Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 369 | 370 | (Page 371) | 372 | 373 | .... | 1898 | newer

  0 0
 • 09/23/14--00:57: KINANA AITEKA CHALINZE PWANI
 •  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kiwangwa ambapo alikagua jengo jipya la wodi ya Wazazi.Kituo cha afya cha Kiwangwa kina uwezo wa kuhudumia watu zaidi ya elfu kumi.
   Katibu Mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali ya ujenzi wa ofisi za CCM kata ya Kiwangwa.
   Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akishiriki ujenzi wa jengo la kituo cha afaya kata ya Miono.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa kata ya Miono
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya Miono ambapo aliwaambia wawe makini katika kuchagua viongozi wa kijiji ili kuepusha migongano na migogoro ya ardhi zinazodaiwa kuuzwa kwa wawekezaji
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka Miono baada ya kumaliza mkutano wake na wananchi wa hapo.
   Soko la Mbwewe ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilikagua, soko hili limegharimu zaidi ya shilingi milioni 200.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wazazi na wanafunzi wa shule ya msingi Msata ambapo alisisitiza wazazi kuwasomesha watoto wao .
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwenye eneo la shule ya msingi Msata mara baada ya kukagua madarasa mawili na maktaba ya kujisomea.
   Kada maarufu wa CCM na Msanii wa ushairi Latifa Kizota akighani utenzi unaofahamika kama Kidumu chama chetu wakati mkutano uliofanyika Chalinze mjini.
   Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akiwasabahi wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara mjini Chalinze.
   Umati wa wakazi wa Chalinze ukimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Chalinze.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akihutubia wananchi wa Chalinze.
   Wakazi wa Jimbo la Chalinze wakisikiliza kwa makini
   Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia wakazi hao na kuwasisitiza juu ya masula muhimu ikiwa kuchagua viongozi bora,kuwapeleka watoto shule ,kujiandikisha huduma za afya ya jamii na matumizi bora ya ardhi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli kwa Makatibu Kata.

  0 0


  Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari mfumo wa usambazaji umeme kwenye Moja kituo cha Mradi “Tanzania Energy Development and Access Program (TEDAP)” unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, kilichopo Mbagala kitakachozalisha megawatt 100 za umeme, kituo hiki kinatarajiwa kuanza kutoa huduma za umeme wa uhakika kwa wakazi wa maeneo ya Kurasini, Kigamboni, Mbagala na Maeneo ya Mkuranga kuanzia Mwezi Agosti, 2015.
  Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi Mbagala lenye MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.
  Baadhi ya mafundi wakiedelea na kazi ya kusuka Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi Mbagala lenye MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba akiwaeleza waandishi wa Mikakati inayowekwa na shirika hilo ikiwemo kutekeleza miradi mbalimbali ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza Umeme ili kuhakikisha wanakabiliana na Tatizo la Umeme Nchini,wakati wa Ziara kwenye Mradi wa “Tanzania Energy Development and Access Program (TEDAP)” unaotekelezwa katika maeneo ya Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwaeleza waandishi wa habari kufurahishwa kwake na ziara hii iliyoratibiwa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) yenye lengo la kuona nini Shirika hilo linatekeleza katika jitihada za kukabiliana na Tatizo la Umeme Nchini.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akimweleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto) wakati wa ziara kwenye Miradi ya umeme Katika Eneo la Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.
  Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Neema Mbuja akiwaeleza jambo wahandisi Emmanuel Manderabona(Kushoto kwake) na Saimon Jilima, wakati wa ziara kwenye Miradi ya umeme Katika Eneo la Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari mtambo wa kuongoza umeme uliopo katika eneo la Gongo la Mboto uliowekwa mfumo wa Sakiti Mzunguko (Ring Circuit) kwenda Mbagala, Sakiti Mzunguko ni Mzunguko mkubwa utakaotoa fursa ya upatikanaji wa umeme kwa muda wote kwani umeme ukikosekana eneo moja ni rahisi kuunganisha kwa kupitia upande wa pili na umeme ukaendelea kupatikana.
  Mitambo Miwili iliyofungwa katika kituo cha KINYEREZI ONE yenye uwezo wa kuzalisha Megawatt 150 za umeme utakaogawanywa katika sehemu mbili kuingia katika gridi ya Taifa, ikiwa ni kujenga msongo wa kilovolt 220 kwenda Kimara na kujenga laini ya msongo wa kilovolt 132 kwenda Gongo la Mboto, Kituo hiki kitagharimu Dola za Kimarekani Milioni 183.
  (PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO)

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his opening remarks during a meeting of the Committee of African Heads of State and Government on Climate change(CAHOSCC) held today at the office of the Permanent Observer Mission of the African Union(AU) to the United Nations in New York. On the right is the Chairperson of the African Union Commission Dr. Nkosazana Dlamini Zuma. In his remarks,President Kikwete who is also the Coordinator of CAHOSCC reiterated his call on the need for Africa to speak with one voice in advancing and championing the continent’s common position and interests on Climate Change.
  Delegates who attended the session on Climate Change in New York. (photo by Freddy Maro).

  0 0

   Ukipitia takwimu za mwaka huu na mwaka jana inaonyesha Nchi za Ulaya na Marekani zimeendelea kuathirika zaidi na uhalifu mtandao, Huku Nchi za mashariki ya kati kuonekana kunyemelewa na wahalifu mtandao. Wakati huo huo takwimu zilitabiria Nchi za Afrika  kuwa katika hali mbaya baadae kutokana na ukuaji wa kasi wa matumizi ya mitandao ambao hauendani sanjari na maandalizi madhubuti ya usalama wa mitandao.

  Mengi yalizungumzwa kuhusiana na tishio jipya katika nchi za kiarabu huku kampuni inayojihusisha na ulinzi mtandao ya Kaspersky wakiandika "NCHI YA SAUDI ARABIA" imedhamiriwa zaidi na wahalifu mtandao kauli ambayo iliambatana na "UTAFITI" ukibainisha kampuni za mashariki ya kati zimeendelea kulengwa na wahalifu mtandao.

  Hatua hiyo ilisababisha nchi hizo za mashariki ya kati kuwekeza zaidi na kuimarisha jitihada zake za mapambano dhidi ya uhalifu mtandao. "JEDDAH" iliyoko Saudi Arabia ilianzisha kituo kipya kilicho imarishwa maalum kwa ajili ya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao na Hivi karibuni "JORDAN" nao wakazindua kituo chao maalum kwa ajili ya kupambana na uhalifu mtandao.

