0 |
|
0 |
|
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wilaya ya Lushoto Ndugu Antepass Richard Mbughuni, Katibu Mkuu ameanza ziara wilaya ya Lushoto ambapo atashiriki shughuli za maendeleo pamoja na kufanya mikutano kuimarisha Chama Cha Mapinduzi .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wananchi wa JEGESTAL wakati wa mapokezi wilayani Lushoto.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa JEGESTAL kabla ya kuanza kushiriki ujenzi wa ofisi ya tawi la JEGESTAL Lushoto Tanga.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi la JEGESTAL Lushoto, Katibu Mkuu wa CCM anafanya ziara mkoani Tanga kuimarisha chama .
0 |
|
0 |
|
- Adai huuzipeleka picha za vurugu nje ya nchi
- Adai Chadema wanafanya ili kukinusuru chama chao
- Awatuhumu kuwatoa kafara waandamanaji
- Asisitiza laaana ya damu za Watanzania hazitawaacha.
0 |
|
0 |
|

Katibu wa Kamati ya uchambuzi wa rasimu hiyo, Esther William (katikati) akisoma tamko la Wanaharakati wa ngazi ya jamii na washiriki wa Jukwaa la wazi la Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) linaloratibiwa na TGNP Mtandao kwa waandishi wa habari leo. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Badi Darusi na Hamadi Masudi Mjumbe (kushoto)

Katibu wa Kamati ya uchambuzi wa rasimu hiyo, Esther William (katikati) akisoma tamko la Wanaharakati wa ngazi ya jamii na washiriki wa Jukwaa la wazi la Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) linaloratibiwa na TGNP Mtandao kwa waandishi wa habari leo. Nyuma ni wajumbe wa kamati hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, TGNP Mtandao Lilian Liundi akifuatilia tamko la wanaharakati wa ngazi ya jamii na washiriki wa Jukwaa la wazi la Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) linaloratibiwa na TGNP Mtandao walipokuwa wakizungumza na vyombo vya habari leo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, TGNP Mtandao Lilian Liundi akifafanua jambo katika mkutano huo kwa wanahabari.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia tamko la wanaharakati wa ngazi ya jamii na washiriki wa Jukwaa la wazi la Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) linaloratibiwa na TGNP Mtandao walipokuwa wakizungumza na vyombo vya habari leo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia tamko la wanaharakati wa ngazi ya jamii na washiriki wa Jukwaa la wazi la Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) linaloratibiwa na TGNP Mtandao walipokuwa wakizungumza na vyombo vya habari leo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakishirikishaja jambo kwenye mkutano na wanahabari.
0 |
|
0 |
|
Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman akionyesha moja ya funguo za gari ya Ambulance zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA), alieshikana mkono ni Mwakilishi wa Shirika hilo Dkt. Natalia Kanem.
Waziri Rashid Seif wakati akilijaribu moja ya gari hilo zilizotolewa na UNFPA katika hafla ilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Gari nne za Ambulance zilizotolewa na Shirika la UNFPA zikiwa zimeegeshwa mbele ya Ofisi ya Wizara ya Afya Mnazimmoja.
Waziri wa Afya Rashid Seif akizungumza na watendaji wa Wizara yake na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za kukabidhiwa msaada wa gari za ambulance uliotolewa na UNFPA.( Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Na RAMADHANI ALI /HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) limekabidhi msaada wa magari manne ya Ambulance kwa Wizara ya Afya ya Zanzibar ambayo yatatumika katika Hospitali nne.
Mwakilishi wa UNFPA Tanzania Dkt. Natalia Kanem alimkabidhi Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman magari hayo katika sherehe zilizofanyika Wizarani Mnazimmoja.
Dkt. Natalia alitaka magari hayo yatumike kwa uangalifu ili kufikia malengo ya millennia ya kupunguza idadi ya vifo vya mama wajawazito na watoto wanaozaliwa hasa katika maeneo ya vijijini. Alisema moja ya sababu inayopelekea vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga ni tatizo la usafiri ambalo linachangiwa na uwezo mdogo wa baadhi ya familia hasa katika maeneo ya vijijini.
