Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 397 | 398 | (Page 399) | 400 | 401 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Katibu na Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege, (mwenye suti nyeusi kushoto) akimkabidhi Mwinjilisti wa Kanisa la KKKT Usharika wa Likamba Wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Bi Martha Musa Kivuyo (mwenye nguo nyeupe), mfano wa hundi ya Shilingi milioni 10 kati ya Silingi milioni 20 (Tsh 20m/-) iliyotolewa na kampuni ya IPTL/PAP, kusaidia kwaya ya Patano la Usharika wa Likamba kuweza kurekodi albam ya nyimbo za injili. 

   Katibu na Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege, (mwenye suti nyeusi kushoto) akipongezwa na Mdhamini na Mlezi wa kwaya ya Patano la Usharika wa Likamba kanisa la KKKT la Arumeru, mkoani Arusha, Bw. Philip Makini baada ya kukabidhi  mfano wa hundi ya Shilingi milioni 10 kati ya Silingi milioni 20 (Tsh 20m/-) iliyotolewa na kampuni ya IPTL/PAP, kusaidia kwaya ya Patano la Usharika wa Likamba kuweza kurekodi albam ya nyimbo za injili. Wakishuhudia ni Mwinjilisti wa Kanisa hilo, Bi Martha Musa Kivuyo (mwenye nguo nyeupe), na Meneja Uhusiano wa Jamii wa IPTL/PAP Bw. Sylvester Joseph pamoja na wanakwaya.
   Katibu na Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege, (kulia) akizindua albam mpya ya nyimbo za injili ya kwaya ya Patano la Usharika wa Likamba Kanaisa la KKKT la Wilaya ya Arumeru, Arusha. Kati kati ni Meneja Uhusiano wa Jamii wa Makampuni ya IPTL/PAP Bw. Sylvester Joseph akifuatwa na Bi.Hellen Zelothe.
   Katibu na Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege, (kulia) akionyesha albam mpya ya nyimbo za injili ya kwaya ya Patano la Usharika wa Likamba Kanaisa la KKKT la Wilaya ya Arumeru, Arusha mara tu baada ya kuuzindua. Wakishuhudia kutoka kulia ni Mfadhili na mlezi wa kwaya hiyo Bw. Philip Makini, ambaye pia ni Afisa Mwandamizi wa jumuia ya Afrika Mashariki, akifuatwa na Meneja Uhusiano wa Jamii wa Makampuni ya IPTL/PAP Bw. Sylvester Joseph akifuatwa na Bi.Hellen Zelothe.
   Moja wa waumini katika Kanisa la KKKT Usharika wa Likamba iliyopo Wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha, Bw. Thedayo Zelothe (kulia) akitoa mchango wake wa fedha pamoja na jogoo wawili wakato wa harambee ya kuchangia kwaya ya Patano la kanisa hilo mwishoni mwa wiki kwa lengo la kurekodi albam ya nyimbo za injili. Aliyebeba majogoo ni Mgeni rasmi katika harambee hiyo ambaye ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege. Wakishuhudia ni Mfadhili na mlezi wa kwaya hiyo Bw. Philip Makini (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CCK) Bw. Renatus Mwabih (wa pili kushoto) akifuatwa Bi.Hellen Zelothe.

   Katibu na Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege, (wa pili kulia) akimpongeza mototo aliyeonyesha umahiri wake wa kucheza na kuimba nyimbo za injili akiwa ni mwanakwaya ya Edeni ya Kanisa la Morovian la Mjini Arusha. Mgeni rasmi alitoa Shilingi milioni moja (Tsh 1m/-) kama mchango wa ada yake ya shule. 


  Wananchi wametakiwa kuwa makini na kauli za wanasiasa kwani sio kila kitu wanachosema ni cha kweli bali baadhi yao hupotosha jamii kwa maslahi yao binafsi.

  Akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia kwaya ya Patano la Kanisa la KKKT Usharika wa Likamba Wilayani Arumeru-Magharibi, Mkoani Arusha mwishoni mwa wiki, Wakili ambaye pia ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege, (ambaye alimwakilisha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPTL/PAP, Bw. Harbinder Singh Sethi) alionya kuwa kauli za upotoshaji katika maswala mbali mbali nchini, hususan ya kisheria zinaweza kuleta madhara makubwa sana kwa taifa.

  “Kama mwanasheria, ningependa kuwashauri wanasiasa wetu kuacha kuingilia mashauri yaliyopo mahakamani au ambayo yameamuliwa na vyombo halali vya kimahakama kwa kutoa kauli ambazo  zinawapotosha wananchi. Wakiendelea na tabia ya kuhoji uhalali wa maamuzi ya mahakama, itapelekea hata wananchi kutokuwa na imani na mahakama zetu, jambo ambalo linaweza kusababisha haki za watu wanyonge kupotea na amani ya nchi yetu kutoweka,” alisema Bw. Makandege.

  Aliongeza kuwa kauli hizo zinachangia kuiathiri jamii ambayo pengine hawajui ukweli kuhusu jambo linaloongelewa kwa kuwa wengi wao wanaamini kuwa kila kauli ya mwanasiasa ina ukweli na inapotokea mwanasiasa anaipotosha jamii madhara yake huwa makubwa sana. 

  Mwanasheria huyo akitolea mfano tuhuma zinazo endelea kuhusu kutwaliwa kwa kampuni ya IPTL na PAP pamoja na fedha za IPTL zilizokuwa katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta (IPTL Tegeta Escrow Account) katika Benki Kuu ya Tanzania, alisema licha ya wanasiasa  kutambua ukweli kwamba akaunti hiyo na fedha zote zilizokuwemo hazikuwa za umma, bado wanaendelea kuiongopea jamii kwamba fedha hizo zilikuwa mali ya umma, bila hata kuhofia madhara yanayoweza kusababishwa na kauli zao, jambo ambalo alisema kuwa linakinzana hata na maandiko matakatifu. 

  Aliongeza kuwa kauli kama hizo sio tu zinahatarisha amani ya taifa letu kwani ni za kichochezi kwa sababu zinaweza kuwafarakanisha wananchi na serikali yao, bali pia zinaweza kuathiri uwekezaji katika nchi yetu kwa kuwakatisha tamaa wawekezaji jambo ambalo linaweza kuhatarisha uchumi wa taifa letu.

  Akifafanua, Bw. Makandege alisema ukweli ni kwamba fedha zote zilizokuwa katika akaunti hiyo ya Escrow hazikuwa za umma bali zilikuwa fedha halali za IPTL, ambazo zilihifadhiwa katika akaunti hiyo ya Escrow kufuatia mgogoro baina ya wabia wa IPTL, Mechmar Corporation (Malaysia) Berhad (“Mechmar”) na VIP Engineering & Marketing Limited (“VIP”). Baada ya mgogoro kuisha kufuatia uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania (Mh. Jaji Utamwa) tarehe 5 Septemba 2013, fedha hizo zililipwa kihalali kabisa kwa IPTL kutokana na mauzo ya umeme kwa Tanesco.

  “Iweje wanasiasa wahoji tu fedha hizo zilizolipwa kwa IPTL kihalali kulipia umeme ambao IPTL ilizalisha na kuiuzia TANESCO na kusambazwa kwa wananchi? Kwani IPTL ni mali ya umma? Je, ilitaifishwa lini?”, alihoji Bw. Makandege. 

  Kwa upende wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Kijamii (CCK) Renatus Mwabhi, ambae pia alishiriki katika hafla hiyo, amewataka wananchi kuchambua kwa umakini matamshi ya viongozi kabla ya kuyaamini kwakuwa siyo viongozi wote wanalitakia kheri taifa hili.

  Mbali na hilo, katibu huyo wa CCK amewataka wananchi na waumini kuliombea taifa kwani kina kila dalili kuwa matendo yanayoendelea hivi sasa hapa nchini yanaweza kuliingiza taifa katika machafuko yasiyo ya lazima.

