Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 402 | 403 | (Page 404) | 405 | 406 | .... | 1897 | newer

  0 0

  IMG_4025

  Mratibu wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) alipotembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNDP wilayani Longido mkoani Arusha katika ziara yake ya siku mbili mara baada ya kuwasili wilayani humo. Katikati ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu aliyeambatana na Mwakilishi huyo.
  Na Mwandishi wetu.

  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amewataka wadau wa mazingira nchini kuwasaidia wananchi wa vijijini hasa wafugaji kutumia nguvu na rasilimali walizonazo kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuendelea kuhifadhi mazingira na viumbe vilivyopo wakiwemo wanyamapori.

  Bw, Rodriguez aliyasema hayo wilayani Longido mkoani Arusha katika ziara yake ya siku mbili ya kutembelea baadhi ya miradi inayofadhiliwa na shirika hilo . Akizungumza baada ya kutembelea na kuzindua mradi wa kuwawezesha wafugaji wa wilaya ya Longido kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kujenga uzio wa kulinda mifugo yao na wanyama wakali Bw, Rodriguez, amesema kutokana na uelewa mdogo wa mabadiliko yanayoendelea kutokea wananchi wengi wa vijijini wanahitaji msaada wa namna ya kuyadhibiti.
  IMG_4027
  Mratibu wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha akiendelea kutoa maelezo kwa Mwakilishi huyo Bw. Alvaro Rodriguez (katikati), wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya.
  Aidha alisema kwa sasa wananchi wengi wanatumia muda na nguvu nyingi kushughulikia matokeo ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na maeneo mengi wamekuwa wakijikuta wanagombana wenyewe kwa wenyewe badala ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya msingi.
  "mara nyingi wananchi wa vijijini kama hawa wafugaji mmekuwa wamekuwa wakilaumiwa kwa matokeo ya yale wanayoyafanya kwa kusukumwa na mabadiliko haya na mengine wangeweza kuyajua wala wasingeyafanya "alisema Rodriguez.

  Aidha Bw. Rodriguez ambaye pia ni Mkuu wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na shirika hilo hapa nchini amewataka viongozi na watendaji wakiwemo watalaam kutumia muda na uwezo wao kuwasaidia wananchi wa vijijini hasa wafugaji na kwamba UNDP itaongeza nguvu kusaidia makundi hayo.
  IMG_4033
  Mratibu wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha akimwoonyesha eneo maalum lililowekwa uzio kwa ajili ya kulinda mifugo na wanyama wa kali Mwakilishi huyo Bw. Alvaro Rodriguez aliyefika wilani hapo kukagua miradi hiyo.

  Mratibu wa mradi wa kudhibiti wanyama wakali kwa kutumia waya na mitii maalumu inayohimili ukame unaofadhiliwa na UNDP Dr. Maurus Msuha ambaye pia ni mtafiti mkuu wa wanyama katika taasisi ya utafiti wa wanyamapori TAWIRI amesema mradi huo umeonyesha mafanikio makubwa kwa kuanza kupunguza uhasama kati ya wafugaji na wanyama pori wanaokula mifugo yao wakiwemo Simba na Fisi.

  Kwa upande wao viongozi na wananchi akiwemo Mkuu wa wilaya ya Longido Bw James Ole Milya wamesema pamoja na changamoto zinazowakabili wanaendelea kutilia mkazo suala la utunzaji wa mazingira na wanyamapori kwani licha ya kuwa ni asili yao ndio msingi wa maisha yao.
  IMG_4039
  Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya (kulia) akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) wakati alipotembelea wilaya hiyo kukagua maendelo ya miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP. Kushoto ni
  IMG_4057
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akisalimiana na na wanawake wa kimasai mara baada ya kuwasili wilayani Longido kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
  IMG_4064
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mheshimiwa James Ole Millya kwa pamoja wakizundua uzio wa kuhifadhia mifugo ya jamii ya wafugaji wilayani Longido wakati alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
  IMG_4070
  Muonekano wa uzio utakaotumika kuhifadhia wanyama wasidhurike na wanyama wakali mara baada ya kuzinduliwa rasmi.
  IMG_4111
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akitoa nasaha zake kwa jamii ya wafugaji wa wilaya ya Longido mkoani Arusha alipofanya ziara ya siku mbili kukagua miradi inayofadhiliwa na shirika la UNDP.
  IMG_4075
  Baadhi ya wakazi wa Longido ambao shughuli zao kubwa ni ufugaji wakimsikiliza Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
  IMG_4121IMG_4077
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akivishwa zawadi ya shuka la kimasai na mmoja wa wafugaji wa wilaya hiyo.
  IMG_4088
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisikiliza maelezo ya zawadi za asali za Nyuki wadogo na wakubwa kutoka kwa jamii za wafugaji wanaofadhiliwa na shirika la UNDP wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi hiyo wilayani humo.

  0 0


  Tanzania Diaspora Initiative (TDI) has launched the TDI Database & Resources center, whose purpose is to improve information dissemination to the Tanzanians in the diaspora by bringing the people together to a common platform to discuss and share ideas that help to ensure their collective progress and their respective communities in Tanzania.

  The diaspora database collects the information of the Tanzanians in the database so as to make it easy to regularly disseminate information concerning various opportunities. This is equally a point of contact that stakeholders can use to share important information.

  Often times, it proves difficult to easily find the relevant information on some specialized areas such as investments, projects management, or document handling in Tanzania as it is usually spread across many institutions. Access to this information might not be so straight forward and may need expert’s advice to lead you through the processes. TDI intends to regularly collect this information, put it in a simple language and update the respective pages to ensure that it is always available for reference and use.

  In order for the Tanzanians in the diaspora to be motivated to invest or contribute towards their communities, they must have access to regular updates regarding investment opportunities, key changes in policies affecting their projects, investments, businesses or aspirations. This is where Diaspora Resource Center comes in.

  Diaspora Resource Center is a member designated area where all information concerning investment opportunities and other key information regarding Tanzania are regularly updated.
  Examples of information that will be available here include: important policies and statutes that may be critical to certain projects, investments or businesses, and changes in these and any other information that might be useful.

  At times, to have a good head start in a project, some projects may require a good knowledge of some sector specific information. The TDI information portal will also enable interaction between TDI and members of the diaspora with regard to this kind of information requirement.

  One of our major goals to spread news to the Diasporas is the near future launch of the Newsletter, which will mainly focus on specific areas that will be useful and relevant to people living outside Tanzania. Currently, we are conducting a survey to determine the best possible contents of this newsletter.

