Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 356 | 357 | (Page 358) | 359 | 360 | .... | 1896 | newer

  0 0


   Baadhi ya nyumba zilizojengwa eneo la Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi.
  Picha na Hassan Silayo. 
   Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Meja Josephat Musira akiwaeleza Waandishi wa habari (Hawapo pichani)kuhusu Mradi wa ujenzi wa Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi ambapo kwa awamu ya kwanza idadi ya nyumba 6064 zinatarajiwa kujengwa na mpaka sasa nyumba 1160 zimeshakamilika kwa ajili ya matumizi, wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika moja ya eneo la maradi Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara hiyo Mhandisi Stephen Mpapasingo.
   Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhandisi Stephen Mpapasingo akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sehemu ya jiko katika moja ya nyumba hizo.
  Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhandisi Stephen Mpapasingo akiwaeleza Waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi, wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika moja ya eneo la maradi Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msemaji wa Wizara hiyo Meja Josephat Musira

  Frank Mvungi-Maelezo
  Serikali yaanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya wanajeshi kote nchini.
  Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Meja Josephat Musira wakati wa  ziara ya waandishi wa habari walipotembelea eneo la Gongo la mboto jijini Dar es salaam ambapo sehemu ya mradi huo inatekelezwa.
  “Lengo la ujenzi wa nyumba hizi ni kupunguza tatizo la muda mrefu la uhaba wa nyumba kwa ajili ya makazi ya Maafisa na askari wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na  Jeshi la Kujenga Taifa.”alisema Meja Musira.
  Akifafanua Meja  Musira amesema awamu ya kwanza ya mradi huo imeanza ambapo  nyumba 6,064 zitajengwa na kugharimu dola za marekani milioni 300, utekelezaji wake unaendelea vizuri  katika Mkoa wa Dar es salaam na Pwani  tayari jumla ya nyumba 3128 zinajengwa.
  Kwa Mkoa wa Dar es salaam Meja Musira amesema nyumba 2,228 zinajengwa katika maeneo ya Lugalo, Gongola mboto, Ukonga, Navy Kigamboni, Ubungo Kibangu, Kunduchi KTC, Mbweni JKT  na Kimbiji.
  Akieleza zaidi Meja Musira amesema nyumba 1,160 kwenye maeneo manne ya Lugalo na Gongolamboto umeshakamilika kwa asilimia 100 na ukaguzi na uhakiki umeshafanyika.
  Kwa upande wa Mkoa wa Pwani Meja Musira alisema  jumla ya nyumba 840 zinajengwa katika maeneo ya msangani,Nyumbu,Kiluvya,Kisarawe na shule ya mafunzo ya awali Kihangaiko.
  Maeneo yanayohusika na mradi huu kwa sasa ni Arusha inatarajiwa kujengwa nyumba (792) Tanga (312) Pemba (320) Morogoro (616) Dodoma (592) Kagera (144) na Kigoma (160).
  Kwa upande wake Mhandisi wa Wizara hiyo Bw. Stephen Mpapasingo amesema mradi huo unatekelezwa kwa awamu na  unalenga kuondoa kabisa tataizo la makazi kwa  Maafisa na askari wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na  Jeshi la Kujenga Taifa
  Mkandarasi wa mradi huu ni kampuni ya Shaghai Construction (Group) General Company  kutoka China

  0 0

  Shiriko lisilo la Kiserikali la Farm Africa kwa kushirikiana na wakulima wa uyoga wa wilaya za Mbulu na Babati wiki iliyopita waliandaa siku maalum ya kula uyoga kwa wakazi wa wilaya hizo.

  Tukio hilo lilifanyika katika katika kitongoji cha Magugu wilayani Babati ambapo wakazi walipata nafasi ya kuonja aina mbalimbali za mapishi ya uyoga.Wakulima 15 wa uyoga walio katika mradi wa Misitu wa Farm Africa walishiriki shughuli hiyo kwa kupika na kugawa  bure uyoga uliopikwa kwa wakazi wa eneo hilo.

