Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

GARI HII PIA ILIKUMBWA NA ILE AJALI YA MABASI MAWILI ILIYOTOKEA JANA MUSOMA,AMBAPO WATU WAWILI WALIOKUWEMO WALIPOTEZA UHAI


NEWZ ALERT:TAMASHA LA FIESTA SASA KUFANYIKA KESHO JUMAPILI MJINI MUSOMA.

$
0
0
 
 MKurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi,Bwa.Ruge Mutahaba kwa niaba ya uongozi wa Clouds Media Group na PrimeTime Promotions  Ltd ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014,ametangaza rasmi kuwa onesho la tamasha hilo lililobeba ujumbe murua kabisa wa sambaza upendo, litafanyika kesho jumapili ndani ya uwanja wa Karume.

Tamasha hilo la Fiesta lilipangwa kufanyika JANA ijumaa mjini Musoma mkoani Mara lakini kufuatia ajali mbaya iliyotokea mkoani humo jana na kusababisho vifo vya watu zaidi ya 40,iliyotokea katika kijiji cha Sabasaba,wilaya ya Butiama mkoani Mara lilisitishwa ili kwenda sambamba na tukio zima katika kuwafariji wakazi wa Musoma na vitongoji vyake,kutoa mkono wa pole,ambapo Wasanii waliotarajiwa kushiriki tamasha hilo na Waandaaji walitoa msaada wa vifaa tiba kwa hatua za awali kusaidia majeruhi waliokuwa wakipelekwa hospitali ya rufaa mjini Musoma.

SHIMIWI YATAKA VILABU VITAKAVYOSHIRIKI KUJISAJILI MAPEMA

$
0
0
Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Ally Katembo akifungua mkutano maalumu wa kupanga ratiba ya Mashindano ya SHIMIWI uliofanyika katika ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam mapema leo. Kushoto kwake ni Katibu wa SHIMIWI Bw. Moshi Makuka (wa pili) na wajumbe wa SHIMIWI wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
Katibu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka (wa pili kutoka kushoto) akitoa mada wakati wa mkutano maalumu wa kupanga ratiba ya timu zitakazoshiriki kwenye SHIMIWI mwaka huu katika ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam mapema leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Ally Katembo na wengine ni wajumbe wa SHIMIWI Taifa wakifuatilia mada.
Mmoja wa Wajumbe wa SHIMIWI akishiriki katika zoezi la kupanga makundi mbalimbali katika ratiba ya michezo ya SHIMIWI.
Kamati maalumu ikipanga ratiba ya makundi mbalimbali katika michezo ya mpira wa miguu,mpira wa pete, bao,karata, riadha,kuvuta kamba na kurusha tufe katika michezo ya SHIMIWI.
Baadhi ya wajumbe wa SHIMIWI na Viongozi wa Vilabu vya Michezo wakifuatilia mada.

=======  ======== ======
Viongozi wa vilabu vya timu zinazotarajia kushiriki kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayotarajiwa kuanza Septemba 27 mjini Morogoro wametakiwa kusajili timu zao mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza hapo baadae wa kushindwa kusajiliwa kutokana na mapungufu ya timu zao.

Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Ally Katembo aliyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano maalumu wa kupanga ratiba ya mashindano ya SHIMIWI uliofanyika ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam mapema leo.

Bw.Katembo alizitaka timu zinazotumia wachezaji walioajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu kuacha tabia hiyo na badala yake watumie wachezaji wenye mikataba ya mwaka mmoja na kuendelea ili kuepuka tatizo la kutumia mamluki kwenye timu zao.

"Tafuteni wachezaji ambao ni wafanyakazi katika Ofisi nyingine za Serikali kama timu zenu zina mapungufu ya wachezaji" alisema Bw. Katembo.

Naye Katibu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka aliwataka viongozi hao kutoa taarifa ya timu ambazo hazitashiriki mashindano hayo mapema iwezekanavyo ili kuepuka gharama zinazotumika katika maandalizi ya timu zao.

"Timu ambazo hazitaweza kushiriki ziwe wazi kusema hazishiriki kwa sababu SHIMIWI inatumia gharama nyingi kwenye maandalizi" alisema Bw.Makuka.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe wa SHIMIWI na viongozi wa vilabu vya timu mbalimbali kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mashirika ya Umma na Halmashauri za Wilaya.

Walawala CUP kuwasha moto Muheza

$
0
0

Mratibu wa mashindano ya OG Walawala Cup,Omari George (kulia) akipokea jezi zitakazotumika katika mashindano hayo kutoka Meneja Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abas Ali Isere katika hafla fupi iliyofanyika Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi Wetu

MASHINDANO ya kuwania Kombe la Walawala wilayani Muheza linatarajia kuanza mapema mwezi huu katika uwanja wa Jitegemee.

Mratibu wa Mashindano hayo, Omari George (OG)akizungumza mjini Dar es Salaam jana alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika ambayo ni pamoja na kuandaa vifaa vya michezo.

Alisema mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yamelenga kuibua vipaji vya wachezaji watakaochukua nafasi ya wachezaji waliowahi kuwika zamani na kujenga heshima ya wilaya Muheza kama vile Kasongo Athumani, ISsa Athumani Mgaya na James Kisaka.

OG alisema mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka kutoka mwaka 2010 kila timu shiriki hupatiwa jezi na washindi hupata zawadi mbalimbali kama vile vikombe, mipira na sare za michezo.

Alisema katika mashindano ya mwaka huu kila timu imepewa jezi seti moja, sare  kwa ajili ya makocha wa timu 18 zinazoshiriki mashindano hayo, sare kwa viongozi wa Chama cha Soka Wilayani (TFF) na waamuzi watakaochezesha mashindano hayo.

Mratibu huyo alisema amekuwa akishirikiana na Kampuni ya Isere kuandaa vifaa vinabyotumika katika mashindano hayo Kutoka mashindano ya Walawala Cup yaanzishwe timu zilizowahi kutwaa ubingwa ni Polisi (2011), City Boys (2012) na Bambino (2013).

Serikali yatumia zaidi ya Bilioni 16 kujenga Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo (the law school of Tanzania).

$
0
0
Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi akiwaeleza jambo waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole.

Afisa Habari wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole akiwaleza waandishi wa habari lengo la uanzishwaji wa Taasisi ya Mafunzo ya Vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria ikiwa ni kuwaongezea ujuzi na stadi za kazi kwa ajili ya kutoa huduma bora na yenye tija ka wananchi, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.

 Mwanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bw. Edwin Rwekaza akiwaleza waaandishi wa habari kuhusu msisitizo unaotolewa na Taasisi hiyo katika mafunzo kwa vitendo ili kuwaongezea ujuzi katika utekelazaji wa majukumu pindi watakapo hitimu, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.
Mhadhiri wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Emil Lukiko akiwaeleza jambo waandishi wa habari (Hawapo pichani) , wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.

Mkuu wa Kitengo cha Mitihani wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Ipyana Mwaikambo akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani), Kuhusu idadi ya wanafunzi waliodahiliwa toka Taasisi hiyo imeanzishwa ambapo alisema zaidi ya wanafunzi 4000 wameshadahiliwa mpaka sasa, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.
 Jengo la Kufundishia(Teaching Block) katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) lenye vyumba 2 vya mihadhara(lecture rooms) vyenye uwezo wa kuingiza wanafunzi 460 kila chumba, vyumba 72 vya semina

 Jengo la Mahakama ya kujifunzia (Teaching Court) lililopo katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) litalofungwa Video Link ili wanafunzi waweze kujionea moja kwa moja namna kesi zinavyoendeshwa


Muonekano wa ndani wa Chumba cha Mahakama katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School)

Muonekano wa ndani wa chumba mihadhara(lecture rooms)
(Picha na Hassan Silayo- MAELEZO).

======  =======  =======
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali yatumia zaidi ya  Bilioni  16 kujenga Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo (the law school of Tanzania).
Hayo yamesemwa  leo jijini Dar es salaam na Msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika taasisi hiyo iliyolenga kuona hatua iliyofikiwa tangu kuanza kwa ujenzi wake mwaka 2010.
“Baada ya kukamilika kwa ujenzi huu mwaka 2013 uendeshaji wa mafunzo ulihama kutoka  chuo kikuu cha Dar es salaam na kuanza kutumika kwa majengo haya ya kisasa yaliyojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Katiba na sheria”
Akifafanua Ngole amesema ujenzi huo umehusisha ujenzi wa Mahakama ya mafunzo, (Teaching Court) vyumba vya madarasa (leacture theartres),Maktaba ya Kisasa (Library) Jengo la Utawala ( Admistration block) Mgahawa na nyumba za watumishi.
Pia Ngole alitoa wito kwa wanasheria wote wanaohitimu katika Taasisi hiyo kuwa tayari kutoa huduma popote pale nchini Tanzania kwa kuwa Serikali imetumia fedha nyingi kuanzisha Taasisi hiyo ili iwanufaishe wananchi wote.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha mitihani  bw. Ipyana Mwaikambo alisema Taasisi hiyo imeshadahili wanafunzi zaidi ya 4000 toka kuanzishwa kwake mwaka 2008 hadi sasa.
Naye Mmoja wa wanafunzi wa Taasisi hiyo Bw. Edwin Rweykaza amesema Taasisi hiyo inatoa msisitizo katika mafunzo ya vitendo na kuwajengea uwezo wa kutimiza majukumu yao mara baada ya kuhitimu.
Kuhusu maadili Rweykaza alibainisha kuwa  ni swala linalopewa kipaumbele kwa wanafunzi wote wanaojiunga na Taasisi hiyo.
Serikali imetimiza  ndoto ya miaka mingi ya kujenga majengo ya kisasa ya Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (The law school of Tanzania) inayotoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria wanaotarajia kufanya kazi kama mawakili kwa lengo la kuongeza stadi na ujuzi wa wanasheria hao katika kuwahudumia wananchi.

SIMBA SC YAINYUKA GOR MAHIA 3-0

$
0
0
Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya 3-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).

Golikipa wa Gor Mahia, Fredrick Onyango akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Gor Mahia ya Kenya, Kennedy Opiyo katika chezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 3-0.
 Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Gor Mahia ya Kenya, Kennedy Opiyo katika chezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 3-0.
 Uniwezi...
 Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akimtoka Kennedy Opiyo.
Okwi akiambaa na mpira huku Kennedy Opiyo akimsindikiza kwa macho.
Okwi akiipangua ngoome ya Gor Mahia.
 Beki wa Gor Mahia, Harun Shakana akijaribu kumzuia.
Okwi akimtoka Harun Shakana.
 Okwi akimtoka beki wa Gor Mahia, Harun Shakana
 Okwi akichuana na beki wa Gor Mahia, Harun Shakana
 Ramadhani Singano 'Messi' akichuana na beki wa Gor Mahia ya Kenya.
 Kikosi cha Gor Mahia.
 Kikosi cha Simba.
Mashabiki wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.

mji wa musoma na vitongoji vyake ni simanzi na majonzi tuu.!

$
0
0
Pichani ni sehemu mojawapo ya mitaa ya Musoma mjini ikiwa na muonekano wa watu wachache mara baada ya kunaswa na Camera ya Globu ya Jamii mapema leo mchana,mji huo umegubikwa na simanzi na manjonzi telee kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili yaliyogongana uso kwa uso likiwe gari ndogo,na kupelekea kuondoa uhai wa watu takribani 40 na zaidi katika kijiji cha Sabasaba wilayani Butiama mkoani Mara.

Waandishi wa habari wapigwa msasa kuhusu namna bora ya kuimarisha uandishi wa habari za shughuli za Bunge

$
0
0
Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Itifaki wa Bunge Maalum la Katiba, Bw. Jossey Mwakasyuka (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari kuhusu kuimarisha Uandishi wa Habari za shughuli za Bunge iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma. Kulia ni Mshauri wa mambo ya Kiufundi toka Shirika la UNDP, Bi. Anna Kochannesyan.
Mhariri Mtendaji Jamhuri Media Limited, Bw. Deodatus Balile akitoa mada mbele ya waandishi wa habari (hawako pichani) inayohusu Athari za Siasa katika uandishi wa Habari za Bunge, Madhara ya Vyombo vya habari kutumika, Miiko na Maadili ya kuzingatia wakati wa semina kwa ajili ya waandishi wa habari iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Kamati za Bunge Maalum, Bw. Athumani Hussein akitoa mada inayohusu Uandishi wa habari za Bunge na Siasa wenye tija kwa Taifa wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma.

RAIS KIKWETE ATUNUKU NISHANI ZA MIAKA 50 YA JWTZ

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete akimtunuku nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Jeshi la Wanachi wa Tanzania JWTZ, Mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange katika sherehe za kutunuku nishani zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ baada ya kuwatunuku nishani katika sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014. Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jeneral Davis Mwamunyange.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue katika sherehe za kutunuku nishani zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ baada ya Rais Jakaya Kikwete kutunuku nishani katika sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014. Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na wapili kushoto ni waziri Mkuu Mstaafu John Malecela.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

SAUTI SOL PERFORMING NISHIKE LIKE ON BEAUTY AND MUSIC NIGHT.