  The possibilities are infinite, we have a lot of ideas that are poised to benefit the Tanzanians in the diaspora to handle their investment and projects back home. These may include, but not limited to, interesting and exciting promotions that Tanzanians Diasporas will find beneficial as these will give them free access to some of the TDI professional services.

  To move towards the aforementioned goals, we have created a diaspora database. Access is still very simple. Simply register by choosing the member type. Based on this registration, we will contact you and provide more details about this information portal.

  Join us and be a part of the bigger community
  --

  The TDI Team

  0 0

  KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akimkaribisha Balozi wa Rwanda hapa nchini, Eugene Kayihura, kabla ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa Rwanda hapa nchini, Eugene Kayihura, akijitambulisha kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kabla ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Balozi huyo, Ernest Bugingo.
   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Balozi huyo. (Picha na Bashir Nkoromo)

  0 0
   Chagua mkoa hapo Juu na  kisha ubonyeze kucheki shule yako

  0 0

  Rais Profesa Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe said Meck Sadik na Meneja wa Huduma za Shirika la ndege la Emirates katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere Bw.  Aboubakar Juma leo Novemba 6, 2014 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea Marekani kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake
   Rais Profesa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na askari polisi pamoja na wafanyakazi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya kupanda ndege ya shirika la Emirates kuelekea Marekani leo Novemba 6, 2014

  0 0

  Baada ya Mwezi Oktoba kuisha ambapo kubwa lilikua ni kukuza uelewa juu ya matumizi salama ya mitandao, Taarifa ya kumalizika kwa mwezi huo inaweza kusomeka "HAPA" Mambo mengi tuliyo yajadili yameonekana kuangaziwa tena kwenye kongamano la maswala ya TEHAMA Jijini Cairo Nchini Misri. Muundo wa kongamano hili ulihusisha meza kuu inayo fungua mijadala na wasikilizaji kuchangia na kuuliza mwaswali pamoja na kupata njia ya kufikia malengo kupitia mada tofauti tofauti.

  Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba, Katika Meza kuu ya Mjadala alio husisshwa alipata kuzungumzia jinsi teknolojia ya habari na mawasiliano inavyo patiwa kipaumbele cha mwishoni na idara za fedha katika mataifa mbali mbali ingawa ni sekta ambayo ina nafasi kubwa sana katika kuleta mabadiliko na kukuza kwa haraka uchumi wan chi yeyote kama itatumika vizuri.

  Aidha, Kwenye Meza kuu ambayo Nilikua nimehusika tulipata kuangazia maswala mbali mbali na huku nikizungumzia kwa kina jinsi usalama mitandao utakapo achwa kupewa kipaumbele unavyo weza kurudisha nyuma jitihada za dhati za kutumika vizuri kwa teknolojia ya Habari ili kukuza uchumi wan chi mbali mbali.

  Pia nilipata kuzungumzia umuhimu mkubwa wa kuhakikisha mataifa ya Afrika yanaongeza jitihada ili kuhakiki Mafunzo yahusuyo usalama mitandao yanakuzwa kwa kasi ili kuhakiika wataalam wa kutosha wanapatikana na kusababisha watumiao vibaya teknolojia ya habari na mawasiliano wanaweza kuangazwa kiurahisi na kudhibitiwa kwa manufaa ya kukuza uchumi wan chi yoyote duniani.

  Katika Mkutano Huu ambao Pia ulihudhuriwa na Mkuu wa  Intel  bwana John E. Davies, Kama anavyo onekana kwenye picha akiwa na Mkuu wa Intel katika Nchi ya Misri, Sikusita kukutana nao na kujadili maswala mbali mbali yahusuyo usalama mitandao huku nikitaka kujua jinsi gani Intel inajipanga kuhakiki uinzi mtandao unakua na nafasi nzuri.


  Katika Kunipatia Majiibu, Nilifarijika kujua ya kua Intel imejipanga kuweka ulinzi mtandao katika vifaa vyake ambavyo kwa kushirikiana na program za Anti-virus kwa pamoja zitaimarisha ulinzi wa kina katika Komputa. Alinihakikishia hatua yao hiyo haita punguza soko la matumizi ya Anti-virus bali kwa pamoja patapatiwa namna ya kuongeza nguvu ili kukabiliana na wimbi la virusi vinavyo tumwa kwenye Komputa za watumiaji ili kuleta athar.

  Aidha, Kwa Upande wa Waziri mwenye dhamana ya Sayansi na Teknolojia Nchini Misri, Enginia Atef Helmy mbali na kuonyewha kufurahi sana kuona mimi nilifanikisha kuhudhuria mkutano huo alinieleza anajitihada za dhati kuhakikisha panapatikana daraja madhubuti la kuunganisha Afrika kuanzia kusini hadi kazkazini.

  Aliifafanua na kusema kwa kushirikiana Nchi za Afrika katika maswala ya Tehama na pia kuimarisha nguvu ya pamoja anaimani kabisa teknolojia ya Habari na mawasiliano ina nafasi kubwa sana ya kuleta mabadiliko katika dunia ya kesho. Pia alinieleza kwa kina ya kua vijana ndio hasa nguvu kazi inayo itajika na dunia ya leo ili kuhakiki mambo yanasogea vizuri.

  Mbali na mijadala mbali mbali, Pia palikua na matukio yakutia saini makubaliano ya kukuza ushirikiano nanchi za bara Asia pamoja na mataifa mengine. Palipatikana Ziara maalum ya kutembelea idara maalum inayo husika na maswala ya ulinzi wa mitandao wan hi ya Misri. Pale tulipata kujionea shughuli mbali mbali zinazocfanyika kuhakiki Nchi ya Misri inabaki salama mitandaoni.

  Huko mbali na kujionea mengi na matumizi makubwa ya teknolojia yanavyo tumika kuhakiki Nchi inabaki salama kiimtandao. Tulipata kuonyeshwa changamoto mbali mbali walizo kumbana nazo kama taifa na ukanda mzima wa Nchi za mashariki ya kati.


  Aidha, Ufafanuzi mzuri wa namna changamoto zimetumika vizuri kuwa Fursa na kuhakiki mambo yanasogea tulipata kujizwa. Na pia tulipata kuonyeshwa jia mbali mbali zinazo tumika nan chi hiyo ili kuhakiki wataalam wa maswala ya usalama mtandao wana zalishwa ipasavyo ili kuweza kukabiliana na changgamoto za uhalifu mtandao zinazo endelea kukua kwa kasi. Mengi yalikuua yanafanana na nilicho kizungumza na kituo cha "MLIMANI TV" ili kutolea ufafanuzi baadhi yam ambo.

