Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

MZEE KASSIM MAPILI ALAZWA MUHIMBILI , RAIS WA SHIRIKISHO LA MUZIKI ADDO NOVEMBER AMTEMBELEA

$
0
0
Kutoka kushoto ni Gwiji wa muziki wa dansi nchini Mzee Kassim Mapili akiwa amekaa kwenye kitanda cha hospitali ya Taifa Muhimbili  kushoto ni Rais wa Shirikisho la Muziki wa Dansi Tanzania Addo November alipokwenda kumjulia hali  leo asubuhi hospitalini hapo.

NA BONGOWEEKEND BLOGSPOT.COM
HALI ya mwanamuziki nguli Kassim Mapili aliyelazwa katika Hospitali  ya Taifa  Muhimbili katika kitengo cha moyo inaendelea vizuri imehafamika.
Mapili ambaye awali alilazwa katika Hopitali ya  Mwananyamala  kutokana na kusumbuliwa na  maradhi ya mapafu kujaa maji  pamoja na moyo kujaa maji ambako alilazwa kwa muda wa siku nne kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili juzi  mchana.
Hayo yalisemwa leo na Rais wa Shirikisho la Muziki  Addo November  ambaye aliefika hospitalini hapo mapema asubuhi kumjulia hali Mapili  ambapo alikiri kuwa amelazwa katika wodi  namba moja  katika Taasisi ya Moyo baada ya kutolewa  katika wodi ya uangalizi maalumu (ICU), Muhimbili.
Aidha November ametoa rai kwa wadau na wanamuziki  viongozi  mbalimbali  kujitokeza kwa wingi kwenda kumjulia hali gwiji huyo wa muziki ikiwa ni sehemu ya kumpa faraja kwa ujumla.
 “Mzee wetu anaumwa sana na amevimba sana  miguu hivyo  ni wajibu wa kila mmoja wetu kutoa msaada wa hali na mali” alisema November.
Wakati Mapili akiwa amelazwa mama yake mzazi  aliyetajwa kwa jina la  Hajena Mussa  Mchikita amefariki usiku wa juzi nyumbani kwake Nachingwea  na atazikwa  leo mkoani Songea alisema November .
Mapili  alitamba na nyimbo za ‘Rangi ya Chungwa’, ‘Mayasa’ ambao aliuimba na Marehemu TX Moshi William enzi za uhai wake  na kutamba vilivyo katika miaka ya 1980.

Glorious kamili uzinduzi wa John Lissu

$
0
0
KUNDi la muziki wa Injili la Glorious Celebration la jijini Dar es Salaam limethibitisha kushiriki katika uzinduzi wa albamu ya Uko Hapa ya msanii John Lissu.

Uzinduzi wa albamu hiyo unatarajiwa kufanyika Oktoba 5 mwaka huu, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, ambapo waimbaji mbalimbali watakuwepo.
 
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayodhamini uzinduzi huo, Alex Msama ilisema maandalizi muhimu kuhusiana na uzinduzi huo yamekamilika.
 
Msama alisema katika taarifa hiyo kuwa anashukuru wasanii hao kukubali kutumbuiza, ambapo pia atakuwepo msanii mahiri nchini Rose Muhando pamoja na kwaya mbalimbali.

Glorious wanatamba na albamu mbalimbali ikiwemo ya Niguse yenye nyimbo za Unaweza Yesu, Ee Roho, Juu ya Mataifa, Mawazo, Ameni Haleluya, Nafsi Yangu, Nakupenda Yesu, Usilie na Niguse.

Msama alisema mbali na Glorious, kuna waimbaji wengine galacha wa nyimbo za injili wamethibitisha kushiriki.

Albamu ya Lissu ambaye ana sifa ya kupiga muziki wa live ina nyimbo 18 zilizogawanywa katika maeneo mawili, ambazo ni Wakusifiwa, Wastahili Sifa, Mataifa ya Kujua, Inuka, Uko Hapa, Nijaze, Nitaongozwa, Wastahili Bwana, Roho Mtakatifu, Mtakatifu na Umeinuliwa.
 
Nyingine ni Yu Hai Jehova, Atikisa, Nijaze, Upendo, Mataifa Yakujue, Umejawa na Ukuu, Fungua Macho, Haleluya na Mungu Ibariki.

Serikali imejipanga kutatua tatizo la makazi kwa watumishi wa umma

$
0
0
Fatma Salum-Maelezo
Serikali imejipanga kutatua tatizo la makazi kwa watumishi wa umma kwa kujenga nyumba Elfu 10 za gharama nafuu kote nchini.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw.Elius Mwakalinga wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na wakala huo jijini Dar es Salaam na Pwani.
 Mwakalinga alisema kuwa  mradi huo wa nyumba elfu 10 unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 18 unahusisha nyumba za viongozi na watumishi wa kawaida wa kada zote.
“Lengo la kujenga nyumba hizi ni kuwapatia  watumishi wa umma makazi bora jirani na maeneo yao ya kazi ili kuongeza tija katika utoaji huduma kwa wananchi. Mradi huu utawawezesha kupata nyumba za kupanga na  kununua kwa gharama nafuu”.  Alisema Mwakalinga.
 
