Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

WATAKIWA KUTOWEKA UPENDELEO KWENYE TASAF III

0
0

 
 Kutoka kushoto waliokaa  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw. Edwin Mwanzinga, Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi Sarah Dumba, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bw. Tadeo Kabonge na Kaimu Mkurugenzi wa Tassaf Taifa Bw. Peter Luanda wakiwa kwenye picha ya pamoja na madiwani wa kata za Halmashari hiyo waliosimama, Picha zote na  James Festo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw Tadeo Kabonge akizungumza kabla ya kufunguliwa kwa warsha hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sarah Dumba akifungua Warsha ya siku moja ufunguzi wa Warsha ya Tasaf inayoendelea mjini Njombe

Na James Festo, Njombe.
Wawezeshaji wa mradi wa  kunusuru kaya masikini unaoendeshwa na mfuko wa maendeleo ya jamii (TASSAF) awamu ya tatu wenye lengo la kuwakwamua wananchi wa kipato cha chini wametakiwa kutowapendelea ndugu zao katika utekelezaji.

Akifungua warsha ya siku moja Mkuu wa Wilaya  wa Njombe  Bi.Sara Dumba  ya kuwajengea uelewa wawezeshaji wa mradi huo kuhakikisha unawanufaisha walengwa ambao ni familia zenye hali duni ya maisha na  watoto ikiwa ni utatuzi wa changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa TASSAF awamu mbili za awali.

“Tunashukuru serikali  kwa kutuchagua kuwa miongoni mwa watakaoanza kunufaika kwa niaba ya wananchi tumeupokea, sasa kazi kwenu wawezeshaji msije mkaanza kupendelea…unampa msaada kwa sababu ni ndugu yako….ni mjomba wako, kinachotakiwa  mradi uwanufaishe wale waliolengwa tu sio watu wengine” alisema Bi Dumba.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tassaf Taifa Bw. Peter Luanda  alisema  umelenga kuzifikia kaya milioni moja ambazo zinaishi katika mazingira magumu na kwa awamu awamu ya kwanza utachukua maeneo machache kwa sababu bado wanafanya tathmini na baada ya kumalizika wataongeza vijiji vingine.

Alisema kuwa mradi huo umelenga kuboresha maisha , kutoa ajira kwa wenye uwezo wa kufanya kazi, kuboresha miundombinu ya maji, afya na elimu, kutoa ruzuku kwa familia maskini hasa akina mama wajawazito pamoja na watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano.

Katika  hatua nyingine aliishukuru Halmashauri hiyo kwa mapokeo waliyoonyesha sambamba na kuchagua wawezeshaji watakao ungana na timu ya Tassaf  Taifa katika mradi huo.

Mradi huo huo uliozinduliwa agost 2012  Mkoani Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete, Utekelezaji wa mradi ukianza mwezi februali 2013 na lengo lake ni kutambua kaya masikini na umeanza na Halmashauri 16  Nchini na inatarajia kuzifikia zote 161.

Naibu Mwanasheria wa Serikali afungua mafunzo ya haki za binadamu Kunduchi leo

0
0
 Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akitoa hotuba yake kufungua rasmi warsha ya siku tano ya mafunzo ya haki za binadamu kwa maafisa kutoka Taasisi 11 za kitaifa za haki za binadamu za nchi za Afrika Kunduchi Beach Resort mapema leo.
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku tano ya mafunzo kuhusu masuala ya haki za binadamu wakifuatilia hotuba ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju (hayupo pichani) iliyotolewa leo Kunduchi Beach Resort. Mafunzo hayo yameandaliwa na Umoja wa Taasisi za Kitaifa za Haki za Binadamu Afrika (NANHRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya mafunzo ya haki za binadamu na Sheria za ki-utu ya Raoul Wallenberg (RWI) ya Sweden na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) kwa ufadhili wa SIDA.
 Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akitoa hotuba yake kufungua rasmi warsha ya siku tano ya mafunzo ya haki za binadamu kwa maafisa kutoka Taasisi 11 za kitaifa za haki za binadamu za nchi za Afrika Kunduchi Beach Resort mapema leo.
 Washiriki wa warsha ya siku tano ya mafunzo ya masuala ya haki za binadamu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju (waliokaa, wa pili kutoka kushoto) muda mfupi baada ya kufungua rasmi warsha hiyo Kunduchi Beach Resort mapema leo.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Taasisi ya mafunzo ya haki za binadamu na Sheria za ki-utu ya Raoul Wallenberg (RWI) ya Sweden, Ms. Janne Holck Clausen (katikati) na Mratibu wa Umoja wa Taasisi za Kitaifa za Haki
za Binadamu Afrika (NANHRI), Ms. Flavia Mwangovya muda mfupi baada ya ufunguzi rasmi wa warsha ya mafunzo ya siku tano kwa taasisi za kitaifa za haki za binadamu Afrika huko Kunduchi Beach Resort leo.

