwa Ubalozi wa Uingereza nchini ni kudhihirisha kwa mara nyingine kiburi cha kuwa na mamlaka (arrogance of power) walicho nacho wanaotuma tuhuma hizi.
Aidha, wanatuhumu kuwa “Kafulila na Zitto wamehaidiwa 15% ya USD 150 million kama deni likilipwa”
Mtanzania anayeweza propaganda dhaifu kama hizi basi anatakiwa ajitafakari. Hata hivyo ni vema wanaotoa tuhuma hizi wathibitishe bila chembe ya mashaka.
Tuhuma #7:
Mbunge Mkono nae ameshikwa hasira kupoteza kazi ya uwakili pale TANESCO. Kafulila na Zitto wanalipwa na Mkono kuvuruga Serikali kwa hasira za kukosa fedha za kitapeli za TANESCO.
Majibu:
Hizi ni tuhuma ambazo sasa tumezizoea kutolewa. Mambo mepesi hayawezi kujibu mambo ya msingi kama tuhuma za wizi wa fedha zaidi ya Tshs bilioni 200 kutoka Benki kuu ya Tanzania. Kukusanya kila propaganda ili kuuhamisha umma ni kupungukiwa hekima na busara.
Aidha, wanaotuhumu wanadokeza kuwa “Naomba tuwe macho na Wabunge wetu achananeni na madai ya Zitto ya wizi. Huyu mtu anafanya biashara na Kampuni ya SHELL na inasemekana analipwa na Ubalozi wa Uingereza. Serikali ya Kenya na tapeli mkubwa Mbunge Mkono nae anawalipa Zitto na Kafulila”.
Watanzania, haya ni maneno ya hasira ya watu wanaokaribia kukamatwa kwa kushiriki wizi wa fedha katika Benki kuu ya Tanzania. Kamwe tuhuma kama hizi haziwezi kutukatisha tamaa katika kupambana ili ukweli ujulikane. Sisi tutapigana kwa ajili ya Taifa, kwa ajili ya mtanzania na tunachotaka ni umma uujue ukweli wa mambo.
Hasira hizi zinatokana na mambo mawili:
Moja ni uamuzi wa kamati ya PAC kuwasweka ndani baadhi ya watendaji wa TPDC kwa kushindwa kutekeleza maamuzi ya Kamati yanayohusu uwazi wa mikataba ya Gesi na Mafuta.
Pili, ni uamuzi wa PAC kuagiza ukaguzi maalumu wa mchakato mzima wa kuanzishwa na kufungwa kwa akaunti ya Tegeta Escrow ambapo zaidi ya shilingi bilioni 200 ziliporwa na zaidi ya shilingi bilioni 12 zinalipwa na TANESCO kila mwezi kwenda kampuni ya PAP inayomilikiwa na Harbinder Singh Seth (50%) na watu wasiojulikana kupitia kampuni ya Simba Trust iliyosajiliwa na kufichwa nchini Australia (50%).
Ieleweke kuwa PAP inalipwa shilingi milioni 400 kila siku kutoka TANESCO izalishe au isizalishe Umeme! Watanzania, PAP itaendelea kulipwa namna hiyo kwa miaka 20 ijayo. Kwa namna ambayo Seth analindwa na baadhi ya watendaji Serikalini na hasa ndani ya Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, kuna fununu kuwa kuna maofisa serikalini wanaomiliki hizo 50% za kampuni ya PAP. Seth pia anamiliki kitalu cha gesi Mnazi bay Kaskazini kupitia kampuni ya HydroTanz.
Hasira hizi walizo nazo wanaonituhumu na Kamati yangu zimewapelekea kugushi nyaraka mbalimbali zinazonituhumu mimi na wenzangu ili kutuogopesha na kutukatisha tamaa katika kutafuta ukweli juu ya suala la uporaji wa fedha kutoka Benki kuu. Lengo lao ni kututoa kwenye mstari. Mimi na wenzangu hatutatoka kwenye mstari, tutashirikiana na wabunge wenzetu kuhakikisha ukweli unajulikana na wezi kuchukuliwa hatua kali.
Harbinder Singh Seth aliiangusha Serikali ya KANU nchini Kenya, sasa anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha Serikali ya CCM wakiendelea kumkumbatia.
Watanzania sio mabwege!
Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC
Dodoma, 9 Novemba 2014