SALAAM ZA RAMBIRAMBI

$
0
0

TUNAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA MKUBWA WA TAIFA.

"Jana September 5 2014 kwenye eneo la Sabasaba Mjini Musoma ilitokea ajali mbaya sana ya mabasi mawili yakiwa na abiria na kulihusisha gari jingine dogo ambapo majeruhi ni zaidi ya 70 na waliofariki ni 39 Wanawake kwa Wanaume kwa mujibu wa taarifa mpya za vifo zilizotoka."

JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA IMEPOKEA TAARIFA ZA AJALI KWA MASIKITIKO  NA MSHITUKO MKUBWA SANA.

TUNAWAPA POLE NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WOTE WALIOPOTEZA WAPENZI WAO KATIKA AJALI HIYO,TUNATOA POLE KWA WATANZANIA WOTE NYUMBANI NA UGHAIBUNI KWA TUKIO  HILI LA KUSIKITISHA.  MWENYEZIMUNGU AWALAZE MAHALA PEMA PEPONI NDUGU ZETU, NA WALE AMBAO NI MAJERUHI MWENYEZIMUNGU AWAJAALIE NAFUU YA HARAKA NA WARUDI KATIKA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU.

INASIKITISHA SANA KUONA AJALI KAMA HIZI ZA BARABARANI ZIMEKITHIRI SASA NA TAKWIMU YAKE NI KUBWA KWA MWAKA INATISHA. NI MATUMAINI YETU SOTE  ZITACHUKULIA HATUA KALI ZA KUDHIBITI HALI  HII YA KUTISHA NA KUSIKITISHA SANA.

TARATIBU ZIFUATWE ZA UKAGUZI WA VYOMBO VYA USAFIRI NA WAFANYAKAZI WOTE WA MAKAMPUNI YA USAFIRI.  MAKAMPUNI YENYEWE NAYO YAKAGULIWE KWAKINA SANA.

TUNAMPONGEZA MH WAZIRI MWAKYEMBE KWA HATUA ZA AWALI ALIZOCHUKUA KWANI SASA BASI WANANCHI HATUTAKI KUSIKIA AJALI HIZI ZA AJABU AMBAZO NYINGI ZINATOKEA KIZEMBE PASIPO NA UNGALIFU WA MADEREVA. NA WATAKAO BAINIKA KUWA NA MAKOSA BASI WACHUKULIWE HATUA STAHIKI. KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUOMBOLEZA YA  MSIBA HUU MKUBWA TUNAMUOMBA MUNGU ATUPE UVUMILIVU NA  UPENDO ZAIDI KWETU SOTE.

MUNGU IBARIKI AFRIKA
MUNGU IBARIKI TANZANIA


Kagutta N.Maulidi
Katibu mkuu
Jumuiya ya Watanzania Italia.
 

UTT ILIVYOSHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA NA UWEKEZAJI 2014 PAMOJA NA MAONYESHO YA WAHANDISI

$
0
0
Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake wakiwa katika banda la Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji 2014, yaliyofunguliwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ofisa Uendeshaji wa UTT, Justine Joseph akitoa maelezo kuhusu fai anayoweza kupata mwanachama  mara baada ya kujiunga na mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania.  
Watu mbalimbali wakisoma vipeperushi vyenye maelezo ya huduma za UTT ili kujua faida za kujiunga na mfuko huo.
Ofisa Mafunzo wa UTT, Hilder Lyimo akitoa maelezo kuhusu huduma wanazotoa kwa watu walotembelea banda la Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji 2014 iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), Waziri Ramadhani akitoa maelezo kwa watu waliotembelea banda lao wakati wa Siku ya Wahandisi iliyoambatana na maonyesho ya biashara yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vijana wakipata maelezo kutoka kwa maofisa wa UTT waliotembelea banda lao wakati wa Siku ya Wahandisi iliyoambatana na maonyesho ya biashara yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), Waziri Ramadhani akitoa maelezo kwa watu waliotembelea banda lao wakati wa Siku ya Wahandisi iliyoambatana na maonyesho ya biashara yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watu wakipata maelezo katika banda la UTT wakati wa  katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji 2014 yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa UTT, waziri Ramadhani akiwa na Ofisa Uhusiano, Glory Temba wakati wa maonyesho ya Wakandarasi yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

BENKI YA CRDB KUJENGA TAWI LA KISASA KATIKA KIWANDA CHA DANGOTE- MTWARA

$
0
0
  Ndege ya Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote ikiwasili katika uwanja wa Mtwara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), akiwa na balozi wa Nigeria, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mtwara, Francis Kasoyaga (wa pili kulia) wakiwa uwanja wa Ndege wa Mtwara wakati wakimsubiri kumpokea Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
  Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akishuka katika Ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mtwara.
 Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akisalimiana na balozi wa Nigeria.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB akisalimiana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
 Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Mtwara, Francis Kasoyaga akipeana mkono na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
 Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
 Ujumbe ulioambatana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote ukifuatilia taarifa za kibenki kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akitoa maelezo kuhusu uzoefu wa benki hiyo katika kuhudumia miradi ya kijamii kwa ujumbe ulioambatana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akitoa maelezo kuhusu uzoefu wa benki hiyo katika kuhudumia miradi ya kijamii kwa ujumbe ulioambatana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akizungumza na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote. Katikati ni balozi wa Nigeria.
 Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia.
 Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akiagana Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mishangu International, Godbless Kweka akipeana mkono na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote.
 Alhaji Aliko Dangote,akisalimiana na wenyeviti wa vijiji vinavyozunguka Kiwanda cha Dangote. 
Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la Benki ya CRDB litakalojengwa karibu na Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Kata ya Mayanga Mtwara Vijijini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote akikata utepe kuzindua ujenzi wa kituo cha Polisi kitakachojengwa jirani na Kiwanda cha Saruji cha Dangote ambapo gharama za ujenzi wa kituo hicho zitagharamiwa na mwekezaji huyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mishangu International, Godbless Kweka na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara.
 Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group of  Industries, Alhaji Aliko Dangote, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mishangu International, Godbless Kweka na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara wakifurahia baada ya uzinduzi huo.
Alhaji Aliko Dangote akisalimiana na baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB pamoja na waandishi wa habari kabla ya kumalizia ziara yake ya kutembelea kiwanda cha Saruji cha Dangote.
 Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Kenneth Kasigila akiagana na Alhaji Aliko Dangote.
Wadau wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla ya chakula cha jioni. Wa pili kulia ni Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu. 

