Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MKUTANO WA KUANDAA RAMANI YA MJI WA ZANZIBAR.

$
0
0
Mkurugenzi  Mipango Miji na vijiji Muhammad Juma akitoa maelezo kwa washiriki wa mkutano wa kuandaa ramani ya Mji wa Zanzibar uliofanyika Hoteli ya Marumaru, Shangani.
Mkurugenzi  Mipango Miji na vijiji Muhammad Juma akionyesha mipaka na maeneo ambayo mji wa Zanzibar  unavyotarajiwa hapo baadae baada ya kukamilika ramani hiyo.
Mshauri mwelekezi kutoka kampuni ya Shapira Hellerman ya Israel,   Jos Hellerman akitoa taarifa  ya ramani ya Mji wa Zanzibar katika mkutano uliozungumzia mpango wa kuandaa matumizi bora ya ardhi katika Hoteli ya Marumaru, Shangani Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa Mjini Mgharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis ambae alikuwa Mwenyekiti wa mkutano wa Mpango  wa kuandaa ramani ya mji wa Zanzibar akizungumza na washiriki wa mkutano huo.
Mrajisi wa Ardhi Zanzibar Bi. Mwanamkaa Abdalrahman akizungumza na washiriki wa mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Marumaru, Shangani.
Baadhi ya washiriki wa mkutano uliojadili mpango wa kuandaa ramani ya Mji wa Zanzibar wakifuatilia maelezo yaliyotolewa kwenye mkutano huo katika Hoteli ya Marumaru. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

TAARIFA YA MSIBA WA DKT KANSOLE NTEVI

$
0
0
IMG-20141025-WA0035
Mpendwa wetu Dr Kansolele Ntevi amefariki dunia tarehe 22/10/2014 Mazishi yanatarajiwa kufanyika jumatatu Tarehe 27/10 / 2014 katika makaburi ya Kinondoni. 

Kutakuwa na ibada ya kuuaga mwili wa mpendwa wetu marehemu Dr. Kansolele Ntevi nyumbani kwake maeneo ya Kunduchi baada ya chuo cha jeshi njiapanda ya Madini,barabara ya vumbi nyumba ya tatu. Kwa mawasiliano na familia piga namba 0767004908 au 0717017820
Pole saana Da Dorothy wa Dorcas catering sisi tulimpenda mungu kampenda zaidi

Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi duniani yafanyika leo jijini Dar es salaam.

$
0
0
 Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma(Kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub(mwenye T-shirt nyeupe) na Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani leo Jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akimlisha keki Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani leo Jijini Dar es salaam.
 Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akimlisha keki mmoja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa  katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani leo Jijini Dar es salaam.
 Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akiteta jambo na moja ya mtoto mwenye tatizo la kichwa kikubwa anayepata huduma Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI).

 Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.

CHUO CHA TAALUMA ZA SAYANSI ZA AFYA ZANZIBAR CHAFANYA MAHAFALI YA 21,WAHITIMU 280 WATUNUKIWA STASHAHADA.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Taaluma za Afya Zanzibar Dkt. Abdalla Ismail Kanduru akitoa tamko la kuwatunuku stashahada wahitimu wa Chuo hicho katika Mahafali ya 21 yalifanyika Mbweni.
 Wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Afya  Zanzibar wakila kiapo cha utiifu mbele ya mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi katika mahafali ya 21 yaliyofanyika chuoni Mbweni.
 Wahitimu wa fani mbali mbali wa Chuo hicho wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) baada ya kuwatunuku stashahada katika mahafali ya 21.
 Wageni waalikwa walioshiriki mahafali ya 21 ya Chuo cha Taaluma za Afya Zanzibar wakifuatilia maadhimisho  hayo yaliyofanyika Chuoni, Mbweni.
 Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimtunuku  zawadi Leila Ali kwa kuwa miongoni mwa wanafunzi  waliofanya vizuri zaidi katika mahafali ya Chuo cha Taaluma za Afya Mbweni Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar katika Mahafali ya 21 yaliyofanyika Chuoni Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Wa kwanza (kulia) ni Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na wa kwanza (kushoto) Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho Dkt. Abdalla Ismail Kanduru. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira wakagua viwanda

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mhe. Dkt injinia Binilith Satano Mahenge (kulia) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mhe. Abdulkarim Hassan Shaha (wapili kulia),Pamoja na  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira wakikaguwa Mazingira katika moja ya kiwanda cha Mifuko ya Plastiki (East African Industy)kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt injinia Binilith Satano Mahenge (wa nne kulia),Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mhe. James Lembeli Mb (wa tano ulia), pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira wakikaguwa mifuko Inayozalishwa na kiwanda cha BinFijaa kilichopo barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt injinia Binilith Satano Mahenge (kushoto),akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mhe. James Lembeli (Mb),baada ya kuwasili kiwanda  kinachozalisha mifuko ya plastiki cha Binfijaa kilichopo barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam.


WAZALISHAJI MATREKTA WACHANGAMKIA FURSA TANZANIA

$
0
0
 KAMPUNI ya URSUS ya kutengeneza matrekta ya kutoka Poland imeonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania na iko tayari kushirikiana na kampuni ya SUMA JKT kutengeneza matrekta hayo.