Dk.Shein Afungua Semina ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya leo

0
0
5wRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa semina ya Viongozi wa juu wa Mikoa na Wilaya za zanzibar na Baadhi kutoka Bara inayohusu Mahusiano na mwingiliano katika siasa na utendaji kwa Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa mikoa ya zanzibar na baadhi Tanzania Bara leo katika Hoteli ya Sea Cliff  Kama nje ya Mji wa Zanzibar.
1wAbdulrahman  Ghasia alipowasili katika viwanja vya Sea Cliff Mangapwani Mkoa wa Kaskazi/ni B Unguja leo alipofika kufungua semina ya Viongozi wa Juu Mikoa na Wilaya za Zanzibar, [Picha na Ikulu.]

Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya Marekani yaendesha kliniki ya masikio mkoani Arusha

0
0
8qMtaalamu wa matatizo ya usikivu kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani, Derek Johson akimfanyia uchunguzi wa awali wamasikio mmoja wa watu wenye usikivu hafifu waliokuja kuhudhuria Kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha jana
9qMratibu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation kutoka Marekani, Derek Johnson akitoa maelezo ya awali kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Meru na chuo cha Biashara cha Arusha, (IAA) waliokuja kujitolea kutoa huduma mbalimbali ya matibabu na uwekaji vifaa vya kuongeza kiwangocha usikivu masikioni kwenye Kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jana. Kushoto ni Msimamizi Mkuu wazoezi hilo, Teddy Mapunda.
 1qMMOJA wa wataalamu wa kuchunguza matatizo ya masikio,Stuart Specer kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani inayoendesha kliniki ya masikio aakitaniana na mkazi wa Arusha,Ally Abdulrahman aliyewahi kuishi nchini humo ambaye kwa sasa ana matatizo ya kusikia kwenye kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo PalaceJijini Arusha jana
3qWanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Meru na chuo cha Biashara cha Arusha (IAA) waliokuja kujitolea wakisaidia kutoa huduma mbalimbali kwenye kliniki ya masikio iliyoratibiwa kwa pamoja kati ya Montage Limited na Starkey Hearing Foundation inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha jana
4qWagonjwa wenyematatizo ya usikivu wakisubiri kupata matibabu kwenye kliniki ya matibabu na uwekaji vifaa vya kuongeza kiwango cha usikivu iliyoratibiwa kwa pamoja kati ya Montage Limited na Starkey Hearing Foundation inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jana.
5qBaadhi ya wanafunzi wa Shule ya MsingiMeru wakisubiri kupatiwa huduma ya matibabu ya masikio kwenyeKliniki inayoendesha na taasisi kutoka Marekani ya Starkey Hearing Foundation inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha jana.
7qDAKTARI, Assay Shibanda(kushoto) na John Yuccas wakimwekea mwanafunzi wa Shule ya Msingi Elbol,Levina Innocent mashine ya kuongeza kiwango cha usikivu kwenye Kliniki inayoendeshwa kwa pamojakati ya Montage Limited na taasisi kutoka Marekani ya Starkey Hearing Foundation ya kuwawekea vifaa vya kuongeza usikivu inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha jana

WAZIRI MKUU PINDA AFUNGUA SEMINA YA ALAT JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

unnamed1
 Waziri Mkuu, Mizengo PInda akihutubia wakati alipofungua semiana ya  Jumuiya ya   Tawala za Mitaa kwenye ukumbi wa hoteli ya Kunduchi jijini Dar e salaam Novemba 10, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed2unnamed3Baadhi ya washiriki wa Semina ya Jumuiya ya Tawala za Mitaa, ALAT wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua semina yao kwenye  ukumbi wa hoteli ya Kunduchi Jijini Dar es salaam  Novemba 10, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed5Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri (wapili kulia), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa, Dr. Didas Masaburi (kushoto) na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda baada ya kufungua semina ya ALAT kwenye ukumbi wa hoteli ya Kunduchi jijini Dar es salaam Novemba 10, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)unnamed6
unnamed7unnamed7Waziri MKuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa  (ALAT) baada ya kufungua semina yao kwenye ukumbi wa hoteli ya Kunduchi  jijini Dar es salaam Novemba 10, 2014.Kushoto ni Mwenyekiti wa ALAT, Dr. Didas Masaburi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KAMPUNI YA PETROGAS YAENDESHA MAFUNZO YA UANDAAJI WA MAPENDEKEZO YA MIRADI KWA WATAALAMU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