MBUNGE WA JIMBO LA NZEGA DR.KHAMIS KINGWANGALLAH ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS 2015

$
0
0
1 
Mchungaji Patrick Saso akifanya maombi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.9 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
10 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.DSC_0103 
Sheikh Abubakary Mwita akiomba dua kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
..............................................................................
Ndugu viongozi mlioko hapa, wageni waalikwa, wanahabari na watanzania wenzangu mnaonisikiliza;

Ni heshima kubwa sana kwangu kupata fursa hii. Ni katika nchi chache sana duniani, mtoto wa maskini kama mimi, aliyewahi kutembea mitaani akiuza karanga, Big G, maandazi, jerebi na samaki ili kusaidia wazazi kupata chochote kwa ajili ya kulisha familia anaweza kuota kuwa Rais wa nchi yake. Kwamba, mtoto aliyeenda shule bila viatu anaweza kuwa Daktari. Hii inamaanisha misingi ya haki na usawa kwa wote iliyowekwa na waasisi wa Taifa hili haikuwa ndoto za alinacha, bali ukweli na uhalisia, na inafanya kazi. Kwamba, siyo lazima uwe mtoto wa tajiri ndiyo uoneshe kipaji chako.

Hili peke yake linanipa sababu ya ziada ya kwa nini nitamani kuota kuwa Rais – nataka niwe mfano hai wa mafanikio ya Ndoto ya waasisi wa Taifa letu, kuwa sote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tuna haki na fursa sawa bila kujali nani anatokea familia ipi. Hii ni Tanzania ya ndoto za waliotutangulia. Ni lazima atokee kiongozi wa kizazi hiki anayetamani kuiongoza Tanzania itakayodumu kwenye misingi hii: kwamba sisi sote ni ndugu, na tuna fursa sawa. Kwamba, kuendelea kimaisha na kibinafsi ni haki ya binadamu na si hisani. Kwamba, mtoto wa mama ntilie kama nilivyokuwa mimi hapa, ana haki na fursa ya kuwa mbunge ama Rais wa nchi, sawa kabisa na mtoto wa Mbunge.

Kwa namna ya kipekee nichukue fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza waasisi wa Taifa letu kwa kusimamia tunu hizi. Niwashukuru pia viongozi wote walionitangulia kwa kuzilinda, na niahidi nitakuwa wa mwisho kuisaliti nchi yangu kwenye mambo haya.

Leo nimefika hapa kwa sababu chama change kina mfumo mzuri ulioasisiwa na Mwl. Nyerere na umelindwa na Wenyeviti waliomfuatia mpaka na sisi tumeukuta. Leo nimefika hapa kwa sababu Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wenzake wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu walitumia misingi imara iliyowekwa na waasisi wa Chama changu kuamua kuwa nami nina haki ya kuwa Mbunge. Leo nazungumza hapa nikiamini kuwa ni misingi hiyo hiyo itatoa uongozi wa Taifa letu katika awamu ijayo. 

