Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU PINDA AWASILI OMAN KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua gwaride baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Muscut wa Royal  Airport kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Oman Oktoba 27, 2014. Kushoto ni Naibu Waziri Mkuu wa Oman Mheshimiwa Sayyid Fahad Mahmoud Al Said. 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiongozana na Naibu Waziri Mkuu wa Oman,  Mheshimiwa Sayyid Fahad Mahmoud Al Said  (kushoto kwake) baada  ya kuwasili kwenye  uwanja wa ndege wa  Kimataifa wa  Muscut wa Royal Airport kwa ziara ya siku mbili nchini humo Oktoba  27, 2014.  
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio Oman baada ya kuwasili kwenye hoteli ya AL Bustan Palace mjini Muscut kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, Oktoba  27, 2014.


JWTZ WATEGUA BOMU LILOTEGWA KATIKA ENEO LA KITUO CHA KURUSHIA MATANGAZO CHA TBC SONGEA

$
0
0
Bomu lililotengenezwa kienyeji  kama linavoonekana katika picha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa mtaaram wa mabomu ambaye ni kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kabla ya kulitegua bomu hili.

Hili ni eneo la tukio ambalo limezungushiwa mkanda huu wa pilisi uliandikwa hairuhusiwi kupita eneo hili,Lakini chini ya huo mti kama inavoonekana katika picha kukiwa na udongo umetifuliwa ndipo mahara ambapo lilitegwa bomu hili la kutengenezwa kienyeji pia hapo ndipo huwa wanakaa askari wa Usalama barabarani kwa kujikinga na jua ama kupumzika pindi wanapokuwa kazini
Bomu lililotengenezwa kienyeji
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji.
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiwa anaonyesha umahili wake alionao aweze kulitegua bila kuleta madhara yoyote yale katika jamii(Picha na demasho.com)
-------------------------
 Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania(JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia matangazo kilichopo mshangano cha shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya saa moja jioni.

Bomu hili linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji nawatu wasiojulikana lilitegwa hatua  zinazokadiliwa thelathini kutoka kitika kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao za kila siku.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwamujibu wa wataalamu wa milipuko kutoka jeshi la Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili linaonekakana limetengenezwa kienyeji.
ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji askari polisi watatu  wakiwa katika doria katika kata ya misufini manispaa ya songea.

Msikhela amesema Jeshi la polisi linafanya jitihada za kuwapata watu hawa wanaohusika na mtandao huu wa utegaji wa mabomu na ulipuaji, Aidha ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa Jeshi la Polisi ili liweze kuwabaini watu wanaousika na matukio ya namana hii.

Na hii ni mara ya pili katika manispaa ya songea kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe Oktoba 16 mwaka huu askari watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,  walijeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo lilisadikiwa kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe mjini songea mkoani Ruvuma.

Askari hao walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika doria ambao ni WP Felista Abel, PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na mtandao huu wa demasho  kwa njia ya simu amesikitishwa na kitendo hicho cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha amani iliyopo katika mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata walewote wanaohusika na vitendo hivi.

TAARIFA KUTOKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

$
0
0
Katika gazeti la Jamhuri la Jumanne Agosti 19 – 25, 2014 ISSN No. 1821-8156 Toleo No. 150, zilichapishwa taarifa potofu zenye  kichwa cha habari;
 
  KASHFA IKULU;

·    Nyalandu atumia Leseni ya Rais kuua wanyamapori 704 bure,
·    Watakaouawa wamo pia tembo 8, chui 8, Simba 8, ndege,
·    Wauaji ni Wamarekani marafiki wa Waziri wa Maliasili.
I.   
Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuwafahamisha Umma kuwa, tuhuma hizi si za kweli. Tuhuma hizi zimetolewa na watu wenye nia ovu  na zimelenga kuchafua jina la Wizara ya Maliasili na Utalii na kumchafua mheshimiwa Waziri Lazaro Nyalandu, kumshushia Heshima, kumdhalilisha kwa umma ili kumpunguzia dhamira, malengo na  kasi ya kupambana na ujangili.

Ukweli ni kwamba Familia ya Freidkin ilipewa Leseni Maalum/Leseni ya Rais (Special License/President’s License) ya kuwinda kwa mujibu wa Kifungu cha 58 (1) cha Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 ikisomwa kwa pamoja na Tangazo la Serikali Na. 273 la mwaka 1974 ambacho kinampa mamlaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori baada kupata ridhaa ya Waziri mwenye dhamana ya Wanyamapori kutoa kibali maalum kwa malipo au bure. Aidha, kibali hicho hutolewa baada ya Waziri kuridhika kwamba kibali hicho kina maslahi kwa taifa na hakikinzani na sheria na mikataba ya kimataifa kama CITES. 

Kufuatana na Kifungu hicho cha 58 (1) Leseni Maalum hutolewa kwa mtu yeyote kwa masilahi ya kitaifa ikiwemo:-
1.    Utafiti wa kisayansi
2.    Makumbusho
3.    Elimu
4.    Utamaduni na
5.    Chakula wakati wa dharura

Maslahi ya taifa ni pamoja na leseni kutolewa kwa watu mashuhuri kama vile Wakuu wa nchi,  Wafalme, Malkia, Wakuu wa dini pamoja na watu ambao katika utendaji wao wametoa michango yenye manufaa maalum kitaifa au michango mikubwa katika shughuli za uhifadhi wa wanyamapori.

Katika utaratibu huu, kwa mwaka 2013 hadi sasa, Leseni ya Rais zimetolwa kwa watu wafuatao:-

Na.    Jina    Kibali Na.    Kampuni iliyowindisha    Bure/Malipo      
1    H.H. Sheikh Abdullah Mohamed Buli Al Hamed    000000657 cha 22/8-6/09/2013    Kilombero North Safaris/Green Mile Safaris    Bure      
2    H. H Sheikh Mohamed Rashid Al Maktoum    0000676 cha 16/01 – 26/01/2014    Ortello Business Corporation (OBC)    Bure      
3    Familia ya Freidkin ya Watu wanane     00006678-85 za 1-21/08/2014    Tanzania Game Trackers Safaris Ltd    Kwa malipo        
4    Kiongozi wa Bohora Duniani            Bure   

Familia ya  Freidkin imekuwa na sifa ya kupewa Leseni ya Rais kutokana na mchango wake mkubwa kwa taifa katika shughuli za uhifadhi wa Wanyamapori kwa kipindi cha zaidi ya  miaka ishirini iliyopita bila kukoma.

Familia ya Freidkin imekuwa ikitoa mchango huo kupitia Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii iitwayo Tanzania Game Trackers Safaris Ltd. Pamoja na Asasi yake iitwayo Freidkin Conservation Fund (FCF tangu miaka ya 1990).