  0 0

   Valerian Luzangi (kushoto) ambaye ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha shampoo za binadamu na wanyama hasa mbwa cha L & V Intergrated Firm akimuonesha Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi,  shampoo  ambayo iko tayari kuuzwa. Tbl kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa ilimpatia  mfanyabiashara huyo chupa 20,000 za kuwekea shampoo. Kiwanda hicho kipo Mikocheni Dar es Salaam.
   Valerian Luzangi (kulia) ambaye ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha shampoo za binadamu na wanyama hasa mbwa cha L & V Intergrated Firm akimuonesha Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi,  shampoo ya kuoshea mbwa ambayo iko tayari kuuzwa. Tbl kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa ilimpatia  mfanyabiashara huyo chupa 20,000 za kuwekea shampoo. Kiwanda hicho kipo Mikocheni Dar es Salaam.
   Mmoja wa wafanyakazi walioajiriwa na kiwanda hicho akiweka maji kwenye pipa tayari kuchanganywa na dawa wakati wa kutengeza shampuu.
   Mfanyakazi wa kiwanda hicho akiweka dawa kwa ajili ya kutengeza shampoo ya kuoshea nywere za binadamu
   Wafanyakazi wakibandika lebo kwenye chupa zenye shampoo
   Chupa zenye shampoo zikiwa tayari

   Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamhuri Leither Product, Jamhuri Oisso (kulia), akimuonesha Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi moja ya viatu wanavyotengeneza katika kiwanda cha kushona viatu kilichopo Manzese, Dar es Salaam kilichowezeshwa mashine na TBL,

   Baadhi ya viatu vinavyotengenezwa katika kiwanda hicho
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamhuri Leither Product, Jamhuri Oisso (kulia), akimuelekeza fundi  Amir Mbungi jinsi ya kushona viatu kwa kutumia cherehani cha kisasa katika karakana yake iliyopo Manzese, Dar es Salaaam. Cherehani hiyo alipewa tuzo na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamhuri Leither Product, Jamhuri Oisso akionesha jinsi ya kutumia mashine za kisasa kubandika soli ya viatu katika karakana hiyo.mashine hiyo alipewa tuzo na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa.

  0 0

  Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia) akimkabidhi msanii wa Orijino Komedi, Mjuni Silvery 'Mpoki funguo ya moja ya nyumba za gharama nafuu walizokopeshwa wasanii  wa kikundi hicho na NSSF wakati wa hafla fupi ya kukabidhi wasanii hao zilizopo Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam hivi karibuni, mkopo huo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15. (Na Mpiga Picha Wetu)
  Baadhi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kukopeshwa wasanii wa kikundi cha Orijino Komedi Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo katika mradi wa ujenzi wa Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.

  Mac Reagan 'Kipara' na Mjuni Silvery 'Mpoki wakiangalia moja kati ya nyumba walizokabidhiwa na NSSF baada ya kukopeshwa na Shirika hilo na mkopo utalipwa kwa kipindi cha miaka 15.
  Kushoto, Mac Reagan, Joti na Mpoki wakiangalia nyumba zao walizokabidhiwa na NSSF.
  Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly akimkabidhi funguo ya nyumba msanii wa Orijino Komedi.  

  Msanii Isaya Mwakilasa 'Wakuvwanga' akipokea funguo ya nyumba yake.

  Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' akipokea funguo ya nyumba yake kutoka kwa Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly (kulia)
  Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abdallah Mselly akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba kwa wasanii kikundi cha Orijino Komedi.
  Msanii Mac Reagan akizungumza baada ya makabidhiano ya nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NSSF Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam.

  Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' akifafanua jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa nyumba.

  0 0

  Pichani (Katikati) ni Mwanaafa Mwinzagu ambae ni Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya wafanyakazi na Wadau wa Kampuni ya Proin Promotions ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la TMT mara baada ya kutangazwa mshindi wa Kitita cha Milioni 50 za Kitanzania katika fainali ya shindano la TMT lililomalizika Mnamo tarehe 30 Aug 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City na Kumtangaza Mwanaafa Kuwa Mshindi kwa Mwaka 2014.
  Mwanaafa Mwinzagu akiwa amembeba Mdogo wake mara baada ya kutangazwa mshindi wa Shindano la TMT 2014 lilifanyika tarehe 30 August 2014 katika Ukumbi wa Mlimani city.
  Mwanaafa Mwinzagu ambae alishiriki Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) huku akiwa ni Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Tandika iliyopo Mjini Mtwara katika Manispaa ya Mtwara amefaulu mitihani yake ya kumaliza elimu ya Msingi Kwa Kupata daraja C huku Masomo ya Hesabu na Sayansi akiwa kafanya vizuri sana kwa Kupata Daraja B.
   Wakati Shindano la TMT lilipofika Mtwara kwaajili ya kusaka vipaji vya kuigiza Ndipo Mwanaafa alipojiunga na Kuja kushiriki Katika SHindano hilo Kubwa na lenye mvuto wa Pekee Afrika Mashariki na Kati. Wakati akihojiwa mara baada ya Kutoka katika hatua ya Kwanza ya Shindano hilo lililofanyika Mtwara na kuhojiwa Mwanaafa Mwinzago alisema 

