Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

AMERICAN SENATORS VISIT SERENGETI NATIONAL PARK

$
0
0
 Director General of TANAPA Mr. Allan Kijazi (right) welcomes the Chairperson of the US Senate Committee on Agriculture, Nutrition and Forestry and Michigan Senator Ms. Debbie Stabenow during the arrival of the US Senators delegation at Serengeti National Park.
 Chief Park Warden for Serengeti National Park Mr. William Mwakilema (right) was also there to welcome the US Senators at Serengeti National Park. 
 US Senators heading to the vehicles ready for their game drive at Serengeti National Park.
 Supporting staff of the US Senates delegation busy taking pictures.
Lions in a relaxing positions enjoying the fiesta at Serengeti National Park.
 Zebras were also there to give US Senators maximum satisfaction of the beauty of Serengeti.
This giraffe could not afford to miss out this important visit by US Senators.

Five American Senators have started a two days visit in Serengeti National Park as part of the official program in the country.

The delegation led by the Senator of Michigan Ms. Debbie Stabenow who is also the Chairperson of the US Senate Committee on Agriculture, Nutrition and Forestry will have an opportunity to witness firsthand the vital role of conservation and good natural resources management in promoting sustainable economic development.

The US Senate delegation will also specifically demonstrate the challenges of combating the Wildlife Trafficking Crisis and methods for mitigation at the local, regional, national and the international level.

While in Serengeti, the delegation will visit sites of local conservation projects, view elephants and rhinos in their natural habitats, meet with leaders on the front lines in the war on poaching, and visit community projects that are working to preserve their natural resources, including threatened species. 

They will also learn about human-wildlife conflict and other issues of importance to local people.

Other Senators in the delegation includes Ms. Cantwell (Washington); Ms. Amy Klobuchar (Minnesota); Ms. Heidi Heitkamp (North Dakota) and Ms. Maize Hirono (Hawaii).


Umoja wa Azaki za Vijana wakutana na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongea na Umoja Azaki za Vijana wakati alipofanya mkutano nao wakati wakiwasilisha mapendekezo ya maboresho ikiwa ni msisitizo katika masuala yao ya vijana, mkutano uliofanyika 02 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.

Kiongozi wa msafara wa Umoja wa Umoja wa Azaki za Vijana Alfred Kiwuyo akisoma taarifa ya mapendekezo ya maboresho ikiwa ni msisitizo katika masuala yao ya vijana, mkutano uliofanyika 02 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Paul Makonda akisisitiza juu ya Katiba kuweka kipengele cha kuwezesha kuundwa kwa Baraza Huru la Vijana la Taifa wakati Umoja wa Azaki za Vijana wakiwasilisha mapendekezo ya maboresho ikiwa ni msisitizo katika masuala yao ya vijana, mkutano uliofanyika 02 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
 Baadhi ya Vijana wanaounda Umoja wa Azaki za Vijana wakisikiliza kwa makini maneno mazuri toka kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba (hayupo pichani) wakati walipokuwa wakiwasilisha mapendekezo ya maboresho ikiwa ni msisitizo katika masuala yao ya vijana, mkutano uliofanyika 02 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.



 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa kazini kufuatilia mambo yakiyoendelea katika mkutano huo wa Umoja wa Azaki za Vijana uliofanyika 02 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.

Kiongozi wa msafara wa Umoja wa Umoja wa Azaki za Vijana Alfred Kiwuyo (kulia) akikabidhi taarifa kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta wakati wakiwasilisha mapendekezo ya maboresho ikiwa ni msisitizo katika masuala yao ya vijana, mkutano uliofanyika 02 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma. (Picha zote na Benedict Liwenga, Malezo-Dodoma)

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA AMANI NA USALAMA WA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA JIJNI NAIROBI

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiteta jambo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairobi katika mkutano wa  Baraza la Amani na Usalama la nchi za umoja wa Afrika (AU) kwenye mkutano wa kuzungumzia masuala ya tishio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla
Nyimbo za AU na Kenya zikipigwa kabla ya  mkutano wa kuzungumzia masuala ya tishio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla  katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairob.PICHA NA IKULU.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairobi leo kujiunga na viongozi wengine wanaounda Baraza la Amani na Usalama la nchi za umoja wa Afrika (AU) kwenye mkutano wa kuzungumzia masuala ya tioshio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla.
  Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairobi katika mkutano wa  Baraza la Amani na Usalama la nchi za umoja wa Afrika (AU) kuzungumzia masuala ya tioshio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Exim ashiriki Fistula Ice Bucket Challenge

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Exim Tanzania, Bw. Yogesh Manek akishiriki zoezi la Ice Bucket Challenge kuunga mkono kampeni dhidi ya ugonjwa wa fistula nchini Tanzania, baada ya kuteuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw, Sunil Colaso. Tukio hilo lilifanyika katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Exim Tanzania, Bw. Yogesh Manek akizungumza na waandishi kabla kushiriki zoezi la Ice Bucket Challenge kuunga mkono kampeni dhidi ya ugonjwa wa fistula nchini Tanzania, baada ya kuteuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw, Sunil Colaso. Tukio hilo lilifanyika katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 
========  ====== =========

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Exim Tanzania, Bw. Yogesh Manek ameshiriki katika Ice Bucket Challenge, kuunga mkono kampeni dhidi ya ugonjwa wa fistula nchini Tanzania, baada ya kuteuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw, Sunil Colaso.

Kabla ya kumwagiwa maji yenye barafu Bw. Manek aliwateua, Ali Mafuruki Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Infotech Investment Group, Shabir Abji, Mwenyekiti wa Hotel ya New Africa na Veena Jog, Mkurugenzi Mtendaji wa Advent Constructions Ltd kushiriki katika zoezi hilo ikiwa ni jitihada za kuwaokoa wanawake wakitanzania wenye tatizo la ugonjwa huo wa fistula.

Akizungumza kabla ya kushiriki, Jumapili, Bw. Yogesh Manek alisema amehamasika kukubali shindano hilo kutokana na idadi kubwa ya maisha inayopotea na ulemavu unaosababishwa na ugonjwa huo: pamoja na zoezi hilo kunakshiwa na mpango wa utunzanji mazingira wa benki hiyo ujulikanao kama ‘Exim Go Green’ Maji kwa matumizi mazuri.

“Namshukuru Bw. Sunil Colaso, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, kwa kunichagua kufanya zoezi hili ambalo nimelipokea kwa heshima kubwa sababu nafahamu urishiriki wangu utaukoa maisha ya walio wengi na kusaidia Tanzania kuwa huru dhidi ya fistula. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo zaidi ya wanawake 8000 ufariki kutokana na fistula, 160,000 upata ulemavu na zaidi ya watoto 40,000 wa chini ya mwaka mmoja ufariki kutokana na ugonjwa huu unaotibika,” alisema.

Alibainisha kuwa Benki ya Exim, imekuwa ni katika mstari wa mbele kuunga mkono shughuli mbali mbali zenye manufaa kwa wanawake, ndiyo maana kampeni ya fistula imekuja kwa wakati muafaka.

“Benki ya Exim imekuwa ikiunga mkono miradi mbali mbali ya kimaendeleo ya kijamii, hususani katika sekta za afya, mazingira na elimu.

“Hii imethibitishwa na baadhi ya shughuli za kijamii tulizofanya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuchangia magodoro katika hospitali ya Mwananyamala, kuijengea shule ya msingi Kilakala vyoo na kushiriki kikamirifu katika shughuli za usafi wa mazingira nchi nzima, ili kuwa na mazingira safi. 