  Katika harambee hiyo zaidi ya shilingi milioni 30 (Tsh 30,000,000/-) zilikusanywa huku kampuni ya IPTL na PAP wakishirikiana na kampuni ya mawakili ya Bulwarks Associate Advocates wakichanga zaidi ya  shilingi milioni ishirini (Tsh 20,000,000/-) ambazo zitachangia katika maendeleo ya kanisa na kuwezesha kwaya hiyo  kurekodi albam yake mpya yenye ujumbe wa neno la Mungu ili kuwawezesha kutimiza azma yao ya kueneza injili kwa watu wote.

  Kwa upande wake, mlezi wa kwaya hiyo ya Patano na kwaya ya Edeni ya Kanisa la Morovian la Mjini Arusha, Bw. Philip Makini ambaye pia ni Afisa Mwandamizi wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), aliwapongeza IPTL/PAP na Bulwarks Associate Advocates kwa msaada waliotoa ambao alisema utawawezesha wanakwaya na Usharika kwa ujumla kufanikisha malengo yao. 

  Naye Mwinjilisti wa Kanisa la KKKT Usharika wa Likamba, Bi. Martha Musa Kivuyo, kwa niaba ya wanakwaya na wanausharika wote, aliwashukuru Makampuni hayo kwa mchango wao uliowawezesha kuvuka malengo ya harambee hiyo iliyotazamia kukusanya Shilingi milioni 20 (Tsh 20m/-)

  0 0
 • 10/29/14--03:40: Article 16


 • 0 0



  Until the recent past, the recounts of most Tanzanians in the Diaspora had been filled with horrific and disappointing experiences regarding mismanagement of funds and investment attempts back home in Tanzania. Most Diasporas entrusted their projects and investments back home to their immediate relations, which, more often than not, led to devastating consequences. Some Diasporas even fear the thought of returning home with little to show for their stay abroad. The question that lingered in most of us was, is there a permanent solution to this problem?

  The solution is found


  In 2012, Tanzania Diaspora Initiative (TDI) was formed. In many ways, this is a response to the needs and concerns of all Tanzanians in the Diaspora. Whether you need to invest, buy land, start a business, follow up on projects, and even get current updates on the information on all of the above, TDI acts as a hub to cater for all your needs.


  Born out of real passion to cater for the needs of Tanzanians in the Diaspora and provide permanent solutions to the series of diaspora related problems and concerns, Tanzania Diaspora Initiative goes further to provide a platform where information can be easily obtained, shared and help in making important decisions about investments and contributing to the wellbeing of the communities back home.


  TDI understands that diaspora is part of Tanzania that has a potential role to play in fast-tracking the country’s economy through various areas such as dividends, investments, expertise and many other areas. However, if these areas aren't fully exploited for the benefits of our economy, Tanzania loses a lot in that front.

  What is TDI?


  TDI is a solution to the Professional needsof the Tanzanians in the diaspora. They key issue is to help bridge the gap between the professional needs of the Diaspora and their actual projects back home. This is what Diaspora need to have a peace of mind in ensuring their investments, projects or businesses are running smoothly while they are continuing with their lives abroad. In other words, TDI helps to save money and time for Diasporas while it handles all the issues locally with qualified professionals in their fields. 


  In order for any project or investment to run smoothly, there is a need of professional involvements. TDI shares the pride of having qualified professionals with a lot of experiences in their respective fields capable of catering for the needs of the Diasporas. 


  The aggregate skills within TDI and at the disposal of Tanzanians in the diaspora include project management, property management, Job opportunities. Investment opportunities, inspection of works and provision of professional reports, estate agency, land-use advise, document processing and management including title deeds, planning permission, and many other tailor-made solutions.

