Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 368 | 369 | (Page 370) | 371 | 372 | .... | 1897 | newer

  0 0


  CK1 Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Biashara na Masoko kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Odilo Majengo (katika) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzindua maonyesho ya Saba ya Magari yajulikanayo kama Atofest jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Biafra.kulia ni Msaidizi Binafsi wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Deodatus Timothy Ndunguru na kushoto ni Mratibu wa maonyesho hayo Bw. Ally Nchahage.CK2Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika banda la Jaffarais Car Wash wakisubiri wateja kwa ajili ya kuwaoshea magari ikiwa ni mchango kwa ajili ya kusaidi wagonjwa walioko hospitali ya Taifa Muhimbili watokanao na ajari za barabarani. Tukio hili limefanyika jana katika viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam.CK2aMsanii Singo Mtambalike aka Rich Rich (aliyeshika mpira wa maji) na msanii wa kike Bi. Kajala Masanja (  aliyeshika ndoo) wakiosha gari la mteja aliyefahamika kwa jina la Furaha Mansoor (hayupo pichani) mara baada ya kufikia makubaliano ya kumuoshe gari mteja kwa ikiwa ni mchango wa kusidia wahanga wa ajari za barabarani waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wasanii hao waliosha gari hilo kwa gharama ya shilingi laki tano za kitanzania.CK2b Mkurugenzi waKampuni ya SBP Bw. Furaha Mansoor (katikati) akiwakatika picha yapamoja na wasanii Singo Mtambalike aka Rich Rich (kushoto) na Kajala Masanja (kulia) mara baada ya wasanii hao kumaliza kumuoshea gari lake wakati wa maonyesho ya magari na zoezi la uchangiaji wa hiari kwa wahanga wa ajari za barabarani waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Biafra CK2c Wasanii Johari Chagula (anayepaka sabuni) na Monalisa (  aliyeshika mpira wamaji) wakiosha gari la mteja aliyefahamika kwa jina la Feisar (hayupo pichani) mara baada ya kufikia makubaliano ya kumuoshe gari mteja huyo kwa ikiwa ni mchango wa kusidia wahanga wa ajari za barabarani waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.CK3 Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Biashara na Masoko kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mahusiano wa Bank ya Afrika Tawi la Tanzania (BOA Bank) Bi. Gereta Gonga alipotembelea banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa maonyesho hayo jana jijini Dar es Salaam.CK4. Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Biashara na Masoko kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Odilo Majengo ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonyesho ya magari akifurahia zawadi ya Kikombe aliyopewa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Kuunganisha wauzaji na wanunuzi wa magari Tanzania kupitia mtandao wa cheki.co.tz Bw. Mori Bencus jana jijini Dar es Salaam. Kampuni ya ndiyo wadhamini wakuu wa maonyesho hayo ya saba ya Atofest ambapo wameingia kwa mara ya kwanza katika biashara hapa nchini Tanzania mwaka 2014 wakiwa na lengo la kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora na kwa wakati.CK5 Gari lenye uwezo wakuimiri katika maeneo yasiyo na barabara zauhakika likiendeshwa katikati ya dimbwi la matope kuonyesha uimara wake,hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam katika maonyeshi ya magari yanayonedelea katika viwanja vya Biafra Kinondoni.

  0 0


  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Makete mh Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho.

  Wananchi waliozaliwa wilayani Makete mkoani Njombe ambao wanaishi nje ya wilaya hiyo, wameshauriwa kuipenda wilaya yao kwa kuja kuwekeza pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ndani ya wilaya hiyo

  Rai hiyo imetolewa hii leo na Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro katika kikao baina yake na wananchi wa Makete waishio jijini Dar es Salaam kilichofanyika jijini humo
  Katika kikao hicho mkuu wa wilaya amewashirikisha mambo mengi ya kimaendeleo katika wilaya ya Makete ikiwemo uwepo wa shule ya sekondari ya wasichana ya Makete Girls secondary ambayo pamoja na kuanza kufanya kazi bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali

  Mh. Matiro amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa bweni na kuwa wanafunzi wanalala kwenye vyumba vilivyojengwa kwa ajili ya madarasa, bwalo, jiko pamoja na maabara ambavyo vinatakiwa viwepo

  Amewaomba wananchi hao kuunga mkono kwa jinsi Mungu alivyowajalia na kwamba yeyote atakayejisikia kuchangia anaombwa kufanya hivyo kwani kila mmoja kwa nafasi yake ana mchango katika shule hiyo ili iondokane na changamoto hizo
  "Ndugu zangu wilaya yetu inawatambua sana. tunaomba na tunahitaji sana ushirikiano wenu katika maendeleo ya makete, tukishirikiana kwa pamoja kwa kadri Mungu alivyotujalia kwa hakika shule hii itaimarika sana" amesema Matiro

  Kwa upande wao washiriki wameoneshwa kufurahishwa na maendeleo ya kasi katika wilaya ya makete huku wakiipogeza serikali kwa juhudi zake za maendeleo hasa katika elimu, barabara, umeme pamoja na mambo mengine huku wakisema wataunga mkono maendeleo ya wilaya yao kwa kadri ya uwezo wao
  Pia wameonesha kufurahishwa na Mh Matiro kuwatafuta na kuzungumza nao kwani wamesema amekuwa mkuu wa wilaya wa kwanza kuzungumza nao toka wilaya hiyo imeanzishwa na kumtaka kuwa na moyo wa kuipenda wilaya ya Makete kama mkuu wa wilaya
   Wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya.

  Baada ya kushirikishwa hivyo wameahidi kushirikiana na mkuu huyo wa wilaya kutatua changamoto hizo.Na Edwin Moshi, Dar es salaam

  0 0

  Komredi Professor Abdulrahaman Mohamed Babu alikuwa mwanasiasa,mwanamapinduzi msomi,mwandishi,mchumi, na ujamaa kwake ulikuwa ni mfumo wa maisha yake.
   
  Tunapowataja na kukumbuka wakongwe wa siasa na wapambanaji waliosimama kidete kuhakikisha kuwa wafrika tuna jikomboa kutoka katika makucha ya ukoloni uwe mkongwe au ukoloni mambo leo,jina la marehem Abdulrahman Mohamed Babu (RIP)alitasahulika, ambaye kama angelikuwa hai leo tarehe 22 September ndio siku yake ya kuzaliwa.
   
  Historia inatuelezea kuwa mwanamapinduzi marehem Prof. A.M.Babu alizaliwa 22 Sept 1924 huko kisiwani Unguja,Zanzibar, na alifariki dunia 05.08.1996, marehem Prof. A.M.Babu anakumbukwa kwa mengi pamoja na kuwa engineer wa mapinduzi ya visiwani 1964 yalimfanya sultani akimbie na kusahau kiremba kitandani

  0 0


   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwapungia mkono wakazi wa Bagamoyo wakati wakiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa shule ya Msingi Jitegemee.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi mshahiri maarufu wa CCM mkoa wa Pwani Ndugu Ali Pongwe baada ya kutoa ushairi mzuri kabla ya kuanza kwa mkutano.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo ambapo aliwasisitiza kujiunga na mfuko wa afya ya jamii pamoja na wazazi kuwapeleka watoto shule pia aliwashauri wazazi kuchagua watu wenye shughuli zao kuingia kwenye kamati za shule kwani kutasaidia sana kupunguza michango isiyo ya lazima.
   Wananchi wa kata ya Magomeni wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
   Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni na kuwataka kuhakikisha watoto watakaochaguliwa kuingia sekondari wanaenda shule kwani kushindwa kufanya hivyo ni kurudisha nyuma maendeleo.Pia aliwataka wananchi wachunge afya zao kwani elimu ya maambukizi ya ukimwi inatolewa ya kutosha hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na afya yake.
   Sehemu ya watu waliohudhuria mkutano.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni ambapo alitoa sifa kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani kwa utendaji wake wenye ufanisi mkubwa pia aliwaambia wananchi hao kuwa vyama vya siasa ndio vimeshafika muda wake kwani havina sera na vimeshindwa kuja na sera mbadala ya kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini.
   Wananchi wakimsikiliza Nape Nnauye ambaye pia aliwataka watendaji wa Serikali kuwa karibu na wananchi kwani kutasaidia kufanikisha maendeleo na kuondoa sintofahamu za wananchi wanaotaka kujua taarifa za maendeleo ya miradi au maeneo husika.
  Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dk.Shukuru Kawambwa akihutubia wakazi wa jimbo lake wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Jitegemee ambapo aliwaambia kero za michango midogo midogo zinaondolewa .
   Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga akihutubia wakazi wa kata ya Magomeni ambapo aliwaambia  wanawake kutokuwa nyuma katika kuomba nafasi za uongozi katika chaguzi zinazokuja.
   Mmoja wa wananchi waliofika kwenye mkutano akiuliza swali kwa Katibu Mkuu wa CCM wakati wa mkutano .

