Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 372 | 373 | (Page 374) | 375 | 376 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandara akifungua mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaofanyika katika hoteli ya Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar Es salaam ukiwashirikisha watafiti na wanamazingira kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania.
  Mkurugenzi wa kituo cha mafunzo ya mabadiliko ya tabianchi cha chuo kikuu cha Dar Es Salaam Profesa Pius Yanda akiwasilisha mada katika mkutano huo.
  Profesa Mukandara akijadiliana na wataalam wanaoshiriki kwenye mkutano huo muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika Kunduchi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
  Wataalam wa mazingira na watafiti kutoka vyuo vikuu mbalimbali kikiwemo cho kikuu cha Dar es salaam na wadau wengine wa mazingira wanaohudhuria mkutano huo wa mabadiliko ya tabianchi katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Profesa Rwekaza Mukandara muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano huo.Picha zote na Vedasto Msungu.

  0 0

   Jengo la gorofa 8 lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.9 lililojengwa na wakala wa Majengo Tanazania (TBA) Katika neneo la Ada Estate Kinondoni Jijini Dar es salaam ambalo litapangishwa kwa watumishi wa umma mara litakapokamilika mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni moja ya hatua za Serikali kutatua tatizo la makazi kwa watumishi wa umma.

   Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa mbele ya  moja ya nyumba za Majaji zinazojengwa na TBA wakati wa ziara yao katika  eneo la masaki jijini Dar es salaam  ili kujionea hatua iliyofikiwa katika  miradi inayotekelezwa na wakala huo,  ambapo wakalo huo unajenga nyumba mbili kila Mkoa ili kukabliana na tatizo la makazi kwa Majaji hapa nchini.

   Mhandisi Edwin Nnunduma  toka  wakala wa amajengo Tanzania (TBA)akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba  mbili zinajengwa katika kila mkoa kwa ajili ya makazi ya majaji wakati wa ziara ya waandishi hao iliyolenga kujionea hatua  iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.

   Moja ya jengo la kisasa lenye gorofa 4lililopo Mbezi beach Dar es salam litakalopangishwa kwa watumishi wa Umma,jengo hilo liko katika hatua za mwisho kabla kuanza kupangishwa  ili kupunguza tatizo la makazi kwa watumishi hao.


   Mhandisi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Edwin Nnunduma  akiwaongoza waandishi wa habari kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba zaidi ya 150 zinazjengwa katika eneo la Mabwe Pande Jijini Dar es salaam ambapo nyumba hizo zitauzwa kwa watumishi wa umma.

   Mafundi wakiendelea na ujenzi katika mradi wa nyumba zaidi ya 150 zinazojengwa na TBA ambapo nyumba hizo zitauzwa kwa watumishi wa umma ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuondoa tatizo la makazi kwa watumishi hao.

   Mhandisi Edwin Nnunduma  toka  wakala wa amajengo Tanzania (TBA) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu lengo la mradi wa nyumba zaidi ya 150 katika eneo la mabwe pande ambapo nyumba hizo zitauzwa kwa watumishi wa umma ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali kupitia wakala huo kujenga nyumba 10,000.

   Sehemu ya nyumba 150 zitakazouzwa kwa watumishi wa umma  ambapo mradi wa ujenzi wake unatekelezwa na TBA katika eneo la mabwe pande jijini Dar es salaam . .(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)  0 0