  How you benefit from TDI


  As TDI works locally in Tanzania, it ensures a strong link to communicate the latest information to the Diasporas from the core sources in Tanzania. These information can be on investments, some changes in rules and regulations, or any interesting information that could be of use for the people who are looking to invest and contribute back to their local communities. These kinds of information are communicated to all valid registered members with the TDI. You can have that chance by simply registering to the TDI and ensure you do not get left out from the important potential information concerning investments or opportunities back home.



  Join us and be a part of the bigger Community


  0 0

   Wajumbe wa Bodi ya Sukari Kilombero wakiwa katika kikao na wajumbe wa Bodi ya Southern Agricultural Growth Corridol of Tanzania (SAGCOT) baada ya ziara yao katika mashamba ya miwa ya wakulima wadogowadogo karibu na maeneo ya Kiwanda cha Sukari Kilombero mkoani Morogoro.
   Mkurugenzi wa ofisi ya SAGCOT Catalytic Trust Fund Bw. John Kyaruzi akizungumza na wajumbe wa Bodi ya SAGCOT katika uzinduzi wa Ofisi yao iliyoko karibu na Hospitali ya Ocean road jijini Dar es Salaam hapo jana.
   Wajumbe hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao hicho kilichofanyika katika Kiwanda cha Sukari Kilombero. 
   Mwenyekiti wa Bodi ya SAGCOT Balozi Ami Mpungwe akizungumza na wajumbe wa bodi katika uzinduzi wa Ofisi hiyo.
  Shamba la Miwa likiwa limeandaliwa kwa kuchomwa moto tayari kwa kuvunwa.

  0 0

    Kiongozi wa Kundi la Kudansi la Wakali Sisi lililoshinda katika Shindano la Dansi mia mia hivi karibuni Yasin Haji (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa waliohudhuria kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kushoto ni Afisa Sanaa kutoka BASATA, Ernest Biseko.
  1.    Kundi la Wakali Sisi likionesha vitu vyeo kwenye Jukwaa la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii.

  1Mdau wa Sanaa kutoka Kikundi cha Sanaa za Majukwaani cha Binti Leo Lena Jackson akizungumza jambo kwenye Jukwaa la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kushoto kwake ni mkongwe wa Sanaa za Maonesho nchini, Baraka Mpelemba maarufu kwa jina la Jangala na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonesho Nkwama Bhallanga.
  1Wadau wa Sanaa wakifuatilia burudani iliyokuwa ikitolewa na Kundi la Wakali Sisi kwenye Jukwaa la Sanaa mapema wiki hii. 



  Wasanii nchini wameaswa kuzingatia muda wanapohitajika kufanya onesho au kazi yoyote ya jamii ili kuepuka kudharaulika na kuonekana watu wa hovyo na wasiyojali muda.

  Rai hiyo imetolewa na Afisa Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ernest Biseko wakati akihitimisha Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki ambapo Kikundi cha Wakali Sisi kilichoshinda kwenye onesho la dansi mia mia kilitoa burudani.

  “Hakuna kitu muhimu na cha msingi kwa msanii kama kuzingatia muda. Wasanii tumekuwa tukilalamikiwa sana kuchelewa kwenye maonesho au kwenye shughuli za kijamii ambazo zinatutaka tuwahi. Hii haipendezi” alisema Biseko. Aliongeza kwamba, wadau wengi wa Sanaa hawafurahishwi hata kidogo wanapoona msanii anafika kwa kuchelewa kwenye shughuli hali ambayo imekuwa ikiwafanya wachukie na kuchukua maamuzi ya kufanya vurugu.

  Mdau mwingine wa Sanaa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Sanaa za Maonesho nchini Nkwama Bhalanga alisema kuwa, wasanii wamekuwa wakidharaulika na kuonekana wa hovyo-hovyo kutokana na kutokuzingatia muda hali ambayo inawafanya washindwe hata kufanya vizuri jukwaani kutokana na muda mfupi wa maandalizi.

  “Msanii lazima afike kwenye tukio walau saa moja kabla ya onesho ili azoee mazingira lakini pia afahamu wapi pa kubadilishia mavazi, kupumzika na kuoga baada ya onesho lake” alisisitiza Bhallanga.