Rais Kikwete afanyiwa upasuaji wa tezi dume Marekani, hali yake inaendelea vyema

$
0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  Dkt.Edward Shaeffer wa  hospitali ya Johns Hopkins (kushoto) na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi  (kulia) muda mfupi baada ya kuwasili ili kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland nchini Marekani Jumamosi asubuhi(picha na Freddy Maro)
=======  ======  ======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa
upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins
iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.

Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji
matibabu ya aina hiyo.

Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja
unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya Mheshimiwa Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.

Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete
kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana.

Imetolewa na

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU
DAR ES SALAAM,
NOVEMBA 9, 2014

DJ JD na DJ FAST EDDIE WAFANIKIWA KUREJESHA MUZIKI WA DISKO KILELENI TENA

$
0
0
 DJ JD akiwa kazini katika ukumbi wa Isumba Lounge jijini Dar es salaam usuiku wa kuamkia leo. Yeye na DJ Fast Eddie wameweza kurejesha utamu wa wapenzi wa muziki kwenda disco kwa wingi kama ilivyokuwa enzi hizo. Hapo Isumba ni mambo ya Old Skul na Mayenu kwa kwenda mbele kila Ijumaa na Jumamosi ambapo vijana wa zamani na wapya huruka majoka hadi lyamba.

Mh. Lowassa azindua helkopta ya kanisa la ufufuo na uzima

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Helkopta ya Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kulia kwa Mh. Lowassa).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mtoto wa Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiiingia ndani ya Helkopta hiyo kuashiria kuizindua rasmi kwa safari mbali mbali za kihuduma ya kiroho,itakayotumiwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiteta jambo na rubani wa Helkopta hiyo muda mfupi baada ya kuizindua.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,Kawe jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Othman Michuzi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasili kwenye viwanja vya kawe lilipo Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa kwenye kwenye jukwaa kuu na mwenyeji wake,Ambaye ni Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Josephat Gwajima (kushoto),Kawe jijini Dar es Salaam leo.Wengine pichani ni Askofu Eliud Isanje (wa pili kulia) na Mchungaji Elifuraha Laswai (kulia).
Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Josephat Gwajima akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Helkopta iliyonunuliwa na Mchungaji huo kwa ajili ya kutoa huduma za kiroho.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwahutubia waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Helkopta itakayotumiwa na Mchungaji huyo katika kazi zake za kiroho,hafla hiyo imefanyika leo kwenye viwanja vya Kawe,Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na baadhi ya wachungaji waliohudhulia kwenye hafla hiyo.
wakielekea kwenye uzinduzi rasmi wa Helkopta.
Helkopta iliyozinduliwa ikipaa kuondoka uwanjani hapo na baadae kurudu mara baada ya kuzinduliwa na Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimsikiliza kwa makini Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wakati akimuelezea kuhusu vitabu vyake alivyoviandika kabla ya kuvizindua rasmi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kwenye vitabu viliyoandikwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kushoto)
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akionyesha moja ya vitabu viliyoandikwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kushoto) wakati alipovizindua rasmi leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,Kawe jijini Dar es Salaam leo.

RAIS KIKWETE AENDELEA VYEMA NA MATIBABU ANAYOPATIWA HUKO MAREKANI

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Tanzania nchini
Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia hali katika
hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, nchini
Marekani, leo Jumapili, siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi
Dume.

Habari kutoka hospitalini hapo zinasema Rais Kikwete anaendelea vyema
na leo asubuhi alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo
yote ni mswano. Tutaendelea kwuashirikisha taarifa ya maendeleo yake
mara kwa mara. Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani
kulijenga Taifa.