  Kilimo cha uyoga ni njia mbadala iliyopo kwenye mradi wa misitu ambapo wakulima badala ya kukata miti kwa ajili ya kuitumia kwa kuwapatia kipato, wanapanda uyoga ambao wanauuza na kuwaingizia kipato.
  Siku ya kuonja uyoga ilikuwa na madhumuni ya kuwahamasisha wakazi wa Babati kuhusu faida za kilimo cha uyoga, mapishi yake na jinsi kilimo hicho kinavyoweza kuwaingizia kipato cha ziada.
   Wananchi wakiburudika na rosti ya uyoga
  Wananchi wakipakuliwa rosti ya uyoga.
   Ni wakati wa kula uyoga!
   Wadau wakipatiwa mafunzo ya kilimo cha uyoga na wakulima walio kwenye mradi wa misitu wa Farm Africa
   Wakulima wakionyesha jinsi uyoga unavyooteshwa
   

  0 0

  MKURUGENZI mtendaji wa Azania benki,Charles Singili amewataka wananchi kuwa na mazoea ya kujiwekea akiba kwa manufaa ya baadae.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa akauni mpya ya benki hiyo iitwayo Dhamira, Singili amesema kuwa utaratibu wa kujiwekea akiba utapunguza tatizo la umasikini kwa wananchi.

  Aliongezea kuwa, endapo wananchi wakipatiwa elimu kuhisu faida za kutunza fedha zao,itasaidia kupunguza hali ya umasikini uliopo sasa.

  "Kwa kutambua matatizo yanayoikabili nchi yetu, Azania bank imeamua kufungua akaunti ambayo itamwezesha mwananchi kutunza fedha bila makato ya aina yeyote" alisema Singili.

  Singili aliongezea kuwa, akaunti ya Dhamira, itamsaidia mwananchi yeyote kutunza fedha kuanzia Sh. 50,000 na atapatiwa riba ya asilimia 8 kila mwenzi.

  Aliongezea kuwa, akaunti hiyo inatafunguliwa na mtu ambae ametimiza miaka 18 na kuendelea na itamsaidia kuweka riba kadri awezavyo.

  "Dhamira akaunti itamsaidia mwananchi kutimiza malengo au ndoto zao, pia kipindi cha chini kuweka akiba ni miezi 12," alisema.
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania,Charles Singili akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa akauni mpya ya benki hiyo iitwayo Dhamira (Dhamira Account) uliofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Benki hiyo,Ubungo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria kwenye uzinduzi huo wakimsikilizwa kwa makini Mkurugeni Mkuu wa Benki ya Azania,Charles Singili.
  Mkurugeni Mkuu wa Benki ya Azania,Charles Singili akimuelekeza namna ya kujaza fomu,Bi. Naomi Mapunda ambaye alikuwa mteja wa kwanza kufungua akauni hiyo ya Dhamira.
  Baadhi ya Maofisa wa Benki ya Azania.

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudenciana Kisaka akizungumza
   
  Na Denis Mlowe,Iringa

  JUMLA ya sh. bilioni 1.3 zimetumika katika ujenzi wa maabara za sayansi, hosteli za wasichana na chumba cha darasa katika shule za sekondari za Ismani, Nyang’ro na Kalenga zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
   
  Akizungumza na wahabari hivi karibuni ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Iringa,Pudenciana Kisaka  alisema kuwa halmashauri kupitia idara ya elimu Sekondari imekamilisha maabara tatu za masomo ya sayansi , chumba cha darasa na hostel katika shule hizo zilizokuwa zina upungufu wa majengo hayo.
   
  Alisema kuwa maabara moja imejengwa katika shule ya sekondari Ismani na ujenzi wake kukamilika  kwa asilimia 100 na inatumika kwa masomo ya Bailojia na imegharimu zaidi ya shilingi milioni 89.
   
  Kisaka alisema shule ya sekondari Kalenga imejengewa maabara mbili ambazo zimekamilika kujengwa na zinatumika kwa masomo ya Fizikia na Kemia na kugharimu shilingi milioni 29.
   
  Aidha alisema halmashauri hiyo imejenga hostel ya wasichana wa shule ya sekondari Kalenga ambao umegharimu sh. Milioni 258 mpaka kukamilika na ujenzi wa chumba kimoja cha darasa shule ya sekondari Nyang’oro  uliogharimu sh. Milioni 13.