Aliongeza kuwa msaada huo ni sehemu ya Mpango maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa ulioanza mwaka 2011 na kumalizika Juni 2015 ambao huenda ukaendelea hadi mwaka 2016 kusadia masuala ya Afya na Lishe. Amesema mpango huo wa miaka minne ambao unahusisha maeneo makuu saba unaendeshwa kwa pamoja na Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa ambayo ni WHO, UNFPA, UNICEF na WFPA.
Mwakilishi huyo wa UNFPA amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kkwete na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Muhamed Sheina kwa juhudi kubwa wanazochukua katika kuimarisha huduma za mama wajawazito na watoto wachanga.
Aliesema UN inathamini juhudi hizo na juhudi za kuimarisha uchumi hivyo aliahidi kuwa wataendelea kuunga mkono kuhakikisha mama wajawazito na watoto wanaozaliwa wanaendelea kuishi katika mazingira yaliyo salama.
Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman, alilishukuru Shirika la UNFPA kwa misaada mbali mbali inayotoa kwa Wizara hiyo na ameahidi kuwa magari hayo yatatumika katika malengo yaliyokusudiwa.Amekiri kuwa tatizo la usafiri kwa mama wajawazito Zanzibar limekuwa likiwasumbua wananchi wengi na inafikia wakati akinamama hujifungua wakiwa kwenye gari wakati wa kupelekwa Hospitali ambazo hazina stara wala hazifai kwa kazi hiyo.
Alieleza matarajio yake kuwa tatizo hilo kwa sasa litapungua kwa kiasi kikubwa baada ya kupatiwa msaada huo ambao umekuja wakati muwafaka ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaelekeza juhudi zake kuimarisha huduma za afya mijini na vijijini.Gari hazo za ambulance ambazo zitapelekwa katika Hospitali ya Kivunge, Mwembeladu, Mkoani na Micheweni zimegharimu shilingi milioni 245,000,000 za kitanzania.
0 |
|
0 |
|
Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa akifafanua jambo kwa wajumbe wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Shina la Pamba jijini Dar es Salaam, mapema jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kutambulisha jumuiya hiyo.Shina hilo lipo katika Kata ya Kivukoni , Manispaa ya Ilala.
Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa(katikati) akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Shina la Pamba jijini Dar es Salaam, mapema jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kutambulisha jumuiya hiyo.Tawi hilo lipo katika Kata ya Kivukoni , Manispaa ya Ilala.Kulia ni Mwenyekiti UWT Kata ya Kivukoni Bibi. Rahilu Nyundo na kushoto ni Mwenyekiti wa UWT Shina la Pamba Bibi. Sophia Mbwille.
Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa akipokea risala ya UWT Shina la Pamba kutoka kwa Mjumbe wa Jumuiya hiyo Bibi. Twihuvila Faith Nyimbo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano wa jumuiya hiyo.
Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa akifurahia jambo na wajumbe wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Shina la Pamba jijini Dar es Salaam, mapema jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kutambulisha jumuiya hiyo.Shina hilo lipo katika Kata ya Kivukoni , Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa UWT Shina la Pamba lililoko katika manispa ya Ilala jijini Dar es Salaam wakimskiliza mgeni rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Kipawa Mhe. Bona Kaluwa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam. Picha zote na Frank Shija, MAELEZO
0 |
|
0 |
|
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasiliamali Watu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. D. Mndeme (kushoto) akizungumza na wanamichezo wa Ofisi yake wakati akiwaaga na kukabidhiwa vifaa vya michezo leo asubuhi kwa ajili ya kuelekea Mjini Morogoro kushiriki katika michuano ya Shimiwi iliyofunguliwa leo. Katikati ni Afisa Utawala wa TTCL Tanzania, Ulrick Swai (kulia) ni Katibu wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Mandia.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasiliamali Watu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. D. Mndeme (kushoto) akipokea sehemu ya vifaa vya michezo (jezi) kutoka kwa Afisa Utawala wa TTCL Tanzania, Ulrick Swai, wakati wa hafla fupi ya kuagwa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais na kukabidhiwa vifaa vya michezo leo asubuhi kwa ajili ya kuelekea Mjini Morogoro kushiriki katika michuano ya Shimiwi iliyofunguliwa leo. Kulia ni Katibu wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Mandia.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano hayo....
Baadhi ya wanamichezo wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakipanda katika basi tayari kwa safari kuelekea Morogoro.