   Diwani wa kata ya Magomeni Bi.Mwanaharusi Jarufu akijibu moja ya maswali yaliotoka kwa wananchi.
   Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo akijibu maswali kutoka kwa wananchi
  Sehemu ya wanachama wapya waliopokea kadi zao za uanachama leo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo zaidi ya wanachama 338 walijiunga na CCM.(Picha na Adam Mzee)

  0 0

   Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wa pensheni wa PPF wakati wa sherehe ya Mwaka iliyofanyika katika Ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Jijini Dar Es Salaam Mwishoni mwa wiki
   Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka akiwapongeza Vijana wanaounda kundi la The Voice ambao ni wasanii wa fani ya Akapela mara baada ya Kutoa burudani katika sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam.
  Kundi la The Voice likitoa burudani katika sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl
  Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika Sherehe ya Mwaka ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Ukumbi wa Blue Pearl.
  Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Janeth Ezekiel akipokea cheti na zawadi kutoka Kwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka mara baada ya kutangazwa kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2013 kutoka Idara ya Mahusiano na Masoko ya Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sherehe ya mwaka ya PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar Es Salaam
   Pichani Juu Ni baadhi ya wafanyakazi kutoka Idara Mbalimbali za Mfuko wa Pensheni wa PPF waliojipatia zawadi kwa kuwa wafanyakazi bora wa Mwaka 2013.
  Wafanyakazi wa PPF wakifuatilia Burudani iliyokuwa ikitolewa na Kundi la The Voice katika Sherehe ya Mwaka ya PPF iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Hotel ya Blue Pearl.
  Mmoja wa wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akimtunza Mmoja ya waimbaji wa kundi la the voice lililokuwa likitoa burudani wakati wa sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika Mwisho mwa Wiki katika hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar 
  Wadau wakiserebuka Muziki mara baada ya wafanyakazi bora kupewa motisha na zawadi zao katika sherehe ya Mwaka ya PPF iliyofanyika Mwishoni mwa Wiki katika Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Jijini Dar Es Salaam.Pichote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

  0 0

  DSC_0005
  Baadhi ya wafanyakazi Kampuni ya Kupakua na Kupakia Kontena Bandarini (TICTS) wakiwasili kwenye ufukwe wa bahari ya hindi maeneo Kata ya Kivukoni kwa ajili ya kushiriki zoezi la kusafisha fukwe hizo katika kuhitimisha kampeni usafi iliyokuwa ikiendeshwa na Kampuni ya Green Waste Pro Ltd mwishoni mwa juma.

  Na Mwandishi wetu

  KAMPENI kubwa ya kuhamasisha usafi iliyokuwa inaendeshwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd katika kata tatu za katikati ya jiji imemalizika kwa ufanisi mkubwa kiasi cha kufanya eneo hilo kumeremeta tena. Kampeni hiyo ambayo ilianza Septemba 6 mwaka huu ilifungwa kwa usafi katika kata ya Kivukoni ambapo kampuni ya TICS ilishiriki kufanya usafi katika fukwe za bahari.

  Katika kampeni zilizoshirikishwa wadau mbalimbali wa mazingira na afya katika kuhamasisha usafi miongoni mwa wananchi pamoja na kufanya usafi viongozi walitumia nafasi hiyo kufunza watu umuhimu wa kushiriki katika kufanya usafi na kuwa wasafi.

  Kata zilizohusika na kampeni hiyo ni kata ya Kisutu, Mchafukoge na Kivukoni. Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa alisema usafi huo umelenga kuweka maeneo ya bandari kuwa masafi na japokuwa wao wapo Temeke waliona kuna kila sababu ya kushiriki usafi kwenye maeneo ya bahari ambayo wanafanyia kazi.

  Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu alisema kampeni hiyo ambayo imefanikiwa, ilikuwa inawakumbusha wananchi wajibu wa kushiriki katika kuweka maeneo safi .
  DSC_0028
  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TICTS, kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd na watendaji wa halmashauri pamoja na viongozi wa kata ya Kivukoni wakichukua vitendea kazi tayari kuanza kusafisha fukwe za bahari ya hindi.

  Alisema katika kampeni hiyo wamefanikiwa kushawishi wananchi kutambua kwamba usafi si kazi ya serikali pekee bali hata wao na kwamba eneo linapokuwa safi ni sifa ya wananchi na wahusika wengine.
  Aliwataka wananchi waguswe kuwa suala la usafi si la serikali bali la kila mmoja kutokana na ukweli kuwa wanapougua kutokana na mazingira kuwa machafu ni tatizo binafsi zaidi japokuwa serikali itawajibika kusaidia tiba.
  Alisema pia kwamba ushiriki wa TICTS katika kampeni hizo siku za mwisho kunadhihirisha kwamba suala la usafi halina mipaka kwani kila mmoja linamgusa kwa namna moja au nyingine hata kama hakai eneo lile.
  Eneo ambalo limefanyiwa usafi ni lile ambapo limetumika kuuza madafu na bidhaa nyingine huku wala madafu wakiacha vifuu katika eneo hilo na hivyo kutia aibu kutokana na eneo hilo kutumiwa kama njia kuu ya viongozi.
  Naye Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena amesema kwamba wamefurahishwa na kampeni hiyo kutokana na mabadiliko makubwa yaliyojionesha katika maeneo ambayo wamekuwa wakiyasimamia usafi.
  DSC_0034
  Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ushiriki wao kwenye zoezi la kusafisha mazingira yanayozunguka fukwe za bahari ya hindi kata ya Kivukoni lililokuwa likiendeshwa na kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Katikati ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena na Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu.
  Alisema kampeni hiyo imefanikiwa kushawishi wananchi kutambua umuhimu wa usafi na kwamba tabia ya kutupa taka hivyo katikati ya mji sasa imepungua sana.
  Pamoja na kushukuru wadau wote walioshiriki katika kampeni hiyo kuanzia manispaa ya Ilala watendaji na wadau wengine wa usafi alisema wananchi wanatakiwa kuendelea kufahamu kwamba suala la usafi ni lao na wala si la makampuni ya usafi pekee.
  Aidha aliwataka wananchi kuhakikisha wanalipia huduma za usafi na pia kuwa na vifaa vya kuhifadhia usafi kuanzia katika majumba yao hadi katika mitaa.
  DSC_0041
  Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TICTS wakimsikiliza Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye maeneo ya fukwe za bahari ya hindi zilizopo katika Kata ya Kivukoni.
  DSC_0045
  Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo alitoa pongezi kwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd kwa kuifanya manispaa ya Ilala kuwa safi na kutaka kampuni zingine za usafi kuiga mfano wa kampuni hiyo na kuwaasa wananchi kutoa ushirikiano wa masuala ya usafi wa mazingira kwa sababu ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha mazingira yetu yanayotuzunguka yanakuwa safi wakati wote.
  DSC_0070
  Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TICTS na Green Waste Pro Ltd wakishirikiana kusafisha fukwe za bahari ya hindi wakati wa kuhitimisha kampeni ya usafi iliyokuwa ikiendeshwa na Green Waste Pro Ltd.
  DSC_0078
  Kulia ni Meneja uhusiano wa TICTS, Jema Kachota na mfanyakazi mwenzake wakielekea kushiriki zoezi la kusafisha fukwe hizo lililokuwa likiendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro Ltd ambapo TICTS nao waliunga mkono kampeni hiyo iliyofikia tamati mwishoni mwa juma.
  DSC_0096
  Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa (kulia) akivaa glovu tayari kushiriki zoezi la kusafisha mazingira yanayoizunguka bahari ya hindi katika Kata ya Kivukoni mwishoni mwa juma. wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa TICTS.
  DSC_0109
  Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa akishiriki kuzoa uchafu uliotapakaa kwenye fukwe hizo akishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wenzake.
  DSC_0119
  DSC_0146
  Umoja ni Nguvu...... wafanyakazi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd wakizoa uchafu uliopo pembezoni mwa fukwe hizo wakati ambao wakati mwingine unapelekea kutoa harufu mbaya kwenye maeneo hayo.
  DSC_0151
  Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima (kushoto) akishiriki zoezi hilo na wafanyakazi wenzake wa kampuni hiyo.
  DSC_0208
  Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa Green Waste Pro Ltd wakiendelea kuchapa kazi wakati wa kuhitimisha kampeni yao iliyoungwa mkono na kampuni ya TICTS.
  DSC_0251
  Kwa picha zaidi ingia hapa

