Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

MROKI AJIPIGA RISASI NA KUFA ARUSHA

$
0
0

MFANYABIASHARA wa Arusha anayemiliki kampuni ya Tanzania Bush Camp yenye kambi za watalii katika hifadhi za Serengeti mkoani Mara na Manyara iliyopo katika mikoa ya Arusha na Manyara, Timoth Mroki (36) amejiua kwa kujipiga risasi tatu kifuani akiwa katika baa maarufu ya Arusha Raha iliyopo la Shams, jijini hapa.

Kisa cha kujiua kwake kimetajwa ni kusababisha ajali, baada ya kuligonga gari jingine katika eneo la Mbauda wakati akitokea katika makazi yake yaliyopo eneo la Kwa Mrombo, jijini hapa.

Alifikwa na mauti katika tukio lililotokea kati ya saa 1:30 na saa 2:00 usiku, ndani ya baa maarufu ya Arusha Raha.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mroki alifika katika baa hiyo baada ya kufanikiwa kuwatishia kwa risasi waendesha bodaboda waliokuwa wamemzingira katika eneo la ajali na kisha kuondoka kwa kasi kwa gari lake aina ya Nissan Navara. 

“Alipiga risasi mbili hewani waliokuwa wamemzunguza wakanywea, akatumia mwanya huo kukimbia na moja kwa moja akafika Arusha Raha pengine kwa lengo la kujificha, na hapo akaanza kunywa…

“Ingawa inaonekana alikotoka alikunywa kidogo, alipofika Arusha Raha alikunywa haraka pombe mbili kali aina ya Valuer na wakati anamalizia ya tatu, akajikuta anazingirwa tena na wale waendesha bodaboda,” anasema mtoa habari huyo na kuongeza kuwa, baada ya kufyatua tena risasi mbili nyingine hewani, lakini bila ya dalili ya watu hao kutishika, ndipo akaamua kujimiminia risasi.

Habari zaidi zinasema wakati anazingirwa, naye akijihami kwa risasi wasamaria wema wakiwa harakati za kupiga simu polisi walishitukia polisi wakiingia katika eneo la tukio lakini tayari Mroki alikuwa ameshajitoa uhai baada ya kujimiminia risasi kifuani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatusa Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, ingawa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi ya wilaya ya Arusha imekiri kuwepo kwa tukio, lakini chanzo chetu kikikataa kutajwa jina gazetini kwa kuwa si wasemaji wa matukio ya jeshi hilo mkoani Arusha.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TETESI ZA KUWEPO MGONJWA ANAYEHISIWA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII 

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TETESI ZA KUWEPO MGONJWA ANAYEHISIWA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA  MKOANI KILIMANJARO

 Utangulizi

Mnamo tarehe 22 Oktoba 2014, Wizara ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ya kuwepo kwa mgonjwa aliyehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola. Mgonjwa huyu mwanaume ana umri wa miaka 37, na mkazi wa Dar es salaam (Kimara ) ambaye alikwenda Kilimanjaro tarehe 20 Oktoba 2014 katika kijiji cha Kirua kwa ajili ya kusalimia ndugu. Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali ( 38.2 0c), maumivu ya Misuli, kuchoka na maumivu ya kichwa pamoja na maumivu ya koo na kupoteza hamu ya kula.
 
Mgonjwa huyu anatibiwa katika Kituo cha Afya Shirimatunda, Kilimanjaro kuanzia tarehe 22.10.2014 ambako yupo hapo hadi sasa. Mgonjwa huyu kikazi ni “Land Surveyor” na hufanya kazi zake nchini na nje ya nchi ikiwemo nchi ya Senegali. Mnamo siku za karibuni alikwenda nchini Senegali kwa kazi za mkataba na kurejea nchini mwanzoni wa Oktoba 2014. Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na historia ya kusafiri kwenda nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola yaani Liberia, Guinea au Sierra Leone.

    Hatua zinazochukuliwa hadi sasa;

     i.        Sampuli ya damu ya mgonjwa kwa ajili ya uchunguzi wa Kimaabara ilifanyiwa uchunguzi na kuonekana kuwa na malaria. Matokeo ya awali dhidi ya magonjwa ya jamii ya ebola yakiwa ni pamoja na Dengue na Chikungunya yanaonyesha kuwa mgonjwa hakuwa na magonjwa haya.
    ii.        Mgonjwa anaendelea kuhudumiwa katika kituo cha Afya cha Shirimatunda.
   iii.        Wanafamilia wa karibu pia wamechunguzwa na kuonekana kuwa hawana dalili za ugonjwa wa Ebola.

Mwongozo wa utambuzi wa ugonjwa huu (Standard Case Definition) unaeleza kwamba ili mgonjwa aweze kuhisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola anatakiwa akidhi vigezo vifuatavyo:
 
i.             Dalili za awali  ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya  misuli, kuumwa na kichwa, na kutokwa na vidonda kooni. Mara nyingi dalili hizi hufuatiwa na kutapika, kuharisha,kutokwa na vipele  vya ngozi, kwa baadhi ya wagonjwa hutokwa na damu ndani na nje ya mwili
ii.            Awe amesafiri kwenda sehemu zilizothibitishwa kuwa na ugonjwa wa ebola ndani ya kipindi cha wiki 3 na hizi zikiwemo Guinea, Sierra Leone na Liberia. Aidha Shirika la Afya Duniani (WHO) limeshatangaza kutokuwepo kwa ugonjwa huu nchini Senegali na Nigreia na hivyo kuzitoa nchi hizi kwenye nchi hatarishi.
iii.           Dalili nyingine ni Kugusa majimaji kutoka kwa mgonjwa, maiti au mnyama      anayehisiwa au kuthibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.

