Uongozi wa Taasisi Ya RafikiElimu Foundation unapenda kuwatahadharisha wananchi wote juu ya kuibuka kwa kundi la watu wanao fanya utapeli mitandaoni kwa kutumia jina la Taasisi ya RafikiElimu Foundation. Siku ya Ijumaa ya leo tarehe 28 FEBRUARI 2013 mnamo majira ya saa 5 kamili asubuhi, ofisi yetu ilitembelewa na mwanadada aliye jitambulisha kwa jina la HAWA MUSSA. Mwanadada huyu baada ya kujitambulisha, aliomba kuonana na HUMAN RESOURCES MANAGER wa Taasisi ya RafikiElimu , baada ya kumuona, ali onyesha fomu aliyopewa kupitia mtandaoni na watu walio jitambulisha kwake kama RafikiElimu Foundation.
Watu hao walitoa tangazo kupitia mtandao wa ZOOM TANZANIA wakidai kuwa wana wa link, wahitimu mbalimbali wa vyuo vikuu na taasisi mbalimbali zisizo kuwa za kiserikali kwa ajili ya kufanya kazi katika taasisi hizo kama volunteers. Mwanadada huyu akaendelea kueleza ya kwamba, baada ya kuona tangazo hilo alivutiwa na kutuma maombi ambapo walimjibu kwa kumpatia fomu aliyo takiwa kuijaza na kuirejesha kwao.
Baada ya kujaza fomu hiyo, walimtumia barua pepe nyingine na kumwambia kwamba maombi yake yamekubaliwa, kisha wakamtumia fomu na kumwambia aijaze, aimbatanishe na CV yake, na kuwatumia pesa kiasi cha shilingi Elfu Tano ( TSH. 5,000/=) kwa njia ya MPESA kwenda namba 0763906931 ( AMBAYO MBAYA ZAIDI, WAMEISAJILI KWA JINA LA RAFIKIELIMU ). Baada ya kuwatumia pesa hiyo, wakamwambia aripoti na fomu yake iliyojazwa, na kuambatanishwa na CV kwa HUMAN RESOURCES MANAGER wa Taasisi ya RafikiElimu Foundation, ( ( Ambaye kwenye barua hiyo walimtaja kama Mr. ALBERT EMMANUEL ) siku ya tarehe 28 FEBRUARI 2013 saa 5 kamili asubuhi.
Sisi kama taasisi, tulishangazwa sana na taarifa hii, kwa sababu kwanza, hatukutoa tangazo la aina hiyo, lakini pili huwa hatuwatozi watu pesa ili kuwatafutia nafasi za kujitolea. Tulifadhaishwa sana, na tukabaini kuwepo kwa utapeli unaofanywa na watu kwa jina letu, hivyo moja kwa moja tukaenda kuripoti tukio hili la uhalifu katika kituo kidogo cha polisi kilichopo katika kituo kidogo cha polisi cha Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam, sehemu ya Mlimani na kupewa RB namba UD/RB/849/2013 WIZI KWA NJIA YA MTANDAO.
Baada ya hapo, tukaenda kulitazama tangazo hilo katika mtandao wa Zoom Tanzania. Tangazo hili lililo wekwa mtandaoni mnamo siku ya tarehe 05 FEBRUARI 2013 lilisomeka kama ifuatavyo :
Volunteer program
Rafiki Foundation
Date Listed: Feb 5, 2013
Areas: Mbeya, Morogoro
Application Deadline: Feb 28, 2013
Position Description:
We are looking for Highly motivated individuals to volunteer in different private Organisation at the following places
1. Iringa (5) posts
2. Njombe (6) posts
3. Dar es salaam (7) posts
4. Mbeya (4) posts
5. Ruvuma (8) posts
6. Morogoro (3) posts
Application Instructions:
Candidates who are interested in such program must write the letter for inquire to the Email Link above then he/she will receive the NGO application form depending to his/her area of interest.
Note: the organisation will provide to you only field allowance when you are out of the office (Field areas), Transport, Tea and Lunch.
Late submission will not be considered.
UDHAIFU WA TANGAZO HILI:
i. Namba waliyo weka haipo ( IT DOES NOT EXIST )
ii. Wanasema " We are looking for Highly motivated individuals to volunteer in different private Organisation ........