  0 0

  DSC_0248
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi Mh. Seif Rashid (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makala, Balozi wa Uturuki nchini, Mh. Ali Davutoglu.
  DSC_0593
  Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid, akisoma hotuba kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  DSC_0415
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
  DSC_0418
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipongezwa na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu baada ya kusoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
  DSC_0279
  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akisoma risala yake kwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
  DSC_0284
  Kaimu Mufti Sheikh Ismail Habibu Makusanya, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ambapo alilaani vikali mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinizim) na kusema kuwa watu wote wanaoshiriki katika mauaji hayo kamwe hawatoiona Pepo ya Mwenyezi Mungu.
  DSC_0384
  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu akisoma ujumbe kwa niaba wa umoja wa mabalozi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
  DSC_0300
  Baadhi ya wadau kutoka taasisi na asasi mbalimbali nchini walioshiriki kwenye maadhimisho hayo.
  DSC_0420
  Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB), Bi. Mary Massay akitoa nasaha kutoka kwa Tume hiyo, ambapo alitoa rai kwa mtu yeyote yule ambaye ana malalamiko au matatizo katika Haki za Binadamu anakaribishwa kwenye tume hiyo kwa ajili kupata msaada wa kisheria.

  DSC_0519
  Shuhuda aliyenusurika kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya meza na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.
  DSC_0534
  Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, akilia kwa uchungu baada ya kusikia shuhuda kutoka kwa mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford (hayupo pichani) ambaye hadi sasa anapewa matunzo na Shirika la Under The Same Sun.
  DSC_0540
  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akimfariji mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar.
  Kwa matukio zaidi ingia humu
  DSC_0007
  Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuhudhuria maadhimisho hayo na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi (wa pili kulia), Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makala (katikati) na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania , Bw. Ali Rajab (kulia) pamoja na viongozi wengine taasisi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinizim). (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog)

  Na Mwandishi wetu
  WAKATI Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon anahimiza serikali duniani kutafuta chanzo cha kukosekana kwa amani na kuongezeka kwa watu wenye misimamo mikali, wasemaji katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa amani Duniani wameitaka serikali ya Tanzania kutupia macho makali mauaji ya albino nchini.

  Akimwakilisha Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika adhimisho lililofanyika viwanja vya Mnazi mmoja leo Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Alvaro Rodriguez, alisema ili kudumisha amani kuna mambo mengi yanatakiwa kufanyiwa kazi hasa kutambua chanzo cha migogoro inayosababisha msuguano mkubwa katika jamii na kukosekana kwa amani.

  Alisema amani ina maana kubwa kwa jamii na ndio maana Umoja wa mataifa miaka 13 iliyopita iliamua kuadhimisha siku hiyo kwa lengo la kushawsihi makundi yanayosigana kupata nafasi ya kuzungumzia na kuona maana ya amani.