  Vile vile nchi nyingine za Mashariki ya kati (ME) zimeendelea kuwekeza na kufungua vituo maalum kwa ajili ya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao katika ukanda huo ambapo imeenda sambamba na uboeshwaji wa sharia mitandao.

  NINI TUNAJIFUNZA KAMA TAIFA?

  Tayari imezoeleka nchi za ulaya na Marekani zimekua vinara kwenye kuwekeza katika mapambano dhidi ya uhalifu mtandao kutokana na athari kubwa ambayo tayari imesha ziona.Na hivi sasa inaonekana Nchi za Mashariki ya kati nazo zikiwekeza katika upande huo.   Nchi za Afrika pia zimeendelea kujipanga na kkuwekeza kwenye sekta hii ambayo inaonekana kuwa tishiokubwa mapema baadae. Jitihada zilizopo zinapaswa kuendana sambamba na kuweka vizuri sharia mtandao huku itafutwa njia rafiki itakayofungua mipaka kwenye mapambano dhidi ya uhalifu huu mtandao ambao hauna Mipaka.


  Maboresho ya mara kwa mara yanahitajika kwenye vituo maalum vya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao pamoja na kuwa na mapitio ya sheria mtandao mara kwa mara kutokana na mabadiliko na ukuaji wa teknolojia inayochangia kasi ya uhalifu mtandao kuongezeka. Haya na mengine nimepata kuya ainisha  kwa kina kwenye andiko linaloweza kusomeka "HAPA"

  0 0


  Shirika la Nyumba la Taifa limetoa mashine hizo zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni 12 pamoja na mafunzo kwa vijana ya wiki mbili ambapo baada ya kumaliza mafunzo Shirika litatoa msaada wa shilingi laki tano kwa kila kikundi kama mtaji , yMakabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Kibaha wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu .Abdulrahman Kinana.
  #Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa pwani Pauline Mrango kwa kutoa mashine 28 za kuwasaidia vijana.2 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali zilizotolewa na shirika la nyumba la Taifa kwenda kwenye halmashauri zote za mkoa wa Pwani.3 
  Hizi ni baadhi ya mashine
  111213 
  Baadhi ya wafanyakazi wa NHC.

  0 0

   Warembo 15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya wengine 15 kufanyika Arusha mjini. Na Father Kidevu Blog.
   Msanii wa Bongo Fleva  Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.
   Warembo wenzao waliobakia wakishangilia burudani ya vipaji kutoka kwa washiriki wenzao.
   wadau wa sanaa ya Urembo Babati wakifuatilia shindano hilo.
  Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, akiwa na waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na Mfanyabiashara Mohamad Bajwa.
   Tunda Man aliburudisha vilivyo ukumbini hapo.
   Jopo la majaji likifuatilia kwa makini shindano hilo

   Ilikuwa ni shwangwe kwa warembo hao ambao wapo Mikoa yua Kaskazini kwa ziara ya kimafunzo katika hifadhi za Taifa.

  0 0
 • 09/23/14--02:59: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0

     Mdau wa Sanaa Henry Mdimu (Kulia) akisisitiza umuhimu wa kuwa na mitandao ya kijamii kwa wasanii (hawapo pichani) katika Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Kushoto ni Afisa Sanaa wa BASATA, Augustino Makame.
     Afisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristides Kwizela (Kulia) akisisitiza jambo kwa Wasanii (Hawako pichani) wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika mapema wiki kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala, Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Katikati ni mdau wa Sanaa Henry Mdimu na Afisa Sanaa wa Baraza hilo Augustino Makame.
    Wadau wa Sanaa pamoja na Wasanii wakipata elimu kuhusu Nafasi ya Mitandao ya Kijamii katika Kukuza Sekta ya Sanaa kwenye mapema wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA.
   =========  ======= ========
  Wasanii wamesisitizwa juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwani waandaaji wa matamasha na matukio mbalimbali ya kisanaa sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakiitumia katika kuwapa kazi.

  Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa lililofanyika mapema wiki hii kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam, mdau wa Sanaa Henry Mdimu alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona wasanii wakitumia kurasa zao kuonesha mambo binafsi kama ya mapenzi na matusi wakati zinapaswa kutumika kwa ajili ya kazi zao za Sanaa na kuwasiliana na mashabiki wao.

  Alisisitiza kwamba si kila kitu kinapaswa kuwekwa kwenye kurasa za kijamii za wasanii na kwamba lazima wasanii wajifunze kutenganisha maslahi au masuala yao binafsi dhidi ya yale ya wapenzi wao na kwamba Sanaa iko kwa ajili ya walaji na si wasanii pekee.

  “Wasanii hawana budi kuelewa kuwa hawatengenezi sanaa au kurasa za mitandao ya kijamii kwa ajili yao. Wanaitengeneza ili kuwasiliana na mashabiki wao kuhusu kazi wazifanyazo na kutafuta fursa za masoko na kazi nje. Lazima waelewe mapromota wa kimataifa hutumia sana kurasa hizi katika kutoa fursa” alisisitiza Mdimu.

  Aliongeza kwamba, msanii yeyote anayefanya kazi ya Sanaa kama kazi yake lazima afikirie kutumia mitandao hii ya kijamii kiweledi katika kujitangaza kwani kutokufanya hivyo ni bora kufanya kazi nyingine maana hiyo ndiyo njia kuu kwa sasa ya kujitangaza na kupata fursa za maonesho mbalimbali ya kimataifa kwa gharama nafuu.

  Kwa upande wake Afisa Sanaa kutoka BASATA, Augustino Makame alisema kwamba Baraza limekuwa mstari wa mbele kusisitiza matumizi sahihi ya teknolojia za kupashana habari muiongoni mwa wasanii na kwamba sasa ni muda wa wasanii kuona umuhimu wa mitandao hii ya kijamii na kuitumia ipasavyo katika kukuza Sanaa zao.


  0 0

   Benjamin Sawe
  Bagamoyo

  Taasisi ya Sanaa Bagamoyo imeaswa kuendelea kutoa mafunzo ya sanaa na utamaduni  ambayo yatakidhi mahitaji ya soko  kwa nchi za Afrika Mashariki.