0 |
|
0 |
|
0 |
|
0 |
|
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola ambapo aliwasisitiza wananchi hao kushiriki kazi za maendeleo na kujiunga kwa wingi kwenye mfuko wa Afya ya jamii.
Umati wa wakazi wa kata ya Mlola wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia wananchi hao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lwandai, kata ya Mlola ambapo aliwaambia wawe makini na matapeli wa ardhi wanaokuja kwa jina la Uwekezaji kwani wamekuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi nchini.
Wazee Maarufu wa kijiji cha Lwandai wakifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anafanya ziara za kujenga na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi,Pia katika mikutano yake ya sasa Katibu Mkuu amekuwa akitoa nafasi kwa wananchi kuhoji maswali ,kutoa maoni au ushauri kuhusu maendeleo yao katika maeneo yao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola wilaya Lushoto.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahamn Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa pamoja wakiwapungia mkono mamia ya watu waliofurika kwenye uwanja wa mikutano wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola wilayani Lushoto.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lwandai ambapo aliwaambia wawe makini na maneno ya wanasiaa ambao wanahusisha hoja ya katiba mpya na uchaguzi wa mwaka 2015, alisema kuwa kuna watu wana sahau kuwa hiyo siyo ajenda ya wananchi na si makubaliano ya vyama vya siasa .
Wananchi wa Mlola wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Kila kona ya uwanja ilijaza watu.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Hemed Mwanga akitoa ufafanuzi juu ya mambo mbali mbali yanahusu maendeleo ya wilaya hiyo wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye uwanja wa mikutano wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola ,Lushoto mkoani Tanga.
Nyuso za matumaini za wakazi wa Mlola.
Deogratius Kisandu akiwasalimia wananchi wa Lwandai kata ya Mlola wilani Lushoto baada ya kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .Deogratius alishawahi kuwa na nyanzifa zifuatazo kwenye chama cha NCCR Mageuzi,Katibu Mwenezi Taifa kitengo cha Vijana (2013) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya NCCR-Mageuzi (2014)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiondoka eneo la mkutano huku akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Hemed Mwanga.
Vitalu vya miti kwenye mradi wa upandaji miti Kwesimu.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka mbole kwenye vitalu vya mradi wa upandaji miti Kwesimu muda mchache kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichambua mche wa mti wakati wa kuandaa vitalu kwenye mradi wa upandaji miti Kwesimu,Katibu Mkuu alisisitiza watu kujali na kutunza mazingira yao .
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wakiwapungia wananchi walipokuwa wakiingia kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlola wakati wa ziara yao ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akikhutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlola, ambapo aliwahimiza wananchi kujiunga kwa wingi kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii ili wawe wanapata tiba bora na familia zao kwa mwaka kwa kulipa sh. 10,000.
Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili kushiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM tawi la Jegestal, alipoanza ziara wilayani Lushoto leo.
 |
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM tawi la Jegestal wilayani Lushoto leo |
Kinana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Henry Shekifu wakipiga makofi kufurahishwa na ngoma ya asili ya kabila la Wasambaa iliyokuwa inatumbuiza katika mkutano Mkuu wa majimbo ya Lushoto, Mlalo na Bumburi leo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akipiga gitaa na kuimba wimbo uliotungwa enzi hizo na babake, Moses Nnauye wakati wa mkutano huo wa majimbo ya Lushoto, Mlalo na Bumburi.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Akina mama wakiimba wakati wa kumlaki Kinana na msafara wake, ambapo alishiriki kuweka mbolea kwenye vitalu pamoja na kupanda miche na miti katika Kijiji cha Kwesimu.
Kinana akiweka mbolea kwenye vimfuko vya kupandia miche
 |
Kinana akitembelea bustani ya kuotesha miche ya miti katika Kijiji cha Kwesimu. Wilaya ya Kilosa imepanda zaidi ya miti milioni moja kwa ajili ya kuhifadhi mazingira. |
Kinana na Shekifu wakisaidia kupandikiza miche ya miti
Akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia baada ya kukagua ujenzi wa Zahanati ya Mbiwi, wilayani Lushoto.
Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili eneo la mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlola
Watoto wakiparamia mti ili waweze kumuoana Kinana katika kkutano wa hadhara katika Kata ya Mlola, Lushoto
 |
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (Maji Marefu) akisalimia wananchi katika mkutano huo |
Nape akihutubia katika mkutano huo ambapo alishangazwa na tabia ya wapinzani ambao wameanza kutangaza sasa kuwa ajenda yao kuu kwenye chaguzi zijazo ni siual;a la katiba..
Nape akiunguruma katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlola, Lushoto leo.
Wazee wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika mkutano huo
Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Henry Shekifu akielezea kwa wananchi kuhusu miradi mbvalimbal inayotekelezwa jimboni humo kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Mze Hoza Ismaili akimuomba Kinana amuarifu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete afanye ziara katika KLata ya Mlola kwani tangu walipotembelewa na Baba wa Taifa, Julius Nyerere enzi hizo hakuna rais mwingine aliyefika eneo hilo.
Kinana akimkabidhi kadi ya CCM aliyewahi kuwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Lushoto kupitia NCCR Mageuzi, Deogratius Kisandu, baada ya kutangaza kujiunga na CCM katika mkutano huo.
0 |
|
0 |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya uendeshaji wa chama cha waandishi wa habari za mazingira kwenye mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa chama cha waandishi wa habari za mazingira JET katika mkutano wa mwaka wa chama hicho ulioganyika jijini Dar Es Salaam, kutoka kushoto ni Mkurugenxi Mtendaji wa JET John Chikomo, Mwenyekiti wa JET Johnson Mbwambo, Katibu Mtendaji wa JET Chris Rweyemamu na Makamu Mwenyekiti wa JET Aisha Dachi.
Baadhi ya waandishi wa habari za mazingira ambao pia ni wanachama wa JET na wajumbe wa mkutano huo wakiwa katika majadiliano wakati mkutano ukiendelea jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo wakiwemo waandishi wa habari za mazingira kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao ni wananchama wa JET wakipitia nyaraka mbalimbali za mkutano huo (picha zote na Vedasto Msungu wa JET)
0 |
|
0 |
|
Baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Ilala wakiwa na mgeni rasmi Alhaji Ramadhan Madabida.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala ambao ni wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho Wilaya ya Ilala wakifuatilia baadhi ya hotuba zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa jumuiya ya wazazi ya ccm wilaya ya ilala.
Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Dar Es Salaam Ramadhan Madabida akiingia Ukumbini kufungua mkutano wa jumuiya ya wazazi ya ccm wilaya ya ilala.
0 |
|
0 |
|
0 |
|
0 |
|
 |
Gari dogo aina ya Suzuki Carry likiteketea moto katikati ya barabara maarufu kama Double Road jirani na makao makuu ya jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro. |
 |
Kikosi cha zima moto cha manispaa ya Moshi kilifika eneo la tukio kwa ajili ya kuudhibiti moto huo. |
 |
Askari wa Kikosi cha zimamoto akijaribu kuzima moto uliokuwa ukiteketeza gari hilo. |
 |
Baadhi ya mashuhuda wakitizama moto ulivyokuwa ukiteketeza gari hilo. |
 |
Askari wa kikosi cha zima moto walifanikiwa kuuzima moto huo. |
 |
Hata hivyo sehemu ya mbele ya gari hilo tayari ilikuwa imeteketea moto kwa kiasi kikubwa.Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini. |
0 |
|
0 |
|
0 |
|
0 |
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri akizungumza na wandishi wa Habari katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Kilimani, juu ya azma ya Serikali kuuendeleza Mji wa Zanzibar ambao utajuilikana kama ukanda wa Biashara wa Darajani kuanzia viwanja vya Malindi hadi viwanja vya Mnazimmoja na maeneo yanayozunguka sehemu hizo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
========= ======== ========
Na SAADA SALEH/MARYAM HIMID/RAHMA KHAMIS ZJMC
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzinibar imuamua kuuendeleza Mji wa Zanzibar kuanzia viwanja vya mpira vya Malindi hadi eneo la viwanja vya Mnazi mmoja na maeneo yanayozunguka sehemu hizo na limepewa jina la Ukanda wa Biashara Darajani .
Haya yalielezwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Haji Omari Kheri alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Kilimani.
Alisema ujenzi wa Ukanda wa Darajani utafanywa kwa pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Wabia ambao tayari wameanza kujitokeza baada ya kupata fununu ya mpango huo.