Akifafanua zaidi  Mwakalinga alisema kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zinatokana na ruzuku ya serikali pamoja na fedha za TBA ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam nyumba hizo zimeanza kujengwa kwenye maeneo ya Bunju, Mbezi Beach, Ada Estate na Masaki na pia eneo la Chalinze mkoani Pwani.
 
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Ushauri kutoka TBA Bw. Edwin Nnunduma alisema kuwa ujenzi wa nyumba hizo unatumia teknolojia ya kisasa inayopunguza gharama na muda wa kukamilika.
 
Pia Nnunduma alisema mpaka sasa ujenzi unaendelea vizuri kwenye mikoa mbalimbali nchini ikiwemo mikoa mipya ya Katavi, Geita, Simiyu na Njombe.
 
Naye Meneja wa Kikosi cha Ujenzi cha TBA Mhandisi Wilfred Dungamu alieleza kuwa kwa sasa wakala huo unatumia kikosi cha wahandisi wa ndani kilichoanzishwa mwaka 2012 na mpango huo umesaidia kupunguza gharama kubwa zilizokuwa zikitumika kuwalipa wahandisi kutoka makampuni binafsi.

WIZARA YA AFYA YAKABIDHI MABASI 6 KWA VYUO VYA AFYA NCHINI.

$
0
0
 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kabla ya kukabidhi mabasi 6 kwa wakuu wa vyuo vya Afya kutoka katika maeneo mbalimbali .Mabasi hayo yatasaidia kuaondoa upotevu wa muda na adha ya usafiri waliyokuwa wakiipata wanafunzi,watumishi na wakufunzi  wa vyuo hivyo  kufika kwenye maeneo ya mafunzo kwa vitendo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akikata utepe kwenye basi moja kati ya sita yaliyonunuliwa kwa ufadhili wa Mradi wa Mfuko wa Dunia mzunguko wa 9 ambayo yamekabidhiwa kwa wakuu wa vyuo vya afya leo jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akikagua mabasi hayo yaliyonunuliwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Dunia mzunguko wa 9 ambayo yamekabidhiwa kwa wakuu wa vyuo  6 vya afya leo jijini Dar es salaam.
Sehemu ya ndani ya mabasi hayo yaliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Mradi wa Mfuko wa Dunia.

Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

========   =======  =========
WIZARA YA AFYA YAKABIDHI MABASI 6 KWA VYUO VYA AFYA NCHINI.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO
25/9/2014. Dar es salaam.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  imekabidhi mabasi 6 kwa  vyuo vya elimu ya Afya kwa lengo la kurahisisha huduma ya usafiri kwa wanafunzi na wakufunzi wanaokwenda kwenye mafunzo kwa vitendo katika maeneo mbalimbali nchini.

Vyuo vilivyokabidhiwa mabasi hayo ni Chuo Kikuu cha Hurbert Kairuki Memorial (HKMU) kilichopo jijini Dar es salaam, Chuo cha Uuuguzi Bagamoyo,Chuo cha Uuguzi Mirembe mkoani Dodoma, Chuo cha Uuguzi Tanga na Chuo cha Tabibu kilichopo mkoani Mtwara.

Akikabidhi mabasi hayo kwa wakuu wa vyuo hivyo leo jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo amesema mabasi hayo yatasaidia kuaondoa upotevu wa muda na adha ya usafiri waliyokuwa wakiipata wanafunzi,watumishi na wakufunzi  wa vyuo hivyo  kufika kwenye  maeneo ya mafunzo kwa vitendo.

“Ninakabidhi magari haya kwenu leo hii yakafanye kazi za kuwahudumia watumishi na wakufunzi wa maeneo yenu ya kazi, Ni wajibu wenu kuhakikisha mnayatunza na kuyafanyia matengenezo kulingana na miongozo iliyopo ili yaweze kudumu” Amesisitiza.

Amesema mabasi hayo 6 yamenunuliwa  kwa gharama ya shilingi milioni 344 kupitia ufadhili wa Mradi wa Mfuko wa Dunia mzunguko wa 9 ambao pamoja na mambo mengine unaisaidia Wizara katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya uzalishaji wa rasilimali watu wa kutoa huduma za afya nchini.

Bw.Pallangyo ameeleza kuwa serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeendelea kujenga uwezo kwa wataalam wa sekta ya afya hapa nchini ,kuongeza udahili kwa wanafunzi kwa lengo kuzalisha rasilimali watu wa kutoa huduma za afya katika maeneo mbalimbali nchini .

Amesema kutokana na kuongezeka kwa kasi ya udahili wa wanafunzi wa fani za afya, Serikali imeendelea kuvijengea uwezo vyuo hivyo kwa kujenga majengo mapya na kupanua yaliyopo ili yaweze kutumiwa na wanafunzi wengi zaidi wa fani za afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafuzo wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Otilia Gowelle akizungumza kabla ya makabidhiano ya magari hayo amesema kuwa Serikali imekuwa ikifanya juhudi ya kuhakikisha kuwa wanafunzi walio katika mafunzo ya kada mbalimbali za afya wanajengewa uwezo kwa kuboreshewa miundombinu, majengo, vifaa vya mafunzo vya maabara ili kurahisha mafunzo yao kwa vitendo.