  Kisaka akizungumzia kuhusu mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha tano alisema idara ya elimu imepangiwa jumla ya wanafunzi 2389 wa kidato cha tano katika shule sita hivyo idadi imeongezeka kutoka 1433 mpaka 2389 sawa na asilimi 156 ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliopokelewa kwa mwaka 2013/2014 walikuwa 1433 sawa na asilimia 93.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa kiwango cha Lami. Wengine walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero, Mama Salama Kikwete, Mbunge wa Viti maalum kutoka Chama cha Wananchi CUF, Mbunge wa Simanjiro Cristopher Ole Sendeka, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi na viongozi wengine wa Kitaifa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Mayamaya –Mela - Bonga Km 188.15. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa Serikali ya Japan kushoto, katikati ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero, Mama Salama Kikwete pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi.

  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli watano kutoka kulia akicheza ngoma na kikundi cha ngoma za asili cha Bicha kabla ya uzinduzi rasmi wa barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa kiwango cha lami.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Salama Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akizungumza na Mzee maarufu wa Wilaya ya Kondoa Balozi mstaafu Mustapha Nyang’anyi kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge.
  Katapila likisafisha sehemu ya Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
  Taswira: ‘Mkeka mpya’ Barabara ya Bicha- Kondoa mjini inavyoonekana mara baada ya kukamilika kwake.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

  0 0  0 0

  Makabidhiano ya bati yaliyofanyika nje zinapojengwa ofisi za chama cha mpira  Mkoa wa Njombe ( Njolefa) kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa shirika la Tanwat Rajeev Singh, Edymund  Munubi afisa tawala wa Tanwat, Katibu wa Chama cha Mpira Mkoa wa Njombe  Steven Njowoka na wa Mwisho ni Afisa Utamaduni na michezo Mkoa wa Njombe Steven Sanga. Picha na James Festo.
   
   ======== ==========  ========
  Na James Festo, Njombe.

  CHAMA  chama cha mpira  Mkoa wa Njombe kimepokea mchango  wa bati, saruji na mbao wenye thamani ya zaidi ya  shilingi milioni  moja kutoka kwa wadau wa michezo zitakazazosaidia kuendelea kujenga ofisi zao ngazi za mkoa.

  Akiongea katika makabidhiano katibu wa chama hicho  Steven Njowoka alisema kuwa wamepokea   michango kutoka kwa wadau  ambapo hapo juzi walifanikiwa kupokea bati 53, Mifuko ya saruji  kumi na mbao  77 vyote vyenye thamani ya shilingi milioni  1,295,000/= na kufanya jumla ya michango kutoka kwa wadau wa michezo kufikia shilingi  milioni  1,891,000/=.

  Njowoka aliendelea kuwaomba wadau mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Njombe kuendelea kuchangia mchango utakaokifanya chama hicho mkoa wa Njombe kukamiliisha ujenzi wa ofisi zenye vyumba saba vilivyofikia hatua ya kupauliwa  kwani hivi sasa wanafanya kazi katika jengo ambalo wamepangishwa.

  "sisi kama chama cha mpira bado tunahitaji kusaidiwa ...lengo letu ni kuwa hosteri yenye uwezo wa kulaza wachezaji na unapotaka  kuchangia usiangalie sura ya Njowoka angalia Njorefa inafa inahitaji nini kutoka kwako"alisema Katibu wa Njorefa.

  Katibu huyo aliwataja wadau wakubwa  waliotoa michango hiyo kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa shirika la Tanwat  Rajeev Singh ambaye  alitoa Bati zenye thamani ya shilingi laki nane, Diwani wa kata ya Uwemba Bw. Edward  Mwalongo ambaye alichangia mbao zenye thamani ya shilingi 355000/= na Mkurugenzi wa kampuni ya Jr fire familigaion  Bw Raymond Ngondola alitoa mifuko  kumi ya saruji yenye thamani ya shilingi 140,000/=.


  Naye Afisa Utamaduni na michezo Mkoa wa Njombe Steven Sanga alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa timu mbalimbali kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti itakayoifanya michezo kusonga mbele  ikiwa pamoja na  kufuata taratibu na kubainisha kuwa viwanja vingi vya michezo Mkoani hapa  vinamilikiwa na taasisi za elimu hali ambayo inawalazimu kuanza kufanya marekebisho ili kuvitumia katika michezo.
   
