Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

serikali yaitaka songea kuboresha makumbusho na vita vya maji maji.

$
0
0


Na Tulizo Kilaga, Ruvuma


Serikali imewataka wakazi wa mji wa Songea kushiriki kuboresha Makumbusho ya Vita vya Majimaji ili kukithi hadhi ya historia husika. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Bi. Eliwasa Maro alisema hayo wakati akijibu swali la mshiriki wa mdahalo wa Kumbukizi za Vita vya Majimaji, John Joseph Ulama aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuboresha makumbusho hayo. Bi. Maro alisema mikusanyo ya makumbusho hupatikana kwa njia ya wakazi wa eneo husika kujitolea. 

Aliongeza kuwa wanaojitolea hutakiwa kujua makusanyo hayo yalipotengenezwa, kazi yake, ilikuwa inatumika lini na sasa hivi inaweza kutumika kwa kazi gani na aliyetengeneza ni nani? “Kwa kuanzia mjukuu mmoja wa Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Chifu Gama, mke wa Dkt. Laurence Gama alimejitolea kuleta makusanyo, tunaomba mliobaki mtoe pia ili tuendeleze makumbusho haya kwa ajili ya historia yenu, kwani hata mkiziacha majumbani kwenu hakuna atayeweza kuzitunza vizuri kuliko makumbusho,” alisema Bi. Maro.

Aliongeza kuwa, Serikali iko tayari kushirikiana na wananchi pindi wanapohitaji makusanyo yao kwa ajili ya shughuli za kimila kwa kuwapa na kuyarudisha baada ya shughuli zao kuisha.


Naye, Mgeni rasmi katika mdahalo huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan M. Bendeyeko aliwataka wananchi kuwaenzi mashujaa wa Vita vya Majimaji kwa kulinda mila, tamaduni na rasilimali zinazopatikana kwenye maeneo yao kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.


Tamasha la Kumbukizi ya Mashujaa wa Vita ya Maji Maji  litafikia kilele Tarehe 27, Februari 2013 ambapo litafungwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki


kumekucha mwanamakuka awards 2013

JR & LK Investment Yaanzisha Tuzo ya Muziki wa Asili

$
0
0


Mkurugenzi wa JR & LK Investment, Mchatta Eric Mchatta (katikati) akizungumza na wanahabari, Pembeni ni Wajumbe wa Kamati hiyo, Kudra-Zake Bhukoli (kulia) na Lilian Kitunga (kushoto).

Na Thehabari.com 

KAMPUNI ya JR & LK Investment inatarajia kuzinduwa tuzo yake ya kwanza kwa wasanii wa Muziki wa Asili itakayojulikana kama 'Mwalimu Nyerere Tanzania Contemporary Traditional Muzic Awards' 

Tuzo hiyo inatarajia kuwakumbuka wasanii wa nyimbo za asili ambazo ndizo zinazobeba utamaduni wa Mtanzania, ambao umekuwa ukifunikwa na tamaduni za nje kwa muda.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa JR & LK Investment, Mchatta Eric Mchatta alisema kampuni hiyo tayari imepewa kibali na 
Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuendesha tuzo hizo.

Alisema kwa mara ya kwanza tuzo hizo zinatarajiwa kuanzishwa kwenye wiki ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  
itakayofanyika kuanzia Oktoba 11, 2013.

Aidha alisema tuzo hizo zina lengo la kuthamini na kuinua kazi za wasanii wa asili, kubadilisha tamaduni na kuheshimu wanamuziki wa asili Tanzania. 

"Mwalimu Nyerere katika siku za uhai wake aliwahi kusema; "Taifa bila tamaduni ni sawa na taifa lililo kufa, kwa kuzingatia usemi huo wa Mwalimu Nyerere, JR & LK Investment imedhamiria kwa dhati kuwainua wanamuziki wanao fanya muziki wa asili kwa njia ya kuwashindanisha kwa kupigiwa kura na wananchi...," alisema Mchatta. 

Alisema kwa sasa Tanzania imepoteza baadhi ya tamaduni, mila, na desturi zake na badala yake kufuata tamaduni za mabara mengine kama Ulaya na sehemu nyinginezo. "Tuzo za muziki asili za Mwalimu Nyerere zinalenga pia kuwaleta Watanzania wa kila rika, kabila, dini na wanaofanya kazi anuai kuungana na kujifunza uzuri na thamani ya kudumisha tamaduni...," alisema kiongozi huyo.

JR & LK Investment imewaomba Watanzania kukaa mkao wa kuunga mkono tuzo hizo ikiwa ni pamoja na wadau kujitokeza kufanikisha shughuli hiyo inayotarajia kuinua muziki wa asili nchini.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

Rais Kikwete akagua Ukumbi mpya Wa Mikutano wa Kimataifa jijini Dar leo.