Babu yangu Kizaa Baba aliishi Kijijini Goweko, Mlimani, na alikuwa mfugaji mkubwa wa ng’ombe na mrina asali mashuhuri. Yeye na mkewe waliishi maisha ya heshima sana pale kijijini. Hawakuwahi kusoma wala kuajiriwa japokuwa Babu yangu aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama Cha TANU na baadaye CCM katika ngazi ya Kata.
Babu yangu na Bibi yangu kizaa mama waliishi Nzega, na ndiyo walionilea baada ya ndoa ya mama yangu na baba yangu kuvunjika. Walinifundisha mambo mengi, kubwa likiwa ni kujiamini, pia kufanya mambo yangu kwa bidii, uadilifu, umakini na kwa nidhamu ya hali ya juu. Bibi yangu huyu hakusoma shule ya kizungu japokuwa alijifunza kusoma na kuandika. Babu yangu alikuwa mjukuu wa Chifu na hivyo alipata fursa ya kusoma Tabora School miaka miwili mbele ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Alifanya kazi mbalimbali chini ya serikali ya wakoloni, na alishiriki harakati za kuanzishwa na kusambaa kwa chama cha TAA na baadaye TANU. Babu yangu aliamini kuwa “binadamu wote ni sawa na kwamba kila mtu anastahili kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake”, na kwamba ukoloni haukuwa kitu cha sawa, na hivyo kujitawala wenyewe dhidi ya wazungu ilikuwa ni haki yetu; pia aliamini katika elimu, na hivyo alifanya juhudi kusomesha mabinti zake watatu, mama yangu aliishia kwenye ualimu kabla ya kuingia kwenye ndoa. Babu aliamini kuwa Tanzania ya mabinti zake itahitaji wasomi, ndoto ambayo ninaishi kuitekeleza kwa ajili ya mabinti zangu wawili na Kaka yao, HK Jr.
Japokuwa bibi na babu yangu wameishatangulia mbele ya haki, naamini wananitazama na kutabasamu huko waliko.
Ninaishi nikiamini kuwa hadithi ya maisha yangu ni mfano hai kwa maisha ya watanzania wengi. Na kwamba, nina deni la kulipa kwa vizazi vijavyo kwa kuwa mimi ninafaidi matunda ya mti uliopandwa na vizazi vilivyonitangulia. Naliona jukumu la kuhakikisha vizazi vijavyo vinafaidi urithi wa Tanzania kuwa ni la kwangu na wenzangu wa kizazi hiki.
Kazi yangu imenifikisha sehemu nyingi sana za nchi yetu – vijijini na kwenye majiji, imenikutanisha na watu wa kila aina – matajiri kwa maskini, wazee kwa vijana – hakuna hata mmoja kati ya watu hawa anayetegemea Serikali itamtatulia kero zake zote. Wanajua wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili wasonge mbele – na wana nia ya kufanya hivyo.
Nenda kwa wafanyabiashara wakubwa kule Pugu Road viwandani, kwa watumishi pale hospitali ya Taifa Muhimbili, ama pale sokoni Kariakoo kwa wafanyabiashara, wote watakuambia hawapendi kuona kodi zao zikitafunwa na wachache pale TRA, ama kulipa posho za bure kwa wabunge na mawaziri kule Bungeni, kulipia mashangingi ya viongozi na watendaji, kulipia tiketi za ndege daraja la kwanza kwa ajili ya safari za viongozi na wataalamu wetu kwenda kujifunza kupambana na umaskini wakati wakirudi wanauacha uzoefu uwanja wa ndege, ama kulipia semina, warsha na makongamano ya wataalamu ya kuandika sera za MKUKUTA, MKURABITA na kuandaa bajeti zisizotekelezwa kila mwaka.
Watanzania wanataka kupata huduma bora za afya, elimu, maji, miundombinu.
Nenda kule kwa watani zangu, Nanyumbu, ama Tandahimba, ama kwa ndugu zangu kule Nduli, Kyela, wazee kule watakuambia hawategemei Serikali itawaletea ubwabwa kwenye sahani za fedha, wanajua Serikali haitowafanyia kila kitu, lakini wanajua kabisa kuwa wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na wamekuwa wakifanya hivyo siku zote. Wanachohitaji wao ni kujengewa mazingira wezeshi kushiriki shughuli zao za kilimo ama biashara, waelekezwe namna ya kuongeza uzalishaji kwa kutumia njia za kisasa za kilimo chenye tija na ufanisi, waelekezwe wanapataje pembejeo, wanapataje mikopo yenye riba nafuu, wanahitaji, mwisho wa siku, wajue wapi watauza mazao yao kwa uhakika na bila kudhulumiwa wala kucheleweshewa malipo.
Watu hawatarajii serikali itabeba mizigo yao yote. Lakini wanaamini kabisa, kwamba tukibadili kidogo tu vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha serikali, tukibadili kidogo namna tunavyoendesha uchumi wetu, tutaweza, kwa kiasi kikubwa, kubadili muelekeo mzima wa maisha ya baadaye ya watoto na wajukuu zetu. Tutatoa uhakika wa kuiondoa nchi yetu kutoka miongoni mwa nchi maskini kabisa duniani.
Na mimi, kama watanzania wenzangu wengi, nina imani kubwa kabisa, kwamba tunaweza kubadili mustakabali wa Taifa letu. Tunaweza kufungua milango ya maisha bora zaidi kwa watanzania. Tutatoa fursa sawa kwa kila mtanzania kuishi kwa matumaini, kwamba atabadili maisha yake wakati wowote ule kuanzia leo. Tutaweza kuamsha ari ya kila mtanzania kuongeza bidii kwenye kazi akitumaini na kuamini kuwa kesho yake itakuwa bora kuliko jana yake, kuwa naye ataishi kwa heshima, raha na starehe ndani ya nyumba yake.
Ninaamini, kutokea ndani kabisa ya mifupa yangu, kuwa tukifanya uchaguzi sahihi wa vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha serikali yetu, haya ninayoyasema si ndoto za mchana. Ni mambo yanayowezekana.
Watanzania wengi wanaamini, kuwa tukifanya uchaguzi sahihi wa vipaumbele vyetu, mabadiliko makubwa, na ya haraka yatatokea kwenye uchumi wetu. Wanaamini tukichagua kiongozi sahihi mwakani, anayejua mahitaji ya nchi yetu kwa sasa na baadaye, tutafanikiwa.
Nyote mliopo hapa na wanaotusikiliza kutokea nje ya hapa mna jukumu la kututazama kwa ukaribu sana, kututathmini na kutupima sote; tuliojitokeza hadharani, walioanza safari za matumaini, wanaotajwa tajwa, na wale wanaosubiri kuoteshwa ili wakati muafaka ukifika muwape taarifa sahihi watanzania, kuwa kati yetu sote, ni nani anafaa kutuongoza kuelekea Tanzania ya ndoto zetu!
Kuwa, ni nani kati yetu ataweza kuwa Amiri-jeshi-mkuu, siyo kwa uanajeshi wake bali kwa uwezo na utayari wake wa kuwashirikisha wataalamu wa majeshi na kuamua kwa busara kutumia nguvu za kijeshi pale inapolazimika baada ya kupima na kuchambua aina nyingine zote za kutafuta suluhu za migogoro kabla ya kuamua vita.
Kuwa, ni nani kati yetu anayeamini katika uhuru, haki na usawa na wajibu wa watu wote, kama unavyolindwa na Katiba, anayeamini katika haki ya kuabudu lakini asiyekuwa tayari kuitumia haki hiyo kuwagawa watanzania kutokana na dini zao.
Kuwa, ni nani kati yetu anayeamini katika Haki ya kupata huduma bora za afya, elimu, maji, kama wanavyopata wabunge na mawaziri wetu, kama wanavyopata mahakimu na majaji wetu, kama wanavyopata wafanyabiashara na wakurugenzi wetu.
Kuwa, ni nani kati yetu ataweza kuhakikisha kuwa watanzania wote wanapata haki hizi bila kutazama hali zao kiuchumi ama daraja zao kijamii.