  Awali katika Jukwaa hilo, Kikundi cha kudansi cha Wakali Sisi ambacho wiki kadhaa zilizopita kiliibuka kidedea kwenye onesho la Dansi Miamia kilitoa burudani ya kuvutia kwa wadau wa Sanaa. 

  0 0

   
  Bunduki aina ya  Pump Action Shortgun iliyokamatwa Njombe.

  Na James Festo, Njombe.

  JESHI la Polisi Mkoani Njombe limethibitisha kuwa linamshikilia mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Elias Nguvumali (28) mkazi wa mtaa wa mjimwema mjini Makambako kwa kosa la kukamatwa na silaha  aina ya Pump Action Shortgun ikiwa na risasi tano.

  Kwa Mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa iliyosainiwa na kamanda wa polisi mkoani Njombe SACP Fulgence Ngonyani  ilisema kuwa tukio hilo lilitokea octoba 26 mwaka huu  majira ya saa 12:30 asubuhi ambapo mtuhumiwa alikutwa na silaha hiyo yenye namba za usajili 007700112 katika mtaa wa mjimwema.

  Taarifa hiyo ilisema kuwa bunduki hiyo ilikuwa ndani ya mfuko na mtuhimiwa alikuwa akitumia silaha hiyo kwenye matukio ya uhalifu ambapo hubadilisha jina lake na kuitwa Nathan Nguvumali.

  Katika hatua nyingine ilisema kuwa mshitakiwa huyo anashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.

  Wakati huo huo mtu mkazi mmoja wa Wilaya ya Makete Mkoani hapa Bi.Tumulikwe Sanga (49) amejeruhiwa baada gari ya jeshi walilokuwa wakisafilia kuacha njia na kugonga kalavati na kupinduka  katika kijiji cha Tandala

  Taarifa hiyo ilisema kuwa tukio hilo lilihusisha gari lenye namba 5968 JWTZ aina ya Land Ashoke mali ya kikosi cha KJ(911 ambayo ilikuwa na watu 17 ambapo watano kati yao ni askari na 12 ni raia wa kawaida.

  Gari hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na askari mwenye namba za usajili MT 84276 CPL Munishi Antony wa  KJ  911  Dodoma lilikuwa limetoka Dododma kuelekea Makete ambalo lilifeli bleki kwenye mteremko.

  Hata hivyo Jeshi la Polisi lilitoa wito kwa madereva kuwa makini pindi wanaendesha vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuvifanyia ukaguzi kabla na baada ya safari ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

  0 0

  1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa la kujadili matumizi ya Nishati itokanayo na joto ardhi katika Nchi za Afrika zinazopitiwa na bonde la ufa. Kongamano hilo limeanza leo Oktoba 29, 2014 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa la kujadili matumizi ya Nishati itokanayo na joto ardhi katika Nchi za Afrika zinazopitiwa na bonde la ufa. Kongamano hilo limeanza leo Oktoba 29, 2014 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. 3Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt Bilal, kufungua kongamano hilo.
  4Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya waliohudhuria kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
  5 Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal. 6 Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal. 7Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo baada ya ufunguzi. 8 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wakati akiondoka eneo hilo baada ya kufungua kongamano hilo. 9Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akifurahia burudani ya ngoma ya asili ya kabila la wamasai wakati akiondoka katika Ukumbi wa AICC baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo.

  0 0

    Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara kutoka Shirika la Posta Tanzania Bw. Fortunatus Kapinga akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio ya shirika hilo ikiwemo matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za shirika hilo hali ambayo imeongeza tija. Kulia ni Meneja barua Bi Fadya Zam.
   Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara kutoka Shirika la Posta Tanzania Bw. Fortunatus Kapinga akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu  utaratibu wa Shirika hilo kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao kupitia vituo vya Mawasiliano ya jamii (Community Information Centres) ambapo huduma hiyo  kwa sasa inatolewa katika Ofisi za Zanzibar, Arusha, Bagamoyo, Mwanza na Mbeya. Kushoto ni Meneja Mifumo ya Mawasiliano Bw. David Mtake na mwisho ni Meneja Masoko  Bw. David George.(Picha na Frank Mvungi-MAELEZO).