PICHA NA IKULU

Marehemu Amigolas kuzikwa kesho alasiri makaburi ya Kisutu jijini Dar

$
0
0

Mwanamuziki Mkongwe kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta Khamis T. Kayumbu, maarufu kama Amigolas (pichani kulia enzi za uhai wake) amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Taarifa za awali ambazo chumba cha habari cha Globu ya Jamii imezipata kutoka kwa vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa marehemu Amigolas alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Moyo mpaka kufariki kwake.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Twanga Pepeta, msiba uko nyumbani kwa mama wa marehemu Mburahati, jirani na shule ya Msingi ya Mianzini.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho Jumatatu alasiri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 

Amigolas atakumbukwa kwa sauti yake nzuri na utanashati awapo jukwaani. Wimbo "Aminata" alioutunga na kuuimba akishirikiana na Ally Choki, Msafiri Diof, Lwiza Mbuttu na Jessica Charles ni moja ya nyimbo bora za Twanga Pepeta wakati huo hadi sasa. Usikilize hapo chini.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi
-Amin

Top 10 Reasons to drink ARGI+

$
0
0


Top 10 Reasons to drink ARGI+

In summary, what are the benefits of taking ARGI+?

1. Is a marvelous daily supplement that supports better health throughout many systems of the body, delivering optimal performance.
2. Supports the immune system. Nitric oxide derived from L-Arginine, is used by white blood cells to attack bacterial etc. as it is toxic to them and makes these immune cells more lethal.
3. Helps maintain a healthy blood pressure and cardiovascular system.
4. Aids bone and tissue growth and repair, so is particularly appropriate after fractures and soft tissue injury.
5. The nitric oxide formed, permits greater blood flow and may improve sexual function.
6. Increases muscle mass and strength, whilst reducing the amount of fatty tissue. A welcome benefit for sports men and women.
7. The pomegranate and fruit components are a rich source of antioxidants, needed to fight the damaging effects of free radicals.
8. Contains an extract of red wine, which helps to reduce blood cholesterol levels.
9. Affects insulin sensitivity so is particularly useful in maintaining blood glucose control.
10. Acts to release anti-ageing hormones. Who wants to look older than their years?

What Vitamins are in ARGI+?

1. Vitamin C-for immune system, a healthy nervous system, concentration sleep and healthy bones and skin.
2. Vitamin K2 – for bone formation, blood clotting, healing and vitality.
3. Vitamin B6 for immune system, a healthy nervous system brain, muscles, oxygen transportation, protein, fat and carbohydrate metabolism.
4. Vitamin D3 – for the immune system, bones, a healthy nervous system and positive mood.
5. Vitamin B9- for new cells, brain, nerves and growth.

WITH SO MANY HEALTH BENEFITS, IT’S NO WONDER L-ARGININE IS GENERATING SO MUCH EXCITEMENT AT ONLY TSH 132,000. CALL 0786139316/0769888605 FOR MORE INFORMATION.

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA MPYA YA AIRTEL MONEY TIMIZA MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi (wa tatu kushoto), Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel, Arindam Chakrabarty (kulia) wakipiga makofi baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Airtel Money Timiza, katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia) baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Airtel Money Timiza mjini Dodoma jana. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi, Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel, Arindam Chakrabarty (kulia).
  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Meneja Uendeshaji kutoka kampuni ya Airtel Tanzania,Bwa.Asupya Naligingwa akitoa maelekeo mafupi namna ya kutumia huduma hiyo mpya ya Timiza wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza, katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano.
   Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia  uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.

Article 3


MASHINDANO YA MASHUA YA MERCEDES BENZ CUP 2014 YAFANA JIJINI DAR

$
0
0
mashua
Moja ya mashua ikisukumwa kurejeshwa katika eneo lake la hifadhi baada ya kumaliza mashindano hayo.

MICHUANO ya siku 2 mwaka ya waendesha mashua za kisasa kuwania kombe la Mercedes Benz kwa mwaka huu imemalizika juzi jioni kwa waendesha mashua Al Bush akisaidia na Pugwash wakitwaa ushindi wa jumla na kutwaa kombe la Mercedes Benz.