Hayo yamesemwa na Rais wa Bodi ya URSUS, Bw. KAROL ZARAJCZYK wakati akitoa maelezo ya kampuni yake mwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokutana na wafanyabiashara wenye nia ya kuwekeza Tanzania jana asubuhi (Jumapili,Oktoba 26, 2014) kwenye hoteli ya Sheraton jijini Warsaw, Poland.

Bw. ZARAJCZYK alisema wanataka kujenga kiwanda hicho nchini Tanzania kwa kutambua nafasi ya kijiografia ya mahali nchi ilipo kuwa ni fursa ya kufungua milango kwa nchi jirani za Afrika Mashariki na Kati.

“Barani Afrika tulianza kupeleka matrekta Ethiopia, Ghana na Guinea. Sasa hivi tumeamua kuja Tanzania na Zambia. Nia yetu siyo kujenga tu kiwanda bali pia kutoa huduma kwa wakulima juu ya uendeshaji na utunzaji wa hayo matrekta,” alisema.

Alisema wako tayari kutoa mafunzo kwa vijana wa Kitanzania kama vile chuo fulani ili waweze kuunganisha matrekta hayo hapa nchini na waweze kuyafanyia ukaranati na kutengeneza vipuri vyake pindi ukitokea ulazima wa kufanya hivyo.

“Tunapenda kujenga kiwanda mahali ambapo itakuwa rahisi kupata vijana wa kuajiriwa au vijana wa kutoka chuoni ili iwe rahisi kuwafundisha pia teknolojia tunayoitumia kutengeneza matreka hayo,” aliongeza.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu alisema atawasilisha maelezo yao kwa Waziri anayehusika na sekta hiyo ili mawasiliano rasmi yafanyike.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, OKTOBA 26, 2014.

POLAND WATAKA KITUO CHA BIASHARA

$
0
0
 WAFANYABIASHARA wa Poland wameiomba Serikali ya Tanzania kuangalia uwezekano wa kufungua kituo cha biashara katika bara la Ulaya.

Wametoa ombi hilo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kikao kilichowashirikisha wafanyabiashara wakubwa 30 na wamiliki wa makampuni 20 wa hapa Poland kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Poland (Polish Chamber of Commerce) jijini Warsaw.

Walisema kuwepo kwa kituo hicho barani Ulaya kutawasadia wao kupata taarifa kuhusu Tanzania kwa urahisi zaidi kuliko ilivyo hivi sasa ambao wanalazimika kwenda London, Uingereza.

Akijibu maombi yao, Waziri Mkuu alisema ombi lao ni la msingi na atawasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe kuona ni nchi gani kituo hicho kinaweza kuwekwa.

Kwa upande wake, Kaimu wa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Bw. Christopher Mvula ambaye alimwakilisha Balozi Philip Marmo, alisema ili kituo hicho kiweze kuanza kazi, ni lazima pawe na jengo la ofisi za ubalozi, ofisi za kituo cha biashara na watumishi mahsusi. Balozi wa Ujerumani ndiye anayeiwakilisha Tanzania nchini Poland.

“Lazima kuwe na watumishi wa kituo lakini vilevile kuwe na Afisa Biashara, Afisa Utalii na Afisa Uhamiaji ili kuharakisha baadhi ya mambo. Siyo kila afisa wa ubalozi anaweza kuendesha kituo cha biashara,” alisema.

Alisema zitahitajika pia fedha za kulipia matangazo kwenye vyombo vya habari vya nchi husika pamoja na vipeperushi na taarifa nyingine za kuitangaza nchi kupitia kituo hicho.

Waziri Mkuu alimaliza ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi alikutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kukutana na baadhi ya wafanyabiashara wa jiji la Warsaw.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, OKTOBA 26, 2014.

Serikali yapiga marufuku ukataji wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake

$
0
0

unnamedWaziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akimsalimia mmoja wa wagonjwa waliofuata huduma katika zahanati ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru ,juzi  alipoitembelea baada ya Mbunge wa jimbo hilo kumlalamikia kuhusu tozo ya ushuru wa magari na wagonjwa wanaopita katik Hifadhi ya Taifa ta Arusha ili kupata huduma katika hospitali hiyo. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini.unnamed1Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akimtaarifu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu juu ya adha wanayopata wananchi wa jimbo klake wakati wakiiingia katika Zahanati ya tiba za Asili cha Ngarenanyuki mkoani Arusha juzi , kutokana  na tozo la pesa kupitia hifadhi ya Taifa ya Arusha. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini.unnamed2Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwa na Mbunge wa Siha ambaye ni Naibu waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri wakikagua kitalu cha miti katika shamba la mitiulioko wilayani humo juzi. Waziri Nyalandu aliruhusu nguzo nza umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kupata umeme n akuondoa mgogoro uliozuia mradi huo kwa muda mrefu.
unnamed3Naibu waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri akiwa na wataalamu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wakikagua msitu wa Siha mkoani Kilimanjaoro alipotembelea juzi . Waziri Nyalandu aliruhusu nguzo nza umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kupata umeme.
……………………………………………………………..
Serikali imepiga marufuku ukataji wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake anatakiwa kuomba kibali kwajili ya kukata mti huo.
Akizungumza wilayani Siha juzi ,Waziri wa Maliasili na Utalii , Lazaro Nyalandu amesema kwamba Tanzania inawez a kuwa jangwa baada ya miaka 15 kutokana na uvunaji mbaya wa bidhaa za miti unaofanyika nchini .
“Tukiendelea kukata miti kma hivi tutakuwa tunatengeneza janga la kitaifa kwa hiyo kwa sasa naomba niseme rasmi kuwa hakuna mtu anaruhusiwa kukata miti au mti hata kama ameupanda nyumbani kwake, ni lazima aombe kibali kwa maafisa wa misitu. Tunatakiwa kushiriki kwa pamoja katika kutunza mazingira yetu” alisema.
Nyalandu alisema kasi ya ukataji miti nchini imekuwa kuubwa kwa sasa kutokana na kuongezeka kw aidadi ya watu na kuwa kwa mwaka mmoja pekee hekta 350,000 hukatwa huku kikiwa hakuna jitihada za kurejesha iliyoondolewa.