0
0
 Mwenyekiti Mtendaji wa  Kampuni ya  Petrogas inayojihusisha na kutoa mafunzo kwa ajili ya  uandaaji wa mapendekezo ya miradi pamoja na usimamizi wake yenye makazi  yake jijini Dar es Salaam  Bw. Greyson  Kiondo akisisitiza jambo kwenye  mafunzo  yanayohusu uandaaji wa mapendekezo ya  miradi na usimamizi wake yaliyoshirikisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini  yanayoendelea mjini  Bagamoyo katika hoteli ya  Stella Maris.
 Msimamizi wa mradi unaohusika na   kuwajengea  uwezo wataalamu wa nishati na tasnia  ya uziduaji (CADESE; Capacity  Development  in the Energy Sector & Extractive Industries) Bw. Paul Kiwele (kulia)  akisisitiza jambo kwenye mafunzo hayo. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga.
 Kamishna  Msaidizi  wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga ( wa kwanza kulia mbele ), msimamizi wa mradi wa CADESE Bw. Paul Kiwele (katikati) na baadhi ya washiriki wakiendelea kufuatilia mada iliyokuwa inawasilishwa na mtaalamu mwelekezi Bw.  Tom Mitro kutoka Petrogas (hayupo pichani)
Mtaaalamu kutoka Petrogas Bw. Tom Mitro akiwasilisha mada  juu ya uandaaji wa mapendekeo  ya miradi katika semina hiyo mbele ya washiriki (hawapo pichani)

Kamishna  Msaidizi  wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga (kushoto) akisoma hotuba ya  ufunguzi  kwa  niaba ya Kamishna wa Nishati na Maendeleo  ya Petroli Mhandisi Hosea Mbise kwenye mafunzo hayo. Kulia ni msimamizi wa mradi wa CADESE Bw. Paul Kiwele

TANZANIA INAHITAJI MASTER PLAN YA NCHI NZIMA - WAZIRI MKUU

0
0

 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania kama nchi inapaswa kuwa na mpango wa kuendeleza mipango miji (master plan) wa nchi nzima unaozingatia ukuaji wa miji yetu.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Novemba 10, 2014) wakati akifungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo Mameya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa za Miji kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.

 “Sasa hivi hapa nchini tuna tatizo la ukuaji mkubwa wa miji yetu na Dar es Salaam ni mmojawapo. Hakuna miundombinu ya majitaka, nyumba zimesongamana, hakuna barabara za uhakika... ukuaji wa miji ni lazima uangaliwe kwa naman ya tofauti na upewe uzito unaostahili,” alisema.

“Lazima tuje na master plan ya miji yote mikubwa kama Arusha, Mwanza na Dar es Salaam hata kama itabidi kutafuta wafadhili ili tuweze kuifanya kazi hiyo. Lazima huo mpango kabambe uwepo kama kweli tunataka kumaliza tatizo hili,” aliongeza.

“Hivi hata ukitaka kupeleka timu ya waokoaji unawapelekaje? Je ukiwapeleka wapite wapi?, watue wapi? Lazima tutafute wafadhili wa kufinance mpango huu,” alisisitiza.

Akitoa mfano Waziri Mkuu alisema kukosekana kwa mipango miji kunaleta matatizo ya wnanchi kupelekewa mahali hata kama hapajaandaliwa. “Kulitokea mafuriko hapa Dar es Salaam, watu wakapelekwa Mabwepande. Je kulikuwa na mpango wowote wa miundombinu ya kuwaweka huko? Je, yakitokea mafuriko mengine, watu watapalekwa wapi?” alihoji.

Alisema kutokuwepo kwa mpango huo kumefanya asilimia 70 ya makazi kujengwa katika maeneo yasiyo rasmi.

Waziri Mkuu pia aliwataka viongozi hao waangalie ni kwa jinsi gani wanaweza kupunguza athari zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi kwenye maeneo wanakotoka. “Kwangu mimi natamani kuona madhara yanayotokana na tabianchi yakipungua. Jaribuni kujiuliza mtaweka mikakati gani ili kupunguza athari za mafuriko,” alisisitiza.

Aliwataka pia waangalie athari za uchafuzi wa mazingira kwa sababu ni changamoto kubwa katika miji mingi hapa nchini. “Pale Kinyerezi wana dampo na wanaona suluhisho ni kuchoma moto lakini hawaangalii madhara ya ule moshi unaotokana na uchomaji taka,” alionya.

Mapema, akielezea kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Eng. Mussa Natty alisema mkutano huo umefanyika ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano (Durban Adaption Charter) yaliyofanyika jijini Durban, Afrika Kusini, Desemba, 2011 ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo la mabadiliko ya tabianchi.

“Wakati tulipoenda Durban, tulienda na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke. Sasa hivi ziko Halmashauri 102 ambazo zimeshatia saini makubaliano haya,” alisema.