$
0
0



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi mkubwa wa mikutano wa Julius Nyerere multi-purpose International conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam. Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali. Picha na Freddy Maro.
Sehemu ya jukwaa kuu
Nafasi za wajumbe wa mikutano
Viti
Upande wa juu

TIB na SIDO yasaini makubaliano ya kujenga maeneo ya viwanda

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) Bw. Peter Noni (wapili Kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO), Bw Michael Laizer, ambayo yanalenga ujenzi wa maeneo ya viwanda kwa wajasiliamali wadogo na wakati. Hafla iliyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni Mwanasheria na Katibu wa Bodi wa TIB Bi. Martha Maeda, na kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bulilo Mafwimbo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) Bw. Peter Noni (Kushoto) wakibalishana mawazo na Mkurugenzi wa Shirila la Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO), Bw Michael Laizer kabla ya kusaini hati ya makubaliano. Makubaliano hayo yanalengaujenzi wa maeneo ya viwanda kwa wajasiliamali wadogo na wakati. Hafla iliyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) Bw. Peter Noni (wapili Kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano na Mkurugenzi wa Shirila la Maendeleo ya Viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO), Bw Michael Laizer, ambayo yanalenga ujenzi wa maeneo ya viwanda kwa wajasiliamali wadogo na wakati. Hafla iliyofanyika jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

======

Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) imesaini makubaliano na shirila la maendeleo ya viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO) yenye lengo la kushirikiana kuweka miundombinu ya viwanda kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo. Mpango huu wa ushirikiano utawezesha ujenzi wa maeneo ya viwanda (industrial areas), ambao utaanza na mkoa wa Dar es Salaam, kabla ya kutanuka katika miji mingine.  

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo jana katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Peter Noni, alisema kuwa lengo ni kuwasaidia wajasiriamali kuweza kuzalisha bidhaa za viwandani.

“Hapa benki tumebaini kwamba kunamatatizo makubwa sana kwa mjasiriamali Mtanzania anapojaribu kuwekeza kwa ajili ya uzalishaji. Vita vya kuondoa umasikini nchini vinategemea uzalishaji. Uzalishaji pia unategemea uwezo wa kupata mikopo kutoka benki.

“Benki yetu ya Rasilimali Tanzania imekuwa ikiwafikia wajasiriamali ili kuwapa mikopo kwa ajili ya kuendeleza biashara zao, lakini wengi wao wanashindwa kufikia vigezo, vinayotokana na gharama kubwa inayohitajika ili kuwekeza katika kiwanda.

“Kwa hiyo, benki yetu kwa kushirikiana na SIDO tumeweza kupanga mkakati wa kuwawezesha wajasiriamali kuondokana na tatizo hilo. Tumekubaliana kuanza kushirikiana kutafuta maeneo ambayo tutayawekea miundombinu ya viwanda ambayo itawasaidia hawa wazalishaji wadogo wadogo kuja kukodi, hatua ambayo itawapunguzia gharama za uendeshaji.

“Huu utaratibu pia utamwezesha mjasiriamali huyu aweze kukopesheka na taasisi za kibenki, kwa sabau atakuwa na mahala maalum pa kuzalishia kwa gharama ndogo,” alisema Noni.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Michael Laizer alisema riba ya  mikopo inayotolewa na mabenki hapa nchini bado ni changamoto kwa wajasiriamali wadogo kwa sababu ni kubwa mno.

“Riba ya mikopo kutoka katika benki za kibiashara hapa nchini bado ni changamoto kwa wajasiriamali wadogo. Riba hizo zinawakwamisha wajasiriamali, zinawaruduisha nyuma na pia wanashindwa kupanua biashara zao,” alisema Bw Laizer.

Alisema ushirikiano wa SIDO na TIB utawasaidia wajasiriamali watakaoingia katika mpango huu kupata maeneo ya kuanza uzalishaji kwa gharama nafuu, alisema kuwa utakuwa ni mkombozi kwa wazalishaji wadogo wadogo nchini. “Tunashukuru uongozi wa TIB kukubali kushirikiana na SIDO katika kusaidia kuwapa maeneo ya kuzalishia bidhaa kwa wingi zaidi ambayo yatasaidia kuwaondolea umasikini na kusaidia kuondoa janga la ukosefu wa ajira nchini,” alisema Bw. Laizer.