Waendesha mashua hao yenye jina la Strophic aina ya Hobie Tiger ikiwa na namba 2653 wakikabidhiwa kombe hilo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CFAO, Wayne McIntosh ambao ndio mawakala pekee wa Mercedes Benz nchini Tanzania.

Akizungumzia mashindano hayo Mratibu wa waendesha mashua hao Michael Sulzar alisema yalikuwa na ushindani mkubwa na kwamba ingawa siku ya kwanza bahari ilikuwa shwari siku ya pili bahari ilikuwa chafu na kufanya wenye mashua kuwa na kazi ya ziada.

Alisema kwa kawaida mchezo huo unakuwa mtamu pale ambapo bahari inakuwa ‘ngumu’ ambapo waendesha mashua hao ni kama vile wanataka kutemwa kutoka kwenye mashua, hivyo wakilazimika kutumia maarifa yao kuidhibiti.
mratibu
Mratibu wa waendesha mashua Michael Sulzar akitangaza matokeo ya mashindano ya kuwania kombe la Mercedes Benz 2014 yaliyofanyika katikati ya wiki. Jumla ya timu kumi na nne (Mashua) zilishiriki katika michuano hiyo ya siku mbili.

Pamoja na washindi hao wa jumla ambao walikuwa katika mashua ya kisasa zaidi yenye Tanga mithili ya baluni washindi wengine ni Tony Hughes na Richard Stanley wakiendesha mashua Popo bawa yenye namba 2648 aina ya Hobie Tiger. Mshindi wa tatu alikuwa Cyrille Girardin akiwa na Olivier Praz waliokuwa na mashua ya Theluji namba 72 aina ya Hobie 16.

Michael Sulzer na Andreas Schimidt wao walipata tuzo ya wawili waliofanya vyema. Wawili hao walikuwa katika mashua Die Wilde 13 yenye namba 1659 aina ya Nacra Infusion. Aliyetwaa tuzo ya uanamichezo bora ni Mark Henderson na Shane Rumbold waliokuwa katika mashua Shark aina ya Hobie tiger.
kombe
Waendesha mashua Al Bush na mwenzake Pugwash wakiwa na kombe la ushindi la Mashindano ya mashua ya siku mbili ya kombe la Mercedes Benz yaliyofanyika jijini Dar es salaam Yatch Club.Washindi hao walikuwa wakiendesha mashua yao yenye jina la Strophic aina ya Hobie Tiger ikiwa na namba 2653.Walikabidhiwa kombe hilo hivi karibuni na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CFAO Motors, Wayne McIntosh (kulia) ambao ndio mawakala pekee wa Mercedes Benz nchini Tanzania.Wa Pili kulia ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed.

Mshindi wa kwanza katika mashua za kawaida alikuwa David Scott akiwa na Christina waliokuwa na mahsua Alphacrucis yenye namba112483 aina ya Hobie16. Mshindi wa pili wenye mashua Polo aina ya Hobie 16 yenye namba 111206 Andrew Boyd na Kim Troll. Mshindi wa tatu alikuwa Roland Van de Ven akiwa na Peter Scheren waliokuwa katika mashua namba 2657 aina ya Hobie Tiger iliyojulikana kama 1.

Jumla ya Mashua 14 zilishindana katika michezo iliyoandaliwa katika klabu ya Yatch ya Dar  s salaam Msasani. Baada ya shamrashamra za kupeana vikombe na tuzo nyingine Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh alipata nafasi ya kuzungumzia michuano hiyo ambayo imekuwa ikidhaminiwa na Mercedes Benz kwa miaka zaidi ya sita sasa.

mtoto
Mtoto wa mshindi wa kwanza katika mashua za kawaida David Scott (ambaye aliendesha mashua hiyo akiwa na Christina) akimsalimia Ofisa Mtendaji mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh kabla ya kukabidhiwa tuzo ya wazazi wake ya ushindi.
tuzo
Mark Henderson na Shane Rumbold wakikabidhiwa tuzo ya uanamichezo bora, walikuwa katika Mashua Shark aina ya Hobie Tiger.
ofisa
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh akizungumza kabla ya kukabidhi kombe la Mercedes Benz kwa washindi wa jumla Al Bush na mwenzake Pugwash. Michuano hiyo ilianzia na kumalizikia Dar Yatch Club Msasani. Kulia aliyebeba kombe hilo ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed.