   Bondia Nasibu Ramadhani Kushoto akitunishiana misuli na Mohamed Matumla baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho jumamosi september 27 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam .
  Mratibu wa mpambano wa ngumi Ibrahimu Kamwe katikati akiwangalia mabondia wa kike Lulu Kayage kushoto na Fatuma Yazidu wanavyo tunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao.
  Lulu Kayage na Fatuma Yazidu wakitambiana baada ya kupima uzito
  Bondia Nassibu Ramadhani akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Mohamedi Matumla  Mohamed Matumla akipima uzito
  Bondia Nassibu Ramadhani na Mohamed Matumla wakinuliwa mikono juu na Mratibu wa mpambano huo Ibrahimu Kamwe katikati  mpambano utakaofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Frends Corner Manzese picha na SUPER D BLOG
  Bondia Juma Fundi na Issa Omari wakinuliwa mikono juu na Mratibu wa mpambano huo Ibrahimu Kamwe katikati  mpambano utakaofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Frends Corner Manzese picha na SUPER D BLOG
  Bondia Lulu Kayage akipimwa na Daktali baada ya kupima uzito kushoto ni m,pinzani wake Fatuma Yazidu

  0 0

  Mhandishi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Valentine Kayombo akiwaeleza waandishi wa Habari(Hawapo pichani) faida zitakazopatikana kutokana na kukamilika kwa Kituo hicho ikiwamo kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za uongozaji ndege, wakati wa Mkutano Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka Hiyo Bi. Bestina Magutu. 
  Inspeka Mwandamizi Idara ya Udhibiti Usalama wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Redemptus Bugumula akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu ongezeko la marubani wanawake nchini ambao wanafikia Takribani Kumi kwa sasa wakati wa Mkutano Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mhandisi Mkuu toka Mamlaka Hiyo Bi.Valentine Kayombo.

    Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Bestina Magutu akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kukamilika kwa maboresho ya kituo cha Mawasiliano ya Radio kwa ajili ya usafiri wa anga kilichopo Mnyusi mkoani Tanga, kilichojengwa na kampuni ya JATRON ya Norway, wakati wa Mkutano Uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mhandisi Mkuu toka Mamlaka Hiyo Bi. Valentine Kayombo.Picha na Hassan Silayo-MAELEZO.  0 0

   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete greets  The Vice President of the World Bank Africa Region Mr.Makhtar Diop in New York in the sidelines of the 69th UN General Assembly  
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete holds talks  with The Vice President of the World Bank Africa Region Mr.Makhtar Diop
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete  talks with  Mr.Michael Bloomberg, former mayor of New York City in his capacity as a United Nation’s Secretary General’s Special envoy for Cities and Climate change at the UN Headquarters in New York. Photos by Freddy Maro
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete  talks with  Mr.Michael Bloomberg, former mayor of New York City in his capacity as a United Nation’s Secretary General’s Special envoy for Cities and Climate change at the UN Headquarters in New York. Photos by Freddy Maro

  0 0

  Kamati ya maandalizi ya bonanza la kusherehekea miaka minne ya ukurasa wa Kandanda katika Facebook (Kandanda Facebook Group) , unawakaribisha wanahabari wote katika mgahawa wa City Sport Lounge, Posta, Dar es Salaam, siku ya Jumapili saa nne asubuhi.

  Mkutano huo wa wanahabari; lengo lake kuu ni kupokea udhamini kutoka kwa mdau wa kandanda nchini na mfanyabiashara , Nassor Bin Slum, pamoja na kuelezea matukio yatakayofanyika siku hiyo ya bonanza.

  Kwahiyo, kamati inawakaribisha wanahabari wote kujumuika na familia ya kubwa Kandanda katika mkutano huo pamoja na kuanza safari ya kuelekea siku hiyo ya tukio hilo Oktoba 25 mwaka huu.


  Kwa niaba ya kamati ya maandalizi, nachukua fursa hii tena kuwakaribisha wadau (Wanahabari)kuja kushuhudia tukio hilo la kihistoria nchini kwa wadau wa Kandanda waliokutana mtandaoni kutengeneza timu na kushindana.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi
  Patoo