Hitimisho

Wizara inapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa hadi sasa HAKUNA MGONJWA yeyote aliyethibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola hapa nchini.  Mgonjwa huyu kutoka Kilimanjaro hana ugonjwa wa Ebola bali anatibiwa kama mgonjwa wa MALARIA.

Adiha Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu ila wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari za kuepuka kupata maambukizi ya ugonjwa huu ambazo:-
o   Kuepuka kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi  na majimaji mengine yanayotoka  mwilini mwa mtu mwenye dalili za ugonjwa  wa Ebola kupitia sehemu zenye michubuko au vidonda.
o    Kuepuka  kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa akiwa na dalili za ugonjwa wa Ebola; badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri. Wataalam watasimamia maziko ikiwa itatokea.
o   Wananchi waepuke mila na desturi  zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kusababisha kuzidi kueneza kwa ugonjwa wa Ebola.
o   Kutoa taarifa mapema kwa viongozi wa Serikali na watoa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye  dalili za ugonjwa wa Ebola.
o   Kuwahi katika vituo vya kutolea huduma za  Afya pale mtu anapohisiwa kuwa na dalili za  ugonjwa huu


Imetolewa na,
Dkt. Donan Mmbando

KAIMU KATIBU MKUU
24 Oktoba, 2014

CHANZO CHA MAJI IKORONGO MKOMBOZI WA MJI WA MPANDA

$
0
0
 Wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiangalia chanzo cha chemichemi ya maji cha Ikorongo kilichoko kilometa 13.2 kutoka Mpanda mjini. Chanzo hicho kina uwezo wa kutoa maji ya kutosha mji wote wa Mpanda.
 Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Magdalena Mkeremi (aliyejifunika mtandio) akifafanua jambo kwa timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi Rais, Tume ya Mipango walipotembelea chanzo hicho hivi karibuni
 Mhandisi Happiness Magalula, Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma (mwenye sweta la blue) akitaka ufafanuzi wa miundombinu ya kuwezesha maji kuwafikia wananchi kutoka katika chanzo hicho. Bomba la inchi kumi limetandazwa kutoka kwenye chanzo hicho mpaka mjini ambako kuna tanki kubwa la maji yanayosambazwa katika mji wa Mpanda na vitongoji vyake
 Tanki la maji lenye uwezo kujaza lita 1,000,000 linalosambaza maji katika mji wa Mpanda, mkoani Katavi
Moja ya bomba la maji katiak shule ya Sekondari ya Shanwa katika mji wa Mpanda ambao wanapata maji kutoka katika chanzo cha maji cha Ikorongo. Anayefungua bomba ni Festo Katanti, Mtalaam wa maji wa Halmashauri (Techenician) nyuma yake ni mwalim Mkuu wa Shule hiyo Emmanuel Nkumbo na kushoto kwa Katanti ni Mhandisi Happiness Mgalula, Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango.


Na Mwandishi wetu, Katavi
Chanzo cha maji cha chemichemi ya Ikorongo ambacho ni cha asili kipo kilometa 13.2 kutoka Mpanda mjini, mkoani Katavi. Chanzo hiki cha maji kinazungukwa na miti na uoto wa asili unaolinda maji hayo yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu.

Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Katavi Magdalena Mkeremi anasema chanzo hiki cha maji ni chemichemi yenye maji masafi yasiyokauka hata wakati wa kiangazi. Chanzo hiki kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita milioni sita kwa siku.Mradi wa maji wa Mji wa Mpanda ni wa gharama nafuu kwa sababu hautumii pampu ya aina yoyote bali maji husambazwa kwa njia ya mserereko (gravity).

Bomba kubwa la maji la inchi kumi limelazwa kutoka kwenye chanzo na kupelekwa Kazima kwenye tanki kubwa la ujazo wa lita milioni moja ambalo limejengwa eneo la kilometa 13 kutoka kwenye chanzo cha maji.  Vile vile  maji kutoka kwenye tanki hilo na kwenda mjini na katika mitaa au vijiji pia hutumia mserereko hivyo, kurahisisha gharama zake.

Mradi huo wa maji wa vijiji kumi au mitaa kumi ya mji wa Mpanda unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia chini ya mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa. “Maji yalikuwa tatizo kubwa hapa kwetu lakini ujio wa mradi huu umerahisisha upatikanaji wa maji mjini na kwenye mitaa ya mji wa Mpanda,” anasema Mhandisi.

Tayari vimejengwa vituo vya kuchotea maji 41 katika mitaa kumi na watu binafsi wapatao 300 wameunganishiwa maji kupitia chanzo hicho cha maji. Amesema mradi huo umetekelezwa kwa muda wa miaka mitatu tangu 2012/13 -2014/15 ambapo umekamilika mwezi Septemba 2014.Amesema ili kuufanya mradi huo kuwa endelevu wamejenga nyumba ya mlinzi ili kulinda chanzo hicho cha maji kisiharibiwe kwa namna yoyote ile ikiwa ni pamoja na kulinda mazingira yanayozunguka eneo hilo.

WAZIRI NYALANDU ARUHUSU WANANCHI WANOENDA KWENYE MATIBABU KITUO CHA AFRICA AMINI KUPITA BILA KULIPA HIFADHINI.