  Hayo yamesemwa na Bw Makongoro Nyerere kwa niaba ya  Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Margaret Ntantongo Zziwa katika Ufunguzi wa Tamasha la 33 la sanaa na utamaduni wa Mtanzania lililofanyika katika Taasisi hiyo mjini Bagamoyo jana

  Bwana Makongoro alisema Sanaa na Utamaduni vinaweza  kutumiwa kuelezea masuala yote  yanayomuhusu binadamu na mazingira yake hususani suala zima la utaliii

  Alisema ni wakati mwafaka kwa jamii kuondokana na dhana ya kuona watalii ni wale wa kutoka nje ya nchi na kusahau kuwa wale wa ndani ambao kwa idadi kubwa ni wengi wa kuwezesha Serikali kukusanya maduhuli ya kutosha.

  Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa TaSUBa Bw. Michael Kadinde alisema sanaa hutumika kuelimisha jamii katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na  Utawala Bora, kuhifadhi mazingira, madahara ya rushwa katika jamii, namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya  Ukimwi na aina nyingine nyingi za utoaji elimu katika jamii.

  Alitolea mfano wa sanaa ya ngoma, nyimbo, hadidhi simulizi, majigambo, uchoraji  na sanaa  nyingine nyingi za makabila mbalimbali vinaeleza  utamaduni wa Mtanzania hivyo  huwa kitambulisho cha jamii.

  Bw. Kadinde alisema sanaa huonya na kutaadhalisha jamii juu ya mambo mabaya yanayoweza kuleta madahara katika jamii ikiwa ni pamoja na kuendekeza rushwa, Vijana au jamii nzima kuwa na tabia zisizokuwa  na heshima .

  Aliomba Bodi ya Utalii ya Tanzania mahali palipo na vituo vya Utalii viwatumie wahitimu  wa TaSUBa kuanzisha vikundi vya sanaa ili watangaze utalii wa nchi ili na kuongeza mapato ya nchi na jamii kwa ujumla

  Alisema kutoa mafunzo ya Sanaa na Utamaduni kwa nchi za Afrika Mashariki kuna changamoto zake ikiwa ni pamoja na upanuzi wa miundombinu ili kukidhi mahitaji ya ufundishaji ambapo iliyopo haiwezi kubeba mzigo mzito wa kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa nchi za Afrika Mashariki.

  Tamasha la sanaa Bagamoyo lilianzishwa mwaka 1982 ambapo mwaka huu kauli mbiu yake ni “Sanaa na Utamaduni katika kukuza utalii”.

  0 0
 • 09/23/14--03:25: Article 7
 • SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA

   


  TAARIFA KWA UMMA KUKANUSHA UVUMI WA KUAJIRI VIJANA 500 NA KUWAPATIA MASOMO YA MAFUTA NA GESI
   Kuna taarifa zimeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na maelezo kuwa:  " Serikali kupitia Shirika la Elimu Tanzania, TPDC kwa ushirikiano na kampuni za oil and gas, wanatarajia kuajiri vijana wapatao 500 katika sekta hii mpya Tanzania kuanzia mwezi Januari na Machi 2015, hivyo wameandaa crush program itakayoanza 6 Oktoba 2014. 

  Walengwa ni vijana wenye elimu ya form 4 na form 6 ambao watasoma kwa miezi 6 na kupelekwa kwenye ajira  moja kwa moja baada ya kuhitimu!..kwa wale wenye elimu kuanzia diploma watasoma kwa miezi 3, kozi ya oil and gas management!...Ada kwa kundi la kwanza ni tshs 1,150,000 na kundi la pili ni Tsh 550,000. Kwa yeyote mwenye kuhitaji fursa hii akachukue fomu Shirika la Elimu Tanzania, application form ni Tsh 20,000 na deadline ni tarehe 30 Septemba 2014".  TPDC inapenda kuwaeleza Watanzania kuwa habari hizo si za kweli na kwamba TPDC haijafanya makubaliano yoyote na Shirika la Elimu kuhusu suala hilo. TPDC inawaasa Watanzania kuchukua tahadhari ya matangazo ya aina hiyo na inapotokea, tafadhali wasiliana nasi kwa namba za simu zilizooneshwa hapo nchini.  IMETOLEWA NA

  KITENGO CHA MAWASILIANO,

  SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA

   

                            BWMPensions Towers, TowerA,

                            Junctionof Azikiwe /JamhuriStreets

                    P. O. Box2774,

                    Tel: +255 22 2200103/4

             Dar-es-Salaam, Tanzania

  0 0

  Na James Festo, Njombe.

  CHAMA cha wanasheria wanawake Nchini Tawla kimewataka wananchi kuacha  kuwanyanyasa wanawake wenye virusi vya ukimwi na watoto  badala yake  kuanza kuwawezesha ili kuweza  kujikwamua kiuchumi  na baadhi yao  kuwalea watoto wao ambao wamekuwa wameachiwa na wazazi wanzao.

  Akizungumza  katika uwasilishaji wa taarifa ya utafiti uliofanywa na
  Tawla,katika kipindi  mwezi februari na  machi kwenye warsha ya siku
  mbili iliyowashirikisha wadau 30 kutoka Mkoa wa Njombe na Iringa,
  mjumbe wa Bodi ya chama hicho Bi. Annamarie Mavenjina alisema kuwa
  katika utafiti huo walioufanya walibaini kuwepo kwa unyanyasaji
  ukiwemo wa ngono ambao unaendelea kusababisha kuongezeka kwa
  maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi .

  Alisema kuwa utafiti huo uliofanyika katika mikoa sita ya Dar es
  Salaam, Pwani, Mbeya, Katavi, Iringa na Njombe  wamelazimika kukaa na
  asasi za kiraia, viongozi wa serikali  pamoja na Dawati la Jinsia na
  Watoto kutoka jeshi la polisi ambao wamekuwa wahusika wakubwa kwa
  kupokea malalamiko hayo, kwa lengo la kubadilishana nao ujuzi juu ya
  namna ya kukabiliana na matatizo ya ukatili wa kijinsia katika sehemu
  hisika.

  Aidha Bi. Mavenjina alisema kuwa mara baada ya kumaliza kuwasilisha
  utafiti wao katika mikoa hiyo utakaochukua muda wa mwezi mmoja
  utekelezaji wa mradi huo utaanza na miongoni kwa shughuli kubwa
  watakayoifanya ni kuhakikisha wanawasaidia wanaonyanyaswa kisheria.