Alieleza kuwa Serikali imeamua kuliendeleza eneo la ukanda huo kwa vile ni kitovu cha shughuli mbali mbali za kiuchumi na kijamii kwa muda mrefu na sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya wananchi wakiwemo wageni wanaotutembelea Zanzibar.
“Sote tumeshuhudia kushuka hadhi kwa Mji wetu kutokana na sababu nyingi zikiwemo msongamano wa watu na baadhi yao kufanya biashara bila ya mpangilio maalumu umelifanya eneo hilo kupoteza haiba nzuri ya mji wetu,”Waziri Haji Omar Kheri alisema .
Amsema uendeleza wa Ukanda wa Biashara Darajani utahusisha Jengo la Biashara la kisasa, ujenzi na ukarabati wa majengo yanayopakana na ukanda wote utakaohusika na utaengenezaji bustani na maeneo ya kupumzikia .
Hatua nyengine alizitaja ni kujenga maegesho ya kisasa ya magari, kuviendeleza viwanja vya michezo vya Malindi na Mnazimmoja na kujenga Mkahawa na Bekari ya kisasa kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii na wenyeji.
Aidha Waziri Haji Omar Kheri amedokeza kuwa Jengo maarufu Darajani la treni (Chawi Building) litafanyiwa matengenezo makubwa na kutumika kwa shughuli za kibiashara zenye asili ya kizanzibari.
“ Mpango huu wa Ukanda wa Darajani utakapomalizika utatoa fursa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo zaidi ya 1000 kwa shughuli mbali mbali na kupunguza tatizo la ajira ,” Waziri alisisitiza.
Alisema katika kukamilisha mpango huo Skuli ya Daraji na Vikokotoni zitaondolewa na majengo hayo yatafanyiwa matengenezo na kuwa majengo ya biashara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ aliwataka wafanya biashara na wananchi kuunga mkono maamuzi ya Serikali katika kufanikisha Mpango huo.
IMETOLEWA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
0 |
|
0 |
|
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema akizungumza wakati wa hafla ya kuwakaribisha waliokuwa wanafunzi wa chuo hicho waliohitimu miaka iliyopita wakati wa mwendelezo wa shughuli mbalimbali za chuo hicho kutimiza miaka 50.
Bw. Alexander Msofe akizungumza na wahitimu wa miaka ya nyuma wa chuo cha CBE kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuchangia maendeleo ya CBE iliyowahusisha wahitimu hao jijini Dar es salaam.
Bw. Isdori Kwayi, mmoja wa wahitimu wa chuo cha CBE mwaka 1972 akitoa mchango wake kuhusu namna chuo hicho kinavyoweza kukusanya fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali ili kuboresha miundombinu yake wakati wa hafla fupi iliyowahusisha wahitimu wa chuo hicho jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wahitimu wa CBE wa miaka iliyopita wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla ya kuchangia maendeleo ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam ambacho kimetimiza miaka 50.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
JAMII YAASWA KUCHANGIA MAENDELEO YA ELIMU.
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
28/9/2014. Dar es salaam.
Wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini wameaswa kujenga utaratibu wa kuchangia miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo ya elimu katika vyuo walivyosoma na kuepuka kutumia fedha nyingi katika kuchangia masuala yasiyo na tija kwa maendeleo ya taifa.
Hayo yamebainishwa jana jijini Dar es salaam na mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema , wakati wa hafla ya kuwakaribisha chuoni hapo waliokuwa wanafunzi wa chuo hicho waliohitimu miaka iliyopita kwenye mwendelezo wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho.
Akizungumza na wahitimu hao amesema kuwa wanayo nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu hapa nchini kwa kushiriki na kutumia sehemu ya mapato wanayopata kupunguza changamoto za elimu za uhaba wa vyumba vya madarasa, maabara na miundombinu mingine isiyo rafiki kwa maendeleo ya wanafunzi.
“Elimu ndio msingi wa maendeleo, sisi tulipata elimu iliyo bora lazima tuchangie kwa sehemu yetu kuonyesha tunayajali maeneo tuliyosoma, hivi sasa mwamko wa watu wengi uko katika kuchangia sherehe na harusi lakini kwenye suala la elimu hali ni tofauti” Amesema Prof. Mjema.