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akiwasili katika kituo cha Afya cha Africa Amini Alama kilichopo katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha(ANAPA)akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar.
Waziri Nyalandu akisalimiana na wagonjwa waliofika katika kituo hicho kwa ajili ya kupata matibabu,Pembeni yake ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar.
Mmoja wa wauguzi katika kituo hicho aliyefahamika kwa jina moja la Nice akitoa maelezo kwa Waziri Nyalandu,wengine ni Mbunge wa Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Pascal Shelutete. 
Waziri Nyalandu akizungumza na mmoja wa wagonjwa aliyekuwa katika kituo hicho ambaye alihitaji kiasi cha shilingi 5000 kwa ajili ya matibabu pesa ambazo alisaidiwa na Waziri Nyalandu .
Waziri Nyalandu akizungumza na mmoja ya watu waliofika katika kituo hicho kwa ajili  ya matibabu waliyefahamiana .
Waziri Nyalandu akisamia wagonjwa.
Waziri Nyandu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki  Joshua Nassar wakipata maelezo toka kwa mkurugenzi wa kituo cha Afya cha Africa Amini wakati alipotembelea kituo hicho kilichopo katika Hifadhi ya TAIFA YA aRUSHA.
Waziri Nyalandu akimsalimia mmoja wa wagonjwa waliokuwa wakipata matibabu katika chumba cha matibabu cha kituo hicho cha Afya cha Africa Amini.
Waziri Nyalandu akiteta jambo na mmoja wa wafanyakazi katika kituo hicho aliyefahamika kwa jina la Jamilah Mongi.
Mkurugenzi wa Kituo cha Africa Amini Cornellia Walner akitoa maelezo mbele ya Waziri Nyalandu,Mbunge Nassar na Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa(ANAPA) Betrita Loibook.
Waziri Nyalandu akitia saini katika kitabu cha Wageni.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akizungumza juu ya Adha wanayoapata wakazi wa Vijiji vya jirani na hifadhi ya Arusha ya kutakiwa kutoa tozo kwa ajili ya kupita katika barabaara ya hifadhi hiyo wakati wakielekea katika kituo hicho cha Afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Arusha(ANAPA) Betrita Loibook akizungumza juu ya tozo hiyo.
Waziri Nyalandu akitoa maamuzi ya serikali kuhusiana na hadha hiyo ambapo ameruhusu wananchi wanaoelekea katika kituo hicho kwa ajili ya kupata matibabu wapite bila ya kutozwa chochote.
Mkutano ukiendelea katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kaskazini.

JENGO LA NSSF KUBADILI TASWIRA YA MJI WA MOSHI.

$
0
0
Jengo jipya linalojengwa na Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii  (NSSF) kukamilika kwake kutabadili taswira ya mji wa Moshi kwa kiasi kikubwa.Ni jengo ambalo limejengwa kisasa  ambalo kukamilika kwake kutapendezesha mji wa Moshi. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

DKT BILAL AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA MAENDELEO RUFIJI

$
0
0
Jumla ya Shilingi Milioni 903 zimekusanywa katika harambee iliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa ajili ya kuchangia miradi ya maendeleo katika wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani.

Kati ya fedha hizo zilizokusanywa katika harambee hiyo iliyofanyika jana tarehe 26/10/2014 katika ukumbi wa Serena Jijini Dar es salaam, Shilingi Milioni 333 ni ahadi ya fedha na Shilingi Milioni 570 zilizobaki ni ahadi ya vifaa mbalimbali vikiwemo vitanda vya wagonjwa na vifaa vya maabara.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Bilal aliwakumbusha wananchi jinsi sera ya kujitegemea ilivyolipatia sifa Taifa la Tanzania hasa wakati wa Awamu ya Kwanza ya uongozi.

Alisema lengo la sera hiyo wakati huo lilikuwa kutoa wajibu kwa kila mwananchi na pia kuwafanya wananchi kama taifa kutambua maana halisi ya uhuru ambao wamekuwa wakiupigania na kuupata.

“Tanganyika na hata Zanzibar zote zilikuwa zikihitajika kwa wakati huo kwanza kuwafanya wananchi watambue uhuru uliambatana na wajibu na pia ilipaswa kwa wananchi kujua kuwa, kazi ya kujitawala yenyewe iliambatana na majukumu ya kujenga na kuendeleza nchi sisi wenyewe,” alidokeza Makamu wa Rais.

Dkt. Bilal alisema hata sasa hoja hizo hazijapitwa na wakati na kwamba wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii katika kujitafutia maendeleo na wajibu wa serikali unabaki kuwa katika kuweka miundo mbinu na mazingira ambayo yanawezesha wananchi kupata maendeleo kwa haraka.

Mapema, akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji, Dkt. Seif Rashid alisema lengo la harambee hiyo, ni kupata fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za afya, elimu na maji.

Katika harambee hiyo, Makamu wa Rais aliahidi kuchangia shilingi Milioni 10 kuunga mkono juhudi za wananchi wa wilaya ya Rufiji katika kujiletea maendeleo yao.
 