WAZIRI MKUU PINDA ATAKA VITA DHIDI YA UJANGILI IWE YA PAMOJA

$
0
0
IMG_5264
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akizungumza na wadau waliohudhuria mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014 wakati akifunga rasmi mkutano huo wa siku mbili.
IMG_5253
Waziri wa Mali asili na utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kushoto) kufunga rasmi mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Magese Mulongo, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu, Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli wakiwa meza kuu.
IMG_5198
Mwakilishi wa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania akichukua taswira za baadhi ya matukio yaliyokuwa yakiendelea mkutanoni hapo.
IMG_5197
Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki mkutano huo.
IMG_5236
Baadhi ya wawakilishi kutoka nchi tisa wakitia saini Azimio la Arusha la kukabili ujangili mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Nchi hizo ni Burundi, Kenya, Uganda, Msumbiji, Tanzania, Sudan Kusini, Zambia, Rwanda na Malawi.
IMG_5205
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kwenye ufungaji wa mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014.

IMG_5224
Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke, akizungumza kwa niaba ya serikali ya Ujerumani.
IMG_5212
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri wa Mali asili na utalii, Mh. Lazaro Nyalandu wakati wa ufungaji rasmi wa mkutano huo uliodumu siku mbili jijini Arusha.
IMG_5268
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiondoka ukumbini hapo mara baada ya kuufunga rasmi mkutano huo.

IMG_5170
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mbunge wa Kahama, James Lembeli, huku Waziri wa Mali asili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akifurahi jambo ndani ya chumba cha mapumziko kabla ya kuelekea kwenye chumba cha mikutano.
IMG_5169
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli (wa pili kulia) kwenye chumba cha mapumziko baada ya kuwasili ukumbi hapo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu.
IMG_5182
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye chumba maalum cha mapumziko.

IMG_5158
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri mara baada ya kuwasili kwenye makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki kufunga Mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Waziri wa Mali asili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu na wa pili kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
* Ataka iundwe timu kufuatilia utekelezaji wa Azimio la Arusha 2014

Na Ofisi ya Waziri Mkuu
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema inahitajika dhamira ya kweli kutoka kwa wadau wote katika kutekeleza Azimio la Arusha la kukabiliana na ujangili na kuendeleza hifadhi za wanyama katika nchi za Afrika Mashariki na zilizo Kusini mwa Ikweta.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni (Jumamosi, Novemba 8, 2014) mara baada ya kufunga mkutano wa kikanda wa siku mbili uliojadili mbinu za kupambana na biashara haramu ya wanyamapori ulioandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Arusha, Waziri Mkuu alisema: “Suala hili linataka uwajibikaji wa pamoja. Mashirika na taasisi, wananchi na viongozi sote kama wadau wakuu, kila mmoja anapaswa kushiriki vita hii kama kweli tunataka tuitokomeze.”

“Kwenye hili Azimio la Arusha na nyie waaandishi wa habari pia mna sehemu yenu mmetajwa... wamesema wanatafuta jinsi ya kushirikiana na vyombo vya habari ili visaidie kutoa elimu kwa jamii kama njia ya kuelimisha umma,” alisema. Waziri Mkuu aliwaeleza waandishi hao kwamba Azimio hilo lina vipengele 20 ambavyo vinataka utekelezaji katika ngazi ya nchi mojamoja, ngazi na kanda na ngazi ya kimataifa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
IMG_5160
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akielekea kwenye chumba cha mapumziko kabla ya kufunga mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Waziri wa Mali asili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu.