  Nao baadhi ya wadau hao, Rajeev Singh na Raymond Ngongola aliwasihi  wazazi kuachana na itikadi ya kudhani michezo ni uhuni badala yake kuanza kufikiria kuwa michezo huchangamsha akili ya mwanafunzi na kuahidi kuendelea kukichangia chama hicho.

  0 0

   Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) juu ya mafanikio ya uzalishaji wa chakula nchini kwenye viwanja vya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) kwenye viwanja vya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Mkuregenzi wa Mipango na Uendeshaji wa NFRA, Anna Ngoo. 
   Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) kwenye viwanja vya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) Charles Walwa na kushoto ni Mkuregenzi wa Mipango na Uendeshaji wa NFRA, Anna Ngoo. 
   Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza. 
   Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza, akiangalia magunia ya vyakula yaliyohifadhi wa kwenye ghala la Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) baada ya kuzungumza na waadhishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza, akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa waandishi wa habari kabla ya kuondoka kwenye viwanja vya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA).Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) Charles Walwa. Picha na Hussein Makame-MAELEZO.

  0 0

  DSC_0045
  Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Balozi wa kampeni ya "Fun For Funds", Madaraka Nyerere (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam dhumuni lake la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za jukwaa la sanaa na ubunifu ili kukuza vipaji vya vijana kupitia mafunzo mbalimbali ya sanaa na kutoa muongozo wa jinsi ya kuanzisha wazo la ubunifu na kulikamilisha.Na kuongeza pia vijana wataunganishwa na majukwaa mengine kama hili kwa nchi za Afrika Mashariki kama vile The Nest, PAWA 254 na Creative Garage yote ya Kenya na Africa Sanaa Kollective ya Uganda.

  DSC_0067
  Balozi wa kampeni ya kuchangisha fedha, “FUN FOR FUNDS” mwanamuziki mzalendo mzee wa ‘Sumu ya Teja’ , Vitali Maembe akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewataka wasanii wenzake kuungana kuwa kitu kimoja katika kukuza utamaduni wetu kwa kubadilishana uzoefu wa kazi zao bila choyo.
  DSC_0104
  Mjumbe wa bodi ya shirika lisilo la kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA), Rose Haji Mwalimu akitoa rai kwa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo (hawapo pichani) na kuwataka kutumia kalamu zao vizuri na kuhakikisha kampeni hii inafanikiwa.

  Madaraka Nyerere, Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere, pamoja na Mwanamuziki Mzalendo Vitali Maembe wameteuliwa na shirika lisilo la kiserikali Culture and Development East Africa (CDEA) kuwa mabalozi wa kushiriki kampeni ya kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuhamasisha jamii kuchangia ujenzi wa jukwaa la sanaa na ubunifu jijini Dar es Salaam.

  Kampeni hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro imeandaliwa na CDEA kupitia njia ya kupanda Mlima Kilimanjaro kuanzia Septemba 7 hadi 13 mwaka huu ili kujenga jukwaa na sanaa na ubunifu litakalowapa fursa wasanii na vijana kukutana, kufikiri na kubuni kwa pamoja ambapo mawazo ya kisayansi yatakutana na sanaa na pia sanaa kukutana na taaluma nyinginezo nyingi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Ayeta Wangusa anasema “ili kufanikisha kampeni yetu ya mwaka mmoja tuliyoipa jina la ‘FUN FOR FUNDS’, tumeona ni vyema kupanda mlima Kilimanjaro kwa kumtumia Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya CDEA, Madaraka Nyerere pamoja na Vitalis Maembe ambaye ni mwanamuziki mzalendo”
  DSC_0090
  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA), Ayeta Wangusa (wa pili kushoto) akielezea lengo la kuanzishwa kwa Jukwaa la sanaa na ubunifu ambalo vijana watapata fursa ya kukutana, kufikiri na kubuni kwa pamoja.