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
27/10/2014

MSANII LULU AITAMBULISHA FILAMU YAKE MPYA IITWAYO MAPENZI YA MUNGU LEO.FILAMU YAINGIA SOKONI LEO

$
0
0
 Msanii wa Sanaa ya Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Alipokuwa akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo amewashirikisha Flora Mtegoha au Mama Kanumba na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Linah Sanga.
 Msanii Wa Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU leo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).Kulia ni Mmoja kati wa wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ajulikanae kama Flora Mtegoha almaarufu kama Mama Kanumba.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Evance Stephen akiongea na wanahabari leo katika Ofisi za Proin Promotions Ltd zilizopo Mikocheni mtaa wa Ursino wakati wa Utambulisho wa Filamu mpya ya Lulu Iitwayo MAPENZI YA MUNGU.
Msanii Elizabeth Michael aka Lulu leo ametambulisha Filamu yake Mpya ambayo imeingia sokoni leo iitwayo MAPENZI YA MUNGU, huku akiwa amemshirikisha Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga na Mama Kanumba.
Wakati akiilezea filamu hiyo leo mbele ya wanahabari Lulu amesema Kuwa Ni Filamu inayofundisha na Kutoa somo kwa mtu yoyote yule ambae yupo hapa duniani kwa kuendelea kuonyesha kuwa MUNGU YUPO. 

Akiongezea kuwa..."Sisi kama binadamu tumekuwa tukifanya mambo mengi sana hapa Duniani na kupelekea kumsahau Mungu na pengine kuendelea kufikiria kuwa yote tuyafanyayo ni kwa uwezo wetu kumbe Sio uwezo wetu na Ni Mapenzi ya Mungu tu ndio yanayofanya sisi kufikia hapa tulipo leo"
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU imekuwa gumzo kabla ya kutoka kutokana na watanzania wengi kuwa na shauku ya Kutaka kumuona Lulu tena mara baada ya Kuonekana  katika Filamu Zake Mbili zilizotangulia za FOOLISH AGE na FAMILY CURSE. Sasa Lulu kuonekana tena katika kiwango cha Juu katika Filamu hii Mpya ambayo imeingia Sokoni Leo.
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU ni filamu inayosambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.

UFUNGUZI WA MAFUNZO YA JOTOARDHI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela akiongea jambo wakati akifungua rasmi mafunzo  ya siku mbili kuhusu masuala ya jotoardhi  kwa washirki kutoka nchi zilizo katika bonde la Ufa . Mafunzo hayo yanatangulia kabla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi litakalofunguliwa tarehe 29 Oktoba, 2014 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
Baadhi ya washiriki wanaohudhuria mafunzo kuhusu masuala la jotoardhi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela hayupo pichani wakati akifungua rasmi mafunzo hayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela (katikati) akiongea jambo na Kamishna Msaidizi anayeshughulia Nishati Jadidifu , Wizara ya Nishati na Madini, Edward Ishengoma (kushoto) mara baada ya kufungua mafunzo kuhusu masuala yanayohusu jotoardhi.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya masuala ya jotoardhi kutoka nchi zilizo katika bonde kla ufa na nyi nyingine duniani, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela (wan ne kulia).

NECTA yafanikiwa kudhibiti udanganyifu na wizi wa mitihani ya taifa nchini.

$
0
0
 Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) bw. Daniel Mafie akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Baraza hilo ikiwemo matumizi ya TEHAMA katika usajili wa watahimiwa na uchakataji wa matokeo ya Mitihani ya Taifa. Kulia ni Afisa Habari wa NECTA John Nchimbi.
 Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Bw. Daniel Mafie akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar s salaam kuhusu utaratibu wa kutoa nakala za vyeti kwa watahimiwa waliopoteza vyeti vyao ambapo utaratibu huo unahusisha uchunguzi wa uhalali wa mwombaji.  Kulia ni Afisa Habari wa NECTA John Nchimbi na kushoto ni Msaidizi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Bi Glee Magemba.
.Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) na Vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga  kuonyesha mafanikio ya Baraza hilo nchini.(Picha na Frank Mvungi-MAELEZO).
 
Frank- Mvungi - MAELEZO
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limedhibiti na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa Mitihani ya Taifa na udanganyifu wakati wa Mitihani katika ngazi mbalimbali za elimu nchini.

Mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo kati ya NECTA na kamati za uendeshaji mitihani katika ngazi za mikoa na wilaya ili kutatua tatizo la wizi wa mitihani ya taifa na udanganyifu wakati wa mitihani uliokuwa ukifanywa kinyume na taratibu za baraza la mitihani.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza hilo Bw. Daniel Mafie wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jjijini Dar es salaam uliolenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa.

Akifafanunua Mafie amesema kuwa katika mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 13 tu ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliobainika kufanya udanganyifu mwaka 2011.

Aidha Mafie aliongeza kuwa katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 272 ikilinganishwa na watahimiwa 789 mwaka 2012 na 3,303 mwaka 2011.

Akieleza zaidi kuhusu mafanikio yaliyofikiwa Mafie alisema Baraza hilo limeweza kusanifu mifumo ya Kompyuta yenye uwezo wa kupanga shule katika makundi ya ubora wa ufaulu katika matokeo ya mitihani ya Taifa.

Katika kukabiliana na tatizo la watu wanaotumia vyeti vya watu wengine au kughushi vyeti wakati wa kuomba ajira au nafasi za masomo katika shule mbalimbali ambapo kuanzia mwaka 2008/2009 Baraza hilo lilianzisha utaratibu wa kuweka picha za watahimiwa katika vyeti vyao.

Katika utaratibu huo vyeti hivyo viliwekewa alama za kiusalam hali ambayo imesaidia Baraza hilo kuwa na uwezo wa kubaini kwa haraka na kuwachukulia hatua wale wanaoghushi vyeti au kutumia vyeti vya watu wengine.