Kuwa, ni nani kati yetu anaamini zaidi katika uhuru na kujitegemea kwenye masoko na malighafi ili kudhibiti uchumi wetu mpana wa ndani, kujitegemea kwenye masoko ya pamba na nguo, kwenye mafuta ya kula, kwenye chakula cha uhakika kwa ajili ya watu wetu, kwenye mafuta na gesi ili tukwepe mtego wa kuwa sehemu ya uchumi, masoko na biashara za hasara na faida za makampuni makubwa ya kimataifa nje ya mipaka yetu. Ili tulinde thamani ya fedha yetu, ili tuwe na uhakika wa ustawi wa maisha ya watu wetu ndani ya nchi bila athari kubwa kutoka nje ya nchi yetu.
Kuwa, ni nani miongoni mwetu anaakisi taswira sahihi zaidi ya watanzania walio wengi, historia yake, rekodi yake, wajihi wake, mtazamo wake, ndoto zake, zinaakisi ‘utanzania’ halisi. Kuwa, yeye ni hitaji sahihi la watanzania.
Wakati ukifika, muwaeleze watanzania ukweli, wafanye uamuzi unaotokana na taarifa sahihi, wachague mtu sahihi.
Mimi, Ndugu zangu, natangaza rasmi sasa, kuwa ninatia nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015.
Na nimefikia uamuzi huu bila kuelekezwa, kusukumwa, kushawishiwa, kupangiwa ama kupanga na mtu ama na kikundi cha watu, bali kwa utashi na utayari wangu. Na ninayasema haya, haswa baada ya kutafakari mambo mengi kwa kina: mahitaji ya sasa na baadaye ya Tanzania ya ndoto zangu, uwepo wa fursa ya kugombea na kushinda uchaguzi ujao, uwezo wangu wa kuchambua mambo, kutafakari, kufanya maamuzi sahihi, kuchukua hatua za utekelezaji na kusimamia utekelezaji, uadilifu na uzalendo wangu, na zaidi nia yangu ya kuwa sehemu ya watanzania wengi tunaotaka kuona mapinduzi ya kifikra katika nchi yetu – mapinduzi ambayo yatatia chachu ya mabadiliko ya namna tunavyochagua vipaumbele vyetu kama Taifa na namna tunavyosimamia utekelezaji wa mambo mazuri tunayojipangia kama Taifa.
Ninatangaza nia ya kugombea Urais nikiwapa fursa watanzania wanipime na kunitazama mwenendo na uwezo wangu, nikiamini kabisa nitapimwa na kuungwa mkono ama kutoungwa mkono si kwa rangi ya ngozi yangu, si kwa jinsi yangu, si kwa umri wangu, na wala si kwa daraja langu kwenye jamii, dini yangu, ama kabila langu. Ninaamini nitapimwa kwa sifa na uwezo wangu, kama mtanzania.
Watanzania tuna sifa moja kubwa; kwenye mambo ya msingi ya kitaifa, tunakubaliana kuwa maslahi ya Tanzania hupanda juu ya maslahi yetu binafsi. Tudumishe utanzania wetu.
Ninaamini katika Ndoto ya Tanzania. Kuwa leo miaka 50 ya kuwa Jamhuri ya Tanzania tuna kila sababu ya kuwa Taifa la dunia ya kwanza, viongozi waliotutangulia wameandaa misingi ya kuifikisha Tanzania kwenye matamanio yetu. Kizazi chetu cha kina jukumu na wajibu wa kuikimbiza Tanzania kufikia kwenye ahadi inayotokana na ndoto za wazee na waasisi wa Taifa letu. Binafsi, niko tayari kulibeba jukumu hilo bila woga wala wasiwasi, maana naamini tusipojitokeza watu kama mimi, tutajikuta tunaongozwa na watu wasiostahili. Nina suluhu ya changamoto kubwa za leo na kesho: kupigana na njaa na kuhakikisha usalama wa chakula kwa watu wetu, tatizo la ajira kwa vijana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi ni miongoni mwa mambo ambayo kizazi chetu kitapaswa kuyafanyia kazi kwa haraka na umakini wa hali ya juu.
Mimi ninaamini kwamba, kama hata mimi nimefika hapa, basi kila mtanzania anaweza, na ana haki ya kufika hapa na kwenda mbele zaidi yangu. Mafanikio siyo haki ya wachache, ni tunu ya Mwenyezimungu kwa kila mtu. Ninaamini ni haki ya kila mtanzania kuota ndoto yake, kuifanyia kazi na kuifikia. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina wajibu wa kutoa fursa kwa watu wake kuota ndoto zao na kufikia mafanikio bila kukwama.
Na ndugu watanzania wenzangu, amini nawaambia, kuwa, mbele yetu tuna kazi ya ziada ya kufanya. Kazi ambayo ninaamini tunaiweza tukiamua; uwezo tunao, sababu tunazo na nia tunayo – sema tuna mapungufu makubwa kwenye kuchukua hatua za kutenda.
Mimi naamini kwamba; E Pluribus unum. Baina ya wengi, mmoja!
Kwamba; Mimi ni mmoja kati ya uwingi wetu. Siwezi kuwa salama kama wengine hawako salama, siwezi kuwa na raha kama wengine wanateseka. Ninaongozwa na ile dhana kwamba, matatizo ya mwenzangu, ni ya kwangu, na si yangu peke yangu, ni yetu sote kama jamii moja.
Hivyo:
- kitisho cha njaa ya familia fulani maskini kule Sakasaka, wilayani Meatu, ni kitisho changu na familia yangu, hata kama siyo familia yangu.
- Kucheleweshewa haki ya kuhukumiwa kwa mtuhumiwa wa mauaji ya kule Sombetini, ni kitisho kwangu pia, hata kama kesi siyo yangu.
- Mzee Makame wa kule Wete, Pemba, aliyefiwa na watoto wake akakosa msaada na yeye hana nguvu za kuzalisha tena, anavyokula mlo mmoja kwa siku ili asukume siku, inaniumiza na kunigusa moyoni, hata kama yeye siyo babu yangu.
- Mama John ni mpishi mzuri wa wali nazi kwa maharage, na ana wateja wengi mtaani kwake maeneo ya Mtaa wa Sikukuu, Sokoni Kariakoo; akifukuzwa, akapigwa virungu, akanyang’anywa pesa zake, akadhalilishwa na kumwagiwa chakula chake na mgambo wa jiji la Dar es salaam kwa kuwa anafanya biashara mahala pasiporuhusiwa, inaniumiza na kunigusa moyoni, hata kama yeye si mama yangu.
- Kama kuna mtoto asiyejua kusoma na kuandika kule Mrijo Chini kwa watani zangu warangi, hiyo inaniuma na kunigusa sana moyoni, hata kama yeye si mwanangu.
- Bwana Kalumanzila ni mmachinga nguo za mitumba mitaani. Yeye huchukua nguo zake kumi kwa kuaminiwa na mwenye belo kutokea soko la Karume, akiuza anachukua kifaida kidogo cha juu kinachozidi hapo juu na kurudisha pesa ya mwenye mali Karume jioni ya siku hiyo. Elfu mbili ama tatu anayopata inamfanya aishi yeye na mkewe na watoto wake. Akifukuzwa barabarani na akanyang’anywa mali, anakosa kazi ya kufanya na analazimika kumtumikia bosi mwenye mali mpaka atakapofidia mali iliyopotea bila kupata cha juu. Shida na madhila anayoyapata bwana Kalumanzila zinaniumiza na kunigusa sana moyoni, hata kama yeye si mjomba wangu.
Tarehe 4, Agosti 2014, Rais Kikwete akihutubia kwenye Kituo cha kimataifa cha maendeleo (Center for Global Development) alisema: “…Nataka na natamani kuwa Rais wa mwisho wa Tanzania kuongoza nchi masikini. Raslimali ya gesi inatoa nafasi na fursa kubwa kwa nchi yetu kuondokana na umasikini. Mimi nimeongoza nchi masikini, lakini nataka mrithi wangu kuongoza nchi yenye ustawi na utajiri…” Mimi nasema hivi: nataka na natamani kuwa Rais wa kwanza wa Tanzania kuongoza nchi Tajiri. Kama nitafanikiwa kuwa Rais, nitatumia miaka ya awali ya uongozi wangu kuikimbiza Tanzania kuelekea kwenye ndoto hii.
Mungu awabariki. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika.