  Akiongea katika ufunguzi wa warsha hiyo  afisa ufuatiliaji na tathmini
  wa Tawla , Juma Mwenga alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuhakikisha
  kila mwanamke anapata uelewa wa namna gani ya kuweza kukabiliana
  namatukio ya unyanyasaji wa kijinsia na kuweza kufikisha taarifa
  sehemu husika ili kulitokomeza kabisa tatizo hilo.

  Alisema kutokana na ukubwa wa  maambukizi ya virusi vya ukimwi katika
  mkoa wa Njombe ndio uliosababisha kuwepo kwa unyanyasaji hali
  inayosabasha waathirika hao kutopata haki zao, hivyo Tawla imeamua
  kuona jinsi gani ya kushughulikia malalamiko ya kesi za ukatili wa
  kijinsia nakuanza kutoa elimu  kwa jamii.

  Naye Abubakar Magege ni Mratibu wa tume ya kuthibiti maambukizi ya
  Ukimwi Mkoani Njombe TACAIDS, aliwaomba wadau mbalimbali kuendelea
  kusaidia kutoa elimu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi ili kila
  mwananachi apateuelewa wakutosha na hatimaye lengo la kufikia
  maambukizi kuwa sifuri litimie.

  "kuelekea kwenye sifuri tatu ambazo sisi kama Nchi tutajipima  ifikapo
  mwaka 2017 kuna sifuri moja ya unyapaa  na lengo ni kushuka kwa
  unyanyapaa kutoka asilimia 31.9 hadi asilimia sifuri ambapo watu
  watakuwa wanatumia dawa bila ya kunyanyapaliwa na tunawaomba wadau  wengine waendelee kutoa elimu mkoani hapa"alisema Magige.

  Kwa upande wao baadhi ya wadau  wakizungumza ni kwa kiasi gani mradi
  huo utaweza kusaidia kupunguza unyanyasaji wa kijinsia katika  mikoa
  hiyo, WP Linda  kutoka dawati la jinsia   kituo cha polisi Mkoani
  Iringa  alisema kuwa kwa sasa wamekuwa wakipokea kesi mbalimbali
  hivyo warsha hiyo itawaongezea ujuzi zaidi katika ufanyaji wa kazi.

  "Warsha hii tumeipokea vizuri kwanza imetuongezea uelewa katika
  utendaji wa kazi,  tatizo lililopo hivi sasa ni wanawake wengi
  wamekuwa hawana uelewa wa kutosha juu ya unyanyasaji  hivyo tumekuwa
  tukitumia mikutano na sehemu mbalimbali zenye mikusanyiko kuendelea
  kutoa elimu" alisema WP Linda.

  Naye Mwelimishaji wa masuala ya ukimwi kutoka mkoani Njombe, Jane
  Gadau ambaye pia alikiri kuwa ni muathirika wa virusi vya ukimwi
  alisema  katika ufanyaji wake wa kazi amekuwa akianza kupata mafanikio
  kwa wananchi kuanza kuelewa namna ya kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

  "niligundulika  kuwa na virusi vya ukimwi mwaka 2001 tangu hapo nikawa
  natumia dawa hadi hii leo, nimekuwa mwelimishaji kwa wananchi wenzangu   na kuwasihi kuwa muwazi na kujiunga na vikundi vitakavyokuwa  vinawezeshwa na  serikali"alisema Bi. Gadau.


  0 0

   Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (kushoto) akifuatilia maonyesho mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana, katikati ni Mtendaji mkuu TaSUBa Bw. Michael J. Kadinde na kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko.
   Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kati akipiga ngoma kama ishara ya uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
   Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kulia akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TaSUBa Bw. Ghonche Materego wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana. Picha hii imechorwa sura ya Mhe. Makongoro na msanii aliyefaamika kwa jina la Sunday Richard Kamangu.
  Baadhi ya watazamaji wakifurahia mambo yalivyokua wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana. Picha zote na: Genofeva Matemu - MAELEZO.
  Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kushoto akimpa mkono wa pongezi msanii Sunday Richard Kamangu baada ya kupokea zawadi ya picha iliyochorwa na msanii huyo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.

  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kushoto, na Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi kulia wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yanaendelea wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
   Wasanii kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo wakitoa burudani  wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.

  0 0

   Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu akiwaeleza waandishi wa Habari (Hawapo pichani) waandishi wa Habari kuhusu Miradi iliyotekelezwa kwa ajili ya kupunguza msongamano katika halmashauri hiyo, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Bw. Frank Mvungi.  Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya IlalaBw. Batimagwa James akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na Manispaa hiyo katika kuhakikisha barabara zinakuwa kwenye hali nzuri katika kipindi chote cha mwaka.kulia ni Afisa Uhusiano wa Halmashauri hiyo Bi Tabu Shaibu.HASSAN SILAYO-MAELEZO.
   
  =========  =======  =======

  HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kupitia Idara ya Ujenzi inahudumia barabara zenye urefu wa kilomita 536.9 ambazo kati ya hizo kilomita 144.2 ni za lami, kilomita 64.7 ni za Changarawe na kilomita 328 ni za udongo.  Huduma hizi ni pamoja na kujenga, kukarabati na kusimamia sheria za matumizi ya barabara katika eneo la Manispaa ya Ilala.

  MIRADI ILIYOTEKELEZWA HADI SASA KWA AJILI YA KUPUNGUZA NSONGAMANO
  Ujenzi wa Barabara ya Mazengo hadi Kibasila kwa kiwango cha Lami Km.1.2
  Ujenzi wa Barabara ya Lindi kwa kiwango cha Lami Km. 0.7
  Ujenzi wa barabara ya Vingunguti  Baracuda- urefu wa 1.3 km unaendelea na tayari mita 880 ziko hatua kuanza kuweka lami nyepesi na lami ngumu. 