Baraza la Mitihani la Tanzania ni Taasisi ya Umma iliyochini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyoanzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 21 ya mwaka 1973 na marekebisho yake ya mwaka 1998 na 2002 kwa ajili  ya kuendesha mitihani ya Taifa kwa lengo la kuweka misingi ya sera ya mitihani, kuendesha mitihani na kutunuku stashahada mbalimbali na vyeti kwa watahiniwa wanaofuzu na kufaulu mitihani iliyo chini yake kisheria.

UFAFANUZI KUHUSU UHABA WA DAWA MUHIMU NA VIFAA TIBA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMI.
Kuna taarifa katika vyombo vya habarii liyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la SIKIKA ,kwamba serikali haijalipa kiasi cha shilingi bilioni 90 kwa bohari  kuu ya dawa  na kusababishia ukosefu  dawa katika baadhi ya hospitali.

Ni kweli bohari kuu ya dawa imepungukiwa fedha za kununulia dawa , lakini sio kwa kiasi cha kushindwa kutoa huduma kabisa  kama inavyoelezwa.  Kiasi cha pesa kinachotajwa  si kigeni na serikali imekua ikitoa kiasi cha fedha kidogo kidogo ili kuongeza uwezo wa bohari  ya dawa iweze kufanya kazi ya kununua na kusambaza dawa.

Katika kukabiliana  na hali hii hospitali zote kupitia waganga wakuu wa mikoa na wilaya zimeagizwa kupeleka asilimia  50 ya mapato yanayotokana na uchangiaji kwenda bohari kuu ya dawa.

Kuhusu ukosefu wa matibabu katika Taasisi ya Saratani ocean road,  ni kweli kwa sasa baadhi ya mashine hazifanyi kazi na zinazofanya kazi ni chache hivyo kuzidiwa  wakati fulani.Hatahivyo wizara imekwisha agiza vifaa hivyo ambavyo ni ghali sana toka Canada na vinategemewa kufika wakati wowote kuanzia sasa na pia ikumbukwe kuwa matibabu yanatotolewa  bila malipo na gharama zote  ni za serikali.

Wizara kwa sasa imeagizwa katika mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN)ambapo wataalam wanamalizia kazi za utekelezaji wa mpango huo. Ambapo pia umezingatia namna ya kukabiliana  na jinsi ya kuhakikisha


dawa zinapatikana kwa wakati katika vituo vya matibabu  na kuiboresha zaidi bohari ya dawa. Baada ya kuanza utekelezaji huo suala la ukosefu wa dawa  na vifaa tiba utapungua  kwa kiasi kikubwa  sana.

Pamoja na wizara kupeleka bohari tyadawa pesa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, hospitali zihakikishe zinapeleka asilimia 50 ya mapato kama zilivyoagizwa na kutokufanya hivyo kiongozi husika atawajibishwa.

Mwisho wizara inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba dawa na vifaa tiba muhimu vinapelekwa katika vituo vyote , pia inaendelea kufanya kazi na taasisi zote zisizo za kiserikali kwa karibu kwa faida ya wananchi wote.

Imetolewa na :-


Dkt. Seif S. rashidi (Mb)
WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII
27/10/2014

PICHA ZA WAZIRI MKUU PINDA NCHINI POLAND NA WAWEKEZAJI

$
0
0
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiandika maelezo muhimu wakati akimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Katanja-Neoval Oil, Bw. NICODEMO SWIACKI (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu kampuni yao ambayo inataka kuwekeza Tanzania kwenye kiwanda cha kusafisha dhahabu (gold refinery) na ujenzi wa hoteli ya kimataifa huko Zanzibar. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Mwigulu Nchemba.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Katanja-Neoval Oil, Bw. NICODEMO SWIACKI (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu kampuni yao ambayo inataka kuwekeza Tanzania kwenye kiwanda cha kusafisha dhahabu na ujenzi wa hoteli ya kimataifa huko Zanzibar. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Mwigulu Nchemba.

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akibadilusha mawazo na viongozi wa kampuni ya Katanja-Neoval Oil baada ya kusikiliza mada yao. Wa pili kulia ni Rais wa Kampuni hiyo, Bw. KRZYSZTOF SWIACKI. (Picha na Irene Bwire wa OWM).

MRATIBU MKAZI WA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR LEO

$
0
0
IMG_3633
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyefika Ikulu ya Zanzibar leo kwa ajili ya mazungumzo.
IMG_3641
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipomtembelea kwenye Ikulu ya Zanzibar leo.
IMG_3646
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiendelea na mazungumzo Mratibu mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Mratibu mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini ofisi ya Zanzibar, Anna Senga (kushoto).

RAIS KIKWETE AWASILI VIETNAM KWA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa Mjini Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Ndugu Nguyen Phu Trong, katika Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho tawala cha nchi hiyo Jumatatu Oktoba 27, 2014.PICHA NA IKULU.

