Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 370 | 371 | (Page 372) | 373 | 374 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF umeanza kuwajengea uwezo wataalamu ngazi ya Kata kutoka mamlaka nane za utekelezaji wa mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kuwawezesha walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masini kuibua miradi inayoweza kutekelezeka ndani ya kipindi kifupi katika mpango wa miradi ya ajira kwa walengwa (Public Works Project kwa lengo la kuwaongezea kipato).

  Akifungua warsha ya kuwajengea uwezo wataalamu hao mjini Bagamoyo mkoani Pwani, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bwana Ladislaus  Mwamanga amesema miradi ya ujenzi itakayoibuliwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini itatekelezwa sambamba na Mpango wa uhawilishaji fedha kwa walengwa jambo litakalosaidia kaya hizo kuongeza  kipato hususan wakati wa kipindi cha hari.

  Bw. Mwamanga ameeleza kuwa lengo kuu la mpango huo ni kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanaondokana na umaskini ili waweze kumudu mahitaji yao muhimu kama vile kupata huduma za elimu, afya na lishe.

  "Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini haulengi tu katika kuhawilisha fedha kwa walengwa bali pia unahimiza ushiriki wa walengwa katika kazi za mikono kupitia miradi ya mbalimbali katika maeneo yao ili waweze kupata kipato, na kuwekeza" amefafanua Bw. Mwamanga.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa miradi wa TASAF Amadeus Kamagenge amesema Mpango huo ni muhimu kwa vile unatoa fursa ya ajira kwa walengwa katika Kaya Maskini, unawezesha kaya za walengwa kupata kipato zaidi, unawapataia walengwa weledi na stadi za mbalimbali wakati wa utekelezaji miradi, unawezesha jamii husika katika maeneo ya utekelezaji kuweza kuwa na rasilimali kama barabara ambazo hubaki na kuendelea kutumika pamoja na kujenga moyo wa kufanya kazi ili jamii iweze kutoka katika umaskini.

  Awali, Mtaalamu wa Mazingira toka TASAF Makao Makuu Bw. Barnabas Jachi alizitaja mamlaka za utekelezaji zitakazoanza kutekeleza mpango huo kuwa ni za Bagamoyo, Kibaha, Chamwino, Mtwara Manispaa, Lindi Manispaa na halmashauri ya wilaya ya Lindi.Warsha hizo zitafanyika katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni mkakati maalum wa TASAF kujenga uwezo wa kitaalamu katika maeneo ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini  PSSN.
    Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akifungua warsha ya kuwajengea uwezo wataalamu wa kisekta Mjini Bagamoyo.
   Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF Bw. Amadeus Kamagenge akielezea manufaa ya mpango unaotoa fursa ya ajira kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini PSSN kwa lengo la kuwaongezea fursa za kipato.
   Mtaalamu wa Mazingira toka TASAF Makao makuu Barnabas Jachi akitoa maelezo ya awali juu ya warsha ya kuwajengea uwezo wataalamu wa kisekta.
   Picha hii na mbili zinazofuatia ni Washiriki wa Warsha ya kuwajengea uwezo wataalamu wa kisekta (katika makundi tofauti) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati waliokaa) Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Miradi TASAF Bw. Amadeus Kamagenge

  0 0

   DHL Commercial Manager, Mr. Ashish Nagewadia and his colleague joined by a retailer at the launch.

  0 0

   
  Wanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wakiwa wamekaa chini na mwalimu wao pembeni kuonesha sehemu ambayo hutumika kama darasa wawapo masomoni.

  ========  ======  ======
  Tunduru

  WANAFUNZI wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wanasomea chini ya mti kutokana na darasa hilo kuendeshwa bila ya kuwa na chumba maalum kwa ajili ya kusomea wanafunzi hao.

  Hali hiyo imebainika baada ya mwandishi wa habari hizi kuitembelea shule hiyo hivi karibuni na kuwakuta wanafunzi wakiwa wamekaa chini huku wakiendelea na masomo hayo nje chini ya mti ulio na kivuli cha kuwahifadhi wakati wa jua kali.

  Akizungumza shuleni hapo Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nakayaya, Christina Mhowera alisema watoto hao wamelazimika kusomea nje baada ya huduma ya elimu hiyo kuanzishwa shuleni hapo bila ya kuwa na jengo maalum kwa wanafunzi wa awali.

  Alisema awali wanafunzi hao walikuwa wakisomea kwenye gofu (jengo mbovu) lililokuwa jirani na shule, lakini walilazimika kuondolewa baada ya jengo hilo kutwaliwa kwa matumizi mengine. Aliongeza kuwa baada ya hapo walihamishiwa kwenye nyumba ya mwalimu kabla ya kukamilika lakini waliondolewa tena na kuanza kusomea nje (chini ya mti) hadi sasa.

  Alisema darasa hilo lenye jumla ya wanafunzi 92 linaendeshwa bila ya kuwa na chumba cha darasa maalum wala madawati kutokana na shule hiyo kukabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa hadi hapo watakapopata darasa maalum kwa ajili ya wanafunzi hao.

  Kwa upande wake mwalimu wa darasa hilo, Teckla Milanzi alisema mbali na darasa hilo kutokuwa na chumba cha darasa, linakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo ya uhaba wa vitendea kazi kama vitabu na vyenzo zingine za kufundishia na hakuna bajeti yoyote inayotumwa kuliwezesha darasa hilo.

  Aidha uchunguzi uliofanywa katika shule nyingine tatu za Wilaya ya Tunduru, yaani Shule ya Msingi Nanjoka, Majengo na Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko kuangalia mazingira ya utoaji elimu ya awali katika shule hizo umebainisha kukabiliwa na changamoto nyingi hali ambayo inahatarisha msingi wa elimu kwa wanafunzi.

  Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nanjoka, Batadhari Mkwela alisema licha ya usajili wa wanafunzi wa awali kuongezeka kila mwaka kumekuwa hakuna bajeti ya kuendesha elimu hiyo.“…Darasa la awali linahitaji vitendea kazi lakini havipo, hatuna vifaa kama vitabu vya kutosha, vyenzo za kufundishia, hakuna bajeti hata ya vifaa hivi toka Serikalini, hatuna madawati maalum kwa ajili ya wanafunzi wa awali,” alisema Mkwela.

  Akizungumzia hali hiyo, Kaimu Ofisa Elimu Wilaya ya Tunduru, Abdul Kazembe alisema vyumba vya madarasa ni changamoto kubwa eneo hilo licha ya msisitizo kuendelea kutolewa wa kila shule ya msingi kuwa na darasa la awali. Alisema mwaka 2013/14 halmashauri ya wilaya hiyo ilihitaji zaidi ya milioni 366.7 lakini ililetewa zaidi ya milioni 196.5 fedha ambayo ni karibia nusu tu ya kiasi kilichopitishwa kwenye bajeti hiyo. 

  “…Kwa hiyo unaweza kuona kwamba ni ngumu kuigawa fedha hii katika matumizi maana kwanza haitoshi na pili hata kilichotegemewa kuja ni pungufu zaidi tena sana, sasa sijui unaweza kugawa kila shule ipate shilingi ngapi…kwani haitoshelezi,” Abdul Kazembe.

  Akifafanua zaidi Kaimu Ofisa Elimu huyo alisema miundombinu ya madarasa ni changamoto kubwa, kwani mwaka 2013 idadi ya mahitaji ya madarasa kwa wilaya nzima ilikuwa ni 1,715 lakini madarasa yaliopo ni 900 na kitu huku mengine yakiwa ni ya muda mrefu na yanaelekea kuchakaa.
  *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  SAM_0783
  Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akipanda boti kuelekea kisiwa cha Nyamango kulikotokea ajali ya moto kwa ajili ya kukabidhi misaada.

  Na Daniel Makaka, Sengerema.

  NAIBU Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charles Tizeba ametoa msaada kwa wahanga wa ajali ya moto na nyumba zilizoezuliwa na mvua ya upepo katika kisiwa cha Nyamango kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

  Misaada aliyoitoa kwa wahanga hao ni Blanketi mia tatu na Magunia manne ya Unga wa Mahindi na moja la Maharagwe vyote vyenye thamani ya shilingi million tatu na laki tano ambavyo vimetolewa kwa kaya hamsini na moja ambazo zilikumbwa na janga hilo Septemba 19 na 20 mwaka huu.

  Akikabidhi misaada hiyo Dk Tizeba aliwataka viongozi kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa na siyo vinginevyo lakini pia aliwaasa wahanga hao hao kutumia misaada kwa lengo la kuwasaidia wakati kamati ya maafa wilaya ya Sengerema ikiwa bado inaendelea kufanya tathimini il iione namna ya kuwasaidia.
  SAM_0723
  Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akiwa ndani ya boti kuelekea kukabidhi misaada katika kisiwa cha Nyamango jimboni kwake.

  Serikali itaendelea kusaidia kadri iwezavyo si kwamba watapewa fidia bali ni misaada tu.Awali Katibu wa kamati ya maafa wilaya Sengerema Bw. Benard Myatilo akitoa taarifa ya wahanga wa tukio hilo alisema kuwa matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo Septemba 19 majira ya saa nane usiku kaya 40 ziliteketea kwa moto na chanzo cha moto huo ni kulipuka kwa Kibatari ndani ya nyumba na tukio la pili kaya 11 kuezuliwa na mvua ilyoambatana na upepo likiwemo jengo la kanisa Katoliki kisiwani humo.

  Pia alisema kati ya wahanga hao hakuna mtu aliyejeruhiwa katika matukio hayo licha mali zote zlizokuwemo kuteketea ambapo hadi sasa kaya saba hazina mahali pakuishi huku zilizobaki zikihifadhiwa na baadhi ndugu na jamaa wanaoishi katika kisiwa hicho.
  SAM_0749
  Muonekano wa baadhi ya nyumba zilizoteketea kwa moto katika kisiwa cha Nyamango wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.
  SAM_0750
  SAM_0753
  Kanisa la Roman Katoliki katika kisiwa cha Nyamango lililoezuliwa na upepo ulioambatana na mvua.
  SAM_0775
  Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba (mwenye suti ya kijivu) akikabidhi misaada ya mablanketi 300 kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Lushamba, Deus Bitulo (kulia kwa naibu waziri) huku Mwenyekiti wa CCM tawi la Nyamango, Japhet Kafula akishuhudia tukio hilo

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kwaluguru wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara katika shule ya sekondari Kwaluguru wilayani Handeni.
  Wananchi wa kata ya Kwaluguru wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana  wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi katika shule ya sekondari Kwaluguru ambapo vyumba 83 vya maabara vinajengwa wilayani Handeni.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege kwenye moja ya vumba vya maabara za shule ya sekondari Kwaluguru.

  Mbunge wa Jimbo la Handeni Dk. Abdallah Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara akishiriki kuweka zege kwenye moja ya vyumba vya maabara vya sekondari ya Kwaluguru.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiujenzi wa ofisi ya CCM Tawi la Kweinjugo kata ya Kwaluguru wilaya ya Handeni
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akicheza ngoma ya asili ya wazigua  .

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika ambapo aliwaambia wajifunze kupima mambo ya viongozi wa siasa wasije wakaingizwa kwenye matatizo bila kutarajia kwani wapo zaidi kwa ajili ya maslahi yao binafsi na si ya wananchi ndio maana wanadiriki kutangaza maandamano wakati wao wenyewe hawapo wameenda nje ya nchi kupumzika.