  "Hiki ni Kipaji kwahiyo sina haja ya kuficha na pia naweza Kukosa kwenye Shule nikapata Kwenye Kuigiza na ndio maana nimekuja Kushiriki" Vilevile alipoulizwa Je Ikitokea Ukashinda itakuwaje Shule na Sanaa? Alijibu kuwa "Ikitokea nikashinda katika ngazi ya Kanda ya Kusini Nitaenda Kambini Dar Es Salaam na kuacha Shule kwanza, Maana Shule Ipo ila Shindano hili linapita tu Kwahiyo Naweza kupata kwenye Sanaa na nikishinda basi nitarudia Darasa".BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»
  Mara baada ya Kuibuka MShindi katika Kinyanganyiro Hiko Katika Ngazi ya Kanda ya Kusini, Timu nzima ya TMT iliweza kumuhoji Mwalimu wake Mkuu ambapo alisema yafuatayo "Huyu Ni mwanafunzi wa Darasa la Saba Kwa Sahivi na Hiki pia ni kipaji lakini Sisi kama Wazazi hatuwezi kuzuia Mtoto kuonyesha Kipaji chake yeye alichofanya alishiriki Mashindano na ameshinda kwahiyo sisi kama walimu wake tutajadiliana jinsi ya kulitatua hili kwa maana hatuwezi kujua labda mshindi wa Milioni 50 hatakuwa yeye"
  Mara baada ya Shindano la TMT kumalizika tarehe 30 August 2014 wiki moja baadae Mwanaafa aliweza Kurejea Mjini Mtwara kwaajili ya Kufanya mitihani yake ya Kuhitimu Elimu ya Msingi na Hatimae mara baada ya kuwasili nyumbani kwao Mwanaafa aliweza kwenda shule kwao kwaajili ya kukamilisha taratibu za kufanya mtihani na kesho Mwanaafa akaweza kufanya Mitihani yake vizuri kwa muda wa siku mbili na alipomaliza Alirejea Jijini Dar Es Salaam ambapo Aliendelea na zoezi la Kurekodi filamu ya Pamoja Ya Washindi wa TMT waliofanikiwa kuingia Hatua ya Kumi Bora huku yeye akiwa ni kinara katika filamu hiyo ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Mapema Mwezi wa Kumi na Mbili katika Mikoa yote ambayo TMT ilipita kwaajili ya kusaka Vipaji.
  Hapo Majuzi kupitia Vyombo mbalimbali vya habari kupitia Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lilitangaza matokeo ya Mitihani ya Elimu ya Msingi na Ndipo tulipofahamu kuwa Mwanaafa ameweza kujitahidi sana katika Mitihani huku akiwa kafanya Vizuri sana katika Masomo ya Hesabu na Sayansi ambapo amepata daraja B huku masomo mengine akiwa amepata daraja C na Kupelekea kupata wastani wa daraja C.
  Kwa Matokeo hayo tunapenda kumpongeza Mwanaafa kwa kuonyesha uwezo wake katika Masomo na hatimaye kufanya vizuri katika Mitihani yake ya Mwisho ya Kumaliza Elimu ya Msingi
  Ikumbukwe kuwa hapo awali Mwanaafa alisema kuwa endapo atashinda Milioni 50 katika fainali ya Shindano la TMT lililomalizika tarehe 30 August 2014 basi atatumia Kiasi hiko cha pesa kwaajili ya kujiendelea kielimu lakini Wakati wa Fainali hiyo Kampuni ya Proin Promotions Ltd iliahidi kumsomesha Mwanaafa hata Kama asingeshinda katika Shindano hilo.
  Kwasasa Mwanaafa yupo chini ya Uangalizi wa Kampuni ya Proin Promotions ambapo kampuni hiyo itamsomesha Kuanzia Kidato cha Kwanza hadi Cha Nne.
  Kampuni ya Proin Promotions Ltd inapenda kumpongeza Mwanaafa kwa kufanya Vizuri katika Mitihani yake ya Kumaliza Elimu ya Msingi na kuonyesha Kuwa Kumbe Bado ni Mshindi hadi Darasani.

  0 0
   Meneja Wa Chama Cha Ushirika wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw.Damai J Mapunda Akitoa Muongozo Jinsi gani Mkutano Utakavyo Endeshwa  
  Mwenyekiti Wa Chama Cha Ushirika cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Erasmo A.Mbilinyi Akiwasilisha taarifa aliyo iandaa kwa kipindi Cha November 2013 Hadi September 2014 Katika Mkutano Huo
   Makamu Mwenyekiti Mpya Bi.Mabel Masas Ambapo Chama Cha TCRA SACOSS kiliweza kufanya Uchaguzi Katika Kuendeleza Kuimarisha Chama Na Kisheria Za Chama
  Bw.Damian.F.Mashauri Mkaaguzi wa COASCO Ambaye aliwakilisha kwaniaba ya wakaguzi wengine Wanaofanya kazi za Ukaguzi katika Vyama Vya Usharika Hapo akitoa Taarifa ya Ukaguzi katika Mkutano waTCRA SACOS.
   Dk. Raymond Mfungahema ambaye aliwakilisha ripoti ya upande wa wajumbe wakamati ya usimamizi waSACOSS ya TCRA
  Washarika wakiendelea kufuatilia kwa umakini Mkutano huo
   Miongoni Mwa Wanachama Cha  Ushirika cha TCRA  walio weza kuhudhuriaMkutano wa Pili  
   Bw.Charlse Thomas Mjumbe wa Bodi Akisisitiza jambo katika mkutano huo
   Bw.Abduh Husein Akitoa mchango wake wa mawazo katika Mkutano huo
   Wanachama wakiwa katika mkutano 
   Bw.Francis MAYILA. akiwa ni Mwana Kamati Ya Usimamizi akichangia Maada Iliyokuwa ikiendelea Katika Mkutano huo
   Masai John Masai  Akiomba Kura  Ya kuchaguliwa Katika Nafasi ya Kuwa Mjumbe Wa Bodi na Hatimaye kuweza Kunyakuwa Nafasi hiyo Baada ya Wanachama Kumpigia Kura 
   Afisa Ushirika Kinondoni Philipo Emannuel Akitoa nasaha katika mkutano huo uliofanyika Katika Ukumbi wa TCRA.
  Omary Mkamba  Afisa Usharika Ambaye Ndiye Aliyekuwa Akiendesha Maada zote zilizo kuwa Zikiendelea Katika Mkutano Huo

  0 0

  GU9A8625
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog)

  RAIS Jakaya Kikwete ameitaka jumuiya ya kimataifa kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na majangili wanaomaliza tembo kwa lengo la kupata pembe zao. Alisema kutokana na biashara nzuri ya pembe hiuzo duniani majangili wamekuwa na soko tayari kiasi cha kuendeleza vitendo vyao.

  Alisema mitandao iliyopo inawezesha kuuawa kwa tembo hao na kufikishwa bidhaa za pembe katika soko haramu ambalo lipo duniani na hivyo bila ushirikiano wa kimataifa wanyama hao ambao ni urithi wa dunia watatoweka kabisa katika miaka ijayo.

  Amesema takwimu zilizopo sasa nchini za tembo zinatisha.
  Alisema mathalani kwa ujangili pekee kwenye mfumo wa ekolojia wa Selou-Mikumi tembo waliobaki ni 13,084 kwa mwaka jana kutoka Tembo 109,419 waliokuwepo mwaka 2006.

  Alisema mfumo uliopo wa ujangili na soko la bidhaa hizo unafanya vita inayoendeshwa na Tanzania kuwa ngumu kama haitapata ushirikiano na mataifa mengine. Alisema kutokana na ukweli huo wanataka mataifa jirani na jumuiya ya kimataifa kuingia katika mapambano ya kudhibiti biashara hiyo na hivyo kuwamaliza majangili na kuendelea kuhifadhi Tembo.

  Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori, alisema serikali ya Tanzania imeanzisha mchakato wa kulinda wanyama pori.
  GU9A8723 
  Baadhi ya wadau kutoka nchi mbalimbali wanaohudhiria mkutano huo akiwemo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto).