“Nimepata faraja kwamba mkutano huu haukuisha kijumlajumla tu, bali umekuja na maazimio 20 ambayo yametengwa kwa ajili yetu sisi wa ndani, mengine yanahusisha ushirikiano wa kikanda na yako mengine yanawahusisha wadau wa maendeleo,” alifafanua.

Ili kutekeleza azimio hili, nimeshauri iundwe timu itakayoshirikisha vyombo vingi zaidi badala ya kuiachia Wizara ya Maliasili na Utalii peke yake. Timu hii ikutane kila baada ya miezi sita ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio haya na ikibidi Waziri atoe taarifa bungeni kuhusu utekelezaji huo,” alisema Waziri Mkuu.

Mapema, akizungumza na washiriki wa mkutano huo wakati wa kuufunga, Waziri Mkuu alisema kuwepo kwa watu wa ngazi tofauti kwenye mkutano huo ni kielelezo tosha cha umakini wao na nia thabiti ya kutokomeza ujangili katika ukanda huu.
IMG_5167
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli kwenye chumba maalum cha mapumziko kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufunga mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014.

“Tumeanzisha vita, tusisahau kwamba bado kuna kazi kubwa mbele yetu na vita haijaisha. Tuzidishe mapambano katika sehemu tatu: kwenye nchi unakofanyika ujangili, nchi ambazo nyara zinapitishwa na nchi zinazopokea ama kununua hizo nyara,” alisema Waziri Mkuu.

“Nakubaliana nanyi kwamba hakuna nchi inayoweza kukabili suala la ujangili ikiwa peke yake. Tunahitaji tuwe na sera mahsusi, sera ya pamoja ya kutuunganisha na kutuongoza wakati tukitekeleza Azimio hili kwa kusaidiana na wadau wa maendeleo,” alisema.

Alisema Azimio hilo litaipa kazi ya ziada ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo kazi kubwa itakuwa ni kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wa wa Azimio hilo unakuwa wa ufanisi. Jumla ya nchi tisa zimetia saini azimio hilo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Nchi hizo ni Burundi, Kenya, Uganda, Msumbiji, Tanzania, Sudan Kusini, Zambia, Rwanda na Malawi.

MAJINA YA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI HAYA HAPA.

$
0
0
Maelekezo Muhimu.

  1. Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014, kidato cha nne mwaka 2013 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita, Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani, Oljoro, Rwankoma na Kimbiji wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi.

  2. Wahitimu hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti tarehe 28/11/2014 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wa kuwapeleka Shule ya Polisi Tanzania tarehe 30/11/2014.

  3. Zoezi la usajili litaanza shuleni hapo tarehe 01/12/2014 hadi tarehe 15/12/2014. Atakaefika kuanzia tarehe 16/12/2014 hatapokelewa.

  4. Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Shule ya Polisi Tanzania mjini Moshi.

  5. Vijana hawa watalazimika kufika shuleni wakiwa na mahitaji yafuatayo:

    1. Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

    2. Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)

    3. Chandarua chenye upana futi tatu

    4. Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)

    5. Pasi ya Mkaa

    6. Ndoo moja

    7. Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=).

    8. Pesa kidogo ya kujikimu.

  6. Kwa mujibu wa kanuni za shule ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa shuleni hapo. Shule itaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.

  7. Angalia orodha kwenye tovuti ya www.policeforce.go.tz au fika Ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya iliyopo Forest barabara ya mahakama kuu.


NSSF walibeba tamasha la Handeni Kwetu 2014

$
0
0
SHIRIKA la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Tanzania, limejitokeza tena kudhamini Tamasha kubwa la Utamaduni linalojulikana kama ‘Handeni Kwetu’, lililopangwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu, katika Uwanja wa Azimio (Kigoda Stadium), wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Hii ni mara ya pili kwa mfuko huo wa hifadhi kudhamini tamasha hili la utamaduni lilioanza mwaka jana, ambapo lilifanyika kwa mafanikio makubwa kwa kushirikisha vikundi vya ndani na nje ya Handeni, wakiwamo wa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kwamba kujitokeza kwa NSSF ni kitendo cha kiungwana kinacholiweka tukio lao katika kiwango kizuri na mafanikio makubwa.