JESHI LA POLISI NJOMBE LAWAFUKUZA KAZI ASKARI WAKE WATATU

$
0
0
http://1.bp.blogspot.com/-boKz-oQYUlg/UY1v9VPfmoI/AAAAAAAAHOA/qszpJxfl5iE/s640/RPC+NJOMBE.JPGJeshi la polisi mkoani Njombe limeamua kuchukua uamuzi mgumu wa kuwafukuza kazi askari polisi wake watatu kwa makosa mbalimbali waliyoyafanya ikiwemo vitendo vibaya kinyume na sheria za jeshi hilo

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa mtandao huu na kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani (pichani) askari hao waliofukuzwa kazi ni EX.G. 3172 PC Ramadhani Iddi Saidi, EX.G. 9693 PC Emmanuel Morson Lyimo pamoja na EX.G. PC Miraji Jumanne Mtea

Kamanda Ngonyani amesema Jeshi la polisi limeamua kutoa adhabu hiyo kali kutokana na vitendo mbalimbali vya utovu wa nidhamu walivyovifanya ikiwemo tukio la hivi karibuni la kupigana hadharani Septemba 2 mwaka huu Mjini Njombe

Amesema wanategemea adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa askari wengine wenye tabia kama hiyo kwani jeshi halitawavumilia askari wake ambao wanakwenda kinyume cha sheria

Katika hatua nyingine Kamanda Ngonyani amewataka wananchi kuwa makini na askari hao waliofukuzwa kazi huku akisisitiza wananchi kutambua kuwa askari hao si watumishi tena kuanzia Oktoba 24, mwaka huu

Na Edwin Moshi

WAZIRI MKUU PINDA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO POLAND

$
0
0
 Baadhi ya Watanzania waishio Poland wakimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani) wakati alipokutana nao mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Sheraton jijini Warsaw, Poland. Waziri Mkuu alikuwa nchini humo kwa ziara ya siku tatu.
  Mmoja wa Watanzania waishio Poland wakiagana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kukutana nao mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Sheraton jijini Warsaw, Poland. Waziri Mkuu alikuwa nchini humo kwa ziara ya siku tatu. (Picha na Irene Bwire wa OWM).
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiagana na Mwenyekiti wa Watanzania waishio Poland (WAPO), Bw. Steven Sambali mara bada ya kukutana nao na kuwaeleza mambo yanayoendelea nyumbani Tanzania. Waziri Mkuu alikuwa nchini humo kwa ziara ya siku tatu.

VOA YAZINDUA MATANGAZO YA ALASIRI VOA EXPRESS.

$
0
0
IMG_5776utoka kushoto waliosimama ni Producer Dwayne Collins, Engineer Zaynab, Sunday Shomari na Harrison Kamau na waliokaa kutoka kushoto ni Idd Ligongo, Esther Githui Ewart, Mary Mgawe na mkuu wa idhaa ya Kiswahili Mwamoyo Hamza. IMG_5781 Timu ya VOA EXPRESS iliyofungua matangazo ya kwanza ya Alasiri saa za Afrika Mashariki saa 10.30 Jumatatu hadi Ijumaa Oktoba 27,2014. Kutoka kushoto Mary Mgawe, Idd Ligongo ,Sunday Shomari, Esther Githui Ewart, Khadija Riyami, Dwayne Collins, Mkuu wa idhaa Mwamoyo Hamza na Harrison Kamau.

MAHAFALI YA PILI YA SHULE YA WAMA NAKAYAMA YAFANA NYAMISATI RUFIJI

$
0
0
001
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro (katikati ), akikata utepe akizindua zahanati kwa ajili ya matibabu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakati mahafali ya pili yaliyofanyika Octoba 27,2014 (kulia), Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, na kushoto ni Kaimu Balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsu.
002
Wangeni waalikwa wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuunza kwa hafla hiyo.
003
004
Wageni wakiwa kwenye hafla hiyo.
005
Kutoka kushoto Kaimu Balozi wa Japan nchini, Kazuyoshi Matsu, WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Wama Nakayama Dr. Ramadhan Dau, Naibu waziri wa Tamisemi.Kassim Majaliwa wakiimba wimbo wa Taifa uliondaliwa na wanafunzi wa shule ya WAMA Nakayama kabla ya kaanza hafla hiyo.
006
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto), akimtambulisha Mkuu wa kwanza wa Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama, Mama Hawa Mabrouk. iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakati mahafali ya pili yaliyofanyika Octoba 27,2014.

007
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya pili yaliyofanyika Oktoba 26,2014.
008
Bendi ya Mjomba Band Mrisho Mpoto ikitoa burudani wakatiti wa hafla hiyo.
009
Baadhi ya wahitimu wa elimu ya sekondari ya kidato cha nne kutoka katika Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani wakifurahia na jambo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe za mahafali ya pili yaliyofanyika Oktoba 26,2014.
0010
Baadhi ya wahitimu wa elimu ya sekondari ya kidato cha nne kutoka katika Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira magumu ya WAMA Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, wilayani Rufiji mkoani Pwani.wakiwa wamejipanga tayari kuelekea seemu maalumu iliondaliwa kwaajili ya kuagwa.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).

JHIKOMAN, ZAWOSE, MAEMBE KUPAMBA ‘KARIBU FESTIVAL’

$
0
0
Px 1
Msemaji wa tamasha la Karibu Music Festival, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo. ..Wapo pia Prof. Jay, Barnaba, Shilole

Na Andrew Chale
WASANII kutoka ndani na nje wanatarajiwa kupamba tamasha la Muziki la Kimataifa la ‘Karibu Music Festival’ litakalofanyika kwa siku tatu kwenye mji wa Kihistoria wa Bagamoyo, Novemba 7 hadi 9 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mapema Oktoba 27, Msemaji wa tamasha hilo Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ alisema maandalizi yamekamilika na tayari wasanii wa awali waliopatikana wapo hadharani wanaendelea na matayarisho huku akiwaomba watanzania na wadau wa burudani kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo.