“Na leo hii, ninashiriki katika Ice Bucket Challenge kuonyesha jitihada zetu kama benki katika kuendelea kuunga mkono shughuli hizo,” alisema Bw. Manek. Alisema kuwa wafanyakazi wote wa Benki ya Exim wameunga mkono zoezi hili la Ice Bucket Challenge ambalo limeanzishwa kwa lengo zuri.
“Tunafuraha kubwa na kiwango cha huruma, ukarimu na hisia zilizoonyeshwa na wafanyakazi wote, wao pia wakishiriki katika zoezi hili muhimu kikamirifu," alisema Bw Manek.
Bw. Manek alibainisha pia, zoezi hilo pia limelenga katika kukuza ushiriki wa wafanyakazi na watu wengine katika shughuli za kijamii ambazo benki imekuwa ikianzisha mara kwa mara ikiwa na lengo la kusaidia kukuza sekta mbali mbali za kiuchumi na kijamii nchini.

Benki ya Exim ni moja kati ya benki kubwa nchini kwa upande wa mali zake za jumla, na kuwa na matawi 32 nchi nzima ikisambaa katika uchumi wa nchi tatu Afrika. 

FILAMU YA ‘MATESO YA UGHAIBUNI’ KUZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif, (Wa pili toka Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea uzinduzi wa Filamu ya Mateso Ughaibuni inayotarajiwa kuzinduliwa siku ya Alhamis Septemba 4, 2014 katika viwanja vya Leadrs Club. Pembeni yake ni Rais Wa Bongo Movie Steve Nyerere na wasanii wengine.

Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
FILAMU ya ‘Mateso Ughaibuni’ ambayo imerekodiwa Uingereza na wasanii Issa Musa ‘Cloud 112’, Riyama Ally, Wastara Juma na Monalisa itazinduliwa Alhamisi hii katika viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif, ambaye kampuni yake ndiyo iliwapeleka wasanii hao Uingereza kwenda kurekodi filamu hiyo, alisema licha ya kampuni yake kujihusisha na mambo ya mavazi na vitu vingine ameona kuna kila sababu ya kuwasaidia Watanzania wanaofanya sanaa ya uigizaji.
Rais wa Bongo Movie Steve Nyerere akiongea machache mbele ya waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa Filamu ya Mateso Ughaibuni. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif na Flora Mvungi.

Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini.
Wafanyakazi wa PSPF nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

HIFADHI YA TAIFA YA KITULO MAKETE YAZIDI KUJIIMARISHA ZAIDI

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akiangalia maporomoko ya maji yaliyopo kwenye hifadhi ya Taifa ya Kitulo.
=======
Hifadhi ya Taifa ya Kitulo iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe imejipanga vilivyo kuongeza vivutio vipya vya utalii hifadhini humo pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara na njia za kupita watalii ili wafurahie vivutio vilivyopo hifadhini humo. 
Akizungumza mbele ya kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Makete iliyofanya ziara hifadhini humo, Kaimu mkuu wa hifadhi ya Kitulo Bw.Pius Mzimbe (pichani juu) amesema kwa hivi sasa wanazidi kuboresha zaidi hifadhi hiyo ambapo kwa mwaka huu wa fedha 2014/2015 wataboresha barabara zilizopo kwenye hifadhi hiyo ili kusaidia kufikika kirahisi kwa vivutio lukuki vinavyopatikana kwenye hifadhi hiyo hasa kwenye maporomoko ya maji pamoja na kujionea mimea ya aina mbalimbali iliyoota kwenye hifadhi hiyo.
 "Kwa mfano kwa sasa tunajenga camp site (vituo vya kupumzikia watalii) ambapo watalii wakiwa hapa watajionea mandhari mabalimbali ikiwemo milima, mimea na vingine, watapanda kwenye milima na kuona maeneo ya mbali na wakichoka watarudi hapa kupumzika na tutawawekea bafu na maliwato kwa ajili yao pamoja na jiko kwa ajili ya kuwapikia vyakula wanavyovipenda hasa vya asili" alisema Mzimbe. 
Amesema kumekuwa na changamoto ya kutofikia baadhi ya vivutio hasa maporomoko ya maji kutokana na ubovu wa barabara wakati wa masika hivyo kwa kuziboresha kutasaidia barabara hizo kupitika muda wote hivyo kuongeza mapato yatokanayo na hifadhi hiyo ya Kitulo. 
Bw. Mzimbe ametoa wito kwa wananchi wa ndani na nje ya Makete kujijengea utaratibu wa kutembelea hifadhi hiyo ili wajionee vivutio mbalimbali ikiwemo maua, ndege, maporomoko ya maji na mimea mbalimbali ambayo ipo hifadhini humo tu na vivutio vingine ambavyo wanavigundua siku hadi siku. 
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Makete ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya Mh. Josephine Matiro amesema wilaya yake imebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali vya kitalii ambavyo vipo ndani ya hifadhi ya Kitulo na vingine vipo nje hivyo wao kama serikali watahakikisha vivutio hivyo vinaendelea kuwepo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadaye. 
 Mh. Matiro amesema ni vyema wanamakete wakajitokeza kwa wingi kufanya utalii wa ndani na kujionea jinsi wilaya yao ilivyobarikiwa na ni jambo la aibu kwa watalii wa nje ya nchi kuja kutembelea hifadhi ya Kitulo ilihali wakazi wa makete hawajawahi kuitembelea. 
 "Kwa mfano leo tumejionea vivutio vingi humu hifadhini, lakini ukipita kwa gari unaishia kuona maua ama ndege lakini ukiingia humu ndani vipo vivutio vingi vya ajabu na vya kuvutia, mimi na kamati ya ulinzi na usalama tumeamua kuonesha mfano, tunaomba wananchi mtuunge mkono kwa kuja kuitembelea hifadhi yetu ya kitulo" alisema Matiro. 
 Wakiwa hifadhini humo wajumbe wametembelea maporomoko ya maji ya Mwakipembo na Numbwe ambayo ni marefu zaidi, pamoja na eneo ambalo linajengwa vituo vya kupumzikia watalii na pia kujione mandhari tulivu ya hifadhi hiyo ya Kitulo. 
 Hifadhi ya Kitulo ipo katika tarafa ya matamba wilayani Makete na inasifika duniani kwa kuwa na maua na ndege na kwa hivi sasa vivutio vingine vya utalii vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku. 

YOUNG AFRICANS NA BENKI YA CRDB WAINGIA MAKUBALIANO YA UTENGENEZAJI WA KADI ZA KISASA ZA UANACHAMA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kulia) akisaini mkataba na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Yanga, Fatma Karume kwa ajili ya kutengeneza kadi za kisasa za uanachama wa klabu hiyo za mfumo wa kieletroniki 'Gold Premium Card'. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Yanga, Mama Fatma Karume akipitia mkataba walioingia na Benki ya CRDB. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akionyesha kadi ya kisasa ya uanachama wa Yanga ikiwa katika mfumo wa kieletroniki kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo, mama Fatma Karume.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga,  Fatma Karume kadi namba moja ya mfumo wa kieletroniki 'Gold Premium Card' mara baada ya benki hiyo kuingia mkataba wa kutengeneza kadi hizo. Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga,  Fatma Karume akizungumza katika hafla hiyo. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay. (katikati)
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei  akizungumza wakati wa hafla hiyo.