FCF imekuwa ikitoa michango mikubwa hususan ya kukabiliana na ujangili.
Bw. Freidkin kwa kupitia Taasisi hii amekuwa akichangia na hata kushiriki katika shughuli za kuzuia ujangili na shughuli za kijamii kwa kufanya yafuatayo:-

a.    Kwa kushirikiana na watumishi wa Idara ya Wanyamapori katika kazi za kuzuia ujangili amekuwa akichangia mafuta ya doria katika Mapori ya Akiba ya Kizigo, Maswa, Moyowosi, Ugalla na Pori Tengefu la Lake Natron
b.    Kutoa magari ambayo hutumika kwenye kuzuia ujangili
c.    Kutoa helikopta kwa ajili ya kufanya doria kwenye mapori husika
d.    Kuchangia  malipo ya doria kwa askari wa Idara.
e.    Kuchangia katika shughuli za maendeleo ya jamii kama vile kujenga vituo vya doria (outposts) na ujenzi wa shule mpya (kwa mfano Kizigo Sekondari/Manyoni)

Vibali vilivyotajwa na Gazeti la Jamhuri la tarehe 19/08/2014, Toleo la 150 vilitolewa kwa familia ya Freidkin ya watu wanane (8) kwa ajili ya uwindaji kuanzia tarehe 1 hadi 21 Agosti 2014 kwenye vitalu vya Lake Natron, Makao open na Makao Wildlife Management Area (WMA), Maswa Kimali na Maswa Mbono kupitia kampuni ya Tanzania Game Trackers Safaris Ltd

Maeneo hayo yaliyowindwa hayahusiani na ugawaji wa vitalu kama ilivyoelezwa na gazeti la Jamhuri ya kuwa Waziri Nyalandu amegawa vitalu zaidi ya vitano kwa kampuni moja.. Leseni ya Rais inatuma kuwinda katika sehemu yoyote ile itakayoonekana inafaa kisheria bila kujali idadi ya vitalu husika kwa vile ni shughuli ya mara moja tu.

Uchambuzi wa makala ya gazeti hili ulitaja vipengele kama:-

a)    Gazeti la Jamhuri liliandika taarifa potofu yenye kicha cha habari;  KASHFA IKULU
Gazeti la Jamhuri liliandika taarifa potofu kuwa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametumia Leseni ya Rais kuwaruhusu marafiki zake Wamarekani wanane kuua wanyamapori 704 bila kulipa hata shilingi moja serikalini.

Tuhuma hizi si za kweli.
Ukweli ni kuwa, Pamoja na leseni hii kuitwa Leseni ya Rais kwa Mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 273 la mwaka 1974, leseni hiyo haitolewi na Ikulu bali hutolewa na Mkurugenzi wa Wanyamapori baada ya kupata ridhaa ya Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Maliasili na Utalii na leseni hiyo haikutolewa bure.

b)    Tuhuma zilizotolewa na gazeti la Jamhuri dhidi ya Waziri Nyalandu ya kuwa ametoa leseni ya Rais kwa rafiki zake Freidkin na familia yake pia si za kweli.

Leseni ya Rais ilitolewa kwa familia ya Freidkin na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kwa kuzingatia utaratibu kama walivyopewa watu wengine ambao wamekidhi vigezo kama ilivyoelezwa hapo juu.

Tuhuma zilizotolewa na gazeti la Jamhuri dhidi ya Waziri Nyalandu ya kuwa ametoa leseni la kuwinda wanyamapori 704 bila malipo pia si za kweli.

Ukweli ni kuwa, si kweli kwamba familia ya Freidkin ilipewa leseni bila malipo kwani familia hiyo  ilipewa Leseni ya Rais baada ya kulipia ada ya vibali (permit fee), ada ya nyara (trophy handling fee) na ada ya uhifadhi (conservation fee) na ada ya wanyamapori watakaowindwa ambayo ingelipwa baada ya uwindaji kufanyika kama ilivyo kwenye Kanuni za Uwindaji wa Kitalii (GN No. 243 Kanuni 21 (1),

Utaratibu huu unatumika kwa wawindaji wote wa kitalii.

Idadi ya wanyamapori wanaotolewa kwenye leseni yoyote kupitia kampuni za uwindaji wa kitalii hutolewa kwa kufuata “Safari Package” na siyo wote wanaowindwa kwa kuwa uwindaji ni wa kuchagua kwa kuzingatia ukubwa na ubora wa nyara, umri, jinsia na iwapo wamepatikana eneo husika. Hivyo kama mwindaji anashindwa kupata mnyama mwenye sifa hizo ni kwamba hatawinda mnyama husika hata kama ameandikwa  kwenye leseni. Hii ndiyo tasfiri ya kisheria ya kulipia wanyama watakaowindwa tu na siyo wanaoandikwa kwenye leseni/kibali.

 Aidha, kulingana na sheria, mwindaji anatakiwa kuandika kila mnyama anayewindwa nyuma ya leseni mara tu baada ya kuwinda kwa kuonesha tarehe mnyama alipowindwa, aina ya mnyama, idadi, jinsia, umri na mahali alipowindwa. Kazi hii huhakikiwa na Afisa Wanyamapori na Mwindaji Bingwa (Profesional Hunter) wa eneo husika kwa mujibu wa Kanuni za Uwindaji wa Kitalii.

c)    Tuhuma kuhusu idadi ya wanyama walioruhusiwa kuwindwa ikiwemo kuuwa tembo wanane (8)

Pamoja na familia ya Freidkin kupewa leseni ya Rais kuwindia, hakuna tembo yeyote wala Simba aliyewindwa. Tuhuma kwa Familia ya  Freidkin kuwinda Tembo wanane na simba si za Kweli. Tuhuma hizo zilikuwa na nia ovu ya kumchafua, kumdhalilisha Mheshimiwa Waziri Nyalandu pamoja na familia ya Freidkin.

Ukweli ni kwamba pamoja na kuwa idadi ya wanyama hao walikuwa wameandikwa kwenye leseni iliyotolewa, lakini wanyama hao hawakuwindwa kwa sababu hawakuwa wamefikia ubora wa Nyara inayotakiwa kuwindwa kisheria.
Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za uwindaji nchini, mnyama tembo anaruhusiwa kuwindwa kwa ajili ya matumizi binafsi na siyo ya kibiashara. Kufuatana na Mkataba wa CITES, Tanzania imekuwa ikiwinda tembo 50 kwa miaka ya 1990 na baadaye kwenye miaka 2000 tembo 200 idadi ya tembo ilipoongezeka.