Amesema kupatikana kwa mabasi hayo 6 ni sehemu ya mpango wa Wizara wa kuwawezesha wanafunzi wa vyuo hivyo kwenda kwenye maeneo ya mafunzo kwa vitendo nje ya vyuo wanavyosoma kwa  urahisi zaidi.
Nao baadhi ya wakuu wa vyuo hivyo vilivyopokea mabasi hayo Prof. Boniface Msamati wa Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki cha jijini Dar es salaam na Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Tanga ,Thomas Marato wakizungumza kwa niaba ya wenzao mara baada ya kupokea mabasi hayo wameishukuru serikali kwa kuwaondolea kero ya usafiri wanafunzi katika vyuo vyao.

Wamesema mabasi hayo yatatumika kuwasafirisha wanafunzi na wakufunzi kwenda katika maeneo mbalimbali nchini na kuwaondolea adha ya kukodi magari kwa fedha nyingi  kwa lengo la kuwapeleka wanafunzi wao kwenye mafunzo kwa vitendo katika maeneo yaliyo nje ya vyuo hivyo.

KATIBU MKUU WA CCM AKISHIRIKI KILIMO CHA UPANDAJI MPUNGA WILAYANI KOROGWE LEO.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchanyata kwa Power tiller kwa ajili ya upandaji miche ya mpunga kwenye vijaruba vya kilimo cha zao hilo cha Umwagiliaji vilivyopo katika kijiji cha Mhenge,Kwamndolwa wilayani Korogwe mkoani Tanga leo.

NYUMBA ZINAPANGISHWA

$
0
0
 Sehemu ya mbele.

 ENEO:      Nyumba ipo  PUGU-Umbali wa  mita 100  toka  Barabara Kuu ya lami.

               Nyumba  3 za familia zipo ndani  ya  eneo  moja  kila  moja  inajitegemea.

UKUBWA: Kila  moja  ina vyumba  3 vya kulala, jiko, siting room kubwa na daining ya kutosha.
 UMEME:  Kila  moja  inatumia  Mita  ya Luku kwa kujitegemea.  pamoja  na  maji.

 PAKING:  Eneo kubwa kwa zaidi ya magari 5 kwa wakati mmoja.
BEI.  Ni maelewano kuanzia miezi  miezi  6  au zaidi kutegemea hitaji la mteja.

 kwa mawasiliano: 0686-569999

     Wako  katika makazi bora na ya kisasa. 

WAREMBO MISS TANZANIA 2014 WATEMBELEAMAKAO MAKUU YA EAC, AICC, AUWSA LEO

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini,John Mongela akisalimiana na Warembo wanaoshiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2014, walipomtembelea ofisini kwake jijini Arusha leo. Warembo hao Septemba 27 wanataraji kupandaa jukwaani kuwania taji la Miss Top Model litakalofanyika jijini Arusha.
 Warembo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mAMLAKA ya maji safi na maji taka Jijini Arusha(AUWSA) walipowatembelea leo
 Wakiwasili AICC
Warembo wanaoshiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2014, wakimsikiliza Ofisa Habari Mwandamizi na Itifaki wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Catherine Kilinda aliyekuwa akiwapa maelezo mbalimbali kuhusina na kazi za kituo hicho walipokitembrelea jijini Arusha leo.Aliyevalia suti ni Rodney Thadeus Ofisa Itifaki.
 Warembo wakiwa ndani ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo

Washiriki wa shindano la Redd’s Miss Tanzania 2014, wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa na benbdera ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) walipotembelea Makao makuu ya Jumuia hiyo jijini Arusha
Warembo wakisambaza upendo kwa Rodney Thadeus.

-NSSF MKOA WA TEMEKE YAWAPA SEMINA WAAJIRI WAKE KUHUSIANA NA MABORESHO YA HUDUMA WANAZOTOA

$
0
0
Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke, Yahya Mhamali akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na Mkoa wa NSSF Temeke kwa Waajiri wake ambayo ilihudhuriwa na Maofisa Rasirimali Watu pamoja na Wahasibu kwa ajili ya uelewa kuhusu moboresho ya formula mpya ya pensheni ambayo imetolewa na SSRA pamoja na huduma zilizoboreshwa kwa kiwango cha Kimatifa kwa NSSF Temeke (ISO). 

Semina hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, wa kwanza ni Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Hudumakwa Wateja waNSSF, Eunice Chiume.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa na Mkoa wa NSSF Temeke kwa Waajiri wake ambayo ilihudhuriwa na Maofisa Rasirimali Watu pamoja na Wahasibu kwa ajili ya uelewa kuhusu maboresho ya formula mpya ya pensheni iliyotolewa na SSRA pamoja na huduma zilizoboreshwa kwa kiwango cha Kimatifa kwa NSSF Temeke (ISO). Kushoto ni Meneja wa Idara za Serikali na Balozi GDE, Rehema Chuma na Meneja Mafao, James Oigo.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori, akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa na Mkoa wa NSSF Temeke kwa Waajiri wake ambayo ilihudhuriwa na Maofisa Rasirimali Watu pamoja na Wahasibu kwa ajili ya uelewa kuhusu maboresho ya formula mpya ya pensheni iliyotolewa na SSRA pamoja na huduma zilizoboreshwa kwa kiwango cha Kimatifa kwa NSSF Temeke (ISO). Kushoto ni Meneja wa Idara za Serikali na Balozi GDE, Rehema Chuma na Meneja Mafao, James Oigo.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.