“Kwa kaddri siku zinavyozidi kwenda na watu kuongezeka baada ya miaka kumi misitu itakuwa inavunwa kw azaidi ya hekta 850,000 nchini kwa mwaka, hii ni hatari kubwa, lazima tufanye jitihada zaidi kukomesha tatizo hili”.

Aliwaagiza wakuu wa wilaya za Arusha na kilimanjaro kuunda timu ili kuandaa  hadidu za rejea kwa ajili ya kupatia kikosi kazi ambacho kitaandaas andiko kw ajili ya kuanzisha mfuko huo.

Mtendaji Mkuu wa wakala wa misditu (TFS) Juma Mgoo alisema kwamba misitu ilianza kutunzwa mtokea enzi za wakoloni lakini tatizio kubwa linalotokea kw asasa ni watu wengi kuivamia kutokana na mahitaji ya nishati na uchomaji wa misitu.

Alisema kwamba kwa msitu wa asili kawaida huwa na mita 30 za ujazo wakati kwa upande wa misitu ya kuoandwea huwa wna ujazo wa zaidi ya mira za ujazo 400 hadi 600 kitu ambacho alishauri  umuhimu w akupanda miti zaidi ili iweze kukabiliana na ongezeko la mahitaji na kuokoa misitu iliyopo.

Waziri Nyalandu alitoa maagizo ya kuruhusu nguzio za umeme kupita katika msitu wa wilayani Siha ili kufanywa wananchi waweze kupata nishati ya umeme ili kuokoa matumizi ya kuni kama nishati na kulinda misitu.

“Umemem ni nishati mbadala badala ya kuni na mkaa kwa hiyo napenda kuwaeleza kwamba ni bora miti michache ikatwe ili pupisha nguzi za umeme ili wananchi wakipata nishati hiyo waache kutumia kuni na kuharibu misitu na kutumia umeme kama nishati mbadala” alisema.

WAZIRI MKUU PINDA ATEMBELEA KIWANDA CHA TREKTA POLAND

$
0
0


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda atatuma wataalamu wa sekta ya kilimo ili waje kufuatilia suala la mahitaji ya trekta ili kuziba pengo la mahitaji yake nchini Tanzania.



Alisema lengo la Serikali la kuanzisha sera ya Kilimo Kwanza lilikuwa ni kuwasaidia wakulima kupata ruzuku ya pembejeo, mbegu bora, na dawa za mifugo ili waweze kuongeza ushalishaji.



“Kutokana na mkopo wa Serikali ya India, tulipata matrekta 1,846 ambayo hayakuchukua muda kuisha. Sasa hivi tunatafuta wabia wengine wa kutupatia zana za kisasa za kilimo kwa sababu matunda yake mazuri tumeyaona, tunataka kilimo cha Mtanzania,” alisema.



Jana asubuhi(Ijumaa, Oktoba 24, 2014), Waziri Mkuu alitembelea kampuni ya Farmers inayotengeneza vipuri pamoja na matrekta ya kulimia na kuvuna yenye ukubwa wa Horse Power 80 na 72 ambayo alielezwa kwamba yanavumilia hali ya udongo mgumu wa Afrika.



Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Farmer, Bw. ZDZISLAW ZUKIEWICZ alisema vifaa vinavyotengenezwa na kampuni hiyo vina waranti ya miaka saba na vinaweza kuhimili udongo wa miamba na mawe wa ardhi ya Tanzania.



Kampuni hiyo inatengeneza matrekta, mashine za kuvuna mazao shambani (combined harvester), mashine za kukata nyasi za malisho ya mifugo pamoja na vipuri vyake. Alisema bei ya trekta ni wastani wa Euro 22,000 na wako tayari kuleta vifaa hivyo Tanzania kama watapewa oda.



Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi alikutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya wafanyabiashara wa jiji la Warsaw.






IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAPILI, OKTOBA 26, 2014

WAZIRI MKUU: SERIKALI KUOMBA MKOPO POLAND

$
0
0
PG4A6900
*Ni wa kujenga maghala makubwa ya kuhifadhia chakula.

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali inaangalia uwezekano wa kupata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland utakaoliongezea Taifa uwezo wa kuhifadhi chakula tofauti na hali ilivyo sasa.

Alisema uzalishaji mwaka huu umetoa ziada ya tani milioni 1.5 za nafaka na tani 800,000 za mpunga ikilinganishwa na ziada ya tani 300,000 iliyokuwepo mwaka jana. “Serikali inakabiliwa na changamoto ya kupata soko la uhakika kwa mazao ya wakulima kwa sababu tulizoea kumtumia Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kama mnununzi mkuu na uwezo wezo wake ni tani 240,000 tu kwa mwaka,” alisema.