Hata hivyo, mwezi Juni 2014 Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii alipunguza idadi hiyo kwa asilimia 50% kutokana na kupungua kwa idadi ya tembo wenye ubora wa  kuwindwa. Aidha, uwindaji huo unazingatia viwango vilivyowekwa kwa mujibu wa Kanuni za Uwindaji wa Kitalii. Endapo tembo aliyeandikwa kwenye kibali au leseni hajafikisha viwango stahiki hatawindwa.

d)    Tuhuma ya  Kuruhusu wageni kuwinda katika vitalu ambavyo siyo vya kampuni husika

Tuhuma hizi si za kweli.
Tuhuma hizi zina nia ovu ya kudhoofisha kasi ya kupambana na ujangili.

Ukweli nu kuwa, Freidkin na familia yake waliruhusiwa kuwinda kwenye vitalu vya Lake Natron, Makao open na Makao Wildlife Management Area (WMA), Maswa Kimali na Maswa Mbono kwa sababu hii ndiyo maana Freidkin na familia yake walipewa Leseni Maalum/Leseni ya Rais kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 243 la mwaka 2010 Kanuni ya 19(2) ambalo linaeleza kuwa mwenye Leseni ya Rais anaruhusiwa kuwinda eneo lolote kama atakavyoelekeza Mkurugenzi wa Wanyamapori. Kwa mantiki hii, si kweli kwamba Mheshimiwa Waziri Nyalandu alikiuka sheria na kugawa zaidi ya vitalu vitano vya kuwindia kwa familia ya Freidkin.

Hivyo, tuhuma ya kuwa Waziri Nyalandu amekiuka kifungu kinachoweka ukomo wa idadi ya vitalu ambavyo ni vitalu vitano kwa kampuni  si za kweli.

Kwa kuzingatia maelezo hayo hapo juu, kutolewa kwa leseni ya Rais kwa familia ya Freidkin kulizingatia sheria, kanuni na taratibu zote za uwindaji.

Tuhuma zote zilizotolewa dhidi ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Mheshimiwa Waziri Nyalandu kuhusu utoaji wa Leseni ya Rais ya kuwindia kwa familia ya Freidkin, zilikuwa na nia ovu ya kuchafua, kudhalilisha na kushusha heshima ya Wizara ya Maliasili na Utalii, na Mheshimiwa Waziri Nyalandu na familia ya Freidkin

e)    Tuhuma kuwa Waziri Nyalandu ameruhusu Tanzania Game Trackers Safari (TGTS) kumilikishwa vitalu vinane pamoja na eneo la wazi na hivyo kukiuka kifungu cha 38(7) cha sheria ya wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 pia si za kweli.

Ukweli ni kuwa kampuni ya Tanzania Game Trackers Safari (TGTS) ndiyo iliyotumika kuwindisha familia ya Freidkin kwenye maeneo matano yaliyotajwa juu na si vitalu vinane kama ilivyoandikwa na gazeti la Jamhuri.
Vilevile kama ilivyoelezwa hapo juu kisheria, mtu mwenye leseni ya Rais ya uwindaji anaruhusiwa kuwinda eneo lolote linalofaa kuwinda kisheria bila kujali ukomo wa idadi ya vitalu.
Tuhuma hizi zilikuwa na nia ovu ya kuchafua, kudhalilisha na kushusha heshima ya Wizara ya Maliasili na Utalii, na Mheshimiwa Waziri Nyalandu na familia ya Freidkin

f)    Tuhuma ya kuwa Waziri Nyalandu ameruhusu uwindaji wa kitalii kufanyika eneo la Makao, sehemu ambayo haijatengwa kama kitalu pia si za kweli.

Tuhuma hizi zinalenga kuchafua jina zuri la Mheshimiwa Waziri na kumpunguzia dhamira, Hari na kasi ya kupambana na ujangili.

Ukweli ni kuwa, eneo la Makao pamoja na kwamba halijatengwa rasmi kama kitalu cha uwindaji, lakini kisheria linaruhusiwa kufanyika shughuli za uwindaji (yaani kwa lugha iliyozoeleka – kuwindwa) kama ilivyo kwa maeneo mengine ya mapori tengefu na mapori ya wazi. Hii ndiyo maana familia ya Freidkin haikugawiwa vitalu bali ilipewa kibali cha kuwinda katika maeneo yaliyotajwa.

2.    Katika gazeti Jamhuri la tarehe 30 machi 2014 toleo namba 129 ilichapishwa taarifa potofu  yenye kichwa cha habari NYALANDU ’ AUZA’ HIFADHI
·    Yeye na lembeli waenda afrika kusini kukamilisha mpango
·    Katibu mkuu njia panda alazimishwa kuidhinisha safari, posho
·    Hifadhi nyingine nazo mbioni kutolewa kwa wawekezaji
    Taarifa hiyo potofu ilielezea kuwa Waziri Nyalandu alikwenda nchini Afrika ya Kusini na kufanya mazungumzo na kampuni ya African Parks Network (APN) kwa ajili ya kuikabidhi uendeshaji wa Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu ikiwemo kuuza hifadhi ya Katavi.
    Tuhuma hizi si za kweli.

    Tuhuma hizi zililenga kuchafua jina la Wizara ya Maliasili na Utalii na kumchafua mheshimiwa Lazaro Nyalandu, Waziri wa Maliasili na Utalii.

Ukweli ni kuwa  Safari ya Waziri Nyalandu kwenda Africa kusini ilikuwa rasmi na ilifuatia maagizo ya Serikali kuhudhuria mkutano wa African Parks Network (APN) wa uhifadhi ulioandaliwa na  asasi hiyo kwa lengo pia la kuhakiki uwepo, utendaji halisi wa taasisi hiyo na kufanya majadiliano kuhusiana na mapendekezo yao.

Huu ni utaratibu wa kawaida wa utendaji serikalini ambapo taarifa ya safari hiyo iliwasilishwa Serikalini kwa hatua zaidi.

Katika mkutano huo, hakukuwa na mikataba yoyote iliyowekwa na Waziri Nyalandu au maamuzi yoyote ya kukabidhi hifadhi za Taifa kama ilivyoelezwa na gazeti la Jamhuri.

Tuhuma hizo zilizolenga kuchafua jina la Wizara ya Maliasili na Utalii na Mhe. Nyalandu.

3     Gazeti la Dira jumatatu, Machi 31 – April 6, 2014, liliandika habari yenye kichwa cha habari “Kashfa za Nyalandu zatikisa. Na vichwa vidogo vya habari vilivyosomeka, Adaiwa kumiliki vitalu, kampuni ya “tours”, Aificha chini ya mwamvuli wa Wachina.