  UCHONGAJI WA BARABARA ZA UDONGO
  Halmashauri imeweza kutekeleza kazi za uchongaji wa barabara za udongo na changarawe kwa kutumia greda lake moja.  Barabara zilizochongwa ni za maeneo ya kata za Ukonga, Pugu, Majohe, Kivule, Msongola, Chanika, Kitunda, Kinyerezi, Tabata, Kimanga, Gongolamboto, Kipawa, Kiwalani, Vingunguti, Upanga Mashariki, upanga Magharibi, Gerezani Ilala, Jangwani, Mchikichini na Buguruni. Barabara hizi zimekuwa zikiharibika wakati wa kipindi cha mvua zinapokuwa nyingi mathalani mvua zilizonyesha katika Mkoa wa Dares Salaam na kuleta maafa. Barabara nyingi ziliharibika kiasi cha kutopitika kabisa hali iliyoathiri huduma mbalimbali.
  Kwa kuliona hilo na kuhakikisha kuwa Barabara hizi zinapitika wakati wote Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imenunua Magreda mawili (2) kwa gharama ya Tshs 1.2 billioni. Pamoja na jitihada hizo yapo maeneo mawili ambayo kwa sasa ni kero

  ENEO LA HYDARI PLAZA
  Eneo hili hujaa maji wakati wa Mvua kutokana na kuwepo kwa Chemba za Maji taka zinazotiririsha maji barabarani na kusababisha mashimo ambayo yamekuwa adha kwa watumiaji wa barabara hiyo. Halmashauri imekuwa ikiziba viraka vya lami bila mafaikio. DAWASCO ambao ndiyo wamiliki wa chemba hizo wametakiwa kuzikarabati chemba zao.  Halmashauri inaendelea na maandalizi ya kuweka zege badala ya lami ili eneo hilo liweze kupitika kwa urahisi.  Kazi hii itafanyika mapema katika mwaka huu wa fedha 2014/2015.

  ENEO LA SHULE YA UHURU WASICHANA HADI UHURU MCHANGANYIKO – BARABARA YA LINDI
  Eneo hili lilifanyiwa ukarabati wa mfereji wa maji ya mvua ili kuyaingiza katika kalavati kuu lilopo katikati ya barabara ya Mismbazi, kisha lami iliwekwa.  Lakini kufuatia eneo hilo kutumiwa na Daladala za Temeke/Tandika – Kariakoo bila udhibiti wa kutosha wameharibu mferefi huo na kusababisha maji kutuama na kuharibu tabaka lote la lami,  Halmashauri ina kusudia kuujenga upya mfumo wa maji ya mvua na kuweka lami kipande hicho katika mwaka wa fedha 2014/2015.

  MASHIMO YA BARABARANI
  Uchakavu wa barabara za lami hasa maeneo ya katikati ya Jiji (Kata na Gerezani, Kivukoni, Kisutu, Mchafukoge, Jangwani, Kariakoo, Upanga mashariki na magharibi). Hali hii inatokana na barabara nyingi katika maeneo haya kuchoka (kuzeeka) kwani nyingi zilijengwa katika miaka ya 1990. Uchakavu huu unachangia kuwepo kwa mashimo mengi kwakuwa zinaharibika kwa wakati mmoja.
  Jambo lingine linalochangia uharibifu wa barabara na kuwa na mashimo ni ukataji ovyo wa barabara kwa lengo la kuweka na kukarabati miundombinu ya maji safi na taka na mikonga ya mawasiliano ya simu. Wakandarasi ambao hurusiwa kufanya kazi hiyo huchukua muda mrefu kurejesha barabara katika hali ya awali. Hali inasababisha maji ya mvua kutuama na kuharibu tabaka la barabara. Halmashauri imekuwa ikiyaziba mashimo hayo kulingana na hali ya upatijanaji wa fedha, Hata hivyo bado hali haijawa bora kwani Barabara hizi zinahitaji matengenezo makubwa ya kuwekwa Lami upya.

  CHANGAMOTO
  ·         Uhaba wa fedha za kukidhi mahitaji ya matengenezo mapya na ukarabati wa barabara, madaraja makalavati na mifereji ya maji ya mvua ukilinganisha na ukubwa wa mtandao wa barabara.
  ·         Ukataji holela wa barabara kwa malengo ya kuweka mifumo ya maji safi, maji taka, mawasiliano (fibre cables), n.k kinyume cha utaratibu ambapo Halmashauri hutoa vibali na kusimamia urejeshaji wa miundombinu iliyoharibiwa.
  ·         Wizi wa mifuniko ya chemba za maji ya mvua kwa ajili ya biashara ya chuma chakavu. 
  ·         Utupaji ovyo wa taka na michanga barabarani, hali hii inasababisha kuziba kwa mifereji ya maji ya mvua na kusababisha uharibu wa barabara kutokana na mafuriko, madibwi makubwa ya maji.  Hii ni kero kwa watumiaji wa barabara.
  ·         Wananchi kuunganisha mfumo wa maji taka ya majumbani kwenda mifereji ya maji ya Mvua.  Hususan katika Kata za Gerezani, Kariakoo, Jangwani, Kisutu na Mchafukoge ambapo baadhi yao wamekamatwa na kutozwa faini na kisha kuziba mifumo hiyo.  Kitendo hiki kinasababisha kuwepo kwa harufu mbaya katika maeneo mbalimbali kwa watumiaji wa Barabara. 

  Mikakakati
  ·         Halmashauri inaendele a kuweka mifuniko ya mifereji ya maji ya mvua. Hadi sasa jumla ya mifuniko 410, ambapo 250 imewekwa kwenye chemba zilizo kuwa wazi na 160 ipo kwa ajii ya dharura
  ·         Kujenga mifereji mipya ya maji ya mvua katika sehemu korofi.
  ·         Kuunda kitengo kitakachodhibiti uzito wa magari kwa kuweka mizani zinazohamishika katika maingilio yote ya barabara kuu za kuingia katikati ya Halmashauri kwa masaa 24.