Akizungumza baada ya kutembelea kampuni ya MLYNPOL ambayo inanunua mazao kwa wakulima na kusindika nafaka jana mchana (Ijumaa, Oktoba 24, 2014) Waziri Mkuu alisema teknolojia ya ujenzi wa maghala makubwa ya kuhifadhia chakula katika muda mfupi ndiyo suluhisho pekee kwa wakulima wa Tanzania katika kipindi tulichonacho.

“Wenzetu wana teknolojia ya kisasa ya ujenzi wa SILOS (maghala makubwa ya kuhifadhia chakula) pamoja na namna bora ya kuhifadhi chakula, na sisi tuna changamoto ya kuwasadia wakulima kuuza mazao kutokana na uzalishaji mkubwa wa nafaka ambao umetokea mwaka huu,” alisema.

Alisema ni mapema mno kujua kiasi cha fedha ambacho Serikali inatarajia kukopa lakini alithibitisha kwamba atatuma timu ya wataalamu kutoka sekta husika ili wafanye mazungumzo rasmi na Serikali ya Poland na kukamilisha taratibu za upatikanaji wa mkopo huo.

Waziri Mkuu ambaye alisafiri km. 500 kwenda mji wa CHOJNOW kilipo kiwanda cha kutengeneza maghala (SILOS) na kusindika nafaka aliguswa na teknolojia inayotumika kwenye kiwanda hicho cha MLYNPOL ambapo kwa siku moja kina uwezo wa kusindika tani 360,000.

Mji wa CHOJNOW upo kusini Mashariki mwa Poland na pia hauko mbali na mipaka ya nchi za Ujerumani, Czeck na Austria. Kwa gari dogo ni kati ya saa 3 hadi 4 hadi kufika miji mkuu ya nchi hizo ambayo ni Berlin, Prague na Vienna.

Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, mmiliki wa kiwanda hicho kikubwa nchini Poland, Bw. WITOLD KARCZEWSKI alisema kiwanda hicho kinaposindika ngano kina uwezo wa kutoa unga laini wa mikate (refined flour), unga wa lishe (grain/brown flour), unga wa kutengeneza pasta na tambi na wa mwisho hutolewa kwa ajili ya chakula cha mifugo.

“Nafaka zikifika, zinasafishwa, zinakaushwa, zinapimwa unyevunyevu uliopo na kuanza kusindikwa kulingana na aina ya nafaka inayoletwa. Tunakusanya mazao haya kutoka kwa wakulima kwenye majimbo 16 ya nchi hii,” alisema.

Akifafanua kuhusu matumiai ya umeme kwenye kiwanda hicho, Bw. ALEKSANDR ZINGMAN ambaye pia ni mshauri na mbia wa Bw. KARCZEWSKI, alisema kiwanda hicho kinatumia megawati moja ya umeme kwa saa moja lakini matumizi yanaweza kupungua kuligana na ukubwa ama udogo wa kiwanda. “Kama Serikali inahitaji kiwanda kidogo zaidi ya hapa, tunaweza kuwajengea na matumizi ya umeme lazima yatapungua,” alisema.

Kampuni ya MLYNPOL ina wafanyakazi 250 ambao kato yao, 200 wanafanya kazi kiwandani kwa shifti tatu za saa nane nane kila moja. Waziri Mkuu anamalizia ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi alikutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya wafanyabiashara wa jiji la Warsaw.

MAKAMU WA RAIS AHUTUBIA WASANII KWENYE MADHIMISHO YA SIKU YA MSANII MLIMANI CITY JANA USIKU OCTOBA 25-2014

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tunzo Edward Said Tingatinga msanii aliyejitolea maisha yake kwa Jamii, kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tunzo Josephat Kanuti msanii aliyejitolea maisha yake katika tasnia ya sanaa Nchini,   kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
 Wasanii wa ngoma kutoka Ukerewe wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
 Msanii wa tasnia ya taarab Isha Mashauzi na kikundi chake nao walikuwepo kwenye maadhimisho ya siku ya msanii Mlimani City.

 Wasanii wa kikundi cha sarakasi nao walionesha umahiri wao kwenye usiku wa maadhimisho hayo.
 Wasanii wa kikundi cha sarakasi nao walionesha umahiri wao kwenye usiku wa maadhimisho hayo.
 Msanii Diamond na skwadi lake wakilishambulia jukwaa
 Wasanii na wananchi mbalimbali waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo wakifuatilia kwa karibu matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kwenye ukumbi huo. (Picha na OMR).

LUNDENGA AKANUSHA UVUMI WA MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEVU KUACHIA TAJI LAKE

$
0
0
MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga, amekanusha uvumi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo, kuwa Sitti Abbas Mtemvu (pichani katikati) amelazimika kuvua taji la Uremo la Tanzania (Redd’s Miss Tanzania 2014). Uvumi wa Sitti kuvua taji hilo umetokana na taarifa zilizotolewa kupitia akaunti ya Facebook mrembo huyo anayelalamikiwa kughushi vyeti vya kuzaliwa, akisema kutokana na vidole vya lawama anavyooshewa kiasi cha kuosa amani, amelazimika kuvua taji ili awe huru. 

“Habari za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana, maneno mengi yasio na tija juu ya hili taji la U-Miss anzania 2014,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu Tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha wanaye ona anastahili taji hili apewe ili niendelee na maisha yangu kwa amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi!!” imeandikwa katika ukurasa huo.