NA CLEZENCIA TRYPHONE

BENKI ya CRDB imeingia mkataba na klabu ya Yanga kwa ajili kutengeneza kadi za kisasa za uanachama wa klabu hiyo, ambazo pia watazitumia kuingilia viwanjani katika mechi mbalimbali za mfumo wa tiketi za kieletroniki.

Yanga imefikia hatua hiyo, kwa lengo la kuitafutia klabu vyanzo vya mapato kwa ajili ya kujiendesha, ili iweze kufikia hatua nzuri zaidi kama ilivyo kwa timu kubwa kama TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na nyinginezo.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo, Mkurugenzi wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei, alisema kuwa mkataba huo ni wa kudumu, ila utaweza kuvunjwa endapo mambo yakienda tofauti na makubaliano.

Kimei aliyasema hayo, katika zoezi hilo lilishuhudiwa na Fatma Karume ambaye ni Mwenyekiti katika Bodi ya wadhamini wa Yanga aliyeweka sahihi katika mkataba huo, pamoja na Francis Kifukwe na Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga.

Akizungumza kwa niaba ya Yanga, Fatma alisema, wao kama timu kongwe hapa nchini, imefarijika kuona benki kubwa kama hiyo ikiwapa sapoti kubwa, ambapo yeye amepewa kadi namba moja.

“Tunafarijika sana, sisi kama Yanga kupata udhamini huu mnono, na Yanga ni taasisi kubwa na ndio maana hata bendera za Taifa zinafanana na rangi ya klabu yetu, sio hao Simba damu tu,”alisema.

Wamiliki, Waombaji leseni za madini watakiwa kufuata Taratibu

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisaini moja ya leseni za uchimbaji madini kwa wamiliki waliokidhi vigezo vya kuapatiwa leseni. Anayeangalia ni Mwanasheria Wizara ya Nishati na MadinI Phines Sijaona.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza mmoja wa waombaji wa Leseni za uchimbaji madini, Mark Stanely mmiliki wa kampuni ya Bafex Tanzania Limited (Kanda ya Kusini Magharibi) wakati wa kikao cha kusaini leseni za uchimbaji madini zilizokidhi vigezo
Kamishna Msaidizi anayeshuhgulia Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi John Nayopa, akifafanua jambo wa wamiliki wa kampuni ya Gemini Exploration & Mining Service Limited mara baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo kumaliza kusaini leseni hizo.


Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewataka wamiliki na waombaji wa leseni  za kuchimba madini kuhakikisha wanayaendeleza maeneo yao kwa kufanya kazi katika muda walioomba kulingana na leseni hizo la sivyo  watafutiwa leseni zao kwa mujibu wa sheria ya madini.


Waziri Muhongo ameyasema hayo wakati akisaini leseni za Kampuni mbalimbali zilizokidhi vigezo vya kupatiwa leseni za uchimbaji madini katika maeneo mbalimbali nchini na kuongeza kuwa, kuanzia sasa Wizara haitaruhusu wamiliki wa leseni za madini kuuza maeneo yao kwa wamiliki wengine na kubadilisha majina ya kampuni kutoka kwa mmiliki mmoja kwenda mwingine badala yake itaruhusu endapo pande mbili zitaingia ubia.


“Hatutakubali wamiliki wa leseni kuuza maeneo yao na kubadili jina kutoka kwa mmliki mmoja kwenda mwingine badala ya kuyaendeleza, lakini kama wanaingia ubia hilo linakubalika” alisisitiza Muhongo.


Kauli ya Waziri imekuja baada ya kubaini kuwa, baadhi ya wamiliki wa leseni za uchimbaji madini kutokuyaendeleza maeneo yao kwa muda mrefu pindi wanapopewa leseni na badala yake kuyauza na kubadili majina ya kampuni jambo ambalo linachochea migogoro katika maeneo husika.


“Wananchi wanategemea mara baada ya kampuni kupewa leseni waombaji waendeleze maeneo yao lakini badala yake maeneo yanakaa bila kuendelezwa jambo ambalo linaibua migogoro”, aliongeza Muhongo.


Aidha, ameongeza kuwa, hatua hiyo inalenga kuwafanya waombaji na wamiliki kuwajibika na kufanya kazi kisasa badala ya kufanya kwa mazoea. “Hatutaki waombaji wafanye kazi kizamani, hatutaki kupotezeana muda katika hili”, alisisitiza Waziri.


Kampuni zilizopata leseni za uchimbaji, ni pamoja na Bafex Tanzania Limited (Kanda ya Kusini Magharibi) Autrad Mining Company Limited, Nyang’wale Diamonds Limited (Kanda ya Kati Magharibi) na Paulo Sungura na Joyce Abinel Sekwao (Kanda ya Magharibi).

MABOSS WA AIRTEL TANZANIA WAENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA FISTULA

$
0
0
Wakuu wa makampuni tofauti pamoja na wakurugenzi wa vitengo mbali mbali vya kampuni ya Airtel Tanzania wameendelea kuonyesha kuguswa kwa kushiriki kutimiza shinikizo toka kwa Mkurugenzi mkuu wa Artel Tanzania alilolitoa wiki moja iliyopita kuhamasisha mapambano dhidi ya Fistula kwa akina mama kwa kuchangisha pesa zitakazotumika kusaidia shughuli mbalimbali wakati wa matibabu kwa wale waliopatwa na tatizo hilo Angalia video hizi kuona kila mmoja alivyofanya mara baada ya kuguswa na kujitoa kuchangia.Adriana Lyamba- Mkurugenzi Huduma kwa wateja Airtel Tanzania. Levi Nyakundi- Mkurugenzi Masoko Airtel Tanzania.

Mahakama Yamfunga Jela Mwizi wa Nyaya za TTCL

$
0
0
Mmoja wa watuhumiwa wa nyaya za simu. Picha hii haina uhusiano na habari hii.  
Mmoja wa watuhumiwa wa nyaya za simu. Picha hii haina uhusiano na habari hii. [/caption] Na Mwandishi Wetu MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam imemuhukumu kwenda jela miaka minne, Shaibu Muhidin Ndina baada ya kupatikana na kosa la kuiba nyaya za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Hukumu hiyo imetolewa Agosti 25, 2014 katika mahakama hiyo na B. Mashabara baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa hilo la wizi wa nyaya(cables) za kampuni ya TTCL zenye thamani ya shilingi milioni 15. 

Awali akisomewa shitaka hilo, Muhidin Ndina anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 11, 2013 maeneo ya Boko Katika Wilaya ya Kinondoni kabla ya kufikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi namba 12/2013. “…Aliiba nyaya (cables) za thamani ya milioni 15…alitenda kosa hilo Januari 11, 2013 Boko Katika eneo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam…” ilisomeka sehemu ya hukumu ya kesi hiyo.