WAFANYAKAZI WA AIRTEL WATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU SHULE YA MSINGI MSASANI

$
0
0
Msimamizi wa miradi kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Mubaraka Kibarabara akimkabithi mwalimu mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya Msasani Lessy Nyambo vitabu vya wanafunzi na vya walimu ikiwa ni sehemu ya shughuli zinazofanywa na wafanyakazi wa Airtel katika kusaidia shule za watoto wenye mahitaji maalumu.
Afisa Rasilimali watu wa Airtel Bi Doris Kibasa akikabithi vitabu kwa mwalimu mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya Msasani Lessy Nyambo mchango uliotolewa na wafanyakazi kwa watoto wa shule yenye mahitaji maalumu. wafanyakazi wa Airtel walitoa mchango huo walipotembelea shule ya msasani Jana
Afisa Rasilimali watu wa Airtel bi Monica Mbwilo vitabu kwa mwalimu mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya Msasani Lessy Nyambo mchango uliotolewa na wafanyakazi kwa watoto wa shule yenye mahitaji maalumu. wafanyakazi wa Airtel walitoa mchango huo walipotembelea shule ya msasani Jana.
watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya msasani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu ya mkononiya Airtel mara baada ya kupokea msaada wa vitabu kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo vilivyotolewa kwa ushirikiano wa wafanyakazi wa Airtel ili kusaidia ufundishaji wa masomo ya elimu kwa watoto wa mahitaji maalumu shuleni hapo

katika kuchangia shughuli za kijamii, wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkoni Airtel kwa pamoja wameshiriki katika kuchanga na kusaidia wanafunzi wa shule ya watoto wenye mahitaji maalumu iliyopo Msasani jijini Dar es salam.

Wafanyakazi hao wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 3 zilizotumika kununua vifaa mbali mbali vya kufundishia.

Akizungumzia mpango huo maalum wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo Afisa Rasilimali watu wa Airtel Bi Doris Kibasa alisema “mkakati huu umewahusisha wafanyakazi wa Airtel katika vitengo tofauti, ninawashukuru kwa kujipanga wao wenyewe na kutumia muda wao kwa kuwakumbuka watoto hawa kwa namna hii

Zoezi hili limewezesha upatikanaji wa jumla ya vitabu vyenye thamani shilingi milion 3 kwa shule ya msasani na kupunguza uhaba wa vitabu kutoka kitabu kimoja kwa watoto watatu hadi kitabu kimoja kwa kila mtoto mmoja.

“tumeona mahitaji ya wanafunzi hawa tulipotembelea shule hii mwishoni mwa mwaka jana. Na kuamua kujipanga ili kuweza kuwasaidi wadogo wetu na majirani zetu ili waweze kufika hapa tulipo sisi leo. Tunaamini kwa kufanya hivi tutakuwa tumeweza kuinua maisha ya watoto hawa na kiwango cha Elimu hapa Tanzania” alisisitiza Bi Doris

nae Mwalimu Mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalum Bw, Lessy Nyambo alisema msaada huo ni mkombozi kwa wanafunzi hao kwani utawawezesha wanafunzi hao kuwa na kitabu kimoja kimoja badala yakutumia kitabu kimoja wanafunzi wawili mpaka watatu. Amesema kwamba wanafunzi hao wanakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi vitakavyowawezesha kuendelea na masomo bila tatizo lolote na hivyo amewahasa mashirika ya umma na wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali katika kusaidia shule za watoto wenye mahitaji maalumu.

Nae mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Msasani Fatuma Ally aliishukuru Airtel kwa kuweza kuwapatia Vitabu ambavyo vitaweza kuwasaidia katika masomo yako.

Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu imedhamiria kuendelea kuboresh kiwango cha elimu nchi na kuleta mabadiliko katika masomo ya sayansi ili kupata wataalamu wengi wasayansi nchini.

Wiki mbili zilizopita tumetoa msaada wa Vitabu na sare za shule katika shule ya msingi ya Kiromo iliyopo mjini Bagamoyo vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 , huku ikitoa msaada wa vitabu kwa shule 4 za sekondari kwa kila mkoa ikiwemo mikoa ya Kagera na Mwanza Lengo ni kufikia shule nyingi zaidi nchini Nzima