  Kandanda 4th Anniversary.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Cleopa Msuya akifafanua jambo, wakati akizungumza na wana hisa wa kampuni hiyo, wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka, uliofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Bw. Roberto Jarrin na Kampuni wa Kampuni hiyo, Bw. Huruma Ntahema.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Cleopa Msuya akifafanua jambo, alipozungumza na wana hisa wa kampuni hiyo, wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka, uliofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Bw. Roberto Jarrin. (Na Mpigapicha Wetu)
   Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin (kulia), akitata jambo na Maofisa wa shirika hilo, Mkurugenzi wa Afrika Mashariki, Bw. Mario Van Gelden (kushoto) na Mkurugenzi wa Rasilimari watu, Bw. David Magese, wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wana hisa, uliofanyika Dar es Salaam
   Mkurugenzi akibadilishana mawazo na baadhi ya wanahisa wa TBL
   Msuya akibadilishana mawazo na viongozi wa TBL WAKATI WA MKUTANO HUO
   Baadhi ya wanahisa wakiwa katika mkutano huo
   Mmoja wa wanahisa akiuliza swali katika mkutano huo
   Mwanahisa akiuliza swali katika kijiji hicho
   Meza kuu
   Wanahisa  0 0

  ILE Filamu kubwa kabisa kutengenezwa katika viunga vya Tanzania ya Tmt movie imeanza maandalizi yake kwa kurekodi filamu mpya huku wasanii waliopatikana kutokana na shindano la Tanzania Movie Talent kuibeba sinema hiyo wakiwashirikisha wasanii wengine waliochaguliwa katika sinema hiyo.

  Akiongea na FC mratibu wa filamu hiyo Staford Kihore amesema kuwa moja ya malengo makubwa ya Proin Promotion ni kuwajenga wasanii wa filamu na kuwapa uwezo wa kuigiza na kufanya kazi kimataifa, katika kuwasimamia wameanza nao kurekodi sinema TMT Movie.

  “Tasnia ipo na inafanya vizuri lakini inahitaji uthubutu kwa kati ya wanaotengeneza sinema wawe tayari kufanya kitu kizuri kinachoweza kuvuka mipaka ndio tunachokifanya sasa baada ya kuwatengeneza kitaaluma wanafanya kazi,”anasema Staford.

  Wasanii wa TMT wamefundishwa na kuiva katika fani ya uigizaji na moja ya alama yao wanayojivunia ni pale ambapo wamepewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao kupitia filamu ya TMT Movie na kuonyesha kile wanachoongea kwa watazamaji na wapenzi wa filamu Swahilihood.

  Filamu kubwa ya Tmt Movie inatarajiwa kuonyeshwa katika majumba ya Sinema Afrika Mashariki na Ulaya pia sinema inaongozwa na Muongozaji mahiri wa filamu Karabani na imeandikwa na Novatus Mgulusi ‘Ras Nova’ zaidi ya wasanii 200 kushiriki katika filamu hiyo.

  Sterring wa sinema hiyo ni milionia wa kutoka Mtwara Mwanaafa Mwizango na nyota wote wa TMT, huku wasanii nyota kibao kutoka tasnia ya filamu Bongo wakipatia nafasi za ushiriki wa filamu hiyo inayojenga ajira kwa jamii nzima.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA NISHATI NA MADINI


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  UENDELEZAJI WA MRADI WA KUUNGANISHA GRIDI ZA UMEME ZA ZAMBIA-TANZANIA NA KENYA (ZTK)

  Napenda kuwajulisha kwamba Wizara ya Nishati na Madini itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Nishati wa wa nchi za Zambia, Kenya na Tanzania unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Septemba, 2014 ambapo Wizara ya Nishati na Madini itakuwa mwenyeji wa mkutano huo utakaofanyika katika hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es Salaam.

  Mkutano huo utajadili juu ya utekelezaji wa mradi wa kuunganisha mtandao wa umeme katika gridi za nchi hizo tatu (Zambia, Tanzania, Kenya) ‘ZTK power interconnector project).

  Aidha, Mkutano huo utatanguliwa na mikutano ya Makatibu Wakuu tarehe 29 Septemba, 2014 na mkutano wa wataalam wa sekta ya Nishati ya umeme kutoka nchi hizo tatu.