Amesema wahitimu hao wana nafasi kubwa ya kuendelea kuwa mfano kwa kuendelea kutoa mrejesho kwa uongozi juu ya nini kifanyike katika kuendeleza sekta ya elimu chuoni hapo sanjali na kueleza mapungufu yaliyopo pamoja na kutoa michango yao juu ya namna ya kuendeleza kiwango cha taaluma.
Amebainisha kuwa chuo hicho kinahitaji kiasi cha shilingi bilioni 3 ili kiweze kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya upanuzi wa kampasi zake, ujenzi wa miundombinu,uongezaji wa vifaa vya kufundishia, madarasa, maabara na kumbi za mihadhara.
Kwa upande wake Bw. Alexander Msofe akizungumza na wahitimu hao kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema chuo hicho kinafurahia matunda ya mafanikio ya kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Amewaambia wahitimu hao kuwa licha ya changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo hicho kimeweza kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kwa mwaka kutoka 25 waliodahiliwa mwaka 1965 hadi 14,000 katika mwaka wa masomo wa 2014/15 pamoja na ongezeko la idadi kozi za masomo zinazotolewa kutoka 1 hadi 6.
Bw. Msofe ameongeza kuwa chuo cha CBE sasa kinatimiza miaka 50 kikiwa chuo pekee Afrika ya Mashariki na katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kinachotoa wanafunzi wa shahada ya vipimo.
Mafanikio mengine ni pamoja na kuongezeka kwa kozi za masomo na ngazi za mafunzo hadi kufikia shahada, kuongezeka kwa wakufunzi wenye shahada za uzamivu (PhD) chuoni hapo pamoja na chuo kuanzisha ushirikiano wa elimu na vyuo vikuu vingine nje ya nchi kikiwemo Chuo Kikuu cha Eastern Finland katika utoaji wa mafunzo ya shahada za uzamivu kwa kutumia TEKNOHAMA kwa nchi za SADC.
Aidha, katika kuelekea tamati ya maadhimisho ya chuo hicho yatakayofanyika Januari 13, mwaka 2015 ameitaka jamii na wahitimu wote wa chuo hicho wajitokeze wingi kutoa michango yao ya hali na mali itakayowezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa na mihadhara, maabara na vyumba vya kulala wanafunzi.
Kwa upande wao wanafunzi waliowahi kusoma chuoni hapo wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa hafla hiyo wametoa wito kwa wadau mbalimbali wenye mapenzi mema kujitokeza kuchangia ukamilishaji wa programu mbalimbali za maendeleo zilizoanzishwa na uongozi wa chuo hicho.
Wamesema kuwa badala ya kuiachia serikali pekee jamii na wahitimu hao wanayo nafasi kubwa ya kuchangia maendeleo ya chuo hicho kutokana na wao kuendelea kufaidika na elimu waliyoipata kipindi wakiwa wanafunzi wa chuo hicho.
Wameiomba serikali kuhakikisha kuwa inaendelea kukisaidia chuo hicho na kukitumia kupata ushauri wa kufanikisha masuala mbalimbali yakiwemo mafunzo kwa wafanyabiashara na uimarishaji wa mifumo ya ukusanyaji wa kodi hapa nchini ili kuondoa tatizo la asilimia kubwa ya watu kukwepa kodi.
0 |
|
0 |
|
The Dodoma University Vice Chancellor Professor Idris Kikula and Rutgers University Chancellor Richard Edwards sign Memorandum of Understanding between the two universities on academic partnership during a brief and colorful ceremony held at New Jersey Rutgers University campusyesterday.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his public lecture on “The role of Academic Partnerships in Finding Solutions to Global Challenges and Advancing Tanzania’s Priorities,” at Rutgers University in New Jersey United States yesterday. The public lecture was preceded by the signing of the Memorandum of Understanding between Dodoma and Rutgers university on academic partnerships.
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete receives a standing ovation shortly after he delivered a public lecture on “The Role of Academic Partnerships in Finding Solutions to Global Challenges and Advancing Tanzania’s Priorities,” at Rutgers University New Jersey Campus yesterday
0 |
|
0 |
|
President Jakaya Mrisho Kikwete meets and hold talks with South Sudan President Salva Kiir during the UN General Assembly in New York yesterday.