  0 0

   Balozi wa Cuba nchini Tanzania Mheshimiwa Dk. Fred Fagudo akiongea na waandishi wa Habari jana Jijini Dar es salaam kuhusu ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi yake, Kushoto ni Mkalimani wa Balozi huyo Bw. Josia Shindika.
  Balozi wa Cuba nchini Tanzania Mheshimiwa Dk. Fred Fagudo akiongea na waandishi wa Habari  jana Jijini Dar es salaam  kuhusu fursa mbalimbali zinazotolewa na nchi hiyo kwa Tanzania katika sekta ya Elimu na Afya.  Kushoto ni Mkalimani wa Balozi huyo Bw. Josia Shindika. (Picha na Frank Mvungi-MAELEZO)

  0 0



   Mkuu wa idara ya data na vifaa vinavyotumia intarnet kutoka Tigo, David Zacharia akielezea wateja watakavyotumia huduma hiyo kwa urahisi,mbele ya Wanahabari jijini Dar leo.

   Mkuu wa ukuaji na ushirikiano wa mitandao ya kijamii kutoka Tigo, Naheed Hirji, akielezea upatikanaji wa huduma hiyo.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo.

  KAMPUNI ya mtandao wa Tigo, imetangaza rasmi ushirikiano kati yao na mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo itatoa ofa ya Intaneti itakayotumiwa kwa bei nafuu kupitia ‘application’ maalum ya Intaneti Organisation.

  Tigo pia inatoa fursa ya wateja kununua simu za kisasa ‘smartphones’ kwa bei nafuu, ili kupata huduma bora ya intaneti na  tovuti za huduma  kama vile elimu, afya, habari na mitandao ya kimawasiliano zitakazopatikana bila malipo

  Akizungumza na kwenye mkutano na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar, mkuu wa idara ya data na vifaa vinavyotumia intaneti kutoka Tigo, David Zacharia, alisema ushirikiano wao na Facebook utaongeza matumizi ya tekinolojia ya kidijitali nchini kwa Watanzania wengi kutumia mtandao wa intaneti.


  0 0





  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili nchini leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere ulioko jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi nchini China na Vietnam.
   Mwamunyange (kushoto) leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere pamoja na baadhi ya viongozi wengine mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi nchini China na Vietnam.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM).

  0 0

  Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii

  Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemwachia kwa dhamana Msanii  wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi  Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz, baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya mahakaman hiyo.

  Chid Benz, alifikishwa mahakamani hapo jana akikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

  Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema alisema mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wa wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazotambulika na wasio walimu pamoja na kusaini hati ya dhamana ya Sh. milioni moja.

  Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda.

  Wakili Kombakono alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.

  Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.

  Wakili huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.

  Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

  Hakimu Lema alisema kesi hiyo itatajwa Novemba 11, mwaka huu.

  0 0

  Ajali mbaya imetokea jioni ya leo katika eneo la Tengeru,Jijini Arusha ikihusisha gari dogo aina ya Toyota Hiace (pichani juu) linalofanya safari zake kati ya Usa River na Katikati ya mji wa Arusha na Lori la Mafuta. Chanzo cha Ajali hiyo inaelezwa kwamba ni hiyo daladala lilikuwa likijaribu kulipita gari jingine ndipo likakutana na loli hilo la mafuta na kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya abiria wote waliokuwa kwenye daladaa hilo ambao idadi yake haijafahamika rasmi.taarifa kamili itawajia baadae kidogo.Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya JAMII Kanda ya Kaskazini.