Lengo la mkutano huo ni kutafuta njia za kutafuta ufumbuzi wa mabadiliko ya tabia kwa kutumia mbinu zinaoendana na mazingira ya hapa nchini (local solutions).
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
11410 – DAR ES SALAAM.
JUMATATU, NOVEMBA 10, 2014

MWANAMUZIKI MKONGWE WA TWANGA PEPETA,AMIGOLAS AZIKWA MAKUBURI YA KISUTU JIJINI DAR LEO

0
0
Waombolezaji wakiuswalia mwili wa marehemu Hamis Zayumba, maarufu kama AMIGOLAS, kabla ya mazishi yake yaliyofanyika leo Jumatatu kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. Amigolas ambaye alikuwa mtunzi na mwimbaji mashuhuri wa bvendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta, alifariki Jumapili jijini.
Mwimbaji na mtuzni, Ali Choki, akiwa na uso wa huzuni wakati wa mazishi ya AMIGOLAS, ambaye kipindi gulani walikuwa bendi moja ya Twanga Pepeta
Waombolezaji wakiwemo wasanii maarufu, wakiwa kwenye mazishi.
Waombolezaji na wasanii wakiwemo wanamuziki wakiwa nyumbani kwa marehemu AMIGOLAS, kabla ya mzishi yake.PICHA KWA HISANI YA K-VIS BLOG

Discussion on USAID African Diaspora Marketplace III

0
0
Discussion with Jeffrey L. Jackson, Senior Private Sector Advisor, USAID. Barbara Span, Vice President, Global Public Affairs, Western Union, Eric-Vincent Guichard, CEO, Homestrings and Zelalem Dagne, ​ CEO, Global Tracking before the launch of the African Diaspora Marketplace III (ADM III), on October 27th 2014 at The Embassy of Tanzania in Washington, DC

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

0
0
Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Moshi vijijini  ,Hussein Jamal akizungumza wakati wa kikao cha makatibu kata na makatibu wa matawi kilichofanyika katika hotel ya King Size Himo.
Mwenyekiti wa Makatibu katika jimbo la Vunjo ,Shaban Mwangi akisoma taarifa ambayo inadaiwa kupikwa kwa lengo la kukivuruga chama hicho katika jimbo la Vunjo.
Baadhi ya viongozi wakisilikiliza kwa makini.
Naibu kamanda wa vijana wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Shirima akizungumza wakati wa kikao hicho kilichokuwa na lengo la kurudisha hali ya amani na umoja ndani ya chama cha mapinduzi jimbo la Vunjo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini Miriam Kaaya akizungumza wakati wa kikao hicho ambacho kilijadili pia tuhuma zilizotolewa dhidi yake.
Makatibu wakila kiapo .
Baadhi ya makatibu katika kikao hicho.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

WAFANYAKAZI AZANIA BANK TAWI LA MOSHI YAHAMASISHA WATEJA KUFUNGUA AKAUNTI YA DHAMIRA.

0
0
Meneja Msaidizi wa Benki ya Azania Joseph Msase akikabidhi fomu ya Akaunti ya Dhamira kwa mmoja wa wateja wa Benki hiyo Benjamini Mengi.
Mteja wa Benki ya Azania Benjamini Mengi akionesha fomu yake baada ya kujiunga na Akaunti ya Dhamira ,wengine ni wafanyakazi wa Benki ya Azania tawi la Moshi,Hajira Mmambe(mwenye kilemba) na familia ya Mengi.
Mtoa huduma kwa wateja katika Benki ya Azania tawi la Moshi ,Happy Msengi akimshawishi Mama Mengi kufungua akaunti ya Dhamira iliyoanzishwa katika Benki hiyo.
Meneja Msaidizi Benki ya Azania Joseph Msese(katikati) akiwa na mtoa huduma kwa wateja Happy Msese wakijaribu kumshawishi kijana Benson Benjamini kufungua akaunti ya Dhamira.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Hajira Mmambe(kushoto) akiendelea kushawishi wateja wapya kujiunga na Akaunti ya Dhamira iliyoanzishwa katika benki hiyo.
Mtoa huduma kwa wateja katika benki ya Azania Mary Machange akiandika maelezo ya mteja  Benki Dowald Mushi alipokuwa akifungua Akaunti ya Dhamira katika tawi la Benki hiyo la Moshi.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.