Tuhuma hizi si za kweli.
Tuhuma hizo zina nia ovu ya kuchafua jina la Mheshimiwa Waziri Nyalandu na   kupunguza kasi yake ya kupambana na ujangili.

4    Taarifa ya kuwa Waziri Nyalandu anatuhumiwa kurefusha msimu wa muda wa uwindaji kuanzia Julai Mosi hadi Machi 30 ambapo ni sawa na muda wa miezi tisa kila mwaka tofauti na muda wa kisheria ambao ni kuanzia Julai Mosi hadi Decemba 31 sawa na miezi 6 kwa mwaka si za kweli.
Ukweli ni kwamba Waziri Nyalandu alitangaza kusudio la kuongeza msimu wa uwindaji kutoka miezi sita kwenda tisa na hii iko ndani ya mamlaka ya waziri kisheria kama ilivyo kwenye Sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 na kanuni zake.

Hii siyo mara ya kwanza kwa mawaziri wenye dhamana ya Maliasili na Utalii kurefusha au kufupisha msimu wa uwindaji.

5    Tuhuma ya kuwa Waziri Nyalandu ni mmoja wa wafanyabiashara wa Uwindaji na yuko karibu kabisa na wawindaji wenye vitalu nchini hazina ukweli wowote.

Waziri Nyalandu ni waziri mwenye dhamana ya kusimamia masuala yote ya Maliasili na Utalii na anapaswa kuwa karibu na wadau wote wa maliasili na Utalii ili kuweza kusimamia vema sekta hiyo. Huwezi kuisimamia vema Sekta husika kwa kuwakwepa wadau husika.

6    Tuhuma ya kuwa Waziri Nyalandu anakabiliwa na kashfa ya kujihusisha na ujangili mkoani Singida pia si za kweli

       Ukweli ni kuwa tuhuma hizo zina nia ovu ya kuchafua jina la Waziri Nzyalandu, kumshushia heshima na hadhi yake kwa lengo la kupunguza na kukwamisha jitihada zake za kukabiliana na ujangili uliokithiri hususan mauaji ya tembo na faru.

     Jitihada zilizofanywa na Waziri Nyalandu hadi sasa ni pamoja na kutafuta fedha na vifaa ndani na nje ya nchi ikiwemo helikopta moja na kuwezesha kuanzishwa kwa mfuko maalum wa kukusanya fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo chini ya uratibu wa shirikal a Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ofisi ya Tanzania.

7    Kashfa za kumhusisha Waziri Nyalandu na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mwanyonye, Rehema Manji kudai kuwa alitishiwa bastola ni kosa kisheria kwani. Waziri Nyalandu hakuwahi kutenda kosa hilo.

Kutajwa kwa mmiliki wa gari namba T 505 BKM kuwa ni la ndugu Lazaro Samwel Nyalandu, mwenye utambulisho wa mlipa kodi (Tin: 105-059-701) si uthibitisho ya kuwa Waziri Nyalandu alihusika kumtishia bastola Rehema Manji. Kashfa hizo zililenga kumchafua, kumshushiaa hadhi  Waziri Nyalandu.
8    Katika gazeti la Jamhuri la Jumanne October 07 – 13, 2014 ISSN No. 1821-8156 Toleo No. 157, zilichapishwa taarifa zenye kichwa cha habari AUNTIE EZEKIEL ATANUA NA NYALANDU MAREKANI.

 Tuhuma hizi si za kweli. Tuhuma hizi zimetolewa na watu wenye nia ovu  na zimelenga kuchafua jina la Wizara ya Maliasili na Utalii na kumchafua mheshimiwa Waziri Lazaro Nyalandu, kumshushia Heshima, kumdhalilisha kwa umma ili kumpunguzia dhamira, malengo na  kasi ya kupambana na ujangili.

Ukweli ni kuwa, Waziri Nyalandu hakuhusika kwa namna yoyote ile na kile kilichoelezwa na gazeti la Jamhuri “Aunty Ezekiel atanua na Nyalandu Marekani” kichwa cha habari hiyo na vichwa vidogo vya habari vilivyoandikwa vililenga kutoa picha potofu kwa umma ili kumchafua, kumdhalilisha, na kuvuruga amani kwa Waziri Nyalandu na familia yake.

Waziri wa Maliasili na Utalii, akiwa nchini Marekani kikazi, alialikwa kuhudhuria shughuli ya kutimiza miaka minne ya blog ya Vijimambo ambayo inamilikiwa na Watanzania waishio Marekani.

Waandaaji wa shughuli hiyo iliyolenga kutangaza Utalii wa Tanzania nchini Marekani walimwalika Waziri Nyalandu kuwa mgeni rasmi. Mwaka jana kwenye sherehe kama hizo alialikwa Rais mstafu Ali Hassan Mwinyi

Wizara ya Maliasili na Utalii haikuhusika na uratibu wa safari ya Msanii Auntie Ezekiel.

Tarifa hizo zimelenga kuchafua Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Mheshimiwa Waziri Lazaro Nyalandu.

Tuhuma za ufisadi, ujangili na matumizi mabaya ya madaraka hazina ukweli wowote. Tuhuma hizo zinalenga kudhoofisha kasi ya Waziri Nyalandu katika kupambana na ujangili.

9    Hoja ya kuwa waandishi wa habari wameshinda na kuwa wameokoa mamilioni ya fedha za umma ambazo zingetumika kulipia mkutano na badala yake mkutano huo ulifanyikia wizarani hazina msingi.
Hoja hizo si za kweli kwa kuwa Mheshimiwa Waziri Nyalandu anatumia kumbi za wizara kufanya mikutano na wadau.

Mikutano ya wizara ya Maliasili na Utalii inayofanyikia kwenye kumbi za mikutano nje ya wizara, inafuata taratibu zote za Serikali na inategemeana na idadi ya washiriki wa mikutano hiyo na aina ya mkutano husika.

Utaratibu huu ni wa kawaida na hutumiwa na watendaji na viongozi mbalimbali wa Serikali na si upotevu wa fedha za umma kama inavyodaiwa na magazeti husika bila kujua uhalisia wa mikutano, idadi ya watu watakaohudhuria mkutano , na wadau wa mkutano husika.

Mikutano hii imekuwa na manufaa makubwa kwa taifa katika swala zima la kupambana na ujangili

10    Tuhuma ya kuwa waziri anafanyia kazi hotelini si za kweli kwa sababu kiongozi wa serikali wa ngazi za juu anakuwa kazini muda wote bila kujali yuko wizarani ama nje ya wizara.

Tuhuma hizo zinalenga kuchafua jina zuri la Waziri Nyalandu, kumkatisha tamaa na kumpunguzia heshima yake kwa umma ili kupunguza kasi yake ya kupambana na ujangili.