  0 0
 • 10/29/14--12:40: HONGERA MZEE WA WARAKA.
 • 001_resized_5 (1)Juu na chini mwandishi wa makala katika safu ya Waraka kutoka Houston ndani ya gazeti la Raia Mwema, Innocent Mwesiga, Pharm.D na mke wake Carretta Mwesiga, FNP wakifurahia miaka 10 ya ndoa yao hivi karibuni katika visiwa vya Bahamas. (Kutoka blog hii tunawapa hongera sana) 002_resized_6(Picha kwa hisani ya Sunday Shomari).

  0 0

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa pili kushoto) akimwongoza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,   Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa pili kulia) kutoka eneo la mkutano katika Ukumbi wa Mikutano wa  Kimataifa AICC mara baada ya ufunguzi wa
  Kongamano la Tano la Kimataifa ambalo linajadili masuala mbalimbali kuhusu matumizi ya nishati ya jotoardhi kwa nchi wananchama  kwa nchi zilizo katika bonde la ufa na nchi nyingine duniani.  Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo na Mkurugenzi wa
  Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Julius Ningu (wa kwanza kulia).
   Sehemu ya Washiriki wanaohudhuria Kongamano la tano la Kimataifa la Jotoardhi kwa nchi zilizo katika bonde la Ufa katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa  wakifuatilia hotuba ya  ufunguzi kutoka  kwa Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  Mohamed Gharib Bilal (katikati) akifuatilia taarifa kuhusu Kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi, wengine kutoka kushoto ni Kamishna wa Miundombinu na Nishati kutoka Umoja wa Nchi za Afrika Dkt. Elham Ibrahimu, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, Naibu wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Stephen Masele, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira kwa Ukanda wa Afrika (UNEP), Mounkaila Goumandakoye, Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya nishati wa Iceland Einar Gunnarsson na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.
   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Gharib Mohamed Bilal mara baada ya kufungua Kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi.

   Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi katika picha ya Pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal baada ya kufungua kongamano hilo.
   Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Nishati, Einar Gunnarsson akitoa taarifa kwa ufupi kuhusu namna nchi  hiyo ilivyoendelea katika masuala ya nishati ya Jotoardhi. Imetajwa kuwa nchi ya Iceland ni miongoni mwa nchi zilizoendelea katika nishati hiyo.
   Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele akipata maelezo kuhusu masuala ya jotoardhi katika moja ya mabanda aliyoyatembelea mara baada ya kufungua Maonesho ya kuhusu masuala ya jotoardhi zikiwemo bidhaa na teknolojia zinazotumika katika nishati hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuendeleza Jotoardhi Tanzania, Mhandisi Boniface Njombe (wa kwanza kushoto mwanzo) akiongea jambo na baadhi ya wageni waliotembelea banda la Kampuni hiyo. Kampuni hiyo ya Jotoardhi ilianzishwa  mwaka 2014 .


  Nishati ya Jotoardhi  inakua Afrika- Bilal

  Makamu wa  Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal amesema ni wakati muafaka kwa Tanzania kuongeza vyanzo vya nishati ya umeme ikiwemo  vitokanavyo na nishati ya jotoardhi kutokana  na  umuhimu wake kwa maendeleo ya kiuchumi, vilevile kutokana  na Tanzania  kuwa  na hazina kubwa yenye viashiria vya jotoardhi.

  Ameongeza kuwa,  nishati ya umeme ni miongoni mwa  maeneo ya
  kipaumbele ya Serikali  kuhakikisha  taifa linakuwa na  nishati ya
  kutosha ya umeme, ya uhakika na nafuu kutokana muhimu wa nishati hiyo
  kwa maendeleo ya kiuchumi, kiviwanda na katika sekta ya kilimo na
  kwamba ni chanzo cha nishati kisichokwisha.

  Aidha, Makamu wa Rais amezitaka nchi wananchama zilizo katika bonde la
  ufa na nchi nyingine  za Afrika kutumia fursa zinazotolewa na
  Mashirika ya Kimataifa na Taasisi zilizobobea katika masuala ya
  jotoardhi kuviendeleza vyanzo hivyo katika nchi zao kwa maendeleo ya
  nchi hizo.