  Alisema pamoja na kuwepo kwa hatua kubwa tangu kupitishwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa la kuadhimisha amani, safari ya kufikia amani ni ndefu na ili kufanikiwa pande zote ni lazima kwenda hatua kwa hatua kwa kushirikiana.
  Alisema mafanikio ambayo yamepatikana ni pamoja na UN kufanikiwa kufundisha kada ya habari juu ya uandishi katika mazingira tete na kusaidia majadiliano ya kitamaduni yanagusa masuala ya amani.
  DSC_0031
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (katikati) akimtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB), Bi. Mary Massay.
  Aidha alisema kwamba wanafanyakazi na Wizara ya mambo ya ndani kuhakikisha kwamba wanastawisha mipango yote inayolenga kuzuia ghasia na kuboresha mipango inayoimarisha amani.
  Akihutubia bada ya mashuhuda kuzungumzia hali ya tishio la amani nchini Tanzania hasa la kukosekana kwa amani miongoni mwa watu wenye ulemavu wa ngozi albino, Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa aliipongeza serikali ya Tanzania kw ajuhudi zake za kuimarisha amani katika kanda ya maziwa makuu na kushiriki katika operesheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa ziliziolenga kuleta hali bora zaidi ya maisha kwa watu wanaoishi katika hekaheka za kivita.
  Akiwa na mwezi mmoja tangu awalisili nchini mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa nchini amesema kwamba anatarajia kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali na wananchi wa Tanzania kuhakikisha taifa la Tanzania linaendelea kuwa na amanai
  Wakati Mwakilishi huyo amesema kwamba watu wengi duniani wanawaonea gere wananchi wa Tanzania kwa amani wlaiyonayo, mwakilishi wa Under the Same Sun, Vicky Ntetema ametaka kupitiwa upya kwa sheria ya uchawi ya mwaka 1928 iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2002 ili kukabiliana na mauaji ya albino nchini ambayo kwa kiasi kikubwa yanachochewa na waganga wa kienyeji.
  DSC_0039
  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid meza kuu.
  Alisema sheria hiyo ina mwanya mkubwa wa wauaji kucheza nayo na kusababisha sehemu kubwa ya kesi zilizopo kushindwa kuwatia hatiani wahusika.
  Alisema wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu mauaji ya albino na ukataji wa viungo umeongezeka.
  Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi 25 za afrika zinazofanya ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi, toka mwaka 2006 watu 74 wameuawa, 56 wamenusurika na 11 wameongezewa ulemavu huku makaburi 18 ya albino yakinajisiwa kwa kufukuliwa.
  Watu wa kituo cha haki za binadamu wamesema pamoja na kuwepo na matukio 120 ya ukatili dhidi ya albino kesi 11 tu ndio zilizofikishwa mahakamani huku tano zikiwa zimekatiwa hukumu ambazo hazijaridhisha.
  Vicky alisema katika matukio yote hayo chanzo ni ushirikina lakini kutokana na kukosekana zimeshindikana kuzimaliza zinavyotakiwa.
  DSC_0082
  Brass band ya jeshi la Magereza ikiongoza maandamano ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho hayo jana.
  Vicky aliitaka jamii kuwalinda albino kwani serikali pekee haiwezi kufanya kitu chochote huku akisema kwamba hesabu ya albino mmoja katika kila wananchi 1,400 haiwezi kulindwa kwa dhati na serikali kutokana na idadi ya polisi kutokua sawa na wananchi.
  Aidha alishauri serikali kutoa msaada wa kisheria kwa waathirika kabla ya kuingia mahakamani ili waweze kusimulia vyema kadhia zao na pia wasiangushwe na wanasheria ambao wanatumia udhaifu wa kisheria kuwatoa watuhumiwa hatiani.
  Pamoja na Vicky Ntetema kushawishi wananchi kulinda albino na kuwafichua wauaji Kaimu Mufti Sheikh Ismail Habibu Makusanya ameitaka serikali kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata utulivu wa kutosha kuendelea na shughuli zaka na kuhimiza mahakama kutenda haki.
  Aliwakumbusha wananchi kama alivyosema Sydina Omar kwamba kila mmoja ataulizwa amefanya nini kukomesha madhila katika jamii wakati wa kiama na kusema serikali isipowajibika itasema nini na wananchi nao pia watajibu nini.
  DSC_0100
  Pichani ni baadhi wadau kutoka taasisi mbalimbali pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja huku wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kuhamasisha amani nchini na kupinga mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar.
  Alisema amani hailetwi kama mvua , inatafutwa na kusema watu wasipotafuta amani na kuhakikisha amani inakuwapo itakuwa shida kubwa kwa taifa hili ambalo miaka yote limeogelea katika bahari ya amani.
  Aliwasihi waumini wa Kiislamu na wananchi wengine kuhakukisha kwamba amani inakuwa ajenda ya kudumu kila wanapokutana pamoja.
  Katika maadhimisha hayo ambapo wananchi walianza maandamano shule ya Uhuru Mchanganyiko hadi viwanja vya Mnazi mmoja, mgeni rasmi Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk Seif Rashid alisema serikali imejipanga kuhakikisha inakomesha mauaji ya albino na kuwataka wananchi kuisaidia kwa kutokuwa waoga kutoa ushahidi na pia kuwaripoti watuhumiwa.
  Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ya haki ya amani kwa watu wote, komesha mauaji ya albino inahamasiaha umma wa Tanzania kulaani,kukemea na kukomesha mauaji kwani yanakwenda kinyume na katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 14 ambayo inaeleza kwamba kila mtu ana haki ya kupata hifadhi katika jamii.
  Aidha waziri alitaka kutekelezwa kwa agizo lake kuhusu tiba mbadala na za asili na kusema serikali itaendelea kulinda amani na kutoa ulinzi kwa wathirika.
  DSC_0108
  Meza kuu ikipoeka maandamano ya siku ya kimataifa ya amani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akimkabidhi nahodha wa Mkolani Fc Meck Lyimo, kombe la ubingwa wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 mara baada ya timu hiyo kuifunga timu ya kata ya Mirongo bao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jumamosi uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza na kuhudhuriwa na mashabiki wengi.
  BOFYA PLAY KUSIKILIZA KILICHOJIRI.
  Kikosi cha timu mabingwa Mkolani Fc katika picha ya pamoja kabla ya kuvaana na Mirongo Fc kwenye mchezo wa fainali Pepsi Kombe la Meya 2014 uliochezwa kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
  Kikosi cha timu Mirongo Fc katika picha ya pamoja kabla ya kuvaana na Mkolani Fc kwenye mchezo wa fainali Pepsi Kombe la Meya 2014 uliochezwa kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
  Ni wakati wa kupata mawaidha toka meza kuu ya wageni na wenyeji wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 ambayo mwasisi wake ni Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula.
  Balozi wa habari wa Pepsi Albert G. Sengo (katikati) akitoa utangulizi kuhusiana na Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, mbele ya meza kuu.
  Katibu Mkuu wa TFF  Selesitine Mwesigwa, (mbele) akiongoza msafara wa Meza kuu kukagua timu kabla ya mchezo wa fainali kuanza,nyuma yake ni muasisi wa mashindano hayo Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza, Stanislaus Mabula, Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Mwanza (MZDFA), Jackson Songola na Meneja wa Kampuni ya SBC Nicolous Coertz.
  Mashabiki wakifuatilia kwa ukaribu michuano hiyo.
  Muasisi wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya, Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akizungumza na mashabiki wengi waliofurika katikauwanja wa Nyamagana kushuhudia fainali hizo, ambapo hadi mwisho timu ya kata ya Mkolani waliibuka Mabingwa kwa kuifunga Mirongo Fc 2-1. Katika Picha anaonekana Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (wa pili toka kushoto) Katibu Mkuu wa TFF  Selesitine Mwesigwa (kushoto) na Meneja wa Kampuni ya SBC Nicolous Coertz (kulia).
  Katibu Mkuu wa TFF  Selesitine Mwesigwa naye alipata nafasi ya kuzungumza na wana Mwanza.
  Meneja wa Kampuni ya SBC Nicolous Coertz naye alipata nafasi ya kuzungumza ambapo aliwateka mashabiki kwa kuitumia vyema lugha ya kiswahili.
  Kundi la sanaa Bujora Dancing Group lilisababisha burudani nyingine ya mvuto.
  Burudani ilikolea macho mbeeeele kwenye tukio.
  Kila mtu na nafasi yake macho kwenye mchezo.
  Mkolani Fc wakitoka kushangilia goli la kwanza lililofungwa kipindi cha pili na Siraji Juma.
  Hii ni moja kati ya zawadi za mshindi wa kwanza ambapo mbali ya kupata Kombe, fedha taslimu shilingi milioni 1.5, na medali ya dhahabu vilevile bingwa wa michuano hiyo aliondoka na Bajaji hili lenye tahamani ya shilingi milioni 4.5
  Mkolani Fc wakishangilia bao la pili na la ushindi lililofungwa na Paul Godfrey.
  Mashabiki wa Mkolani wakiwa wamembeba kocha wa timu yao mara baada ya mchezo kumalizika wakiwa na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Mirongo Fc.
  Zawadi ikiwa chini ya ulinzi.
  Mwamuzi Bora wa Mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 ni David Albert.
  Wafuatiliaji aka mashuhuda.
  Mwamuzi Bora wa Mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 ni David Albert, akishangilia mara baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi laki mbili, aliyekabidhi ni diwani wa Kata ya mirongo mhe. Mkama.
  Meneja wa SBC watengenezaji wa vinywaji vya Pepsi  Nilolous Coertz (Kushoto) akimkabidhi fedha taslimu shilingi laki mbili na kiatu cha dhahabu mfungaji bora wa mashindano Paul Godfrey wa Mkolani Fc aliye kuwa na magoli nane (8) 
  Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida akikabidhi kombe la mshindi wa tatu kwa timu ya Sokoni Fc.
  Katibu Mkuu wa TFF  Selesitine Mwesigwa akikabidhi kombe kwa washindi wa pili wa Pepsi Kombe la Meya 2014 timu ya Mirongo Fc, ambapo pia aliwakabidhi kitita cha shilingi milioni mbili taslimu.
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akimkabidhi funguo na vidhibitisho vyote vya zawadi ya gari la mizigo Bajaji kwa ajili ya kuanzisha ujasiliamali, na mpokeaji ni Nahodha wa timu mabingwa Mkolani Fc Meck Lymo.
  Wacha shangwe zitawale.
  Mabingwa Mkolani Fc.
  TIMU ya Kata ya Mkolani FC imeibuka mabingwa wapya wa Kombe la Meya 2014 baada ya kuichapa timu ya Kata ya Mirongo bao 2-1 juzi katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

  Awali katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ulioanza mapema saa 8:00 mchana kwa timu ya Sokoni FC kuichapa Mnadani FC bao 3-0na kuibuka mshindi wa tatu wa michuano hiyo huku magori ya Sokoni yakifungwa na Joseph Mwajalila dakika 33 kwa penati na Salimu Hamis dakika 39, 51na kuwapa tiketi ya ushindi wa tatu.

  Fainali hiyo iliyoshuhudiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TFF  Selesitine Mwesigwa, muasisi wa mashindano hayo Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza, Stanislaus Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Mwanza (MZDFA), Jackson Songola na Katibu wa MZDFA, Nasibu Mabrouk.