  Mchakato huo ni pamoja na kuimarisha doria , kuendesha operesheni za kukabiliana na ujangili. Alisema pamoja na kuwapo kwa juhudi za makusudi za kukabiliana na ujangili serikali ya Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za kifedha na raslimali watu.
  Aidha kumekuwepo na ushiriki mdogo kutoka kwa wananchi katika vita dhidi ya ujangili.

  Alisema kutokana na haja ya kukabili ujangili na kuwa na hifadhi endelevu, Februari mwaka huu mataifa ya Botswana, Chad, Garbon na Ethiopia yalitiliana saini mkataba wenye lengo la kupunguza mahitaji ya bidhaa za wanyamapori, kuimarisha sheria zilizopo dhidi ya ujangili na pia hifadhi na kusaidia maendeleo ya maeneo yanayokabiliwa na changamoto ya uwindaji haramu.

  Rais Kikwete alisema katika hotuba yake kwamba kuwepo kwa mataifa hayo katika mkutano huo ni kuendeleza makubalino ya kutojishughulisha na biashara za bidhaa za wanyamapori kwa miaka 10 au hadi hapo tembo waliopo bara la Afrika watakapokuwa wameondoka katika hatari ya kuangamizwa katika uso wa dunia na majangili.

  GU9A8943
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza kwenye mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori uliofunguliwa rasmi leo jijini Arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Aidha rais alisema kwamba mkutano huo wa Arusha unatarajiwa kuona namna ya kuendelea utekelezaji wa makubaliano ya London, Uingereza ya hifadhi ya wanyamapori walio katika hatari ya kutoweka akiwemo Tembo.
  Alisema kutokana na mfumo wa ikolojia na hifadhi ya wanyama na majirani zake, Tanzania inataka majirani kushiriki katika kulinda na kuhifadhi ikolojia hiyo na wanyama waliopo na sio kuiachia Tanzania pekee.
  Tanzania ikiwa na eneo la kilomita za mraba 943,000 asilimia 30 ya eneo lake na 15 imetumika kwa hifadhi ya wanyamapori na misitu.
  Amesema eneo hilo hutumiwa zaidi kwa ajili ya utalii wa wanyamapori ambapo asilimia 17 ya pato la taifa linatokana na utalii huo.
  Wakati huo huo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ,ameipongeza Tanzania kwa kuitisha kikao cha kujadili ujangili na uhifadhi endelevu wa misitu.
  GU9A8824
  Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush Arha akiwakaribisha wadau wanaoshiriki mkutano huo kutoa maoni yao katika udhibiti wa ujangili ulioshika kasi.
  Akizungumza kwa niaba ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Kenya na Msumbiji alisema Umoja wa Mataifa unajisikia furaha kuona mataifa wanachama yanakabilian na changamoto ya ujangili na uhifadhi wa misitu kwa namna ambavyo itasaidia kizazi kijacho.
  Mratibu huyo alisema kwamba ujangili unatishia maendeleo, mazingira na usalama kitu ambacho Umoja wa Mataifa unakipiga vita.
  Anasema biashara ya bidhaa za wanyamapori zinahatarisha uwepo wa wanyama ambao tayari wapo katika hatari ya kutoweka, unasababisha rushwa na migogoro ambayo inahatarisha maihsa ya watu.
  Alisema kwa sasa dunia imekuwa ikipungukiwa na tembo wa Afrika kwa kasi isiyokubalika kutokana na vitendo vya majangili na hivyo kutaka jamii kushirtikiana kukabiliana na vitendo hivyo.
  Mratibu huyo amesema uhalifu unaofanyika kwa wanyamapori na misitu ni lazima ukomeshwe kwa manufaa ya wananchi .
  GU9A9238
  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Tonia Kandiero akizungumza katika mkutano huo.
   
  Alisema Tanzania inastahili kupongezwa kwa kuitisha mkutano wa kujadili ujangili Mei mwaka huu na sasa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kikanda wa kukabiliana na ujangili.
  Alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kuimarisha ushirikiano wake na mamlaka mbalimbali zinazoendelea kukabiliana na ujangili na kupotea kwa misitu duniani ili kuhifadhi urithi wa dunia.
  Alisema Umoja huo kupitia mashirika yake mbalimbali watawezesha mambo mbalimbali ili kukabiliana na ujangili na uharibifu wa misitu.
  Alisema itaendelea kusapoti programu zinazokuza uchumi wa wananchi waliopo karibu na hifadhi za wanyamapori na misitu ili waone umuhimu wa kushiriki kuhifadhi wanyama na misitu husika.
  GU9A9173
  Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mh. Sinikka Antila pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke nao ni miongoni mwa wadau wanaohudhuria mkutano huo.
  GU9A9016
  Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano),Ummy Mwalimu akishiriki mkutano huo.
  GU9A9099
  Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush Arha akiteta jambo na mgeni rasmi Waziri wa Mali asili na utalii, Mh. Lazaro Nyalandu.
  GU9A9278
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) Bw. Philippe Poinsot (katikati) akimsikiliza mdau kutoka AWF akitoa maoni yake kwenye mkutano huo uliofunguliwa rasmi leo jijini Arusha.
  GU9A8659 
  Pichani juu na chini ni washiriki mbalimbali wa mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu uliofunguliwa rasmi leo jijini Arusha.
  GU9A9041GU9A9042  GU9A9175GU9A9072GU9A9304

  0 0

  Balozi wa China nchini Tanzania,Mh. Lu Youqing akizungumza na vyombo vya habari mjini Arusha leo juu ya tuhuma za kuhusishwa kwa Ndege ya Rais wa China kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii,Mh. James Lembeli.

  Serikali ya China imelaani vikali uzushi uliotolewa na vyombo vya magharibi kutuhumu ndege ya Rais huyo kutumika kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.

  Akizungumza leo mjini Arusha Balozi wa China Lu Youqing alisema kuwa huo ni uongo mkubwa ambao ulikuwa na nia ya kutia aibu taifa lake na Tanzania kwa ujumla.

  Alisema kwamba Taifa lake hutoa adhabu kali kwa mtu anayefanya uovu kama ujangili, "Kama mwandishi angeweza kuthibitisha hao maafisa wangechukuliwa hatua kali, na hilo liko ndani ya uwezo wangu kwanini ameshindwa kuwataja?"

  Lu alisema kwamba Adhabu kama hiyo si kwa mtu aliyekutwa na nyara tu bali hata kwa muongo, "Mwandishi huyo ni muongo na anatakiwa aadhibiwe".