Hadi sasa kuna mafanikio makubwa yaliyojitokeza katika suala zima la kupambana na ujangili ikiwemo Kupungua kwa kiasi kikubwa kwa mauaji ya tembo. Idadi ya tembo katika ikolojia ya Serengeti - Maasai Mara imeongezeka, kupungua kwa matukio ya ujangili katika Pori la Akiba  Selous kuanzia mwezi machi 2014 hadi sasa, wadau wengi kujitokeza katika kusaidia suala zima la kupambana na ujangili wa wanyamapori nchi kama Marekani, Ujerumani, China, Uingereza.

Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa taarifa kwa umma kwamba tuhuma zote zilizotolewa na hata zitakazoendelea kutolewa na gazeti la Jamhuri dhidi ya Wizara ya Maliasili na Utalii na dhidi ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Lazaro Nyalandu zinalenga kulichafua jina la Wizara ya Maliasili na Utalii na pia kuchafua jina la Mheshimiwa Waziri Lazaro Nyalandu na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya gazeti la Jamhuri na chombo chochote cha habari kitakachotoa taarifa za kuchafua jina la Wizara ya Maliasili na Utalii na Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Lazaro Nyalandu.

TAARIFA HII IMETOLEWA NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

Airtel yaipeleka Airtel Trace Music Stars Mikoani

$
0
0
 
 Msanii  chipukizi wa kijiwe cha Matofali jijini Morogoro ajulikanaye kwa jina la Jibwa Kali akionyesha umahiri wake wa kuimba wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo
 Msanii  chipukizi ajulikanaye kwa jina la Hamisi Ramadhani aka Brashi Waya 2akionyesha umahiri wake wa kuimba wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo. Pichani ni mashabiki na vijana wa kijiwe cha Matofali mkoani Morogoro.
Meneja Uhusiano wa Airte Bwana Jackson Mmbando akiongea na wasanii chipukizi wa Kijiwe cha Matofali mkoani Morogoro wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo.




·         Wasanii chipukizi kutoka morogoro watembelewa katika vijiwe vyao na kujiunga na mashindano ya Airtel Trace.

Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel imeendelea kuwafikishia wateja wake na wapenzi wa muziki katika mikoa mbalimbali na kuwaunganisha katika mashindano ya kutafuta mwamamuziki chipukizi ya Airtel Trace yaliyozinduliwa rasmi nchini mwanoni mwa mwezi octoba. Airtel imetembelea Mkoa wa Morogoro na kuzindua rasmi huduma ya Airtel Trace music star katika vijiwe mbalimbali mkoani hapo.

Akizungumza na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya katika vijiwe mbalimbali mjini Morogoro, Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema huduma hiyo inamuwezesha mtu yeyote mwenye kipaji cha kuimba  kujiunga na kushiriki kwa kupitia simu ya mkononi kwa kupiga namba 0901002233 kisha kurekodi wimbo wake na kuutuma.

Mashindano haya yanatoa mwanya wa watanzania wenye ndoto za kuwa wanamuziki nyota kupata fulsa ya kuzifikia ndoto zao. Sambamba na hilo tutakuwa na washindi watakaojishindia zawadi mbalimbali hapa nchini kama vile pesa taslimu na nafasi ya kushinda na kushiriki mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini south Afrika na kushirikisha washindi wengine toka nchi 13 barani afrika ambabo Mshindi wa Afrika atapata nafasi ya nafasi kwenda kurekodi wimbo wake nchini Marekeni na kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa msanii nguli wa muziki Akon huko nchini Marekani
Nao baadhi ya wasanii waliokutwa kwenye vijiwe vyao waliweza kushiriki shindano hilo kwa kurekodi nyimbo zao kupitia Airtel Trace muziki star huku wakiishukuru Airtel kwa kuwaletea huduma ambayo itawakomboa wasanii chipukizi wasio na uwezo.

Ambapo Hamis Ramadhan  aka brash waya 2 alikuwa na haya ya kusema” tunashukuru Airtel kwa kutuletea mshindano haya kitaani kwani tunavipaji lakini tunashindwa kupiga hatua kwakuwa uchumi ni mdogo tunaamini kwa kuppitia Airtel Trace tutatoka , kukubwa ni kusaidia na kupigiana kura ili tufanikiwe, tunaamini Airtel Trace Tanzania Atatokea Morogoro na hivyo natoa wito kwa wanamorogoro wajiunge kwa wingi na kutumia nafasi hii ili kubuka kuwa masuper star.

Kwa upande wake Ramadhani Nguyao alisema “ nimefurahia mpango mkubwa na wakwanza Tanzania utakaowawezesha wasanii chipukizi kupata fulsa ya kuimba na kurecord wasanii wakubwa kama Akon. Mimi nimevutia na ntajiunga na mashindano haya na waomba watanzania wengi  na wasanii wenzangu wa Morogoro na nje ya Morogoro kujiunga na kushiriki katika mashindano haya ya Airtel Trace Music Stars.

Mashindano ya Airtel Trace Music Stars yalizinduliwa rasmi nchini Mwanzoni na October na yatadumu kwa muda wa mienzi sita ambapo fainali ya mashindano haya inategemea kufanya Mwaka kesho Machi 2015 nchini South Afrika.
 

KIBONZO CHA NATHANI MPANGALA

AFRICA DIASPORA MARKETPLACE III LAUNCHED AT TANZANIA EMBASSY

$
0
0
The Embassy of Tanzania in Washington, DC hosted the launch of the African Diaspora Marketplace III (ADMIII), on October 27th 2014. ADM is an opportunity for African diaspora members who are involved in businesses in their home country to acquire a grant from the United States Agency for International Development (USAID), which works together with Western Union and Homestrings to provide grants and technical support to these businesses. 