Alisema kwa kuliangalia hilo, wameamua kutoa haki ya jina, ambapo sasa tamasha lao litakuwa linajulikana kama NSSF Handeni Kwetu, wakiamini kuwa ni ishara nzuri ya ushirikiano baina yao na wadau wote wa shirika hilo.

“Yapo mashirika mengi Tanzania bila kusahau kampuni ambazo zingeweza kudhamini matukio ya aina hii ambayo yana mchango mkubwa kwa taifa letu, lakini baadhi yao yamekuwa magumu mno kudhamini au hata kuyasaidia kwa namna moja ama nyingine.

“Shirika kama NSSF linapoamua kuingia kudhamini ni kuonyesha jinsi wanavyoithamini jamii yao, jambo ambalo kwetu sisi ni furaha kubwa na kuona ipo haja ya kutafuta namna ya kurudisha fadhira kwa wadau hawa muhimu nchini Tanzania,” alisema.

Kwa mujibu wa Mbwana, siku ya tamasha, kutakuwa na shughuli ya kusajili wanachama wapya wa kujiunga na NSSF, ili waweze kunufaika na huduma za mafao kwenye Shirika hilo kubwa la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii hapa nchini.

Wadhamini wengine wa tamasha hilo ni pamoja na Phed Trans, SmartMind & Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd kwa kupitia kitabu cha ‘Ni Wakati wako wa kung’aa, Handeni Kwetu Foundation, Wait & Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt Ltd na Michuzi Media Group.

UNDP WAZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI NOONDOTO NA ELANG’ATADAPASH

$
0
0
IMG_4368
Pichani juu na chini ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikata utepe kuzindua rasmi mradi mkubwa wa maji wa kwa vijiji vya Noondoto na Elang’atadapash uliosaidiwa na UNDP. Kushoto ni Mratibu Kitaifa kutoka UNDP, Bw. Nehemia Mususuri akishuhudia tukio hilo.
IMG_4373
IMG_4399
Jiwe la msingi kama linavyosemeka pichani.
IMG_4420
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wakazi wa vijiji vya Noondoto na Elang’atadapash mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji.
IMG_4428
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akinawa mikono na maji hayo mara baada ya kuzindua rasmi tangi kubwa la maji kijijini hapo.
IMG_4438
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa jiji cha Elang’atadapash, Bi. Nabulu Kumokndare kama ishara ya kuzindua rasmi mradi huo.
IMG_4451
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akikagua kisima cha maji cha kijiji hicho.
IMG_4483
Wanyama wakinywa maji safi na salama wakati wa sherehe za kuzinduliwa rasmi kwa mradi mkubwa wa maji utakaohudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.

IMG_4471
Mbuzi wakinywa maji kwenye josho maalum litakalotumika kuhudumia mifugo ya vijiji hivyo.
IMG_4521
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akizungumza na wakazi vijiji vya Noondoto na Elang’atadapash ambapo aliwaasa kutunza mradi huo kwani maji ni uhai.
IMG_4560
Mzee wa kijiji cha Elang’atadapas, Miaroni Lailuda akimwombea dua na baraka Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez pamoja na shirika lake kwa msaada huo.
IMG_4605
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua mradi huo.
IMG_4156
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro akiongoza gari ya Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye kijiji cha Elang’atadapash wilayani Longido kuzindua mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na UNDP.

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amewataka wananchi wa Longido kwa kushirikiana na viongozi wao kutunza vyanzo vya maji katika wakati huu ambapo mabadiliko ya tabia nchi yanafanya maeneo mengi kuwa makame.