  Kongamano hilo limefunguliwa leo tarehe 29 Oktoba, 2014 na
  kuwashirikisha washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi wananchama  kutoka
  katika bonde la Ufa na nchi nyingine duniani, zikiwemo taasisi za
  Kimataifa  zinazohusika na masusla ya jotoardhi na nchi nyingine
  zilizopiga hatua katika nishati hiyo ikiwemo Iceland na litaendelea
  hadi tarehe 31 Oktoba,2014.

  0 0


  Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum (Katikati) akionyesha kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 wakati akikizindua katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana Oktoba 29, 2014. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Ofisa kutoka Shirika la Maendeleo la DPG, Sinikka Antila, Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu. Picha/Video zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

  Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 wakati akikizindua katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana Oktoba 29, 2014. Wanaoshuhudia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Veronika Kazimoto (kulia) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (katikati).

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa akimfafanulia jambo Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum mara baada ya kufanya uzinduzi.

  Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akimkabidhi chapisho Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu.

  Wawakilishi toka Mashirika mbali mbali ya Kimataifa wakiwa katika picha ya pamoja.
     Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, akihutubia wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2011/12 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana Oktoba 29, 2014.

  Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini.
  Waandishi wa habari nao hawakuwa mstari wa nyuma.
  Meza kuu ikifuatilia kwa makini.
  Wanafunzi wa Chuo cha Takwimu nao walifika.
  Wawakilishi toka mashirika ya kimataifa nao walifika.

  Furaha ya kukutana pamoja.
  Picha ya Pamoja.

  0 0

  Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira imeendelea na ukaguzi katika Migodi ya dhahabu kufahamu utekelezaji wa Sheri a ya Mazingira. Katika Mgodi wa Bulyanhulu Kamati iliangalia jinsi maji yenye kemikali yanavyohifadhiwa na udhibiti wa taka za plastiki mgodini  hapo. Migodi iliyotembelewa mpaka sasa ni Mgodi wa North Mara, Geita na Bulyanhulu. Hii leo Kamati hii itaendelea na ziara yake katika mgodi wa Buzwagi.
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi wa kisheria mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira. Kamati hiyo iko katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Sheria ya Mazingira katika Migodi. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mh. James Lembeli (wa tatu kulia), Mh. John Mnyika na Mh. Henry Shekifu wajumbe wa Kamati hiyo. Wa kwanza (kushoto) ni Bw. Peter Burger, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu.
   Pichani ni taka za plastiki zilizohifadhiwa vizuri kwa ajili ya urejelezwaji katika Mgodi wa Bulyanhulu.
   Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu wakati wa ukaguzi katika Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.
  Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu mara baada ya ukaguzi katika Mgodi huo kuona utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.

  0 0

  Msanii wa filamu, Mzee Manento amefariki dunia hapo jana. Globu ya Jamii bado inafuatilia kwa karibu kujua chanzo cha kifo cha Muigizaji huyu mahiri wa filamu hapa nchini.Baadhi ya filamu alizowahi kuigiza Mzee Mnento ni Hero of the church, Dar to Lagos, Fake pastor n.k 
  Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina.

  0 0


   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akiowaonyesha mabango ya filamu za Tanzania wageni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (hawapo pichani) walipotembelea ofisi za Bodi hiyo ili kujifunza namna ya Uendeshwaji wa Bodi ya Filamu jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Silyvester Sengerema.
   Kutoka kushoto ni Afisa Mult Media kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA) Bi. Jacquline Kinyanjui, Afisa Mult Media kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya Bi. Mercy Tepla na Afisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. George Charles wakisikiliza maelezo kutoka kwa uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania walipotembelea ofisi za Bodi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
  Ujumbe kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya wakiwa katika kikao cha pamoja na Watendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania jana jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija, WHVUM

   

older | 1 | .... | 397 | 398 | (Page 399) | 400 | 401 | .... | 1898 | newer