Jazzphaa aliwataka baadhi ya wasanii wa nje na ndani na nchi zao katika mabano ni Panda (Japan), Maria Kate (Ufaransa), IFE Pianki (Uganda), Masayo (Japan), Fantuzz (Marekani), Shiwe Musique (Comoro), Dwembede (Kenya) na Mbiye Ebrima (Guinea).
px2
Mwanamuziki wa Msafiri Zawose anayepiga nyimbo za Cigogo, akionjesha vionjo vya moja ya nyimnbo zake kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho kwa wanahabari.

Makundi na majina ya wasanii kutoka nyumbani ni pamoja na Afrikabisa Band, Wahapahapa, Segere Original, Jahazi, The Spirit Band na Mama Africa. Wengine ni Cocodo Band, Hokororo Band, Swanu Gogo Vibes, Swahili Vibes, Fimbo Band, Abeneko Music, Man Kifimbo, Saganda na Msafiri Zawose.

Wasanii wengine ni Msafiri Zawose ‘Chibite Zawose’, Tongwa Ensemble, Leo Manyika, Swahili Blues, Profesa Jay, Shilole, Juma Nature, Barnaba, Vitalis Maembe na Jhikoman. Aidha, Jazzphaa aliongeza kuwa lengo la tamasha hilo ni kukuza na kurasimisha tasnia ya muziki kwa umakini zaidi na kukuza uchumi wa eneo la Bagamoyo ambalo ni la kihistoria.
px 3
Mmoja wa viongozi wa kundi la muziki wa Pwani ‘taarab’ kutoka kundi la Jahazi, akiongea machache.

Kwa upande wa viingilio, alisema kitakuwa ni sh 5,000 kwa kila Mtanzania huku kwa atakayekata tiketi ya siku tatu, kwa pamoja, ni sh. 12,000. “Tamasha hili litakuwa likifanyika usiku na mchana. Wasanii wote watakaokuwepo katika tamasha hili watalazimika kupiga muziki kwa kutumia ala za asili za muziki ‘Live’ na siyo ‘Playback’” alisisitiza Jazzphaa.

Kwa upande wake, Meneja wa tamasha hilo, Richard Lupia alisema tamasha hilo mbali ya burudani, wasanii pia watapata nafasi ya kujifunza jinsi ya kuunadi muziki wao duniani kwa njia mbali mbali ambako kutakuwa na warsha kutoka kwa wataalamu toka pembe zote za dunia. Pia alisema katika tamasha hilo kutakuwa na sanaa za Michoro, mavazi na kuchonga zitakuwa zikioneshwa eneo la tamasha.

“Semina na mijadala ya jinsi ya kuupeleka muziki wa Tanzania katika hatua nyingine za kimaendeleo zitatolewa kwa wasanii mbalimbali. Mbinu za kuuza kazi zao kwenye masoko ya kimataifa na kutafuta soko duniano kote hii itakuwa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa hapa hapa nchini” alisema Lupia.
px 4
Msanii nguli wa reggae, Jiko Manyika ‘Jhikoman’ akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo.
crew ya Karibu Festival na baadhi ya wasanii
Crew ya Karibu Festival na baadhi ya wasanii.

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YANDAA MAFUNZO YA SIKU TANO KWA BOTI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR.

$
0
0
 Mrajisi wa Bodi ya Chakula,Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othaman Simai akizindua Mafunzo ya siku tano ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi ambayo yanalenga kuanzisha Chombo maalum cha pamoja cha Usajili wa Dawa katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.
 Mratibu wa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Patrick Mwesigye kutoka nchini Rwanda akitoa nasaha zake kwa Watendaji hao katika Uzinduzi wa Mafunzo hayo huko Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View.
 Mkuu wa Kitengo cha Dawa na Vipodozi Zanzibar Bora Lichanda akifafanua Jinsi Kitengo chao kinavyofanya kazi kwenye Mafunzo ya siku tano ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi ambayo yanalenga kuanzisha Chombo maalum cha pamoja cha Usajili wa Dawa katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.
  Mkuu wa Bodi ya Madawa na sumu Nchini Kenya Dkt. Ronald M. Inyangala akichangia kitu katika mafunzo hayo.
 Mratibu wa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi kutoka Zanzibar Hidaya Juma Hamad akizungumza na Wanahabari nje ya Ukumbi wa Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View ambapo mafunzo hayo ya siku tano yanafanyika.

 Mgeni rasmi Mrajisi wa Bodi ya Chakula,Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othaman Simai (kati kati) waliokaa akiwa katika Picha ya pamoja ya Washiriki wa Mafunzo ya siku tano ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi ambayo yanalenga kuanzisha Chombo maalum cha pamoja cha Usajili wa Dawa katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki. (Picha na Makame Mshenga- Maelezo-Zanzibar).



Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar.

Jumuiya ya Afrika Mashariki imeandaa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula,Dawa na Vipodozi Zanzibar  ikiwa ni Mkakati wa kuunda Chombo maalum cha pamoja cha usimamizi na usajili wa Dawa utakaofanywa katika nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

Mafunzo hayo ya siku tano yanalengo la kuweka Msimamo wa Pamoja na Viwango sawa kwa Bodi za Vyakula na Dawa ili Dawa itakaposajiliwa katika nchi moja ikubalike kimatumizi katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Mafunzo hayo katika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View Mrajisi wa Bodi ya Chakula,Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhan Othaman Simai amesema kuwepo kwa Chombo cha Usimamizi wa Pamoja katika Nchi hizo kutasaidia kuondokana  na Tatizo la Uingizwaji wa Dawa zisizofaa Kimatumizi katika nchi hizo.