  Katika mkutano huo, Mashirika ya umeme kutoka katika nchi hizo zitawasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya kuunganisha mtandao wa umeme pia watajadili na kusaini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mradi (Heads of Agreement – HOA).

  Mwaka 1995, Mashirika ya umeme ya Zambia, Tanzania na Afrika Kusini yalianza kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kutathimini uwezekano wa kuunganisha mifumo ya gridi za umeme za Zambia na Tanzania. Upembuzi huo ulikamilika mwaka 1998 na kuthibitisha kuwa kuunganishwa kwa gridi za nchi husika kuna faida za kiuchumi, kijamii, kiufundi na kifedha.

  Mwezi Januari, 2001, Mawaziri wanaosimamia masuala ya Nishati wa Zambia, Tanzania na Kenya walikutana ambapo Serikali ya Kenya ilionesha nia ya kushiriki katika mchakato wa kuendeleza mradi kwa lengo la kupata fursa ya kununua umeme wa bei nafuu kutoka Zambia.  Hali hii ilibadili upeo wa mradi na kujulikana kama Zambia -Tanzania - Kenya Power Interconnector Project.  Mradi huu unahusisha sehemu kuu zifuatazo:


  i.      Ujenzi wa laini ya msongo wa 400kV yenye uwezo wa kusafirisha MW 400 kutoka kituo cha kupoozea umeme kilichopo Pensulo, Zambia hadi kituo cha kupoozea umeme cha Mwakibete, Mbeya kwa upande wa Tanzania,

  ii.    Kuimarisha mfumo wa usafirishaji umeme  nchini kwa ajili ya kuwezesha kusafirisha umeme unaotosheleza, wenye ubora na uhakika katika maeneo ya kaskazini, kaskazini mashariki na magharibi hadi kufikia Kenya kwa kujenga njia mpya ya kusafirisha umeme kutoka Mbeya hadi Singida katika msongo wa kV 400, na

  iii.  Ujenzi wa laini ya kusafirisha umeme yenye msongo wa kV 400 kutoka Arusha hadi Nairobi

  Aidha, mradi wa ZTK ni mmoja kati ya miradi ambayo kwa siku nyingi imekuwa katika Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Umeme (PSMP) kama miradi mhimili ambayo kuendelezwa kwake kutachangia kuwepo kwa vyanzo vya umeme mbadala kutoka nchi za jirani na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa kero ya upungufu wa umeme ambayo imekuwa ikiikumba nchi yetu mara kwa mara ambayo imesababisha kutoa huduma ya umeme kwa mgawo. Aidha, mradi huu pia utafungua uhusiano wa kibiashara kati ya makampuni ya umeme ya nchi wanachama kwani mifumo ya usafirishaji umeme imepangwa iwe na uwezo wa  kusafirisha umeme pande mbili  (bi-directional) kwa  ajili ya kununua na kuuza umeme kupitia masoko ya East African Power Pool (EACPP) na Southern African Power Pool (SAPP).

  Kuunganisha gridi za umeme za nchi jirani ni moja ya mkakati wa kipaumbele ili kuepuka matatizo ya nchi moja kukosa umeme wakati nchi ya jirani inao umeme wa ziada kama ilivyoainishwa katika Power System Master Plan (PSMP). Aidha, ni moja kati ya malengo ya shirikisho la NEPAD kuona kuwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zinakuwa na ushirikiano wa karibu katika masuala ya kuinua uchumi ambapo huduma ya umeme wa uhakika inahitajika.