Akizungumzia uvumi huo, Lundenga alisema hakuna ukweli juu ya taarifa hiyo, na kwamba kama lingekuwa na ukweli ni wazi kwamba Sitti angeiarifu kampuni yake, inayoratibu kinyang’anyiro hicho kilichotimiza miaka 20 mwaka huu. “Hakuna taarifa iliyotufikia hadi sasa kuhusiana na taarifa hizo. Sitti anajua anapaswa kufanya nini kama anaamua kulitema taji, ambapo anapaswa kutuarifu sisi kabla ya kuripoti hilo mahali popote. Kwa kuwa hajafanya hivyo, tunaamini hilo halipo na bado tunamtambua kuwa mrembo wetu,” alisema Lundenga.

Kwa upande wa mama wa mrembo huyo, alisema ameshtushwa na taarifa za mwanaye kujiuzulu na kusema si za kweli, kwani kama angepanga kufanya hivyo asingefanya kwa kificho, badala yake angeitisha mkutao na wanahabari: “Hawezi kujiuzulu kienyeji hivyo na hata mimi mama yake sina taarifa hizo, hayo ni matumizi mabaya ya mitandao.

PROF.TIBAIJUKA ASISITIZA USHIRIKIANO DUNIANI KUKABILI CHANGAMOTO MBALIMBALI

$
0
0
DSC_0060
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akisoma risala yake kwenye hafla hiyo ambapo alitoa pongezi kwa Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Serikali na kuahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana bega kwa bega na Umoja huo kuhakikisha malengo ya milenia yanafikiwa kwa asilimia mia moja.
DSC_0062
Profesa Tibaijuka na Bw. Rodriguez wakijiandaa kufanya "cheers" ya kuutakia kheri Umoja huo.
DSC_0036
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Profesa Tibaijuka kuzungumza na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
DSC_0074
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakigonganisha glass "Cheers" kuutakia kheri Umoja huo kwa kutimiza miaka 69.
IMG_3257
Pichani juu na chini baadhi ya wageni waalikwa wakiwamo mabalozi na wadau wa taasisi mbalimba za serikali na zisizoza kiserikali waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar mwishoni mwa juma.

IMG_3258
Kwa picha zaidi ingia humu
IMG_3160
Baadhi ya wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini wakiwapokea wageni waalikwa kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.

Tanzania imetaka jumuiya za kimataifa na washirika wa maendeleo kuhakikisha wanashirikiana na Umoja wa Mataifa kuhakikisha kwamba madhumuni ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) yanafikiwa.

Umoja wa Mataifa ulianzishwa miaka 69 iliyopita kuhakikisha amani, maendeleo na ukuaji wa demokrasia ili kuifanya dunia hii kuwa mahali bora pa kuishi.Kauli ya Tanzania imetolewa kupitia Waziri wake wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka mwishoni mwa wiki wakati wa kilele cha sherehe za miaka 69 ya Umoja wa Umoja.

Alisema hayo katika hafla ya mchapalo ya kuadhimisha miaka 69 ya UN iliyofanyika jijini dar es salaam.

Alisema jukumu la Umoja wa Mataifa la kuwezesha maisha bora duniani haliwezi kufanikiwa kama kusipokuwapo ushirikiano wa dhati wa kukomesha changamoto zinazokabili dunia hii kama umaskini uliokithiri, ugaidi na magonjwa.
IMG_3187
Alisema kwa miongo mitatu Umoja wa Mataifa umejituma katika kutekeleza wajibu wake hasa katika kuleta usawa wa jinsia, ulinzi wa mazingira, kuelekeza maendeleo ya pamoja na kuhakikisha amani inapatikana.

Alisema mikutano mbalimbali ya kimataifa iliyofanyika kama ile ya Stockholm, Vancuva, Beijing ililenga kuweka msimamo wa pamoja ambao unawezesha dunia kuwa mahali pa amani ambapo mataifa yanashirikiana kuiweka salama dunia, kwa kuangalia changamoto za demokrasia,mabadiliko ya hali ya hewa na usawa wa binadamu huku suala la wanawake na watoto likitiliwa maanani.

Alisema juhudi za Umoja wa Mataifa umewezesha mabadiliko makubwa kuwepo ambapo dunia kama moja inafanya juhudi za kuimarisha ushiriki wa wanawake katika maendeleo, kuwa na sauti moja katika kukabiliana na majanga mbalimbali yakiwemo vita na magonjwa.
Hata hivyo alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika sekta mbalimbali za afya, amani na maendeleo na kuleta usawa wa jinsia na kushughulikia afya na maendeleo ya wanawake na demokrasia, bado UN ina changamoto kubwa inayoambatana na maendeleo yaliyopo.

Alisema umaskini uliokithiri na ugaidi umekuwa chanzo kipya cha migogoro inayotishia amani na maendeleo ya dunia. Alizitaka nchi wanachama kuungana kuhakikisha kwamba changamoto hizo zinatokomezwa.
IMG_3219
Akimkaribisha Waziri Tibaijuka kuongea Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, alisema kwamba wamefurahishwa na hatua iliyofikiwa na Tanzania katika kutekeleza malengo ya milenia na kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kwamba malengo yale ambayo hayakufikiwa yanafanyiwa kazi katika mpango wa maendeleo ujao.