 Uharibifu wa miundombinu ya umma zikiwemo nyaya za simu za Kampuni ya TTCL umekuwa ukishamiri maeneo kadhaa jambo ambalo limekuwa likisababisha hasara kubwa kwa kampuni na usu mbufu kwa wananchi na watumiaji wa huduma za TTCL. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

SHIRIKA LA NYUMBA TANZANIA (NHC) LAKARABATI SHULE YA HASSANGA JIJINI MBEYA

$
0
0
 Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas  Kandoro akikata utepe kuzindua ukarabati wa Madarasa manne na Jengo moja la Utawala katika Shule ya Msingi Hasanga uliofanyika leo Uyole Mbeya.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas  Kandoro, viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa Tanzania (NHC), Viongozi wengine wa Serikali na Walimu wa Shule ya Msingi ya Hasanga wakifurahia Baada ya Kuzindua Rasmi ukarabati wa ujenzi huo.
Meza kuu
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akizungumza na wananchi, wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi ya Hasanga katika Sherehe ya kukabidhi Majengo ya Shule hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Mchechu akizungumza jambo wakati wa Sherehe hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigallah King akimkaribisha Mkuu wa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro.
Meya wa Jiji la Mbeya Atanus Kapunga akitoa neno la Shukurani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Akiwakaribisha Wageni katika Sherehe hizo
Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Mbeya Anthony Komba akisoma Taarifa ya ukarabati wa Shule hiyo
 Mwalimu Neema Sanga (Kushoto) akisoma  Risala ya Shule 
Baadhi ya Wageni waalikwa na Meza Kuu
 Baadhi ya Wanafunzi na Wazazi 
Wanafunzi wakiimba Ngonjera 
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Abbas Kandoro Akiendesha Harambee
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akikagua Baadhi ya Majengo
Muonekano wa Baadhi ya Majengo ya Shule ya Msingi Hasanga yaliyokarabatiwa na Shirika la Nyumba la Taifa 
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua tukio.

CHINI NI VIDEO FUPI YA HARAMBEE ILIYO ONGOZWA NA MKUU WA MKOA

***********
SHIRIKA la Nyumba la Taifa(NHC) limefanya ukarabati wa majengo ya shule ya Msingi Hassanga iliyopo Uyole jijini Mbeya ambayo alisoma Mkurugenzi Mkuu Nehemia Mchechu.

Makabidhiano ya mradi huo umefanyika leo katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuriwa na Mkurugenzi mkuu, viongozi wa Halmashauri ya Jiji, Wilaya na Shirika la Nyumba ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alikuwa mgeni rasmi.

Aidha ukarabati wa majengo manne na jengo moja la utawala uliofanywa na shirika la Nyumba(NHC) umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 31.
Mkurugenzi mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu,katika taarifa yake iliyosomwa na Meneja wa Shirika hilo Mkoa wa Mbeya,Antony Komba, amesema Shirika hilo liliamua kufanya ukarabati wa jengo la utawala na madarasa manne ya shule hiyo kama sehemu ya mchango wake kwa jamii kufuatia maombi yaliyofanywa na Kamati ya shule ya kuombwa ukarabati wa majengo hayo.

Amesema kazi ya ukarabati ilianza Aprili 19 na kukamilika Agosti 20, Mwaka huu ambapo Shirika lilikarabati Jengo la utawala katika ujengaji upya wa kuta za jengo , bimu na uezekaji upya wa paa, upigaji lipu, sakafu na rangi pamoja na kuweka milango na madirisha ya alminium kwa gharama ya shilingi Milioni 22,77,900.

Ameongeza kuwa ukarabati katika madarasa manne ulihusu upigaji upya wa lipu ukutani, utengenezaji wa sakafu , utengenezaji wa shata za madirisha pamoja na upakaji rangi uliogharimu shiringi Milioni 8,803,000 na kufanya jumla ya shilingi Milioni 31, 577,900.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, mbali na kulishukuru shirika hilo kwa msaada wao huo pia ametoa wito kwa Wanafunzi na Walimu pamoja na uongozi wa kamati ya shule kuyatunza majengo hayo ili yaweze kudumu.

Hata hivyo katika hatua Nyingine Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alilazimika kuendesha harambee nyingine baada ya Mkurugenzi wa NHC, Mchechu kujibu risala ya walimu walioomba kukarabatiwa majengo mengine ambapo alisema kama wataweza kuchangia chochote Shirika litaweza kumalizia.
Katika harambee hiyo ambayo pia ilichangiwa na Shirika Mkuu wa Mkoa alifanikiwa kukusanya Shilingi Milioni moja na laki tatu ambazo alizikabidhi kwa Mkurugenzi wa Shirika ambaye baada ya kupokea aliahidi kuanza ujenzi kesho wa majengo mengine manne.

Nao Walimu wa Shule ya Msingi Hassanga katika Risala yao kwa Mgeni rasmi,iliyosomwa na Mwalimu Neema Sanga, wamelipongeza shirika la Nyumba kwa kukarabati majengo hayo.
Wamesema ukarabati wa Vyumba vine vya madarasa, ofisi ya Walimu pamoja na Ofisi ya Mwalimu Mkuu ni moja ya kutambua umuhimu wa Elimu na kujenga mazingira rafiki ya kufundisha na kujifunzia.

RITA NA NBS WAENDESHA MAFUNZO YATAKAYOWEZESHA KUFANYA TATHMINI YA KINA YA MATUKIO MUHIMU YA MWANADAMU.

$
0
0
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Eliya Ntandu akifungua mafunzo ya siku sita ya maofisa watakaoshiriki katika Tathmini ya kina ya Matukio Muhimu ya Mwanadamu. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa NBS, Bi Aldegunda Komba, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk. Albina Chuwa, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi Emmy Hudson na Kamishna wa Sensa, Hajjat Amina Mrisho Said.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi. Emmy Hudson akitoa maelezo kuhusu ushiriki wa RITA katika tathmini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu ushiriki wa NBS katika tathmini.
Picha ya Mgeni Rasmi na washirki wa Mafunzo.



Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wanaendesha mafunzo ya siku sita kwa maofisa watakaoshirki kufanya tathmini ya kina ya Usajili na Takwimu za matukio muhimu ya mwanadamu ambayo ni Vizazi, Vifo, Ndoa na talaka. Mafunzo hayo yamefunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Eliya Ntandu Jana Jumanne tarehe 2 Septemba 2014 na yanafanyika katika ukumbi wa 88 Motel, Mkoani Morogoro.

Mafunzo hayo yanawashirikisha maofisa kutoka taasisi mbali mbali zinazohusika na masuala ya usajili wa wananchi ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya kuwapa uwezo wa kufanya tathmini ya kina ya mifumo na sheria zilizopo zinazohusika na usajili wa matukio muhimu ya mwanadamu ambayo ni Vizazi, vifo, Ndoa na Talaka .

 Tathmini inategemewa kufanyika tarehe 15 -30 Septemba 2014 katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini na maofisa waliopewa mafunzo wataweza kukusanya taarifa katika vituo vya tiba, vituo vya polisi, ofisi za wasajili wa wilaya, ofisi za kata, nyumba za ibada na katika makazi ya wananchi.

 Matokeo ya Tathmini yanategemewa kutoa mwelekeo katika mchakato wa kuweka vipaumbele na mipango ya utekelezaji wa mfumo thabiti wa usajili wa raia na utoaji wa takwimu za matukio muhimu, mfumo utakaokuwa kiungo muhimu katika utekelezaji wa utawala bora na pia chanzo cha msingi cha takwimu za matukio kama vizazi, ndoa, talaka na vifo na sababu zake.

RITA NA NBS wanafanya tathimini hii ikiwa ni utekelezaji wa moja ya maazimio ya  Mkutano Mawaziri wanaohusika na masuala ya usajili wa raia wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Mwaka 2012 katika Jiji la Duban, Afrika ya Kusini. Kwa mujibu wa azimio hilo kila nchi mwanachama inatakiwa kufanya tathmini hii na kuwasilisha matokeo yake katika kikao kama hicho kinachotegemewa kufanyika  mwanzoni mwa mwaka ujao.