  Wangusa anasema fedha zitakazopatikana kwenye kampeni hii maalumu zitatumika kusaidia uzalishaji wa kazi za ubunifu za njia mbalimbali za mawasiliano-bunifu, kuwekeza katika kuanzisha maabara ya Filamu(yaani film lab) na kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli za Jukwaa la sanaa na ubunifu.

  Kwa upande wake Madaraka Nyerere anasema, “Nimekuwa nikipanda Mlima Kilimanjaro mara kwa mara kwa lengo la kuchangia ujenzi wa shule na shughuli nyinginezo za maendeleo, hivyo mwaka huu nimeona nifanye jambo hili kuhamasisha uchangiaji wa jukwaa hili la sanaa na ubunifu kwa kushirikiana na CDEA”.

  Madaraka anawaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia katika kampeni hii ili kufanikisha kufikiwa kwa lengo lake. “Wadau watakaopenda kuunga mkono zoezi hili,wanaweza kutuma michango yao kwa njia zifuatazo: M-PESA: 0765544714, TIGOPESA: 0713160668 Au Benki: CRDB BANK PLC, Jina la Akaunti: CULTURE AND DEVELOPMENT EAST AFRICA TZS ACC: 0150210421400, USD ACC: 0252210421400, SWIFTCODE: CORUTZTZ”

  Kwa upande wake Mzee wa ‘Sumu ya Teja’, Vitali Maembe amesema pamoja na kuwa hii ni mara ya kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro amefanya mazoezi ya kutosha kumuwezesha kufika kwenye kilele jambo ambalo ni ndoto yake kubwa kama mwanamapinduzi wa kimuziki.

  Culture and Development East Africa (CDEA) ni shirika lisilo la kiserikali linalotoa huduma kwa wasanii, viongozi wa utamaduni, wajasiriamali, maafisa utamaduni na mipango miji. Pia hufanya kazi na Mashirika makubwa ya kimaendeleo, taasisi za kiraia na Elimu katika maendeleo ya utamaduni, mipango na utekelezaji kwa Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
  DSC_0113
  Vitali Maembe akitoa vionjo vya wimbo wake Vuma.
  DSC_0121
  Vitali Maembe akionyesha moja ya kazi zake za sanaa atakazoenda kuzitundika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro panapo majaliwa.
  DSC_0146
  Picha ya pamoja baada ya mkutano na waandishi wa habari.
  DSC_0009
  Afisa Habari wa shirika lisilo la kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA), Mandolin Kahindi akitambulisha viongozi wa CDEA kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) pamoja na dhumuni la kuitisha mkutano huo.

  0 0

  Maswala ya udukuzi yameendelea kushika kasi katika maeneo mbali mbali ulimwenguni ambapo mataifa mbali mbali yameamua kuunganisha nguvu ya pamoja kupambana na uhalifu mtandao. Katika "UCHAMBUZI" nilio uandikia nilibainisha umuhimu wa kupata chombo kimoja chenye jukumu la kupambana na uhalifu mtandao ambacho kitatoa nguvu kubwa ili kuweza kukabiliana na hali mbaya ya uhalifu mtandao hivi sasa.

  Kundi jipya lenye makao yake barani ulaya linalounganisha pamoja nchi wanachama wa bara ulaya pamoja na Canada, Colombia, Australia na marekani limedhamiria kuunganisha mataifa mengine na kuhakiki maswala mbali mbali yahusuyo usalama mtandao yanafanyiwa kazi ipasavyo.

  Kwa wafatiliaji wa habari za maswala ya usalama mitandao watakua wamepata  kuona taarifa mbali mbali za hivi karibuni zenye kuonyesha ukuaji wa kasi wa uhalifu mtandao ambapo umetabiriwa kushika kasi zaidi kadri muda unavyo zidi kwenda ambapo uhalifu mwingi wa sasa unategemewa kuhamia katika mitandao.

  Katika andiko la naibu mkurugenzi wa chombo cha uingereza kinacho shughulikia maswala ya uhalifu mtandao pamoja na kiongozi  wa kundi jipya la muunganiko wa nchi la kukabiliana na uhalifu mtandao kama inavyo someka "HAPA" wame elezea ukuaji wa changamoto mbali mbali kwa vyombo vya usalama katika mataifa mengi na kusisitiza kuna umuhimu mkubwa wa kuunganisha nguvu za pamoja ili kuweza kufanikiwa katika vita dhidi ya uhalifu mtandao.