MSD YAWEKA WAZI WANAOWALINDA WANAOTOROSHA DAWA NJE YA NCHI

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani akielezea kuhusu utendaji wa bohari hiyo pamoja na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo, zikiwemo za vyombo vya dola kuwafumbia macho baadhi ya wafanyabiashara wanaouza dawa za serikali kiholela pamoja na wanaokamatwa kwa kutorosha dawa hizo nje ya nchi. Taasisi zilizomwagiwa lawama hizo ni baadhi ya maofisa kutoka vyombo vya dola, serikalini na wafanyabiashara. Mwaifwani alidokeza hayo wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti z\ilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini.
 Meneja wa Ufuatliaji wa Mipango Kazi na Mpango Mkakati wa Bohari ya Dawa (MSD),  Cosmas Nalimi akielezea jinsi MSD ilivyojidhatiti kuboresha huduma nchini, wakati wa Kongamano la Nane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) la kujadili tafiti zilizofanywa na wanahabari kuhusu matumizi ya fedha zinazochangwa na wananchi kwa ajli ya masuala ya afya katika halmashauri 26 nchini. Kongamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Mtwara. Baadhi ya dawa za msd inadaiwa zinauzwa nje ya nchi ikiwemo Cameroon.
Msajili wa Baraza la Pharmacy Tanzania, Dk. Midred Kinyara, akielezea mikakati ya usajili wa maduka ya dawa  baridi vijijini wakati wa kongamano hilo.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

MWENYEKITI WA WAMA MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 700 KWA HOSPITALI KUU YA MKOA WA RUKWA

$
0
0
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dr. John Gurisha orodha ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.2.2013 hospitalini hapo. Vifaa hivyo vimeletwa nchini na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka Marekani na vina thamani ya shilingi milioni mia saba.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dr. John Gurisha moja ya vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.2.2013. Baadhi ya vifaa hivyo ni mashine za Ulta Sound, X-Ray, Upasuaji, tiba ya macho, tiba ya kinywa na meno, mgongo, mifupa, mashine ya dawa za usingizi, vitanda maalum (TCU beds) n.k. Kushoto anaeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. 
Baadhi ya vifaa tiba alivyokabidhi Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete vikiwa na thamani ya shilingi milioni mia saba. Vifaa hivo pamoja na vingine ambavyo bado vipo kwenye kontena vimeletwa nchini na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka Marekani. 
Mama Salma Kikwete akiongea na wadau wa sekta ya afya na wananchi waliokusanyika katika viwanja vya hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimkaribisha Mama Salma Kikwete kuzungumza na wadau wa afya katika viwanja vya hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa ambapo alikabidhi vifaa tiba kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba. Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Mama Salma kwa jitihada anazozifanya yeye na taasisi yake katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha huduma za afya nchini, alimuhakikishia kuwa Serikali yake ya Mkoa itahakikisha inasimamia vizuri sekta ya afya kutimiza ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2010-2015 ambazo ni pamoja na kuimarisha huduma za afya nchini. 
Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daudi Nasib akielezea kwa kifupi kazi na majukumu ya taasisi hiyo kwa wadau wa afya waliohudhuria hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa tiba kutoka WAMA kwa uongozi wa hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa. Miongoni mwa malengo makuu ya taasisi hiyo ni kuimarisha afya ya mama na mtoto na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma ya afya nchini. 
 Ndugu Abdul Kimario wa shirika laProject C.U.R.E kutoka Marekani ambae shirika lake limeshirikiana na WAMA kuleta vifaa tiba hivyo hapa nchini akitoa ufafanuzi wa matumizi ya baadhi ya vifaa hivyo kwa wadau wa afya waliokusanyika kushuhudia makabidhiano hayo. 
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mzee Protas Kimario kitambulisho cha matibabu ya uzeeni kuwakilisha wazee wengine 458 zoezi lililoenda sambamba na kukabidhi vifaa vya tiba kwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa tarehe 26.02.2013. Jumla ya vitambulisho 4356 sawa na asilimia 96% katika Manispaa ya Sumbawanga vimeshatengenezwa kwa ajili ya matibabu ya wazee. 
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta funguo za pikipiki kwa ajili ya vituo vya afya vya Wilaya hiyo katika jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). Jumla ya Pikipiki kumi kutoka Water Rid zilikabidhiwa kwa ajili ya huduma hizo katika Mikoa ya Rukwa na Katavi. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

UFUNGUZI WA WARSHA YA WADAU KUJADILI MWONGOZO WA KITAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI JUU YA WAKULIMA NA WAFUGAJI NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula akiwa katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa Warsha ya Kupitia na Kujadili Muongozo wa Kitaifa wa Mabadiliko ya tabianchi juu ya Wakulima na Wafugaji Nchini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula akifungua Warsha ya Wadau ya Kupitia na Kujidili Muongozo wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Tabianchi juu ya Wakulima na Wafugaji Nchini Kulia Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Julias Nihgu Warsha imefanyika kwenye Hotel ya Palmtree Village Bagamoyo. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Sazi Salula akimsikiliza jambo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Raisi Bw Richad Muyungi mara Baada ya Ufunguzi waWarsha ya Wadau wakupitia na Kujadili Muongozo wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Tabianchi juu ya Wakulima na Wafugaji Nchini.
Mkurugenzi Msaidizi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Richad Muyungi akimwambia jambo Afisa Mazingira Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw Daniel Nkondola Mara baada ya Ufunguzi wa Warsha ya Wadau wa Kujidili Muongozo wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Tabianchi juu ya Wakulima na Wafugaji Nchini Warsha imefanyika Hotel ya Palmtree Village [Picha na Ali Meja].