Mkongo wa Taifa wasaidia kushuka kwa gharama za mawasiliano nchini

$
0
0

Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bi. Prisca Ulomi akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya mkongo wa Taifa ikiwamo kusaidia kushuka kwa gharama za Mawasiliano nchini. Kushoto ni Mkurugenzi huduma za mtandao wa TTCL Mhandisi Joram Lujara.
Mratibu wa Ufundi kutoka Ofisi ya Mkongo wa Taifa Mhandishi Anifa Chingumbe akiwaonesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) maeneo ambayo mkongo wa Taifa umepita, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 

(Picha na Hassan Silayo)

Frank Mvungi
Serikali imesema Mkongo wa Taifa umesaidia kushuka kwa gharama za  mawasiliano kwa watumiaji wa mwisho nchini kutoka sh.147 kwa dakika mwaka 2009 hadi shilingi 62 kwa dakika mwaka 2013.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mawsiliano Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Bi Prisca amesema kuwa mkongo wa taifa umesaidia pia kushuka kwa gharama za intaneti kutoka shilingi 36,000 hadi shilingi 9000/Gb kufikia mwaka 2013.
“Mkongo wa Taifa umesesaidia kuharakisha usambazaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara”alisisitiza bi Ulomi.
Katika hatua nyingine, Bi Ulomi alisema faida nyingine ya Mkongo ni kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uwezo wa kusafirisha masafa.
Akieleza kuhusu gharama Bi Prisca amesema gharama za maunganisho ya mawasiliano ya simu za mkononi kutoka  kampuni moja kwenda nyingine  (interconnection fees) ambapo sasa gharama imepungua kutoka sh. 115 hadi shilingi 34.92 kwa dakika.
Mkongo wa Taifa umesaidia kuongeza ushirikiano wa kikanda  kati ya nchi za Afrika Mashariki na kati ambapo nchi za Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, Uganda, na Kenya ambapo hali hiyo imeongeza fursa za kibiashara na kukuza uchumi wa nchi.

Kufikia mwaka 2013 makampuni yafuatayo yalikuwa yameunganishwa na mkongo wa Taifa ni TTCL, TIGO, Zantel,  Airtel, Vodacom, Simbanet na infinity.

JESHI LA POLISI LATOA ONYO KALI KWA WANAOTUMIAJI VIBAYA MITANDAO

$
0
0
MSEMAJI wa Jeshi la Polisi, Advera Senso akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Septemba 3,2014 kuhusu kupiga marufuku watu wanaotumia mitandao kinyume na taratibu.HABARI/PICHA NA PHILEMON SOLOMON

======== ======  ======
JESHI la Polisi nchini limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kutuma ujumbe wa matusi, uchochezi, picha za utupu sanjari na kukashifu viongozi wa Serikali, dini na watu mashuhuri.

Akizungumza Dar es Salaam, Septemba 3,2014  Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema kuwa tayari baadhi ya watu wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo na wengine wanaendelea kuhojiwa.

"Kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii na simu za kiganjani kinyume na malengo yaliyokusudiwa kwa kusambaza taarifa za uchochezi, kashfa,kuchafua viongozi wa Serikali.

"Wengine wamekuwa wanasambaza picha utupu ambazo hazina maadili, hali ambayo ni kosa la jina, ingawaje mwingine anaweza hasijue kuwa kufanya hivyo ni kosa lakini sheria haitamuacha, alisema.

Senso aliendelea kubainisha kuwa kuvunja kutofahamu sheria kwa kutoifahamu si sehemu ya kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria, atakabainika kutenda kosa hilo bila kujali anaifahamu sheria au la, atachukuliwa adhabu kali.

Alisema oparesheni ya kuwabaini wanaosambaza ujumbe zinaendelea nchi nzima kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakamata waharifu wa aina hiyo.

Aliongeza kuwa hatua hiyo pia inawatia hatiani wale wote wanaotumia mitandao kufanya utapeli na kujipatia kipato kwa watu mbalimbali nchini sanjari na blogs zinazosambaza picha chafu ambazo ni kinyume na maadili.

"Wapo baadhi ya watu wanatumia mitandao ya simu kutapeli watu na kujipatia kipato, hivyo nao ni sehemu ya waharifu wanaotafutwa na jeshi la polisi na yeyote atayekamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yake," alisema.

Hivyo alisisitiza kuwa Jeshi hilo linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uharifu huo, na kuwataka wale wanaotumiwa wa aina hiyo kutousambaza kwa wengine bali waufute.

Pia aliziomba kampuni za simu za mkononi pindi wanapoona ujumbe wa aina hiyo wasiruhusu uende kwa mwingine ili nao wawe sehemu ya kupambana na uovu huo.

Microsoft Windows Phone 8.1yatambulishwa Tanzania kupitia Lumia 930, Lumia 630 and Lumia 530

$
0
0
 Meneja uzalishaji wa kampuni ya Nokia Afrika Mashariki, Kingori Gitahi akiwaonesha waandishi wa habari moja kati ya simu tatu zilizozinduliwa.

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Nokia Afrika Mashariki, Bi.Lilian Nganda akizungumza na waandishi wa habari Septemba 3,2014 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya Nokia aina ya Lumia 530, 630 na 930.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia tukio la uzinduzi wa simu hizo.
 Kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishuhudia uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.
Miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishuhudia uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.HABARI / PICHA NA PHILEMON SOLOMONI

WAFANYABIASHARA na watumiaji wengine wa simu za kiganjani wamepata matumaini mapya baada ya simu nyingine tatu aina ya Nokia Lumia 530, 630 na 930 kuzinduliwa.

Kwa mujibu wa Meneja uzalishaji wa kampuni ya Nokia Afrika Mashariki, Kingori Gitahi akizungumza Dar es Salaam, Septemba 3, 2014  wakati wa kuzindua simu hizo alisema zinauwezo mkubwa kwa matumizi ya mtandao.

"Naamini kwa wafanyuabiashara na watumiaji wa kawaida watakuwa wamepata fursa nzuri ya kutumia na kupkea email kwa urahisi sanjari na kuchukua picha za video na zilizomo katika mitandao kwa wepesi,"alisema.

Pia aliongeza katika kuhakikisha wanatoa huduma nzuri za uhakika wameshirikiana na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Vodacom na Airtel ambao hutoa vifurushi mitandao kwa wateja watakaonunua simu hizo.

Gitahi aliongeza kuwa simu hizo zinauwezo wa kupiga picha kwa haraka zaidi na kurekodi matukio mbaliombali kwa ustadi mkubwa na anaamini watu wengi watakuwa watumiaji wazuri ili kujiweka katika kiwango cha kimataifa.

RAIS Kikwete akutana na Bibi yake Rais Obama wa Marekani,jijini Nairobi leo

$
0
0


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Bibi yake Rais wa Marekani,Mh. Barack Obama,Mama Sarah Obama walipokutana Leo kwenye hoteli ya Villa Rosa Kempiski  jijini Nairobi, Kenya, wakati Rais Kikwete akijiandaa kurejea nchini.Mama Sarah Obama anatarajia kuzindua taasisi ya kusaidia elimu kijijini Kogelo nchini Kenya,alikozaliwa Baba yake na Rais Obama wa Marekani itakayofahamika kama (Sarah Obama foundation) ambapo atajenga shule kuanzia za awali mpaka sekondari. Rais kikwete sasa hivi yuko mjini Kondoa kuendelea na ziara yake ya Mkoa wa Dodoma.PICHA NA IKULU

Wajumbe Kundi la 201 watoa tamko dhidi ya wanaolichafua Bunge Maalum la Katiba na Wajumbe wa kundi hilo.