  Imeandaliwa na;
  Tabu F.Shaibu- Afisa Uhusiano
   


  0 0

   President Jakaya Mrisho Kikwete greets Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
    President Jakaya Mrisho Kikwete invites  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
   President Jakaya Mrisho Kikwete in talks with  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue and their delegation who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
   President Jakaya Mrisho Kikwete bids farewell to Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
   President Jakaya Mrisho Kikwete chats with President Zuma of South Africa and First Lady Bongi Ngema-Zuma during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York
    President Jakaya Mrisho Kikwete chats with President Zuma of South Africa and First Lady Bongi Ngema-Zuma during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York
   President Jakaya Mrisho Kikwete greets American civil rights activist and Baptist minister  Rev. Jesse Louis Jackson, Sr during a reception of the occasion of 20 years of Freedom and Democracy of South Africa held at the River Club 447 in New York
   President Jakaya Mrisho Kikwete chats with Mama Graca Machel when they met in Washington DC
   President Jakaya Mrisho Kikwete makes his keynote speech for the 3rd Bunengi African First Ladiues Discussion of Science, Technology, engineering and Mathematics (STEM) in New York
   President Jakaya Mrisho Kikwete makes his keynote speech for the 3rd Bunengi African First Ladiues Discussion of Science, Technology, engineering and Mathematics (STEM) in New York.STATE HOUSE PHOTOS

  0 0

   Mkurugenzi Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mikazi Bw. Justo Lyamuya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taratibu za upimaji wa viwanja nchini na kutoa tahadhari kwa wananchi kutumia makampuni ambayo hayakusajiliwa katika shughuli za upimaji Ardhi, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu wa Baraza la Upimaji na Uthamini wa Wizara Hiyo Bw. Nassor Duduma.  Katibu wa Baraza la Upimaji na Uthamini wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mikazi Bw. Nassor Duduma akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu ufuataji wa Sheria katika shughuli za upimaji ardhi kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1957 sura namba 324, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Wizara Hiyo Bw. Clarence Nanyaro. Hassan Silayo-MAELEZO

  0 0


  Mkuu wa kitengo cha sheria CHADEMA, Tundu Lisu, (Katikati), akiongozana na washtakiwa kwenye kesi ya kukusanyika isivyo halali wakati wakitoka mahakama ya wilaya ya Dodoma Jumanne Septemba 23, 2014. Lisu ambaye alikuwa akiwatete washtakiwa hao ambao baadhi yao ni viongozi wa chama hicho mkoani Dodoma, alisema, walishtakiwa kwa kosa la kukusanyika isivyo halali hapo Septemba 18, mwaka  huu,wiki iliyopita na waliachiwa huru kwa dhamana.
  Lisu akiongozana na washtakiwa wakati wakitoka mahakani hapo, Jumanne Septemba 23, 2014

  0 0

   
  Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
   
   
  Mitandao ya kijamii ni mizuri katika kuhabarisha umma endapo inatumiwa kulingana na madhumuni iliyotengenezwa, kwani ina nguvu ya kusambaza habari kwa haraka na kwa wakati hapa duniani.
   
  Pamoja na umuhimu nwa mitandao hii ya kijamii, kuna baadhi ya watu ambao wao hujiona kuwa wameendelea katika ulimwengu wa kisayansi na teknolojia kiasi cha kuanza kuitumia mitandao hiyo kinyume na malengo kwa kutumia kuiba taarifa mbalimbali za watu na hata usalama wa maeneo muhimu ikiwemo benki, ofisini, mashuleni na sehemu kadha wa kadha.
   
  Watu hawa kwa jina la kisayansi na teknolojia hujulikana kama ‘Hackers’ au Wezi wa mitandao kwa kisawahili, na wamekuwa wakivumbua mbinu mbalimbali kila kukicha ili kuweza kutimiza adhma yao ya kuingilia mitandao mingi iliyopo duniani na wakati mwimngine wamekuwa wakitumika katika shughuli za kigaidi ulimwenguni.
   
  Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali toka mitandaoni, kuna mbinu nyingi zitumiwazo na hackers hawa katika kuiba taarifa mbalimbali kutoka kwenye takirishi (Computer) hata simu za mkononi kwa njia ya mtandao (internet) na njia hizi huwa zimekuwa zikiboreshwa kila kukicha.
   
  Wezi wa mitandao wengi wamekuwa wakitumia visaidizi vya kompyuta (softwares) zijulikanazo kama Keyloggers ambazo ni hatari sana katika kuiba taarifa toka sehemu yoyote endapo tu mmiliki wa kompyuta ataiacha kompyuta yake kutumiwa na watu wasiofahamika ama katika ofisi mtu mharibifu ataingia na kuingiza katika mfumo wa kuongozea kompyuta kisaidizi kama hiko, kutokana na hilo software hizo hukusanya taarifa za mtu pasipo mtumiaji kujua kinachoendelea na taarifa hizo hutumwa kwa njia ya barua pepe kwenda kwa mharifu ambaye yeye anakuwa anazipata kadri atakavyo juu ya chochote akifanyacho mtu, na moja ya sifa za software hizo ni kwamba hazionekani ndani ya mfumo wa kuongozea kompyuta kirahisi.
   
  Mbinu nyingine watumiazo watu hao ni kwa njia ijulikanayo kwa kimombo kama ‘Phising’ ambapo ukurasa unaofanana sawia na ukurasa halisi wa website hutengenezwa kwa madhumuni thabiti ya kuiba nenosiri ama taarifa zozote kuhusiana na kitu chochote, njia hii ni hatari pia ingawa haina tofauti sana na njia ile ya key logging kwani katika njia hii kazi kubwa inayofanyika ni kuweko kwa kurasa feki ambayo inayofanana na kurasa halisi ya website fulani.
   
  Ili tuweze kujikinga na matukio haya ya wizi wa taarifa kwa njia ya mtandao kuna mambo muhimu ya kuzingatia ambayo tunapaswa kuwanayo makini wakati wote tunapozitumia kompyuta zetu.
   
  Kwaza kabiasa, ili tuweze kujiepusha na njia itumiwayo na hackers ijulikanayo kama Key-logging ni vema kuepuka kuazimisha kompyuta zetu kwa watu tusiowajua ama kutumia mbinu ya kubofya kitufe cha Ctrl + shift + Alt + K vyote kwa pamoja ili kuweza kujua uwepo wa kisaidizi kama hiko katika kompyuta na kama ikitokea kimekuja kisanduku kinachokudai kuweka nenosiri basi ujue hapo kuna mtu anachunguza taarifa zako katika kompyuta yako pasipo wewe kujua, hivyo chukua tahadhari kwa kumtafuta mtaalam aweze kuondoa kisaidizi hiko.
   
  Pia yatupasa kuhakikisha kuwa Windows Firewalls zilizopo ndani ya mifumo ya kuongozea kompyuta zetu ziko wazi wakati wote kwani firewall inasaidia kulinda takirishi yako dhidi ya wezi wa mitandao (hackers) ambao wanaweza kujaribu kuiharibu kwa lengo la kutaka kupata taarifa zilizomo ndani, kufuta taarifa, na hata kuiba baadhi ya neno siri za baadhi ya taarifa zako.
   