  Waziri wa maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu aliunga mkono kauli hiyo na kusema kuwa ilikuwa na nia ya kuchafua hali ya hewa kutokana na mkutano wa kimataifa ulioanza leo jijini Arusha.

  "Hata tulipokwenda na rais Kikwete jijini London kwa mkutano wa kimataifa juu ya ujangili gazeti la Dail Mail lilitoa habari za kashfa kuhusu Tanzania siku moja kabla ya mkutano na hii leo ndio limetokea"

  Alisema nashukuru wadau wa uhifadhi ambao kwa kiwango kikubwa wamehudhuria kikao chetu muhimu cha leo ambacho kitaleta mabadiliko makubwa katika vita dhidi ya ujangili.

  Kikao hichio kilihudhuriwa na mawaziri kutoka nchi tisa za Afrika ukanda wa bahari ya Hindi na afrika mashariki na Kati pamoja na wawakilishi wa mashirika mbalimbali na balozi wa nchi nyingi wanaowakilisha nchi zao.


  0 0

   Dangote akiwa katika kikao na baadhi ya wahandisi na mafundi wa wanaojenga kiwanda hicho
   Dangote akitumia gari kukagua ujenzi wa kiwanda hicho
   Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote akiwa kwenye gari huku akipata maelezo ya ujenzi wa kiwanda hicho kutoka kwa mafundi na wahandisi ya Dil & Sinoma inayojenga kiwanda hicho kitakachokuwa cha tatu kwa ukubwa Afrika.
   Msafara wa Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Groupof Industries), Alhaji Aliko Dangote, ukikagua ujenzi wa kiwanda hicho kinachotarajiwakuanza kazi Aprili, mwakani. Awamu ya kwanza ya kiwanda hicho ujenzi wake ukikamilika

  kitakuwa kinazalisha tani 6000 kwa siku. 
   Dangote akiangalia moja ya majengo yanayoendelea kujengwa kiwandani hapo
   Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria, akizungumza na Meneja Mkuu wa Kiwanda kikubwa cha cha saruji cha Dangote Tanzania, Daljit Singh (katikati), alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho,mkoani Mtwara. Kushoto ni Kenneth Kasigila ambaye ni Msaidizi Maalumu wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, iliyopewa fursa ya kwanza kujenga benki karibu na kiwanda hicho.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


   Alhaji Aliko Dangote akitabasamu baada ya kuwasili eneo la ujenzi wa kiwanda hicho


   Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, ambaye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Ponsiano Nyami (kushoto), akizungumza na Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote, muda mfupi kabla ya mfanyabiashara huyo kuondoka Uwanja wa Ndege wa Mtwara jana, baada ya kukagua ujenzi wa kiwanda chake.
   Dangote akisindikizwa kwenda kupanda ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara
   Dongote akiagana na Kaimu Mkuu wa Mkoawa Mtwara, Ponsiano Nyami
   Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote, akiaga alipokuwa akiondoka na ndege yake kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara jana. Alitumia takribani saa mbili kuwepo nchini, baada ya kuwasili asubuhi saa 1:42 na kuondoka saa 3:42 baada ya kupata maelezo ya ujenzi na kukagua kiwanda chake.
   Ndege ikiwa imepaa

   Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria, akiteremka kwenye ndege alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara, kwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha saruji kinachojengwa mkoani humo.

   Dangote akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa kampuni hiyo nchini, Esther Baruti (kushoto)
   Dangote akisalimiana na Balozi Mdogo wa Nigeria nchini, Adamu Mussa
   Dangote akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa kampuni ya Dangote nchini, Esther Baruti na Balozi Mdogo wa Nigeria nchini, Adamu Mussa
   Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of

  Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria, akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa kampuni hiyo nchini, Esther Baruti (katikati) pamoja na Balozi Mdogo  wa Nigeria nchini, Adamu Mussa alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho, mkoani Mtwara
   Balozi Mdogo wa Nigeria, Adamu Mussa akizungumza na Dangote Uwanja wa Ndege wa Mtwara
   Dangote akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni inayojenga kiwanda hicho ya Dil & Sinoma, baada ya kuwasili eneo la ujenzi wa kiwanda.

  0 0

  GU9A7905

  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akibadilishana mawazo na kushoto ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na kulia ni Charles McNeill, UN-REDD Programme (UNDP) kabla ya kuanza kwa kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha.

  Na Mwandishi wetu, Arusha

  TANZANIA imesema ipo tayari kuendeleza juhudi za kimataifa za kupunguza kuendelea kuliwa kwa tabaka la ozone kwa kuhakikisha kwamba inatunza misitu na kuwaelimisha wananchi juu ya menejimenti ya misitu hiyo. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge wakati wa kufungua kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha.

  Alisema ingawa Tanzania kwa sasa ina hekta milioni 48.1 za misitu na mapori ambayo sawa ni asilimia 55 ya eneo lake, Tanzania kupitia misitu hiyo inanyonya zaidi ya tani milioni 76 za hewa ya ukaa ingawa yenyewe inatoa chini ya tani hizo.

  Hata hivyo alisema kwamba pamoja na juhudi za serikali kuna changamoto kubwa katika kutunza misitu hiyo ambapo kiwango cha ukataji wa misitu kwa sasa ni kiasi hekta 372,000 kwa mwaka sawa na asilimia 1.1 ya eneo la ardhi la nchi.  Katika hali ya kawaida na endelevu eneo linaloruhusiwa kuvuna kwa mwaka linaweza kutoa mita za ujazo milioni 42.8 kwa mwaka wakati mahitaji halisi ni mita za ujazo Milioni 62.3 kwa mwaka.

  “Asilimia 92 za mahitaji ni kwa ajili ya nishati kama kuni na mkaa.” Alisema akionesha changamoto zinazokabili serikali ya Tanzania pamoja na ukweli kuwa mabadiliko ya tabia nchi tayari yameonesha ukali wake nchini.
  GU9A7946
  Afisa Mawasiliano wa Sektretariet ya Program ya Umoja Mataifa ya-REDD, Jennifer Ferguson-Mitchell (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wanaohudhuria kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha.