Aidha alishukuru Tanzania kwa kuipatia UN eneo la kujenga makazi kwa ajili ya mashirika yake yanayofanyakazi nchini . Pia alisema kwamba wakati Umoja wa Mataifa unajikita katika kufanikisha maisha bora kwa wakazi wa duniani, inatambua changamoto zake zilizopo sasa ambapo mamilioni ya wananchi wanateseka kwa kunyonywa, usafirishaji haramu wa watu na kufanyishwa utumwa wa kingono.
IMG_3179
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Balozi Egon Kochanke wakati wa zoezi la kupokea wageni kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.

Alisema ili kuwa na maendeleo na haki ni lengo la Umoja wa Mataifa kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika maendeleo ya kubadili dunia kuwa mahali bora pa kuishi.
Alisema wakati mpango wa malengo ya milenia unaisha mwakani ni vyema mataifa yakaendelea kufikiria kutekeleza yale ambayo haya kuwezekana katika agenda zao za maendeleo.

Alisema amefurahishwa na kauli ya serikali ya Tanzania kwamba imejipanga kuhakikisha inadhibiti ugonjwa wa Ebola na pia kuandaa mipango kwa vijana kupata ajira na kukabili mabadiliko ya tabia nchi. Aidha katika hotuba yake amesema kwamba kwa kuzingatia kwamba nguvu kazi kubwa sasa ni vijana ni vyema jamii ikaacha vijana waongoze kwa kuwa wao ndio wazazi wa kesho na pia ndio nguvu inayotakiwa katika ubunifu na uendeshaji wa shughuli za maendeleo.

Aidha alisema jumuiya ya kimataifa ni lazima itambue ushirikiano kama njia pekee ya kukabiliana na changamoto za dunia kwani hakuna nchi moja inayoweza kufanya shughuli yoyote peke yake.
IMG_3201
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa,Valerie Msoka wakati wa zoezi la kukaribisha wageni kwenye hafla mchapalo ya maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
IMG_3211
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi akiteta jambo na baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker (waliyeshikana mkono) kwenye hafla mchapalo iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa Tanzania kusheherekea miaka 69 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.
IMG_3250
Mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa FAO, Diana Templeman mara baada ya kuwasili kwenye hafla hiyo.
IMG_3252
Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akiwasili kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
DSC_0029
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
IMG_3255
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati hafla hiyo ikiendelea.

WAWEKEZAJI WA KIGENI WATUPIWE JICHO NA SHUGHULI ZAO

$
0
0
Je ! Huu ndio uwekezaji wenyewe ? Idara ya Uhamiaji mpo wapi ?

ah !  "MGENI WA MUNGU HUYU" mwache ajitafutie riziki ! 

Baadhi ya wawekezaji wa kigeni au pengine watumishi raia wa kigeni wamekuwa wakivunja sheria za nchi kwa kujiingiza au kufanya shughuli zisizo katika mikataba yao ya kazi,au nje ya vibali vyao vya kufanyakazi hapa nchini Tanzania,lakini uvunjwaji wa sheria za nchi unaofanywa na wageni hawa unasaidiwa na sisi wenyewe kwa kuzingatia zile mila zetu na misemo ya ah !  "MGENI WA MUNGU HUYU" mwache ajitafutie riziki.
 
Matokeo yake tumekuwa na wachoma mahindi  mtaani kutoka china,wabeba zege pia,Kumradhi pengine makahaba au changudoa kwenye madangulo ya siri.
 
tunaweza kuwa na wakaanga samaki, walinzi "Kolokoloni" kutoka Thailand na Bangladesh,inawekana kabisa tunao hapa nchini wapishi na tour guider kutoka nchi za ulaya !Kwa mtindo na utamaduni wetu huu wa ah! wache "WAGENI WA MUNGU " wajitafutie ridhiki   tutajikuta tunao akina mama ntilie wa kigeni.
 
Tunajiuliza wale wawekezaji wanajiusha na biashara za mitumba au maduka ya nguo kariakoo hivi vibali aliwapa nani? yaani muuza mtumba na duka la sukari atoke china,Yemen,Bangladesh ulaya ! hii kweli inaingia akilini kwa watanzania? Sasa wawekezaji hawa kigeni wanafanya shughuli hizi mcha wa jua kali tena kweupe.
 
Mkondo wa sheria ya nchi unavunjwa walinzi wa sheria wako wapi?
Wizara zinazohusika amlioni hili au ndio ah! TUWAACHE WAGENI WA MUNGU wajitafutie ridhiki ?  Watanzania ukarimu ni jadi yetu ! misemo hii haifanani kabisana ukiwikaji wa sheria za uhamiaji na ajira za nchi, kwani katu kwame uruma nahaki havikai pamoja.

MKUTANO WA UKAWA HAPO JANA KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI

$
0
0
 -Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakionesha hati za waraka walizotiliana saini za ushirikiano katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalimu Seif Sharifu Hamad , akihutubia kwenye mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dk. Emanuel Makaidi akihutubia kwenye hafla hiyo kabla ya kutiliana saini waraka wa ushirikiano.
 Makatibu wakuu wa vyama vinavyuunda Ukawa, wakionesha ishara ya mshikamano baada ya kusaini waraka huo wa ushirikiano. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrord Slaa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalimu, Seif Sharifu Hamad na Katibu Mkuu wa Chama NLD, Tozi Matwange.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lisu (kulia), akimkaribisha Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jusa Ladhu, kuzungumza katika mkutano huo.
 Wafuasi wa ukawa wakionesha vidole vitatu juu wakimaanisha kuikubali serekali tatu inayotakiwa na Ukawa.
 Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa 
kwenye mkutano huo.
 Waendesha bodaboda ambao ni wafuasi wa Ukawa wakiingia kwa maandamano katika viwanja vya Jangwani.
 