  Ili kujikinga na wizi wa taarifa zetu katika kompoyuta zetu, tunapaswa kuzingataia kuingiza ama ku-update Vizuizi virusi (Antivirus) mara kwa mara kwani vizuizi hivyo vimetengenezwa kwa ajili ya kuzuia virusi ama visaidizi kompyuta chokozi ili zisiweze kuiingia ndani ya mfumo wa kompyuta na endapo ikitokea imegundua kirusi cha namna yoyote ile, basi inafanya kazi ya kukiondoa ama kukifanya kisiweze kudhuru kompyuta wakati wote.
   
  Bila shaka lolote, Virusi vinaweza kuharibu mfumo wa kuongozea kompyuta pasipo mtumiaji mwenyewe kujua licha ya baadhi ya vizuizi virusi kuwa na tabia ya kuji-update vyenyewe.
   
  Kuweka ama ku-update Antispyware Technology ni jambo linghne la usalam dhidi ya hackers kwani Baadhi ya spyware huwa na tabia ya kukusanya taarifa za mtu pasipo ridhaa yake kama ilivyo kwenye key-logging na Phising au huwa na tabia yakuweka matangazo yasiyo na ulazima katika kurasa Fulani iliyopo katika mtandao wa kompyuta, sasa hii ni hatari kwa usalama wa taarifa za mtu kwani hutumika pia kukwapua, hivyo hatunabudi kuwa makini na baadhi ya matangazo yenye kututaka kupakua visaidizi fulani pasipo malipo kwani mara nyingi huwa ni feki na wakati mwingine huwa na virusi vyenye kuweza kutumika kuiba taarifa ndani ya takirishi yako.
   
  Katika hali yoyote ile ni vema kwa watumaiji wa mitandao ya kijamii kuepuka kutunza nenosiri katika kompyuta zao kwa lengo la kuondoa usumbufu wakati wanapotaka kuingia tena katika kurasa zao kwani njia hiyo nayo ni hatari kwasababu mtu anapoacha nenosiri lake liko (logged in) au unaposema (remember me next time) unatengeneza njia rahisi kwa hacker kujua nenosiri lako kwa kufanya kitendo kijulikanacho kama (Inspect elements Q) yaani zile doti zinazowakilisha neno siri lako (******).
   
  Katiko hilo, mharifu anachokifanya hapo ni kuhailaiti hizo doti (nyota) kisha anabofya katika kipanya upande wa kulia (right clicking) kisha anaenda mwisho katika sehemu iloandikwa (inspect elements Q) kisha anafanya uhariri (editing) katika kipengele kilichokuwa hailaitedi kwa rangi ya bluu kilichoandikwa neno ‘passoword’, hapo anafuta na kuandika neno ‘TEXT’ kisha anabofya kitufe cha ‘Enter’ na akishamaliza kufanya hivyo nenosiri lenyewe linajibadilisha kwenda mfumo wa maneno badala ya doti kama ilivyokuwa hapo mwanzo, hivyo humuwezesha kujua tarakimu za nenosiri la akaunti yako ya mtandao wa kijamii uliocha wazi.
   
  Njia nyingine ya jinsi ya kujikinga na wizi wa kimtandao, tunahitaji kuwa makini na vitu tunavyopakuwa toka mitandaoni hasa vibebaji (attachments) toka kwa watu tusiowafahamu au wakati mwingine kwa watu tunaowajua kwani hata hao hutumika katika kusaidia kuibwa kwa taarifa zetu kwa malengo yao binafsi.
   
  Pia ni vema kuepuka kukubali marafiki tusiowajua katika mitandao mingi ya kijamii ikiwemo facebook, twitter, Whatsapp, na mingineyo kwani baadhi ya hackers wanatumia majina yasiyosahihi (fake names) kuomba urafiki kisha hutumia mwanya huo pia katika kuiba taarifa zetu kiurahisi.
   
  Kwa upande wa mabenki, ni vema kuachana na mifumo ya kizamani ya kuongozea kompyuta iliyounganishwa na Mashine za kutolea fedha maarufu kama (ATM) au Automatic Teller Machine kwa kimombo, kwani hiyo ni hatarishi kwasababu mifumo ya kizamani, mfano Microsoft Windows XP ni mifumo ilikwishapitwa na wakati na hata Kampuni yenyewe ya Microsoft imewataka watumiaji kuwa makini nayo kwani haina-updates tena hali inayopelekea kuwa katika hatari ya kuvamiwa na wezi wa mitandao kwa kutumia software za kisasa zenye uwezo wa hali ya juu katika kuiba taarifa.
   
  Katika matumizi ya kadi zetu za kutolea fedha benki (ATM Cards) tunapaswa kuwa makini kuepuka kushea namba za siri kwa marafiki au wapenzi na tujitahidi kuacha tabia ya kutumia nenosiri la kadi hizo kama nenosiri katika akaunti za mitandao ya kijamii kwani hackers nao wamekuwa watu wazuri wa kubashiri taarifa pindi wanapomlenga mtu.
   
  Ili kujiweka salama dhidi ya wezi wa mitandao, basi tujitahidi kutoa taarifa zozote za kiusalama kwa vyombo vya usalama yaani Polisi au kupeleka malalamiko kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pindi tunapoona taarifa za uvunjwaji wa sheria za matumizi ya mitandao, mfano mtu akiona kuna hitilafu katika taarifa za muamala wa fedha zake katika akaunti yake ya benki fulani basi atoe taarifa kwa benki husika ili wao waweze kutafuta tatizo na kutoa ufumbuzi.

  Pamoja na haya yote Watanzania wamehimizwa kuacha matumizi mabaya ya mitandao ya jamii ikiwemo kuweka picha za utupu, kusababisha ugomvi, kuwahimiza wengine kwa mambo yasiyo ya kweli, kupotosha jamii na kuvuruga maendeleo.

  Akitoa rai hiyo Meneja mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bwana Innocent Mungy alisema kuwa kuna ongezeko la matumizi ya intanenti kwa watanzania hasa mitandao ya kijamii ambayo ni facebook, twiter, Instagram, BBM, LinkedIn na Blogs mbalimbali kwa mambo yasiyofaa na kuleta athari kwa jamii.

  Alisema matukio yanayofanyika katika mitandao hiyo na kuleta athari ni utapeli, kulipiza kisasi na ugomvi unaoanzia mitandaoni na kuendelea hadi kwenye uhalisia.