The Marketplace was initiated in 2009 in recognition that many Africans in the US are involved in projects in their home country but could use some extra help in terms of funding and technical support. ADM III will be open for application submission toward the end of 2014 and will focus mainly on funding African businesses that are looking to increase the use of ICT in their work. More information available at www.diasporamarketplace.org

Jeffrey L. Jackson, Senior Private Sector Advisor, USAID speaking about the launch of ADM III. 
H.E. Ambassador Liberata Mulamula sharing her remarks to the audience of the ADM III launch. Since ADM I and II had only one Tanzanian participant, she encouraged those in the Tanzanian diaspora to take advantage of this opportunity and apply for the grant funding. As a woman Ambassador, she was heartened to announce that the ADM has a strong partnership with the African Womens Entrepreneurship Program (AWEP), and that there is a special effort to promote women-owned businesses.
Linda Etim, Deputy Assistant Administrator for Africa, USAID
Barbara Span, Vice President, Global Public Affairs, Western Union
Liesl Riddle, Professor, George Washington University School of Business
Eric-Vincent Guichard, CEO, Homestrings
Zelalem Dagne, ​
CEO, Global Tracking, ADM Awardee
Manager of Global Technology & Investment PLC, 

H.E. Ambassador Amina S. Ali, Permanent Representative of the African Union Mission to the USA 

Ambassadors and representatives of the African diplomatic corps in Washington DC

MAADHIMISHO YA MWEZI WA HUDUMA KWA WATEJA WA NBC YAZIDI KUNOGA

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Rukia Mtingwa (kulia) akizungumza na mteja wa benki hiyo, Job Mwakibinga katika tawi la Mlimani City ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yanayoendelea ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja ambapo maofisa wa benki hiyo hutembelea matawi mbalimbali na kuhudumia wateja.
 Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Rukia Mtingwa (katikati) akizungumza na mteja wa benki hiyo, Job Mwakibinga katika tawi la Mlimani City ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja ambapo maofisa wa benki hiyo hutembelea matawi mbalimbali na kuhudumia wateja. Kulia ni Mkuu wa Matawi ya NBC, Gaudence Shawa.
 Mkuu wa Matawi ya Benki ya NBC, Gaudence Shawa (kulia) akizungumza na na mmoja wa mteja wa benki hiyo katika tawi la Mlimani City ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja ambapo maofisa wa benki hiyo hutembelea matawi mbalimbali na kuhudumia wateja.

 Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Rukia Mtingwa (kushoto) akizungumza na mmoja wa wateja wa benki hiyo katika tawi la Mlimani City ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC.
Baadhi ya wateja katika Tawil la NBC Mlimani City wakipewa viburudisho wakati wakisubiri kuhudumiwa. Ili kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja maofisa wa benki hiyo hutembelea matawi mbalimbali ili kuzungumza na kupata maoni yao kuhusu ubora wa huduma wazipatazo. 

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YAKE RASMI YA SIKU MBILI VIETNAM

$
0
0
 President Dr Jakaya Mrisho Kikwete lies a wreath at
the Mausoleum of the First President Ho Chi Minh in Hanoi on  his last
leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014 .
 
  President Dr Jakaya Mrisho Kikwete visits the Hung Fen Food Stuff
Corporation at Trung Son in Hanoi on his last leg of his two-day
official visit to Vietnam today October 28, 2014
  President Dr Jakaya Mrisho Kikwete in a souvenir photo with workers of  the Garment 10 Corporation textile mill he visited at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014
 :President Dr Jakaya Mrisho Kikwete shown some historical items as
he visits the Garment 10 Corporation textile mill at Nguyen Van Linh
Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on  his last leg of
his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014
President Dr Jakaya Mrisho Kikwete visits the Garment 10
Corporation textile mill at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward,
Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit
to Vietnam today October 28, 2014.PICHA NA IKULU.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA MWEZI WA WANAWAKE WAJASILIAMALI (MOWE) JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi rasmi wa Maonesho ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, wakati aliwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 28, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Maonesho ya mwezi wa Wanawake Wajasiliamali (MOWE).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi msaidizi wa Kampuni ya Kazymate, Mariam Mjewa, kuhusu Jarida maalum la ‘Mchakarikaji’  wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Chupa ya kinywaji cha Dodoma Wine wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Viatu (makubazi) na kusikiliza maelezo kutoka kwa Bi Hadija Rashid wa Kikundi cha Wajasiliamali cha Vumilia Corporation kutoka Pemba, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia bidhaa na kusikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kikundi cha Wajasiliamali Walemavu cha Women Clief Mafinga, Fatina Kangessa, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu wa Kitaifa wa Program kuendeleza Ujasiliamali kwa Wanawake, Noreen Toroka, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya GS 1, Ester Budili, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali na wageni waalikwa katika maonesho hayo. Picha na OMR

Tanzania yaeleza mipango yake ya kuendeleza Jotoardhi

$
0
0
 Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo katika Bonde la Ufa katika kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wa nchi zilizo katika Bonde la Ufa wakijadiliano jambo wakati wa kikao cha wajumbe hao kujadilia masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Jotoardhi kwa nchi wananchama.
 Baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wan chi zilizo katika Bonde la Ufa wakiendelea na kikao kujadili hatua mbalimbali zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao, kuangalia faida zalke, changamoto na namna ya kuzitatua.
Mmoja wa Wakufunzi wa mafunzo yanayoendelea leo  kabla ya kufunguliwa rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa ya Jotoardhi akitoa mafunzo kwa baadhi ya washiriki wanaohudhuria mafunzo hayo jijini Arusha.


Tanzania yaeleza mipango yake ya kuendeleza Jotoardhi
Na Asteria Muhozya, Arusha.

Tanzania imeeleza mipango yake ya kuendeleza masuala yanayohusu nishati jadidifu mbele ya Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo katika Bonde la Ufa katika kongamano la Tano la Kimtaifa la Jotoardhi linaloendelea jijjini Arusha.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho kwa niaba ya Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Jotoardhi Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Paul Kiwele amesema kuwa lengo la kukutana kwa kamati hiyo ni kuzungumzia hatua zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao.

Bw. Kiwele ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo ameeleza kuwa, lengo jingine la kikao hicho ni kuangalia faida zilizopatikana kupitia nishati hiyo pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali na  kuona namna bora ya kuzitatua.

Ameongeza kuwa, pendekezo la nchi wanachama kupata misaada mbalimbali ya kuendeleza masuala ya jotoardhi katika nchi zao  ikiwemo ya kifedha limepitishwa na mashirika kadhaa ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uhifadhi wa Mazingira  ( UNEP) na Umoja wa nchi zilizo katika bonde la Ufa (ARGEO).

Aidha, Bw, Kiwele ameongeza kuwa, kikao hicho kimeamua kuipa nafasi Tanzania kusaidiwa kuendeleza masuala ya jotoardhi katika eneo lenye viashiria vya jotoardhi la Ngozi, Mkoani Mbeya.

Kikao hicho cha Kamati ya Watoa Maamuzi ni miongoni mwa shughuli zinazoendelea katika kongamano la tano la jotoardhi ambapo linakwenda sambamba na mafunzo mbalimbali yanayotolewa kuhusu masuala ya jotoardhi ikiwemo masuala ya utafiti, uchorongaji na masuala ya fedha.

 Kongamano hilo litafunguliwa rasmi tarehe 29 Oktoba, 2014, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal jijini Arusha na litawashirikisha washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi mbalimbali duniani.