0 |
|
0 |
|
Baadhi ya watu wakiwa wanafuatilia mashindano hayo ya SHIMIWI yanayo endelea Mjini Morogoro katika uwanja wa Jamuhuri
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Netball wakiwa wanajiandaa na Mchezo wao
Afisa wa PSPF akimsajili uanachama mmoja wa wanamichezo walikuwepo katika Mashindano hayo ya SHIMIWI
Aliyevaa Tshirt ya Blue ni Afisa Masoko wa PSS Bwana Delphin Richard akitoa maelezo kwa wanachama wa PSPF wakati Michezo hiyo ikiendelea
Michezo ikiwa inaendelea
Baadhi ya wachezaji wakiwa katika mapumziko.
0 |
|
0 |
|
Engineer Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na Tamasha kubwa la upendo kwa mama linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid tarehe 02-11-2014
Engineer Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na wanahabari kuhusiana na Tamasha la Upendo kwa mama ambalo linalenga kutoa mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwawezesha kujiajiri pamoja na kuwaombea na kuwashukuru kwa moyo wa upendo waliyonayo kwa kujitoa katika kusimamia familia na malezi
Mratibu wa Tamasha la Upendo kwa mama Bw. Linus Kilembu akiongelea maandalizi ya Tamasha kuwa limekamilika kwa asilimia 90
Engineer Carlos Mkindi mwenyekiti wa Tamasha la upendo ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akifanyiwa mahojiano na wanahabari katika studio za mkundi production zilizopo njiro mkoani Arusha
Kampuni ya Makundi Production ya jijini Arusha iko katika maandalizi ya kufanya tamasha kubwa la aina yake litakalo julikana kwa jina la UPENDO WA MAMA ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba 2014 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
Tamasha hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili wakubwa kutoka Kenya, Sara K, na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku likipambwa na Ambwene Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester Bukuku, Matha Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula, Matumaini, Eline Patrick bila kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani Arusha pamoja na Kwaya Mbalimbali.
Lengo la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA linalengo la kutoa Mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri, vilevile utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa upendo waliyonao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia Familia na malezi ya watoto.
Studio ya Mkundi nakamati ya maandalizi ya Tamasha la UPENDO KWA MAMA wanatoa nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika yote ambayo yako tayari kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)
0 |
|
0 |
|
Wachezaji wa WIZARA ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo wakijifua kabla ya kuanza mechi yao leo dhidi ya timu ya Polisi leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mchezo wa mpira wa pete kati ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo na Polisi leo mjini Morogoro.
Wizara ya Habari yatakata SHIMIWI Morogoro.
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
28/09/2014
Shamrashamra za mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) zimepamba moto kwa timu mbalimbali kumenyana katika michezo mjini morogoro
WIZARA ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo leo wameanza vema mashindano hayo kwa kuwapa kichapo timu ya Polisi kwa mchezo wa mpira wa pete kwa kuwachapa magoli 45 kwa 01 dhidi ya wapinzani wao na kuibuka washindi katika mechi hiyo.
Ushindi huo umetiwa hamasa ambapo wachezaji hao wanatambua kuwa Wizara hiyo ndio yenye dhamana ya kusimamia michezo nchini.
Wakicheza kwa umahiri, huku wakitambua kuwa wao ndio wanaopaswa kutoa mfano kwa timu nyingine zinazoshriki mashindano hayo,wacheaji hao walizitumia idara zote katika mchezo huo kikamilifu hivyo wailioibuka kidedea katika mchezo huo.
Akizungumzia ushindi wao Nahodha wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Johari Kachwamba amesema kuwa siri ya ushindi huo ni nidhamu na kuzingatia maelekezo ya mwalimu na mazoezi wakati wote wa maandalizi ya mashindano hata wakati wa mashindano yanayoendelea.
Kachwamba amesema kuwa wanaendelea kujifua na hawabweteki na ushindi huo walioupata leo kwani mashindano mashindano ndio yanaanza.
Aidha, timu ya kuvuta kamba wanaume ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeshinda baada ya timu ya RAS Tanga kutokutokea uwanjani hapo, hivyo kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Mechi zilizochezwa leo uwanja wa Jamhuri Morogoro ni pamoja na kuvuta kamba wanawake kwa wanaume, mpira wa pete, na mpira wa miguu ambapo mwaka huu timu 54 zinashiriki mashindano hayo.