 Baadhi ya Maofisa wa NSSF waliohudhuria semina hiyo.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Idara ya Matekelezo NSSF Mkoa wa Temeke, Nour Aziz (kushoto), Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Hudumakwa Wateja waNSSF, Eunice Chiume (wa pili kushoto), Meneja wa Idara za Serikali na Balozi (GDE), Rehema Chuma na Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke, Yahya Mhamali.
 Washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na Meneja Mafao wa NSSF, James Oigo.
 Meneja Mafao wa NSSF, James Oigo akitoa mada katika semina hiyo.
 Washiriki kutoka makampuni na taasisi mbalimbali Temeke wakiwa katika semina hiyo.
 Washiriki kutoka makampuni na taasisi mbalimbali Mkoa wa NSSF Temeke kwa Waajiri wakeTemeke wakiwa katika semina hiyo.

UTANDAWAZI GROUP KUNOGESHA TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO

$
0
0
NA ANDREW CHALE, BAGAMOYO

KUNDI maalufu la ngoma asili la Utandawazi Theater Group ‘Matwigachallo’  jioni ya kesho wanatarajiwa kuwasha moto wa aina yake kwenye tamasha la Kimataifa la 33 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, lililoanza Septemba 22 mwaka huu kwenye viunga vya chuo hicho.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa tamasha hilo, Abmic am Bafadhil ‘Bura’ alieleza kuwa, kundi hilo ambalo kwa sasa limejizolea umaalufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania, linatarajiwa kutoa burudani ya ngoma za asili sambamba na watoto wadoigo wanaotia fola kwa sasa katika sanaa hiyo ya utamaduni, Watoto wadogo Gozibet Bwere (4) na Nyambuli Aginess Muganga (5).
“Kundi la Utandawazi ‘Matwigachallo’, la Ukerewe, litawasha moto kwa burudani ya aina yake, pamoja na watoto wao wadogo wenye uwezo na kipajimkikubwa cha kuimba, kucheza na kupiga ngoma” alieleza Bura.

Na kuongeza kuwa, watoto hao wamekuwa maalufu kwa sasa hasa katika sherehe za Kitaifa na Kimataifa kwa kupata kuonyesha uweo wao hivyo kwa uwepo wao kwenye tamasha hilo, itatoa fursa kwa watu mbalimbali kuwaona.

Mbali na kundi hilo la Utandawazi, pia kutakuwa na Umoja Culture Flying Carpet ambao wataonyesha michezo mbalimbali ya sarakasi, ngoma, muziki na michezo mingine kibao.

Aidha, Jumamosi kutatanguliwa na mahafali ya 25 ya Chuo hicho huku wahitimu wa 37 wakitarajiwa kutunukiwa vyeti vyao, ambao Wanawake 11 na wanaume 26.

TBL YATOA MSAADA WA VISIMA VYA MAJI ZANZIBAR NA MBAGALA

$
0
0

Mwakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Zanzibar Samir Manji ( wa tatu kushoto),  akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 51 wananchi wa majimbo ya Chumbuni na Mpendae ikiwa ni msaada wa kampuni hiyo kwa ajili ya mradi wa uchimbaji wa visima vya maji safi na salama katika majimbo hayo juzi. Wa pili kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu
Mwakilishi wa Mauzo ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Bw. Alen Mwebuga (kushoto), akimkabidhi Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table Maternity Home, Dkt. Baturi Luhanda, mfano wa Hundi ya sh. Milioni 20, kwa ajili ya kusaidia kuchimba kisima cha maji. Wengine katika picha ni Afisa Uhusiano wa TBL, Bi. Doris Malulu (wa pili kulia), Mhandisi wa mradi huo, Bw. Onesmo Zakaria na Rais wa Rotary Klab Agnes Batenga. (Na Mpigapicha Wetu)

TWANGA PEPETA WAFANYA SHOO YA NGUVU KWENYE CLUB YA MAISHA JIJINI DAR

$
0
0
 Kiongozi na mwimbaji  wa bendi ya 'Twanga Pepeta, Luiza Mbutu (wa pili kutoka kulia), akiwa na Kalala Junior (wa pili kutoka kushoto) pamoja na  Haji Ramadhani (wa kwanza kulia) wakitoa burudani kwa mashabiki wao kwenye shoo iliyofanyika club ya Maisha jijini Dar 
 Waimbaji wa Twanga Pepeta wakitoa burudani kwenye shoo iliyofanyika kwenye club ya Maisha jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
  Kiongozi na mwimbaji  wa bendi ya 'Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akicheza moja ya nyimbo zao kwenye shoo hiyo.
 Wacheza shoo wa Twanga Pepeta wakifanya ya kwao kwenye club ya Maisha jijini Dar.
Wadau wakiwa kwenye picha ya pamoja