WANANCHI WA MUHEZA WAHAMASIKA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII, ZAIDI YA KAYA 65 ZENYE WANACHAMA 390 WAHAMASIKA NA KUJIUNGA PAPO HAPO

0
0
 Msanii wa Maigizo mkoani Tanga Dr.Nyau na swahiba wake wakifanya yao kwenye uzinduzi wa wa Kampeni ya Kuhamasisha, wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) leo uliofanyika kata ya Potwe wilayani Muheza ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390
zilifanikiwa kujiunga.
Wananchi kutoka sehemu mbalimbali kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza ambaye hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390
walihamasika na kujiunga papo hapo.
  Mkuu wa wilaya ya Muheza Subira Mgalu kushoto akipokea risiti ya malipo mara baada ya kujiunga kuwa mwanachama wa mfuko wa afya ya Jamii (CHF) leo wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika kwenye Kata ya Potwe wilayani humo anayemkabidhi risiti hiyo ni Afisa Tabibu wa Zahanati ya Potwe wilayani humo Dr.Samweli Mudhihiri ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 walihamasika na kujiunga papo hapo. PICHA ZOTE NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
 Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subira Mgalu na wafanyakazi wa mfuko wa Bima ya Afya mkoani Tanga,viongozi wa Kata ya Potwe na wanafunzi wa shule ya msingi kwenye Kata hiyo leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga.
 Picha namba moja ni  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu akisisitiza, jambo wakati uzinduzi wa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) kwenye kata ya Potwe wilayani Muheza uliofanyika leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 walihamasiska na kujiunga papo hapo.
 Wananchi kutoka sehemu mbalimbali kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza ambaye hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390
walihamasika na kujiunga papo hapo.
 MAAFISA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) wahamasika kwenye zoezi hilo na kuamua kuwalipia wanafunzi wa shule za msingi wapatao 80 kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi
kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) wilayani humo ambapo zoezi hilo linaendelea kwa muda wa siku kumi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) wilayani Muheza George Mhada kushoto akipokea fedha kutoka kwa Diwani wa Kata ya Potwe katikati Rashid Mdachi  anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) wilayani humo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga.
MAAFISA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wahamasika kwenye zoezi hilo na kuamua kuwalipia wanafunzi wa shule za msingi wapatao 80 kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi
kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) wilayani humo ambapo zoezi hilo linaendelea kwa muda wa siku kumi.

TCRA yakutana na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania leo

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Prof. John Nkoma akitoa hotuba yake wakati wa ufungumzi wa Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wenye lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Othman Michuzi.
Inginia Andrew Kisaka akitoa Mada katika  Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania wenye lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali katika wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini.
Moja ya Mada zinazoendeleo kutolewa katika Mkutano huo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),Assah Mwambene akitoa hotuba yake wakati  akifunga Mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini na wamiliki wa Blogs (Bloggers) Tanzania uliokuwa na lengo la kutoa mafunzo ya namna ya kutoa taarifa mbali mbali wakati wa Chaguzi mbali mbali hapa nchini,unaoendelea kufanyika hivi sasa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wanablog waliohudhulia Mkutano huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam.

Watanzania waaswa kutumia teknolojia mpya na za kisasa kuzalisha mazao na sekta nzima ya kilimo

0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge akifungua rasmi Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi  kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal,itakayofanyika kwa muda wa  siku mbili katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ,kuhusu umuhimu wa Kongamano hilo lililoandaliwa na Benki Kuu ya Dunia kwa ushirikianao na Ofisi ya Makamu wa Rais. Anayefuatia wa pili kulia Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,maliasili na Mazingira  Mhe. James Lembeli, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bw. Philippe Dongier (kulia) pamoja na Bw.Vel Gnanendran Mkuu wa Ofisi ya DFID nchini Tanzania.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Ndg. Sazi Salula (katikati), akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (kulia), pamoja na Mkurugenzi Msaidizi - Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt.Richard Muyungi katika Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi  iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.
 Sehemu ya Washiriki kutoka Nje na ndani ya Nchi wakisikiliza kwa makini hotuba inayotolewa na mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani).

 Mgeni Rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mhe. Dkt Injinia Binilith Satano Mahenge (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki kutoka Ndani  na Nje ya Nchi waliohudhuria katika Kongamano la ukuaji wa uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi .
=======  =======  =======

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge amewasihi Watanzania kutumia teknolojia mpya  na za kisasa katika kuzalisha mazao na sekta nzima ya kilimo kwa ujumla ili kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo misitu. Aliyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Ukuaji wa Uchumi unaohimili mabadiliko ya Tabia Nchi. Lililofanyika jijini Dar Es Salaam. Alifungua Kongamano hilo kwa Niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Gharib Bilal.
Aliongeza kuwa Mikoa na Wilaya zote Tanzania  zinatakiwa kuweka sera endelevu ambazo zitaweza kuhakikisha kukabiliana na uharibifu wa Mazingira. Aidha alisema kuwa zipo juhudi ambazo Serikali imezichukua katika  kuhakikisha utunzaji wa  mazingira unatekelezwa na pia  kuzuia uharibifu wa mazingira kwa njia moja au nyingine.
Akiongea katika Kongamano hilo Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Philippe Dongier alisema Kongamano hilo ni fursa adhimu kwa ajili ya majadiliano kuhusu program za maendeleo ya Tanzania zinavyoweza kustawi licha ya kuwepo kwa mabadiliko ya tabia Nchi. Hivyo basi Watanzania hawana budi kuwa waangalifu sababu mabadiliko ya Tabia Nchi yana athari kubwa.
Mwisho Waziri Mahenge aliwashukuru Wadau mbalimbali ambao wamehudhuria kongamano hilo kutoka ndani na nje ya Nchi. Akiwasihi sana kuendelea kutunza mazingira na pia aliwaomba watembelee vyanzo mbalimbali vya Utalii vilivyopo Nchini Tanzania ili kukuza uchumi .
 Kongamano hilo ni muendelezo ya Mkutano wa New York kuhusu mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu na limehudhuriwa na washiriki kutoka Ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania.