   Ndikilo amesema mashindano hayo yamewezesha vijana kuonyesha vipaji vyao, hivyo ni vyema sasa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakawatumia vijana walionesha uwezo kuunda timu ya Mwanza City FC kama ilivyofanya Jiji la Mbeya.

  “Ni bora mkaunda timu ya Mwanza City FC ili kushiriki ligi na huenda ikatinga ligi kuu Bara kama walivyofanya wenzetu wa Mbeya na sasa timu ya Mbeya City FC inashiriki ligi kuu, kwani timu zetu kongwe katika Mkoa huu za Toto FC na Pamba FC zimeonekana kuishiwa mbinu na kufanya vizuri ili kurejea ligi kuu,”alisema.

  Katika mchezo huo mkali wa vuta ni kuvute kilishuhudia timu hizo zikienda mapumziko zikiwa hazijafungana na kipindi cha pili mchezaji Siraji Juma aliwainua mashabiki kwa kuandika bao la kwanza na bao la pili likifungwa na Paulo Godfrey huku katika hekaheka ya kuokoa mpira ulioelekezwa langoni mwake akijikuta akijifunga na hadi mwisho wa mchezo wadau wa michezo walishuhudia timu ya Mkolani ikitangazwa kuwa mabingwa kwa kuinyuka Mirongo Fc bao2 - 1.
    
  Mashindano hayo ya kombe la Meya 2014 yaliyodhaminiwa na Kampuni ya kutengeneza vinywaji vya Pepsi (SBC), Ndikilo alikabidhi bingwa timu ya Mkolani FC zawadi ya kombe, fedha tasilimu Sh milioni 1.5, medali ya dhahabu na Bajaji ya mizigo yenye thamani ya Sh milioni 4.5, mshindi wa pili alinyakuwa Sh milioni 2, kombe dogo na medali ya fedha.

  Timu ya Sokoni FC iliyoibuka mshindi wa tatu ilijinyakulia fedha tasilimu Sh milioni 1, medali ya shaba na kombe dogo, mfungaji bora Paulo Godfrey akiwa na bao nane na kunjinyakulia kiatu cha dhahabu na Sh laki mbili, mwamuzi bora kutoka Kituo cha Alliance ilichukuliwa na David Albert na kupata Sh laki mbili huku timu ya Kata ya Mahina FC ikipata Nidhamu bora na Sh laki mbili.

  PICHA/HABARI NA GSENGO

  0 0

   Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Stamina na Ney wa Mitego wakilishambulia jukwaa mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Morogoro mapema jana ndani ya uwanja wa Jamhuri.
   Msanii wa Bongo Fleva Vanessa Mdee a.k.a V-Money akitumbuiza mashabiki waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwenye Tamasha la Fiesta 2014.
   Mmoja wa mashabiki aliyekuwa kwenye Tamasha la Fiesta akishangilia huku akiwa amebebwa na mwenzake.
   Vanessa Mdee akipagawisha jukwaani.
   Umati uliyokuwa umefurika kwenye Tamasha la  Fiesta 2014, ukishangilia moja ya burudani zilizokuwa zikitolewa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
    Umati uliyokuwa umefurika kwenye Tamasha la  Fiesta 2014, ukishangilia moja ya burudani zilizokuwa zikitolewa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
   Mashabiki wakishangweka
   Makomando wakiwajibika jukwaani hapo.
   Ommy Dimpoz akiimba na mmoja wa mashabiki aliyekuwa akiimba kwenye nafasi ya Vanessa Mdee katika wimbo wa Me & U.
   Msanii wa kike Linah wa kwanza kutoka kushoto akiwajibika jukwaani na mmoja wa wanenguaji wake.
   Chipukizi wa Bongo Fleva Mo Music akikamua kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta mjini Morogoro, usiku wa kuamkia leo.
   Mmoja wa mashabiki akiwa amebebwa jujuu wakati shangwe za Serengeti Fiesta 2014 zikiendelea usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Fid Q akifanya yake kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
   Mashabiki wakishangilia
   Baba Levo na Peter Msechu wakipagawisha jukwaani hapo
   Kundi la Weusi kutoka nyanda za Kaskazini wakifanya makamuzi yao kwenye jukwaa la Fiesta, usiku wa kuamkia leo mjini Morogoro.

  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (lushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es Salaam, Rashid Mpinda.  Msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7 unatokana na mapato yaliyopatikana katika  tamasha la Pasaka na Krismasi. (Picha na Francis Dande) 
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Ltd, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada kwa vituo vya yatima jijini Dar es Salaam.
  Watoto wa kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kituo hicho, Halima Ramadhan wa tatu kulia.
   Watoto wa kituo cha Maunga cha Kinondoni wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Kituo hicho, Rashid Mpinda (mwenye kofia).
  Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa cha Mbweni nje Kidogo ya jijini la Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa cha Mbweni nje Kidogo ya jijini la Dar es Salaam.
  Msama akiwa amembeba mtoto anayelelewa katika kituo cha Tovichodo cha Temeke.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (lushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es Salaam, Rashid Mpinda.  Msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7 unatokana na mapato yaliyopatikana katika  tamasha la Pasaka na Krismasi.

   Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es Salaam, Rashid Mpinda akimshukuru Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kwa misaada aliyotoa.
   Msama akiwa amembeba mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Maunga.
  Watoto wakimshukuru Msama baada ya kuwapatia msaada wa vyakula mbalimbali.
   Mkurugenzi wa Kituo cha Tovichodo cha Temeke, Honoratha Michael akipokea sehemu ya msaada wa vyakula kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama.

  Na Francis Dande 
   
  KAMPUNI ya Msama Promotions Ltd ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, juzi ilitoa misaada ya kiutu kwa vituo vitatu vya kulea yatima vya wilayani Kinondoni na Temeke.
  Msaada huo ambao ni utekelezaji wa programu ya kampuni hiyo kama moja ya kurejesha sehemu ya faida itokanayo na uratibu wa matamasha ya muziki wa injili kwa jamii.

  Msama Promotions Ltd ambayo pia ni waratibu wa tamasha la muziki wa injili la Pasaka na Krismas, si mara ya kwanza kwao kutoa misaada ya aina hiyo kwa vituo vua yatima na watu wengine wenye mahitaji kama wajane na wazee.

  Vikundi vilivyonufaika na msaada huo Jumapili, ni kituo cha Kulea Watoto Yatima  cha Mwandaliwa cha Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Maunga pia cha Kinondoni.

  Aidha, misada hiyo imewafariji watoto yatima wa kituo cha Tovichido cha Wilayani Temeke akisema amefanya hivyo baada ya kuguswa na hali halisi inayowakabili.

  Msama alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa watu wenye uwezo, makampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii  kwani nao wana haki ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine.

  Kwa upande wa misaada iliyokabidhiwa kwa vituo hivyo, ni mchele, sukari, unga, mafuta ya kula, chumvi, unga wa ngano na vingine vingi kwa ajili ya matumizi ya kila siku nyumbani, vyote vikiwa na thamani ya shilingi mil 7.

  Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Katibu wa Kituo cha  Maunga, Rashid Mpinda   alitoa pongezi kwa Msama kutokana na misaada hiyo na kuwasihi wengine waige mfano huo wa kusaidia makundi maalum.

  Akielezea changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mpinda alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma hadi kufukuzwa kwa kukosa karo, hivyo kushindwa kupata elimu.

  Msama kwa upande wake alisema jukumu la karo za wanafunzi hao analibeba yeye pamoja na sare  kutokana na kuguswa kwake na kilio cha watoto hao.