  J-CAT imedhamiria kuzileta pamoja nchi wanachama pamoja na mataifa mengine yatakayo onyesha utayari ili kuweza kukabiliana kwa pamoja dhidi ya uhalifu mtandao ambapo matumaini makubwa yatakua ni kukusanya taarifa za kiuhalifu kutoka katika makampuni ya serikali na binafsi ili kubaini aina za uhalifu na kujua maeneo athirika zaidi ili kuweza kuunganisha nguvu. Nchi zaidi zitaenelea kushirikishwa baada ya majaribio ya mpango huu wa kuunganisha nguvu kuweza kufikia pazuri.

  Aidha, Chombo cha upelelezi cha Marekani (FBI) kupitia taarifa inayosomeka "HAPA" imebainisha kulipa kipaumbele cha juu swala la mapambano dhidi ya uhalifu mtandao kutokana na kilicho zungumzwa na mkurugenzi wake ya kuwa nchi hiyo tayari imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na wahalifu wanao onekana na kwa sasa wahalifu mtandao kua ndio changamoto yake kubwa na hivyo wameazimia kuanza mapambano na uhalifu huo.

  Kwa upande mwingine katika mkutano mkuu wa maswala ya usalama mtandao wa mwisho wa mwaka ambapo nimeteuliwa kuwa katika panel ya washauri mada zinazotegemewa kujadiliwa na wataalam kutoka maeneo yote duniani ni pamoja na kutafuta njia rafiki ya kufikiwa kwa malengo ya kuunganisha hasa bara la afrika kuweza kuwa na njia ya pamoja ya kupambana na uhalifu mtandao huku maswala ya kisheria  za kimtandao yanavyo sumbua mataifa mbali mbali nini utatuzi wake. 
  Panategemewa kupatikana taarifa kamili ya mkutano huo mapema ili watanzania ( wenye ufahamu wa maswala ya usalama mtandao) nao waweze kushiriki.

  0 0


  0 0

   Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma mchana huu.

  Watu zaidi ya 35 wamepoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 86 kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio hivi sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi,liliisukuma ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.

  Hali iliyoipelekea basi hilo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.Picha na Ahmad Michuzi,Musoma.
  Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
  Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 35 kupoteza maisha hapo hapo,wakishuhudia tukio hilo la ajali.
  Buldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.
  Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
  Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.

  Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
  Uokoaji ukiendelea.
  Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.


  0 0


  Mkurugenzi wa Didas Entertainment, almaarufu kwa jina la Didas Facion akiongea wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni iliyofanyika jana Septemba 4, 2014 katika viwanja vya Leadrs Club. Pembeni yake ni  Msanii Wastara Juma na  Rais Wa Bongo Movie Steve Nyerere. Mfuko wa Pensheni Kwa Watumishi wa Umma PSPF.

  Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akiongea machache wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni iliyofanyika jana Septemba 4, 2014 katika viwanja vya Leadrs Club.

  Rais Wa Bongo Movie Steve Nyerere akitema cheche.

  Wazazi wa mwanadada Didas...

  Bendi ya YAMOTO akimwaga burudani.
  Wageni waalikwa.
  Msanii H. Baba akiwanga burudani.
  Mke wa H.Baba, Flora Mvungi akitoa burudani sambamba na wacheza shoo wake.
  Baba na Mama wakitoa burudani.
  Wasanii waliohudhuria uzinduzi huo.

  0 0

  5 
  Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akikabidhi mashine ya kufyatulia matofali mwenyekiti wa kikundi cha Mbagala Youth Group Said Mponda baada ya kuzipokea kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa NHC ambalo limetoa mashine kwa vikundi hivyo ili kusaidia serikali katika kupambana na tatizo la ajira nchini kwa vijana mashine hizo zilikabidhiwa kwa mkuu wa wilaya na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC tawi la Temeke Bw. Wencenslaus Tillya. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
  3 
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akipokea mashine za kufyatulia matofali kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Wilaya ya Temeke Bw. Wencenslaus Tillya ambazo zilikabidhiwa kwa vikundi vya vijana wilayani humo.
   