SEMA KUTUMIA MILIONI 396/- KUWEKA SAWA MAZINGIRA MASHULENI IRAMBA

0
0
DSC02082
Meneja wa shirika la SEMA, Ivo Manyanku, akizungumza kwenye uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba. Kulia mwenye miwani ni mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda.

Na Nathaniel Limu, Iramba.
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Sustainable Environment Management Action (SEMA),linatarajia kutumia zaidi ya shilingi 396 milioni kugharamia utekelezaji wa mradi wa usafi mashuleni na mazingira kwa ujumla,katika shule saba ba kata saba za wilaya ya Iramba.
Fedha hizo ni ufadhili kutoka shirika la WaterAid Tanzania.

Hayo yamesemwa na meneja wa SEMA,Ivo Manyanku, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani,siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingirav nchini, iliyofanyika katika kijiji cha Tulya wilayani Iramba. Alitaja baadhi ya malengo ya mradi huo, kuwa ni pamoja na kuhamasisha na kuelimisha wanafunzi na jamii kwa jumla namna bora ya kunawa mikono.
DSC02101
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo dunia na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika kimkoa katika kijiji cha Tulya wilayani humo.

“Pia kuwaelimisha wanafunzi wa kike waliopevuka (kuvunja ungo) njia bora zitakazowasaidia kuwa wasafi kipindi chote cha siku zao za hedhi”,alifafanua Ivo na kuongeza kwa kusema;
“Shughuli zingine ni ujenzi wa vyoo bora na kuwahamasisha wanafunzi na jamii kwa ujumla kuvitumia kikamilifu.Tutawaelimisha na kuwaahamasisha kunawa mikono pindi wanapotoka chooni kujisaidia”.

Kwa upnde wake afisa afya wa wilaya ya Iramba,Yohana Dondi,alisema kuwa wilaya ya Iramba ina kaya zenye vyoo bora ni aslimia 42,vyoo kubalika 52,vyoo visivyokubalika asilimia 18 na bila vyoo,ni aslimia sita. Kwa mujibu wa afisa huyo,nchi zinazoendelea,asilimia 70-80 ya maradhi yote,yanasababishwa na maambukizi yatokanayo na vinyesi,hivyo kuwa ni kisababishi namba moja cha vifo.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu,ni Choo bora na mikono safi kwa afya bora,heshima na usawa”.
DSC02092
Spider man kutoka Temeke jijini Dar-es-salaam akitoa burudani ya kutembea juu ya waya kwenye hafla ya uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini iliyofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba.
DSC02060
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda (wa nne kutoka kushoto) akitoa maelekezo juu ya ujenzi wa choo bora cha shule ya msingi Tulya.Wa tatu kushoto ni meneja wa shirika la SEMA,Ivo Manyanku.
DSC02075
Baadhi ya wakazi wa kata ya Tulya,waliohudhuria uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani,siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba.(Picha zote na Nathaniel Limu).

SHEREHE ZA UZINDUZI WA STUDIO ZA KITUO KIPYA CHA UTANGAZAJI GHETTO RADIO TANZANIA ZAFANA

0
0
 
  
Meneja wa Ghetto Radio ya Sibuka FM  94.5 Bw. Edward Rukaka  aliyeshika Mkasi ,akiizindua Rasmi Studio hiyo na kuitambulisha kwa wadau. kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Bahati nasibu Tanzania Bw. Abbas Tarimba akishuhudia uzinduzi huo.
 Mkurugenzi wa Ghetto Radio Kenya Bw. Majimaji akizungumza wakati wa usiku wa kuzindua Rasmi Studio ya Kurushia matangazo ya Radio ya Ghetto Radio ya Sibuka FM Nchini Tanzania hivi karibuni
 Mkurugenzi wa Sibuka George Nangali kulia akiwa na
Mkurugenzi wa Ghetto Radio Matt Brouwer  wakati wa Sherehe Fupi za  uzinduzi wa Studio hiyo iliyopo mtaa wa Hananasifu Kinondoni.
Katikati ni Balozi wa Ghetto Radio ya Sibuka FM Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva Juma Nature wakati wa uzinduzi huo