  0 0

  Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki maonyesho ya nyumba yaliyofanyika jijini Dar es Salaam inategemea umeanza hivi karibuni.
  Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village alisema “Kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zitakuwa tayari ifikapo Januari 2015. 
  Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule, maduka eneo la Kigamboni. 
  Mradi huu unajengwa kwenye eneo takriban eka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018. 
  Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wa kazi hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika.
  Wafanyakazi wa Dege Eco - Village wakiwahudumia wateja wao waliofika katika banda lao.
  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village akibadilishana mawazo na mfanyakazi mwenzake.
  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village akiongea na mteja ambaye alikuwa akiweka kumbukumbu katika daftari la wageni waliofika banda la Dege Eco - Village ndani ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Dege Eco-Village wakiwa katika picha ya pamoja.
  Wananchi wakionyeshwa mpangilio wa nyumba utakavyokuwa.
  Muonekano wa banda la Dege Eco-Village.
  Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Dege Eco -Village Bw. Adam akiongea na waandishi wa habari kufafanua jambo. 
  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village akibadilishana mawazo na wateja waliofika katika banda lao.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2014 kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne Marie Kaarstad, (wa pili kulia) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Tanzania, nchini Rwanda, Mhe. Ali Said Siwa, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 22, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania, nchini Rwanda, Mhe. Ali Said Siwa, leo Septemba 22, 2014. Picha na OMR.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amekutana na mabalozi wa Norway na Balozi mteule wa Tanzania nchini Rwanda na kufanya nao mazungumzo ofisini kwake ikulu jijini Dar es Salaam.

  Balozi wa Norway nchini Tanzania mheshimiwa Hanne Marie Kaarstad ndiye alikuwa wa kwanza kufanya mazungumzo na mheshimiwa Makamu wa Rais ambapo licha ya kufika kujitambulisha alimueleza mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa atajitahidi kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili katika kipindi chake kama Balozi na kwamba Tanzania ni nchi rafiki kwa Norway na akasisitiza kuzidi kuimarisha uhusiano hasa katika masuala ya utunzaji wa mazingira.

  Kwa upande wake mheshimiwa Makamu wa Rais alimuelezea Balozi Hanne kuwa, Tanzania inajivunia uhusiano wake na Norway na kwamba uhusiano huo kwa sasa unazidi kuimarika na tena Tanzania inategemea kujifunza mengi toka Norway kutokana na nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi zenye teknolojia ya juu katika masuala ya gesi na mafuta.

  Balozi Hanne ambaye aliwahi kufanya kazi nchini Tanzania pia alionesha kufurahishwa kwake na maendeleo ambayo Tanzania inapiga na akafafanua kuwa mji wa Dar es Salaam ni kiashiria kimojawapo kinachoonesha wazi kuwa Tanzania inakuwa kwa kasi.

  Pia, Mheshimiwa Makamu wa Rais alimpokea Balozi Ali Said Siwa aliyepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda na akamtaka Balozi huyo kuhakikisha anasaidia mahusiano baina ya nchi zetui kuzidi kuimarika huku akimsisitizia kuhusu uhusiano wetu kama majirani na pia wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Balozi Siwa alitumia nafasi hiyo kumshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa uteuzi wake na akaahidi kuiwakilisha vema Tanzania nchini Rwanda.


  0 0

  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Mhe. Samuel Sitta akiongoza bunge hilo leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Amon Mpanju akisoma Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Ezekiel Olouch akichangia mada wakati wa usomaji wa Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Pindi Chana akichangia mada wakati wa usomaji wa Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Selemani Jafo akichangia mada wakati wa usomaji wa Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia mjadala bungeni wakati wa usomaji wa Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Concilia Niyibitanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo jijini Dar es Salaam.Kuliani Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kissui na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Frank Mvungi.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kissui akionyesha Kitabu cha Sera ya Maendeleo ya Vijana kwa waandishi wa habari wakati alipokuwa akito ufafanuzi kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) leo jijini Dar es Salaam. Kuliani ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Concilia  Niyibitanga.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa kuhusu Mfuko wa Vijana wakati wa mkutano wa msemaji wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na waandishi hoa uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija

  0 0

  The newly expected couple sitting together with their Patron Ansigar Mtandika and Matron Neema Njau.
  The newly expected couple Richard Miller and Kara Lee from America poses in a picture at Shira Cave point shortly before descending to a place where they exchanged vows in Mount Kilimanjaro yesterday.
  Chief Park Warden for Kilimanjaro National Park Erastus Lufungulo (right) and TANAPA’s Corporate Communications Manager Pascal Shelutete (second left) poses in a picture with the newly expected couple at Shira Cave point shortly before they exchanged vows in Mount Kilimanjaro.


  0 0

  Na Beatrice Lyimo- MAELEZO.
  Mfuko wa Pensheni (PSPF) umedhamini siku ya Msanii Tanazania itayoadhimishwa Oktoba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City kwa dhumuni la kuwapa mafunzo wasanii ili waweze kujikwamua kiuchumi.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi amesema kuwa kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Sanaa ni kazi” ambayo itajumisha fani mbalimbali kama vile Taarabu, Muziki wa dansi, ngoma za asili na muziki wa msanii kutoka nje ya nchi.

  Njaidi ameongeza kuwa fani nyingine ni uchezaji shoo, dansi za mitaani, Bongo fleva, maonesho ya mitindo ya mavazi, sanaa kwa watoto na maonesho ya sanaa ya ufundi.

   “Tumeona umuhimu wa kuwepo kwa maadhimisho haya kama vile Mei Mosi, siku ya UKIMWI Duniani, Siku ya Wanawake Duniani ikiwa ni chachu ya kuhamasisha wasanii na wadau wake kuthamini sanaa nchini” alisema Njaidi.

  Siku ya Msanii ni mradi uliobuniwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na kampuni ya Haak Neel Production ili kuungana na wa sanii dunia ni kote kuadhimisha siku ya kimataifa ya Msanii inayofanyika kila mwaka kwa lengo la kumtambua msanii, kazi zake na mchango wake katika jamii.

  Aidha,Njaidi alisema kuwa PSPF imekuwa mstari wa mbele kutoa fursa kwa watu wote kujiunga na mfuko kwa ajili ya kujiwekea akiba ya uzeeni.

  Zaidi ya hayo Njaidi amesema kuwa wasanii wamejiajiri na hawana mpango mzuri wa kuweka akiba ya uzeeni, huvyo PSPF imeamua kushirikiana na BASATA katika kuandaa Siku ya Msanii kwa kuwapa elimu wasanii wote ili waweze kujiandaa kwa maisha ya badae.

  Mbali na hayo PSPF inatoa fursa kwa watu wote kujiunga na mfuko kwa ajili ya kujiwekea akiba ya uzeeni, hivyo kushirikiana na wasanii katika kuwapa elimu na waweze kujiandaa kwa maisha ya badae.

  0 0

  Na Lydia Churi, MAELEZO

  Askari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji nchini wametakiwa kuwa waadilifu, waaminifu, watii na watekelezaji wa sheria zote za nchi kwa kuwa hizo ni miongoni mwa sifa za askari bora.

  Akifunga rasmi mafunzo ya awali ya uzimaji wa moto katika viwanja vya ndege kwa askari  100 wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Airwing, Ukonga jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Pereira Ame Silima amewataka askari hao kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani vitawapelekea kufukuzwa kazi na kukatisha ndoto za maisha yao.

  Alisema nidhamu ya kazi, Ushirikiano na kujituma katika mema ni miongoni mwa mambo matatu yatakayowasaidia askari hao kufanikiwa katika kazi zao  pamoja na maisha yao kwa ujumla.

  Naibu waziri huyo aliwahakikishia askari hao kuwa Serikali itaboresha miundombinu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi vya kisasa ikiwemo mitambo ya kisasa ya uzimaji wa moto na uokoaji na  vyuo vya mafunzo ili jeshi hilo liondokane na changamoto zilizopo kwa haraka. 