===============   =========  ==========
Monica Sapanjo- Ofisi ya Makamu wa Rais


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Sazi Salula amewataka wadau wa sekta ya kilimo  nchini hasa wakulima wadogo wadogo  kujitahidi  kufahamu athari  na  changamoto mbalilmbali zinazoikabili sekta hii kutokana na athari za  mabadiliko ya tabianchi. Alitoa rai hiyo wakati akifungua warsha ya siku mbili  ya kitaifa ikihusisha wadau mbalimbali kuandaa  mwongozo wa taarifa za kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa  jamii za wakulima na wafugaji nchini.

Aliwaomba wajumbe wa warsha hiyo kutoa maoni yao ya kitaalamu ili kuhakikisha   mwongozo unakuwa tayari kwa matumizi ya jamii za wakulima na wafugaji nchini mapema iwezekanavyo hasa ikinzingatiwa kuwa athari sasa zimeanza kuwa kubwa sana. Alisema  mwongozo huu  ni muendelezo wa juhudi za serikali katika kushughulikia masuala ya mabadiliko ya tabianchi. "Juhudi hizi zitaiwezesha nchi kuhimili atahari za mabadiliko haya na kuchangia juhudi za kimataifa za kupunguza gesijoto" alisema Bwana Salula.

Warsha hiyo ya siku mbili imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ufadhili wa Serikali ya Japana kupitia UNDP,  kwa ajili ya kujadili mwomgozo huu wa kusaidia wakulima na wafugaji wadogo wadogo kuhimili  mabadiliko ya tabianchi. Washirki wa warsha hiyo  ni kutoka kwenye taasisi  mbalimbali  ikiwa ni pamoja na  Ofisi ya Waziri mkuu, Wizara ya maji, Wizara ya habari na michezo, Wizara ya kilimo na baraza la Mazingira la Taifa(NEMC, Jumuia ya Wakulima Tanzanaia na asasi mbalimbali zisizo za kiserikali.

Madhumuni ya mwongozo huu ni kuwasaidia wakulima na wafugaji  kuendeleza shughuli zao za ufugaji na ukulima katika maeneora ambayo yamebadilika kutokana na mabadiliko ya tabianchi.


MBUNGE WA VITI MAALUM,DKT MARY MWANJELWA AZIINDUA ALBAMU YA VIDEO NA AUDIO YA UPENDO MWANTIMWA.

$
0
0

DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AZINDUA ALBAMU YA VIDEO NA AUDIO YA UPENDO MWANTIMWA NA KUMCHANGIA KIASI CHA SHILINGI MILIONI MOJA KWA AJILI YA KUNUNULIA VYOMBO VYA MUZIKI.

DK MARY MWANJELWA MARA BAADA YA UZINDUZI WA ALBAMU YA YESU YUAJA AKIONYESHA DVD HIYO KWA WAALIKWA WENGINE KUJA KUMCHANGIA UPENDO MWANTIMWA ILI APATE HELA YA KUNUNULIA VYOMBO VYA MUZIKI KWA AJILI YA KUENEZA NENO LA MUNGU. VYOMBO HIVYO VINAGHARIMU KIASI CHA SHILINGI MILIONI 10 MWESHIMIWA DK MARY MWANJELWA AMEMCHANGIA UPENDO KIASI CHA MILIONI MOJA NA AMEAHIDI KUENDELEA KUMCHANGIA .
DK MARY MWANJELWA AKIMKABIDHI UPENDO MWANTIMWA  SHILINGI MILIONI 1 KAMA MCHANGO WAKE WA KWA AJILI YA KUNUNULIA VYOMBO VYA MUZIKI.KWA PICHA ZAIDI YA TUKIO HILI BOFYA http://mbeyayetu.blogspot.com

UWF PRESENTS MWANAMAKUKA AWARDS 2013

BOHARI YA DAWA (MSD) YAONESHA VIFAA TIBA VYA KISASA KATIKA MAONESHO YA WADAU WA HUDUMA ZA AFYA KUSINI MWA AFRIKA

$
0
0
 Ofisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD),Florida Sianga (kulia)) akiwaelekeza Monica Gofrey (kushoto) na Geofrey Kandi kifaa tiba aina ya sterilizer inayotumia gesi katika maonesho ya Shirikisho la Wadau wa Huduma za Afya Kusini Mwa Afrika, leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. (PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
                                              Wageni hao wakiendelea kupata maelezo
 Kitanda cha wagonjwa ambacho ni baadhi ya vifaa tiba vinavouzwa na MSD
                                              Kifaa Tiba aina ya kitasishaji 'Starilizer' inayotumia gesi
                                                                 Kitanda cha kujifungulia
 Kabati la kusambazia dawa wodini 'Dispensing Trolley'
                                           Banda la MSD linavyoonekana kwenye maonesho hayo


clouds Fm yanyakua tuzo ya ubora (superbrands) mara ya tatu mfululizo.