MAMA SALMA AHUTUBIA MKUTANO WA WAKE WA MARAIS WA UN WA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE NA WASICHANA KIFEDHA

$
0
0
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Kim Simplis Barrow, Mke wa Waziri Mkuu wa Belize na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Wanawake na Watoto. Mama Barrow kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa ndio walioandaa mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi kuzungumzia masuala ya kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha.na“First Ladies Global Call to Action Conference on Women and Girls’ Financial Health.” Tarehe 25 Septemba,2014.PICHA NA JOHN  LUKUWI
IMG_2605 
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Joyce Banda, Rais Mstaafu  wa Malawi muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi ulizungumzia namna ya kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha huko New York tarehe 25.9.2014.IMG_2632 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Sera na Mipango katika Umoja wa Mataifa Bwana John Hendra. Bwana Hendra aliwahi kuwa Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania wakati wa mkutano wa kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York tarehe 25.9.2014.IMG_2645 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika Mkutano wa kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha ulioandaliwa na Mke wa Waziri Mkuu wa Belize Mama Kim Barrow akishirikiana na Umoja wa Mataifa. Kushoto kwa Mama Salma ni Mke wa Rais wa Suriname Mama Lisbeth Venetiaan      na kulia ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ndugu Tuvako Manongi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika Mkutano wa kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha ulioandaliwa na Mke wa Waziri Mkuu wa Belize Mama Kim Barrow akishirikiana na Umoja wa Mataifa. Kushoto kwa Mama Salma ni Mke wa Rais wa Suriname Mama Lisbeth Venetiaan      na kulia ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ndugu Tuvako Manongi.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake kwenye mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa uliozungumzia masuala ya kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha huko New York Marekani tarehe 25.9.2014.IMG_2674 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake kwenye mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa uliozungumzia masuala ya kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha huko New York Marekani tarehe 25.9.2014.IMG_2682 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake kwenye mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa uliozungumzia masuala ya kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha huko New York Marekani tarehe 25.9.2014.IMG_2703 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na Mama Joyce Banda (kushoto) na wa kwanza kulia ni Mama Dianne Stewart, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uhusiano wa Shirika la United Nations Populations Fund akifuatiwa na Bi Mpule Kwelagobe, Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa MPULE Institute for Indogenous Development.IMG_2713 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa. Kutoka kushoto ni Mama Kim Barrow, Mke wa Waziri Mkuu wa Belize, Mama Joyce Banda na wa kwanza kushoto ni Mama Dianne Stewart.IMG_2718 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa. Kutoka kushoto ni Mama Kim Barrow, Mke wa Waziri Mkuu wa Belize, Mama Joyce Banda na wa kwanza kushoto ni Mama Dianne Stewart.

Usajili wa mbio za Rock City wazinduliwa Mwanza

$
0
0
Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula akionyesha fomu ya kujisajili kushiriki mbio za kilomita tano zitakazofanyika Oktoba 26 baada ya kuzindua usajili wa washiriki wa mashindano ya Rock City Marathon jijini Mwanza, jana
 Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula akiongea muda mfupi kabla ya kuzindua usajili wa washiriki wa mashindano ya Rock City Marathon jijini Mwanza jana ambapo alichukua fomu ya kujisajili kushiriki mbio za kilomita tano zitakazofanyika Oktoba 26.
 Mratibu wa mashindano ya mbio za Rock City Marathon 2014, Mathew Kasonta, akiongea wakati wa uzinduzi wa usajili wa washiriki wa mashindano hayo jijini Mwanza jana ambapo Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula, alichukua fomu ya kujisajili kushiriki mbio za kilomita tano zitakazofanyika Oktoba 26.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Riadha mkoa wa Mwanza, Charles Kimune, akiongea machache kabla ya kumkaribisha Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula, kuzindua usajili wa washiriki wa mashindano hayo jijini Mwanza jana ambapo Mabula alichukua fomu ya kujisajili kushiriki mbio za kilomita tano zitakazofanyika Oktoba 26.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Riadha mkoa wa Mwanza, Charles Kimune, akiongea machache kabla ya kumkaribisha Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula, kuzindua usajili wa washiriki wa mashindano hayo jijini Mwanza jana ambapo Mabula alichukua fomu ya kujisajili kushiriki mbio za kilomita tano zitakazofanyika Oktoba 26.


Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula amekuwa mtu wa kwanza kujisajili Kanda ya Ziwa kushiriki mbio za Rock City Marathon, huku akiwataka viongozi kuhakikisha wanafufua mchezo huo ili kuurejesha kwenye hadhi yake kimataifa.


Akizindua usajili wa ushiriki wa mbio hizo jijini hapa jana, Mabula alisema mbio hizo zinalenga kutambua na kukuza vipaji vya riadha nchini, kutangaza vyanzo vya utalii na kuongeza kipato kwa vijana ikizingatiwa kuwa michezo ni mojawapo wa fursa za ajira.