  Akizungumza awali, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Viwanja vya ndege Mhandisi Thomas Haule  aliiomba serikali kuimarisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuwapatia vifaa vya mafunzo vya kisasa pamoja na mafunzo ili kuendeleza huduma bora zinazotolewa na viwanja vya ndege nchini.

  Alisema teknolojia ya kisasa na hasa magari ya zimamoto ya kisasa yanahitajika ili kupanua viwanja vya ndege nchini. Hivi sasa kuna kituo kimoja cha zimamoto katika kiwanja cha ndege cha Dar es salaam na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Sehemu ya tatu (Terminal 3) ya uwanja huo kitahitajika kituo kingine ikiwa ni pamoja na kupanda hadhi kwa kiwanja hicho kutoka category 9 hadi ya 10.

  Wakati huo huo, Kaimu Kamishna Generali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Lt. Col Lidwino Simon Mgumba alisema lengo la mafunzo hayo kwa askari wa Zimamoto na Uokoaji ni kukabiliana na upungufu wa askari katika vituo vilivyoko kwenye viwanja vya ndege.  Aliongeza kuwa mafunzo hayo yalianza na askari 101 na kumalizika na askari 100 ambapo askari mmoja alitoroka mafunzo baada ya kushindwa kuhimili mafunzo hayo.

  Aidha kabla ya kufunga mafunzo hayo, Mgeni rasmi alishuhudia onyesho la uzimaji wa moto kwenye ndege iliyowaka likifuatiwa na gwaride ambalo  alilikagua na baadaye kulifuatiwa na kiapo cha utii kwa askari waliofuzu mafunzo hayo 

  Mafunzo hayo ya miezi miwili ya uzimaji wa moto kwenye viwanja vya ndege kwa askari wa jeshi la Zimamoto na uokoaji yamefanyika katika awamu ya pili ambapo awamu ya kwanza yalifanyika mwaka jana.

  0 0

  Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
   
  BUNGE Maalum la Katiba limepitisha marekebisho ya Kanuni ili kuliwezesha kufikia hatua ya mwisho ya upigaji kura kuanzia  tarehe 29 Septemba hadi tarehe 2 Oktoba mwaka huu.
   
  Hatua hiyo ililenga kumaliza vikao vya Bunge hilo kwa muda uliopangwa kwa mujibu wa Sheria wa tarehe 4 Oktoba mwaka huu.
   
  Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta wakati alipokuwa akitoa maelezo ya utangulizi kuhusuwa uwasilishwaji wa Azimio la kupitisha Marekebisho ya Kanuni za Bunge hilo.
   
  Mhe. Sitta amesema kuwa inakadiriwa kuwa wajumbe wasiopungua 480 wanatarajiwa kupiga kura na kutokana na Kanuni zilivyokuwa kabla ya mapendekezo ya mabadiliko hayo ingechukuwa siku nyingi kukamilisha zoezi la upigaji kura kwa kupitia kifungu kwa kifungu.
   
  “Kanuni zilivyo hivi sasa kama hatutafanya mabadiliko itachukua kwa wastani wa dakika kama mbili kwa kila mjumbe kupiga kura kwa kila kifungu ambapo kwa siku tutamia wastani wa dakika 960 kwa ibara moja, tunatarajia ibara zitakuwa 300…ameongeza kwa ibara  hizo tungehitaji siku 300 kukamilisha zoezi hilo ambao muda huo utakuwa kinyume na utaratibu uliopangwa tutakuwa tunamaliza ibara moja kwa siku moja”, alisema Sitta.
   
  Amesisitiza kuwa marekebisho yaliyanyika yalilenga kuhakikisha kazi ya upigaji kura inakuwa rahisi na inamalizika katika muda uliopangwa wa kisheria wa siku 60.
   
  Awali akiwasilisha maelezo ya marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014 kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum Amon Mpanju alisema kuwa Kanuni zilifanyiwa mabadiliko ni ya 36 na 38.
   
  Amesema kuwa marekebisho hayo yatamwezesha mjumbe aliye nje ya maeneo ya Bunge kwa ruhusa ya maandishi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kupiga kura ya wazi na siri kwa njia ya nukushi  na mtandao.
   
  Mpanju ameongeza hatua nyingine ni kumwezesha mjumbe kupiga kura katika muda usiozidi siku saba kwa urahisi na ufanisi.
   
  Akitoa ufafanuzi wa wajumbe walioko Hijjah, Sheikh Norman Jongo amesema mjumbe anayetekeleza ibada hiyo hakatazwi kupiga kura ili mradi hajafikia hatua za mwisho wa ibada hiyo.


  0 0

  Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
  22/09/2014.
   
  Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya homa ya hemoraji ikimaanisha ugonjwa wa kumwagika damu bila kuganda (Viral Haemorrhagic Fevers).
   
  Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, ugonjwa huu ni hatari na unasababishwa na kirusi kiitwacho ebola kwani kirusi hicho ni moja kati ya familia ya virusi watatu toka katika familia ya filoviridiae.
   
  Kuna aina tano za kirusi cha ebola ambao ni bundibugyo ebolavirus (BDBV), Zaire Ebolavirus (EBOV), Reston Ebolavirus (RESTV), Sudan Ebolavirus (SUDV) na Tai Forest Ebolavirus (TAFV).
   
  Ni ugongwa unaoua kwa kasi na tafiti zinaonyesha kwamba katika orodha ya watu 10 walioambukizwa na virusi vya ugonjwa huo, basi wastani kati ya watano au tisa hufariki.
   
  Aina hizo tatu za virusi, yaani BDBV, EBOV na RESTV, ndiyo inayongoza kwa kusababisha mlipuko wa ugonjwa huo Barani Afrika wakati aina nyingine za virusi hao wanapatikana katika nchi za Asia, yaani Ufilipino na Thailand.
   
  Taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa kwa mara ya kwanza ugonjwa huu uliripotiwa kutokea mnamo mwaka 1976 katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na taarifa zinaeleza kuwa hatari ya mgojwa kupoteza maisha ni asilimia 90.
   
  Tafiti zinaonyesha kuwa, kuwa Popo wanaopenda kula matunda wanaeneza ugonjwa huo bila wao kuaathirika na katika jamii yetu ugonjwa huo huweza kuambukizwa kutoka mtu mmoja mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine baada ya kugusana na damu au maji maji kupitia michubuko au majeraha yaliyopo juu ya ngozi.
   
  Pia watu ambao wako katika hatari ya kupata ugonjwa huo ni jamii inayoishi karibu na jamii ya wanyama ambao mara nyingi ni Nyani, Sokwe, Tumbili pamoja na Popo.
   
  Licha ya watu walio na maambukizi ya ugonjwa huo kapata nafuu, lakini bado wanaweza kuwaambukiza wengine kwa njia mbalimbali, mfano kwa njia ya kujamiana.
   
  Wataalam wanaamini kuwa virusi vya ugonjwa huo huwa havienei kwa njia ya hewa bali kwa mtu kugusana na majimaji ya mwili, kama vile matapishi, mate, jasho, machozi, ama manii au shahawa ya mtu aliyeathirika na ugonjwa huo.
   
  Kwa upande mwingine hata Madaktari na wauguzi, wanaowatunza wagonjwa wa ebola, watu wenye uhusiano wa karibu na mtu aliyeambukizwa, watu wanaogusa maiti ya mtu mwenye virusi hivyo wapo katika hatari ya kuambukizwa virusi vya Ebola.
   
  Ishara na dalili muhimu ya ugonjwa huu ni hali ya kutokwa na damu katika sehemu tofauti za mwili kama vile katika ufizi, pua, katika njia ya haja, lakini kabla mgonjwa hajafikia daraja hilo, kwanza mtu huwa na homa kali, viwango vya joto vya mwili hupanda sana, kisha anaweza kuwa anajisikia kutapika, na hata kutapika kwenyewe, kuharisha, na pia kuwa mnyonge huku viungo vyake vikiwa na maumivu.
   