  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu akisalimia wakazi wa Handeni kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia.

  Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Handeni ambapo aliwaambia watu wanatakiwa kupewa fursa na kurahisishiwa maisha yao hivyo kodi ndogo zinatakiwa ziangaliwe upya kwani zimekuwa kero kwa wafanyabiashara ndogo ndogo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na madereva wa boda boda wa Chanika Handeni.
   Watu wakiwa wamemzunguka Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kumaliza mkutano wake Soko la zamani Chanika wilayani Handeni.

  0 0


   Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt,Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya muendelezo wa harakati zake za kusaidia kuimarisha ulinzi wa Wanyama aina ya Tembo ili wasiuwawe hapa nchini,ikiwa ni Bia iliyobeba jina la Mnyama huyo,ambapo wametoa vifaa mbali mbali vya kusaidia ulinzi huo,ikiwa ni pamoja na Darubini kubwa (Binoculars) na trimble GPS ambazo zitasaidia katika harakati za kupambana na ujangili katika mbuga za wanyama nchini.Kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete.
   Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari kwenye Mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa TBL jijini Dar es Salaam,ikiwa ni pamoja na upokeaji wa vifaa kutoka kwa bia ya Ndovu Special Malt.Kulia ni Meneja wa Bia ya Ndovu,Pamela Kikuli
  Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika hifadhi ya Serengeti,Agricola Lihiru akielezea namna ya matumizi ya vifaa hivyo na faida yake katika kupambana na ujangili kwenye hifadhi za wanyama nchini.
  Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt,Pamela Kikuli akikabidhi baadhi ya vifaa hivyo kwa Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete na Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika hifadhi ya Serengeti,Agricola Lihiru.Picha zote na Othman Michuzi.

  0 0

  Viongozi na wawakilishi wa timu shiriki za Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup wakizionesha jezi watakazozitumia katika michano hiy, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni jijini Dar es Salaam.
   Dr Mwaka (kulia), Dauda wakimkabidhi mwakilishi wa timu shiriki za Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup jezi.
  Mdhamini Mkuu wa michuano ya  Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup ,Dr Mwaka akifafanua jambo mbele ya wanahabari kuhusiana na michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni jijini Dar es Salaam.
  Mmoja wa Waratibu wa Mwaka Sports Extar Ndondo Cup  Alex Luambano kutoka Clouds FM (aliyesimama) akiwatambulisha baadhi ya waratibu,wasiamizi na Wadhamini  wa Dr Mwaka Sports Extar Ndondo Cup inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya viongozi wa timu shiriki wa Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup wakiwa na waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika kwenye kiota cha maraha cha Escape One,Mikocheni jijini Dar. 
  Mratibu wa Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup kutoka Clouds FM, Shafih Dauda akielezea ushiriki wa michuano hiyo kwenye Ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Juma Kasandiko (kulia) akimkabithi vitabu mkuu wa shule ya shule ya Sekondari Shibula James Chisanda vilivyotolewa na Airtel chini ya mpango wake wa Airtel Shule yetu.
  Waalimu wa shule ya Sekondari Shibula wakifurahia vitabu mara baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Airte kukabithi vitabu hivyo chini ya mpango wake wa Airtel shule yetu ambapo shule hiyo imepokea vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi millioni moja na Laki tano
  Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shibula wakifurahia vitabu vya sayansi walivyokabidhiwa na Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel, chini ya mpango wa Airtel shule yetu Airtel ilikabithi vitabuvya sayansi vyenye thamani ya shilingi millioni moja na nusu kwa shule hiyo.
   
  ======= ======  =====
  Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Shibula iliyoko Mkoani Mwanza wamefaidika na vitabu kupitia mradi wa Airtel shule yetu ambapo Airtel imetoa msaaada wa vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni moja na Laki tano vitakavyowawezesha wanafunzi hao kupata elimu bora.

  Kwa zaidi ya miaka 10 sasa mpango huu wa Airtel shule yetu umekuwa ukisaidia shule za sekondari kwa kuwapatia nyenzo muhimu kma vile vitabu, vifaa za kufundishia , madawati, kuboresha majengo ya shule lengo likiwa ni kuboresha ubora katika kutoa elimu nchini.

  Akiongea wakati wa hafla ya kikuabithi vitabu Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Ziwa Bwana Raphael Daudi alisema “ Airtel imewekeza kiasi cha kutosha katika kusaidia malengo mkakatika katika sekta ya elimu kwa kushirikiana na serikali katika kutoa elimu bora. Kwa kupitia mradi wa Airtel Shule yetu tumeweza kuzifikia shule zaidi ya 1000 zilizoko katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuwapatia vifaa vya kujisomea na kupunguza changamoto za uhaba wa vitabu huku tukifanikiwa kupunguza uwiano wa kitabu kwa mtoto kutoka watoto 6 kwa kitabu kimoja hadi watoto 2 kwa kitabu kimoja.

  Leo tunatoa vitabu vya masomo ya sayansi ikiwemo Hisabati Fizikia, Kemia na Baiologia kwa shule ya Shibula sekondari tukiamini utachangia katika kuongeza kiasi cha ufaulu na kuchochea wanafunzi wengi kujiunga na masomo ya sayansi. Tutaendelea na jitihada hizi katika kuboresha sekta ya elimu na kuhakikisha tunazifikia shule nyingi zaidi nchini aliongeza Daudi.

  Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemema Mkoani Mwanza Juma Kasandiko ameishukuru Airtel kwa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari zilizoko mwanza na kuwaasa wanafunzi kutumia muda wao kujisomea na kuacha tabia ya utoro shuleni na kwa kufanya hivyo kutasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo na Mwanza kwa ujumla.

  Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Shibula Bwana James Elias Chitanda alisema” Napenda kuwashukuru Airtel kwa kutoletea msaada huu wa vitabu shule ni hapa, vitabu ni nyenzo muhimu katika kuongeza maarifa na ujuzi hivyo vitabu hivi vitasaidia kuhamasisha wanafunzi wengi kujisomea na kuongeza upeo, vitawasadia walimu kuandaa masomo yao na kuwahamasisha wanafunzi wengi kujiunga na masomo ya sayansi na kuongeza idadi ya wanasayansi kwa ujumla.

  Tunatoa wito kwa makampuni mengine kujiunga na kuchangia katika sekta ya elimu kwani ina mahitaji na changamoto nyingi.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa Benki ya NBC, Pius Tibarazwa, akizungumza katika hafla waliyowaandalia wanasheria kutoka makampuni mbalimbali ili kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kuwapa maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika kitengo hicho kilichopo ndani ya Jengo la Coco Plaza, Dar es Salaam jana.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa Benki ya NBC, Pius Tibarazwa (katikati), akibadilishana mawazo na baadhi ya mawakili waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kukutana na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenkizinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni, Joseph Ngiloi na Proctus Ishengoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kulia), akifurahi na baadhi ya mawakili waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni, Joseph Ngiloi, Mkurugenzi Mtendaji wa muda wa NBC, Pius Tibazarwa na wakili Proctus Ishengoma.
  Meneja Mahusiano ya Wateja wa kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha Benki ya NBC, Subira Mwaya (kushoto) akiwa na Wakili wa Kampuni ya Summit Attorneys, Bilal J. Bilal wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (katikati), akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla waliowaandalia wanasheria kutoka makampuni mbalimbali ili kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kuwapa maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Mhe. Andrew Chenge (kushoto) akiwasili bungeni kwa ajili ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, leo 24 Septemba, 2014. Kulia ni mjumbe wa Bunge hilo, Dkt. Tulia Ackson.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Bunge Maalu la Katiba, Mhe. Andrew Chenge akiwasilisha Rasimu iliyopendekezwa ndani ya bunge hilo leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongoza bunge hilo leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.


  0 0

   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akifungua mafunzo ya siku 27 kwa wakufunzi na wadadisi  kutoka  Tanzania Bara na Zanzibar  watakaoendesha  Utafiti wa Tathmini ya utoaji wa Huduma za Afya nchini 2014/15 leo mkoani Kilimanjaro.
   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza na washiriki wa mafunzo ya Utafiti wa Tathmini ya utoaji wa Huduma za Afya nchini  leo mkoani Kilimanjaro.
   Mkufunzi wa mafunzo ya wasimamizi na wadadisi wa Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya nchini Bi. Saumu Said akiendelea kutoa mafunzo kwa washiriki wa utafiti huo mkoani Kilimanjaro leo.
   Washiriki wa mafunzo ya Wasimamizi na wadadisi wa Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya nchini wakiendelea na mafunzo  yatakayowawezesha kufanya utafiti huo mkoani Kilimanjaro leo.
   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akisalimiana na wakufunzi na wadadisi  kutoka  Tanzania Bara na Zanzibar  watakaoendesha  Utafiti wa Tathmini ya utoaji wa Huduma za Afya nchini 2014/15 walio kwenye mafunzo leo mkoani Kilimanjaro.
   =======  ========  =======
  SERIKALI YAWATAKA WASIMAMIZI NA WADADISI WA UTAFITI WA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI KUZINGATIA WELEDI.
  Na. Mwandishi wetu – Kilimanjaro.
  24/9/2014.

  SERIKALI imewataka wasimamizi na wadadisi wa Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa huduma za Afya nchini mwaka 2014/15 kuzingatia weledi katika utekelezaji wa majukumu yao na kuepuka  kukusanya takwimu zisizo wakati wa utafiti huo utakaofanyika nchi nzima kuanzia Oktoba 13 mwaka huu.

  Aidha, imewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya, madakatari na wafanyakazi wa vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini  kutoa ushirikiano kwa wadadisiwatakaoendesha utafiti huo ili waweze kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika maeneo yao kwa lengo lakupata taarifa sahihi zitakazofanikisha utafiti huomuhimu kwa maendeleo ya taifa.

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku 27 kwa wakufunzi na wadadisi  kutoka  Tanzania Bara na Zanzibar  watakaoendesha  utafiti huo  amesema kuwa wakufunzi, wadadisi na wataalam  hao wanayo nafasi kubwa ya kufanikisha upatikanaji wa takwimu sahihi zitakazotoa taswira halisi ya utoaji wa huduma ya afya nchini kwa mwaka 2014/2015.

  Amesema utafiti huo utaiwezesha serikali kutathmini utekelezaji wa mipango mbalimbali nakufikia malengo iliyojiwekea kitaifa na kimataifa kwa kuboresha na kuendelea  kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wake.

  Amesema Serikali imekuwa ikitekeleza programu mbalimbali za kuboresha huduma za afya na maisha ya Watanzania kwa kupitia Mikakati ya Kimataifa na Kitaifa ikiwemo ile ya Malengo ya Milenia ya Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011 -2016).

  Amezitaja programu nyingine kuwa ni pamoja ile ya Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025, Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania Bara (MKUKUTA) na Mkakati wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA) kwa upande wa Zanzibar.

  Dkt. Seif amesema katika juhudi hizo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imekuwa na jukumu la kusimamia programu mbalimbali za afya na kufuatilia utekelezaji na utoaji wa huduma za afya nchini.

  Ameeleza kuwa wakati wa utafiti wa kwanza wa Kutathmini Utoaji wa Huduma za Afya  nchiniunafanyika na Ofisi ya Taifa ya Takwimu mwaka 2006,Tanzania ilikuwa na  jumla ya vituovya kutolea huduma za afya5669,kati ya hivyo 224  zilikuwa ni hospitali, 541 vikiwa  ni vituo vya afya na zahanati 4904.