  Mabadiliko ya tabia nchi yanayotokana na kuzidi kwa joto katika tabaka la ozone kumesababisha kupanda kwa bahari wka sentimeta 19 na kusababisha baadhi ya visiwa katika pwani ya Tanzania kuzama kama cha Maziwe kilichopo wilaya ya Pangani.
  Aidha alisema keundelea kuyeyuka kwa barafu ni dalili nyingine ya Tanzania kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi kwa hiyo taifa la Tanzania linajikita pamoja na mataifa mengine kuhakikisha kwamba programu ya Umoja wa mataifa ya kuhifadhi misitu inafanikiwa.
  Aidha alisema kwa mazingira ya sasa ambapo tani milioni 1 ya mkaa huzalishwa nchini kwa mwaka huu nusu yake ikitumika jiji la Dar es salaam na majiji ya Arusha na Mwanza yakitumia kiasi kinachobaki kunahitaji juhudi za ziada kuongeza kasi ya upandaji miti kiasi cha hekta 185,00 kwa mwaka katika kipindi cha miaka 16 ijayo.
  Waziri Binilith alisema pamoja na Tanzania na mataifa mengine ni laizma kushirikiana katika kupunguza kasi ya ukataji miti katika misitu huku wananchi wake wakisaidiwa njia nyingine ya kuendesha maisha yao.
  GU9A7961
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge akisamiana na Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano kufungua kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha. Wa pili kulia ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD kutoka nchi wadau Dk Chea Sam Ang kutoka Cambodia Naibu Mkurugenzi Mkuu kitengo cha Misitu wizara ya kilimo, Misitu na Uvuvi.
  Alisema mikakati ya kutunza misitu ili kupunguza kiwango cha joto duniani pia itasaidia kunyanyua uchumi wa wananchi, kuondoa umaskini na kutengeneza mtengamano wa mazingira na ekolojia hasa kwa jamii ambayo inategemea misitu kuwezesha maisha.
  Waziri huyo aliwataka wadau waliopo katika mkutano huo wa siku mbili kujadili na kubadilishana uzoefu na kuhakikisha kwamba mkakati wa Umoja wa mataifa wa kukabiliana na mseleleko wa joto kwa kuwekeza katika kuhifadhi misitu unafanikiwa.
  Umoja wa Mataifa una mpango wa kuhifadhi misitu unaojulikana kama Reduce Emissions from Deforestation and Forest Degradation (REDD+) unatarajia kuanza 2016-2020.
  Wakati huo huo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza awali alishukuru mchango wa Norway katika kuwezesha utekelezaji wa programu ya UN REDD+ nchini Tanzania na maeneo mbalimbali duniani.
  Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa mkutanoni hapo Norway imechangia dola za Marekani milioni 11 kuwezesha kutekelezwa kwa majukumu ya Umoja wa Mataifa katika kufanikisha programu hiyo katika nchi mbalimbali.
  GU9A7967
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiani na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano. Katikati ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO).
  Utoaji wa hela hizo umeelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kitengo cha kimataifa cha mabadiliko ya hali ya hewa katika Wizara ya hali ya hewa na mazingira ya Norway.
  Akizungumza wakati wa kumkaribisha Waziri Dk Binilith Mahenge, wawakilishi mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa mataifa (– UNDP, UNEP, na FAO),Sekretarieti ya UN REDD, wajumbe wa bodi ya sera ya UN REDD, Mashirika yasiyo ya kiserikali, Mwakilishi huyo wa UN alisema mafanikio yanayopatikana kwa sasa na duniani ni matokeo ya uwezeshaji wa Norway na wadau wengine katika mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuhifadhi misitu.
  Alisema kazi ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa ni kuhakikisha wanatoa msaada wa kitaalamu na misaada mingine kuiwezesha serikali kutimiza wajibu wake.
  Alisema Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na nchi nyingine 56 duniani wanaounda UN-REDD wamefanya vyema kuziwezesha nchi hizo kuwa tayari katika kutekeleza programu husika kwa manufaa ya nchi zao na dunia kwa ujumla.
  GU9A8214
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge akisoma hotuba yake wakati akifungua kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha.
  Alisema Tanzania kama nchi nyingine duniani zinazoendelea inakumbana na changamoto kubwa ya kuhifadhi misitu hasa kutokana na wananchi wake wengi kutegemea sana misitu kwa mambo mbalimbali yanayohusu maisha yao.
  Aidha alisema kama taifa lina uwezo mdogo wa kusimamia sera na sheria zinazohusu hifadhi ya misitu.
  REDD+ ambayo imeanza kutekelezwa nchini Tanzania mwaka 2008, mikakati ya utekelezaji wa mkakati huo imefanywa na kupitishwa na Bunge la Tanzania mwaka 2013.
  Kukiwa na kikosi kazi cha kuwezesha kutekeleza UN REDD+ Tanzania pia imepongezwa kwa kuanzisha miradi tisa yenye lengo la kuwezesha utekelezaji wa malengo ya REDD+
  Aidha katika utekelezaji wake serikali imejikita katika vipato vingine kwa jamii inayoishi karibu au ndani ya misitu kwa kuwa na kilimo kinacholinda mazingira na ufugaji nyuki.
  GU9A8249
  Meza kuu kutoka kushoto ni Head, UN-REDD Programme-Secretariat, Bw. Mario Boccucci, Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD kutoka nchi wadau Dk Chea Sam Ang kutoka Cambodia Naibu MkurugenzI Mkuu kitengo cha Misitu wizara ya kilimo, Misitu na Uvuvi, Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) na Thais Linhares-Juvenal kutoka sekretarieti ya programu ya Umoja wa Mataifa ya kuhifadhi misitu (UN-REDD) wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.
  Alvaro alisema kutokana na mafanikio yaliyopatikana kwa sasa UN na serikali ya Tanzania wanakamilisha awamu ya pili ya UN REDD+ kwa kuangalia uzoefu uliopatikana katika awamu ya kwanza.
  Utekelezaji wa awamu ya pili utafanyika mara tu fedha zitakapopatikana.
  Naye Abbas Kitogo ambaye ni Meneja wa miradi ya nishati na mabadiliko ya tabia nchi (UNDP) alisema kwamba mkutano huo wa 13 utawezesha kubadilishana uzoefu wa sekta mbalimbali katika kutunza misitu huku wananchi wakiendelea kuneemeka.
  Alisema nchini Tanzania kumekuwepo na miradi ya kujenga uelewa, kutengeneza mpango wa kutekeleza yanayotakiwa kufanywa na kujenga uwezo kwa wadau ili kujua REDD na kufuatilia athari za utekelezaji wa mradi huo.
  GU9A8136
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma risala wakati wa ufunguzi wa kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika Ngurdoto Jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge.
  GU9A8261
  Pichani juu na chini ni wadau wanaohudhuria kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachoendelea kwenye hoteli ya Ngurdoto Jijini Arusha.
  GU9A8296GU9A8315GU9A8055GU9A8387
  Mkurugenzi Mkuu wa kitengo cha kimataifa cha mabadiliko ya hali ya hewa katika Wizara ya hali ya hewa na mazingira ya Norway, Bw. Morten Nordskag akitangaza mchango wa serikali ya kuchangia dola za Marekani milioni 11 kuwezesha kutekelezwa kwa majukumu ya Umoja wa Mataifa katika kufanikisha programu hiyo katika nchi mbalimbali katika kikao hicho.
  GU9A7982
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye tete-a-tete na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.GU9A8347
  Mmoja wa washiriki akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
  GU9A8469
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ( wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa UN-REDD Kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Eduardo Rojas ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya misitu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) huku Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (katikati) akifafanua jambo kwa mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) wakati wa zoezi la kupiga picha ya pamoja.
  GU9A8445
  GU9A8466
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mh. Binilith Mahenge kwenye picha ya pamoja na wadau wanaohudhuria kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa REDD+ kinachofanyika hoteli ya Ngurdoto Jijini Arusha.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi semina ya mafunzo ya Kiislamu (IJITIMAI) iliyofunguliwa jana Novemba 7, 2014 kwenye Msikiti wa Jabalhira, mjini Morogoro. 
   Sehemu ya waumini wa dini ya kiislam waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa IJITIMAI, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi IJITIMAI hiyo katika msikiti wa Jabalhira, mjini Morogoro. Picha na OMR