$
0
0
Mkurugenzi wa Mradi Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer akimkabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa. Joseph Kusaga mara baada ya Clouds Fm Radio kuibuka na tuzo hiyo ya Superbrand kwa mara ya tatu mfululizo. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu (kati) pamoja na Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrands Afrika Mashariki, Bw Jawad Jaffer kwa pamoja wakimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga kwa Couds Fm redio kuibuka na tuzo hiyo ya ubora kwa mara ya tatu mfululizo. Tukio hilo lilifanyika hivi karibuni katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

KWANINI UFUBAE,NJOO @AK CLASSIC TUKUNG'ARISHE NA OTENTIKA!!

$
0
0

   HII NI SET NZIMA YA BIDHAA ZA OTENTIKA KWA NGOZI KAVU(DRY SKIN) AMBAYO INAJUMUISHA SABUNI,SERUM,LOTION YA MWILINI,CREAM YA USONI.MARA NYINGI ILI KUPATA MATOKEO MAZURI UNASHAURIWA KUTUMIA ZOTE,INGAWA KULINGANA NA UWEZO WA MFUKO UNAWEZA KUTUMIA KIMOJA KIMOJA INARUHUSIWA PIA.

 HII NI SET YA BIDHAA ZA OTENTIKA KWA WATUMIAJI WENYE NGOZI YA KAWAIDA(NORMAL SKIN) AMBAYO MJUMUISHOWA WAKE NI KAMA ULIVYOBAINISHWA HAPO JUU ISIPOKUWA TU HIZI NI KWA WATU WENYE NGOZI YA MCHANGANYIKO.


WALE WATAAALAM WA KUIWEKA NGOZI YAKO SAWIA  @AK CLASSIC COSMETICS LEO WANAKULETEA BIDHAA ZA OTENTIKA!!HIZI NI BIDHAA ZENYE UBORA WA KIPEKEE KUTOKA SWITZERLAND,BIDHAA ZA OTENTIKA TOFAUTI NA BIDHAAA ZINGINE KILA MTUMIAJI ANATUMIA BIDHAA INAYOENDANA NA AINA YA NGOZI YAKE(KAMA NI YA MAFUTA SANA AU KAVU),NI BIDHAA AMBAZO ZIMEKUBALIKA SANA..KWANI HAZICHUBUI NGOZI,ZAIDI HUSAIDIA KUONDOA MABAKA,HARARA NA KUBWA ZAIDI HUIFANYA NGOZI YAKO ING'AE(GLOW) NA KUWA RANGI MOJA NA KUBAKI YENYE MUONEKANO WA KUVUTIA,WENGI WALIOITUMIA BIDHAA HIZI WAMEZIKUBALI,WEWE JE UNANGOJA NINI?
   KWA MAELEZO  ZAIDI INGIA www.akclassic.blogspot.com au wapigie 0713468393/0753482909.

SAUDI ARABIA'S PRINCE AMR AL FAISAL VISITS EXIM BANK

$
0
0
 Saudi Arabia’s Prince Amr Al Faisal (left) explains a point to the Exim Bank Tanzania Chief Executive Officer Dinesh Arora (right) during a visit to the bank’s headquarters in Dar es Salaam yesterday. Looking on at the centre is the Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant
 The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (left) explains a point to Saudi Arabia’s Prince Amr Al Faisal (right) who paid a visit at the bank’s headquarters in Dar es Salaam yesterday. Centre is the Sudanese ambassador Dr. Yassir Ali who was part of the delegation
 The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (left) shares a word with the Sudanese Ambassador Dr. Yassir Ali (right) during a visit by Saudi Arabia’s Prince Amr Al Faisal (not in photo) yesterday
 YOU’RE WELCOME: The Saudi Arabia’s Prince Amr Al Faisal (left) receives a bouquet of flowers during a visit to the bank’s headquarters in Dar es Salaam yesterday. Looking on at the right is the Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant
 TheSaudi Arabia’s Prince Amr Al Faisal (right) signs a visitor’s book during a visit at Exim Bank yesterday.
 