( RafikiElimu Foundation, huwa hatu 'deal' na private organizations. Tuna deal na NON-GOVERNMENTAL ORGANIZATIONS ).
iii. Namba za simu walizo weka, hazipo kwenye blogu yetu.
iv. Katika tangazo lao, hakuna link inayo onyesha anuani ya blogu yetu.
v. Wametoa tangazo lao kwa lugha ya kiingereza, sisi kama RafikiElimu Foundation hatujawahi kutoa tangazo kwa lugha ya kiingereza.
vi. Kiingereza walicho tumia ni kibovu sana.
HATUA TULIYO CHUKUA BAADA YA KULIONA TANGAZO HILI NI KUUFAHAMISHA UONGOZI WA MTANDAO WA ZOOM TANZANIA, KUHUSU TANGAZO HILO LA KITAPELI ILI KUWANUSURU WANANCHI WENGINE ZAIDI NA TUNASHUKURU ZOOM TANZANIA WAMEPOKEA TAARIFA YETU NA KUAHIDI KULISHUGHULIKIA TATIZO HILO KWA KULIONDOA KATIKA TOVUTI YAO .
MAELEZO YA KWENYE FOMU YA MATAPELI HAWA
UDHAIFU WA FOMU HII :
1. Namba zao walizo zitoa kwenye fomu hizi za kitapeli, hazipatikani muda wote, wakati namba zetu zinapatikana muda wote.
2. Katika fomu yao ya kitapeli, hawajaandika location ya ofisi zilipo, hawajaweka sanduku la barua, blog adress wala namba za simu zinazo patikana.
3. Hakuna logo.
4. Hakuna sahihi.
5. Hakuna jina
6. Hakuna muhuri.
Tulipo jaribu kuwapigia kwa namba walizo ziweka kwenye mtandao ambazo ni +255 22 524 3785 tukajibiwa ya kwamba namba hizo hazipo ( the number your dialing are not existing ).
Na tulipo jaribu kuwapigia kwa namba 0763906931 nazo zikawa hazipatikani muda wote.
Taasisi yangu kwa kushirikiana na jeshi la polisi, tunafanya msako mkali dhidi ya mtu ama watu hawa na tunaahidi ya kwamba tutawakamata ndani ya muda ambao si mrefu sana na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
OMBI : Kama na wewe ni miongoni mwa walio tapeliwa na watu hawa, tafadhali wasiliana nasi kwa simu 0782405936 ili tushirikiane katika kuhakikisha wahalifu hawa wanatiwa mbaroni na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
TAMKO LETU : Tunalaani vikali kitendo kilicho fanywa na ama kinacho fanywa na wahalifu hawa, kwani mbali na kuiba pesa za watanzania masikini kama wao, kitendo hiki kinachafua jina la taasisi yetu ambayo inafanya kazi zake kwa kushirikiana na wananchi.
ANGALIZO KWA WANAO TAFUTA KAZI :
i. Unapo tuma maombi ya kazi katika sehemu yoyote ile halafu ukaambiwa utume pesa ili kupatiwa kazi hiyo, jua kwamba huo ni utapeli na kazi hiyo haipo.
ii. Hakikisha unazifahamu ofisi za taasisi hiyo zilipo kabla ya kuchukua maamuzi yoyote yanayo husisha pesa.
iiii. Ni vyema kufanya uchunguzi ili kujiridhisha kama taasisi hiyo kweli ipo.
iv. Unapoona tangazo la kazi, na kuvutiwa nalo, jitaidi kuwapigia simu walioweka tangazo na kuwauliza maswali mawili matatu kuhusu kazi hiyo.
HATA HIVYO : Ninashukuru, mpaka sasa ni mtu mmoja tu ndie aliyeripoti kutapeliwa na watu hao kwa jina la taasisi yetu. Hii ina maana kuwa watanzania wengi wameelimika kwa sasa, inawezekana watu wengine wali lishtukia tangazo hili na kuachana nalo.
ZINGATIA : Taarifa yoyote inayo husu taasisi ya RafikiElimu Foundation, lazima iripotiwe kwenye blogu yetu ambayo ni :
http://www.rafikielimu.blogspot.com// taarifa yoyote ile ambayo haijaripotiwa kwenye blogu yetu hii, haihusiani na taasisi yetu wala taasisi yetu haitawajibika kwa vyovyote vile na taarifa yetu.
Imetolewa na
UONGOZI,
RAFIKIELIMU FOUNDATION,
DAR ES SALAAM.
0782405936