TAMASHA LA FIESTA 2014 LASAMBAZA UPENDO WA KUTOSHA KWA WAKAZI WA MUSOMA.

$
0
0
Wasaniii walioshiriki tamasha la Fiesta 2014 wakiwa na mishumaa jukwaani wakisambaza upendo na kuwafariji wale wote waliopotelewa na ndugu zao,waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea  hivi karibuni wilayani Butiama mkoani Mara,ambapo watu zaidi ya 40 walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa musoma wakiwa ndani ya uwanja wa Karume,wakati tamasha la Fiesta 2014,likiendelea huku shangwe za hapa na pale zikiwa zimetawala kila kona ya uwanja.
 Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Barnaba ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la Waharade akiwaimbisha wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la fiesta 2014
 Mmoja wa wasanii kutoka kundi la Weusi ,Nick wa Pili akiwarusha wakazi wa mji wa Musoma usiku huu kwenye tamasha la Fiesta 2014,lililofanyika ndani ya uwanja wa Karume.
 Sehemu ya wakazi wa Musoma waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Karume.
  Mwanadada machachari awapo jukwaani,Shilole akiimba kwa madaha kabisa kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
 Pichani kati ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Rachael akiwa sambamba na madansa wake wakilishambulia jukwaa la fiesta vilivyo usiku huu ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma
 Mashabiki wakishangilia burudani iliyokuwa ikitolewa na wasanii mbalimbali jukwaani usiku huu
 Mmoja wa wasanii anaeokuja juu katika anga ya muziki wa hip hop,Young Killer a.k.a Msodoki akiimba jukwaani.
 Wakazi wa Musoma walivyojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2014 katika uwanja wa Karume usiku huu.
 Jicho la samaki  likiwa limewakusanya pamoja mashabiki wa tamasha la Fiesta lililokuwa likiendelea ndani ya uwanja wa Karume,mjini Musoma.
PICHA NA MICHUZI JR-MUSOMA

NAPE AZUNGUMZIA WAJIBU WA MATAWI YA CCM YA NJE NCHI KWA VIONGOZI WA CCM UINGEREZA

$
0
0
 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa mashina ya CCM Uingereza  ambapo aliwaambia matawi ya CCM nje ya nchi yawe mawakala wa kuleta mabadiliko ndani ya chama pamoja na kuwaunganisha watanzania kujikomboa kiuchumi
 Baadhi ya viongozi wa mashina ya CCM Uingereza wakifuatilia mafunzo kutoka kwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliyekuwa akitoa somo juu ya Wajibu wa Matawi ya CCM nje ya Nchi.
 Viongozi wa mashina wakisikiliza kwa makini
 Viongozi wa mashina ya CCM nchini Uingereza wakiandika pointi muhimu.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa mashina ya CCM nchini Uingereza .
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa mashina ya CCM London nchini Uingereza mara baada ya kutoa somo linalohusu Wajibu wa Matawi ya nje ya CCM katika ukumbi wa kituo cha mafunzo Barking,London ya mashariki.
Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye akijibu  maswali mbalimbali kutoka kwa mwandishi maarufu nchini Uingereza Ayoub Mzee mara baada ya kumaliza kutoa semina kwa viongozi wa mashina ya CCM nchini Uingereza.

BENKI YA EXIM YASHIRIKI MAONYESHO KATIKA SIKU YA WAHANDISI 2014

$
0
0
 Meneja Biashara Kubwa na Uwekezaji wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Justin Wambali (kulia) akimpatia kipeperushi chenye maelezo ya huduma zitolewazo na benki ya Exim mmoja kati ya wahandisi alipotembelea banda la benki hiyo wakati wa Siku ya Wahandisi inayoadhimishwa kila mwaka iliyoambatana na maonyesho ya biashara yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Meneja Msaidizi Biashara Kubwa na Uwekezaji wa Benki hiyo, Bw. Joseph Lema na Bw. Thobius Samwel (watatu kulia) ambaye pia ni Meneja Msaidizi Biashara Kubwa na Uwekezaji wa benki hiyo.
 Meneja Msaidizi Biashara Kubwa na Uwekezaji wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Joseph Lema (Katikati) akizungumza na baadhi ya wahandisi kuhusu huduma zitolewazo na benki ya Exim walipotembelea banda la benki hiyo wakati wa Siku ya Wahandisi inayoadhimishwa kila mwaka iliyoambatana na maonyesho ya biashara yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja Biashara Kubwa na Uwekezaji wa Benki hiyo, Bw. Justin Wambali na Meneja Msaidizi Biashara Kubwa na Uwekezaji Thobius Samwel (watatu kulia).
 Meneja Msaidizi Biashara Kubwa na Uwekezaji wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Thobius Samwel (watatu kulia) akizungumza na baadhi ya wahandisi kuhusu huduma zitolewazo na benki ya Exim walipotembelea banda la benki hiyo wakati wa Siku ya Wahandisi inayoadhimishwa kila mwaka iliyoambatana na maonyesho ya biashara yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja Biashara Kubwa na Uwekezaji wa Benki hiyo, Bw. Justin Wambali na Meneja Msaidizi Biashara Kubwa na Uwekezaji Joseph Lema (Katikati). 
Meneja Biashara Kubwa na Uwekezaji wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Justin Wambali (kulia) akizungumza na Mhandisi Fedson Tella (kushoto) kuhusu huduma zitolewazo na benki ya Exim alipotembelea banda la benki hiyo wakati wa Siku ya Wahandisi inayoadhimishwa kila mwaka iliyoambatana na maonyesho ya biashara yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Rock City Marathon 2014 kuzinduliwa keshokutwa

$
0
0

UZINDUZI wa msimu wa sita wa mbio za Rock City Marathon 2014
zilizoanza mwaka 2009, zikiwa na lengo la kukuza Utalii wa Ndani
kupitia michezo, unatarajia kufanyika Septemba 10, kwenye Hoteli ya
New Afrika, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa mbio hizo, Bi. Grace
Sanga, alisema kuwa baadhi ya wanariadha, viongozi wa vyama vya
riadha, viongozi wa Baraza la Michezo Tanzania na wadau mbali mbali wa
mchezo wa riadha nchini wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo.

Bi. Grace alisema kuwa pamoja na maandalizi ya mbio za mwaka huu za
Rock City Marathon kuboreshwa zaidi  ukilinganisha na miaka
iliyotangulia, wawakilishi wa wanariadha na viongozi mbali mbali
watapata fursa ya kuzungumzia changamoto zinazokumba mchezo wa riadha
nchini na jinsi ya kukabiliana nazo.

“Tuko tayari kwa mbio za Rock City Marathon 2014, zitakazofanyika
Oktoba 26. Kamati ya Maandalizi imeweka mikakati mizuri ili
kuhakikisha mbio za mwaka huu zinakuwa bora na zenye mafanikio
kulinganisha na misimu iliyopita,” alisema Bi. Grace.
Mratibu huyo alisema kuwa kwa kutokana na uendeshaji wa kuridhisha wa
mbio hizo, wadhamini wengi wamejitokeza kuwezesha kuzifanya mbio hizo
kuwa bora zaidi mwaka huu.