  Amesema kumekuwa na maboresho makubwa katika sekta ya afya hadi kufikia mwaka 2013 ambapo takwimu zinaonyesha kuwepo kwa  vituo  6767 vya kutolea huduma ya afya nchini , hospitali 256, vituo vya afya 701 na zahanati 5810.

  Nyote ni mashahidi kuwa toka kipindi hicho mpaka sasa serikali imeendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi wake,sasa tuna huduma ya kuzuia maambukizi ya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ambayo inapatikana  katika vituo vyote vinavyotoa huduma za mama mjamzito” Amesisitiza.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumzia mafunzo hayo amesema kuwa washiriki watakaofaulu na kukidhi vigezo vilivyowekwa  watashiriki katika zoezi la kukusanya takwimu za utafiti huo  kwa kipindi cha miezi minnekuanzia  tarehe 13 Oktoba 2014 .

  Amesemautekelezaji wa utafiti huona mafunzo hayo unafanywa kwa pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii - Tanzania Bara, Wizara Afya - Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na Shirika la ICF International la Marekani ambao pia wanatoa ushauri wa kitaalamu katika kufanikisha utafiti huo.
   
  Dkt. Chuwa amefafanua kuwa utafiti huo utahusisha ukusanyaji wa takwimu katika sehemu za kutolea huduma za afya kwa lengo la kufahamu utayari wa vituo vinavyotoa huduma za afya na huduma bora za afya kwa wananchi.
   
  Aidha amezitaja hudumazitakazoguswa na utafiti huo kuwa ni pamoja pamoja na Huduma za Afya ya Uzazi, Afya ya Watoto, Maradhi ya Kuambukiza kama vile Kifua Kikuu, UKIMWI, Malaria pamoja na Maradhi yasiyo ya kuambukizakama vile magonjwa ya Kisukari na Moyo.
   
   Amefafanua kuwa lengola kufanyika kwa utafiti huo ni kuiwezesha serikali kujua ni kwa namna gani vituo vinavyotoa huduma ya afya vimejipanga kutoa huduma bora ya afya kwa kuangalia upatikanaji wa huduma mbalimbali, vifaa, dawa, miundombinu na rasilimali watu kwa kada mbalimbali.
   
  Kuhusu utafiti huo Dkt. Chuwa amesema ni wa pili kwa ngazi ya kitaifa ukifuatiwa na ule wakwanza uliofanyika mwaka 2006  na kuongeza kuwa utahusisha sampuli wakilishi ya vituo vya kutolea hudumavya serikali ,binafsi, mashirika ya umma na vinavyomilikiwa na madhehebu ya dini ambavyo vimetayarishwa,  hospitali maalum zote, hospitali zote za mikoa , wilayana baadhi ya vituo vya afya na zahanati.

  Naye mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Ibrahimu Msengi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema kuwamkoa huo unaendelea na juhudi za kuboresha huduma  za afya zinazotolewa katika vituo vya  afya pamoja  kwa lengo la kuboresha hali ya maisha ya wakazi wa Kilimanjaro na kukuza pato la mkoa huo.

  Amesema mkoa umeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya afya iliyopo ili iweze kuakisi ukuaji wa Pato la Mkoa na mahitaji ya wananchi katika kupata huduma za afya zilizo bora kulingana na ongezeko la idadi ya Watu.

  Amefafanua kuwa utafiti huoumekuja wakati muafaka ambapo mkoa huo na mikoa mingine nchini inahitaji kuboresha huduma za afya katika vituo vyotevya kutolea huduma.

  0 0

  SAM_0535
  Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Nyerembe Munasa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Bima la Taifa (NIC) katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kitaifa jijini Arushaa  katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid, ,aliyeshika mice ni meneja wa shirika hilo Mkoa wa Arusha na Manyara Bw.Godwin Ole Kambaine
  SAM_0534Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)Mkoa wa Arusha na Manyara Bw.Godwin Ole Kambaine akitoa maelezo mafupi kuhusu shirika hilo kwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Nyerembe Munasa mara baada ya kutembelea banda hilo jijini Arusha katikati  ni meneja masoko na utafiti wa shirika hilo kutoka makao makuu Bw.Elisante Maleko
  SAM_0529
  Mdau aliyetembelea banda hilo la Shirika la Bima la Taifa (NIC) akiwa anauliza maswali yanayohusu shirikika hilo lengo nikutaka kufahamu zaidi shughuli za shirika,kushoto ni Afisa wa Bima Bi.Costancia Komanya
  SAM_0526
  Meneja masoko na utafiti wa shirika la Bima la Taifa (NIC) kutoka makao makuu Bw.Elisante Maleko akiwa anatoa ufafanuzi kwa mdau aliyefika katika banda lao ambapo alisema kuwa pamoja na bima nyingine pia wanatoa huduma ya bima ya matibabu (madecare) ambao ni mpango maalum wa shirika hilo kutoa matibabu kwa wananchi wa kada zote itakapotokea kaumwa na michango ni midogo.
  SAM_0521
   Muonekano wa banda la shirika la Bima la Taifa (NIC) katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabaranijijini Arusha
  Meneja masoko na utafiti wa shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elisante Maleko amewataka watanzania kuona shirika hilo ni mali yao kwa kuwa shirika hilo ni mali ya umma na michango ni midogo hivyo kila mwananchi kumudu
  Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na  wadau mbalimbali waliyotembelea banda lao katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid jijini Arusha
  Bw.Maleko alisema kuwa shirika hilo lina bima ya matibabu amabayo ni mpango maalum wa shirika hilo kutoa kinga ya matibabu kwa wananchi wa kada zote itakapotokea kuumwa na michango ni midogo na kila mwananchi anamudu kujiunga na huduma zinapatikana nchi nzima
  Pia alisema Bima za nyumba  inakinga na majanga ya wizi,moto,tetemeko na mafuriko hivyo kuwataka wananchi kukatia nyumba zao bima(Habari na Picha Pamela Mollel wa jamiiblog)