  Ili kuweza kutambua mtu ama mgonjwa ameambukizwa na ugonjwa huo, njia ya pekee ya kuthibitisha hilo ni kupitia vipimo vya maabara.
   
  Huduma ya kwanza ambayo mgonjwa wa Ebola anaweza kupewa kwanza kabisa ni vema kumfikisha mgonjwa huyo katika Kituo cha Afya haraka kwa haraka kwani kuvigundua virusi vya ebola kunahitaji maabara ambayo ina uwezo wa kutosha.
   
  Katika kuzingatia matibabu ya mgonjwa wa Ebola jambo la kwanza ni kuchunguza na kuhakikisha kwamba mtu ana virusi hivyo, pili ni kumtenga na watu wengine ili yeye mwenyewe asidhurike zaidi na asiwadhuru wengine na katika kufanya hivyo haimaanishi kwamba mgonjwa huyo anatengwa kwa kunyanyapaliwa, lengo ni kuepusha maambukizi yasiendelee kwa watu wengine ambao hawana ugonjwa huo.
   
  Taarifa nyingi kuhusiana na ugonjwa huu zinasema kuwa mpaka sasa hakuna dawa maalumu ambayo inatumika kuwatibu wale walio na virusi vya ugonjwa huo kwani dawa zilizoko sasa ni zile ambazo ziko ngazi ya majaribio ili kuweza kuona namna gani zinaweza kukabiliana na ugonjwa huo.
  Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa kauli ya kwamba hatari ya kuambukizwa kwa ugonjwa huo kwa njia ya safari za ndege ni chini sana, hata hivyo, watu hushauriwa kuwa waangalifu kuhusiana na hali yao na afya na ile ya wasafiri wengine.
   
  Tahadhari ni bora kuliko kinga, ili kujihadhari na ugonjwa huo endapo utakuwa umeonekana kuingia nchini mwetu hatunabudi kujiepusha kugusana na majimaji yote yanayotoka kwenye mwili wa mtu ambaye atakuwa ameathirika na ugonjwa huo, na pia ni vema tukatumia dawa za kuuwa vijidudu katika choo, katika matapishi, katika mate na majimaji yoyote ya mgonjwa.
   
  Bila shaka ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika endapo tu sote tutachukua hatua, hivyo ni muhimu kwa kila mmoja kuwajibika katika hili na kutoa taarifa mapema kwa Viongozi wa Serikali na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za ugonjwa huo.
   
  Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizochukua tahadhadhari kubwa na mapema ingawa hakuna kesi yoyote iliyoripotiwa juu ya uwepo wa ugonjwa huo hapa nchini.
   
  Kwa kuanzisha mafunzo maalum kwa Kikosi Kazi yenye lengo la kudhibiti ugonjwa wa Ebola, Serikali imetoa mafunzo kwa mamia ya Watumishi wa Afya watakaokwenda kuhudumia abiria wanaoingia na kutoka nje ya nchi.
   
  Sambamba na hilo, Serikali imeweza kufanikisha kuingiza nchini sehemu ya vifaa vya kubaini hatua za awali za ugonjwa wa Ebola kwa kupima hali ya joto la mwili kwa wasafiri kutoka nje nchi wanaotumia viwanja vya ndege  vilivyokuwa vimeagizwa na Serikali vilikwisha wasili jijini Dar es salaam.
   
  Vifaa hivyo vinavyohusisha kamera zenye uwezo wa kubaini joto la mwili wa msafiri kwa umbali wa mita 100 bila  kumgusa muhusika ambayo viliagizwa kutoka nchini Afrika ya Kusini.
   
  Wakati wa siku ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Steven Kebwe alisema kuwa kuwasili kwa vifaa hivyo ni moja ya juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama kwa kuuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.
   
  Aidha alisema kuwa vifaa hivyo vitapelekwa katika maeneo ya Viwanja vya ndege na maeneo yanayotumiwa na raia wa kigeni kuingia nchini vikiwemo vya Dar es salaam, Zanzibar, Kilimanjaro,Mbeya na Mwanza.
   
  Licha ya kuwepo kwa juhudi hizo, bado Serikali inaendelea na mpango wa kuagiza vifaa zaidi vya kuwezesha shughuli ya upimaji wa afya kwa wasafiri wanaotembea yaani vifaa vya (Scanners) vitakavyowezesha kubaini afya za wasafiri wengi zaidi kwa wakati mmoja.
   
  Aidha, aliwataka wataalam wa afya kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa kwa kuhakikisha wanawapima abiria wote wanaotoka nje ya nchi bila kujali hadhi walizonazo ili kuweza kubaini kama wana maabukizi au dalili zozote za ugonjwa wa Ebola.
   
  “Nataka mfanye kazi yenu kwa kuzingatia weledi wa taaluma yenu na kwa kuzingatia yale mliyojifunza, mvitumie vifaa hivi kupima kila abiria ili kubaini joto lake bila kujali cheo wala hadhi yake maana janga hili ni kubwa” Alisema Dkt. Kebwe.
   
  Akizungumzia kuhusu matunzo ya vifaa hivyo, aliwataka wataalam hao kuhakikisha wanavitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu na kutimiza malengo yaliyokusudiwa ya kuwasaidia wananchi kutokana na vifaa hivyo kugharimu fedha nyingi.
   
  Katika hatua nyingine Mh. Kebwe alifafanua kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaendelea na shughuli ya utoaji wa Elimu ya Afya kuhusu ugonjwa wa huo ili kuwawezesha wananchi kuchukua tahadhari na kuzielewa dalili za ugonjwa huo na namna ya kujingika endapo utagundulika nchini.
   
  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), Bw. Cosmas Mwaifwani ambaye Ofisi yake ilihusika katika uagizaji wa vifaa hivyo alisema kuwa mahitaji ya vifaa hivyo kwa sasa yameongezeka kutokana na umuhimu wake na jinsi vinavyofanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
   
  Alisema kuwa upimaji kwa kutumia vifaa hivyo unatumia teknolojia ya kubaini mionzi ya joto kutoka katika mwili wa binadamu pindi vinapoelekezwa katika maeneo ya macho na masikio ya mwili wa binadamu.
   
  “Vifaa hivi vinauwezo wa kutunza picha na kumbukumbu za msafiri, muda, joto la msafiri na tarehe aliyoingia nchini na vifaa hivi vina uwezo wa kupata takwimu kutoka kwenye hali ya majimaji au jasho la Binadamu pindi kinapoelekezwa kwake”, alisema Mwaifwani.
   
  Mwaifwani aliongeza kuwa MSD inaendelea kuimarisha uwezo wake kwa kuongeza vifaa zaidi kutoka nchi za Ubelgiji na China huku akisisitiza kuwa Bohari hiyo imejiandaa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kwa kujenga uwezo wa kuwa na dawa za kutibu hali ya magonjwa yanayoambatana na homa hiyo.
   
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege nchini, Bw. Moses Malaki akizungumza kwa niaba ya Viwanja vya ndege nchini alielezea hali hiyo ya upatikanaji wa vifaa  katika maeneo hayo kuwa itaongeza ufanisi wa uchunguzi wa afya kwa wasafiri na kuondoa usumbufu kutokana na uwezo wa vifaa hivyo kumpima msafiri akiwa mbali.
   
  Pamoja na juhudi za serikali katika kuzuia usiingie nchini ugonjwa huo na hali ya kukaa kwa tahadhari, jamii nchini hainabudi kuzingatia elimu itolewayo na wataalam wa afya juu ya namna ya kujikinga ili kuweza kuudhibiti vema ugonjwa huo kwani mpaka hivi sasa tayari Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa zaidi ya watu 560 wamepoteza maisha nchini Sierra Leone na wengine zaidi 2,600 wamefariki dunia huko Afrika ya Magharibi.

older | 1 | .... | 368 | 369 | (Page 370) | 371 | 372 | .... | 1897 | newer