$
0
0
 Askofu Amos Muhagachi akitoa tamko juu ya tuhuma mbalimbali dhidi ya kundi la 201 la wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo 03 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa Spika, Mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa kundi la 201 ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Francis Michael akikanusha kuhusu madai ya wajumbe wa kundi hilo kupewa rushwa kuhusu mchakato wa Katiba Mpya.
 Sheikh Hamid Jongo akiviasa vyombo vya habari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya unafanikiwa kwakuwa hata wao (vyombo vya habari) unawahusu pia.
Askofu Donald Mtetemela akichangia mada wakati wa mkutano wa kutoa tamko kuhusiana na tuhuma mbalimbali dhidi ya kundi la 201.
Baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia tamko hilo leo 03 Septemba, 2014 katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Spika Bungeni mjini Dodoma.(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma).

=========  ======== ======
Wajumbe Kundi la 201 watoa tamko dhidi ya wanaolichafua Bunge Maalum la Katiba na Wajumbe wa kundi hilo.
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
03/09/2014.
WAWAKILISHI wa Taasisi za dini wa Bunge Maalum la Katiba toka wajumbe 201 wametoa tamko lao dhidi ya tuhuma mbalimbali zinazoendelea katika kulichafua Bunge hilo ikiwemo baadhi ya wajumbe wa kundi hilo wakituhumiwa kudaiwa kupewa rushwa.
Tamko hilo limetolewa leo 03 Septemba, 2014 na viongozi wa kiroho akiwemo Askofu wa Kikristo Amos Joseph Muhagachi pamoja na Sheikh Hamid Masoud Jongo wakiwa wameongozana na Mwenyekiti wa kundi hilo la 201, Mhe. Dkt. Francis Michael na wajumbe wengine wa kundi hilo, wakati walipofanya mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Spika uliopo Bungeni mjini Dodoma.

Akisoma tamko hilo, Askofu Amos Muhagachi ambaye pia ni Mjumbe wa kundi hilo amesema kuwa kama ilivyoelezwa hapo awali kabla ya kuanza kwa shughuli za Bunge hilo, kila mjumbe alikula kiapo cha kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kadiri ya uwezo wake na ufahamu wake, kufanya kazi zinazomhusu bila upendeleo.

Askofu Muhagachi ameendelea kusema kuwa wameshangazwa na kusikitishwa  kuona kwamba mchakato wa kutayarisha Katiba itakayopendekezwa na Bunge hilo kwa wananchi unachafuliwa taswira yake, Bunge Maalum la Katiba linachafuliwa, shughuli zake kuingiliwa na kupotoshwa na wajumbe wenzao walioko nje ya Bunge hilo, makundi, taasisi na vyombo mbalimbali vya habari, uhalali na ukweli wa shughuli za Bunge hilo unapotoshwa na wananchi wanaaminishwa mambo yasiyo na ukweli.
“Upotoshwaji huu umezua mijadala mbalimbali katika jamii ya Watanzania  bado unaendelezwa”, alisema Muhagachi. Aidha, Muhagachi amezitaja baadhi ya tuhuma zinazotolewa na wajumbe wenzao dhidi ya Bunge hilo na wajumbe wa kundi hilo zikiwemo.

 “Bunge Maalum la Katiba halina uhalali kwa kuwa hao wajumbe wenzetu walioondoka wameliondolea uhalali wake kwa vile hawapo, kwamba Kanuni za Bunge Maalum la Katiba zinavunjwa ovyo ovyo, Kwamba kinachojadiliwa sasa katika Bunge hili ni Waraka mwingine na si Rasimu iliyotayarishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

 Inadaiwa na watu pamoja na Taasisi mbalimbali kwamba viongozi wa dini, wajumbe wa Bunge hilo na wajumbe wa kundi la 201 kwamba wanapewa rushwa baadhi ya Vyombo vya Habari vimeandika tuhuma hizi, pia madai mengine ni kwamba wajumbe waliomo katika Bunge hili ni wachache ikilinganishwa na hao waliopo nje ya Bunge na tuhuma ya nyingine ni ile ya kwamba Bunge hili lazima lisitishwe au livunjwe na Mhe. Rais.

“Tunapenda kuwafahamisha Watanzania wenzetu kwamba mchakato wa Katiba una hatua tatu kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na mpaka hivi sasa ni hatua moja iliyokamilika, aidha hatua ya pili ndiyo inayoendelea na hatua ya tatu bado haijaanza”, alisema Muhagachi.

Akitoa tamko hilo, Askofu Muhagachi amesema kuwa wao kama wawakilishi wa Taasisi za Dini, ambao kuuhubiri, kuutangaza na kuusimamia ukweli ni moja ya majukumu yao katika jamii, hivyo wameskitishwa na taarifa potofu zinazosambazwa kwa makusudi na makundi, taasisi na baadhi ya vyombo vya habari.

“Tukiwa kama wajumbe wa Bunge hili ambao tunafahamu kwa kina na tunaridhika na kila hatua ya mchakato huu, tuna wajibu wa kusahihisha upotofu huu unaoendeshwa kwa makusudi na hivi kuwaeleza Watanzania ukweli na hali halisi inayojiri hapa Bungeni, Watanzania msifadhaishwe na wala msibabaishwe, hali ni shwari, mchakato unaendelea kwa amani na utulivu”, alisisitiza Muhagachi.

Naye Sheikh Hamid Masoud Jongo ameviasa vyombo vya habari kutilia mkazo katika kutoa taarifa zilizosahihi ili mchakato wa Katiba uendelee kwa amani kwani nao ni moja ya kundi la watu inayowahusu.

“Vyombo vya habari vina nguvu ya kuhabarisha umma juu ya mambo mengi yanayoendelea nchini, ni vema tukishirikiana sote kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa tunapata Katiba yetu kwani hata nyie Katiba hii inawahusu hasa katika kudai haki na uhuru wa vyombo vya habari”, alisema Sheikh Jongo.

Aidha, Mwenyekiti wa wajumbe wa Kundi hilo la 201, Mhe. Dkt. Francis Michael ameongezea kwa kukanusha suala la rushwa kwa wajumbe wake huku akisisitiza kuwa wajumbe wake katika kundi hilo ni watu wenye heshima zao hivyo madai hayo hayana ukweli wowote ule.

TIMU YA MAJAJI KWA AJILI YA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI YATEMBELEA MGODI WA NORTH MARA

$
0
0
 Afisa Uhusiano wa Kijiji cha Matongo Bw. Magesa  Wanjara akionesha jinsi ya kutumia bomba la kisima cha maji kilichofadhiliwa na  mgodi wa North Mara mbele ya  timu ya majaji, sekretarieti na wajumbe wengine.
 Meneja Mahusiano wa  Mgodi wa North Mara Bi Fatuma Mssumi (mbele) akielezea shughuli za mgodi wa North Mara mbele ya jopo la majaji waliotembelea mgodi huo ili kuendelea na zoezi lake la  kumtafuta  mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.

 Afisa Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo ( wa tano kutoka kushoto) akielezea mchango wa mgodi wa North Mara katika uwezeshaji wa kikundi cha vijana katika mradi wa kitalu cha mboga za majani, mbele ya majaji na sekretarieti iliyotembelea kitalu hicho. (kinachoonekana kwa nyuma)
 Mwenyekiti wa Umoja wa Kikundi cha Vijana cha Nyakegema Bw. Zacharia Mwita ( wa pili kutoka kulia) akitoa maelezo mbele ya  timu ya majaji  na wajumbe wengine  kuhusu mchango wa mgodi wa North Mara kwa kikundi hicho kupitia mradi wake wa mboga za majani. Kikundi hicho kina jumla ya  vijana 578 kutoka  katika vijiji saba  vinavyouzunguka mgodi huo.