 Saudi Arabia’s Prince Amr Al Faisal (centre) poses for a group photo with some of Exim Bank Management staff and members of his delegation
 TheSaudi Arabia’s Prince Amr Al Faisal (right) gets a spectacular view of Dar es Salaam city from Exim Tower during a visit at Exim Bank yesterday. Second left is the Exim Bank Tanzania Chief Executive Officer Dinesh Arora.
Saudi Arabia’s Prince Amr Al Faisal (left) receives a gift from one of Exim Bank staff

Mwanza, Dodoma zachomoza Tamasha la Pasaka

$
0
0



"MIKOA ya Mbeya na Dodoma imechomoza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka 2013", Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa kuongezwa kwa mikoa hiyo kunaifanya idadi ya mikoa ambayo tamasha hilo litafanyika kwa mwaka huu kufikia mitano.

Msama alisema baada ya Tamasha la Pasaka kufanyika Dar es Salaam Machi 31, siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, kisha Aprili 2 ni Uwanja wa Samora Irringa. “Aprili 6 itakuwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Hiyo ni mikoa ambayo mashabiki wameipigia kura kwa kiasi kikubwa tamasha lifanyike maeneo hayo.

“Tunaamini mashabiki wetu watapata  fursa nzuri ya kufurahia tamasha hilo, ambalo mwaka huu tumepanga mikoa saba tutumbuize, lakini bado tunaangalia mikoa mingine miwili,” alisema Msama katika taarifa hiyo na kuongeza kuwa kamati yake ilikuwa ikiendesha kura za maoni kwa mashabiki wachague tamasha hilo lifanyike wapi mwaka huu na kuwa mikoa hiyo ndiyo iliyopendekezwa zaidi.

Wakati huohuo, Msama alisema baadhi ya wasanii tayari ameanza kumalizana nao kwa ajili ya tamasha hilo na kuwa wakati wowote kuanzia leo wataanza kutangazwa rasmi.

Tamasha la mwaka jana lililofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kasha Uwanja wa Jamhuri Dodoma baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

Zawadi za Mashindano ya Mpinga Cup zatangazwa

$
0
0
Kiongozi mkuu  maandalizi ya Mashindano ya Mpinga Cup ametangaza zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa timu zitakazoshiriki katika michuano ya Mpinga Cup inayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodabado wa jijini dar esa saalam yanayotegemea kufanyika leo katika viwanja vya Oysterbay police kwa muda wa wiki moja.

Akitangaza zawadi hizo ASP Emilian Kamwanda ambaye ni msaidizi Mwandamizi wa polisi na Kiongozi wa maandalizi ya michuano ya mpinga cup alisema” leo tunayo furaha kutangaza zawadi mbalimbali za washindi katika mashindano hayo ambayo yana lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikiki (bodaboda). Na zawadi hizi ziko kama ifuatavyo.

Mshindi wa kwanza atapata Kombe, Pesa taslimu shilingi million moja, jezi  set moja, kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1, mshindi wa pili atapata pesa taslimu shilingi laki tano, jezi seti moja , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1 na mshindi wa tatu atapata  pesa taslimu shilingi laki tatu, , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1,Aidha zawadi zitatolewa kwa Mchezaji bora na Goalkeeper bora ambapo  kila mmoja atapata  pesa taslimu shilingi laki moja,  vocha za kufanya manunuzi Mr Price zenye thamani ya Laki moja na kofia ngumu (helmet) 1.Timu tano zitakazoshindwa pia hazitaondoka hivihivi , zitazawadiwa kila moja mipra na kofia ngumu Helmet.

Mashindano ya Mpinga Cup yameandaliwa na Jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel, Rotary club, Mr.Price, Home Shopping Center  pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ili kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya sheria mbalimbali za usalama , kuimarisha uelewa wao wa matumizi ya barabara kwa lengo la kuendelea kudhibiti  ajali za barabarani pamoja na elimu ya Polisi jamii.

Mashindano haya yanatarajiwa kutimua mbio kuanzia tarehe leo katika viwanja vya Polisi Oysterbey   kwa kushirikisha timu 8 za waendesha pikipiki. Mpinga Cup itaendelea katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala na Temeke na hatimaye kutafuta mshindi wa mkoa wa Dsm.

Tigo yaboresha huduma za mawasiliano na KABAANG!

$
0
0
Meneja Chapa ya Tigo bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya  kifurushi cha KABAANG kwa ajili ya wateja wao.kulia ni bi. Jacqueline Nnunduma Mtaalam wa ubunifu wa ofa za Tigo.
Mbunifu wa ofa za Tigo bi. Jacqueline Nnunduma akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya kifurushi cha KABAANG.kushoto bw. William Mpinga Meneja Chapa ya Tigo.
Mshindi wa Tigo smartcard promotion bw. Julius Raphael Kanza akiwa uwanja wa ndege J.K Nyerere akiongea na waandishi wa habari kabla ya safari yake ya kuelekea Madrid nchini Hispania kutazama mechi kati Real Madrid na Fc Barcelona jumamosi wiki hii itakayofanyika kwenye uwanja Santiago Bernabeu.