CHID BENZ APANDISHWA KIZIMBANI JIJINI DAR LEO KWA SHITAKA LA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA,AKOSA DHAMANA, KESI YAKE KUTAJWA TENA NOVEMBA 11

$
0
0
MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi Abdallah Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Chid Benz amefikishwa  mapema leo saa 3:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusomewa mashitaka yake. Saa 7:50 mchana alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo, hakimu aliamuru msanii huyo kutolewa nje ili akave vizuri nguo baada ya suruali aliyokuwa amevaa mlegezo maarufu kama kata kei kuonyesha nguo yake ya ndani.
“Kwanza mtoeni nje aende akavae nguo hizo zinazodondoka…” aliamuru Hakimu.

Saa 7:54 alirejeshwa ndani ya chumba cha mahakama upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda, ulimsomea mashitaka yake.

Wakili Kombakono alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.

Wakili huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvua dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.

Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na dhamana dhidi ya mshtakiwa.

Hakimu Lema alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazoamini na siyo walimu na dhamana ya Sh. Milioni moja.

Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na amepelekwa mahabusu hadi Novemba 11, kesi hiyo itakapotajwa.

PICHA ZA TUKIO LA MSANII CHIDI BENZI AKIPELEKWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO KWA SHITAKA LA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA.

$
0
0
 Msanii wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini leo Dar es Salaam kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
 Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akiingia Mahakamani leo.
 Chidi Benzi akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi.

Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
 Chidi Benzi akipanda karandinga kwa ajili ya kuelekea katika mahabusu ya Segerea.

Na Mwandishi Wetu

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benzi’ leo amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la matumizi ya dawa za kulevya.


Chid Benzi, alipandishwa kizimbani majira ya saa nane mchana, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, ambaye alimtaka msanii huyo atolewe nje kutokana na uvaaji mbaya wa suruali yake kwani alivaa ‘Kata kei’ ili avae vizuri nguo.


Akisomewa mashitaka yake, na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono, alidai kwamba mnamo 24 Oktoba 2014, Chidi Benzi alikutwa na dawa hizo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Alidai kwamba, shitaka la kwanza linalomkabili ni kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya sh.38, 638. Pia shitaka la pili ni kukutwa na gramu 1.72 za dawa kulevya aina ya Bangi yenye thamani 1,720.


Mbali na hilo, shitaka la tatu ni kukutwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa hizo za kulevya, ambapo alikutwa na Kifuu cha nazi kitupu na kijiko kimoja.


Hata hivyo, wakili huyo alidai kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika. Hakimu Lema alihairisha kesi hiyo hadi Novemba 11, mwaka huu baada wadhamini kushindwa kujitokeza kwa haraka.


Hakimu Lema alisema, mshitakiwa huyo anatakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili wa kudumu pamoja na bonfdi ya Sh.milioni 1.


Hali hiyo ya kushindwa kupata dhamana ilizua hali ya simanzi kwa familia yake, kutokana na kuchelewa kujitokeza kwa wadhamini wake mbele ya Hakimu na hivyo kushindwa kupata dhamana.


Chidi Benzi alikamatwa na dawa za kulevya katika hatua ya ukaguzi kwaajili ya kupanda ndege ya Fastjet akielekea jijini Mbeya, juzi jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

NEWS ALERT: AJALI MBAYA YATOKEA YOMBO VITUKA MWISHO WA LAMI

$
0
0
Gari aina ya Hiace ambayo ni daladala yenye namba za usajili T769 AFP imedondokewa na Kontena ambalo lilikuwa limebebwa kwenye lori huko Yombo Vituka Mwisho wa Lami, Ajali hii imetokea muda mfupi tu uliopita na kupelekea hofu ya kupoteza abiria wote waliokuwamo katika Daladala hiyo

Ripota wetu anaendelea kutafuta habari kutoka eneo hilo la tukio.Picha na Mdau wa Lukaza Blog  Samora Julius

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO, MHE. DKT. PINDI CHANA(MB.) ATEMBELEA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI ARNAUTOGLU, DAR ES SALAAM.

$
0
0
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.), leo tarehe 28 Oktoba, 2014 amefanya ziara katika Chuo cha  Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu – Ilala, Dar es salaam, kwa lengo la kukagua maendeleo ya utoaji wa mafunzo kwa wananchi.
Chuo cha  Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu hutoa mafunzo ya muda mrefu, muda mfupi na mafunzo nje ya chuo, ambayo yote yamelenga katika kutoa stadi na maarifa mbalimbali yanayowawezesha washiriki kupata ujuzi ili waweze kujiajiri wenyewe au kuajiriwa katika Taasisi mbalimbali kwa lengo la kuzalisha mali na hivyo kujiongezea kipato na kupunguza umaskini.
Kwa upande wa mafunzo ya muda mrefu asilimia kubwa ya Wanafunzi wanaojiunga na Chuo hiki ni watu wenye ulemavu, wengi wao wakiwa na ulemavu wa akili.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi na uongozi wa wanafunzi wa Chuo cha  Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Ilala – Dar es salaam , wakati alipofanya ziara Chuoni hapo  leo Oktoba 28, 2014.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana(Mb.) akiongea na watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu ( hawapo pichani), wakati alipofanya ziara Chuoni hapo, leo Oktoba 28, 2014. Kushoto ni Bwana Stephen Saro,  Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Bibi Pulcheria Ndamugoba.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana(Mb.) akikagua mazingira ya utoaji wa mafunzo katika madarasa ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, ikiwa ni pamoja na kuhojiana na washiriki wa mafunzo (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014. Kulia ni Bwana Stephen Saro, Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Bibi Pulcheria Ndamugoba.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) akiangalia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakitolewa kwa washiriki wa darasa la Uashi, katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014.

 Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Bibi Pulcheria Ndamugoba akitoa ufafanuzi kuhusu eneo la chuo kwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) wakati alipofanya ziara katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014. 
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) akisisitiza jambo, wakati wa alipokuwa akikagua maeneo ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014.