  0 0

   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani, linaloendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha. Kongamano hilo limefunguliwa leo Septemba 24, 2014.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia burudani ya ngoma ya asili wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Septemba 24, 2014 kwa ajili ya kufungua Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani.
    Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Septemba 24, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amkabidhi zawadi Shadrack Kishimba, kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani, linaloendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, amkabidhi zawadi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani, linaloendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
   Picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Dkt. Joan Pastor, (kulia) na Lesedi Lesetedi baada ya kufungua rasmi Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani, linaloendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mtoa mada, Faith Basiye kutoka nchini Kenya (wa pili kushoto) baada ya kufungua rasmi Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani, linaloendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha. Kulua kwa Makamu ni Emmanuel Johannes. Picha na OMR.

  0 0

  WASANII_6[1]
  Msanii wa filamu nchini Tanzania maarufu kama Mzee Chilo akiwa katika picha ya pamoja na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Angellah Kairuki leo 24 Septemba, 2014 katika viwanja vya Bunge hilo mjini Dodoma.
  WASANII_7[1]
  Kiongozi wa msafara wa wasanii walifika katika Bunge Maalum la Katiba Bw. Simon Mwakifwamba akiwa katika picha ya pamoja na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Angellah Kairuki leo 24 Septemba, 2014 katika viwanja vya Bunge hilo mjini Dodoma.
  WASANII_27[1]
  Baadhi ya wasanii wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fenella Mukangara (wa pili toka kushoto) wakati alipokutana nao maeneo ya viwanja vya bunge hilo leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.WASANII_10[1]
  Baadhi ya Wasanii wakijadiliana jambo mara baada ya kutoka nje ya Bunge Maalum la Katiba leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  WASANII_33[1]
  Wasanii wakiendelea kumsikiliza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fenella Mukangara wakati alipokutana nao maeneo ya viwanja vya bunge hilo leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  WASANI_50[1]
  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fenella Mukangara akiwa katika picha ya pamoja na wasanii maeneo ya viwanja vya bunge hilo leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

  0 0

   Waandishi wakiwasili kituo cha kupoza umeme Mbagala wakipokewa na Meneja Miradi Mhandisi Emmanuel Marirabona,(wa tatu kushoto) wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba,(kushoto) na Meneja Miradi-Ufuaji Umeme, Mhandisi Simon Jilima,(wa pili kushoto). 
   Transfoma ya kuchuja nguvu za umeme iliyopo Mbagala.
   Wafanyakazi wakiendelea na kazi katika kituo cha Mbagala.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco,Felchesmi Mramba,(kulia) na Meneja Miradi Emmanuel Marirabona.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene (kulia) akizungumza na waandishi zamira ya kutembelea vituo vya kuzalisha Umeme Jijini Dar es Salaam akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco,felchesmi Mramba.
   Waandishi wakiwa katika kituo cha Umeme Gongolamboto.
   Transfoma ya inayowekwa Gongolamboto.
   Mashine ikisafisha mafuta ya transfoma yaliyopo katika mapipa.
   Mafuta ya transfoma
   Waandishi wakiwa kituo cha Kinyerezi.
   Maofisa habari wa Tanesco.Neema Mbuja (wa pili kushoto) na Khadija Ahamed (kulia).
   Waandishi wakioneshwa eneo la Kinyerezi.
   Jengo la Utawala likiendelea kujengwa kituo cha Kinyerezi.
   Waandishi wakipewa maelezo na Meneja Miradi -ufuaji umeme,mhandisi Simon Jilima (katikati)
   tenki litakalowekwa maji ya kuzimia moto endapo utaleta taabu Kinyerezi.
  Transfoma kubwa iliyopo kituo cha Kinyerezi.

  0 0

  Photo Credits: UN Photo/Ryan Brown
  Septemba 23, 2014, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk Jakaya Kikwete, ambaye pia ni kiongozi wa kamati ya viongozi wa nchi na serikali za Afrika kuhusu mabadiliko ya tabianchi alihutubia kikao kilichoandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Kin Moon kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi duniani. 
  Hii ni hotuba yake, kwa hisani ya Umoja wa Mataifa

  0 0


   Abate mstaafu wa Abasia ya Peramiho Jimbo kuu katoliki la Songea Lambert Doerr OSB katikati wa kati akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa Waumini wa Parokia ya Mbingamharule Wilayani Songea Mkoani Ruvuma,kama sehemu ya kumpongeza baada ya kutimiza miaka 50 ya Umisionari hapa Nchini.
  Waumini wa Parokia ya Mbingamharule Jimbo kuu katoliki la Songea mkoani Ruvuma,wakifuatilia kwa makini adhimisho la misa Takatifu ya shukurani ya kutimiza miaka 50 ya Umisionari ya Abate mstaafu wa Abasia ya Peramiho LambeDoerr hapa Nchini.(PICHA NA JULIUS KONALA) 
  -----------------
  Na Julius Konala wa demasho.com,Songea
  BAADHI ya Wasomi mkoani Ruvuma,wamemtaja Abate mstaafu Lambert Doerr OSB wa Abasia ya Peramiho kuwa ni Mwanahistoria wa karne ya 21 kutokana na mchango wake mkubwa wa kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo hapa Nchini ikiwemo katika nyanja ya Elimu.

  Matamko hayo yalitolewa na Wasomi hao kwa nyakati tofauti wakati walipokuwa wakitoa mada mbalimbali katika kongamano lililoandaliwa kwa ajili ya kuzungumzia juu ya maisha na kazi zilizofanywa na Abate huyo katika kipindi chake cha miaka 50 ya Umisionari hapa Nchini lililofanyika kwenye ukumbi wa Nyerere chuo kikuu cha Sauti tawi la Songea.