Tigo Tanzania imezindua bidhaa mpya ijulikanayo kama "KABAANG" ambayo itawapa wateja wake fursa ya kupata muda wa maongezi wa bure, kifurushi cha intanet na ujumbe mfupi bila kikomo kwa kujumuisha huduma hizi kuu tatu kwenye kifurushi kimoja.

“KABAANG” ni kifurushi cha wiki ambacho mteja akijiunga anapata dakika 300 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao wowote ule, anapata kifurushi cha intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi bila kikomo.

" Tuliona kuna haja kubwa sana ya kuzindua bidhaa itakayohusisha mahitaji mbalimbali ya wateja wetu kwenye kifurushi kimoja cha bei nafuu na kitakachowapatia wateja matumizi mbalimbali. 

Kifurushi hiki cha wiki kinamruhusu mteja kutumia huduma mchanganyiko ipasavyo na kwa bei nafuu kabisa na kitawafaa sana wajasiriamali na waajiriwa wa mashirika mbalimbali kwani kitawawezesha kuwasiliana kwa simu, sms na barua pepe muda wowote wakati wakiendelea na mambo mengine kwa shilingi 9000 tu wateja wa Tigo wanapata huduma nyingi na bora zaidi ” alisema Ndg. William Mpinga, Meneja wa chapa ya Tigo.

Ndg. Mpinga aliendelea kwa kusema " kwa kutumia KABAANG wateja wetu wataweza kuwasiliana vizuri zaidi kwani itapunguza mzigo wa uhitaji wao wa kutaka kuwasiliana kila wakati kwani inawapatia bidhaa iliyojumuisha mahitaji yao makuu ya mawasiliano kikazi na kwenye biashara. Mteja anahitaji laini moja tu ya simu kufurahia bidhaa hii bora kutoka Tigo".

Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi atume neno "Kabaang" kwenda 15711, na baada ya hapo atapata ujumbe wa kuadhimisha kujiunga na kuweza kutumia kifurushi. Kabaang inapatikana kwa wateja wote wa Tigo wenye simu zinazotumia intaneti na kinagharimu shilingi 9,000 tu kwa wiki.

kumekucha....!

Waziri Muhongo atembelea Makao Makuu ya Kampuni ya BG Group, Reading - UK

$
0
0


Mh waziri Muhongo akisalimia na CEO wa BG Chris.
Mh waziri Muhongo akisalimia na CEO wa BG Chris katika picha ya pamoja na ujumbe wake na wa kampuni hiyo.
======  ======  ======

Urban Pulse Creative inakuletea picha ya ziara ya Mh waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alipotembelea makao makuu kampuni ya BG Group inayofanya kazi ya uchimbaji wa gesi na mafuta ili kuangalia ufanisi wake na jinsi gani itakavyoweza kutunufaisha sisi watanzania kama ikipewa fursa ya kuwekeza nchini kwetu. 

BG group ni mojawapo ya kampuni kubwa duniani inayoongoza katika uchimbaji, utunzaji, usambazaji wa gesi asilia.Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996 BG Group imeweza kujiimarisha zaidi kwa kujijengea uzoefu mkubwa na historia nzuri katika sekta hii nyeti ya nishati. Pamoja na kuwa makao yake makuu yakiwa mjini Reading nchini Uingereza vilevile kampuni hii ishafanya kazi katika nchi ishirini duniani ndani ya mabara matano tofauti ikiwa na wafanyakazi zaidi ya elfu sita kutoka mataifa mbalimbali duniani. 

Katika ziara hii Mh waziri Muhungo aliambatana na Mh Balozi wetu Peter Kallaghe, Mr Sosthenes Masau Bigambo Massola, Dr Athanas Simon Macheyeki (Geological Survey Tanzania), Mr Seleman Hatibu Chombo ( Idara ya Nishati na Madini Tanzania) na Mr Bikash Dawahoo mwakilishi kutoka Ubalozi wa Uingereza Tanzania
 Makao makuu ya Kampuni ya BG
 Mh Waziri Profesa Muhongo akipokea maelezo kutoka kwa injinia wa BG Group
 Control room ya BG Group
Mh Waziri akifuatilia maelezo kutoka kwa msemaji wa kampuni ya BG ambapo ramani inaonesha live shughuli zainazoendelea katika visima vya gesi inayochimba nchini Tanzania
Mh Waziri akitembelea makao makuu ya BG Group
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>