 Afisa Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo (wa tatu kutoka kulia) akitoa maelezo mbele ya majaji, sekretarieti na wajumbe wengine juu  ya mchango wa mgodi wa North Mara katika ujenzi wa shule ya sekondari ya Ingwe ( inayoonekana kwa nyuma)
Mwenyekiti wa Jopo  la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (kushoto) akisalimiana na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ingwe Bw. Alfred Joseph mara timu hiyo ilipofanya ziara kwenye shule hiyo iliyofadhiliwa na  mgodi wa North Mara. 

 Mkuu wa Wilaya  ya Tarime  Mhe. John Henjewele (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jopo  la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe ( wa pili kutoka kulia) mara timu hiyo ilipofika kwenye ofisi yake kabla ya kuanza ziara  yake rasmi kwenye mgodi wa North  Mara.
 Mwenyekiti wa Jopo  la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (kushoto) akisalimiana na  Afisa Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw.  Zakayo Kalebo (kulia) mara baada  ya jopo hilo kuwasili kwenye mgodi huo.
 Afisa Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo (wa tatu kutoka kushoto) akielezea mchango wa mgodi wa North Mara katika ujenzi wa nyumba za  wauguzi wa zahanati ya Matongo (zinazoonekana nyuma)  mbele ya timu ya  majaji  na sekretarieti iliyotembelea mradi wa nyumba hizo. Mradi wa nyumba hizo uligharimu   Dola za Marekani 100,000.

TAARIFA YA WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA TOKA WAJUMBE 201 KUHUSU MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA

$
0
0
 Sisi Wawakilishi wa Jumuiya na Taasisi za Dini, tuliopendekezwa na Taasisi zetu na baadaye kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kushauriana na Rais wa Zanzibar kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na kula kiapo cha utekelezaji wa jukumu hili kubwa.

Tukiamini kuandaa Katiba Mpya kwa maridhiano ya Kitaifa kwa wananchi wote, tulipokea jukumu hili kama wajibu wetu Kitaifa.  Aidha tunaamini kwamba katika kupata maridhiano ya Kitaifa ni muhimu kuheshimu kila wazo na fikra inayotolewa na kuunganisha fikra hizo kwa usahihi, kwa njia ya kidemokrasia kwa kupiga kura na kukubaliana na matokeo ya wengi.

Kama ilivyoelezwa hapo awali, kabla ya kuanza shughuli za Bunge Maalum, kila mjumbe alikula kiapo cha kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kadiri ya uwezo wake na ufahamu wake, kufanya kazi zinazomhusu, bila upendeleo na kumuomba Mwenyezi Mungu amsaidie. 

Tumeshangazwa na kusikitishwa sana kuona kwamba mchakato wa kutayarisha Katiba itakayopendekezwa na Bunge hili kwa wananchi, unachafuliwa taswira yake.  Bunge Maalum la Katiba linachafuliwa na, shughuli zake kuingiliwa na kupotoshwa na wajumbe wenzetu walio nje ya Bunge, Makundi, Taasisi na Vyombo mbali mbali vya habari, uhalali na ukweli wa shughuli za BungeMaalum la Katiba unapotoshwa.  Wananchi wanaaminishwa yasiyo na ukweli.

Upotoshwaji huu umezua mijadala mbali mbali katika jamii ya Watanzania na bado linaendelezwa kama ifuatavyo:

1.   Kwamba Bunge Maalum la Katiba halina uhalali kwa kuwa hao wajumbe wenzetu walioondoka wameliondolea uhalali wake kwa vile hwapo, wakiwepo Bungeni basi uhalalai wake utakuwepo - utapatikana;
2.   Inadaiwa kwamba Kanuni za Bunge Maalum la Katiba zinavunjwa ovyo ovyo;
3.   Inadaiwa pia, kwamba kinachojadiliwa sasa katika Bunge hili ni Waraka mwingine na si Rasimu iliyotayarishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyowasilishwa rasmi Bungeni na kuanza kujadiliwa na wajumbe;
4.   Inadaiwa na watu na Taasisi mbali mbali, kwamba viongozi wa dini, wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na wajumbe wa Kundi la 201, wanapewa rushwa. Isitoshe Vyombo vya habari vimeandika tuhuma kama hizi.
5.   Inadaiwa pia kwamba wajumbe waliomo katika Bunge hili ni wachache, ukilinganisha na hao walioko nje ya Bunge hilo;
6.   Bunge hili, kwa tuhuma hizo, lazima lisitishwe au livunjwe na Mhe. Rais.

Kabla ya kuanza kuusahihisha upotoshwaji huo, sisi Wawakilishi wa Taasisi za Dini mbali mbali na Wajumbe wa Kundi la 201 katika Bunge Maalum la Katiba, tunapenda kufahamisha umma wa Tanzania mchakato wa kutayarisha Katiba Mpya ulivyo kisheria.

Tunapenda kuwafahamisha Watanzania wenzetu kwamba mchakato huu una hatua tatu kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.  Mpaka hivi sasa ni hatua moja imekamilika.  Hatua ya pili ndiyo inayoendelea, na hatua ya tatu bado haijaanza.

Hatua ya kwanza ni ile ya uandaaji wa Rasimu. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 iliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba, chini ya kifungu cha tano cha sheria hiyo.  Tume hii ilipewa jukumu la kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba, kuanisha na kuchambua maoni ya wananchi na kisha kuandaa rasimu ya Katiba.  Kazi hiyo ilifanyika kwa kipindi cha takriban miaka miwili na hatimaye Rasimu ya Katiba ilikamilika.

Hatua ya pili ilikuwa ni kuipeleka Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum la Katiba, ambalo liliundwa kwa shughuli maalum ya kuandika Katiba inayopendekezwa, ili ifikishwe kwa wananchi ambao wataamua waikubali au waikatae kwa kuwa wao ndio wenye maamuzi ya mwisho.  Hawa ni Watanzania wote wenye uwezo wa kupiga kura kwa kutoa maoni yao.  Hoja ya Mamlaka ya Bunge hili hatujazungumzia kwa vile imefikishwa Mahakama Kuu ya Tanzania ili kupata tafsiri sahihi ya mamlaka ya Bunge hili.  Tunachoweza kusema ni kwamba jukumu kuu la Bunge hili ni kutengeneza Katiba inayopendekezwa na Bunge ili ifikishwe kwa wananchi  waipigie kura ya maoni.  Hatua hii ya pili bado inaendelea.

Hatua ya tatu ni pale Bunge Maalum la Katiba tutamkabidhi Mhe. Rais Katiba inayopendekezwa ambayo itafikishwa kwa wananchi ili waikubali kama wataridhika nayo au kuikataa kama haikidhi matarajio yao.

Hatua hii ni ya mwisho wananchi wakiikubali tunapata Katiba Mpya wakiikataa, tunaendelea na Katiba tuliyonayo.

Kilichotokea ni kwamba, wajumbe wenzetu walio nje ya Bunge hili wameamua kuukiuka utaratibu uliowekwa kisheria.  Badala yake wamepeleka Rasimu ya Katiba kwa wananchi wakati mchakato wa kutayarisha Katiba inayopendekezwa bado haujakamilika.