 
Mkurugenzi wa kituo cha afya cha Iran Nchini Tanzania Dkt. Farhad Arjomandi akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mtangazaji maarufu wa  Ghetto Radio ya Sibuka FM Basil Jonas Juu ya Studio hiyo
Dj Bling Kutoka Ghetto Radio ya Kenya akielezea uzoefu wake katika ... Ku mix Mix  Ngoma mbalimbali ambazo zinagusa kila rika la wasikilizaji..
 Wadau mbalimbali wakiwa katika Sherehe hiyo ya Uzinduzi wa Studio za Ghetto Radio ya sibuka Fm.
 Kulia ni Bw. Kelvin Guninita mfanyakazi wa Sibuka Media akiwa katika sherehe hizo za uzinduzi  wa studio za Ghetto Radio ya  Sibuka Fm.
Meneja wa Ghetto radio Tanzania Bwana Edward Rukaka akiwaonesha wageni waalikwa sehemu mbalimbali za studio hiyo
Wadau mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Meneja wa kituo hicho cha Radio Bw. Edward Rukaka jinsi shughuli zinavyofanyika ndani ya studio hizo za Ghetto Radio.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Bahati Nasibu ya Taifa Bwana Abbas Tarimba akimsikiliza kwa makini Meneja wa Ghetto Radio Tanzania Bw. Rukaka
 Wakurugenzi wa Key Media nao walihudhuria sherehe hizo za uzinduzi wa studio ya Ghetto Radio Tanzania.
 Katika picha ya pamoja ni Balozi wa Ghetto radio Tanzania msanii wa mziki wa Bongo Fleva Juma Nature na Violeth Okina wa kwanza  kulia ambaye ni Meneja Mauzo wa Ghetto Radio Tanzania katika sherehe hizo.

TAZAMA MKUTANO WA TCRA NA WAMILIKI WA BLOGS ULIVYOFANYIKA LEO JIJINI DAR

0
0

Updates: Hali ya Rais Kikwete yazidi kuimarika,awasiliana na wananchi kwa simu yake ya mkononi

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatatu, Novemba 10, 2014, alianza kuwasiliana na mamia kwa mamia ya wananchi mbali mbali nchini kujibu ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wa kumpa pole, kumtakia heri na nafuu ya haraka ambao amekuwa anatumiwa na wananchi tokea mwishoni mwa wiki.

Tangu alipofanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) Jumamosi iliyopita kwenye Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, Rais Kikwete amepokea mamia kwa mamia ya SMS zikimpa pole na kumtakia nafuu ya haraka.

Rais Kikwete bado anaendelea kujibu SMS hizo na wananchi ambao wamemtumia SMS Rais Kikwete waendelee kusubiri majibu ya Mhe. Rais kwa sababu anakusudia kujibu SMS zote ambazo ametumiwa.

Aidha, Rais Kikwete jana alizungumza kwa simu na uongozi wa juu wa Tanzania kwa mara ya kwanza tokea afanyiwe upasuaji. Rais alizungumza na Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda.

Wakati huo huo, madaktari wanaondelea kumtibu Rais Kikwete jana waliondoa bandeji kwenye sehemu ambako alifanyiwa upasuaji wakieleza kuwa hali yake inaendelea vizuri na anapata nafuu kwa kasi nzuri.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasiliana na baadhi ya wananchi waliokuwa wakimjulia hali kupitia simu yake ya mkononi kupitia ujumbe mfupi(sms) leo Jumatatu.Rais Kikwete anayepata matibabu katika hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore Maryland nchini Marekani anaendelea vizuri na anafanya mazoezi mara kwa mara na afya yake inaendelea kuimarika(picha na Freddy Maro)

Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Novemba,2014

MREMA AENDELEA NA MIKUTANO JIMBONI KWAKE VUNJO.

0
0
Mkutano wa hadhara wa chama cha Tanzania Labour (TLP) uliokuwa ukihutubiwa na Mbunge wa jimbo la Vunjo Agustine Mrema jirani na matanki ya Maji katika kijiji cha Mieresini wilaya ya Moshi vijijini.
Afisa uhusiano wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Frolah Nguma (aliyesimama)akitoa ufafanuzi juu ya maswala ya maji baada ya Mbunge Mrema kumtaka kufanya hivyo muda mfupi baada ya maofisa wa Mamlaka hiyo kufika katika Matenki ya Maji kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida.
Msimamizi mkuu wa (MUWSA) Kituo cha Himo Brucevictor Sangawe akitoa ufafanuzi kwa wananchi mbele ya mbunge wa jimbo la Vunjo ,Agustine Mrema juu ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya ukanda wa juu katika mji wa Himo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Mbunge Mrema.
Mh Mrema akifuatilia maelezo ya maofisa wa Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) walipokuwa wakitoa maelezo kwa wananchi (hawapo pichani)  ,Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya kasakazini.