  Imetolewa na;

  Badra Masoud
  Msemaji,
  Wizara ya Nishati na Madini


  0 0


  1[3]Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe, Fabiola Massula (kushoto) akizungumza wakati wa mashindano ya vipaji vya wanawake (WOMEN TALENT SYSTEM) ilifanyika Septemba 25,2014 katika Hotel ya JB BELMONT jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mshereheshaji wa shoo hiyo. Benki hiyo ni mmoja wa wadhamini wa shoo hiyo.2[1]Mkurugenzi wa Women Talent System, Angels Howell (katikati) akizungumza jambo kuhusiana shoo hiyo (kulia kwake), Meneja kutoka Mmi Tanzania, Paolo Frattari.
  6[1]Rais wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa  Martina Maurizio akionesha uwezo wake wakuvunja vibao kwakutumia mkono.7[1]Profesa  Martina Maurizio akionesha uwezo kwa jiwe lilokuwa limewekwa kifuani kwake na kunjwa kwakutumia nyundo.8[1]Profesa  Martina Maurizio akionesha uwezo kwa jiwe lilokuwa limewekwa kifuani kwake na kunjwa kwakutumia nyundo.

  3[1]Rais wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa  Martina Maurizio (kushoto), akipiga makofi kushiria kufulaishwa na jambo wakati wa mashindano ya vipaji vya wanawake (WOMEN TALENT SYSTEM) ilifanyika Septemba 25,2014 katika Hotel ya JB BELMONT jijini Dar es Salaam.4[1]Wageni waalikwa pamoja na wasanii wakifuatilia shoo hiyo.5[1]Wacheza shoo walioandaliwa kutoa burudani wakionesha uwezo wao.9[1]
  10[1]Wacheza shoo walioandaliwa kutoa burudani wakionesha uwezo wao.

  0 0

  Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali wa ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Gabriel Madebe akifungua semina ya wadau ya uhamasishaji wa matumizi takwimu za kilimo zinazopatikana kupitia Kanzi rasmi ya takwimu za kilimo inayopatikana katika anwani ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu yawww.nbs.go.tz leo jijini Dar es salaam.
  Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bi. Julia Stone akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa semina ya uhamasishaji wa matumizi ya Kanzi ya takwimu za Kilimo nchini leo jijini Dar es salaam.
  Mratibu wa Kanza ya Takwimu za Kilimo Tanzania Bw. Basike Mteleka akijibu maswali ya wadau mbalimbali waliohudhuria semina ya uhamasishaji wa matumizi ya Kanzi ya takwimu za Kilimo nchini.
  Wadau mbalimbali waliohudhuria semina ya uhamasishaji wa matumizi ya Kanzi ya takwimu za Kilimo nchini Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa semina hiyo leo jijini Dar es salaam.


  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka ( wa tatu kutoka kulia mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Ubalozi wa Uholanzi, wawakilishi kutoka bandari ya Rotterdam ya uholanzi pamoja na wawakilishi kutoka kampuni ya BAM ya uholanzi aliokutana leo mchana ofisini kwake kujadiliana kuhusu kuwekeza katika bandari ya Mtwara kwa mkopo wa bei nafuu. Kulia kwa Dk. Mwinjaka ni Balozi wa Uholanzi Nchini, Mr. Jaap FREDERICKS. (Picha na kitengo cha mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

  0 0

   
  Miss Tanzania Photogenic 2014, Evelyn Baasa.
   Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya
  Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2014, wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi   wa taji hilo, Evelyn Baasa (katiakti) jana. Wengine kutoka kushoto ni Nicole  Sarakikya, Lilian Kamazima, Lilian Timothy na Dorice Mollel.
   Warembo wakilisakata rumba kabla ya kuatangzwa kwa matokeo hayo.
   Baadhi ya warembo wakipiga picha ya pamoja na mshindi huyo wa Taji la Miss Tanzania Photogenic 2014
  Father Kidevu Blog, Arusha


  MlimbwendeEvelyn Baasa (19) jana aliibuka kidedea kati ya walimbwende wenzake 30 na  kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2014.
  Kwa kushinda taji hilo Baasa ambaye alinzania mbio za taji la Miss Tanzania katika Kitongoji cha Karatu naabadae kuingia Miss Arusha na Kanda ya Kaskazini amekuwa   mrembo wa kwanza kuingia Nusu Fainali ya mashindano Miss Tanzania 2014. 
  Shindano hilo ni moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo  washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusu Fainali ya shindano hilo litakalo  fanyika mapema mwezi ujao. 
   
  Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss   Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa Shindano la Miss   Tanzania, Hashim Lundenga ‘Uncle’ amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga  picha na wadau wa masuala ya urembo  wa masuala ya urembo Tanzania walikaa na kumchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.
  Majaji  waliowezesha kupatikana kwa mshindi huyo ni Mpigapicha mkongwe wa masuala ya urembo nchini Mroki Mroki ambaye anafanyakazi na Magazeti ya Serikali ya Daily News na Habarileo, Mtayarishaji wa vipindi Elliud Pemba wa True Vision na Afisa Itifaki Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Mukhsin Kassim.
  Taji la Redd’s Miss Tanzania Photogenic lilikuwa linashikiliwa na Redd’s Miss Tanzania  2013 Happyness Watimanywa.Warembo wengine waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Miss Photogenic ni Dorice Mollel, Nicole Sarakikya, Lilian Timothy na Lilian Kamazima.
  Kesho warembo hao watachuana tena kuwania taji la Miss Top Model katika shindano litakalofanyika Triple A jijini Arusha.

  0 0


  PG4A9520[1]
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizungumza  wakati alipozindua Mfuko wa CCM Mshikamano VICOBA kwenye ukumbi wa White House mjini Dodoma Septemba 25, 2014.PG4A9745[1]Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) akifurahia zawadi ya kitenge alichokabidhiwa na Rais wa VOCOBA nchini , Devota Likokola (kuahoto) kwa niaba ya wanachama wa  Mfuko wa CCM Mshikamano  VICOBA katika uzinduzi wa mfuko huo kwenye  ukumbi wa White  House mjini Dodoma Septemba 25, 2014. Katikati ni Naima Malima, mke wa Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko hicho kipya cha MV Tegemeo.
   Kivuko kipya na chakisasa cha MV Tegemeo kama kinavyoonekana, kimetengenezwa kama mfano wa Meli kutokana na huduma zake.
   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal jinsi kivuko kipya cha MV Tegemeo kitakavyofanya kazi.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Marceline Magesa akimuonesha Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal baadhi ya sehemu ndani ya Kivuko hicho kipya.

  0 0

  DSC_0316

  Chief Executive Officer, MeTL Group, Hon. Mohammed Dewji.

  0 0  0 0


   Katibu  Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishona nguo kwenye ofisi ya Veronica Simba (kushoto) iliyopo Mombo Sokoni,kulia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini Ndugu Stephen Ngonyani ,Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya siku moja katika wilaya ya Korogwe Vijijini ambapo licha ya kukagua miradi mbali mbali ya ujenzi wa maabara na ofisi za CCM alipata nafasi ya kuwahutubia wananchi na kuwasikiliza  .
    Katibu  Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuelekeza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kushona nguo kwenye ofisi ya Veronica Simba (kushoto) iliyopo Mombo Sokoni.
   
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakinunua matunda kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara Mombo.

   Diwani wa kata ya Mombo akishangiia baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kutamka wazi kuwa katika kuhakikisha wanapata halmashauri ya mji mdogo.
   Mama akiwa amembeba mwana ili awaone viongozi wake vizuri kwenye uwanja wa mikutano Mombo ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihutubia.
   Wananchi wakiwa wamekaa kwa shauku ya kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahan Kinana.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akiwapungia watu wakati wa kuwasili kwenye uwanja wa mikutano mjini Mombo akiwa pamoja  na Katibu wa NEC Itikadi Nape Nnauye
   Katibu Mkuu akiwapugia watu waliojazana kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mombo
   Umati wa wakazi wa Mombo uliojitokeza kwenye Mkutano wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mombo ambapo aliwaambia wananchi hao wanachofanya wapinzani ni biashara, kwani kwao kuandamanisha watu ni mtaji mzuri wa kuwaingizia pesa kutoka nje.