“Mnajua jinsi tunavyohangaika kutangaza utalii wetu, lakini kupitia mashindano haya ambayo yapo kwenye kalenda ya mwaka ya Chama cha Riadha Tanzania (RT) tutatangaza utalii wetu kupitia mchezo huu,” alisema Mabula na kuongeza:


“Viwango vya riadha kwa miaka mitano tangu mashindano haya yaanzishwe vimekuwa vikipanda, ambayo pia ni faida kwa wadhamini ambao wanawekeza rasilimali watu na fedha, hivyo yamekuwa na mafanikio.”


Alisema angependa mshindi wa kwanza hadi watatu atoke jijini Mwanza ili kuendelea kutoa sifa kwa mkoa huu, lakini kubwa ni fursa ya vijana kujipatia kipato kwa sababu hivi sasa michezo ni biashara.


Mabula aliwapongeza wadhamini wa Rock City Marathon kwa mwaka huu kwa kusaidia kufanikisha uandaaji wa mashindano hayo kwa mara nyingine tena katika jiji la Mwana, akiwataja kuwa ni Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Makampuni ya TSN kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy pamoja na African Barrick Gold, IPTL, Air Tanzania, New Mwanza Hotel, Nyanza Bottling, Sahara Media Group, Continental decoders, New Africa Hotel, PPF, Tanapa na Tanzania Tourist Board. 
  

Waandaji wa mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 26, Kampuni ya Capital Plus International Ltd (CPI) wamegawa washiriki kwa madaraja mbalimbali; Mashindano kwa wote itakuwa kilomita 21, kilomita tano ni kwa ajili ya walemavu wa ngozi (Albino) pamoja na washiriki kutoka makampuni na mashirika mbali mbali, Wazee kuanzia umri wa miaka 55 watakimbia kilomita tatu na watoto chini ya umri wa 12 kilomita mbili.


Naye Kaimu Meneja wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Mwanza, Shaaban Luanda ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo alisema Kazi yao kuu ni kuhifadhi jamii, hivyo kupitia michezo wanaamini watakuwa wamelinda afya ya jamii.


Awali, akimkaribisha Mabula, Makamu Mwenyekiti wa chama cha riadha mkoa wa Mwanza, Charles Kimune alisema licha ya changamoto zinazokabili mashindano hayo kwa miaka mitano iliyopita, yamendelea kupata mafanikio.


Mratibu wa mbio hizo, Mathew Kasonta alisema, “Wote mnakaribishwa kuchukua fomu zinazopatikana katika ofisi za Capital Plus International zilizopo posta mpya jengo la ATC ghorofa ya tatu, Chuo cha Mtakatifu Agustino Mwanza, Ofisi zote za Utamaduni na Michezo wilaya ya Mwanza, Uwanja wa Nyamagana na pia zinapatikana kwenye tovuti ya www.therockcitymarathon.blogspot.com

Mahojiano na kipindi cha Makutano Show kuhusu kura ya uhuru wa Uskochina somo kwa Muungano wetu

$
0
0
Mahojiano na dadangu Fina Mango katika kipindi chake cha Makutano Show kinachorushwa na kituo cha redio cha Magic FM, Dar es Salaam. Masahihisho: Katika mhojiano hayo nimeeleza kwa makosa kuwa Great Britain inaundwa na England yenye mji mkuu London, Wales yenye mji mkuu Cardiff, na GLASGOW yenye mji mkuu Edinburgh. Niliitaja Galsgow kimakosa badala ya Scotland. Kadhalika, katika mahojiano hayo kuna sehemu nimesema kimakosa kwamba moja ya ugumu ulioikabili kambi ya NO ni jinsi ya kuitetea hoja ya mafuta. Nililenga kusema 'kambi ya YES na sio NO. Mahojiano na dadangu Fina Mango katika kipindi chake cha Makutano Show kinachorushwa na kituo cha redio cha Magic FM, Dar es Salaam. Masahihisho: Katika mhojiano hayo nimeeleza kwa makosa kuwa Great Britain inaundwa na England yenye mji mkuu London, Wales yenye mji mkuu Cardiff, na GLASGOW yenye mji mkuu Edinburgh. Niliitaja Galsgow kimakosa badala ya Scotland. Kadhalika, katika mahojiano hayo kuna sehemu nimesema kimakosa kwamba moja ya ugumu ulioikabili kambi ya NO ni jinsi ya kuitetea hoja ya mafuta. Nililenga kusema 'kambi ya YES na sio NO.

PRESIDENT KIKWETE ADDRESSES THE 69TH UN GENERAL ASSEMBLY IN NEW YORK

$
0
0

President Jakaya Mrisho Kikwete exchange views with the Minister of State in the Zanzibar's First Vice President's Office  Hon Fatma Abdulhabib Fereji before the President delivered  his speech during the General Debate of the 69TH UN General Assembly in New York
President Jakaya Mrisho Kikwete speaks during the "Every Woman, Every Child High Level Event" at the Trusteeship Council Chamber of the United Nations in New York.  To his left is the Prime Minister of Canada, Hon Stephen Harper. Others from left are Ms Sue  Desmond-Hellmann,  Chief Executive Officer of the Bill & Melinda Gates Foundation, Mr Kevin Jenkins, President and Chief Executive Officer of World Vision International, Kenya;s First Lady Mama Margaret Kwenyatta, Hon Margaret Chan and The African Leaders Malaria Alliance (ALMA)  Executive Secretary, Joy Phumaphi
Part if the Tanzanian officials follow up the General Debate of the 69TH UN General Assembly in New York
President Jakaya Mrisho Kikwete delivers his speech during the General Debate of the 69TH UN General Assembly in New York
President Jakaya Mrisho Kikwete delivers his speech during the General Debate of the 69TH UN General Assembly in New York.