  Akitoa mada katika kongamano hilo Padre Dr.Xsaver Komba,alisema kuwa moja ya mchango wa uliotolewa na Abate Lambert wakati akiwa Mwalimu bora na mwadilifu katika Seminari ndogo ya Likonde na Seminari kuu ya Peramiho alifundisha kwabidii kwa kufuata misingi ya ualimu iliyopelekea  kutoa wasomi wengi ambao miongoni mwao ni viongozi wakubwa wa Serikali na Dini.

  Alisema kuwa michango mingine aliyoitoa ni pamoja kuwaunganisha Waafrika kuwa kitu kimoja na wazungu kwenye nyumba za kitawa, kuwasomesha baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mbinga Mharule kwa kuwalipia ada ya shule,kusogeza huduma ya maji safi na salama kwa kilometa saba,kujenga zahanati,ujenzi wa barabara ya Lambert yenye urefu wa kilometa tatu,kusaidia wazee wasiojiweza,watoto Yatima pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya dini ya kikristu na waislamu.

  Alisema kuwa maadhimisho hayo ya Jubilei ya miaka 50 ya Umisionari Nchini yatakwenda sambamba na na uanzishwaji wa chuo cha ufundi cha Mtakatifu Lambert mjini hapa kitakachotoa fani ya kompyuta,ushonaji na uselemala kama sehemu ya kumuenzi.

  Naye mmoja wa watoa mada na mwanafunzi  aliyefundishwa na Abate huyo,Dr.Damas Mbogoro ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali hapa Nchini alimwelezea Abate Lambert kuwa ni mtu  ambaye hakuwa mchoyo wa elimu na kudai kwamba alikuwa karibu na watu katika kusikiliza shida na matatizo yao.

  Kwa upande wake mgeni rasmi katika kongamano hilo,Padre Dastan Mbano ambaye alimwakilisha Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Songea Damian Dallu,alisema kuwa Abate Lambert ni hazina kubwa sio kwa upande wa kanisa peke yake bali ni kwa jamii nzima.

  Mbano alisema kuwa kazi nzuri na kumbukumbu za Abate huyo zinapaswa kutangazwa,kuenziwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya faida ya vizazi vijavyo huku mwakilishi wa Baraza la mila kasian Shauritanga,alisema kuwa wamisionari Wabenediktini wa Abasia ya Peramiho watakumbukwa kwa mchango wao wa kusaidia kutunza kumbukumbu za mila na desturi za wangoni katika makumbusho ya vita ya majimaji na kuupatia mkoa na taifa kwa ujumla sifa pekee ya utunzaji.

  0 0

  DSC_0014
  Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye, akiwakaribisha na kuwatambulisha wawezeshaji kwa washiriki wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika masuala ya masoko na Tehama kwa mameneja na waandishi wa habari takribani 60 kutoka Redio jamii mbalimbali nchini, yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.

  Na Mwandishi wetu, Sengerema.
  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema litaendelea kusaidia kuimarika kwa redio za jamii nchini kwa kuwa ndio nyenzo muhimu za maendeleo ya wananchi kwa kuwapa sauti katika huduma na shughuli zao.

  Kauli hiyo imetolewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa mameneja na watendaji takribani 60 kutoka Redio jamii mbalimbali nchini, mafunzo yanayofanyika kwenye kituo cha Redio Sengerema FM.

  Katika mafunzo hayo watendaji hao watafunzwa masuala ya Tehama na utafutaji wa soko kwa lengo la kufanya redio hizo kuwa endelevu na kujiendesha zenyewe kwa kuweza kutekeleza miradi yake na kuendelea kushirikiana na wananchi.
  Mafunzo hayo ni utekelezaji wa mradi wa miaka mitatu wa kuwezesha redio za jamii nchini unaoendeshwa na UNESCO baada ya redio hizo nyingi kusaidiwa kuanzishwa katika miaka ya karibuni.
  DSC_0045
  Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akizungumza na Mameneja na waandishi wa habari kutoka redio tisa za jamii wanaohudhuria mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika masuala ya masoko na matumizi ya Tehama yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Kushoto mgeni rasmi Ofisa mdhani kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed.

  Kwa mujbu wa Yusuph mradi wa SIDA ambao umekuwa ukitekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu umeshughulika na uboreshaji wa redio hizo ili kuzipatia uwiano na pia kuziwezesha kutumia Tehama kuhabarisha wananchi pia kutokana na mafanikio yaliyopatikana mradi huo utaendelea kwa miaka mingine mitatu.

  Ametaja mafanikio hayo kuwa yamepatikana kwa ushirikiano wa Redio za jamii pamoja na shirika hilo hali iliyofanya kuyavuta mataifa mengine kuchangia kwa ajili ya kuendelea kuzijengea uwezo redio za jamii kupitia shirika hilo.

  Ameongeza kuwa kufanikiwa kwa redio za jamii nchini Tanzania katika mradi huu wa SIDA kumefanya mashirika mengi yanayotaka kufanyakazi na wananchi wa kawaida kukimbilia UNESCO kutambua redio za jamii ambazo zinaweza kufanyakazi nayo. Mradi huo wa Tehama unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO ni sehemu ya mradi wa UNESCO katika nchi saba za Afrika , Tanzania ikiwamo.
  DSC_0036
  Baadhi ya Mameneja na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali za jamii wakimsikiliza Bw. Al Amin Yusuph kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.


  Katika mafunzo hayo yanayofanyika mjini Sengerema, elimu inatolewa kwa wakuu wa vituo na waandishi wa habari kutoka redio Micheweni FM, Orkonerei FM, Pambazuko FM, Mtegani FM, Kahama FM, Redio FM, Kyela FM, Fadeco Radio na Pangani FM.