   Umati wa watu ukimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Tanga Aisha Kigoda pamoja na Dk. Edmund Mdolwa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Mombo.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mombo.
  Wananchi wakifuatilia mkutano wa Kinana mjini Mbombo
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa kwenye kiti tayari kupokea zawadi kutoka kwa wamasai wanaoishi Mombo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi kutoka kwa wamasai wa Mombo.
   Katibu wa CCM Ndugu Abdulrahman akipeana mkono wa shukrani kwa kiongozi wa wamasai wa Mbombo Samng'o Maika ambaye ni mwenyekiti wa Tawi la Chang'ombe ,Mombo.

  0 0

  President Jakaya Mrisho Kikwete chats with  Cable News Network (CNN) 's Richard Quest and Maggie Lake when he visited  CNN Studios at the  Time Warner Cente in New York.  

  CNN is an American basic cable and satellite television channel that is owned by the Turner Broadcasting System division of Time Warner. The 24-hour cable news channel was founded in 1980 by American media proprietor Ted Turner.  Upon its launch, CNN was the first television channel to provide 24-hour news coverage, and was the first all-news television channel in the United States.

  While the news channel has numerous affiliates, CNN primarily broadcasts from its headquarters at the CNN Center in Atlanta, the Time Warner Center in New York City, and studios in Washington, D.C. and Los Angeles. CNN is sometimes referred to as CNN/U.S. to distinguish the American channel from its international sister network, CNN International.
  President Jakaya Mrisho Kikwete poses with CNN's Richard Quest and Maggie Lake when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York
  President Jakaya Mrisho Kikwete presents an elephant doll to  CNN's Richard Quest when he visited CNN Studios at the Time Warner Cenytre  in New York. Right is Ms. JulietRugeiyamu Kairuki, the Executive Director of the Tanzania Investment Centre. The Tour was jointly organized by the TIC and CNN as part of an on going partnership to promote Tanzania  as an attractive destination for investment and tourism. 
  They also discussed  the forthcoming African Journalist of the year Awards Ceremony to be held in Dar es salaam later this year.

  0 0

   Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka (kulia), akitoa maelezo ya mradi ujenzi wa daraja hilo kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari, wanaotembelea mradi mbalimbali ya uwekezaji unaofanywa na NSSF. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Creasentius Magori.
   Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakijaribu kupita kwenye njia ya dharura, kwa ajili ya kuangalia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, unaofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
   Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakimsikiliza kwa makini, Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka (mwenye koti kulia), wakati akitoa maelezo ya mradi ujenzi wa daraja hilo, wakati wahariri hao, walipotembelea miradi mbalimbali ya uwekezaji inayofanywa na NSSF. Wa tatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Cresentius Magori. 
   Wahariri wa Vyombo vya Habari wakimshuhudia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cresentius Magori, akipita kwenye kwenye kivuko cha muda, wakati wakitoka kuangalia mradi mkubwa wa Ujenzi wa daraja la kisasa la Kigamboni, Dar es Salaam jana.
   Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakimsikiliza kwa makini, Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi Karrim Mataka (mwenye koti), wakati akitoa maelezo ya ujenzi wa daraja hilo, wakati wahariri walipotembelea miradi mbalimbali ya uwekezaji inayofanywa na NSSF.
   Wahariri wa Vyombo vya Habari wakipita kwenye daraja la muda, lililojengwa kwa ajili ya kupitisha vifaa vya ujenzi, walipofanya ziara ya kuangalia miradi mikubwa ya uwekezaji inayofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam jana.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Cresentius Magori, akijibu maswali ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, walipotembelea mradi mkubwa wa uwekezaji katika Kijiji cha DEGE Eco, Kigamboni, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Lodovick Mroso na Meneja Kiongozi wa Mahusiano na Huduma kwa Wateja, Eunice Chiume.

older | 1 | .... | 372 | 373 | (Page 374) | 375 | 376 | .... | 1897 | newer