RAIS KIKWETE AONDOKA NCHINI VIETNAM BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI NCHINI HUMO

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza (wa pili kushoto), Mbunge wa Ilala na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mussa Azzan Zungu (kulia), Mbunge wa Tumbe Mhe Rashid Ally Abdallah (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini China Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahman Shimbo muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam jijini Hanoi leo Oktoba 28, 2014.
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na wenyeji wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam leo Oktoba 28, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na wenyeji wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam leo Oktoba 28, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza na Balozi wa Tanzania nchini China Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahman Shimbo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam jijini Hanoi leo Oktoba 28, 2014. PICHA NA IKULU

customized wristbands for you

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

$
0
0
Wanahitajika wasichana wa kuuza duka kubwa liliopo posta jijini dar es salaam, wenye uwezo wa kufanya Marketing, na Online Sales. 
wawe na uwezo wa kuzungumza kiingereza na kiswahili fasaha. elimu kuanzia diploma.
wasiliana nasi kwa namba zifuatazo 0756608383 na 0713608383

Wanawake waaswa kutumia fursa iliyopo katika sekta ya bahari.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Usalama wa Mazingira Majini Bw. Tumpe Mwaijande kutoka Wizara ya Uchukuzi kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka akiongea na wajumbe wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) wakati wa ufunguzi wa mkutano wao wa mwaka unaofanyika jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Msaidizi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO) Pamela Tansey akiwasilisha mada wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) uliaofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Veronica Maina akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) uliaofanyika leo jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa mkutano wa mwaka wa WOMESA mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo. (Picha na Eleuteri Mangi –MAELEZO)


 Mjumbe wa sekretarieti ya Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) Bi. Veronica Maina akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) uliaofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Mwenyekiti wa WOMESA kutoka Mauritius Bi. Meenaksi Bhirugnath-Bhookun akitoa mada wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika  uliaofanyika leo jijini Dar es salaam.
 Dkt. Faustina Ncheye kutoka WOMESA Tanzania akimpima afya Bi Tumaini Namoya mjumbe wa mkutano huo kutoka Kenya.


Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Wanawake wameaswa kutumia fursa iliyopo katika sekta ya bahari kwa kupata elimu na mafunzo ya sekta hiyo ambayo ni msingi wao katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia ukuaji sayansi na teknolojia inayoongezeka kwa kasi duniani.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Mazingira Majini Tumpe Mwaijande kutoka Wizara ya Uchukuzi kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA) unaofanyika leo jijini Dar es salaam.

Akisoma hotuba kwa niqaba ya Katibu Mkuu huyo, Mwaijande amewataka wajumbe wa mkutano huo (WOMESA), wawe tayari kujadili masuala yanayojenga na kukuza ushiriki wa wanawake katika sekta ya bahari katika nchi zao.

Katika mkutano huo wa siku nne ambao umeanza leo oktoba 28 na unatarajiwa kumalizika Oktoba 31 mwaka huu, mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo mpango mkakati wa WOMESA kuhusu ushiriki wa wanawake katika masuala ya sekta ya bahari katika nchi wanachama.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO) Pamela Tansey amesema kuwa WOMESA imekuwa msatari wa mbele katika kumwendeleza mwanamke kwenye sekta ya bahari.

Pamela amesisitiza kuwa wajumbe wa mkutano huo ni vema waelewe na kusimamia dira ya WOMESA ambayo lengo lake ni kuwawezesha wanawake kupata ajira katika sekta ya masuala ya bahari kwa njia ya kupta elimu na mafunzo katika kuendeleza taaluma yao juu ya masuala ya bahari.

Mkutano huo wa WOMESA unajumuisha wajumbe 52 kutoka nchi mbalimbali wanachama zikiwamo Ethiopia, Namibia, Komoro, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Mauritius na Kenya.

Nchi nyingine ni Angola, Sudani, Lesotho, Uganda, Somalia, Eritrea, Botswana, Rwanda, Madagaska, Afrika Kusini, Msumbiji, Burundi, Malawi, Djibout, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.

Mkatano huo wa siku nne unafanyika nchini chini ya ufadhili wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Taasisi ya Masuala ya Bahari Tanzania (DMI),   shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) kwa kushirikiana na  Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP). 

Rais Kikwete Mgeni Rasmi maadhimisho ya miaka 10 ya Utumishi wa Umma.

$
0
0
 Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu Kongamano la maadhimisho ya Miaka 10   ya Tume hiyo tangu kuanzishwa kwake ambapo Kongamano hilo litawahusisha Mawaziri, KatibuMkuu Kiongozi na Watendaji Wakuu kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea,Taasisi na Mashirika ya Umma. Kulia ni Naibu katibu wa Tume hiyo Bi NeemaTawale.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu Kongamano la maadhimisho ya Miaka 10   ya Tume hiyo tangu kuanzishwa  kwake ambalo litafanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere tarehe 30 Oktoba, 2014 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kushoto ni Naibu Katibu wa Tume hiyo Bi Rose Elipenda na kulia ni Naibu Katibu  Bi Neema Tawale akifuatiwa na Naibu Katibu Bi Rose Mboya. (Picha na Frank Mvungi-MAELEZO)
 
Frank  Mvungi-Maelezo
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kongamano la maadhimisho ya Miaka 10 ya Tume  ya Utumishi wa Umma yatakayofanyika jijini Dar es salam Oktoba 30 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Julius  K. Nyerere.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam  na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi Claudia Mpangala wakati wa Mkutano na waandishi wa habari ulio lenga kutoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho hayo.

Akifafanua kuhusu siku hiyo Mpangala amesema Kongamano hilo la siku moja litaanza saa 2:00 asubuhi hadi 11:00 jioni ambapo pamoja na mambo mengine kongamano hilo litahusisha historia ya Utumishi wa Umma kabla na baada ya Uhuru.

“Kauli mbiu katika  maadhimisho hayo ni Imarisha Uzalendo,Uadilifu na Uwajibikaji katika Kusimamia Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma ili kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini” alisemaMpangala.

Akizungumzia wageni watakaoshiriki Mpangala amesema kongamano hilo litawahusisha Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi, Watendaji Wakuu kutoka katika Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Idara  zinazojitegemea, Taasisi na Mashirika ya Umma, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu.

Pia Mpangala alitoa wito kwa waalikwa wote kuhudhuria  kongamano hilo kwa lengo la kuonaTume ilipotoka, ilipo na inapoelekea kwa kuyatazama mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 na mwelekeo wa Tume katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Tume ya Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 9 (1) cha sharia ya Utumishi wa Umma NA. 8 ya mwaka 2002 ambapo kwa mujibu wa kifungu cha 9 (3) cha sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa kwa sharia Na 18 ya mwaka 2007.

Ziara ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira katika Migodi

$
0
0
 Mtaalamu kutoka Mgodi wa Geita akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira juu ya utekelezaji wa sheria ya Mazingira katika mgodi huo.  Wengine katika picha ni wajumbe wa Kamati hiyo.
 Kutoka kulia, Mh. James Lembeli Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira akitoa maagizo kwa wataalamu wa mgodi wa Geita (hawapo pichani) juu ya Hifadhi endelevu ya Mazingira kwa mujibu wa Sheria. Wapili kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu na wengine ni wajumbe wa Kamati hiyo.
Katika jitihada za kuhifadhi mazingira katika Mgodi wa Geita, pichani ni eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya utupaji wa taka zinazoharibika.

 Sehemu ya Mabwawa yanayotumika katika shughuli za uzalishaji katika Mgodi wa Geita.


Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images