CHOMBO CHOCHOTE KITAKACHO KIUKA MAADILI YA HABARI KUKIONA CHAMOTO

$
0
0
Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Juma Nkamia akitoa hutuba yake kwenye uzinduzi wa Nembo ya radio Triple A fm na kuwataka wamiliki na wanahabari kuhakikisha wanafuata maadili ya taaluma ya uandishi wa habari iwe kazini au nje ya kazi zao.
Serikali imesisitiza kuwa haitavifumbia macho vyombo vya habari vitakavyo kiuka maadili ya habari na kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali vyombo hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia wakati akizindua logo ya redio Triple A fm jijini hapa huku akiwataka wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao iliwaweze kuitumikia jamii bila ya kuleta uchochezi kwa jamii utakaopelekea uvunjifu wa amani.
Naibu Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia akiwa na Bodi ta wakurugenzi wa Kampuni ya The Blue Triple A Ltd ambayo ni kampuni tanzu ya Radio Triple A fM inayoongozwa na Mkurugenzi wake kulia na kushoto Mr&Mrs Papa King Mollel wakiwa katika picha ya pamoja baada ya naibu waziri kuzindua nembo ya Radio hiyo jijini hapa

Nkamia alisema kuwa Taaluma hiyo inaweza kuileta jamii katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili uaoendelea hapa nchi au kuzidi kuumomonyoa maadili hayo kwani wao kazi yao ni kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha jamii inayovizunguka vyombo hivyo hivyo vinamchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.

"Lengo hapa ni kuhakikisha kuwa vymbo vya habari haviwi ndio kichocheo cha uvunjifu wa amani ila nawasihi muwe kichocheo katika suala zima la kupiga vita mmomonyoko wa maadili yetu kwa nyinyi mpo karibu zaidi na jamii"alisisitiza Nkamia

Kwa Upande wake Meneja wa Tcra kanda ya kaskazini Anethy Matindi aliwakemea mablogger kwa kupachika picha zinazo vunja sheria za nchi ikiwemo pia kupachika picha zisizofaa kwa jamii na kuwa dawa yao ipo inakuja
Baadhi ya viongozi wa serekali wa jiji la Arusha nao waliudhuria  uzinduzi huo.Matindi alisema kuwa imekuwa ni tabia kwa vyombo vya habari kutofuata maadili hivyo akavitaka kuacha mara moja kutumia vyombo hivyo kwa kukiuka taaluma na weledi wa tasnia hiyo

Naye meya wa jiji la Arusha Gaudency Lyimo alisema kuwa anaipongeza Triple A Fm kwa kuweza kusogeza habari kwa jamii ya wakazi wa jiji la Arusha ambapo taarifa zimekuwa zikifika kwa wakti hivyo kuchangia kukua kwa sekta mbali mbali na kuleta maendeleo kwa jamii
Meya wa Jiji la Arusha Gaudensi Lyimo akitoa nasaha chache kwa wageni waliohudhuria uzinduzi huo kwenye ukumbi wa blue Frem uliopo kwenye klabu ya usiku ya TRIPLE A NIGHTY CLUB ya jijini hapa

Mkurugenzi wa The Blue Triple A Ltd Papaa King aliwashukuru viongozi wote waliohudhuria katika uzinduzi huo huku akitabaisha kuwa Redio hiyo itafuata taratibu zote za kisheria katika kujiendesha ikiwemo kuwapa maslahi mazuri wafanyakazi wake iendane na viwango .
 Sehemu ya wafanyakazi wa Radio Triple A fm wakiwa katika picha ya pamoja kulia na kushoto kwa naibu waziri Nkamia ni Meneja wa redio hiyo Fredy Mumburi  kushoto ni mkurugenzi wa  redio hiyo Papa king molel baada ya uzinduzi wa logo ya redio hiyo jijini hapa mwishoni mwa wiki picha kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AILAUMU BENKI YA DUNIA KWA KUTOZISAIDIA NCHI MASIKINI

Mtandao wa Wanawake na Katiba Wawapongeza Wajumbe wa Bunge la Katiba...!

$
0
0
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Prof. Ruth Meena (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi na wajumbe wengine wa mtandao wa wanawake na Katiba.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Prof. Ruth Meena akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Usu Mallya (katikati) akizungumza katika mkutano huo na wanahabari. Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Usu Mallya (katikati) akizungumza katika mkutano huo na wanahabari.
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
…………………………………………………………………………………………..
MTANDAO wa Wanawake na Katiba Tanzania umewapongeza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na hasa wajumbe waliokuwa mstari wa mbele kupigania masuala mbalimbali yaliyokuwa yanapendekezwa na mtandao huo juu ya uwepo wa Katiba inayopendekezwa yenye mtazamo wa kijinsia.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Prof. Ruth Meena akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku moja baada ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma tayari kwa zoezi la kuanza kupigiwa kura kifungu kwa kifungu na wajumbe wa bunge hilo.