Alvaro alisema hayo wakati akizindua mradi mkubwa wa maji wa kwa vijiji vya Noondoto na Elang’atadapash uliosaidiwa na UNDP ambao unahudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.
Mratibu huyo alisema kwamba utunzaji wa vyanzo vya maji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 92 utawezesha wanawake kuendelea kushiriki katika kazi nyingine za jamii badala ya kuhangaika kutwa kusaka maji.

Aidha alisema viongozi wanatakiwa kuendelea kutoa elimu wa kutunza vyanzo vya maji na mradi huo ili uwe endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
IMG_4168
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akiongozana na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro (kulia) mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Elang’atadapash tarafa Kitumbeine wilaya ya Longido mkoani Arusha kuzindua mradi mkubwa wa maji uliosaidiwa na UNDP ambao utahudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.

Aliwashukuru wakazi wa eneo hilo kwa kuthamini na kutambua kwamba mradi huo ni wao na hivyo kuamini kwamba watafanya kila waliwezalo kuutunza hasa kwa kuzingatia matatizo yaliyopo sasa ya ukame na mabadiliko ya tabia nchi. Mradi huo ambao ulifanyiwa kazi na shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists initiative,baada ya kupata ruzuku ya UNDP umelenga kuboresha maisha ya watu, afya ya mifugo na wanyamapori kwa kuwapatia maji safi na salama.

Aidha fedha zilizotolewa na UNDP zimefanyakazi ya kujenga tangi la mita za mraba 45 katika kijiji cha Elang’atadapash,matangi ya kuvuna maji ya mvua matano na kila moja likiwa na mita za mraba tatu, ukarabati wa matangi matatu ya kuwezesha msukumo wa maji,kukabarati vituo vya kuchotea maji vinne na kufundisha vyama vya ushirika vya watumia maji 10 katika kata za Ketumbeine, Elang’atadapash na Iloirienito zilizopo wilayani Longido.
IMG_4171
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisalimiana na wanawake wa Kimasai wa kijiji cha Elang’atadapash alipowasili kijijini hapo kuzindua mradi wa maji unaofadhiliwa na UNDP.

Aidha wananchi wamefunzwa namna ya kufanya menejimenti ya maji.
Katika risala yao iliyosomwa na Mike Olemokoro wa Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists initiative IPI Tanzania, wananchi hao pia wamesema mchango wao wa kazi na pia wa halmashauri katika masuala ya kiufundi yamechukua asilimia 40. Maji hayo yanatarajiwa kuwasaidia wananchi wa kata za Ketumbeine, Elang’atadapash na Iloirienito.
IMG_4181
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na mmoja wakazi wa kijiji hicho aliyefika kumlaki. Kulia ni Diwani wa viti maalum kata ya Elang’atadapash wilayani Longido Naini Mokoro.
IMG_4196
Na hili ndio tangi la mita za mraba 46 katika kijiji cha Elang’atadapash lililojengwa na UNDP kwa ajili ya kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji hicho ambalo litahudumia wakazi 9,700 na mifugo 47,700.
IMG_4202
Mratibu Kitaifa kutoka UNDP, Bw. Nehemia Mususuri akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Katikati ni Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro.
IMG_4209
Kikundi cha wakinamama wa Kimasai wakitoa burudani kwa mgeni rasmi kabla ya kuzindua mradi huo wa maji.
IMG_4275
Meza kuu.
IMG_4296
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la wafugaji la Ilkisongo Pastoralists Initiative (IPI) Bw.Mike Olemokoro (mwenye shati jekundi) wakisoma risala pamoja na mkalimani wa lugha ya Kimasai kwa mgeni rasmi Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_4311
Diwani wa viti maalum kata ya Elang’atadapash wilayani Longido Naini Mokoro, akimvisha kikoi Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kama shukrani ya jamii ya wafugaji na wakazi wa kata hiyo.
IMG_4316
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akipokea fimbo yenye heshima ya uchifu wa kimasai kutoka kwa Diwani wa viti maalum kata ya Elang’atadapash wilayani Longido Naini Mokoro.
IMG_4329
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipozi na baadhi ya wakina mama wa Kimasai wa kijiji cha Elang’atadapash.

Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images