AFRICA’S REGIONAL NETWORK FOR YOUTH POLICIES EXPERTS LAUNCHED AT THE FIRST GLOBAL FORUM ON YOUTH POLICIES ON BAKU, AZERBAIJAN.

0
0
Invest in Youth Logo
Africa made history during the closing session of the just concluded First Global Forum on Youth Policies, held in Baku, Azerbaijan by announcing the birth of African Network of Youth Policy Experts (AfriNYPE) to advance the cause of youth policies in the region.

The network was announced at the closing plenary session attended by over 700 invited delegates constituting of experts, researchers, professors, government representatives across the world, and the United Nations Secretary-General's Envoy on Youth, Mr. Ahmad Alhendawi.
A member of the Steering Committee, Adeola Austin Oyinlade, Human rights lawyer and Youth rights/policy expert from Nigeria described the unveiling as ‘good news from Africa’.

According to Mr. Oyinlade who is also a resource person to the African Union (Youth Division) on the implementation of African Youth Charter, the network’s objectives include establishing a comprehensive research and studies unit, in order to collect reliable data and analyse the current situation of youth policies in order to advise key African Stakeholders on concrete and practical mechanisms, for a more inclusive development and implementation of these policies, while improving legal enabling environment of youth participation in decision making.

Ms. Karima Rhanem, a civil society and youth policy expert from Morocco told the gathering that prior to the global forum, young African delegates to the forum engaged in intensive dialogue, through social media and desk research review to do situation analysis of youth policies in the region, mappings and SWOT analysis, which subsequently produced a concrete strategic document that led to the emergence of AfriNYPE.

According to Ms. Rhanem, AfriNYPE is a collective initiative of experts on youth policies in Africa who shared understanding of the urgent need for concrete development and implementations of youth policies in an African context.

interview with MAG TV
Seleman Kitenge interviewed with MAG TV.
Yvonne Akoth, a gender equality expert from Kenya and a panelist during the Forum mentioned the need for young African voices to be heard in public policy and youth policy development processes, in preparation for the Post2015 Development Goals.

This would be one of the objectives of AfriNYPE, ‘a network that would build the capacity of young people, by enabling them to understand the importance of policy implementation in addressing issues affecting their overall development’ said by Ms. Akoth.

On the strategy to achieve its objective, Abiola Hamid, a youth leader and Youth expert from Nigeria said the network will develop a common and workable understanding of youth policies with theoretical and practical key indicators. He added that the network intends to create a database and fact files as reference point for youth policy research in Africa, and carry out assessments and evaluations of African youth policies, implementations and impacts on the lives of African youths.
interview with UN Radio
Seleman Kitenge interviewed with UN Radio in Baku Azerbaijan.
On what he wants to do differently, Mr. Seleman Kitenge, Communication Personnel and Under Secretary General For Media-GIMUN from Tanzania responded, “I want to see young people have enough understanding of all matters related to policy, as well as being able to have a platform to voice out their views and being part of the problem solving, not being seen as a problems’.

On membership of the Network, Michael Zinkanell from Austria who is working with youth empowerment projects in Uganda said “our members consist of youth policy experts, who are directly working with youth empowerment and/or youth policies, targeting the youth in Africa.
All members should commonly value a democratic, fair and gender-balanced approach on how to improve young African’s life through policy development and implementation, regardless of ethnicity, religion, sexuality, or political orientation’.

Adding further, LombeTembo, an economist and a member of the Youth Governance and Accountability Task Team under Restless Development UK from Zambia said the Network membership base is made up of ‘African youth activists, researchers, policy experts and members of civil society organisations who attended the just ended First Global Forum on Youth Policies’. According to Ms. Tembo, ‘we are looking to widen our membership base and will be reaching out to African youth and youth -led organisations within Africa, as well as African youths in the Diaspora’.
meeting with Envoy2 
Seleman Kitenge(second left) and his counterparts in a special meeting with the UN Secretary General’s Envoy on Youth Ahmad Elhandawi.

During the AfriNYPE steering committee meeting with the United Nations Secretary-General's Envoy on Youth, Ahmad Alhendawi charged the young network to take it from ideas to actions.
While also speaking to the United Nations News Centre, Mr. Alhendawi said “we have seen young Africans come together to establish a network for researchers on youth policies. We have seen countries pledging support and commitment and resources to support the global initiative on youth policies. I’ve seen people debating issues around youth policies.”

Since the forum ended in Baku, delegates have returned to their various countries to renew their commitment, engagement and advocacy on youth policy matters. The First Global Forum on Youth Policies was hosted by the Government of Azerbaijan in Baku on 28-30th October, 2014 and was co-organised by the office of the UN Youth Envoy, Council of Europe, UNDP, and UNESCO with technical support of Youthpolicy.org
with minister of sport
Seleman Kitenge with the Minister of Youth and Sport of Azerbaijan,H.E Azad Rahimov.
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images