  4 
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akikabidhi mashine kwa mwenyekiti wa kikundi cha Sokoine Youth Development William Gabriel.
  Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akikabidhi mashine ya kufyatulia matofali mwenyekiti wa kikundi cha Chang'ombe Youth Development Eunice Mlwale baada ya kuzipokea kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa NHC
  8Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akikabidhi mashine ya kufyatulia matofali mwenyekiti wa kikundi cha Chapakazi Youth Youth Nathanaeli Daniel Kidaila baada ya kuzipokea kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa NHC9Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akiwa katika picha ya pamoja na vikundi hivyo mara baada ya kukabidhi mashine za kufyatulia matofali kwa vikundi vya vijana vya Temeke ambazo zimetolewa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC Kulia kwa Mkuu wa Wilaya ni Wencenslaus Tillya Meneja wa NHC Temeke na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana.10Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba NHC na baadhi ya maofisa wa Manispaa ya Temeke.11Baadhi ya waandishi wa habari na vijana waliojitokeza katika makabidhiano hayo wakiwa katika hafla hiyo12 
  Baadhi ya mashine za kufyatulia matofali zilizokabidhiwa kwa vikundi hivyo.13 
  Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akimzikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana wakati alipokuwa akitoa shukurani zake kwa shirika la Nyumba NHC kwa kutoa mashine hizo, wa pili kutoka kulia ni Wencenslaus Tillya Meneja wa NHC wilaya ya Temeke.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua mkutano wa wadau wa mifugo kwenye ukumbi wa hoteli ya Malaika jijini Mwanza Septemba 5, 2014.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana (kushoto) baada ya kufungua mkutano wa wadau wa sekta ya mifugo kwenye ukumbi wa hoteli ya Malaika jijini Mwanza, Septemba 5, 2014. Kulia ni mfugaji na Mkulima kutoka Kiteto. Papian Emmanuel.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Kaimu Mkuu wa Mwanza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kufungua mkutano wa wadau wa mifugo kwenye ukumbi wa hoteli ya Malaika jijini Mwanza, Septemba 5, 2014. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameitaka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kufanya upya sensa ya mifugo kwani ya mwisho ilifanyika miaka 30 iliyopita.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Septemba 5, 2014) wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa wadau wa mifugo hapa nchini ulioanza leo kwenye hoteli ya Malaika jijini Mwanza.

  Waziri Mkuu amesema ni vigumu kwa wafugaji kutaja idadi halisi ya mifugo waliyonayo lakini kama Wizara hawana budi kuweka mbinu za kisasa za kufanya sensa hiyo hata kama itawachukua miaka miwili.

  0 0

   Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,pichani wa tatu shoto Ruge Mutahaba akiwa sambamba na baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajiwa kutumbuiza leo usiku mjini Musoma kwenye tamasha la Fiesta,lakini hata hivyo Uongozi wa Clouds Media Group,Prime Time Priomotions ambao ndio waandaaji pamoja na Wadhamini wa tamasha hilo kwa pamoja wamekubaliana kuahirisha onyesho hilo mpaka hapo baadae itakapotangazwa tena.

  Kuaihirishwa huko kunafuatia ajali mbaya na ya aina yake iliyopelekea simanzi na majonzi makubwa wakazi wa mji wa Musoma na vitongoji vyake.Waandaji wa tamasha hilo pamoja na Wasanii pia walipeleka vifaa mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma ya awali kwa majeruhi mbalimbali waliopatwa na ajali hiyo,Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara.
  Mtangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu sambamba na Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la kisanii Shilole sambamba na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba wakikabidhi vifaa tiba mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma ya awali kwa majeruhi mbalimbali waliopatwa na ajali hiyo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk.Samsoni Winani.
   Mganga Mkuu wa mkoa wa Mara,Dk.Samsoni Winani akifafanua jambo kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili, Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika kijiji cha SabaSaba,nje kidogo ya mji wa  Musoma mchana huu.Ambapo DK Samsoni alisema kuwa ajali hiyo ni aina yake na haijawahi tokea tangu ajali ya aina hiyo ilivyotokea mnamo mwaka 1996.
   Mkuu wa Wilaya ya Busega Paul Mzindakaya akimpa pole Mganga Mkuu wa mkoa wa Mara,Dk.Samsoni Winani kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili, Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika katika kijiji cha eneo la SabaSaba,nje kidogo ya mji wa  Musoma mchana huu.