Amesema Chombo hicho kitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo hilo kwa vile kutakuwa na Mikakati ya kupeana taarifa za karibu kuhusu Dawa zinazosajiliwa na kusambazwa katika nchi zao.

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo Patrick Mwesigye kutoka nchini Rwanda amesema Malengo ya Jumuiya hiyo ni kuhakikisha Vitengo vyote vya Nchi Wanachama vinajengewa uwezo na Ufanisi ili viwe katika Ubora unaofanana.

Amesema kwa sasa kila nchi inatathmini na kusajili Dawa kivyake na kwamba kukamilika kwa Mafunzo hayo itakuwa ni hatua kubwa ya kufikia Makubalianao ya kuanzishwa kwa Chombo kimoja cha Usajili wa Dawa katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.

Akizungumza pembeni ya Mkutano huo Mratibu mwenza kutoa Zanzibar  Hidaya Juma Hamad amesema kukamilika kwa Chombo hicho kutasaidia sana upatikanaji wa Dawa salama katika nchi husika. Amesema sambamba na hilo kutasaidia kupunguza gharama na matumizi mengi ya rasilimali ambayo yangetumika katika nchi zingine.

“Dawa Moja kuisajili inaweza kuchukua miaka miwili kwa hiyo Dawa hiyo itakaposajiliwa katika nchi moja itakuwa na uhalali wa kutumika katika nchi nyingine bila kusajiliwa tena, na hapo gharama kubwa zitakuwa zimeepukwa” Alisema Hidaya.

Pamoja na Zanzibar kupewa mafunzo hayo bado inakabiliwa na Changamoto nyingi zinazokwaza ufanisi wao ikiwemo uhaba wa Fedha, Ofisi ndogo na Idadi ndogo ya Wataalamu na Watendaji wa kukagua Maduka ya Dawa, Vyakula na upekuzi bandarini.

TANZANIA YAKATAA RASMI NDOA ZA JINSIA MOJA KWENYE AGENDA ZA MAENDELEO YA MILENIA

$
0
0
001
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Wanawake, Anna Collins akitoa hotuba yake wakati akifungua warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.iliofanyika Makao Makuu ya Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Oktoba 27, 2014 jijini Dar es Salaam.

SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa. Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.

“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy.

Amesema kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si agenda ya maendeleo.

002
Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini zinazoendelea.

Balozi Mushy aliongeza kwamba serikali ya Tanzania imeweka msimamo huo zaidi hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete aliagiza hivyo kwa maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Waziri husika kukataa shinikizo la kukubali swala ushoga kama agenda za maendeleo. Amesema kwamba watanzania wanataka maswala yanayowagusa kama vile maji, elimu, huduma bora za afya, miundombinu ya umeme, ajira, umaskini na kuondoa umaskini wa kipato.

Balozi Mushy alifafanua zaidi kwamba mambo ya ushoga na ndoa za jinsia yanakwenda kinyume na maadili ya watanzania, maisha, historia, utamaduni, mila na desturi za mtanzania sinakataza maswala ya ushoga. Amesema kwamba serikali inatambua kwamba sheria ya mwenendo wa makosa ya kujamiiana yaliwekwa na mkoloni mwingereza kabla ya uhuru na serikali ya Tanganyika imerithi kutoka kwenye serikali ya mwingereza.
003
Mkurugenzi wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza kwenye warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.

“Watanzania na Afrika kwa ujumla inataka malengo ya millennia na haki za binadamu zizifike mahali kuwadharirisha watu kutoka bara hili kwa kuruhusu mambo yanayokwenda kinyume na historia yao, mila na desturi za mwafrika,”aliongeza.
Kwa upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano amesema kwamba malengo ya milenia kwa kiasi kikubwa yamefikiwa na Tanzania hasa katika upande wa elimu na kupunguza vifo vya wakinamama na watoto wakati wa kujifungua.
“leo tumekutana hapa kuzungumza ni kwa kiasi ngani nchi yetu ya Tanzania imefikia malengo ya milenia na changamoto ni zipi katika malengo mapya ambayo ni 17 badala ya 8 ya awali,” aliongeza
Dkt Mashindano alifafanua kwamba ni lazima sasa serikali kutazama katika Nyanja za ubora katika huduma hizi muhimu kwa jamii baada ya kufikia lengo la kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule kwa asilimia 85.
004
Mhadhiri wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano akifafanua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu maswala ya malengo ya milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.
Aliongeza kwamba Tanzania na dunia kwa ujumla wameona ni muhimu kuweka agenda ya ubora katika kila agenda za malengo ya milenia kwa nchi zote ambao ni wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Dkt Tausi Kida, Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii, amesema kwamba malengo haya ya milenia ni lazima yaguse maisha ya watu katika ngazi ya chini ili matokeo chanya yaweze kuonekana kwenye jamii
Amesema kwamba ni lazima nchi zilizoendelea ziweke mkazo katika kuhakikisha kwamba nchini zinazoendelea zinajengewa uwezo wa kutafuta fedha za kutimiza malengo ya milenia.
005
Mdau akichangia mada yake.
006
Wadau wakifurahia jambo wakati ya warsha hiyo.
007
Wadau mbalimbali walioudhuria wakifuatilia mada mbalimbali.
008
009
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images