  0 0

   Mfanyakazi wa Michuzi Media Group Bw. Salumu Mwingiriko a.k.a Manywele akifungua dansi na mkewe Kurthum Abubakar usiku wa kuamkia leo katika sherehe ya kumeremeta kwao iliyofana sana katika ukumbi wa Kilimanjaro katika Uwanja wa Sabasaba jijini Dar es salaam
   Ankal na mai waifu wake wakipokea keki toka kwa maharusi kwa niaba ya wafanyakazi wa Michuzi Media Group
   Picha ya pamoja na maharusi. Kulia ni Hamisi Makuka mpiga picha wa MMG
  Maharusi wakiserebuka kwa furaha. 

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini linalotarajiwa kuanza Novemba 10 katika halmashauri 16. Wengine (walioketi) ni Mkurugenzi wa fedha wa TASAF Bw. Isaya Wambura (wa pili kushoto), meneja masijala ya walengwa Philipine Mmari (wa kwanza kushoto), Mtaalamu wa Mafunzo Mercy Mandawa (wa pili kulia) na Meneja Rasilimali watu Tecla Makundi.
   Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiri wa mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akitoa neno la ufunguzi wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa (hawapo pichani) kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini linalotarajiwa kuanza Novemba 10 katika halmashauri 16 nchini . Aliyekaa kushoto ni  Mkurugenzi wa fedha wa TASAF Bw. Isaya Wambura.
   Afisa Ufuatiliaji na tathmini wa TASAF Bw. Paul Luchemba akitoa mada juu ya malengo ya warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini katika ukumbi wa AMECEA Kurasini Jijini Dar es Salaam
   Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini unaotekelezwa na TASAF kupitia Mpango wa kunusuru kaya maskini  PSSN wakifuatilia mjadala baada ya uwasilishaji wa madajuu ya mwongozo wa mpango katika ukumbi wa TEC-Kurasini jijini DSM
   Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini unaotekelezwa na TASAF kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini PSSN wakifuatilia maelekezo toka kwa wawezeshaji.
   Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini  unaotekelezwa na TASAF wakisikiliza mada zinazowasilishwa na wawezeshaji wa warsha hiyo kwenye ukumbi wa TEC jijini DSM


  TASAF YAENDESHA WARSHA YA MAFUNZO KWA WAWEZESHAJI NGAZI YA TAIFA KUHUSU TUKIO LA UTAMBUZI WA KAYA MASKINI UKUMBI WA TEC DSM


  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umeendesha mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini linalotarajiwa kufanyika kuanzia  Novemba 10 katika halmashauri 16 nchini.

  Akifungua  Warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga amesisitiza kuwa suala la nidhamu,uaminifu ,kujituma na kuzingatia taratibu kuwa silaha muhimu katika ufanikishaji wa  utekelezaji wa mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  ambao umeanza kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.

  Bw. Mwamanga ametoa msisitizo huo wakati akifungua warsha ya siku moja ya mafunzo hayo katika ukumbi wa TEC jijini Dar es Salaam ambako amebainisha mambo muhimu yanayochangia  TASAF kufanya vizuri katika nyanja mbalimbali za utekelezaji wa shughuli zake ukiwemo utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na zilizo katika Mazingira hatarishi ambapo amesema kuwa nguzo kuu ni uwajibikaji wa pamoja na kuzingatia taratbu za Mpango.


  0 0

  Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) aliyechukua nafasi yake pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk.
  Sitti Abas Mtemvu amelivua taji hilo baada ya kuiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania, November 5 mwaka huu, kuhusiana na uamuzi wake huo.
  Mrembo huyo alikuwa akikabiliwa na shutuma za kudanganya umri wake, jambo ambalo lilililazimu Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata) kutokana na agizo la wizara  husika kufuatilia ukweli wake.
  “Baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu. Wameniwekea maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati siyo,” amesema kwenye barua hiyo.
  Miss Tanzania aliyechukua nafasi ya Sitti Mtemvu, Lilian Kamazima pichani kulia.
  “Shutuma hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu. Sasa kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014,” ameongeza.

  “Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.”
  Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi. 
  “Leo nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo niliochukua.” Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamazima.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitazama baadhi ya picha za kumbukumbu za Mahakama ya Kimbari zilizo katika ukumbi huo wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ICTR, ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
    Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

  0 0

   Hii ndio ile barabara ya Ukonga Mazizini- Moshi Bar ambayo inadaiwa kugharimu kiasi cha shilingi Milioni 90 kuikarabati kwa kiwango cha changarawe kwa umbali wa kilometa tatu. Picha hizi ni madimbwi ya mwanzo tu ya hizo kilometa tatu.(Picha na Father Kidevu Blog).
  Meya Jerry Silaa wa Ilala ambaye ni Diwani wa Gongo la Mboto alipotembelea aliwaambia wananchi kuwa fedha za ujenzi huo ni kutoka mfuko wao ni . PICHA ZA CHINI NI SIKU MEYA SILAA ALIPOTEMBELEA UJENZI WAKE.
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibarkilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni utekelezaji wa miradi yadharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinuulitokea baada ya Mvua kubwa. Mradi huoambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.
  Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar
  Mwonekano wa Bara barabara hiyo

older | 1 | .... | 402 | 403 | (Page 404) | 405 | 406 | .... | 1897 | newer