Sisi Wawakilishi wa Taasisi za Dini, ambao kuuhubiri, kuutangaza na kuusimamia ukweli ni moja ya majukumu yetu katika jamii, tumesikitishwa sana na taarifa potofu zinazosambazwa kwa makusudi na makundi, taasisi na vyombo vya habari mbali mbali na tukiwa wajumbe wa Bunge hili ambao tunafahamu kwa kina na tunaridhika na kila hatua ya mchakato huu.  Tuna wajibu wa kusahihisha upotofu huu, unaoendeshwa kwa makusudi na hivi kuwaeleza Watanzania ukweli na hali halisi inayojiri hapa Bungeni.  Watanzania msifadhaishwe na wala msibabaishwe.  Hali ni shwari.  Mchakato unaendelea kwa amani na utulivu.

Katika kusahihisha upotofu unaozungumzwa kupitia mijadala na midahalo mbali mbali katika jamii, tunaomba kufafanua hali ilivyo kama ifuatavyo:-

TUHUMA KWAMBA BUNGE MAALUM LA KATIBA KUKOSA UHALALI
Jambo hili si kweli hata kidogo kwani kuna wajumbe wa aina tatu Bungeni ambao wamewekwa na kutambuliwa kisheria.  Hawa ni kama wafuatao:
1.   Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2.   Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
3.   Wajumbe 201 walioteuliwa na Mhe. Rais, baada ya kupendekezwa na Taasisi, Mashirika na makundi mbali mbali nchini,

Uhalali wa Bunge unakuwapo wakati wajumbe kutoka makundi hayo matatu wapo Bungeni, na si Vyama vya Siasa pekee.  Iwapo kwa mfano wajumbe wa 201 wakiamua kutoshiriki katika shughuli za Bunge, basi sehemu moja muhimu ya Bunge haitakuwapo na uhalali wa Bunge hautakuwepo.

Hata hivyo, Kanuni za Bunge Maalum la Katiba zimeweka idadi ya akidi ambayo ni nusu ya wajumbe wote wa Bunge Maalum.  Akidi hii ikifikiwa Bunge huendelea na shughuli zake.  Akidi hii hufikiwa kila wakati BungeMaalum linapokutana.  Hii inamaanisha kwamba Bunge Maalum la Katiba linaendesha shughuli zake kwa misingi ya sheria na taratibu zilizojiwekea.  Bunge lina uhalali wa kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria.

TUHUMA KWAMBA KANUNI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA ZINAVUNJWA
Suala hilo halijawahi kutokea.  Kanuni za Bunge Maalum la Katiba zilipitishwa na wajumbe wote kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sheria Namba 83.  Vile vile uendeshaji wote wa shughuli za Bunge zinafanywa kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Maalum.  Kanuni hizo zinatoa fursa ya Bunge Maalum kuzirekebisha pindi inapobainika ipo haja ya kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni Namba 87.  

WARAKA MWINGINE UNAJADILIWA NA SI RASIMU YA TUME
Hili nalo si kweli.  Tunawahakikishia Watanzania wote kwamba sisi kama Wawakilishi wa Taasisi za Dini miongoni mwa wajumbe wa Kundi la 201, kwa ujumla tunasema hii si kweli.  Ni upotoshaji wa makusudi.  Tunaijadili Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ibara kwa ibara.  Ibara nyingi zimeachwa kama zilivyo.  Kuna ibara ambazo zimeboreshwa au kurekebishwa, kuna ambazo zimeondolewa na kuna nyingine mpya ambazo zimewekwa ili kuweka mambo ya msingi ambayo Rasimu haikuyazingatia au haikuyaona.

WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI, WAJUMBE WA KUNDI LA 201 WA BUNGE LA KATIBA KUPEWA AU KUPOKEA RUSHWA
Sisi Wawakilishi wa Taasisi za Dini na Wajumbe wa Kundi la 201 wa Bunge hili tumesikitishwa sana na taarifa hii iliyosambazwa na baadhi ya watu, na kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari aidha kupitia kwenye mijadala, midahalo na makongamano  mbali mbali.  Baadhi yetu sisi Viongozi wa Kiroho tumeapishwa viapo vya uadilifu katika uongozi wetu wa kiroho na tuko mstari wa mbele kuongoza waumini wetu kuepuka dhambi ya tamaa ya fedha, na kusema uongo.  Taarifa kama hizo hazionyeshi heshima kwa dini au nafasi zetu za kipekee katika uongozi wa kiroho.  Taarifa hizi zinatangazwa kwa makusudi na watu mbali mbali  kupita vyombo vya habari kwa malengo ya kisiasa na kutudhalilisha sisi Viongozi wa kiroho mbele ya umma.  Tunaomba tabia hii ikomeshwe.

TUHUMA KWAMBA BUNGE KUWA NA WAJUMBE WACHACHE
Hili nalo si kweli.  Wajumbe wanaohudhuria Bunge wanakidhi akidi inayohitajika kwa mujibu wa kanuni.

HOJA YA KUSITISHWA AU KUVUNJWA KWA BUNGE MAALUM
Hii ni hoja inayozungumzwa katika mijadala mbali mbali katika jamii.  Msingi wa hoja hiyo ni kutokuueleza umma ukweli ulioko Bungeni kwa kupeleka taarifa potofu kwa wananchi kwamba Bunge Maalum limekosa mwelekeo.  Hatuoni sababu za hoja hii kutiliwa maanani kwa kuwa hakuna sababu za msingi na za kisheria za kufanya hivyo. 

HITIMISHO
Kumekuwa na taarifa mbali mbali zenye malengo ya ama kuingilia shughuli za Bunge hili au kutudhalilisha sisi wajumbe ambao si Wabunge au Wawakilishi.  Wajumbe 201, ambao mchango wao katika mijadala ya Kamati mbali mbali umekuwa na uzito wa pekee, hautambuliki katika taarifa hizo ambazo zimejaa malengo ya kisiasa zaidi kuliko ukamilishaji wa shughuli za Bunge Maalum.

Kuna taarifa nyingine zimesambazwa zikiwa na upotoshaji mkubwa, licha ya kwamba Taasisi zinazosambaza taarifa hizo zina wajumbe wake katika Bunge Maalum.  Wajumbe hao wangeweza kuzielimisha Taasisi zao ukweli ulipo hapa Bungeni, na hivyo kuwafikishia wasomaji wao taarifa zilizo za kweli na ili kulijengea Bunge hili heshima machoni pa umma wa Tanzania na Kimataifa.   Udhalilishaji kama huu unatuumiza hata sisi wajumbe ambao kwa hiari yetu tuliamua kubaki Bungeni na kuyatimiza hayo ambayo tulitumwa tuje tuyakamilishe.

Kama tulivyosema hapo awali ni wajibu wetu kama Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Bunge hili kuutaarifu umma hali halisi katika shughuli za Bunge Maalum na kuwasihi wapotoshaji kwamba wauheshimu ukweli na wawaheshimu watanzania kwa kuwaeleza ukweli.

Ahsanteni sana.  



…………………….                           …………………………
SHEIKH HAMID MASOUD JONGO             ASKOFU AMOS JOSEPH MUHAGACHI
           BAKWATA                                            KIKRISTO

WAZIRI MKUU PINDA NA WAJUMBE MBALIMBALI WA BUNGE LA KATIBA LEO MJINI DODOMA

$
0
0
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ,Mohamed Raza  (kushoto) na Ally Juma Othman Ally (katikati) wakizungumza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 4, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ally Juma Othman Ally kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Septemba 4, 2014.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimana na Meya wa Songea, Charles Mhagama,kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 4, 2014. Katikati ni Mbunge wa Songea mjini ,Dr. Emmanuel Nchimbi.

  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pida na Anne Kilango Malecala wakiteta kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 4, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images