Prof. Meena alisema Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania haunabudi kuwapongeza wajumbe wote wa bunge maalum na hasa wale waliowaunga mkono kupaza sauti juu ya madai ambayo waliwasilisha kupitia mtandao wao na njia nyingine mbalimbali kushinikiza katiba inayopendekezwa kuwa na mlengo wa kijinsia ili kutoa usawa wa kijinsia.

Alisema Rasimu ya Katiba inayopendekeza imeonesha mwelekeo wa kutoa usawa wa kijinsia jambo ambalo mtandao huo unaamini ni mafanikio makubwa kwao na kwa jamii inayojali usawa wa kijinsia. Aliongeza kuwa yapo mambo kadhaa ambayo walipendekezwa yatajwe kwenye katiba kama umiliki wa ardhi kumtambua mwanamke na kutajwa kwa umri wa mtoto jambo ambalo wanaamini litapunguza kilio cha ndoa za utoto suala ambalo wanaharakati wa masuala ya kijinsia wamekuwa wakilipigia kelele siku zote.

“…Tunapenda kutoa pongezi kwa wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kwa moyo waliouonesha kujali masuala ya kijinsia kwa kiasi chake…tunaunga mkono rasimu ya Katiba inayopendekezwa kwa kuamini ni mwanzo mzuri wa kuonesha usawa wa kijinsia…,” alisema Prof. Meena akizungumza na wanahabari.

Kwa upande wake Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania, Usu Mallya akizungumza alisema licha ya mafanikio yao kwa mtandao wao wamehoji baadhi ya mapendekezo ambayo yamekataliwa na wajumbe hao ilhali yanamuelekeo mzuri juu ya uwajibikaji wa wanasiasa kwa wapigakura wao.

Alisema wameshangazwa na kitendo cha wajumbe wa bunge la katiba kuruhusu kipengele ambacho kimeweka utaratibu kuwa Rais wa nchi anaweza kushtakiwa ilhali wamepinga kipengele za kutoa fursa kwa wapiga kura kumuwajibisha mbunge wao baada ya kumchagua pale wanapoona ameshindwa kuwawakilisha kama walivyokubaliana. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA ZIARANI MKOANI TANGA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kulima shamba la mpunga kwenye mradi wa kilimo kwanza wa Skimu ya Mahenge.
 Mifereji ya maji kwenye shamba la skimu ya Mahenge

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyeka majani kwenye eneo la soko la sabasaba mjini Korogwe.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kujenga zahanati Mahenge kwa Mndolwa.
Mbunge wa Korogwe mjini Bw. Yusuph Nassir akielezea mipango ya maendeleo ya jimbo lake wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya Mahenge Kwamndolwa .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa vyumba vya maabara vya shule ya sekondari ya Old Korogwe.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Korogwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi ambapo aliwaasa vijana kuwa makini na wanasiasa wanaotanguliza madaraka kuliko utu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa Korogwe walifurika kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi hao kuchagua viongozi bora kwenye chaguzi zote zijazo,kuhakikisha watoto wao wanaenda shule na wasirudishwe kwa sababu ya ada na mwisho aliwasisitiza wakazi wa Korogwe kujiunga na mifuko ya Afya ya jamii.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mheshimiwa Mrisho Gambo kusalimia wananchi wa Korogwe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Mazoezi.
 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mheshimiwa Mrisho Gambo akiwahutubia wakazi wa Korogwe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi ya Mazoezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Korogwe kwenye mkutano uliokuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa na shauku ya kuuliza maswali kuhusu maendeleo yao ya Korogwe.
(Picha na Adam Mzee)

TBL YAFANIKISHA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA WIKI YA NENDA KWA USALAMA

$
0
0
 Kaimu mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka akikabidhiwa zawadi ya fulana  na Mkurugenzi wa uhusiano na sheria wa TBL, Steven Kilindo yenye ujumbe wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani baada ya mkuu huyo kuzindua rasmi upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha. katikati ni Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga na kulia ni kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Willie Mwamasika
Kaimu mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka akizungumza jambo mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya kuanza kwa wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha. kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa uhusiano na sheria wa TBL, Steven Kilindo na kulia ni Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga na kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Willie Mwamasika
 Mganga mkuu wa macho wa jeshi la polisi Dk Charles Msenga kulia akimpima uwezo wa kuona macho dereva wa kampuni ya usafirishaji wa abirianya Abood basi Morogoro, Augustino Mpepwa wakati wa uzinduzi wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya uzindui wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, zaidi ya madereva 200 wanatarajiwa kupimwa afya katika vituo vya Mikese Morogoro, Mkata mkoani Pwani na Makuyuni mkoani Arusha.

 DK YOHANA KIBONA KUMPIMA DC ANTHONY MTAKA AFYA KULIA NI DK CHARLES MSENGA MGANGA WA JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU PIX NO 5
DR YOHANA KIBENA akiwaandikisha madereva tayari kupimwa afya zao katika Hospitali ya Polisi ya Morogoro. TBL imefadhili upimaji wa afya hizo.
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images