Vijana wa chama cha chadema wakiwa juu ya gari wakifuatilia matukio mbalimba yaliyokuwa yakiendelea uwanjani hapo. Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com

Mbio za Rock City 2014 zatiafora

$
0
0
Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mwanza, Bw. Hamis Faki (wa pili kushoto) akitoa hotuba wakati wa kuhitimisha Mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza Jana.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini Suleiman Nyambui,akiwapa maelekezo wakimbiaji wa Km 21, kabla ya mbio kuanza,kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
Mratibu wa Mbio za Rock City Marathon 2014 kutoka kampuni ya Capital Plus International Limited (CPI), akizungumza na waandishi wa habari juu ya muitikio mkubwa ulionyeshwa katika Mbio za mwaka huu zilizofanyika Jijini Mwanza Jana.
 Mwanariadha kutoka Mkoani Manyara Joseph Panga,akimaliza mbio za KM 21 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana,wakati wa mbio za Rock City Marathon 2014, akifuatiwa na Sammy Nyokaye kutoka Kenya(kulia).
 Wanariadha wakianza kukimbia mbio za km 21 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana,wakati wa mbio za Rock City Marathon 2014.


Mbio za Rock City 2014 zatiafora
  • Mtanzania ashinda mbio za kilometa 21
Mwandishi Wetu, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo ameagiza maofisa utamaduni na michezo kuandaa mikakati jinsi ya kushiriki kikamilifu mashindano ya Rock City Marathon mwakani.
Akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio  kwenye uwana wa CCM Kirumba kwa niaba ya Ndikilo jana, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza alisema licha mbio hizo kufanyika mkoani hapa kwa miaka sita, Mwanza haijafanya vizuri na kuagiza ofisa utamaduni kuandaa mkakati wa kutelekezwa kwa ajili ya mashindano mwakani.
Ndikilo alisema Tanzania inaweza kurejea ramani ya dunia kwenye michezo na kwamba, kinachohitajika ni maandalizi  hasa  kuanzia shule za msingi.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI) yamefanikishwa kwa udhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), TSN Group kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy, pamoja na African Barrick Gold, IPTL, Air Tanzania, New Mwanza Hotel, Nyanza Bottling, Sahara Media Group, Continental decoders, New Africa Hotel, PPF, Tanapa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). 

Naye Rais wa RT, Andrew Mtaka aliagiza waandaji wa mashindano ya riadha nchini kuanza kuwaweka wanariadha kambini kabla ya mashindano, huku akiwataka walimu kutowachosha wanamichezo hao.

Mtaka alisema uhamasishaji wa mbio hizo umekuwa mkubwa na kuwataka waandaji wengine nchini kuiga Kampuni ya Capital Plus, kwani ushiriki wa watoto kwenye mashindano hayo umekuwa mkubwa.

“Waandaaji wote wa mashindano ya riadha wahakikisahe wanazingatia ushiriki wa watoto na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), nitaendelea kulea vijana walioonyesha vipaji ili wawekwe kwenye benki yetu ya wachezaji,” alisema Mtaka.

Alisema tayari wameomba Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ili kuwaisaidia wachezaji kuweka kambi nje ya nchi kama alivyofanya wakati wa michauano ya Jumuiya ya Madola.

Katika mashindano hayo, Joseph Panga kutoka Manyara ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kumaliza kwa muda wa saa 1:02:36, akifuatiwa na Mkenya Sammy Nyokaye aliyetumia muda wa saa 1:02:39.

Mbio hizo za kilomita 21 zilizofanyika zilianzia Uwanja wa CCM Kirumba kupitia Barabara ya Uwanja wa Ndege hadi Mzunguko wa Samakisamaki na kurudi hadi Uwanja wa Ndege Mwanza na kumalizikia Kirumba.

Nafasi ya tatu upande wa wanaume ni Festus Talam kutoka Kenya aliyetumia muda wa saa 1:03:05, huku upande wa wanawake Kanda ya Kaskazini ikionekana kutawala mbio hizo, mshindi wa kwanza ni Mathalia Elisante aliyetumia muda wa saa 1:14:25 akifuatiwa na Mary Naali aliyetumia saa 1:15:34 na Adelina Audata saa 1:23:01.

Washindi wa kwanza waliibuka na kitita cha Sh1.5 milioni kila mmoja, washindi wa pili Sh900,000 na washindi watatu Sh700,000.

Akizungumzia siri ya ushindi wake, Panga alisema mashindano ya mwaka jana alishika nafasi ya sita na kwamba, hiyo ilikuwa chachu ya kujituma kufanya zaidi mazoezi na kula vizuri.

“Maandalizi ya mwaka huu ni mazuri ila washiriki ni wachache na hiyo imetokana na wengi wamekwenda kwenye vilabu yao kwa ajili ya mashindano, lengo langu ni kuhakikisha nakimbia Olimpiki ya kimataifa,” alisema.