  “Kuna utapeli wa kutumia huduma za mawasiliano na ugomvi wa makundi yakugombana kupitia mitandao kwa majina kama timu fulani na timu fulani inayosababisha kuvunjika kwa amani na kusababisha matusi pande zote,” alisema Mungy.

  Mungy aliongeza kuwa ni kosa la jinai kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 na kutaka mawasiliano yatumike vizuri kudumisha amani ya Tanzania.

  “Mamlaka inapenda kuukumbusha umma kuwa ni kosa la jinai kuuza laini ya simu iwapo siyo wakala au mtoa huduma, kutumia simu isiyosajiliwa, kutumia njia yeyote ya mawasiliano kuvuruga amani na kumsaidia mtu mwingine atende kosa,” alisema.

  Kwa mujibu wa Mungy ni kosa la jinai kuweka picha za marehemu, mtoto na zinazoonesha utupu katika mitandao ya kijamii huku akibainisha kwamba faini ya kosa hilo ni shilingi za Kitanzania 750,000 na kifungo cha miezi mitatu gerezani.

  Kutokana na haya, lazima tutambue kuwa mitandao ya kijamii si dhambi wala si vibaya kuitumia, kwani haijatengenezwa kwa madhumuni ya kumkomoa fulani ama kwa lengo la kuelimisha watu juu ya namna ya kuiba taarifa za watu wengine, bali inetengenezwa ka madhumuni ya kuwakutanisha watu wa sehemu mbalimbali duniani kuweza kuhabarishana juu ya mambo mbalimbali japokuwa baadhi ya watu hao wamekuwa wakiitumia vibaya kinyume na maelngo ya uwepo wake.

  0 0

   
   Mmoja wa Marappa mahiri kutoka nchini  Marekani atambulikae kwa jina la Clifford Joseph Harris,'T.I' ni mmoja wa wanamuziki watakaoangusha bonge la shoo la kusambaza upendo kwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake,katika onesho la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika ndani ya Viwanja vya Leaders Club   jijini Dar es Salaam Oktoba 18.
  T.I atafanya makamuzi pamoja na wasanii wengine mahiri wa hapa nchini,watakao pangwa kushusha bonge la burudani kwa wale watakaobahatika kupangwa kwenye orodha ya Oktoba 18, mwaka huu jijini Dar. 

  Nguli huyo mwenye albamu nane ambazo ni I'm Serious, Trap Muzik, Urban Legend, King, T.I. vs. T.I.P., Paper Trail, No Mercy na Trouble Man: Heavy Is the Head ambapo nyingi kati yake zimefanya vyema katika soko la muziki. 

  T.I ameshinda tuzo tatu za Grammy tangu aanze safari yake ya muziki.  

  Baadhi ya singo kali alizoachia mkali huyo na kufanya vyema ni "Bring Em Out", "What You Know", "Big Shit Poppin' (Do It)", "Swagga Like Us" (FT Kanye West, Jay-Z na Lil Wayne), "Dead and Gone" (FT Justin Timberlake), "Ball" (FT Lil Wayne) na "No Mediocre" (FT Iggy Azalea).

  0 0


  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (katikati) pamoja na Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Rufaro Chatora (kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa kuboresha ushirikiano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

  Shirika la Umoja wa Mataifa nchini UN lakutana na wanahabari kujadiliana na kudumisha ushirikiano wao katika habari ambapo wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wamekuna na viongozi mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ili kujadili kwa pamoja.

  UN wameeleza kazi zinazofanywa na shirika hilo ili waweze kushirikiana kwenye mambo mbalimbali katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, elimu na kuzifahamu kazi za mashirika hayo hapa nchini.

  Hivyo waandishi na wahariri wa habari wameombwa kudumisha ushirikiano katika kazi zote zinazofanywa na mashirika yanayosaidia nchini kwa kiasi kikubwa. Pia wameweza kuzungumzia ugonjwa wa Ebola ambao umeibuka kwa kasi sana hivyo kuwataka kuweza kuandika habari zinazowajuza jamii ili kuweza kuuepuka.

  Nia na madhumuni ya mkutano huo na wahariri wa vyombo vya habari ni kuweza kujenga ushirikiano madhubuti baina yao na kuweza kushirikiana kwa karibu katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wahiriri wa vyombo vya habari nchini ambapo alielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini ikiwemo utekelezaji wa agenda mbalimbali za malengo ya milenia.
  Bwana Clioni akiendesha mjadala baina ya viongozi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini.
  Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan akitoa salamu kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati wa mkutano wa kuendeleza ushirkiano baina ya Umoja wa Mataifa na vyombo vya habari nchini.
  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole akitoa shukrani kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati walipokutana na wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuboresha ushirikiano na mahusiano baina yao.
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha mkutano huo baina ya Umoja wa Mataifa na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.
  Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kuboresha mahusiano baina yao na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
  Untitled
  Mkutano ukiendelea huku wengine wakipitia makabrasha mbalimbali yenye taarifa za Umoja wa Mataifa.
  Mmoja wa wahariri akihoji swali kwa viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakati wa mkutano huo.
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa wakati wa mkutano huo.
  Picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa kuboresha mahusiano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mashirika ya umoja wa mataifa nchini.
   

  0 0

  SAM_0448
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo akimkabidhi Tuzo mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya BE FORWARD TANZANIA bw. Daniel Mtaalam  wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kitaifa jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid, kwa kutambua mchango na jitihada zao za kutoa elimu ya usalama barabarani ambapo pia kampuni hiyo ni wadhamini wakuuTUZO
  Tuzo waliyotunukiwa kampuni ya BE FORWARD TANZANIA katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid
  IMG_1278
  Mmoja wa wadau katika maadhimisho hayo akifurahia ujio na ushiriki wa kampuni ya BE FORWARD TANZANIA kwa kutoa elimu ya usalama barabarani
  IMG_1279
  Wadau wakipata elimu ya usalama barabarani na kujua shughuli zinazofanywa na kampuni ya BE FORWARD TANZANIA katika banda lao
  IMG_1243
  Maofisa wa kikosi cha usalama barabarani wakitoa elimu kwa wadau waliotembelea banda la BE FORWARD TANZANIA katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kitaifa jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid (Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

older | 1 | .... | 369 | 370 | (Page 371) | 372 | 373 | .... | 1898 | newer