  0 0


  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia madhara ya mapigo ya silaha mbalimbali wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
  Sehemu ya askari wakitoka katika mapambano wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakisimama kwa wimbo wa Taifa wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
  Askari wa kikosi cha mizinga akichukua taswira meza kuu wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakipata picha ya kumbukumbu na sehemu ya wapiganaji wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza askari wanawake walioshiriki katika mapambano wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014. PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Edwin Moshi, Makete

  Walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Iwawa iliyopo Makete mkoani Njombe wametakiwa kutoridhika na kubweteka na shule hiyo kushika nafasi ya nne kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita 2014 yaliyotangazwa miezi michache iliyopita

  Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro katika hafla ya kuwapongeza walimu wa Iwawa sekondari baada ya shule hiyo kushika nafasi ya 4 kitaifa, nafasi ya 2 kikanda na nafasi ya 1 kwa mkoa wa Njombe katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu

  Amewapongeza walimu kwa jitihada zao za kufundisha pamoja na moyo wa wanafunzi katika kujisomea ambavyo kwa pamoja vimepelekea kuitangaza wilaya ya Makete kielimu na kuwataka kupanda na kushika nafasi za juu katika mitihani inayofuata
  "Ni kweli mnastahili pongezi lakini nawaombeni ongezeni bidii ili mitihani inayokuja mwakani mpande zaidi ya hapa, muitangaze wilaya yetu, tukishirikina pamoja tunaweza" amesema Matiro

  Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi kushirikiana katika kuchangia maendeleo ya shule kwani serikali inaunga mkono jitihada zao pale tu inapoona wamechangia

  Amesema kumekuwa na kasumba ya watu wachache kuwakatisha tamaa wananchi wengi wenye moyo wakuchangia miradi ya shule, na kusema wananchi wasikatishwe tamaa na watu wa aina hiyo kwani serikali haiwaachii peke yao, wao wakichangia kwa kiasi fulani serikali nayo humalizia palipobakia huku akisisitiza kuwa kwa shule zenye upungufu wa walimu, serikali inalitambua tatizo hilo na ndiyo maana inapanga walimu wapya kila mwaka katika shule hizo na mwishowe upungufu huo utamalizika

  Awali akisoma taarifa ya shule kwa mkuu wa wilaya, mkuu wa shule hiyo Mwl. Antony Ng'wavi amesema shule yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja na walimu jambo ambalo linachangia kupungua kasi ya ufaulu kwa kiasi kikubwa zaidi, huku akiahidi kuwa mwakani shule yake itafanya vizuri kuliko mwaka huu

  0 0

   Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Mohamed Aziz Abood  Akimkabidhi cheti Kada UVCCM Wilaya ya Morogoro mjini CCM,Wakati wa kufunga kambi ya UVCCM kutoka kata za Manispaa ya Morogoro eneo la Morning Site kata ya Milimani
   Mbunge wa Jimbo la Morogoromjini Mh Aziz Abood akiwaongoza vijana wakati wa kula kiapo mara baada ya kumalizika kwa kambi ya umoja wa vijana ccm wilaya ya Morogoromjini Akiwa sambamba na Katibu wa ccm wilaya ya Morogoro mjini nyuma,Pamoja na Katibu wa uvccm wilaya ya morogoro mjini Kulia.
    Baadhi ya washiriki waliomaliza kambi ya Uvccm Wilaya ya Morogoro mjini jana.

  Washiriki wa Kambi ya Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Morogoro wakila Kiapo Mbele ya Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini

    Mbunge wa Jimbo la Morogoromjini Mh Aziz Abood  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kambi ya UVCCM Wilaya ya Morogoro Mjini.
   Mbunge wa Jimbo la Morogoromjini Mh Aziz Abood  akitangaza rasmi kumalizioka kwa kambi hiyo.

older | 1 | .... | 356 | 357 | (Page 358) | 359 | 360 | .... | 1896 | newer