  "Kuna mambo mengi yamefanikiwa.. kikubwa zaidi kumpa nafasi mwananchi kujieleza na kueleza matumaini yake.." alisema Yusuph ambapo aliongeza kwamba kutokana na mradi huo kufanikiwa zipo nchi na mashirika ambayo yapo tayari kuchangia uimarishaji wa redio za jamii nchini.Hakuzitaja nchi hizo.

  Alisema kutokana na mafanikio yaliyopo ya redio hizo kuwa karibu na jamii, SIDA kwa kushirikiana na UNESCO wametengeneza programu hiyo ili kuwezesha kuwepo kwa matumizi ya mtandao katika kukusanya habari, kuziboresha na kuzitumia kwa manufaa ya wananchi.
  DSC_0005
  DSC_0060
  Ofisa mdhamini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi Redio Jamii Micheweni, Ali Mohamed, akitoa baraka zake tayari kuanza mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika masuala ya masoko na Tehama mameneja na waandishi wa habari takribani 60 kutoka redio za jamii mbalimbali nchini, yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.

  Alisema kutekelezwa kwa mradi huo ni utekelezaji wa azimio la Windhoek la mwaka 1991 linalohimiza matumizi ya redio jamii katika kuboresha maisha ya wananchi kutokana na kuonekana dhahiri kwamba wananchi wanapokuwa na nafasi ya kujieleza wanaweza kufanya makubwa zaidi.

  Akifungua mafunzo hayo Ofisa mdhamini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar na Mjumbe wa bodi ya usimamizi redio jamii Micheweni, Ali Mohamed aliwataka mameneja na watendaji wa radio hizo kutekeleza ushauri wa UNESCO ikiwa na pamoja na kutekeleza maagizo ya utengenezaji wa vipindi vya vijana ili kupata nafasi ya kushindania nafasi moja ya upendeleo kwenda Paris , Ufaransa mwakani kwa tamasha la redio za jamii.

  Aidha aliwataka watendaji kuwa makini katika kazi zao kutokana na serikali kuweka mazingira sahihi ya uendeshaji wa radio hizo kwa manufaa ya umma.
  DSC_0092
  Mkufunzi wa darasa la mameneja wa redio mbalimbali za jamii Mkurugenzi Mtendaji wa ASMET, Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha mafunzo ya siku tano ya namna ya kuingiza kipato pamoja na kutafuta masoko kwa ajili ya kuendeleza vituo vyao yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yanayoendelea kwenye kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.
  DSC_0079
  Baadhi ya mameneja wa redio mbalimbali za jamii wanaohudhuria mafunzo ya siku tano ya masoko na ujasiriamali yanayofadhiliwa na mradi wa SIDA na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
  DSC_0120
  Meneja wa kituo cha redio Orkonerei FM, Bw. Lucas Kariongi akihoji swali kwa mkufunzi wakati wa mafunzo hayo.
  DSC_0101
  Mhasibu wa kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre, Bw. George Tumbo akiongaza washiriki wenzake katika kazi za vikundi wakati wa mafunzo hayo.
  DSC_0171
  Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akiendesha mafunzo ya matumizi ya Tehama kuwajengea uwezo wa kuweka kumbukumbu za vipindi na kukusanya vyanzo vya habari kwa kutumia "Tablet" kwa waandishi wa habari wa redio mbalimbali za jamii yanayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na shirika la UNESCO yanayoendelea kwenye kituo cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
  DSC_0156
  Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akitoa maelekezo ya matumizi ya "TABLET" katika kuhifadhi na kuandaa habari kwa kutumia kifaa hicho.
  DSC_0142
  Pichani juu na chini ni washiriki wa mafunzo hayo wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Teknolojia mpya ya "TABLET".
  DSC_0136

  0 0


   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Special Representative of the UN Secretary General on Sexual Violence in Conflict Dr.Zainab Bangura at the UN Headquarters in New York this morning.
   -President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets with Queen Maxima of the Netherlands in her capacity as United Nations Secretary General Special Advocate for Financial Inclusion for Development at the UN Headquarters in New York. Third Left is the Permanent Secretary in the Ministry of Finance Dr. Servacius Likwelile and fourth left is Tanzania’s Permanent Representative in the UN Ambassador Tuvaku Manongi(photos by Freddy Maro).

  0 0

   Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Penehupifo Pohamba, Mke wa Rais wa Namibia muda mfupi kabla ya kuhudhuria mkutano Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu masuala ya saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti na saratani ta tezi la kiume (prostate cancer) huko New York tarehe 24.9.2014. Mkutano huo umefadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Taasisi ya Princess Nikky Global Initiative ya nchini Nigeria. 
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Debby Rechler (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Yvonne Feinstein ambao ni wafanyakazi wa Tanzania Children Fund wakati wa mkutano wa Wake wa Marais uliofanyika huko New York nchini Marekani tarehe 24.9.2014. Aliyesimama kushoto kwa Mama Salma ni Jill Bishop, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TET Foundation ya Marekani.

   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kikao cha Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kichozungumzia masuala ya saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti na saratani ya tezi la kiume huko New York tarehe 24.9.2014. 
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mama Penehupifo Pohamba mara baada ya kuhutubia mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika uliofanyika New York tarehe 24.9.2014. Katikati ni Princess Nikky Onyeri, Mmiliki wa Taasisi ya Princess Nikky Global Initiative and Forum of African First Ladies Against Cervical,Breast and Prostate Cancer ya Nigeria. 
   Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika wakimsikiliza Mama Salma alipokuwa anahutubia mkutano huo. 
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Princess Nikky Onyeri (kushoto) na Gill Bishop mara baada ya mkutano. PICHA NA JOHN  LUKUWI.

older | 1 | .... | 370 | 371 | (Page 372) | 373 | 374 | .... | 1897 | newer