“Baada ya kufanya maandalizi ya Rock City Marathon kwa mafanikio kwa
miaka tano mfululizo na kuweza kupandisha kiwango chake, makampuni na
mashirika mengi yamejitokeza kudhamini mbio za mwaka huu kwa lengo la
kuiboresha zaidi. Miongoni mwa wadhamini wetu mwaka huu ni pamoja na
NSSF, TSN Group, African Barrik Gold, IPTL, TTB, TANAPA, New Mwanza
Hotel, Nyanza Bottling Company, Sahara Communications, New African
Hotel, Continental decoders, ATCL, PPF, Umoja Switch, and Bank M,”
alisema Bi. Grace.

Rock City Marathon zinaandaliwa na Kampuni ya Capital Plus
International (CPI), kwa ushirikiano na Chama cha Riadha Tanzania
(RT), pamoja na Chama cha Riadha mkoa wa Mwanza (MRAA), ambazo
zimewavutia washiriki wengi wa ndani na nje ya nchi.

Bi. Grace aliongeza kwamba, mbio hizo zitakuwa na vipengele vitano kwa
msimu huu, ambavyo ni mbio za kilometa 21 (wanawake na wanaume) na
zile za kilometa tano kwa wakimbiaji kutoka makampuni mbalimbali,
kilometa tatu kwa watu wenye ulemavu, kilometa tatu kwa watu wazima
(zaidi ya miaka 55) na kilometa mbili kwa watoto walio kati ya miaka 7
mpaka 10.

“Tunatarajia watu wengi kujitokeza mwaka huu, kwa kuwa tumejipanga
vizuri kwa msimu huu. Tumejifunza kupitia mbio za mwaka jana, hivyo
Kamati ya Maandalizi imekuja na mpango madhubuti utakaoboresha mbio
zetu kwa mwaka huu,” alisema Bi. Grace.

SEMINA YA FURSA YAWAONESHA DIRA WAKAZI WA SHINYANGA

$
0
0
 
 SEMINA ya Kamata Fursa Jitathimini,Jiamini,Jiongeze inayoendeshwa sambamba na burudani za Serengeti Fiesta 2014, leo imeendelea kwa kuwapatia dira ya maisha na namna ya kuwafanya wajikwamue kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi wakazi wa Mkoa wa Shinyanga mjini ndani ya Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Uhuru iliyopo mjini humo.
Semina hiyo ambayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ilikuwa ya aina yake, kwani baadhi ya vitu na mbinu alizowapatia wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wengi wao wameonesha hali ya kuelewa baadhi ya mafunzo na mbinu hizo na kuaahidi kuzifanyia kazi ipaswavyo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
 Msanii wa Bongo Fleva, Lammeck Ditto, pia alipata fursa ya kusimulia baadhi ya maisha aliyopitia na kuwataka wakazi wa Shinyanga waendelee kujitathimini na kujiamini kwa kila hatua wanayoipiga katika kujikwamua kwenye maisha yao ya kila siku.
 Baadhi ya Wahudhuriaji wakiwa kwenye semina hiyo ya fursa.
Mtangazai wa Clouds FM, Shafi Dauda hakuwa nyuma kuzungumza na wanamichezo wa Shinyanga na kuwaonyesha fursa zinazopatikana kupitia michezo.
 Meneja wa Maxcom Africa, ‘Max malipo’,  Bernard Munubi  ambaye aliwapatia mbinu za mafanikio na namna ya kujikwamua kiuchumi kupitia mashine za Max Malipo ambazo kwa kiasi kikubwa sasa zimeweza kuwapatia ajira wakazi wengi nchini.
Naye mzungumzaji kutoka  kampuni ya GSI Tanzania,Afisa Mwanadamizi wa kampuni hiyo Tanzania,Pius Mikongoti akizungumza kwenye semina hiyo ya fursa ikiwemo na kuwapa mbinu za kujikwamua kupitia kampuni hiyo.

FUJO KATIKA SHOW YA DIAMOND NCHINI UJERUMANI YADAIWA KUSABABISHA HASARA YA EURO 300,000,YADAIWA PROMOTA HAKUWA NA BIMA.

$
0
0
PROMOTER BRITTS EVENT MATATANI MJINI STUTTGART,UJERUMANI
Polisi wamesema mpaka kieleweke, M-Nigeria Roho Juu

Stuttgart,Ujerumani,
Anayejiita promota Biritts Event - inayomilikiwa na Awin Williams Akpomiemie raia wa Nigeria amejikuta katika mashaka baada ya ripoti ya polisi kuthibitsha jumla ya hasara ya Euro 300,000(Tsh.600 Million) zilizo sababishwa na fujo ya siku ya jumamosi 30 Augost 2014 baada ya msanii wa NASIB ABDUL AKA DIAMOND PLATINUMZ kuchelewa kufika ukumbini mjini Stuttgart,ujerumani.
 
Baada ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo imegundulika kuwa muandaaji wa onyesho hilo Mr.Awin Williams Akpomiemie aliudanganya utawala wa ukumbi wa
Sindfingen kwa kukodisha ukumbi huo kwa ajili ya african paty na mkutano sio onyesho la muziki kama alivyofanya,na kusababisha fujo zilizotia hasara ya euro 300,000 ( T-shilingi millioni 600=) ambazo inatakiwa alipe,kwa promota huyo.
 
Awin Williams Akpomiemie hakuwa na bima ya ku-cover au kulinda onyesho hilo na ukumbi lilipofanyika ambapo ni ukumbi wa mikutano na maonyesho ya bidhaa siyo muziki.

taarifa za uhakika polisi imelipeleka swala hilo kwa ofisi ya sheria (Stadt Anwalt)
ya mji wa Stuttgart ili ichukue mkondo wa sheria ambao unamweka roho juu
bwana Awin Williams Akpomiemie - BRITTS EVENTS, Polisi inaendelea 
kumuhoji kwa kujihusika na biashara zingine haramu. 
Wakati huo huo tahasisi mbali mbali na jumuiya za wafrika nchini ujerumani na jirani zimelaani vikali tabia za raia huyo wa nigeria Awin Williams Akpomiemieza kuwadanganya washabiki na kulivunjia hadhi na sifa bara la Afrika nchini ujerumani ,tahasisi na jumuiya hizo zimewaonya watu kujiepusha kabisa na
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images