Hata hivyo, Nyokaye alisema mwaka jana alishika nafasi ya nne ingawa washiriki walikuwa wengi tofauti na mwaka huu, huku akishauri Chama cha Ridhaa Tanzania (RT) kujikita zaidi shuleni ambako wanaweza kupata wanariadha wazuri.

Mahindano hayo yanayoandaliwa na Kampuni ya Capital Plus kila mwaka yamo kwenye kalenda ya RT, huu ni mwaka sita tangu kuanzishwa.

Washindi wa kilomita tano wanaume ambazo ni maalumu kwa walemavu wa ngozi (albino) ni Pascal Charles, Pascal Emmanuel wote kutoka Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza na George Joseph kutoka Ilemela.

Upande wa wasichana mshindi ni Irene Joseph, Asterina Abel na Saidati Haji wote kutoka wilayani Ilemela, mkoani Mwanza.

Mita 100 washindi wasichana ni Kabula Hamis, Anita Elias na Damari Charles na wanaume ni Erick Charles, Jumanne Roche na Lugera Machumu. Washindi wa mita 400 upande wa wasichana ni Leticia Richard, Pili Hamisi na Paschalia Sylveter.

WAZIRI KAWAMBWA AWA "LAIGWANANI" ACHANGISHA MILIONI 35 UKARABATI WA SHULE YA ENABOISHU MKOANI ARUSHA

$
0
0
 .Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa(kulia)akikabidhiwa Usinga unaomtambulisha kama mzee wa jamii ya Kimaasai(Laigwanani) na Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi  ya Kaskazini Kati mkoani Arusha,Solomon Masangwa wakati wa harambee ya kuchangia  ukarabati wa Miundombinu iliyochakaa ya Shule ya Sekondari ya Enaboishu,Shule hiyo imeanzishwa miaka  48 iliyopita na KKKT.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akitoa hotuba yake wakati wa  harambee ya kuchangia  ukarabati wa Miundombinu ya Shule ya Sekondari Enaboishu,kushoto ni Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Masangwa,Mkuu wa Shule hiyo,Lesion Ole Sekioni na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo ambaye ni mhitimu wa Shule hiyo,Elisante Ole Gabriel.
 Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Maswangwa akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Profesa Elisante Ole Gabriel aliyebuni mpango wa kuwakutanisha wanafunzi waliosoma Shule hiyo kuchangia maendeleo ya elimu,yeye akiwa mmoja wao.

 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na Wafanyakazi wa Shule ya Enaboishu
 Baadhi ya Walimu wa Shule hiyo wakifatilia kwa makini harambee ya kuchangia maendeleo ya Shule ya Sekondari Enaboishu mkoani Arusha.
 Waimbaji wa Empowered Girls Club wakitoa burudani iliyovuta hisia za watu waliohudhuria hafla hiyo.
 Waimbaji wa Empowered Girls Club wakifurahia kitita cha Sh.200,000 walizopewa na mgeni rasmi,Waziri wa Elimu,Dk Shukuru Kawambwa kwa kutoa burudani iliyovuta hisia za watu waliohudhuria hafla hiyo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akipongenzwa na  wanafunzi  wa Shule ya hiyo baada ya kufanikisha harambee .

President Kikwete Visits Shandong Provincial Hospital in China

$
0
0
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete signs a VIP book shortly after he arrived at Shandong Provincial hospital in China this evening. Shadong hospital has been sending doctors to Tanzania since 1978 to date is support to Tanzania’s Health policies
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his entourage to China pose for a group photo with some members of Staff of Shandong Provincial Hospital when the President toured the hospital, thanked the hospital staff for their support for Tanzania’s health programs and appealed for enhanced cooperation between the hospital and Tanzania’s health institutions. President Kikwete in on a seven day State Visit to China at the invitation of President Xi Jinping of China.(photos by Freddy Maro).

UTT YATOA ELIMU YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWA WAKAZI WA MBEYA

$
0
0
 Wakazi wa Mbeya wakipata Elimu ya Uwekezaji wa Pamoja kutoka kwa Ofisa Mafunzo wa UTT AMIS, Hilda Lyimo wakati wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yaliyofanyika Mbeya.
Ofisa Mafunzo wa UTT AMIS, Hilda Lyimo akitoa ufafanuzi Uwekezaji wa Pamoja kwa wakazi mjini Mbeya wakati wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara.
Ofisa Mafunzo wa UTT AMIS, Mwanahamisi Sakuru akitoa Elimu ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wakazi wa jijini Mbeya.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga wakitoa elimu juu ya uwekezaji wa pamoja kwa wakazi wa Mbeya waliotembelea Maonyesho ya ya Kimataifa ya Biashara kwenye Ukumbi wa Mkapa, Soko Matola Mbeya.

China to Boost Bagamoyo Special Economic Zone

$
0
0
A permanent Secretary in the Ministry of Finance Dr.Servicius Likwelile, a representative from the Sultanate of Oman together with an official from China Merchants Holdings International sign a memorandum of Understanding(MoU) between the Government of Tanzania, China Merchants  Holdings international and State General Reserve Fund of Oman on a Strategic Partnership for the Development of Bagamoyo Special Economic Zone(SEZ).The Signing ceremony took place at the Shenzen Hilton Hotel in China in the Presence of President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete (photo by Freddy Maro).
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images